uhuru wa kweli - GetValue
-
Upload
khangminh22 -
Category
Documents
-
view
10 -
download
0
Transcript of uhuru wa kweli - GetValue
UHURU WA KWELI ii
Hakimiliki © Mwandishi
Baraka Shibanda
Simu: +255 767 495 842 | +255 768670143 |
+255 621054592
Baruapepe: [email protected]
Haki zote zimehifadhiwa!
Kitabu Kimefanyiwa Ubunifu na:
LD-Lamax Designs, +255 764 793 105
Haki zote za kitabu hiki zimehifadhiwa.
Hairuhusiwi kutoa nakala sehemu yoyote ya
kitabu hiki kwa namna yoyote bila idhini ya
mmiliki wa kitabu hiki, isipokuwa kwa kunukuu
kuliko ruhusiwa kisheria.
UHURU WA KWELI iii
YALIYOMO
SHUKRANI ------------------------------------------------------------------ ix
DIBAJI ----------------------------------------------------------------------- xiii
UTANGULIZI ---------------------------------------------------------------- xv
SURA YA KWANZA --------------------------------------------------------- 1
Kwanini iwe hivi? ------------------------------------------------------- 1
SURA YA PILI -------------------------------------------------------------- 21
Kwanini niuishi ukale ------------------------------------------------- 21
SURA YA TATU ------------------------------------------------------------ 61
Mbona sio asili yangu ------------------------------------------------ 61
SURA YA NNE ------------------------------------------------------------ 105
Sikuumbwa kwa kusudi hili ---------------------------------------- 105
SURA YA TANO ---------------------------------------------------------- 123
Nitasimama tena ----------------------------------------------------- 123
SURA YA SITA ------------------------------------------------------------ 171
Yesu Kristo alimaliza yote msalabani ---------------------------- 171
SURA YA SABA ----------------------------------------------------------- 189
Mimi si mfungwa tena ---------------------------------------------- 189
SURA YA NANE ---------------------------------------------------------- 205
Nimebarikiwa --------------------------------------------------------- 205
SURA YA TISA ------------------------------------------------------------ 223
Mimi ni mshindi ------------------------------------------------------ 223
UHURU WA KWELI iv
SURA YA KUMI----------------------------------------------------------- 243
Nitakiri hivi daima --------------------------------------------------- 243
HITIMISHO --------------------------------------------------------------- 265
KUHUSU MWANDISHI ------------------------------------------------- 267
UHURU WA KWELI v
VIFUPISHO
1 Falme: 1 Wafalme
1 Kor: 1 Wakorintho
1 Pet: 1 Petro
1 Samw: 1 Samweli
1 Timo: 1 Timotheo
1 Yoh: 1 Yohana
2 Kor: 2 Wakorintho
2 Yoh: 2 Yohana
3 Yoh: 3 Yohana
Ayu: Ayubu
BHND: Biblia ya Habari Njema
CCT: Christian Council of Tanzania
Dan: Daniel
Ebr: Waebrania
Efe: Waefeso
Filip: Wafilipi
UHURU WA KWELI vi
Gal: Wagalatia
Hes: Hesabu
Hos: Hosea
Isa: Isaya
KJV: King James Version
Kol: Wakolosai
Kut: Kutoka
Luk: Luka Mtakatifu
Mark: Marko Mtakatifu
Mat: Matendo ya Mitume
Math: Mathayo Mtakatifu
Mhu: Mhubiri
Mwa: Mwanzo
NEN: Biblia ya NENO
NIV: New International Version
Rum: Warumi
Tit: Tito
UHURU WA KWELI vii
TPT: The Passion Translation
UDOM: University of Dodoma
Ufu: Ufunuo
USCF: University Students Christian Fellowship
Yak: Yakobo
Yer: Yeremia
Yoh: Yohana Mtakatifu
Zab: Zaburi
UHURU WA KWELI ix
SHUKRANI
angu nianze huduma hii ya uandishi sikuweza kupiga
hata hatua moja bila Mungu, Roho Mtakatifu.
Namshukuru sana Roho Mtakatifu rafiki yangu kwa
kuniwezesha kwa kiwango kikubwa kisichoelezeka hasa
pale nilipochoka, na kutaka kuahirisha kazi hii. Roho
Mtakatifu amekuwa akinipa msukumo mkubwa sana,
usioelezeka, kwa sababu kuna wakati hali yangu ya ndani
ilichoka. Kwa neema yake niliweza kuandika, hata katika
hali hiyo hiyo ya kuchoka. Kusudi niweze kutimiza ule
utumishi nilioitiwa katika kuhubiri na kufundisha kwa njia
ya uandishi tangu mwaka 2015.
Aidha napenda kuwashukuru sana hawa wafuatao; Apostle
Shemeji Melayeki amenisaidia sana kwa kiwango kikubwa
tangu nilipomwomba kunisaidia kuhariri kitabu hiki na
kuniandikia dibaji. Hakusita kunikubali na kufanya kazi hii,
bila kujali kuwa hatuna ukaribu sana wa mawasiliano na
kutofahamiana. Apostle Shemeji Melayeki amekuwa ni
mtumishi ambaye Mungu amekuwa akimtumia kwa
kiwango kikubwa sana hasa katika nchi ya Tanzania.
Amekuwa akifundisha ufunuo wa neno la kweli juu neema
ya Mungu na kujitambua hali tukijua tumezaliwa mara ya
pili (tumeokoka) na sisi ni nani katika Yesu Kristo. Nami
T
UHURU WA KWELI x
nimalize kwa kusema Apostle Shemeji Melayeki
umebarikiwa sana.
Bila kusahau katika kila huduma kuna watu nyuma yake
wanaoibeba kama ilivyo kawaida. Huduma ya injili ya Kristo
ni bure kutolewa kwa mataifa yote lakini kupelekwa
inapelekwa kwa gharama kubwa sana. Inawezekana hata
hiki kitabu kisingeweza kukufikia mkononi mwako
kukisoma leo hii pasipo msaada wa kifedha kutoka kwa
hawa wafuatao. Tumpe Sanjala, Eliasi Mlwafu, Charles
Mwaipaja, napenda kusema Mungu amewabariki sana.
Zaidi sana niwashukuru wazazi wangu ambao walinisaidia
kunijengea msingi wa kusimama imara katika kumtumikia
Mungu. Bwana Fredy Ambindwile Shibanda na Bi Bupe
Amoni Sanjala Mungu amewabariki sana. Bwana Yesu
amekwisha walipa kwa huduma njema sana.
Asanteni sana LD-Lamax Designs kwa kupangilia kitabu hiki
kuwa katika mfumo unaoweza kusomeka kirahisi na
kuifanya huduma hii kuwa na mvuto kwa wasomaji wote.
Pia nipende kuwashukuru watumishi mbalimbali ambao
wamekuwa wakinitia moyo, kunishauri na kuniombea au
kujifunza kutoka kwao katika huduma hii ili niweze
kufanikisha huduma hii. Ninakushukuru sana Shukuru
Sanga, Baraka Maliaki, Clintoni Sanga, Mwl Samweli
Mkumbo, Mwl Aliko Mwalulili, Mwl Tuntufye Mwakyembe.
UHURU WA KWELI xi
Pia nathamini kuwezeshwa kwa maombi na ushauri na timu
yangu yote ya huduma ya Udhihirisho wa Nguvu za Mungu
(Godly Power Manifestation Ministry [GPM]). Mimi nikiwa
kama Mwanzilishi wa huduma hii na kupewa maono haya
tangu tarehe 12 ya Mwezi Januari Mwaka 2017. Nimeona
kutiwa moyo sana na hawa ndugu zangu, tupo timu kubwa
kiasi ambacho siwezi kuwataja wote kwa majina. Mungu
awabariki sana sana na neema ya Kristo iendelee
kuwahifadhi.
Ninamshukuru baba yangu mlezi wa kiroho Mchungaji
Nelson Shoo amekuwa akinisaidia kiroho tangu nimfahamu
namshukuru sana. Namshukuru baba Mchungaji mlezi wa
USCF-CCT UDOM Chaplaincy, Mchungaji Timothy Erasto
Chimeledya amefanyika baraka sana tangu nimfahamu.
Kwa mara ya kwanza alinishauri kwa kiwango kikubwa
katika uandishi wa kitabu cha YAJUE MAISHA na kitabu cha
KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU. Kwakweli asingenitia moyo
katika hatua za awali za uandishi wa vitabu huenda leo hii
usingeweza kukiona kitabu hiki mikononi mwako. Mungu
amekubariki sana baba Erasto Timothy Chimeledya neema
ya Mungu iendelee kukuhifadhi katika huduma hii ya
ushauri.
UHURU WA KWELI xiii
DIBAJI
azi aliyoifanya Yesu Kristo kwa mateso yake, kufa,
kufufuka na kuingia katika utukufu wake ni kazi ya
heshima sana. Huo ndio ukombozi kamili wa
mwanadamu. Hapo ndipo adui yetu mkubwa aliposhindwa
yaani dhambi na matokeo yake. Ndiyo maana mitume wa
Yesu Kristo walihubiri kwa nguvu sana habari za ufufuo wa
Yesu Kristo wakisisitiza matokeo yake; yaani toba iletayo
ondoleo la dhambi ikiwekwa muhuri na ubatizo wa Roho
Mtakatifu. Haya mambo mazuri mno.
Baraka Shibanda anatumia lugha rahisi kabisa kuelezea
umuhimu wa kazi ya Yesu na matokeo yake kwenye maisha
ya mwamini kwa namna ambayo ataona uhalisia wa maisha
ya ushindi ndani yake Kristo.
Ninaamini wakati unasoma kwa utulivu mkubwa utaona
ukisogea hatua katika kudhihirisha kazi ya msalaba wa Yesu
Kristo na kutembea katika uhalisia wa UHURU WA KWELI
ndani ya Yesu Kristo.
Apostle Shemeji Melayeki
Bachelor degree in Agricultural Economics
Email: [email protected]
Simu: +255763965297, +255714548565
K
UHURU WA KWELI xiv
Mwanzilishi wa huduma ya Global Family Gathering
Ministries
Dar-es-salaam, Tanzania
UHURU WA KWELI xv
UTANGULIZI
atazamio ya Mungu Baba yetu juu ya ulimwengu
hususani duniani ilikuwa ni kuifanya dunia iliyojaa
amani, upendo na furaha. Mambo haya yamekuwa ni ndoto
si kwa wasiomwamini Kristo tu bali kwa waaminio pia.
Kiuhalisia amani, upendo na furaha zilitakiwa kuwa
chemichemi zinazotokea kwa wote wanaomwamini Kristo
na kuiathiri dunia ili iweze kufurika amani, upendo na
furaha. Kinyume chake idadi kubwa ya waaminio
wamekuwa ndio watu wanaoonekana kuwa ni watu wenye
shida, misukosuko, matatizo yaliyowapelekea kuwa na
huzuni, maisha ya kufeli na kukata tamaa.
Haikutarajiwa kuwa maisha ya kushindwa ni utambulisho
kwa wale wanaomwamini Kristo. Ingawa wapo idadi kubwa
ya wasiomwamini Kristo pia wanaishi maisha ya kushindwa.
Je, Ni kweli Mungu anafurahia wanadamu kuteseka? Au
Mungu anataka wanadamu waishi maisha ya kushindwa?
La hasha! Luka anaandika katika kitabu chake, Luka sura ya
pili kuanzia mstari wa tisa. Malaika anawatokea katika
utukufu wa Bwana na kuwaambia. “Nawaletea habari
njema ya furaha kuu kwa watu wote. Maana leo katika mji
wa Daudi amezaliwa , kwaajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo
Bwana”
M
UHURU WA KWELI xvi
Neno mwokozi ni nomino ambayo kitenzi cheke ni okoa.
Katika lugha ya kigiriki neno okoa linatafsiriwa kama “sozo”.
Neno hili limebeba mambo matatu uponyaji, ukombozi na
ustawi (mafanikio kamilifu). Kwa hiyo wakati malaika
anapeleka taarifa wachungaji kuwa katika mji wa Daudi
amezaliwa mwokozi ambaye ni Kristo Bwana. Maana yake
Kristo amezaliwa ulimwenguni kwaajili ya kuleta uponyaji,
ukombozi na ustawi (mafanikio kamilifu). Baada ya malaika
kutoa taarifa hiyo mara walikuwepo malaika, wingi wa jeshi
la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema;
“Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa
watu aliowaridhia” [Luk 2:14]
Maana yake Mungu alikusudia kwa mara nyingine dunia
yote iwe ni dunia yenye amani, upendo na furaha. Ukomo
wa mateso, huzuni, uchungu, kukataliwa na kushindwa
ulitatuliwa baada ya mwokozi Yesu Kristo kuja duniani. Hii
ni neema kubwa na ya ajabu mno ambayo akili ya
kibinadamu haiwezi kueleza kwa kiwango cha utoshelevu.
Katika kitabu cha Yohana 8:32, Yesu alikuwa anawaambia
Wayahudi waliomwamini Yesu kuwa;
“tena mtaifahamu kweli, na hiyo kweli itawaweka huru”
[Yoh 8:32]
Yesu alipowaambia Wayahudi tena waliomwamini kwa
lugha nyingine waliookoka. Walichanganyikiwa wakasema
UHURU WA KWELI xvii
mbona hatujawahi kuwa watumwa wakati wote na sisi tu
uzao wa Ibrahimu? Yesu anawaaambia katika mstari wa
thelathini na sita;
“Basi Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli”
[Yoh 8: 36]
Kumbe walikuwa wanamwamini Yesu Kristo lakini bado
walikuwa wamefungwa. Yesu aliwaambia hakuna namna
wanaweza kufunguliwa kuwa huru pasipokukaa katika neno
lake [neno la Kristo] (Yoh 8:30). Neno la Kristo ndio
linapelekea kuijua kweli na kuwa huru kweli kweli.
Kitabu hiki UHURU WA KWELI ni kitabu kinachomueleza na
kumfunua Kristo kama mkombozi kutusaidia kuwa huru
kupitia neema yake aliyoifunua katika yeye ili kutusaidia
kuponywa, kufunguliwa na kuwa na mafanikio kamili. Yesu
alikuja kusuluhisha chanzo cha matatizo yote. Wako watu
waliosongwa na ulevi mbaya (bad addictions) wa aina mbali
mbali (unywaji wa pombe, kuvuta bangi, kuangalia picha na
mikanda ya uchi). Wengine wamekuwa na mitazamo hasi
iliyotokana na imani potofu inayopelekea kujitahidi kwa
juhudi zao katika kulitimiza kusudi la Mungu. Katika
huduma, kazi, vipawa na karama walizopewa. Lakini
mambo haya yote tunaweza kuyafikia kwa neema ya Kristo.
UHURU WA KWELI xviii
Kitabu hiki kitakusaidia kupata ufahamu juu ya
mambo yafuatayo:-Kumsaidia mtu aliyeathirika na
ulevi mbaya (bad addictions) wa aina zote
ulioshindikana kupitia neema ya Kristo.
Kuwa na mtazamo sahihi ambao utapelekea kuwa
na imani itakayokusaidia kudhihirisha uponyaji,
ustawi (mafanikio) na kuishi maisha ya kimbingu
ukiwa duniani kupitia neema ya Kristo.
Kuwa na ufahamu juu ya kuwa na udhihirisho kamili
juu ya huduma, kazi, kipawa na karama zilizoko
ndani yako kupitia neema ya Kristo.
Namna ya kulitimiza kusudi la Mungu kikamilifu
kupitia neema ya Kristo.
Kwa Neema ya Roho Mtakatifu nakukaribisha tuweze
kujifunza UHURU WA KWELI katika Kristo Yesu ili tuweze
kufikia uponyaji, ukombozi na mafanikio kamilifu kama
Mungu alivyokusudia katika maisha yetu.
UMEBARIKIWA.
UHURU WA KWELI 1
SURA YA KWANZA
KWANINI IWE HIVI?
wanini iwe hivi ni swali ambalo linawatesa watu wengi
wakiwa wamefika katika hali ya kujidharau kujiona
hawafai kutokana na vile wanavyovifanya kwenye maisha
yao. Watu wengi wanapofikia hatua hii ya kujidharau huwa
wanaamua kuendelea kufanya makosa zaidi. Wengine
hukosa tumaini kabisa na kuamua kufia dhambini kwa
sababu wanaona haiwezekani kabisa kuwa watu wema
tena (watakatifu). Wakati mwingine kuona haifai kuokoka
na kurudia hali yao ya kawaida waliyokuwa nayo hapo
awali.
Kwanini iwe hivi?
Ni swali ambalo limewatesa watu wengi kiasi ambacho
wengine imewapelekea kukosa mwelekeo zaidi. Aidha kwa
kuendelea kufanya makosa zaidi, wengine wamechukua
maamuzi ya kujinyonga kwa sababu wanaona hawafai
kabisa uwepo wao katika jamii kutokana na tabia mbaya
walizo nazo. Inaweza ikawa ni ulevi wa matumizi ya
madawa ya kulevya, ulevi wa uzinzi, wizi, ujambazi.
K
UHURU WA KWELI 2
Ulevi ni nini? (What is addiction)
Ni kitendo kinachofanyika kwa kujirudia bila kujitambua.
Kuwa na msukumo usiotarajiwa wa kujirudia rudia, ambao
unaweza kuleta madhara ya kisaikolojia, kiafya, kitabia hata
kiuchumi pia. Hali hii imepoteza uwezo binafsi wa watu na
kujikuta wakifanya mambo ambayo hawakutaka kufanya
kabisa.
Tuangalie mifano ya hawa watu wawili Yuda Iskariote
mwanafunzi wa Yesu na Petro mwanafunzi wa Yesu
waliokuwa na swali la namna hii; kwanini iwe hivi? Lakini
kila mmoja alichukua maamuzi tofauti;
Mfano wa Yuda, alivyojinyonga;
“Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona yakuwa
amekwisha kuhukumiwa, alijuta, akawarudishia wakuu wa
makuhani na wazee vile vipande thelathini vya fedha,
akasema, Nalikosa niliposaliti damu isiyo na hatia.
Wakasema, Basi haya yatupasani sisi? Yaangalie haya
wewe mwenyewe. Akavitupa vile vipande katika hekalu,
akaondoka, akaenda kujinyonga” [Math 27:3-5]
Yuda alikutana na wakati mgumu sana kwenye maisha
yake, alijikuta alivyomsaliti Yesu haikuwa tarajio lake
akajikuta amechanganyikiwa. Huenda na yeye alijiuliza
UHURU WA KWELI 3
swali la namna hii kwanini iwe hivi? Kwanini nimemsaliti
mwana wa Adamu? Hatimaye ushawishi wa Shetani
alimwingia akaenda kujinyonga, lakini unafikiri mtazamo
wa Yesu juu ya kujinyonga kwa Yuda unautazamaje? Yesu
alipenda kujinyonga kwa Yuda? La hasha Yesu mwenyewe
aliwahi kusema maneno haya;
“Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi, wapate
kutubu” [Luk 5:32]
Kama Yesu alikuja kwa waliopotea, alikuja kuhakikisha watu
wanabadili mitazamo yao na kugeuka katika njia mbaya.
Kama Yesu alikuja kwa wenye dhambi maana yake hakuna
ulevi, majuto, dhambi au majuto yasiyo sameheka mbele ya
Bwana Yesu. Mtazamo wa Yesu kwa Yuda ilikuwa ni kutubu
na sio kujinyonga.
Mfano wa Petro alivyotubu;
“Na Petro alikuwa chini behewani; akaja mmoja wa vijakazi
wa Kuhani mkuu, akamwona Petro akikota moto;
akamkazia macho, akasema, Wewe nawe ulikuwapo
pamoja na yule Mnazareti, Yesu. Akakana, akasema, Sijui
wala sisikii unayoyasema wewe. Akatoka nje hata
ukumbini; jogoo akawika. Na yule kijakazi akamwona tena
akaanza tena kuwaambia wale waliosimama pale, Huyu ni
mmoja wao. Akakana tena. Kitambo kidogo tena wale
UHURU WA KWELI 4
waliosimama pale wakamwambia Petro, Hakika u mmoja
wao, kwakuwa u Mgalilaya wewe. Akaanza kulaani
kuapiza, Simjui mtu huyu mnayemnena. Na mara jogoo
akawika mara ya pili. Petro akalikumbuka lile neno
aliloambiwa na Yesu, Kabla ya kuwika jogoo mara mbili,
utanikana mara tatu. Na alipofikiri, akalia” [Mark 14: 66-
72]
Swali la kujiuliza kati ya Yuda na Petro ni nani ambaye
alikuwa amekosea zaidi?
Yuda alimsaliti Yesu lakini Petro alimkana Yesu mara tatu
wazi wazi. Nakwambia Petro alistahili ajinyonge kama
alivyofanya Yuda lakini Petro alirudi kutubu huku akilia kwa
machozi. Hakuna uovu usio sameheka kwa Bwana, hakuna
ulevi usiosameheka, hata kama wanadamu wote watasema
haufai kabisa umeoza kwa dhambi huwezi kurudi kwa Yesu
kumtumikia. Yesu bado anakuita na bado anakuhitaji
kwaajili ya ufalme wake. Petro huenda naye alijiuliza swali
kwanini iwe hivi? Lakini alijua yupo mkombozi wake, lipo
tumaini lake, akatubu. Petro hakujali watu watasemaje
baada ya kutubu kwa sababu alimkana Yesu wazi wazi
mbele yao, bali aliangalia neema ya msamaha wa Kristo
maishani mwake, alitubu na kusamehewa.
UHURU WA KWELI 5
Unaweza ukawa na matendo maovu ambayo watu
wakasema haufai tena, hutakiwi tena kutubu. Unaweza
ukawa unafanya dhambi ya sirini na imekutesa huenda
hakuna mtu anayejua ikafika mahali mpaka ikakulevya.
Inawezekana Shetani anaachilia mashitaka kwenye nafsi
yako kwamba haufai tena huwezi tena kusimama, huwezi
tena kumtumikia Mungu. Yesu alishachukua udhaifu wako
wote, alibeba uovu wako wote, alishanyang’anya hati ya
mashitaka kwa Shetani akaigongomelea msalabani.
Haleluyaa! Anachokushitaki Shetani leo kuwa huwezi
kurudi tena kwa Mungu, huwezi kumtumikia Mungu.
Anachokwambia Shetani leo kuwa umefanya dhambi sana
haufai kabisa kuwa mototo wa Mungu, haufai hata
kumsogelea Mungu ni kwa sababu hujajua tu kuwa Yesu
alikufia msalabani. Moja ya kitu kilichomfanya Kristo afe
msalabani ilikuwa ni kunyang’anya hati ya mashitaka
ambayo Shetani anakushitaki leo.
Kama ni hivyo ni wakati wako sasa wa kusimama na
kumwambia Shetani asikushitaki tena rudi kumtumikia
Mungu amua kutubu (kugeuka). Umebeba kusudi la
Mungu, umebeba majibu ya vizazi vingi, usikubali
kukandamizwa na Shetani kifikra kuwa hauwezi kurudi kwa
Baba. Mungu anakutegemea sana kuujenga ufalme wake
ndio maana Shetani hataki urudi anajua utakuwa hasara
kwenye ufalme wake.
UHURU WA KWELI 6
Jiulize swali kwanini iwe hivi? Jiulize kwanini umtumikie
Shetani?
Mwambie Shetani asikutaabishe tena! Kwa sababu
alishapondwa kichwa na uzao wa mwanamke (Yesu Kristo
wa Nazareti). Kupitia huyo majuto hayapo tena,
kudharauliwa hakupo tena, hukumu haipo tena, mateso
hayapo tena. Swali kwanini iwe hivi? Yesu amelijibu
msalabani kuwa hakuna mzigo mzito usio sameheka kwake.
Kiri namna hiyo ili uweze kutoka mahali ulipo uanze kuishi
maisha ya ushindi na utakatifu. Kwa maana kwa moyo mtu
huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata
wokovu (Rum 10:10).
Fuatisha sala hii kwa Imani;
“Bwana Yesu asante kwa neema na upendo wako, wewe
uliyejifanya mwenye dhambi ili nipate haki. Wewe
uliyejifanya mwenye dhambi ili niwe mtakatifu, wewe
uliyedharaulika ukaaibika ili niheshimike, wewe uliyejifanya
maskini ili niwe tajiri.Wewe uliyekuwa dhaifu ili mimi
nitukuzwe najua unafahamu hali yangu mbaya
iliyonikamata. Baba nakutazama wewe ili unisaidie kutoka
kwenye vifungo hivi, nisaidie kutoka kwenye huu ulevi
(….taja tatizo lako unalotaka kutoka….). Asante Bwana Yesu
kwasababu kwa damu yako ulinisamehe pale msalabani.
UHURU WA KWELI 7
Kama katika kuchekwa na maumivu makali ulisamehe
naomba nisamehe pia. Nakiri kutembea kwa upya katika
maisha yangu na kuishi maisha ya ushindi. Asante
kwasababu umenifanya kuwa mmoja katika familia ya
Mungu Mtakatifu mwenye uweza wote.” Amen
Ukiwa umetamka sala hii umeshaingia kwenye familia ya
watakatifu (umeokoka). Nifuatilie kwenye email au namba
za simu zilizoko mwanzoni mwa kitabu kuna zawadi yako
nimekuandalia. Umebarikiwa sana.
Ulevi wa ugonjwa wa mwanamke aliyekuwa akitokwa
damu miaka kumi na miwili jinsi ulivyoponywa.
“Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda
wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali
zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu
yoyote, alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi
lake; mara hiyo kutokwa damu kwake kulikoma. Yesu
akasema, Ni nani aliyenigusa? Basi, watu wote walipokana,
Petro alimwambia, Bwana mkubwa, makutano haya
wanakuzunguka na kukusonga. Yesu akasema, Mtu
alinigusa, maana naona ya kuwa nguvu zimenitoka. Yule
mwanamke, alipoona ya kuwa hawezi kusitirika akaja
akitetemeka, akaanguka mbele yake, akamweleza mbele
ya watu wote sababu yake ya kumgusa, na jinsi
UHURU WA KWELI 8
alivyoponywa mara. Akamwambia Binti, imani yako
imekuponya; enenda zako na amani.” [Luk 8: 43-48]
Mama huyu aliyetokwa damu kwa miaka kumi na miwili,
alikuwa amedharauliwa na jamii kutokana na ugonjwa
wake, pia alikuwa ameugua ugonjwa ambao ulimtesa kiasi
cha kumlevya, hali hiyo ilimpelekea kuona ni sehemu ya
maisha yake. Katika jamii ya Waebrania ilikuwa ni
utamaduni, mtu aliyekuwa akitokwa damu alihesabiwa
kuwa ni najisi. Watu wa namna hii hawakuruhusiwa
kushiriki ibada wala maeneo yenye mikusanyiko kwahiyo
walikuwa wanatengwa kabisa. Mama huyu alikuwa
akitafuta msaada kwa waganga wa kienyeji, mali zake zote
ziliishia huko lakini ndani yake baada ya kuona hali yake
mbaya huenda alijiuliza moyoni mwake swali hili kwanini
iwe hivi? Nimetokwa damu mwaka wa kumi na mbili sasa,
mali zangu zote zimeishia kwa waganga wa kienyeji, jamii
yangu imenitenga. Huenda alilia kwa uchungu hali mbaya
anayoipitia, Kwanini iwe hivi? Akaazimia moyoni mwake
mimi nitakwenda kwa Yesu, nikashike upindo wa vazi lake
tu ili nipone.
Na alipokwenda kwa imani ulevi wake wote wa ugonjwa
uliomtesa miaka kumi na miwili ulimtoka. Najisikia
kumtukuza Mungu kwaajili ya hili, hakuna ulevi
unaoshindikana kwa Bwana. Ukimtwika fadhaa yako yeye
UHURU WA KWELI 9
anakubebe mzigo wake na kukupa nira yake iliyonyepesi
kuibeba (1Pet 5:7, Zab 55:22, Math 11:28-30) anaibadili
huzuni kuwa furaha kwenye maisha yako. Hakuna mzigo
usioweza kupumzishwa kwa Bwana, hakuna ulevi usioweza
kuachwa kwa Mungu aliye hai, upindo tu wa Yesu unaweza
kukusaidia kutoka kwenye hali mbaya iliyoshindikana
kwenye maisha yako. Ni zamu yako sasa jiandae kiri
umefunguliwa kupitia damu ya Mwanakondoo (Yesu Kristo)
msalabani.
Mwanamke mjane wa Serepta jinsi alivyopokea muujiza
wa kuzidishwa kiuchumi maradufu juu ya ulevi wa hali
yake mbaya ya kiuchumi.
“Basi, akaondoka, akaenda Sarepta, hata alipofika langoni
pa mji, kumbe! Mwanamke mjane alikuwako akiokota kuni;
akamwita, akamwambia, Niletee, nakuomba, maji kidogo
chomboni nipate kunywa. Alipokuwa akienda kuleta,
akamwita akasema, niletee, nakuomba, kipande cha mkate
mkononi mwako. Naye akasema kama BWANA, Mungu
wako aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na
mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili
niingie nijipikie mimi na mwanangu, tuule tukafe. Eliya
akamwambia, Usiogope; enenda ukafanye kama
ulivyosema; lakini unifanyie kwanza mkate; kisha ujifanyie
nafsi yako na mwanao. Kwa kuwa BWANA, Mungu wa
UHURU WA KWELI 10
Israeli, asema hivi, Lile pipa la unga halitapunguka, wala ile
chupa ya mafuta haitaisha, hata siku ile BWANA
atakapoleta mvua juu ya nchi. Basi akaenda, akafanya
kama alivyosema Eliya; nayeye mwenyewe, na Eliya, na
nyumba yake, wakala siku nyingi. Lile pipa la maji
halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawa
sawa na neno la BWANA alilonena kwa kinywa cha Eliya”
[1Falme 17: 10-16]
Mwanamke mjane alikuwa amekata tamaa na hali yake
mbaya ya uchumi kiasi cha kumlevya. Unajua kwenye
ufahamu wake alikuwa anawaza kufa tu! Hakuona tena
ladha ya kuendelea kuishi kwa sababu ya hali yake mbaya
ya kiuchumi. Huenda alijiuliza swali juu ya hali yake mbaya
ya kiuchumi, kwanini iwe hivi? Akaamua kufanya maamuzi
ya kusubiri kifo kutokana na hali yake ya uchumi iliyokuwa
mbaya mno.
Mtumishi wa Mungu Eliya alimwambia ukanifanyie kwanza
mkate, unajua nini Mungu alikuwa anatafuta kwa yule
mwanamke? Ni imani, ili amwezeshe kutoka kwenye hali
yake mbaya ya kiuchumi. Yule mwanamke pamoja na hali
yake mbaya alienda mbele ya mtumishi wa Mungu Eliya
huku akiwa amemfanyia mkate. Akasema, nitaenda hivi hivi
na hali yangu mbaya ya kiuchumi na Bwana, Mungu
akamzidisha maradufu. Hata sasa hakuna linaloshindikana
kwa Bwana, Mungu anakusubiri wewe uende kama ulivyo
UHURU WA KWELI 11
wewe muamini tu ili akufanye kuwa mpya na kubadilisha
historia ya maisha yako leo.
Ayubu alipoondokewa na mifugo yake, watumishi wake
na binti zake. Mke wake alipomsaliti na kuumwa ugonjwa
wa majipu. Baadaye kubarikiwa kwa baraka zaidi ya
mwanzo.
“Ilitukia siku moja hao wanawe na binti zake walipokuwa
wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao
mkubwa, mjumbe akamfikilia Ayubu na kumwambia, Hao
ng'ombe walikuwa wakilima, na punda walikuwa wakilisha
karibu nao; mara Waseba wakawashambulia,
wakawachukua wakaenda nao; naam, wamewaua hao
watumishi kwa makali ya upanga, mimi peke yangu
nimepona, mimi tu, kukuletea habari. Huyo alipokuwa akali
akinena, akatokea na mwingine, na kusema, Moto wa
Mungu umeanguka kutoka mbinguni na kuwateketeza
kondoo, na wale watumishi, na kuwaangamiza; mimi peke
yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. Huyo
alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na
kusema, Wakaldayo walifanya vikosi vitatu,
wakawaangukia ngamia, wakaenda nao, naam,
wamewaua wale watumishi kwa makali ya upanga; mimi
peke yangu nimepona, mimi tu, kukuletea habari. Huyo
alipokuwa akali akinena, akatokea na mwingine, na
UHURU WA KWELI 12
kusema, Wanao na binti zako walikuwa wakila na kunywa
divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa; mara, tazama,
upepo wenye nguvu ukatoka pande za jangwani, ukaipiga
hiyo nyumba pembe zake nne, nayo ikawaangukia hao
vijana, nao wamekufa; na mimi peke yangu nimepona,
mimi tu, kukuletea habari. Ndipo Ayubu akainuka,
akalirarua joho lake, kisha akanyoa kichwa chake, na
kuanguka chini, na kusujudia; akasema, Mimi nilitoka
tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena
huko uchi vilevile; Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina
la Bwana na libarikiwe. Katika mambo hayo yote Ayubu
hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa
upumbavu. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana,
akampiga Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu
hata utosi wa kichwa. Naye akashika kigae cha kujikunia;
akaketi majivuni. Ndipo mkewe akamwambia, Je! Wewe
hata sasa washikamana na utimilifu wako? Umkufuru
Mungu, ukafe. Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena
kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je!
Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na
mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya
dhambi kwa midomo yake.” [Ayu 1:13-22, 2:7-10]
Ayubu aliondokewa wafanya kazi wake, wanyama wake,
binti zake, kupigwa ugonjwa wa majipu. Ugonjwa wa Ayubu
ulimfanya ajikune kutoka uwayo wa miguu yake mpaka
utosini kiasi cha kumlevya. Mke wake alimshauri amwache
UHURU WA KWELI 13
Mungu na kumkufuru ili afe lakini Ayubu hakuwa tayari.
Baadae mke wake akamkimbia, lakini alisimamia imani yake
kwa Bwana. Kwa siku moja alitokewa na matatizo magumu
sana, lakini alitamka neno moja tu kwa ujasiri. “Bwana
alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe”. Hii ni
kwa sababu Ayubu alimtumaini Bwana hakuangalia hali
ngumu aliyopitia. Huenda alijisemea kwanini iwe hivi?
Lakini alipomtazama Bwana akaona faraja na baraka
kwenye maisha yake. Kwa sababu Ayubu alijua yote
yanayoonekana nje kwa mwilini hata yakipotea bado
yanaweza kurejea maradufu. Ayubu alijua baraka zake halisi
zinapatikana ndani yake ndio maana alimtumaini Bwana.
Na baadaye maandiko yanasema;
“Basi hivyo Bwana akaubarikia huo mwisho wa Ayubu zaidi
ya mwanzo wake; naye alikuwa na kondoo kumi na nne
elfu, na ngamia elfu sita, na jozi za ng'ombe elfu, na punda
wake elfu. Tena alikuwa na wana waume saba, na binti
watatu” [Ayu 42:12-13]
Pamoja na hali mbaya aliyokuwa nayo Ayubu hakumkufuru
Mungu alimtumaini Mungu na Mungu akambariki Ayubu
katika mwisho wake na mwisho wake ukawa wa baraka
kuliko mwanzo.
UHURU WA KWELI 14
Stephano aliyepigwa mawe mpaka kufa
“Enyi wenye shingo gumu, msiotahiriwa mioyo wala
masikio, siku zote mnampinga Roho Mtakatifu; kama baba
zenu walivyofanya, na ninyi ni vivyo hivyo. Ni yupi katika
manabii ambaye baba zenu hawakumwudhi? Nao
waliwaua wale waliotabiri habari za kuja kwake yule
Mwenye Haki; ambaye ninyi sasa mmekuwa wasaliti wake,
mkamwua; ninyi mlioipokea torati kwa agizo la malaika
msiishike. Basi waliposikia maneno haya, wakachomwa
mioyo, wakamsagia meno. Lakini yeye akijaa Roho
Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni,
akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama upande
wa mkono wa kuume wa Mungu. Akasema, Tazama! Naona
mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama
mkono wa kuume wa Mungu. Wakapiga kelele kwa sauti
kuu, wakaziba masikio yao, wakamrukia kwa nia moja,
wakamtoa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao
mashahidi wakaweka nguo zao miguuni pa kijana mmoja
aliyeitwa Sauli. Wakampiga kwa mawe Stefano, naye
akiomba, akisema, Bwana Yesu, pokea roho yangu. Akapiga
magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi
hii. Akiisha kusema haya akalala. Na Sauli alikuwa akiona
vema kwa kuuawa kwake.” [Mate 7:51-60]
UHURU WA KWELI 15
Katika eneo hili hatuoni Stephano akiwaombea laana
waliompiga kwa mawe. Tena hatuoni akielekeza macho
yake kwa wale waliokuwa wakimpiga kwa mawe. Katikati ya
maumivu makali Stephano alisamehe na kusema. “Tazama
naona mbingu zimefunguka na mwana wa Adamu
amesimama mkono wa kuume wa Mungu”. Kwa sababu
Stephano alijua tumaini lake liko mikononi mwa Mungu,
huenda Stephano alisema kwanini iwe hivi? Lakini Stephano
alikua yuko mtetezi wangu Yesu Kristo. Na Yesu yupo tayari
hata katika magumu unayopitia kukuvusha na
kukustahilisha, kukufanya kuwa mtakatifu na mwenye haki.
Yesu amponya mtu aliyekuwa na udhaifu wa kupooza
miaka thelathini na nane.
“Baada ya hayo palikuwa na sikukuu ya Wayahudi; naye
Yesu akakwea kwenda Yerusalemu. Na huko Yerusalemu
penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa
Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano. Ndani ya
hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala,
vipofu, viwete, nao waliopooza, [wakingoja maji yachemke.
Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka,
akaingia katika ile birika, akayatibua maji. Basi yeye
aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona
ugonjwa wote uliokuwa umempata. Na hapa palikuwa na
mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini
UHURU WA KWELI 16
na minane. Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya
kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka
kuwa mzima? Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina
mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati
ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu.
Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende.
Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro lake,
akaenda. Nayo ilikuwa ni sabato siku hiyo.” [Yoh 5:1-9]
Huyu kiwete alikuwa amekaa birikani kwa mda wa miaka
thelathini na nane, ni rahisi sana kukata tamaa. Unaweza
ukawa na tatizo lakini huenda hujawahi kabisa kusubiri kwa
mda mrefu namna hii kama huyu mgonjwa. Huenda aliona
yeye ndio dunia nzima inamuonea, huenda alijiuliza swali
juu ya ugonjwa wake kwanini iwe hivi? Lakini alipokutana
na Mkuu Yesu Kristo alimwambia sina mtu wa kunitia
birikani, kwa sababu kuna watu hutangulia mbele yangu na
kuponywa. Fikiria ni kwa kiasi gani alikuwa ameathirika,
lakini Yesu alimwambia simama jitwike godoro lako uende,
na yule mtu akaponywa siku ile. Inawezekana kabisa
nawewe kunaeneo unaona giza ni tatizo la mda mrefu sana
na inawezekana umewategemea watu wakusaidie lakini
haijawezekana. Inawezekana umekuwa na matumaini
kuwa kiko kitu kitakusaidia kuvuka hapo lakini ni kwa mda
mrefu sasa haijawezekana. Yesu anasema huruma zake
UHURU WA KWELI 17
hazikomi yeye anampa kila mwenye kiu chemichemi ya maji
ya uzima wa milele bure. Kwa hiyo, ukimuamini na
kumwabudu yote yatakuwa yako (Luk 4:7, Ufu 21:6, 22:1,
22:17).
UHURU WA KWELI 18
Tathmini kupitia maswali kutoka katika Sura ya Kwanza
1: Kutokana na sura hii ulevi ni nini?
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………
2: Kwanini Yuda hakupaswa kujinyonga?
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………
3: Namna gani ya kutoka kwenye ulevi wa aina zifuatazo?
(i)Ulevi wa ugonjwa uliokaa mda mrefu
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………
(ii)Ulevi wa kupoteza mali, fedha na watu uliowapenda
UHURU WA KWELI 19
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………
(iii)Ulevi wa kukataliwa na kupingwa katika
kazi/huduma/karama/kipawa ulichopewa na Mungu
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………...
(iv)Ulevi wa kudharauliwa na kukataliwa na jamii yako
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
UHURU WA KWELI 21
SURA YA PILI
KWANINI NIUISHI UKALE
kale ni kawaida ya kuishi katika desturi, mila, mapokeo
au hali ya uzamani katika mazingira yaliyobadilika au
kuboreshwa zaidi. Ni kuishi kwenye mazoea ya hali ya ulevi
wa dhambi, kufeli, hali ngumu ya maisha. Nataka nikuulize
hili swali la msingi wewe uliyeshika kitabu hiki na kukisoma
tena kwa maandishi ya wino mzito, kwanini uishi ukale?
Unafikiri kwanini unaona huwezi kutoka kwenye shida uliyo
nayo? Kwanini unakaa kwenye ulevi wa kutojibiwa haja
yako kwa mda mrefu?
Inawezekana unaona umekufuru (umemkufuru
Mungu)
Inawezekana unakiri umeharibikiwa. Kwa hiyo,
huwezi kufanikiwa
Inawezekana unashuhudiwa huwezi kusamehewa
Inawezekana unashitakiwa ndani yako
(kuhukumiwa)
Kama nilivyo kuuliza swali kwa maandishi ya wino mzito
nataka nikujibu swali kwa maandishi ya wino mzito kuwa
inawezekana kuishi upya! Kutokea kwenye;
U
UHURU WA KWELI 22
Utimilifu wa kazi ya msalaba wa Kristo
Wingi wa neema ya Kristo
Upendo wa Kristo
Utimilifu wa kazi ya msalaba wa Kristo.
Ili kufikia kiwango cha utimilifu unaoutaka kwenye maisha
yako lazima uamini utimilifu wa kazi ya msalaba wa Kristo.
Jitihada za kutoka kwenye ulevi mbaya wa kiuchumi,
magonjwa, uzinzi, kukataliwa, kudharauliwa zinatakiwa
kujengwa kwenye msingi wa utimilifu wa kazi aliyoifanya
Kristo msalabani. Lifahamu jambo hili kuwa Kristo alijitahidi
kuitimiza sheria yote ili utoke katika hali ya utumwa wa
laana ya sheria na wa ulevi wa kila aina ambao Shetani
ameendelea kukushitaki kuwa huwezi kutoka. Shetani
anajua Kristo alichokifanya msalabani ndio maana anataka
kukukandamiza kifikra ili usiweze kutoka katika hali mbaya
uliyo nayo. Shetani alishabaki kuwa ni mshitaki wetu,
maandiko yanasema hivi;
“Mwe na kiasi na kukeshsa; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi,
kama simba aungurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta
mtu ammeze” [1Pet 5:8]
Shetani hawezi kuja kukusifia kwa jambo lolote jema
ulilofanya ndio maana ukifanya dhambi au kosa
UHURU WA KWELI 23
anakukandamiza zaidi na kukuwekea mzigo mzito moyoni
mwako. Kusudi lake ni kukumeza ili usiweze kusogea mbele
za Bwana wala kurejea kwa Bwana Yesu. Lengo la Shetani
kukukandamiza ufahamu sio ili urudi kwa Bwana lengo lake
uendelee kukaa kwenye hali ya dhambi uliyonayo ndio
maana ukikosea utaona ndani yako anaanza kukuhukumu.
