MS-July-02-2021-080.pdf - Mwananchi Scoop

14

Transcript of MS-July-02-2021-080.pdf - Mwananchi Scoop

BONIFACE MEENA@MongiBoniMhariri Mtendaji Maudhui Mtandaoni (MCL)

DETRICIA PAMBA@detriciapambaMhariri

SAPHINIA SULEIMAN@saphiniasuleim1Mwandishi

JANETH JOVIN@jovinjanethMwandishi

JOHN MKONGWA@John MkongwaMbunifu Picha

ALPHONCE TENDEGA@phonce_tendegaMpiga Picha

NEEMA MWANKINA@Neema_MwankinaMwanasaikolojia

INNOCENT NDAYANSE@Innocent_NMwandishi

WAANDAAJI

WASANIFU

WACHANGIAJI

Tufuatilie@ Mwananchi Scoop

Tufuatilie@ Mwananchi Scoop

TWITTER/LINKEDIN

Imetayarishwa na kusambazwa na MWANANCHI COMMUNICATIONS LIMITEDPlot no: 34/35 Mandela RoadDar es Salaam- TanzaniaTel: +255 625 602 118Email: [email protected]

WHO’S HOT- DETRICIA PAMBA

Wengi walimjua kama Mtangazaji wa Clouds FM, ambaye kwa sasa anatangaza kupitia kit-

uo cha EFM, lakini kijana huyu sasa ni kati ya watu waliotumia kipaji chao kuingia kwenye entrepreneurship.

B Dozen amekuwa akifa-nya kazi ya utangazaji kwa zaidi ya miaka 12, lakini pia si kazi ya utangaza-ji pekee inayomuweka mjini; ni mmiliki wa duka la nguo la Born To Shine.

Hamisi Mandi ilikiwa ndilo jina lake halisi, BDoz-en ametoka mbali na jina hilo la kisanii.

Wengi wanaweza kuwa wanamkumbu-ka B12. Huyo B12 ndi-ye huyu BDozen, yaani kilichobadilika ni kuita-ja namba 12 kwa jina badala ya tarakimu na alipewa jina hilo na Marehemu msanii Albert Ngwea na Gardner G Habash

Name: Hamisi Mandi Birthdate: July 22nd Work: Radio & TV Personality

4 Mwananchi Scoop July 2, 2021

-SAPHINIA SULEIMAN

PFUNK “NAACHA UPRODUCER”

Yaap!!! kama kawa, kama dawa mwanan-gu mwenyewe, mara nyingi Friday inakua

na vibe lake tofauti sana na siku nyingine za wiki na vibe la mzee mzima PFunk leo ni hili hapa.Kutoka kwenye ukurasa wake wa Instagram. PFunk aachia yake ya moyoni unajua ameandika nini? Nakushushia waraka huu hapa.

“Nimeishi studio life kwa zaidi ya miaka 28, miaka 28 ya kusikiliza kelele za vyombo vya muziki usiku na mchana, miaka 28 ya kuandaa nyimbo za watu tofauti waliofanya vizuri katika nyakati tofauti,”

“Maisha na umri vimeniintroduce kwenye ulimwengu mwingine, ni muda ambao nahitaji utulivu zaidi, ku-enjoy nature, kusafiri sehemu tofauti nikiwa na camera, tuwe pamoja katika career yangu mpya ya ilm Making and Video Production, Thank you and Wel-come in my Journey,”ameandika PFunk.

Aiseee niambie unayaonaje maamuzi ya mtu mzima Majani? Amezingua au kazi iendeleeee? Tuambie kwenye ukurasa wetu wa Instagram @MwananchiScoop.

Huko mitandaoni leo habari kubwa ni shutuma alizotupiwa msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria, Wiz-kid.

Nyota huyo wa muziki anashutumiwa kuwa alimlipa mwimbaji Rihan-

na ili amtangazie (kupromote) wimbo wake “Essence” ambao

alionekana akiucheza wakati ameenda live Instagram.

