Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

263
1 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA TATU Kikao cha Tano - Tarehe 4 Novemba, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, maswali, tunaanza na Ofisi ya Waziri Mkuu, atakayeuliza swali la kwanza ni Mheshimiwa Gaudence Kayombo, kwa niaba yake naona Mheshimiwa Mwambalaswa unaweza kumwulizia! Na. 53 Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbinga Kuwa Mamlaka Kamili MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA (K.n.y. MHE. GAUDENCE C. KAYOMBO) aliuza:- Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbinga umekamilisha vigezo vyote kuwa Mamlaka kamili ya Mji:- Je, ni lini Serikali itaridhia na kutekeleza ahadi hiyo ya Mheshimiwa Rais? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Gaudence C. Kayombo, Mbunge wa Mbinga Mashariki, kama ifuatavyo:-

Transcript of Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

1

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

BUNGE LA TANZANIA_______________

MAJADILIANO YA BUNGE_______________

MKUTANO WA KUMI NA TATU

Kikao cha Tano - Tarehe 4 Novemba, 2013

(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua

MASWALI NA MAJIBU

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, maswali, tunaanzana Ofisi ya Waziri Mkuu, atakayeuliza swali la kwanza niMheshimiwa Gaudence Kayombo, kwa niaba yake naonaMheshimiwa Mwambalaswa unaweza kumwulizia!

Na. 53

Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbinga Kuwa Mamlaka Kamili

MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA (K.n.y. MHE.GAUDENCE C. KAYOMBO) aliuza:-

Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbinga umekamilishavigezo vyote kuwa Mamlaka kamili ya Mji:-

Je, ni lini Serikali itaridhia na kutekeleza ahadi hiyoya Mheshimiwa Rais?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALAZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali laMheshimiwa Gaudence C. Kayombo, Mbunge wa MbingaMashariki, kama ifuatavyo:-

2

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba, mwaka 2010,Mheshimiwa Rais, aliahidi kupandisha hadhi Mamlaka yaMji Mdogo wa Mbinga kuwa Halmashauri ya Mji. Ahadi hiiilitokana na ukweli kwamba, Mamlaka hii imeonekanakukua kwa kasi, kwa maana ya ongezeko la watu nashughuli za kiuchumi na kijamii na hivyo Serikali inaona ipohaja ya kuipandisha hadhi ili kuingiza dhana ya MpangoMiji kwa lengo la kuzuia ukuaji holela, kuchochea ukuaji wauchumi na kuboresha huduma za jamii.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, mchakato wakuupandisha hadhi Mji wa Mbinga bado unaendelea naofisi yangu bado haijapokea maombi kutoka Mkoa waRuvuma. Tunamwomba Mheshimiwa Mbunge, ashirikianena Uongozi wa Mkoa il i kuharakisha mchakato wakuupandisha hadhi Mji wa Mbinga. (Makofi)

MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA: Mheshimiwa Spika,ninashukuru sana kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri.Pamoja na hayo nina swali dogo la nyongeza.

Kwa kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mbinga,inafanana kabisa na Mamlaka ya Mji Mdogo waMakongorosi Wilayani Chunya, ambayo nayo upo katikamchakato wa kuwa Mji Mdogo kamili, kufuatana na ahadiza Mheshimiwa Rais:-

Je, ni lini Serikali itakamilisha kuipa Mamlaka kamiliMamlaka ya Mji Mdogo wa Makongorosi?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALAZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): MheshimiwaSpika, napenda kujibu swali la nyongeza la MheshimiwaVictor Mwambalaswa, kama ifuatavyo:-

Mchakato wa kufanya Mji wowote kuwaHalmashauri ya Mji au kugawanywa kwa Wilaya au Kata,kwa kiasi kikubwa kunategemea Mamlaka za Serikali zaMitaa zenyewe, Halmashauri, Mkoa pamoja na Ofisi yaWaziri Mkuu. Kwa hiyo, kwa sasa hivi sina nafasi ya kuweza

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (TAMISEMI)]

3

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kusema ni lini, kwa sababu bado mchakato huo katikangazi ya Mkoa wa Mbeya haujakamilika na kuletwa katikaOfisi yetu.

MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongezakama ifuatavyo:-

Kwa kuwa pia katika Halmashauri ya Wilaya yaNamtumbo katika Tarafa ya Sasawara, Kata ya Lusewa,tuliomba Mji Mdogo Serikalini. Vigezo vyote tumeshatimizana maombi hayo yapo katika Ofisi ya TAMISEMI:-

Je, Serikali imefikia wapi kutamka rasmi mamlaka yaMji Mdogo Kata ya Lusewa?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALAZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): MheshimiwaSpika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa VitaKawawa, Mbunge wa Namtumbo, kama ifuatavyo:-

Napenda nimhakikishie kwamba, litakapokuwatayari suala lake tutalishughulikia, lakini mpakaninavyozungumza, suala linalohusu Mji wa Lusewa halijafikamezani kwangu. Kwa hiyo sina uhakika kama kwelililishatoka katika Mkoa wake. Ninachomwomba, tukitokatuwasiliane ili tuone na tuweze kujua limefikia wapi aulimekwama wapi.

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tuendelee,kwanza miji inazidi kuongezeka. Sasa twende kwaMheshimwia Moses Machali, swali linalofuata.

MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Spika, kablaya kujibiwa kwa swali langu, ningependa niwafahamisheWananchi pamoja na Waheshimiwa Wabunge, juu ya haliya Mheshimiwa Dkt. Mvungi; ni kwamba, nimetaarifiwa naMheshimiwa Mbatia, ambaye yuko Hospitali ya Muhimbilikuwa, anaendelea vizuri na Madaktari wanajitahidi kuweza

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (TAMISEMI)]

4

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kupigania afya yake. Kwa hiyo, waondoe wasiwasi, naaminiatapona.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo haya mafupi,naomba swali langu namba 54 lipatiwe majibu. Ahsante.

Na. 54

Uhitaji wa Watumishi Katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu

MHE. MOSES J. MACHALI aliuliza:-

Wastani wa Watumishi wa Afya katika Hospitali yaWilaya ya Kasulu ni 600 lakini kwa mujibu wa Taarifa ya DMOwatumishi waliopo sasa ni 186 ambao ni wachache sana:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza watumishikwenye Hospitali hiyo?

SPIKA: Pamoja na taarifa nzuri, lakini siyo utaratibu.Mheshimiwa Waziri wa Nchi, majibu!

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALAZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali laMheshimiwa Moses J. Machali, Mbunge wa Kasulu Mjini,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua upungufu waWatumishi wa Sekta ya Afya Nchini. Hivyo basi, iliona nivyema kuwa na mkakati maalum wa kuajiri wahitimu wotewanaomaliza Vyuo Vikuu vya Afya.

Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Kasulukwa sasa ina jumla ya watumishi 359 wa kada mbalimbaliza afya, wakiwemo Madaktari na Wauguzi, ambaowanatoa huduma za afya kwenye Wilaya ya Kasulu.Hospitali ya Wilaya ina watumishi 206, Vituo vya Afya vina

[MHE. M. J. MACHALI]

5

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

jumla ya watumishi 52 na Zahanati zina jumla ya watumishi101.

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia umuhimu wawatumishi wa kada za afya, katika Mwaka wa Fedha wa2012/13, Serikali ilitoa kibali cha kuajiri watumishi 41 wa Sektaya Afya, ambapo hadi mwezi Oktoba, 2013 jumla yawatumishi 28 wa kada za afya wamesharipoti katikaHalmashauri ya Wilaya ya Kasulu.

Mheshimiwa Spika, Serikali inao mkakati wakuhakikisha kuwa inadahili wanafunzi wengi katika Vyuo vyaAfya pamoja na kuwalipia wanafunzi hao kupitia Bodi yaMikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu. Aidha, Serikalihuwapanga watumishi wote wa Sekta ya Afya moja kwamoja katika Halmashauri kadiri wanavyohitimu mafunzokatika vyuo. Serikali itaendelea kuajir i wataalamumbalimbali wa kada za afya kadiri watakavyokuwawakihitimu mafunzo na kufaulu ili kuondokana na upungufumkubwa wa kada hiyo muhimu.

MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize maswali mawili yanyongeza:-

(i) Kwa kuwa katika Hospitali ya Wilaya yaKasulu inaonekana tuna-shortage kubwa sana yaMadaktari hasa Medical Doctors, walikuwa wawili lakiniwengine wamepelekwa kwenye Wilaya Mpya; na kwa kuwamadaktari walioko pale wakati mwingine wanaachakuomba madaktari wa kutosha kutoka katika Wizara yaAfya kwa lengo la kutaka kulinda nafasi zao. Je, Serikaliitakuwa tayari kutupatia Madaktari wa kutosha ikiwa kamani ombi maalum ili kuweza kuziba pengo lililopo hivi sasa?

(ii) Katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu zipochangamoto nyingi kama ukosefu wa madawa wakatimwingine na hii inatokana na uzembe na vitendo vya wiziwakati mwingine; vimetokea na vingine tumewezakudhihirisha. Wakati wa Bunge la Bajeti, niliomba special

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (TAMISEMI)]

6

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

audit ya kuja kufanya ukaguzi kwenye Hospitali ya Wilaya,lakini ahadi zilitolewa kwamba, watafanya na hakunaambacho kimefanyika mpaka leo hii, gharama za matibabuzimepandishwa. Je, Serikali itakuwa tayari kupitia Wizaraya TAMISEMI pamoja na Wizara ya Afya, kuweza kutupatiaile timu ambayo niliomba hapa Bungeni na mkaahidikwamba mtaleta ili twende tukafanye special audit?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALAZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): MheshimiwaSpika, napenda kujibu maswali ya nyongeza ya MheshimiwaMachali, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, suala la kwanza kwamba,madaktari hawaombi madaktari wenzao kwa kulinda vyeovyao, sidhani kwa sababu uchache ule unawaongezeawao mzigo mkubwa wa kufanya kazi. Katika hali yakawaida, sidhani kama kuna daktari ambaye angependaafanye kazi za madaktari sita peke yake; kwa sababu badoatapokea mshahara mmoja na bado marupurupu yakeyatabaki vilevile, hawezi kupokea ya madaktari ambaohawapo.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, suala la kuombaikama siyo la madaktari wenyewe ni la Halmashauri.Napenda nikuhahakikishie kwamba, Wizara ya Afya naTAMISEMI, wote tunashiriki katika kuhakikisha kwamba,tunapeleka watumishi katika Halmashauri kwa mujibu waikama na kwa jinsi wanavyopatikana katika soko la ajira.

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la Special Audit,sasa hivi ipo timu kule Kasulu ambayo inafuatilia masualambalimbali ya matumizi ya fedha na matumizi ya madarakakatika Mji wa Kasulu.

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo lanyongeza.

[MHE. M. J. MACHALI]

7

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Kwa kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mpandaimegawanywa na kutoka Halmashauri ya Wilaya Nsimbona Halmashauri ya Mji Mpya wa Mlele; na wote haowamekuwa wakichukua wafanyakazi kutoka HalmashauriMama ya Wilaya ya Mpanda na kufanya tatizo kuwakubwa sana la ukosefu wa Madaktari katika Halmashauriya Wilaya:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuleta watumishiwa kada ya afya kwenye Hospitali ya Wilaya ya Mpandasambamba na Vituo vya Afya ambavyo kimsingi katikamaeneo yote hata yaliyogawanywa bado kuna tatizo laukosefu wa Madaktari? Serikali inaleta lini madkatari hao?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALAZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): MheshimiwaSpika, napenda kujibu swali la nyongeza la MheshimiwaKakosi, kama ifuatavyo:-

Kuhusu suala la kupeleka Madaktari katikaHalmashauri mpya na Halmashauri nyingine, napendanimhakikishie kwamba, mara tu wahitimu wa kada ya afyawatakapokuwa wamemaliza na tutakapokuwatunapanga, maeneo mapya tutawapa kipaumbele chapekee, kuhakikisha tunapunguza tatizo la upungufu wawatumishi.

MHE. EZEKIA D. WENJE: Mheshimiwa Spika, ni kwelikwamba, nchi nzima maeneo mengi kuna matatizo yaupungufu wa Madaktari. Kuna maeneo mengi yenye vyuo,kwa mfano, Mwanza kuna Chuo cha Bugando na Bukumbi.Sasa kwa nini Serikali isitoe agizo kwa Halmashauri zote nchinizifanye jitihada binafsi za ku-partner na vile vyuo kwamkataba ili waweze ku-train watu wengi kwa mkatabawaende kufanya kazi kwenye hizi Halmashauri? Kwa niniSerikali isitoe agizo sasa Halmasahuri zote zifanye jitihadabinafsi za ku-partner na hivyo vyuo kwa mkataba wapatewatumishi?

[MHE. M. S. KAKOSO]

8

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALAZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): MheshimiwaSpika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ezekiah Wenje,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyotangulia kusemakwamba, tunao mkakati wa kuhakikisha tunaondoa tatizohilo na sasa hivi ninavyozungumza tunavyo vyuo vingitumevianzisha na vingine tumevifufua. Sasa kusemaHalmashauri tuziagize zikasomeshe, mimi nadhani kidogoitakuwa ngumu, kwa sababu tatizo siyo uwezo wa Serikalikusomesha, tatizo ni nafasi katika vyuo hivyo. Labdaniziombe Halmashauri ambazo zipo jirani na maeneo hayo,kama zinao uwezo wa kutusaidia kutujengea mabweni navyumba vya madarasa, nadhani hilo litakuwa ni la busarana tutawawezesha Halmashaxuri hizo, zikijenga ambazovyuo vipo katika maeneo yao, tutawapa upendeleo kwaajili ya udahili wa wanafunzi kutoka maeneo yao, ambaowatamaliza na kufanya kazi katika maeneo yao.

Na. 55

Uwiano Katika Mpango wa Rasilimali Fedha

MHE. SYLVESTER M. MABUMBA aliuliza:-

Tanzania ni moja kati ya Mataifa ambayowalijiwekea mikakati ili kutekeleza ipasavyo Malengo yaMilenia (MDGs); na kwa kuwa bado miaka miwili kufikiamwaka 2015:-

(a) Je, ni mikakati gani Taifa l imejiwekeakuhakikisha kwamba rasilimali za Taifa zinagawiwa kwauwiano ili kuliwezesha Taifa letu kuendelea kuwa moja?

(b) Je, baada ya 2015, Taifa linajiandaajekuhakikisha kuwa uchumi wake unakua kwa maana yaGDP; na kubadilika kutoka uchumi wa sasa na kuwa Taifalenye uchumi wa kati?

9

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NAURATIBU) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali laMheshimiwa Sylvester M. Mabumba, Mbunge wa Dole,lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, kuna vigezo mbalimbalivinavyotumika katika kuhakikisha kuwa, rasilimali za Taifazinagawiwa kwa uwiano katika maeneo mbalimbali nchini.Vigezo hivyo ni pamoja na idadi ya watu, vipaumbvelevya Taifa na mazingira halisi kama vile maeneo yapembezoni ambayo hayafikiki kwa urahisi au jamiii zinazoishikwa kahamahama kufuata malisho ya mifugo.

Mheshimiwa Spika, mgawanyo wa rasilimali za Taifahugawanywa kwa kufuata maeneo makubwa yafuatayo:-

(i) Rasilimali zinazotengwa kwa ajili ya Miradi yaKitaifa ambayo matokeo yake huwanufaisha Wananchiwote. Miradi ya aina hiyo ni kama vile miradi ya uzalishajiwa umeme ambao kwa kuboresha uchumi, kila mwananchiananufaika.

(ii) Eneo lingine ni la Miradi ya Kitaifa ambayoinasaidia kuondoa vikwazo vya kiuchumi kama vilemiundombinu. Aina hii ya Miradi ni kama vile reli, barabara,bandari na viwanja vya ndege. Kwa kuzingatia mazingirahalisi kama vile maeneo ya pembezoni ambayo hayafikikikwa urahisi, Miradi ya aina hii hugharimiwa Kitaifa, kwa ajiliya kukwamua maeneo husika. Miradi kama vile barabarazinazounganisha Mikoa na ujenzi wa miundombinu ya msingiinayopunguza gharama za uzalishaji na kufanya biashara,ni mifano mizuri ya Miradi hii. Aidha, Miradi hii pia huvutiauwekezaji wa sekta binafsi pamoja na kuunganisha masokona kuwezesha Wananchi kuongeza kipato na kujiajiri katikashughuli mbalimbali za uzalishaji.

(iii) Kwa upande wa Halmashauri za Wilaya, Mijina Majij i, fedha za maendeleo, zinagawanywa kwa

10

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kuzingatia vigezo, kama vile idadi ya watu, ukubwa waeneo, vifo vya watoto chini ya miaka mitano, kiwangocha umaskini, umbali wa kupata huduma za kijamii hasaelimu, afya na maji. Vigezo hivi vinatumika kuhakikisharasilimali za Taifa zinagawanywa siyo tu kwa uwiano mzuri,bali pia kupunguza tofauti za maendeleo baina ya maeneohusika.

(iv) Sheria na Kanuni zinazoongoza matumizi yarasilimali za pamoja hususan ardhi, maji na misitu zinatumikakuhakikisha manufaa kwa Taifa zima na kwa namnaambayo ni endelevu.

(b) Mheshimiwa Spika, Tanzania ni miongoni mwaMataifa 189 yaliyoridhia Malengo la Maendeleo ya Milenia(MDGs - 2015). Majadiliano ya Kitaifa yaliyoendeshwa naChuo Kikuu cha Dar es Salaam na ESRF mapema mwakahuu, kwa niaba ya Tume ya Mipango, yamebainishaumuhimu wa kuendelea kutekeleza MDGs baada yamwaka 2015, pamoja na kutoa msukumo zaidi katika uborawa elimu, tija katika sekta za uzalishaji, usimamizi makiniwa rasilimali za nchi na kuimarisha mafanikio yaliyofikiwakatika utekelezaji wa MDGs. Ili kuhakikisha ukuaji wa GDPunaongezeka ili nchi ifikie hadhi ya nchi ya kipato cha katimwaka 2025; Serikali itajielekeza kutekeleza Mpango Elekeziwa miaka mitano mitano kati ya miaka 15, ambaounatekelezwa kupitia mipango ya miaka mitano mitano.Lengo ni kuongeza uwekezaji katika maeneo ya kimkakatihasa miundombinu ya nishati na usafirishaji; ki l imo;maendeleo ya viwanda; maendeleo ya rasilimali watu naujuzi; na uendelezaji wa huduma za utalii, biashara na fedha.

MHE. SYLVESTER M. MABUMBA: Mheshimiwa Spika,nashukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri,naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza kamaifuatavyo:-

(i) Kwa kuwa Mheshimiwa Waziri ameelezakwamba, rasil imali zetu hugawiwa kwa kuzingatiavipaumbele vya Kitaifa, maeneo ya pembezoni na hali za

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU)]

11

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kimazingira. Je, vigezo hivi vimetumikaje katika kusaidiamaeneo ya Mikoa ya Lindi, Rukwa, Katavi, Shinyanga,Mwanza na Geita, ambayo kwa sasa bado inaonekana niMikoa ya pembezoni sana hata fursa za kimaendeleohazionekani?

(ii) Kwa kuwa ameelezea Mheshimiwa Wazirikwamba, Malengo ya Milenia baada ya mwaka 2015,tutaendelea kutekeleza tena. Ningependa kujua kwa sasaTanzania imefikia kiwango gani katika kutekeleza Malengohaya ya Milenia? Ahsante.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NAURATIBU): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawiliya nyongeza ya Mheshimiwa Sylvester M. Mabumba, kamaifuatavyo:-

Vipaumbele vya Kitaifa ambavyo vimesaidia katikakukwamua maendeleo ya pembezoni na Mikoa aliyoitajakama vile Rukwa, Kigoma, Mwanza na mahali pengine, nikama ifuatavyo:-

Nimesema katika jibu langu la msingi kwamba, eneoambalo linasaidia sana ni lile la miundombinu. Kwa mfano,katika Mkoa wa Rukwa, ambao kwa miaka mingi sanaulikuwa haupitiki na ingawa uzalishaji wake ni mkubwa, sasatunawekeza katika kutengeneza barabara ambazozitawawezesha Wananchi wa Rukwa, Kigoma na Ruvuma,kuweza kufikisha mazao yao sokoni. Kwa kweli bila kuwana miundombinu, hata kilimo hakiwezekani kwa sababuhawawezi kufika sokoni, kwa hiyo, wanalima kwa wingi lakinihawawezi kupata maendeleo makubwa. Kwa hiyo,tumewekeza miundombinu katika maeneo hayo. Mikoayote aliyoitaja, tunaifikia kwa njia ya barabara.

Vilevile tunatengeneza reli kwenda katika Mikoa yaKigoma, Mwanza na kadhalika. Siyo hivyo tu, lakini vilevileumeme ambao ni muhimu sana kwa ajili ya maendeleo,sasa unasambazwa katika maeneo yote. Katika mpangotulionao, tuna grid ambayo itaunganisha Mikoa ambayo

[MHE. S. M. MABUMBA]

12

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ilikuwa haijafikiwa, ikiwemo Rukwa, Kigoma, pamoja naRuvuma. Kwa hiyo, mipango hiyo itasaidia sana kupanuauchumi katika maeneo hayo na kuwezesha uwekezaji katikamaeneo hayo.

Kuhusu maeneo gani ambayo tumefanikiwa katikaMilenia, kwa kweli tumefanikiwa katika maeneo mengi; kwamfano, katika suala la kupunguza vifo vya watoto chini yamiaka mitano, kumekuwepo na maendeleo makubwa naupungufu wa vifo umekuwepo, ingawa tunapenda kuonaya kwamba, tunaendelea kupambana zaidi na jambo hili,kwa sababu hata akifa mtoto mmoja bado ni mtoto.

Yapo maeneo mengine; elimu kwa mfano, pamojana kwamba, tuna matatizo ya kuboresha elimu kutokanana upanuzi mkubwa, lakini watoto wengi sasa wanasomana moja ya Lengo la Milenia ilikuwa ni kuhakikisha watotowengi wanaingia shuleni. Yapo maeneo mengi, MheshimiwaMabumba, nitakupa maelezo zaidi wakati wowote ukihitajikuona kila kipengele cha Milenia tulichoweza kutekeleza.

MHE. KAIKA S. TELELE: Mheshimiwa Spika, ahsantekwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza.

Jirani zetu Kenya hapa kutokana na Katiba yaompya wameanzisha Mfuko wa kusaidia maeneo ambayoyamekuwa nyuma kwa maendeleo kwa muda mrefu,wanaita Equalization Fund. Je, Serikali haioni kwamba nimuhimu tukaiga jambo hili kutoka kwa jirani zetu kwasababu ni jambo la maendeleo? (Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NAURATIBU): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali moja lanyongeza kutoka kwa Mheshimiwa Mbunge waNgorongoro, kama ifuatavyo:-

Mimi nadhani ni jambo jema kujifunza mambo memakutoka popote. Kwa hiyo, kama Kenya wao wameanzishaMfuko wa namna ile, tutajifunza, tutausoma kwanza tujuemakusudio yake ni nini na unakusudia kusaidia vipi. Kwa

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU)]

13

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

hiyo, tunaweza vilevile tukajifunza kama tunavyojifunzakatika sehemu nyingine Duniani.

SPIKA: Ahsante. Naomba tuendelee Wizara yaKatiba na Sheria.

Na. 56

Jengo la Mahakama ya Mwanzo Kibaha

MHE. SILVESTRY F. KOKA aliuliza:-

Jengo la Mahakama ya Mwanzo kwenyeHalmashauri ya Mji wa Kibaha ni bovu kabisa:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Jengo jipyala Mahakama hiyo ili liweze kutoa huduma zake sawasawa?

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali laMheshimiwa Silvestry F. Koka, Mbunge wa Kibaha Mjini,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa kwamba, Jengola Mahakama ya Mwanzo Kibaha Maili Moja ni bovu. Hatahivyo, Serikali kwa mwaka huu wa fedha imetenga fedhakwa ajili ya ujenzi wa Jengo la Mahakama ya Mwanzo MailiMoja - Kibaha. Mpaka hivi sasa taratibu za kumpataMshauri Mwelekezi kwa ajili ya usimamizi wa ujenzi wa Jengohilo zinakamilishwa ili kuwezesha ujenzi huo kuanza maramoja.

Mheshimiwa Spika, ni mpango wa Serikali kujengamajengo mapya katika Mahakama zote ambazo majengoyake ni mabovu na chakavu. Hata hivyo, kutokana naufinyu wa bajeti uliopo, tutaendelea kujenga majengo yaMahakama kadiri hali ya fedha itakavyoruhusu.

SPIKA: Ahsante, Mahakama kweli.

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU)]

14

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. SILVESTRY F. KOKA: Mheshimiwa Spika, pamojana majibu mazuri ya Serikali, lakini ninayo maswali mawili yanyongeza.

(i) Katika Jengo la Mahakama ya Mkoa ndipohapo vilevile Mahakama ya Wilaya inafanya shughuli zake;na jambo hili limeleta mkanganyo na kuchelewesha kesikwa sababu vyumba vya Mahakimu kufanyia kazi hiihavitoshi; kwa maana sasa Mahakama ya Wilaya hainamajengo, lakini vilevile samani na vitendea kazi ni duni sana.Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kujenga Mahakamaya Wilaya na kuboresha vitendea kazi pamoja na samanikatika Jengo hilo?

(ii) Kumekuwa na malalamiko sana kwaWatumishi wa Mahakama kutokana na masilahi yaombalimbali ikiwa ni pamoja na fedha za sale, fedha kwaajili ya nyumba (In House Allowance) au kulipia mapango;jambo ambalo linawafanya waishi katika maeneo ambayoni hatarishi. Vilevile mazingira haya hufanya hata Idara yaMahakama kwa namna moja au nyingine, kujihusishakupokea rushwa na mambo mengine. Je, Serikali inampango gani kuhakikisha wanapata stahili zao ili kuboreshahuduma ya Mahakama?

SPIKA: Ahsante na wengine ulizeni maswali kwa kifupitafadhali. Mheshimiwa Naibu Waziri majibu!

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaSpika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza yaMheshimiwa Silvestry F. Koka, Mbunge wa Kibaha Mjini,kama ifuatavyo:-

Kwanza kabisa, kuhusiana na ujenzi wa Jengo laMahakama ya Wilaya ya Kibaha, napenda kumwarifuMheshimiwa Mbunge kwamba, katika mwaka huu wafedha, tutajenga Mahakama za Wilaya sita na Katika Mkoawa Pwani, Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo nimojawapo. Hali ya fedha ikiruhusu katika miaka inayokujatutaangalia uwezekano wa kujenga Jengo la Mahakama

15

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ya Wilaya ya Kibaha, lakini tunatambua changamotowalizonazo, kwa hiyo, hali ikiruhusu tutazingatia.

Kuhusiana na samani na vitendea kazi, tayaritumeshatangaza zabuni mbalimbali nchi nzima na pindizabuni hizo zitapokamilika, basi tutanunua vifaa mbalimbali,samani na vitendea kazi kwa ajili ya Mahakama hizo.

Swali la pili kuhusiana na masilahi ya Watumishi waMahakama na kwamba wengi wamekuwa wakijiingizakatika vitendo vya rushwa. Kwanza kabisa, napendakusema kwamba, rushwa ni adui wa haki. Nimekuwanikisisitiza mara kwa mara hapa kwamba, kama kunamtumishi katika Idara ya Mahakama, ambaye anaonahawezi kwendana na maadili ya Mhakama, basi ni vyemaapishe. (Makofi)

Napenda kurudia tena, lakini pia niombeWaheshimiwa Wabunge mtusaidie, kupitia Sheria ya JudicialService Act, Kifungu cha 40, kinaeleza kabisa kwamba,kuna Kamati mbalimbali za Maadili za kushughulikianidhamu na maadili za Mahakimu. Kwa upande waMahakama za Mwanzo, Mahakimu wa Mahakama zaMwanzo, nidhamu zao zinasimamiwa na DCs, lakini pianidhamu za Mahakimu wa Wilaya na Mkoa zinasimamiwana Wakuu wa Mikoa. Kwa hiyo, naomba na ninyi mtusaidiekufuatilia vikao hivi vya Kamati ya Maadili viweze kuketimara kwa mara ili wale wote wanaojishughulisha na vitendohivi vibovu, basi waweze kuchukuliwa hatua stahiki zakinidhamu.

Kuhusiana na masilahi, kwanza kabisa, katikamasuala ya posho za nyumba, tayari suala hili tunalitambuana tumeshaanza kulifanyia kazi. Tumeshaanza sasa hivikulipa Wasajili wote wa Mahakama na lengo letu nikuhakikisha kwamba, tunalipa watumishi wote waMahakama. Kuhusiana na sare, vilevile tayaritumeshawaagiza Wasajili wote Wafawidhi katika ngazi zaWilaya, kuhakikisha wanatuletea orodha ili sare ziwezekupatikana hukohuko waliko.

[NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA]

16

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Spika,ahsante sana. Naomba niiulize Serikali, kwa sababuimekuwa ahadi ya muda mrefu sana ya kujengaMahakama ya Mwanzo ya Nyamikoma iliyoko Kwimba.

(Hapa mlio wa simu ulisikika)

SPIKA: Nimeshaagiza simu zinafungwa.

MHE. RICHARD M. NDASSA: Tangu enzi za MamaNagu, Mheshimiwa Celina Kombani, akaja Chikawe One,akaja Chikawe Two, sasa naomba tuambiwe ni lini hasaSerikali itajenga Mahakama hiyo ya Mwanzo Nyamikoma?

SPIKA: Nani mwenye simu azime aliko! MheshimiwaNaibu Waziri majibu!

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaSpika, ahsante. Naomba kujibu swali la MheshimiwaNdassa, kama ifuatavyo:-

Kwanza kabisa ni kwamba, ahadi hii tunaifahamuna ni kweli imekuwa ya muda mrefu na amekuwa akitoleamfano wa Mawaziri mbalimbali ambao wamepita katikaWizara hii. Tulishajibu kwamba, hapatatokea ChikaweThree na wala hapatatokea Kairuki Two na katika mwakahuu wa fedha Mahakama hii ya Nyamikoma itajengwa.

MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Spika,ahsante.

SPIKA: Ukiuliza kwa kifupi, wengi itawafikia.

MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Spika,nashukuru. Kwa kuwa ahadi ya Serikali ya muda mrefu yakujenga Mahakama Kuu Mkoa wa Singida mpaka sasahaijatekelezeka. Je, Serikali itakuwa tayari kutenga fedhakatika bajeti ijayo?

17

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaSpika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa DianaChilolo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Kwanza kabisa, napenda kutoa maelezo yautangulizi ili ieleweke kwamba, ujenzi wa jengo lolote laMahakama Kuu, unagharimu si chini ya takribani shilingibilioni 6.5. Kwa hiyo, hali ya fedha itakaporuhusu, napendakumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kuwa, tutajitahidi haliya kifedha ikiruhusu katika Mwaka wa Fedha wa 2014/15,tutazingatia ujenzi wa Mahakama Kuu Singida.

MHE. MCH. ISRAEL Y. NATSE: Mheshimiwa Spika,ahsante kwa kunipa nafasi. Naomba kumwulizaMheshimiwa Waziri, Mahakama ya Mwanzo ya Wilaya yaKaratu ilianza kujengwa kwa kasi sana, ghafla ime-stop,kulikoni; nini kimetokea?

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaSpika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Natse, kamaifuatavyo:-

Kwanza kabisa, nampongeza kwa namna ambavyoanafuatilia ujenzi wa Mahakama hii. Mimi mwenyewe nilifikana ndiye niliyehamasisha ujenzi huu wa Mahakama yaMwanzo Karatu kupitia nguvu za Wananchi pamoja naSerikali ya Wilaya ya Karatu. Nini kimetokea; ni changamotoza hapa na pale, unajua Wananchi wakiwa wanachangiahali ya kifedha ikiwa inagotagota, ndiyo hayo yaliyotokea.Sisi pia kama Mahakama, tunaiangalia kwa karibu kuonani kwa namna gani tunaweza kuongeza nguvu il iMahakama hii iweze kumalizika mapema.

MHE. MOZA A. SAIDY: Mheshimiwa Spika, nashukurukwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Kwa kuwa Mahakama nyingi za Mwanzo na hatazile za Wilaya hasa katika Wilaya ya Kondoa, zipo karibuna makazi kabisa ya watu, jambo ambalo linasababisha

18

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ufanisi wa Mahakama kuwa ni kama kero. Je, Serikaliinasemaje kuhusiana na suala hili?

SPIKA: Hilo swali ni geni kabisa, naomba ujibu tu!

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaSpika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Moza Saidy,Mbunge wa Viti Maluum, kama ifuatavyo:-

Kwanza kabisa, azma nzima ya Serikali ni kusogezahuduma za Kimahakama karibu zaidi na Wananchi. Kwahiyo, hatuwezi kukimbia Wananchi na kusema kwambainaleta vurugu. Mahakama ni Mahakama, nidhamu zakezinaeleweka, kwa hiyo, nipende tu kumhakikishia kwamba,huo ndiyo utaratibu wenyewe, ni lazima ziwe karibu zaidina Wananchi.

SPIKA: Ahsante. Naomba tuendelee na swalilinalofuata. Mheshimiwa Rebecca Mngodo, atauliza swalihilo.

MHE. REBECCA M. MNGODO: Mheshimiwa Spika,ahsante. Kwa niaba ya Wanawake wote wanaoonewana kunyimwa haki zao hapa Tanzania, naomba sasa swalilangu lipatiwe majibu.

Na. 57

Chama cha Mawakili Wanawake (TAWLA)

MHE. REBECCA M. MNGODO aliuliza:-

Je, ni wapi Chama cha Mawakili Wanawake(TAWLA) hufanyia kazi zake?

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Katibana Sheria, naomba kujibu swali la Mheshimiwa RebeccaM. Mngodo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

[MHE. M. A. SAIDY]

19

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Spika, Chama cha MawakiliWanawake Tanzania (TAWLA), kilianza kazi zake katika Jijila Dar es Salam, Mtaa wa Posta kwenye Jengo la Avalon.Kwa sasa Makao Makuu ya Ofisi zake yamehamishiwakwenye Jengo la TAWLA, Kitalu Na. 33, Ilala Shariff Shamba,karibu na Hospitali ya Amana, Dar es Slaam. Aidha, TAWLAinazo Ofisi zake pia katika Jiji la Arusha, Dodoma na Tanga.Pia kwa maelezo zaidi, ningependa Mheshimiwa Mbungeafuatilie Tovuti ya TAWLA, www.tawla.or.tz.

MHE. REBECCA M. MNGODO: Mheshimiwa Spika,naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza kamaifuatavyo:-

(i) Kwa kuwa kwa maelezo ya MheshimiwaWaziri, TAWLA inaendelea kufanya shughuli zake mijinihususan Dar es Salaam, Tanga, Dodoma na Arusha kulikovijijini ambako asilimia kubwa ya wanawake wanateseka.Kwa mfano, Mama Ruth Timotheo anayeishi Msitu waTembo Meru, ambaye kesi yake ya kunyang’anywa ardhikwa miaka kumi sasa haijamalizika. Je, wanawake vijijiniwaendelee kuteseka hadi lini?

(ii) Kwa kuwa wanawake wengi walioko Vijijinihawana elimu ya kutosha; je, pale wanapokuwawameonewa au kunyanyasika wanawezaje kuvijuavyombo vinavyotoa msaada wa kisheria? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: MheshimiwaSpika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza yaMheshimiwa Rebecca M. Mngodo, kama ifuatavyo:-

Kwanza kabisa, naomba ifahamike kwamba, TAWLAni Shirika lisilokuwa la Serikali. Kwanza, hata suala hili lilivyokujanilikuwa nacheka namtania Mheshimiwa Waziri wangukwamba, itabidi nianze kueleza pale karibu na barabaraya vumbi, pale kwa mshona viatu ndipo ofisi zilipo. Hii niNGO.

[NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA]

20

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Pili, kuhusiana na masuala ya elimu kwa wanawakembalimbali wa vijijini na watu wengine wanaohitaji kujuamasuala ya kisheria, sisi kama Wizara tumejipanga, tutakujana Sheria ya Huduma za Msaada wa Kisheria. Kama kilakitu kitaenda sawasawa, mwakani mapema sanatunatarajia kuwasilisha Sheria hii Bungeni. Lengo kubwa laSheria hii kwa hivi sasa, masuala ya huduma ya msaadawa kisheria kupitia kifungu cha tatu cha Sheria ya Msaadawa Kisheria kwa Masuala ya Jinai ya mwaka 1969, inatolewatu katika makosa ya Mauaji na ya Uhaini.

Kwa hiyo, lengo letu ni kuja na Sheria hii tuangaliesasa ni kwa namna gani masuala mengine ya madai, yamirathi, ya ardhi, pamoja na mambo mengine, ili basi walewasiokuwa na uwezo waweze kupata huduma hii. Lengokubwa pia ni Wizara kuangalia kwa namna gani inaratibuwatoa huduma za msaada wa kisheria. Vilevile tunatarajiakuangalia ni kwa namna gani tunaweza kuwatambua rasmisasa wasaidizi wa kisheria au paralegals ili waweze kufikakatika sehemu zote nchini. Ahsante.

SPIKA: Naomba tuendelee na Wizara ya Elimu naMafunzo ya Ufundi. Mheshimiwa Catherine Magige, ataulizaswali hilo!

Na. 58

Programu ya Kuongeza na Kuboresha Vyuo vya Ufundi

MHE. CATHERINE V. MAGIGE aliuliza:-

Tanzania inatekeleza Malengo ye Milenia pamojana lengo la pili linalohusu upatikanaji wa elimu bora kwawote na kwamba kufikia mwaka 2015 tunalazimika kupimautekelezaji wa lengo hilo ili kuona kama tunaendana naviwango vya Kimataifa:-

(a) Serikali ina mpango gani wa kuanzishaProgramu Maalum hasa za ufundi kwa wanafunzi kama wale

[NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA]

21

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

wa Kidato cha Nne waliofeli kwenye mtihani wa mwaka2012?

(b) Je, Serikali haioni umuhimu wa kuongeza nakuboresha vyuo vya ufundi na kuweka mazingira rahisi kwawanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne kujiunga na vyuohivyo?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDIalijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Catherine Valentino Magige, Mbunge wa VitiMaalum, lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali ilianzisha Mamlaka yaElimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na Baraza la Taifala Elimu ya Ufundi (NACTE) ili kusimamia na kudhibiti elimu yaufundi katika ngazi mbalimbali za Elimu na Mafunzo ya UfundiStadi. Wanafunzi wanaojiunga na Vyuo hivi ni walewaliomaliza Elimu ya Msingi na Sekondari.

Mheshimiwa Spika, Serikali haina mpango wakuanzisha Programu Maalum hasa za Ufundi kwa ajili yakuwasaidia wanafunzi waliofeli kwenye Mtihani wa Kidatocha Nne mwaka mwaka 2012, bali imekuwa ikiwashauriwazazi au walezi kuwashawishi watoto wao kurudia Mtihaniwa Kidato cha Nne. Kwa mwaka 2013, jumla ya watahiniwa60,507 wa kujitegemea wamesajiliwa kufanya mtihani huoambao unaanza leo na vijana hao 60,000 wanaendeleana mtihani. Kati ya watahiniwa hao, watahiniwa 3,578wakiwemo wasichana 2,020 na wavulana 1,558, walifelikatika Mtihani wa Kidato cha Nne kwaka 2012, tayariwamejisajili kurudia mtihani huo unaoanza leo.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa katika Vyuo vya UfundiStadi kuna programu za fani mbalimbali za muda mfupi namuda mrefu, ambazo wanafunzi waliomaliza Elimu ya Msingina Sekondari wanaweza kujiunga kwa vile mafunzoyatolewayo katika Vyuo hivyo huzingatia stadi moja tu

[MHE. C. V. MAGIGE ]

22

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kama vile uashi, ufundi bomba, ushonaji, uchoraji, kilimo namifugo. Sambamba na Vyuo vya Ufundi Stadi, kuna vyuoambavyo vimesajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE), vinavyotoa kozi mbalimbali za kuwapatiawanafunzi hao ujuzi katika fani mbalimbali za kada ya katina kada ya juu (katika ngazi ya Cheti, Stashahada, Shahadana Shahada ya Juu) kama vile Ufamasia, Uhasibu, TEHAMA,Utalii na Ualimu. Baadhi ya Vyuo hivyo ni pamoja na Chuocha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Elimu ya Biashara(CBE), Chuo cha Uhasibu (TIA), Chuo cha Magonjwa yaAkili Hospitali ya Mirembe, Ilembula School of Nursing,Haydom School of Nursing, Kilosa Clinical Officers Center,St. Marys Teachers’ College na Capital Teachers’ College.

Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikiongeza nakuboresha Vyuo vya Ufundi na kuweka mazingira rahisi kwawanafunzi ili waweze kupata stadi mbalimbali. Kati yamwaka 2010 hadi 2012, Serikali kupitia VETA, imesajili jumlaya Vyuo vya Ufundi Stadi 75, sawa na asilimia 10.8 ya Vyuo618 vilivyokuwepo. Aidha, katika kipindi hicho; jumla ya Vyuo8, sawa na asilimia 3.2 ya Vyuo 248 vilivyokuwepo vilisajiliwana Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE).

MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawilimadogo ya nyongeza.

(i) Kwa kuwa kumekuwa na malalamiko yamuda mrefu kwamba wanaorudia mitihani wamekuwahawatendewi haki katika usahihishaji na hivyo kupelekeamatokeo yao kuwa mabaya tofauti na wengine. Je, Serikaliina jitihada gani ya kuondoa kasoro hizi?

(ii) Kwa kuwa sasa kuna mapendekezo yamadaraja ya ufaulu; je, Serikali imeona hili ndilo suluhisho lamkanganyiko wa ufaulu uliojitokeza hapo nyuma?

[NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI]

23

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili yanyongeza ya Mheshimiwa Catherine Valentino Magige,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, nimpongezeMheshimiwa kwa kulileta swali hili la nyongeza, hasa lamalalamiko ya madaraja na hawa vijana wanaorudia.Nitoe ufafanuzi kidogo; Mheshimiwa Spika, unipe dakikamoja mbele il i angalau Watanzania waelewe japotumeshaanza kutoa ufafanuzi kwenye vyombo mbalimbalivya habari.

Mheshimiwa Spika, yeye mwenyewe amesemakulikuwa kuna malalamiko na sisi baada ya kupatamalalamiko hayo ndiyo maana tumekuja na majibu yakusuluhisha malalamiko. Kwa mfano, wanafunzi hawaanaosema Mheshimiwa Mbunge, hawa wanaojitegemea,ni kweli huko nyuma continuous assessment zao zilikuwahazifikir iwi na Baraza la Mitihani na hivyo walikuwawanakosa kitu fulani; lakini kwa mwaka huu, kwa mitihaniinayoanza leo, tumesema kwamba, tutachukua zile alamawalipokuwa shuleni 40 to 60. Maana yake 40 itakuwa ndiyocontinuous assessment na mtihani wa mwisho utachukuaalama 60 kama tulivyo-calculate kwamba kwenye projecttutawapa alama tano, mtihani wa form three muhula wakwanza alama tano na mtihani wa form three muhula wamwisho alama tano na mtihani wa mock ambaowanasimamiwa na wasimamizi wa nje tutawapa alama 10na mtihani wa form two ambao unasimamiwa nawasimamizi na mtihani wa kitaifa tutawapa alama 15; ilikumuwezesha mtoto anapokuwa form one mpaka formfour, miaka mine, aonekane amefanya kitu fulani kule shuleni.

Ninajua Waheshimiwa Wabunge wote mmepitiaVyuo Vikuu, mtajua kabisa kwamba, continuous assessmenthata kwenye Vyuo Vikuu ipo. Mwaka wa kwanzawanatunza zile alama zako, kwa hiyo, unakuta zinatunzwa40 na mtihani wa mwisho una alama 60. Kwa hiyo, jambohili tulilolifanya lisilete tena mkanganyiko bali ni katika

24

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kuendelea kuelimishana na Watanzania wataendeleakutuelewa.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Mheshimiwa anaulizakwamba, je, kushusha haya madaraja ndiyo suluhisho lakuwaokoa vijana wanaokuwa wamefeli mitihani hasa wamwaka 2012? Jibu ni la hasha, hatujashusha madaraja walahatujaweka viwango tofauti na vilivyokuwa. Tumeongezamadaraja kuwatambua watoto kwamba, kulikuwa namrundikano wa alama katika daraja moja. Kwa mfano,Baraza la Mitihani walikuwa wanatumia kwamba F inaanzia0 – 34 lakini unakuja unajiuliza na ukizingatia kulikuwa hakunacontinuous assessment ambazo zinaingia pale, tofauti naSera inavyosema kwamba kuwe na continuous assessmentya alama 50 kwa 50. Mtihani wa continuous assessmentutunze alama 50 na mtihani wa mwisho alama 50, lakini sisitumefanya 40 to 60; sasa je, hawa wanafunzi waliokuwawamepata alama 34 nao wamepata F?

Kwa hiyo, tumeanza kuzi-grade zile alama kwamba,tuweke madaraja yatofautiane kwa ngazi ya kumi kumi,lakini bado daraja la ufaulu litaendelea kuwa ni 40, maanayake 40 ndiyo ngazi ya kufaulu akipata alama C. Siyokwamba Watanzania kama wanavyoandika kwenyemitandao na kwenye magazeti kwamba basi mwanafunziakipata alama 19 ama 20 ndiyo amefaulu tunampelekaform five. Kwenye selection itakuja na mambo mengine,lakini katika kuyapanga madaraja tumeanzia na F,tumeanzia na E, tunakwenda C, B na kwenye B tumewekana B+ ambayo hata Vyuo Vikuu ipo hiyo.

Naomba niwahakikishie Watanzania kwamba,tunafanya hivyo lakini ni katika kutoa ule mrundikano waalama kwenye daraja moja. Labda hata hili ambalo lilikuwalimejitokeza mitaani kwamba labda tumefuta division zero,hatujafuta division zero itaendelea kuwepo. Ni mkanganyikotu wa taarifa zilizokuwa zimejitokeza kwamba kulikuwa nadivision five. Division five haipo ila kutaendelea kuwa nadivion one, division two, division three, division four nadivision zero kama kawaida. (Makofi)

[NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI]

25

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

SPIKA: Mheshimiwa Waziri, naomba mlete Kauli yaSerikali, kwa sababu naona tunajibiwa tu. Tunaendelea naMheshimiwa Selemani Jafo, swali linalofuata!

Na. 59

Ukosefu wa Gari Idara ya Elimu Ukaguzi

MHE. SELEMANI S. JAFO aliuliza:-

Idara ya Elimu Ukaguzi Wilayani Kisarawe haina garikwa ajili ya kufanya shughuli za Ukaguzi jambo linaloshushaari ya kufanya kazi kwa Maafisa Elimu Ukaguzi Wilayani.

Je, ni lini Serikali itaipatia gari Halmashauri ya Wilayaya Kisarawe kwa ajili ya kazi za Idara ya Elimu ya Ukaguzi?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDIalijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Selemani Saidi Jafo, Mbunge wa Kisarawe,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wakutoa usafiri kwa Ofisi zake za Ukaguzi wa Shule nakipaumbele ni kwa Halmashauri za Wilaya zenye mazingiramagumu kufikika kama ilivyo Halmashauri ya Wilaya yaKisarawe.

Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ilikuwa miongonimwa Wilaya za kwanza kabisa kupatiwa gari aina ya ToyotaLand Cruiser Hard Top, lenye Namba za Usajili DFP 3065,lililotolewa na UNICEF mwaka 2006, lakini kwa bahati mbayagari hilo liliibwa mwaka huo huo. Watuhumiwa wa tukio hilowalishtakiwa Mahakamani katika Mahakama ya HakimuMkazi Mkoa wa Pwani (Kibaha), (Case No. RM/27/2007),lakini waliachiwa huru baada ya kuonekana hawana hatia.

26

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Spika, kwa sasa Idara ya Ukaguzi waShule ina jumla ya magari 112 kati ya 166 yanayohitajikakatika Ofisi za Ukaguzi Kanda na Wilaya. Hivyo, kunaupungufu wa magari 54; 9 yakiwa ni kwa ajili ya Ofisi yaUkaguzi wa Shule Kanda na 45 yakiwa ni kwa upungufu waOfisi za Ukaguzi wa Wilaya ikijumuisha na Wilaya ya Kisarawe.

Napenda kumhakikishia Mheshimiwa Mbungekuwa, Wizara yangu itaendelea kununua magari yakutosheleza kadiri fedha zitakavyopatikana nakuyasambaza katika Halmashauri ambazo hazina magariikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.

MHE. SELEMANI S. JAFO: Mheshimiwa Spika, ahsante.

(i) Pamoja na majibu ya ufafanuzi yaMheshimiwa Waziri, nilipenda kujua nini mpango wa Serikali(time frame), kwa sababu tuna miaka saba hatuna gari laukaguzi pale Kisarawe; sasa nilitaka kujua kwamba ninimpango wa Serikali kuipatia Wilaya ya Kisarawe gari?

(ii) Kwa kuwa nilimwona Mheshimiwa NaibuWaziri akitembelea Wilaya mbalimbali katika suala zima laukaguzi. Je, yupo tayari kuja Kisarawe kuhakikisha kwambatunashirikiana kwa pamoja kuboresha elimu yetu Wilaya yaKisarawe?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu naMafunzo ya Ufundi, napenda kujibu maswali mawili yanyongeza ya Mheshimiwa Selemani Saidi Jafo, Mbunge waKisarawe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli Mheshimiwa Mbungeanataka tutaje time frame ya lini tutapeleka gari Kisarawe,lakini tayari Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundiimeshapata kibali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, cha kununuamagari tisa, ambapo magari matatu yatapelekwa kwenyeOfisi za Kanda, hasa Kanda ya Kigoma kule Magharibi na

[NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI]

27

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Kanda ya Kusini kule Iringa na Kanda ya Morogoro Kandaya Kati.

Vilevile tunao mpango wa Global Partnership forEducation (GPE), unaofadhiliwa na nchi wahisanimbalimbali. Idara ya Ukaguzi kwa kipindi hicho cha mwaka2014/2015, tunatajia kupatiwa magari 36 yatakayogawiwakatika Ofisi za Ukaguzi ngazi ya Kanda na Wilaya. Hatuahiyo itawezesha Idara kukagua shule kwa ufanisi zaidi naWilaya ya Kisarawe ndipo itakapopata gari kwa kutumiamfumo huo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili kwambanikatembelee Wilaya ya Kisarawe; Wilaya ya Kisarawe nijirani na Dar es Salaam, kwa mwito wa MheshimiwaMbunge, Bwana Selemani Jafo, mimi nikuahidi tu kwamba,nitakuja. Vilevile nitakuja kuiona na shule ambayo wakatinikipitia swali hili, nilikuwa naongea na Mkurugenzi wakoakaniambia kwamba, umefanya juhudi kubwa kutoa milioni36 kwenye Mfuko wako wa Jimbo umejenga Shule yaMnegele, Kata ya Kibuta. Mimi nakupongeza sana naWaheshimiwa Wabunge na wengine tufuate mfano huu wakutumia fedha za Mfuko wa Jimbo kuinua elimu kwenyemajimbo yetu. Ahsante sana. (Makofi)

MHE. HAROUB MOHAMED SHAMIS: MheshimiwaSpika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali lanyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu elimu ipo katikaMpango wa Maendeleo ya Taifa wa Miaka Mitano naIdara hii ya Ukaguzi tunaiona kama inapwaya sana. Je,Serikali ina mpango gani wa kuiimarisha Idara hii ya Ukaguziili kuweza kujenga elimu bora katika nchi kwa ajili ya mpangohuu ambao tunaujadili uweze kwenda vizuri?

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Spika, napenda kumjibu Mheshimiwa HaroubShamis, swali lake fupi la nyongeza kama ifuatavyo:-

[NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI]

28

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Ameitaka Wizara itoe mchanganuo wa namna ganiya kuiimarisha Idara hii ya Ukaguzi. Tunao mpango wakuifanya Idara hii kuwa Mamlaka ili ijitegemee, iweze kupatamafungu peke yake, iweze kuimarisha Idara hii ya Ukaguzi.Kwa hiyo, nadhani ni mpango wa mwaka mmoja mpakamiwili, Idara hii itakuwa imeshakuwa mamlakainayojitegemea.

MHE. JOSEPHINE J. NGENZABUKE: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya MheshimiwaNaibu Waziri, nina swali moja la nyongeza.

Kwa kuwa maeneo mengi nchini Idara ya Ukaguziimekuwa ikipatiwa magari lakini inashindwa kuendeshamagari hayo kutokana na ukosefu wa pesa na kupelekeashule nyingi nchini kutokufanyiwa ukaguzi ipasavyo namatokeo yake shule hizo kufanya vibaya. Je, ni lini sasaSerikali itamaliza tatizo hil i i l i Idara ya Elimu iwezekujitegemea? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI:Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu naMafunzo ya Ufundi, napenda kujibu swali moja la nyongezala Mheshimiwa Josephine Genzabuke, Mbunge wa VitiMaalum kutoka Mkoa wa Kigoma, kama ifuatavyo:-

Kwanza, napenda kumhakikishia kwamba, Mkoawake wa Kigoma ni miongoni mwa Mikoa ambayo itapatamagari ya Idara ya Ukaguzi; na kama nilivyosema kwamba,watapata gari moja kwa ajili ya Kanda ya Kigoma; kwahiyo, hilo hongera sana. Vilevile tutakapokuwa tunaletagari hilo Kigoma, tutaweka na bajeti kwa ajili ya kununuamafuta ili ukaguzi wa shule Mkoa wa Kigoma uwezekufanyika.

Utakumbuka ni wiki tatu tu zimepita, mimi nilikuwahuko Kigoma kwa ziara ya Mheshimiwa Waziri Mkuu,tumejifunza mambo mengi sana, tumetembea Wilaya zoteza Kigoma na tumeona tabu iliyopo kwa ajili ya Idara yaUkaguzi. Kwa hiyo, tutahakikisha kwamba, tutafanya kazi

[NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI]

29

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kubwa kuokoa kutokana na mazingira yaliyopo kwa Mkoawa Kigoma.