Mfano;
Ukikosea utasikia wewe ni Mkristo wa namna gani
anafanya hivi na anaenda kanisani?
Wewe ni mtu wa namna gani? Yaani unajiita umeokoka
na unafanya hivi?
Ivi wewe ni mtumishi wa Mungu kweli?
Na hii ndio sababu kubwa ndani yako unaona umemkufuru
Mungu, unakiri umeharibikiwa, unashuhudiwa huwezi
kusamehewa, unashitakiwa umehukumiwa. Mpendwa
unatakiwa kujua Shetani anapigana vita zake kwa akili
sana, hakuna vita ngumu kama Shetani akiamua
kukugandamiza kiufahamu. Hasa katika Vita ya kutoka
kwenye hali mbaya/ulevi wa aina yoyote.
Ni lazima tujue namna ambavyo tunaweza kushinda nguvu
ya mashitaka ya Shetani kwenye maisha yetu kwa
kuendelea kutenda kwa haki kama vile Mungu
alivyotufanya wenye haki katika Yesu Kristo ili tuishi katika
haki yake. Ni mapenzi ya Mungu tuishi maisha ya utakatifu,
UHURU WA KWELI 24
ni mapenzi ya Mungu tuishi maisha yenye baraka na
mafanikio. Kwa kuwa tunaishi katika mwili yako makosa
huwa yanayotokea kwenye maisha yetu. Tatizo kubwa
linakuja ni pale ambapo umekosea na kushindwa kutoka
kwenye makosa/dhambi.
Ndio maana utaona kuna watumishi wa Mungu wengi
waliacha utumishi, kuna wengine walikuwa wanamcha
Mungu na wameokoka waliacha imani (wokovu). Kwa
sababu ya mashitaka ya Shetani juu ya yale waliyoyafanya.
Shetani utaona mara nyingi anawasemesha kwenye
fahamu zao kuwa huwezi kuendelea kumtumikia
Mungu/kumwabudu Mungu ni bora uache kumtumikia
Mungu. Vita ya namna hii huwezi kuishinda tu kwa kufanya
maombi ya kuvunja mapepo na majini ama mizimu,
pamoja na kufanya maombi ya mfungo nilazima utumie
silaha inayozidi silaha anayoitumia Shetani ili kumshinda.
Ndio maana Paulo aliwaambia Wakorintho hivi;
“Maana ingawa tunaenenda kwa jinsi ya mwili, hatufanyi
vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za
mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha
ngome) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka,
kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila
fikra ipate kumtii Kristo” [2Kor 10:3-5]
Paulo alisisitiza sana kuwa pamoja na kwamba tunaenda
kwa jinsi ya mwili, vita zetu hazifanyiki kwa jinsi ya mwili
UHURU WA KWELI 25
yaani jitihada, juhudi za kimwili kutoka kwenye ulevi wa
aina yoyote. Nahimizwa na Roho Mtakatifu nirudie
kukuandikia mstari huu; {tukiangusha kila mawazo na kila
kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu} kazi ya
Shetani ambayo anaifanya kwa kasi kubwa, na imepoteza
wengi kwenye ulimwengu huu wa sasa wa kumuabudu
Mungu ni kuinua ufahamu kandamizi wenye mlengo wa
kupinga kazi kubwa aliyoifanya Mkuu Yesu Kristo
Msalabani.
(Namshukuru Mungu, Roho Mtakatifu kwasababu kitabu
hiki kimekufikia mkononi mwako, kupitia ufunuo huu
uwekwe huru, kifikra na kuishi maisha ya utakatifu, ustawi,
kuinuliwa na ushindi daima). Tunaweza kushinda vita hii ya
kupinga na fikra za Ibilisi kwa kuamini kazi kamilifu ya
msalaba aliyoifanya Kristo, hii itapelekea kuwa na mambo
yafuatayo:-
Kuwa na imani sahihi
Kuondokana na hukumu/hatia ya Shetani
Nguvu ya fikra chanya
Kuwa huru
Ili tuweze kuamini kazi kamilifu ya msalaba ni lazima tujue
yafuatayo:-
Msalaba ulikuwa na kazi gani
Aliyeubeba msalaba ni nani
UHURU WA KWELI 26
Kwanini Mungu alitumia njia ya msalaba tu ili
kumponda Shetani kichwa
Kwanini zilihitajika juhudi za Yesu kuikamilisha kazi ya
msalaba
Msalaba ulikuwa na kazi gani?
Napenda ufahamu kuwa msalaba kazi yake ilikuwa ni
kumkamilisha mwanadamu, kutoka agano la kale kuingia
agano jipya ambalo maandiko yanashuhudia kuwa ni agano
imara. Mwanadamu ambaye alikuwa anaonekana kwenye
agano la kale ni muasi, mwenye dhambi, mwenye laana,
asiye na haki, Kupitia Msalaba wa Kristo Yesu akamilishwe
na kuingizwa agano jipya kuwa mwanadamu mtakatifu,
mwenye baraka na mwenye haki, aliyetukuzwa asiye na
mawaa wala hatia (Rum 5:12-21, 8:29-30 Efe 1:3-6). Ni kwa
kazi ya msalaba tu! Mwanadamu anaweza kuwa mtakatifu,
mwenye baraka na haki ya Mungu. Natamani uelewe hili
kwa msisitizo wa Roho Mtakatifu kuwa,
Ukiingizwa kwenye agano jipya ni agano lilio bora zaidi,
kujisimamisha katikati ya maagano mawili (agano la kale
na agano jipya) matokeo yake ni kuwa na imani isiyo sahihi.
UHURU WA KWELI 27
Kuna wakati fulani ukiwauliza Wakristo tabia za Mungu ni
zipi, kumetokea mtafaruko mkubwa kwa Wakristo kujibu
tabia za Mungu kwa maoni tofauti tofauti. Utakuta
wengine wanakwambia Mungu anaghadhabu sana,
wengine wanasema anahuruma sana, wengine wanasema
kuna dhambi ukifanya hauwezi kusamehewa kabisa na
kutengwa na Mungu, kuna wengine wanasema hakuna
dhambi isiyosameheka.
Naomba leo ujue hili wazi kwamba Wakristo wengi
wanachanganya tabia halisi za Mungu kwa sababu hawajui
tabia halisi za Kristo. Kristo alikuja kuanzisha agano jipya,
kazi yake timilifu inapatikana kwenye utimilifu wa kazi ya
msalaba. Kupitia kazi hiyo utamfahamu Mungu jinsi alivyo
kwa sababu Yesu alisema; Mimi ndimi njia, na kweli, na
uzima mtu haji kwa Baba ila njia ya mimi (Yoh 14:6). Ukiwa
ni Mkristo unayesoma kitabu hiki naandika kwa maandishi
ya wino mzito kuwa “Ili ufahamu tabia za Mungu ni lazima
ufahamu tabia za Yesu Kristo”
Kristo alikuja kufunua tabia halisi za Mungu akiwa duniani.
Biblia inashuhudia kuwa yaliyokuwa yakifanyika agano la
kale ilikuwa ni kivuli cha mambo yanayokuja yaani
kuundwa kwa mfumo mpya (agano jipya). Maana yake
tunatakiwa kutembea katika mfumo mpya/agano jipya.
Utasikia mtu anakiri ameokoka lakini mtu huyo mwisho wa
siku ataka kutembea na mfumo wa sheria za agano la kale.
UHURU WA KWELI 28
Agano jipya ni kama mkataba mpya japokuwa agano jipya
la Kristo ni zaidi ya mkataba kwakuwa halina mwisho
tutatembea nalo mpaka mwisho wa ulimwengu huu (ni
agano la milele).
Mkataba wowote unaposainiwa huwa na kanuni za
kuufuata. Inawezekana wanaohusika ni watu wale wale
waliokuwa na mkataba wa mwanzo. Mkataba mpya
ukisainiwa ujue kuna mambo mapya yanawekwa na
tunatakiwa kutembea na mkataba huo. Kristo kufa
msalabani na kumwaga damu yake ilikuwa ni ishara ya
kuingia kwenye agano jipya ndio maana Paulo aliwaambia
Waebrania kuwa;
“Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza
kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na
kuchakaa ki karibu na kutoweka” [Ebr 8:13]
Na kupitia damu ya Yesu Kristo tuliingizwa ndani ya agano
jipya kwa sababu hakuna agano pasipo kumwaga damu.
Kupitia damu ya Yesu Kristo tuliingizwa kwenye agano jipya
lililobora (Ebr 9:22-28)
Kama tuko kwenye agano jipya la Kristo uwe na uhakika
kuna mambo yamebadilika. Biblia inashuhudia kwamba
agano jipya limelifanya lile agano la kwanza (agano la kale)
kuwa kukukuu na kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki
karibu na kutoweka. Sisi kama tuliookoka (Tulio ndani
UHURU WA KWELI 29
Kristo) yaani ndani ya agano jipya la Kristo lazima kuna
namna mpya ya kutembea nalo. Huwezi ukawa
umeanzisha mkataba mpya wenye namna mpya za
kutembea nazo wakati huo huo unataka kufuata kanuni za
zamani.
Mfano katika mkataba wa kwanza wa biashara katika
kampuni uliyoajiriwa uliokuwa nao ulikuwa unatakiwa
kutoa dola mia kila mwaka na kulipa dola kumi kila mwezi
ili kukamilisha miadi ya biashara mliyoweka na muajiri
wako. Inatokea kila mwezi unaotakiwa kurejesha dola kumi
kiwango chako cha kufanya marejesho hakifikii dola kumi
kwa mwezi. Wakati fulani unawasilisha dola 2, wakati
mwingine dola 1 wakati mwingine unashindwa kabisa
kuwasilisha marejesho ya dola katika kampuni. Inapofikia
wakati wa mwisho wa mwaka katika dola mia moja
unawasilisha dola saba tu katika kampuni.
Wakati mwingine miaka mingine hakuna marejesho yoyote
ya dola katika biashara. Muajiri wako anaamua kuweka
mkataba mpya na wewe na kukwambia deni lote la nyuma
nimekulipia nataka tuanzishe mkataba mpya na wewe.
Sasa hautalipia gharama yoyote ile ili kupata hisa
unazozihitaji kazi yako itakuwa ni kupanua mipaka ya
biashara na badala yake kampuni itawajibika kukulipa dola
mia kila mwezi na dola elfu moja kwa kazi tu ya kupanua
mipaka ya biashara ya kampuni. Hii ni ajabu sana! Hii ni
UHURU WA KWELI 30
habari njema! Lakini jambo la ajabu sana ni kwamba wewe
unataka uendelee na mkataba ule ule uliopita unataka
ulipie deni ambalo huwezi kulilipa na pia uendelee kufanya
marejesho kwenye kampuni badala ya ya wewe kulipwa na
kampuni.
Hivi ndivyo walivyo Wakristo wa sasa inasikitisha sana!
Yesu alipoangikwa msalabani alitangaza kuwekwa huru na
dhambi zetu zote na kulipa deni yote ya dhambi tuliyokuwa
tunadaiwa, akatufutia makosa yote na kila uovu. Kristo
alitutoa katika hali ya utumwa ya kulipa gharama ya
makosa yetu tunayofanya na kutufanya kuwa wafalme,
makuhani, matajiri. Lakini bado wewe unataka kulipa
gharama ya deni ambalo kwanza hukuweza kulilipa
mwanzo na bado unang’ang’ania kukaa kwenye utumwa
wa dhambi.
Inasikitisha sana, fikiri kama ni wewe uko kwenye nafasi ya
Yesu ni namna gani ungekuwa unajisikia. Naamini kati ya
mambo ambayo yanahuzunisha sana ni watu kuishi ndani
ya utumwa wakati kiuhalisia ni wafalme na kulipa gharama
ya dhambi, makosa na uovu wakati yalishalipiwa.
Hatutakiwi kabisa kuishi maisha waliyokuwa nayo agano la
kale maana sisi tumefanyika kuwa agano liliobora zaidi ya
agano lile la kwanza. Kwa Imeandikwa hivi;
UHURU WA KWELI 31
“basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano
lililo bora zaidi” [Ebr 7:22]
Agano alilolifanya Mungu kupitia Yesu Kristo ni bora kuliko
agano la kwanza (agano la kale). Kama sio bora huu mstari
usingeandikwa kwenye biblia kama vile ambavyo yako
mambo mengi yaliyotendeka na Yesu Kristo, mitume na
manabii na hayakuandikwa. Roho Mtakatifu kuuruhusu
huu mstari kupitia mtume wake Paulo kuuandika ni kwa
sababu alijua una matokeo makubwa.
Aliyebeba msalaba ni nani?
Kabla sijakwambia aliyebeba msalaba ni nani nataka ujue
maana ya msalaba.
Msalaba ni kujikana, kujikataa kujikinai.
“Akawaambia watu wote, Mtu ye yote atakaye kunifuata
na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku
anifuate” [Luk 9:23]
Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake kila mtu
abebe msalaba wake kwakuwa Yesu alikuwa hajafa bado
msalabani. Kwa lugha nyepesi walikuwa hawana uwezo wa
kuokoka. Lakini Petro alikuja kusema tumtwike Yeye (Yesu
UHURU WA KWELI 32
Kristo) fadhaa zenu zote maana hujishughulisha sana kwa
mambo yenu (2Pet 5:7).
Kwakuwa Kristo alikuwa alishateswa msalabani watu wote
walikuwa na uwezo wa kumtwika Kristo fadhaa zao zote.
Kwa maana rahisi kujikana ni kujikataa, Kristo alikufa
msalabani ili tusiendelee kukaa katika hali ya kukataliwa,
alikataliwa, alijikinai na kujikana Yeye ili mimi na wewe
tukubalike. Tusibebe laana yoyote wala aina yoyote ya
mateso.
Msalaba ni upatanisho
Msalaba huo unamstari wa ulalo na wima. Mstari wa ulalo
unaonyesha upatanisho kati ya watu na watu. Mstari wa
wima unaonyesha upatanisho kati ya wanadamu na
Mungu. Kristo alitupatanisha kwa njia ya msalaba.
Aliyebeba msalaba ni nani?
Aliyebeba msalaba ni Kristo. Wote tulioungwa na Kristo
hatutakiwi kubeba matatizo yetu, hata hivyo hatukuweza.
UHURU WA KWELI 33
Tunatakiwa tumbebeshe Kristo kwa sababu Yeye aliweza
kubeba matatizo yetu. Usijibebeshe matatizo yako kwa
sababu huwezi mtwike Kristo kwa sababu Yeye anaweza
kubeba ulevi wa uzinzi, wizi, hali mbaya ya uchumi, na kila
aina ya ulevi Yeye anaweza kubeba. Hakuna mwanadamu
anayeweza kushinda dhambi kwa nguvu zake, hakuna
mwanadamu anayeweza kushika sheria asivunje hata
moja. Kuishi kwa sheria ni kuishi chini ya laana huwezi
kuishi chini ya sheria ukabarikiwa vivyo hivyo huwezi kuishi
katika Kristo ukalaaniwa (Gal 3:13).
Dhambi hupata nguvu unapoamua kuishi kwa sheria,
Shetani ni furaha yake kukuona unaishi kwa sheria kwa
sababu mara zote hutumia sheria kukushitaki kuwa
umekosea na haufai kuendelea kuwa na uhusiano na
Mungu. Naomba uelewe sheria sio tu amri kumi za Mungu
sheria ni mfumo wa kanuni ambao mtu amejiwekea
zinazomuwekea kuishi kwa kiwango fulani ili kuweza
kufikia utakatifu, kukubalika mbele za Mungu au katika
mafanikio yoyote yale.
Kwa mfano unaweza kujiwekea mfumo wa maisha
kwamba ili nifanikiwe nilazima nifanye jambo fulani.
Kuweka kanuni fulani, mipango au mfumo wa kufuata ili
ufanikiwe ni jambo jema. Lakini hatutakiwi kuamini
kufanikiwa kupitia kanuni, mipango au mifumo ya maisha
tunayoishi. Kwa sababu kwa kufanya hivyo tutamzuia
UHURU WA KWELI 34
Mungu kufanya zaidi ya uwezo tulio nao. Haki ambayo ni
kibali cha mtu kusimama mbele za Mungu inaweza kuja
kwa matendo ya sheria lakini pia inaweza kuja kwa njia ya
Yesu Kristo, lakini biblia inatuhakikishia haki ya Kristo ni
bora zaidi kuliko haki zetu za matendo ya sheria (matendo
mema). Tunahesabiwa haki ya Mungu kwa njia ya imani
iliyo katika Kristo Yesu.
Yaani haki ya matendo ya sheria maana yake unapata kibali
cha kupokea vitu vya Mungu kwa sababu ya juhudi ya
kuishika sheria. Haki hii kuna vitu itakuzuia usivipate
kwenye maisha yako ndio maana Kristo alisema;
“Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo
haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe
katika ufalme wa mbinguni” [Math 5:20]
Yesu alikuwa anamaanisha kwamba ipo haki iliyozidi haki
ya waandishi na mafarisayo ambayo ni bora zaidi kuliko ya
waandishi na mafarisayo. Angalia aina ya haki waliyokuwa
nayo mafarisayo na waandishi ilikuwa ni haki ya matendo
ya sheria. Yaani kufunga mara mbili kwa juma, kuomba
kutoa zaka, kuwasaidia wahitaji nk. Mambo haya
niliyoyataja ni mambo mema sana na tunatakiwa
kuyafanya.
Tatizo wengi wanayofanya haya, wanafanya kama sheria
na sio kwa moyo wa kupenda. Yaani wanafanya
UHURU WA KWELI 35
wakitegemea malipo kutoka kwa Mungu kwa matendo yao
na wanayaishi hayo kwa imani wakitegemea kuwa
watakuwa watakatifu au watafanikiwa kwa sababu ya hayo
wanayoyafanya. Ndio maana waandishi na mafarisayo
walikuwa wanajivunia haki ya matendo yao ya sheria
wakasahau yupo Yesu anayeweza kuwakamilisha zaidi
kupata haki iliyo bora zaidi ya haki ya matendo yao ya
sheria. Ndio maana Yesu alitoa mfano huu;
“Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja
Farisayo, wapili mtoza ushuru. Yule Farisayo akasimama
akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa
kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi,
wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi
nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato
yangu yote. Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali,
wala hakuthubutu kuinua macho yake mbinguni, bali
alijipiga piga kifua akisema, Ee Mungu uniwie radhi mimi
mwenye dhambi. Nawaambia, huyu alishuka kwenda
nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa
maana kila ajikwezaye atadhiliwa, na ajidhiliye
atakwezwa” [Luk 18:10-14]
Kumbe haki yetu inatakiwa izidi haki ya mafarisayo ambayo
ni ya matendo ya sheria.Fanya jambo jema katika maisha
yako na kuliishi lakini hiyo utambue kuwa sio sababu
inayokufanya kuwa mtakatifu sana,kufanikiwa, wala
UHURU WA KWELI 36
kuhesabiwa haki mbele za Mungu. Mungu anataka uamini
kufanikiwa katika Kristo Yesu zaidi ya kila jambo jema
unalolifanya.
Haki tunayotakiwa kuwa nayo inatakiwa izidi haki ya
mafarisayo ya matendo ya sheria ambayo hupatikana
kupitia Kristo Yesu.
Ndio maana Yesu aliendelea kuwaambia watu mmesikia
watu wa kale walivyoambiwa, usiue, na mtu akiua
itampasa hukumu. Bali mimi nawaambieni, kila
amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu
akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu
akimwapiza, itampasa jehanum ya moto. Maana yake Yesu
aliitimiliza sheria jinsi ilivyotakiwa kuwa na kuwaeleza
kuwa bila Yeye (Yesu Kristo) mtu hawezi kuitimiza sheria
inavyopaswa. Kwa sababu katika yeye kuna ukamilifu wa
sheria yaani Yeye ni kilele cha sheria ndio maana
tunatakiwa kuishi katika yeye (Yesu Kristo).
Kwa sababu sheria inakikomo, inakiwango chake cha
mwisho, juhudi au uwezo binafsi wa mwanadamu kumtii
Mungu unakikomo chake. Ndio maana maandiko
yanasema;
“Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye
ahesabiwe haki” [Rum 10:4]
UHURU WA KWELI 37
Maana yake tunahesabiwa haki iliyobora zaidi ya Kristo
Yesu kwa njia ya imani. Ukimuamini Kristo unahesabiwa
haki, haki hii haitokani na matendo ya sheria haki hii
inatokana na Mkuu Yesu Kristo. Kwakuwa Kristo aliitimiza
sheria yote pale msalabani ili usiishi tena ndani ya laana ya
dhambi, kukataliwa na mateso.
Kwanini Mungu alitumia njia ya Msalaba tu kumponda
Shetani kichwa?
Nikukumbushe habari hii kabla ya Yesu kuanza kuteswa
alipokuwa bustani ya Gethsemane, akawaambia wanafunzi
wake, Roho yangu inahuzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni
hapa mkeshe pamoja nami, alipoanguka kifulifuli, akaomba
akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee
kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako
yatendeke (Luk 22:40-42).
Maana yake ilikuwa ni mapenzi ya Mungu, Yesu Kristo kufa
msalabani. Kwenye mapenzi ya Mungu kuna ukamilifu,
ndio maana Yesu alisema sio kila aniambiaye Bwana,
Bwana atakayeingia katika ufalme wa mbinguni. Maana
yake mapenzi ya Mungu ni ukamilifu. Mungu alimtoa Yesu
kufa msalabani kwaajili ya kututoa kwenye laana na mizigo
ya dhambi, kila aina ya ulevi na kutuondoa kwenye laana
ya sheria. Nguvu ya dhambi ilikuwa ni sheria ndio maana
UHURU WA KWELI 38
Mungu aliamua kumwondoa mwanadamu kwenye huo
mfumo na kumwacha aishi tu kupitia Mwanawe mpendwa
Kristo Yesu. Ndio maana imeandikwa hivi;
“maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila
akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote” [Yak
2:10]
Sheria nguvu yake ilikuwa katika kukosea. Ikitokea
umekosea katika neno moja wema wote ulikuwa
unabatilika kuwa ubaya. Na huu ndio mfumo ambao
Shetani aliupenda kuuishi na ndio maana ukikosea anaanza
kukushitaki ndani yako. Ashukuriwe Mungu kwa sababu
alituondoa kwenye laana ya mashitaka ya Shetani kupitia
Kristo Yesu. Roho Mtakatifu alikuja kutushuhudia sheria
yake katika Kristo Yesu ambayo ndiyo inayotuweka huru
mbali na sheria ya dhambi na mauti na kutufanya kuwa
watakatifu kwa neema yake(Rum 8:2, Tit 2:11-12).
Tangu mwanzo wa kuumbwa kwa ulimwengu ilikuwa ni
mpango wa Mungu tuishi katika Kristo Yesu.
Katikati ya bustani ya Edeni kulikuwa na mti wa ujuzi wa
mema na mabaya pamoja na mti wa uzima. Mungu
alimkataza Adamu kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema
na mabaya ambao ulikuwa ni ishara ya matendo ya sheria
(Mwanz 2:17). Mungu alitaka mwanadamu aishi tu kupitia
mti wa uzima ambao ilikuwa ni picha ya Yesu Kristo. Ndio
UHURU WA KWELI 39
maana Mungu aliwazuia wasiiendee njia ya matunda ya
mti wa uzima (Kristo).
Mwanadamu alipokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema
na mabaya (sheria). Mungu aliwafukuza bustanini kwa
sababu mwanadamu alichagua mfumo mwingine kabisa
wa kuishi tofauti na ule alioukusudia tangu mwanzo.
Katikati ya bustani kulikuwa na mti wa uzima. Swali la
kujiuliza kwanini Mungu asingewaruhusu kula mti wa
uzima ili waishi milele? (Mwa 3:22-24) Jibu ni jepesi kabisa
Mungu hakutaka kuchanganya maisha ya matendo ya
sheria na wakati huo huo kuishi katika Kristo. Mungu
alitaka mwanadamu aishi katika Kristo peke yake ambao ni
mti wa uzima.
Ndio maana wakati huu hatutakiwi kuishi kwa sheria tena,
bali tunatakiwa kuishi katika Kristo Yesu. Kibali zaidi ya
matendo ya sheria hupatikana kwa njia ya msalaba tu. Ili
tuweze kufanikiwa zaidi ya mema tunayoyafanya ni lazima
tuishi katika Yesu Kristo na neema ya msalaba.
Kwanini zilihitajika juhudi za Yesu kuikamilisha kazi ya
msalaba?
Kristo alijitahidi kufuata kila sheria na kanuni zote. Ili sisi
tusiishi tena chini ya laana ya sheria na torati. Iliandikwa
kuwa Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwakuwa
UHURU WA KWELI 40
alifanywa laana kwaajili yetu; maana imeandikwa,
Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti (Gal 3:13).
Ilibidi ajitahidi kutukomboa kutoka kwenye laana ya torati
na sheria ili sisi tuwe huru tuishi tu kupitia Yeye (Kristo).
Kwani Mungu anashida na torati au sheria?
Mungu hana shida na torati au sheria kama jinsi ambavyo
Biblia inaeleza kuwa mti wa ujuzi wa mema na mabaya
(sheria) ni ishara ya sheria au torati. Kazi yake ilikuwa ni
moja tu kukuwezesha kujua mema na mabaya, na
kwakuwa mwanadamu alichagua mti wa ujuzi wa mema na
mabaya yaani kuishi kwa sheria. Mungu alimruhusu Musa
kuleta sheria kumi za Mungu. Ambazo hakuna hata mmoja
ambaye aliweza kuishi kwa hizo. Wengi walikuwa
wanafuata baadhi nyingine wanazivunja. Mpaka wakati
Kristo alipokuja kutukomboa hakuwepo hata mmoja
aliyeweza kuzifuata kikamilifu. Ambapo maandiko
yanasema ikiwa mtu ameishika sheria akajikwaa katika
neno moja amekosa juu ya yote. Maana yake tulikuwa tuko
chini ya laana na hukumu ya sheria.
Ndio maana Mafarisayo na Waandishi walikuwa
wanajitahidi kufuata sheria lakini bado hawakuweza kufikia
kiwango cha kukubalika na Mungu alikokuwa anahitaji.
Ndio maana Kristo (Mungu aliyehai), Elohim, Mungu
UHURU WA KWELI 41
anayeishi akaamua aje mwenyewe kusudi aitimize sheria
yote ili Yeye akae kwenye nafasi yetu na sisi tukae kwenye
nafasi yake. Kristo alipokuja ulimwenguni alijifanya hana
utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa mfano wa
wanadamu; akajinyenyekesha akawa mtii (mwenye juhudi)
hata mauti ya msalaba. Kwahiyo Kristo ilibidi ajitahidi
kutimiza sheria yote ili sisi tutembee ndani ya neema yake
na tuwezeshwe ndani ya neema yake.
Wingi wa neema ya Kristo Yesu.
Neema ni kustahilishwa kusiko stahili, kibali au mafanikio
unayoyapata pasipo kazi au matendo, juhudi au sheria.
Kristo alipokuja duniani alikuja akiwa na neema na kweli.
Maandiko yanasema hivi;
“Kwakuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na
kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo” [Yoh 1:17]
Kwa maana hiyo ukweli uko upande wa neema. Yesu
alipokuja alikuja kuachilia neema ili watu wajitosheleze
kwa neema yake. Watu wengi wanaamini katika neema
lakini hawaamini katika utoshelevu wa neema ya Kristo.
Wakristo wengi wanaamini katika kuchanganya neema ya
Kristo na matendo yao, sheria au kanuni. Wakati Kristo
alikuja kwaajili ya kumsaidia mwanadamu aondokane na
hali ya kutumainia juhudi binafsi ili kupokea uponyaji,
UHURU WA KWELI 42
imani au mafanikio. Kwa sababu kama ikiwa kwa neema
haiwi kwa matendo tena na kama ikiwa kwa matendo haiwi
neema tena (Rum 11:6).
Neema haiusishi matendo kabisa, inahusisha kwenye
kuwezeshwa zaidi kupitia utimilifu wa Kristo wa kile
alichokifanya pale msalabani. Ndugu yangu lazima uelewe
kwamba tuko kwenye agano la neema na sio agano la
matendo ya sheria (agano la kale). Na hii ndiyo
ilimsababisha Kristo kufa pale msalabani lengo lake ni
kukuweka huru kabisa na uhuru huu utaanza kuuona
kwenye maisha yako na mipaka yako kwenye maisha yako
itavunjika. Ukiambatana na imani hii utaanza kutawala
dhambi kwa sababu dhambi haitakuwa na uwezo wa
kukutawala, utaweza kutawala katika kila eneo kwenye
maisha yako (Rum 5:17, 6:14). Baada ya kuanza kuweka
imani hasa kwenye kile Kristo alichokifanya na sio
unachokifanya utaona matunda yake. Ndio maana Paulo
aliwaambia Wagalatia hivi;
“Siibatili neema ya Mungu; maana, ikiwa haki hupatikana
kwa njia ya sheria, basi Kristo alikufa bure” [Gal 2:21]
Maana yake haki yako inabatilishwa kwa matendo ya
sheria. Tukisema ili tupokee uponyaji, imani, msamaha wa
dhambi au mafanikio nilazima tufuate kanuni fulani
ambazo tumejiwekea tunaibatili neema ya Kristo na ile
Kristo kufa msalabani ilikuwa ni bure.
UHURU WA KWELI 43
Kuwa ndani ya agano la neema ni kutojihesabia kabisa
juhudi zako na kuhesabia hasa juhudi za Kristo alizozifanya
pale msalabani kwa ajili yetu.
Shetani hapendi kabisa kuona mtoto wa Mungu imani ya
kuamini utimilifu wa kazi aliyoifanya pale msalabani.
Shetani anapenda upewe haki, utakatifu, mafanikio kwa
kuangalia kile unachokifanya na sio utoshelevu wa neema
ya Kristo. Shetani anajua kufanya hivyo utakuwa
umejichorea mipaka mwenyewe ya kupokea zaidi katika
jambo lolote unalolitaka litokee kwenye maisha yako kwa
ukamilifu. Shetani anajua ukiamini utimilifu wa kazi ya
msalaba aliyoifanya Yesu Kristo huwezi kutimiza kusudi la
Mungu alilokuwekea ndani yako. Ukiamua leo kuanza
kuamini kuanzia saa hii kupitia ukamilifu wa kazi ya Kristo
msalabani utaanza kuona vifungo vyote kwenye maisha
yako vimefunguka kabisa.
Mipaka ya juhudi zako binafsi inavunjika na kuanzia hapo
utaanza kuona jinsi ambavyo unaanza kuakisi maisha ya
kimbingu ukiwa duniani. Shetani hapendi watoto wa
Mungu wawe na hii imani ndio maana katika makanisa
mengi unapoanza kufundisha habari ya neema watu
wanaanza kuwa na mashaka. Shetani anaweka hofu ndani
yao kwa sababu anajua ukiifahamu siri hii kwenye maisha
yako hautakuwa mtumwa tena katika kile unachokifanya,
UHURU WA KWELI 44
na utaanza kuona ustawi na mafanikio makubwa sana
kwenye maisha yako bila kutumia nguvu kabisa.
Kuwa ndani ya neema ni kuamini kupitia juhudi za Kristo
alizozifanya pale msalabani ni kamilifu kuliko kile chema
unachokifanya.
Kuwa ndani ya neema haimaanishi usifanye jambo lolote
kuhusu mafanikio yako, uponyaji wako au utakatifu. Kuwa
ndani ya neema ni kuacha kutumainia na kuamini kile
chema unachokifanya na kutumainia na kuamini zaidi kile
alichofanya Yesu msalabani. Kuwa na tabia njema ni jambo
jema sana lakini jua kuwa wewe ni Mtakatifu kwa sababu
ya kile alichofanya Yesu msalabani na si kwa sababu
yamatendo yako mema. Kiwango cha utakatifu ambao
Mungu aliutaka alikifunga kwa Yesu Kristo ndio maana
alitaka tuamini alichofanya Yesu Kristo, ili tutakapoamini
tuone matunda yake, matokeo yake katika macho ya damu
na nyama. Yesu Kristo ni Mungu aliyejifunua kwa umbo la
mwanadamu, alipoona matendo yetu yanatuchorea
mipaka katika viwango vya mafanikio tunavyotakiwa
kufika. Aliamua kushuka mwenyewe ili asimame kwenye
nafasi yetu kusudi yeye afanye kwa nafasi yetu ili kuondoa
mipaka iliyokuwa inatuzuia kwa kujitahidi ambako
hakukufaa kitu kuweza kufika pale Mungu mwenyewe
alitaka tufike.
UHURU WA KWELI 45
Mkuu Yesu Kristo aliamua kutimiza kila kitu ambacho
kilistahili tukifanye kwaajili yetu, na kwa namna hiyo
akatuondolea mipaka kabisa ya kufika tunakotakiwa kufika
bila juhudi wala jitihada binafsi. Kipindi hiki cha agano
jipya, yaani agano la neema huwezi jitetea tena kuwa
sijaweza fanya jambo fulani kwenye maisha yangu kwa
sababu nguvu, uwezo au juhudi zangu zilikuwa ndogo.
Kristo alifanya zaidi ya pale uwezo wako ulikoma kusudi
akufikishe kwa neema yake mwenyewe aliyoiachilia bure
pasipo kuangalia matendo yetu. Ndio maana maandiko
yanasema hivi;
“Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala
kwasababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi
wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika
uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo” [Rum 5:17]
Adamu alipoasi tulihesabiwa ni wenye dhambi sio kwa
sababu tulifanya dhambi ila kwa sababu Adamu aliasi
tuliingizwa kwenye mkumbo wa dhambi na dhambi
ilitutawala. Ndio maana tunahesabiwa watakatifu sio kwa
sababu ya matendo yetu ila ni kwa sababu ya kumwamini
Yesu Kristo. Ndio maana hakuna mtu anayeweza kujisifu
kwa matendo mema aliyonayo na asiokoke kwa sababu
atahukumiwa sio kwasababu ya mema anayoyafanya ila
kwa sababu hakuliamini jina la mwa na pekee wa Mungu
UHURU WA KWELI 46
(Yesu Kristo) [Yoh 3:18]. Matokeo ya dhambi ni mauti
ilitawala sasa unaona ni kwa jinsi gani ilikuwa mbaya.
Hali hii ndiyo inasababisha kila mtu amhitaji Kristo kwenye
maisha yake, huwezi kusema mimi sina dhambi kwakuwa
sikufanya. Yupo aliyefanya ambaye ni Adamu akakufanya
na wewe kuwa mwenye dhambi ukweli huu huwezi
kuukwepa. Ashukuriwe Mungu kwa sababu imekuwa ni
ajabu sana kuwa kupitia Yesu Kristo tulipokea wingi wa
neema na kipawa cha haki tulivipokea ambavyo
havikutokana na juhudi ya matendo yetu. Sasa utaona ni
kwa jinsi gani Mungu ni mwenye haki. Sisi ambao
hatukustahili kuhesabiwa dhambi kwa sababu ya dhambi
ya Adamu ndio ambao hatukustahili kupokea wingi wa
neema na kipawa cha haki katika Kristo Yesu.
Neema tuliyoipokea ilikuwa kutusaidia kustahilishwa
tusivyostahili na kipawa cha haki ambayo ni zawadi
tuliyoipokea inayotupa ujasiri wa kusimama mbele za
Mungu ili vitusaidie kutawala. Jinsi gani Mungu alivyo
waajabu yaani kupitia wingi wa neema na kipawa cha haki
vitusaidie kutawala. Kama ni hivyo basi tunahitaji kuufunua
sana uzuri wa wingi wa neema ya Kristo na kipawa cha haki
kwa wingi kwa kujifunza na kuyajaza maarifa yake moyoni
mwetu ili tuweze kutawala na kufikia kiwango cha imani ,
utakatifu na mafanikio kama vile Mungu anataka ifikie
UHURU WA KWELI 47
katika utimilifu wake wa kimo katika kumjua Yeye (Kristo
Yesu).
Kuwa ndani ya neema sio dhamana ya kuishi maisha ya
dhambi, lakini ni nguvu inayotusaidia kuishi katika haki,
kiasi na utakatifu.
Naomba utambue hili kuwa ndani ya neema sio kuishi
maisha yasiyo na mwelekeo, maisha yenye dhambi au
maisha yasiyo na nidhamu. Kinachotufanya tuwe na
kiwango cha utakatifu, haki,kiasi na nidhamu binafsi ni
neema pekee. Huwezi kufikia kiwango cha utakatifu ambao
Mungu anautaka kama uko nje ya neema. Huwezi kuwa na
nidhamu katika maisha nje ya neema. Ukijihesabia
utakatifu kwa kile unachokifanya hautaweza kwa sababu
juhudi zako ni bure mbele za Mungu pasipo imani ya
ukamilifu wa kazi ya Kristo Msalabani. Lazima ujikabidhi
kwenye neema ya Kristo halafu yeye mwenyewe ataachilia
utakatifu, nidhamu, kiasi na haki ambayo unatakiwa kuwa
nayo ambayo hii sio kwa sababu ya juhudi zako, bali kwa
sababu ya juhudi za Kristo msalabani. Maandiko yanasema
hivi;
“Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu
hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema” [Rum 6:14]
Tukiwa chini ya sheria ni rahisi kutawaliwa na dhambi.
Neema ya Kristo pekee ndiyo inayoweza kutusaidia
UHURU WA KWELI 48
kuitawala dhambi na kuishi katika utakatifu ambao Mungu
anautaka. Paulo aliandika hivi;
“Maana neema ya Mungu iwaokowayo wanadamu wote
imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa
za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa,
katika ulimwengu huu wa sasa; tukilitazamia tumaini lenye
baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu
mkuu na Mwokozi wetu” [Tit 2:11-13]
Neema ya kristo ipo kwaajili ya kutusaidia kuishi katika
utakatifu, haki na kiasi. Huwezi kuwa ndani ya neema hali
bado ukaendelea kuishi katika dhambi. Vivyo hivyo huwezi
kuwa na ndani ya neema na usistawi na kufanikiwa. Neema
inapokuwa nyingi kwako ndivyo kiwango cha kuwa na
uwezo wa kutenda mambo kinakuwa kikubwa na ndivyo
kiwango chako cha kutawala kinakuwa kikubwa. Ndio
maana neema ya Kristo Yesu inazidishwa katika kumjua
Yesu Kristo (2Petro 1:2 KJV) ili kuweza kufikia kiwango cha
utakatifu ambao Mungu anautaka ni kwa njia ya neema ya
Kristo na kumjua Yeye (Yesu Kristo).
Kipindi cha agano la kale watu walijitahidi kutenda
matendo mema kwa sheria lakini bado hawakuweza kufikia
kiwango cha utakatifu ambao Mungu anautaka. Ndio
maana Kristo aliamua kufa kwaajili yetu ali aachilie neema
ya Kristo itusaidie kufikia kiwango cha utakatifu ambao
Mungu anautaka. Ndio maana Paulo pamoja na kwamba
UHURU WA KWELI 49
alifanya kazi ya mhubiri wa injili kwa juhudi zote lakini
hakutumainia anachokifanya. Alitumainia zaidi neema ya
Kristo ndio maana aliwaambia Wagalatia hivi;
“Siibatili neema ya Mungu; maana, ikiwa haki hupatikana
kwa njia ya sheria, basi Kristo alikufa bure” [Gal 2:21]
Paulo pamoja na kuwa na juhudi na jitihada alizokuwa nazo
lakini bado hakutumainia juhudi na jitihada alizokuwa nazo
bado aliitumainia neema ya Yesu Kristo. Ndio maana
anasema siibatili neema ya Kristo, kwa sababu kuibatili
neema ya Kristo ni kumfanya kuwa Yesu Kristo alikufa
msalabani bure.
Kutembea ndani ya neema ya Kristo sio maisha ya uvivu,
uzembe au dhambi, bali ni maisha ya kukusaidia
kukamilisha kusudi la kuumbwa kwako kikamilifu.
Wa-Kristo wengi wanaamini kufikia kusudi la kuumbwa
kwao wanatakiwa kujitahidi sana, kujitesa na kupambana ili
waweze kufanikisha kusudi la kuumbwa kwao hapa duniani.
Haiwezekani kufikia kusudi la kuumbwa kwako kwa juhudi
zako, kujitesa, wala kupambana. Katika agano la kale kila
mmoja alijitahidi kuwa mtakatifu kwa matendo ya sheria
lakini bado hawakuweza. Ndio maana utawaona
Mafarisayo na Waandishi walikuwa wanajitahidi kufuata
sheria kwa juhudi sana lakini bado hawakuweza kufikia
utakatifu ambao Mungu aliutaka. Kwa maana hatuwezi
UHURU WA KWELI 50
kulifanya kusudi la Mungu kikamilifu, kuishi maisha ya
utakatifu ambao Mungu anautaka kwa matendo ya sheria.
Yesu Kristo alipokufa msalabani aliachilia wingi wa neema
na kipawa cha haki ili tuweze kutawala dhambi na kila kitu
tunachokihitaji.
Mungu anapenda tufanye kazi kwa juhudi zote, tujitahidi
kwa kadri tunavyoweza lakini tusitumainie uwezo wetu
binafsi, juhudi au jitihada tunazozifanya kwenye mafanikio
yetu ili tuweze kufikia Mungu anataka tufike. Mungu
anataka tuamini kwa asilimia zote kwenye neema yake tu
kwa sababu kupitia neema yake tunaweza kufika pale
ambapo Mungu anataka tufike au kufikia kiwango cha
mafanikio ambayo tulitamani kuona yanatokea kwenye
maisha yetu.
Upendo wa Kristo.
Paulo aliwaambia Warumi hivi:-
“Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki
au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?”
[Rum 8:35]
Paulo aliwaaambia Warumi ni jambo gani linaloweza
kututenga na upendo wa Kristo? Maana yake hakuna jambo
linaloweza kututenga na upendo wa kristo katika maisha
UHURU WA KWELI 51
yetu. Upendo wa Kristo uko pale pale, tuwe na shida au
adha upendo wa Kristo uko pale pale, tuwe na njaa au uchi
upendo wa Kristo uko pale pale, tuwe na hatari au upanga
upendo wa Kristo uko pale pale.