Mtumiaji wa Twitter ambaye ametambulika kwa jina la

Sandra Lah ameandika kuwa Wizkid na timu

yake walimlipa Rihanna ili kuukuza wimbo huo kupitia mitandao ya kijamii huku

akisisitiza kuwa sio mara ya kwanza kwa Wizkid kucheza

mchezo kama huo.

-JANETH JOVIN

Huko mitandaoni leo habari kubwa ni shutuma alizotupiwa msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria, Wiz-kid.

Nyota huyo wa muziki anashutumiwa kuwa alimlipa mwimbaji Rihan-

na ili amtangazie (kupromote) wimbo wake “Essence” ambao

alionekana akiucheza wakati ameenda live Instagram.

Mtumiaji wa Twitter ambaye ametambulika kwa jina la

Sandra Lah ameandika kuwa Wizkid na timu

yake walimlipa Rihanna ili kuukuza wimbo huo kupitia mitandao ya kijamii huku

akisisitiza kuwa sio mara ya kwanza kwa Wizkid kucheza

mchezo kama huo.

WIZKID ASHTUMIWA KUMLIPA RIHANNA

July 2, 2021 Mwananchi Scoop 5

- INNOCENT A. NDAYANSE (ZAGALLO)

Walitumia takriban nusu

saa wakivitesa viungo vyao kwa namna iliyozikonga

nafsi zao. Naam, na wote

waliridhika.

Baada ya kuoga Masum-

buko alitulia chumbani

humo akim-subiri mwajiri

wake ampe majukumu ya

ajira yake.

SIMULIZI

MWAKA ulika-tika Masum-buko akiwa katika ajira

hiyo, ajira yenye majukumu mawili tofauti. Akawa ak-iendelea ‘kuwatibu’ Mwana-hawa na dada yake, Chausi-ku kwa zamu, tiba ambayo aliitoa huku kila aliyetibiwa akisisitiza siri kutunzwa.“Usimwambie Mwanaha-

wa...” mara kwa mara Chausi-ku alimwonya Masumbuko.

“Usimwambie dada... wala usionyeshe hali yoyote inay-oweza... kumfanya akatush-tukia...” Mwanahawa naye alisisitiza, msisitizo ambao aliutoa hususan wanapokuwa katikati ya starehe.

Masumbuko alibadili-ka; alinenepa, akanawiri na kunang’anika. Kwa nini asipendeze ilhali kila ali-chokihitaji alikipata? Haya maisha aliyoishi hapa haya-kutofautiana na kuishi parad-iso. Naam, alistahili kupen-deza.

Ikaja siku. Waziri Kisu Makalikuwili, mume wa Chausiku alirejea ghafla kuto-ka katika moja ya safari zake za ndani na nje ya nchi. Siku hiyo alionekana kuelemewa na uchovu mwingi, na hata hakuonekana kuchangamka.

Baada ya mlo wa usiku ali-kaa kidogo kwenye sofa na kutazama televisheni kwa muda mfupi kisha akaenda chumbani kulala.

Mkewe alishangaa. Hiyo haikuwa kawaida ya mumewe kuwahi kulala,

hususan siku anayorudi kuto-ka safari. Mara kwa mara al-ipokuwa akitoka safari, baada ya kula aliketi sofani akinywa toti kadhaa za pombe kali. Usiku huu hakufanya hivyo.

“Leo hata hataki kunywa whisky!” Chausiku alim-wambia Mwanahawa kwa mnong’ono.

“Ni ajabu,” Mwanahawa alisema.

Wakati huo Masumbu-ko alikuwa amekwishaingia chumbani mwake kulala. Mwanahawa na Chausiku wakabaki sebuleni kwa muda mfupi kisha kila mmoja aka-tokomea chumbani kwake.

Chausiku alipoingia chum-bani tu alimuuliza mumewe, “Vipi sweet, mbona leo mape-ma?”