Na. 60

Chuo cha Maendeleo ya Wananchi

MHE. SAID AMOUR ARFI aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuendeleza Chuocha Maendeleo ya Wananchi Msaginya ili kiweze kutoamafunzo ya ufundi stadi na stadi za maisha?

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NAWATOTO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Said Amour Arfi, Mbunge wa Mpanda Mjini,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Chuo cha Maendeleo yaWananchi Msaginya ni miongoni mwa vyuo 55vinavyosimamiwa na Wizara yangu kwa madhumuni yakutoa maarifa na stadi kwa Wananchi mahali chuo kilipo.

Mheshimiwa Spika, ili kutekeza azma ya Serikali yakuhakikisha katika kila Wilaya kunakuwepo walau chuokimoja kinachotoa mafunzo ya ufundi stadi, Serikali iliamuaVyuo vya Maendeleo ya Wananchi vilivyopo katika Wilayazisizo na Vyuo vya VETA viboreshwe ili viweze kutoa mafunzoya ufundi stadi sanjari na mafunzo ya elimu ya Wananchi.Utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mpango huoumehusisha vyuo 25 vya Maendeleo ya Wananchi.

Mheshimiwa Spika, wakati wa zoezi la kubaini vyuohivi, Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Msaginya kilikuwakatika Wilaya ya Mpanda ambayo ilikuwa na Chuo chaVETA. Baada ya mgawanyo mpya wa Wilaya, Chuo chaMaendeleo ya Wananchi Msaginya kipo katika Wilaya yaMlele ambayo haina Chuo cha VETA. Hivyo, Chuo hiki

[NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI]

30

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kimepangwa kuwemo katika awamu ya pili ya utekelezajiwa mpango wa maboresho wa Vyuo vya Maendeleo yaWananchi.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, kwa kutambuaumuhimu wa Chuo hiki na hali halisi ya majengo namiundombinu iliyopo, Serikali kwa mwaka huu wa fedhaimetenga shilingi milioni 290 kwa ajili ya ukarabati wamajengo ya Chuo hiki.

MHE. SAID AMOUR ARFI: Mheshimiwa Spika, pamojana maelezo ya Mheshimiwa Waziri, nina maswali mawili yanyongeza kama ifuatavyo:-

(i) Je, ni lini awamu ya pili itaanza na itachukuamuda gani kukamilika ili Chuo hiki cha Msaginya kiwezekuanza kutumika?

(ii) Kwa kuwa Wizara yako ilikuwa imetengafedha kwa ajili ya ukarabati kwa Mwaka huu wa Fedhawa 2013/14; napenda kujua ni kiasi gani cha fedhakimepelekwa na kazi iliyofanyika imefikia kiwango gani?

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NAWATOTO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawiliya nyongeza ya Mheshimiwa Said Arfi, kama ifuatavyo:-

Awamu ya pil i ya Maboresho ya Vyuo vyaMaendeleo ya Wananchi, itaanza Mwaka wa Fedha wa2014/15. Ninapenda kukutaarifu Mheshimiwa Mbungekwamba, katika Mpango wa Maendeleo ambaoMheshimiwa Wasira ameuwasil isha na tunaujadili,mojawapo ya eneo ambalo litatengewa fedha ni suala lakuboresha Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi kikiwemoChuo cha Maendeleo ya Wananchi Msaginya.

Kwa hiyo, nimwombe Mheshimiwa Mbungekwamba, wakati Mheshimiwa Wasira ana-concludemjadala wake, kuhakikisha Vyuo vya Maendeleo ya

[NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO]

31

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Wananchi vinawekewa msisitizo ili itakapokuja hatua yakutenga rasilimali fedha basi na chuo chako kiwemo.

Mheshimiwa Spika, suala la kiasi gani cha fedhakimepelekwa katika Chuo cha Msaginya, ni kwamba, hadisasa hatujapeleka fedha, lakini nakuthibitishia kwamba,tutapeleka fedha kabla ya mwaka wa fedha kumalizika.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Ritta Kabati,utafuatiwa na Mheshimiwa Ntukamazina.

MHE. RITTA KABATI: Mheshimiwa Spika, nakushukurukwa kunipa nafasi.

Kwa kuwa Serikali i l ikuwa na mpango wakukipandisha hadhi Chuo cha Maendeleo kil ichopoRungemba, Mkoa wa Iringa kutoka kutoa mafunzo yaStashahada mpaka Shahada; je, ni lini Serikali itatimizaahadi hiyo? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NAWATOTO: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri waMaendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, ningependa kujibuswali la nyongeza la Mheshimiwa Ritta Kabati, Mbunge waViti Maalum, Mkoa wa Iringa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, bado tupo katika majadilianoya kuhakikisha kwamba, tunapandisha hadhi ya Chuo chaMaendeleo ya Jamii cha Rungemba ili kuweza kutoaShahada badala ya Stashahada, lakini kwa sasa hivitumejikita katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru;na juzi Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ilikitembelea ilikukipa hadhi ya kuwa Chuo Kikuu. Kwa hiyo, nikuthibitishietu kwamba, hilo nalo liko ndani ya uwezo wetu.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)

[NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO]

32

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. DEOGRATIAS A. NTUKAMAZINA: MheshimiwaSpika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali moja lanyongeza.

Kwa kuwa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FolkDevelopment College) cha Lemela Ngara kimechakaasana kwa muda mrefu, completely dilapidated; je, Serikaliinaweza kukifufua kikawa Chuo cha Ufundi cha Wilaya?

SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu!

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NAWATOTO: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Deogratias Ntukamazina, Mbuge wa Ngara,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Chuo cha Maendeleo yaWananchi Ngara kipo katika Mpango wa Awamu ya Piliya Maboresho ya Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi. Namininafurahi kwamba, Mheshimiwa Wasira, katika mpangowake, eneo ambalo amelisisitiza pia katika Human CapitalDevelopment, ni pamoja na kuboresha miundombinu navifaa vya kujifunzia na kufundishia katika Vyuo vyaMaendeleo ya Wananchi.

Mheshimiwa Spika, naomba sasa wakatiutakapokuja ku-allocate resources, baada ya kupitishaMpango wa Maendeleo wa Mwaka 2014/2015, tuone ilecommitment ya Mheshimiwa Wasira katika Mpango waMaendeleo inakuwa translated katika fedha. Kwa hiyo,hilo ninaomba sana Waheshimiwa Wabunge mtusaidieitakapokuja sasa kujadili Bajeti.

Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana.

SPIKA: Hakuna Mpango wa Mheshimiwa Waziri,isipokuwa kuna Mpango wa Nchi. (Kicheko)

33

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Na. 61

Kukamilika kwa Mradi wa Gesi Mtwara

MHE. MBAROUK SALIM ALI aliuliza:-

(a) Je, ni lini Mradi wa Gesi Mtwara utakamilika?

(b) Je, ni sekta zipi na kaya ngapi zitafaidika naMradi huo utakapokamilika?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.GEORGE B. SIMBACHAWENE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Mbarouk Salim Ali, lenye sehemu (a) na (b),kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, hivi sasa Shirika la Maendeleoya Petroli Tanzania (TPDC), limetangaza zabuni ya kumpatamshauri wa kufanya kazi ya kutathmini Athari za Mradi waMazingira na Jamii (Environmental and Social ImpactAssessment – ESIA), upembuzi yakinifu (Feasibility Study),kusanifu miundombinu ya usambazaji wa gesi asili, pamojana kusimamia kazi ya ujenzi wa Mradi. Kazi hii itafanyikakwa Mikoa ya Mtwara na Lindi na inatarajiwa kuchukuamiezi sita baada ya kupatikana kwa mshauri.

Mheshimiwa Spika, matokeo ya tathmini naupembuzi ndiyo yatakayoelekeza muda wa kuanza nakukamilika kwa Mradi wa Gesi katika Mikoa ya Mtwara naLindi.

Mheshimiwa Spika, kama ilivyoelezwa hapo awali,Mradi wa Gesi kwa Miji ya Mtwara na Lindi hivi sasa upokatika hatua za awali za upembuzi yakinifu ili kupatamchanganuo wa idadi ya watumiaji na makisio ya awali yamahitaji kwa sekta mbalimbali. Upembuzi huu unahusishamchanganuo wa matumzi ya gesi asil i viwandani,majumbani, katika taasisi na kwenye magari.

34

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. MBAROUK SALIM ALI: Mheshimiwa Spika,ninashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri.Pamoja na majibu yake hayo, ninayo maswali mawili yanyongeza kama ifuatavyo:-

(i) Upatikanani wa gesi unaonekana kukaribia;na kwa kuwa tunahitaji kupunguza utumiaji wa mkaa ilikutunza mazingira yetu; je, kipi kianze; kutoa mafunzo kwajamii au upembuzi yakinifu? (Makofi)

(ii) Inaonekana kwamba, ajira na shughuli zoteza kiuchumi kwa sasa zimeelekezwa au zimewashirikisha zaidiwatu kutoka nje. Je, ni lini shughuli hizo zitarudi kwaWatanzania? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA NIASHATI NA MADINI (MHE.GEORGE B. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Spika, napendakujibu maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, utoaji wa elimu wakati woteimekuwa ndiyo shughuli ya maana na ya kwanza katikauendelezaji wa Sekta hii ya Gesi na kwamba, upembuziyakinifu ni lazima ufanyike. Lazima pia hili nalo liendesambamba kwa sababu tunahitaji sasa kuanza kuitumiahii gesi, huku tukiendelea kuona umuhimu wa kutoa hiyoelimu kwa Wananchi. Haya yote ni muhimu kwa sababumatokeo yanahitajika haraka.

Mheshimiwa Spika, ajira zinawashirikisha wageni; nikweli katika awamu hii ambayo sasa utaalam zaidiunahitajika katika utafutaji na uchimbaji, bado sisi hatukuwatumejenga uwezo kwa watu wetu kwa ajili ya kufanyashughuli hizo, ni wachache tu ndiyo ambao wanashirikianana hao katika deep sea katika utafutaji wa gesi.

Nikubaliane na Mheshimiwa Mbunge kwamba,tunayo mikakati mingi tu ya kuhakikisha Wazalendo naowanashiriki hasa tutakapoanza kuiendeleza gesi hii,ambayo kwa kiasi kikubwa bado tuko katika utafutaji naujengaji wa miundombinu. Kwa yale maeneo ambayo

35

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

wazawa wanaweza wakafanya kazi, tutajitahidi sanakatika local content kuhakikisha kwamba, wanapataumuhimu wa kwanza. (Makofi)

MHE. DAVID Z. KAFULILA: Mheshimiwa Spika,ninakushukuru kwa kupata nafasi ya kuuliza swali lanyongeza.

Mheshimiwa Spika, gesi ni sehemu kubwa sana yauchumi na mwaka 2011 nikiwa Uholanzi, Kampuni ya Shell,i l ionesha kwamba, il ishafanya utafiti wa uchumi waTanzania katika Sekta ya Gesi, impact ya gesi kwenyeUchumi wa Tanzania mpaka kufikia mwaka 2030. Ninaombakujua Serikali hii imekwishakufanya utafiti wa mchango waSekta ya Gesi utaongeza Pato la Taifa kwa kiasi gani kufikiamwaka 2025 kama Dira ya Taifa? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE.GEORGE B. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Spika, napendakujibu swali la Mheshimiwa David Z. Kafuli la, kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni dhahiri na lipo wazi kabisakwamba, gesi itakuza uchumi wetu kwa kiasi kikubwa sana.Ni dhahiri kwamba, maeneo yatakayokuzwa zaidi, kwanza,upatikanaji wa nishati utasukuma kwa kiasi kikubwamaendeleo ya viwanda na mahusiano ya sekta nyinginekutokana na rasilimali hii.

Mheshimiwa Spika, kwa hesabu na kwa idadi, sinakumbukumbu nzuri, lakini kazi kubwa imefanywa naWataalam wetu na tuna hakika by 2030 tutakuwa namaendeleo makubwa na nchi hii itakuwa na maendeleomakubwa kama walivyo wenzetu wa Malaysia na nchinyingine ambazo wamenufaika sana na gesi waliyoipatakatika nchi zao. (Makofi)

[NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI]

36

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaombatuendelee na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

Na. 62

Kuboresha Huduma ya Mawasiliano

MHE. ENG. ATHUMANI K. MFUTAKAMBA aliuliza:-

Hivi sasa kumekuwa na malalamiko mahali pengiya kukatikakatika kwa mawasiliano ya simu hasa ya Tigoambayo ni moja ya wazabuni walioshinda kutoa hudumavijijini katika Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCAF):-

(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaelekezaTigo kuboresha huduma zao?

(b) Je, Serikali haiwezi kuweka utaratibuutakaowezesha kampuni za simu za mkononi kupokeamawasiliano kupitia mnara mmoja na kwa kufanya hivyomawasiliano yaweze kupatikana huko Loya na LutendeJimboni Igalula?

WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIAalijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Eng. Athumani R. Mfutakamba, Mbunge waIgalula, lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kumekuwepo namalalamiko kutoka kwa wateja kuhusu huduma isiyoridhishakutoka kwenye baadhi ya Kampuni za Simu. Katikakushughulikia suala hilo, Serikali kupitia Mamlaka yaMawasiliano Tanzania (TCRA), ilikwishaziagiza kampuni zoteza simu ikiwemo Kampuni ya Tigo, kuboresha huduma zaokwa Wananchi na itaendelea kukumbusha utekelezaji waagizo hilo. Aidha, utoaji wa huduma bora ni miongoni mwamasharti ya kisheria kuhusiana na leseni walizopewa watoa

37

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

huduma za mawasiliano na Serikali kupitia TCRA na zipoadhabu mbalimbali kwa kampuni zinapokiuka sheria hiyo.

Ili kuondoa utata kati ya taarifa za Kampuni za Simuzinazoonekana kuridhisha kinyume na malalamiko yaWananchi, Serikali imefanya jitihada za kusimika mtambowa Telecom Traffic Monitoring System (TTMS), katika Ofisi zaMamlaka ya Mawasiliano Tanzania. Pamoja na kusaidiauhakiki wa mapato, mtambo huo utaweza kupima viwangohalisi vya ubora vinavyotolewa na watoa huduma ilihatimaye hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yawatakaoshindwa kutimiza viwango vilivyowekwa.

Mheshimiwa Spika, Bugne lako Tukufu lilitunga Sheriaya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) mwaka2010, ambayo imeweka utaratibu kupitia Kanuni zaMiundombinu kwa Kampuni za Simu kuchangiamiundombinu ikiwemo minara. Aidha, Kampuni za Simuzinaelewa umuhimu na manufaa ya kutumia mnara mmoja(Infrastructure Sharing), katika kusambaza huduma zamawasiliano kwa lengo la kuongeza tija kwa kampuni husikakulingana na matakwa ya Sheria ya EPOCA ya mwaka 2010na Kanuni zake za mwaka 2011. Hata hivyo, ni vyemaikafahamika kwamba, minara ina ukomo wa kubeba vifaavya mawasiliano (Transmission Equipment), ambazo ukizidiuna madhara ikiwemo kuhatarisha usalama wa Wananchina wakazi wa maeneo husika. Kabla ya kuchangia,kampuni husika hufanya tathmini ya kitaalam juu ya uwezowa minara ili kuepuka athari hasi katika maeneo husika.Serikali inaendelea kuhamasisha Kampuni za Simu kutumiamiundombiu ya mawasiliano ikiwemo minara ya simu kwakushirikiana. Kwa kufanya hivyo, gharama za uendeshajizitashuka na hivyo kuleta tija kwa makampuni ya simu nawatumiaji wa huduma za mawasiliano kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kuzingatia ushauri wakutumia mnara mmoja kupeleka mawasiliano kwenyemaeneo mbalimbali ya nchi, Serikali kupitia Mfuko waMawasiliano kwa Wote, imeyajumuisha maeneo hayo yaLoya na Lutende huko Igalula katika ujenzi wa miundombinu

[WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA]

38

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ya mawasiliano katika awamu ya kwanza (WB Phase 1),unaotekelezwa kupitia Fedha za Benki ya Dunia, ambapoutekelezaji wa Mradi huo unaendelea kupitia kwa Kampuniya Simu ya MIC (T) Ltd. (Tigo). Jumla ya Dola za Kimarekani372, sawa na shilingi za Kitanzania milioni 626.4 zimetengwakwa ajili ya kupeleka mawasiliano katika Kata hizo.

MHE. ENG. ATHUMANI R. MFUTAKAMBA: MheshimiwaSpika, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri.Ninaomba kuuliza maswali mawili madogo ya nyongezakama ifuatavyo:-

(i) Wananchi wa Lutende na Loya, wanatakawajue tarehe ambayo Kampuni ya MIC Tanzania Limited(Tigo), itaanza ujenzi wa minara hii ili wafanye sherehe yauzinduzi?

(ii) Sasa hivi unapopiga simu hasa kwenda nchiza nje kutafuta Wawekezaji kuja Igalula hata kamamawasiliano hayakuunganishwa unakatwa shilingi 548wakati wewe hukuongeza na wakati huo huo Voda nayohata hailipi pango kule Goweko; hii inakuwaje? Ninaombamajibu. (Makofi)

WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NATEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, katika utaratibu wakupeleka miundombinu ya mawasiliano katika Kata hizombili, kazi imeanza na mwishoni mwa mwezi huu kazi yakuweka minara kwenye Kata hiyo itakuwa imekamilika.

Kunako mwanzoni mwa mwezi Januari, 2014 vifaavya mawasil iano, Transmission Equipment v itakuwavimekamilika na minara hiyo itaanza kuwashwa mwishonimwa mwezi Januari, 2014 na Wananchi watapata hudumahiyo ifikapo mwishoni mwa mwezi Januari, 2014.

Swali la pili kuhusu kukatwa pesa kabla hujampatamtu unayemtafuta huko nje; kiutaratibu unatakiwa zikatwepesa zako baada ya kupata answer buzz signals au sautiya yule mtu unayemtafuta. Sasa kama unakatwa kabla

[WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA]

39

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ya kupata hiyo sauti, hilo ni kosa. Ninaomba Mheshimiwauwasiliane na Kampuni ya Simu, kama Makampuni ya Simuyatashindwa kurejesha hela yako, tafadhali uwasiliane naMamlaka ya Mawasiliano Tanzania, kama Mdhibiti na yeyeatalishughulikia suala hilo.

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, ninaomba utulivusijui kuna vurugu gani humu ndani.

MHE. AGRIPINA Z. BUYOGERA: Mheshimiwa Spika,ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi niulize swali moja lanyongeza.

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na ahadi ya mudamrefu ya kujenga Minara ya Simu katika vijiji vya mpakani.Ninataka kujua ni lini Vijiji vya Kitanga na Herushingo minarahiyo itakamilishwa?

Mheshimiwa Spika, ahsante.

WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NATEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ninaomba kumjibuMheshimiwa Mbunge, swali lake la nyongeza kamaifuatavyo:-

Ni kweli kumekuwa na ahadi muda mrefu, lakinikwanza tuelewe uwekaji wa mawasiliano hasa mitamboinachukua muda mrefu, karibu miezi mitatu mpaka miezisita. Sasa hivi tunatekeleza awamu wa kwanza ambayoinaendelea vizuri. Tunaamini itakapofika mwakani, kuanziamwezi Januari, 2014 awamu ya kwanza yote itakuwaimekamilika. Sasa hivi tuna awamu ya pili ambayo Tendertumeshaitangaza na tunafungua wiki hii, ambapo baadhiya vijiji vyako Mheshimiwa Mbunge vitakuwemo kwenyeawamu hii.

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, muda tulionaoumekaa vibaya sana. Tunaendelea na swali linalofuata.

[WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA]

40

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Na. 63

Mamlaka Zinazosimamia Vivutio Vya Utalii

MHE. REBECCA M. MNGODO (K.n.y. MHE. JOSHUA S.NASSARI) aliuliza:-

Njia mojawapo ya kuinua Utalii endelevu ni kujengamahusiano mazuri kati ya Mamlaka zinazosimamia vivutiovya utalii na wananchi wa maeneo husika:-

(a) Je, ni jitihada gani zimefanywa ili kujengamahusiano mazuri kati ya Wananchi wa Kata za Songoro,Maji ya Chai, Leguruki na Ngarenanyuki ambazozimepakana na Hifadhi ya Wanyamapori ya Arusha naMlima Meru?

(b) Je, ni hatua gani zilizochukuliwa kutatuamigogoro ya muda mrefu kati ya Hifadhi ya Taifa Arusha naWananchi wa Kata za Leguruki na Ngarenanyuki?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali laMheshimiwa Joshua Samwel Nassari, Mbunge wa ArumeruMashariki, lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Hifadhi ya Taifa Arusha, inajengamahusiano mazuri na Wananchi waishio katika Kata zaSongoro, Maji ya Chai, Leguruki na Ngarenanyuki, ambazoni miongoni mwa Kata zinazopakana na Hifadhi ya TaifaArusha, kwa kutoa elimu ya uhifadhi na utunzaji wa mazingirakupitia ziara za kimafunzo, kutoa huduma za kijamii kamamatibabu bure kwa Wananchi katika Zahanati iliyopo palekatika Hifadhi; usambazaji wa maji kwa ajili ya matumizi yanyumbani na mashambani. Kwa mfano, Mto Ngarenanyuki,bomba la maji la Nkwasenga, bomba la maji la Songoro,Ngongongare, Ngurdoto na Kilinga na kuchangia Miradimbalimbali inayoibuliwa na Wananchi. Katika kipindi chakuanzia Mwaka wa Fedha wa 1996/97 hadi 2011/12, Hifadhi

41

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

imechangia Miradi ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi189,489,399.

Mheshimiwa Spika, hatua zilizochukuliwa na Hifadhiya Taifa ya Arusha katika kujaribu kutatua migogoro katikaKata ya Ngarenanyuki ni pamoja na kufanya vikaombalimbali na Kata na Vijiji vinavyohusika ili kuwaeleweshaWananchi ambapo mpaka kati ya hifadhi ya kijiji husikaunakopita; kuweka alama za kudumu ambazo zinajulikanakama (beacons) hasa katika maeneo yasiyokuwa na alamaza kudumu; kuhamasisha Jamii kuhusu umuhimu wa Hifadhihiyo; kuchangia Miradi mbalimbali ya Jamii kama ujenzi wamadarasa ya shule za msingi, nyumba za Walimu, nyumbaza waganga, samani za ofisi ya Kata, kutoa ajira ndogondogo zisizo za kiutaalam kwa Wanajamii wanaozungukaHifadhi na vilevile kutoa ajira za kudumu kwa wale ambaowana ujuzi.

MHE. REBECCA M. MNGODO: Mheshimiwa Spika,ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali moja lanyongeza.

Kwa kuwa mojawapo ya migogoro ya muda mrefukatika Wilaya ya Arumeru Mashariki kati ya Hifadhi naWananchi wanaoishi katika Kata za Reguruki naNgarenanyuki ni pale Wanawake wanapoingia katika msituwa Hifadhi zilizopo karibu na Mlima Meru kuchanja kuni.Baadhi yao wanaposhikiliwa na Maaskari kwa muda namatukio ya kubakwa yametokea. Je, Serikali inalijua hilona nini tamko lake kwa Maaskari hao wanaofanya vitendohivyo viovu? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaSpika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa RebeccaMngodo, kwa ufupi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni marufuku kwa Askari yeyotewa Wanyamapori kupiga Wananchi na ni marufuku kubaka,ni kinyume cha sheria. Wale ambao kwa sababu yoyoteile katika kutekeleza na katika kusimamia sheria ya halali

[NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII]

42

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ambayo tumeiweka kwa kutunza Hifadhi na kusimamiamaeneo ya uhifadhi, endapo watajihusisha na vitendo vyakuvunja sheria ya nchi, sisi wenyewe tuko tayarikuwachukulia hatua.

Tumeendelea kuwakamata Maaskari ambao siyowaadilifu na ninaomba nilihakikishie Bunge lako Tukufukwamba, Askari yeyote ambaye atavunja maadiliyaliyowekwa na Serikali katika kutekeleza kazi yake,tutamkamata, tutamwondoa kazini na tutamfunguliamashtaka kisheria.

MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Spika, ahsantena mimi kunipatia fursa ya kuuliza swali la nyongeza.

Kwa kuwa sasa hivi tunaanza kuona hali ngumu yaWanyamapori na Vivutio vikubwa vya Wanyamapori niTembo, Simba na Chui, lakini wenzetu kutoka Asia hasaChina, wameingia katika zoezi gumu la kuhakikishawanyama wetu wanatoweka. Nitatoa mfano; tulikwendakatika Katavi, Wachina wamekutwa wamechukua lori zimala Meno ya Ndovu na wakaachiwa. Hata jana tarehe 4Novemba, 2013, uthibitisho tena Mchina amekutwa naMeno ya Ndovu 700, sawa sawa na kuuwa Ndovu 350.

Je, Serikali inatoa tamko gani kwa wenzetu kutokaAsia, kuwa wanatuletea fujo na kuhakikisha Utalii waTanzania unakufa? Je, Waziri anatoa tamko gani ndani yaBunge hili ili Watanzania tuwe na faraja na hao wenzetukutoka Asia? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaSpika, naomba kujibu swali moja la nyongeza la MheshimiwaRiziki Lulida, kama ifuatavyo:-

Tuna tatizo kama nchi na suala kubwa sana laujangili linaloendelea. Ninakubaliana sana na MheshimiwaMbunge kwamba, kuna raia wa nchi za kigeni ambaotumewatia nguvuni na wengine tumewatia nguvuni hivikaribuni, kwa jitihada zinazotokana na mafanikio ya

[NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII]

43

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

operation ambayo imekuwa ikiendelea na kwa ushirikishwajiwa Wananchi, Maaskari wetu wa Wanyamapori naVyombo vingine vya ULinzi na Usalama, kuhakikishakwamba, hali hii ya kupotea kwa wanyamaporiinatokomezwa.

Ninaomba niseme kwamba, zoezi hili ni gumu, zoezihili linapaswa kuwa endelevu na zoezi hili Serikali haitaliacha,kwa namna moja au nyingine, tunajipanga upya.Ningeomba nitoe wito kwa Wabunge na Wananchi wotekwa ujumla kwamba, tushirikiane katika kuhakikishawanyamapori wa Tanzania watalindwa hasa kwa suala lakutoa taarifa ambazo zinasaidia sana kukamatwa wahalifu.Pia nitoe onyo kwa watu wanaodhani kwamba, nchi hiiwanaweza kuja kama wageni, halafu wakajiingiza katikashughuli za kuvunja sheria zetu. Hatua ambazo tutazichukuani kutomfumbia macho mtu yeyote aliyetoka katika Taifalolote Duniani.

SPIKA: Ahsante, tunaomba tuendelee na swalilinalofuata, Mheshimiwa Mariam Nasoro Kisangi.

Na. 64

Msitu wa Mwandege, Vikindu na Mlamleni

MHE. MARIAM N. KISAGI aliuliza:

(a) Je, Serikali ina mpango gani wa Msitu uliopoMwandege, Vikindu na Mlamleni kutokana na kukua kwaJiji la Dar es Salaam na Mji mdogo wa Mkuranga?

(b) Je, Serikali ina mpango gani wa kurudishamsitu huo katika Halmashauri za Mkuranga na Temeke nakubadilisha matumizi yake ili utumike kihalali kuliko sasaambapo kuna ujenzi unaofanyika kinyemela?

(c) Je, Serikali inapata faida gani za ziada katikamsitu huu zaidi ya uhifadhi wa mazingira?

[NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII]

44

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Mariam Nasoro Kisangi, Mbunge wa VitiMaalum, lenye sehemu (a), (b) na (c), kwa pamoja kamaifuatavyo:

Mheshimiwa Spika, kupitia Wakala wa Huduma zaMisitu Tanzania inasimamia uendelezaji wa msitu naimefanya na kuboresha yafuatayo:-

- Imepima na kusafisha mipaka na kuwekamabango ya kutambulisha eneo hili la msitu.

- Imeanzisha bustani ya miti au mimea(botanical gardens) ambayo itahifadhi uoto wa asili wamaeneo ya Pwani na uhifadhi wa viumbe hai.

- Imeongeza watumishi na vitendea kazi kwaajili ya kulinda na kuhifadhi Msitu huo.

- Ujenzi wa Ofisi umeshaanza kwa ajili yakuanzisha utalii ikolojia na ipo katika maandalizi ya kupandamiti katika mipaka na maeneo ya wazi ili kuboresha uotohuo wa asili.

- Wakala imetenga maeneo mazuri kwa ajiliya ufugaji wa nyuki na kuchimba mabwawa ya samaki.

Kutokana na juhudi zinazofanywa na Wakala, Serikalihaioni umuhimu wa kuzikabidhi Wilaya za Mkuranga naTemeke na kubadilisha matumizi ya Msitu huu. Hii ni kwasababu mpango uliotajwa hapo juu unaonesha nia njemaya Serikali ya kutumia msitu kwa matumizi halali na kwamba,Serikali itawaondoa watu wote wanaofanya ujenzi wakinyemela ndani ya Msitu huo wa Hifadhi.

Mheshimiwa Spika, faida za ziada ambazo Serikaliinapata katika Msitu huu ni zaidi ya uhifadhi wa mazingirakama ifuatavyo:-

45

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

- Eneo la mafunzo ya uhifadhi na utalii ikolojia;kwa mfano, hivi karibuni aliyekuwa Kamanda wa SkautiTanzania, Mheshimiwa Abdulkarim Shah, Mbunge waMafia, aliomba kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misituili waweze kutumia msitu huo kwa mafunzo ya WanaskautiTanzania na sisi tupo tayari kushirikiana na wanaskautinchini.

- Kuanzisha utali i ikolojia ambaoutawashirikisha Wananchi wanaoishi karibu na msitu kwalengo la kuwanufaisha kiuchumi.

- Katika mkakati wa ushirikishwaji, umetengwaUkanda wa Ufugaji Nyuki ndani ya Hifadhi hiyo kwa ajili yashughuli za ufugaji wa nyuki na uzalishaji wa makundi yanyuki na pia kuchimba mabwawa ya samaki kwa manufaaya Wananchi wanaouzunguka Msitu huo.

- Kuanzisha bustani ya miti au mimea(botanical garden) kwa ajili ya kutunza mimea yu miti haiya Ukanda wa Pwani kwa ajili ya utafiti wa mafunzo.

MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali lanyongeza.

Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa NaibuWaziri, ambayo nimeridhika nayo na nimeona ukwelialiyoyasema yanaendelea kutendeka katika eneo hilo,lakini pia nina maswali mawili ya nyongeza.

(i) Kwa kuwa Serikali imeonesha juhudi kubwaya kuendeleza msitu huo na kazi inaendelea na ninaombaiwe endelevu. Je, Serikali haioni sasa kuna haja ya kuanzishamakumbusho ya viumbe hai ili kusaidia Wanafunzi wawezekujifunzia na Walimu waweze kufundishia kupitiamakumbusho hiyo?

(ii) Kwa kuwa walinzi wakuu wa Hifadhi hiyo yaMsitu ni Wakazi wa maeneo ya Mwandege, Vikindu, Churi,

[NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII]

46

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mbagala na Mkuranga kwa ujumla. Je, Serikali inawasaidiavipi Wananchi wa eneo hil i katika kukabiliana nachangamoto zinazowakabili?

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba ujibu kwakifupi sina muda.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaSpika, naomba kujibu kwa ufupi sana maswali mawili yanyongeza ya Mheshimiwa Mariam Kisangi, kama ifuatavyo:-

Kwanza, tunamshukuru sana na tunampongeza kwapongezi ambazo amezitoa, lakini nimhakikishie kwamba,ushauri alioutoa kuhusu makumbusho na mambo ambayoyanaweza yakasaidia Wanajamii na hasa Wanafunzikuendelea kujifunza ni ushauri ambao naupokea.

La pili, jinsi ambavyo tunategemea Wananchiwaendelee kufaidi ikiwa ni pamoja na wale ambaowanashiriki katika kuulinda Msitu huu na kuutunza ni kamanilivyosema awali kwamba, tunawaruhusu kwa mfanoWananchi kushiriki kuweka mizinga ndani ya hifadhi,tunachimba mabwawa ndani ya hifadhi, ambayo tunaaminiyatatumika kama mabwawa ya kutunzia samaki ambaowatawafaidisha Wananchi walio nje ya hifadhi hii naninaamini hii ni sehemu ya ushirikishwaji wa jamii ambao niendelevu.

SPIKA: Mheshimiwa Mchungaji Msigwa, swali fupi!

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika,nakushukuru. Kwa kuwa changamoto hizi za misitu ambayoipo karibu na miji zimeleta shida kidogo kwa wakazi wamijini. Changamoto hii inafanana na Manispaa ya Iringaambayo kuna kitu kinadharia kinaitwa Msitu wa Kilolo,ambao kimsingi haupo. Kwa nini Wizara yako imeendeleakusuasua kuruhusu programu za Manispaa ya Iringaziendelee kufanya kazi katika eneo hili ambalo msitu kimsingihaupo?

[MHE. M. N. KISANGI]

47

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba ujibu kwakifupi!

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaSpika, naomba nijibu swali moja la nyongeza la MheshimiwaMchungaji Msigwa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, tumelipokea hili suala la Msituwa Kilolo, Wizara yangu kupitia kwa Halmashauri husika,kupitia kwa Mheshimiwa Msigwa na kupitia kwa Wadauwengine wa Iringa, wamelielezea sana hili suala. Ninaombanimhakikishie tu Mheshimiwa Msigwa kwamba, tunaendeleakulifanyia kazi hili suala ili tufikie uamuzi ambao ni mwafaka.

Na. 65

Maoni ya Wananchi wa Kiloleni kwa Wizaraya Maliasili na Utalii

MHE. SAID J. NKUMBA aliuliza:-

Wakazi wa Kata ya Kiloleni wamekuwa wakilalamikakuwa na eneo dogo la kilimo na eneo kwa ajili ya mifugo:

Je, ni lini maombi ya Wananchi hawa kwa Wizaraya Maliasli na Utalii yatazingatiwa?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali laMheshimiwa Said Juma Nkumba, Mbunge wa Sikonge,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua Kata yaKiloleni kuwepo katika Wilaya ya Sikonge, Mkoa wa Tabora,ambayo upande wa Mashariki inapakana na Msitu waHifadhi wa Nyahua Mbuga ambayo upande wa Kusiniinapakana na Msitu wa Hifadhi wa Ipembampazi.

48

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Msitu wa Hifadhi wa Nyahua Mbuga una ukubwawa Hekta 679,896 na uliohifadhiwa na Tangazo la SerikaliGN. No. 79 la tarehe 26 Machi, 1954 kwa ramani ya JB 175.Msitu huu unasimamiwa na Wakala wa Huduma za MisituTanzania (TFS) na usimamizi wa kazi za kila siku hufanywa naWataalamu wa Misitu waliopo katika Wilaya ya Sikonge.

Msitu wa Hifadhi wa Ipembampazi una ukubwa wahekta 134,680.0 na ulitangazwa kwa Tangazo la Serikali GN.345 ya tarehe 23 Machi, 1955 kwa Ramani Namba JB 179.Pia msitu wa Ipembampazi unapakana na Msitu waSikonge, ambao ni mali ya Wilaya na unasimamiwa naHalmashauri ya Wilaya ya Sikonge.

Mheshimiwa Spika, umuhimu wa misitu hii ni moja,vyanzo vya maji vya Mito Nkwazi, Malingwe na Chonakutoka Msitu wa Nyahua Mbuga hadi maeneo yatambarare ya Wilaya ya Igunga na Singida. Msitu waIpembampazi ni chanzo cha Mto Uruwa na ni hifadhi yamaji yanayotumiwa na wakazi wengi na mifugo katikaWilaya ya Sikonge. Msitu wa Sikonge ni chanzo cha maji yamabwawa yaliyochimbwa Ulyanyana na Igigwa, kwa ajiliya kilimo cha umwagiliaji na maji ya Mji wa Sikonge.

Maeneo ya Msitu hasa kandokando ya mito, vilimana ardhi chepechepe ni muhimu kuhifadhiwa kwa ajili yakuhifadhi bioanuwai ya aina mbalimbali za miti na mimea,wadudu na hata wanyamapori. Misitu mingi ni mapito yawanyama wanaohama kutoka katika Pori la Akiba laRungwa kwenda Msitu wa Ipembampazi na Mapori yaWembele kwenda Mapori ya Inyonga Mashariki. Pia katikaMisitu hii kuna vitalu vya uwindaji wa kitalii na kienyeji. Misituhii ni muhimu kwa uvunaji wa mazao ya misitu na ni eneonyeti kwa ufugaji wa nyuki na kuzalisha asali na nta ya mitiya miombo.

Mheshimiwa Spika, mwisho, usimamizi wa Misitu yaHifadhi ya Mkoa wa Tabora ikiwemo hii ya Wilaya yaSikonge, imekuwa na changamoto nyingi hasa za uvamizi ilikupisha shughuli nyingine za kibinadamu ambazo kwa kiasi

[NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII]

49

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kikubwa, zimeathiri sana ubora na hadhi ya misitu husika.Hivyo, Wizara inatoa wito kwa Wananchi wote, kujiepushana suala la kuomba kumega maeneo ya misitu iliyohifadhiwakwa umuhimu wa hifadhi za maji na bioanuwai, kwa kuwakuendelea kuharibu misitu kutasababisha janga kubwa laugomvi wa maji kama tunavyoshuhudia baadhi yamigogoro iliyopo kati ya wafugaji na wakulima.

MHE. SAID J. NKUMBA: Mheshimiwa Spika, pamojana majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina swali dogomoja la nyongeza.

Kwa kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa laWananchi katika maeneo hayo ya Mipaka ya Hifadhi naVijiji; maana mipaka mingine imewekwa kabla ya Uhuru,lakini kwa kuwa maeneo mengi nchini yenye Mipaka yaHifadhi na Vijiji, mengine yalishapoteza kabisa hadhi yahifadhi na ongezeko la Wananchi kama nilivyosema. Je, nikwa nini sasa Wizara isingekuwa na utafiti wa kina wauhalisia katika maeneo yote nchini ambayo yanapakanana Hifadhi hasa kwenye Vijiji ili kuwahakikishia Wananchiambao wamekaa wengine wanahangaikia ardhi na ardhiipo ambayo imeshapoteza hadhi ya kuwa Hifadhi?

SPIKA: Naomba ujibu kwa kifupi sana, maana jibulako lilikuwa refu mno!

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: MheshimiwaSpika, kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, naombanijibu swali la Mheshimiwa Nkumba, kwa ufupi kamaifuatavyo:-

Moja, tunakubaliana sana na Mheshimiwa Mbunge,kwa hoja yake ya kuwakilisha Wananchi hasa changamotohii tunayoiona ya ufinyu wa ardhi ambayo imeyagusamaeneo mengi sana nchini.

La pili, ni maslahi mapana ya uhifadhi na masilahimapana ambayo nchi yetu na vizazi vijavyo ni lazima vijevikute misitu hii ambayo sisi tumepewa wajibu wa kuitunza.

[NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII]

50

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Ningeomba tu kusisitiza kwamba; kwanza, lazimatutengeneze matumizi bora ya ardhi sehemu zote nchini ilimaeneo ambayo yametengwa kama Hifadhi yaendeleekubaki kama Hifadhi na yana faida lukuki ambazo kwa kwelisina haja hata ya kuzieleza hapa. Naomba kusemakwamba, Wizara yangu itashirikiana na Mheshimiwa SaidJuma Nkumba, yeye mwenyewe, ikiwa ni pamoja na sisikufika kuangalia haya maeneo, lakini tuhakikishe kwamba,maeneo yote ambayo yana migogoro inayofanana na hiiyanapatiwa ufumbuzi endelevu.

Na. 66

Raia wa Kigeni Kuzagaa Maeneo ya Vijijini

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU aliuliza:-

(a) Je, ni sababu zipi zinazopelekea raia wakigeni kuzagaa hovyo katika maeneo ya vij i j ini nakushindania fursa kibiashara na wazawa?

(b) Je, kwa nini Serikali isiamuru raia hao kubakikatika maeneo ya miji mikuu tu?

NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NAMICHEZO (K.n.y. NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YANCHI) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mamboya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali la MheshimiwaMurtaza Ally Mangungu, Mbunge wa Kilwa Kaskazini, lenyesehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kuna sababu mbalimbalizinazowafanya raia wa kigeni kuingia nchini. Sababu hizi nikama vile uwekezaji, wafanyakazi wa mashirika yamaendeleo na wategemezi wao (wanafamilia),wanaojitolea (volunteers), watalii na kadhalika.

[NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII]

51

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Spika, sababu kubwa ni Sera ya Taifaya Uwekezaji inayoruhusu mgeni kuingia nchini, kuwekezamtaji wake katika eneo analoona atapata maendeleo yaWananchi wake. Eneo hilo linaweza kuwa mjini au kijijini,kutegemea ilipo fursa hiyo na ambayo huwa imetajwa naSerikali katika Mkoa husika kwa kutumia Kamati za Ushauriza Mkoa.

Mheshimiwa Spika, kwa makundi mengine yawageni kama Wafanyakazi wa Mashirika ya Maendeleo,huombewa Vibali Maalum kutokana na shughuliwanazokwenda kufanya.

Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hiikumwomba Mheshimiwa Mbunge na Wananchi kwa ujumla,kutoa taarifa za raia yeyote wa kigeni anayezagaa nchinibila kibali kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ili hatua stahikiza kisheria zichukuliwe dhidi yake.

Mheshimiwa Spika, Serikali haijaamuru raia wa kigenikubaki mijini, kwa sababu Sera ya Uwekezaji iko wazi kuhusufursa za uwekezaji zilizopo na aina ya uwekezaji unaohitajika.Hivyo, raia wa kigeni anapokidhi matakwa ya uwekezajinchini, huwekeza ilipo fursa hiyo, iwe kijijini au mjini, kwa kuwania ya Serikali ni kusambaza maendeleo na uwekezaji nchinzima.

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Spika,nashukuru.

(i) Ninapenda kujua Sera hii ya Uwekezajiimeundwaje kiasi kwamba haifanyiwi uhakiki kwa mitaji yauwekezaji kwa wawekezaji hao kutoka nchi za nje kamamfano wa nchi zote duniani ikiwemo China, Marekani, HongKong na kadhalika. Imefikia hatua wafanyabiashara haowanaoitwa wawekezaji, wameingia kwenye biashara yauuzaji bidhaa (trading), wamefungua maduka; huu niuwekezaji wa aina gani? (Makofi)

[NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO]

52

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

(ii) Kazi ya ulinzi na usalama wa kulinda mipakayetu ni jukumu la Vyombo vya Dola, leo hii Wananchiwatawezaje kujua raia huyu wa kigani amepewa kibali chaaina gani! Hii inaonesha ni kiasia gani ambavyo Serikali sasainataka kukwepa majukumu na kurudisha jukumu hili kwaWananchi!

Sasa tamko la Serikali ni lini uhakiki wa wageni haoutafanywa kwa sababu sasa hivi kuna operation yakuwaondoa wageni ime-base zaidi kwa raia wa kigeni wanchi zinazotuzunguka, hao wanaotoka mbali kwenyeMabara mengine kwa nini wanaachwa wanazagaa hovyo?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (UWEKEZAJINA UWEZESHAJI): Mheshimiwa Spika, napenda kumshukurusana Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa kujibu maswali vizurisana na mimi naomba niongezee hasa kwa kujibu swali hilila pili.

Mheshimiwa Spika, kufanya biashara siyo uwekezaji,uwekezaji ni kwenye kilimo, viwanda na maeneo mengineya uzalishaji.

Pili, unapotaka kufanya biashara ni lazima uwe naleseni ya biashara na unapofanya mambo bila leseni yabiashara ni kosa. Kuna mamlaka zinazotoa leseni, ninahakika mamlaka hizi zinajua masharti na utaratibu wa kutoaleseni. Kwa hiyo, kama kuna wageni ambao wanafanyabiashara bila utaratibu hayo ni makosa.

La pili, uwekezaji wowote ni lazima ulete masilahikwenye nchi ambayo inapokea wawekezaji. Inabiditujipange vizuri, wawekezaji wanapotoka nje hata wale wandani, wanachotafuta ni faida kwa mtaji wanaowekeza.Vilevile nchi na Wananchi tujue sisi tunapata manufaa ganina faida gani na kwa hiyo, swali la Mheshimiwa Mbunge nila manufaa makubwa kwamba ni lazima tufanye kila wakatina kuona tunapata manufaa gani.

[MHE. M. A. MANGUNGU]

53

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Kwa hivyo, Kituo cha Uwekezaji Taifa (TIC) tunakipamaelekezo kifuatilie wawekezaji wote kuona kwamba,mikataba inafuatwa na pili yale manufaa tuliyokuwatunayategemea tunayapata ili tuweze kujifunza kwauwekezaji unaokuja na tuchukue hatua stahil i kwawawekezaji waliopo ambao hawawekezi kwa mujibu wamkataba ambao umewekwa.

Mheshimiwa Spika, ahsante.

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu ya sehemuya kwanza.

NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NAMICHEZO: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mamboya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali la MheshimiwaMurtaza Mangungu, sehemu (a).

Kwanza nimshukuru Waziri wa Nchi, Ofisi ya WaziriMkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji kwa maelezo mazuri. Hatahivyo, niseme tu kwamba, Sera hii ya Uwekezaji imeundwamwaka 1996 na Sheria yake ya mwaka 1997 na imeelezakwamba, wawekezaji raia wa nje wanapitia TIC (TanzaniaInvestment Centre) wanapata vibali na pia wanapata Hatiya Ukaazi ya Daraja A pale wanapotimiza vigezo kupitia Kituocha Uwekezaji (TIC).

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naona maswaliyamekwisha na leo tuna muda mchache wa kufanya kazizetu. Kwa hiyo naomba niwatambue wageni walioko hapaambao ni:

Wanamichezo 50 kutoka Halmashauri ya Wilaya yaMbozi, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Mheshimiwa Erick Minga (Diwani) pamoja na MakamuMwenyekiti, Mheshimiwa Allan Mgula. Naomba walipowasimame. Ahsante sana. (Makofi)

Tunao pia Madiwani 20 kutoka Halmashauri ya Wilayaya Chunya, wakiongozwa na Mheshimiwa Makamu

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI]

54

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo anaitwa Mheshimiwa BoscoMwanginde. Wako wapi hawa Waheshimiwa Madiwani?Ahsante, karibuni Waheshimiwa Madiwani. (Makofi)

Tuna wanamichezo 45 kutoka Halmashauri ya Wilayaya Kyela, eeh naomba wanamichezo kutoka Kyelawasimame kama wako ndani. Nafikiri watapata mudabaadaye.

Kuna wanamichezo 32 kutoka Wilaya ya Biharamulowakiongozwa na Afisa Utamaduni wa Wilaya, Bi. Esther Abel,wako wapi? Wanasema ni watumishi, nil idhani niwanamichezo. Nadhani nao pia wamekosa nafasi humundani.

Pia tunao vijana 13 kutoka Makete wakiongozwa naNdugu Erasto Mahenge ambaye ni Mwenyekiti wao, wakowapi hawa? Aah, ahsante. Karibuni sana. (Makofi)

Shughuli za kazi; Makamu Mwenyekiti wa Kamati yaBunge ya Huduma za Jamii, Mheshimiwa Steven Ngonyani,anaomba niwatangazie Wajumbe wa Kamati yake kwamba,leo Saa 7.00 mchana watakuwa na Kikao pale basement.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwandana Biashara, Mheshimiwa Mahmoud Mgimwa, anaombaniwatangazie Wajumbe wa Kamati yake kwamba, leo Saa7.00 mchana watakuwa na kikao katika Ukumbi wa PiusMsekwa ‘B’.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria naUtawala, Mheshimiwa Dkt. Pindi Chana, anaombaniwatangazie Wajumbe wa Kamati yake kwamba, leo Saa7.00 mchana watakuwa na kikao katika Ukumbi Na. 231.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama,Mheshimiwa Anna Abdallah, anaomba niwatangazieWajumbe wa Kamati yake kwamba leo Saa 7.00 mchanawatakuwa na kikao katika Ukumbi Na. 219.

[SPIKA]

55

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo yaJamii, Mheshimiwa Jenista Mhagama, anaombaniwatangazie Wajumbe wa Kamati yake kwamba, leowatakuwa na kikao cha pamoja na Kamati ya Hesabu zaSerikali za Mitaa (LAAC) kujadili mchango wa Serikali katikaMfuko wa Akinamama na Vijana katika Serikali za Mitaanchini, kitakachofanyika Saa 7.30 mchana katika Ukumbi waMsekwa. Mtajua huko huko maana Msekwa ziko nyingi.(Makofi)

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu,Mheshimiwa Peter Serukamba, anaomba niwatangaziewajumbe wa Kamati yake kwamba, leo Saa 7.00 mchanawatakuwa na kikao katika Ukumbi Na. 227.

Wengine hawakuchapa matangazo yao, nitayasomakama yalivyo, lakini siku nyingine wachape.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoana Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mheshimiwa Dkt. KhamisKigwangala, anaomba niwatangazie Wajumbe wa Kamatiyake watakaopenda kuhudhuria kikao hiki wafike bila kukosa.Kikao kitafanyika Saa 7.00 mchana katika Ukumbi wa Msekwabaada ya kuahirisha shuguli za Bunge. Sasa hapa kunaKamati mbili zinakutana Ukumbi wa Msekwa, kwa hiyo,muangalie mtakavyogongana na kuamua wenyewe hukohuko.

Kiongozi wa Kambi ya CUF, Mheshimiwa Rashid AliAbdallah, anaomba niwatangazie Waheshimiwa Wabungewa CUF kwamba, watakutana leo Saa 10.00 jioni palebasement.

Halafu nina matangazo kutoka kwa Mwenyekiti waBunge Sports Club, Mheshimiwa Iddi Azzan, anaombaniwatangazie matokeo ya mchezo wa kirafiki uliofanyika sikuya Jumamosi wa Mpira wa Miguu na Mpira wa Pete. Kwa

[SPIKA]

56

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

upande wa Mpira wa Miguu, Bunge Sports Club walipatagoli moja dhidi ya Travel Ports ambao walipata sifuri (0). Golila mchezo huu lilifungwa na Mheshimiwa Dkt. KhamisKigwangala na nyota wa mchezo alikuwa Sadifa JumaKhamis. (Makofi)

Mpira wa Pete, Bunge Sports Club walifunga magoli24 dhidi ya Mahonda Queens kutoka Zanzibar waliopatamagoli manne (4). Nyota wa mchezo alikuwa MheshimiwaEugen Mwaiposa. (Makofi)

Aidha, Waheshimiwa Wabunge mnaombwakuhudhuria mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya Michezo yaMabunge ya Afrika Mashariki, yatakayofanyika mweziDesemba nchini Uganda. Kwa hiyo, nawapongeza hawaWachezaji nyota na wengine mshiriki kama tulivyosema,mashindano ya Afrika Mashariki yanakuwa magumu, kwahiyo, mfanye vizuri ili safari hii mrudishe kikombe. Mwaka janatulirudisha cha Netball tu, mwaka huu mjitahidi mrudishevikombe vyote. (Makofi)

Baada ya kusema hayo, Mheshimiwa Said Nkumba!

MHE. JUMA S. NKUMBA: Mheshimiwa Spika,nimesimama kwa mujibu wa Kanuni ya 68(7) inayosema:“Halikadhalika Mbunge anaweza kusimama wakati wowoteambapo hakuna Mbunge mwingine anayesema na kuombaMwongozo wa Spika, kuhusu jambo ambalo limetokeaBungeni mapema ili Spika atoe ufafanuzi kama jambo hilolinaruhusiwa au haliruhusiwi kwa mujibu wa Kanuni”.

Mheshimiwa Spika, ni juzi tu Waheshimiwa Wabungena Bunge lako Tukufu lilijadili kwa kina suala la dharura juu yauonevu ambao wamefanyiwa wananchi wetu katikamaeneo mbalimbali kuhusiana na Operesheni Tokomeza.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo jana na juzi Waziri waMaliasil i na Utali i, Mheshimiwa Khamis Kagasheki

[SPIKA]

57

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ameonekana akinukuliwa kwenye vyombo vya habariakisema kwamba, Wabunge wanasema sema tu ndani yaBunge, lakini hawajali rasilimali za Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vile vile Mheshimiwa Waziriamesema kwamba hatishwi na maelezo ya Wabunge yakumtaka ajiuzulu na yeye hatoki mpaka maamuzi ya Raisaliyemteua. Sasa kwa kuwa yeye mwenyewe MheshimiwaWaziri ndiye aliyetoa kauli ya kusitisha operesheni hii Tokemezana kitendo cha kuwakamata Wachina ni zoezi tu la Serikalila kila siku ambalo linaweza likaendelea bila operesheni.(Makofi)

Je, Mheshimiwa Waziri aliyetoa kauli ndani ya Bungena anatoka nje anabeza maamuzi ya Bunge, anakejeliBunge, naomba Mwongozo wako kama jambo hil ilinaruhusiwa. (Makofi)

SPIKA: Waheshimiwa mmesimama kwa ajili ya nini?Hakuna, kufanyaje!

MJUMBE FULANI: Mwongozo!

SPIKA: Aah, tusiwe na Mwongozo, Mwongozo tu kilawakati.

Alichokisema Mheshimiwa Nkumba nadhani ni sualaambalo ningependa kusiwe na matumizi mabaya yamidomo, kwa sababu tukishakubaliana hapa, kwenda tenakusema vitu vingine ni kuwasha moto pale ambapo pengineulikuwa unaendelea kuwaka vizuri. Nadhani ni matamkoambayo siyo makini. Tuendelee.

Si nimeshatoa Mwongozo. (Makofi)

Tuendelee Katibu!

[MHE. JUMA S. NKUMBA]

58

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

HOJA ZA SERIKALI

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo yaTaifa kwa Mwaka 2014/2015

(Majadiliano Yanaendelea)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunao wachangiajiwengi, lakini itabidi mjadala huu ufungwe leo. Sasa wenginewatapata nafasi na wengine hawatapata. Ingependezasana kama tusingekuwa tunajirudia rudia kwa sababu kamatukij irudia rudia Kanuni inasema ikifika mahali watuwanajirudia rudia tena ndiyo inakuwa mnafunga mjadala.Kwa hiyo, nitakuwa na wasemaji wafuatao;

Kamati ya Mipango, jamani naomba tusimameKamati ya Mipango, nimesahau.