Tunatakiwa kujua upendo wa Kristo haupungui kwa sababu
ya shida au changamoto tunazokutana nazo. Chanzo cha
Kristo kuja ilikuwa kwa sababu ya upendo wake ndio maana
maandiko yanasema hivi;
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata
akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye
asipotee, bali awe na uzima wa milele” [Yoh 3:16]
Jambo la muhimu kutambua ni kuwa Mungu aliufunua
upendo wake kupitia Kristo. Aliona mwanadamu
alivyokuwa anapata shida katika hali ya dhambi na maisha
aliyokuwa nayo. Ndio maana Kristo alitupenda kwanza,
akatuchagua na kutuweka ndani ya ufalme wake.
Haijalishi ni eneo gani gumu unapitia inawezekana ni uzinzi
ndio unaokutesa, inawezekana ni uongo, inawezekana ni
ugonjwa umekutesa kwa mda mrefu kiasi ambacho
umeupa jina kuwa ni ugonjwa wako. Upendo wa Kristo uko
pale pale bado Kristo anakuhitaji kwenye ufalme wake kwa
sababu wewe ni wathamani sana.
UHURU WA KWELI 52
Kuwa mtu wa kuathiriwa na upendo wa Ki-Mungu
Watu wengi ukiwaambia kuhusu kuishi upendo wa ki-
Mungu kwenye maisha yao wanafikiri hawawezi kuwa na
upendo kama wa Mungu kwa sababu ni wa Mungu. Kama
ingekuwa upendo wa ki-Mungu katika Kristo Yesu
haiwezekani isingeandikwa kuwa;
“mkaenende katika upendo, kama Kristo naye
alivyowapenda ninyi tena akajitoa kwaajili yetu, sadaka na
dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato” [Efe 5:2]
Kwa hiyo, ni lazima tuwe na upendo kama alikuwa nao Yesu
Kristo ndio maana tumeagizwa kuenenda katika upendo
wake
Biblia katika agano jipya haitufundishi upendo wowote ule
isipokuwa upendo wa ki-Mungu. Upendo wa ki-Mungu
unaachilia ndani yako kwa njia mbili;
Kujifunza upendo wa Mungu kupitia Yesu Kristo
Upendo wa Mungu kumiminwa kwa njia ya Roho
Mtakatifu
UHURU WA KWELI 53
Kujifunza upendo wa Mungu kupitia Yesu Kristo.
Katika agano jipya Mungu ameudhihirisha upendo wa
Mungu kwenye maisha ya mwanadamu. Kwanza kwa
kumtoa mwanaye pekee. Maandiko yanasema
“Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili
auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika
yeye” [Yoh 3:17]
Kumbe Mungu alimtuma Mwana ulimwenguni ili asiwepo
wa kupotea. Siku zote Mungu anapenda ukae katika njia
sahihi. Mungu anapenda uishi katika afya njema na
mafanikio katika eneo ambalo unatamani ufanikiwe.
Upendo wa Mungu kumiminwa kwa njia ya Roho
Mtakatifu.
Paulo anasema hivi;
“na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu
limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho
Mtakatifu tuliyepewa sisi” [Rum 5:5]
Kwa hiyo, upendo wa ki-Mungu ili uweze kuwa sehemu ya
maisha yetu nilazima tujifunze kwa Roho Mtakatifu. Kwa
sababu maandiko yanasema pendo la Mungu limekwisha
kumiminwa ndani yetu.
UHURU WA KWELI 54
Tabia za Upendo wa ki-Mungu katika Yesu Kristo.
“Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo
hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti
mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili
yote. Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali
ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma;
yakiwapo maarifa, yatabatilika.” [1Kor 13:4-8]
Tuangalie mistari hii katika Biblia ya Habari Njema (BHND)
“Mwenye upendo huvumilia, hufadhili; mwenye upendo
hana wivu, hajidai, wala hajivuni. Mwenye upendo hakosi
adabu, hatafuti faida yake binafsi, wala hana wepesi wa
hasira; haweki kumbukumbu ya mabaya, hafurahii uovu,
bali hufurahia ukweli. Mwenye upendo huvumilia yote,
huamini yote, hustahimili yote. Upendo hauna kikomo
kamwe. Kama kuna vipaji vya kutangaza ujumbe wa
Mungu, hivyo vitatoweka siku moja; kama ni vipaji vya
kusema lugha ngeni, vitakoma; kama kuna elimu, nayo
itapita.”
UHURU WA KWELI 55
Tafsiri ya Biblia ya NENO (NEN), imeandikwa;
“Upendo huvumilia, upendo hufadhili, upendo hauoni wivu,
hauna majivuno, hauna kiburi. Haukosi kuwa na adabu,
hautafuti mambo yake, haukasiriki upesi, hauweki
kumbukumbu ya mabaya. Upendo haufurahii mabaya bali
hufurahi pamoja na kweli. Upendo huvumilia yote, huamini
yote, hutumaini yote, hustahimili yote. Upendo haushindwi
kamwe. Lakini ukiwepo unabii, utakoma; yakiwepo
maarifa, yatapita.”
Kutoka katika tafsiri hizi tunaweza kuorodhesha yafuatayo
kuhusu tabia za upendo;
Huvumilia
Hufadhili
Hauoni wivu
Haujidai (hauna majivuno)
Hauna kiburi
Haukosi kuwa na adabu
Hautafuti faida yake binafsi
Haukasiriki upesi
Hauweki kumbukumbu ya mabaya
Haufurahii mabaya
Hufurahia kweli (Neno la Kristo)
Huvumilia yote
UHURU WA KWELI 56
Huamini yote (Katika Kristo)
Hustahimili yote
Haushindwi (Hauna kikomo) kamwe
Upendo wa namna hii unakuja kwa kujifunza pendo la
Kristo kwetu. Tukiathirika na upendo wa Kristo tunaweza
kuathirika katika tabia na kuziishi hizi tabia. Ndio maana
Mtume Paulo anasema, “tukaenende (tukatende) kama
Kristo naye alivyotupenda na akajitoa kwaajili yetu, sadaka
na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato” (Efe
5:2). Ili tuweze kufanikiwa kuwa na upendo kama wa Yesu
Kristo ili tuenende nao nilazima tujifunze upendo wa Kristo
kwetu. Kubali kuathiriwa na upendo wa Kristo kuanzia sasa
ili uanze kukuathiri kwenye tabia zako.
UHURU WA KWELI 57
Tathmini kupitia maswali kutoka katika Sura ya Pili
1: Kutokana na surah ii ukale ni nini?
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
2: Elezea kwa ufupi namna gani ya kutoka kwenye ukale
kupitia yafuatayo:-
(i)Utimilifu wa kazi ya msalaba wa Kristo
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
(ii)Wingi wa Neema ya Yesu Kristo
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
(iii)Upendo wa Yesu Kristo
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
3: Ukamilifu wa kazi ya msalaba wa Kristo unasaidia katika
mambo yafuatayo, yataje:-
UHURU WA KWELI 58
(i)………………………………………………………………………………………
…………………………………………
(ii)………………………………………………………………………………………
………………………………….......
(iii)……………………………………………………………………………………
………………………………………….
(iv)……………………………………………………………………………………
………………………………………….
4: Kuishi kwa Neema ya Kristo kunasaidia katika mambo
yafuatayo, yataje:-
(i)………………………………………………………………………………………
…………………………………………
(ii)………………………………………………………………………………………
……………………………………....
(iii)……………………………………………………………………………………
………………………………………….
(iv)……………………………………………………………………………………
………………………………………...
(v)………………………………………………………………………………………
……………………………………….
UHURU WA KWELI 59
5: Elezea kwa ufupi namna gani ya kuathirka na upendo wa
Kristo?
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………..
UHURU WA KWELI 61
SURA YA TATU
MBONA SIO ASILI YANGU
sili inajumuisha tabia za kitu. Mwanadamu aliumbwa
kwa asili ya Mungu, Mungu aliposema na tumfanye
mtu kwa mfano wetu na kwa sura yetu. Mungu alitaka tuwe
na tabia kama za Mungu katika Maisha yetu. Tuwe
watakatifu kama alivyo Mungu (1Petro 1:16), tuwe na
mamlaka kama alivyokuwa Mungu, tuwe watawala kama
alivyo Mungu, tuwe wenye haki kama alivyo Mungu. Paulo
aliandika hivi;
“Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili
wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe
mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale
aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita,
hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao
akawatukuza.” [Rum 8:29-30]
Paulo aliwaaambia Warumi tangu asili Mungu alitujua na
alituita ili tufanane na Mwana wake (Yesu Kristo). Na
Mungu alivyotuita alituheasabia haki na kututukuza katika
Kristo Yesu (tuliookoka). Paulo anasema hivi katika
Waefeso;
A
UHURU WA KWELI 62
“Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo,
aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu
wa roho, ndani yake Kristo; kama vile alivyotuchagua katika
yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe
watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.
Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe
kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi
yake. Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo
ametuneemesha katika huyo Mpendwa.” [Efe 1:3-6]
Imeandikwa kuwa kabla ya misingi ya ulimwengu kuumbwa
Mungu kwa mapenzi yake mwenyewe. Alitubariki kwa
baraka zote za rohoni kupitia mwanawake Yesu Kristo ili
tuwe watakatifu watu wasio na hatia mbele za Mungu. Na
anasema ametuneemesha kwa neema yake katika huyo
mpendwa. Kutokana na Warumi 8:29-30 na Waefeso 1:3-6
maana yake ni kwamba kwa Mapenzi ya Mungu mwenyewe
pasipo kulazimishwa mtu au kitu chochote. Mungu
alituchagua kabla ya misingi ya ulimwengu kupitia mwana
wake Yesu Kristo ili tuwe watakatifu, wenye haki, watu
wasio na hatia na kututukuza kwa neema yake mwenyewe
kupitia mwana wake wa pekee.
Sio kwa juhudi zetu wala sio kwa matendo yetu kufanywa
watakatifu, wenye haki, tusio na hatia na kutukuzwa kwa
neema yake. Bali ni kwa mapenzi ya Mungu kupitia Yesu
Kristo. Mungu hakuhitaji juhudi zako, matendo yako wala
UHURU WA KWELI 63
uadilifu wako bali alituchagua yeye mwenyewe pasipo
madai ya matendo yetu.
Tuangalie mfano wa Yakobo na Esau.
“Isaka akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, maana
alikuwa tasa. Naye Bwana akamwitikia, na Rebeka mkewe
akachukua mimba. Watoto wakashindana tumboni
mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini?
Akaenda kumwuliza Bwana. Bwana akamwambia,Mataifa
mawili yamo tumboni mwako,Na kabila mbili za watu
watafarakana tangu tumboni mwako.Kabila moja litakuwa
hodari kuliko la pili,Na mkubwa atamtumikia mdogo. Siku
zake za kuzaa zilipotimia, tazama! Mapacha walikuwamo
tumboni mwake. Wa kwanza akatoka, naye alikuwa
mwekundu mwili wote kama vazi la nywele. Wakamwita
jina lake Esau.
Baadaye ndugu yake akatoka, na mkono wake unamshika
Esau kisigino. Akaitwa jina lake Yakobo. Isaka alikuwa
mwenye miaka sitini mkewe alipowazaa. Ikawa Isaka
alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione,
akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia,
Mwanangu. Naye akamwitikia, Mimi hapa. Akasema,
Tazama, sasa mimi nimekuwa mzee, wala sijui siku ya kufa
kwangu. Basi, nakuomba, chukua mata yako, podo lako na
UHURU WA KWELI 64
upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo;
ukanifanyie chakula kitamu namna ile niipendayo,
ukaniletee, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa.
Na Rebeka akasikia, Isaka aliposema na Esau mwanawe.
Basi Esau akaenda nyikani awinde mawindo, ayalete.
Rebeka akamwambia Yakobo mwanawe, akisema, Angalia,
nimemsikia baba yako akisema na Esau, ndugu yako,
akinena, Niletee mawindo, ukanifanyie chakula kitamu ili
nile, na kukubariki mbele za Bwana kabla ya kufa kwangu.
Basi, mwanangu, sikiliza sauti yangu kama
nitakavyokuagiza. Enenda sasa kundini ukanitwalie wana-
mbuzi wawili walio wema, nami nitawafanya chakula
kitamu kwa baba yako, namna ile aipendayo. Kisha
utampelekea baba yako, apate kula, ili akubariki kabla ya
kufa kwake.
Yakobo akamwambia Rebeka mamaye, Esau ndugu yangu
ni mtu mwenye malaika, na mimi ni mtu laini. Labda baba
yangu atanipapasa, nami nitakuwa machoni pake kama
mdanganyifu; nami nitaleta juu yangu laana wala si
mbaraka. Mamaye akamwambia, Laana yako na iwe juu
yangu, mwanangu, usikie sauti yangu tu, enenda ukaniletee
wana-mbuzi. Akaenda, akawatwaa, akamletea mamaye.
Mamaye akafanya chakula kitamu namna ile aliyopenda
babaye.
UHURU WA KWELI 65
Kisha Rebeka akatwaa mavazi mazuri ya Esau mwanawe
mkubwa, aliyokuwa nayo nyumbani, akamvika Yakobo
mwanawe mdogo. Na ngozi za wana-mbuzi akamvika
mikononi, na katika ulaini wa shingo yake. Naye akampa
Yakobo mwanawe mikononi mwake hicho chakula kitamu,
na mkate alioufanya. Akaja kwa baba yake, akasema,
Babangu. Akasema, Mimi hapa, U nani wewe, mwanangu?
Yakobo akamwambia babaye, Mimi ni Esau, mzaliwa wako
wa kwanza, nimefanya kama ulivyoniambia. Ondoka,
tafadhali, ukae kitako, ule mawindo yangu, ili roho yako
inibariki.
Isaka akamwuliza mwanawe, Imekuwaje umepata upesi
namna hii, mwanangu? Akasema, Kwa sababu Bwana,
Mungu wako, amenifanikisha. Isaka akamwambia Yakobo,
Karibu, tafadhali, ili nikupapase, mwanangu, nione
kwamba wewe ndiwe mwanangu Esau, ama siyo. Basi
Yakobo akamkaribia Isaka, babaye, naye akampapasa,
akasema, Sauti ni sauti ya Yakobo, lakini mikono ni mikono
ya Esau. Wala hakumtambua, kwa maana mikono yake
ilikuwa kama mikono ya Esau, ndugu yake, yenye malaika;
basi akambariki.
Akamwuliza, Wewe ndiwe kweli mwanangu Esau?
Akasema, Ndimi. Akasema, Niletee karibu nami nipate kula
mawindo ya mwanangu, ili roho yangu ikubariki.
Akamsogezea karibu, naye akala; kisha akamletea mvinyo,
UHURU WA KWELI 66
akanywa. Isaka, baba yake, akamwambia, Njoo karibu
sasa, ukanibusu, mwanangu. Akakaribia akambusu. Naye
akasikia harufu ya mavazi yake, akambariki akasema,
Tazama, harufu ya mwanangu Ni kama harufu ya shamba
alilolibariki Bwana.
Ikawa Isaka alipokwisha kumbariki Yakobo, na alipokuwa
Yakobo ndiyo kwanza ametoka mbele ya Isaka, baba yake,
mara Esau ndugu yake akaja kutoka katika kuwinda kwake.
Naye pia amefanya chakula kitamu akamletea babaye,
akamwambia baba yake. Babangu na aondoke, ale
mawindo ya mwanawe, ili roho yako inibariki. Isaka, baba
yake, akamwuliza, U nani wewe? Akasema, Mimi ni
mwanao, Esau, mzaliwa wako wa kwanza. Isaka
akatetemeka tetemeko kuu sana, akasema, Ni nani basi
yule aliyetwaa mawindo akaniletea? Nami nimekwisha kula
kabla hujaja wewe, nikambariki; naam, naye atabarikiwa.
Esau aliposikia maneno ya babaye, akalia kilio kikubwa cha
uchungu sana, akamwambia babaye, Nibariki na mimi,
mimi nami, Ee babangu. Akasema, Nduguyo amekuja kwa
hila, akauchukua mbaraka wako. Akasema, Je! Hakuitwa
Yakobo kwa haki, maana amejitia mahali pangu mara mbili
hizi? Alichukua haki yangu ya mzaliwa wa kwanza, na sasa
amechukua mbaraka wangu. Akasema, Je! Hukuniwekea
na mimi mbaraka? Isaka akajibu, akamwambia Esau,
Tazama, nimemfanya awe bwana wako, na ndugu zake
UHURU WA KWELI 67
wote nimempa kuwa watumishi wake; kwa nafaka na
mvinyo nimemtegemeza, nami nikufanyie nini sasa,
mwanangu?
Esau akamwambia babaye, Una mbaraka mmoja tu,
babangu? Unibariki mimi, mimi nami, Ee babangu. Esau
akapaza sauti yake, akalia. Isaka, baba yake, akajibu,
akamwambia,Angalia,penye manono ya nchi patakuwa
makao yako,Na penye umande wa mbingu unaotoka juu.
Kwa upanga wako wewe utaishi, nawe utamtumikia
nduguyo; Na itakuwa utakapoponyoka, Utalivunja kongwa
lake katika shingo yako. Esau akamchukia Yakobo kwa ajili
ya ule mbaraka babaye aliombarikia. Esau akasema moyoni
mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo
nitakapomwua ndugu yangu Yakobo. [Mwa 25:21-26, 27:1-
27, 30-41]
Katika mfano huu utagundua kwamba hakuna jambo baya
alilofanya Esau wala hakuna jambo jema alilofanya Yakobo.
Mungu alimpa mbaraka Yakobo kwa sababu alimchagua
kuwa mrithi wa baraka za baba yake Isaka. Hii ni kwa sababu
Mungu alimchagua Isaka tangu akiwa tumboni mwa mama
yake Rebeka kuwa Mrithi wa baraka za Isaka.
UHURU WA KWELI 68
Mungu ametufanya kuwa miungu duniani maana yake tuna
mamlaka kama aliyonayo Mungu kwenye maisha yetu.
Mungu ametufanya kuwa washindi kwa sababu tunatokana
na yeye, ndio maana maandiko yanashuhudia hivi;
“Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda
ulimwengu; na huku ndiko kuushindako ulimwengu, hiyo
imani yetu” [1Yoh 5:4]
Asili yetu ni kushinda kwenye maisha yetu. Mungu anataka
tutembee kama washindi, watakatifu, wenye haki, wenye
mamlaka, tunaomlingana Mungu. Yesu alipokuja duniani
alikuja kwaajili ya kurejesha ufalme wake. Ndio maana Yesu
alipoanza huduma yake kwa mara ya kwanza alianza kwa
kutamka hadharani kutubu na kuiamini injili. Imeandikwa;
“Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya Mungu,
akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu
umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili” [Mark 1:14b-15]
Neno “tubuni” ni neno ambalo kwenye lugha mama, lugha
ya kiebrania limetumika neno “teshuvah” maana yake
geuka. Neno tubuni limetokana na neno la kigiriki
“metanoia” maana yake badili mtazamo. Neno “injili”
kwenye lugha ya kigiriki limetumika neno “eungalion”
maana yake “habari njema”. Maana yake Yesu aliposema
“tubuni na kuiamini Injili” alikuwa anamaanisha hivi
“geukeni, badilisheni mtazamo wenu na kuiamini habari
UHURU WA KWELI 69
njema.” Tafsiri ya biblia ya The Passion Translation (TPT)
imetumia neno “kuambatana” maana yake geukeni,
badilisheni mtazamo wenu na kuambata na injili.
Kama ni hivyo basi kumbe tunaweza kusema Kristo alikuwa
anasema geukeni, badilini mtazamo wenu. Ufalme wa
Mungu unahitaji watu waliogeuka na kuacha njia zao
mbaya walizokuwa nazo, ufalme unahitaji watu ambao
walishabadilisha mtazamo. Sio rahisi sana kutembea na
ufalme wa Mungu kama bado hujabadili mtazamo wako.
Ukijua mamlaka, utawala na mfumo mzima wa uongozi wa
ufalme wa Mungu kuna aina ya maisha huwezi kuishi tena.
Huwezi kuwa mtumwa wa dhambi (Yoh 8:34) wakati unajua
unatakiwa kutawala, ukijua kuwa ukiwa duniani unatakiwa
kutawala kila kitu.
Yesu hakuja duniani kwaajili tu ya watu kwenda mbinguni,
alikuja kurudisha kile mwanadamu alichopoteza kwenye
bustani ya Edeni ambacho ni ufalme wake (ufalme wa
Mungu).
Mwanadamu kwa mara ya kwanza, Mungu alimuumba kwa
kusudi la kutembea ndani ya ufalme wake. Ndio maana kwa
mara ya kwanza Mungu anasema hivi;
“Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa
sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa
UHURU WA KWELI 70
angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye
kutambaa kitambaacho juu ya nchi.” [Mwa 1:26]
Wakatawale maana yake Mungu alimpa utawala wa ufalme
wake ili audhihirishe hapa duniani. Kwa tafsiri nyepesi
Mungu alikuwa anasema; “kama jinsi tunavyotawala
mbinguni kwa mfano huo ndivyo ninavyowapa kutawala
duniani.” Kutawala inajumuisha kusimamia na kuongoza.
Kristo alikuja kwaajili ya kuurudisha ufalme wake hapa
duniani kwa sababu tuliupoteza. Ndio maana mifumo yetu
ya kufanikiwa iko tofauti kabisa na mifumo ya ulimwengu
huu. Ndio maana Yesu anasema;
“Mimi siombi kwamba awatoe katika ulimwengu; bali
awalinde na yule mwovu. Wao si wa ulimwengu, kama
mimi nisivyo wa ulimwengu.” [Yoh 17:15-16]
Kama Yesu alisema ninyi sio wa ulimwengu huu kama mimi
nisivyo wa uliomwengu huu. Maana yake ni kwamba yoyote
aliyeko ndani ya Kristo ameumbwa kwenye mfumo tofauti
kabisa wa kufanikiwa na watu wa mataifa. Mifumo yetu ya
kufanikiwa iko tofauti kabisa na mifumo ya ulimwengu huu.
Ndio maana hatutakiwi kuamini kwenye mafanikio kama
vile ulimwengu unavyoamini. Kwa mfano ulimwengu
unaamini kwenye kufanya kazi sana ndio ufanikiwe. Lakini
sivyo biblia inavyotufundisha kwa watoto tulioko ndani ya
ufalme wa Mungu. Ndio maana Yesu aliwaambia wanafunzi
wake;
UHURU WA KWELI 71
“Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au
Tuvae nini? Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa
sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji
hayo yote. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki
yake; na hayo mtazidishiwa.” [Math 6:31-33]
Yesu alikuwa anawaonyeshja watu kipaumbele kwa yoyote
aliye katika ufalme (aliyeokoka) ni kuutafuta ufalme (kuishi
jinsi ufalme unavyotaka). Tafsiri ya Biblia ya Habari njema
inasema;
“Basi, msiwe na wasiwasi: ‘Tutakula nini, tutakunywa nini,
tutavaa nini’. Maana hayo yote yanahangaikiwa na watu
wasiomjua Mungu. Baba yenu wa mbinguni anajua
kwamba mnahitaji vitu hivyo vyote. Bali, shughulikeni
kwanza juu ya ufalme wa Mungu na matakwa yake, na
hayo yote mtapewa kwa ziada.”
Kumbe tukiushughulikia kwanza ufalme wa Mungu baada
ya hapo kuhusu kula, kunywa na kuvaa haitakuwa shida.
Kama ni hivyo basi uwe na uhakika ukiuishi ufalme wa
Mungu kula, kunywa na kuvaa haitakuwa jambo
unaloliwaza kwenye ufahamu wako. Kwa sababu
utakapoanza kuishi kama ufalme unavyotaka kula, kunywa
na kuvaa vitakuwa kwenye maisha yako kwa kiwango cha
kujitosheleza. Mungu alitufanya kuwa watu wa tofauti sana
(tuliookoka) kiwango ambacho hatutakiwi kupambana
kabisa kuhusu kutafuta kula, kunywa au kuvaa.
UHURU WA KWELI 72
Kwa sababu hatutatofautiana na watu wa mataifa kwa
sababu na wao kwenye ufahamu wao hutafuta hayo hayo.
Kumbe kama ni hivyo basi ukweli ni kwamba kila kitu
tunachokihitaji kwenye maisha yetu yaani kula, kunywa,
kuvaa ni vitu vinavyopatikana kirahisi tukiutumikia kwanza
ufalme wa Mungu.
Balozi wa Tanzania anapokuwa nchi ya Marekani huwa
anakuwa ndani ya uangalizi wa nchi ya Tanzania. Nchi ya
Tanzania huwa inahakikisha analindwa, anatunzwa kwa kila
kitu; kuhusu kula kwake, kunywa kwake, kuvaa kwake,
kulala kwake, ulinzi wake. Hayo ni mambo ambayo
hayafikirii kabisa kwenye ufahamu wake kwa sababu ni
wajibu wa serikali ya Tanzania kumhudumia. Kazi aliyonayo
balozi wa Tanzania huko Marekani ni kuitangaza nchi na
kuionyesha nchi uzuri wake, utajiri wake, maeneo ya utalii.
Hiki ndicho kilichoko kwenye ufahamu wake.
Vivyo hivyo tunapokuwa ndani ya ufalme wa Mungu Mungu
anataka tuishi jinsi ufalme unavyotaka tuishi halafu hayo
mambo mengine ya chakula, mavazi na malazi ni wajibu wa
ufalme wa Mungu kutuhudumia. Tunaishi kwenye dunia
inayotuelekeza tufanye mambo mengi sana, kila mmoja
atakwambia fanya hivi na vile ili uweze kufanikiwa. Lakini
kanuni ya ki-Mugu ni nyepesi ishi kwanza ufalme halafu
hayo mengine utazidishiwa. Ndio maana Kristo
UHURU WA KWELI 73
aliwafundisha wanafunzi wake namna nzuri ya kuomba
aliwaambia;
“Basi ninyi saline hivi; Baba yetu uliyembinguni , Jina lako
litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa
duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu.” [Math
6:9-11]
Maana yake kipaumbele cha kwanza ili uweze kupata riziki
ni ufalme wake. Huwezi kuanza kuona matokeo mazuri ya
ufalme kama hauishi ufalme. Ili uweze kuishi kwa ufanisi
ndani ya ufalme unahitaji kujibu maswali yafuatayo:-
Ufalme unakutambua wewe ni nani?
Ufalme unataka ufanye nini?
Ufalme umekupa uwezo gani?
Ufalme umeadhimia nini kwenye hatima yako?
Ufalme unakutambua wewe ni nani?
Kila mmoja wetu Mungu alimuumba akiwa amemuwekea
kitu cha kufanya (utambulisho). Utambulisho huu ndio
unaokutofautisha wewe na watu wengine wote duniani. Na
utofauti huu ndio unaokupa wewe uwezo wa kufanya kitu
ambacho ufalme wa Mungu umekuitia kukifanya katika
kizazi hiki. Mungu alimjua Yeremia ndio maana alimwambia
hivi Yeremia;
UHURU WA KWELI 74
“Kabla sijakuumba katika tumbonalikujua, na kabla
hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii
wa mataifa” [Yer 1:4]
Mungu alimtambua Yeremia kuwa yeye ni nani. Mungu
alimtakasa (alimtenga) maalumu kwaajili ya kumuweka
Yeremia kuwa nabii wa mataifa. Mungu akamuwekea
Yeremia muda, nyakati na majira (Mhu 3:1). Kila mmoja
ameumbwa akiwa amewekewa kitu cha kufanya
ulimwenguni tofauti na watu wote duniani. Watu wengi
hawaamini hili ndio maana wanaishi maisha yasiyokuwa na
nidhamu (kufanya jambo kwa wakati). Mungu hakutuumba
kukaa duniani milele ndio maana alituweka ulimwenguni
kwa wakati, kusudi na majira. Lengo lake tuwe majibu
katika huu ulimwengu. Kuna watu hawatavushwa maisha
yao kwa sababu wanakusubiri wewe tu ndio uje uwatoe
kwenye shida na changamoto zao. Sasa jiulize na jijibu
mwenyewe ufalme wa Mungu unakutambua wewe ni nani?
Ni rahisi kujibu hili swali ukiwa ndani ya ufalme yaani
kuokoka. Unapookoka unaingizwa kwenye ufalme wa
Mungu na hapo ni rahisi sana kupata majibu ya swali letu
kwa sababu utakuwa umezaliwa kutokata na Baba
(Mungu). Sura yako itamfanania Mungu kwa sababu Mungu
alituumba kwa mfano na kwa sura yake mwenyewe (Mwa
1:26)
UHURU WA KWELI 75
Tuangalie mfano wa Utawala wa Mungu
Makao makuu (Mbinguni)
Mungu (Baba, Mwana, Roho)[Mfalme]
Maeneo ya utekelezaji (Duniani)
Mwanadamu (Balozi)
Malaika (watumishi wa mwanadamu)
Dunia
Shetani
Ufalme unataka wewe ufanye nini?
Biblia inasema;
“Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla
hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii
wa mataifa” [Yer 1:4]
Mungu alimtambua Yeremia kama nabii wa Mataifa. Ndio
maana Mungu alimwambia Yeremia nakujiua vizuri kabisa
kuwa wewe ni nabii wa Mataifa kwa sababu ndivyo
nilivyokuumba. Tena alimwambia angalia nimekuweka leo
juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung’oa, na kubomoa, na
kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda. Muulize
Mungu amekuweka ufanye nini? Biblia inasema;
UHURU WA KWELI 76
“Kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni
Mungu, wala hapana mwingine, Mimi ni Mungu, wala
hapana aliye kama mimi. Nitangazaye mwisho tangu
mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka
bado; nikisema shauri langu litasimama, name nitatenda
mapenzi yangu yote” [Isa 46:9-10]
Kumbe Mungu anapokuweka ulimwenguni anafahamu
mwisho wako kabla ya Mwanzo wako. Anakuwekea muda
na nyakati katika kutekeleza kusudi lako. Tambua kusudi
lako leo.
Ufalme umekupa uwezo gani?
Lazima utambue ufalme umekupa uwezo gani ndani yako.
Uwezo aliouwekeza Mungu ndani yako ni ule wa kukusaidia
kutimiza lengo/kusudi la Mungu kwenye maisha yako.
Lazima utambue Mungu amewekeza mambo gani ndani
yako. Unaweza kutambua uwezo ulioko ndani yako kwa
kuangalia mambo yafuatayo:-
Unapenda kufanya mambo gani
Mungu anakutambua wewe ni nani
Ufalme wa Mungu unakutambua wewe nani
Hatima ya maisha yako ni nini
UHURU WA KWELI 77
Ufalme wa Mungu umeazimia nini kwenye hatima yako
Maandiko yanasema;
“Kwa kila jambo kuna majira yake, na wakati kwa kila
kusudi chini ya mbingu” [Mhu 3:1]
Lazima utambue kuwa Mungu amekuumba kwa kusudi
maalumu akiwa amekuwekea muda, majira na nyakati za
kutimiza hilio kusudi. Nilazima utambue mwisho
wako/hatima yako kwa sababu hautaishi milele duniani
kutimiza hilo kusudi.Biblia inasema;
“Maana nayajua mawazo ninayo wawazia ninyi, asema
BWANA, ni mawazo ya amani wala si mabaya, kuwapa
ninyi, tumaini siku zenu za mwisho” [Yer 29:11]
Tafsiri ya biblia ya King James Version (KJV) Habari njema
inasema hivi;
“Maana naijua mipango niliyonayo kwa ajili yako, mipango
ya kukupatia utajiri na sio majanga, mipango ya kukupeleka
kwenye hatima yako na tumaini lako.”
Maana yake Mungu amekusudia kukufikisha kwenye
hatima yako. Watu wengi wanafikiri hatima zao ziko mbele
yao. Lakini hatima yako haiko mbele yako, hatima yako iko
ndani yako nilazima ujue hatima yako ni nini. Kwa kufanya
hivyo itakusaidia kuwa na hamasa ya kutaka kufika
UHURU WA KWELI 78
unakotakiwa kufika. Jitiishe chini ya Roho Mtakatifu ili
akuonyeshe hatima yako (kusudi lako).
Namna ya kuushirikisha ufalme wa Mungu kwenye
maisha yako kwa njia ya sadaka ili utende kazi kwa niaba
yako.
Ufalme wa Mungu.
Ni mfumo wa maisha wa kimbingu wenye utaratibu na
kanuni ambao unaweza kuratibiwa duniani kama mbinguni.
Ndio maana Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kuomba
kuhusu ufalme wa mbinguni hivi;
“Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako
litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa
duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu
Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo
wadeni wetu. Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule
mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu,
hata milele. Amina” [Math 6:9-13]
Moja ya jambo muhimu sana kulifahamu ni kwamba Yesu
aliwafundisha wanafunzi wake kuomba ufalme wake kuja.
Yesu alijua ufalme wa Mungu (mfumo wa maisha wa
UHURU WA KWELI 79
kimbingu) unaweza pia kuwa dhahiri duniani. Na ufalme wa
Mungu ukiwa dhahiri duniani basi huwa unafurikisha na
mahitaji ya kila siku (kula, kunywa, kuvaa, ulinzi). Kuna
muhimu mkubwa wa kuushirikisha ufalme wa Mungu
wakati wote, unapoushirikisha ufalme wa Mungu moja kwa
moja unaruhusu ufalme wa Mungu kutenda kazi kwa niaba
yako.
Moja ya njia inayoweza kuushirikisha ufalme wa Mungu
kutenda kazi kwa aniaba yako ni sadaka. Sadaka inaweza
kutumika kuushirikisha ufalme wa Mungu kutenda kazi kwa
aniaba yako. Ufalme wa Mungu ukitenda kazi kwa aniaba
yako uwe na uhakika unakuondoa kwenye mfumo tegemezi
wa uchumi wa duniani na kukuweka kwenye uchumi wa
mfumo wa ufalme wa Mungu. Inawezekana ukawa
unafanya biashara ndogo, au kipato chako cha mshahara ni
kidogo lakini ukiamua kuuhusisha ufalme wa Mungu
kutenda kazi kwa aniaba yako.Unaweza ukawa na kipato
kidogo au mshahara mdogo lakini ukaweza kufanya mambo
makubwa zadi yasiyoendana na kipato chako au mshahara
wako. Sadaka ni njia nzuri ya kuuhusisha ufalme wa Mungu
kutenda kazi kwa aniaba yako.
UHURU WA KWELI 80
Sadaka ni nini?
Ni kitu chochote kinachotolewa madhabahuni kukusaidia
kuuhusisha ufalme wa Mungu kutenda kazi kwa aniaba
yako. Kuna sadaka za aina nyingi kuna sadaka ya mda,
sadaka ya mwili, sadaka mali au fedha. Vitu vyote hivi
unaweza kuvitumia kutenda kazi kwa aniaba yako. Katika
agano jipya watu walihimizwa kutoa sadaka kwa moyo wa
kupenda wala si kwa kulazimishwa. Tutaangalia aina moja
ya sadaka (sadaka ya fedha) jinsi inavyoweza kuuhusisha
ufalme wa Mungu kwa aniaba yako.
Zingatia yafuatayo kabla ya utoaji wako wa sadaka (ya
fedha) kabla ya kutoa;
i. Mungu anautazama moyo kabla ya utoaji wako wa
sadaka
Hakikisha unauelewa sahihi kwenye moyo wako kabla ya
utoaji wa sadaka. Mungu anautazama moyo kwanza ili
uweze kupata matokeo sahihi ya utoaji wa sadaka yako.
Biblia inatuonyesha kuwa kuna watu walikuwa na sadaka
nzuri lakini kwa sababu mioyo yao haikuwa na ufahamu
sahihi kuwa Mungu anahitaji nini. Mungu alikataa sadaka
zao na aliwakataa na wao wenyewe. Mfano Mfalme Sauli
Mungu alikataa sadaka yake na alimkataa yeye kukaa
UHURU WA KWELI 81
kwenye nafasi yake kwasababu hakuwa na utii. Samweli
alimwambi; kutii ni bora kuliko dhabihu (1Samw 15:22).
Kwahiyo ni muhimu moyo wako kuwa na ufahamu sahihi ili
sadaka yako iweze kuleta matokeo ndio maana
imeandikwa;
“Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana
wanadamu hutazama sura ya nje, bali Bwana huutazama
moyo” [1Samw 16:7b]
Katika utoaji wa sadaka katika kipindi tulichonacho cha
agano jipya, ni tofauti kabisa na utoaji wa sadaka wa kipindi
cha agano la kale. Na ili usiweze kuleta mgogoro na Mungu
katika utoaji wako wa sadaka lazima uzingatie yafutayo:-
Hatutoi sadaka ili tubarikiwe [tulishabarikiwa
kwa baraka zote za rohoni katika Kristo Yesu (Efe
1:3)]
Hatutoi sadaka ili tuwe wenye haki [sisi tayari
tumehesabiwa haki kwa kumwamini Yesu Kristo
(Rum 8:29-30, Rum 5:17, 2Kor 5:21)
Hatutoi sadaka ili tuwe na kibali mbele za Mungu
(Tulishapata kibali kwa kumwamini Yesu Kristo)
Hatutoi sadaka ili tuwe watakatifu au watu
wema (Tulishafanywa kuwa watakatifu watu
wema tusio na mawaa kwa kumwamini Yesu
Kristo)
UHURU WA KWELI 82
Hatutoi sadaka ili tuwe matajiri tulishafanywa
matajiri kwa kumwamini Yesu Kristo (2Kor 8:9)
Sadaka katika sura ya agano jipya inatolewa kwaajili ya
nini?
Tunatoa sadaka kwaajili ya yafuatayo:-
Tunatoa sadaka ili kuwatunza watumishi
Tunatoa sadaka kwaajili ya wahitaji (yatima,
wajane, wagonjwa, wasiojiweza)
Sadaka inatolewa kwaajili ya huduma ya injili
Kazi zote hizi za sadaka sio kazi yetu ni kazi ya Mungu
mwenyewe. Mungu mwenyewe anawajibika kuwatunza
watumishi, kuwatunza wahitaji na kushughulika na kazi
yake ya injili. Ukiwa umezaliwa mara ya pili (uliyeokoka)
hata usipotoa sadaka huwezi kulaaniwa kwa sababu tayari
Yesu Kristo alikuwa ni sadaka kamilifu ambayo ni sadaka
aliitoa Mungu inayomridhisha. Na aliitoa kwaajili yetu ili
kusudi Kristo afanyike laana kwa aniaba yetu. Hatubarikiwi
kwa sababu tunatoa sadaka tunabarikiwa kwa sababu ya
kile alichofanya Yesu Kristo msalabani kwaajili yetu. Kwa
sababu hiyo hakuna namna kilichobarikiwa kinaweza kuwa
laana. Ndio maana Mungu alimkatalia Balaamu kulaani
UHURU WA KWELI 83
wana wa Israeli kwasababu Mungu alikuwa tayari
ameshawabarikia (Hes 22:12).
Kwa maana hiyo haimaanishi kuwa hakuna haja ya kutoa
sadaka. Kila imani ina hatua zake, Mungu anatusisitiza kuwa
tumebarikiwa katika Kristo ili tusipambane kutafuta
kubarikiwa. Hata hivyo hakuna jambo sasa tunaweza
kufanya likazidi sadaka kamilifu ya Yesu Kristo iliyotolewa
kwaajili yetu. Ndio maana maandiko yanasema Yesu Kristo
alitolewa sadaka mara moja kwaajili ya dhambi zetu
(zilizopita, zilizopo na zijazo), na wokovu wetu. Neno hili
wokovu limetokana na neno la kigiriki “sozo” ambalo
lilikuwa na maana ya ukombozi, ustawi (mafanikio) na
uponyaji. Kwahiyo Kristo alitolewa sadaka kamili kwaajili ya
dhambi zetu kikamilifu, ustawi (mafanikio) kamili na
uponyaji kamili. Ndio maana imeandikwa;
“mkaenende katika upendo, kama Kristo naye
alivyowapenda ninyi tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na
dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato” [Efe 5:2]
Kristo ni sadaka kamilifu iliyotolewa kutufanikisha katika
kila eneo kwenye maisha yetu. Ukitoa kitu chochote hali
kwamba unataka kubarikiwa au kufanikiwa lazima utaleta
mgogoro na Mungu, na kwa namna hiyo hautapata
matokeo sahihi.
UHURU WA KWELI 84
Kwanini ni muhimu sana kutoa sadaka kama tumesha
barikiwa?
Kumbuka nimekwambia kuwa sio kazi yako kuwatunza
watumishi ni kazi ya Mungu. Sio kazi yako kuwatunza
wahitaji ni kazi ya Mungu, sio kazi yako kuhudumia injili ni
kazi ya Mungu. Sasa ukianza kuhudumia watumishi,
kuwatunza wahitaji na kuendeleza kazi ya injili kwa sadaka
yako unasimama kwenye nafasi ya Mungu. Kwa namna hiyo
unakuwa umeuhusisha ufalme wa Mungu na kwa namna
hiyo ufalme wa Mungu utaanza kutenda kazi katika
unachokifanya kwa aniaba yako. Na kwa namna hiyo
utaanza kuona kula, kunywa, kuvaa, malazi, ulinzi na
mahitaji yako vikimiminwa kwenye maisha yako.
Imeandikwa hivi;
“Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa
kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme
mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa
maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na
kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;
nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja
kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia. Ndipo wenye
haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona
una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? Tena ni
lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi,
tukakuvika? Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au
UHURU WA KWELI 85
kifungoni, tukakujia? Na Mfalme atajibu, akiwaambia,
Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa
hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi” [Math
25:34-40]
Tuangalie jinsi mama mjane wa Serepta aliutumikia
ufalme wa Mungu na ufalme wa Mungu ukafanya katika
eneo la uchumi kwa niaba yake.