“Uchovu tu,” mzee Kisu Makalikuwili alijibu huku ka-jilaza chali kitandani, macho kayafumba kama aliyetopea usingizini.

“Lakini kumbuka tuna mi-aka mitatu sasa,” Chausiku alisema. “Tuna miaka mitatu, na hatuna mtoto. Inabidi tu-jitahidi.”

Mzee Kisu Makalikuwili al-imsikia, akamwelewa. Lakini hakuwa timamu kisaikolojia siku hiyo. Alifumbua macho na kumtazama kidogo mkewe kisha akayafumba tena.

“Umeyadharau niliyok-wambia, eti?” Chausiku al-imuuliza.

“Sijayadharau maneno yako,” Mzee Kisu Makaliku-wili aliyafumbua macho tena na kumtazama Chausiku sawia. “Nimekuelewa. Lakini kwa leo, acha nipumzike.”

Chausiku ambaye waka-ti huo alikuwa amejitanda

kanga moja tu bila hata ya nguo nyingine huko ndani, alisema, “Ok, nakuacha up-umzike.” Akasonya na kupan-da kitandani.

Dakika takriban kumi zilikatika huku wakiwa wamelala katika kitanda chao kikubwa na cha kifa-hari kupindukia. Hatimaye waziri Kisu Makalikuwili akaanza kukoroma. Chausiku akamtazama kwa hasira kupi-tia mwangaza hafifu wa taa

6 Mwananchi Scoop July 2, 2021

SEHEMU YA

Sasa inaendelea

iliyomulika humo chum-bani.

Kwa mara nyingine aka-sonya. Akalitazama dari kwa jicho kali, kisha tarat-ibu akajitoa kitandani kwa kunyata.

Wakati usiku ukiwa ni mtulivu, jumba zima la Kisu Makalikuwili likiwa kimya, mlango wa chumba cha Masumbuko uligong-wa taratibu. Masumbuko

aliusikia na akaelewa. Aka-jitoa kitandani taratibu na kuufungua. Chausiku aka-jitoma ndani!

Ujio huu wa Chausiku chumbani humo haukum-shangaza Masumbuko. Hii haikuwa mara ya kwanza kwa Chausiku kuja nyaka-ti kama hizo. Alishakuja mara nyingi, na kilichom-leta ni kile alichomwambia Masumbuko siku ya kwan-

za ya ajira yake; kumpa penzi.

Ndiyo, halikuwa ni jam-bo la kumshangaza Ma-sumbuko, lakini kwa siku hii na usiku huu lilimshtua na kumtisha. Iweje huyu mwanamke amjie waka-ti huu ambao mumewe yupo? Hii siyo kumhata-rishia uhai wake?

Akaduwaa na kuba-ki akimkodolea macho

Chausiku. Akiwa bado katika hali hiyo, Chausi-ku akamvamia na kum-kumbatia, kisha akam-busu shavuni. “Nimeliacha limelala. Tufanye haraka mpenzi,” alimwambia Ma-sumbuko huku bado akiwa amemng’ang’ania.

Masumbuko alijitu-tumua, akamsukuma. Akamuuliza, “Mama, huo-ni kuwa hii ni hatari?!”

“Acha utoto, Masumbu-ko!” Chausiku alimkunjia uso. “Mimi nd’o namjua yule. Akilala, amelala. Zin-duka yake ya kwanza ni baada ya saa nzima.”

Masumbuko alishusha pumzi ndefu na kubaki akimtazama Chausiku. Chausiku, ambaye sasa al-izidisha uchokozi. Zaidi ya kumkumbatia, aliipitisha mikono kifuani kwa Ma-sumbuko na mkono mmo-ja ukashuka chini zaidi am-bako ulipenyezwa ndani ya bukta kisha ukaanza kutalii kwa namna ya kipekee.