(Hapa Wabunge walikaa kama Kamati ya Mipango)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, naombatukae. Samahani! Nilikuwa nasema leo ndiyo siku yetu yamwisho, kwa hiyo, naomba wachangiaji wafuataowajiandae. Nitamwita Mheshimiwa Stephen Ngonyani,Mheshimiwa Dkt. Kebwe Stephen Kebwe, MheshimiwaHerbert Mntangi na atakuwepo Mheshimiwa Naomi Kaihula.

Tuanze na hao kwanza halafu tutaendelea.Mheshimiwa Stephen Ngonyani!

MHE. STEPHEN H. NGONYANI: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza nianze kwa kukushukuru sana kwa kunipa nafasi ilikuchangia huu Mpango wa Maendeleo. Nianze kwakuipongeza Serikali kwa kazi nzuri ambayo wameshaanzakutuonesha, lakini vilevile nilikuwa na mapendekezo yanguambayo nataka Serikali iyaone katika huu Mpango ambaotunaujadili leo wa mwaka 2014/2015.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri Serikali ingemaliziampango wa mwaka 2012/2013. Hii ingetusaidia sana kuujadili

59

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mpango wa 2014/2015 kwa sababu mambo mengiyamejadiliwa hapa, lakini hakuna hata moja ambalolimeanza kufanyiwa kazi. Kwa mfano, Mkoa wa Tanga, naonaumesahaulika kabisa. Kuna bandari ya Tanga ile yaMwambani inajadiliwa kila siku, lakini kutenda kwake inakuwani ngumu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna bandari ya nchi kavupale Korogwe, alikuja Waziri kutoka Uganda akaunganahapa na Waziri wa Uchukuzi, tukaenda mpaka Korogwe,wakatupa maneno mazuri tukafikiria kwamba Serikali sasaimeamua kuwa na utendaji mzuri wa kazi. Cha kushangazampaka leo imekuwa kama ni hadithi, hakuna chochotekinachoendelea katika Mkoa wa Tanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii tunajadili tu hapa reliya kati, lakini ukichunguza si reli ya kati peke yake, hata reliya Tanga - Arusha ilikuwa imeanza muda mrefu. KatikaMpango huu kuna mkakati gani wa kutengeneza hii reli? Kwasababu reli ya Tanga – Arusha – Musoma ni muhimu sana,ndiyo maana barabara hizi hazidumu, zinaharibika kilawakati. Ningeishauri Serikali huu Mpango wa mwaka 2014/2015 hebu tumalize kwanza haya ambayo tumeshayaanziakazi, ingetusaidia sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii tunasema KilimoKwanza, hiki kilimo kwanza tunampelekea nani? Kamawananchi wa Mkoa wa Tanga hawana mahali pa kulima,hiki Kilimo Kwanza kinakwenda wapi? Tunazungumziamashamba ambayo hayaendelezwi. Leo tunaomba Serikalimshughulikie masuala ya mashamba ambayo wananchiwengi wanataka kulima, lakini wakalime wapi, wakatiwakilima huku wanapambana na wafugaji na ambao woteni wakulima? Wakilima huku wanapambana na wenyewemashamba, wakilima huku wanapelekwa Polisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipenda sana Serikaliyangu ya Chama cha Mapinduzi, lakini hili tungelifanyia kazikwanza, kwa sababu tunayaongea hapa kila siku natunayaachia hapa hapa, tukirudi hakuna anayekwenda

[MHE. S. H. NGONYANI]

60

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kumuona Mbunge akihukumiwa na wananchi ambayeataweza kumsaidia, kila mmoja anabeba mzigo wake. IliSerikali ionekane inafanya haya mambo makubwa,ningeomba yale mambo ambayo tulikuwa tumeshayaanzayafanyiwe kazi rasmi ili wananchi waipende Serikali yao kamasasa hivi tunavyoipenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inaniuma sana, tumejadilimambo mengi sana hapa, lakini yanaishia ndani ya Bunge,hakuna chochote ambacho kinaendelea. Leo tunakwendakujadili ya mbele wakati ya nyuma hatujayafanya? Hivi kunamtu kweli anaweza kukuelewa huko nje? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeomba, kama kweliSerikali inatupenda hasa Mkoa wa Tanga, wasimamiekwanza bandari ya Tanga, bandari ya nchi kavu, wasimamiekiwanja cha ndege cha Tanga. Kiwanja cha ndege chaTanga katika Mpango huu hakimo. Nimeona viwanja chungunzima lakini kiwanja cha Tanga hakina maana, kwani ndegehazitui? Kwani wananchi wa Tanga hawataki ndege? Kwaniwananchi wa Tanga hawataki kusafiri kwa ndege? Naombakwanza haya yasimamiwe, yakisimamiwa haya sisi sotetutakuwa tunaiunga mkono mia kwa mia Serikali yetu yaChama cha Mapinduzi, lakini kinyume cha hapo tutakuwatunajidanganya, tutakuwa tunajidanganya sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana Serikali sikivuya Chama cha Mapinduzi, hebu yale mashamba ya kuleKorogwe ambayo hayaendelezwi, ambayo wananchi kulewanasumbuliwa wapewe wananchi wafanye kazi. Yalemashamba ya chai, wakulima wa chai mpaka leo hiiwanakatwa sh. 200 kila wanapokwenda kuongea na Serikaliwakiomba zile fedha wanazokatwa ziongezwe, haziongezwi.Sasa leo hii tunaposema maendeleo ya miaka mitano ni yapikama mkulima analima shamba lake, analiandaamwenyewe, anavuna chai lakini kwenye kulipwa halipwi zilefedha zinazotakiwa? Tutakuwa tunawasaidia wakulimakweli? (Makofi)

[MHE. S. H. NGONYANI]

61

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi binafsi nimefurahiasana mipango hii, lakini sisi ni wepesi sana wa kuandaamipango mizuri, lakini wanaofaidi ni wananchi wa nchinyingine. Kuna nchi jirani imechukua mipango kutokaTanzania, leo hii imetushinda. Nchi jirani tu! Yaani sisi ni wepesiwa kupanga mambo, lakini wanaofaidika ni nchi za jirani,kwanini tusianzie kwetu? Kuna kizuizi gani hapa? Rais tunayemsafi, Mawaziri ni hao wazuri, hakuna tatizo hawa watendajiwa chini nyie mnawaachia wa nini? Kwa sababu kamawatendaji wa chini mnawaachia wanafanya wanavyotakamatokeo yake ndiyo haya lawama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali ya Chamacha Mapinduzi, hebu tumalizeni mipango ya mwaka 2012/2013; wananchi wa Mombo wapate mashamba, wananchiwa Mkoa wa Tanga, yale mashamba ya mkonge ambayohayaendelezwi wagawiwe, mashamba ya misufi kuleKorogwe ambayo yamekaa kwa muda mrefu hayana mtuwapewe wananchi, mashamba ya chai ambayo wananchiwanalima kila siku wanakatwa fedha yao walipwe. Nafikirihili litakuwa ni wazo zuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nisiwachoshe, kwa hayamachache, naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana, Mheshimiwa Dkt. Kebwe!

MHE. DKT. KEBWE S. KEBWE: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia Mwongozowa Mpango wa mwaka 2014/2015.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninayo maelezo machacheya kilio ya utangulizi kabla sijakwenda katika hoja. NaiombaSerikali sikivu ya Chama cha Mapinduzi, katika dharuraambayo imetokea katika Jimbo la Serengeti kuna ukameambao haujawahi kutokea zaidi ya miongo mitatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukame huu hauna tofautina uliotokea Ngorongoro na Monduli mwaka jana au mwakajuzi. Kwa hiyo spell hii ambayo imeingia Wilaya ya Serengeti

[MHE. S. H. NGONYANI]

62

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

imesababisha upungufu mkubwa wa chakula. NaombaSerikali, Wanaserengeti tuna asili ya kulima, hatujawahikuomba chakula Serikalini, lakini katika mazingira hayayaliyopo, tunaomba chakula kiende, wananchi wauziwe kwabei ya chini, bei nafuu kuliko ilivyo hivi sasa ambapo debemoja la mahindi ni sh. 18,000 hadi 20,000, bei ambayo kwakweli ni ghali sana kwa wananchi wa kawaida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, si hilo tu, kukithiri kwa temboambao wanazunguka. Kuna kundi la tembo zaidi ya 50wanaranda randa katika vijiji zaidi ya 20 ambavyo viko kandokando ya hifadhi. Wiki iliyopita katika Kata ya Isenye, Kijiji chaIharara waliua ng’ombe na madhara mengine makubwayanatokea, kama jana nimepata taarifa katika Kijiji chaIsarara, Kata ya pale Kisangura. Mazingira yote hayayanasababisha upungufu mkubwa sana wa chakula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hoja nimepitia kitabuchote, kurasa zote ambacho kinapungua, naomba Mipangowaitazame kwa makini, kwa sababu unavyokuwa namwongozo ni lazima kuwe na vital statistics kuoneshakwamba ulifikia wapi katika kiwango cha maendeleo navigezo vingine. Hata UNDP katika vigezo vya maendeleohuwezi kukosa vital statistics ikiwemo umri wa kuishi, vifo vyaakinamama na watoto. Vigezo kama hivyo ni vizuri vinakuwakatika utangulizi ili unavyojielekeza katika kutengenezaMpango, unajielekeza kupunguza vifo kwa kiwango kipi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia ijaribu kuangaliamwongozo huu unatwambia kweli pato la Taifa limekua.Uzani wa kipato cha kila Mtanzania kutoka 800,000 kwenda1,000,000 ina-sound vizuri katika masikio, lakini je, tafsiri yakeiko wapi kwa wananchi wa kawaida. Kwa hiyo, kukua kwaPato la Taifa kuendane na uhalisi wa maisha, maisha yanazidikuwa makali kwa Watanzania wengi. Kwa mfano,tunaposema per capital imekwenda kwa milioni 1,000,000,hivi tafsiri ya yule mwananchi wa Serengeti anaitafsiri vipina kiwango cha maendeleo hiki yeye anaona vipi?Angependa aone kwamba huduma za jamii anazipata kwaurahisi kadiri anavyohitaji.

[MHE. DKT. K. S. KEBWE]

63

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia Mipango ambayoinajichomoza kwa mfano, BRN; BRN katika Mpango wa MiakaMitano ambayo tuna –operate kwenda kwenye OperationalPlans haikuweko. Kwa hiyo, ni vizuri ku-harmonize BRN naMipango mingine ambayo tayari ilishakuwa documentedkwenye Five Year Plan. Katika miaka mitano mitano hiikwenda katika miaka 15 kwa maana ya 2025, hainareconciliation. Kwa hiyo, ni vizuri kuwe na uwiano mzuri ku-capture miradi kama hii na hii inatupa historia ya nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni vizuri tujifunze,mara nyingi tunapanga mipango, lakini dharura zinakuwanyingi, katika Mipango vitu viwili lazima viangaliwe; disciplineya matumizi ni lazima iangaliwe na hapa ndio pale sasatunaambiwa TRA wamekusanya, wamezidi malengo, lakinisasa utekelezaji wa mipango haupo, kwa sababu hakunadiscipline ya matumizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine katika kupangamipango ni vizuri mipango ile ambayo ni ya maendeleo izidiile ya matumizi ya kawaida. Isiwe historia ya nchi yetutunasema mipango kila mwaka, lakini inakuwa ni bajeti yakutafuna, bajeti ya kula, bajeti ya matumizi. Kwa sababurecurrent inakuwa ni kubwa kuliko development expenditure,kwa njia hiyo hatuwezi kuendelea.

Mheshimiwa Spika, lakini ambacho tunakiona namara nyingi Bunge hili tumepigia kelele suala la usimamizi, sizuri, tujaribu kuangalia mipango ambayo inajichomoza kwakila mwaka, kunakuwa na viporo vingi, kwa sababu ya halihalisi ya usimamizi, mipango haiendi vizuri. Pia ile value formoney katika miradi, tukipita katika maeneo mbalimbali kwamfano, na-declare interest nipo katika Kamati ya TAMISEMI,tumepita katika maeneo mengi ya Wilaya na Mikoa, viporovya miradi ni vingi mno. Kwa hiyo, nashauri katika Mwongozohuu wa Mpango ambao tunakwenda kuandaa 2014/2015kusiwe na miradi mipya, ni vizuri tujikite katika miradi ambayoipo ili tuweze kuikamilisha ili twende katika miradi mingine.

[MHE. DKT. K. S. KEBWE]

64

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Spika, lakini pia mipango ambayotumeisikia siku nyingi tangu miaka ya 60 katika awamu yakwanza ni vizuri sasa iende kwa vitendo. Mara nyingitumeambiwa kuna upembuzi yakinifu, kuna mikakatiinaendelea, tupo mbioni, suala la reli ya kutoka Tanga-Arushampaka Musoma limekuwa ni wimbo na umezoeleka kwaWatanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ni vizuri wakatiMheshimiwa Waziri anahitimisha atwambie kuna mpangogani kuhusu reli ya Tanga-Arusha- Musoma. Si hilo tu katikauwanja wa ndege ambao ulikuwa umepangwa kurahisishausafiri katika nchi na nchi nyingi duniani ndivyowanavyofanya, uwanja wa pale Musoma umechoka,umechakaa na ni mdogo na upo katikati ya Mji. Kwa hiyo,ni vizuri kujenga uwanja mwingine mpya, uwanja mkubwaambao utarahisisha usafiri katika Kanda ya Ziwa na hataMaziwa Makuu na kurahisisha utalii kwenda Serengeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika juhudi ambazoWilaya ya Serengeti tumefanya kujenga uwanja wa ndegeunder PPP na huyu mdau wa Grumet Reserve, ni vizuri Serikaliiunge mkono kama ambavyo imeanza kwa kutoa kibali kwabajeti ili kusudi kazi hii iende vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunamshukuru huyuMwekezaji tayari ameishatoa bilioni tano zipo kwenye Boditunangoja kibali cha Serikali. Kwa hiyo Wizara ya Mazingiratunaomba tupate kibali haraka na mipango ioneshekwamba PPP tunajenga vipi ule uwanja ili uweze kwishamapema iwezekanavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata Mheshimiwa Rais maranyingi tukikutana akitembelea kule Serengeti anaulizatumefikia wapi. Kwa hiyo, ni vizuri suala hili ambalo litafunguasasa utalii katika Maziwa Makuu na hususan Western Corridorya Serengeti tuweze kupata uwanja huo. Nina hakika hiyo nikengele ya kwanza.

[MHE. DKT. K. S. KEBWE]

65

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Spika, suala la mchango wa utalii katikanchi yetu katika Pato la Taifa ni kidogo sana. Hatuwezi kubakina wimbo kwamba Tanzania tuna vyanzo vizuri vya kitalii, ninchi ya pili duniani badala ya Brazil. Sasa wimbo huu ni fursa,unatusaidia vipi? Kwa mfano, Pato la Taifa tunavyosematumekwenda mpaka asil imia 17.2 ya income, badohatujafanya chochote kwa vyanzo hivi ambavyo tunavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, utalii wa ndanihatuja-capture vizuri kwa takwimu ambazo tunazo, ni asilimiambili tu ya fursa ambayo tunaipata katika utalii wa ndani.Sehemu hii tuifungue vizuri tuachane na kero ambazozinasababisha kuongeza kodi. Kwa mwaka jana tulipigakelele sana, lakini Serikali ikalazimisha kupitisha viwango katikamageti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa bahati mbaya sasa hililina-operate katika Mbuga ya Serengeti tu, hususan WesternCorridor upande wa Mashariki kule kuna Ngorongoro ambayoni Mamlaka, hawana viwango hivi, viwango hivi vilikuwa sh.1,500, lakini ghafla vikaenda mpaka sh. 10,000 na tukapigakelele katika Bunge lililopita, ikaenda kwenye sh. 5,000. Hatahivyo, sh. 5,000 kutoka 1,500 ni mzigo mkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Mkuualivyotembelea kule Serengeti katika Maadhimisho ya Bondela Mto Mara ambako nchi ya Kenya na Tanzaniatunashirikiana tulimweleza kuhusu suala hili. Kwa hiyoningependa Serikali isitishe viwango vile mara moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishukuru Wizara yaMaliasili na Utalii wakati nachangia wakati wa Bajeti nilitoaonyo ambalo Wanaserengeti walinituma kwambahatutaweza kuunga mkono bajeti ya Wizara kama itakuwana mazingira hayo ambayo ni kandamizi kwaWanaserengeti.

Mheshimiwa Spika, kwa suala nzima ambaloWanaserengeti wamenituma, ni namna gani viwango vileambavyo Serikali inawatoza viondoke kwa sababu wewe

[MHE. DKT. K. S. KEBWE]

66

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

upo ndani Wilaya, unasafiri kwenye Wilaya yako halafu badounatozwa, kwa kweli hata haiingii akilini.

Mheshimiwa Spika, kwa kumaliza suala zima lamipango upande wa afya ni vizuri tuanze kutazama,mtazamo wa dunia ulivyo. Kwa sababu tunavyokuwa naVituo hivi vidogo vingi inakuwa ni too costly na kada zilewakati mwingine ukienda nazo unakuta kwamba hatamahitaji ya dunia sehemu zingine ukienda hawa Madaktari...

(Hapa Kengele ya pili ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante naona kengele imelia.

MHE. DKT. KEBWE S. KEBWE: Mheshimiwa Mwenyekiti,nitaongeza kwa kuchangia kwa maandishi. Nashukuru sana.(Makofi)

SPIKA: Haya nashukuru. Nilimwita Herbert Mntangiatafuatiwa na Mchungaji Natse, halafu atafuatiwa naMheshimiwa Mtutura Abdallah Mtutura na Mheshimiwa RajabMohamed ajiandae.

MHE. HERBERT J. MNTANGI: Mheshimiwa Spika,naomba nikushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangialeo katika Mpango huu wa Bajeti inayokuja mwaka 2014/2015. Nianze kwa kusema yafuatayo:-

Kwanza, tathmini ambayo imefanywa ya utekelezajiwa Mpango uliopita inaonesha upungufu katika maeneoyafuatayo:- Kwanza, miradi mingi haijakamilika na ipo nyumaya wakati, kwa sababu zifuatazo:- Moja, ni kwambakumekuwa na matatizo ya upatikanaji wa fedha katikautekelezaji wa miradi hiyo. La pili, kuna taratibu hizi zamanunuzi zimekuwa pia zikichangia kucheleweshautekelezaji wa miradi hiyo mikubwa. La tatu, kumekuwa naucheleweshaji wa tathmini ya malipo ya fidia. Sasa kama

[MHE. DKT. K. S. KEBWE]

67

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

tathmini ya Mpango uliopita inaonesha upungufu huumkubwa nini maandalizi yetu ya kuondoa upungufu huo iliMpango huu unaokuja kwa hakika uweze kutekelezwa vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini katika Mpangounaokuja una kitu kinachoitwa Big Results Now (BRN) kamahuu tuliouona upungufu katika Mpango uliopitahatutauchukulia hatua ni wazi kabisa Mpango wetu wa BRNhautafanikiwa badala ya kuwa Big Results Now utakuwa BigFailure Now. Sasa lazima tujipange vizuri, lazima tutumiehekima na busara, tujipange vizuri tufanye kazi itakayoletamaendeleo mazuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa wenzetu wa Zambiawametengeneza bomba la mafuta kutoka Dar es Salaammpaka Zambia, sisi Watanzania tulikuwa na Mpango wakujenga bomba la mafuta kutoka Dar es Salaam mpakaMwanza ambapo ingesaidia sana katika kupunguza bei yamafuta kwa watumiaji wadogo. Mpango huu umezimwa.Sasa hivi kweli kama tunataka kupunguza gharama kwa ninihaturejeshi mpango huo ili kuchangia katika kupunguza beiya mafuta kwa watumiaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mapendekezo yangu nikuurejesha upya mpango huo wa ujenzi wa bomba la mafutakutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza ili vile vile kupunguzaathari kubwa ambazo tunapata sasa ya magari makubwayanayobeba mafuta kutoka Dar es Salaam na kuendeleakuharibu barabara zetu, kwa nini mpango huu hatuutekelezi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzetu Kenya wamejengapipeline yao na wameshirikiana na Uganda. Sasa hivi bombalile la Kenya linakaribia mwisho wa mpaka wa Kenyakuendelea kuingia Uganda ambapo Uganda tungewezakuwasaidia kwa bomba la mafuta la kutoka Dar es Salaamhadi Mwanza. Sasa sisi kweli tunataka mabadiliko makubwa,lakini mambo ambayo tunatakiwa tuyafanye hatuyatekelezi.

Mheshimiwa Spika, lakini yapo mambo menginekatika utekelezaji wa miradi yetu, gharama ni kubwa. Kwa

[MHE. H. J. MNTANGI]

68

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

mfano, gharama ambazo tunalipa kwa ajili ya Miradi yaMaendeleo ya Mpango ule wa dharura, hela tunazowalipaIPTL, Aggreko, Symbion ni hela nyingi kupita kiasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tuna mpango wakuzalisha umeme wa Kinyerezi ambao ukianza Kinyerezi I,Kinyerezi II na Kinyerezi III ni megawati 1,400 je, tuna mpangogani wa kuachana sasa na IPTL wakati tunazalisha megawati1,400 kwa nini tuendelee kubaki na IPTL wanaotupamegawati 100 tu kwa gharama zisizokuwa na uhalali wowote.Gharama ni kubwa kupita kiasi. Kwa nini na tunajiandaavipi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu Serikali ije hapa naitwambie Mkataba wa IPTL unakwisha lini? Mkataba waAggreko unakwisha lini, mkataba ule wa Symbion wa dharuraunakwisha lini ili waondoke baada ya sisi kuzalisha umemeunaotokana na mkakati huu ambao tumeupanga sasa.

Mheshimiwa Spika, matatizo ya upatikanaji wa fedha;mradi wa umeme wa Kinyerezi I umekwishaanzakutekelezwa na mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Nishati naMadini na tumekwenda pale. Tulipokwenda mwezi mmojatu uliopita, tatizo hilo limezungumzwa na wale Wakandarasiwaliopo site walikuwa wanasema wapo tayari kuondokakwa sababu fedha hawajapata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunasema Big ResultsNow, fedha hakuna za kutekeleza mradi wa umeme,Wakandarasi wanataka kuondoka, hivi kweli tutafanikiwa!Hatuna maandalizi mazuri katika mpango wa upatikanaji wafedha. Kwa hiyo tujitahidi katika kutekeleza hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini jambo lingine ni mpango nahili nalielekeza kwa Wizara ya Maji. Mheshimiwa Waziri waMaji alikuwepo hapa asubuhi na nilimwandikia kikaratasikuhusu mpango wa maji ambao ni ahadi ya MheshimiwaRais katika Wilaya ya Muheza, tunataka kuwa na uhakikafedha zinatengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

[MHE. H. J. MNTANGI]

69

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni tulikuwa nampango katika Kanda ya Kaskazini ikiwemo Mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na wenzetu wa Manyara wa Uwekezaji ambaotuliufanya na wawekezaji wengi walikuja pale katika Mkutanoule Tanga. Kitu kikubwa ambacho lazima kifanyike nikwamba, lazima tuwe na miundombinu ya uhakikaitakayowezesha kuvutia wawekezaji.

Moja, kati ya miundombinu hiyo, sawa ni barabara,maji, na kubwa ni umeme. Sasa haya mambo lazimatuyatekeleze. Kwa hiyo, tunaomba kuwa na uhakikakwamba, mradi wa maji wa Muheza kutoka Mto Zigiunakuwepo katika Mpango huu wa Bajeti na fedhazinatengwa ili mradi huo utekelezwe kwa uhakika. Hiyo niahadi ya Mheshimiwa Rais, ni lazima iheshimiwe na lazimaitekelezwe.

Mheshimiwa Spika, lakini lingine pia Muheza tunaahadi ya Mheshimiwa Rais ambayo ni barabara ya kutokaMuheza kwenda Amani. Naomba niseme kwamba kaziinayofanyika sasa ni nzuri kwamba barabara inaimarishwa.Lakini dhamira na ahadi ya Mheshimiwa Rais ni barabara hiyokujengwa katika kiwango cha lami.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina uhakika mpango huowa kuweka lami barabara hiyo utakuwepo katika bajeti hii.Kwa hiyo, hili nalo nalielekeza kwa Mheshimiwa Waziri waMiundombinu na nina uhakika ndani ya bajeti, fedha hizokwa ajili ya kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lamizinatengwa ndani ya bajeti hii inayokuja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuendelee kuimarisha miradiya uzalishaji wa umeme. Katika Wizara ya Nishati, mipangomizuri ipo, lakini je, itatekelezwa? Tumesema Kinyerezi moja,mbili na tatu ni megawati 1,400, lakini ukichukua na miradimingine ambayo ipo katika mapendekezo uzalishaji utakuwazaidi ya megawati 3,000, lakini je, tunasema kweli megawati3,000 zitakuwepo kabla ya mwaka 2016?

[MHE. H. J. MNTANGI]

70

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama zitakuwepo itakuwani vizuri, na mpango wetu utaweza kufanikiwa, lakini kamahatutafikia viwango hivyo, ni wazi kabisa mipango yetu mingiitashindikana, Watanzania hatutapiga hatua. Kwa hiyo,tujitahidi tuboreshe bandari ya Dar es Salaam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tuache mtindoambao umewakatisha tamaa wawekezaji na umeikatishatamaa nchi jirani na wengine wamekwishaanza kujitoa;rushwa iliyokithiri katika bandari yetu ya Dar es Salaam, lakinina vilevile huko barabarani magari yanakopita. Bila kuondoamatatizo hayo mizigo ambayo tumekuwa tukisafirisha kwauhakika kwenda Rwanda na Burundi na DRC itapungua auitakwisha kabisa na wenzetu kweli watahamia hukowalikokwenda kwa kutumia bandari ya Mombasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile Waganda walikujana wakawa tayari kusaidia kuweka fedha kwa ajili yautekelezaji wa mpango wa ujenzi wa reli hii ya kutoka Tangakuelekea Arusha na kwenda hadi Musoma, wenzetuWaganda walikuwa tayari, sisi Watanzania ambako eneokubwa la hiyo reli itakuwa ndani hatukutoa.......

(Hapa kengele ya pili ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MHE. HERBERT J. MNTANGI: Nakushukuru na naungamkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Mchungaji Natse, atafuatiwa naMheshimiwa Mtutura Abdallah Mtutura na Mheshimiwa RajabMohamed ajiandae.

MHE. MCH. ISRAEL Y. NATSE: Mheshimiwa Spika,nashukuru kwa kunipa nafasi ili nichangie katika Mpango waTaifa. Kwanza, nilikuwa naangalia, sisi Watanzania Idara yetuya Mipango imekuwa maarufu sana kuwa na Mipango mizuri,ambayo utekelezaji wake haufiki mwisho na hii mipangomizuri mingi imebaki kwenye makabati bila kufikia lengo kwawahusika.

[MHE. H. J. MNTANGI]

71

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Spika, nataka kuzungumza maeneomachache sana ambayo kwayo tumekuja na dhana ya BigResults Now. Moja ni juu ya Kilimo Kwanza. Nafikiri ni kwelitangu mwanzo kilimo ni mkombozi wa Mtanzania, lakini kilimohiki kwa kuangalia tu hali ya hewa kutegemea mvuahatutafika mbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumezungumza hata katikamipango iliyopita kwamba tuondoke kwenye kilimo chakusubiri mvua, twende kwenye kilimo cha umwagiliaji nampango huu hauweki wazi dhamira ya dhati ya Serikalikuhakikisha kwamba, inatia nguvu kubwa katika kilimo chaumwagiliaji na kwa kuchagua maeneo na kuhakikishakwamba maeneo kadhaa yatalisha nchi hii chakula na hatakuuza ziada nje kama ambavyo wenzetu wanafanya,wakulima wachache wenye kuzalisha kwa nchi nzima nahata kuuza ziada.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapozungumzia juu yakil imo hiki cha umwagiliaji, mabonde mengi yapo,imeshindikana kilimo hiki kuwa makini kwa sababu kunajambo la hifadhi ya mazingira ambayo inaingiliana ilikuhakikisha kwamba vyanzo vya maji vinatunzwa sawasawa.Kumekuwa na uharibifu mkubwa wa mazingira katikamaeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano kule katika Bonde laEyasi ambalo ni maarufu kwa wakulima wa vitunguu, mpungana mahindi. Bonde lile lingesimamiwa vizuri schemes ambazozimejengwa, zingine zimejengwa chini ya kiwango,zingesimamiwa vizuri zingezalisha vya kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baya kuliko yote Bonde lilelimevamiwa na watu wachache wenye tamaa ya utajiri waharaka na kuharibu mazingira; kukata miti, kufunguamashamba kwenye vyanzo vya maji, lakini hakuna hatuainayochukuliwa. Kwa hiyo, niiombe Serikali bila kuonea aibubaadhi ya watendaji, maana haya yanafanywa nawatendaji, yanafanywa na viongozi waandamizi wa Chama

[MHE. MCH. I. Y. NATSE]

72

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Tawala, bila kuonea haya ili kuweza kuwa na uhakika nakilimo cha umwagiliaji katika Bonde la Iyasi. Bonde lilelihifadhiwe kwa afya ya wananchi wote kule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tunahitaji kuwekezakatika miradi michache ambayo tunaweza kupima ufanisiwake kuliko kuwa na miradi mingi na mwisho wa siku hakunajambo ambalo linatupa matumaini. Kwa hiyo, niiombe Serikalituwe na mipango ya uhakika ambayo inapimika na mwishotupate matokeo yanayoitwa Matokeo Makubwa Sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikitoka kwenye kilimo, nikweli kuwa, Mungu alipoumbad alikamilisha kazi yake sikuya saba kwa kumuumba mwanadamu, maana yakewanyama walikuwepo na maana yake mwanadamualimkuta mnyama lakini mwanadamu alipewa kazi ya kutiishaviumbe vyote hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kusema nini?Nataka kusema kuwa, migogoro ya wakulima na wafugajina Hifadhi zetu za Taifa hivi ni vitu vinavyohitajiana. Katikakuboresha kilimo tunahitaji kuangalia pia na hao wafugajiwawe wapi, hilo sitaki kulizungumzia kwa kuwalimezungumzwa na litawekewa utaratibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwenye suala la hawawanyamapori, tunawapenda na tunawahitaji. Nafikirikinachokosekana kwetu Watanzania ni uzalendo wakuipenda nchi yetu na resources zake, kwa sababu haiingiiakilini kuona kuwa, kila siku tunatangaza vita vya ujangiliunaoendelea katika Hifadhi zetu, naona hakuna dhamira yakweli kwa Watanzania wote kwa ujumla hasa wale ambaowamepewa dhamana ya kulinda maliasili hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu haiwezekanileo tunasikia pembe za ndovu zimekamatwa kule na zinginekule na askari tunao. Ni kweli tunahitaji kuwa na dhamira yakweli katika mambo haya. Ili tuweze kuwa na mpango, ilituweze kuwa na rasilimali kwa maendeleo ya Watanzania.

[MHE. MCH. I. Y. NATSE]

73

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa natafakari hapakuwa hata tukiunda hii Kamati Teule inakwenda kufanya nini,maana majibu ya haya mambo yote tunayo, wahusikatunawafahamu, haingii akilini kuwa tembo wameuawaSelous, wameuawa Ngorongoro na kwingineko na kwambawatu hawafahamiki, haingii akilini hata kidogo. Lakini kwaajili ya taratibu na kutafuta ushahidi ni sawa na naafiki kuwani lazima tuwe na dhamira ya kweli ya Uzalendo kwa nchiyetu na mali zake hapo tutaweza kujikomboa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la umeme Vijijini;World Bank imechimba visima virefu Tanzania nzima, lakininaona mradi huu ambao sasa tunasema The Big Result Nowhauwezi kukamilika vizuri kama umeme hautakwenda katikamaeneo haya, kwa sababu huko vijijini visima virefu bilaumeme haina maana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika maeneo mengi kamakule kwangu Karatu, maji yapo lakini namna ya kuyavutahayo maji yaje juu wananchi watumie, ni kasheshe. Kwa hiyo,niombe Serikali tuweke nguvu zaidi katika maeneo hayo iliwananchi waweze kunufaika na tuone Matokeo MakubwaSasa kule Karatu kwa maji. Ni kweli Matokeo Makubwa Sasaamekuja Waziri Mkuu, amekuja Waziri wa Maji, Naibu Waziri,lakini hatimaye hakuna maji. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi zimefanyika kwelindogondogo za hapa na pale, lakini hakuna maji, tunatakakuona maji Matokeo Makubwa Sasa, kwa hiyo nafikiriseriousness katika kazi bado ni hitaji letu kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kuhusu elimu;tukitaka kuona Matokeo Makubwa Sasa tunahitajikutengeneza mazingira mazuri ya shule zetu, ya Walimu nawanafunzi. Hilo litatusaidia kuhakikisha tunaona MatokeoMakubwa Sasa, kuwa wanafunzi watapata kile ambachotumekusudia na Walimu watapata kile ambachowanapaswa kupata na wafundishe vizuri.

[MHE. MCH. I. Y. NATSE]

74

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tusitegemee MatokeoMakubwa Sasa kama hatutaandaa mazingira bora kwa shulezetu hasa kwa Walimu. Tutabadili viwango vya kufaulu,tutafanya kila hali, lakini kama hatutatengeneza...

SPIKA: Mheshimiwa umepata bonus hii ilikuwa yapili, sorry!

Sasa nimwite Mheshimiwa Mtutura Abdallah Mtuturaambaye atafuatiwa na Mheshimiwa Rajab Mohammed naMheshimiwa Brigedia Ngwilizi ajiandae.

MHE. MTUTURA A. MTUTURA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii. Ukiangalia kitabu hikicha Mheshimiwa Waziri, ukurasa wa 20 aya hii ya 34inazungumzia vipaumbele vya Taifa na hapa vipaumbelehivyo vya kimkakati vimetanguliwa na Nishati, Barabara, Reli,Bandari, Usafiri wa Anga, Maji Safi na Maji Taka, Teknolojiana Habari. Najua kuwa kipaumbele cha Taifa bado elimu ninamba moja ingawa hapa hakijatajwa. Kwa hiyo, katikakuchangia kwangu nitazingatia hivi vipaumbele ambavyovimetajwa hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa muono wangu,naungana na Waziri kabisa kuwa kipaumbele cha kwanzakiwe ni nishati, lakini badala ya kipaumbele cha pili kuwabarabara naishauri Serikali kuwa kipaumbele cha pili kiwereli kwa sababu ya umuhimu wake kiuchumi katika nchi hii,kwa sababu tumeona barabara nyingi zinajengwa, lakiniathari zinazopata barabara zile kutokana na kutokuwepokwa reli ni kubwa na gharama kubwa sana za Serikalizimetumika katika kuzikarabati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kama kipaumbelecha pili kitakuwa ni reli, nadhani hata hizo barabara chacheambazo tumefanikiwa kuzijenga zitaweza kuimarika.Kipaumbele cha tatu kiwe ujenzi wa bandari na hasa bandariya Dar es salaam kwa zile gati mbili gati namba 13 na 14.(Makofi)

[MHE. MCH. I. Y. NATSE]

75

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kumekuwa namkanganyiko kidogo kati ya Bandari ya Dar es Salaam na ileya Bagamoyo, kwa kuzingatia kuwa sasa hivi tuko katika wazola kuwa na Big Results Now, kwa maana ya MatokeoMakubwa ya Haraka Sasa, hatuwezi kupata MatokeoMakubwa ya Haraka Sasa hivi kama rasilimali chachetulizonazo tutazielekeza Bagamoyo ambako kunahitaji fedhanyingi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naishauri Serikalikuwa waendelee na fikira zao za mwanzo za kujenga gatinamba 13 na 14 na vilevile kujenga bandari ya nchi kavu yakule Kisarawe ili ule mzigo ambao hauko tayari kuingizwamelini, basi uweze kulundikana kule Kisarawe. Naamini kabisakuwa, Serikali itajenga uwezo mkubwa wa kuweza hatakujenga hiyo Bandari ya Bagamoyo na Bandari zingine zaMtwara pamoja na Tanga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipaumbele cha nnekielekezwe kwenye barabara badala ya kuwa ni kipaumbelecha pili na cha tano kielekezwe kwenye maji safi na majitaka. Siyo siri mimi ni Mbunge wa CCM, lakini kutokana nahali iliyopo huko Vijijini sasa hivi na baadhi ya Miji katika nchiyetu maeneo ambayo Chama changu kitatafunwa sana nieneo hili la maji. Naomba tuwe makini sana kwa miaka hiimiwili ya bajeti tuliyobakiwa, tuhakikishe kuwa kero ya majivijijini na kwenye Miji inaondolewa haraka iwezekanavyo,kinyume cha hivyo kazi yetu itakuwa ni kubwa sana huomwaka wa 2015.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tujenge matumaini kwawananchi juu ya kuwapatia maji safi na salama. Bahatimbaya maji hayana mbadala, usafiri una mbadala unawezaukaamua kusafiri kwa ndege, kusafiri kwa treni, kusafiri kwagari, kusafiri hata kwa miguu na baiskeli na bodaboda, lakiniunapokosa maji hayana mbadala, huna pa kukimbilia. Kwahiyo, tuwasaidie Watanzania wanyonge walioko vijijini katikakuhakikisha kuwa tunatatua tatizo la maji. (Makofi)

[MHE. M. A. MTUTURA]

76

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niangalie katika nyanjambalimbali za uchumi; nchi yetu bado haijajitosheleza katikazao la sukari, tumekuwa na viwanda takribani vikubwa vine;Kiwanda cha Kilombero yaani Kilombero one na two, Mtibwa,kule Kilimanjaro na kule Kagera, lakini bado tuna maeneomengi mazuri na makubwa ambayo yanaweza kuzalishasukari nyingi ikatosheleza katika nchi yetu na bado tukawezakusafirisha nje ya nchi. Maeneo hayo ni kama Bonde la MtoRufiji na vilevile Bonde la Mto Ruvuma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miaka ya nyuma tulikuwana mpango wa kuanzisha shamba kubwa sana la miwakatika Bonde la Mto Ruvuma, lakini mpango huu umekwishana hausikiki tena. Naomba sana Serikali aidha, kwa kutumiamashirika yake ya ndani kwa kuweka mazingira muafaka kwawahisani, waje wafungue mashamba makubwa ya kulimamiwa na kufungua kiwanda kikubwa sana cha sukari katikaBonde la Mto Ruvuma hususani katika Wilaya yetu ya Tundurukwa sababu tunayo maeneo mengi ambayo Wakulimawanaweza wakapata zaidi ya hekari 5,000 za kuzalisha miwana kufungua kiwanda cha kuzalisha sukari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna suala hili la ujenziwa Bandari ya Mtwara na reli ya kutoka Mtwara hadiMbambabay ili iweze kusafirisha makaa ya mawe pamojana Chuma cha Liganga. Nimesikia minong’ono kuwa kunawazo la kubadilisha wazo hili la kuijenga hii reli ya kutokaMtwara kwenda huko Mbambabay, kwa maana wanaonahuenda isiwe na tija.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwahakikishie Watanzaniawenzangu kuwa, tija bado ipo na itaendelea kuwepo kwasababu dhamira ya kujenga reli hii ni kujaribu kufufua wazoambalo Marais wetu waliotangulia akina MheshimiwaBenjamin Mkapa na Rais wa Msumbiji na Malawi ili Ukandahuu wa Kusini mwa Tanzania na Kaskazini mwa Msumbiji naupande wa Mashariki mwa Zambia na Malawi wawezekutumia usafiri ambao utawaletea tija.

[MHE. M. A. MTUTURA]

77

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukitoka Malawi kuja Pwaninjia fupi kabisa ni ya kupitia Mtwara. Wenzetu wa Malawiwanalazimika kupitia Dar es Salaam kwa sababu hawanabarabara mbadala, lakini reli hii ikijengwa tutapata mzigomkubwa sana wa kutoka Zambia na Malawi ambao utapitiahapa, lakini vilevile Kaskazini mwa Msumbiji nao watanufaika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi miongoni mwa BigFour katika nchi yetu ni pamoja na Mkoa wa Ruvuma ambaounazalisha chakula kwa wingi sana, mahindi pamoja naTunduru sasa hivi imejitokeza katika kilimo cha mpunga, Mikoakaribu yote ya Kusini wanategemea mchele kutoka Tunduru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama reli hii itakuwepo,uwezekano wa kusafirisha mahindi kwa njia ya treni mpakaBandari ya Mtwara, halafu mahindi hayo yakasafirishwa njeya nchi itawajengea uchumi ulio imara wananchi wetu waUkanda huu wa Kusini. Vile vile mzigo mkubwa sanautategemewa wa makaa ya mawe ya Ngaka pamoja naLiganga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba wazo hilila kujenga reli na siyo wazo la kuijenga reli, ni wazo la kufufuareli ambayo zamani ilikuwepo, libaki palepale ili wananchihawa wa kusini waweze kunufaika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, korosho za Tunduru sasa hivihazinunuliki kwa sababu wanunuzi wengi wanashindwakwenda Tunduru kununua kwa sababu wanasema ni mbali.Reli ikiwepo wachuuzi wengi wa kutoka nje ya nchi watakujakununua korosho Tunduru kwa bei nzuri kwa sababu usafiriwa bei nafuu wa reli hiyo ambayo tunaitarajia utakuwepo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipafursa hii na naunga mkono hoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Sasa nimwite Mheshimiwa RajabMohammed, atafuatiwa na Mheshimiwa Brigedia Ngwilizi naMheshimiwa Pauline Gekul.

[MHE. M. A. MTUTURA]

78

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMMED: MheshimiwaMwenyekiti, naomba nikushukuru kwa kunipatia nafasi hii.Niseme tu kuwa, Watanzania tumekuwa mahodari sana wakupanga mipango, tumekuwa mahodari sana katika sualala uandishi kiasi cha kuwa wananchi kwa sasa wanaanzakutupa majina ya ajabu ajabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna jambo kubwaambalo linatafuna nchi hii, ambalo linakwaza maendeleoya nchi hii, ambalo linasababisha matumizi makubwa yaSerikali kupanda kila mwaka, ambalo linasababisha hatawafadhili wetu kuanza kupunguza kasi yao ya kutusaidia, basini suala la nidhamu katika matumizi ya fedha za Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimejaribu kukipitia kitabukizima ambacho Waziri amekiwasilisha hapa sikuona maelezoya aina yoyote ya mpango mkakati wa Serikali ambaounaweza kutushawishi na sisi kutoa mapendekezo yetu aukuongeza nyama katika mipango ile iliyozungumzia sualazima la nidhamu ya matumizi fedha za Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lazima tukubali kuwandani ya nchi yetu, nidhamu ya matumizi ya fedha za Serikaliimeshuka kwa kiwango cha chini kabisa, ni hali mbaya kabisa.Nenda katika taasisi zote, nenda katika Halmashauri zotenchini huko ndiyo kumeoza kabisa, nidhamu ya matumizi yafedha za Serikali haipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hata kamatungeweka kipaumbele kimoja tu bila ya kuzingatia suala lanidhamu ya matumizi, basi hatuwezi kufanikiwa. Haya yoteyaliyozungumzwa hapa, yaliyowekwa hapa, ni maelezo tu,lakini nidhamu ya matumizi ya fedha za Serikali hakuna nahili nataka nilithibitishe hata ndani ya Bunge lako angalia vitivya Mawaziri hapo, vitupu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wewe kwa mara mbilitumekusikia hapa unawaambia Mawaziri kuwa jamani kituambacho tunakiongelea ni kikubwa, ni mipango ya nchi,Mawaziri ni lazima muwepo ndani ya Bunge, msikilize

79

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

michango, leo Mawaziri wale wanaohusika hasa wanatakiwahuu mpango wausikilize. Wasikilize maoni yetu sisi Wabunge,hawafiki hata kumi hapa. Kama wanabisha wanyanyuemikono hapa, kama watafika kumi hapa. Aibu, tena ni aibukubwa, waliobaki ni Mawaziri wadogo tu, pengine sijui hatakama ndani ya Baraza la Mawaziri wanaingia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sijui hata tunafanya nini.Ikiwa kama leo Mawaziri ambao tunataka hii Big Result Nowiweze kufanya kazi, wanashindwa kukaa hapa kutusikiliza.Nakubaliana na wananchi wanaosema kwamba, this is BetterResign Now, hawana sababu ya kuendelea kuwepo. Hiimipango tunapanga kwa ajili ya kuendesha nchi. Leo waowaingia mitini. Basi hata Spika hamumheshimu? Hata Spika?Ni aibu!

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la nidhamu yamatumizi ya fedha ningependekeza kwa Serikali kwamba,hiki ndio kiwe kipaumbele chetu cha kwanza. Bila ya kuwana nidhamu ya matumizi ya fedha za Serikali, haya yotetunayozungumza kule kwetu tunaita halindwa, haitaleta tijayoyote. Leo wananchi wetu wote na hasa vijana wetuambao sasa hivi wanamaliza shule. Wanachokijua wao nikwamba, nipate kazi, kesho niwe na gari. Nipate nyumbanzuri ndani ya mwezi mmoja kwa sababu yeye anapopitamitaani, anasikia tu hii nyumba bwana ya kijana wa TRA,kaanza kazi juzi tu. Hili jengo ni la Waziri, hili jengo la…

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hii yote imetokana nanidhamu ya kutokuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha zaSerikali. Kwa hiyo, namwomba Mheshimiwa Waziri aunaiomba Serikali, hebu ituletee mpango wao mkakati na iweni kipaumbele cha kwanza, nidhamu katika matumizi yafedha za Serikali. Kiundwe chombo kama wanatakatufanikiwe, ambacho kitakuwa kinashughulikia suala zima lanidhamu ya matumizi ya fedha za Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, actually sio matumizi tu, hataukusanyaji wa mapato. Trend yetu inaonekana, katikakukusanya mapato. Safari hii tumeona katika mpango

[MHE. R. M. MOHAMMED]

80

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kwamba Serikali itakusanya almost eleven trillion, ni kidogo.Mheshimiwa Mbunge mmoja wa hapa Dole, aliwahi kutoaushauri mwaka jana kwamba jamani hebu tuundeni Tumeikawachunguze hawa wakusanyaji mapato, kwani mapatomengi yanapotea. Hapa Taarifa inasema trilioni moja, lakinini imani yetu kwamba zinazokusanywa, ni twice ya hii trillionmoja, lakini zipo mifukoni mwa watu, kwa sababu ya kukosanidhamu ya fedha za Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niende suala lamiundombinu hasa suala la Bandari. AlizungumzaMheshimiwa Mtutura, Gati namba 13 na 14. Ikumbukwekwamba, Gati hizi mbili ndizo zilizosababisha baadhi yaMawaziri, kutimuliwa. Leo ni jambo la kushangaza humukwamba imetajwa Gati namba moja mpaka namba saba,lakini imeachwa Gati namba 13 na 14 ambayo feasibilitystudy yake ilishamalizika, Wakandarasi walishapatikana,fedha zile za mkopo tulizoambiwa zilikuwa tayari, how comeleo mnatuletea Gati namba moja mpaka namba saba,kwamba ndio kwanza upembuzi yakinifu. Bila ya kutupaTaarifa za Gati namba 13 na 14.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna nini hapa? Au ndiohaya maneno ya watu kwamba, yule Mchina mliompaBagamoyo, ndiye ambaye kaingilia huu mchakato namba13 na 14, kwa sababu kampuni ni ile ile. Tunaomba maelezoya Serikali kuhusiana na Gati namba 13 na namba 14. Ili hizikwa vile michakato yake ilishamalizika. Kwa nini zisianze Gatihizi mbili kwanza? Tunaanza kushughulikia namba moja nanamba saba, Mwambani, Bagamoyo. Hebu tujaribunikuangalia na yale ambayo tunayazungumza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie suala la kilimo.Katika Taarifa ya Waziri, anaeleza ekari ambazo kwa kwelihazijafanyiwa mchakato. Tulikuwa na Kilimo Kwanza, Serikalihebu ituambie kwanza tumekwama wapi kwenye KilimoKwanza? Tumepata mafanikio gani katika Kilimo Kwanzampaka sasa hivi tunataka kuingia katika msamiati mwingine?Hebu tuambieni kwanza hiki Kilimo Kwanza tumefikia wapi ilitujue sasa tunaondokaje pale, tunakwenda katika msamiati

[MHE. R. M. MOHAMMED]

81

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

mpya? Tusijaribu kuleta misamiati ambayotunawachanganya wananchi. Tupeni taarifa kamili ya KilimoKwanza tumefikia wapi na tumekwama wapi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mmetupa taarifa za TASAF,kila Mbunge kakubaliana na taarifa za TASAF na kafurahiakabisa, lakini leo mnatupa kitu ambacho…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Brigedia Ngwiliziatafuatiwa na Mheshimiwa Gekul na Mheshimiwa Lowassa.

MHE. BRIG. JEN. HASSAN A. NGWILIZI: MheshimiwaMwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachozungumza hapa niMpango wa Maendeleo ya mwaka 2014/2015 ambaoMpango huu umezalishwa kutokana na Mpango wa MiakaMitano 2011/2012 mpaka 2015/2016, ambao huo ndioutatupeleka kwenye mpango wetu wa 2025.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa il i tuendeleeWatanzania tunakubaliana tunahitaji watu, ardhi, siasa safina uongozi bora. Lakini hapo ndio mwisho wetu wa kufikiri.Huo ni mwanzo tu kwa ajili ya maendeleo ya watu. Lakinikwa ajili ya maendeleo ya nchi unahitaji vitu vingine vinne,niliwahi kuvisema naomba kurudia.

Tunahitaji miundombinu kwa maana yacommunicaton infrasturucture, iwe ni Reli, Barabara, usafiriwa Ndege, Maji na vile vile Teknohama (TEHAMA), yote hiyoimeingia kwenye mfumo wa usafiri. Hivyo kama hatutapangakatika mipango yetu ya maendeleo ili kufungua nchi yetu,basi tujue kwamba tunatwanga maji kwenye kinu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nazungumza hivyo?Kwa sababu nchi kama hatujaiwekea miundombinukuifungua, basi hakuna tofauti na yale ambayo yanawapata

[MHE. R. M. MOHAMMED]

82

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ndugu zetu Wakongo. Kongo walipata uhuru kabla yetu nampaka leo hii nchi haijaunganishwa kutoka kusini kwendakaskazini. Nchi yetu hii mpaka sasa hivi tunazungumzia miaka50 na zaidi. Bado hatujaleta mfumo rasmi wa jinsi yakuunganisha. Ndio maana leo hii tunazungumzia reli ya katikana kwamba ni hiyo tu ambayo tunatakiwa kuiangalia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunasahau kwamba kunareli ya Tanga, mpaka Arusha, mpaka Musoma; tuna reli kutokaMtwara mpaka Songea mpaka Liganga huko Mchuchuma.Kwa sababu tupende tusipende tunaweza tukajidanganyakwamba kwa miaka hii, kumi na tano au ishirini, hatuhitajihiyo reli, lakini katika miaka 50 inayokuja itabidi tujenge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa nini tungojeemuda wote huo? Kwa nini tusijenge hivi sasa? Kama hatujengireli hivi tunatazamia kile chuma cha Mchuchuma na Ligangatunakitoa vipi kule? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili tuendelee, hayo mamboya mawasiliano kwa njia ya reli, barabara, bandari ni moja.Tunahitaji nishati, nishati hiyo iwe inatokana na gesi, mafutaau maji, lakini bado tunahitaji nishati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka sasa hivi tume-zeroin sana sana kwenye suala la gesi. Lakini tunasahau kwambamaji vile vile ni chanzo muhimu cha umeme. Hapa sasa hivitunazungumzia mazingira, tunaona kwamba, kwa sababuya hali yetu ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi, basihaitawezekana kutegemea maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile tunajua kwambakwa muda mrefu tumekuwa tunazungumzia suala la bwawala Stigler’s Gorge. Sioni kokote likizungumzwa hili na Stigler’sGorge katika upembuzi yakinifu wake lilikuwa limekusudiwakunywesha Bonde zima la Mto Rufiji. Bonde lile la Mto Rufijibila Stigler’s Gorge huwezi ukategemea kwambautalinywesha, utakuwa unategemea maji yanayotiririkakwenye Mto.

[MHE. BRIG. JEN. H. A. NGWILIZI]

83

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati tunazungumzia sualala Stigler’s Gorge vile vile katika Mipango yetu sikuona,tumezungumza sijui Bwawa la Kidunda, bwawa lile ni kwaajili ya maji ya kunywa lile. Hakujazungumzwa suala la kujengamabwawa kwa ajili ya kuhimili kilimo cha umwagiliaji. Tunamabonde mengi, tuna uwezo mwingi wakujenga mabwawayale lakini naona hilo katika Mpango huu liko silent.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili uendelee unahitaji chumakama kile ambacho tunacho Liganga na Mchuchuma. BilaChuma huwezi ukafanya chochote, utategemea tu itabidikuagiza chuma kutoka nje, lakini tunacho. Sijasikia mipangomahsusi ya ku-develop Chuma chetu tulichonacho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho wa yote, tunahitajisayansi na teknolojia kwa maana ya pamoja na elimu nakadhalika. Bila kuwatayarisha Watanzania katika SNT,hatuwezi ku-meet deadline hizi ambazo tumejiwekea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ili tuweze kutekelezayote hayo, tunahitaji fedha, fedha hizo hatuna. Ndiyo maananaomba niungane na Kamati ya Bajeti, kwamba Serikalihaijaweza kutumia fursa ya kukopa. Ukurasa wa nane wamaoni ya Kamati unaeleza pale, kwamba Kamatiinashangazwa na kitendo cha Serikali kusita kukopa ndaniya ukomo huu kwa ajili ya Miradi wa Maendeleo. Fedhaambayo imekopwa ya kiasi cha shilingi bilioni 118.6 ni pungufukwa shilingi bilioni 161.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huo ndio ukomo ambaoumewekwa Kimataifa, kwamba Tanzania tunaweza kukopakiasi hicho. Kitu gani kinatufanya tushindwe kukopa wakatifursa hiyo ipo. Kwa hiyo, naomba kusisitiza kwamba,haitawezekana kufikia malengo ya huu Mpango waMaendeleo kama hatutakopa. Kama hatutakopa maanayake tuendelee kutegemea Wafadhili na Wafadhili ndio haotunajua wana ugumu wa kutoa fedha hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niingilie suala la majirani,tumelizungumza sana hapa. Kenya, Uganda, Rwanda

[MHE. BRIG. JEN. H. A. NGWILIZI]

84

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

wanafanya hivi. Maoni yangu ni kwamba, wanafanya hayokwenye nchi zao. Kenya, Uganda, Rwanda na majirani wote,wao ni majirani, tupende tusipende, jirani huwezi ukasemakwa sababu anafanya hivi humtaki akae pale, ataendeleakuwepo tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana. Sasa nimwite MheshimiwaGekul, atafuatiwa na Mheshimiwa Lowassa nafikiri naMheshimiwa Batenga.