“Basi, akaondoka, akaenda Sarepta, hata alipofika langoni
pa mji, kumbe! Mwanamke mjane alikuwako akiokota kuni;
akamwita, akamwambia, Niletee, nakuomba, maji kidogo
chomboni nipate kunywa. Alipokuwa akienda kuleta,
akamwita akasema, niletee, nakuomba, kipande cha mkate
mkononi mwako. Naye akasema kama BWANA, Mungu
wako aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na
mafuta kidogo katika chupa; name ninaokota kuni mbili
niingie nijipikie mimi na mwanangu, tuule tukafe. Eliya
akamwambia, Usiogope; enenda ukafanye kama
ulivyosema; lakini unifanyie kwanza mkate; kisha ujifanyie
nafsi yako na mwanao. Kwa kuwa BWANA, Mungu wa
Israeli, asema hivi, Lile pipa la unga halitapunguka, wala ile
chupa ya mafuta haitaisha, hata siku ile BWANA
atakapoleta mvua juu ya nchi. Basi akaenda, akafanya
kama alivyosema Eliya; nayeye mwenyewe, na Eliya, na
nyumba yake, wakala siku nyingi. Lile pipa la maji
UHURU WA KWELI 86
halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawa
sawa na neno la BWANA alilonena kwa kinywa cha Eliya”
[1Falme 17: 10-16]
Mwanamke mjane alikuwa amekata tamaa na hali yake
mbaya ya uchumi kiasi cha kumlevya. Lakini alipoamua
kuutumikia ufalme wa Mungu ufalme wa Mungu
ulishughulikia uchumi wake. Kumbe unapohusika
kuwahudumia wahitaji kwa sadaka yako, watumishi wa
Mungu, huduma ya injili hayo yote unamfanyia Mungu, na
kwa namna hiyo unakuwa umeushirikisha ufalme wa
Mungu kutenda kazi kwa niaba yako.
Namna gani ya kuitumia sadaka kuuhusisha ufalme wa
Mungu kutenda kazi kwa niaba yako?
Tumia sadaka yako kama mbegu. Kumbuka unapotoa
sadaka yako moja kwa moja unauhusisha ufalme wa Mungu
kukusimamia na kutenda kazi kwa aniaba yako. Ni agizo la
Mungu tangu Mwanzo Mungu alipomuagiza Adamu kuilima
bustani katika kila mche Mungu aliweka na mbegu ndani
yake (Mwa 1:11-12). Hata baada ya gharika, bado Mungu
aliendelea kuweka utaratibu wa kupanda na kuvuna.
Imeandikwa;
UHURU WA KWELI 87
“Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno,
wakati wa baridi na wakati wa hari, wakati wa kaskazi na
wakati wa kusi, mchana na usiku, havitakoma” [Mwa 8:22]
Mungu aliamuru kuwa majira ya kupanda na kuvuna kuwa
havitakoma. Kupanda na kuvuna vipo katika muendelezo,
ndio maana ili uweze kuvuna lazima upande. Unaweza
kuanza kutumia fedha yako kupanda, ili uweze kuvuna.
Kumbuka mbegu ziko za aina nyingi, kila mbegu
inayopandwa inakusudi lake. Mbegu ya mahindi lazima
ilete mazao ya mahindi. Mbegu ya harage lazima izae
maharage, kadhalika pia katika mbegu nyingine. Kiwango,
ubora, shamba, wakati na kiasi cha mbegu ni msingi wa
kujua matokeo ya hiyo mbegu itakuwaje. Kabla hujapanda
mbegu lazima ukusudie upandaji wako wa mbegu, na kiasi
cha mbegu kiendane na matokeo unayoyatarajia. Ndio
maana imeandikwa;
“Kwa habari za kuwahudumia watakatifu sina haja ya
kuwaandikia. Maana najua utayari wenu, ninaojisifia kwa
ajili yenu kwa Wamakedonia, kwamba Akaya ilikuwa tayari
tangu mwaka mzima; na bidii yenu imewatia moyo wengi
wao. Lakini naliwatuma hao ndugu, ili kujisifu kwetu kwa
ajili yenu kusibatilike katika jambo hili; mpate kuwa tayari,
kama nilivyosema; kusudi, wakija Wamakedonia pamoja
nami, na kuwakuta hamjawa tayari, tusije tukatahayarika
sisi, (tusiseme ninyi), katika hali hiyo ya kutumaini. Basi
UHURU WA KWELI 88
naliona ya kuwa ni lazima niwaonye ndugu hawa
watangulie kufika kwenu, na kutengeneza mapema karama
yenu mliyoahidi tangu zamani, ili iwe tayari, na hivi iwe
kama kipawa, wala si kama kitu kitolewacho kwa unyimivu.
Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba;
apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na
atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni,
wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye
kwa moyo wa ukunjufu. Na Mungu aweza kuwajaza kila
neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna
siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema; kama
ilivyoandikwa, Ametapanya, amewapa maskini, Haki yake
yakaa milele Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na
mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na
kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu” [2Kor
9:1-10]
Ilikuwa ni utaratibu wa kanisa la Korintho kuwatunza
watumishi, ndio mana Paulo anasema kwa habari ya
kuwahudumia watakatifu sina haja ya kuwaandikia. Paulo
anaendelea kusema apandaye haba atavuna haba,
apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Anasema na
kila mtu atende kama alivyokusudia moyoni mwake, maana
yake katika kupanda lazima uazimie matokeo unayoyataka
katika kupanda kwako. Ndio maana anasema yeye
apandaye mbegu atawapa mbegu na kuzizidisha naye
ataongeza mazo ya haki yenu. Kama vile Mungu
UHURU WA KWELI 89
anavyotujua kuwa sisi ni wenye haki wake vivyo hivyo
anasema katika kupanda atatuzidisha na kuongeza mazao
ya haki yetu.
Mambo ya kuambatanisha (kuzingatia) ili sadaka yako
iweze kuuhusisha ufalme wa Mungu kwa niaba yako
kikamilifu:
Imani
Usahihi wa sadaka kama mbegu
Mahali pa kutoa/kupanda (shamba/madhabahu)
Neno la Kristo
Wakati wa kutoa
ii. Toa sadaka yako kwa Imani.
Sadaka inapotolewa kama mbegu, imani ni sehemu ya kiini
cha mbegu. Ili uweze kupata matokeo nilazima unapoamua
kutoa sadaka yako kama mbegu itoe ukiwa umeunganisha
na imani ya kujua kuwa utapokea matokeo unayoyatarajia.
Biblia inatueleza kuwa;
“kwa sababu Mwenye haki ataishi kwa imani” [Gal 3:11b]
UHURU WA KWELI 90
Maandiko yanaonyesha pia;
“Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye
akisita-sita, roho yangu haina furaha naye” [Ebr 10:38]
Pia maandiko yanaendelea kutuambia;
“Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana
mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye
yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao” [Ebr
11:6]
Ili uweze kupata matokeo unayoyatarajia katika utoaji wako
wa sadaka kama mbegu hakikisha unaambatanisha imani
yako katika utoaji wako wa hiyo sadaka. Kujua kuwa uko
katika hali ya imani katika utoaji wako wa sadaka ni rahisi.
Utajua uko katika imani unapotoa hiyo sadaka endapo
utaona tayari unachokitaka kutoka kwa Mungu kimefanyika
au kimetokea tayari hata kama hujakishuhudia kwa macho
ya damu na nyama. Unapotoa hiyo sadaka yako
unapoambatanisha na imani yaani kiini cha mbegu
unaruhusu matokeo ya upatikanaji wa matokeo wa hiyo
mbegu yawe halisi mwilini.
Kumbuka huwezi kutenganisha mbegu na kiini. Gamba la
mbegu ni sadaka yako unayoitoa imani ni kiini Kwahiyo ili
hiyo mbegu iote lazima uweze kuambatanisha vyote viwili.
UHURU WA KWELI 91
Kama hutafanya hivyo utakuwa umeharibu mbegu yako na
hutaona matokeo. Ni sawa sawa unataka kupanda mbegu
za mahindi halafu kabla hujapanda unaanza kuzitolea
mbegu viini. Uwe na uhakika hazitaota na utakuwa
umepoteza sadaka yako bure. Kwahiyo hakikisha unatoa
sadaka hiyo kwa imani.
Unaposhughulika na upandaji wako wa mbegu kwa njia ya
sadaka unauruhusu ufalme wa Mungu kutenda kazi kwa
aniaba yako (kushughulika na mahitaji yako). Kula, kunywa,
kuvaa, malazi, ulinzi, sasa unapoamua kutoa sadaka yako.
Inaweza kuwa unapata msukumo wa kupeleka sadaka yako
wahitaji (yatima, wajane, wagonjwa), watumishi, au
kwaajili ya huduma ya injili. Kwa namna hiyo ndivyo
unaugusa moyo wa Mungu na ukigusa moyo wa Mungu
moja kwa moja unakuwa umeuruhusu ufalme wa Mungu
kutenda kazi kwa aniaba yako.
Inawezekana unahitaji nyumba ya gharama fulani, gari ya
gharama fulani, unataka kufungua kampuni kwa gharama
fulani, unataka kufungua kiwanda, au jambo lolote
unalotaka kulianzisha. Hakikisha Unapotoa sadaka yako
kama mbegu adhimia kuwa ninapotoa hii sadaka kwaajili ya
ufalme wa Mungu. Ninatarajia hiki ninachokitaka
nimekipokea, inawezekana hauna uwezo kabisa wa kujenga
hiyo nyumba, kuwa hilo gari, kampuni au kiwanda cha
gharama unayohitaji. Ukitoa hiyo sadaka na ukaamini
UHURU WA KWELI 92
umeshapata matokeo unaruhusu kile kiini cha imani yako
katika hiyo mbegu kilete matokeo.
Usahihi wa sadaka kama mbegu.
Usahihi wa sadaka yako unatokana na muongozo wa Roho
Mtakatifu au msukumo wa matarajio unayoyataka
kuyaona. Kumbuka usahihi wa sadaka yako kama mbegu
hautokani tu na jinsi unavyoona inafaa bali pia kwa uongozi
wa Roho Mtakatifu. Ndio maana biblia inashuhudia kuwa;
“Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba
atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na
kuwakumbusha yote niliyowaambia” [Yoh 14:26]
Kwa kuwa sisi tulioamini Roho Mtakatifu yupo kutufundisha
ni muhimu kumsikiliza ushauri wake katika utoaji wa sadaka
ili tuweze kupata matokeo sahihi. Roho Mtakatifu anaweza
kukupa msukumo wa kutoa hiyo sadaka yako kwa wahitaji,
watumishi au huduma ya injili. Kumbuka kusikiliza juu ya
kiwango anachokwambia utoe. Kwa mfano unaweza ukawa
unapata msukumo wa kutoa sadaka kwa yatima. Lakini sasa
utajuaje kuwa hiki ndio kiwango sahihi cha kupeleka huko?
Utajua kwa kusikiliza ushauri anaokupa Roho Mtakatifu.
Kwa mfano Roho Mtakatifu anaweza kukwambia peleka
dola mia moja au dola hamsini. Aidha kama hujaelewa vizuri
namna ya kumsikiliza Roho Mtakatifu anaweza kuzungumza
UHURU WA KWELI 93
na wewe kwa ishara. Ishara rahisi sana anaitumia Roho
Mtakatifu ni amani. Ndio maana imeandikwa na amani ya
Kristo iamue mioyoni mwenu (Kol 3:15a).
Unapopata msukumo wa kupeleka sadaka yako kwa
yatima. Ukitaka kupeleka dola ishirini husikii amani, dola
hamsini husikii amani, mpaka unafikisha dola mia ndio
unajisikia amani. Ukiona hivyo ipeleke hiyo sadaka ni sahihi,
kwa sababu amani ya Kristo imeamua hivyo. Au kinyume
chake ni hivi unaweza ukawa unapeleka kiwango kikubwa
kuliko vile inavyotakiwa. Huenda unataka kupeleka dola
mia mbili unakosa amani kumbe Roho Mtakatifu anataka
upeleke dola mia moja hiyo nyingine aidha uifanyie kitu
kingine au upande mahali pengine. Ni muhimu kumsikiliza
Roho Mtakatifu, msukumo wa ndani na amani iliyo ndani
yako.
Kumbuka matokeo ya sadaka yako kama mbegu
yanategemea sana usahihi wa hiyo mbegu. Ndio maana
imeandikwa apandaye haba atavuna hapa apandaye kwa
ukarimu atavuna kwa ukarimu. Fikiria unashamba la heka
moja halafu unambegu sado moja. Uwe na uhakika utapata
matokeo ambayo hukuyatarajia , mazao yako yatakuwa
kwa uchache sana. Ushauri wa Roho Mtakatifu na amani ya
Kristo vinamchango mkubwa sana kukujulisha usahihi wa
sadaka unayotoa.
UHURU WA KWELI 94
iii. Mahali pa kutoa/kupanda (madhabahu/shamba)
Zingatia kuwa sio kila mbegu inaweza kuota mahali popote.
Kila mbegu ina mahali pake sahihi kwa kuota mbegu ya
mahindi sio katika kila udongo,ardhi au shamba inaota.
Kadhalika pia mbegu ya karanga na mbegu za aina nyingine
zinaota na kustawi vizuri katika eneo sahihi. Peleka sadaka
yako mahali ambapo unaelekezwa na Roho Mtakatifu
upeleke au mahali unapojisikia amani. Aidha wewe
mwenyewe unaweza kutamani kutoa sadaka yako. Ili
uweze kupanda hiyo mbegu mahali sahihi zingatia mambo
mawili ya msingi. Uhai wa madhabahu unayopelekea na
imani kuhusu hiyo madhabahu, Je! Imani ya hiyo
madhabahu unayotaka kupeleka wana imani na kupanda na
kuvuna? Au hiyo madhabahu ina uhai? Ukipeleka kwenye
madhabahu ambayo inakosa hivi vitu viwili sadaka yako
itapata shida sana kuota.
Kumbuka kuwa biblia inatueleza wazi kuwa chuma hunoa
chuma (Mith 27:17a). Fikiria unapeleka sadaka kwenye
madhabahu isiyoamini kuhusu ustawi wa sadaka yako. Hiyo
madhabahu moja kwa moja haina uhai na kwa namna hiyo
utakuwa unatoa sadaka yako kwenye shamba kame. Na
kwa namna hiyo sadaka yako kamambegu itakauka
haitaota, na kwa namna hiyo hautaona matokeo ya hiyo
sadaka. Kwa mfano unataka kutoa sadaka yako kwa
mtumishi fulani au kusapoti kazi ya injili fulani Je, huyo
UHURU WA KWELI 95
mtumishi au hiyo huduma ina imani juu ya ustawi wa hiyo
sadaka yako.
iv. Neno la Kristo.
Neno la Kristo ni ulinzi wa sadaka yako kama mbegu . Neno
la Kristo linasimamia ahadi ambayo imekwisha kuwako.
Kumbuka kila kitu Yesu Kristo alishafanya pale msalabani
kwa ajili yetu. Ili tuweze kuuishi huo uhalisia wa kupokea na
kuuishi katika macho ya damu na nyama lazima
tuambatanishe na neno lake. Ni sawa na kumwambia
Bwana kuwa hii sadaka siitoi kwa sababu inastahili kuliko
wewe. Ila kwa sababu ya kile umekifanya tayari kwenye
neno lako kwaajili yangu. Kumbuka imani yaani kiini cha
mbegu hakiwezi kustahimili pasipokuwa na neno.
Biblia inatueleza umuhimu mkubwa wa kuwa na neno la
Kristo tunapopanda. Tuangalie mfano huu;
“Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake; naye
alipokuwa akizipanda, nyingine zilianguka karibu na njia,
zikakanyagwa, ndege wa angani wakazila. Nyingine
zikaanguka penye mwamba; zilipoanza kumea zikakauka
kwa kukosa rutuba. Nyingine zikaanguka kati ya miiba, na
miiba ikamea pamoja nazo ikazisonga. Nyingine
UHURU WA KWELI 96
zikaanguka penye udongo mzuri; zikamea, zikazaa moja
kwa mia. Alipokuwa akinena hayo alipaza sauti akisema,
Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie. Wanafunzi wake
wakamwuliza, Maana yake nini mfano huo? Akasema,
Ninyi mmepewa kuzijua siri za ufalme wa Mungu; bali
wengine kwa mifano, ili wakiona wasione, na wakisikia
wasielewe.
Na huo mfano, maana yake ni hii; Mbegu ni neno la Mungu.
Wale wa karibu na njia ndio wasikiao, kisha huja Ibilisi
akaliondoa hilo neno mioyoni mwao, wasije wakaamini na
kuokoka. Na wale penye mwamba ndio wale ambao
wasikiapo hulipokea lile neno kwa furaha; nao hawana
mizizi, huamini kitambo kidogo, na wakati wa kujaribiwa
hujitenga. Na zilizoanguka penye miiba ni wale waliosikia,
na katika kuenenda kwao husongwa na shughuli na mali,
na anasa za maisha haya, wasiivishe lo lote. Na zile penye
udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa
mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa
matunda kwa kuvumilia” [Luk 8:5-15]
Biblia inaweka wazi kuwa kati ya moja ya siri za ufalme wa
Mungu ni kupanda na kuvuna. Baada ya Yesu kuulizwa na
Wanafunzi wake maana yake nini mfano huo? Yesu
akawajibu kuwa ninyi mmepewa kuzijua siri za ufalme wa
Mungu lakini wengine hawazijui ndio maana alisema nao
UHURU WA KWELI 97
kwa mifano kusudi wakiona wasione na wakisikia wasisikie.
Sasa tulio wana wa ufalme (tuliookoka) Mungu ametujalia
neema ya kuzijua siri za ufalme wa Mungu moja ya siri hizi
ni kupanda na kuvuna. Kupanda ndani ya ufalme wa Mungu
na kuvuna ndani ya ufalme wa Mungu. Na moja ya mhimili
anaotaja katika kupanda kwenye ufalme wa Mungu ni neno
la Mungu.
Ili uweze kuisimamia sadaka kama mbegu uliyopanda
lazima uweze kusimamia neno. Ambalo linakuhakikishia
uhalali wa kumiliki hicho ulichonacho katika Yesu Kristo ili
kiweze kuleta matokeo. Hii itakusaidia kuimwagilia mbegu
yako na kuipalilia mpaka ilete matokeo kwa hakika ulikuwa
unayatarajia. Yesu aliwafunulia wanafunzi wake juu ya
mambo yanayoweza kupoteza uhakika wa ile mbegu kuleta
matokeo. Yesu anaanza na kusema Shetani anaweza
kuliondoa lile neno lililoko ndani yako na kwa namna hiyo
anasababisha usiamini na kuokoka. Kwa mfano unaweza
ukawa umepanda sadaka yako na ulitarajia ilete matokeo,
huenda ulitamani baada ya miaka kadhaa, mwaka mmoja
au miezi au siku kadhaa. Baada ya hapo unaona bado huoni
matokeo, ikifika kwenye hiyo hali ni rahisi sana kukata tama
na kuona sadaka uliyotoa kama mbegu ulipoteza, na kwa
namna hiyo Shetani analiondoa lile neno la ahadi uliopandia
sadaka yako. Kwa sababu hiyo imani yako inaondoka na
kwa namna hiyo tayari ile mbegu inakuwa imeshaharibika,
kwahiyo huwezi kuona matokeo.
UHURU WA KWELI 98
Kwahiyo, ili usimpe nafasi ya kuondoa imani yako juu ya
sadaka kama mbegu uliyopanda kwa ajili ya matarajio
unayoyataka, kubali kuambatana na neno la Mungu bila
kujali matokeo uliyoyatarajia unaona yamechelewa. Yesu
anaendelea kusema kuna mambo mengi yanayosababisha
usiambatane na neno. Jambo lingine ni wale ambao
wanaamini kupitia neno na wanalipokea kwa furaha baada
ya muda kitambo kifupi wanajitenga. Lile neno linakuwa
halina mizizi wanashindwa kupata matokeo. Yesu anasema
wako wengine ambao wanalisikia neno lakini kwa sababu
wanasongwa na shughuli, mali na anasa wanashindwa
kuivisha. Hali hiyo inasababisha wanashindwa kupata
matokeo sahihi juu upandaji wao na wanashindwa kuivisha
kwa sababu wanasongwa na mambo ya duniani. Ni kama
vile unatoa sadaka yako halafu watu wengine wanaanza
kukusonga kuwa umepoteza sadaka yako ili usiamini na kwa
namna hiyo unashindwa kuivisha.
Katika ule mstari wa 15, Biblia Tafsiri ya Habari Njema
inasema hivi;
“Na zile zilizoanguka kwenye udongo mzuri ndio watu wale
wanaolisikia neno, wakalizingatia kwa moyo mwema na
wautii. Hao huvumilia mpaka wakazaa matunda”
UHURU WA KWELI 99
Tafsiri ya Biblia ya Neno inasema hivi:
“Lakini zile mbegu zilizoanguka kwenye udongo mzuri ni
mfano wa wale ambao hulisikia neno la Mungu na kulishika
kwa moyo mnyoofu wa utii, nao kwa kuvumilia kwingi
huzaa matunda”
Biblia inatusisitiza sana kumbatana na neno, usijaribu hata
kidogo kuacha kuambatana na neno kwa sababu unaona
umechelewa kuona matokeo. Yesu alisema kwa wale
wanaolishika neno na kulizingatia kwa moyo mwema na wa
utii, huvumilia mpaka kuzaa kwingi matunda. Ukiambatana
na neno sawa sawa katika upandaji wa sadaka yako
ukalizingatia kwa uvumilivu lazima utapata matokeo.
Usiruhusu kitu chochote kikachangia katika kuififisha imani
yako kama ni Shetani, watu wanokuzunguka wanakukatisha
tama juu ya upandaji wa sadaka yako. Wakumbushe kwa
njia ya neno kuwa bado Mungu anaendelea kushughulika
na sadaka kama mbegu niliyoipanda kwake. Kwa uvumilivu
wako wa kusubiri na kuendelea kuipalilia sadaka yako na
kuimwagilia maji utaona kuzaa matunda kwingi sana kupitia
hiyo sadaka. Ndio imeandikwa;
“Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka
mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na
kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na
mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu,
litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali
UHURU WA KWELI 100
litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo
yale niliyolituma” [Isa 55:10-11]
Kumbuka kuambatana na neno katika utoaji wa sadaka
yako kama mbegu. Neno lilitoka katika kinywa cha Mungu
lazima litimize mapenzi ya Mungu na kutimiza yale neno
limetumwa.
v. Wakati wa kutoa sadaka.
Wakati wa kutoa sadaka yako ni wakati ambao umepewa
maelekezo na Roho Mtakatifu wa kupeleka, au wakati
unajisikia amani kupeleka, kumbuka wakati una umuhimu
sana katika kuchangia matokeo ya hiyo sadaka. Mfano
umeambiwa na Roho Mtakatifu wakati huu peleka sadaka
kiasi fulani kwa yule mjane. Ujue ni wakati sahihi wa
kupeleka, huenda huo muda ndio wakati huyo mjane
anauhitaji na hiyo sadaka. Ukiwa na utii ndani yako wa
kutoa wakati huo unaruhusu sadaka yako kuleta matokeo.
Sio kila mbegu inayopandwa hata kama ni sahihi na
imepandwa kwenye shamba sahihi inaota kila wakati. Ndio
maana mbegu nyingi zinapandwa wakati wa masika kusudi
ziweze kuota kwa urahisi. Zingatia kutoa sadaka yako kwa
wakati ili uweze kupata matokeo inavyostahili. Ikiwa Roho
Mtakatifu au amani ya kristo inakuongoza kupeleka wakati
huo, zingatia kutoa wakati huo ili upate matokeo chanya.
UHURU WA KWELI 101
Tathmini kupitia maswali kutoka katika Sura ya Tatu
1: Kutokana na sura hii, asili ni nini?
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
2: Yesu alikuja ili kuturejesha kwenye asili yetu. Taja hiyo
asili
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
3: Namna gani ya kuishi ndani ya Ufalme wa Mungu?
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………
4: Ili uweze kuishi ndani ya ufalme wa Mungu kwa ufanisi
unahitaji mambo yafuatayo:-
(i)………………………………………………………………………………………
…………………………………………
UHURU WA KWELI 102
(ii)………………………………………………………………………………………
……………………………………....
(iii)……………………………………………………………………………………
………………………………………….
(iv)……………………………………………………………………………………
………………………………………….
5: Taja jambo linaloweza kuuhusisha ufalme wa Mungu
kwa vitendo
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
6: Taja vipaumbele ambavyo Mungu anaviangalia kabla ya
utoaji wako wa sadaka
(i)………………………………………………………………………………………
…………………………………………
(ii)………………………………………………………………………………………
……………………………………....
(iii)……………………………………………………………………………………
………………………………………….
(iv)……………………………………………………………………………………
………………………………………….
UHURU WA KWELI 103
(v)………………………………………………………………………………………
……………………………………….
(vi)……………………………………………………………………………………
………………………………………….
7: Taja sababu za utoaji wa sadaka katika sura ya agano
jipya
(i)………………………………………………………………………………………
…………………………………………
(ii)………………………………………………………………………………………
……………………………………….
(iii)……………………………………………………………………………………
………………………………………….
8: Kwanini ni muhimu kutoa sadaka tuliobarikiwa katika
Kristo Yesu?
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………
9: Taja viambatanishi vya utoaji wa sadaka yako kama
mbegu katika sura ya agano jipya uli uweze kupata
matokeo sahihi
UHURU WA KWELI 104
(i)………………………………………………………………………………………
…………………………………………
(ii)………………………………………………………………………………………
……………………………………….
(iii)……………………………………………………………………………………
………………………………………….
(iv)……………………………………………………………………………………
………………………………………….
(v)………………………………………………………………………………………
………………………………………
UHURU WA KWELI 105
SURA YA NNE
SIKUUMBWA KWA KUSUDI HILI
ungu alimuumba mwanadamu ili aweze kutawala
kila kitu duniani, ndio maana maandiko yanasema;
“Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa
sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa
angani na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye
kutambaa kitambaacho juu ya nchi” [Mwa 1:26]
Baada ya anguko mwanadamu yaani baada ya Adamu
kumwasi Mungu utawala ulichukuliwa na Shetani. Tangia
hapo mwanadamu aliishi ndani ya utumwa na kutawaliwa
na dhambi. Ashukuriwe Mungu ambaye alimtuma Mwana
wake wa pekee ili aje aurudishe utawala tuliopoteza
bustani ya Edeni ndio maana sentesi ya Kwanza kuisema
Yesu ilikuwa ni kwa habari ya ufalme. Marko aliandika hivi;
“Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya Mungu,
akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu
umekaribia, tubuni na kuiamini injili” [Mark 1:14b-15]
Maana yake jambo la kwanza lililomleta Kristo ilikuwa ni
kurejesha ufalme wa Mungu. Yesu anasema katika
kuurejesha ufalme wake kuna kanuni mbili za kuufuata;
M
UHURU WA KWELI 106
Kutubu
Kuiamini injili
Kutubu na injili vikiambatana vinairejesha ufalme. Kutubu
kunabadilisha mtazamo lakini injili inamuokoa mtu. Ndio
maana Paulo alisema kwa ujasiri kwamba;
“siionei haya injili, kwasababu ni uweza wa Mungu uuletao
wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza na kwa
Myunani pia” [Rum1:16]
Ni injili pekee inayoweza kuleta ukombozi bila injili watu
wanaendelea kutenda dhambi, bila injili watu wanaishi
maisha ya umaskini, bila injili watu wanaishi maisha ya
utumwa.
Injili ni habari njema ya neema ya Yesu Kristo. Neema ni
upako wa msaada usiostahili, kibali cha kukubalika pasipo
kustahili. Paulo alishuhudia kuwa alikuwa akiihubiri habari
njema ya neema ya Mungu. Maandiko yanasema;
“Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa ni kitu cha thamani
kwangu kama kumaliza mwendo wangu wa huduma ile
niliyoipokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia habari njema ya
neema ya Mungu” [Mate 20:24]
Kumbe injili ni habari njema ya neema ya Mungu. Hakuna
mahali injili inashindwa kumtoa mtu. Ukiona kuna mahali
mtu anahubiriwa anashindwa kutoka ujue hiyo sio injili ni
UHURU WA KWELI 107
fundisho tu. Neema ya Mungu hakuna mahali ambapo
inafeli, ina nguvu ya kutawala dhambi, utumwa, umaskini.
Ukiwa ndani ya neema ya Mungu utatawala hakuna jambo
litashindikana kwenye maisha yako. Ndio maana Paulo
alishangaa sana kuona Wagalatia wameacha injili ya neema
ya Mungu na kugeukia injili ya namna nyingine. Maandiko
yanasema;
“Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye
aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya
namna nyingine” [Gal 1:6]
Wagalatia walihubiriwa injili ya neema ya Kristo lakini
wakarudi nyuma na kuanza kufuata mafundisho ya
matendo ya sheria. Paulo aliendelea kuwasisitiza Wagalatia
kuwa; “Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao
na kutaka kuigeuza injili ya Kristo. Lakini ijapokuwa sisi au
malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yoyote
isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe”
Anakazia alichoongea kwa msisitizo kuwa; Kama
tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye
yote akiwahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo
mliyoipokea, na alaaniwe. Paulo anasema kwanini mtu
asipoihubiri injili ya neema ya Kristo alaaniwe. Paulo
anasema hivi;
UHURU WA KWELI 108
“Kwa maana, ndugu zangu injili hiyo niliyowahubiri,
nawajulisha ya kuwa siyo ya namna ya kibinadamu. Kwa
kuwa sikuipokea kwa mwanadamu wala sikufundishwa na
mwanadamu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo” [Gal 1:6-12]
Kumbe injili ya neema ya Kristo haikuja kwa mafundisho ya
mwanadamu yoyote ndio maana Paulo anasema ni injili
aliyofunuliwa na Yesu Kristo. Injili isiyo ya matendo ya
sheria, ni injili ya kuitegemea na kuiamini neema ya Yesu
Kristo. Ndio maana Paulo aliwaambia Warumi siionei haya
injili kwasababu ni uweza wa Mungu uletao wokovu.
Neema ya Mungu haitegemei matendo ya mtu bali utendaji
wa Yesu Kristo na kazi aliyoifanya pale msalabani kwaajili
yetu. Paulo anasema hivi;
“Lakini ikiwa kwa neema haiwi kwa matendo tena, au hapo
isingekuwa neema” [Rum 11:6]
Kumbe neema ikiwa ni kwa matendo ni batili, neema
haihesabiwi kwa matendo kabisa, ikiwa inahesabiwa kwa
matendo ni ujira sio neema. Ujira ni mshahara anaoupata
mtu kutokana na kazi aliyoifanya. Neema ni zawadi
tuliyoipokea kutoka kwa Mungu iliyoachiliwa kwa njia ya
Yesu Kristo kupitia kazi yake aliyoifanya msalabani. Yohana
alishuhudia kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa,
neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo (Yoh
1:17).
UHURU WA KWELI 109
Ndio maana Paulo alikuwakumbusha Waefeso kuwa ni
neema ya Yesu Kristo ndiyo iliyotuokoa. Imeandikwa hivi;
“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani;
ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha
Mungu; wala si kwa matendo mtu awaye yote asije
akajisifu” [Efe 2:8-9]
Wokovu tuliopewa kwa njia ya Yesu Kristo ni zawadi.
Zawadi ni jambo lolote unalopewa sio kwa sababu
umeomba au kwa sababu umefanya kwa juhudi zako.
Zawadi yoyote inayotolewa na mtu anakupa sio kwa sababu
ulifanya jambo fulani bali anakua ameamua kukupa bure.
Wokovu tulioupokea ulikuwa ni kwa neema. Hakuna
mwanadamu aliyestahili kuupokea kwa sababu wote
tulikuwa tumekosea kwa sababu ya mtenda dhambi mmoja
(Adamu). Ndio maana aliwaombea watu kwa neno la
neema ya Mungu, anasema hivi;
“Basi sasa nawaweka katika mikono ya Mungu, na kwa
neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa
urithi pamoja nao wote waliotakaswa” [Mate 20:32]
Neno la neema ya Mungu linaweza kuwajenga watu na
kuwapa urithi pamoja. Neno la neema ya Mungu linapojaa
ndani ya mioyo ya Mungu linajenga imani inayowasaidia
watu katika kuwajenga kuwapa urithi ulio katika Kristo
Yesu. Kama Paulo alivyowaandikia Warumi kuwa ili muweze
UHURU WA KWELI 110
kuwa na imani ya kuwajenga nilazima kusikia neno la Kristo;
imeandikwa ; Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia
huja kwa neno la Kristo (Rum 10:17). Kumbe hatuhitaji
kujijenga imani ndani yetu isipokuwa ni imani ya kusikia
neno la Kristo ambayo ni neema yake. Neema ya Kristo
inafunua urithi tulio nao ndani ya Kristo matendo ya sheria
yanafunua nafsi ya mtu mwenyewe. Ndio maana Paulo
anasema hiyo neema haikutokana na nafsi zetu.
Neema ya Mungu inataka wakati wote kumfunua Kristo
alilotenda msalabani kwaajili yetu. Nafsi zetu zinapenda
tujifunue wenyewe kwa ubora wa kazi zetu. Yesu alipokufa
msalabani ilikuwa ni mbadala wa sisi wenyewe. Yesu
anataka nafsi zetu zijazwe na picha yake ili tunapojitazama
tumuone yeye. Kwa hakika kuna mambo hatuwezi
kuyapokea au kuyafikia bila neema yake. Matendo yetu
mema yanashindwa kabisa kufikia kiwango cha kukubaliwa
na Mungu na kufikia kiwango ambacho Mungu anataka.
Ndio maana Kristo ilibidi afe msalabani ili tufanyike warithi
wa mambo yote aliyokuwa nayo kwaajili yetu. Waebrania
aliandika hivi;
“Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake
aliyeifanya. Kwa maana agano la urithi lina nguvu
palipotukia kufa kwa mtu; kwakuwa halina nguvu kabisa,
akiwa yu hai yeye aliyelifanya” [Ebr 9:16-17]
UHURU WA KWELI 111
Na sisi tulifanyika kuwa warithi halali kwa sababu ya uzao
halali wa ahadi aliyopewa baba yetu Ibrahimu kupitia Yesu
Kristo.
“Na kwa kuwa ninyi ni wa Kristo, basi mmekuwa uzao wa
Ibrahimu, na warithio sawa sawa na ahadi” [Gal 3:29]
Neno la neema ya Kristo linaachilia kibali cha kuwa warithi
halali wa mambo yote aliyotupigania Kristo msalabani.
Mambo hayo ni kama vile:-
Kuishinda dhambi na kuitawala (Rum 6:14)
Kushinda umaskini (2 Kor 8:9)
Kushinda magonjwa (1 Pet 2:24)
Kufanywa wenye haki (2Kor 5:21)
Kufanywa washindi (Rum 8:37)
Kubarikiwa (Efe 1:3)
Tumefanyika wenye haki kwa sababu ya neema ya Kristo
Yesu.
Haki ni kibali cha kusimama mbele za Mungu. Agano la kale
liliwapa watu wachache kibali cha kusimama mbele za
Mungu, na ilikuwa kwa sheria. Hakuna mwanadamu yoyote
aliyekuwa anaruhusiwa kuingia kupeleka haja zake kwa
Mungu isipokuwa kuhani mkuu.
UHURU WA KWELI 112
Biblia inashuhudia kwamba; Lakini katika hema hiyo ya pili
kuhani mkuu huingia peke yake, mara moja kila mwaka;
wala si pasipo damu, atoayo kwaajili ya nafsi yake na kwa
dhambi za kutokujua za hao watu. Roho Mtakatifu
akionyesha neno hili, ya kwamba njia ya kupaingia
patakatifu ilikuwa haijadhihirishwa bado, hapo hema ya
kwanza ilipokuwa ingali ikisimama; Lakini Kristo akiisha
kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema
yatakayokuwapo, kwa hema iliyokubwa na kamilifu zaidi,
isiyofanyika kwa mikono, maana yake isiyo ya ulimwengu
huu, wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu
yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu,
akiisha kupata ukombozi wa milele (Rum 9:7-8, 11-12).
Yesu alipokufa msalabani aliachilia uhuru wa kila mmoja wa
kupaingia patakatifu pa patakatifu ambapo aliruhusiwa
kuhani mkuu wa kipindi cha agano la kale. Yesu ambaye ni
kuhani mkuu, mjumbe wa agano jipya, kupitia Yeye
aliachilia kibali cha kuingia patakatifu pa patakatifu, yaani
kibali cha kusimama mbele za Mungu. Ndio maana Mungu
alimtambulisha Yesu katika maeneo mawili eneo la kwanza
ni katika mto Yordani na eneo la pili ni katika mlima mrefu
alipoenda kuomba na Petro, Yakobo na Yohana (math 17:1-
5). Katika maeneo yote sauti ilisikika kutoka mbinguni
ikisema;
UHURU WA KWELI 113
“Huyu ni mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa
naye; msikieni yeye” [Math 3:16-17, 17:5]
Mstari huu katika Tafsriri ya biblia ya KJV ametumia neno
“well pleased” yaani niko radhi naye. Mungu akituona
anamuona Kristo ndani yetu na kwa huyo tunapata haki ya
kusogea mbele za Mungu na kuzungumza naye.
Pazia la hekalu lilipasuka vipande viwili kwa ishara ya
kuonyesha kuwa kila mmoja ana uhuru wa kupaingia
patakatifu pa patakatifu na kuwa na haki ya kusema na
Mungu. Maandiko yanasema;
“Naye Yesu akiisha kuipaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa
roho yake. Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande
viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba
ikapasuka” [Math 27:50-51]
Kupasuka kwa pazia la hekalu kuliashiria uhuru wa kila
mmoja kumfikia Mungu. Katika agano la kale ilikuwa
haiwezekani kabisa mwenye dhambi kukubaliwa mbele za
Mungu na kusamehewa. Katika agano jipya Mungu
anamtafuta mtu aliye mwovu, mwenye dhambi ili amfanye
mtakatifu. Agano la kale lilikuwa haliruhusu kabisa mtu
aliye mwovu, mwenye dhambi kuingia hata kwenye
nyumba ya ibada.
Ilikuwa ni kujitaksa kwanza kabla ya kusogelea uwepo wa
Mungu. Ndio maana kuhani mkuu wa agano la kale ilikuwa
UHURU WA KWELI 114
ni lazima ajitakase kwanza kabla hajaingia patakatifu pa
patakatifu. Agano jipya tumepewa neema kila mmoja
anaweza kumwendea Mungu jinsi alivyo na Mungu
mwenyewe akamfanya kuwa mtakatifu hi ni neema ya
ajabu sana.
Baada ya Yesu kufa msalabani aliamua kuwa radhi na
yoyote aliamua kumkubali Yesu Kristo na kumwamini. Hata
kama ni mwenye dhambi anafanywa kuwa mtakatifu
kupitia Kristo, hata kama hana haki anafanywa kuwa
mwenye haki kupitia Yesu Kristo. Agano la kale msamaha
wa dhambi ulikuwa wa mda, kufanywa mwenye haki ni kwa
mda tu. Sadaka za wanyama zilikuwa hazina uwezo wa
kuindoa dhambi moja kwa moja. Ilitakiwa kila mwaka
itolewe sadaka, lakini kupitia Yesu Kristo mara moja tu
tulifanywa kuwa wenye haki mbele za Mungu (1Pet 3:18,
Ebr 9:28). Paulo aliandika kuwa;
“Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa
kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
Basi tu wajumbe kwaajili ya Kristo, kana kwamba Mungu
anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwaajili ya
Kristo mpatanishwe na Mungu. Yeye asiyejua dhambi
alimfanya kuwa dhambi kwaajili yetu, ili sisi tupate kuwa
haki ya Mungu katika Yeye” [2Kor 17, 21]
UHURU WA KWELI 115
Tulikuwa wenye dhambi kwaajili yetu alifanyika mwenye
dhambi ili sisi tufanywe kuwa wenye haki. Upendo wake
kwetu ni wa ajabu sana ndio maana alipozibeba dhambi za
ulimwengu mzima. Mungu hakutaka kabisa hata kuwa naye
karibu, wala kumtazama kwa sababu Mungu anachukia
dhambi. Maandiko yanashuhudia kuwa; Na kama saa tisa,
Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Elo, Eloi, lama
sabakthani? Yaani Mungu wangu, Mungu wangu, mbona
umeniacha? (Math 27:46)
Kama vile Mungu alivyokuwa yuko radhi na mwanawe
Mpendwa Yesu Kristo. Kila anayemwamini anahesabiwa
haki katika mambo yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa
torati ya Musa. Kama maandiko yanavyosema kuwa;
“Basi, na ijulikane kwenu, ndugu zangu, ya kuwa kwa huyo
mnahubiriwa msamaha wadhambi; na kwa yeye kila
amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote
asiyoweza kuhesabiwa haki kwa torati ya Musa” [Mate
13:38-39]
Torati maana yake ni sheria, Wayahudi waliishi kwa sheria
tu katika kipindi cha agano la kale vitabu rejea vinaonyesha
kuwa kulikuwa na sheria zaidi ya mia sita ambazo walikuwa
ni lazima wayafuate. Kuna makosa yalikuwa hayawezi
kusamehewa kabisa adhabu yake ilikuwa ni kifo. Biblia
inashuhdia kuwa Mwanamke aliyezini na mwanaume
alitakiwa kupigwa mawe mpaka kufa.
UHURU WA KWELI 116
“Waandishi na Mafarisayo walimkamata mwanamke
aliyekuwa amezini na mwanamke biblia inasema;
Waandishi na Mafarisayo wakamleta mwanamke
aliyefumaniwa na uzinzi, wakamweka katikati.
Wakamwambia Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa
alipokuwa akizini. Basi katika torati, Musa alituamuru
kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe
wasemaje? Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili
wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama,
akaandika kwa kidole chake katika nchi. Nao walipozidi
kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi
miongoni mwenu na awe wa kwanza kumtupia jiwe.
Akainama tena, akaandika kwa kidole chake katika nchi.
Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka
mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho
wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke
amesimama katikati.
Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke,
akamwambia Mwanamke, wako wapi wale washitaki
wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?
Akamwambia hakuna Bwana. Yesu akamwambia wala
mimi sikuhukumu. Enenda zako wala usitende dhambi
tena” (Yoh 8:3-11).
UHURU WA KWELI 117
Yesu hakuwa na shida na sheria alitaka kutenda haki katika
sheria ndio maana aliwaambia yoyote asiye na dhambi awe
wa kwanza kumpiga mawe mwanamke huyu. Jambo
lililosababisha Yesu kuwaambia wanafunzi wake yoyote
asiyekuwa na haki iliyozidi haki ya Waandishi na Mafarisayo
ni kwasababu ya unafiki wa Mafarisayo. Maandiko
yanashuhudia kuwa Waandishi na Mafarisayo walikuwa
wakiwatwika watu mzigo mzito wa sheria hali wao
wenyewe walikuwa hawawezi kuzifuata (Math 23:23).
Napenda neno alitamka Yesu kwa yule mwanamke baada
ya wale washitaki wake kumwacha, Yesu alimwambia;
“Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende
dhambi tena”. Kazi ya sheria ni hukumu, Yesu
hakumhukumu bali alimsamehe dhambi zake na
kumwambia asitende dhambi tena. Kumbe tukiwa ndani ya
Kristo tunapewa zawadi ya kutohukumiwa
kinachotupelekea kutofanya dhambi tena. Kumbe sheria
haiwezi kumsaidia mtu asitende dhambi bali ni Kristo ndiye
anayeweza Kumsaidia mwanadamu asitende dhambi na
kufanywa mwenye haki. Biblia inasema;
“Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote
waliohukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki
watu wote walihesabiwa haki yenye uzima. Kwa sababu
kama kwa kuasi mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika
hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja
UHURU WA KWELI 118
watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki” [Rum
5:18-19].