Kama kuna mtu ambaye Masumbuko alimchukulia kama mtaalamu wa miche-zo ya mapenzi basi ni huyu Chausiku. Japo alikuwa na mwili mkubwa na akiwa na uvivu wa kiwango fulani kitandani, hata hivyo ali-jua ‘kumtayarisha’ mwan-amume. Kwa hilo Masum-buko alimvulia kofia.

Chausiku alijua kuitumia mikono yake kupita kila yalipohifadhiwa mashetani ya mwanamume rijali. Na hakuwa na hiyana kuu-tumia ulimi wake kunyon-ya sehemu yoyote ya mwili wa mwanamume aliyem-wingia moyoni.

Ni kutokana na uwe-zo wake huo wa kuchezea mwili wa mwanamume, Masumbuko hakuwa-hi kujisikia kukinaishwa naye. Tangu alipoanza kufanya ngono na Hap-py huko Nzega, hakuwahi kutembezewa ulimi kuto-ka kwenye paji la uso hadi nyayoni, ulimi huo ukil-amba na kunyonya popote

palipostahili kulambwa na kunyonywa.

Kabla Happy hajaondoka kwenda Marekani walifan-ya mapenzi zaidi ya mara kumi. Siku nyingine wali-kuwa wakitumia hata zaidi ya saa nzima wakiwa katika starehe hiyo. Lakini Happy hakuwa na cha ziada, zaidi ya kuchojoa nguo na kum-karibisha Masumbuko ka-tikati ya miguu yake kisha akatulia kama maji mtung-ini, akimwacha Masumbu-ko ahangaike kivyake.

Happy alikuwa ni mzuri sana kwa sura na umbile, lakini hakujua kuvitumia vidole vyake na kinywa chake hususan ulimi kama huyu Chausiku, mke wa waziri.

Dosari pekee aliyokuwa nayo Chausiku ni ile am-bayo pia Happy alikuwa nayo. Uzito. Ndiyo, alikuwa mzito wakati wa kile kipin-di maalumu. Hakuweza kuvishughulisha vilivyo viungo vyake isipokuwa tu kulialia na kubwatabwa-ta kwa sauti iliyotoka kwa taabu, akimsifia Masum-buko katika utendaji na kukisifia kila kiungo cha Masumbuko.

Kwa hapo ndipo ali-potofautiana na mdogo wake, Mwanahawa ambaye hakujua au hakuwa na muda wa kuchelewa kwa kumwandaa mwanamume, lakini alijua kumpokea na kumridhisha vilivyo pindi alipomkaribisha katikati ya miguu yake. Alikuwa mwepesi, alikuwa mjuzi wa ‘miondoko’ na alijaali-wa pumzi.

July 2, 2021 Mwananchi Scoop 7

8 Mwananchi Scoop June 25, 2021

People say ‘there is noth-ing sweet w i t h o u t

sweating for it.’ Kwa wale wapambanaji wenzangu itakua wananipata vyema sana kwa kauli hii, lakini pia waswahili wanase-maaa ‘hakuna mkate mgumu mbele ya chai.’

Sijui unanipata hapo

walau kwa mbaali hivi, haimaanishi hivyo am-bayo unafikiri mtu wangu ila ukiupindua vizuri huo usemi utanielewa hapa.

Hii misemo yote kwa pamoja inabebana, siku zote unapotaka kwenda mbele usiogope mishale utakayokumbana nayo njiani, kikubwa kabilia-na nayo angalia kule un-

akokwenda na ulipotoka hakika utafika yerusalem.

Makala ya leo tutak-wenda kumuangazia Pas-chal Busenga maarufu kama Ganslay, ambaye ni mwanafunzi kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) akiwa anachukua course ya Pe-troleum Ge-

o l o g y l a k i n i pia ana kipaji ki-kubwa sana cha uComedian.

Ganslay ni Co-median ambaye amejikita zaidi kufanya vicheke-sho vya kisomi, wenyewe wanaita

GANSLAY MWANACHUO MWENYE KIPAJI CHA COMEDY

yaani ni “Stand-Up Comedy,” humo mtu unakula suti yako kali, yaani unalipuka kinoma kisha unaingia mzigoni.