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Mwenyekiti,nikushukuru kwa kunipa nafasi ili nichangie machacheyaliyopo katika Mpango uliopo mbele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote nisemekwamba nchi yetu haijakosa mipango. Nchi yetu ni mahirikuwa na Mipango, lakini political will, ukubali wa kisiasa waviongozi tulionao ndio tatizo, kwa sababu tunaona katikakitabu alichotupatia Mheshimiwa Waziri deni la Taifa linakuakufikia trilioni 24.4 na mpango huo unatekelezwa kwa trilioni8.9 wakati fedha za ndani ni trilioni 2.9.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unaona ni jinsi gani hata zilefedha chache tunazozikopa zinapotea kwa njia zipi.Kwasababu kama deni la Taifa linakua na tunakuwa naMipango ya mwaka mmoja, miaka mitano hadi miakamingapi, lakini hakuna political will. Hakuna usimamizi waviongozi ambao wanapeleka fedha zikaenda kwa wakatina tukatengeneza mipango tuliyonayo, ni janga kwa Taifana ni aibu kwa Taifa letu miaka 52 ya uhuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipaumbele katika Mpangohuu tulionao, ni suala zima la miundombinu. Mimi kama NaibuWaziri Kivuli nilishauri katika mwaka wa Bajeti uliopita,tukazungumzia sana kuhusu bandari yetu ya Dar-es-salaam,tunakazungumzia ujenzi wa bandari unaoendeleaBagamoyo, lakini tukazungumzia jinsi ambavyo tunapanua

[MHE. BRIG. JEN. H. A. NGWILIZI]

85

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

hizi barabara na madhara yake au umuhimu wake kwawananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nishauri tena Serikali hiiambayo inaitwa sikiivu, lakini nina wasiwasi kwamba haisikii.Suala zima la wenzetu wa East Africa kujitoa, naombamsinibeze, ninyi ambao mpo katika madaraka na mmepewanafasi hizi na Watanzania. Kwa sababu lazima tutapatamdororo wa uchumi, Bandari ya Dar-es-Salaam, wenzetuwameitenga, lakini wakati huo huo tunataka tupelekevipaumbele hivi, tuendelee kujenga bandari Bagamoyo,mara Kisarawe mara wapi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niishauri Serikali mkatafakarikwa upya mawasiliano tuliyonayo na wenzetu na athari yauchumi ambayo tunakwenda kuipata dhidi ya mipango hiituliyonayo. Tukiendelea hivi usishangae uchumi wetuukadorora na pato la Taifa likashuka, lakini wakati huo huohatuko tayari ku-review mpango tulionao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaweza tukawa nampango, lakini unapoanza safari, ukifika nusu ya safari lazimau-review na unapoona mambo hayaendi ni vizuri Serikaliikakaa chini na ku-review mipango tuliyonayo. Je, hiimipango tuliyotunga tangu wakati huo kuna sababu yakuendelea nayo, kuna sababu ya miundombinu kuendeleakuwa kipaumbele au kuna mambo mengine lazimatuyaweke hata kama safari yetu ilikuwa miundombinu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nishauri tu kwamba Waziriwa Ujenzi na uchukuzi wakae chini. Kwa mfano, kuna zoezizima la Wizara ya Ujenzi kutengewa fedha nyingi sasa katikahuu Mpango kwa sababu huu Mpango ndio unatupelekeakwenye Bajeti. Tuna fedha nyingi tunatenga karibu ya trilionimoja katika barabara zetu, lakini wakati huo upande wauchukuzi unadorora. Nishauri wakae chini waangalie, kunasababu ya Mheshimiwa Magufuli kuendelea kupewa fedhanyingi wakati Wizara nyingine ambayo inategemeana na hiiinatengewa fedha chache.

[MHE. P. P. GEKUL]

86

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mpango huu tulionaoupande wa barabara, nishauri Serikali kuna wale wananchiambao walikuwa katika mita ziliongezeka katika kupanuabarabara kutoka 22 zikafika mita 30. Wale wananchi sio waMkoa wangu wa Manyara tu ambao wanalalamika kuhusubarabara inaunganisha Dodoma na Manyara. Wananchi wapale Bonga hawajalipwa katika mita 30 muda mrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inasema kwamba hiiMipango ni endelevu na hifadhi ya barabara itunzwe kwampango tulionao sasa wa nchi nzima. Tuangalie kwa ninitusiwape kipaumbele wale wananchi ambao wamekaamuda mrefu na wanaidai Serikali fidia kwa nini tusiwapatiefidia hizo? Naomba mkae chini Wizara hii mwangalie kwamapana zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la maji vijijini. Wabungewengi wamechangia katika hili, nishauri, mradi wa Maji waWorld Bank umeshindwa. Tulitenga katika Bajeti iliopita zaidiya bilioni 184 kwa maji vijijini. Mheshimiwa Waziri amesemakwamba ni asilimia 57 tu ya wananchi wanaokaa vijijini,wananchi milioni 22 ndio wana access na maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwa Mkoa wanguwa Manyara na kwa Mikoa mingine Mradi wa World Bankumeshindwa na ndio maana nasema lazima tuangalienyuma tulipotoka, huku tunakokwenda tunafika autunaendesha tu hili gari ilimradi lifike?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nishauri sasa tusijifiche,Serikali isifanye World Bank kama kichaka cha kujificha dhidiya matatizo ya wananchi ya maji. Tuangalie, tupange fedhazetu za ndani, vile visima ambavyo sasa World Bankwameshatujengea hadi hapo kwa mkopo ule, visima vinamaji, tutenge fedha zetu tutandaze sasa mabomba majiyaende kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu kati ya Wizaraambayo inaongoza kwa maswali mengi Bungeni ni Wizaraya Maji. Hata tatizo la maji katika Jiji la Dar-es-Salaam

[MHE. P. P. GEKUL]

87

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mnyika amekuwa akilisemea sana, lakini ni kwanchi nzima. Kwa nini tusitenge fedha zetu za kupeleka majisasa vijijini kupitia visima hivi tukatenga fedha za kutandazayale mabomba, haya maji yakafikia kwa wananchi. Badalaya Waziri kuja kila siku na kusema maji yamepatikana, visimavimechimbwa, lakini hayajawafikia wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali kwamba,tu-review mpango mzima wa World Bank ili hata hayamaswali ya Wabunge yaishe kabisa, maji yapatikane kwawananchi, vinginevyo ni janga kubwa kwa Serikali ya CCM.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la afya, kwa kwelibajeti ya Wizara ya Afya tuliyotenga last time katika mwakawa bajeti ilikuwa zaidi ya bilioni tisa kwa ajili ya kusafirishawagonjwa wale ambao wanafuata matibabu nje ya nchi.Hivi tunavyoongea Wizara ya Afya ile bajeti imesha-bust. Tunawagonjwa wengi tunawapeleka nje ya nchi wenye matatizoya cancer na matatizo ya moyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali hivi nimpaka lini tutatibu watu wetu nje ya nchi kwa miaka 52 yauhuru? Ni kwa nini tusitenge fedha kwa ajili ya kununua vilevifaa vinavyohitajika pale Ocean Road, kwa nini tusikate huumrija wa kupeleka wagonjwa nje ya nchi, tutibiwe viongoziwote humu ndani ya nchi kama vile wananchiwanavyotibiwa hapa katika nchi hii. Naomba hili lifanyiwekazi, vinginevyo ni aibu kwa Serikali yetu kwa miaka 52 yaUhuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Utawala Bora,nimeona katika kitabu hiki Waziri akisema kwamba, miongonimwa mambo ambayo ametoa kipaumbele ni ujenzi wamajengo ya PCCB.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni juzi tu Rais wakatianahutubia Viongozi wa CCM hapa Dodoma akasemaathari ya rushwa ndani ya Chama chake, lakini mnaonaMaaskari barabarani wakichukua rushwa peupe, mabasiyote yanatoa shil ingi 5000, shil ingi 10,000, Viongozi

[MHE. P. P. GEKUL]

88

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

mnafahamu, Mahakimu Mahakama ya Mwanzowananyanyasa wananchi wetu, wanachukua rushwawaziwazi, PCCB hawafanyi kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwa Mkoa wanguwa Manyara hawatusaidii kabisa, hatuna sababu ya kutengafedha, eti tunajenga majengo ya PCCB wakati Mabarazaya Ardhi yamejaa rushwa, Mahakamani rushwa, hospitalini,barabarani rushwa kweupe kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili halitakubalika naWabunge tuungane, suala la PCCB kujengewa majengomazuri wakati Walimu hawana nyumba za kuishi, wakati Polisihawana nyumba za kuishi, wale wanaochukua rushwa naPolisi wanaongoza katika ripoti mbalimbali, lakini asubuhitumeona kwamba, hata Mahakama za Mwanzo hazipo,kuna sababu gani ya kujenga ofisi za PCCB wakatiwameshindwa kufanya kazi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, unakwenda kwenyeuchaguzi rushwa inatolewa na sheria tumeitunga, unaitaPCCB wanasema mpaka tuongee na Hosea! Kwa nini hayayanaendelea na sisi Wabunge tunatenga fedha kwa ajili yakuwapa watu ambao wameshindwa kazi yao! Naomba hizifedha za PCCB zikalipe posho za Wenyeviti wa Vijiji ambaompaka sasa hawana posho, hizi pesa za majengo ya PCCBzikalipe mishahara ya Walimu, Madaktari, Polisi; rushwa nchihii PCCB wameshindwa kuidhibiti. Naomba iondoke katikavipaumbele vyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe, tunakwendakwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Nimwite sasa MheshimiwaEdward Lowassa atafuatiwa na Mheshimiwa Batenga.

[MHE. P. P. GEKUL]

89

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. EDWARD N. LOWASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kukushukuru kwa kunipatia nafasi ya kuchangiamapendekezo haya ya Mpango wa Maendeleo, lakini nianzekwa kumpongeza Waziri na Tume ya Mipango kwa kazi nzurimliyoifanya, hongereni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekaa Bungeni hapa zaidiya miaka 20, ni lazima nikiri kwamba Kamati yetu ya Bungeinafanya kazi nzuri sana. Sijawahi kuona toka nimekuwaBungeni Kamati inayofanya kazi nzuri kiasi hiki kamailivyofanya kwa wakati huu, hongereni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikupongeze wewemwenyewe kwa kuleta pendekezo la kuwa na Kamati yaBunge ya Bajeti, ni wazo zuri sana na linazaa matunda mazurisana, hongera sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yamesemwa mengi, kwahiyo utaniwia radhi nikirudia, lakini nianze na machache.Jambo la msingi moja lililozungumziwa sana ni resources zakufanya kazi hii, je fedha zipo na kama zipo zinatumikaje nauzoefu huko nyuma umekuwaje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ya Bunge imeelezavizuri sana kwamba, kuna matatizo ya fedha kutotumika vizuri,kuna matatizo ya Tume ya Mipango kutosimamia fedhazikapatikana vizuri. Lakini la pili wamesema kuna vipaumbelevingi mno, kwa hiyo, utekelezaji wake unakuwa ni matatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa nijikite kwenyesuala la vipaumbele vingi mno. nadhani tungechaguavipaumbele vichache tukavisimamia, tukavitekeleza. Tukiwana vipaumbele vingi kwa wakati mmoja hatutekelezi vyote.Tuangalie nini kinawezekana, nini muhimu ambachomkikianza kitakwenda kwa kingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mapendekezomachache, ningekuwa mimi ningeanza na kipengele chaajira. Huwezi kuzungumza mipango bila kuzungumza habariya ajira, huwezi kupanga mipango yeyote bila kuzungumza

[MHE. E. N. LOWASSA]

90

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

habari ya ajira. Kukiri kwamba kuna Watanzania wengiwaliomaliza form four, waliomaliza form six, waliomalizadarasa la saba waliopo mitaani hawana kazi, hawana ajira,tusipoangalia watakuja kula sahani moja na sisi,tusipowashughulikia. Siyo lazima yatokee yaliyotokeaKaskazini mwa Afrika, lakini tusipoangalia yatatufika na sisihayo hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, simwoni Waziri wa Fedhahapa, kwenye Mkutano wa World Bank mwaka huu walikaakuzungumza habari ya mdororo wa uchumi Ulaya, nchi mojaambayo uchumi umedorora sana na Spain. Spain ikatoamfano kwamba, walikuwa na unemployment inayofikiavijana asilimia 50, wakaamua bajeti yao na mipango yao yakufufua uchumi wao inajikita kwenye jobs created,umezalisha ajira ngapi ndipo unapojua uchumi unakwendaje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ikawa kila Mwekezajianayekuja, anapewa sharti la kuwekeza katika ajira ya vijana.Katika miaka miwili, mitatu Spain imetoka kwenye matatizohayo kwa sababu imeangalia suala la ajira. Ni lazimatuliangalie suala la ajira kwa umakini sana, ni muhimu sana.Mipango mingine haiwezekani bila kutazama suala la ajira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kuwapongezaMkuu wa Mkoa wa Tabora na Mkuu wa Wilaya ya Igunga,wameanza kuangalia suala la ajira ya Vijana. Inawezekanasana kila mmoja akiamua kulishughulikia, kila Wizara ikiamuakulishughulikia, linawezekana. Yule Mkuu wa Mkoa na yuleMkuu wa Wilaya wameamua kuchukua vijana waliomalizaChuo Kikuu wamewatafutia mashamba, wamewatafutiatrekta, wale vijana wanafanya kazi nzuri sana. Kwa hiyoinawezekana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, benki ya CRDB imeamuakushughulika na vijana ambao hawana collateral,wanachukua vyeti vya kumaliza Chuo Kikuu anapewamkopo, ni hatua ya kutoa ajira kwa vijana. Kwa hiyo,pendekezo langu la kwanza, ajira ndio ingekuwa kipaumbelechetu cha kwanza.

[MHE. E. N. LOWASSA]

91

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pendekezo la pili ni elimu,ameisemea vizuri msemaji, tuangalie jamani mjadala huu juuya elimu tusiupuuze, liko tatizo la msingi katika elimu yetu. Hizihatua zinazochukuliwa hazitoshelezi. Nilitegemea Kamati hiiingepata taarifa ile ya Waziri Mkuu iliyotolewa juu ya elimukama ingetupa baadhi ya matatizo wanafanya nini ilituangalie tunafanya nini. Haitoshi kuchukua wanafunzi wengikumaliza Vyuo Vikuu wakati akienda kwenye market digrii ilehaifai, haipo katika market. Unamfundisha ana digrii lakinikazi hamna. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzetu Wajerumaniwanagawa digrii nusu na hawa walio na skills nusu, yuleanayemaliza Skills ana hakika ya ajira, yule anamaliza ChuoKikuu ana hakika ya ajira. Sisi wanaomaliza Chuo Kikuu hapawengi hawana hakika ya ajira kwa sababu ya aina yaeducation tunayoitoa, we are not imparting skills. Kwa hiyo,ingekuwa ni maoni yangu, kipaumbele cha pili kingekuwa nielimu, tuipe mkakati unaostahili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kelele zinazopigwa nawananchi juu ya elimu; inafaa tufanye mjadala nchini,tuzungumze, kuna tatizo gani na elimu yetu, tufanye nini chauhakika. Tusipoangalia tutaachwa na Jumuiya ya AfrikaMashariki, tutaachwa na SADC, tutaachwa na dunia,tutakuwa wababaishaji katika soko la dunia. Tuwasaidievijana wetu, tubadilishe mfumo wa elimu, tuangalie tunawezakufanya nini kizuri zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipaumbele cha tatu kwamaoni yangu, ni reli ya kati. Namsifu sana Dkt. Magufuli kwakazi nzuri sana aliyoifanya ya barabara, lakini barabara zilezimeanza kuharibika kwa kasi ya hali ya juu sana. NimetokaSingida juzi, inaharibika vibaya sana, ile ya Shinyangainaharibika vibaya sana, kwa sababu malori yanayopita nimalori ambayo yanapaswa kutembea kwenye treniyanatembea kwenye barabara, barabara zinaharibika sana.Nawaomba muiangalie reli ya kati kwa haraka sana. (Makofi)

[MHE. E. N. LOWASSA]

92

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, muda umekwenda, lakinisuala lingine tuangalie suala la foleni Dar es Salaam, it isnightmare! Nakupongeza sana Dkt. Mwakyembe kwa kazinzuri unayoifanya hongera sana, keep it up. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini haitoshi jamani, mudawa saa tunazopoteza Dar es Salaam ukizipanga kwa ajili yauzalishaji ni muda mrefu sana. Serikali haiwezi kukaa hivi hivi,this is a disaster! Haiwezekani mkakaa hivi hivi, mtafute njiaya kuangalia mnafanyeje foleni ya Dar es Salaam, sasa siyokungoja, it must be done now, vinginevyo tunaharibu sanauchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho. ni ile PresidentialImplementation Unit. Napongeza sana uamuzi wa Serikalikuanzisha Presidential Implementation Bureau, hongerenisana, lakini ningetaka mjiulize maswali machache, je, wanameno? Tatizo la nchi hii mnazungumza mambo, hakunautekelezaji! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunazungumza lakinidiscipline ya Malaysia na hapa ni tofauti, hapa kuna Uswahilimwingi wa kukaa bila kutekeleza mambo, mnaamua lakinihamtekelezi. Kinatakiwa chombo ambacho kinawezakufanya maamuzi magumu na yakawa maamuzi magumuyanayotekelezeka kweli kweli. Bila kujivisha joho la kufanyamaamuzi kwa utekelezaji wakawa na sanction wanazowezakufanya itakuwa ni kazi bure. Ni uamuzi mzuri, lakiniusipoangaliwa itakuwa ni kazi bure, ni lazima wawe na menoya kuuma. Mkishakubaliana mambo yafanyike. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haiwezekani katika nchi kilamtu akawa analalamika, Kiongozi analalamika, mwananchianalalamika, Serikali inalalamika. Haiwezi ikawa ni jamii yakulalamika, awepo mtu mmoja anayefanya maamuzi naanayechukua hatua. Bila kuchukua hatua tutaendeleakulalamikiana. (Makofi)

[MHE. E. N. LOWASSA]

93

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, nirudie moja laAfrika Mashariki, tusigombane na Kagame na Uhuru naMuseveni hamna haja, wameamua kwenda Sudan ya Kusini,sisi tunaweza kwenda East Congo ambako ni kuzuri zaidi.Tunachohitaji ni kufufua reli ya kati. Tukifufua reli ya katitutafanya vizuri zaidi kuliko wao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Batenga, atafuatiwa naMheshimiwa Moza Said.

MHE. ELIZABETH N. BATENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante kwa kunipa nafasi ili nichangie kidogo katika mjadalaulio mbele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ningekuwa nimepatanafasi, ningesema dakika tano zangu apewe MheshimiwaLowassa aliyemaliza kuzungumza sasa hivi kwa kuwa alikuwaanatupeleka vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mipango ni mizuri nanampongeza Mheshimiwa Wassira kwa namnaalivyowasilisha, lakini pia nimpongeze Mwenyekiti wa Kamatiyetu ya Bajeti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mipango hii ni mizuri, lakinikama kila Mtanzania, nasema kila Mtanzania kwa sababuinaonekana kwamba watu wengi hawafanyi kazi kwa kadriya uwezo wao wote. Kwa hiyo, Serikali ina kazi kubwa yakuhamasisha watu kufanya kazi, kila mtu mahali alipo awezekufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, muda mwingi ofisi nyingiukienda unakuta kila Ofisi ina TV, watu wana simu, mtuanaweza akawa ana simu mbili tatu, muda mwingi sana

[MHE. E. N. LOWASSA]

94

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

anaupoteza kwenye kupokea simu na kuongea na simu nakuangalia TV. Nakuwa na mashaka sana kama atakuwa nauwezo mkubwa wa kufanya ile kazi iliyomweka pale ofisini.Kwa hiyo, naomba matumizi ya TV, matumizi ya simu maofisiniyaweze kupangiwa utaratibu ili kuwaruhusu watu wawezekufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia nizungumziekuhusu miundombinu mingi ya nchi yetu ambayo mingi sasahivi haifanyi kazi. Reli ya kati haifanyi kazi kwa uwezo wakewote, reli ya TAZARA haifanyi kazi kwa uwezo wake wote, hiiinasababisha hata bandari kwa mfano, bandari ya Mwanza,bandari ya Bukoba, bandari ya Musoma na bandari nyinginekutoweza kufanya kazi kwa uwezo wake kwa sababu haipatimzigo wa kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono kwambakwanza tutengeneze vile vilivyopo, reli ya kati itengenezwevizuri na hata reli ya TAZARA iweze kutengenezwa ilikupunguza matumizi ya barabara kwa malori hayamakubwa, kwa sababu barabara zinakula pesa nyingi nazinatengenezwa kwa bei kubwa, lakini baada ya mudainaharibika hivyo inabidi kufanyiwa matengenezo. Kwa hiyo,naomba sasa tujielekeze kwenye kutengeneza reli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie reli niliyoisomakatika ukurasa wa tisa wa hotuba ya Mheshimiwa Wazirikwamba. kuna reli itatengenezwa kutoka Isaka kupita Kezakwenda Msongati. Sehemu ilipo Keza naifahamu kwa sababundiyo kwetu. Lakini jirani na Keza kuna mradi wa KabangaNickel ambao umesuasua muda mrefu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakuwa wakati mwinginetunausikia wakati mwingine unapotea masikioni hatuusikii,sasa hatuelewi Serikali inafanya nini kwa sababu hii reliambayo itatoka Isaka kupita Keza kwenda Msongati, Burundiwao wenzetu watakuwa wana nickel ya kusafirisha, sisi

[MHE. E. N. BATENGA]

95

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Tanzania tutakuwa tumenufaika nini na hii reli ambayo itapitakatika maeneo yale ya Keza, Mgarama na kupita kwendaBurundi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali ioanishemipango yake, Waziri wa Nishati nilisikia ametia sahihimkataba wa kufua umeme eneo la Rusumo. Umeme huuwa Rusumo kama kweli utafanikiwa, lakini pia na reli hiiinayokwenda Msongati itafanikiwa, basi Mradi wa KabangaNickel uanze ili na sisi hiyo reli iweze kutusaidia badala yakwenda kusaidia wenzetu wa nchi jirani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba wahusika wafanyehima kuhakikisha kwamba huu mradi wa Kabanga Nickelkama kuna matatizo, kama ni wawekezaji hawajapatikana,lakini pia hata miundombinu bado haijawa tayari, vitu vyotehivi viwe tayari ili maeneo yale na yenyewe yaweze kufaidihayo matunda ya uhuru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema hizodakika zangu kama ningekuwa nimepanga vizuri,Mheshimiwa aliyenitangulia angeweza kuzitumia kwamafanikio zaidi.

MWENYEKITI: Aliyetangulia hawezi kurudiaameshamaliza, ulikosea. (Kicheko)

Mheshimiwa Moza hayupo, Mheshimiwa MkiwaKimwanga atafuatiwa na Mheshimiwa Diana Chilolo.

[MHE. E. N. BATENGA]

96

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. MKIWA A. KIMWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Nami ningependa kuchangia kidogo Mpango waMaendeleo ya Taifa. Nikianzia na eneo la utawala bora,ningependa katika mpango huu ungetueleza wazi kwasababu haukuingiza mpango wa uundwaji wa Mikoa mipya,Wilaya mpya, Halmashauri, Kata na Miji midogo.

Kwa hiyo, ili kuendana na mpango ambao unawezaukakidhi vigezo, ni vyema hivi vitu vingeingia kwenyempango; hii Mikoa, Wilaya, Kata zingeingia kwenye mpangokwa sababu tunapoamua kuanzisha utawala wa maeneomapya hutumia gharama kubwa sana. Hivyo ningeombampango huu ungezingatia hayo, kwani katika mpango wakuunda Mikoa mipya tunahitaji ardhi, watu na rasilimali viendesambamba. Tusiangalie tu wingi wa watu bila kujua ardhikama inaweza ikatosha na hii ndiyo inapekelea ugomvi bainaya wakulima na wafugaji kwa sababu tunaanzisha Mikoamipya, Wilaya mpya, Kata mpya bila kuzingatia ardhi. Je,matumizi yatakuwa yako sawa na mipango ambayotumeenda nayo?

Kwa hiyo, ningeomba Mheshimiwa Waziriatakapokuja kufanya majumuisho aweze kuingiza huuuundwaji wa utawala mpya katika mpango ambaoametuletea hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa hatuzingatii hilo,ndiyo maana tumeshindwa kufikia malengo ya mpangokwamba matumizi ya kawaida yawe asilimia 65 na matumiziya maendeleo yawe asilimia 35. Hapo hatutafikia kamahatutaweka mipango yetu vizuri ili tuweze kutoka tulipo natusiwe na mipango ya kuandika bila utekelezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa niongeleekidogo suala la uvuvi. Katika uvuvi inachangia pato la Taifaasilimia mbili. Lakini kuna wavuvi zaidi ya laki tatu katikabahari, mito na maziwa makuu, wavuvi wanafanya kazi yauvuvi. Pia tunapata tani zisizopungua 40,000 katika uvuvi huo.Lakini katika mpango nilikuwa na pendekezo dogo. Haowavuvi wakubwa wa meli ambazo zinazokuwa katika bahari

97

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

[MHE. M. A. KIMWANGA]

ya Hindi wanatozwa leseni tu za uvuvi. Mimi nilikuwanapendekeza hawa sasa walipe mrahaba ili nchi iwezekujiendesha na tuweze kupata pesa na tuweze kuepukakuwasumbua wavuvi wadogo wadogo ambaowanasumbuliwa bila sababu zozote za msingi. Kama hawawavuvi wakubwa watalipa mrahaba, unaweza ukachangiakuendeleza wavuvi wadogo na wao wakaweza kukopeshwakupitia mrahaba huo huo na wao wakaweza kujikwamua.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi Serikali inawabanazaidi wavuvi wadogo kwa kuwatoza leseni zaidi ya maramoja. Mvuvi mdogo anaweza akakata leseni katika Wilayaya Ilemela, lakini akiingia Wilaya ya Nyamagana tu,anaombwa leseni nyingine. Akate leseni nyingine au alipefaini au alipie ushuru. Akitoka hapo akienda Sengeremaanaombwa tena leseni hiyo hiyo Lakini hawa wavuviwakubwa hawalipi mrahaba, wanavua wanatumalizia malizetu za asili kuanzia kwenye madini, mpaka kwenye uvuvi.Wao wanajiita tu wawekezaji, lakini ningependekeza katikaMpango huu wavuvi waongelewe kwa uwazi zaidi na wavuviwakubwa walipe mrahaba ili wavuvi wadogo wawezekujikwamua na siyo kuangamizwa kila siku. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuongelea tenakuhusu suala la Vyuo vya VETA. Mpango unasema kwambakatika masuala ya elimu katika Vyuo vya VETA kufikia mwaka2025 tutapata wahitimu ambao ni watalaam 635,000, lakinimpaka sasa tumeshapata wataalam 116,000 tu. Huu Mpangounaonekana unasuasua na kwa usuasuaji huu, hatutafikiamalengo ya Mpango. Ni vyema sasa tukaangalia walimukatika Vyuo vya VETA, vitendea kazi katika Vyuo hivi nakuwajali wanafunzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kwambatumejenga Vyuo vya VETA, lakini Vyuo vingi tunajenga havinavitendea kazi, havina mabweni ya kulala wanafunzi; natunafahamu kabisa wazi, kuna vijana wamemaliza Kidatocha Nne, kuna vijana wanamaliza Darasa la Sabawanajiunga na VETA, lakini ukiangalia hata malazi yao, yaani

98

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

[MHE. M. A. KIMWANGA]

hakuna mabweni. Vijana wengi wanatakiwa kwenda kukaanje ya mabweni. Huu ni mwanzo wa kuwaachia watotowengi uhuru wengine wakiwa wadogo ambao wamemalizaDarasa la Saba, kujitegemea pasipo na sababu.

Sasa katika Mpango huu wangeongea wazi, pamojana kwamba wataongeza Vyuo vya Ufundi, lakini waongeewazi kwamba wataongeza wataalam, wataongezavitendea kazi, waweze kwenda sambamba na mpango waTaifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ningependa kuchangiakidogo upande wa maji. Ni aibu kwa Mikoa ya Kanda yaZiwa; pamoja na kwamba tunaambiwa kuna Mpango waMiradi Mikubwa, lakini ni aibu upande wa Kanda ya Ziwa,mtu anakaa hata mita 200 haifiki eti naye ana shida ya maji.Huu Mpango ungekwenda vizuri ukaangalia wale watuwalioko kando kando ya maziwa angalau iwe Ziwa Victoria,Ziwa Tanganyika na ziwa lingine lolote lile ili watu hawawaweze kupata maji bila usumbufu.

Kama Mpango hautawaangalia watu wanaokaakando ya kando ya maziwa, hawa watu wanaokaa mbalizaidi, kwa mfano hawa wanaotaka maji ya Ziwa Victoriayaende Tabora, yatafika leo kama mtu anakaa kando yaziwa hapati maji?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tungewaomba, pamoja najitihada ambazo Serikali inafanya, iongeze mara mbili ilituweze kufika vizuri katika Mipango ambayo tunayoipanga.Siyo kupanga tu! Kikubwa tungeomba utekelezaji. Kwasababu kama kupanga tumeshapanga sana, lakiniutekelezaji ni hafifu. Tungeomba utekelezaji uende kwa kasina Mpango wenyewe tunaoujadili na pia tungeombaWaheshimiwa Mawaziri wasikil ize haya waendewakayafanyie kazi ili tuweze kutoka hapa tulipo na tuwezekusonga mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)

99

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MWENYEKITI: Ahsante. Nilisema anayefuata niMheshimiwa Diana Chilolo, atafuatiwa na MheshimiwaPamba. Wengine nitawataja baadaye.

MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nitumie nafasi ya awali kabisa kukupongeza wewebinafsi kwa kazi nzuri uliyofanya ya kuunda Kamati ya Bajetiambayo ni Kamati mtambuka. Kwa kweli Kamati hiiimeonesha jitihada za juu sana. Ninaamini kama Kamati hiitutaiunga mkono na tutatoa ushauri sambamba na Kamatihii, ninaamini sasa Bajeti ya nchi yetu itakwenda vizuri, italetamaendeleo kwa maslahi ya Watanzania. Mungu akubarikisana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile nimpongezeMheshimiwa Waziri mwenye dhamana kwa kuleta mpangowa bajeti nzuri kabisa na naomba tu uwe tayari kupokeaushauri wa Waheshimiwa Wabunge ili uweze kuboreshampango wako. Baada ya kupongezi hizo na kumpongezaMwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, sasa naomba nishauribaadhi ya mambo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siku zote kupanga nikuchagua na sisi lazima tuwe watu wa kuchagua na vile vileunapochagua vipaumbele vyako katika kuandaa bajetiyako, lazima uangalie: Je, una uwezo wa kifedha kwa kiasigani? Ni lazima sisi Waheshimiwa Wabunge tuisaidie piaSerikali, ni jinsi gani inaweza ikapata fedha. Ninaamini Serikaliinashindwa kutekeleza mipango yake vizuri kwa sababu yakuwa na fedha ndogo. Ndiyo maana kila wakati tunaambiwasungura mdogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani Serikalihaijaangalia vizuri vyanzo vyake vya fedha. Nilikuwanaongea na msomi mmoja Dar es Salaam wa Chuo Kikuuambaye alifanya research kwa mitaa minne tu ya Dar esSalaam, pale Sinza, akaenda Makongo Juu, akaenda mitaaminne tu, akagundua kwamba endapo Serikali ingejikitakutafuta kodi ya nyumba tu zinazopangishwa pamoja nanyumba za biashara kwa mitaa minne tu, yule dada wa Chuo

100

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

[MHE. D. M. CHILOLO]

Kikuu Dar es Salaam alipata Shilingi bilioni 28. Kama mitaaminne inaweza ikatoa Shilingi bilioni 28: Je, tukikusanyamapato hayo kwa Kinondoni nzima, tukienda Ilala, tukiendaTemeke na nchi nzima kwa ujumla, tutakuwa na fedha kiasigani? Ninaamini kabisa vyanzo vyetu tukiviboresha natukavisimamia kwa kina, mipango yetu ya bajeti itakwendavizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata tukiamua kwambasasa tunahakikisha tunapeleka umeme kwenye vijiji vyote,itawezekana kwa sababu tutakuwa na fedha. Hatuwezitukawa tunaweka mipango bila kuwa na fedha. Namshukurusana Mheshimiwa Lowassa hapa, ametoa mifano ya Igungana Tabora ya DC aliyeamua kuwashika vijana wasomi,kuwapa ardhi na vitendea kazi, kuzalisha kilimo.

Ni kweli, ardhi yetu hatujaitumia vilivyo katika kilimo.Tunapita ardhi nyingi humo njiani tukitembea, unakutahamna chochote kinachoendelea. Siyo hiyo tu, hatatukienda kwenye kilimo cha umwagiliaji, tumejikita kwakiwango gani? Kimezalisha pato la nchi hii kwa kiwango gani?Tunapozungumza mipango, ni lazima tuzungumze: Je, fedhatunazipata wapi? Hebu tuangalie fedha, tuhakikishetunazalisha fedha kikamilifu katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabungehawa wameshauri mambo mengi sana na mambo hayawameyaona katika nchi za wenzetu. Hivyo, naomba safariza Wabunge nje ya nchi kwenda kujifunza, bado MheshimiwaSpika unatakiwa kuendelea kufanya hivyo kamaunavyofanya sasa hivi, Waheshimiwa Wabunge waendeleekupata elimu ili waendelee kuishauri Serikali yetu. Unawezaukaishauri Serikali yako kama na wewe unakuwa na upeomzuri wa uelewa kwamba wenzetu katika mipango yaowanafanya nini? Wamefanikiwaje? (Makofi)

Mheshimiwa Lowassa ametoa mifano ya nchimbalimbali ambazo zimefanikiwa. Sasa ni sisi Kamati yetu hii,lazima tuipe kipaumbele itembee, ijifunze ilete mipango hiyokatika nchi yetu. Tukifanya hivyo, nchi yetu ina uwezo kabisa

101

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

[MHE. D. M. CHILOLO]

kuondoka katika nchi masikini na kuwa katika nchi yenyeuwezo hata wa kati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo natakaniseme, ni kweli utekelezaji wa mipango yetu unakuwa dunikwa sababu hata wasimamizi wana mishahara duni. Kilamradi unaoanzishwa, mtendaji wa Serikali anahakikishakwamba amemega hapo, amejenga barabara, amejengana nyumba yake. Wanafanya hivyo kutokana na umaskini.Hebu katika mipango yetu tuangalie na mishahara yawatumishi, tuhakikishe nayo imekaa vizuri ili tutakapowapamajukumu ya kusimamia miradi ya maendeleo, wawezekusimamia vizuri na iweze kukamilika.

Mheshimiwa Spikia, baada ya kusema hayo,nakushukuru sana, na ninaunga mkono Mpango huu.(Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante kwa kunipunguzia muda. Sasanitamwita Mheshimiwa Pamba, atafuatiwa na MheshimiwaRitta Kabati na Mheshimiwa Augustino Masele atakuwa wamwisho kuongea asubuhi hii.

MHE. SALEH A. PAMBA: Ahsante sana MheshimiwaSpika ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati hii, kwa kunipa nafasina mimi niweze kuchangia katika Mpango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mengi yameshazungumzwa.Kwa hiyo, itaonekana kama nayarudiarudia lakini kunamaeneo ambayo nitapenda yaweze kuwekewa mkazo hasawakati wenzetu wa Tume ya Mipango watakapotuleteampango kamili. Kwa sababu walichotuletea hapa nimapendekezo tu ya maeneo mbalimbali ambayoyataingizwa kwenye Mpango.

Wakati nikitaka kufanya hivyo nataka nichukue nafasihii kwanza ni-declare kwamba mimi ni Mjumbe wa Kamatiya Bajeti ambayo iliuchambua Mpango huu kwa kina sana.Napenda nimpongeze Mwenyekiti wangu na Kamati nzima

102

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

[MHE. S. A. PAMBA]

kwa ripoti nzuri ambayo imeletwa hapa ili kulisaidia Bungelako. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna matatizo kidogo katikampango huu hasa katika masuala ya uandishi. Ukiangaliakutoka ukurasa wa 13 mpaka wa 47 kuna maneno mengiambayo yameelezwa humo ndani ambayo katika utaratibuwa kuandika wangeweza kuyaleta tu kwenye Jedwali nakuwa na focus zaidi katika Mpango wenyewe. Lakini ambalonataka kulizungumzia limezungumzwa vizuri zaidi hasa katikaeneo la ugharamiaji wa Mipango.

Mpango wetu huu tuliouandaa wa miaka mitanotunataka tutumie Shilingi trilioni 44, lakini hali halisi ni kwambamakusanyo yetu na mapato yetu ni Shilingi trilioni tano tu.Kwa misingi hiyo, maana yake ni kwamba mpango huulazima urudi tena hasa ule mpango wa miaka mitano uruditena ili tuweze kuangalia resources tulizonazo. Kwa hiyo, tunaresources kidogo. Kwa misingi hiyo, lazima turudi na kuwezakutoa vipaumbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia katika Mpangohuu ni kwamba tuna upungufu karibu Shilingi trilioni tatu kwakila mwaka. Kwa hiyo, hatuwezi kuendelea kupangamipango mikubwa wakati fedha zenyewe hazipo.

Wabunge wengi hapa kwamba kupanga nikuchagua na ni kweli, lazima tufike mahali kwamba tuchaguemiradi michache ili kusudi kwa fedha chache tulizonachotuweze kuzitekeleza. Kwa hiyo, napenda nishauri yafuatayo,kwa wenzetu wa Mipango wakati watakapokuja naMpango. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza ambalo napendakushauri ni kwamba tusiazishe miradi mipya mingine.Tutekeleze miradi ile ambayo tunayo sasa hivi; na kamatunataka kuanzisha miradi mipya basi tuwe na uhaka wafedha, kama ni za ndani au ni za nje ili tuweze kusonga mbele.(Makofi)

103

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

[MHE. S. A. PAMBA]

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wa pili ambaonataka kuuzungumzia, ni kwamba ukipitia katika taarifa hiiambayo imeletwa na Serikali, utaona miradi mingi sanaimekuwa ni viporo. Kwa hiyo, katika mpango unaokuja lazimakuwe na commitment ya Serikali ya kuhakikisha kwambatunamaliza katika kipindi cha miaka miwili iliyobaki kabla yauchaguzi, miradi yote viporo ili kusudi tuweze kujenga imanikwa wananchi na kuweza kusonga mbele. Hayo ni maeneomawili ambayo nilifikiri ni muhimu sana katika kutekelezaMpango wowote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuteleza Mpangokuna changamoto mbalimbali. Mipango yote hiitunayoizungumzia ya Shilingi trilioni 5.2 tunazungumzia juu yacommitment na tunazungumzia juu ya manunuzi. Asilimia 70ya fedha za Serikali zinakwenda kwenye manunuzi natumeona kabisa kwamba tunayo matatizo makubwa naSheria ya Manunuzi. Mpango huu wote ambao tutaupitishahautakuwa na maana kama hatutafanya marekebisho yadhati kabisa katika Procurement Act. Naomba wenzetu waSerikai kwamba ili tuweze kusonga mbele kwa speedtunayoitaka, walete Bungeni hata kwa certificate ya dharuratuhakikishe kwamba tunafanya mabadiliko haraka katikaSheria hii ambayo itakuwa ni kikwazo katika kutekelezaMpango huu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Lowassaamezungumza vizuri sana na sipendi kurudia yale ambayoamezungumzia. Lakini moja nalo ambalo ni kikwazo pia, siyoSheria bali ni maamuzi, decision making; urasmu mkubwandani ya Serikali katika kutoa maamuzi. Miradi mbalimbali,miradi ya ubia kati ya Sekta Binafsi na Serikali na sekta nyingineya Umma inachukua muda mrefu sana. Watu wanazungukakutoka Ofisi moja mpaka Ofisi nyingine, at the end of the dayhawapati maamuzi. Nchi haziendeshwi namna hii! Nchizinaendeshwa kwa kutoa maamuzi ya haraka. Hao wenzetutunaozungumzia kwa mfano Malaysia wanatoa maamuzi yaharaka, wanachukua commitment! Ukipewa madaraka yakuongoza, toa maamuzi wenzako wakusahihishe kamaumekosea.

104

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

[MHE. S. A. PAMBA]

Kwa hiyo, hayo ni maeneo ambayo yanatakakubadilisha focus na utendaji wetu ndani ya Serikali nakuhakikisha kwamba maamuzi yanatolewa haraka hasamaamuzi yanayohusu masuala ya kiuchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambaloningependa kuzungumzia ni maeneo ambayo naona katikaMpango hayajapewa umuhimu. Katika mipango yote, eneola kwanza ambalo lina potential kubwa lakini halijapewaumuhimu, halijapewa fedha ni eneo la uvuvi. Mchango wakeni 1% tu katika pato la Taifa. Mwaka juzi, mwaka jana, hakunafedha zilizotolewa katika eneo hili. Wenzetu wa mipangomwende mkaweke fedha ili kusaidia sekta hii ambayo inapotential kubwa ya kuinua uchumi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalonapenda nilichangie ni utalii. Nchi yetu imebarikiwa, wotetunajua na utalii ni eneo ambalo wewe unaweza ku-tape tuna kupata pesa pale, lakini hatutumii fedha za kutosha katikakutangaza utalii. Unatumia dola milioni 10 wenzakowanatumia dola milioni 100. Watakwenda kule ambakokumetangazwa! Nimeona bajeti ya utalii haitoshi hatakidogo. Kutoa tangazo katika CNN ni Dola milioni mbili. Walemnaowaona Malaysia wanatangaza kwenye CNN na ma-Television ya Kimataifa ni gharama kubwa. Wapeni pesa zakutosha, watalii watakuja nchini. Tanzania ina vivutioambavyo ni unparallel, huwezi kuvilinganisha na nchi yoyoteduniani, lakini hatujaweka fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho ambalo natakakulizumgumzia ni kwamba Tanzania tumeingia katika uchumiwa gesi, lakini hakuna maandalizi. Hakuna maandalizi yakuhakikisha kwamba, tunafaidika vipi na gesi hii? Katikamiaka mitano ijayo Tanzania itaingia katika uchumi wa gesi;tunataka maeneo mawili yafanyiwe kazi haraka na yaletwehapa Bungeni. Moja, Sera ikamilike haraka sana. Pili, mleteSheria ya Gesi hapa Bungeni. Hatuwezi kwenda hivi hivi bilakujua kwamba nchi yetu itafaidika vipi, wananchi wetuwatafaidika vipi katika economy hii ambayo ni kubwa sanahapa duniani. (Makofi)

105

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

[MHE. S. A. PAMBA]

Mheshimiwa Mwenyekiti, hayo ni maeneo ambayolazima yafanyiwe kazi haraka. Hatuwezi kuacha makampuniyaliyoko kule Mtwara yaka-dictate, yakatulazimisha kufanyamambo ambayo wao wanaendelea kwa sababu, Serahakuna. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria muda waMzungumzaji kwisha)

MHE. SALEH A. PAMBA Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja asilimia mia kwa mia. Ahsante sananakushurukuru kwa nafasi.

SPIKA: Ahsante sana. Namwita Mheshimiwa RittaKabati, atafuatiwa na Mheshimiwa Augustino Masele.

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti,nachukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu nakukushukuru wewe kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangiaMapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwaMwaka 2013/2014. Lakini kabla sijachangia, kwanzanikupongeze kwa kuteuwa Kamati ya Bajeti, Kamati ambayoimekuwa ikifanya vizuri sana na nikushukuru kwa kutuleteahaya Mapandekezo ya Mpango mapema kabla hatujaanzakujadili bajeti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma ukurasa wa 48 waKitabu cha Mpango, unaonesha maeneo ya kipaumbelekatika mwaka 2014/2015, lakini utaona Mpango umejikitakatika maeneo machache yanayoendana na programu yaThe Big Results Now (BRN), yaani matokeo makubwa sasa.Pamoja na hayo, ningependa kujua vigezo vilivyotumikakatika kuchagua miradi ya vipaumbele. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kabla yayote nimpongeze Waziri wa Ujenzi, kwa sababu barabaranyingi sana zimejengwa; naipongeza sana Serikali.Tumetembea maeneo mengi sana na tumejionea jinsiambavyo barabara zimejengwa. Hata katika Mkoa wetu waIringa kwa mfano barabara ya Mtera – Iringa, Mafinga – Iringa

106

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

[MHE. R. E. KABATI]

ni kati ya barabara ambazo zimejengwa na Serikali yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nina masikitikomakubwa sana kuhusiana na Serikali kutokutoa kipaumbelekatika reli ya kati. Wabunge wengi sana waliochangiawameelezea kuhusiana na hii reli ya kati. Kwa kweli, naombaniungane nao kwamba, Serikali sasa itoe kipaumbele katikakujenga reli hii. Hii itasaidia kwanza kudumu kwa barabarazetu na vilevile itasaidia sana kukuza uchumi kwa sababu,tumekuwa tukitumia pesa nyingi sana katika kujenga hizibarabara na kufanya matengenezo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma ukurasa wa 53,Serikali katika mipango yake imesema, ili kuboresha eneo lautalii itaendelea kujenga miundombinu na kukarabatimiundombinu ya usafiri, lakini haijaainisha ni maeneo ganiyamepewa kipaumbele. Kwa mfano, katika Mkoa wetu waIringa ipo mbuga ya wanyama ya Ruaha National Park. Hii niya pili kwa Afrika kwa ukubwa. Mwaka 2012 nilileta swali languhapa kwamba hii barabara ni mbovu, miundombinu yakesiyo mizuri na tuna imani kama hii barabara ingeimarishwana kujengwa vizuri ile mbuga ya wanyama ingewezakutusaidia sana katika utalii na ingeweza ikakuza kipato naingeleta ajira kwa wana-Mkoa wa Iringa na Taifa kwa ujumla.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tuna kiwanja chandege, kiwanja ambacho kama kingepewa kipaumbele,kikajengwa kingeweza kusaidia watalii wengi kuja na kusaidiakatika uchumi wetu. Sasa ningeomba Serikali iangalie, kamaimeshasema katika mpango wake kwamba itajengamiundombinu katika maeneo ya utali i, basi i jengemiundombinu hiyo ya Kiwanja cha Ndege cha Nduli katikaMkoa wetu na vilevile iimarishe ile barabara inayokwendakatika mbuga za wanyama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ukurasa wa 53,wamezungumzia kuhusu elimu ya mafunzo na ufundi.Wamesema kwamba, mpango wa kuimarisha mafunzo kwa

107

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

[MHE. R. E. KABATI]

kuongeza mbinu ya kugharamia elimu nchini. Naipongezasana Serikali yetu kwa kuweza kutenga zaidi ya shilingi bilioni306 ambazo walikidhi kuwapa wanafunzi 29,754 kati yawanafunzi 31,649 ambao ni sawa na 96%. Lakini vijana wetuwanakabiliwa na changamoto kubwa sana katika huumkopo ambao wanapewa katika vyuo vyao; wanafunzikushindwa kupata mikopo hiyo kwa wakati, matokeo yakekumekuwa na vurugu vyuoni, migomo mingi, kisha wanaletampaka maandamano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Wizara ya Elimu,hebu iliangalie hili suala kwa umakini mkubwa sana. Tunasikiauchungu sana tunapoona vijana wetu wanashindwa kuifikiaile mikopo. Ile the Big Result tutaipataje kama vijana hawakutwa nzima wanafanya maandamano, wanafanya vuruguna Serikali imeshaamua kuwasaidia hawa vijana wawezekupata hii mikopo? Ningeomba Bodi ya Mikopo hii iangaliweupya ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wote wanapatiwaile mikopo.

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Serikaliyetu; sasa hivi Mkoa wetu wa Iringa una vyuo vingi, zaidi yavinne. Sasa tunajisikia vibaya kwamba tunapokuwa katikamaofisi yetu, vijana hawa mara nyingi wamekuwa wakijawakitaka tuwasaidie ni jinsi gani ya kupata mikopo wakati nihaki yao ya msingi. Kwa hiyo, naiomba Serikali izingatie sanavijana wetu waweze kupatiwa hiyo ili waweze kuwa ndiowataalamu wetu, tunawategemea katika nchi hii; ndioMarais wetu Mawaziri wetu wajao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kitabu cha Mpango,sijaona kama imetengwa fedha kwa ajili ya Researchers. Sasasijui bila utafiti tutaweka mipango gani? Ningeomba Serikaliiangalie, itoe kipaumbele kwa watafiti wetu. Tunajuakwamba, tukifanya utafiti vizuri katika miradi mingi itatusaidiasana kuhakikisha kwamba tunapanga mipango mizuriambayo inatekelezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipanafasi hii. Ahsante.

108

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

SPIKA: Ahsante. Namwita sasa MheshimiwaAugustino Masele.

MHE. AUGUSTINO M. MASELLE: Ahsante MheshimiwaMheshimiwa Mwenyekiti, ambaye ni Spika wa Bunge letu kwakunipa nafasi hii ili na mimi niweze kutoa mchango wangukatika mpango huu wa Serikali yetu unaohusu maendeleoya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nami niungane nawenzangu kukupongeza wewe kwa kutuanzishia hiyo Kamatiiliyo makini na ambayo kwayo imepelekea kuwepo naMapendekezo mazuri ya Mpango wa Maendeleo wa nchiyetu. Hakuna nchi yoyote duniani ambayo imewezakuendelea isipokuwa na mipango endelevu. Kwa ajili hiyo,napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Nchi kwakuweza kuja na Mpango wetu mzuri wa Maendeleo ambaokwa ujumla umesheheni mambo mbalimbali yaliyoko katikaVitabu vyake vyote viwili; kile kidogo pamoja na hiki kikubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu imejaliwa mambomengi, ina rasilimali za kutosha. Mambo yaliyosalia ni yanamna gani tunavyoweza kujipanga na kuyasimamia.Mipango yote iliyoelezwa katika Kitabu cha Mpango waMaendeleo wa Miaka Mitano na huu tunaoujadili kwa leowa 2014/2015 ni mapendekezo ambayo yanatakiwa yapewemsukumo wa kipekee na zaidi sana upatikanaji wa fedhakwa wakati; maana tunapoendelea kuwa tunapanga halafuhatutekelezi, tutakuwa tunatengeneza madeni ambayotutakuja kudaiwa mbele ya safari, hasa ikizingatiwa kwamba,kila baada ya miaka mitano kuna uchaguzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Reli ya Kati naBandari ya Dar es Salaam ni suala ambalo haliepukiki.Tunapaswa kuhakikisha kwamba tunawekeza ipasavyokatika suala la bandari. Maana ukiangalia nchi za wenzetu,nchi za Uarabuni, nchi za Mashariki ya Mbali, zimeendeleakwa kuwekeza zaidi katika Bandari zao. Nasi Mwenyezi Mungukatika uumbaji wake ametujalia kuwa na vitu vyote vitatu;tuna anga, tuna maji, tuna ardhi. Kwa hiyo, tukiwekeza katika

109

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

[MHE. A. M. MASELLE]

mambo yote haya matatu, nina uhakika kwamba tutapigahatua kwa haraka sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la umeme. Nchi zoteambazo zimeendelea duniani hapa zimewekeza kwakiwango kikubwa katika umeme. Nami niseme tu kwamba,tumshukuru Mungu kwa sababu sisi Waafrika alituumba naakatuweka katika Bara hili ambalo kimsingi halifikwi na yalemajira mawili yenye hatari; wakati wa summer na wakati wawinter. Nchi za wenzetu wanaweza ku-survive wakati huo kwakutumia umeme. Kukiwa na summer wanatumia umemekuhakikisha kwamba wanapata baridi na wakati wa winterwanatumia umeme kuhakikisha kwamba wana-heatmazingira yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwetu sisi kwa sababu yakutokuwa na haya majira, inawezekana ndiyo maanatumekuwa tukipuuzia namna ya kuzalisha umeme wauhakika. Maana vinginevyo, nchi hii tungeweza kuangamiakama tusingekuwa tumejaliwa na Mungu kuishi katika nchiambayo ina joto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba tukwamba, pamoja na majaliwa haya ambayo Munguametusaidia tukawa na hali ya hewa nzuri, basi tujipe pongezikwa kuwa na hiyo hali, lakini tujizatiti katika kuhakikishakwamba, tunazalisha umeme ambao utatuhakikishiakwamba, tunawekeza masuala ya viwanda. Maana bilakuwa na umeme huwezi ukawekeza viwanda vya kuboreshathamani ya mazao ambayo yanazalishwa katika nchi yetu.

Kwa mfano, nchi yetu inazalisha pamba; kwa hiyo,upo uwezekano mkubwa tu wa kuwekeza viwanda vya nyuzina nguo. Tuna mifugo mingi tu ambayo na yenyewe inawezaikawa ni chanzo kizuri tu cha kuwekeza katika viwanda vyabidhaa za ngozi, zikiwemo viatu na mambo menginembalimbali kama mikoba na vitu vingine. Vitu hivi tukivizalishakatika nchi yetu, tunaweza tukaviuza katika nchi za wenzetuna tukapata fedha za kigeni ambazo zinaweza zikaendelezauchumi wetu.