Kwa sababu ya utii wa Yesu Kristo tuliingizwa katika hali ya
wenye haki. Ndio maana Yesu bado anakuita, hata ukiwa
ulifanya ubaya kiasi gani bado anasema anakupenda, bado
anasema anakuhitaji katika ufalme wake. Paulo aliyekuwa
Sauli wakati wa nyuma aliwauwa watu wengi, maelfu ya
watu waliokuwa wakimshuhudia Yesu Kristo. Yesu
alimhitaji Sauli kwenye ufalme wake alimsamehe na
kumfanya kuwa mtume wa watu wa Mataifa, ambaye
alibatizwa kuwa Paulo. Leo hii tunasoma vitabu yake zaidi
ya nusu ya vitabu vya agano jipya kaandika yeye. Haki
tuliyopewa ilikuwa kwa sababu ya juhudi ya Yesu Kristo
msalabani sio kwa sababu yetu sisi wenyewe.
Tunahesabiwa haki ya Mungu kwa njia ya imani kwa neema
yake. Matendo yetu yalishindwa kufikia kiwango cha haki
au utakatifu aliokuwa anautaka Mungu. Ndio maana
Mungu alimtoa Mwanawe wa pekee Yesu Kristo ili kupitia
yeye tupewe haki yake kwa njia ya neema yake. Ndio maana
maandiko yanasema;
“Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria;
inashuhudiwa na torati na manabii; ni haki ya Mungu iliyo
kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio.
Maana hakuna tofauti; kwa sababu wote wamefanya
dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;
UHURU WA KWELI 119
wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya
ukombozi ulio katika Kristo Yesu” [Rum 3:21-24]
Haki ya Mungu ipatikanayo kwa njia ya imani ya Yesu Kristo
inaachilia amani ipitayo akili zetu na kutuweka huru. Paulo
anasema;
“Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na
mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu
Kristo ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani
kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na
kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu” [Rum 5:1-2]
Haki ya matendo ya sheria ni haki inayopatikana kwa
matendo mazuri ya mtu binafsi, yaani unahesabiwa haki
kutokana na kile unachokifanya. Haki ya pili ni haki ambayo
unahesabiwa sio tu kwa sababu ya matendo mazuri/mema
unayoyafanya bali kwa sababu ya Kristo. Haki hii tunaipokea
kwa njia ya imani ya Yesu Kristo. Ndio maana Paulo
aliwaambia aliwaambia Wagalatia mmetengwa na Kristo
mnaotaka kuhesabiwa haki kwa matendo ya sheria. Haki ya
matendo ya sheria imepunguka, haiwezi kufikisha matakwa
ya Mungu kwenye maisha yetu. Mungu mwenyewe anataka
tuishi kwa haki ya Yesu Kristo ambayo inapatikana kwa njia
ya imani. Maandiko yanasema;
“Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa
sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema. Maana
UHURU WA KWELI 120
sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya
imani” [Gal 5:4-5]
Kuishi kwa haki ya matendo ya sheria ni sawa na kusema
Yesu Kristo alikufa bure msalabani, haki ya Mungu haiwezi
kunisaidia jambo lolote kwenye maisha yangu. Ndio maana
Paulo aliwasisitiza sana Wagalatia kuishi kupitia haki
ipatikanayo kwa njia ya imani. Paulo anasema;
“siibatili neema ya Mungu; maana, ikiwa haki hupatikana
kwa njia ya sheria, basi Kristo alikufa bure” [Gal 5:21]
Haki ya Mungu inapatikana kwa njia ya imani ya Yesu Kristo,
matendo yetu mazuri mbele za Mungu yanaonekana ni deni
(Rum 4:4). Mbele za Mungu matendo yetu mazuri biblia
inashuhudia kuwa ni mafu (Ebr 9:14). Ili tukubalike mbele
za Mungu na matendo yetu mema yawe hai mbele za
Mungu nilazima tukubali kumwani Yesu Kristo aliyekufa
kwaajili yetu akafanyika mwenye dhambi ili sisi tuwe haki
ya Mungu (2Kor 5:21).
UHURU WA KWELI 121
Tathmini kupitia maswali kutoka katika Sura ya Nne
1: Ufalme wa Mungu unarejeshwa kwa viambatanishi
muhimu viwili, vitaje?
(i)………………………………………………………………………………………
…………………………………………
(ii)………………………………………………………………………………………
……………………………………….
2: Injili ni nini?
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
3: Neno la Neema Ya Kristo linaachilia kibali cha kuwa
warithi halali wa mambo yote aliyotupigania Yesu Kristo
msalabani. Yataje
(i)………………………………………………………………………………………
…………………………………………
(ii)………………………………………………………………………………………
……………………………………….
(iii)……………………………………………………………………………………
…………………………………………
UHURU WA KWELI 122
(iv)……………………………………………………………………………………
………………………………………….
(v)………………………………………………………………………………………
……………………………………….
(vi)……………………………………………………………………………………
………………………………………….
UHURU WA KWELI 123
SURA YA TANO
NITASIMAMA TENA
akumbuka mtumishi wa Mungu mmoja aliyekuwa na
kansa ya tumbo, kwa vile alivyokuwa mtumishi
mkubwa, walienda watumishi mbali mbali wakubwa
na maarufu kumuombea. Kwa kipindi kirefu aliweza
kuombewa bila kupata matokeo yoyote, kwa kadri
walivyomuombea ndivyo hali ilizidi kuwa mbaya.
Alipokwenda hospitali hakuweza kupatiwa matibabu hali
ilikuwa mbaya sana. Madaktari walithibitisha kuwa kansa
yake imefikia hatua ya mwisho kwa hiyo asingeweza
kupona. Akapewa maelekezo ya kumsaidia kutunza
ugonjwa wake ili usimuue kwa kasi. Huku nafsi yake ikiwa
imejaa majonzi na huzuni, akawa akifikiri kuhusu huduma
yake.
Anasema ndani yake hakuwa anashuhudiwa kazi ya
huduma yake ameimaliza. Lakini pia kutokana na maelezo
ya madaktari maana yake alikuwa anahesabiwa siku za
kufa. Mbele yake anaona giza mwanga hakuna, tumaini
limepotea, hawezi tena kutumika, hawezi tena kuwa na
uwezo wa kuruka ruka akihubiri injili kama alivyokuwa
akifanya.
N
UHURU WA KWELI 124
Ni miezi minne sasa bado Mungu alimuacha hai yuko
kitandani, kitanda kilikuwa rafiki yake kama mbinguni na
Mungu visivyoweza kutenganishwa. Siku alizokuwa
zimehesabiwa kuwa hai zilipita, akawa akiishi kwa neema.
Amefika mahali hawezi kutembea, hukaa kwa msaada, kula
kwa msaada, nafsi yake ikainama mwisho anauona
umekaribia.
Akaanza kupanga utaratibu wa kuwaachia urithi kwa mke
wake na watoto, na kuwapa ushauri. Akiwa anafanya hivyo
ndani yake anashuhudiwa kazi yake bado hajamaliza.
Akaandika urithi na kuwatia moyo watoto wake kuishi
katika utauwa na kumtafuta Mungu. Ndugu zake waliokuwa
mbali walianza kusogea karibu kumsalimia. Sio kwa lengo la
kumsalimia kama walivyokuwa wakisema bali kuepusha
usumbufu kuwa akifariki wasipate shida kusafiri kwenda
kwenye mazishi yake.
Siku moja akiwa kitandani huku moyo wake ukiwa na
maswali, akawaza moyoni mwake ivi kweli Mungu
ameshindwa kuniponya na hii kansa? Akasema nitaenda
kuangalia kwenye biblia Mwanzo mpaka ufunuo ili nione
kama kweli Mungu ameniandikia kufa na huu ugonjwa.
Akawa akisoma kwa shida anatafuta uthibitisho wa
kujiridhisha kuwa hawezi kupona. Akajisemea moyoni kama
nikikuta Mungu ameandika nitakufa kwa ugonjwa
nitakubaliana naye la kama si hivyo sitakubali kufa.
UHURU WA KWELI 125
Akawa akisoma na kuipitia biblia kuangalia mahali
palipoandikwa kuwa atakufa kwa ugonjwa. Hakuona mahali
popote, alipoendelea kusoma akakuta mahali
pameandikwa;
“Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili
wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe
hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake
mliponywa” [1Pet 2:24]
Andiko hili lilimtia moyo akasema sina sababu ya kufa kwa
sababu nilishalipiwa deni la dhambi. Mimi ni mwenye haki,
akaendelea kujisemea moyoni mwake kwa kupigwa kwake
mliponywa. Siku zikapita, wiki zikapita hadi mwezi ukapita,
lakini bado hali yake iliendelea kuwa mbaya. Akasema
moyoni mwake sitajali mimi nataka kufa kupitia hili andiko.
Siku zikaendelea kupita, wiki ukafika mpaka mwezi wa pili
ulifika bila kuona matokeo.
Siku moja usiku akiwa amelala kitandani, aliwaona watu
wamekuja wakiwa wamevaa mavazi meupe ya kidaktari
wakiwa wameshika visu na vyombo vya upasuaji. Akiwa
usingizini akawa anaona wanamvua nguo ya juu wanaanza
kunyofoa nyama kwenye ule uvimbe (kansa). Anasema
ilikuwa ni kama mda wa dakika tano wale watu wakapotea.
Aliposhtuka usingizini anaona kweli kabisa vifungo vya shati
lake vimefunguliwa, na anaona kwenye tumbo lake hakuna
mahali penye maumivu kama vile hajawahi kuumwa kabisa.
UHURU WA KWELI 126
Akapiga kelele kwa nguvu huku akisema nimepona!
nimepona! Ameni haleluya
Ugonjwa ulikuwa hauponyeki, madaktari walisema
amechelewa hawezi kupona, watumishi wakubwa na
maarufu walimuombea lakini hakupona. Bado alimuamini
Mungu na alipokea uponyaji. Hii inaonyesha wazi haijalishi
ni changamoto gani ngumu unapitia lakini bado Mungu
anaweza kukusimamisha.
Moja ya vitu vimekuwa changamoto kubwa sana hasa
katika kizazi hiki ni kuziishi changamoto zao na mambo
yaliyopita. Paulo alisema hivi;
“Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha
kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo
nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele” [Filip 3:13]
Paulo alijua kuwa huko nyuma aliwahi kuwatesa watumishi
wa Mungu kwa kuwauwa na kupinga wokovu. Kiasi
ambacho alikuwa akifikiria makosa yake, Lakini alifika
mahali akaacha kufikiria mambo yote yaliyopita kwenye
maisha yake na kusema “natenda neno moja tu
nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo
mbele”. Kwa sababu alijua mambo yaliyofanyika nyuma
hayana nafasi ya kuamua hatima yake.
UHURU WA KWELI 127
Kuwa na changamoto katika maisha bado hakukuzuii wewe
kuishi vile unavyotakiwa kuishi. Unaweza kuwa na
changamoto, unashida, uchumi wako sio mzuri,
changamoto kwenye ndoa yako na mahali popote pale
lakini bado ukaendelea kuishi vile unavyotakiwa kuishi.
Wakati wote Mungu yuko tayari kushughulika na
changamoto zako hata kama zinaoneka ni ngumu kiasi gani,
hata kama zinaonekana hazitatuliki. Angalia maagizo
ambayo Mungu aliwapa wana wa Israeli;
Wakasafiri kutoka mlima wa Hori kwa njia ya Bahari ya
Shamu; ili kuizunguka nchi ya Edomu, watu wakafa moyo
kwa sababu ya ile njia. Watu wakamnung'unikia Mungu, na
Musa, Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili
tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji,
na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu. Bwana akatuma
nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi
wakafa. Watu wakamwendea Musa, wakasema,
Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung'unikia Mungu,
na wewe; utuombee kwa Bwana, atuondolee nyoka hawa.
Basi Musa akawaombea watu. Bwana akamwambia Musa,
Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa
kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi. Musa akafanya
nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka
amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.
[Hes 21:4-9]
UHURU WA KWELI 128
Wana wa Israeli walikuwa katika safari kuelekea Misri
walifika mahali wakachoka. Wakataka kufuata njia zao kwa
sababu walichoka na ile njia, wakamnung’unikia Musa.
Mungu akatuma nyoka za moto zikawauma watu wengi
wakafa, wakarudi kwa Musa. Kumwambia awaombee kwa
Mungu wawaondolee nyoka, Musa akawaombea kwa
Mungu. Mungu akamwambia Musa jifanyie nyoka wa shaba
na kila atakayemwona ataishi. Musa alipoifanya ile nyoka
ya shaba na kila aliyeitazama ile nyoka ya shaba aliishi.
Inawezekana kuna watu nyoka zilikuwa zikiwauma lakini
kila aliyeitazama nyoka ya shaba aliishi.
Nyoka ya shaba ilikuwa ni lugha ya picha inamuwakilisha
Yesu Kristo katika agano jipya aliyeinuliwa mtini kwa sababu
ya makosa yetu na dhambi zetu. Kristo anashuhudia kuwa
alikuja kuzivunja kazi za yule adui mwovu Shetani. Pia
anasema alikuja kushughulikia maisha yetu tena maisha
tele. Imeandikwa;
“Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja
ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.” [Yoh 10:10]
Shetani kazi yake ni kuiba kuchinja na kuharibu, lakini
ashukuriwe Yesu alikuja ili tuwe na uzima KJV anasema ili
wawe na maisha tena maisha tele. Maana yake tukiishi
katika Kristo tunaweza kusimama tena, Bwana atatuinua na
kutuweka mahali tunapostahili. Kama ni hivyo basi hatuna
budi kuishi katika Kristo maana yeye ndiye mwenye maisha
UHURU WA KWELI 129
na yeye ndiye anayeweza kutusimamisha wakati wote
kwenye maisha yetu. Paulo aliandika hivi;
“tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena
kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye
aliyekufa akafufuka kwa ajili yao.” [2Kor 5:15]
Tafsiri ya Biblia ya Habari Njema anasema hivi;
“Alikuja kwaajili ya watu wote, ili wanaoishi wasiishi
kwaajili yao wenyewe, bali kwaajili yake yeye aliyekufa,
akafufuliwa kwaajili yao”
Biblia inashuhudia kuwa tunatakiwa kuishi kwaajili yake
yeye aliyekufa na kufufuliwa kwaajili yetu yaani Yesu Kristo.
Kwanini tunatakiwa kuishi katika Kristo Yesu?
Tangu mwanzo haikuwa mpango wa Mungu tuishi
kwaajili yetu, bali tuishi katika yeye (Yesu Kristo).
Roho zetu zimeathiriwa kwa zawadi, vipawa,
huduma na kazi ambavyo haviwezi kujidhihirisha
kuwa halisi katika macho ya damu na nyama kwa
nguvu zetu bali kwa msaada wake mwenyewe (Yesu
Kristo).
Hakuna jambo tutalifanya sisi wenyewe likawa ni
bora mbele za Mungu bila neema ya Kristo.
UHURU WA KWELI 130
Lolote tutakalolifanya kwa juhudi zetu, hata kama
limefikia kiwango cha mwisho cha juhudi zetu bado
litaonekana liko chini ya kiwango mbele za Mungu
pasipo neema ya Mungu.
Kufanya jambo lolote sisi wenyewe bila kupitia kwa
Yesu Kristo ni sawa na kusema sihitaji msaada wako
Mungu.
Kufanya jambo lolote sisi wenyewe bila neema ya
Kristo ni kuishi maisha ya kuchanganyikiwa, msongo
wa mawazo na maisha ya kufeli.
Kufanya sisi wenyewe bila neema ya Kristo ni sawa
kusema sihitaji msaada wako mkombozi (Yesu
Kristo). Ni kukataa kazi kamilifu ya Kristo iliyofanyika
pale msalabani.
Kufanya sisi wenyewe ni kujizuia sisi halisi
kujidhihirisha katika macho ya damu na nyama.
Tangu mwanzo haikuwa mpango wa Mungu tuishi kwaajili
yetu, bali tuishi katika yeye (Yesu Kristo).
Yesu Kristo alikuwepo tangu mwanzo kwenye uumbaji,
japokuwa biblia imemuelezea kwa lugha ya picha. Kwa
maana nyepesi ni kwamba alikuwepo lakini alikuwa
hajajifunua.
UHURU WA KWELI 131
i. Yesu ni nuru.
Mungu wakati anaumba dunia alisema na Iwe nuru. Kama
ilivyoandikwa;
“Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru” [Mwa 1:3]
Ile nuru iliyotokea ikaangaza duniani. Ikaangaza mchana na
usiku alikuwa ni Yesu Kristo.
Yesu Kristo aliye nuru aliwaongoza wana wa Israeli mchana
na usiku kwa mfano wa nguzo. Maandiko yanasema;
“Bwana naye akawatangulia mchana ndani ya wingu
mfano wa nguzo, ili awaongoze njia; na usiku, nadi ya moto
mfano wa nguzo, ili kuwapa nuru; wapate kusafiri mchana
na usiku” [Kut 13:21]
Yesu ndiye aliwaongoza Wana wa Israeli mchana na usiku
kwa mfano wa nguzo. Yesu ndiye aliyeachilia nuru wakiwa
jangwani na kuwaongoza.
Daudi alishuhudia kuwa Bwana ni nuru. Imeandikwa kuwa;
“Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope
nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?”
[Zab 27:1]
Daudi alisema hakuna wa kumhofu kwa sababu Bwana
yaani Yesu Kristo ni nuru yake na wokovu wake.
UHURU WA KWELI 132
Katika Isaya iliandikwa kuwa Bwana ni nuru. Imeandikwa;
“Jua halitakuwa nuru yako tena wakati wa mchana, Wala
mwezi hautakupa nuru kwa mwangaza wake; Bali Bwana
atakuwa nuru ya milele kwako, Na Mungu wako atakuwa
utukufu wako” [Isa 60:19]
Katika Isaya iliandikwa kuwa jua halitakuwa nuru wala
mwenzi. Alisema Bwana atakuwa nuru ya milele na
utukufu.
Yohana anashuhudia kwamba Yohana mbatizaji alikuja ili
aishuhudie ile nuru yaani Yesu Kristo. Imeandikwa;
“Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote
wapate kuamini kwa yeye” [Yoh 1:7]
Yesu alisema mwenyewe kuwa ni nuru ya ulimwengu na
yoyote anayemfuata hatakwenda gizani. Biblia inasemsa;
Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya
ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe,
bali atakuwa na nuru ya uzima” [Yoh 8:12]
Yesu alirudia tena kusema mda aliopo ulimwenguni yeye ni
Nuru ya ulimwengu. Imeandikwa;
“Muda nilipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu”
[Yoh 9:5]
UHURU WA KWELI 133
Kwa mara ya tatu Yesu alirudia kesema mimi ni nuru ya
ulimwengu na anayemwamini asikae gizani.
“Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu
aniaminiye mimi asikae gizani” [Yoh 12:46]
Yohana alifunuliwa kuwa nuru na taa ya mbinguni ni
Mwanakondoo yaani Yesu Kristo.
“Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa
maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni
Mwana-Kondoo” [Ufu 21:23]
ii. Yesu ni Neno.
Neno la uumbaji lililokuwa likitoka kinywani mwa Mungu.
Neno la uumbaji alikuwa ni Yesu Kristo, yaani Yesu Kristo
ndiye aliyekuwa akiumba. Imeandikwa;
“Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako
kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo
alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala
pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Ndani
yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru
ya watu. Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.
Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake
Yohana. Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru,
UHURU WA KWELI 134
wote wapate kuamini kwa yeye. Huyo hakuwa ile nuru, bali
alikuja ili aishuhudie ile nuru. Kulikuwako Nuru halisi,
amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu.
Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata
kuwako, wala ulimwengu haukumtambua. Alikuja kwake,
wala walio wake hawakumpokea. Bali wote waliompokea
aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale
waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa
mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa
Mungu. Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi
tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee
atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.” [Yoh 1: 1-14]
Yohana anashuhudia kwamba hapo mwanzo palikuwa na
Neno ambaye alikuwa Mungu. Huyo neno alifanyika mwili,
tukauona utukufu wake kama wa Mwana pekee yaani Yesu
Kristo.
iii. Yesu ni Mti wa Uzima.
Mti uliopandwa katikati ya bustani ya Edeni alikuwa ni Yesu
Kristo. Biblia inashuhudia kwamba;
UHURU WA KWELI 135
“Bwana Mungu akachipusha katika ardhi kila mti
unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa
uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na
mabaya” [Mwa 2:9]
Katikati ya bustani kulikuwa na mti wa uzima na mti wa ujuzi
wa mema na mabaya. Mti wa uzima alikuwa ni Yesu Kristo
japokuwa umezungumziwa kwa lugha ya picha. Lakini pia
katikati ya bustani kulikuwa na mti wa ujuzi wa mema na
mabaya ilikuwa ni sheria za Musa zimezungumzwa kwa
lugha ya picha. Shetani alipokuwa anawadanganya Adamu
na Hawa, unaweza kufikiri alisema uongo mkubwa kumbe
ni kidogo. Shetani alianza kwa kuwadanganya Adamu na
Hawa halafu baadaye akaanza kuwaambia ukweli. Biblia
inashuhudia kwamba;
“Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa
maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula
matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi
mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya” [Mwa
3:4-5]
Kumbe Shetani aliwadanganya Adamu na Hawa kuwa
hamtakufa. Huu ni uongo kwa sababu Mungu aliwaagiza
Adamu na Hawa kuwa wakila matunda ya mti wa ujuzi wa
mema na mabaya msiyale wala kuyagusa msije mkafa (Mwa
3:3). Shetani alivyosema hamtakufa aliwadanganya.
Baadae Shetani akaendelea kuwaeleza ukweli kwamba siku
UHURU WA KWELI 136
mtakayokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya
ulioko katikati mtafumbuliwa macho (maana yake mtakuwa
na ufahamu). Mkijua mema na mabaya, yaani mtaujua
wema na ubaya, na hiki ndicho kilichowatokea Adamu na
Hawa baada ya kula tunda. Biblia inashuhudia kwamba;
“Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula,
wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa,
basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na
mumewe, naye akala. Wakafumbuliwa macho wote wawili
wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini,
wakajifanyia nguo” [Mwa 3:6-7]
Kumbe Adamu na Hawa walipokula tunda ni kweli
walifumbuliwa macho wote wawili. Wakajikuta wako uchi,
kumbuka Mungu aliwaumba tangu mwanzo Alipomuumba
Adamu (Mwa 2:7) na Hawa (Mwa 2:21-23). Walikuwa
hawana ufahamu kuwa wako uchi, walianza kupata
ufahamu wa kujua kukaa uchi ni kubaya baada ya kula
tunda.
Mungu hakutaka Adamu na Hawa waishi kwa kujua mema
na mabaya (kuishi kwa sheria) bali waishi katika yeye.
Walipokula matunda ya ujuzi wa mema na mabaya Mungu
aliwafukuza katika bustani ya Edeni. Jambo la kushangaza
Mungu aliwazuia Adamu na Hawa wasiirudie njia
inayoiendea mti wa uzima (yaani Yesu Kristo). Kwa sababu
UHURU WA KWELI 137
Mungu hakutaka waishi kwa kuchanganya ujuzi wa mema
na mabaya na wakati huo huo kuishi katika Kristo Yesu.
Yesu ni mti wa uzima.
Yohana alionyeshwa maono kuwa Yesu Kristo ni mti wa
uzima. Imeandikwa;
“Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza
na wa mwisho. Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri
kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango
yake. Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na
wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye
uongo na kuufanya. Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu
kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi
ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye
kung'aa ya asubuhi” [Ufu 22:13-16]
Yesu Kristo alisema yeye ni Alfa na Omega, ukisoma tafsiri
ya biblia ya King James Version (KJV). Anasema
wamebarikiwa wote wanaofanya amri zake na wana haki
katika mti wa uzima yaani Yesu Kristo. Ukiwa ndani ya Kristo
unakuwa na haki ya kuingia katika milango ya mji ule yaani
mbinguni. Baadae anasema ni mimi Yesu niliye shina na
mzao wa Daudi nyota yenye kung’aa asubuhi.
Yohana alifunuliwa kuwa Yesu ni mti wa uzima ulioko
katikati ya bustani ya Mungu. Biblia inasema;
UHURU WA KWELI 138
“Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho
ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula
matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu”
[Ufu 2:7]
Mti wa ujuzi wa mema na mabaya ni sheria ya Musa.
Japokuwa wapo watumishi wa Mungu waliweza kuujua
ubaya kabla ya sheria kumi za Musa. Kwa mfano Yusufu
aligundua kuwa uzinzi ni ubaya mkubwa kwa Mungu na
alikataa kulala na mke wa Potifa (Mwanz 39:9b). Maana
yake ni neema pekee inayoweza kukusaidia kushinda
dhambi. Mti wa ujuzi wa mema na mabaya ulikuwa
unazungumziwa kwa lugha ya picha kuwa ni sheria za Musa.
Kwa sababu ya tabia za sheria za Musa zilivyokuwa
ziliwekwa ziliwekwa ili watu waweze kujua mema na
mabaya.
Tuangalie ngazi tatu za sheria [lakini Mungu anataka tuishi
kwa sheria yake (sheria ya Mungu)].
UHURU WA KWELI 139
i. Ngazi ya kwanza ya sheria (sheria ya Musa)
Sheria Kumi za Mungu.
Imeandikwa;
“Mungu akanena maneno haya yote akasema, Mimi ni
Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri,
katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila
mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu
cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani,
wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala
kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni
Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba
zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami
nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri
zangu.
Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana
hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi,
utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya
Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe,
wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako,
wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala
mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita
Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote
vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana
UHURU WA KWELI 140
akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa. Waheshimu baba
yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika
nchi upewayo na Bwana, Mungu wako. Usiue. Usizini.
Usiibe. Usimshuhudie jirani yako uongo. Usiitamani
nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako;
wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe
wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani
yako. [Kut 20:1-17]
Mti wa ujuzi wa mema na mabaya uliokuwa
unazungumziwa zilikuwa ni sheria kumi za Mungu, kwa
sababu ya tabia zake kwa mfano usizini, kinyume cha
kutozini ni kuzini. Sheria zilikuwa zinaeleza ubaya na wema
kwa wakati mmoja, sheria hizi zilitolewa ili watu wajue
mema na mabaya.
Ndio maana Paulo anasema hivi;
“kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki
mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua
dhambi huja kwa njia ya sheria. Lakini sasa, haki ya Mungu
imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na torati na
manabii; ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika
Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti;
kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na
utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema
yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; ambaye
Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya
UHURU WA KWELI 141
imani katika damu yake,ili aonyeshe haki yake ,kwa sababu
ya kuziachilia katika ustahimili wa MUNGU dhambi zote
zilzotangulia kufanywa. apate kuonyesha haki yake wakati
huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabu haki yeye
amwaminiye Yesu.
Ku wapi, basi, kujisifu? Kumefungiwa nje. Kwa sheria ya
namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! Bali kwa sheria
ya imani. Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa
haki kwa imani pasipo matendo ya sheria. Au je! Mungu ni
Mungu wa Wayahudi tu? Siye Mungu wa Mataifa pia?
Naam, ni Mungu wa Mataifa pia; kama kwa kweli Mungu
ni mmoja, atakayewahesabia haki wale waliotahiriwa
katika imani, nao wale wasiotahiriwa atawahesabia haki
kwa njia ya imani iyo hiyo. Basi, je! Twaibatilisha sheria kwa
imani hiyo? Hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.
[Rum 3:20-31]
Paulo anathibitisha kwamba hakuna mwanadamu mwenye
mwili atakayehesabiwa haki wa matendo ya sheria. Halafu
anatoa sababu ya matendo ya sheria (sheria za Musa) kuwa
kutambua dhambi au kuwa na maarifa ya dhambi kama KJV
alivyosema. Sheria za Musa zilikuja kwaajili ya kujua mema
na mabaya, yaani wema na ubaya ulijulikana kwa sheria za
Musa na biblia inaeleza wazi hakuna atakaye hesabiwa haki
kwa sababu ya hizo sheria bali kwa njia ya Kumwamini Yesu
UHURU WA KWELI 142
Kristo. Paulo anaendelea kusema hiyo haki ya Mungu
ipatikanayo kwa njia ya sheria inashuhudiwa na torati yaani
sheria (KJV) na manabii. Kuwa haki ya Mungu hupatikana
kwa imani ya Yesu Kristo. Maana yake sheria na manabii
zinakubali kuwa kwa imani ya Yesu Kristo tunahesabiwa
haki. Paulo anasema sasa ku wapi kujisifu? Kwa sababu
kujisifu kwa matendo ya sheria kumefungiwa nje (KJV
anasema kumeondolewa) yaani hakuna awezaye kujisifia
kwa sababu ya matendo ya sheria (matendo meama). Lakini
kila mtu ana uhuru wa kujisifia kwa sheria ya imani yaani
Sheria ya kumwamini Yesu Kristo. Paulo anamalizia kwa
kusema kinyume cha kuwa na sheria ya imani yaani kutaka
kuhesabiwa haki kwa matendo ya sheria, ni kuifanya sheria
ya imani sio kitu bali sheria ya matendo ya sheria ambayo
hatuwezi kuhesabiwa haki ya Mungukwa hiyo.
Ndio maana Paulo aliwaandikia Wagalatia hivi;
“hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa
matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi
tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya
Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo
ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki”
[Gal 2:16]
UHURU WA KWELI 143
Paulo anaendelea kusisitiza kwamba hakuna mwenye mwili
atakayeweza kuhesabiwa haki kwa matendo ya sheria. Bali
tunahesabiwa haki kwa njia ya imani ya Yesu Kristo
tunahesabiwa haki. Paulo anaendelea kusisitiza kuwa wale
walio wa matendo ya sheria wako chini ya laana.
Imeandikwa;
“Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako
chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu
asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha
torati, ayafanye” [Gal 3:10]
Maana yake kila mtu anayeishi kwa matendo ya sheria yuko
chini ya laana. Yaani kuishi kwa matendo ya sheria hali
kwamba umekataa kumwamini Yesu Kristo na kukubali
kuipokea haki yake kwa imani na kuishi kwa matendo yako
mema (matendo ya sheria) uko chini ya laana. Ndio maana
Luka alishuhudia kwamba;
“Basi na ijulikane kwenu, ndugu zangu, ya kuwa kwa huyo
mnahubiriwa msamaha wa dhambi; na kwa yeye kila
amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote
asiyoweza kuhesabiwa haki kwa torati ya Musa” [Mat
13:38-39]
Luka alisema kwa Yesu Kristo tunahubiriwa msamaha wa
dhambi na kwa yeye tunahesabiwa haki katika mambo
tusiyoweza kuhesabiwa haki kwa sheria ya Musa. Ndio
UHURU WA KWELI 144
maana Paulo alisema mmeanguka katika hali ya neema
mnaotaka kuhesabiwa haki kwa matendo ya sheria (Gal
5:4).
Je tutende dhambi hali tukijua tunahesabiwa haki kwa
imani ya Yesu Kristo?
La hasha! Paulo alijibu swali linaloendana na hili. Biblia
inasema;
“Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi
kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena
katika dhambi? Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa
katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi
tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti
yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia
ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika
upya wa uzima” [Rum 6:1-5]
Paulo anasema sisi tuliobatizwa katika Yesu Kristo tulizikwa
na Yesu Kristo katika mauti yake. Maana yake tuliifia
dhambi na ndio maana Yesu Kristo alivyofufuka tulifufuka
pamoja naye. Na kwa namna hiyo tulihesabiwa haki pamoja
naye ili kusudi tuenende katika upya wa maisha (KJV
anasema).
UHURU WA KWELI 145
Mungu anataka tuishi katika Yesu Kristo peke yake.
Mungu anataka tuishi katika yeye (Yesu Kristo). Adamu na
Hawa walipokula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya
(sheria za Musa). Mungu hakutaka waende kula matunda
ya mti wa uzima (Yesu Kristo). Imeandikwa;
“Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama
mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije
akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa
uzima, akala, akaishi milele; kwa hiyo Bwana Mungu
akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo
katika hiyo alitwaliwa. Basi akamfukuza huyo mtu,
akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya
Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda
njia ya mti wa uzima” [Mwa 3:22-24]
Mwanadamu alipokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema
na mabaya (sheria za Musa) alikuwa amejichafua kiasi
ambacho Mungu hakutaka auendee mti wa uzima (Yesu
Kristo), kwa sababu sio mfumo wa maisha ambao Mungu
aliukusudia, yaani mfumo wa kuishi kwa sheria na kuishi
katika Yesu Kristo. Mungu alikusudia watu waishi katika
yeye tu yaani Yesu Kristo . Hii ndiyo sababu baada ya
anguko la Adamu na Hawa Mungu aliandaa mpango wa
kumwondoa mwanadamu kutoka kuishi maisha ya
matendo ya sheria, na kuanza kuishi maisha katika Yesu
Kristo (2 Kor 5:14-15).
UHURU WA KWELI 146
(ii) Ngazi ya pili ya sheria
Yesu aliongezea ukali katika sheria za Musa. Lakini alisema
hata katika hizo hamjakamilishwa bado. Mathayo 5:17-48
17:Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii;
la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
Yesu hakuja kuitangua torati, au kuivunja torati bali alikuja
kuitimiliza torati, Mungu hana shida na sheria wala hakuna
shida yoyote katika sheria za Mungu. Yeye Mungu hakutaka
tuishi kwa torati, bali kwa neema. Sheria ni nzuri, ni takatifu
na ni kamilifu lakini huwezi kuwa mkamilifu au mtakatifu
kwa kuishi kwa matendo ya sheria. Bali kwa kuishi katika
yeye (2Kor 5:15), kwa sababu ukiishi katika yeye unakuwa
mkamilifu na mtakatifu kwa njia ya imani.
Sheria ya Musa ilikuwa haijatimilika lakini Yesu alikuja
kuitimiliza kwa njia ya neema na kweli. Yohana aliandika
kuwa; torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli
zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo. Maana yake neema na
kweli zilikuja kuitimiliza sheria ya Musa. Ukiishi kwa sheria
ya Musa pamoja na kwamba ni nzuri, kamilifu na takatifu,
lakini bado mbele za Mungu haitakufanya uwe mkamilifu au
mtakatifu. Utahesabiwa kuwa mkamilifu na mtakatifu kwa
kuishi kwa neema na kweli yaani neno la Mungu katika Yesu
Kristo.
UHURU WA KWELI 147
18: Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi
zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati
haitaoondoka ,hata yote yatimie.
Yesu anaendelea kusisitiza kuwa hata mbingu na nchi
zitakapoondoka hakuna torati itakayoondolewa hata yote
yatimie. Yesu hakuja kuvunja sheria bali kuitimiliza kwa
neema na kweli.
19: Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi
zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo
kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda
na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa
mbinguni.
Anaendelea kusema yoyote atakayevunja amri hizo zilizo
ndogo, na kuwafundisha watu hivyo ataitwa mdogo kabisa
katika ufalme wa mbinguni. Atakayezitenda na kuzifundisha
ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. Nilazima
uzitende kwa ukamilifu na kuzifundisha. Yesu anasisitiza
kuwa hakuja kuvunja sheria bali kuitimiliza sheria.
20: Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo
haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe
katika ufalme wa mbinguni.
UHURU WA KWELI 148
Yesu anasema haki yenu isipozidi haki ya Waandishi na
Mafarisayo hamtaingia kamwe katika ufalme wa Mbinguni.
Haki ya Waandishi na Mafarisayo ilikuwa ni ya matendo ya
sheria. Waandishi na Mafarisayo waliamini kuwa haki ya
matendo ya sheria ndiyo itakayowapa kibali cha kuingia
mbinguni pamoja na kwamba wanamkataa Yesu Kristo.
Yesu aliweka wazi kuwa haki yenu nilazima izidi haki ya
waandishi na Mafarisayo, ambayo hiyo haki haipatikani kwa
matendo ya sheria bali kwa imani ya Yesu Kristo. Paulo
aliwaambia Warumi; Lakini mtu afanyaye kazi, ujira wake
hauhesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni (Rum 4:4)
Maana yake mara zote jambo unalolifanyia kazi sio neema
tena bali ni deni. Mungu akitazama juhudi zako binafsi
halafu haoni ukimuishia Yesu Kristo kazi yako ni bure mbele
zake. Waandishi na Mafarisayo waliamini kwa matendo ya
sheria tu wanahesabiwa haki mbele za Mungu. Hawakujua
kumbe matendo yao ya sheria hayawezi kuwakamilisha
asipokuwepo Yesu Kristo. Ndio maana Yesu alitoa mfano
huu;
“Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni
wenye haki, wakiwadharau wengine wote. Watu wawili
walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili
mtoza ushuru. Yule Farisayo akasimama akiomba hivi
moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si
kama watu wengine, wanyang'anyi, wadhalimu, wazinzi,
UHURU WA KWELI 149
wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi nafunga mara mbili
kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote. Lakini
yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu
hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua
akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.
Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake
amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye
atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa” [Luk 18:9-14]
Maombi yana nguvu sana ya kuleta majibu, sadaka na fungu
la kumi likitolewa kwa imani linaleta matokeo makubwa
sana kwenye maisha ya mtu. Kibinadamu Farisayo alikuwa
yuko sawa ni Mtakatifu na anastahili kuhesabiwa haki lakini
shida ilikuwa kwenye eneo la imani alikoweka Farisayo,
Farisayo aliamini matendo yake ya sheria yanaweza
kumkamilisha. Kufunga na kutoa zaka akasahau kwamba
akifanya hayo yote bila kuweka imani yake kwa Mungu
atakuwa anafanya kazi bure. Yaani mbele za Mungu
atakuwa anadeni kama ilivyoandikwa katika Warumi 4:4.
Je tusifunge na kuomba hali tukijua tumeshahesabiwa
haki kwa imani na sio matendo ya sheria?
Hapana! Nilazima tufunge na kuomba kwa sababu kufunga
na kuomba ni mpango halisi wa Mungu kwa mwanadamu.
Fahamu kwamba jambo lolote unalolifanya, likiwekewa
UHURU WA KWELI 150
imani hilo kuwa ndio linalokuleta majibu. Tambua kwamba
Mungu analihesabu kuwa ni tendo la sheria. Ukiamini
kwamba mpaka niombe au nifunge ndio nitapata majibu,
au maombi yangu na kufunga yanajitosheleza mbele za
Mungu kunipatia haki au ninachokihitaji. Ukajifungia kuwa
sheria na ukajiwekea kuwa huo ndio msimamo wako, kuwa
bila kufanya hivyo huwezi kupata unachokitaka kwa
Mungu.
Jua kwamba imani yako iko katika matendo yako na sio kwa
Mungu. Hivi ndivyo huyu Farisayo alikuwa akiishi, sadaka
inaweza kuuhusisha ufalme wa Mungu kutenda kazi kwa
aniaba yako. Vivyo hivyo maombi, kufunga na matendo
mema havina shida kuvifanya, shida inaanzia pale
utakapoanza kuyaamini hayo kuwa kwa hayo pekee
yanakufanya kuwa mwenye haki mbele za Mungu na kuwa
mwongozo wa maisha yako, na sio katika imani ndani ya
Yesu Kristo, hapo jicho la Mungu linaona unafanya matendo
ya sheria. Hiki ndicho kilikuwa kimemsababisha Farisayo
asihesabiwe haki.
Fikiria kama Farisayo angeenda mbele za Mungu kuomba
kwa unyenyekevu. Na kumwambia Mungu pamoja na
kwamba ninafunga, pamoja na kwamba ninatoa zaka katika
mapato yangu yote. Bado ninaamini wewe ndiye
unayeweza kunisaidia na kunipa baraka na kuniwezesha.
Naamini Farisayo angehesabiwa haki kuliko Mtoza ushuru.
UHURU WA KWELI 151
Ni muhimu sana kufanya kwa juhudi zote matendo mema,
lakini ni muhimu zaidi kufanya kwa juhudi huku imani yetu
ikiwa mbele za Mungu. Yesu Kristo aliyekufa kwaajili yetu
kwa juhudi zake ili sisi tupate kibali, neema na haki kwaajili
yake.
21: Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu
akiua, itampasa hukumu.
22: Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake
hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake,
itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum
ya moto.
23: Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku
ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,
24: iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako,
upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka
yako.
25: Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja
naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na
kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.
26: Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe
kulipa senti ya mwisho.
UHURU WA KWELI 152
27: Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;
28: lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye
mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye
moyoni mwake.
29: Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali
nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee
wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
30: Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe
mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja
kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
31: Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati
ya talaka;
32: lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe,
isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi;
na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
33: Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape
uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako;
34: lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa
mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;
35: wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu
yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa
Mfalme mkuu.
UHURU WA KWELI 153
36: Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya
unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
37: Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa
kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.
38: Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino
kwa jino;
39: Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu;
lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili.
40: Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako,
mwachie na joho pia.
41: Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja,
nenda naye mbili.
42: Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe
kisogo.
43: Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na,
Umchukie adui yako;
44: lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu,
waombeeni wanaowaudhi,
45: ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni;
maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema,
huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
UHURU WA KWELI 154
46: Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata
thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi
yayo hayo?
47: Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani
la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama
hayo?
Yesu aliongeza ukali wa sheria ya Musa, pamoja na sheria
zilizokuwa zimeandikwa katika kitabu cha torati, lakini bado
hizo sheria zote alizozitaja zilikuwa haziwezi kutukamilisha.
Katika mstari wa mwisho katika sura hii ya tano Yesu
anamalizia kwa kusema;
48: Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa
mbinguni alivyo mkamilifu.
Yesu anasema mtakuwa wakamilifu kama Baba yenu wa
mbinguni alivyo mkamilifu. Huu ni wakati ujao ndio maana
anasema mtakuwa wakamilifu, ingekuwa kwa hizo sheria
alizooneza makali zingekuwa ni kamilifu basi angesema;
Hata sasa mmekuwa wakamilifu kwa hizo sheria, lakini kwa
sababu hata hizo haziwezi kutukamilisha kuwa wakamilifu
na watakatifu ndio maana akasema mtakuwa wakamilifu.
UHURU WA KWELI 155
(iii) Ngazi ya tatu ya Sheria (sheria ya Mungu kamilifu)
Yesu Kristo ni sheria iliyokamilifu. Warumi 10:1-4
1: Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua
yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe.