Wajanja wengi show kama hizi wanazielewa bhanaa au sio, basi twende kuitazama safari yake ya sa-naa, elimu yake na future yake ni ipi hapo mbeleni.

Akiwa mwa-ka wa pili chuoni, bado kijana huyu anakomaa na kita-bu chake kwani course anayoi-somea nadhani unaielewa, yaani sio ya kispotispoti mtu wangu lazima ugangamale.

KWANINI WATU WANAKUITA GANSLAY?

“Ganslay ni jina ambalo nilipewa na wanafunzi wenzangu wakati niko

form 3 baada ya kupigwa suspension mbili mfu-

lulizo, maana nilikaa wiki mbili yaani nili-pigwa ya kwanza, niliporudi nikakaa siku mbili nikapewa nyingine hivyo baa-da ya adhabu ndipo wenzangu wakani-pa hilo jina.”

“kipindi hiko nlikua nasoma Seminary na hapo ndipo nika-wa maarufu zai-di hata sasa hivi chuoni ukiuliza Paschal hawa-

jui, wanafahamu kwa jina hilo la

Ganslay.”

UNAIZUNGUMZIAJE COURSE YAKO?

“Kiukweli course yangu ni ya moto sana hadi wakati mwingine watu wananiuliza sana, hivi unawezaje kufanya sanaa na hii course unayoisoma kama mtu anasoma sociology in-amvuruga, vipi wewe unawezaje?”

“Ila kiukuweli binafsi ni-mejitoa sadaka kwanza kipa-ji ninacho napangilia sana mambo yangu mimi napiga msuli ule wenyewee ukini-kuta siku kwenye usomaji wangu unaweza kunionea huruma pia mara nyingi san-aa najihusisha nayo wikiendi tu”

Kwanini umeamua kuin-gia kwenye comedy?

“Sanaa imeendelea sana jamii ya zamani na sasa ni tofauti awali mtu akionekana ni mchekeshaji anaonekana hana akili timamu kulingana nay ale mazingira ya comedian wengi”

“Lakini sasa hivi comedy imeenda milage sana watu wanafanya kazi kisomi na weledi zaidi kwani sio hadi uweke kitambi, ufanye mazingira ya wendawazimu ndo uchekeshe hapana now days comedian it acrt different sana na inakubalika zaidi kwenye jamii”anase-ma

KILICHOKUVUTIA ZAIDI NI NINI?

“mimi nimeanzia comedy form 5 nikiwa bwenini napiga story watu wanaenjoy basi ndo nikaamua kuanzisha stand up bila mimi mwenyewe kujua kama ni stand up hapo ndi-po nilipooanza na watu waliikubali.

JAMII INAMCHUKULIA VIPI KIJANA ANAYEFANYA COMEDI-AN?

“Aiseee kwanza mtaani tu watu wanatabia wakishakuona umejikita kwenye masuala watu wanakuchukulia tofauti wanakuaona huna akili, ushaanza kuchanganyikiwa, shule imekushinda yaani mambo mengi hawaamini

July 2, 2021 Mwananchi Scoop 9

“SHOW YANG YAKWAN-ZA NILIKUJA KUIFANYA MOSHI PALE WAKIWEMO WANAFUNZI WOTE NA HAPO NDIPO NIKAZIDI KUPOKEWA ZAIDI NA MASHABIKI ZANGU NA KUZIDI KUONA I HAVE SOMETHING UNIQUE AND SPECIAL TO ME”

sana kwenye hii sanaa”anasema“Siku ya kwanza wakati nafanya

sikujua kama watu wameona na-kumbuka dada yangu alikusanya clip zangu nakuonyesha kwa wa-zazi wangu hapo ndipo walipoku-gundua kuwa nafanya kazi hii”

FAMILIA INACHUKU-LIAJE KIPAJI CHAKO?