110

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

[MHE. A. M. MASELLE]

Mheshimiwa Mwenyekiti, mara nyingi nimekuwanikiuliza hapa suala la kuanzishwa kwa Mamlaka ya Hifadhiza Wanyamapori; na Wizara ya Maliasili imekuwa ikiahidikwamba itatuletea Sheria itakayounda hiyo Mamlaka. Sasanashauri kupitia Mpango huu kwamba, suala hili lipewekipaumbele, kwa sababu mimi ninakotoka tuna pori la akibala Kigosi, lakini pori hili limeonekana halina maslahi kwetu kwasababu ya ukubwa wake, lakini lina watumishi kama 30 tu,lakini miundombinu yake ni hafifu na wakati mwingine hatahuu uhujumu uchumi unaofanywa na Wawindaji haramu nawenyewe unaathiri eneo hili ambalo kimsingi, kamalingeendelezwa, lingeweza kuchangia kwa vile lingevutiawawekezaji na watalii kutoka nchi za nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie pia suala lakiwanja cha ndege cha Mwanza. Najua sasa hivi nchi yetuimeshakuwa na viwanja vya ndege vya Kimataifa vitatu; chaSongwe na kile cha Dar es Salaam pamoja na chaKilimanjaro. Mimi nashauri kwamba, hata kiwanja cha ndegecha Mwanza na chenyewe kipewe kipaumbele kuwakiwanja cha ndege cha Kimataifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo,nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa Wabunge, kamainavyoonekana muda umekwenda, dakika tano hazitoshimtu mwingine kuchangia. Tukaporudi, utaratibu wa jioniutakuwa kama ifuatavyo:-

Tutakapofika hapa atapewa nafasi MheshimiwaJoseph Mbilinyi na Mheshimiwa Chiku Abwao dakika tanotano. Watafuatia na Mheshimiwa Mosi Kakoso naMheshimiwa Michael Laizer. Hawa ndio watazungumzahalafu baada ya hapo tunatoa nafasi kwa Mawazirimbalimbali kujibu hoja zilizotokana na mjadala, halafu saa12.30 tunampa nafasi Mtoa Hoja, atakuwa na muda mfupiuliobakia ku-wind.

Kwa hiyo, Bunge linarejea. (Kicheko)

111

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

(Bunge lilirudia)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kama nilivyokuwanimeeleza kwamba tutakuwa na hawa Wachangiajiwachache kutoka kwa Wabunge halafu Mawaziri watajibu,lakini Mawaziri watakapojibu watajibu kama Wachangiaji tu.Kwa hiyo, wana dakika zao kumi kumi kila mmoja. Halafututarudi katika mfumo wa Bunge, ndio Mtoa Hoja atapewanafasi ya kujibu hoja. Sasa huo ndiyo utaratibu wa Bunge.

Kwa hiyo, hiyo ndio nafasi tutakayofanya mchana,kwa hiyo, kwa sasa sina tangazo lingine. Nasitisha shughulimpaka saa 11.00 jioni.

(Saa 7.00 mchana, Bunge lilisitishwa hadi Saa 11.00 jioni)

(Saa 11.00 jioni Bunge lilirudia)

Hapa wabunge walikaa kama Kamati ya Mipango

(Majadiliano yanaendelea)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, kabla yakusitisha shughuli za Bunge asubuhi, nilikuwa nimewatajawafuatao kama ndio wasemaji wetu wa kwanza;Mheshimiwa Joseph Mbilinyi atachangia dakika kumi naMheshimiwa Chiku Abwao; Mheshimiwa Moshi Kakoso naMheshimiwa Michael Laizer. Mheshimiwa Joseph Mbilinyi,dakika tano.

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi kuchangia Mpango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naanza kupotezakidogo interest ya debate za Bunge kwa sababu imekuwasasa kama kila siku toka nimeingia hapa kwa mwaka wa tatunasema vitu hivyo hivyo na nikisikiliza wenzangu, piawanasema vitu hivyo hivyo. Kwa hiyo, tumekuwa humu ndanitunaongea mambo hayo hayo. Kwa sababu sasa hivi nimwaka wa tatu toka nimeingia hapa nadai ambulance kwa

112

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

[MHE. J. O. MBILINYI]

ajili ya Hospitali ya Rufaa Mbeya lakini kila mwaka naambiwakwamba bajeti itatengwa, bajeti itatengwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapozungumzamaendeleo mimi naamini kwamba hakuna maendeleo bilawatu kuwa na afya. Ile Hospitali pale majengo yake ni mazuri,nawapongeza management sasa hivi Hospitali ni safi katikaHospitali safi za nchi hii, lakini haina vifaa, haina CT-Scan,haina MR mashine ya kufanyia vipimo vinavyohitajika vyenyehadhi ya Hospitali ya Rufaa. Mtu anapohitaji tu vipimo kamahivyo inabidi aangalie safari ya kwenda Dar es Salaam. Bajetiyenyewe wanayopewa Hospitali ya Rufaa, unasikia Hospitalikama KCMC wanapewa zaidi ya bilioni 10, Rufaa nikiuliziaunasikia wanapewa 1.5, 1.8 bilioni. Sasa unauliza kwamba ileRufaa gani kama Mkoa wa Mbeya sasa hivi una watu wengizaidi ya takribani milioni 2.7? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunazungumzia maendeleoya uchumi, kutanua bandari, lakini sisi Mbeya hatuna bahari,kwa hiyo, tunasema bandari ya nchi kavu.

Kwa mwaka wa tatu nimekuwa naiomba, nashukurukwenye bajeti iliyopita Mheshimiwa Dkt. Mwakyembeamatuahidi, lakini kwa sababu nimezoea kwamba ni vile vile,inabidi nitumie fursa hii kusisitiza kwamba ile dry port ni muhimusana kwa uchumi na kama nakumbuka Mheshimiwa Sitta juziwakati anazungumzia network ya reli na umbali na unafuuwa mizigo, unaona wazi kabisa hata sisi pale ile dry portikianza kazi tutapunguza umbali kwa watu kutoka Congo nawatu watakuwa wanafanya shughuli zao pale nawataendelea kuchangamsha uchumi wa Mbeya ikiwemokwa Mheshimiwa Kaka Dkt. Mwakyembe kule Kyela. Kwahiyo, natumia fursa hii kusisitiza umuhimu wa ile Bandarikupatikana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ile bandari haiihitaji bajetiya kujenga, inahitaji kibali tu na utaratibu wa kiserikali ili tuanzekufanya kazi pale, ajira kutoka 40 sasa hivi tufikishe ajira 250/300 za direct kwa mujibu wa wataalamu wa palewanavyosema.

113

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

[MHE. J. O. MBILINYI]

Mheshimiwa Mwenyekiti, michezo pia ni maendeleo,lakini kwenye Mpango huu sijaona wala sijasikia mtuakizungumzia michezo. Inaonekana kwamba badohatuamini kwamba michezo inaweza ikachangia uchumi aupato la Taifa hili na pia hata kuchangia katika kutangazautalii wa nchi hii. Lakini michezo bado imekuwa nyuma katikamijadala. Niwape big up Mbeya. Sisi Mbeya tunajitahidi namichezo, Chama chetu Mbeya City kule kinafanya vizuri,napata heshima hata ndani ya Bunge; nikikutana na Raiswa Simba, Mheshimiwa Rage ananiangalia vizuri kidogo, kwakujua tu kwamba ninakotoka kuna Mbeya City.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchukua fursa hiikuwaasa vijana kule Mbeya kama Mbunge wao, wapunguzemizuka. Kushangilia kwa kurusha mawe siyo sehemu yakushangilia, wataiharibu mizuka ambayo tayari imeshakaasawa. Chama chetu kinakwenda vizuri, nchi nzima inajua sasahivi kwamba Mbeya kuna Mbeya City, kwa hiyo, tutumienguvu zetu katika kushangilia na kuendelea kuhamasisha timuyetu ili tuwe na justification ya kwa nini michezo ni kitu muhimuna inatakiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la wamachinganaona bado kabisa limekuwa na utata. Bado kwenyeHalmashauri zetu tunajadili kuondoa wamachinga hapa,kuwaondoa wamachinga pale bila kuja na mipangomadhubuti. Nilikuwa China; wanasema kusafiri ni kujifunza.

Sasa tunakwenda nchi za watu kujaribu ku-adopt vituvigumu ambavyo hatuviwezi, tunashindwa kuiga vitu vyepesikama suala la kuangalia wamachinga wanafanyaje kazi.Nimekwenda down town Beijing, mmachinga anauzamahindi ya kuchemsha, Polisi anapita pale na hamna nchiyenye Polisi wakali kama China kwa historia; lakini kuna mamantilie pale anauza samaki, anauza nini, kila kitu na hauoniuchafu ndani. Kuna mtu pale Mmachinga down town Beijingkabisa, anauza mahindi ya kuchemsha, hauoni Polisianamsumbua, amepewa utaratibu wa usafi, elimu ya usafi,hauoni hata jani moja limedondoka chini, unakwendasehemu…

114

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

(Hapa kengele ililia kuashiria mudawa Mzungumzaji kwisha)

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Time is too short. Thank youvery much. (Kicheko/Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Chiku Abwao.

MHE. CHIKU A. ABWAO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipatia nafasi ili nami nichangie hoja hiiya Mpango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa muda ni mdogonitachangia hoja moja tu ambayo inatokana na pato la Taifa.Mheshimiwa Waziri katika kitabu cha Mipango ukurasa wapili, amezungumzia kwamba pato la Taifa linakuwa na kwanusu ya mwaka 2013 limeongezeka kuwa 7% toka 6.9%. Lakiniukiangalia hata ukuaji huu wa pato la Taifa bado ni mdogo,na kwa kiwango kikubwa haueleweki kwa wananchi waliowengi ambao ni maskini. Kwa hiyo, tunaendelea kulalamikana umaskini na hata ukisema kwamba kuna ukuaji wa patola Taifa kwa wananchi wa kawaida wanaona kama vile nimzaha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa naona nichangiejuu ya hoja hii kwa kuiomba Serikali, kwa kuwa sasa hivi kunawanavyuo wengi wamesoma, wamehitimu vyuoni na wengiwamechanganyikiwa kwa kweli hawajui wafanye nini, kwasababu ajira zimekuwa chache. Nafikiri umefika wakati sasawa kuangalia huu mtaji wa nguvu kazi ya wanavyuo ambapoSerikali iweke mpango mahususi tu kwa makusudi kabisakuwasaidia wasomi hawa kwamba wakimaliza Vyuo vyetivyao viwe mitaji kwa sababu kutokana na hali halisi,hawakopesheki. Kwa hiyo, bila kuwasaidia kwa makusudihawatakopesheka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ionekane vyetivyao ndiyo mtaji wao na kwa kutumia wataalamu ambaonajua tunao wengi tu Tanzania, wasaidie hawa wanavyuokuandaa mipango kazi, waandikie michakato ya kazi hasa

115

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

[MHE. C. A. ABWAO]

kuelekeza nguvu zao katika vijiji, wakaboreshe kilimo,wakopeshwe kule kwa kusimamiwa na wataalamu wetu iliwaweze kuendesha kilimo na hii itasaidia sana kuboreshauchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu hatuna shidakatika ardhi, tuna ardhi ya kutosha. Kwa hiyo, wakisaidiwawanavyuo hawa, wakapewa wataalamu ambao kwakusaidiana nao wakawaandikia michakato ya kazi, programzao zikafanyiwa kazi kuhakikisha kwamba Serikali inakuwanao kwa kuwafuatilia utendaji wao wa kazi, nina imani kabisakilimo kitafanikiwa. Kwa Sera ya Kilimo Kwanza nadhaniitakuwa ndiyo chanzo cha kuifanikisha zaidi.

Vile vile wanachuo watapata matumaini kwa kujuakwamba hata kama hakuna ajira, wataweza kujiari kwa njiahizo kwa sababu Serikali itakuwa nao bega kwa begakuhakikisha kwamba wanapata mikopo na katika kuboreshakilimo pia itasaidia kwa sababu watapanuka zaidi, watakopamashine za kusindika, watakuwa na viwanda vidogo vidogona matokeo yake ajira zitaongezeka na uchumi utaongezekakwa kiasi fulani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo la wanachuo ni kubwasana, kama Serikali haitaangalia kwa kina ni jinsi ganitutawasaidia vijana hawa, tutajikuta tunajiingiza katikamatatizo makubwa. Mheshimiwa Lowassa siku moja aliwahikusema kwamba vijana hawa ni bomu la petrol. Naminakubaliana naye kabisa, ipo siku litakuja kulipuka, litatuleteamaafa makubwa.

Kwa hiyo, tunawajibika kabisa kuhakikisha tunawekamazingira mazuri ili wanavyuo waweze kufarijika kwa kupataajira kwa kusaidiwa na Serikali. Kazi pia wanapata kwa taabu,maana wanaambiwa wawe na uzoefu. Wana uzoefu wakipindi gani? Mtu anatoka chuoni, atakuwa na uzoefu ganizaidi ya kwenda field kwa muda mfupi sana ambao badounaonekana siyo uzoefu, kwa sababu anaangaliwa uzoefuwa kwamba awe ameajiriwa sehemu nyingine, ndiyo aendeakafanye kazi sehemu nyingine. Bado ni tatizo.

116

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

[MHE. C. A. ABWAO]

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Serikali iangaliekwa kina hasa namna ya kutumia huu mtaji kwa sababusiamini kama Serikali ilivyoamua kusomesha wanavyuo,kukopesha wanavyuo mikopo haikuwa na lengo. Nafikirilengo lilikuwa ni kuboresha maisha ya wanavyuo hawa,kuongeza uchumi wa nchi yetu na hasa kuondokana na hilitatizo la umaskini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzangu wengiwameshazungumza, mimi nimeona dakika zangu tanonizungumzie hili suala moja tu la kuongeza ukuaji wa pato laTaifa ikiwa ni pamoja na kupunguza umaskini wa nchi yetuna kuwasaidia wanavyuo ambao kwa kweli kwa sasawamechanganyikiwa hawaelewi wafanye nini; elimu zaosasa imekuwa hazina thamani kwa sababu wanakosa namnaya kuzifanyia kazi na kujiondoa katika janga la umaskini nashida ya ajira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa haya machachenakushukuru. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana, umejadili vizuri. NamwitaMheshimiwa Moshi Kakoso na atafuatiwa na MheshimiwaLaizer.

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Nianze kuchangiakwenye suala la bandari. Bandari ni kitu muhimu sana katikauchumi wa nchi inayokua. Bandari yetu ya Dar es Salaambado kuna matatizo mengi ambayo yanahitaji kufuatiliwakwa kina ili iweze kuwa na ushindani mzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi ya kipekeekumpongeza Waziri husika Mheshimiwa Dkt. Mwakyembekwa kazi nzuri aliyoifanya, lakini bado anahitaji kuzama kwakina ili aweze kutatua matatizo yaliyopo ndani ya bandariile. Unapoimarisha bandari, unasaidia uchumi wa nchi hii.Kuna kero ambazo zinafanya watumiaji wa bandari wawena mashaka kutumia bandari yetu. Mimi naamini zile kerozikiondolewa zitasaidia sana kushawishi nchi zinazotumia

117

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

[MHE. M. S. KAKOSO]

bandari ile mfano Malawi, Congo, achana na hii nchi yaRwanda inayokuwa na matatizo; lakini tukiimarisha bandariyetu itasaidia sana kukuza uchumi kwa nchi tu ambazozinatumia Bandari yetu; Zambia, Malawi, DRC na tukiimarishabandari nyingine kama ile ya Mtwara, bandari ndogo ndogoza Ziwa Tanganyika zitasidia sana kukuza uchumi wa nchiyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa naomba hiloliangaliwe kwa kina na waliangalie kwa umuhimu wa ainayake ili tuweze kukuza uchumi wa Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ni reli. Huwezikuwa na uchumi mzuri kama reli haifanyi kazi. Maeneo mengikatika nchi zinazoendelea reli ndiyo kiungo muhimu sana chauchumi wa nchi yoyote ile inayokuwa kiuchumi. Reli yetu yakati ndiyo reli muhimu sana ambayo inaweza ikapunguzaughali wa maisha kwa Watanzania. Usafirishaji kwa njia yabarabara una gharama kubwa sana tofauti na reli. Miminaamini tulkiimarisha reli ya kati inaweza ikachangia patokubwa sana la uchumi wetu, lakini sambamba na hiyo reli yakati bado kuna branch za reli ambazo zinahitaji kuimarishwaikiwepo reli ya kutoka Kaliuwa kwenda Mpanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wengi wa Wilayaya Mpanda wanategemea sana huduma ya reli, lakini reliiliyopo kwa sasa haifanyi kazi vizuri na treni inayotumika badoni chakavu. Kwa hiyo, tulikuwa tunaomba uimarishwaji wareli ya kati sambamba na zile branch ziweze kuimarishwakatika hali iliyo bora ili ziweze kufanya kazi vizuri. Mimi naaminikama tutaimarisha reli hizi zikafika mpaka kule kwetu Mpandana kukawa na mpango unaokamilisha kuweza kupeleka relimpaka ukanda wa Ziwa Tanganyika eneo la Kalema,tunaweza tukapata kuitumia bandari ile ya Kalemie pamojana bandari inayojengwa pale eneo la Kalema. Mimi naombaeneo hili liangaliwe kwa kina ili tuweze kusaidia uchumi wanchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalohalijazungumziwa sana ni eneo la Sekta ya Uvuvi. Tunalo Ziwa

118

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

[MHE. M. S. KAKOSO]

Tanganyika ambalo halijafanyiwa uzalishaji mzuri kwenyemaeneo ya ukanda wa ziwa kwa sababu hakuna vituambavyo vinasaidia ukuaji wa Sekta ya Uvuvi.Nilikuwanaomba eneo hili liangaliwe na liweze kupewa umuhimusana. Kukiwa na uvuvi ambao unaweza ukavuliwa kisasa,tukatengeneza miundombinu, inaweza ikasaidia kukuzauchumi wa nchi, tena kwa Wananchi na pato la Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sekta ya Kilimo ni muhimusana kwa maendeleo ya Taifa la Tanzania. Watanzania waliowengi wanategemea sana Sekta ya Kilimo. Lakini kwenyesekta hii bado hawajaweka fedha za kutosha. Wananchiwalio wengi sasa hivi wanalima kilimo cha mazoea, badoTaifa linahitaji kuandaa wataalam wa kutosha ili wawezekuwasaidia wakulima wadogo wadogo ambao watawezakuzalisha katika kiwango ambacho, kwanza watafukuza njaa;pili, watakuwa na pato la ziada kama wananchi lakini Serikaliitanufaika na pato hilo la Taifa kutokana na mazaoyatakayokuwa yanazalishwa hatimaye kuanza kuuzwa nje.Lakini kitu cha ajabu ambacho kwenye Sekta ya Kilimo kinauakabisa uchumi wa wananchi ni mipango mibovu ya Serikalihasa ya kuagiza chakula cha kutoka nje kama vile mchele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Watanzania walio wengiwamepoteza rasilimali zao kubwa kwenye Sekta ya Kilimona hatimaye kuacha kuwekeza kwa kiwango kikubwa kwasababu mazao wanayozalisha wananchi walio wengihayana soko na badala yake, Serikali inaingia katika vitendovya ajabu vya kukopa wananchi mazao yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa naomba Serikaliiangalie sana na iwekeze fedha za kutosha, hasa kwenyeununuzi wa mazao. Watakapokuwa wananunua mazaowatawapa motisha wakulima waweze kuzalisha kwakiwango kizuri na hatimaye wakapata ziada itakayokuwainakwenda nje. Lakini tofauti na ilivyo kwa sasa, wakulimawengi kile kilichozalishwa bado wanaidai Serikali kituambacho kinavunja moyo sana wakulima washindwekufanya shughuli zao kwa nia nzuri.

119

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

[MHE. M. S. KAKOSO]

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini bado kuna matatizoambayo Serikali inatakiwa iangalie na kuyarekebisha katikakipindi muafaka. Eneo hilo ni ugomvi kati ya wakulima naSerikali, hasa kugombania maeneo ya misitu na hifadhi.Karibu maeneo mengi sana Serikali imehodhi ardhi ambayowakulima au wanachi walio wengi ambao shughuli zaowanazotegemea ni kilimo, hawana mahali pa kufanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ifike mahali iangaliekwamba Watanzania huko nyuma tulikuwa wachache, sasahivi tumeongezeka na nina mifano tu kwamba katika Mkoawangu ninakotoka Mkoa wa Katavi asilimia kubwa ya Mkoaule ni mapori, hifadhi ya Taifa ya Katavi, game Reserve, kilakitu kilichopo pale, hasa misitu ni mali ya Serikali. Lakiniwananchi wanazidi kuongezeka katika maeneo yale yaleambayo walikuwa wanafanyia kazi toka kipindi hicho chanyuma. Naiomba Serikali iangalie upya, ifike mahali ipanuewigo iwaachie wakulima maeneo na yaweze kufanyiwa kaziili yaweze kuzalisha.

Kwenye suala la vijana, vijana ndio wanaotegemewakatika Taifa hili, lakini Serikali bado haijawekeza vizurikuwasaidia kundi kubwa la vijana. Vijana wanahitajikuandaliwa mazingira ambayo yatawasaidia kufanyashughuli zao pale wanapokuwa wanahitaji kwenye uzalishaji.Nilikuwa naomba Serikali iandae mpango maalum nakutenga fedha za kusaidia makundi ya vijana ambaowanapomaliza shule hawana shughuli za kufanya. Ni Serikaliikiandaa mazingira ambayo yatawasaidia vijana hawa niimani yangu kuwa watakuza uchumi kwa sababu watakuwawanafanya shughuli zilizo halali zinazowaingizia kipato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, nilikuwa naombanizungumzie suala la misamaha ya kodi. Ni vizuri Serikaliiangalie misamaha ya kodi isiyokuwa na maana, lazimatuache kuifuta, vinginevyo tunaliingiza Taifa letu katikamazingira ambayo hayazalishi vizuri. Ni vyema tukaangaliahasa kwenye Sekta ya Madini, kuna misamaha mingi ya kodiambayo hainufaishi Serikali au Taifa kwa ujumla. Ni vyema

120

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

[MHE. M. S. KAKOSO]

tukaweka mikakati itakayosaidia kukuza uchumi na kudaikipato kikubwa kwenye sekta ya Nishati hasa ya Madini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.

MWENYEKITI: Ahsante. Sasa namwita MheshimiwaMichael Laizer.

MHE. MICHAEL L. LAIZER: Mheshimiwa Mwenyekiti,nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi nichangie mpangohuu wa Serikali.

Mheshimiwa Spika, kila nchi ina mipango, nausipokuwa na mipango kwa kweli hakuna utakachowezakufanya. Lakini Mpango huu unastahili wananchi wenyewewauelewe, waufahamu kabisa kwa sababu Mpango huu niwa kwao. Kwa hiyo, ni lazima washirikishwe na ni lazima itatuematatizo yao na lazima waone faida ya mipango hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kila mwaka inavipaumbele. Mwaka uliopita tulikuwa na kipaumbele chabarabara kwamba ni lazima barabara zijengwe na kwelinaishukuru Serikali kwa sababu wamejenga barabara nyingisana. Kuna barabara zinazounganisha nchi na nchi, Mikoa,Wilaya mpaka nyingine zinaunganisha Tarafa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tuangalie kwa sababuwakati mwingine kuna miradi inafanyika chini ya kiwangona kupoteza fedha za wananchi.

Nikitoa mfano, barabara kutoka kwenda Arushakwenda Namanga, imejengwa kwa muda wa miaka minesasa. Lakini ukiangalia kabla hawajamaliza, eneo ambalowamemaliza imeanza kubomoka. Sasa barabara hiyoimeanza tena upya kukarabatiwa kama mwanzowalipokuwa wakijenga. Mwanzoni waliweka madarajamadogo, sasa wamevunja tena wanaweka madarajamakubwa kana kwamba hawakuangalia kwenye mipangoyao kwamba barabara hizo au madaraja hayo yanahitajikayawe makubwa.

121

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

[MHE. M. L. LAIZER]

Kwa hiyo, hiyo ni upotezaji wa fedha za wananchi.Kwa hiyo Serikali iangalie miradi kama hiyo kwa sababuhatutamaliza vipaumbele. Tuhakikishe kwamba vipaumbeletunavyochagua visiende mwaka mwingine, tumalizemapema kwa sababu kuna vipaumbele vingine ambavyotumeviacha bila kuzifanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambaloningependa kulizungumzia ambalo Serikali hawakuwekakwenye Mpango ni Kiwanda cha Magadi Soda, Lake Natron.Mheshimiwa Rais alipofungua Bunge hili alisema mwenyeweni lazima tujenge Kiwanda cha Lake Natron kwa sababumagadi hayo yanakaa bila kutumiwa, bila kuwafaidiawananchi.

Vile vile Mheshimiwa Rais alipotembelea Wilaya yaLongido, aliwaambia tena wananchi ni lazima katika kipindichake Kiwanda cha Lake Natron kitajengwa ili wananchivijana wapate ajira katika kiwanda hicho. Lakini sikuonakatika Mpango huu, Serikali hawakuweka kabisa kwenyeMpango, naomba waweke kwa sababu bado inawezekanasasa, na ndiyo maana tunachangia Mipango hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia majirani zetu,hawataki miradi kubwa kabisa iliyoko mpakani, kila mradiwanapiga vita. Wanapiga vita mradi wa magadi, wanapigavita barabara ya Mto wa Mbu, Engaruka, Loliondo naMugumu. (Makofi)

Ukiangalia barabara ya lami inayotoka Nairobiinaingia mpaka inafika Masai Mara. Haikuingia ndani yaMasai Mara lakini imefika Masai Mara, na sisi hatukusemakwamba tutajenga barabara ya lami ndani ya Serengeti.Jambo lingine ambalo wanapiga vita hata uwanja wa ndegewa Serengeti, na uwanja wa ndege wa Serengeti ni kilomita17 kutoka Serengeti (hifadhi). Eti wanasema nyumbuwatatupa mimba! Kitu cha ajabu, na sisi tunakubali! Sasawenzetu wanatuzidi, wao wanapanga mambo yaowenyewe, lakini sijawahi kusikia Serikali ya Tanzania ikiingiliamiradi ya Kenya. (Makofi)

122

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

[MHE. M. L. LAIZER]

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ninalopendakuzungumzia; ukiangalia kila Mkoa una mahitaji au una zaolake. Wilaya yetu ya Longido, Monduli, Ngorongoro na baadhiya Wilaya nyingine tunategemea mifugo. Lakini kwenyemipango hii haikuweka kabisa suala la mifugo. Sisitunategemea Kiwanda cha Kenya Meat Commission.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zaidi ya asilimia 40 ya mifugoinayochinjwa pale inatoka Tanzania, mbuzi ni asilimia 60.Lakini Serikali ya Tanzania, sisi hatuna hata mapatotunayopata kwa mifugo inayokwenda kwenye kiwanda kile.Kwanini tusijenge kiwanda chetu Arusha? Mifugo ya Tanzaniaisipokwenda kwenye hicho kiwanda, kinafungwa. Lakini sisitunakaa tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwa hili suala laviwanda vya nyama, vijengwe na kule kwetu Arusha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambaloningependa kulizungumzia ni matumizi mabaya ya fedha zaSerikali. Ukiangalia miradi ya maji, miradi inayoibuliwa ni fedhanyingi sana, kila mtu anashangaa, lakini Serikali haioni.Sijawahi kuona kwamba kisima kinachimbwa kwa Shilingimilioni 300, sijawahi kuona! Lakini kwenye utaratibu huu ipo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, naomba Serikali hiiitambue sasa kwamba mifugo inahitaji maeneo. Kwaninikuna maeneo ya wanyamapori na imetengwa kabisa?Kwanini kuna maeneo ya misitu na imetengwa kabisa?Kwanini kuna maeneo ya wawekezaji, nao wametengewamaeneo? Kwa nini kuna maeneo ya makaazi, lakini hakunahakuna maeneo ya mifugo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tunataka mgogorohuu uishe na wafugaji wawe na imani na Serikali, hebu sasatengeneni maeneo ya mifugo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.

123

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MICHANGO KWA MAANDISHI

MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Mwenyekiti, mojaya vipengele ambavyo katika Taifa hili vimekuwa kero kubwakwa wananchi ni maji. Hivyo, basi ningeiomba Serikalikuazimia mwaka wa fedha 2014/2015 kuwa Mwaka wa Majikwa Taifa zima kwa kuhakikisha zaidi ya asilimia 75% ya nchi,wananchi wanapata maji, kwa kuwa hili linawezekana katikaMpango wa Matokeo Makubwa Sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala kuruhusu maeneo yamipaka (borders) kufanya kazi saa 24 tofauti na sasa, litasaidiakuongeza mapato katika Taifa, kutanua wigo wa ajira na sokokwa Mataifa ya karibu, hivyo nchi kuwa katika biashara mudawote. Mfano wa mipaka hiyo ni Tunduma ambayo kwa mweziinaliingizia Taifa Shilingi bilioni mbili. Hivyo, kuruhusiwabarabara hiyo kufanya kazi saa 24 itaongeza mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. ZARINA S. MADABIDA: Mheshimiwa Mwenyekiti,ni suala zuri sana kujadili maendeleo ili kuweka mipango kablaya bajeti. Lakini ingekuwa ni bora sana kama mpangoungetoa utekelezaji wa mwaka 2013/2014 ili ijulikane wakatitunazungumza ya mwaka 2014/2015 tusirudieyaliyojitekelezwa mwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vipaumbele ni vingi. Kwaupande wangu ningeweka miundombinu, Kilimo na Viwandandiyo vipewe msisitizo na sekta nyingine zipewe fedha zakawaida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imefanya kazi kubwasana kujenga barabara, lakini kwa sababu barabarazinabeba mizigo mizito sana, ni hatari, zitaharibika harakakama tulivyoshuhudia kwa barabara nyingi. Nashauriyafuatayo:-

(1) Reli zote ziimarishwe kwa kujengwa upya;

124

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

(2) Tusisubiri mfadhili/mwekezaji ajenge, badalayake Serikali ijenge;

(3) Ijengwe reli ambayo itakidhi mahitaji ya sasana miaka 50 ijayo;

(4) Kwa kuwa nchi yetu itakuwa na umeme wakutosha, tujenge reli ya kutumia umemeambayo itaenda kasi, asubuhi Dar es Salaamjioni Mwanza au Kigoma au Arusha naMtwara;

(5) Serikali isitegemee fedha ya bajeti kujenga reli,bali ifanye mkakati mahsusi kutenga fedhaza kutosha; na

(6) Serikali kwa kutumia gesi yetu inakopesheka,tufanye mkakati huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kama inatakakutatua msongamano wa magari Dar es Salaam, ni lazimaitanue daraja la Salender na Gerezani; itanue maeneo yoteya makutano, kuboresha na kutia lami njia za ndani ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, flyovers zitasaidia, lakinituelezwe zinapita wapi. Flyover inayounganisha daraja laKigamboni linasemekana kwenda TAZARA, lakini watu wengikutoka Kigamboni wanaenda mjini na siyo TAZARA. Reli yaabiria ya Dar es Salaam inatumia injini za masafa marefu,tuwekeze kwa kuweka injini inayofaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tubadilishe mtazamo waKilimo, siyo kweli kwamba 75% ya Watanzania ni wakulima,bali ni waishio vijijini. Tuige Malysia ambao walibadilimsimamo wa nchi na kufanya 35% tu ndiyo wakulima, nahivyo kulima kwa tija na kuweza kuzalisha chakula nabiashara. Ili kutoa ajira nyingi hasa kwa vijana, viwanda vingivianzishwe. Viwanda hivyo, viwe vidogo, vya kati na vikubwa,viwepo kote, vijijini hadi mijini.

[MHE. Z. S. MADABIDA]

125

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini mpango wa hivyovipaumbele vitatu vitatoa maendeleo, ajira na kukuzauchumi wa nchi yetu.

MHE. SABREENA H. SUNGURA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nami napenda Mpango wa Serikali uzingatie yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango uoneshe ni jinsi ganiSekta ya Afya itakomboa akina mama kutokana na vifo vyamama na mtoto, Elimu ya Afya ya Uzazi na ni jinsi ganiitapunguza vifo hivyo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kitengo vya Damu Salamani vyema sasa katika mpango huu, Hospitali ya Tumbi ipewemamlaka ya kisera kutunza damu yake yenyewe bilakutegemea kwenda Dar es Salaam kwenye Ofisi ya DamuSalama kipindi cha emergence. Hivyo watu wengi hupotezamaisha kutokana na traffic jam kutokea Kibaha hadi Dar esSalaam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vyema mpango huu ujikitekatika special economic zone kwa sababu fursa zipo, lakinikinachokosekana ni wawekezaji kuja kuwekeza. TanzaniaInvestment Centre iweke mikakati ya kuleta wawekezaji,hivyo kukuza uchumi wa Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa, ni vyemaMpango huu uwekeze kwenye Sekta ya Maji, upatikanaji wamaji safi na salama na pia uwekaji wa mita kwa watumiaji iliwaweze kulipa gharama halali kutokana na matumizi ilikuondoa migogoro mbalimbali inayopatikana katikamaeneo ya Kigoma Manispaa na sehemu nyingine nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. YUSSUF HAJI KHAMIS: Mheshimiwa Mwenyekiti,nachukua nafasi hii adimu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwakuniwezesha kuwa miongoni mwa wachangiaji katika madahii muhimu.

[MHE. Z. S. MADABIDA]

126

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango wa Maendeleo waTaifa wa mwaka 2014/2015 ni muhimu sana kwa Taifa, kamamipango itakwenda sawasawa na usimamizi mzuri. Mimibinafsi ningependa Serikali ielekeze mipango yake katikauvuvi na hasa kwa wavuvi wadogo wadogo. Wavuvi wadogowawezeshwe kwa kupewa elimu, wapatiwe zana za kisasaili na wao waweze kuvua bahari kuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango huu wa uvuvi wabahari kuu ni muhimu kwa maendeleo na ajira kwa vijanawetu. Jambo muhimu ni mipango na usimamizi madhukuti.Sambamba na bahari, tunayo maziwa, mito na mabwawa.Vyote inapasa kusimamiwa na kuwawezesha vijana wetukatika uvuvi wa kisasa wenye tija na maslahi kwa Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile Mpango huuuelekezwe katika Kilimo kwa mazao ya chakula na biashara.Wakulima wadogo wawezeshwe kwa vifaa kama matrekta,mbolea, mbegu bora pamoja na tafiti mbalimbali zakitaalam. Vijana wetu waliopitia JKT wapewe kipaumbelekatika Mpango huu. Pamoja na mafunzo ya ulinzi ambayowanapatiwa, lakini hufunzwa shughuli mbalimbali kamaufugaji, kilimo na fani nyingi nyinginezo. Kwa kuwa siyo rahisikuwaajiri katika ulinzi wote, mimi nadhani ni wakati muafakakuwakusanya vijana katika sekta ambazo wamejifunza, naSerikali iwawezeshe katika nyanja zote. Hii itasaidia ajira kwavijana pamoja kuongeza uzalishaji na kukuza pato la Taifa.

Mheshimkiwa Mwenyekiti, mpango haujazungumziamaendeleo ya michezo ambayo ni muhimu kwa vijana naTaifa. Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizokuwa na hadhikubwa kwa kuwa na wanamichezo wenye viwango hasakatika riadha, mpira wa miguu, mchezo wa ngumi naadhalika. Lakini kwa sasa michezo mingi imepotea naimekosa msisimko hasa Kimataifa. Hivyo mpango huuungeangaliwa kwa upana kurejesha heshima ya Taifa letu.Kama tukijipanga vizuri, ukubwa wa nchi na wingi wa watutulionao ni rasilimali tosha kujikomboa katika michezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

[MHE. Y. H. KHAMIS]

127

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Mwenyekiti, mojakati ya changamoto inayotukabili kama Taifa na kupunguzamakusanyo/mapato ya Serikali ni misamaha ya kodi. Nimuhimu sana Serikali ikalichukulia kwa uzito wa pekee, kishakulitafutia ufumbuzi wa kudumu. Ni aibu, ukosefu wa umakinikwa nchi, kutoa msamaha wa kodi kwa mwaka kwa kiwangoambacho ni asilimia 27% ya makusanyo yake ya mwaka naasilimia 4.3% ya pato la Taifa. (Rejea CAG 2013).

Mheshimiwa Mwenyekiti, wachambuzi wa uchumi(kama ilivyoainishwa na Ripoti ya ESAUVP) (2013, Pref.Maliamkono et-al) inabainisha wazi kwamba misamaha yakodi ilikuwa muhimu kwa nia ya kuwavutia wawekezaji kipindiambacho nchi haikuwa na miundombinu ya kutosha,changamoto ambayo kwa sasa inapungua kwa kiwangokikubwa. Inakuwaje badala ya misamaha ya kodi kupunguakwa kadiri miundombinu inavyoboreka, misamaha husikainaongezeka? Katika hatua nyingine, nyongeza kwa mwakammoja yaweza kuongezeka kwa 78%. (Kwa mwaka wa fedha2010/2011 na 2011/2012, misamaha ya kodi iliongezeka tokatrilioni 1.016 mpaka trilioni 1.8 mwaka 2012).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nchi ambayoinashindwa kutekeleza mipango ya maendeleo na (Mpangowa Taifa) kutokana na kuwa na ufinyu wa bajeti – kusamehetakriban trilioni mbili, ni mzaha na ukosefu wa umakini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni muhimu Serikali ikaanzakushughulikia changamoto hii kwa kuhakikisha wanafanyamambo yafuatayo:-

(1) Kuweka ukomo wa misamaha ya kodi nakuhakikisha kuwa misamaha haitolewi zaidi ya kikomokilichowekwa. Lazima ukomo ujulikane ili kuiwezesha Serikalikubaini miradi ambayo inahitaji misamaha na ambayohaihitaji;

(2) Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali akaguemisamaha yote ya kodi iliyotolewa ili kupima kama kunamatumizi sahihi ya fedha za umma;

128

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

(3) Utaratibu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) wa kutoa misamaha ya kodi udhibitiwe/kusimamiwaipasavyo. TIC akiwa kama mwangalizi wa Makampuni hayayaliyopewa misamaha, anatakiwa kujiridhisha kwambamotisha husika haitumiwi vibaya. Uzoefu umeonyeshakwamba ufuatiliaji husika huwa haufanyiki;

(4) Mamlaka wanayopewa Mawaziri (MfanoWaziri wa Madini) wakati wa kusaini Mikataba ya Madini(MDA) inayotoa vivutio vya uwekezaji, inatakiwa iangaliwekwa jicho pana au kudhibitiwa;

(5) Serikali kusimamia utekelezaji wa sheriambalimbali zilizotungwa na Bunge. Sheria ya Kodi ya Mapato(ITA 2004) kifungu cha 10 (3) inahitaji kwamba mikataba yoteiliyosainiwa baada ya tarehe 1 Julai, 2004 kutopewamisamaha ya kodi. Licha ya kuwepo kwa kifungu hicho,Serikali imeendelea kusaini mikataba yenye kifungukinachoruhusu misamaha ya kodi;

(6) Sheria ya Kituo cha Uwekezaji (TIC) lazimaifanyiwe mabadiliko ili iweze kubainisha ukomo wa misamahaya kodi; na

(7) Serikali itunge sera/iandae mwongozo wakutoa misamaha, ambao unaelezea usimamizi na misamaha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya pili ni umuhimu waSerikali na Kamati ya Bajeti kufanyia kazi changamotozinazozikabili Halmashauri nyingi katika kukusanya mapato,wakati kiuhalisia zina uwezo wa kukusanya zaidi yakinachokusanywa.

Ni muhimu kuhakikisha Halmashauri zote zinatakiwakutambua vyanzo vyote vya mapato yao ya ndani (vyakisheria), kisha kuwe na database ambayo itakuwa updatedkila mara kwa kadiri mazingira yatakavyoruhusu. Hali hiiitasaidia utaratibu unaotumika sasa wa Halmashaurikukusanya mapato kwa kubahatisha/kwa mazoeapasipokuwa na takwimu sahihi za walipa kodi.

[MHE. H. J. MDEE]

129

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inawajibika pia kutoamwongozo/maelekezo kwa TRA kutoa taarifa sahihi zamapato ya mwaka ya Makampuni kwa Halmashauri ilikuziwezesha kupata service levy iliyo sahihi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo Serikaliinatakiwa kuliangalia kwa umakini kama sehemu ya chanzocha mapato ni ardhi kupitia Kodi ya Ardhi. Kifungu cha 33cha Sheria ya Ardhi Na. 4 cha mwaka 1999, kinatamkabayana kwamba mwenye hati miliki pamoja na masharti yavifungu vingine, anatakiwa kulipa kodi kama ilivyoelekezwana Sheria ya Fedha za Umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utafiti uliofanywa na Idaraya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, baada ya kupewakazi husika na Wizara ya ardhi kuweza kubaini kama tozombalimbali (land rent, fees, levies) za ardhi au malipomengine yanayotakiwa kutozwa kwa wamiliki wamashamba, wanafanya hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utafiti husika uligunduakwamba kati ya mashamba 763 (ekari 902,403)yaliyotembelewa, ni mashamba 278 (36.45) tu ndiyo yaliyolipakodi ya ardhi (2002) kama sheria inavyotaka. Wamiliki wamashamba 432 (56.6%) waliohojiwa walikiri kwambahawajalipa kodi husika. Lakini walipotakiwa kuonyeshauthibitisho (ushahidi wa risiti) kuonyesha kama ni kweliwalikuwa wamelipa kodi husika, ni mashamba 102 yaliyowezakuthibitisha. Hiyo imetuambia kwamba mashamba mengine643 yawezekana kabisa hayakulipiwa kodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hatua nyingine,iligundulika kwamba asilimia 43.47% ya wenye mashambawaliohojiwa walikiri kwamba hawajawahi kulipa kodi kabisa.Ikumbukwe kwamba hii ni sehemu ndogo tu ya mashambayaliyotembelewa. Kodi hizi zingelipwa ipasavyo, ingesaidiakuongeza mapato ya Serikali kwa kiwango kikubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka kufikia mwaka 2002,viwanja vyenye hati vilikuwa ni 995,000 tu. Sasa kama kigezo

[MHE. H. J. MDEE]

130

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

cha kutozwa kodi ni kuwa na hati miliki, na kwa kuwa viwanjavyenye hati miliki ni vichache sana; tafsiri yake ni kwambaSerikali inakosa mapato mengi sana kwa sababu tuhaijagundua umuhimu wa ardhi katika mipango yake.Lazima mtazamo huu mgando ubadilike. Ardhi na upimajiwa ardhi ina kila sababu ya kuchukuliwa kwa uzito wakipekee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukisimamia nidhamu yakutoza kodi kwa wamiliki wa mashamba, itafanya watu wawena nidhamu ya kutumia ardhi kwa uzalishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kodi za majengo, hilini eleo ambalo Serikali haijalifanyia kazi vya kutosha.Likisimamiwa ipasavyo, litakuwa na mchango mkubwa sanakatika pato la Serikali.

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kupata nafasi ya kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya kuelezea mpangompya wa maendeleo, swali la kujiuliza ni kwa kwamba, kwakiasi gani mpango wa mwaka 2012/2013 umetekelezwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la reli,barabara zetu kwa kiasi kikubwa zimetengenezwa kwa lami,lakini barabara hizi haziwezi kudumu kwa muda mrefu kwasababu bado malori yenye uzito mkubwa yanazitumiabarabara hizo kusafirisha mizigo badala ya kusafirisha kwamabehewa ya treni. Imekuwa ni hadithi sasa Treni ya TAZARA,Reli ya Kati na Kaskazini; ni lini Serikali itaamua kuchukuamaamuzi magumu na kubomoa reli zote na kuweka za kisasaza mwendo wa kasi, ukizingatia tayari umeme wa uhakikaSerikali imeshaanza kuishughulikia?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu deni la Taifa. KatikaMpango wa Taifa, Serikali inatueleza kuhusu ukuaji wa patola Taifa kwamba umekua kwa asilimia 7.0% ukilinganisha na6.9 mwaka 2012. Lakini hapo hapo deni la Taifa la ndani nanje limeondgezeka kwa Shilingi trilioni 24.49. Haiingii akilini

[MHE. H. J. MDEE]

131

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kwamba deni ni kubwa kuliko bajeti ya nchi, halafu wataalamwanatueleza uchumi unakua. Utakuaje? Ndiyo maanamaendeleo mengi hayafanyiki. Kumekuwa na matatizo yakuiba kila sekta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano, Kil imo chaUmwagiliaji. Kilimo hiki hakiwezi kukamilika bila kuchimbavizima vya maji vya kutosha kila mahali. Mradi wa maji vijijinibado ni tatizo, vijiji vingi havijafanikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee Jiji la Dar esSalaam. Jiji letu hili ndiyo kioo cha nchi yetu, lakini mpakasasa hivi wakazi wa Dar es Salaam hawana maji safi nasalama kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Mpaka leo hiibaadhi ya wakaazi wanachota maji ya chumvi na machafukutoka baharini. Hii ni hatari. Lazima tuwe na watu wenyeafya ili kuwa na nguvukazi imara. Kwa kutumia maji yasiyosalama, magonjwa ya milipuko ya kuhara, typhoid nakadhalika hutokea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu usafiri wa anga,niipongeze Serikali kwa kukarabati viwanja vingi vya kurukiana kutua ndege sehemu nyingi nchini. Je, Serikali sasa inamikakati gani ya kuhakikisha Shirika letu la ndege ATCLlinafufuka kama njia ya maendeleo na kuliongeza pato laTaifa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu utalii, ningependakujua, ni kwa jinsi gani mpango huu umejikita katikakuendeleza utalii endelevu wenye kujali mazingira ikiwa nipamoja na kuongeza na kupanua vivutio vya utalii? Naombamajibu.

MHE. SALOME D. MWAMBU: Mheshimiwa Mwenyekiti,katika mpango huu, maeneo mengi hayapewi kipaumbelekatika utekelezaji wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la maji bado ni tatizo.Ahadi ya visima 10 bado haijakamilika. Mpango huuunasuasua. Nashauri Serikali ijitahidi kuchimba visima vifupi

[MHE. L. F. OWENYA]

132

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ili wakati wa mvua viweze kusaidia kupunguza tatizo la majivijijini. Wilaya ya Mkalama, vijiji vingi havina visima;wanatumia maji yasiyo salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano Kata za Msingi,Miganga, Mwangeza, Mwanga, Iguguno, Ibaya, Ilunda naNduguti. Huu ni mfano tu wa baadhi ya Kata katika Jimbo laIramba Mashariki, Kata ambazo hazina maji. Naishauri Serikalikuwa, visima vifupi bado vinahitajika katika Jimbo langu.Hivyo, Serikali iziwezeshe Halmashauri kupata fedha zamaendeleo za kutosha ili ziweze kuchimba visima vifupi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali ioneumuhimu wa kuweka mawasiliano, mitandao ya simuisambazwe nchi nzima, kwani kasi ya kusambaza inasuasua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa elimu, Serikaliizidi kuongeza bajeti ya Wizara ya Elimu. Pia uchambuaji wamikopo izingatie watoto ambao hawana uwezo nawanaotoka katika mazingira magumu (maskini).

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali ipelekeumeme katika Wilaya zake mpya. Kasi iongezeke ili iwezekusukuma shughuli za maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MHE. MAHMOUD H. MGIMWA: MheshimiwaMwenyekiti, awali ya yote, naishukuru sana Serikali kwa kuletaMpango wa Maendeleo wa Mwaka 2014/2015. Kwanza,naanza kwa kuzungumzia bajeti ya mwaka 2013/2014.

Mheshimiwa Mwenyekiti, makusanyo ya robo mwaka85.7% mpaka sasa yanatokana na mapato ya ndani, naasilimia 32.4% yanatokana na mapato ya nje. Hii inatoataswira kuwa Serikali inashindwa kutekeleza majukumu yake.Mfano, Wizara ya Maji mpaka sasa imepatiwa Shilingi bilioni43, kati ya Shilingi bilioni 157.

[MHE. S. D. MWAMBU]

133

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2012/2013 Serikaliilipanga bajeti ya Shilingi trilioni 15, mwaka 2013/2014 Shilingitrilioni 18 na mwaka 2014/2015 Shilingi trilioni 20. Kila mwakakumekuwa na ongezeko la matumizi, lakini miaka yoteimeshindwa kufikia malengo yake na pia imeshindwakuainisha vyanzo vya mapato. Ni vyema safari hii Serikaliikaainisha vyanzo vya mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tume ya Mipango ni “thinktank ya Serikali”. Imefanya vizuri katika maeneo mengi, lakinisasa imekuwa kero kwa kuchelewesha baadhi ya miradiambayo tayari imeshapitishwa na Bunge kwa kisingizio chakuhakiki. Mfano, mradi wa Kurasini (Logistic Hub) nakusababisha fidia katika KMO kuwa kubwa kutoka bilioni 60hadi bilioni 94.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wakati muafaka sasa kwaSerikali kuangalia upya Sheria ya Manunuzi ambayo inaletagharama kubwa, mianya mingi ya rushwa na udanganyifumkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imefanya vizuri katikamaeneo ya miundombinu na hasa barabara, lakini badoSerikali inahitaji kuongeza nguvu katika eneo la reli ambaloni nyeti sana kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tutajielekeza zaidikatika reli, kutasaidia kupunguza gharama za usafiri, ambazoautomatically zitasaidia kupunguza gharama za uzalishajimali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukuaji wa pato la Taifa kwaasilimia 6.9% - 7.0% ni kweli katika nusu ya mwaka, lakini kunamaswali ya kujiuliza: Je, ukuaji wa pato la Taifa umekwendasambamba na kuondoa umaskini? Je, matabaka ya walionacho na masikini yameongezeka?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfumuko wa bei umeshuka,lakini ungeshuka zaidi kama umeme wa uhakikaungekuwepo na kwa bei nafuu.

[MHE. M. H. MGIMWA]

134

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile tungeimarisha zaidiusafiri wa reli kuliko wa barabara. Serikali isitishe uagizaji wamchele toka nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wakati muafaka sasa waSerikali kutueleza mikakati yake ya kulipa madeni yawazabuni wa ndani ambao wamepoteza mwelekeo sababuya Serikali. Ni mikakati gani Serikali imeweka kwa ajili yakudhibiti deni la ndani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado Serikali imeshindwakutekeleza kwa uhakika miradi ya maji na umeme vijijini. Nivyema sasa Serikali ikatatua tatizo la umeme, ambalolimesababisha hasara kwa viwanda vingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali bado haina dhamiraya kweli ya kuanzisha Benki ya Wakulima ambayo itakuwamkombozi kwa wakulima hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu viwanda, Serikaliimenyamaza kimya kuhusu EPZ – Bagamoyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. SILVESTRY F. KOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nianze na kupongeza Mpango wa Maendeleo ya Taifa.Niseme kuwa mipango ni mizuri, lakini uwezo na utekelezjiwake unaenda ukisuasua sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri kuwa ikibiditupunguze vipaumbele ili tuwe na vichache tutakavyowezakuvikamilisha kwa muda mfupi, tarajiwa na kukidhimategemeo ya wananchi vyema kuliko vingi ambavyovinasuasua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mojawapo ya vipaumbelekabisa katika Jimbo langu la Kibaha Mjini na nchi kwa ujumlani maji safi na salama. Katika mipango ya Serikali ni pamojana utekelezaji wa miradi ya maji katika vijiji/mitaa 10 na kazihii imeanza.

[MHE. M. H. MGIMWA]

135

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha kusikitisha ni jinsiambavyo walishajitahidi hata kuchangia asil imiawanazostahili na wakandarasi walishaanza kazi site. Lakinifedha hazipatikani za kutosha na kwa wakati, jambo ambalolinatishia hata Wakandarasi kuacha miradi na kuongezagharama za ujenzi wa miradi hii. Swali la kujiuliza, fedha zabajeti zilipangwa tena mapema kabisa, zimekwenda wapiau hazijakusanywa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi mkubwa wa maji RuvuJuu uliotajwa ukurasa 24, katika kitabu hiki cha Mapendekezoya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2014/2015,ni muhimu sana kutoa huduma hii ya maji safi na salama kwaMiji ya Kibaha. Lakini cha kusikitisha, ahadi hii ambayoilitakiwa ifanyiwe utekelezaji toka mwaka 2012, bado hadileo Novemba, 2013 hata dalili za kuchimba mtaro wa bombahazijawepo, na huku wananchi wakitaabika na kusikia ahaditunazowapa kutoka Serikalini. Tunaomba Serikali sasa itoekipaumbele katika mradi huu ili wananchi wapungukiwe nakutaabika na ahadi ya Serikali itimie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maendeleo yoyote yale namtaji wa kwanza kwa binadamu ni ardhi tuliyopewa naMwenyezi Mungu. Wananchi walio wengi wana maisha dunina rasilimali kuu waliyonayo ni ardhi, na Serikali ilishaanzishampango wa kuwasaidia wananchi kurasimisha na kufanyaardhi za wananchi ziwe na dhamani tambulika wawezekuitumia kujiletea maendeleo. Hii ni pamoja na Mkurabita.Mradi huu wa Mkurabita umeishia vitabuni na magazetini tu.Ukienda vijijini hata kwenye Kata, wananchi hawaelewimpango huu wa Serikali. Wito wangu, naomba sasa Serikaliitoe utaratibu maalum na kuelimisha wananchi kuhusuMkurabita ili wananchi walio wengi waweze kufaidika narasilimali hii muhimu katika kujiletea maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu sasa imeingiakatika miradi mikubwa ya utafiti na uchimbaji madini, utafitina uchimbaji wa mafuta na gesi; na tayari kupitia Makampunimakubwa ya shughuli hizo duniani, yameshagundua gesiMtwara, Lindi na Kilwa.