Paulo aliwaombea watu waokolewe. Kwasababu alijua
wokovu unapatikana bure kwa njia ya imani ya Yesu Kristo.
2: Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa
ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa.
Paulo alisema wanajuhudi katika Mungu lakini si katika
maarifa. Kama lilivyo kanisa la sasa wanajuhudi katika
Mungu lakini si katika maarifa. Na ndio maana Mungu
anawakataa watu wasikae katika nafasi ya ukuhani
(uongozi). Hosea aliandika hivi;
“Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa
kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa
wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau
sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto
wako” [Hos 4:6]
UHURU WA KWELI 156
Kumbe kwa kukosa maarifa watu wanaangamizwa, na
Mungu anawaondoa katika nafasi ya ukuhani (uongozi)
kwake, kwa sababu ya kusahau sheria ya Mungu, Mungu
naye anasema atawasahau watoto wako.
3: Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na
wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini
ya haki ya Mungu.
Paulo anaendelea kusema; hawaijui haki ya Mungu,
wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe. Tafsiri ya biblia ya
King James Version (KJV) anasema; Kwa maana ni wajinga
wa haki ya Mungu. Kwa sababu ni wajinga wa haki ya
Mungu, wanaenda kujitafutia haki zao wenyewe na
kuzipeleka mbele za Mungu. Wakifikiri watahesabiwa haki
kwa hizo, lakini kumbe sivyo Mungu anavyoitazama haki.
4: Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye
ahesabiwe haki.
Paulo anathibitisha kuwa Yesu Kristo ni mwisho wa sheria.
Tafsiri ya biblia ya New International Version anasema; Kwa
maana Yesu Kristo ni kilele cha sheria. Pasipo yeye huwezi
kuhesabiwa haki. Ndio maana Mungu anataka uishi kwa
kumtegemea yeye na kumwamini yeye, Ameni Haleluya.
UHURU WA KWELI 157
Katika yeye kuna kuhesabiwa haki, utakatifu, kuto kuwa na
hatia, kutukuzwa, ni wafalme, kubarikiwa (Rum 8:29-30, Efe
1:3-6, 1:21, 2:6). Sheria nyingine si kitu kama haumtumainii
Yesu Kristo na hauishi katika yeye, Paulo alisema hivi;
“Namshukuru Mungu kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi
kama ni hivyo kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu”
[Rum 7:25a]
Paulo anasema anamshukuru Mungu kwa Yesu Kristo na
kuitumikia sheria ya Mungu. Ipatikanayo kwa njia ya imani
ya Yesu Kristo. Ndio maana imeandikwa hivi katika Biblia ya
Habari Njema;
“Alikufa kwaajili ya watu wote, ili wanaoishi wasiishi
kwaajili yao wenyewe, bali kwaajili yake yeye aliyekufa,
akafufuliwa kwaajili yao” [2Kor 5:15]
Kumbe hatutakiwi kuishi kwaajili yetu tena bali kwaajili ya
Yesu Kristo aliyekufa kwaajili yetu na kufufuka kwaajili yetu.
Juhudi zetu, maarifa yetu, uwezo wetu binafsi
hautatusaidia kitu bila msaada wa Yesu Kristo na kuamini
kikamilifu kazi aliyoifanya pale msalabani kwaajili yetu.
Ndio maana Marko aliandika hivi;
UHURU WA KWELI 158
“nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote,
na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa
nguvu zako zote” [Mark 12:30]
Ukisoma Tafsiri ya KJV anasema Kumpenda Bwana Mungu
wako kwa moyo wako wote na nafsi yako yote na akili yako
yote hii ndiyo sheria ya kwanza. Sheria yetu ya kwanza
nilazima tumwamini Yesu Kristo kwaajili ya kile
alichokifanya pale msalabani kwaajili yetu kikamilifu.
Roho zetu zimeathiriwa kwa zawadi, vipawa, huduma na
kazi ambavyo haviwezi kujidhihirisha kuwa halisi katika
macho ya damu na nyama kwa nguvu zetu bali kwa
msaada wake mwenyewe (Yesu Kristo).
Mungu, Roho Mtakatifu alishaachilia zawadi, vipawa,
karama, huduma na kazi kwa njia ya imani kupitia Yesu
Kristo, ambavyo hivyo navyo tulivyopewa haviwezi
kujidhihirisha kikamilifu bila msaada wake mwenyewe, ndio
maana Yesu Kristo aliwaambia wanafunzi wake;
“Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu
nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi
ninyi hamwezi kufanya neno lo lote” [Yoh 15:5]
Ili tuweze kuwa dhahiri katika macho ya damu na nyama
tunahitaji sana msaada wa Mungu. Ili tuweze kufanikisha
UHURU WA KWELI 159
tunachokihitaji, na kila tulichoitiwa kukifanya, kwa sababu
bila Yesu Kristo hatuwezi kufanya jambo lolote. Katika
ulimwengu wa roho kwa imani kupitia Yesu Kristo kila
tunachotakiwa kuwa nacho kila mmoja kwa nafasi yake na
kusudi ansapewa. Kiwango cha kujifunua kwa hicho
ulichopewa kuwa sehemu yako, kutategemeana na
kiwango cha kumtegemea yeye na kuishi katika yeye (Yesu
Kristo). Neema na kweli zilikuja kupitia Kristo (Yoh 1:17) ili
kusudi zitufundishe kuishi katika yeye, ili kutuwezesha
kuishi kwa haki, kiasi, na utakatifu kupitia neema yake (Tit
2:11-12).
Ni kusudi la Mungu sasa kukuona umekuwa kufikia utimilifu
wa Kristo na kuwa dhahiri katika macho ya damu na nyama
kama alivyo Yesu Kristo. Imeandikwa katika Waefeso 4:13-
16
13: hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na
kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu
mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu
wa Kristo
Kiu ya Mungu kama alivyotuchagua tangu asili ili tuwe kama
Mwana wake wa pekee yaani Yesu Kristo (Rum 8:29-30).
Mungu anataka ili tuweze kuwa watu wakamilifu nilazima
tuwe na maarifa kupitia mwana wake wa pekee Yesu Kristo,
UHURU WA KWELI 160
ili tuwe na kimo, cheo au kiwango sawa cha utimilifu kama
Yesu Kristo alivyo.
14: ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na
huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya
watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.
Kumbe kinyume na kuwa na ufahamu wa kumjua Mwana
wa Mungu yaani Yesu Kristo ni kuwa kama mtoto mchanga
na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, hila, ujanja na
udanganyifu, suluhisho la hili ni kumjua sana mwana wa
Mungu.
15: Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata
tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo.
Tukiishika kweli yaani neno la Mungu na upendo wake na
kumfikia Yesu Kristo katika yote. Maana yake maisha yetu,
ufahamu wetu, baraka zetu, huduma, vipawa na kazi zetu
ziendane na jinsi Yesu Krsto alivyo.
16: Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na
kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya
UHURU WA KWELI 161
utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate
kujijenga wenyewe katika upendo.
Kupitia karama, huduma, zawadi na kazi tulizopewa kila
mmoja kwa kusudi lake, tukiunganishwa na msaada wa kila
mmoja kwa nafasi yake. Mungu anataka tuwe hivyo ili
kuukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo wa
Yesu Kristo. Kumbe basi ni muhimu kumjua Kristo ili tusiwe
kama watoto wachanga, bali tukue tufikie kimo kama Yesu
Kristo alivyo. Ili tuweze kuukuza mwili wa Kristo katika
upendo kila mmoja akisimama kwa nafasi yake katika
kusudi alilopewa.
Hakuna jambo tutalifanya sisi wenyewe likawa ni bora
mbele za Mungu bila neema yake
Tuangalie kisa cha mfalme Sauli;
Wakati huo Samweli akamwambia Sauli, Bwana alinipeleka
nikutie mafuta, uwe mfalme wa watu wake Israeli; basi
sasa, isikilize sauti na maneno ya Bwana. Bwana wa
majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu mambo
hayo Amaleki waliyowatenda Israeli, jinsi walivyowapinga
njiani, hapo walipopanda kutoka Misri. Basi sasa enda
ukawapige Amaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo
navyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na
UHURU WA KWELI 162
mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng'ombe na kondoo,
ngamia na punda.
Ndipo Sauli akawaita watu, akawahesabu huko Telemu,
askari waliopanda farasi mia mbili elfu, na watu wa Yuda
kumi elfu. Sauli akaufikilia mji wa Amaleki, akauvizia
bondeni. Sauli akawaambia Wakeni, Haya! Enendeni zenu,
mkashuke ili kujitenga na Waamaleki, nisije
nikawaangamiza ninyi pamoja nao; maana mliwatendea
wana wa Israeli mema, walipopanda kutoka Misri. Basi hao
Wakeni wakaondoka, wakajitenga na Waamaleki. Sauli
akawapiga Waamaleki, toka Havila uendapo Shuri,
unaokabili Misri.
Akamkamata Agagi, mfalme wa Waamaleki, yu hai,
akawaangamiza hao watu wote kwa upanga. Lakini Sauli
na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo
walio wazuri, na ng'ombe, na vinono, na wana-kondoo, na
cho chote kilicho chema, wala hawakukubali
kuwaangamiza; bali cho chote kilichokuwa kibaya na
kibovu, ndicho walichokiangamiza kabisa. Ndipo neno la
Bwana likamjia Samweli, kusema, Najuta kwa sababu
nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma,
asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru. Samweli
akasikitika, akamlilia Bwana usiku kucha.
Samweli akaondoka asubuhi na mapema ili aonane na
Sauli; Samweli akaambiwa ya kwamba, Sauli alifika
UHURU WA KWELI 163
Karmeli, na tazama, akajisimamishia ukumbusho,
akageuka, akapita, akatelemkia Gilgali. Samweli
akamwendea Sauli; naye Sauli akamwambia, Ubarikiwe na
Bwana, nimeitimiza amri ya Bwana. Samweli akasema,
Maana yake nini, basi, hiki kilio cha kondoo masikioni
mwangu, na huu mlio wa ng'ombe ninaousikia? Sauli
akasema, Wamewaleta kutoka kwa Waamaleki; maana
watu waliwaacha hai kondoo na ng'ombe walio wazuri, ili
wawatoe dhabihu kwa Bwana, Mungu wako, nao
waliosalia tumewaangamiza kabisa.
Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Ngoja, nami
nitakuambia neno aliloniambia Bwana usiku huu. Naye
akamwambia, Haya, sema. Basi Samweli akasema, Ingawa
ulikuwa mdogo machoni pako mwenyewe, je! Hukufanywa
kuwa kichwa cha kabila za Israeli? Naye Bwana akakutia
mafuta uwe mfalme wa Israeli. Kisha Bwana akakutuma
safarini, akasema, Enenda ukawaangamize kabisa wale
Waamaleki wenye dhambi, upigane nao hata
watakapoangamia. Mbona, basi, hukuitii sauti ya Bwana,
bali ukazirukia nyara ukafanya yaliyo maovu machoni pa
Bwana?
Sauli akamwambia Samweli, Hakika mimi nimeitii sauti ya
Bwana, nami nimemleta Agagi, mfalme wa Waamaleki,
tena nimewaangamiza Waamaleki kabisa. Ila watu
waliteka nyara, kondoo na ng'ombe walio wazuri, katika
UHURU WA KWELI 164
vitu vilivyowekwa wakfu, kusudi wavitoe dhabihu kwa
Bwana, Mungu wako, huko Gilgali. Naye Samweli akasema,
je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu
Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora
kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu. Kwani
kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri
na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye
naye amekukataa wewe usiwe mfalme.
Ndipo Sauli akamwambia Samweli, Nimefanya dhambi;
maana nimeihalifu amri ya Bwana, pia na maneno yako;
kwa sababu naliwaogopa wale watu, nikaitii sauti yao. Basi
sasa, nakuomba, unisamehe dhambi yangu; rudi pamoja
nami, nipate kumwabudu Bwana. Samweli akasema,
Sitarudi pamoja nawe; kwa sababu umelikataa neno la
Bwana, Bwana naye amekukataa wewe, usiwe mfalme wa
Israeli. Naye Samweli alipogeuka, aende zake, Sauli
akaushika upindo wa vazi lake, nalo likararuka. Basi
Samweli akamwambia, Leo Bwana amekurarulia ufalme wa
Israeli, naye amempa jirani yako, aliye mwema kuliko
wewe. Tena Yeye aliye Nguvu za Israeli hatanena uongo,
wala hataona majuto; maana siye mwanadamu, hata
ajute. Akasema, Nimekosa; lakini uniheshimu sasa,
nakuomba, mbele ya wazee wa watu wangu, na mbele ya
Israeli, rudi pamoja nami, nimwabudu Bwana, Mungu
wako. Basi Samweli akarudi na kuandamana na Sauli; naye
Sauli akamwabudu Bwana. [1Samw 15:1-31]
UHURU WA KWELI 165
Sauli alipewa maagizo na Bwana aende kuwapiga
Waameleki na kuviharibu vitu vyote na kuangamiza kila
mwanaume na mwanamke,mtoto, ng’ombe, na kondoo na
ngamia na punda. Sauli akakiuka agizo la Bwana akawaua
Waameleki lakini akamwacha hai mfalme Agagi wa
Waameleki, kondoo walio wazuri, ng’ombe vinono, na
kondoo na kila kilichokuwa chema. Lengo la Sauli lilikuwa ni
kumtolea Bwana dhabihu (sadaka), akafikiri Mungu
anapenda sana sadaka. Mungu akasema ninajuta kwakuwa
nimemtawaza Sauli kuwa Mfalme juu Israeli, Mungu
akamkataa Sauli asiwe Mfalme juu ya Israeli. Samweli
akamwambia Sauli kutii ni bora kuliko dhabihu (sadaka) na
kusikia kuliko mafuta ya beberu.
Tujiulize swali la Msingi, kwani Sauli alifanya kosa gani
mpaka Mungu aseme najuta nimemtawaza kuwa mfalme
juu ya Israeli?
Sauli alifikiri kwa kufanya mambo ambayo anafikiri Mungu
yanampendeza sana yaani kutoa dhabihu (sadaka) bila
kuishi vile Mungu anavyompa maelekezo ataonekana kuwa
bora mbele za Mungu. Kumbe mbele za Mungu aliona
amefanya kosa kubwa, yaani amefanya dhambi wakati
kiuhalisia Mungu anajifunua sana ukimtolea sadaka lakini
kwa sababu Sauli alienda kinyume na maelekezo ilikuwa
dambi kwake.
UHURU WA KWELI 166
Watu wengi wanapenda kuishi kwa miongozo ya kwao,
wanaigilizia kwa watu wengine walifanikiwaje baada ya
hapo wanaanza kuishi kwenye maisha ya watu wengine.
Wakati wote wanaishi maisha ya kufeli kwa sababu
hawataki kumuishia Mungu (Yesu Kristo). Sisi tulio katika
agano jipya tumepewa agizo la kuwa na maarifa ya ki-
Mungu, ili tumfananie Yesu Kristo ili tuishi kwa utimilifu
kama Yesu Kristo (2Kor 5:15). Nje ya kumuishia Kristo ni
kuishi maisha ya majuto, dhambi, kufeli, msongo wa
mawazo na kuchanganyikiwa. Kinyume cha kumuishia
Kristo hakuna jambo jema utafanya mbele za Mungu
litakuwa bora, mpaka umejizatiti kuishi sawa sawa kuishi
katika Kristo.
Lolote tutakalolifanya kwa juhudi zetu, hata kama
limefikia kiwango cha mwisho cha juhudi zetu bado
litaonekana liko chini ya kiwango mbele za Mungu.
“Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja
Farisayo, wa pili mtoza ushuru. Yule Farisayo akasimama
akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa
kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang'anyi,
wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi
nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato
yangu yote. Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala
hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali
UHURU WA KWELI 167
alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi
mwenye dhambi. Nawaambia, huyu alishuka kwenda
nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa
maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye
atakwezwa” [Luk 18:10-14]
Kibinadamu Farisayo alikuwa na haki ya kuhesabiwa haki
kuliko Mtoza ushuru, lakini kosa la Farisayo lilikuwa ni
kutumaninia juhudi zake na uwezo wake kuhesabiwa haki.
Kama ilivyokuwa kanuni Mafarisayo walimkataa Yesu
walifikiri kwa juhudi zao ndio wanahesabiwa haki pasipo
kuishi katika Kristo. Ni vyema kufanya kila jambo kwa juhudi
lakini tusitumainie juhudi zetu bali tuishi katika Kristo na
kuamini ukamilifu wa kazi yake aliyoifanya kwaajili yetu.
Kufanya jambo lolote sisi wenyewe bila kupitia kwa Yesu
Kristo ni sawa na kusema sihitaji msaada wako Mungu.
Mungu alimtoa Mwana wake wa pekee, ili awe mbadala
wetu, Mungu kwa mapenzi yake mwenyewe aliamua
kumtoa Kristo. Ili aje kutusaidia na Kristo kusimama kwenye
nafasi yetu na sisi tukae kwenye nafasi yetu. Yesu Kristo
hakuwa na hatia lakini alifanyika mwenye hatia kwaajili
yetu, Yesu Kristo alikuwa mtakatifu lakini alifanyika
mwenye dhambi kwaajili yetu. Yesu Kristo alikuwa mwenye
UHURU WA KWELI 168
haki lakini alifanyika asiye na haki ili sisi tuwe wenye haki
katika yeye. Imeandikwa;
“Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani
mwake. Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano;
alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye
ahukumuye kwa haki. Yeye mwenyewe alizichukua dhambi
zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo
ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa
kwake mliponywa. Kwa maana mlikuwa mnapotea kama
kondoo; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mwangalizi
wa roho zenu” [1Petr 2:22-25]
Kama Kristo alikufa kwaajili yako akafanyika mwenye
dhambi ili uwe mtakatifu, na mwenye haki. Kutafuta
utakatifu wako binafsi na haki yako ni kumfedhehi Mwana
wa Adamu na kuikanyaga damu yake, ni sawa na kusema
Yesu Kristo alikufa bure, hakuna alilonisaidia, au
hakunisaidia kikamilifu. Ndio maana unataka kujitahidi
wewe mwenyewe binafsi, ni sawa na kumwambia Mungu
sihitaji msaada wako. Ukiamua kuishi kwa juhudi zako yeye
atakuacha ujiishie mwenyewe na mwisho wake utakuwa ni
mtu wa kushindwa na kufeli. Kubali kuanza kuishi katika
Kristo ili uwe mtoshelevu na mkamilifu mbele za Mungu.
UHURU WA KWELI 169
Tathmini kupitia maswali kutoka katika Sura ya Tano
1: Kutoka katika sura hii namna gani ya kuambatana na
neno la Mungu ili uweze kupata matokeo?
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………
2: Taja sababu saba kwanini tuishi katika Yesu Kristo?
(i)………………………………………………………………………………………
…………………………………………
(ii)………………………………………………………………………………………
……………………………………….
(iii)……………………………………………………………………………………
………………………………………….
(iv)……………………………………………………………………………………
………………………………………….
(v)………………………………………………………………………………………
……………………………………....
(vi)……………………………………………………………………………………
………………………………………….
UHURU WA KWELI 170
(vii)……………………………………………………………………………………
…………………………………………
3: Tofautisha kati ya kuishi kwa sheria na kuishi kwa neema
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………
4: Kutokana na ulivyojifunza katika sura hii, taja ngazi tatu
za sheria
(i)………………………………………………………………………………………
…………………………………………
(ii)………………………………………………………………………………………
……………………………………….
(iii)……………………………………………………………………………………
………………………………………….
5: Taja sheria iliyokamilifu (Mungu anayoiangalia)
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
UHURU WA KWELI 171
SURA YA SITA
YESU KRISTO ALIMALIZA YOTE MSALABANI
“Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema,
imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake” [Yoh
19:30]
Biblia inaposema roho yake biblia ya kigiriki imetumia
maneno “ekpneo” na ekpsucho”. Maana yake kutoa pumzi
nje. Baada ya Yesu kutoa pumzi nje alipumzika.Yesu
alipopumzika ndiko tunapotakiwa kuanzia. Maandiko
yanasema;
“Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu
yake, na kutufanya kuwa ufalme, makuhani kwa Mungu
naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una yeye hata milele na
milele.Amina” [Ufu 1:5]
Katika mstari huu tafsiri ya biblia ya kiingereza KJV
inaonyesha kuwa tulioshwa kwa damu yake kupitia damu
yake tulifanywa kuwa wafalme na makuhani. Yesu
alikamilisha kila alichotakiwa kukifanya kupitia msalaba
wake. Msalaba wa Kristo ni hatima ya mambo yote
yaliyokuwa yakitutesa. Ndio maana Paulo ameandika;
UHURU WA KWELI 172
“Maana Kristo hakunituma ili nibatize, bali niihubiri Habari
Njema; wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo
usije ukabatilika. Kwa sababu neno la msalaba kwao
wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu
ya Mungu” [1Kor 1:17-18]
Msalaba ilikuwa ni hatima ya Yesu Kristo kuja katika
ulimwengu huu, ndio maana pasipo Kristo sisi ni bure,
pasipo msalaba hakuna chochote ambacho kimebadilika.
Pasipo Kristo ni kuibatili neema ya Kristo ndio maana kuishi
nje ya neema ni kuibatili neema ya Kristo. Ndio maana
Paulo aliandika kuwa msalaba kwao wanaopotea ni upuzi
bali sisi tunaokolewa ni nguvu ya Mungu.
Ndio maana Paulo aliwaandikia Wagalatia;
“Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu cho chote ila
msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo
ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa
ulimwengu” [Gal 6:14]
Paulo anasema haonei fahari juu ya kitu chochote ila
msalaba wa Bwana Yesu Kristo. Msalaba wa Kristo
unaonyesha upatanisho kati ya Mungu na wanadamu na
upatanisho wa wanadamu kwa wanadamu. Msalaba wa
Kristo ni kiwakilishi cha upendo wa Mungu katika maisha
yetu; ndio maana imeandikwa;
UHURU WA KWELI 173
“Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani,
vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; ili kila
mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye. Kwa
maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa
Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali
awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma
Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali
ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye
hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa
sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu” [Yoh
3:14-18]
Yesu Kristo kutolewa msalabani, ilikuwa ni kiwakilishi cha
upendo wa Mungu kwenye maisha yetu. Mungu
alimuhukumu Yesu msalabani kwa aniaba yetu, tulistahili
adhabu sisi, tulistahili kuteswa sisi, tulistahili kufa sisi.
Mungu alimtoa sadaka Mwana wake wa pekee Yesu Kristo
ili sisi tuwe huru, katka maisha (dhambi, magonjwa,
vifungo) (Rum 5:17). Hukumu ya Mungu iliishia msalabani
hakuna namna aliyemwamini Yesu Kristo atahukumiwa bali
ambaye hajamini hukumu yake imekwisha tolewa.
Imeandikwa;
“Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu
hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema” [Rum 6:14]
Dhambi haina nguvu tena ya kututawala kwa sababu Yesu
Kristo aliikomesha na kuishinda pale msalabani. Mauti na
UHURU WA KWELI 174
kuzimu nguvu yake imeshindwa kwa sababu ya Yesu Kristo.
Tulitakiwa kuhukumiwa adhabu kali sana lakini Yesu
alihukumiwa na alipewa hiyo adhabu kusudi kila
anayemwamini Yeye asihukumiwe. Ndio maana Paulo
aliwaandikia Warumi;
“Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika
Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio
katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya
dhambi na mauti. Maana yale yasiyowezekana kwa sheria,
kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu,
kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa
mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi,
aliihukumu dhambi katika mwili; Kwa maana wale
waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale
waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. Kwa kuwa nia ya
mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. [Rum
8:1-6]
Kila aliyeko ndani ya Yesu Kristo hawezi kuhukumiwa, kwa
sababu Mungu alimtuma mwanawe mwenye mfano wa
mwili wa dhambi. Ili aihukumu dhambi katika mwili yake,
ndio maana kila anayemwamini yeye ahukumiwi kwa
sababu Mungu alimhukumu Yesu Kristo kwa aniaba yetu.
Ndio maana msalaba wa Kristo kwao wanaopotea ni upuzi
bali msalaba ni nguvu ya Mungu kwetu sisi. Kwa njia ya
yeye (Yesu Kristo) kupitia damu yake na jina lake
UHURU WA KWELI 175
tulitakaswa na kuondolewa dhambi zetu; Ndio maana Yesu
aliwaambia Wanafunzi wake;
“Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na
maandiko. Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba
Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba
mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na
ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. [Luk 24:46-
47]
Yesu aliwaambia Wanafunzi wake kwa jina lake watu
watahubiriwa toba ya ondoleo la dhambi. Petro naye
alitekeleza ujumbe huo alioambiwa na Bwana Yesu wa
kuhubiri toba ya ondoleo la dhambi kwa imani ya jina la
Yesu.
“Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa
jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi
mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu” [Mat 2:38]
Luka pia alihubiri ya kuwa hata manabii wanashuhudia ya
kuwa kwa jina la Yesu kila anayemwamini hupata ondoleo
la dhambi.
“Akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudia ya kuwa huyu
ndiye aliyeamriwa na Mungu awe Mhukumu wa walio hai
na wafu. Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba
kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi”
[Mat 10:42-43]
UHURU WA KWELI 176
Ndio maana Yesu Kristo kupitia mwili wake msalabani
aliuondoa uadui kati yetu na Mungu ili atufanye kuwa watu
wapya ndani ya nafsi yake na kutufanyia amani.
Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo
sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili
kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya
amani. [Gal 2:16]
Kupitia nafsi ya Yesu Kristo kupitia damu ya msalaba wake
alivipatanisha vitu vyote. Vitu vyote vilivyo juu ya nchi na
vilivyo mbinguni. Kwa sababu hiyo mimi na wewe tumepata
upatanisho.
Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae; na
kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha
kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye,
ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni. [Kol
1:19-20]
Yesu Kristo alinyenyekea mpaka mauti ya msalaba,
kwasababu kupitia msalaba ilikuwa ni ukamilifu wa kazi
iliyomleta duniani. Alihakikisha anafikia msalabani ili
kuhitimisha kiliochomleta duniani kwaajili ya ukombozi.
UHURU WA KWELI 177
“tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu,
alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya
msalaba” [Filip 2:8]
Ndio maana hakuna hati ya mashitaka tena, hukumu wala
uadui akaondoa vyote visiwepo tena, akavigogomelea
msalabani. Ndio maana alivua enzi yake na mamlaka
akashuka kuja kwetu KJV anasema akaviweka wazi na
kuvishangilia kupitia huo msalaba;
akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa
hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo
tena, akaigongomea msalabani; akiisha kuzivua enzi na
mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri,
akizishangilia katika msalaba huo. [Kol 2:14-15]
Kristo aliidharau aibu yake, ndio maana aliustahimili
msalaba kusudi aikamilishe kazi yake na kumaliza kazi yote
iliyomleta. Paulo anaendelea kusema; Tumezungukwa na
wingu kubwa la mashahidi namna hii tupige mbio na
kuweka kando kila mzigo mzito tukimtazama Yesu Kristo.
“Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa
la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito,
na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa
saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,
tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza
imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele
UHURU WA KWELI 178
yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi
mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu” [Ebr 12:1-2]
Na kwasababu hiyo ndio maana Petro aliandika;
“Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili
awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa
zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa
mambo yenu” [1Pet 5:6-7]
Mtwike Yesu Kristo fadhaa zako, uwe unachangamoto ya
kiuchumi, kudharauliwa kukataliwa, msongo wa mawazo.
Mtwike Yesu Kristo msalabani baada ya hapo kuwa huru.
Ikiwezekana andika shida yako kwenye diary mkabidhi Yesu
aishughulikie hiyo shida yako. Shetani akikukumbusha
kuwa mbona Mungu wako anachelewa kukujibu? Wewe
muonyeshe mahali ulipoandika. Mwambie Mungu
anashughulikia, mwambie Mungu analifanyia kazi.
Mwambie kwa sababu Yesu alimaliza yote msalabani
kwaajili yangu majibu yangu yapo karibu sana, na asubuhi
yangu ipo mlangoni. Usikubali Shetani akukandamize
ufahamu wangu, usikubali Shetani ukukumbushe jinsi
ulivyofeli. Mwambie Yesu wangu alishafaulu na alifanikiwa
pale msalabani kwaajili yangu kwahiyo sitafeli tena.
UHURU WA KWELI 179
Mshinde Shetani kwa neno la ushuhuda na damu ya
Mwanakondoo (Yesu Kristo) Msalabani.
Ndio maana imeandikwa;
“Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa
wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka
ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa
ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu,
mchana na usiku. Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-
Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao” [Ufu 12:10-11a]
Kazi ya Shetani usiku na mchana ni kukushitaki,
kukuhukumu, kukulaghai, kukuonyesha kushindwa na
kufeli. Hakuna namna tunaweza kumshinda Shetani zaidi
kushuhudia neno na damu ya Mwanakondoo. Yesu Kristo
aliyekufa kwaajili yetu akachukua udhaifu wetu na
masikitiko yetu. Kumbe Shetani kumshinda ni rahisi sana
tumia mambo mawili kumshinda; neno la ushuhuda na
damu ya Yesu Kristo. Ndio maana Yesu alimshinda Shetani
kwa neno la ushuhuda; imeandikwa;
“Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka
Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini
nyikani, akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu;
hata zilipotimia, aliona njaa. Ibilisi akamwambia, Ukiwa
ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate. Yesu
akamjibu, Imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate
UHURU WA KWELI 180
tu. Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za
ulimwengu kwa dakika moja. Ibilisi akamwambia, Nitakupa
wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi
mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. Basi,
wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako.
Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana
Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. Akamwongoza
mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya kinara cha hekalu,
akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe
chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake
wakulinde; na ya kwamba,mikononi mwao watakuchukua,
Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. Yesu akajibu
akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.
Basi alipomaliza kila jaribu, Ibilisi akamwacha akaenda zake
kwa muda” [Luk 4:1-13]
Shetani hawezi kukwambia wewe unanguvu kiasi gani
katika Kristo, wala hawezi kukwambia wewe ni nani katika
Yesu Kristo. Mshinde kwa neno la ushuhuda wa Yesu Kristo,
akikwambia na wewe unamaisha yamechoka umechakaa.
Mwambie imeandikwa katika Yesu Kristo nimebarikiwa kwa
baraka zote katika ulimwengu wa roho (Efe 1:3). Kwahiyo
subiri udhihiridsho wa baraka zangu ziko njiani, akikwambia
unajiita mtakatifu wewe! Umesahau ulivyozini! umesahau
ulivyoiba! umesahau ulivyodanganya! Umesahau ulivyo
laghai! Mwambie imeandikwa mimi ni Mtakatifu (Rum
UHURU WA KWELI 181
8:29-30, Efe 1:3-6), sina mawaa wala hatia katika Kristo
Yesu Kristo alilipia gharama ya haya yote unayonishitaki
miaka elfu mbili iliyopita, na kwasababu hiyo kwa neema
yake sitarudia tena, kwa sababu Yesu Kristo hata sasa
anaishi ndani yangu.
Damu ya Mwanakondoo (Yesu Kristo).
Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi
juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na
nyuma, kimetiwa muhuri saba. Nikaona malaika mwenye
nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N'nani astahiliye kukifungua
kitabu, na kuzivunja muhuri zake? Wala hapakuwa na mtu
mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza
kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. Nami nikalia
sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua
hicho kitabu, wala kukitazama. Na mmojawapo wa wale
wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya
Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile
kitabu, na zile muhuri zake saba.
Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai
wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo
amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye
pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za
Mungu zilizotumwa katika dunia yote. Akaja, akakitwaa kile
UHURU WA KWELI 182
kitabu katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya
kile kiti cha enzi. Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye
uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka
mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na
vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni
maombi ya watakatifu.
Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe
kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa
kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako
watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu;
nao wanamiliki juu ya nchi. Nikaona nikasikia sauti ya
malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale
wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu
kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu, wakisema kwa sauti
kuu, Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa, kuupokea
uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu
na baraka.
Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya
nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake,
nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na
uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-
Kondoo, hata milele na milele. Na wale wenye uhai wanne
wakasema, Amina. Na wale wazee wakaanguka,
wakasujudu. [Ufu 5:1-14]
UHURU WA KWELI 183
Mwanakondoo (Yesu Kristo) mzee wa siku yeye aliyeshinda
alikubali kufungua kile kitabu na muhuri zake. Alipokitwaa
kile kitabu wenye uhai wane na wale wazee ishirini na nne
walianguka wakasujudu mbele zake. Wakisema unastahili
kukichukua kile kitabu na kuzifungua mihuri zake, sauti za
malaika wengi zilisikika. Kwa hesabu yao ni ilikuwa elfu
kumi mara elfu kumi mara elfu wakisema unastahili
Mwanakondoo kwa damu yako. Uliwanunua watu wa kila
kabila, lugha na jamaa na taifa, na kupitia damu yako (yaani
wale waliomwamini) uliwafanya kuwa wafalme, makuhani,
wakamtukuza milele yote mwanakondoo (Yesu Kristo).
Ndio maana kupitia damu yake tuliokolewa. Ndio maana
Paulo aliandika;
“Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo
mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu
zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya
ulimwengu huu, wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali
kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika
Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. Kwa
maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya
ndama ya ng'ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu
hutakasa hata kuusafisha mwili; basi si zaidi damu yake
Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi
yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa,
UHURU WA KWELI 184
itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate
kumwabudu Mungu aliye hai?” [Ebr 9:11-14]
Yesu alijitoa nafsi yake na kupitia damu yake tulitakaswa na
kuwa watu tusio na uchafu wala mawaa.
Yohana aliandikia makanisa saba kuwa tulioshwa kwa
damu ya Yesu;
“Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na
iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na
aliyekuwako na atakayekuja; na zitokazo kwa roho saba
walioko mbele ya kiti chake cha enzi; tena zitokazo kwa
Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza
wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye
atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake”
[Ufu 1:4-5]
Yesu aliyemzaliwa wa kwanza na mkuu wa wafalme wa
dunia alitupenda na kutuosha dhambi zetu, ndio maana
tunatakiwa kwenda nuruni kwasababu damu ya Yesu
ilitusafisha dhambi zetu;
“bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru,
twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana
wake, yatusafisha dhambi yote” [1Yoh 1:7]
UHURU WA KWELI 185
Petro aliandika tulikombolewa si kwa vitu viharibikavyo,
fedha wala dhahabu. Bali kwa damu ya thamani ya
Mwanakondoo (Yesu Kristo) asiye na hila wala mawaa.
“Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu
viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika
mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; bali
kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na
ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo” [1Pet 1:18-19
Kupitia damu ya Yesu tulipata neema ya kupaingia
patakatifu kwa ujasiri bila hofu na uwoga. Yesu alibadili
historia pale msalabani na kupitia Yeye tukafanyika wana
ndio maana tunapoenda kwa Mungu tunaenda kwa Baba
yetu kuongea naye,
“Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia
patakatifu kwa damu ya Yesu” [Ebr 10:19]
Yesu aliingia patakatifu kupitia damu yake mara moja na
kuupata ukombozi wa milele;
“wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake
mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha
kupata ukombozi wa milele” [Ebr 9:12]
Ukombozi huu ni ukombozi usiohusisha mchango wowote
kutoka kwako. Ulijitosheleza na hivyo wewe ni nafasi yako
UHURU WA KWELI 187
Tathmini kupitia maswali kutoka katika Sura ya Sita
1: Taja maana ya haya maneno ya kigiriki “ekpneo na
ekpsucho”
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
2: Taja mfumo wa maisha unaopelekea kuto tawaliwa na
dhambi
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
3: Namna gani ya kushinda hila/uongo wa Shetani. Taja
mambo mawili
(i)………………………………………………………………………………………
…………………………………………
(ii)………………………………………………………………………………………
……………………………………….
UHURU WA KWELI 189
SURA YA SABA
MIMI SI MFUNGWA TENA
Maandiko yanasema;
“Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana
amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema;
amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo,
kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa
habari za kufunguliwa kwao” [Isa 61:1]
Isaya alitabiri ujio wa Yesu Kristo mpakwa mafuta (Masihi
wa Bwana) kuwa atakuja kuwahubiri; wanyenyekevu habari
njema, kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia
mateka uhuru wao na waliofungwa habari za kufunguliwa
kwao. Maneno haya aliyotabiri Isaya yalitimia Yesu
alipokuja duniani. Yesu alipokwenda Nazareti alipewa
kitabu cha nabii Isaya kukisoma. Imeandikwa;
“Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia
mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma
kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu
kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Na
kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. Akakifunga
chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote
waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho.
UHURU WA KWELI 190
Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia
masikioni mwenu” [Luk 4:18-21]
Yesu alithibitisha kuwa alikuja kuwatangazia wafungwa
kufunguliwa kwao, vipofu kuona tena na kuwaacha huru
waliofungwa. Na kuwaambia wote kuwa maneno haya
yametimia masikioni mwenu. Yesu ilikuwa ni desturi yake
kila mahali alipopita aliwafungua watu waliokuwa
wamekamatwa na kuteswa na ibilisi. Imeandikwa;
“habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta
kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na
huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na
Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye. Nasi tu
mashahidi wa mambo yote aliyoyatenda katika nchi ya
Wayahudi na katika Yerusalemu; ambaye walimwua
wakamtundika mtini. Huyo Mungu alimfufua siku ya tatu,
akamjalia kudhihirika, si kwa watu wote, bali kwa
mashahidi waliokuwa wamekwisha kuchaguliwa na
Mungu, ndio sisi, tuliokula na kunywa pamoja naye baada
ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu. Akatuagiza
tuwahubiri watu na kushuhudia ya kuwa huyu ndiye
aliyeamriwa na Mungu awe Mhukumu wa walio hai na
wafu. Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa
jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi
[Mate 10:38-43]
UHURU WA KWELI 191
Katika uweza wa nguvu za Roho Mtakatifu Yesu Kristo
alikuwa akitenda kazi na kuwaponya wote walioonewa na
Ibilisi, Mungu alikuwa akitenda kazi pamoja naye. Luka
anathibitisha kuwa walitumwa kuwa mashahidi wa mambo
yote aliyoyatenda katika Wayahudi na Yerusalemu kwamba
aliuawa na kutundikwa mtini (msalabani), na kushuhudia ya
kwamba kwa jina lake Yesu kila aaminiye apate ondoleo la
dhambi. Dhambi haziondolewi kwa kulia kwa machozi
dhambi zinaondolewa kwa kuamini jina la Yesu na
kumwamini mwana wa Mungu. Imeandikwa;
“Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa
jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi
mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu” [Mate 2:38]
Petro aliwaambia tubuni mkabatizwe kwa jina lake Yesu
Kristo Mpate ondoleo la dhambi na kupokea kipawa cha
Roho Mtakatifu. Maana yake kwa kuliamini jina la Yesu
watu wanapata ondoleo la dhambi. Luka pia aliandika kuwa
kwa kuamini jina la Yesu tunapata ondoleo la dhambi;
“Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo
atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote
watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la
dhambi, kuanza tangu Yerusalemu” [Luk 24:45-46]
UHURU WA KWELI 192
Luka aliandika kuwa iliandikwa kuwa Kristo atateswa na
kufufuka siku ya tatu na mataifa yote watahubiriwa kwa jina
lake toba ya ondoleo la dhambi.
Toba sio kulia kwa machozi juu ya makosa uliyofanya;
toba ni kubadili mtazamo na kugeuka.
Neno toba katika biblia ya kigiriki limetumika neno
“metanoia” maana yake badili mtazamo katika lugha mama
ya kiebrania limetumika neno “teshuvah” maana yake
geuka. Kulia kwa machozi ukiwa umefanya kosa sio toba
toba ni kubadili mtazamo na kugeuka. Unaweza ukalia lakini
bado ukawa hujabadili mtazamo na haujageuka. Ndio
maana kuna idadi ya watu wengi ambao wanaenda mbele
za Mungu wanalia na kuomba msamaha juu ya makosa yao
lakini baada ya mda wanarudia makosa yale yale. Tafsiri
nyepesi ni kwamba hawakutubu, toba halisi inahusisha
kugeuzwa nia ya ndani kwa kubadili mtazamo na matokeo
yake yatakuwa ni kugeuka. Ndio maana imeandikwa;
“Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa
kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya
Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu” [Rum
12:2]
Nia ya ndani ikibadilishwa inapelekea kujua mapenzi ya
Mungu na ukamilifu. Nia ya ndani inageuzwa kwa kulisikia
UHURU WA KWELI 193
neno la Kristo na ufunuo kutoka kwake. Neno la Kristo
likikaa ndani linapelekea kujua mapenzi ya Mungu na
ukamilifu. Paulo anaandika kuwa;
“Bali ninyi, sivyo mlivyojifunza Kristo; ikiwa mlimsikia
mkafundishwa katika yeye, kama kweli ilivyo katika Yesu,
mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani,
unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; na
mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya,
ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu
wa kweli” [Efe 4:20-24]
Ukijifunza katika Yesu Kristo nilazima uuvue utu wa zamani
na tama zake yaani uongo, wizi, uzinzi, kuabudu miungu
mingine, husuda, fitina na mwenendo mzima wa utu wa
zamani. Vyote hivi vinaondolewa kwa kujifunza katika Yesu
Kristo kweli yake na ufunuo wa Yesu Kristo ndio maana
imeandikwa;
“Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi;
mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika
ufunuo wake Yesu Kristo” [1 Pet 1:13]
Kupitia ufunuo wa Yesu Kristo neema inafunuliwa
inayopelekea kugeuzwa nia na kufikia kiasi (uwezo wa
kujizuia) na utimilifu. Utimilifu unapatikana kwa kujifunza,
kukaa darasani na kulisikia neno la Kristo (Efe 4:13).
UHURU WA KWELI 194
Yesu Kristo alituweka huru na kila aina ya vizuizi na
vifungo.
Maandiko yanasema;
“Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo
kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. Kwa
maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote
tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha
kati kilichotutenga” [Efe 2:14]
Tafsiri ya Biblia ya NENO (NEN) inasema hivi;
“Lakini sasa katika Kristo Yesu, ninyi ambao hapo kwanza
mlukuwa mbali na Mungu, sasa mmeletwa karibu kwa njia
ya damu ya Kristo. Kwa maana yeye mwenyewe ndiye
amani yetu, aliyetufanya sisi tuliokuwa wawili, yaani,
Wayahudi na watu wa Mataifa, tuwe wamoja kwa kuvunja
kizuizi na kubomoa ule ukuta wa uadui uliokuwa kati yetu”
Yesu Kristo kupitia damu yake alitufanya kuwa wamoja na
kuvunja vizuizi vyote vilivyokuwa vimetutenga kati yetu.