“Niseme tu kwamba katika familia mtu ambaye anaweza kukataa jambo lako li-sifike kokote ni ‘Mama’ hivyo nil-ianza na m a m a y a n g u k w a n z a n a ku m -b u k a kipin-d i

ambachonaanza nilipata fursa ya kushiriki kwenye Futuhi niliwaza sana je nitatoboa nyumbani wa-takubali?”

“Mama alisema ila mwangu akili zote hizo ulizonazo shuleni kwe-li unaenda kuchekesha jamani? Alinishangaa kidogo”

“lakini baadaye nilipomueleza na kumshawishi akaniapa ma-jibu haya akasema mwanangu sikukatazi nakuruhusu lakini

hakikisha hai affect maso-mo yako hilo ndo lamu-

himu”alisema.

KITU GANI HAUTOKI-SAHAU?

“Daah ki-ukweli ni siku ambayo nilik-

wenda kwenye show ya pili pili tour

nilkua backstage nikaam-biwa nikachekeshe na mimi

nlkua sijawahi kufanya hivyo mbele za watu, tulikuwa wawili na mwenzangu ndo tulikua tunafanya

hivyo”“ K u m b e

kwenye

stand up mtu anasimama mwenye jukwaani unafanya yako aiseee ilinishinda ile siku nilisikitika sana ndo ilkua mara yakwangaza ku-jitokeza kwenye game”

CLIP YAKO YAK-WANZA ULITOA MWAKA GANI?

“Clip yangu ya kwanza nilitoa tarehe 8/12/ 2019 tulishoot ki-pande kimoja ambacho kilingha-rimu shilingi elfu 60000 baada ya kumaliza form six ndipo nilipoan-za rasmi yani ile ileee”

“2020 ndiyo nilifungua show yangu mwenyewe ilifanyika pale tegeta kibo complex akiwemo Oka, kapozo”anasema.

JE KUNA MAFANIKIO AMBAYO UNAJIVUNIA?

Kiukweli now days ndiyo nao-na kwasababu comedy pays ukiwa serious na kazi yako llazima uone mafanikio nashukuru Mungu ni-mepiga hatua now nakubali sana kwa mashabiki zangu najivunia”

PLATFORM GANI UNAZITUMIA KUJITAN-GAZA?

“Natumia youtube channel yakwangu ninayo,lakini pia post kwenye instagram account pamo-ja na Tiktok nayo naitumia nime-ongeza subscriber youtube takrib-ani 1.7k lakini nimebaze mnoo instagram kutupia clip zangu mbalimbali.”

Ni idea gani umekubeba zaidi?“Ebwanaaa umenikumbusha

jambo la msingi sana kiukweli Idea yamkali mani imefanya vizuri sana asana tiktok imenipa followers 10k na inamiezi miwili tu you can’t im-agine this hivyo hii idea imenibeba mnoo”

MALENGO YAKO “Mimi Ganslay kama Ganslay

kiukweli nitafurahi na kumshuku-ru ambapo siku moja nikibahatika kupata fursa katika kundi la Cheka tu! Hiyo ndiyo ndoto yangu kwenye hii tasnia” anasema Ganslay.

Stay Informed.The Truth wherever you are.

Read Mwananchi, The Citizen and MwanaSpotifrom wherever you are; another way to enjoy today's

newspaper at your convenience.

Sign up and buy your dailytoday! epaper.nationmedia.com

DownloadNation ePaper

ePaper can also be accessed through

MITINDO-JANETH JOVIN

June 25, 2021 Mwananchi Scoop 12

ATHARI ZA LIPSTICK KIAFYA

Habari mso-maji wa dondoo za fashion, ni wiki ny-

ingine tena tunakutaka hapa kujuzana mambo mbalimbali yanayohusu urembo, mitin-do na mavazi ambayo najua huenda unayajua lakini mimi nakujuza tu zaidi.

Mpendwa msomaji wetu leo hii tutaangalia rangi ya kupaka kwenye midomo maarufu ‘lipstick’ na athari zake kiafya kwa msichana.