[MHE. S. F. KOKA]

136

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na jitihada zaSerikali kushirikisha Watanzania, bado hatujaweza kuwa nasera nzuri zaidi ya kuwezesha Watanzania na hasaMakampuni ya wazawa kuwa sehemu ya biashara hii kubwana yenye faida kubwa. Pamoja na kuhimiza Makampuni yaKitanzania kutoa huduma katika Makampuni haya, yaani“Supply of Goods and Services”, bado Makampuni ya Mafutana Gesi yanakuja na Wakandarasi wao. Tunaomba Serikaliiweke bayana sharti la kuwapa Makampuni ya Kitanzaniayenye uwezo na ushindani kipaumbele katika kutoa hudumambalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, badotunaishauri Serikali iweze kuweka utaratibu wa kuwashawishina kulazimisha Makampuni makubwa yatokayo nje kuwekezakwenye mafuta na gesi, yaweze angalau hata kutoa asilimiakidogo ya ubia na Makampuni ya ndani, hata 5% tu. Hiiitaweza kujenga uwezo mkubwa kwa Makampuni yaKitanzania na kuweza jamii kufikiwa haraka na kwa ukaribumaendeleo ya kiuchumi yatokanayo na miradi hii mikubwanchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MHE. CHRISTINA L. MUGHWAI: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru kupata fursa hii ili nami niweze kutoamaoni yangu katika Mpango wa Maendeleo ya Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu imekuwa ni hodarisana kuandaa mipango ya maendeleo ambayo matokeoya utekelezaji wake hayaonekani wazi. Tumekuwa namipango mingi, mfano MKUKUTA, MKURABITA, Mpango waMaendeleo wa Miaka Mitano, na sasa Big Results Now, nakadhalika. Hivi kweli kati ya hizi zote, ni mpango gani hasatunaoufuata? Je, upi ulifuta mwingine, na ni sababu zipizilizopelekea kuanzisha mpango au sera mpya bila kuelezasababu za kutokutekelezwa kwa sera nyingine?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa tupo katika mwakawa tatu wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka

[MHE. S. F. KOKA]

137

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mitano, lakini cha kushangaza katika taarifa yake, Serikalihaijaeleza ni kwa kiwango gani mpango huu umetekelezwahadi sasa? Kiasi gani cha fedha kimetumika, na miradi ganibado haijatekelezwa na itakamilika lini? Kiasi gani cha fedhakinatarajiwa kutumika na kitatoka wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuja na mpangoama sera ya Matokeo Makubwa Sasa. Hivi kweli matokeohaya makubwa yatakujaje iwapo fedha za maendeleozilizotolewa kwa robo ya mwaka huu ni asilimia 11 tu? Niwakati upi ambapo Serikali itajali mpango wake wamaendeleo kwa kuutengea fedha za kutosha za utekelezajikama mpango wenyewe unavyoelekeza?

Mheshimiwa Mwenyekiti, imefika wakati sasa Serikaliyetu iheshimike kwa kutenda na siyo kwa idadi ya mipangotuliyonayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. MESHACK J. OPULUKWA: MheshimiwaMwenyekiti, katika mpango ujao naomba Serikali iwekemkakati muhimu wa kumaliza tatizo la kulipa fidia kwawananchi wa kigamboni (New City).

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Serikali iweke mikakatiya kutosha kuweka mipaka maeneo yote yanayozungukahifadhi zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

MHE. RACHEL M. ROBERT: Mheshimiwa Mwenyekiti,mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifayanatakiwa kuainisha malengo mahsusi ya kila mwakakutokana na vipaumbele. Kuna tatizo la kuweka vipaumbelevisivyokuwa na specific targets, ambavyo mwisho wa sikumpango unakuwa mgumu kutekelezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna matatizo ambayoyanahusisha au yanachangiwa na vyombo vinavyotekeleza

[MHE. C. L. MUGHWAI]

138

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

mpango huu ambavyo havisimamiwi ipasavyo katikautekelezaji wake katika mpango wa kila mwaka. Kuna hajasasa ya Serikali kuhakikisha inasimamia kwa karibu sanavyombo hivi ili viweze kuleta tija.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vizuri sana mpango wamaendeleo ukalenga kujibu au kutatua tatizo kubwa laumasikini kwa kila Mtanzania, ukizingatia zaidi ya Watanzaniamilioni 40 hawana kazi zinazoeleweka. Kitendo cha mipangokama hii kuishia kwenye makaratasi kunaleta manung’unikomakubwa na hasa kama hayatatekelezwa kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfumuko wa bei hauendanikabisa na kipato cha Mtanzania. Vijana walio wengiwamekosa ajira na huku thamani ya Shilingi ikizidi kushuka.Tofauti ni kubwa sana kati ya aliyenacho na asiyenacho. Hiiinatokana na pengine pesa zinatumiwa vibaya na watuwachache bila kuchukuliwa hatua. Kwa mtaji huu sasa kilasiku tutakuwa tunapoteza muda kuandaa mipango kilamwaka isiyotekelezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi imekuwa mingi sanana kibaya zaidi mingi haijatekelezwa, na hata kamaimetekelezwa, basi ni kwa kiwango cha chini kabisa. Pesanyingi za umma zinapotea huku walengwa wakikosa hudumamuhimu kama afya, maji na miundombinu ya barabara nahata nishati ya umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na Serikalikuendelea kutekeleza miradi ya maji iliyoibuliwa katikaProgramu ya Matokeo Makubwa Sasa, bado kunachangamoto nyingi sana katika baadhi ya miradi. Kamamradi wa Lake Victoria ambao sasa unatoa huduma katikaMiji ya Shinyanga na Kahama, kuna malalamiko mengiambayo wasambazaji wanalazimika kutoza bili kubwa za majiili kukidhi gharama za uendeshaji.

Maheshimiwa Mwenyekiti, tatizo ni kwamba Serikalihaitoi ruzuku ili mradi kama huu usimuumize mtumiaji wamwisho, na hata kama inatoa ruzuku, basi haitoshi.

[MHE. R. M. ROBERT]

139

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Upatikanaji wa maji vijijini ni mdogo, kwani fedha nyingizinapotea katika kuchimba visima ambavyo havitoi maji. Je,Serikali haioni kuna haja ya kupima kwanza sehemuinayotakiwa kama kuna maji? Lakini pia kwa nini Halmashaurizisifanye kazi hiyo zenyewe bila kutoa kazi kwa Wakandarasiambao wamekuwa wakilipwa pesa nyingi na kuacha visimahavitoi maji?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango unaelezautaongeza upatikanaji wa matumizi ya pembejeo, zana zaKilimo na huduma za ugani. Lakini mpaka sasa bado kunatatizo kubwa la ucheleweshaji wa pembejeo kwa wakulima,na matokeo yake wakulima wanauziwa kwa bei kubwa sanana wafanyabiashara wanaoleta pembejeo zao kwa wakati.Serikali iangalie suala hili kwani wakulima wamekuwawakipata hasara sana kutokana na ucheleweshaji wapembejeo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huduma za ugani badozinalegalega, kwani Maafisa Ugani waliopo hawatoshi nahivyo kusababisha Kilimo kisicho na tija, na mazao yanakuwani hafifu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la afya bado nikitendawili. Pamoja na mipango mizuri, Serikali bado ina kazikubwa kuhakikisha miundombinu na upatikanaji wa hudumaza afya na ustawi wa jamii. Bado hospitali nyingi nchini hazinamadawa, vifaa na hata Madaktari wa kutosha. Kama vituhivi hakuna, hata iletwe mipango yenye asali, bado tutakuwahatujamaliza tatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushiriki wa sekta binafsikuwekeza kwa wingi katika huduma za afya nchini, bilakuzisaidia ni kuziongezea mzigo zisizouweza kuutua. Kunaumuhimu sasa kuhakikisha kama ni ruzuku, basi iende kwawakati katika Hospitali hizi binafsi na za Mashirika ya Dinikuweza kutoa huduma nzuri kwa jamii zinazoizunguka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

[MHE. R. M. ROBERT]

140

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ukurasawa 48 unaonyesha maendeleo ya kipaumbele katika mwaka2014/2015. Lakini mpango umejikita katika maeneomachache yanayoendana na program ya Big Results Now.Ningependa kujua ni vigezo gani vilitumika katika kuchanguahiyo miradi ya kipaumbele? Pamoja na hayo, ningependakuzungumzia mambo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imejitahidi sanakujenga kwa kiwango cha lami barabara nyingi sana nchinizikiwemo za Mkoa wetu wa Iringa, zikiwemo za Mtera – Iringa,Iringa - Mafinga; na mikoa mingi sana imefunguka kwa sasa.Lakini inasikitisha sana kuona bado Serikali haijatilia umuhimumkubwa sana katika uimarishaji wa Reli ya Kati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, najua kuwa hili lilishakuwaeneo la kipaumbele, lakini siku zote halitengewi pesa yakutosha. Najua uimarishaji wa Reli ungesaidia sana hata hizibarabara nyingi tulizozijenga kudumu na uchumi wa nchi hiiungekua kwa kasi zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kuhusu Utalii.Ukurasa ule wa 53, inasema: “Serikali ili kuboresha eneo lautalii nchini, itaendelea kujenga na kukarabati miundombinuya usafiri katika maeneo ya utalii.” Lakini haijaainisha nimaeneo yapi? Kwa mfano, Mkoa wetu wa Iringa una mbugaya Ruaha National Park ambayo ni ya pili kwa ukubwa Afrika,lakini barabara inayoelekea huko mpaka leo haipo kwakiwango cha lami. Kiwanja chetu cha Ndege cha Nduli badohakijapewa kipaumbele, hakijulikani lini kitakarabatiwa. Niimani yangu kama miundombinu hii ingepewa kipaumbelekatika mpango huu, ungeweza kusaidia sana kukuza ajirana pato la Mkoa wetu na Taifa kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, l ingine kuhusu ElimunaMafunzo ya Ufundi. Katika ukurasa wa 53, Serikaliinategemea kuimarisha mfumo wa kuongeza mbinu yakugharamia elimu nchini. Naipongeza Serikali kwa kuwezakutenga zaidid ya Shilingi bilioni 306 ambazo waliokidhi vigezovya kukopeshwa ni wanafunzi 29,754 kati ya wanafunzi 31,647

141

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ambao ni asilimia 96%. Lakini zipo changamoto ambazozinapelekea wanafunzi kushindwa kupata mikopo hiyo kwawakati, kisha kuleta vurugu, migomo na kisha maandamanovyuoni. Baadhi ya kezo hizo ni:-

(i) Maafisa kuchelesha taarifa za batch zamikopo za wanafunzi;

(ii) Mfumo mzima wa mtando wa (OLAS),mtandao upo chini sana (network); na

(iii) Wengi wao hawajui matumizi ya mfumo huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma Taarifa ya Bodi yaMikopo katika mitando ya tarehe 23 Oktoba, 3013,imebainisha changamoto hiyo kuwa zaidi ya wanafunzi 6,364taarifa zao hazikukamilika licha ya Bodi hiyo kutoa muda waziada wa wiki mbili, ni wanafunzi 3,151 tu ndio waliwezakukamilisha taarifa zao kwa usaili kwa asilimia 48% na wengineasilimia 52% hawakukamilisha taarifa, aidha kukosa taarifa,wakiwemo hata wanafunzi wa Mkoa wa Iringa. Kwa hiyo,tunaitaka Serikali iangalie upya hii Bodi ya Mikopo,ikiwezekana ifumuliwe na tunaweza kubani mengi zaidi yahayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Vyanzo vya Mapatoya Ndani; katika ukurasa wa 57 unaonesha jinsi Mpango huuutakavyoendelea kutumia vyanzo vipya vilivyopendekezwana Bunge na pia itabuni vyanzo vingine. Ningeomba wakatiWaziri atakapokuwa anajibu, basi atupatie ufafanuzikwamba hivyo vyanzo vipya ni vipi na vyanzo vilivyobuniwani vipi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. MARIAM R. KASEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nichukue nafasi hii kuchangia hoja yaMapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2014/2015 kama ulivyowasilishwa hapa Bungeni.

[MHE. R. E. KABATI]

142

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na mambo mengiya msingi yaliyopo katika mpango, yapo pia mambo muhimuambayo hayakutajwa katika mpango huu. Kwa kuwaMpango huu ndiyo dira ya bajeti ya mwaka 2014/2015,nimeona ni vyema nikaanza kuikumbusha Serikali kwambakatika Ilani la Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi, tuliahidikwanza ujenzi wa Reli kutoka Mtwara hadi Mchuchuma, kaziambazo hadi hivi sasa hazijaanza na katika Mpango huuhaimo: Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kuwaujenzi huu wa reli unaanza kabla ya mwaka 2015 ili kuendanana utekelezaji wa Ilani yetu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, reli hii ni kiungo muhimusana, kwani hali ya uchumi katika Mkoa wa Mtwara inakuakwa kasi sana kutokana na gesi iliyogundulika mkoani humo.Lakini hata hivyo, katika mapendekezo ya Mpangouliowekwa Mezani umeonesha kuwa kutakuwa namwendelezo wa upanuzi wa Bandari ya Mtwara na bandarihuru. Hivyo ni dhahiri kwamba Ujenzi wa Reli ni muhimu sanaili kuweza kusaidia usafirishaji wa mizigo ambayo itakuwainapitia katika Bandari hii. Hivyo ni msingi kabisa ujenzi wa relihii uingizwe katika mpango huu wa utekelezaji, uanze kablaya mwaka 2015 ili kutimiza ahadi ya Ilani ya Uchaguzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalonapenda kuikumbusha Serikali, pamoja na kwambaimeelezwa katika Mpango huu, ni ujenzi wa Hospitali ya Rufaaya Kanda ya Kusini ambayo inajengwa Mtwara, lakini kwakasi ndogo sana. Hospitali hii ni muhimu sana katika kandahii, kwani ongezeko la watu ni kubwa sana; na kwa kuwahali ya uchumi inakua, tunatarajia kwamba kutakuwa naviwanda ambavyo pia vitaongeza idadi ya watu. Hivyo,umuhimu wa uharaka wa ujenzi huu ni muhimu sana.

Naiomba Serikali kwamba mpango ambaoumepangwa na ujenzi wa jengo la mapokezi na Idara yaWagonjwa wa Nje, bado itakuwa ni hatua ndogo sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naiomba Serikalikuangalia namna ambavyo wanaweza kuweka kwenye

[MHE. M. R. KASEMBE]

143

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

mpango, ujenzi wa jengo la kulaza wagonjwa, kwaniikumbukwe kuwa hii ni Hospitali ya Rufaa, na wagonjwawanatoka mbali na wengine ni wagonjwa waliojiweza. Hivyo,haitawasaidia sana kama watakuwa wanatibiwa katika wodiya nje. Pia ikumbukwe kwamba Ujenzi wa Hospitali hii ni wamuda mrefu sana, lakini unakwenda kwa kusuasua sana.Hivyo, naomba mpango huu uelekeze nguvu zake katikaujenzi wa hospitali hii muhimu kwa wakazi wa Kanda ya Kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MHE. DEOGRATIAS A. NTUKAMAZINA: MheshimiwaMwenyekiti, nianze kwa kuunga mkono hoja, na kwakumpongeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano naUratibu) - Mheshimiwa Stephen Wasira na Tume yake yaMipango, kwa kazi nzuri ambayo wameianzisha ya kusimamiauchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema wakatinachangia kwa kusema kwamba tatizo kubwa ambaloSerikali haina budi ilishughulikie na ikiwezekana ilitatue, nikuleta uwiano mzuri kati ya mipango inayoandaliwa nautekelezaji wake. Tuondoe imbalance hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ni kwa Serikalikusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato kwa kuipatia TRAviwango (targets) vya juu. Pia kwa maoni yangu, Tume yaMipango ina wataalam wazuri, bado capacity ya Hazinakusimamia makusanyo ya mapato ni mdogo. Pia mindsetya Watendaji wa Hazina inatakiwa ibadilike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali iwezesheMKURABITA iweze kurasimisha mali na biashara za wanyongewaweze kulipa kodi. The informal sector which is a sleepinggiant should be tapped. Mimi nitaendelea kuwa YohanaMbatizaji, kwa kupiga kelele nyikani (voice in the wildness)kuhusu umuhimu wa Serikali kuwa serious na suala la kuinuahali ya wanyonge (wazawa) kwa kuwa na sera ya upendeleo(preferential treatment) kwa wazawa – kama ilivyo katikanchi za Malaysia, Zimbabwe na South Africa.

[MHE. M. R. KASEMBE]

144

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo siri kwamba uchumiwetu uko mikononi mwa Watanzania wenye asili ya asia,kama inavyokuwa Malaysia, uchumi wao ulikuwa mikononimwa Wachina. Lakini Waziri Mkuu – Mahadhir Mohamadkatika miaka ya 1980 alibadilisha hali hiyo kwa kuanzisha seraza upendeleo kwa wazawa, na sasa indiginous Malays wana-compete na Wachina katika biashara bila wasiwasi.

Mheshimiwa Spkika, kama Tume ya Mipangoitasimamia utekelezaji wa miradi ya vipaumbele, naishauriTume isaidie kujenga capacity ya Idara za Mipango katikaHalmashauri zote waweze kuwa na uelewa wa mipango naumuhimu wa utekelezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee kuhusu UtawalaBora. Viongozi wengi Serikalini hawako serious, hawawajibikiila wanafurahia vyeo kujinufaisha. Siyo kama zamani wakatiwetu. Kuna mmomonyoko wa maadili ya viongozi mkubwasana. Katika hali hii ya leadership crisis, kweli tutasimamiamiradi na kupata Big Results Now?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri kwambatukamilishe ujenzi wa Uongozi Institute ili viongozi wote wajuu wapigwe msasa kwa kupewa leadership skills na the ABCof Management. Lakini pia wapewe mazoezi ya kijeshi, kamatulivyokuwa tunafanya Kivukoni College zamani, ili kujenganidhamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema katikamchango wangu jana kuwa Serikali iwe serious katikakuwekeza katika Hospitali zetu za Rufaa kwa kujenga vituovya kushughulikia magonjwa makubwa kama Magonjwa yaMoyo, Figo na Saratani ili kuokoa fedha nyingi zinazotumikakuwapeleka wagonjwa nje ya nchi. Hii itakuwa ni pamojana kununua vifaa tiba vya kutosha. Pia kuwamotishaMadaktari Bingwa wasikimbie kutafuta kazi katika nchinyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mipango ya Maendeleoshould address matatizo sugu ya Maji na Umeme. Hivyo

[MHE. D. A. NTUKAMAZINA]

145

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ndivyo vichocheo halisi vya maendeleo ya uchumi. Tatizo lamaji ni kubwa sana, we should be very serious about it.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, mimi binafsi huwanawaogopa wawekezaji. They are very sophisticated in termsof technology and management systems. Wanawezawakatuibia kwa urahisi. The Government should regulate theprivate sector without stifling it. Private sector iwe mhimili,lakini Serikali iongoze uchumi. Nadharia ya “Invisible Hand”tuwe waangalifu nayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. DAVID Z. KAFULILA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nafasi ya Tanzania kwa Afrika na mwenendo wa biasharaduniani baina ya wakubwa wa dunia Ulaya, Marekani naChina, inapaswa kutengenezewa mkakati. Mpaka sasa USAna Ulaya inaitazama Tanzania na South Africa kama strategiccountries kwa uchumi wa Afrika. Hivyo, Serikali iwe na mkakatimpana katika eneo hili badala ya kubaki kuwa inashirikishwatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafasi ya BRELA katikauchumi wa soko ni muhimu sana kwa sababu wawekezajiwa ndani na nje wote wanategemea sana ufanisi wa BRELA.Bahati mbaya sana BRELA imeoza, haiendi na wakati naimekuwa kero na inasababisha usumbufu mkubwa kwenyebiashara hasa katika maeneo ya Trade Mark, licence nakadhalika. Nashauri ifumuliwe na kusukwa upya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, agenda ya maji ipewemsukumo katika utekelezaji. Maji ni kero namba moja kwamujibu wa utafiti wa Synovate 2009. Ziwa Tanganyika linaasilimia 17% ya fresh water duniani na bado Tanzania ni nchiya 11 kwa kuwa na mito mingi duniani. Lazima utolewemsukumo maalum kwa Mkoa wa Kigoma na nchi nzimahakuna maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania itumie nafasi yakeya mahusiano na China kukabili changamoto ya vijana wengi

[MHE. D. A. NTUKAMAZINA]

146

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kukosa ajira kwa sababu ya kukosa ujuzi. Nashauri tujengevyuo vya kutosha kama mpango maalum ili vichukue vijanawengi kwa kuwapatia ujuzi (skills) kupitia vyuo vya kativinavyotoa vyeti na diploma. Hii ni elimu muhimu sana katikakujenga Taifa la watu wanaojitegemea. China wamefanyavizuri katika eneo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nafasi ya Stock Market kwauchumi wa soko. Soko la Mitaji ni nguzo muhimu sana katikakuwafanya wananchi washiriki uchumi wao, uwazi wa kodina hivyo kuongeza mapato ya Serikali na kupunguza tatizola mlingano wa ushiriki wa wananchi katika uchumi wao.Mpaka sasa Domestic Market Capitalization ni asilimia 10%ya GDP wakati nchi kama Kenya, Domestic MarketCapitalization ni asilimia 40% ya GDP. Mpaka sasa tangutubinafsishe mashirika zaidi ya 300, lakini mashirika yaliyokuwalisted katika Stock Market ni 11 tu. Ni muhimu Serikali ihakikishekuanzia mashirika yote ambayo Serikali inamiliki kwa asilimiafulani, yawe listed katika Stock Market. TumezungumzaBungeni muda mrefu kuhusu mashirika hayo kuwa listed, lakiniWizara ya Fedha na Wizara zingine hakuna utekelezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Hifadhi ya Jamii.Moja ya changamoto kubwa inayokabili watu wengi nahususan wazee, ni tatizo la huduma ya hifadhi ya jamii.Naishauri Serikali isisitize fomula moja kwa Mifuko ya Hifadhikwa maslahi ya jamii. Mifuko hii iunganishwe, uwe Mfukommoja kwa urahisi wa usimamizi. Zaidi Serikali itenge fedhakuchangia wateja kutoka sekta isiyo rasmi kama njia yakuwahamasisha kujiunga na Mifuko ya Hifadhi. BadoTanzania ina asilimia ndogo sana (asilimia 6%), ya wananchiwake waliopo kwenye Mifuko. Rwanda, Serikali inachangiaasilimia 50% kwa wajasiriamali waliopo kwenye Mifuko. Sisituanze walau na asilimia 10%.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu hoja ya bima kwawananchi. Bima ni eneo muhimu sana kwa ustawi wa uchumina maisha ya watu. Mpaka sasa insurance penetration rationi asilimia 0.9%, ukilinganisha na nchi kama Kenya ambayoni asilimia 2.6%. Serikali lazima iwe na mpango wa kuhakikisha

[MHE. D. Z. KAFULILA]

147

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

sekta ya bima inakua na yenyewe Serikali iwe mstari wambele kuonyesha mfano. Mpaka sasa magari yote ya Serikalihayana bima. Nashauri magari yote ya Serikali yakatiwebima. Majengo yote ya Serikali hayana bima, nashaurimajengo yote ya Serikali yakatiwe bima. Huu utakuwa mfanomzuri na utaongeza uwezo wa NIC. Pia kwa kuwa kunamakampuni mengi ya kigeni nchini yanayokata bima kwamakampuni ya nchi zao, naishauri Serikali iweke utaratibukuhakikisha makampuni hayo ya bima ya nje lazimayashirikiana na makampuni ya ndani kuhakikisha Serikaliinatambua mapato ya makampuni hayo na hivyo kupatakodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utawala bora bado nichangamoto kubwa. Mawaziri wengi hawatimizi wajibu wao.Mipango ni mingi na mizuri. Utaona nchi zingine zinatekelezamipango tuliyobuni Tanzania, lakini bado nchi yetu tuliobunimipango hiyo tumeshindwa. Kuna umuhimu wa kupitia upyaSheria ya Utumishi wa Umma kwa sababu kuna vizuizi vingivinavyomlinda mtumishi, matokeo yake kuwa chanzo chauzembe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti,napenda kwanza kumpongeza mtoa hoja kwa mpangomzuri aliouwasilisha ambao umeainisha mambo kadhaayatakayotiliwa mkazo kwa mwaka 2014/2015 kwa ajili yamaendeleo ya Taifa letu. Binafsi nimevutiwa namapendekezo yaliyowasilishwa na niseme tu kuwa naungamkono hoja hususan katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu utalii. Katika maelezoyake, Serikali imesema kuwa inakusudia kujenga nakuboresha vivutio vya utalii nchini. Hili ni suala la msingi sana.Ingawa muda wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleowa mwaka 2013/2014, unaonyesha kuwa idadi ya wataliiwanaokuja nchini imeongezeka na kufikia 1,077,058 mwaka2012 bado idadi hii ni ndogo mno ukilinganisha na vivutiotulivyo navyo na pia uwezo tulio nao. Ni vyema mamlaka

[MHE. D. Z. KAFULILA]

148

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

zinazohusika zikaongeza idadi, juhudi, maarifa na ubunifukatika kutangaza vivutio hivyo tulivyo navyo ili wataliiwaongezeke. Kuongezeka kwa watalii ni kuongezeka kwapato la fedha za kigeni, kukua kwa ajira kwa wananchi wetuna kuongezeka kwa mapato ya kodi pamoja na faidanyingine nyingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati Tanzania tukijitapakwa watalii milioni moja kwa mwaka 2012, Malaysia ambakondio tumejifunza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BigResults Now), mwaka huohuo walipokea watalii milioni 24.6na kupata dola bilioni 1.8! Dubai, Falme za Kiarabu, nchindogo kabisa, walipata watalii milioni 9.3 na kuingiza dolabilioni 4.6 kwa mwaka 2011. Hata majirani zetu Kenyawametupita kwa idadi ya watalii. Tunahitaji kuongeza bidiikatika hili ili tunufaike ipasavyo na sekta ya utalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu rasilimali, nimesomapia katika mapendekezo haya ya Mpango wa Maendeleokwa mwaka 2014/2015 kwamba changamoto zilizojitokezakatika utekelezaji wa 2012/2013 ni pamoja na ufinyu warasil imali fedha, hususani upatikanaji wa mikopo yakugharamia miradi. Tatizo la ufinyu wa rasilimali fedhalinaweza kuongezeka kama hatutazingatia ushauri waKamati ya Bunge ya Bajeti kuhusu mapendekezo hayakwamba sasa Serikali irejee katika utaratibu ambao ilikuwaikiutumia katika kipindi cha kabla ya mwaka 1994/1995 waCapital Budget kwa kukopa kutoka Taasisi kadhaa za fedhaili kuendesha bajeti na mapato yanayopatikana yakalipiemadeni. Hii itasaidia kuondokana na tatizo la rasilimali fedhana pia kuwezesha miradi mbalimbali ya Serikali kutekelezwakwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuondokana na tatizola rasilimali fedha, nashauri pia Serikali iongeze vyanzo vipyavya mapato badala ya kuendelea na utaratibu uleule wakodi kwa wafanyabiashara na watumishi kama chanzo kikuu.Aidha, ni vyema pia Serikali ikaangalia namna ya kupunguzamatumizi yake ya kawaida ili fedha zitakazookolewa hapazitumike kwa matumizi ya maendeleo.

[MHE. C. V. MAGIGE]

149

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo naonaSerikali inapaswa ijipange upya katika mapendekezo hayani suala la ajira. Nimesoma kwa kuridhika namna wahitimutoka Vyuo vya Elimu ya Juu wanavyoongezeka. Hata hivyonimekuwa najiuliza kuwa iwapo kasi ya ongezeko hilo lawahitimu linaendana na nafasi za ajira zilizopo katika soko?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vyema Serikali ikawekamikakati madhubuti katika suala la ajira kwa kutoa fursa kwasekta binafsi kuajiri zaidi. Aidha, natoa wito pia kwa vijanawenzangu kwamba wazingatie uwezekano wa kujiajiri binafsina pia Serikali katika mapendekezo iweke mikakati yakuwasaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mikopo, nimeona piakatika mapendekezo haya, mpango na mikakati ya Serikalikwa maendeleo na ustawi wa wanawake. NaipongezaSerikali kwa kutoa fedha kuisaidia Benki ya WanawakeTanzania ambapo kwa mwaka 2012/2013, Serikali ilitoa shilingibilioni 1.1 na kuiwezesha Benki hiyo kufikisha mtaji wa shilingibilioni 8.2 na hatimaye Benki hiyo kufikisha utoaji wa mikopokwa wanawake wajasiriamali 10,607.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hatuahizo, nashawishika kuamini kwamba bado mapendekezohaya yanahitaji kuboreshwa kumsaidia mwanamke hususanwa vijijini. Nashawishika kuamini kwamba wanawake wengiwaliofaidika na mkopo ni wale walioko mijini. Hivyo basi,Serikali ijipange kuisaidia Benki ya Wanawake ili kuwezakuwafikia wanawake wa vijijini ambao ndio wengi na wenyeuhitaji zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. SUSAN L. A. KIWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,katika Kitabu cha Mpango, ukurasa 13, 2.2.1(ii), utekelezajiunaonyesha kufungua Ukanda wa SAGCOT kwa barabaraya Kidatu – Ifa – Lupilo – Malinyi – Londo – Lumecha/Songea,ni vizuri. Hata hivyo, pamoja na Serikali kuahidi kujengabarabara ya Ifakara – Mlimba kwa kiwango cha lami, pia

[MHE. C. V. MAGIGE]

150

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mlimba – Taweta – Madeke/Njombe ili kufungua barabaraya Kilombero - Njombe ambapo ndilo eneo linalozalishampunga na cocoa kwa wingi na ndiko kwenye mradi mkuwawa KPL. Sijaona mahali popote kwenye Mpango huuinapozungumzia kuhusu barabara hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu maji, Mpangoumezungumzia upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es Salaamkatika miradi mbalimbali ukiwemo na mradi tarajiwa waBwawa la Kidunda lililopo Morogoro Vijijini. Hata hivyo,Mpango hauzungumzii chochote kuhusu kupeleka maji yaBwawa la Kidunda katika Wilaya ya Morogoro na Manispaaya Morogoro ambapo kuna tatizo kubwa la maji. Hivyonaishauri Serikali iboreshe Mpango kwa kuingiza usambazajiwa maji Morogoro na Manispaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali iingizekwenye Mpango, Mradi wa Maji wa Mji wa Ifakara kwenyechanzo vya Kiburubufu ambapo andiko la gharama ya mradihuu limeshafikishwa ofisi ya Waziri na Naibu Waziri. Sababuza kusisitiza mradi huu ni kutokana na ongezeko la watu katikamji huo, takriban 150,000; pia kuna Chuo Kikuu cha MadaktariWauguzi, Tawi la Chuo cha SAUTI na vyuo vingine vidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango umezungumziamiradi mingi ya umwagiliaji, ambayo itatekelezwa katikaWilaya za Kilombero na Ulanga. Pamoja na nia njema hiyo,Mpango hauzungumzii ujenzi wa maghala katika Wilaya hizo.Pia hauzungumzii upatikanaji wa soko la mpunga, ambapohivi sasa wakulima wa Wilaya hizo wamekumbwa na umaskinikwa kubaki na mpunga, hali ya soko na bei ya mcheleimeporomoka; ambapo imesababishwa na Serikali kuletamchele toka nje, pia kufunga mipaka kwa mchele kutouzwanje. Wakulima wa mpunga wako kwenye hali mbaya,wameshindwa kulipa mikopo, kufanya maendeleo ya watotowa shule na makazi na kadhalika. Wananchi wa Kilomberona Ulanga wanasubiri Kauli ya Serikali hapa Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa mpunga –Ngalimia, Morogoro wa hekta 31,500; umeathiri wananchi wa

[MHE. S. L. A. KIWANGA]

151

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Kata ya Mlimba, Wilaya ya Kilombero, Kijiji cha Miembeni.Mradi na mipaka inaonyesha karibuni eneo la kij i j ilinalotumiwa kwa kilimo, linaingia kwenye mradi huo. Hiiitaleta athari kubwa kwa wananchi wa Mlimba na Miembeni.Hivyo, naishauri Serikali ikarekebishe mipaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri Mpango uone hajaya kuishauri TRA kukopesha mashine za risiti. Nashaurikwamba kwa kupitia mashine hizo, wananchi wapewemotisha ambapo mwananchi atakayedai risiti kwa kilaanachonunua na baada ya muda maalum na kiwangomaalum kitakachopendekezwa; mtumiaji huyo atarudishiwaasilimia fulani ya pesa. Hiyo itazidisha ari ya kudai risiti kwamanunuzi na Serikali kupata mapato ya kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali iachane na kodisumbufu kama za kulipia laini za simu kwani watumiajiwengine hawana hata simu, bali laini tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. DKT. ANTONY G. MBASSA: MheshimiwaMwenyekiti, napenda kuchukua fursa hii kuchangiamachache katika Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleowa Taifa 2014/2015.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna Taifa lolotelitakaloweza kukuza uchumi wake, kuleta hali bora ya maishakwa watu wake; kama hakuna mpango makini wamaendeleo uliowekwa na kuridhiwa na wananchi wake. Ilikuweza kufanikisha Mpango mzima wa Maendeleo,yafuatayo ni muhimu sana kuzingatiwa:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, kuwa na miradimichache inayotekelezwa badala ya kuwa na miradiambayo haiwezi kutekelezwa. Hakika tumekuwa na miradimingi sana ambayo haina ufanisi mzuri. Hii inatokana na kuwana vyanzo vichache vya mapato na muda mwinginekutotolewa kwa fedha za miradi husika kwa wakati. Maranyingi miradi hii hutekelezwa kwa ubora usiofaa, aidha kwa

[MHE. S. L. A. KIWANGA]

152

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

sababu ya muda wa utekelezaji kwisha au sababu yauchache wa fedha. Napendekeza kuwepo na miradimichache ya kipaumbele na itekelezwe kwa ufanisi mkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, ni kupunguza matumizimakubwa ya Serikali. Suala hili limekuwa likijadiliwa aukuongelewa mara kwa mara lakini bila ya utekelezajiwowote. Suala hilo linajitokeza katika zabuni mbalimbalizinazotangazwa na Serikali kupitia Bodi za Manunuzi.Manunuzi haya hugharimu fedha nyingi sana na kuna tofautikubwa sana baina ya bei inayotangazwa na bei halisi yabidhaa kwa wanunuzi wa kawaida. Aidha, nashauri kupitiaBodi za Zabuni na Manunuzi kuwa makini katika kutoa zabunihizo. Bodi zizingatie hali halisi ya bei iliyopo sokoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu, Serikali kutotoa fedhakwa wakati. Imekuwa hali ya kawaida kwamba fedha nyingiza miradi kuletwa au kutolewa zikiwa zimechelewa sana.Taratibu za pesa pale zinapofika zimechelewa, taratibu zamatumizi zisipokamilika, italazimu pesa hizo zirudishwe Hazina.Mbali na hayo, itabidi zifanyike semina na warsha mbalimbaliambazo nyingine hazina manufaa au tija kwa Taifa hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuondoa kero hii, nashauripesa ziwe zinatolewa kwa wakati muafaka na kufanya kaziiliyokusudiwa. Kuwepo na utaratibu wa kumalizia miradiiliyopitishwa kabla ya kuanzisha au kupendekeza miradimipya. Hii itaondoa utitiri wa miradi ambayo haifanikiwi aukutekelezwa kwa manufaa ya wananchi ambao ndiowalengwa hasa au ndio waibuaji wa miradi hiyo kulinganana fursa, vikwazo na mazingira yaliyopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni matumaini yangu kuwahoja hizi zikizingatiwa, zitaboresha hali ya Mpango huu waMaendeleo wa Taifa wa 2014/2015. Katika hilo, hakikautekelezaji wa mipango ya kipaumbele utazingatiwa nakupunguza utekelezaji wa miradi mingi inayofanyika chini yakiwango na usimamizi duni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

[MHE. DKT. A. G. MBASSA]

153

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. MUSTAPHA B. AKUNAAY: MheshimiwaMwenyekiti, Mpango wa Maendeleo wenye vipaumbele sitakwa gharama ya shilingi trilioni 20 unawezekana kamayafuatayo yatatendeka:-

(1) Fedha zikipangwa, zikapatikana kwa mudawake;

(2) Wako wataalam mahiri wa kuongozautekelezaji wake; na

(3) Serikali na Maofisa wake Wakuu – Mawaziri,Makatibu Wakuu, Wakurugenzi wa Idara mbalimbali, Wakuuwa Mikoa na Wakuu wengine watajali muda; yaani kuwahikazini na kutoa uamuzi katika muda unaostahili. Kusiwe nauendeshaji wa Kamati – yaani hakuna uamuzi mpaka kikao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, Watanzania lazimawawe na tabia (culture) ya kazi. Watu waache uvivu wakucheza pool, bao na kuliwa. Napendekeza kwamba pombeya aina ya viroba ikatazwe na vijijini kuwe na masaa maalumya kufungua baa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, Mpango huu iliufaulu ni lazima uwe na “monitoring” ama “evaluationmechanism”. Ikibidi kama hali imebadilika, kuwa na midtermreview kukwepa miradi inayokwama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. LEDIANA M. MNG’ONG’O: MheshimiwaMwenyekiti, naanza kwa kuunga mkono hoja hii ambayoimeletwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano naUratibu).

Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza kwa kuchangia hojakwa kukubaliana na Mpango wa Serikali wa MatokeoMakubwa Sasa (Big Results Now). Matokeo Makubwa Sasayanajikita katika maeneo mbalimbali yakiwemo barabara,madaraja na vivuko. Hata hivyo, naomba Waziri anipe

154

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

majibu kwa nini barabara ya Musoma – Mugango hadiBusekela (Majita Road) haipo kwenye Mpango wa Serikali?Barabara hii ni kiungo kwa Wilaya mbili, Wilaya ya Bundakwenda Kwimba na Wilaya ya Ukerewe kwenda Visiwa vyaIrugwe).

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii imo kwenyeahadi za Mheshimiwa Rais Kikwete wakati wa kampeni napia Rais wa Awamu ya Tatu. Barabara hii ndiyoinayotegemewa kiuchumi na wananchi wa Wilaya yaButiama, Tarafa ya Nyanje na wananchi wanaotoka Ukerewekwenda Visiwa nilivyovitaja. Barabara hii ikijengwa kwakiwango cha lami, itafungua uchumi wa Wilaya ya Butiama.Ni lini ahadi hii itatekelezwa kwa kujenga barabara hii? Bajetiijayo lazima Serikali ihakikishe barabara hii inajengwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta ya utalii ni muhimu,hivyo barabara ya Iringa – Ruaha National Park ikamilike kwakujengwa kwa kiwango cha lami. Pia barabara iendayoKitulo National Park kutoka Mufindi hadi Kitulo nayo ijengwekwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mikopo kwa wanawake nimuhimu ili kupata mitaji. Banki ya Wanawake iwafikiewanawake Mikoani badala ya kuwa kwenye Kanda chachepeke yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. BETTY E. MACHANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti,kuna haja kubwa mpango wa 2014/2015 ulenge elimu.Hakuna Taifa limeendelea duniani bila wananchi wake kuwana elimu ya kutosha. Tunaishukuru Serikali na wananchikuchangia ujenzi wa shule za kata, ambazo zitakuwamkombozi wa Watanzania kama tutaendelea kuwekezakatika shule hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ripoti ya World Bankya 2004 iliainisha nafasi za kazi Tanzania zilivyochukuliwa nawageni kwa sababu ya elimu yetu kutokuweza kukidhi

[MHE. L. M. MNG’ONG’O]

155

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

mahitaji (demands) za soko la ajira. Mwaka 2006 tulijengashule kila kata. Leo ni miaka saba na kiwango cha umaskinihakipungui kwa sababu elimu inayotolewa haina ubora wakutosha (quality education).

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafiti zinaonyesha kwambawanafunzi ambao wanaingia Vyuo vya Ualimu wanaingiana ‘grades’ ndogo na hivyo kuwa na uwezo mdogo katikayale masomo waliyosomea kufundisha. Wale wanaoajiriwana idara nyingine zisizo elimu, tafiti zinaonyesha kuwawanakuwa hawana stadi za kazi zinazoridhisha waajiri; hivyoajira nyingi kuchukuliwa na wageni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kujenga Taifa la watuambao wameelimika, ambao wanaweza kutatua nakusimamia changamoto za maendeleo zinazolikabili Taifa hili;tuwekeze heavily kwenye elimu kwanza. It is high time Serikaliichoshwe na lawama za wananchi kuhusu elimu, ifanye kazimajengo machakavu ya shule, upungufu wa madawati,ukosefu wa maabara, ukosefu wa vitabu, vyumba vyaWalimu, Walimu wa Sayansi na maslahi ya Walimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la pili ni kuongeza tijakwenye kilimo, hasa katika mazao yenye thamani kubwa.Zao la kahawa linaleta pato kubwa la Taifa. NingetarajiaSerikali i je na mpango kabambe wa kuboresha nakuendeleza zao la kahawa.

Wakulima wa kahawa wanalalamikia bei kubwa yadawa ya kahawa, ambayo kimantiki dawa hizi zilipaswa ziwena ruzuku ili wakulima wapate motisha zaidi ya kulitunza zaola kahawa. Badala yake ruzuku imewekwa tu kwenye micheya kahawa, ambayo hata hivyo wakulima wanaoipata niwachache. Iko haja Serikali ijue Big Results Now ni pamojana bumper harvest ya kahawa kutoka Kilimanjaro, Kigoma,Mbeya, Kagera, Mbinga na kwingineko na siyo kwa Mkoammoja tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, liko pendekezo la kuhimilichangamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi.

[MHE. B. E. MACHANGU]

156

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Tumeshuhudia ukame takriban miaka mitatu (3) kwa Ukandawa Kaskazini (Manyara, Arusha na Kilimanjaro). Tumeshuhudiapia maporomoko ya udongo Wilayani Same na Mwanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tafiti zilizofanyika Kimataifaza Sera za Chakula zilionya katika mkutano wake Berlin 2013kuwa sera sahihi za kuzuia na kukabiliana na mabadiliko yatabia nchi, nchi za Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara,zitaathirika sana na kuongezeka kwa ukosefu wa ajira,kuongezeka kwa utapiamlo, upungufu wa mazao hasaifikapo 2050. Tayari tafiti za mama na mtoto za 2010zinaonyesha kwamba watoto wa Tanzania wameathirika nautapiamlo kwa asilimia 42%.

Mheshimiwa Mwenyekiti, iko haja ya Serikali kuidhibitihali hii kwa kuweka fedha katika utafiti, miundombinu vijijini,umwagiliaji, usimamizi wa uvunaji wa maji ya mvua nausambazaji maji. Pia fedha ziwekwe katika mpangokabambe wa kupanda miti na kulinda misitu yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutumia fursa ya ongezekola watu nchini kuleta manufaa ya uchumi (demographicdividend) kwa kupunguza kiwango cha utegemezi/wafanyakazi. Kiwango cha uzazi (fertility rate) ya mama waKitanzania anayeweza kuzaa ni watoto 6 – 7. Taarifa za afyazinaonyesha kuwa wanawake 390 hufa kila mwaka, wakatiwa kujifungua.

Sambamba na hilo, kiko kilio kikubwa cha uhaba waMadaktari, uhaba wa Wauguzi, ukosefu wa magari yakubebea wagonjwa pamoja na vifaa vingine kama X-rays,Ultra Sound katika Zahanati na Vituo vya Afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkutano wa Kimataifa waMaendeleo wa Idadi ya Watu (ICPD) uliofanyika Cairo (Misri)1994 na mwingine uliofanyika Istambul mwaka 2012; ulikuwana agenda zilizotaka nchi zote duniani kutekeleza maazimioambayo ni pamoja na kupunguza na kuondoa vifo vyawatoto, vifo vya mama wajawazito na kupunguza kiwangocha uzazi kwa kila mwanamke anayeweza kuzaa. Utekelezaji

[MHE. B. E. MACHANGU]

157

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

wa maazimio haya hapa Tanzania, hasa katika eneo lamaendeleo ya idadi ya watu, ni chini ya asilimia 20% kwakipindi cha miaka 20.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kweli Serikali inampango wa kutumia idadi ya watu kupata demographicdividend, iko haja mambo tajwa pamoja na elimu, genderequality, ajira kwa vijana, reproductive health, populationstructure, migration na kadhalika ifanyiwe kazi. Serikali itengekitengo kinachojitegemea katika Tume ya Mipango, kifanyiekazi maudhui ya maendeleo ya idadi ya watu (populationdevelopment). Nchi nyingi zimeanzisha commissions zapopulation na zimefanikiwa katika hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu nishati, Serikaliiharakishe mchakato wananchi wapikie gesi. Gesi iingizwekwenye nyumba kama umeme. Hii itasaidia sana wananchikutokukata miti kwa ajili ya mkaa endapo bei ya gesi itakuwandogo ili mtu wa kipato cha chini aweze kununua. Mpangohuu utaokoa misitu, utatunza mazingira, mapato zaidiyatapatikana katika sekta ya utalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu viwanda, Serikaliifufue/itwae hati za viwanda vilivyobinafsishwa ambavyovimefanywa maghala. Kama products ambazo zilikuwazitengenezwe na viwanda hivyo zimepitwa na wakati (mfanoKiwanda cha Magunia, Moshi); basi mpango wa PPPuharakishwe kutungiwa Kanuni, tenda zitangazwe, sektabinafsi wakishirikiana na Serikali (Halmashauri/Wizara),waanzishe viwanda katika maeneo yenye fursa katika Wilayambalimbali nchini mfano maeneo ya Mikoa ya Big Six.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna sababu ya mahindikusafirishwa kupeleka Burundi, Congo, Malawi na kadhalikabadala yake viwanda vianzishwe ili viongeze thamani, wauzeunga Congo, Malawi na kadhalika. Yapo maeneo yenyemifungo mingi, asali, matunda na kadhalika na yenyeweyaangaliwe kwenye suala zima la viwanda

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

[MHE. B. E. MACHANGU]

158

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. DKT. PINDI H. CHANA: Mheshimiwa Mwenyekiti,hali ya uchumi. Ukuaji wa pato la taifa kwa asilimia 7% mwaka2013, maeneo ya ukuaji ni pamoja na usafiri na mawasiliano(asilimia 18.4%). Hivyo, ni muhimu kuongeza usafiri – yaanibarabara, viwanja vya ndege na mawasiliano, hususanikatika maeneo ambayo hayana usafiri fasaha, hayana lami.Mfano barabara ya Njombe – Ludewa – Itoni na barabaraya Njombe – Ludewa – Lupingu. Pia mawasiliano huongezauchumi na mzunguko wa fedha. Kuna maeneo mengihayana mawasiliano ya simu. Mfano Mikumi, Ruaha, Mbuyuni(Kitonga), Ludewa, Lugurawa, Manda, Lupingu hakunamawasiliano ya simu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni muhimu maeneo mengiya nchi yetu yakawa accessible-communicated. Barabarazikiwa mbaya, unatumia muda mrefu sana kusafiri naunachelewa kuzalisha. Usafiri ni muhimu, hivyo lazimagharama za usafiri ziwe za chini ili usafiri uwe ni huduma(service).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna nauli za vij i j ini,wananchi wanatozwa bei kali sana. Sasa SUMATRA wapoDar es Salaam tu. Je, nauli za ndege ni taasisi gani ina-control? Mfano nauli ya ndege kutoka Dar es Salaam –Njombe – Dar es Salaam – Rukwa unaambiwa US$ 500. Hii nibei ya return ticket ya Dar es Salaam – Dubai (Economy Class)au Dar es Salaam– Nairobi. Usafiri unaongeza kipato kwaasilimia 18.4%. Iweje Tanzania hatuna Shirika la Ndege, kutwatunawachangia KQ/SA/Emirates, siyo sawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfumuko wa beiumepungua kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wachakula. Sisi wananchi wa Mkoa wa Njombe(Wanging’ombe, Njombe, Ludewa) ni miongoni kwa watutunaozalisha chakula kwa wingi. Hata hivyo, kutokana nabarabara, wanaonunua zaidi chakula ni FDR Serikali.

Naomba kuuliza, kwa nini tunawakopa wakulimamahindi? Maana wao wakipeleka watoto shule inabidi adazilipwe immediately. Pia ushuru wa mazao unacheleweshwa

159

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

sana kulipwa Halmashauri ya Ludewa. Sasa kwa niaba yaakina mama, wanaomba fedha za mahindi zilipwe maramoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mwenendo waviwango vya riba, kwa mujibu wa Taarifa ya Bunge,mwenendo wa viwango vya riba za benki bado ni kubwa.Interest ya Fixed Deposit ni ndogo na interest ya loan nikubwa. Sasa hivi tuna changamoto ya ajira katika nchi yetu.Kwa nini hizi benki zisikopeshe vijana? Mradi endelevu nazile fedha za mabilioni ya JK, NMB nilitarajia ziwe revolvingfund hata leo watu wakakope, hususan vijana. Naombaufafanuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, akiba ya fedha za kigeniukilinganisha na Deni la Taifa na misamaha ya kodi. MpakaJulai, 2013 akiba ya fedha za kigeni ni US$ milioni 4353.4 wakatimpaka Juni, 2013 Deni la Taifa ilikuwa ni bilioni 15.29. Je, Seraya Misamaha ya kodi inasemaje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, usafiri ni pamoja namadaraja. Daraja la Mto Ruhuhu, Daraja la Kivukoni –Kigamboni (Dar es Salaam), ni maeneo muhimu ambayoSerikali lazima iwe makini kutekeleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, reli ya kikanda, Serikali inampango gani kujenga reli kutoka Ludewa – Mchuchuma/Liganga hadi Makambako?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukurasa wa 20, mradi wamakaa ya mawe Mchuchuma – Njombe. Mradi huuutakapokamilika unatarajiwa kuzalisha megawati 600.Napenda kujua ni l ini unatarajiwa kuzalisha umememegawati 600?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

[MHE. DKT. P. H. CHANA]

160

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. GOODLUCK J. OLE-MEDEYE: MheshimiwaMwenyekiti, naunga mkono hoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa ahadi za Rais.Kuanzia bajeti na Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2011/2012 hadi 2013/2014, nimekuwa nikiomba kuwa ahadi zaMheshimiwa Rais alizotoa kwenye Jimbo langu wakati wakampeni za Uchaguzi Mkuu 2010 na pia kwenye ziara yakebaada ya uchaguzi; ziwekwe kwenye Mpango waMaendeleo na kutengewa fedha kwa ajili ya kutekelezaahadi za Rais kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ni miradi ya maji safi.Tarehe 17/9/2010, Mheshimiwa Rais akihutubia mkutano wahadhara kwenye Uwanja wa Emaoi, aliahidi kuwa Serikaliitaandaa mpango kamambe (master plan) wa maji kwaHalmashauri yote ya Wilaya ya Arusha na kutenga fedha kwaajili ya utekelezaji ili ifikapo 2015, kero ya maji kwenye Wizarahiyo iwe ndoto.

Naomba kuwa chini ya BRN, Mpango wa Maji waHalmashauri ya Wilaya ya Arusha utengewe fedha za kutoshaili kuondoa kero ya maji ambayo inaelekea kugharimu, siyonafasi za uongozi tulizo nazo tu, bali shinikizo la damu linawezakutupata na hivyo kutugharimu uhai.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, barabara. Tarehe 17/9/2010, Mheshimiwa Rais aliahidi kuwa:-

(i) Atajenga barabara ya lami toka njia pandaya barabara kuu iendayo Nairobi na Ngaramtoni hadi SelianiDDH, Emaoi/Sambasha.

(ii) Barabara zote za Wilaya hiyo zitatengenezwakwa kiwango cha changarawe ili zipitike mwaka mzima.

(iii) Tarehe 1/11/2012, Mheshimiwa Raisalipozindua Hospitali ya Wilaya ya Olturumet, aliahidi kuwaSerikali itajenga barabara ya lami toka Radio Habari Maalumhadi Hospitali ya Olturumet.

161

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kulinda heshima yaMheshimiwa Rais wetu, naomba barabara hizo ziwekwekwenye Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2014/2015. Zitengwe fedha kwenye bajeti ya 2014/2015 ili ahadihizo zitekelezwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu, ujenzi wa reli. Ilikuboresha miundombinu ya uchukuzi kwa ushoroba wa kati(central corridor) hadi kufikia nchi jirani za Burundi, Rwandana Congo; nashauri reli ya kati ijengwe upya kwa gaugempya. Reli hiyo itakapokamilika, itaongeza uwezo wakusafirisha mizigo ya wawekezaji na nchi jirani na hivyokuongeza tija katika uchumi wa Taifa letu. Aidha, kukamilikakwa reli hiyo kutapunguza uharibifu wa barabara kutokanana wingi na ukubwa wa mizigo inayobebwa kwa malori.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. VITA R. M. KAWAWA: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba nimpongeze Mheshimiwa Waziri Stephen Wasirapamoja na Tume ya Mipango, kwa kuandaa Mapendekezoya Mpango wa Maendeleo 2014/2015 na Mheshimiwa Wazirikuwasilisha vizuri sana kwa muhtasari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeelezwa kuwa juhudinzuri zilizofanyika, zimesababisha kupungua kwa mfumuko wabei na hii imetokana a ongezeko la mazao ya chakula(mahibndi, mpunga na mtama). Hii imejidhihirisha baada yamavunzo ya mazao ya chakula hapa nchini. Ushauri wangukwa Serikali, lisitumike suala la kupunguza mfumuko wa beikwa kuagiza mazao hayo nje, ambapo inawaumizawakulima, wanababaika na soko. Tutumie utaratibu huu kwakununua na kuingiza sokoni chakula kinacholimwa nchini kwawingi, lakini pia tusiwakope wakulima mazao yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunasema katika mipangoyetu na hata katika mapendekezo ya Mpango huu, kuwatunahitaji msukumo mkubwa katika kukuza sekta hii ya kilimo.Sekta hii ndiyo yenye kuajiri watu wengi, ndiyo Serikaliinawekeza fedha nyingi katika pembejeo na mitandao ya

[MHE. G. J. OLE-MEDEYE]

162

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

umwagiliaji na sehemu za kuhifadhia mazao yanayonunuliwana Serikali. Hata hivyo, inapofika suala la soko la mazao yamkulima ili kukuza pato la mkulima na Serikali za Mitaa, SerikaliKuu:-

(i) Inanunua kwa kukopa.

(ii) Inafunga masoko ya mazao ili kuuza nje yanchi.

(iii) Inaagiza chakula kutoka nje ili kupunguzapato lao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Serikali itaendeleahivi, itakuwa ndoto kufikia mapema nchini yenye uchumi wakipato cha kati cha Mtanzania cha Shs. 1,670,032/= – Shs.6,500,000/=. Serikali inapoamua maamuzi ya kusaidia mtuaweze kuongeza pato, lazima ifungue milango yote; siyo tukufungua mmoja na mwingine tunafunga. Ushauri wangu nikwamba:-

(i) Serikali iendelee kusaidia pembejeo za kilimocha wakulima wa hali ya chini inavyopaswa.

(ii) Inunue mazao kwa fedha taslimu.