Yesu Kristo kwa njia ya msalaba alituacha huru na kubomoa
kila vizuizi na vifungo vilivyokuwa vimetutenga kati yetu sisi
wanadamu na Mungu. Imeandikwa;
UHURU WA KWELI 195
“Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa
roho yake. Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande
viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba
ikapasuka” [Math 27:50-51]
Pazia la hekalu lilipasuka vipande viwili kuashiria kuwa tuko
huru kupaingia patakatifu pa patakatifu. Hakuna kizuizi tena
katika Yesu Kristo kila aliye na Yesu Kristo amekuwa na
uhuru kweli kweli sasa anaweza kupaingia patakatifu. Ndio
maana Yesu Kristo baada ya kufa alienda kuzimu
kunyang’anya funguo za mamlaka na kuzimu alizokuwa
nazo Shetani;
“Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu
aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu,
akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, na
aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata
milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za
kuzimu” [Ufu 1:17-18]
Yesu anazo funguo za mauti na kuzimu na aliishinda mauti
na kuzimu kutuacha huru na gereza la dhambi na mauti.
Imeandikwa;
“Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo
Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti”
[Rum 8:2]
UHURU WA KWELI 196
Kwa njia ya Msalaba wa Yesu Kristo tuliachwa huru mbali na
sheria ya dhambi na mauti. Paulo anasema;
“Bali kwa ajili ya ndugu za uongo walioingizwa kwa siri;
ambao waliingia kwa siri ili kuupeleleza uhuru wetu tulio
nao katika Kristo Yesu, ili watutie utumwani; ambao hata
saa moja hatukujitia chini yao, ili kwamba kweli ya Injili ikae
pamoja nanyi” [Gal 2:4-5]
Paulo anaeleza kuwa wako watu ambao hawakubali kujitia
chini yao lengo lao lilikuwa ni kuwatia utumwani. Lengo lao
lilikuwa kuwaweka utumwani kwa kuipotosha kweli ya injili
ya Yesu Kristo. Ndio maana Paulo anasema tulikataa kujitia
chini yao kusudi kweli ya injili ikae pamoja naye. Maana
yake kweli ya injili ikihubiriwa watu wanawekwa huru,
yoyote anayeijua kweli ya injili hawi mtumwa. Injili ya kweli
inayomuweka mtu huru ni kupitia neno la Kristo, ndio
maana Yesu Kristo alisema;
“Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini,
Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi
wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli
itawaweka huru” [Yoh 8:31-32]
Kupitia neno la Yesu Kristo watu wanawekwa huru kweli
kweli. Yesu alikuwa anawaambia Wayahudi na walioamini
kuwa kaeni katika neno. Kwa sababu wakikaa katika neno la
Yesu Kristo waijua kweli na hiyo kweli itawaweka huru.
UHURU WA KWELI 197
Kwahiyo kupitia Kristo na neno lake tu awekwa huru ukiwa
na Kristo unakuwa huru ukikaa katika neno lake (kujifunza)
unakuwa na kutoka kuwa mototo mchanga ili uwe mtu
mzima. Kusudi ufikiri kama Kristo, unene kama Kristo na
utende kama Yesu Kristo. Ndio maana imeandikwa;
“Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli”
[Yoh 8:36]
Kupitia Yesu Kristo tunakuwa huru, huwezi ukawa ndani ya
Kristo ukawa na vifungo, magonjwa, laana, mikosi. Ukiona
umeamini halafu nafsi yako au Shetani anakwambia wewe
ni mfungwa ujue huo ni uongo. Uongo tunautambua kwa
kulijua neno la Kristo kila kilicho kinyume na neno la Kristo
ni uongo, kwahiyo usisite kuupinga huo uongo. Ndio maana
imeandikwa;
1: Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye
mkulima.
2: Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi
lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.
3: Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno
nililowaambia.
UHURU WA KWELI 198
4: Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi
lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu;
kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.
Yesu anasema Baba ni mkulima (Mungu Baba), Yesu ni
mzabibu na sisi ni matawi, Yesu anasisitiza kuwa sisi
tumekuwa safi katika lile neno alilotuambia. Neno hilo ni hili
anasema; tukae ndani yake Kristo ndiyo maana anasema
pasipo Yeye sisi hatuwezi kuzaa kwahiyo nilazima tukae
ndani yake.
5: Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu
nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi
ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
Kila anayekaa ndani ya Yesu Kristo huzaa sana pasipo Yesu
Kristo sisi hatuwezi kufanya neno lolote.
6: Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na
kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni
yakateketea.
Yesu anasema na mtu asipokaa ndani yake
(asipoamini/asipozaliwa mara ya pili/asipookoka) hutupwa
nje na kutupwa motoni yaani katika jehanamu ya moto
7: Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa
ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa [Yoh
15:1-7]
UHURU WA KWELI 199
Tukikaa ndani yake kwa maana ya kumwamini na tukilishika
neno la Yesu Kristo. Kila lolote tutakaloomba tutatendewa.
Tunajibiwa maombi kwa kumwamini Kristo na kulishika
neno la Kristo. Ukienda mbele za Mungu ili upokee majibu
ya maombi yako nilazima tuwe na neno la Yesu Kristo na
tuimwamini Yesu Kristo tukalishika neno lake tunakuwa
huru kweli kweli. Ndio maana Yesu aliwaombea wanafunzi
wake kuwa;
“Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli” [Yoh
17:17]
Kwahiyo neno la Kristo linatutakasa na kutuweka huru kwa
njia ya imani ya Yesu Kristo. Kwahiyo tukiijua kweli ya neno
la Mungu tunafanyika huru kweli kweli. Kwa sababu hakuna
jambo lolote litatusumbua kwenye maisha yetu katika kila
eneo. Ndio maana tunapaswa kulifuata neno la kweli ya
Yesu Kristo. Maandiko yako wazi kwa sababu kila kitu
tulichokuwa tunakihitaji kwaajili yetu Kristo alishamaliza.
Katika eneo la uchumi, afya, amani, furaha Yesu alimaliza na
kutupigania pale msalabani;
i. Katika eneo la uchumi imeandikwa;
“Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi
alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili
UHURU WA KWELI 200
kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake”
[2Kor 8:9]
Kwasababu ya Kristo aliyekuwa tajiri lakini akafanyika
maskini kwaajili yetu ili kupitia umaskini wake sisi tupate
kuwa matajiri. Ni jukumu letu kuambatana na hili neno na
kuliamini na kuliishi.
ii. Katika eneo la afya imeandikwa;
“Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili
wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe
hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa
[1Pet 2:24]
Kupigwa kwa Yesu kilikuwa chanzo cha sisi kupokea
uponyaji. Tunatakiwa kuambatana na hili neno kuliamini na
kuliishi. Ugonjwa ukija wewe sema Yesu alikufa kwaajili
yangu bila kujali hali ya nje. Ukishikilia baada yam da
uponyaji utakuwa juu yako.
iii. Katika eneo la amani imeandikwa;
“Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo
yenu na nia zenu katika Kristo Yesu” [Filip 4:7]
UHURU WA KWELI 201
Katika Yesu Kristo kuna amani ipitayo akili zote. Kupitia hiyo
amani inatuhifadhi mioyo yetu na nia zetu. Ndio maana
Yesu aliwaambia wanafunzi wake;
“Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo
mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni
mwenu, wala msiwe na woga” [Yoh 14:27]
Amani ya Kristo inatupa ujasiri na sio uwoga, amani ya
Kristo inatuhifadhi katika nia zetu na mioyo yetu.
iv. Katika eneo la furaha imeandikwa;
“Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini”
[Filip 4:4]
Katika Bwana Yesu tunakuwa na furaha suku zote.
Inawezekana kuwa na furaha siku zote katika Yesu Kristo.
Kama ingekuwa haiwezekani isingeandikwa. Ndio maana
Luka aliandika; Kwa maana ndani yake tunaishi,
tunakwenda, na kuwa na uhai wetu (Mate 17:28a)
“Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo
simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la
utumwa” [Gal 5:1]
UHURU WA KWELI 202
Biblia ya Habari Njema inasema hivi;
“Kristo alitupa uhuru, akataka tubaki huru. Basi, simameni
imara wala msikubali tena kuwa chini ya nira ya utumwa”
Katika Yesu Kristo tunakuwa huru, Yesu anataka tuwe huru
ndio maana anasema tusimame wala tusikubali kuwa chini
ya nira ya utumwa. Sisi sio watumwa kabisa ndani ya Yesu
Kristo tuko huru kabisa ndani yake. Amen Haleluya!
UHURU WA KWELI 203
Tathmini kupitia maswali kutoka katika Sura ya Saba
1: Kwanini wewe uliyeamini(uliyeokoka) uko huru (sio
mfungwa)?
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
2: Eleza kwa ufupi maana halisi ya toba
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
3: Yesu alimaliza kila kitu kinachohusu maisha yetu pale
msalabani. Taja baadhi ya maandiko yanayoonyesha
ushahidi kuwa Yesu Kristo alimaliza pale msalabani katika
maeneo yafuatayo:-
(i)Katika eneo la uchumi
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
UHURU WA KWELI 204
(ii)Katika eneo la afya
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
(iii)Katika eneo la amani
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
(iv)Katika eneo la furaha
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
UHURU WA KWELI 205
SURA YA NANE
NIMEBARIKIWA
Maandiko yanasema;
“Mungu akamwambia Balaamu, Usiende pamoja nao; wala
usiwalaani watu hawa, maana wamebarikiwa” [Hes 22:12]
Ilikuwa ni mpango wa Mungu tangu mwanzo tubarikiwe
kupitia Yesu Kristo. Mungu alimbarikia Ibrahimu ili kusudi
atakayemwamini Mwana wake wa pekee Yesu Kristo.
Ahesabiwe baraka ya Ibrahimu kwa njia ya imani.
“Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na tazama,
kondoo mume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake
katika kichaka. Basi Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo
kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya
mwanawe. Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-
yire,kama watu wasemavyo hata leo,Katika mlima wa
BWANA itapatikana. Malaika wa Bwana akamwita
Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni akasema, Nimeapa
kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno
hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, katika
kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao
wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko
pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; na
UHURU WA KWELI 206
katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa
sababu umetii sauti yangu” [Mwa 22:13-18]
Ibrahimu alipoamua kumtoa mwana wake wa pekee Isaka,
bila kumzuilia. Mungu akaapa kuwa atambariki na
kuuzidisha uzao wake, kama nyota za mbinguni na kama
mchanga wa baharini. Mungu alimuahidi Ibrahimu kupitia
baraka alizobarikiwa mataifa yote ya dunia yatabarikiwa.
Mungu alituingiza kupokea baraka ya Ibrahimu kwa njia ya
kumwamini Yesu Kristo. Ndio maana imeandikwa;
“Basi, tusemeje juu ya Ibrahimu, baba yetu kwa jinsi ya
mwili?” [Rum 4:1]
Kumbe sisi tumefanyika watoto wa Ibrahimu kwa jinsi ya
mwili kwa njia ya imani ya Yesu Kristo. Ndio maana Paulo
aliandika;
“Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa
Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi” [Gal 3:29]
Kumbe sisi tumefanyika kuwa uzao wa Ibrahimu yaani
watoto wa Ibrahimu kwa jinsi ya mwili njia ya imani ya
kumwamini Yesu Kristo. Kwa sababu hiyo sisi ni warithi
sawa sawa na ahadi ya Ibrahimu.Kama vile Mungu
alivyomuahidi Ibrahimu kuwa uzao wako utakuwa kama
nyota za mbinguni na mchanga ulioko pwani. Sisi ni zao lake
UHURU WA KWELI 207
tuliofanywa kupitia imani ya Yesu Kristo. Kwa sababu hiyo
tuna haki ya kumiliki na kuwa warithi halali wa baraka
alizobarikiwa Ibrahimu na uzao wake. Ndio maana biblia
inasema;
“Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa
alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa,
Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti; ili kwamba
baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo,
tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani” [Gal 3:14]
Kristo alifanyika laana ili atukomboe tusikae chini ya laana
na kwa njia ya imani katika yeye sisi tuliomwamini Yesu
Kristo tumebarikiwa sawa sawa na baraka ya Ibrahimu.
Kwasababu hiyo tunatakiwa kukiri wakati wote sisi ni
wabarikiwa na si walaaniwa kwa jina la Yesu Kristo.
Tumebarikiwa kwa kumwamini Yesu Kristo na kwa namna
hiyo hamna mtu yoyote anayeweza kutulaani.
Usikubali mtu yoyote anayekwambia umelaaniwa wakati
umemwamini Yesu Kristo. Mpuuzie kabisa hakuna namna
wewe uliyebarikiwa unaweza kuwa laana tena. Laana zote
alizibeba Yesu Kristo, laana za matendo ya sheria alizibeba.
Mimi na wewe kwakuwa hatuishi tena chini ya sheria bali
tunaishi katika Yesu Kristo hatulaaniwi.Ndio maana
imeandikwa;
UHURU WA KWELI 208
“Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa
alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa,
Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti” [Gal 3:13]
Laana zote alizibeba Kristo msalabani na kwasababu hiyo
mimi na wewe tuliomwamini Yesu Kristo hatuwezi kuwa
laana tena.
Sisi hatumo katika giza tena bali tupo katika nuru
Hakuna mtu awaye yoyote anaweza kuturudisha kwenye
giza tena. Hakuna namna yoyote inayoweza kumfanya
aliyemwamni Yesu Kristo kurudi gizani tena. Ndio maana
Paulo anaandika kuwa;
9: Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa
takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza
fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika
nuru yake ya ajabu
Sisi ni mzao mteule, tumeteuliwa na Mungu kwa njia ya
imani. Tumefanyika kuwa kuhani wa kifalme, tumefanyika
kuwa taifa takatifu na kuwa chini ya milki ya Mungu. Mungu
katutangazia fadhili zake ili tutoke gizani tuingie katika nuru
UHURU WA KWELI 209
yake ya ajabu biblia ya Habari njema anasema alitutoa
gizani na kutuingiza katika mwanga wake mkuu.
10: ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la
Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata
rehema.
Petro anaendelea kuthibitisha kuwa hatukuwa taifa, lakini
kwa kumwamini Yesu Kristo tumekuwa taifa la Mungu na
tumepata rehema kwa imani ya Yesu Kristo.
11: Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni
tamaa za mwili zipiganazo na roho.
Anaendelea kusema sisi kama wasafiri katika hii dunia
tuziepuke tama za mwili zipinganazo na roho. Kwasababu
sisi sio wa ulimwenguni humu kama wasafiri tunatakiwa
kuachana na tamaa za mwilini.
12: Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo
huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo
matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.
[1Pet 2:9-12]
UHURU WA KWELI 210
Petro anaendelea kusema kuwa watu wa mataifa
(wasiookoka) watutazamapo wayatazamapo matendo yetu
mazuri wamtukuze Mungu wetu. Imeandikwa;
“Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa
kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa
mapya” [2Kor 5:17]
Yesu Kristo ndiye aliyetufanya kuwa wapya; alituondoa
gizani na kututoa katika kongwa la utumwa tuliokuwa
tumebebeshwa akatufanya kuwa huru kweli kweli. Kama ni
hivyo basi tunatakiwa kutembea kama jinsi tulivyoitwa
kuwa katika yeye (Yesu Kristo). Ndio maana Paulo
aliwakumbusha kanisa la Korintho kuhusu wito wao katika
Yesu Kristo waliposahau na kuanza kuishi kama watu wa
mataifa;
“Je! Mtu wa kwenu akiwa ana daawa juu ya mwenzake
athubutu kushitaki mbele ya wasio haki, wala si mbele ya
watakatifu? Au hamjui ya kwamba watakatifu
watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu
utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo
ndogo? Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si
zaidi sana mambo ya maisha haya? Basi, mkiwa na mahali
panapohukumiwa mambo ya maisha haya, mwawaweka
kuwa waamuzi hao waliohesabiwa kuwa si kitu; katika
UHURU WA KWELI 211
kanisa? Nasema hayo nipate kuwatahayarisha. Je! Ndivyo,
kwamba kwenu hakuna hata mtu mmoja mwenye hekima,
awezaye kukata maneno ya ndugu zake? Bali
mwashitakiana, ndugu kwa ndugu, tena mbele yao
wasioamini.
Basi imekuwa upungufu kwenu kabisa kwamba
mnashitakiana ninyi kwa ninyi. Maana si afadhali
kudhulumiwa? Maana si afadhali kunyang'anywa mali
zenu? Bali kinyume cha hayo ninyi wenyewe mwadhulumu
watu na kunyang'anya mali zao; naam, hata za ndugu zenu.
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa
Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme
wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala
wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala
walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi. Na baadhi
yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini
mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana
Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu” [1Kor 6:1-11]
Kanisa la Korintho lilipoteza sura na picha katika mwenendo
katika wito walioitiwa katika Kristo Yesu. Kanisa la Korintho
walikuwa wakishitakiana wao kwa wao tenambele ya wasio
amini. Kanisa la Korintho walikuwa waasherati, waabudu
sanamu, wazinzi, walevi, wanyang’anyi, watukanaji, ilifika
mahali mpaka wakawa wanafanya ufiraji na ulawiti. Paulo
aliwakumbusha kuwa Hamjui kuwa Watakatifu
UHURU WA KWELI 212
watauhukumu ulimwengu na malaika? Aliwakumbusha
kuwa hamjui mlipokuwa watu wa mataifa kabla hamjaamini
mlikuwa watu wa matendo ya namna hiyo? Paulo
anaendelea kusema hamjui kuwa mlipoamini mlioshwa,
mlitakaswa, mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu
Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.
Paulo aliwaambia mtu aliyekiumbe kipya, aliyemwamini
Yesu Kristo kama alivyokuoshwa rohoni, walivyotakaswa na
kuhesabiwa haki kwa imani ya jina la Bwana Yesu Kristo na
katika Roho wa Mungu haifai kuenenda kama watu wa
mataifa. Kumbe kila aliyeamini katika jina la Bwana Yesu
anaoshwa, anatakaswa na kuhesabiwa haki. Paulo kwa
neema ya Mungu aliweza kulirekebisha kanisa la Korintho
kwa kuwaelekeza kilichotokea baada ya wao kuamini
(kuokoka). Paulo alijua kutofautisha kati ya mtu wa asili na
mtu aliyeamini na kufanywa kuwa kiumbe kipya. Alijua
hakuna namna ambavyo watu walianza kuufuata utu wa
kale wanaweza kugeuzwa nia zao. Ni kwa kuwaambia tu
jinsi walivyo katika Yesu Kristo na si vinginevyo.
Ukiendelea kusoma sura hii mpaka ule mstari wa ishirini
bado Paulo alikuwa anawaeleza Wakorintho waliokolewa
vipi katika Yesu Kristo. Sura ya 11 Paulo anawapa ushauri
namna ya kuepukana na matendo ya utu wa zamani (mtu
asiyeokoka). Wewe ukiwa kama mtumishi wa Mungu
unayetumika katika eneo lolote inawezekana ukawa ni
UHURU WA KWELI 213
Mchungaji, Mwalimu, Mwinjilisti, Nabii, Mtume kumbuka
kulikumbusha kundi unalolihudumia hasa walioamini. Kuwa
wao ni wakina nani katika Yesu Kristo. Kwa sababu
ukiwaambia watu jinsi wasivyo katika Kristo Yesu, aidha
kwa kuwaambia ni wenye dhambi, hawafai, hawana haki, ni
machangudoa, wametoka nuruni na kurudi gizani
kwasababu ya matendo yao ya mtu wa kale. Unawavika
kongwa zito ambalo kutoka kwake haiwezekani kwa sababu
unakuwa unawakumbusha mtu mwingine kabisa jinsi
wasivyo katika Yesu Kristo. Paulo aliweza kulirekebisha lile
kanisa la Korintho kwa neema ya Mungu kwa
kuwakumbusha wao ni wa kina nani katika Yesu Kristo
hakuongezea kile alichokuwa anakiona kwa mtazamo wake.
Paulo angeweza kuwaambia Wakorintho ninyi ni walawiti,
waasherati, wazinzi, wafiraji, wanyang’anyi, msio na haki
kwa sababu ya matendo yenu ya mtu wa kale. Aliwaambia
wao ni wakina nani katika Kristo wao ni wa kina nani na kwa
namna hiyo ile kweli ilitenda kazi na kwa neema ya Mungu
wakabadilika. Kumbuka kuwa hakuna kitu kinachoweza
kumuweka mtu huru isipokuwa kweli na kweli ni neno la
Kristo.Kinyume na hapo utakuwa unahuduma kinyume na
agizo la Bwana Yesu. Sisi ni watumishi wa Mungu katika
Kristo Yesu tulioitwa kuhudumu katika mwili wa Kristo
tunapohudumu kinyume na wito tulioitiwa katika Kristo
hatulijengi kanisa bali tunalibomoa kwa mikono yetu huku
tukijiita ni watumishi wa Mungu. Ndio maana Yohana
UHURU WA KWELI 214
anatukumbusha sisi tulioitwa katika Kristo Yesu tunapaswa
kudumu katika mafundisho ya Yesu Kristo imeandikwa;
“Kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya
Kristo, yeye hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho
hayo, huyo ana Baba na Mwana pia. Mtu akija kwenu, naye
haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani mwenu,
wala msimpe salamu. Maana yeye ampaye salamu
azishiriki kazi zake mbovu. [2Yoh 1:9-11]
Kama imeandikwa kuwa asiyedumu katika mafundisho ya
Kristo hana Mungu je si zaidi sana yule asiyefundisha
mafundisho ya Kristo? Yohana anasema mtu asiyeleta
mafundisho ya Kristo hapaswi kukaribishwa nyumbani na
wala hapaswi kupewa salamu. Kumpa salamu ni kushiriki
kazi zake mbovu, inawezekana kwa kujua au kutokujua
umehubiri au umewafundisha watu kinyume na habari
njrma ya neema ya Kristo.
Kama ile aliyopewa Paulo hiyo huduma kutoka kwa Bwana
Yesu, lakini sasa umejua anza kuhubiri injili ya neema ya
Yesu Kristo (Mat 20:24) ili watu wasibadili tu matendo yao
kuwa halisi katika Yesu Kristo zaidi sana wageuzwe nia zao
na kufanana na Kristo kikamilifu kama ilivyokuwa kusudi la
Mungu tangu asili (Rum 8:29-30). Waeleze watu jinsi
walivyogeuzwa kutoka gizani kwenda nuruni na kuwaambia
kweli jinsi ambavyo haiwezekani kurudi tena gizani.
UHURU WA KWELI 215
Waeleze watu uhalisia wao wajitambue wao ni wakina nani
katika Yesu Kristo.
Mungu anamtazama kila aliyeamini (aliyeokoka kama
Yesu Kristo).
Mungu akikutazama wewe uliyeokoka umefanana na Kristo
kwa asilimia miamoja. Ile thamani ambayo Mungu amempa
Yesu Kristo kama alivyomfanya kuwa mzaliwa wa kwanza
kwa ndugu wengi (yaani kuwa kaka yetu sisi tulimwamini)
[Rum 8:29-30]. Kwa namna hiyo kila alichokifanya Yesu
Kristo na wewe pia ulikuwepo ndani yake.
Kumbuka biblia inatueleza kuwa Kristo alidharauliwa,
alitukanwa, alifedheheshwa, alipigwa mijeledi, alipata aibu
tulikuwa ndani yake. Alipokataliwa tulikuwa ndani yake,
alipoteswa, hata alipochoka, hata alipokuwa anaonekana
hana thamani. Alipoibeba hiyo hukumu tulikuwa ndani
yake, alipokufa tulikuwa ndani yake, hata alipofufuka
tulikuwa ndani yake. Sisi tulishiriki mateso ya Yesu kwa
imani na hata Kristo alipokwenda kuzimu kunyang’anya
funguo za mauti na kuzimu tulikuwa ndani yake. Alipopaa
mbinguni na kuketi mkono wa kuume tulikuwa ndani yake,
hata sasa tuko ndani yake.
Kama ni hivyo basi hatuna sababu ya kulipia gharama mara
mbili, hakuna namna tunatakiwa tena kulipia gharama ya
UHURU WA KWELI 216
dhambi tulizolipa gharama katika Kristo Yesu. Kulipia
gharama ya kutoka kwenye vifungo, magonjwa, umaskini,
upweke, kukataliwa vyote tulilipia pale msalabani katika
Kristo Yesu. Mungu hawezi kuwa mwenye haki
kukuhukumu mara mbili kulipia gharama ya dhambi
uliyoifanya pale katika bustanini ulupokuwa ndani ya
Adamu (mtu wa kale aliyeasi). Hakuna namna tena
unatakiwa kulipia gharama ya ugonjwa na umaskini ulionao
tulilipia pale msalabani katika Kristo Yesu. Ninakushauri
ndugu yangu unayesoma kitabu hiki najua viko vitabu vingi
sana hapa duniani lakini kwakuwa umepata neema ya
kusoma kitabu hiki basi Mungu amekusudia, kwa neema
yake na ufunuo ulioko katika kitabu hiki juu ya neema ya
Yesu Kristo uweze kuwekwa huru kweli kweli.
Usikubali kulipa gharama mara mbili.
Ni mfumo wa dunia hii ndio unaotusisitiza kuwa ili uweze
kufikia kiwango fulani cha mafanikio unatakiwa
kupambana. Na wakati mwingine tumekewa utaratibu na
kanuni na miongozo ya kufanikiwa kiuchumi, kiroho. Na
tukaamini hivyo na kuweka kuwa ni muongozo wa maisha
yetu. Kiufupi ulimwengu huu umetutengenezea mfumo wa
kulipia gharama zaidi kupata vitu. Kuliko kufurahia zawadi
tulizopokea baada ya kulipia gharama ya mateso tuliyopata
katika Yesu Kristo. Biblia inateleza kwamba;
UHURU WA KWELI 217
“Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.
Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli” [Yoh
17:16-17]
Yesu aliposema wao si wa ulimwengu huu kama nisivyo wa
ulimwengu huu hakuwa anamaanisha kuwa hatutakiwi
kuishi katika huu ulimwengu. Ukisoma sura hii ya kumi na
saba mstari wa kumi na tano. Yesu aliomba mwenyewe
kuwa mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu bali
uwalinde na yule mwovu. Yesu anaposema wao si wa
ulimwengu huu anamaanisha kuwa mfumo wetu wa
maisha uko tofauti kabisa na mfumo wa huu ulimwengu.
Kwasababu hiyo hatupaswi kuenenda sawa sawa na mfumo
wa ulimwengu huu katika kila eneo. Kiuchumi
tumetofautiana sana na mfumo wa uchumi wa nyumbani
kwetu (mbinguni). Ndio maana Yesu aliwafundisha
wanafunzi wake kuomba ufalme wa Mungu kuja duniani
(Math 6:9). Lengo ni kwamba ukija uwasaidie kuishi sawa
sawa na ufalme wa Mungu unavyokusudia.
Tatizo linaanzia pale ambapo tunataka kuishi kwa kufuata
kanuni za ulimwengu kiuchumi, kiroho na katika kila eneo.
Kwa bahati mbaya mfumo wa ulimwengu umekuwa na
msukumo mkubwa kutushawishi. Kiasi ambacho tukaanza
kuchukua mifumo yao tukaihalalisha kwetu tulioamini,
tukaiishi na kuiweka kuwa miongozo ya maisha yetu.
Tukabadili sura ya kanisa kama jinsi linavyotakiwa kuwa
UHURU WA KWELI 218
kama jinsi Kristo alivyo, kanisa likageuzwa kuwa na sura ya
vyama vya siasa. Na kwa namna hiyo kanisa limeshindwa
kuvuka kiuchumi, na kiroho limekuwa kama watu
waliotelekezwa na Baba yao. Kwa sababu tunataka kuishi
kulingana na mifumo ya ulimwengu huu. Na kama
umeamini (umeokoka) sio rahisi kabisa kufanikiwa
kwasababu mfumo wa uchumi wa ulimwengu huu uko
tofauti kabisa na mfumo wa ufalme wa Mungu. Kwa hiyo
kila utakapokuwa unafanya sawa sawa na mfumo wa huu
ulimwengu utakuwa unakukataa. Sababu sio kuwa huwezi
kufanikiwa sababu hujataka kuambatana na mfumo halisi
wa ufalme wa Mungu kama jinsi ulivyo.
Kumbuka sisi ni wa agano jipya kila tunachokifanya ni
muhimu kuambatana na agano letu. Kama utakuwa ni mtu
uliyefanywa katika agano jipya ukataka kuishi katika agano
la kale. Hautafurahia kabisa alichofanya Yesu Kristo kwaajili
yako utabaki kufeli siku hadi siku. Lazima ukubali
kuambatana na injili ya Yesu Kristo na kuambatana na
ufalme wa Mungu ili kusudi uone matoeo. Mfano Wakristo
wengi wamekuwa wakiamini usemi huu kuwa “asiyefanya
kazi na asile” na kwa namna hiyo watu wamekuwa
wakijitesa kwa shughuli nyingi na kuona hamna mtu yoyote
anaweza akawasaidia isipokuwa kwa kazi wanazozifanya.
Wakati huo biblia kwamba;
UHURU WA KWELI 219
“Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye
ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtauwa, imani yake
mtu huyo imehesabiwa kuwa haki” [Rum 4:5}
Ukianza ule mstari wan ne unaeleza wazi kuwa mtu
afanyaye kazi ujira wake hauhesabiwi kuwa ni neema bali ni
deni. Mstari huu wa tano biblia inaeleza kuwa yule
asiyefanya kazi na anamwamini yeye yaani Yesu Kristo mtu
huyo imehesabiwa kuwa ni haki. Hii mistari haimaanishi
kuwa usifanye kazi, hii mistari inaonyesha kuwa imani yako
unaiweka wapi unapofanya kazi. Maana ulimwengu huu
unataka tutumikie kazi tuamini kuwa kazi ndiyo
inayotufanya tufanikiwe. Lakini biblia inatuambia kuwa
tukimwamini hata tukiwa bado hatujafanya kazi
tunahesabiwa haki. Kwahiyo shida haipo kwenye kufanya
kazi shida ipo kwenye imani yaani unaamini nini kazi au
unamwamini Yesu Kristo. Na kwa namna hiyo ukihamisha
imani yako kutoka kwenye kazi ukamwamini Yesu ambaye
alihakikisha anakufa kwaajili yako. Ili wewe usiwe mtumwa
wa kazi bali ufurahie neema ya kazi aliyoifanya msalabani
kwaajili yako.
Na ukianza kuamini namna hiyo utaanza kuona kila
unachokifanya, hakitaendeshwa na mfumo wa ulimwengu
huu bali ufalme wa Mungu. Kumbuka ufalme wa Mungu
unapoanza kutenda kazi kwaajili yako uwe na uhakika.
Mafanikio kwenye maisha yako yatafurika kwa sababu
UHURU WA KWELI 220
umeamua kukubali kwa kuamini kitu ambacho Yesu Kristo
amefanya kwenye maisha yako. Usikubali kulipia gharama
mara mbili kila kitu unachohitaji ulilipia pale msalabani
katika Yesu Kristo. Kubaliana na huu ukweli ambatana nao,
amini uanze kufurahia zawadi ya wokovu kwenye maisha
yako leo.
UHURU WA KWELI 221
Tathmini kupitia maswali kutoka katika Sura ya Nane
1: Kwanini tumebarikiwa katika Kristo Yesu?
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
2: Ni nani aliyetukomboa kutoka katika laana?
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
3: Kwanini aliyebarikiwa hawezi kulaaniwa?
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………4:
Kwanini aliyeamini (aliyeokoka) hawezi kutoka nuruni
kurudi gizani?
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
5: Kwanini Mungu anatufananisha na Yesu Kristo?
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
UHURU WA KWELI 222
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………
6: Kwanini usikubali kulipa gharama mara mbili?
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………
UHURU WA KWELI 223
SURA YA TISA
MIMI NI MSHINDI
atika waandishi katika biblia Paulo alikuwa ni miongoni
mwa watu walioifunua siri ya ushindi kwenye maisha
yao, kwasababu alijua siri ya ushindi kwenye maisha
yao haitegemeani na nguvu alizo nazo, ujuzi au maarifa
aliyo nayo. Kwasababu aliamini uwezo wake alio nao, nguvu
na maarifa si kitu mbele za Mungu katika Yesu Kristo. Paulo
anashuhudia kwamba;
“Kama ilivyoandikwa ya kwamba, kwa ajili yako tunauawa
mchana kutwa, tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa
kuchinjwa. Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na
zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda” [Rum 8:37]
Paulo alizungumza kwa lugha ya falsafa kuwa tunauawa
mchana kutwa. Kimsingi sio kwamba tunauawa mchana
kutwa bali ni kwamba sisi si wa ulimwengu huu ambao
Kristo anashuhudia kuwa; Kama mngekuwa wa ulimwengu,
ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake lakini
kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua
katika ulimwengu, kwasababu hiyo ulimwengu huwachukia
(Yoh 15:19).
K
UHURU WA KWELI 224
Ndio maana ulimwengu unatafuta kila namna ya kutuchinja
kama ilivyoandikwa tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa
kuchinjwa. Ndio maana usiku na mchana Shetani haachi
kutufuatilia kama jinsi Yohana alivyoandika kuwa;
“Kwahiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao huko. Ole
wan chi nabahari! Kwa maana yule ibilisi ameshuka kwenu
mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati
mchache tu” [Ufu 12:12]
Ili kuhakikisha anaharibu kusudi la Mungu kama
alivyotuchagua katika kizazi hiki. Ndio maana ulimwengu
unatuchukia, Shetani anapigana na sisi kwa sababu anajua
jinsi tulivyo. Tuko tofauti na yeye ndio maana imeandikwa;
Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake;
basi ufalme wake utasimamaje? (Math 12:26). Kwa hiyo
tunapigana na Shetani kwa sababu hayuko upande wetu.
Ndio maana sisi tuliompokea Kristo katika eneo la
mafanikio katika eneo lolote lile tunakutana na vita kubwa
isiyo ya kawaida inaweza kuwa vita ya uchumi, vita ya
huduma na katika kila eneo kwenye maisha yetu ya kiroho
na kimwili. Shetani anajua ana mda mchache ndio maana
anapambana tusiachilie kusudi la Mungu katika ulimwengu
huu kama alivyotuchagua. Ashukuriwe Mungu kwasababu
neno la Mungu linashuhudia kuwa lakini katika mambo
UHURU WA KWELI 225
hayo yote tunashinda na zaidi ya kushinda kwa yeye
aliyetupenda yaani Yesu Kristo.
Katika maeneo napenda kumuelewa Paulo kama jinsi Roho
Mtakatifu alivyomfunulia kuandika mstari huu bila kuweka
hali ya kutegemea huo ushindi kutoka kwetu binafsi. Bali ni
kuwa na ushindi huo kwa sababu ya yeye aliyetupenda
(Yesu Kristo). Kwa hiyo ushindi wetu hautokani na hali
tulizo nazo, iwe ni umaskini, magonjwa, udhaifu wa aina
yoyote hayajaorodheshwa.
Ingekuwa sababu ya kushindwa kwetu ni umaskini basi
Paulo angesema hauwezi kushinda kama wewe ni maskini.
Kama ingekuwa ni ugonjwa au udhaifu wowote ulio nao
Paulo angesema kwa sababu ya ugonjwa au udhaifu ulio
nao hauwezi kushinda. Lakini Paulo anaweza msisitizo
katika kumtaja yeye aliyetupenda yaani Yesu Kristo
tunashinda na zaidi ya kushinda.
Tafsiri nyepesi ya andiko hili maana yake ni nini? Maana
yake ni kwamba hatushindi na zaidi ya kushinda kwasababu
ya jinsi tunavyoshindana. Bali ni kwasababu ya jinsi
ambavyo Yesu Kristo alitupigania na alishinda na zaidi ya
kushinda pale msalabani. Jamani hii ni ajabu sana, hii ni
habari njema! Kumbe! Kushinda kwetu ugonjwa sio kwa
sababu ninapigana mimi. Ila ni kwasababu yake Yesu Kristo
UHURU WA KWELI 226
aliyepigana kwaajili yangu akashinda na zaidi ya kushinda
kama maandiko yanavyoshuhudia kuwa; Bali alijeruhiwa
kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya
amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi
tumepona (Isa 53:5).
Kumbe hatushindi na zaidi ya kushinda umaskini kwa
sababu tunapigana sisi bali ni kwa sababu Yesu Kristo
alipigana na umaskini na kwa neema yake Bwana wetu Yesu
Kristo alifanyika maskini ili kwamba sisi tupate kuwa
matajiri kwa umaskini wake (2Kor 8:9).
Ushindi na zaidi ya ushindi tulio nao katika Yesu Kristo ni
ushindi ambao upo kwa namna ya rohoni. Kwa tafsiri
nyingine naweza kusema kuwa ni ushindi ambao uko rohoni
lakini haujadhihirishwa kwa namna mwilini. Kazi yetu ni
moja ni kuudhihirisha ushindi tulio nao rohoni kwa namna
mwilini.
Kwa maneno mengine ni kwamba kuna namna ambavyo
tunatakiwa kuwa na imani ya kushinda na zaidi ya kushinda
ili imani tuliyo nayo iweze kujifunua mwilini. Ili tuweze kuwa
na imani ya aina yoyote lazima tujue imani inahitaji nini, ili
tuweze tuweze kutembea nayo.
UHURU WA KWELI 227
Maandiko yanasema hivi;
“Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni
bayana ya mambo yasiyoonekana” [Ebr 11:1]
Mstari huu tafsiri ya biblia ya kiingereza King James Version
(KJV) katika neno bayana ya mambo yasiyoonekana
ametumia neno “the evidence of things not seen”. Maana
yake ni uhalisia wa vitu ambavyo bado havijaonekana kwa
namna ya mwilini. Kwahiyo ikiwa wewe ni mgonjwa na
mwili unalalamika kabisa unaumwa, haibadilishi ukweli
kuwa wewe ni mzima. Kama wewe ni maskini huna hata
dola moja mfukoni haibadilishi kwamba wewe ni tajiri.
Kadhalika katika maeneo mengine unapopitia shida, taabu
au changamoto yoyote ile haibadilishi ukweli kuwa hiyo
taabu, shida au changamoto ilisha isha.
Jiepushe kuwa na imani ya kuamini ushindi wako
kutokana na hali ya mazingira inavyoonekana nje [au
ulimwengu wa mwili].
Unaweza kuamia kuanzia sasa katika changamoto ya aina
yoyote ile inayoonekana mwilini. Kuitafutia majibu ya
kiroho na kuacha kuishi kutokana na mazingira ya nje. Mara
zote mwili na roho zimepingana. Ndio maana Paulo
aliwaandikia wagalatia kuwa; Kwa sababu mwili hutamani
ukishindana na roho, na roho ikishindana na mwili; kwa
UHURU WA KWELI 228
maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka
(Gal 5:17).
Siku zote mwili utakwambia hicho unachokiamini hakiwezi
kuwa, mwili utakupa uthibibisho kuwa huoni maumivu ya
uvimbe unao usikia. Mwili utakwambia huoni jinsi ulivyo
maskini huna hata dola moja mfukoni, hata jana usiku
umelala njaa. Siku zote mwili utakupinga kuwa haiwezekani
hicho unachokiamini rohoni kikawa halisi.
Kuna namna nzuri ya kuushinda mwili wako usiwe na nguvu
ya kushinda kile unachokiamini rohoni. Paulo aliandika hivi
kwa Wakolosai;
“Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi” [Kol 3:2]
Katika mstari huu Biblia tafsiri ya King James Version (KJV)
kwenye neno yafikirini yaliyo juu ametumia neno “set your
affection on things above”. Maana yake lenga ufahamu
wako kuathiriwa na mambo yaliyo juu. Tafsiri ya biblia ya
The Passion Translation (TPT) Anasema mstari huu namna
hii. Nimetafsiri kwa lugha ya Kiswahili hivi;
“Ndio, sherehekea hazina za ulimwengu wa roho na ujijaze
mawazo, ya uhalisia wa ulimwengu wa roho, na sio
uharibifu wa ulimwengu wa mwili”
Mara zote mawazo ya ulimwengu wa mwili ni kutaka
kutuonyesha kuwa uhalisia wa hazina za mbinguni sio kweli.
UHURU WA KWELI 229
Kwa kuangalia hali ya wakati huo unayopitia, Lakini biblia ya
TPT inatuhakikishia kuwa; tusherehekee hazina za
ulimwengu wa roho na kuachana na uharibifu wa
ulimwengu wa mwili kwasababu hazina za ulimwenmgu wa
roho ni halisi. Ulimwengu wa mwili una uharibifu mwingi,
lakini ashukuriwe Mungu tukienenda katika roho uharibifu
huu hautatupata. Kwa namna ambavyo unafikiri na
kutafakari hazina halisi za mbinguni na kuishi kuwa sehemu
yako ya maisha. Bila kuangalia mazingira ya nje ndivyo
unavyojiweka kwenye nafasi ya kupokea katika ulimwengu
wa mwili mambo ambayo yako rohoni.
Kwahiyo ukitaka udhihirisho wa neno la Mungu ambalo ni
kweli kama Yohana alivyoandika kuwa; “Uwatakase kwa ile
kweli; neno lako ndiyo kweli” (Yoh 17:17). Nilazima kuliishi
hilo neno. Jambo lolote nje ya neno la Mungu ni uongo, siku
zote Shetani anapenda tuamini uongo wake. Neno la
Mungu likisema wewe ni mshindi na zaidi ya kushinda
Shetani anakwambia umeshindwa na zaidi ya kushindwa.
Neno la Mungu linapokwambia wewe ni tajiri, Shetani
anasema wewe ni maskini, neno la Mungu likisema
umepona Shetani anasema unaumwa bado kwani huoni
uvimbe au maumivu uliyonayo, huoni hospitali
wamekwambia una ugonjwa bado. Ndivyo Shetani
anapenda ujione.
UHURU WA KWELI 230
Jambo la muhimu ni kuacha kuamini uongo wa Shetani na
kuishi uhalisia wa ulimwengu wa roho kupitia neno lake.
Hata Shetani akisema wewe ni maskini bado, wewe ni
mgonjwa, akisema huwezi kufanikiwa katika jambo hili
usimzingatie. Kwa kuwa na imani hiyo ndio mwanzo wa
udhihirisho wa ulimwengu wa roho kupitia neno la Mungu
kwenye maisha yako.