Lipstick ni aina ya vipodo-zi vyenye rangi mbalimbali vinavyotumika kupaka katika midomo hasa ya wanawake ili kuongeza urembo na mvu-to wao.

Historia ya kupaka rangi kwenye midomo kwa kusudi la urembo inaonyesha kuwa jambo hili lilianza zamani sana na inasemekana kuwa lilianzia huko Misri.

Wanawake wa Kimisri wakati huo walikuwa wana-paka rangi nyekundu kwenye midomo yao ili kuonyesha kuwa wako wanavutia.

Ingawa matumizi ya rangi ya kupaka midomoni kati-ka siku zetu inaweza kuwa na makusudi tofauti na yale ya zamani na kupendwa na wasichana au wanawake wa kisasa wanaokwenda na wakati katika urembo, lak-ini bado ni muhimu kuan-galia athari zake kwa afya ya jamii na mwili wa mtumiaji

mwenyewe.Vipodozi hivi hutengen-

ezwa kutokana na viambato mbalimbali na inasemeka-na kuwa baadhi ya viambato hivyo si salama kwa afya.

Watafiti wa mambo ya afya ya jamii wanase-ma kuwa wanawake wengi wanaotumia rangi za kupaka midomoni wanachoangalia zaidi ni urembo na mvuto wao na wanasahau kuangalia upande wa pili wa athari zake kwa afya zao.

Katika utafiti uliofany-wa huko Marekani na US Consumer Group “Campain for Safe Cosmetics” Oktoba 2007, ripoti yao ilionyesha kuwa lipstick nyingi karibu theluthi moja, zilikuwa na madini ya ‘lead’ kwa kiwango kikubwa zaidi ya kile kilicho salama kwa afya ya binada-mu.

Viambato vingine vyenye madhara ambavyo vinapa-tikana katika rangi hizi kwa mujibu wa utafiti huo na vy-anzo mbalimbali vya habari za afya ya jamii ni pamoja na Butylated Hydroxyanisole (BHA), Coal tar (petroleum) na aluminum (Lakes color).

Inaelezwa kuwa matatizo ya kiafya yanayosababishwa na rangi hizi, hayatokei kwa haraka na ni mara chache sana waathirika wa rangi hizi kuhusisha utokeaji wa magonjwa wanayopata na mtindo wao wa maisha wa kutumia vipodozi hivi.

Wataalamu hao wa afya wanasema wanawake wa-jawazito wanaotumia lipstick, huwaweka watoto wao wal-ioko tumboni katika hatari ya kupata magonjwa wa mtin-dio wa ubongo na matatizo ya akili.

Wasichana na wanawake wanashauriwa kujiepusha na matumizi ya rangi hizo kwa ajili ya kulinda afya zao. Lakini kama hakuna njia zingine zilizo salama zaidi za kukamilisha urembo wako, unashauriwa kuepuka kujil-ambalamba midomo pale un-apokuwa umepaka rangi hizo za mdomoni.

Kwa kufanya hivyo wataal-amu wanasema kunapunguza kiasi cha viambato hatarishi vinavyoingia mwilini kwa njia ya kumeza, ingawa kiasi kingine kinaweza kupenya kupitia katika ngozi laini ya midomo na kuingia ndani ya damu.

Najua ni vigumu kwa wa-sichana wengi kuacha kupata lipstick kutokana na mazoea lakini ni vizuri wakatambua kuwa si salama kwa afya yao.

Kwa ushauri tu kama in-akuwia vigumu kuacha kupa-ka rangi hiyo basi pia hakiki-sha pindi unapotaka kula kitu chochote ifute kwanza mido-moni mwako.

Pia unapotaka kulala hakikisha unaoga na kuifuta rangi hiyo midomoni mwako kwa kufanya hivyo kutaweza kusaidia kupunguza tatizo.

ATHARI ZA LIPSTICK KIAFYA

July 2, 2021 Mwananchi Scoop 13