(iii) Ihakikishe maghala ya kuhifadhia mazao yaovijijini yanajengwa, kwani hata kama Serikali itashindwakununua yatakuwa yamehifadhiwa vizuri vijijini na kupatasoko lingine yakiwa salama na sivyo ilivyo sasa kwambainasisitiza kununua mahindi yao, wanabaki hawana pakuyahifadhi, mvua zinaanza kunyesha, mlanguzi anakwendakunua mazao kwa bei anayotaka yeye ya chini, mkulimaanaona bora auze kuliko kuona mazao yake yanaharibika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imetueleza hatuainazochukua za kujenga maghala makubwa. Nawapongezalakini mipango lazima pia ielekezwe katika source ya mazaohayo, kuwe na maghala ya kuhifadhia chakula. Ni lazimatumfikirie mzalishaji maskini – mkulima mdogo.

[MHE. V. R. M. KAWAWA]

163

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu gesi, naombakuishauri Serikali kwamba tuanze mapema kuandaaMpango, Sera na Sheria ya Mapato ya Gesi yatatumikaje.Mimi nashauri tuwe na Sheria ya Mapato na Matumizi ya Gesiyatakayokuwa ring fenced ili yaelekezwe katika miradi yamaendeleo maalum itakayosaidia Watanzania wotewatakaoona matokeo ya haraka na itakayochocheakusaidia maendeleo yao.

Pia mapato ya miradi hiyo kusaidia kulipa mikopotuliyokopa, kupunguza mzigo wa madeni tuliyo nayo.Mipango mingine ya kuendeleza vijana wetu kuwaelimishaufahamu na ustadi, nao uendelee tena kwa kasi mno ilituweze kuwa na wajuzi wengi katika eneo hili la gesi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, ili tuweze kuwekezakifaida lazima pia sekta muhimu ziende pamoja katikakuwekeza ili kupata huduma wezeshi. Mfano maji, barabarana umeme katika maeneo ya miradi. Lazima tu-combineprogram zetu za sekta hizi na tusimamie, ziende sambambaili kurahisisha uwekezaji na kutupa sisi pia “negotiation power”kwamba nasi tumewekeza kiasi gani kama Serikali katikaeneo la miradi kurahisisha uwekezaji, hivyo, kuwa na nguvukatika majadiliano ya mgawanyo wa mapato ya miradi nawawekezaji kwa kuthaminisha uwekezaji na miundombinuyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MHE. HAJI KHATIB KAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, sektaya uvuvi hapa nchini ni moja ya sekta inayoweza kuchangiazaidi katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini kamailivyoainishwa kwenye Mkakati wa Kukuza Uchumi naKupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA) na Ilani ya Uchaguziya CCM ya mwaka 2005 – 2010.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni kutokana na ukwelikwamba nchi yetu imebarikiwa kuwa na maeneo mengi yamaji baridi na maji ya bahari yenye rasilimali nyingi za uvuvi,ambapo shughuli za uvuvi hufanyika. Tanzania Bara ina

[MHE. V. R. M. KAWAWA]

164

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Ukanda wa Pwani wenye urefu wa kilomita 1,424 na upanawa maili za majini 200. Eneo hilo la bahari limegawanyikakatika maji ya kitaifa yenye upana wa maili za majini 12, sawana kilomita za mraba zipatazo 64,000 na eneo la bahari kuu(deep sea) lenye upana wa maili za majini 188, sawa nakilomita za mraba zipatazo 223,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la maziwa makuumatatu ambayo ni Ziwa Victoria lenye kilomita za mraba68,800 ambapo Tanzania humiliki asilimia 51% sawa nakilomita za mraba 35, Ziwa Tanganyika lenye kilomita zamraba 32,900 ambapo Tanzania humiliki asilimia 41% sawana kilomita za mraba 13,489 na Ziwa Nyasa lenye kilomita zamraba 30,800 ambapo Tanzania humiliki asilimia 18.51% sawana kilomita za mraba 5,700. Pia yapo maziwa ya kati namadogo 29.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na hali hiyo naiwapo kweli Serikali ina nia ya dhati ya mapendekezo yaMpango huu wa Maendeleo wa Taifa, basi ni wakati sasakuwawezesha wavuvi kwa kuwapatia mikopo ya fedha,kuwawezesha kitaalam pamoja na kuwatengenezeamiundombinu ya kuwawezesha kupata vifaa vya uvuvi kwabei nafuu. Iwapo Serikali itafanya hivyo kwa wavuvi, basikwa kweli dhamira hii ambayo ni njema kwa wananchi naTaifa kwa ujumla wake, hasa kwa sekta hii ya uvuvi inawezakufikiriwa. Iwapo itashindikana na kutokana na jinsi Serikaliilivyo jilabu juu ya jambo hili, itakuwa ni aibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha ajabu na ambachokimekuwa kikiwavunja moyo na kuwakatisha tamaa kabisawavuvi wa nchi hii hasa wale wavuvi wa eneo la Dar esSalaam (Minazi Mikinda Kigamboni), wavuvi ambaowanawezesha Mkoa wa Dar es Salaam na maeneo menginekupata kitoweo cha samaki, wapo baadhi ya Watendaji waSerikali na baadhi ya vyombo vya ulinzi huwasumbua wavuvihawa na kuwanyanyasa, hata pale ambapo hawajavunjasheria. Baadhi ya vyombo vya ulinzi vinavyowanyanyasawavuvi hawa ni Police Marine pamoja na JWTZ.

[MHE. H. K. KAI]

165

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile vyombo hivi kwakuendeleza manyanyaso kwa wavuvi hawa, wakatimwingine huwafuata baharini na kuvifungasha vyombo vyawavuvi hawa pamoja na kuwatishia na kuwapeleka PoliceMarine ambako wanapaki vyombo vyao. Ili wawaachiewavuvi hawa, ni hadi pale wavuvi hawawatakapotengeneza mazingira ya rushwa ndipowanawaachia. Hii ni aibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, mwaka 2012hadi kufikia mwezi wa sita (Juni, 2013), Serikali haijatoa lesenikwa wavuvi wa eneo la Dar es Salaam lakini Police Marinewanawalazimisha wavuvi kutoa leseni na hata palewanaposema hatuna sababu kila tunapofuata kwenye ofisihusika tunaambiwa leseni bado au vitabu vya lesenihatujaletewa; wakati huohuo Watendaji wa Serikali ambaoni Maafisa wa Fisheries wanafahamu wanachoongea wavuvina wanajua ni kweli leseni hazijatoka, unadhani ni nini maanayake? Ndiyo maana nikasema kwamba baadhiwanashirikiana na vyombo vya ulinzi nilivyovitaja kuwatesawavuvi na kuwanyanyasa. Vipi tutafanikiwa kwenye mpangohuu wa Maendeleo wa Taifa? Hii ni aibu.

Mimi binafsi sifikirii hata kidogo kwa kweli kamatutafikia kwenye Mpango huu mwema wa maendeleo yaTaifa, kama wapo Watendaji wa Serikali ambao hawana nianjema na mpango huu wa Taifa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ardhi, mara nyingi nakwa muda mrefu nchi yetu kumekuwa kukijitokeza matatizona mizozo ya ardhi, jambo ambalo baadhi ya maeneo yanchi yetu wananchi wamekuwa wakilalamikia maeneo hasayale ambayo kuna wawekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi kwanza kabisanapenda ku-declare interest, ni Mjumbe wa Kamati ya Ardhi,Maliasili na Mazingira. Kamati yetu hii tulifanya ziara ya kikazikatika Jimbo la Mufindi (la Mheshimiwa Kigola) ambako yupomwekezaji anayemiliki Kiwanda cha Kutengeneza Karatasi(Mufindi Paper Mill). Kiwanda hiki kwa muda mrefu kina mizozo

[MHE. H. K. KAI]

166

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

na waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda hiki kabla hakijauzwakwa mmiliki wa kiwanda hiki, kutokana na madai ya malipoyao na vilevile kwenye kiwanda hiki yapo malalamiko yabaadhi ya vijiji katika eneo hili wakidai kuporwa maeneo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya Kamati yetukupata nafasi ya kutembelea kiwanda hiki na kufanyamazungumzo na uongozi wa Mufindi Paper Mill na vilevilekukutana na wanakijiji cha Isaula ambao wanalalamikia eneolao kuporwa na Mufindi Paper Mill; Kamati tulichobainihatukuona matatizo ya ardhi, isipokuwa Kamati tulichokionani Sitofahamu. Kwa bahati mbaya sana Kamati ilichobaini nimizozo, matatizo pamoja na sitofahamu. Yote hayoyanasababishwa na Serikali inayoongozwa na CCM. Hii niaibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwa nini niseme Serikalihii inayoongozwa na CCM na inayojiita sikivu ndiyoinayosababisha? Kwa mfano, kutokana na madai yawaliokuwa wafanyakazi wa kiwanda hiki kabla ya kumilikiwana Mufindi Paper Mill, Serikali na mmiliki wa MPM kwa maraya kwanza walikaa pamoja kujadili juu ya tatizo hili na mmilikiwa MPM alikubali kutoa kiasi cha shilingi bilioni moja (1) katiya shilingi bilioni tatu (3) wanazodai watu hao na zinazobakiailipe Serikali, bahati mbaya Serikali ilishindwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, mmiliki waKiwanda cha MPM kwa sababu anataka mzozo huuumalizike, mara ya pili walipokutana tena na Serikalikuzungumzia jambo hili, mmiliki huyo alikubali fedha zoteambazo ni malipo ya wafanyakazi hao wa kiwanda hichokabla hajamiliki yeye, fedha ambazo ni shilingi bilioni tatu (3)kuzilipa; isipokuwa tu alichohitaji ni guarantee ya Serikali vipiitamlipa fedha hizo lakini hadi sasa Serikali hii inayojiita sikivuimeshindwa. Hii ni fedheha na aibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu wanakijiji cha Isaulabaada ya kuwasikiliza, walichotuambia wao hawanamatatizo na mwekezaji kwa sababu walipokutana wao,wanakijiji na mwekezaji huyo kuzungumzia kuhusu eneo lao

[MHE. H. K. KAI]

167

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ambalo mwekezaji alipanda miti, mwekezaji alikubalikwamba alikosea na eneo hilo akawaachia wanakijiji.Isipokuwa wanakijiji hao tatizo walilotulalamikia ni kwambabaada ya mwekelezaji kupanda miti katika eneo lao hilo,walilalamika Wizarani na Waziri alipeleka wataalam lakinihadi leo hawajapata mrejesho wa Serikali ama Wizara husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, rai yangu kutokana namapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa ili uwezekufanikiwa, ni vizuri sasa Serikali hii ihakikishe kila penyemigogoro ya ardhi isimamie na kuimaliza kabisa na paleambapo Serikali imewaahidi wananchi, itekeleze ahadi hiyo.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti,Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwamwaka 2014/2015 yametaja miradi mbalimbali ya kitaifa. Katiya miradi hiyo, uko pia Mpango Maalum wa Maji katika Jiji laDar es Salaam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa uamuzi waBaraza la Mawaziri wa mwaka 2011, Mpango huo utekelezajiwake ilikuwa mwaka 2013. Hata hivyo, kutokana na udhaifukatika utengaji wa rasilimali na kukosa uharaka wa utekelezajihata kwa fedha ambazo zimetengwa, maamuzi hayo yaBaraza la Mawaziri hayatakuwa yametekelezwa nakukamilika mwaka 2013. Aidha, Mpango wa Maendeleo waMiaka Mitano uliopitishwa Juni, 2011, sehemu kubwa ya miradiilipaswa iwe imekamilika 2013/2014 na mingine imalizike 2014/15.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, Mpango tunaojadilisasa ufanyiwe marekebisho kwa kurejea Mpango waMaendeleo wa Miaka Mitano na michango yangu Bungeni2011/2012 na 2013 na Hoja Binafsi niliyowasilisha tarehe 4Februari, 2013. Aidha, Serikali itoe majibu iwapo kauliiliyonukuliwa kwenye vyombo vya habari tarehe 2 na 3Novemba, 2013 na Waziri wa Maji, Mheshimiwa Prof. JumanneMaghembe kuwa miradi ya Dar es Salaam itakamilika 2017,ndiyo ratiba mpya ya utekelezaji? Waziri wa Nchi, Ofisi yaRais (Mahusiano na Uratibu). Mheshimiwa Stephen Wasira

[MHE. H. K. KAI]

168

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

atumie majumuisho kueleza ni lini hasa Mkutano na Rais juuya Maji Dar es Salaam, kwa kuzingatia ahadi yake katikaMkutano wa Bunge la Bajeti kuwa “nikae mkao wa kula”.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na Bunge hilikutambulisha wanamichezo mara kwa mara, michezo naburudani ni sekta ambayo haijapewa kipaumbele katikaMpango wa Miaka Mitano na hata katika Mpango wamwaka tunaoendelea kuujadili. Hivyo, marekebishoyafanyike kwa kurejea Sera ya Michezo na Sera ya Utamaduninchini na mipango mbalimbali na kuingiza michezo katikaMpango wa mwaka 2014/2015. Vipaumbele vya kuingizwani pamoja na kukuza vipaji na michezo kwa Serikalikushirikiana na Vyama vya Michezo vyote na Vyama vyaWasanii katika kutekeleza program za michezo na sanaashuleni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Serikali iongeze nguvukatika kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya michezo naburudani. Aidha, Serikali inayoongozwa na CCM irejesheviwanja vilivyohodhiwa na CCM ili vitumike kwa ufanisikwenye maendeleo ya michezo na burudani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi ya kitaifa ya sekta yanishati. Ipo miradi ya umeme na ya gesi asili kati yavipaumbele. Nishati ni chanzo cha ongezeko la gharama zamaisha na athari kwa uchumi wa nchi. Hivyo, Serikali itoemajibu, sababu za Wizara ya Nishati kueleza inakusudia tenakupandisha bei ya umeme ikiwa ni siku chache baada yaWaziri wa Fedha kukutana na IMF na Benki ya Dunia (WB)Marekani Oktoba 2013.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, ni kwa nini Serikaliinafanya nyaraka za mikataba na ripoti za uendelezaji wamiradi ya gesi vinakuwa siri hata baada ya mimi kamaMbunge kuomba kwa Sheria ya Kinga, Haki na Madarakaya Bunge?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya uchumi wa nchihaijaweza kuongeza ajira rasmi na kuweka mazingira ya

[MHE. J. J. MNYIKA]

169

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kuwezesha ajira zisizo rasmi na hivyo kushindwa kuwezeshaufumbuzi wa matatizo ya ukosefu wa ajira, hususan kwavijana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali iwasilishe BungeniUtafiti wa Ajira na Mapato (Employment And Earnings Survey)ya mwaka 2011 na kuharakisha kufanya tathmini ya nguvukazi(labour force survey) ili mipango na bajeti izingatie hali halisi.Novemba Mosi ni Siku ya Vijana Afrika, hivyo ni wakatimuafaka Serikali kupokea mchango wa kuzingatia Mkatabawa Vijana wa Afrika ambao nchi yetu imeridhia, sasa uwekwekatika vipaumbele vya Mipango ya Maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mapendekezo ya Mpango,kipengele cha 2.3.11, juu ya kazi na ajira, kinaonesha kasi yautekelezaji ni mdogo. Katika kifungu cha 3.3.14 kimesemakwamba katika mwaka 2014/2015 kutatekelezwa programuya kukuza ajira kwa vijana. Hata hivyo, Serikali ikumbukekwamba toka mwaka 1993/1994 palianzishwa Mifuko yaMaendeleo ya Vijana. Hata hivyo, pamekuwepo na udhaifuna ufisadi katika Mifuko hiyo na pia kiwango cha fedhakinachotengwa kimekuwa kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nyongeza kidogo ya mwakawa fedha 2012//2013 ya shilingi bilioni 6.1 ni ndogoukilinganisha na mahitaji ya mikopo na mitaji kwa vijana.Hivyo, kama ilivyofanywa kwa sehemu ya fedha za marejeshoya malipo ya Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), shilingi bilioni40 kwenye Benki ya Rasilimali (TIB), Serikali ifuatilie zaidi yatrilioni moja zilizotolewa na kudhaminiwa wakati wa kunusuruuchumi (stimulus package) zielekezwe kwenye Mifuko yaVijana na Wanawake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Mwanasheria Mkuuwa Serikali atengue barua yake ya tarehe 16 Aprili, 2013 yenyeKumb. Na. AG CC/N.10/1 ili kuwezesha Muswada Binafsi waBaraza la Vijana la Taifa uchapwe kwenye Gazeti la Serikalikwa kuwa utawezesha kuanzishwa Mfuko wa Maendeleo yaVijana wenye usimamizi thabiti. Mwanasheria Mkuu azingatiekwamba Muswada niliowasilisha nilizingatia Ibara ya 135(2)

[MHE. J. J. MNYIKA]

170

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ya Katiba ya Nchi na hivyo haufungwi na mashafrti ya Ibaraya 99 ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, Serikali iwasilisheBungeni taarifa ya utekelezaji wa wa Sheria ya KuhamasishaAjira ya mwaka 2004, ambayo imeielekeza Kamati zakuchochea kazi na ajira kuundwa katika ngazi zote tano zautawala kuanzia kwenye Mitaa/Vijiji mpaka katika Serikali Kuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, iwapo Serikalihaitatoa majibu thabiti juu ya mchango wa Mpango waMaendeleo kwenye maendeleo ya wanawake na vijana,ziada ya mapendekezo yaliyotajwa kwenye sheria kwa sasaambayo haikidhi mahitaji, nitawasilisha Hoja Binafsi kwenyeMkutano huu wa Bunge kuhusu suala hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya uchumi wa nchi yetuhailingani na matarajio ambayo Mpango wa Maendeleo waMiaka Mitano uliweka, ambayo mapendekezo ya awamutatu zilizotangulia kuanzia 2011 zilipaswa ziwe zimeyatimizamwaka 2013.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, Mpango waMaendeleo wa Taifa 2014/2015 ujikite katika kurekebishakasoro ya ukuaji wa uchumi wa nchi, kuelezwa kuwa unakuahuku uchumi wa wananchi ukishuka na kuongezeka kwaumaskini wa kipato. Pamoja na mfumuko na bei kushuka nakuwa tarakimu moja, bei za bidhaa na huduma hazijashuka.Hivyo, Serikali ieleze ni kwa vipi Mpango huo utawezesha beiya bidhaa kushuka kwa kuongeza uzalishaji na kurekebishakasoro kupitia bajeti katika maeneo ambayo Sheria za Fedha2011, 2012 na 2013 zimechangia ongezeko la bei?

Mheshimiwa Mwenyekiti, udhaifu wa miundombinuya Jiji la Dar es Salaam iwe ni ya usafiri na usafirishaji, nishati,TEHAMA, maji safi na majitaka; ingekuwa na mchangomkubwa wa kupungua kero kwa wananchi asilimia 10% yanchi na pia ingewezesha ongezeko la mapato kwa Taifa nahivyo kutoa mchango kwa maeneo mengine ya nchi.Kiwango cha fedha kilichotengwa, kilichotolewa na

[MHE. J. J. MNYIKA]

171

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kilichotumika kwenye utekelezaji wa miradi ya Kitaifa ya Jijila Dar es Salaam kuanzia 2011 mpaka 2013 ni pungufu sanaya Jedwali la Mpango wa Miaka Mitano katika sekta husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, katika Mpango waMaendeleo wa Mwaka 2014/2015 na bajeti ya mwaka tajwa- Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Wizara ya Maji na Wizara yaFedha; irejee kipengele cha A.1.1.4 na kutenga fedha kamilikwenye miradi ya maji safi na maji taka kuziba pengo laupungufu wa miaka iliyotangulia na kuonesha kwa vitendohatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa miradi kwakugawa kandarasi vipande kwa Wakandarasi tofauti kamainavyofanyika kwa barabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, i l i kupunguzamsongamano kwa haraka pamoja na mradi wa Mabasi yaHaraka unaoendelea (DART), narudia kusisitiza kamailivyokuwa kwa mwaka 2011, 2012 na 2013 wakati wamichango yangu juu ya mipango na bajeti; Ofisi ya Rais, Tumeya Mipango, Wizara ya Fedha na Wizara Ujenzi – zirejeekifungu cha A.1.2.1 na kutenga fedha za barabara zapembezoni za mchujo na barabara za mzunguko (ring roads).Kiasi kinachohitajika kwa kazi hii ni wastani wa fedhazisizopungua bilioni 100. Mpaka sasa kwa miaka mitatu, kiasikilichotengwa kwa barabara hizo zilizotajwa kwa majinakatika Jiji la Dar es Salaam hakijafikia hata robo (25%), nakiasi halisi kilichotolewa ni kidogo zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuongeza vyanzo vyamapato ya kutekeleza miradi, Serikali ipunguze misamahaya kodi, ipunguze matumizi ya Serikali hasa katika ununuziambapo gharama ambazo Serikali inanunua bidhaa nahuduma ni 2% - 10% ya bei ya kawaida ya soko. Asilimia 40%ya ununuzi wa umma umekaliwa na ufisadi au ununuzi usiona thamani halisi (value for money) na hivyo kukwamishamiradi ya maendeleo. Ili kuongeza ufanisi wa ufuatiliaji natathmini, Serikali iwasilishe Bungeni mikataba yote ambayoMawaziri waliingia kupitia Mpango wa Matokeo ya Haraka(BRN).

[MHE. J. J. MNYIKA]

172

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. GAUDENCE C. KAYOMBO: MheshimiwaMwenyekiti, napenda kuipongeza Serikali juu ya Mpango uliomzuri, ingawa una changamoto kubwa na fedha ya kutoshakuweza kutekeleza miradi na mipango tuliyo nayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naamini kuwa nchi hiini tajiri sana na fedha haipaswi kuwa ni tatizo. Tunalo tatizokubwa la kuweka vipaumbele vyetu, tunalo tatizo lanetworking, tunalo tatizo la ubinafsi, tatizo la kuwa ndani ya‘box’ kwa kuamini kwamba maeneo fulani tu ya nchi ndiyopengine yenye haki zaidi kuliko mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano, mradi wa mkaa/umeme Ngaka. Mradi huu ulianzishwa kwa nia ya kuchimbamakaa ya mawe ili kufua umeme wa MW. 400. Uchimbaji wamakaa ya mawe unaendelea lakini uwekaji wa mitambo yakufua umeme umekwama kwa miaka minne (4) sasa kwakitu kinachoitwa majadiliano kati ya ZAWCOM na TANESCObado hayajakamilika. Wakati huohuo nchi ina upungufumkubwa wa umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TANESCO inatumia Sh. 4.5billion kwa siku ili kuzalisha umeme, US cts 45 – 50 badala yaUS cts 7 – 10. Hizo fedha za siku moja zingeweza kabisakuifanya TANESCO ijenge power station pale NtunduwaroMbinga na kupata umeme wa nafuu. Kwa nini Tume yaMipango na Wizara ya Fedha hailioni hilo? Kwa nini mradihuu wa kimkakati haupewi fedha na Serikali na ushiriki waSerikali ni mdogo mno. Kwa hiyo, fedha zipo, swali ni kwambatunazitumia wapi? Wananchi wakilalamika, Serikali inatumianguvu kubwa kuwanyamazisha. Hivi Serikali haina njia nzuriya kuongea na wananchi wa Ntunduwaro kamainavyoongea kwa ustaarabu na wawekezaji Wazungu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, miundombinu, licha yamradi mkubwa wa makaa ya mawe, Ruvuma ni Mkoaunaozalisha chakula kwa wingi. Usafirishaji wa makaa yamawe unafanywa kwa malori na chakula vivyo hivyo.Barabara hizi ni za vumbi, hivyo kuleta madhara makubwa.Suluhisho (short term) ni kuweka lami barabara ya Kitai –

173

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Ruanda – Lituhi. Midterm ni kujenga reli toka Mtwara – Songea– Mbinga – Mbamba Bay pamoja na tawi toka pale Kitaikwenda Ruanda (Ntunduwaro) Lituhi ili kubeba makaa yamawe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maoni yangu ni kwambanchi yetu ina madini mengi ya aina mbalimbali. Serikali iwena mpango madhubuti wa namna ya kuvuna madini yetukwa faida ya Watanzania hasa wachimbaji wadogowadogo, kama wachimbaji wa Saphire katika Wilaya yaMbinga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bei ya mazao ya Kilimo.Serikali iharakishe programu ya kuhakikisha wakulima wamazao ya biashara kama kahawa, pamba na koroshowanafaidika pale bei za mazao hayo zinapoporomoka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, CARMATEC imefanya kazinzuri ya kubuni na kutengeneza trekta. Sasa Serikali iiwezeshekuzalisha matrekta hayo. Halmashauri za Wilaya zinawezakuhusishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. HAMAD ALI HAMAD: Mheshimiwa Mwenyekiti,kitabu cha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo yaTaifa (uk. 2) (kif. 1.2) aya ya 2, inasema na imeonesha kukuakwa pato la kila mtu kwa mwaka 2012. Kwa maelezo hayo,pato hili lilikuwa wastani wa 2847. Hata hivyo, shabaha yaMpango (uk.11)(a), kuongeza pato hadi asilimia 7.1 ambapopia Mtanzania atakuwa anapata pato chini ya Shs. 4000. Hiini kuwakebehi wananchi. Kama bado shabaha ya mpangoni kuendelea na kupata mlo mmoja usiokamilika, hapahatuwezi kuwa na maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania ni ya wakulima,wafugaji, wavuvi na wafanyakazi. Kwa muda mrefu sasa,Serikali imekuwa ikilizungumzia tatizo la wakulima na wafugajibila kulipatia ufumbuzi wa kudumu tatizo hili na hali inaashiriamatatizo endelevu baina ya wakulima na wafugaji. Wavuvi

[MHE. G. C. KAYOMBO]

174

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

wanapata shida kubwa toka Serikalini kwa kushurutishwavifaa vya kisasa ambapo Serikali haijioni kuwa ina wajibu walazima wa kuwawezesha wavuvi hao.

Pia Serikali inalalamika kuwa samaki wanaibiwa lakinihadi leo haina mpango wowote wa kuwa na meli zake zakuvulia samaki hao kwa maendeleo ya nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, linaloonekana kwa Serikalini kuwaonea wananchi ambao wameshindwakuwatengenezea mazingira mazuri ya kuweza kujiendelezana kukuza vipato vyao. Jambo hilo la Serikali kushindwa kuwana mpango madhubuti wa kufanya makundi haya kufanyaharakati zao kwa amani na wao hawataweza pia kuungamkono Mpango wa Serikali wa Maendeleo, wakijua kwambaSerikali hiyohiyo ndiyo inayoua kwa risasi mifugo yao lakinipia ndio wanaochoma moto nyavu za wavuvi bila utaratibumbadala wa Serikali kwa makundi haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Serikaliinaonekana kushindwa kufikiria njia mbadala yakuwawezesha makundi haya kuweza kujiendeleza, Serikalisasa inatumia nguvu isiyo ya kawaida kujihami kwakuwanyanyasa wananchi, kuua mifugo yao na kadhalikabadala ya kuwa na mipango mizuri itakayowasaidia watuwetu. Hatuwezi kufikia maendeleo tunayoyataka, maanatunasema tu bila kuwa na utekelezaji wa tunayopanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya uchafuzi wamazingira, Serikali itilie maanani na ichukue hatua ya dhatiya kuhakikisha kwamba nishati mbadala ya gesi inawafikiawananchi katika maeneo yao mbalimbali na kwa bei nafuuili kuondoa au kupunguza wimbi lililopo la ukataji miti kwaajili ya mkaa wa kupikia. Jambo hili litasaidia kupunguzauchafuzi wa mazingira utokanao na ukataji wa miti nauchomaji wa mkaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.Ahsante.

[MHE. H. A. HAMAD]

175

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. SHAFFIN A. SUMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti,naunga mkono hoja. Kwanza, naipongeza Serikali kwa kazinzuri na mpango mzuri iliyouleta Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha muhimu hapa nikuhakikisha kwamba maelezo yote yanatekelezwa. Hatahivyo, kutokana na mfumo wa cash budget, ratiba yamipango haiendi sawia na kalenda. Ni bora Serikali ikaonauwezekano wa kupata mkopo wa muda mfupi wakatitukisubiri TRA ikikusanya mapato. Pia TRA inatakiwa ijipangevizuri zaidi kukusanya mapato kwa sababu niwafanyabiashara 1.7 milioni tu wanaolipa kodi Tanzania,jambo ambalo linahitaji kufanyiwa kazi zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna makampuni mengi Dares Salaam ambayo hayalipi kodi ipasavyo na chanzo chatatizo hili ni kupitisha bidhaa nyingi bandarini bila kulipiwaushuru. Bado mtandao wa walaji upo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali pia isiachie miradi yamaendeleo iliyopo. Kwa mfano, zao la tumbaku linaingizapato kubwa katika Taifa letu. Hata hivyo, wakulima waliowengi Mkoani Tabora bado wanatumia jembe la mkono ilawanazalisha sana tumbaku. Kwa sasa wananchi haowanahitaji msaada na msukumo mkubwa kwa sababu fedhawalizokuwa wanadai kupitia Chama cha Msingi, hazipo natena zimeshaibiwa. Naishauri Serikali ili isipoteze mapatomakubwa, ione namna ya kuwalipa fedha zao ili zao latumbaku lisidorore.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali iharakishe mchakatowa kufufua reli ya kati ili kupunguza mfumuko wa bei wa kilamara, ambao unatokana na bei ya mafuta kupanda kilamara. Hata hivyo, tumbaku yote inayozalishwa Taborainaweza kusafirishwa na reli kupelekwa Morogoro, soko lausafirishaji lipo, ni Serikali tu yenyewe inajichelewesha lakinipia reli ya kati ni tegemeo kubwa kwa nchi za jirani. Sokolipo, sisi wenyewe tu hatulioni.

Mheshimiwa Spika, bandari ya Tanga ina umuhimu

176

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

wa kipekee. Tunaweza kutumia bandari zetu kutuliza mbioza wenzetu wa Kenya. Leo wao wanajivunia bandari yaMombasa na wanajua kabisa kuwa pamoja na kwamba sisiTanzania tuna fursa nzuri zaidi kuliko Kenya lakini tumelalasana. Muda umefika, tuamke sasa tutekeleze yale yotetunayoyapanga. Ahsante.

MHE. DKT. DAVID M. MALLOLE: MheshimiwaMwenyekiti, nashukuru sana kwa kupata nafasi hii ili naminitoe mchango wangu wa maandishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilimo cha umwagiliaji. Enziza Ukoloni, mabwawa mengi sana yalichimbwa hapaDodoma Mjini. Mabwawa haya sasa yamejaa tope nakukosa uwezo wa kutunza maji mwaka mzima. Serikaliielekeze nguvu zake katika kuchimba tope za mabwawahaya, hasa yale ya Hombolo, Vikonje, Makutupora,Mbalawala na Mkalama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maji haya yatasaidia sanakilimo cha umwagiliaji wa mboga-mboga kwa matumizi yaidadi kubwa ya wananchi na wanafunzi wa Vyuo Vikuu vyaDodoma (itachukua wanafunzi 40,000) na Vyuo vya St. John,CBE, Chuo cha Mipango, Chuo cha Hombolo na kadhalika.Maji haya pia yatasaidia kunyweshea mifugo yetu naumwagiliaji wa mashamba makubwa ya zabibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda (Kiwanda chaZabibu). Dodoma Mjini inahitaji kiwanda kikubwa cha zabibu.Wananchi wamekata tamaa na kilimo cha zabibu. Hakunasoko na hakuna kiwanda cha zabibu. Ni wakati muafakasasa Serikali itamke kama wananchi waendelee na kilimocha zabibu au kama waache kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zao la zabibu ndiyoukombozi pekee wa kiuchumi wa watu wa Dodoma. Kwavile zao hilo linakubaliana na hali ya hewa na uhaba mkubwawa mvua ambao husababisha njaa kila mwaka hapaDodoma. Wananchi wakiuza zabibu, wanapata hela,watanunua chakula, watajenga nyumba bora,

[MHE. S. A. SUMAR]

177

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

watasomesha watoto na kufanya mambo mengi yakimaendeleo. Tunaomba jibu la soko na kiwanda kikubwacha zabibu kwa ajili ya wakulima wa zabibu Dodoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. MICHAEL L. LAIZER: Mheshimiwa Mwenyekiti,Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa miaka iliyotanguliana huu wa sasa, ni mizuri sana. Sina wasiwasi kwa Mpangohuu wa 2014/2015. Tatizo ni utekelezaji. Kuna mamboambayo yanaleta utata kwa wananchi kuhusu uchumi waTaifa:-

(a) Kukua kwa pato la Taifa, kwani hawaonitofauti na miaka iliyopita.

(b) Mfumuko wa bei za bidhaa na huduma yajamii, inawanyima wananchi kuona unafuu wa kupungua aukushuka kwa mfumuko wa bei.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Longido ni Wilayaya wafugaji kwa asilimia 95%. Uchumi wao waliopewa naMwenyezi Mungu ni mifugo, wanyamapori na magadikwenye Ziwa Natron. Katika mambo haya matatu, hakunamikakati iliyowekwa au mpango mzuri ili wananchi na Taifazima wafaidike. Napenda kuikumbusha na kueleza Serikalikuhusu uchumi ambao tunao, lakini wanaofaidika niWakenya tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, mifugo (ng’ombe)wote wa Wilaya ya Longido na Ngorongoro wanauzwa Kenyakwa sababu huko ndiko kuna Kiwanda cha Nyama (KMC)ambapo wanachinja ng’ombe 500 kwa siku (asilimia 60 ning’ombe wa Tanzania. Kenya hawawezi kujitosheleza,wakikosa mifugo wa Tanzania watafunga kiwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, hakuna utaratibu waTanzania kupata ushuru wa mifugo wanaokwenda kuuzwaKenya, wanapitishwa njia za panya. Nilitegemea Kiwandacha Nyama kingejengwa Arusha ili Watanzania wapate soko

[MHE. DKT. D. M. MALLOLE]

178

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

la mifugo na Serikali kupata mapato ya mifugo wengiwanaouzwa Kenya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutowekwa Kiwanda chaMagadi kwenye Mpango. Kwa masikitiko makubwa,nashangaa kutowekwa Kiwanda cha Magado Soda ya LakeNatron Soda Ash kwenye Mpango. Rais, Mheshimiwa JakayaM. Kikwete alipofungua Bunge hili mwaka 2010, alisema nilazima kijengwe kiwanda hicho. Tena alipofanya ziaraWilayani Longido, aliwaambia wananchi kwamba hatatokamadarakani kabla ya kiwanda hicho kuanza. Hii ni ahadi yaRais mwenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa kuna vita ya kiuchumikati ya Kenya na Tanzania. Wakenya wanadai ujenzi waKiwanda cha Magadi – umbali wa kilomita 30 kutoka ZiwaNatron utaharibu mazingira ya Ziwa hilo na mazalia yaFlamingo wakati wao wamejenga cha mita 300 tu kutokaLake Magadi. Wanaendelea na uzalishaji, hao Flamingowanaingia mpaka kiwandani. Baraza la Madiwaniwametembelea Kiwanda cha Magadi Soda Kenya,wakawakuta hao ndege ndani ya kiwanda. Wakenyawanapinga kiwanda kwa vile magadi kwetu ni mengi, walasiyo ya kuchoronga kama walivyochoronga huko Engaruka;ni ya kukusanya tena kwa wingi sana. Eneo la mazalia yaFlamingo ni kilomita 50 toka eneo la kiwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wakenya wanapingabarabara ya Arusha – Loliondo – Mugumu kwa sababu wataliiwatafika Mbuga za Serengeti na Ngorongoro bila kutumiandege. Barabara itarahisisha usafiri bila kutumia gharamakubwa. Wakenya wanapinga ujenzi wa Kiwanja cha NdegeSerengeti – umbali wa kilomia 20 toka Serengeti. Mbuga yaNorth Mara, barabara ya lami inafika kwenye mbuga. Kwanini iwe nongwa ikifika Mugumu au Loliondo, ambapo siyondani ya Mbuga?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mgawanyo wa kekiya Taifa. Kwa hili, baadhi ya maeneo wanakosa pesa zamiradi hasa Wilaya ya Longido. Kila bajeti wanayopanga

[MHE. M. L. LAIZER]

179

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

hawapati fedha, hawajawahi kupata zaidi ya asilimia 27%.Matatizo ni mengi, hata kwenye Mipango ya mwaka huu2014/2015, hatutegemei chochote. Naomba ujenzi waKiwanda cha Magadi Soda – Lake Natron uwekwe kwenyeMipango ya mwaka huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Mnada mkubwa waMifugo ujengwe pamoja na Kiwanda cha Nyama Arusha.Tanzania waweke utaratibu mzuri unaoeleweka wa kupelekamifugo Kenya na kulipa ushuru Tanzania, kuliko kwenda kulipaKenya tu. Nategemea kama mtaangalia ukweli bilaupendeleo, mtakubaliana na mchango wangu. Tatizo lawapangaji ni upendeleo, hili ndiyo tatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Mungu awabarikisana.

MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMMED: MheshimiwaMwenyekiti, hali na mwenendo wa uchumi wa dunia ni kwelisiyo wa kuridhisha kutokana na sababu mbalimbali pamojana mabadiliko ya tabianchi. Hata hivyo, ukiangalia rasilimalizilizopo Tanzania pamoja na vivutio vya kitalii tulivyo navyo,ni dhahiri kwamba bado Tanzania inayo fursa kubwa zaidiya kukuza uchumi wake. Kasi ya ukuaji wa uchumi waTanzania haiendani kabisa na hali ya kipato cha mwananchina rasilimali tulizo nazo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali ama kwakutumia wataalam wake wa ndani au hata wa kutoka nje(consultants) kukaa na kuangalia upya mifumo na mipangoyetu ya kiuchumi (environmental reform), pia kuangalia upyabaadhi ya sera zetu. Ni imani yangu kwamba majawabuyake yanaweza kutuondoa hapa tulipo na kupiga hatuanyingine mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuangalia mifumoyetu, hivyo ni vyema kupata mrejesho wa tathmini ya kinakuhusu mradi wa “Kilimo Kwanza” kwani ni jambo lakushangaza kuona kwamba Kilimo kinachangia asilimia 1.4%ya pato la Taifa, ilhali eneo letu la kilimo ni kubwa. Maeneo

[MHE. M. L. LAIZER]

180

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kwa ajili ya upatikanaji wa maji ya umwagiliaji yapo, maziwamakubwa yametuzunguka na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado Serikali haijachukuadhamira ya dhati katika eneo la Uvuvi. Katika taarifa yaSerikali hakuna sehemu ambayo Serikali imeoneshaimejipangaje sasa katika bahari na maziwa tuliyonayo kukuzauvuvi na namna ya kuboresha wananchi wake wa Kandaya Ziwa, Lake Tanganyika, Lake Nyasa na wa Ukanda waPwani watakavyoweza kuwasaidia ili kuwa na uvuvi wa kisasawenye tija zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni aibu iliyo wazi kwambahivi sasa uvuvi unachangia asilimia 2% tu katika pato la Taifailhali uvuvi pekee iwapo utaendelezwa, unaweza kuchangiaasilimia 3% ya pato la Taifa. Naishauri Serikali kuandaamazingira endelevu na yaliyo wezeshi ili sasa ijikite katika uvuviwa bahari kuu. Sambamba na hilo, kuimarisha ulinzi katikaeneo hilo ili kuzuia meli zilizo nyingi kutoka nje ya nchi yetukutokuendelea kuiba rasilimali ya samaki tuliyonayo katikabahari kuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala la makusanyoya kodi, bado mianya ya ukwepaji kodi haijapatiwa udhibitiulio bora. Pamoja na hilo bado katika ngazi ya Halmashauri,utaalam na ubunifu wa kuibua vyanzo vya mapato ni mdogo.Pia hakuna udhibiti mzuri wa ukusanyaji wa mapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeshauri Serikalikuiboresha Tume ya Mipango kirasilimali ili watu wawezekushuka katika ngazi ya Halmashauri ili kuzisaidia badala yawao kubaki ofisini na kutia miongozo tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo, nivyema sasa Serikali ikasitisha uanzishaji wa Halmashauri mpyanchini ili kwanza ikae ifanye evaluation. Ni dhahiri miradi mingiya Serikali iko katika mamlaka za Serikali za Mitaa, lakini tijayake imekuwa ni dhaifu sana.

[MHE. R. M. MOHAMMED]

181

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, uwezo wa Halmashauri zetukujiendesha hivi sasa kwa kutumia mapato yao ya ndanihayazidi asilimia kumi. Average hii si hali nzuri hata kidogo.Ni vyema Serikali kupeleka nguvu za kitaalam kwenyeHalmashauri zetu katika kusimamia mapato na miradi yamaendeleo ili ilete tija. Hivi sasa Halmashauri zimejaa madenina zipo kwa ajili ya kusubiri ruzuku kutoka Serikali Kuu tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. SYLVESTER MASSELE MABUMBA: MheshimiwaMwenyekiti, Mpango huu wa Maendeleo wa Taifa ni sehemuya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya mwaka 2025.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna nia safi ya kutakakufikia malengo ya Dira ya Taifa, ni wakati muafaka sasatuviangalie upya vipaumbele vyetu kwani si ki latulichokiainisha kwenye mpango ni kipaumbele. Nijuavyomimi, kipaumbele ni kitu ambacho kikitekelezwa kitachangiakukua kwa sekta zingine pia kwa wakati badala yakutekelezwa kwa ufanisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hotuba ya MheshimiwaWaziri imeonesha vipaumbele vya miundombinu ya reli,barabara, umeme, maji; vilevile sekta za kilimo, afya, elimu,madini, bandari na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo yaliyoorodheshwahapo juu yanahitaji kuangaliwa upya. Mfano, kati ya reli nabarabara, kipi kiwe kipaumbele cha kwanza. Reli ni muhimukwa usafiri wa uhakika ambao pia utaziwezesha barabarazetu kupata relief ya mzigo mkubwa unaosafirishwa naambao huziharibu barabara zetu mara kwa mara. Mapatoyatokanayo na usafirishaji wa mizigo, yataongezeka na ajiranyingi zitapatikana.

Mpango unapaswa kuonesha namnatutakavyokabiliana na Traffic Jam katika miji mikubwa hapanchini. Traffic Jam imepunguza efficiency na productivity.Hali hii inaathiri sana uzalishaji na ukuaji wa uchumi.

[MHE. R. M. MOHAMMED]

182

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta ya umeme ni muhimusana kwa uchumi wa nchi yetu. Je, Serikali imejipanga vipikatika kuwapatia umeme wananchi walioko mijini na vijijini?Tukifanikiwa kuvitekeleza vipaumbele hivi, hata sekta za elimu,maji na afya zitaweza kuboreshwa. Vinginevyo shule nahospitali zitaendelea kutokuwa na umeme wa uhakika hatamaabara hazitafanya kazi. Sekta ya Kilimo bila ya umeme,reli na barabara; haiwezi kukua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali kuviangaliaupya vipaumbele vyetu. Naomba kuwasilisha na naungamkono hoja.

MHE. ZAYNAB M. VULLU: Mheshimiwa Mwenyekiti,Serikali ina mpango wa kuanzisha Benki ya Wakulima. Je,Serikali imejipanga vipi katika kuviwezesha vikundi mbalimbalina hata wakulima wadogo wadogo na hasa wa vijijini?Itawafikia vipi?

Wanawake na vijana ni miongoni kwa wakulimaambao wanahitaji kuwezeshwa. Je, Serikali imejipanga?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vyema mikopo hiyo isiwena riba kubwa sana.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba kuchangia kwa kushauri juu ya nini kifanyike ilituweze kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja (IndividualEconomy).

Mheshimiwa Mwenyekiti, inashangaza na huwanajiuliza ni nini hasa kazi ya Wizara ya Mipango na Uvuvipamoja na Wizara ya Kilimo? Tumeendelea kushuhudiamigogoro mingi kati ya wafugaji na hifadhi, wafugaji nawakulima, wafugaji na watu katika makazi yao. Mgogorohuu kwa kiasi kikubwa wanaathirika wafugaji ambapo hivikaribuni tumeshuhudia Operation Tokomeza ambayo kwahakika ililenga kutokomeza Watanzania maskini hukuikiwaacha walengwa.

[MHE. S. M. MABUMBA]

183

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja bilaoperation ya kutokomeza, operation ya uwindaji haramu/wawindaji haramu; lakini siyo kuwaonea wananchi nakuwageuza kitega uchumi chao. Mfano, operation iliyoanzaMkoani Mara tarehe 14/10/2013 ambapo tumeshuhudiawananchi wakichomewa nyumba pamoja na mali zao zote,wakipigwa na wengine kuuawa. Mfano Mzee Peter MaseyaMarwa wa Kijiji cha Mvito aliyechukuliwa nyumbani kwakena siku ya pili yake walimrudisha wakiwa wameshamuua kwakipigo kichwani. Tumeshuhudia ng’ombe, mbuzi na kondoowakitokomezwa na hiyo operation tokomeza. Kiukweli nifedheha sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesoma mpango, lakinikwa masikitiko makubwa sijaona mpango madhubuti wakumwinua mkulima, mfugaji na hata Mtanzania mwingineambaye si mkulima wala mfugaji. Tumeshuhudia wafugajiwakitozwa jumla ya Sh. 180,000/= kwa ngombe, wasipokuwanazo zinapigwa risasi na au kupigwa minada.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napendekeza kwambaWizara ya Mifugo na Uvuvi ijikite zaidi katika LivestockManagement, tofauti na sasa ambapo tumejikita hasa katikaVeternary Issues tu. Wizara ina wajibu na kutaka kujua kunamifugo mingapi na iweze kukuza kiwango cha ubora chamifugo/ufugaji (quality products). Ili hii ifanikiwe inabidi Wizarana huu Mpango uzingatie kuwapatia wafugaji maeneombadala ya kulishia mifugo yao, (ikibidi hata zero grazing).Kutoa elimu juu ya ufugaji bora na siyo bora kufuga, kwambaili ufugaji uwe na tija (productivity) ni lazima tuzingatie qualityna siyo quantity. Tuwe na Maafisa Mifugo ambaowatahakikisha tunakuwa na breedings zitakazotoa mazaobora, pia Wizara ihakikishe upatikanaji wa maji kwa ajili yamifugo. Hii itasaidia sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wakati sasa WizaraMama/mtambuka kwa maana ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Kilimo; Ardhi, Nyumba na Makazi pamoja na Wizara yaMaliasili, zikae na kupata/kutafuta ufumbuzi wa jinsi ganitutakuwa na ufugaji wenye tija, kilimo chenye tija, makazi

[MHE. E. N. MATIKO]

184

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

bora na hii itatoa fursa ya ukuaji wa uchumi kwa kilaMtanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wakati sasa wa kuwa namipango madhubuti ambapo kilimo na ufugaji zinatakikanazitegemeane (compatible). Mfano wafugaji/mifugo itatoambolea na ardhi yenye tilling kwa ajili ya wakulima. Wakatihuo huo wakulima (farmers) watatoa ardhi/malisho kwa ajiliya mifugo yao kwa muda huku wakifuatilia malisho mahalipengine. Hili likitekelezwa vizuri, ardhi kwa ajili ya ufugajiitatuondolea jangwa na kuongeza rutuba kwenye ardhi/udongo; na hivyo kutoa fursa za kiuchumi, vilevile itatoamaendeleo na kuwepo (coexistence) ya mifugo, kilimochenye tija na ulinzi imara wa hifadhi zetu (wildlife).

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, kwa kifupi kabisanapendekeza miundombinu ya reli kutoka Bandari ya Dar esSalaam hadi Chalinze ambapo tutaanzisha bandari kavuChalinze. Hii itasaidia sana kupunguza msongamano wamagari ambao unazorotesha uchumi wa nchi yetu, kwanimuda mwingi unapotea katika foleni, unaweza kukaa zaidiya masaa matatu (3) au matano (5) toka Dar es Salaam hadiChalinze. Hii ni sababu ya kuwepo na malori ndani ya Jijihadi Chalinze. Reli itasaidia sana kutatua hili tatizosambamba na uboreshaji wa reli ya kati na ile ya kutokaTanga hadi Musoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tunahitaji mkakatiutekelezwe wa kuondoa kero ya maji hasa kwenye Majijikama Dar es Salaam. Hii ni aibu sana.

MHE. ROSWEETER F. KASIKILA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa afya hii.Nikushukuru na wewe kwa nafasi hii ya kupokea mchangowangu wa maandishi. Pia nimpongeze Mheshimiwa Wazirimwenye dhamana hii, Katibu Mkuu na Watendaji wotewalioandaa Mpango huu wa 2014/2015.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kitabu cha Mpango,ukurasa wa 49 – 53 vimeorodheshwa vipaumbele sita

[MHE. E. N. MATIKO]

185

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ambavyo vina shughuli (activities/vipengele) 41 ambavyoutekelezaji wake kwa kufikia viwango vya kuridhisha/kufikiamalengo kutahitaji fedha nyingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuanzia ukurasa 53 – 56yameorodheshwa maeneo mengine 15 (refer kitabu), lakinisi kwamba haya maeneo yatakaa dormant, nayo piayatahitaji fedha nyingi tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa uzoefu, mipangoimekuwa ikipangwa, lakini utekelezaji wake umekuwa duni;na hii imepelekea kuwa na viporo vingi, lakini yote hayayamekuwa ni kwa sababu ya ufinyu wa bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Matokeo Makubwa Sasa(BRN – Big Results Now) ya Mpango huu yanahitaji fedha.Niishukuru Serikali kwa ujenzi wa barabara zinazounganishamikoa, lakini Bajeti ya barabara inayotengwa kwaHalmashauri kwa ajili ya barabara za vijijini ni chini ya asilimia10% kati ya asilimia 30% wanazotengewa, lakini hii ni kwa ajiliya ufinyu wa bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ratiba ya Vikao vya Bajetiilibadilika na kuanza Aprili – Juni ili Wizara, Taasisi, Halmashauri,Manispaa na Majiji yaanze kupewa fedha (mafungu) iliwaanze utekelezaji robo ya kwanza ya mwaka husika wafedha. Lakini hadi sasa (Oktoba) baadhi ya Wizara naHalmashauri hazijapelekewa fedha, ni kwa ufinyu wa bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uhaba uliokithiri wawatumishi, wataalam, madawa, vitendanishi, vifaa tiba, lakinina ukamilishaji wa majengo ya Zahanati na Vituo vya Afyaambavyo wananchi kwa nguvu zao wamejitahidi kujenga,lakini ufinyu wa bajeti husababisha uhaba huo nakutokamilisha majengo hayo ikiwa ni pamoja na nyumba zawatumishi wa shule za msingi, maabara za sekondari nakadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maoni yangu katika hili nakwa sababu fedha zinakuwa hazitoshi, natoa maoni kuwa

[MHE. R. F. KASIKILA]

186

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

vyanzo vipya vya mapato vibuniwe vyenye mapatomakubwa vikijumlishwa na vyanzo vilivyopo sasa; ukusanyajiwa mapato kwa uaminifu na weledi ufanyike. Kilaanayepaswa kulipa kodi na alipe. Kodi ikusanywe kwaukamilifu na fedha itakayokusanywa itumike kwa kadri yampango (miradi).

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ni wakati muafaka waKamati za Kudumu za Bunge (Kamati Mtambuka) wakati ujaowa Vikao vya Kamati vya Maandalizi ya Bunge la Bajeti,Kamati ziombe Wakuu wa Mikoa na Halmashauri katikamipango yao waoneshe majedwali yanayoonesha vyanzovya mapato, vya zamani na vipya; mafanikio nachangamoto katika ubunifu wa vyanzo na ukusanyajimapato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MHE. NASSIB SULEIMAN OMAR: MheshimiwaMwenyekiti, kwanza naunga mkono Mpango huu waMaendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya uchumi ya nchi yetuimeimarika sana. Kama wanavyosema wataalam kuwakatika kipindi cha miaka kumi uchumi wetu utaushindauchumi wa Kenya. Kadhalika baada ya ugunduzi wa Gesi,Mafuta na Madini; uchumi wa Tanzania utakaribia uchumiwa nchi za Kiarabu kama Dubai katika kipindi cha miaka 20.Jambo muhimu ni kusimamia mipango yetu ya maendeleo.“Big Results Now” ni jambo muhimu sana kwa nchi yetu.Vipaumbele sita vilivyopendekezwa kama vitasimamiwavizuri, nchi yetu itapiga hatua kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukuaji wa uchumihauendani sambamba na kupungua kwa umaskini nchini.Hivyo, ukuaji wa uchumi lazima ulenge vijijini ambako hali zakimaisha za watu wetu ni mbaya. Kilimo ndiyo mwokozi wetu.Pembejeo, viuadudu, mbegu na matrekta lazima vipatikanekwa wakati ili wakulima wetu waweze kuongeza uzalishajiwa mazao ya kilimo.

[MHE. R. F. KASIKILA]

187

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kuwapatiavijana na akinamama mikopo yenye riba na masharti nafuuili wengi waweze kupata mkopo kwa azma ya kupunguzaumaskini.

MHE. REBECCA M. MNGODO: MheshimiwaMwenyekiti, katika hali halisi ya maisha ya Watanzania,Mpango wa Maendeleo haujaweza kurahisisha au kusaidiakufanikisha maendeleo katika maeneo yale ambayo yakonyuma kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ingawa mapendekezo yaMpango wa Maendeleo yanaonesha kwamba pato la Taifalimekua kwa kiwango cha asilimia 7.0% ikilinganishwa naukuaji wa asilimia 6.9% mwaka 2012, lakini ukuaji huohauonekani katika maisha ya Mtanzania wa kawaida. Sektazilizokuwa na viwango vikubwa vya ukuaji ni pamoja na usafirina mawasiliano kwa asilimia 18.4%. Ukuaji huo wa pato katikasekta ya Mawasiliano haumgusi mwananchi na walahaujaweza kumsaidia katika kujikwamua kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba,miundombinu yaweza kuwa kipaumbele katika mpango huu.Lakini tunahitaji nguvu kubwa katika mageuzi ya maendeleokatika uboreshaji wa reli. Reli ni njia pekee ambayo yawezakurahisisha usafirishaji wa bidhaa mbalimbali za biashara nachakula kwa bei nafuu na ni usafiri wa uhakika katikakurahisisha usafirishaji kutoka nchi moja kwenda nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nguvu kubwa ielekezwekatika kujenga reli imara za kisasa kwa kutumia uwekezajimkubwa ambao faida zake zitaonekana kwa kipindi kirefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nchi kama yetuambayo elimu haijapewa kipaumbele kwa miaka mingi,jambo ambalo limepelekea kuzalisha Taifa lisilo na utamaduniwa kufanya kazi kwa bidii, badala yake tumetegemeaMataifa makubwa kwa kuwa ombaomba na kuwakopa kilamara.