Tuangalie mfano huu;
Basi Nebukadreza akatoa amri kwa hasira na ghadhabu,
waletwe hao Shadraka, na Meshaki, na Abednego. Basi
wakawaleta watu hao mbele ya mfalme. Nebukadreza
akajibu, akawaambia, Enyi Shadraka, na Meshaki na
Abedinego, je! Ni kwa makusudi hata hamtumikii mungu
wangu wala kuisujudia sanamu ya dhahabu
niliyoisimamisha? Basi sasa, kama mkiwa tayari wakati
mktakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na
zeze, na santuri, na zomari, na namna zote za ngoma,
kuanguka na kuisujudia sanamu niliyoishimamisha, ni
vema; bali msipoisujudia, mtatupwa saa hiyo hiyo katika
tanuru iwakayo moto; naye ni nani Mungu yule atakaye
waokoa ninyi na mikono yangu? Ndipo Shadraka, na
Meshaki, na Abedinego, wakajibu, wakamwambia mfalme,
Ee Nebukadreza, hamna haja ya kukujibu katika neno hili.
UHURU WA KWELI 231
Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza
kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na
mkono wako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo, ujue, Ee
mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako,
wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.
Ndipo Nebukadreza akajaa ghadhab, na sura ya uso wake
ikabadilika juu ya Shadraka, Meshaki, na Abedinego, basi
akatoa amri watie moto ile tanuru mara saba kuliko desturi
yake kutiwa moto. Kisha akawaamuru baadhi ya watu
mashujaa wa jeshi lake kuwafunga Shadraka, Meshaki, na
Abedinego, na kuwatupa katika ile tanuru iliyokuwa
ikiwaka moto. Basi watu hao wakafungwa, hali wamevaa
suruali zao, na kanzu zao, na mavazi yao mengine,
wakatupwa katikati ya ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto.
Basi kwasababu amri ya mfalme ilikuwa ni kali, na ile
tanuru ilikuwa ina moto sana, mwako wa ule moto
ukawaua wale watu walio washika Shadraka, na Meshaki,
na Abednego. Na watu hao watatu, Shadraka, na Meshaki,
na Abednego, wakaanguka, hali wamefungwa, kati kati ya
ile tanuru iliyokuwa inawaka moto. Ndipo Nebukadreza
akastaajabu, akainuka kwa haraka; akanena, akawaambia
mawaziri wake, Je! Hatukutupa watu watatu, hali
wamefungwa, kati kati ya moto? Wakajibu wakamwambia
mfalme, Kweli, Ee mfalme. Akajibu, akasema, Tazama,
mimi naona watu wane, nao wamefunguliwa, wanatembea
katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wan
UHURU WA KWELI 232
ne ni mfano wa mwana wa miungu. Kisha Nebukadreza
akaukaribia mdomo wa ile tanuru iliyokuwa inawaka moto.
Akanena akasema, Enyi Shadraka, na Meshaki na
Abedinego, watumishi wa Mungu aliyejuu, tokeni, mje
huku. Ndipo Shadraka, na Meshaki na Abedinego wakatoka
katika ule moto. Na maamiri, na manaibu, na maliwali, na
mawaziri, waliokuwa wamekusanyika pamoja,
hawakuwaona watu hao, ya kuwa ule moto ulikuwa hauna
nguvu juu ya miili yao, wala nywele za vichwa vyao
hazikuteketea, wala suruali zao hazikubadilika, wala harufu
ya moto haikuwapata hata kidogo. [Dan 3:13-27]
Shadraka, Meshaki na Abedinego waliamua kutozingatia ni
kitu gani mfalme anawa amrisha ambacho sio sahihi.
Waliamua kuishi uhalisia wa neno la Mungu kama Daudi
alivyoandika kuwa;
“Huwafanya malaika zake kuwa pepo, Na watumishi wake
kuwa moto wa miali” [Zab 104:4]
Shadraka, Meshaki na Abedinego walijua siri huu kuwa
Mungu anawafanya watumishi wake kuwa miali ya moto.
Ndio maana hawakukubali kuitumikia miungu ya mfalme
Nebukadreza. Ile imani ya kuokolewa katika moto
ikajifunua kuwa halisi kwenye tanuru la moto. Watu
waliowashika Shadraka, Meshaki na Abedinego kwa
UHURU WA KWELI 233
muwako tu wa ule moto uliwaua lakini Shadraka, Meshaki
na Abednego haukuwa na nguvu juu ya miili yao, nywele za
vichwa vyao, hata harufu ya moto haikuwapata. Huyu ni
Mungu mwenye uweza wote, huyu ni Mungu aliyeziumba
mbingu na nchi.
Hii ndio maana ya halisi ya kuwa kwa imani kila jambo
lisilowezekana linaweza kuwezekana. Ebu tujifunze kwa
hwa watumishi Shadraka, Meshaki na Abedinego kama
Mungu aliwatetea katikati ya jaribu gumu na zito namna
kwa imani zao. Je si zaidi sana Mungu kujifunua kwenye
ugonjwa ulio nao, si zaidi sana Mungu kujifunua katika
umaskini ulio nao. Ni rahisi sana ndio maana Yesu
aliwaaambia Wanafunzi wake;
“Yesu akawaambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake
aaminiye” [Mark 9:23]
Kwa imani hufanya bonde kuwa mlima mrefu na mlima
mrefu kuwa bonde. Kwa imani palipopotoka pananyooka
na palipoparuza panasawazishwa. Kwa imani bahari huwa
nchi kavu na nchi kavu huwa bahari yenye kina kirefu.
Kuanzia sasa anza kufurahia uhalisia wa hazina iliyoko
katika ulimwengu wa roho kupitia neno la Mungu hakuna
jambo litakalo shindikana kwenye maisha yako.
UHURU WA KWELI 234
Biblia inakiri kuwa sisi tumebarikiwa sio kwa sababu yetu
bali kwasababu ya Yesu Kristo aliyekufa msalabani
kwaajili yetu.
Yohana alimwandikia mpenzi wake Gayo hivi;
“Mzee kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli. Mpenzi
naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya
yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo” [3 Yoh 1:1-2]
Mstari huu kwa tafsiri ya biblia ya The Passion Translation
(TPT) imetafsiriwa hivi;
“Mpenzi naomba ufanikiwe katika kila njia na uendelee
kufurahia afya njema kama nafsi yako ifanikiwavyo”
Maana yake ni kwamba baraka ni jambo la rohoni, sio
jambo ambalo liko mwilini. Ndio maana Yohana alitaka
mpenzi wake Gayo afanikiwe kama alivyofanikiwa katika
ulimwengu wa roho katika kila njia na afya yake. Kwasababu
yoyote aliye ndani ya Kristo kila baraka iko pamoja naye.
Paulo aliandika hivi;
“Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo,
aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu
wa roho, ndani yake Kristo; 6: Na usifiwe utukufu wa neema
yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.”
[Efe 1: 3, 6]
UHURU WA KWELI 235
Kumbe Mungu alishatubariki baraka zote katika ulimwengu
wa roho. Hatukubarikiwi baraka za mambo madogo
yanayohesabika, bali ametubariki kwa baraka zote katika
ulimwengu wa roho. Pia ametuneemesha yaani kupewa
upako wa msaada tusio stahili na kibali cha kukubalika
tusivyostahili katika Mpendwa yaani Yesu Kristo.
Baraka ni nguvu ya upako inayomsaidia mtu kufanikiwa
kimwili. Au ni maneno mazuri au mambo mazuri
yanayotamkwa juu ya mtu yanayotarajiwa yatokee katika
maisha ya mtu. Biblia inaposema tumebarikiwa maana yake
tumepewa nguvu ya upako ya kutusaidia kufanikiwa mwilini
kabisa.
Tuangalie maandiko mengine yanayoonyesha uhalisia wa
jinsi tulivyo katika Kristo Yesu.
Paulo anasema hivi;
“Macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito
wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wake katika
watakatifu jinsi ulivyo; na ubora wa ukuu wa uweza wake
ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa
nguvu za uweza wake; aliotenda katika Kristo alipomfufua
katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika
ulimwengu wa roho; juu sana kuliko ufalme wote, na
mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala
UHURU WA KWELI 236
si ulimwenguni hum utu, bali katika ule ujao pia” [Efe 1:18-
21]
Maandiko yanaposema na utajiri wa utukufu wake katika
watakatifu jinsi ulivyo. Anamaanisha kuufunua uzuri wa
utajiri wa baraka zilizoko ndani yetu katika macho ya damu
na nyama. Ua lina kikonyo chenye rangi ya kijani pamoja na
uzuri wa rangi inayojidhihirisha nje ya kikonyo cha hilo ua.
Uzuri wa ua unaoneka kwenye udhihirisho wa rangi
iliyojitokeza nje. Ua lisipotoa nje udhihirisho wa rangi ubora
wake unakuwa umepunguka. Kama Paulo alivyosema
Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo
anamaanisha udhihirisho wa baraka tulizonazo katika
ulimwengu wa roho kuwa dhahiri katika ulimwengu wa
mwili. Kwa maana hiyo basi Mungu hawezi kupokea
utukufu wake pasipo udhihirisho wa baraka hizo kujifunua
katika macho ya damu na nyama.
Biblia inashuhudia kuwa katika uweza wa nguvu zake katika
Kristo Yesu kama tulivyoketishwa pamoja naye katika
ulimwengu wa roho kwa jinsi tulivyofufuliwa pamoja naye
(Efe 2:6). Tuliwekwa juu sana kuliko ufalme wote, na
mamlaka, na nguvu na usultani na kila jina linalotajwa
katika ulimwengu huu na ule ujao pia. Lakini pamoja na
hayo yote tuliyopewa kwenye ulimwengu wa roho
UHURU WA KWELI 237
yatakuwa bure kama yasipojifunua na kwa dhahiri katika
macho ya damu na nyama.
Paulo aliwaandikia Warumi hivi;
“Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala
kwasababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi
wa neema na kile kipawa cha haki watatawala katika
uzima kwa yule mmoja, Kristo Yesu” [Rum 5:16-17]
Kumbe hatuhitaji kuomba neema ya Kristo wala kuomba
kipawa (zawadi) cha haki. Kwa sababu ni vitu tulivyo navyo.
Biblia inaposema kutawala maana yake ni mkakati wa
kisheria unaotusaidia sisi tulioamini (tuliookoka) kutawala
kisheria. Maana yake tumepewa wingi wa neema na kipawa
cha haki ili vitusaidie kutawala katika maisha. Kutawala
dhambi, kutawala umaskini, kutawala changamoto za kila
aina kwenye maisha yetu.
Kwanini baraka tulizobarikiwa hazijidhihirishi mwilini?
Ni kwasababu ya vita ya Shetani. Watoto wa Mungu wengi
hawafanikiwi kwa sababu ya vita za shetani. Shetani
asingependa kabisa yoyote anayemwamini Kristo
alichobarikiwa kwenye ulimwengu wa roho kiwe dhahiri
katika ulimwengu wa mwili. Ndio maana anatumia hila
yaani udanganyifu, uongo au ulaghai.Hila au kitu
UHURU WA KWELI 238
kinachoonekana ni chema au kina wema lakini nyuma yake
au ndani yake kimebeba maangamizi makubwa sana.
Maandiko yanasema hivi;
“Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika
uweza wa nguvu zake.Vaeni silaha zote za Mungu, mpate
kuweza kuzipinga hila za Shetani” [Efe 6:10-11]
Kama ni hivyo basi kumbe Shetani anapokuja kupigana vita
na wewe ili udhihirisho wa baraka, utajiri, ufalme na yote
tuliyopewa katika ulimwengu wa roho usijidhihirishe
anatumia hila. Kwa tafsiri nyepesi ni kwamba Shetani
anatumia hila ili kutucheleweshea udhihirisho wa baraka
tulizo nazo au zisitokee kabisa.
Shetani alitumia hila kumdanganya Adamu na hawa
kwenye bustani ya Edeni na kupitia hao tukaingizwa
kwenye laana ya mauti na kuondolewa ufalme. Kwasababu
hiyo tukaondolewa kwenye nafasi ya utawala kama vile
Mungu alivyotuagiza kutawala samaki wa baharini, ndege
wa angani, wanyama kila chenye kutambaa nan chi yote pia
(Mwa 1:26), tukamuuzia Shetani utawala tuliokuwa nao
tukawa watumwa na kuwekwa nafasi ya mwisho katika
ngazi ya utawala. Ashukuriwe Mungu kwasababu alishuka
mwenyewe (Yesu Kristo) kuja kurejesha utawala uliopotea
ili tuendelee kumiliki na kutawala.
UHURU WA KWELI 239
Tuangalie hila aliyotumia Shetani kumdanganya Hawa
kwenye bustani ya Edeni.
Musa aliandika;
“Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula,
wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa,
basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na
mumewe, naye akala” [Mwa 3:6]
Kumbe Shetani hakwenda na majeshi ya farasi, wala
hakwenda na mkuki kwenye bustani ya Edeni bali alitumia
hila ya kumdanganya kwa maneno ya uongo kama Paulo
alivyoshuhudia kuwa;
“Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa
kwa hila yake, asije akawaharibu fikra zenu, mkauacha
unyofu na usafi wa Kristo” [2Kor 11:3]
Shetani anapigana vita zake kwa akili sana. Ndio maana
anatumia hila ili kutudanganya kwenye fikra zetu na
kuharibu mpango wa Mungu kwenye maisha yetu. Kwa
sababu najua kusudi la Mungu ni kutaka kuona baraka zake
na ahadi zake zinajidhihirisha kwenye maisha yetu. Ndio
maana maandiko yanasema;
“Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita
kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili,
bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome)
UHURU WA KWELI 240
tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho
juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikra ipate
kumtii Kristo” [2Kor 10: 3-5]
Kumbe kazi ya Shetani ni kutuambia uongo kwenye fikra
zetu ili tuamini uongo wake. Ili kile ambacho ni halisi Mungu
amekiahidi kisitokee kwenye maisha yetu. Ndio maana
tunatakiwa kuziteka fikra zetu zipate kumtii Kristo.
Kwasababu tukiunganishwa mawazo yetu katika Kristo Yesu
na kumtazama wakati wote tutaakisi uweza wake, ukuu
wake, utajiri wake na ufalme ndani yake na kuwa hivyo
halisi katika maisha yetu ya mwilini.
UHURU WA KWELI 241
Tathmini kupitia maswali kutoka katika Sura ya Tisa
1: Ni nani aliyetupa kushinda?
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………...
2: Kwanini aliyeokoka hawezi kushindwa?
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………
3: Kwanini ushindi wetu hautokani na hali yetu ya nje/
mazingira yanayoonekana kwa macho ya damu na nyama?
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………
4: Elezea kwa ufupi, uhalisia tulionano katika Kristo Yesu
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
UHURU WA KWELI 242
…………………………………………………………………………………………
……………………………………
5: Taja sababu moja, inayosababisha baraka tulizobarikiwa
katika ulimwengu wa roho zijidhihirishe mwilini.
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………
UHURU WA KWELI 243
SURA YA KUMI
NITAKIRI HIVI DAIMA
“Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa
chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani
tulihubirilo. Kwasababu ukimkiri Yesu kwa Kinywa chako ya
kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu
alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo
mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata
kupata wokovu” [Rum 10:8-10]
Mdomo ni mtaji wa ukiri, mdomo ni silaha ambayo
ikitumika vizuri inabadilisha hali ya maisha ya mtu. Mdomo
kwa lugha ya kiingereza yaani “mouth” limetokana na lugha
ya kigiriki “stoma” maana yake “the edge of a” maana yake
“makali ya”.Maana yake mdomo ni kibebeo cha maneno
yanayotoka katika ulimi wako. Kwahiyo basi kupitia mtaji
wa mdomo na utaamua uwe mtu mkuu au uwe mtumwa.
Yakobo aliandika kwamba;
“Tena angalieni merikebu; ingawa ni kubwa kama nini, na
kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo
sana, ko kote anakoazimia kwenda nahodha. Vivyo hivyo
ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu.
UHURU WA KWELI 244
Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa
sana. Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi,
umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote
unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao
huwashwa moto na jehanum. Maana kila aina ya
wanyama, na ya ndege, na ya vitambaavyo, na ya vitu
vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa
na wanadamu. Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu
usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti. Kwa huo twamhimidi
Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu
waliofanywa kwa mfano wa Mungu. Katika kinywa kile kile
hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo
kuwa hivyo. Je! Chemchemi katika jicho moja hutoa maji
matamu na maji machungu? Ndugu zangu, Je! Mtini
waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Kadhalika
chemchemi haiwezi kutoa maji ya chumvi na maji matamu”
[Yak 3: 4-12]
Yakobo ameufananisha ulimi na usukani mdogo wa meli,
ndio maana anasema ijapokuwa ni usukani mdogo lakini
nahodha anaweza kuelekeza meli nzima kupitia huo
usukani mdogo. Kupitia ulimi unaweza kubariki au kulaani
maisha yako au maisha ya wengine. Yakobo anaendelea
kusema haifai katika kinywa chako kutoka baraka na laana,
anaendelea kusema chemichemi haiwezi kutoa maji
UHURU WA KWELI 245
matamu na maji machungu. Maana yake ikitokea kwenye
kinywa chako kunatoka maneno ya baraka na laana basi
ujue kunashida mahali. Tumepewa nafasi ya kusimamia
baraka tu yaani kutamka kwa mdomo kupitia ulimi maneno
ya baraka.
Ndio maana Yesu aliwakataza Yakobo na Yohana kutamka
maneno ya kuua. Biblia inasema;
“Yesu akamwambia, Msimkataze, kwa kuwa yeye ambaye
si kinyume chenu yu upande wenu. Ikawa, siku za kupaa
kwake zilipokuwa karibu kutimia, yeye aliukaza uso wake
kwenda Yerusalemu; akatuma wajumbe kutangulia mbele
ya uso wake; wakaenda wakaingia katika kijiji cha
Wasamaria, ili kumtengenezea mahali. Lakini wenyeji
hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake
kwenda Yerusalemu. Wanafunzi wake Yakobo na Yohana
walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto
ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye
alivyofanya]? Akawageukia, akawakanya. [Akasema,
Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.] Kwa maana
Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali
kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine” [Luk
9:50-56]
Yakobo na Yohana walifikiri wako sahihi kutaka kutamka
maneno ya kuua kwa kualika moto ushuke kutoka
mbinguni. Lakini Yesu Kristo anawaambia hamjui roho
UHURU WA KWELI 246
mliyonayo, Mwana wa Adamu hakuja kuangamiza roho za
watu bali kuokoa. Kwahiyo haijalishi ni jambo gani baya
unakutana nalo tamka kwenye mdomo wako baraka tu na
sio laana. Uwe umeumizwa, uwe umefadhaishwa, uwe uko
katika hali ngumu bado hutakiwi kukiri laana kwenye
maisha yako au kwenye maisha ya wengine.
Maeneo tunayotakiwa kukiri wakati wote kwenye maisha
yetu kupitia imani ya Yesu Kristo;
Nitakiri mimi nimebarikiwa
Nitakiri mimi ni mrithi
Nitakiri mimi ni mfalme
Nitakiri mimi nimeponywa
Nitakiri mimi ni mshindi
Paulo aliwaandikia hivi Wakorintho;
“Kwa maana kujisifu kwetu ni huku, ushuhuda wa dhamiri
yetu, ya kwamba kwa utakatifu na weupe wa moyo utokao
kwa Mungu; si kwa hekima ya mwili, bali kwa neema ya
Mungu; tulienenda katika dunia, na hasa kwenu ninyi.
Maana hatuwaandikii ninyi neno, ila yale msomayo, au
kuyakiri; nami nataraji ya kuwa mtayakiri hayo hata
mwisho” [2Kor 1:12-13]
UHURU WA KWELI 247
Paulo aliwaambia Wakorintho kuwa tunawaandikieni hayo
kwasababu ninatarajia mtayakiri hayo hata mwisho.
Nitakiri mimi nimebarikiwa
Ilikuwa ni mpango wa Mungu tangu mwanzo tubarikiwe
kupitia Yesu Kristo. Mungu alimbarikia Ibrahimu ili kusudi
atakayemwamini Mwana wake wa pekee Yesu Kristo.
Ahesabiwe baraka ya Ibrahimu kwa njia ya imani.
“Ibrahimu akainua macho yake, akaangalia, na tazama,
kondoo mume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake
katika kichaka. Basi Ibrahimu akaenda akamtwaa huyo
kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya
mwanawe. Ibrahimu akapaita mahali hapo Yehova-
yire,kama watu wasemavyo hata leo,Katika mlima wa
BWANA itapatikana. Malaika wa Bwana akamwita
Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni akasema, Nimeapa
kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno
hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, katika
kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao
wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko
pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; na
katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa
sababu umetii sauti yangu [Mwanz 22:13-18]
UHURU WA KWELI 248
Ibrahimu alipoamua kumtoa mwana wake wa pekee Isaka,
bila kumzuilia. Mungu akaapa kuwa atambariki na
kuuzidisha uzao wake, kama nyota za mbinguni na kama
mchanga wa baharini. Mungu alimuahidi Ibrahimu kupitia
baraka alizobarikiwa mataifa yote ya dunia yatabarikiwa.
Mungu alituingiza kupokea baraka ya Ibrahimu kwa njia ya
kumwamini Yesu Kristo. Ndio maana imeandikwa;
“Basi, tusemeje juu ya Ibrahimu, baba yetu kwa jinsi ya
mwili?” [Rum 4:1]
Kumbe sisi tumefanyika watoto wa Ibrahimu kwa jinsi ya
mwili kwa njia ya imani ya Yesu Kristo. Ndio maana Paulo
aliandika;
“Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa
Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi” [Gal 3:29]
Kumbe sisi tumefanyika kuwa uzao wa Ibrahimu yaani
watoto wa Ibrahimu kwa jinsi ya mwili njia ya imani ya
kumwamini Yesu Kristo. Kwasababu hiyo sisi ni warithi sawa
sawa na ahadi ya Ibrahimu. Kama vile Mungu alivyomuahidi
Ibrahimu kuwa uzao wako utakuwa kama nyota za
mbinguni na mchanga ulioko pwani. Sisi ni zao lake
tuliofanywa kupitia imani ya Yesu Kristo. Kwasababu hiyo
tuna haki ya kumiliki na kuwa warithi halali wa baraka
alizobarikiwa Ibrahimu na uzao wake. Ndio maana biblia
inasema;
UHURU WA KWELI 249
“Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa
alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa,
Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti; ili kwamba
baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo,
tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani” [Gal 3:14]
Kristo alifanyika laana ili atukomboe tusikae chini ya laana
na kwa njia ya imani katika yeye sisi tuliomwamini Yesu
Kristo tumebarikiwa sawa sawa na baraka ya Ibrahimu. Kwa
sababu hiyo tunatakiwa kukiri wakati wote sisi ni
wabarikiwa na si walaaniwa kwa jina la Yesu Kristo.
Nitakiri mimi ni mrithi
Kupitia Yesu Kristo tulifanyika wana na Warithi kwa njia ya
Imani.
“Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto,
hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote; bali
yu chini ya mawakili na watunzaji, hata wakati uliokwisha
kuamriwa na baba. Kadhalika na sisi, tulipokuwa watoto,
tulikuwa tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia.
Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma
Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa
chini ya sheria, kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya
sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana. Na kwa
kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa
UHURU WA KWELI 250
Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba” [Gal
4:1-6]
Kabla hatujamjua Yesu Kristo tulikuwa kama watoto, lakini
Kristo alipokufa kwaajili yetu alitufanya tuwe wana cheo
cha wana kilitupa nafasi ya kuwa warithi. Ili tuweze kuwa
wana nilazima tuwe na ufahamu kuhusu Yesu Kristo.
Ukiokoka unafanyika mwana ili uwe uanze kuwa mwana
halisi lazima uwe na ufahamu kupitia Yesu Kristo (Efe 4:13).
Kumbe unaweza kuwa mtoto mchanga katika Kristo pia
unaweza kuwa mwana katika Kristo. Mtoto mchanga katika
Kristo ni yule aliye katika Kristo (aliyeokoka) lakini hajui haki
zake kupitia Yesu Kristo. Mwana katika Kristo ni yule
aliyekatika Kristo (aliyeokoka) na anajua haki zake katika
Yesu Kristo. Ndio maana Paulo aliwaambia Wakorintho;
“Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama
na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye
tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo.
Naliwanywesha maziwa sikuwalisha chakula; kwa kuwa
mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi, kwa
maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana,
ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya
mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?”
[1Kor 3:1-3]
UHURU WA KWELI 251
Wakorintho walikuwa ni watu wa tabia za mwilini, akili ya
mwilini ndio maana Paulo aliwaambia kama kwenu kuna
fitina ninyi si watu wa mwilini? Ndio maana mnaenenda
kwa jinsi ya kibinadamu, ndio maana Paulo aliwaambia
Waefeso wazidi kumfahamu sana Mwana wa Mungu. Ili
waweze kufikia kimo na utimilifu wa Kristo (Efe 4:13),
kwasababu alijua bila kumfahamu sana Mwana wa Mungu
ni rahisi kutekwa na mapokeo ya wanadamu. Ndio maana
Paulo aliwaambia Wakolosai;
“Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure
na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya
wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya
ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo” [Kol 2:8]
“Ee Timotheo, ilinde hiyo amana; ujiepushe na maneno
yasiyo ya dini, yasiyo na maana, na mshindano ya elimu
iitwayo elimu kwa uongo; ambayo wengine wanaikiri hiyo
wameikosa Imani. Neema na iwe pamoja nanyi” [1Timo
6:21]
Kwa hiyo, kumbe kuna mafundisho yanayofundishwa kwa
mapokeo ya wanadamu na mengine ni yale yanafundishwa
kwa jinsi ya Kristo. Mafundisho yanayoweza kukukuza
kufikia kimo na utimilifu wa Kristo ni yale yanayofundishwa
UHURU WA KWELI 252
kwa jinsi ya Kristo na sio mapokeo. Ndio maana maandiko
yansema tunatakiwa kumjua sana Mwana wa Mungu ili
tufikie kimo na utimilifu wa Kristo ili tusiwe watoto
wachanga. Tukitupwa huku na huku na kuchukuliwa na kila
upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukifuata njia
za udanganyifu (Efe 4:14).
Ndio maana Paulo alimsisitiza motto wake Timotheo kuwa;
mtu yoyote akifundisha elimu nyingine, wala hayakubali
maneno yenye uzima wa Bwana wetu Yesu Kristo. Wala
mafundisho yenye utauwa basi mtu huyo hafahamu neno
lolote (1Tim 6:3-4). Ndio maana akamkumbusha kuwa kwa
sababu ya watu kusikiliza elimu ya mapokeo, elimu isiyo ya
Kristo. Ndio maana Paulo alimsihi Timotheo alipokuwa
anakwenda Makedonia. Awakataze wengine wasifundishe
elimu nyingine na wala wasiangalie hadithi zisio na ukomo
ambazo hazileti imani katika Mungu (1Timo 1:3-4).
Tumefanyika kuwa wana wa Mungu kupitia kifo cha Yesu
Kristo pale msalabani.
“Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti
ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini
ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya
urithi wa milele. Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo
mauti yake aliyelifanya. Kwa maana agano la urithi lina
UHURU WA KWELI 253
nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu
kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya” [Ebr 9: 15-17]
Kupitia kifo cha Yesu Kristo pale msalabani tulifanyika
warithi kupitia ile mauti yake na kuingizwa kwenye agano la
urithi wa kila alichokifanya Yesu Kristo kwaajili yetu.
Tunatakiwa kukiri wakati wote kwenye maisha yetu kuwa ni
warithi halali kupitia agano la kifo alilolifanya Yesu Kristo
pale msalabani.
Nitakiri mimi ni mfalme.
“macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito
wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika
watakatifu jinsi ulivyo; na ubora wa ukuu wa uweza wake
ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa
nguvu za uweza wake; aliotenda katika Kristo alipomfufua
katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika
ulimwengu wa roho; juu sana kuliko ufalme wote, na
mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala
si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia” [Efe 1:18-
21]
“Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye
katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu” [Efe 2:6]
UHURU WA KWELI 254
Sisi tuaminio tulifufuliwa pamoja na Kristo, tukaketishwa
katika ulimwengu wa roho na kuwekwa juu sana kuliko
ufalme wote, mamlaka, nguvu na usultani.
Tumefanyikakuwa wafalme kupitia kufa kwake na
kufufuliwa kwake.
Kifo cha Yesu msalabani ilikuwa ni mwanzo wa kutawala
kwetu tunayemwamini.
“Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema,
imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake” [Yoh
19:30]
Biblia inaposema roho yake biblia ya kigiriki imetumia
maneno “ekpneo” na ekpsucho”. Maana yake kutoa pumzi
nje. Baada ya Yesu kutoa pumzi nje alipumzika.Yesu
alipopumzika ndiko tunapotakiwa kuanzia. Maandiko
yanasema;
“Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu
yake, na kutufanya kuwa ufalme, makuhani kwa Mungu
naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una yeye hata milele na
milele.Amina” [Ufu 1:5b-6]
KJV anasema tulifanywa kuwa wafalme. Yaani kupitia damu
ya Yesu Kristo tulifanywa kuwa wafalme. Kama ni hivyobasi
tunatakiwa kukiri kila wakati kuwa sisi ni wafalme kupitia
UHURU WA KWELI 255
Yesu Kristo. Kifo cha Yesu Kristo msalabani ilikuwa ni
mwanzo wakutawala, alipopumzika, ulikuwa ni mwanzo wa
kutawala kwetu. Mfalme mara zote huwa ni mtu
aliyepumzika, hana msongo wa mawazo, hapambani,wala
hana mashaka lakini kila anachokitaka anakipata. Sio kwa
sababu anatafuta ila kwa sababu ya nafasi yake kinachompa
nafasi hiyo ni kiti alichokalia cha ufalme. Watu wengine
watamtumikia, au mazingira ili mradi apate anachokitaka
hiyo ndiyo kanuni ya mfalme. Unahitaji kutambua kuwa
wewe ni mfalme katika Kristo Yesu.
Mfalme:- Ni mtawala katika nchi huru inayojitegemea,
asiyechaguliwa na mtu yoyote, anayerithi nafasi kwa njia
ya uzo halali.
Mungu alitufanya kuwa wafalme halali kwa uzao kipitia
Yesu Kristo kwa njia ya kurithi ambaye ni uzao wa
kifalme.Ndio maana imeandikwa;
“Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa
takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza
fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika
nuru yake ya ajabu” [1Pet 2:9]
UHURU WA KWELI 256
Tabia za mfalme;
Anatoa amri
Ni mtu wa maamuzi
Anaishi kwa uadilifu
Anaunda na kuhamasisha ubunifu kwa wengine
Anaacha urithi kwa wengine
Anabariki maisha ya wengine
Nitakiri mimi ni mfalme katika Kristo Yesu kila wakati.
Nitakiri mimi nimeponywa
Isaya alitabiri kabla ya Yesu kufa msalsabani kuwa;
“Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa
maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na
kwa kupigwa kwake sisi tumepona” [Isa 53:5]
Petro aliandika katika Waraka wake wa kwanza kuwa;
“Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili
wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe
hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake
mliponywa” [1Pet 2:24]
UHURU WA KWELI 257
Yesu Kristo kwa kupigwa kwake tuliponywa, na adhabu ya
amani ya Yesu Kristo ilikuwa juu yake. Alibeba dhambi zetu
na kuachilia haki kwaajili yetu, haki ya uponyaji ni mali yetu
kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. Yesu alipopigwa
mijeledi tulikuwako ndani yake na kwa kupigwa kwake sisi
tukahesabiwa kuwa ni wazima. Hatuna haja ya kujiumiza
tena kwa sababu sadaka ilikwisha kutolewa (sadaka ya
Mwana kondoo) ili kusudi tufanyike wazima.
Tunatakiwa kumla Yesu Kristo mwili wake akiwa
ameokwa na sio mbichi
Tuangalie maelekezo waliyopewa Wana wa Israeli kuhusu
kumla Mwanakondoo;
Bwana akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri,
akawaambia, Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi
kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu.
Semeni na mkutano wote wa Israeli, mkawaambie, Siku ya
kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana-kondoo, kwa
hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana-kondoo kwa watu
wa nyumba moja; na ikiwa watu wa nyumba ni wachache
kwa mwana-kondoo, basi yeye na jirani yake aliye karibu na
nyumba yake na watwae mwana-kondoo mmoja, kwa
kadiri ya hesabu ya watu; kwa kadiri ya ulaji wa kila mtu,
UHURU WA KWELI 258
ndivyo mtakavyofanya hesabu yenu kwa yule mwana-
kondoo.
Mwana-kondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka
mmoja; mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi. Nanyi
mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule; na
kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni. Nao
watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo
miwili na katika kizingiti cha juu, katika zile nyumba
watakazomla. Watakula nyama yake usiku ule ule,
imeokwa motoni, pamoja na mkate usiotiwa chachu; tena
pamoja na mboga zenye uchungu.
Msiile mbichi, wala ya kutokoswa majini, bali imeokwa
motoni; kichwa chake pamoja na miguu yake, na nyama
zake za ndani. Wala msisaze kitu chake cho chote hata
asubuhi, bali kitu kitakachosalia hata asubuhi mtakichoma
kwa moto. Tena mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa viuno
vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu
mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya
Bwana. Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami
nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri,
wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu
juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana.
Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba
mtakazokuwamo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu
yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu, nitakapoipiga
UHURU WA KWELI 259
nchi ya Misri. Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu, nanyi
mtaifanya iwe sikukuu kwa Bwana; mtaifanya iwe sikukuu
katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele [Kut 12:1-14]
Wana wa Israeli walipewa maelekezo ya kumla
Mwanakondoo akiwa ameokwa motoni. Pamoja na kichwa
chake, miguu yake na nyama zake za ndani. Wana wa Israeli
waliambiwa wasisaze kitu chochote. Wana wa Israeli
ilikuwa inawakilisha aliyeamini (aliyeokoka),
Mwanakondoo alikuwa anamuwakilisha Yesu Kristo. Wana
Wa Israeli waliambiwa wamle mwanakondoo akiwa
ameokwa pamoja na kichwa chake, miguu yake na nyama
za ndani. Alikuwa anazungumziwa Yesu Kristo kuwa
unatakiwa kumuangalia Kristo msalabani akiwa
amehukumiwa kwa ghadhabu kuu. Akiwa ameteseka kwa
kiwango cha mwisho kwaajili yako, na kwa namna hiyo
ukiona hivyo uzima utakuwa unaachiliwa kuanzia kichwani.
Kama unamatatizo au ugonjwa wa ubongo, miguuni kama
unamatatizo ya miguuni, nyama za ndani NIV amesema
viungo vya ndani. Maana yake maini, figo, mapafu, moyo,
kongosho, utumbo, tumbo, bandama. Vyote utaponywa
kwa kuangalia adhabu na mateso makuu aliponing’inizwa
pale msalabani. Kama wana wa Israeli walivyopewa
maelekezo ya kula kila kitu akiwa ameokwa. Na sisi pia
tunatakiwa kumla Yesu Kristo kila kitu, na utakapokuwa na
ugonjwa wa kichwa, miguu, viuongo vya ndani. Yaani iwe ni
UHURU WA KWELI 260
figo, mapafu, moyo, kongosho, utumbo, tumbo, bandama
vyote vitaponywa kupitia adhabu aliyoipata Yesu Kristo
msalabani.
Wakati mwingine umeshindwa kupona sio kwasababu
haujaponywa ila kwa sababu hujajua Yesu Kristo
alichofanya kwaajili yako. Ukimtazama Yesu Kristo halisi na
mateso yake huhitaji kujiumiza wewe ili uponywe kwa
imani tu. Utaanza kuona ugonjwa uliokamata kongosho
yaani kisukari, uwe ni ugonjwa wa moyo yaani shinikizo la
damu, iwe ni kansa ya ini, iwe ni kansa ya mapafu. Kupitia
Yesu Kristo uponyaji utaachiliwa tena sasa hivi, unahitaji
kumwamini Yesu Kristo kikamilifu ili upokee uponyaji wako
sasa. Kiri kuanzia sasa kwa kupigwa kwa Yesu Kristo
uliponywa. Ameni haleluya!
Nitakiri mimi ni mshindi.
Sasa tumebakiwa kukiri kuwa ni washindi, tulishapiganiwa
na Mungu vita zote zinazohusu maisha yetu. Ndio maana
Daudi alimwambia Goliati hivi;
“Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana
haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya
Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu” [1Samw
17:47]
UHURU WA KWELI 261
Kama Daudi alikuwa katika kipindi cha agano la kale alikiri
kuwa vita si vyake ni vya Bwana. Maana yake aliamini yeye
mwenyewe hawezi kupigana akashinda bali Bwana
anaweza kumpigania akashinda. Daudi alimshinda yule
mfilisti (Goliati) kwa sababu Bwana alimpigania je si zaidi
sana wewe uliye katika agano jipya? Habari njema hi hii
kwamba; wewe uliye katika agano jipya ulishapiganiwa
tayari na Yesu Kristo. Na ulishashinda miaka elfu mbili
iliyopita. Wewe unatakiwa kuamini kuwa ulishashinda na
kukiri ushindi ulionao. Paulo anathibitisha hili
alipowaandikia Warumi;
“Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki
au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?
Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya
kushinda, kwa yeye aliyetupenda” [Rum 8:35, 37]
Kumbe tulishashinda katika yeye kiri kuwa wewe ni mshindi
wakati wote kwenye maisha yako. Bila kujali unanjaa au
umeshiba, bila kujaliunadhiki au la, bila kujali upo kwenye
hatari au upanga. Kiri mimi ni mshindi, Ameni Haleluya!
UHURU WA KWELI 262
Tathmini kupitia maswali kutoka katika Sura ya Kumi
1: Kwanini tunatakiwa kukiri kwa mdomo wakati wote
tuliyokirimiwa katika Kristo Yesu?
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
……………………………………
2: Taaja maana yam domo kwa kigiriki
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………...
3: Taja maeneo matano tunayotakiwa kukiri wakati wote
katika Kristo Yesu
(i)………………………………………………………………………………………
…………………………………………
(ii)………………………………………………………………………………………
……………………………………....
(iii)……………………………………………………………………………………
…………………………………………
UHURU WA KWELI 263
(iv)……………………………………………………………………………………
………………………………………….
(v)………………………………………………………………………………………
……………………………………….
UHURU WA KWELI 265
HITIMISHO
ujua wewe ni nani katika Yesu Kristo ni muhimu sana,
ili uweze kuanza kuona udhihirisho wa uhalisia ulio nao.
Ukijua haki zako katika Kristo Yesu sio rahisi kuishi
maisha yasiyo na haki. Kujua baraka zako, utakatifu, imani
na utimilifu ni muhimu sana. Kuanzia sasa nakushauri
kuambatana na injili ya neema ya Kristo. Maana hii ndiyo
injili ambayo Bwana Yesu alitutuma tuihubiri kwa mataifa
yote, na ndiyo injili inayokujulisha wewe ni nani katika Yesu
Kristo. Biblia imeandika kuwa;
“Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema imekwisha.
Akainama kichwa akaisalimu royo yake” [Yoh 19:30]
Kama Yesu Kristo alisema imekwisha pale msalabani. Basi
ujue alimaliza kila kitu kinachohusiana na maisha yetu pale
msalabani na uwe na uhakika hakuna kitu ambacho Yesu
Kristo hakufanya kinachohusiana na maisha yako. Kama ni
hivyo basi hali tukijua hivyo hatuna sababu ya kujitafutia
mambo yetu wenyewe. Muhimu ni kuwa tujitambue sisi ni
wa kina nani katika yeye. Ili tufurahie ile zawadi ya wokovu
kutoka kwake.
Tujue uhalisia wetu kupitia injili yake na neno lake Yesu
Kristo na kwa namna hiyo nakushauri kusoma vitabu
vinavyokusaidia kujua wewe ni nani katika Yesu Kristo.
K
UHURU WA KWELI 266
Sikiliza kwa wingi CD, nyimbo, mahubiri mafundisho
yanayokusaidia kujua wewe ni nani katika Yesu Kristo. Soma
sana vitabu vinavyokusaidia kujua wewe ni nani katika Yesu
Kristo. Kwa namna hiyo nafsi yako ikigeuzwa huku nje
kuuona uhalisia wako ndani ya Yesu Kristo haitakuwa shida.
Utaona uhalisia wako wa jinsi ulivyo katika Kristo Yesu. Zile
baraka zote ulizipokea katika Yesu Kristo, haki yako
uliyopewa zawadi, utakatifu na kutukuzwa utaanza
kuvishuhudia kwenye maisha yako halisi ya mwilini.
Natamani siku kuona ukishuhudia kuwa neno la Kristo
limebadilisha maisha yako kabisa na umekuwa hodari
katika Bwana. Bwana wa mbinguni amekubariki sana.
UHURU WA KWELI 267
KUHUSU MWANDISHI
araka Fredy Shibanda ni Mtumishi wa Mungu ambaye
Mungu amempa huduma ya Uinjilisti na Ualimu.
Alihitimu kidato cha nne mwaka 2013 katika shule ya
Sekondari Chanji iliyoko mkoa wa Rukwa-Tanzania. Baada
ya hapo mnamo mwaka 2014-2016 alifanikiwa kuchaguliwa
kujiunga na masomo ya kidato cha tano na sita katika Shule
ya wavulana Songea (Songea boys). Iliyoko Mkoa wa
Ruvuma, wilaya ya Songea, Tanzania.
Baada ya hapo alifanikiwa kujiunga na masomo katika chuo
kikuu cha Dodoma (UDOM), Dodoma-Tanzania. Kuanzia
mwaka 2016 mpaka mwaka 2019 alifanikiwa alihitimu
masomo yake ya Stahahada katika utaalamu wa maabara
ya afya.
Baraka Fredy Shibanda pia ni mwanzilishi na kiongozi mkuu
wa huduma ya Udhihirisho wa Mungu (Godly Power
Manifestastion Ministry) [GPM]. Aliyoianzisha mnamo
mwaka 2017, inayolenga kuhubiri injili na kufundisha neno
la Kristo katika nchi ya Tanzania na duniani kote. Huduma
hii inaendeshwa na misheni kutoka kitabu cha Matendo ya
Mitume Sura ya kwanza mstari wa nane. Inayosema,
“Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho
Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika
B
UHURU WA KWELI 268
Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata
mwisho wa nchi”
Pia huduma hii imekuwa ikiwatunza watoto yatima na kila
wenye uhitaji angalau mara moja kwa mwaka. Kufanya
mikutano na semina za mara kwa mara ili kuweza kuifikishia
dunia habari njema. Kuanzia Tanzania, nje ya nchi na
duniani kote kwa watu wote waliookoka na wasiookoka.
Pia ni Mwinjilisti na Mwalimu.
Anapatikana katika mitandao ya kijamii ifuatayo:-
YouTube: GPM Ministry
Facebook: Evangelist and Teacher Baraka Shibanda
Twitter: Evangelist and Teacher Baraka Shibanda
Instagram: Evangelist and Teacher Baraka Shibanda