[MHE. N. S. OMAR]

188

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napendekeza elimu ipewekipaumbele. Taifa likiwa na wananchi walioelimika katikamaeneo mbalimbali, sekta nyingine zitaendelea kwa urahisikwani tutakuwa na watalaam wetu wenyewe na tutakuwana watu wenye kujali muda wa kazi na wenye kufanya kazikwa bidii na hivyo kuwa na ustaarabu wa kulipa kodikutokana na kuelimika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchumi wetu unawezakukua, kwa kuwa na watu wenye afya. Suala la afyahalijatupiwa macho. Uchumi hujengwa na watu wenye afyanzuri. Wasomi wazuri wenye afya nzuri hujenga uchumi imara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

MHE. ANNAMARYSTELLA J. MALLAC: MheshimiwaMwenyekiti, Mpango huu ni mzuri kama utatekelezwa kamaulivyokusudiwa, lakini napata wasiwasi kwa sababu mipangoni mingi na bado inakwenda taratibu kwa kusuasua. Mfano,Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza na suala la Elimu.Mpango kwa kuusoma tu ni mzuri, kiutekelezaji unaonakwamba:-

(a) Nyumba za Walimu hakuna. Walimu wanaishikatika mazingira magumu;

(b) Watoto wanasoma huku wakikaa chini,madawati hayatoshi na miti tunayo;

(c) Walimu hawatoshi; na

(d) Shule za Kata hazina Maabara. Je,tutawapataje Wanasayansi kwa kusoma nadharia?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija kwenye Kilimo;tunaelewa wazi Kilimo ni uti wa mgongo na ndiyo ajira kwaWatanzania wengi na tulihamasishwa sana kujikwamuakupitia:-

[MHE. R. M. MNGODO]

189

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

(a) Kilimo cha Kufa na Kupona; na

(b) Siasa ni Kilimo na sasa Kilimo Kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na wananchikujituma, Serikali imekuwa ikichelewesha upatikanaji wapembejeo kupitia Wakala wa Pembejeo. Mbolea inakujakwa kuchelewa, inakuta mkulima amepanda mazao bilambolea ya kupandia, vivyo hivyo ya kukuzia. Maafisa Kilimohawana tabia ya kuwazungukia wakulima kutoa elimu yanamna ya kulima kilimo bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kil imo cha tumbaku;tumbaku ni zao linalochangia kuingiza pato la Taifa. Lakiniwakulima hawa wamekuwa wakicheleweshewa pesa zamauzo mpaka misimu miwili mkulima hajalipwa pesa yake.Je, pembejeo anunue na nini? Pia je, hayo ni maisha borakwa kila Mtanzania?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali kusimamiaVyama vya Ushirika viweze kumjali mkulima na kutoa hudumaya pembejeo kwa wakati, pia kusimamia bei nzuri na masokokwa mkulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu maji; suala la majikatika kuleta uhai na kusukuma maendeleo, ni suala nyetisana katika Mpango huu. Mpaka sasa tuna miaka mitatu yaMpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ambaoutasambaza maji vij i j ini na kuhakikisha wananchihawatembei mwendo mrefu kufuata maji, lakini mpaka sasawananchi wanatembea umbali mrefu sana kutafuta maji nawengine vijijini wanakunywa maji ya madimbwi wakichangiana wanyama. Hii imesababisha ongezeko la maambukizimapya ya UKIMWI kutokana na wanawake kubakwawanapofuata maji umbali mrefu. Naomba Serikali itambuehili na kuweka mazingira mazuri ya upatikanaji wa maji iliwanawake wasibakwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Utawala Bora.Utawala bora ni nguzo katika kusimamia maendeleo yenye

[MHE. A. J. MALLAC]

190

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

mafanikio. Bila utawala bora, nidhamu ya kazi hakuna namafanikio ya maendeleo hayapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utawala tulionao ni wakutumia nguvu na usiozingatia haki za binadamu walaheshima ya mtu. Wananchi sasa hivi wanaishi maisha yawasiwasi, woga na hofu. Viongozi hawana nidhamu waokwa wao, hawaheshimiani, hawana upendo,hawathaminiani, wamejawa chuki na fitina mahali pa kazina kuchafuana. Hali hii inahamia mpaka kwa wananchi wakawaida wanaoongozwa. Upendo na heshima vimepungua,na chuki na fitina ndivyo vimeshika nafasi. Ndiyo maana sasahivi kumekuwa na matukio ya mauaji ya kinyama nakumwagiana tindikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali:-

(i) Idumishe amani kwa kusisitiza upendomiongoni mwa jamii, ikianzia kwa viongozi; na

(ii) Ipambane na rushwa kwa dhati, kwani rushwani chanzo cha chuki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, napenda kumaliziakwa kusema kwamba rasilimali watu ithaminiwe. Nchi bilawatu hakuna kazi wala miundombinu. Kwani watuwanauawa hovyo na askari wetu, kila kukicha ni risasi za motokwa wananchi kwa kosa dogo tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ikae chini itafakarinini hasa tunahitaji nchini. Suluhisho la tatizo nchini siyo kupigarisasi, siyo kuchoma nyumba na mifugo na mali za wananchi.Ni kurudisha nyuma Taifa na kuwatia umaskini wananchi.Ahsante.

MHE. CYNTHIA H. NGOYE: Mheshimiwa Mwenyekiti,awali ya yote naomba kuipongeza Serikali kwa kuandaaMpango mpya wa Serikali kwa mwaka 2014/2015. Naombakuchangia hoja hii katika maeneo machache kamaifuatavyo:-

[MHE. A. J. MALLAC]

191

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wazi kabisa uchumi wetuhutegemea kilimo, maliasili na mifugo, lakini tumeachamambo muhimu ambayo yanapaswa kuzingatiwa ili sektahizi zichangie maendeleo endelevu hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapozungumzia kilimokwa hakika ni lazima tuzungumzie kilimo cha umwagiliajiambacho kinaweza kufanyika mwaka mzima. Tatizo kubwaninaloliona ni mipango yetu kutoliweka suala la hifadhi yamazingira na hasa hifadhi ya vyanzo vya maji kwa uzitomkubwa. Ni lazima Wataalam wetu wa Mipango waanzekuliona suala la mazingira kama jambo la lazima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tutaendelea kuliachasuala la mazingira kama agenda isiyo ya umuhimu, mipangoya kKilimo Kwanza au mpango wa SAGCOT; haina maanayoyote, haina uendelevu wowote. Ni matumaini yangu nanashauri mpango huu uweke bayana program za upandajimiti kwa kila Kaya, kuhifadhi vyanzo vyote vya maji, misituyote ihifadhiwe ili tuwe na uhakika wa upatikanaji wa mvuaza uhakika kwa ajili ya kilimo na mifugo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mifugo; ni muhimuSerikali yetu ianze kuiga mfano wa namna nchi nyingine kamaNamibia wanavyofanya. Kuna haja ya kila Mkoa kutengamaeneo kwa ajili ya mifugo tu, ambako kutajengwamabwawa ya maji kwa ajili ya mifugo, kupanda nyasi zamifugo na wafugaji watengewe maeneo hayo. Wafugajiwenyewe wataamua kuwa na idadi ya mifugo kulingana naukubwa wa maeneo waliyopewa. Uzururaji wa mifugohautakuwepo tena na kuondokana na mapigano kati yawakulima na wafugaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la amani na utawalabora, ni lazima yaangaliwe kwanza. Hakuna mpangowowote wa maendeleo utakaowezekana kutekelezekaiwapo wananchi hawana usalama wa uhakika. Mipangoya kusimamia usalama wa nchi yetu ianze kuangaliwa kwamakini sana ili vyombo vyetu vifanye kazi vikiwa na amanibila vikwazo.

[MHE. C. H. NGOYE]

192

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mipango ya Maji; hakunanjia yoyote itakayofanikiwa wala miradi ya kuwa endelevukama mipango ya hifadhi ya vyanzo vya maji itapuuzwa nawafugaji, wakulima na wawindaji. Upatikanaji wa vyanzovya fedha una njia nyingi katika nchi yetu, hasa kamatutaziangalia sana hifadhi zetu za wanyama, ambayo nimaeneo ya kitalii. Hata hivyo, utalii mwingine ambao ni wamilima, maua na kadhalika. Maeneo hayo hayajaangaliwakwa karibu ili yatoe mchango wa kiuchumi hapa nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, naishauri Serikaliijikite zaidi katika kuwawekea mipango mizuri ya maendeleoWanawake na Vijana, kwani haya ni makundi muhimukiuzalishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo hayomachache, naunga mkono hoja hii.

MHE. FATUMA A. MIKIDADI: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza kabisa napenda kupongeza kwa Mpango, kwaniMpango umetaja mambo mazuri na yanayomgusamwananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi niongelee juu ya jinsiya kuendeleza uchumi nchini ili kukuza uchumi wetu:-

(1) Kuendeleza elimu nchini.

(2) Kuendeleza maji – maji ni muhimu.

(3) Kuendeleza kilimo – chakula ni muhimu.

(4) Nishati na madini – ili kuendeleza viwanda.

(5) Utalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo haya matano (5)yatakuza uchumi wetu. Tuna rasilimali za kutosha sanaambazo ni nyenzo za kuendeleza uchumi huo. Tujipange,tuendeleze ili tufufue uchumi wetu. Naomba kuwasilisha.

[MHE. C. H. NGOYE]

193

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. MILTON M. MAHANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti,kwanza naunga mkono hoja hii, lakini ningependanizungumzie suala la mikakati ya kukuza ajira nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niipongeze Serikali kwakuainisha mikakati na program za ajira zitakazoshughuliwana Serikali mwaka 2014/2015.

Hata hivyo, uzoefu unaonesha kwamba, Wizara yaKazi na Ajira inayosimamia programu hizi za ajira huwahaipewi fedha za maendeleo kwa ajili ya kutekelezaprogramu na mikakati hiyo.

Kwa mfano, mwaka huu (2013/2014) Wizara hiiimepata sifuri kwa miradi ya maendeleo. Kama program namikakati ya kukuza ajira iliyooneshwa kwenye Mpango huuhaitapangiwa fedha za maendeleo ya kuitekeleza, tutakuwahatuoneshi umuhimu wa kushughulikia tatizo hili kubwa la ajirakwa vijana.

Aidha, Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango umeelezakwamba Serikali itatekeleza tafiti za hali ya nguvukazi na haliya utaalam nchini.

Pia kwenye maelekezo ya uandaaji wa mipango nabajeti 2014/2015, MDAs wametakiwa kujaza fomu za uzalishajiwa ajira kwenye maeneo yao. Mambo yote haya yanahitajiuwezo wa kifedha na nyenzo ili Wizara ya Kazi na Ajira iwezekufuatilia, kutekeleza na kubaini ukuzaji wa ajira hadi ngaziya chini ya Halmashauri za Wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara pia imeshindwakutekeleza na kukamilisha mradi wa Labour MarketInformation System (LMIS) kwa ukosefu wa fedha zamaendeleo. Ni matumaini yangu kwamba mwaka 2014/2015, Wizara ya Kazi na Ajira itaanza kupewa kipaumbelekinachostahili kuliko sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.

194

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. DKT. MAUA ABEID DAFTARI: MheshimiwaMwenyekiti, naunga mkono hoja na pia naomba kuchangiaifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Dira yetu ya Maendeleo ya2025 ni kuendeleza ujenzi wa uchumi wa kisasa na Taifalinalojitegemea. Na Serikali imeweka vipaumbele vyakutekeleza katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano(5) ambavyo ni miundombinu, kilimo, viwanda vinavyotumiamalighafi za ndani na kuongeza thamani, maendeleo yarasilimali watu na ujenzi na uendelezaji wa huduma za utalii,biashara na fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sekta ya Kilimo badohaijasimamiwa kisawasawa. Upo umuhimu wa kukuza kilimokuanzia ngazi ya familia, kwa familia kuwezeshwa kupataardhi ya kutosha ya kilimo, wakopeshwe pembejeo za kilimo,elimu bora kwa wakulima na ufuatiliaji thabiti wa Mabwanana Mabibi Shamba. Uingizaji wa power tillers dhaifuhazikusaidia sana wanyonge, bado wananchi wengiwanatumia jembe la mkono.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, uingizaji wa mbegumbaya za mahindi kumeathiri sana kilimo cha mahindi,Arusha na Nyanda za Juu. Vituo vya Utafiti wa Mazao mbalimbali vinahitaji sana kuboreshwa. Watafiti wapatiwe zanana vifaa na pia kupewa motisha. Aidha, kufufuliwa kwamaeneo ya utafiti na watafiti kupewa nafasi ya kwendakupata mawazo mapya ya kitafiti toka nchi nyingine.Matokeo ya tafiti mbalimbali kurejeshwa kwa wakulima kwalengo la uzalishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Sekta ya Uvuvi. Nisekta isiyo na wenyewe. Wavuvi wanavua kwa bahati na sikisayansi. Wanaofaidika ni wavuvi wa bahari kuu wenyevifaa. Nao hawa wana matatizo ya rasilimali zetu za samakikwa kuwavua samaki wakubwa na hasa wadogo nakuwatupa baharini wakati tayari wamekufa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna monitoring system

195

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

yoyote wanayofanyiwa wawekezaji wakubwa, badala yakewavuvi wadogo wadogo ndio wanaoandamwa na makundimbalimbali. Ni vyema wavuvi wadogo wadogo wasaidiwekupata unafuu wa kodi kwenye nyavu, mashine za boti; napale wanapobahatika kununua mbao za kuchongamajahazi/boti za uvuvi. Wavuvi wadogo wadogowanachangia sana uchumi wa nchi yetu, wawezeshwe.Tunashukuru kufutwa kwa kodi za nyuzi, ile haileti impactkubwa kwa wavuvi wetu wadogo wadogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Uchukuzi; reli zetuzinahitaji kuboreshwa na ikiwezekana kuongeza matawi ilizisaidie uchukuzi kwenye maeneo ya uzalishaji mali.Tunang’ang’ana na kuboresha barabara, na kusahau kuwaiwapo reli itaboreshwa kubeba mizigo mizito, barabaraitapata nafuu na itadumu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea kusemakwamba sioni mantiki kwa reli zetu kuchangia Road Toll yabarabara. Huyu ni mpinzani wake, iweje leo reli ife kwakunufaisha barabara? Mabilioni ya fedha yatokanayo naroad toll ambayo reli inachangia kwa barabara siyo haki.Reli na barabara zote zina umuhimu wake na zote zipewekipaumbele sasa. Ujenzi wa reli ya Dar es Salaam – Isaka,sasa tufikirie reli hiyo iende Burundi kwanza badala yaRwanda. Waache Rwanda wajenge reli yao na Uganda naKenya na Sudan. Kwanza Rwanda haituhitaji Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Viwanda; napendakujua ule uamuzi wetu kutaka Viwanda vyetu vya Pambakutengeneza nyuzi na kuuza nje badala ya kuuza pambasafi, umefikia wapi? Je, ule uamuzi wetu wa kubanguakorosho hapa hapa nyumbani badala ya kupeleka koroshozetu raw umefikia wapi? Yote hayo ni maamuzi yenye tija,ila hayakutekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza Wizara kwa kazinzuri na pia kwa Bunge kuunda Kamati ya Bajeti ambayoinafanya kazi nzuri ya kuisaidia Serikali mambo mengi.

[MHE. M. A. DAFTARI]

196

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

MHE. NAOMI A. M. KAIHULA: Mheshimiwa Mwenyekiti,nashukuru kwa Mwenyezi Mungu kwa kunipatia afya njemana wasaa huu wa kuweza kuchangia Mpango huu.

Kwanza, Mheshimiwa Mwenyekiti, yahusu suala lakukua kwa uchumi na kuhusu kuongezeka kwa pato lawastani kwa kila mtu kwa kiwango cha asilimia 17.9%. Jambohili bado halijajibu utata wa viulizo vya wananchi kwambambona ongezeko hilo haliendani na hali halisi ya kipato chawananchi wa hali ya chini ambao pato lao linazidi kiushukahata kuwa chini ya dola moja kwa sasa hivi? Hii inaoneshajinsi gani mipango hii siyo shirikishi. Matokeo yake ni kuwepokwa takwimu kwenye maandishi yasiyowalenga wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, Mpango huu piahaukuchukulia kwa umakini sekta muhimu kama viwanda nabiashara, ambazo ikiwa zingepangwa vizuri kwa kufufuaviwanda muhimu vilivyohujumiwa na Serikali ya CCM, basiajira zingeongezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Serikali hii haijaona kuwakuna umuhimu wa kuanzisha na kuendeleza viwanda vyakusindika na kufungasha vyakula kwa ajili ya kuwapawananchi nafasi ya kufungua na kupenyeza masoko yamajirani zetu ambao wengi wao wana uhitaji wa vyakula nasisi Mungu katukirimia tunu hiyo. Kuongeza thamani kwamazao ya kil imo kwa kuyasindika na kuyafungasha,kungepunguza adha kubwa ya wananchi kudodewa namazao yao ya kilimo. Manufaa makubwa ambayoyangepatikana ni kupunguza utegemezi wa mazao hayakwa nchi za jirani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la utegemezihaliangaliwi kwa umakini. Mpango haujaonesha jitihada zamakusudi za kuondokana na utegemezi wa misaada tokanje na mikopo kutokana na washiriki kutoka nje. Kwanikusema kweli haina faida kihivyo iwapo mipango madhubutiya kuwa na sera nzuri za kuondoa misamaha ya kodiinayotolewa kiholela kwa wawekezaji kwa kisingizio rahisi chavivutio vya wawekezaji. Tatizo siyo misamaha ya kodi, bali ni

197

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

udhaifu wa utangazaji wa vivutio hivyo katika Balozi zaTanzania na ukosefu wa elimu ya uwekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Utawala Bora; suala hili piani muhimu katika utekelezaji na mafanikio ya Mpango, lakiniMpango huu haujatilia maanani sana. Mpango unapaswakuzingatia mkakati wa kuwashughulikia wahujumu wa uchumiambao idadi yao inaongezeka kwa kasi. Mfano, viongozina wataalam ambao wanatayarisha mipango hafifu namikataba hafifu kwa ajili ya faida zao binafsi au kwa ajili yamanufaa binafsi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia haujaonesha jinsi ganigrand corruption inayoendelea sasa hivi na inayoathiriuchumi kwa sehemu kubwa, inaweza kudhibitiwa. Mfano,wauaji wa tembo, mikataba mibovu ya madini, gesi, uranina kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango usipange ukiwa naitikadi za watawala vichwani. Hili litasababisha mpangokushindwa kabisa kuanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Deni la Taifahalioneshi kupungua.

MHE. AUGUSTINO M. MASELE: MheshimiwaMwenyekiti, naiunga mkono hoja ya Mheshimiwa Waziri waNchi kwa kuwa ina maslahi makubwa kwa Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ilivyo ada kwamba,kupanga ni kuchagua na Tanzania kama Taifa, tunavyovipaumbele vingi katika kuhakikisha nchi yetu inapiga hatuakatika kuelekea kwenye maendeleo kama Dira ya Taifa yaMaendeleo ya 2025.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza MheshimiwaWaziri wa Nchi pamoja na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipangokwa kuja na vipaumbele vichache ambavyo vina mchangomkubwa katika ukuzaji wa uchumi wa nchi hii. Sektazilizoainishwa kama vipaumbele ni pamoja na:

[MHE. N. A. M. KAIHULA]

198

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

(i) Miundombinu;

(ii) Kilimo;

(iii) Viwanda vinavyotumia malighafi za ndani kuongeza thamani;

(iv) Maendeleo ya Rasilimali watu; na

(v) Uendelezwaji wa huduma za utalii, biashara na fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hakika kuwepo kwaMipango ya Maendeleo ni jambo moja na kuwepo kwaufuatiliaji wa dhati wa mipango yenyewe na ndipo wazo lakuwepo kwa falsafa ya Matokeo Makubwa Sasa (Big ResultsNow) lilibuniwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza pia hatua yakuanzishwa kwa Presidential Delivery Bureau. Kwa kuwepokwa kitengo hiki ni jambo la kheri na naishauri Serikali ioneuwezekano wa kuwashirikisha Watanzania waliooneshaubunifu mkubwa na kuzifanya taasisi zao kufanya vizuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali iwajumuishe katikaPresidential Delivery Bureau. Watu hao ni kama akina Dkt.Ramadhan Dau wa NSSF, Nehemiah Mchechu wa Shirika laNyumba na Dkt. Kimei wa Benki ya CRDB. Watanzania hawawameonesha kuwa na vipaji, akiwemo pia Ndugu Mfugalewa TANROADS. Wazalendo hawa wachache wameoneshauwezo mkubwa wa kuziongoza taasisi zao na kwa jinsi hiyowatamshauri Mheshimiwa Rais pamoja na Tume ya Mipangokuhusu mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big ResultsNow).

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, naishauri Serikaliichukue hatua za makusudi za kuajiri wataalam mabingwawa kutoka Mataifa yaliyoendelea; mabingwa hao wawe ni

[MHE. A. M. MASELE]

199

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

wale waliothibitika kutoa michango katika Mataifambalimbali. Ni dhahiri kuwa Mataifa yanayopiga hatua kwaharaka kama Korea Kusini, Malasyia na Uchina, yamekuwana Tume za Mipango kama ya kwetu na zikatumia mbinu zakupata wataalam kutoka nchi zilizoendelea. Mifano ni mingi,ikiwemo pia nchi ya Iran.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utajir i wa nchi yetuunatuweka katika nafasi nzuri ya kuweza kuwa na ushawishiwa kupata wataalam mabingwa kutoka nchi zilizoendelea,cha msingi hapa ni kuwalipa mafao mazuri. Ukiwepo mkakatikabambe wa kuwepo kwa Presidential Delivery Bureau, ninaimani kubwa kuwa nchi yetu itakuwa tayari kuhakikishakwamba teknolojia mbalimbali zinazopatikana duniani kotetunaweza kupata kwa aidha:-

(a) Kuomba Mataifa yaliyoendelea yatupatie.

(b) Kuhakikisha tunatenga fedha kwa ajili yakununua teknolojia husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina imani na Serikali yaCCM kwamba, ni sikivu na zaidi sana niishauri kuwa mchakatowa uchimbaji wa Makaa ya Mawe na Chuma kule Ligangana Mchuchuma ili kuhakikisha nchi yetu inafanikiwa katikaMapinduzi ya Viwanda na kuikabili biashara ya vyumachakavu inayotishia uwepo wa miundombinu ya nchi yetuinayohujumiwa na watu wasiokuwa na nia njema na nchiyetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.

MWENYEKITI: Ahsante sana. Sasa nawaita wafuatao:Mheshimiwa Simbachawe na atafuatiwa na MheshimiwaSaada Salum, Mheshimiwa Eng. Lwenge, MheshimiwaGoodluck Ole-Medeye, atafuatiwa na Mheshimiwa AdamMalima, halafu Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe.

[MHE. A. M. MASELE]

200

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGEB. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sanakwa kunipa nafasi na mimi nianze kwa kuunga mkono hojaya Serikali ya Mipango ambayo ni mapendekezo kama hatuaya mwanzo ya bajeti ya mwaka unaofuata wa fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ingawa nilitegemea kupatamawazo ya nini tufanye, lakini hapa kwa kiasi kikubwanitajikita kwenye yale ambayo yamesemwa na WaheshimiwaWabunge ambayo kwa kiasi kikubwa hapa ni kutoa taarifaya baadhi ya mambo ambayo pengine hayaeleweki vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Sekta ya Nishati naMadini limezungumzwa sana suala la utayari wa Serikali juuya uchumi wa gesi na hapa imesemwa sana juu yautayarishwaji wa Sera ya Gesi na Sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hii kulitaarifuBunge lako Tukufu na Watanzania kwa ujumla kwambamchakato wa Sera ya Gesi umekamilika na Sera ya Gesiimekamilika tangu tarehe 10 Oktoba, 2013, nakinachosubiriwa sasa ni maandalizi ya sheria. Ingawayalikuwa yanaenda sambamba na utayarishaji wa Sera hii;maandalizi ya sheria ambayo na yenyewe inabadilika kwakiasi kikubwa, kwa hiyo, mchakato huo baada ya muda nawenyewe utakamilika ili kwanza tutayarishe sera ndiyobaadaye tutayarishe sheria. Hali kadhalika gesi master planna yenyewe itafuata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zoezi hili limechukua mudamrefu kwa sababu ya umakini tunaopaswa kuwa nao katikakutumia rasilimali hii. Tumejifunza kutoka kwenye nchimbalimbali maana rasilimali hii sisi siyo wa kwanza duniani,nchi mbalimbali zimegundua rasilimali hii, lakini tumejifunzana huko kuna mazuri na mabaya ya kujifunza na ndiyo maanasisi tumejitahidi kuhakikisha kwamba hatufanyi kosa katikajambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalolimezungumzwa sana na Waheshimiwa Wabunge juu ya

201

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Sekta ndogo hii ya gesi ni suala zima la ushirikishwaji waWatanzania. Ushirikishwaji wa Watanzania hapaumezungumzwa katika nyanja mbili. Moja, imezungumzwakatika nyanja ya ushirikishwaji katika ile local content kwambaWatanzania nao wanashiriki vipi katika uchumi wa gesi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa hatuwezi kusemakwa kiwango ambacho tumegundua gesi tuliyoigundua sasakwamba tuko kwenye full implementation, kabisa ya kusemakwamba sasa tunazalisha na tunatumia zao hili ambalotumelipata. Kwa hiyo, sasa bado tuko kwenye hatua ya awalisana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, gesi tuliyonayo kwa sasa niile ya Songosongo ambayo inatumika kuzalisha umemeambayo tunazalisha Dar es Salaam, lakini na ile ya Mnazibayambayo tunamia kuzalisha umeme tunaozalisha kule Mtwarana ambao umesambazwa katika Mkoa wa Mtwara. Gesinyingine iko kwenye kina kirefu na bado haijaanza kutumikana itachukua muda kwenda kuitumia hiyo. Kwa hiyo,nichukue nafasi hii kuwaambia Waheshimiwa Wabungekwamba hatujachelewa, ila haraka yetu pia inapaswa tuwemakini sana kuhakikisha kwamba hatukosei. Hatujachelewabado, hii rasilimali bado, pengine zaidi ya miaka mitano ijayondipo tutakapoanza kuitimia rasilimali hii vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini eneo la pili, lilikuwa nisuala la ushirikishwaji wa Watanzania katika utafutaji nauchimbaji wa gesi. Vyovyote utakavyosema, suala hililinahitaji mjadala wa kutosha. Unaposema kuwashirikishaWatanzania katika uchimbaji na utafutaji, Serikali imewekaShirika la TPDC ambalo ni Shirika la Umma la Watanzania wotekwamba litutazamie na lilinde maslahi yetu, Watanzaniawote. (Makofi)

Sasa unaposema sekta binafsi, sijui ni kikundi chawatu, lazima hapa uje na jibu useme kabisa ni nani huyotumpe? Uje useme kabisa, tunampa nani kwa niaba yaWatanzania? Serikali yenyewe imeona TPDC ndiyo itachukuarasilimali ile.

[NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. G.B. SIMBACHAWENE)]

202

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu uko hivi: Serikalikupitia Wizara Nishati na Madini inatoa leseni kwa TPDC, TPDCwanamtafuta mbia, wanashirikiana naye, kwa kuwa TPDCinawakilisha Watanzania wote, wanashirikiana na hiyokampuni nyingine itakayokuwa imekuja kuwekeza auMakampuni ya kuja kuwekeza na pale TPDC inakuwainatunza share za Watanzania kati ya asilimia 65 hadi 75.(Makofi)

Sasa unaposema Watanzania lazima waingie katikasekta hiyo, washiriki katika kuchimba na kutafuta, lazima uwepia specific kwamba tunampa nani kwa niaba yaWatanzania? Hapa lazima Watanzania wakubali kwambampeni fulani, lakini ukisema tu hivi halafu ikabakia hewanihivi, kidogo inakuwa ni vigumu sana kueleza hili jambo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine lililozungumzwahapa ni launching ambayo imefanyika ya tarehe 25 Oktoba,2013. Tumefanya uzinduzi huu. Uzinduzi huu hauna maananyingine yoyote zaidi ya kuweka tu kusema jamani sisi tunavitalu vya gesi, vipo. Kwa mujibu wa sera hii ambayo iko tayari,tumewakaribisha wawekezaji wa ndani na wa nje washirikikatika kuingia kwenye mnada huu wa vitalu, hakunaaliyezuiwa, wote wanaruhusiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama exceptionszinatafutwa, basi tujadiliane hapa tu-discuss tusemeexceptionals hizo zimkumbe nani, nani apendelewe, hilo nijambo lingine. Lakini kwa maana ya sera, sisi tumesemaWatanzania, na wasio Watanzania washiriki katika zoezi hili.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, limezungumzwa sualalingine la umeme katika Wilaya mpya. Wilaya mpya ambazohazina umeme ni Wilaya 13. Katika Wilaya hizi 13, tayariWakandarasi wameshapatikana na sasa hivi tunapoelekeani kuanza kwa utekelezaji wa miradi hiyo ya Wilaya hizi 13.Wilaya hizi zinajulikana, ni Wilaya ya Chemba, Kyerwa, Mlele,

[NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. G.B. SIMBACHAWENE)]

203

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Uvinza, Kakonko, Buhigwe, Momba, Nanyumbu, Kalambo,Mkalama, Nyasa, Busega na Itilima. Huku Wakandarasiwameshapatikana, tunaenda kwenye utekelezaji.

Kwa miradi ya REA kwa ujumla ambao tulisemakwamba utekelezaji wake utatuchukua katika mwaka huuwa fedha na utaanza, Mikoa mingine imepata Wakandarasilakini Mikoa mingine kumi haijapata Wakandarasi namchakato unaendelea, mwisho wa mwezi huu tunawezatukakamilisha mchakato wa kupata Wakandarasi ili kuwezakutekeleza miradi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, limezungumzwa suala labomba la mafuta kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.Bomba hili tulifika hatua nzuri akapatikana kampuni inaitwaNuru Oil ambao walisema watajenga hilo bomba lakini piawatajenga na refinery.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kusuasua huku kunatufanyatufikirie upya wazo hili la kuiachia hii kampuni na tuone namnanyingine. Lakini wazo hili bado liko pale pale. Ni muhimu sanakwa uchumi wa Taifa kuwa na bomba hili la mafuta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine lililozungumzwa niumeme unaotokana na makaa ya mawe wa Ngaka. Tukokatika hatua ya negotiation katika PPA kati ya TANESCO nawenzetu wa NDC wakishirikiana na hiyo kampuni, mbia waona hali ya mazungumzo inaenda vizuri ingawawanachobishania pale ni bei za umeme, tutaona namna yaku-speed up hilo zoezi. Aidha, Liganga na Mchuchuma,mkandarasi yuko site anaendelea na mgodi wa Kiwira nikwamba STAMICO wameshakabidhiwa, mchakatounaendelea ili waweze kupata mbia ili waweze kuendeshamgodi ule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekaa hapa Bungenimiaka saba, nimejifunza sana namna ya michango yaWabunge na namna ya kufanya ili Bunge liweze kuwa naufanisi. Ni lazima tujikite sana kwenye kanuni zetu. Kanuni ya94, inasema, Serikali italeta mpango na baadaye Wabungewatachangia na kuishauri Serikali. Lakini kwa kiasi kikubwa

[NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. G.B. SIMBACHAWENE)]

204

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

nimeshuhudia hapa zaidi sana ni kulaumiwa, kusemwa, sasahata hatupati ule mchango ambao tungesema tuuchukuekama Serikali ili tuweze kuboresha huu mpango ambaoumekuja ambao ni mapendekezo. (Makofi)

Nichukue nafasi hii kuwaomba WaheshimiwaWabunge kama wana mawazo mazuri bado fursa ipo naSerikali sisi tutaendelea kupokea, Wizara yangu ya Nishati naMadini tutaendelea kupokea mawazo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, dunia hii changamoto zipo,zilikuwepo enzi ya mitume wote, enzi ya Yesu Kristo nachangamoto zilikuwepo na matatizo hazikwisha akajaMuhammad, matatizo hayakwisha na mpaka tutamaliza sisimatatizo hayatakwisha. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Sasa unatuambia akina Muhammad,imekuwaje? Mheshimiwa Saada Salum, atafuatiwa na Eng.Lwenge.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA MKUYA SALUM):Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nashukuru kwa kupata fursahii ya kuweza kuchangia hoja ambayo tumeileta sisi kamaSerikali ya Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo mwaka2014/2015.

Aidha, katika mchango wangu vilevile nitajikita katikakutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali ambazo zimetolewa naWaheshimiwa Wabunge. Kimsingi hoja zote ni valid natutajaribu kwa uwezo wetu kuchukua mawazo mapyaambayo yametolewa na Waheshimiwa Wabunge kwa ajiliya kuboresha utendaji kazi wetu Serikalini na pamoja nautekelezaji wa ufanisi wa bajeti hii ya Serikali.

Kulikuwa kuna hoja ya utaratibu huu wa Cash budgetambayo tunatumia sasa hivi as against utaratibu wa Capital

[NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. G.B. SIMBACHAWENE)]

205

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Budget ambao tulikuwa tukitumia kabla, miaka ya nyumaya 1995/1996 na kuendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti pamoja na WaheshimiwaWabunge, tutakumbuka kwamba, katika miaka ya 1995/1996wakati Serikali inaendelea kufanya mageuzi ya kiuchumi naya kifedha, Utaratibu wa Capital budget ndiyo ambaoulikuwa ukitumika. Concept nzima ya utaratibu huu ambaoWaheshimiwa Wabunge wengi wamesisitiza kwamba, kwasababu ya matitizo yaliyopo kwenye cash budget, turudikwenye utaratibu wa capital budget.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tuchukue fursa hiikujikumbusha hali ilikuwaje wakati tulipokuwa tukitumiautaratibu wa capital budget. Kwa muda huo Bunge lilikuwalinaidhinisha mapendekezo ambayo yameletwa na Serikali,mapendekezo ya mipango pamoja na fedha zake. Bungelinaidhinisha matumizi ya taasisi za Serikali kutumia kama vileambavyo imependekezwa katika mpango yao, bila kutiliamaanani kiasi ambacho Serikali itaweza kukusanya kutokavyanzo vyake vya ndani na vyanzo vya nje. Kwa maana hiyotukiondoka hapa, muda huo ilikuwa ni kwamba, haya kilaTaasisi iende ikatumie according to vile ambavyo imepangana imeidhinishwa na Bunge.

Utaratibu huu il i ingiza Serikali katika madenimakubwa. Kwa nini? Kwa sababu, Wizara inapotoka hapabajeti inakuwa imeshaidhinishwa. Wakati huo kila Wizara inaaccount yake Benki. Kwa hiyo, kwa sababu ilikuwa Hazinaina-issue ile ex-chequer, kwa hiyo, kila Taasisi ilikuwa na uwezowa kutumia kutokana na kile ambacho kiliidhinishwa hapana Bunge, bila kujali ni kiasi gani kama Serikali tungeweza ku-collect. Muda huo Serikali iliingia katika madeni makubwa,kwa sababu Taasisi zinatumia bila kujali kile ambachokitapatikana, bila kujali miongozo ya bajeti, bila kujali kitukingine chochote. Taasisi zilikuwa zinatumia kutokana namahitaji yake, lakini hatuja-consider mahitaji ya nchi nzimaau uwezo wa nchi nzima kuweza kukusanya mapato ya ndanina ya nje. Kwa hiyo, utaratibu huu uliingiza Serikali katika denikubwa.

[NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. S. M. SALUM)]

206

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wengi wetu ambaotulikuwepo, at least sisi ambao tumesoma katika documentsmbalimbali, kuna ripoti mbalimbali zimetayarishwa, tulionakwamba Serikali iliingia sana kwenye madeni makubwawakati huo. Ndiyo maana ikasababisha Serikali hii ya Tanzaniakuingia katika ule mpango ule wa Highly Indebted PoorCountries (HIPC). Sababu mojawapo ilikuwa ni utaratibu wakutumia capital budget.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mageuzi hayoyaliendelea, Serikali kwanza tulikuwa katika StructuralAdjustment Program, tukaingia HIPC na mpaka sasa sasa hivituko katika utaratibu huu wa PSI kwa sababu tuna-guide ulemlolongo wetu wa matumizi ili uende na kile ambachokinapatikana. Nadhani hii ni logic.

Waheshimiwa Wabunge, naomba mtu-support katikahili, kwa sababu ni utaratibu ambao tumefanya kuiwezeshanchi sasa iweze kutumia kwa kile ambacho inakipata, kileambacho inaweza kukusanya na kile ambacho tunawezakukopa kutoka kwa washirika wa maendeleo.

Kwa hiyo, hiyo ilikuwa ni nia njema sana ya Serikali.Kwa hiyo, tunaomba Waheshimiwa Wabunge mtu-supportkatika hili. Tuna nia njema, tunataka mipango ya mendeleotuitekeleze, lakini kwa sababu tunakuwa constrain namapato.

Kwa hiyo, sasa hivi tunaelekea huko, na nawaombaWaheshimiwa Wabunge sasa tujitahidi kwa pamoja sotetuweze sasa tu-guide kujua mechanism nzima ya kuwezakutumia kutokana na kile ambacho kipo katika nchi na kileambacho tunaweza kukopa katika kutoka kwa mashirika yamaendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa kuna suala lingineambalo Wabunge walikuwa na wasiwasi sana kuhusiana naDeni la Taifa. Deni la Taifa limekua. Hii haina ubishi na kutokamwaka jana mpaka mwaka huu deni la Taifa limekua kwakiasi cha dollar billion 1.39. Kwa nini?

[NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. S. M. SALUM)]

207

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Kwa sababu tukikumbuka Waheshimiwa Wabunge nikwamba, deni la Taifa lina-constitute vilevile madeni ambayoyalichukuliwa miaka ya nyuma. Kwa hiyo, madeni ambayoyaliyochukuliwa miaka ya nyuma; miaka ya 1930, miaka 1940hususan concessional loans ndiyo zina-mature sasa hivi. Kwahiyo, ingawa tunalipa na ingawa tunaendelea kukopa, lakinitukumbuke vilevile tunalipa deni ambalo huko nyumalilichukuliwa kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo.Kwa hiyo, tusiwe na wasiwasi sana kwamba deni la Taifalinakua, halikui kwa sababu tunachukua cash na tunatumia,lakini lina-constitute vilevile mikopo ambayo ilichukuliwamiaka ya nyuma na sasa hivi ina-mature na ndiyo ambayotunaendelea kulipa pamoja na mikopo mingine ambayotunagharamia miradi ya maendeleo. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, kitu cha msingi hapa,tushirikiane kuhakikisha kwamba Serikali inachukua mikopokwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo. Wengi wetutumempongeza sana Dkt. Magufuli kutokana na kuonabarabara nyingi sasa hivi zinapitika, zimejengwa. Tujuekwamba barabara zile zimejengwa. It goes a long side withhata hiyo mikopo ambayo tunachukua. Tunachukua mikopo,tunaingiza kwenye miradi ya maendeleo ikiwemo barabaraambazo Waheshimiwa Wabunge tunashukuru kwambawengi wenu mmeipongeza Serikali katika hili, kwa hiyo tuonevilevile ni jinsi gani Serikali inakopa na inaingiza fedha zamkopo katika miradi ya maendeleo ikiwemo barabara.(Makofi)

Wengi wetu hapa tumelisimamia suala la reli, lakinitukumbuke kwamba Serikali itakapomaliza mchakato wakewa fedha, mchakato wa ku-mobilise hizo resources, tujue denila Taifa litakuwa, lakini kitu cha muhimu, tunaelekeza kwenyemiundombinu ya reli ambayo italeta tija. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa kuna eneo lingine,Waheshimiwa Wabunge wamepigia kelele kuhusiana na huuukomo ambao umewekwa na IMF na Benki ya Dunia.Tumeona kwamba hii labda ni kuinyima fursa Tanzaniakukopa mikopo mikubwa ya kibiashara ili kugharamia miradi

[NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. S. M. SALUM)]

208

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ya maendeleo. Hili nalo ni eneo lingine ambalo WaheshimiwaWabunge lazima tulizingatie. Tunapokopa lazima kunakuwakuna vigezo vya kukopa. Kwa sasa ukomo ambaotumewekewa katika kukopa vyanzo vyetu ni asilimia mojaya pato la Taifa. Kwa nini iwe ni asilimia moja ya pato la Taifa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Benki yoyote inawezaikamkosesha mwananchi wa kawaida lakini ikaikopeshaSerikali, kwa sababu ndiyo mkopeshaji ambaye tukiingiakwenye mikopo ile ya TB’s ndio yenye uhakika zaidi. Sasakama tutakopa zaidi ya kiwango cha asilimia moja, kutokanana measurements mbalimbali, tutaikosesha private sectorkuweza kukopa kwenye vyanzo vya ndani, maana banks niza kibishara. Maadam Serikali imetoa TB, kila mtu anakwendaku-invest kwenye TB. Mwananchi wa kawaida, vikoba,wakulima, watakuwa hawana nafasi ya kukopa katikaMabenki kwa sababu pesa yote sasa imekuwa investedkwenye TB zao.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. SAADA MKUYA SALUM):Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Naibu Waziri wa Ujenzi,Mheshimiwa Lwenge.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti,awali ya yote nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ya miminiweze kuchangia mapendekezo ya mpango wa maendeleowa mwaka 2014/2015. Kwanza, kabisa nampongezaMheshimiwa Wasira kwa kuleta Mpango mzuri ambaonaamini kabisa unatekeleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza WaheshimiwaWabunge wasiwe na wasiwsi kusema tunapanga vitu vingi.Siku zote lazima u-think big. Ukitaka kufanikiwa, uwe na

[NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. S. M. SALUM)]

209

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

malengo makubwa. Huwezi kuanza na malengo madogohalafu utegemee kufanikiwa.

Waheshimiwa Wabunge, sasa kwa sekta yamiundombinu, ukipitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi, kuanziaukurasa wa 72 mpaka 78, zimeandikwa barabara nyingi sanahapa. Sasa hapa huwezi kuiacha barabara kwa sababutumewaahidi wananchi kwamba barabara hizi zotetutazitengeneza. Ndiyo maana tumetengeneza utaratibu;kwanza tumeanzisha huo Mfuko wa Barabara ili tuwezeshebarabara nyingi zilizoko Mikoani. Barabara kilometa 33,000ni barabara kuu na barabara za Mkoa ziweze kutengenezwakwa ajili ya fedha ambazo una uhakika kwamba zipo nawengi mnasema barabara za TANROAD ni nzuri, ni kwasababu tunao Mfuko unaotengeneza barabara hizo. (Makofi)

Sasa tukianzia kwenye Ilani, ni kwamba toka mwaka2005, Rais wetu Mheshimiwa Jakaya Kikwete alipoingiamadarakani alianza na hii Big Results ambayo inazungumzwaleo, akaamua kuzishambulia za nchi hii, ili kuunganisha mikoayote. Lengo lilikuwa Mikoa yote iunganishwe kwa barabaraza lami. Kwa hiyo, ndiyo maana kilometa zinazojengwa sasahivi ni nyingi sana, karibu kilometa 11,891, hazijapata kutokeakwamba zinajengwa kwa wakati mmoja. Sasa katika hizibarabara tumeziweka katika maeneo makuu matatu.Kwanza, tunazikarabati barabara zile ambazo zimeshapitamuda wake. Kwa sababu barabara huwa zinasanifiwa kwamiaka 20. Sasa barabara ikitumika zaidi ya miaka 20 kwavyovyote vile, na il i upate economic rate of returninayotakiwa, lazima uifanyie ukarabati.

Kwa hiyo, kwanza Ilani imetuagiza tuzifanyie ukarabatibarabara zile; pili, tuzitengeneze barabra nyingine mpya; natatu, tuzifanyie upembuzi yakinifu. Kwa hiyo, kuna makundihaya matatu makubwa. Sasa tulivyoanzisha mwaka huu wafedha uliokwisha 2013; huu mpango wa matokeo makubwasasa, tumeweka miradi 25 inayohusiana na barabara.Kwanza, tunataka tushughulikie miradi inayoondoamsongamano wa Bandari ya Dar es Salaam ili kufunguauchumi wa nchi. (Makofi)

[NAIBU WAZIRI WA UJENZI]

210

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Kwa hiyo, miradi yote inayoanzia Dar es SalaamBandarini mpaka kuunganisha na nchi jirani, ukianzia nacentral corridor, ndiyo tumeweka kipaumbele. Kwa sasa hivitunataka tupanue barabara, kwa mfano kuanzia bandarinipale mpaka Tazara, badala ya kuwa njia mbili ziwe njia tatu.Kwa hiyo, tunasema ni njia sita. Halafu kutoka pale TAZARAmpaka Air port, pia tunapanua zinakuwa tatu tatu kilaupande.

Kutoka pale airport kwenda mpaka Pugu, tunapanuakuwa njia sita vilevile. Ukitoka Pugu unaunganisha naMorogoro Road, nayo tunakwenda na njia sita; halafu ukitokapale Mbezi unaunganisha na Bunju hii njia ya Kawe kwendaBagamoyo nayo tunapanua kwa njia sita. (Makofi)

Kwa hiyo, unakuta kwamba, barabara hii pamoja naku-congest Bandari ya Dar es Salaam, lakini pia utapunguzamsongamano wa Dar es Salaam, kwa maana ya kwambamagari mengine yataweza kwenda Airport, hayana haja yakupita katikati ya Mji. Hilo la msongamano wa Jiji la Dar esSalaam Waheshimiwa Wabunge wamelisema kwa nguvusana, tunaafiki ni kweli msongamano upo lakini Serikaliimeshaanza kuchukua hatua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna hii miradi ambayoinaendelea, mradi wa mabasi yanaoyoenda kwa kasi, nimojawapo katika miradi ambayo tutapunguzamsongamano. Lakini pia Japan wamekubali kujenga fly overpale TAZARA, Japan pia wamekubali kujenga fly overnyingine ya Ubungo. Tunaendelea na mipango ya kujengafly over ya pale Magomeni, Morocco na pia Wachinawamekubali kufadhili ili kupanua Surrender Bridge. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naamini kabisakwa maana ya msongamano wa Dar es Salaam, hatua zipona tumeweka kwenye big results, naamini kabisa tunahitajirasilimali fedha kama Shilingi bilioni 531, kuweza kutekelezamiradi ya Big Results. Tunapozungumza habari za fursa zakuichumi, kuna wengine wamezungumza kwambatungefanya barabara chache, lakini naamini kabisa

[NAIBU WAZIRI WA UJENZI]

211

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

tumetengeneza nchi hii katika Kanda tisa kuunganisha.Maana barabara huwezi ukatengeneza kipande kimojahalafu ukaacha kipande kingine. Tunazungumza maisha borakwa kila Mtanzania, maana yake kila mmoja apate fursa zakiuchumi na kijamii. (Makofi)

Kwa hiyo, kuna barabara nyingine inawezekanahawalimi, lakini wanafuga, au pengine kuna hospitali kubwa.Kwa hiyo, kila mahali unakuta barabara ni muhimu ijengwe.Ndiyo, maana unakuta tumeshika nchi nzima. Kama kunaeneo ambalo unadhani kuna Watanzania wengimmepongeza ni katika Sekta ya Barabara kwambatunafanya vizuri.

Naomba mtuunge mkono ili tuweze kuendelea namipango hii iliyopo. Tunataka tuunganishe Mikoa yote yaTanzania kwa barabara za lami za uhakika na hivyo kaziinaendelea kwa kasi kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna barabarazinazounganisha nchi jirani. Hizo pia ziko kwenye mpangokatika hizi kilomita 11,174 zinazoendelea, na tumeziwekakwenye mpango na zinashughulikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nijibu baadhi ya hojaambazo Waheshimiwa Wabunge wamekuwa wakichangia.Nianze na suala la msongamano wa Dar es Salaamnimeshalielezea. Lakini niseme habar ya barabara ya ndunguSomanga naona Waheshimiwa wawili, watatuwamezungumza kwa uchungu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli barabara yaNdundu – Somanga, mkandarasi huyu amesuasua lakinikimkataba, tulimpa mpaka Desemba, 2013 kumaliza. Mpakasasa kilometa 40 za rami ameshamaliza kati ya kilometa 60.Yaani ukichukua over roll progress ya Mkandarasi yule,amefikia asilimia 90% ya Mkataba ule. Naamini kabisa kazihii itakwisha. Kwa sababu asipomaliza, ikifika Desemba

[NAIBU WAZIRI WA UJENZI]

212

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

tutaanza kumkata liquidated damages. Maana tunatozatozo kwa ucheleweshaji wa kazi hiyo.

Eneo lingine ambalo Mheshimiwa Mbunge mmojaamezungumzia ni suala la kupunguza Mfuko wa Barabarakuchangia huduma za reli. Naomba niwarejeshe kwamba,sheria inasema kwamba, fedha ambazo zinatengwa kwa ajiliya Mfuko wa Barabara zinakuwa ni kwa ajili ya Mfuko waBarabara, hakuna vinginevyo.

Naomba sana kama kuna mawazo mapya ya kutakafedha hizo ziingie kwenye mfuko mwingine, basi ni suala lakubadilisha sheria hii.

Waheshimiwa wengine wamezungumzia habari zabarabara za Mikoa. Mimi niwahakikishie kwamba, kwasababu tuna fedha za Mfuko wa Barabara, kazi yake kubwani kufanya matengenezo. Asilimia 90% ya fedha za Mfuko waBarabara ni kufanya matengenezo, asilimia kumi ni miradiya maendeleo.

Kwa hiyo, pamoja na hizi kilometa 11,000tulizozungumza kuna baadhi ya maeneo katika Mikoatunajenga barabara za lami kwa kutumia fedha za Mfukowa Barabara, ile asilimia kumi ambayo imeruhusiwa kisheria,lakini kwa sehemu kubwa tunataka fedha hizi zifanye kazi yamatengenezo. Kuna baadhi ya Wilaya bahati nzuri nisemehapa kwamba, fedha za Mfuko wa Barabara wamezitumiakwa kazi ambayo siyo ya barabara.

Sasa kwa mfano umeweka fedha barabara halafuunakuta mtu anazitumia fedha zile kwa kuendea seminaambayo haihusiani na barabara, hiyo kitu hairuhusiwi.

Kwa hiyo, hiyo naomba tukubaliane kwamba fedhaza mfuko zitumike kwa ajili ya barabara ili wananchi wotewaweze kufaidika kwa maendeleo ya kazi ambayoinaendelea. (Makofi)

[NAIBU WAZIRI WA UJENZI]

213

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja hii yaMpango wa Maendeleo. Naomba sana tufikirie kikubwa ilinchi yetu iweze kwenda haraka katika kunusuru maendeleoya nchi hii. Ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante. Sasa namwita Naibu Waziriwa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mheshimiwa Adam Malima.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA:Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimshukuru MwenyeziMungu na nikushukuru wewe kwa kuniruhusu kuchangia hojahii kwa niaba ya Waziri wa Kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitambue nafasi yapekee na michango ya Waheshimiwa Wabunge ambayomingi sana imejikita kwenye suala la kilimo hasa kwakutambua nafasi ya pekee ya kilimo na wadau wake katikamaendeleo na mustakabali wa Taifa hili kwa leo na kwa hukombele tunakokwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuzielezea hoja hizi vizuri,natarajia kwamba Mheshimiwa Waziri wa Nchi atazifafanuabaadaye zaidi. Naomba tu kusema kwamba, kila maratunapozungumza, tunasema Tanzania is an agricultural basedcountry; na zipo nchi za namna tatu; kuna agricultural based,kuna transforming countries na kuna organized. Sisi Tanzaniais an agricultural based. Sasa sisi tukisema as an agriculturalbased country, we have 70% of our population, yaani asilimiasabini na zaidi ya Watanzania ambao wanategemea mojakwa moja uchumi wao kwenye Sekta ya Kilimo.

Sasa kwa upande wa Tanzania kimahesabu, kwawatu milioni 45 walioko leo, tunachosema ni kwamba watumilioni 32, wanategemea uhai wao kutokana na uchumi huuwa kilimo. Kwa maana hiyo, ifikapo mwaka 2025, tukisematutakuwa na Watanzania milioni 60, Watanzania milioni 42watakuwa wanategemea Sekta ya Kilimo moja kwa moja.Maana yake nini?

[NAIBU WAZIRI WA UJENZI]

214

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Maana yake ni kwamba, kwa wale milioni 42wanaozalisha kwa ajili ya milioni 60 wote, ni lazima maandaliziyao yaanze kufanyika leo. Maandalizi ya kwenda huko mbeleya kuhakikisha kwamba nchi yetu hii, is self sustaining countrykwa maana ya chakula, yanaanza kwa mipango kama hiiambayo Serikali na Tume ya mipango wameileta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme jambomoja; katika michango ya Wabunge, mimi najua kabisa,nimeiangalia i le hotuba ya Mpango wenyewe, uleMwongozo wa Mpango ukurasa 51 unatoa vipaumbele,unatoa na changamoto zilizokuwepo.

Nilichoelewa mimi, ni kwamba WaheshimiwaWabunge walikuwa wanasema, pamoja na maelezo yaleyaliyokuwemo kwenye vitabu, lakini maelezo yale yalikuwayanaonekana kama business as usual; kama maelezoambayo wamesoma kwenye mipango ya mwaka jana namwaka juzi na mwaka majuzi.

Waheshimiwa Wabunge, walikuwa wanatakamaelezo ya kina zaidi ili utekelezaji wa mipango hii uendeukanufaishe wakulima na Watanzania moja kwa moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme tu kwambanimeilewa ile tafisiri, kwa sababu kwenye uchumi mwaka1992, Norman Lamonta Chancellor of Shark wa Uingereza,aliambiwa pamoja na kwamba, uchumi wetu unakua,hatuoni Waingereza.

Sasa Eddie George akiwa Gavana wa Bank ofEngland, wakabaini usemi unasema: “a feel good factor.”Kwa hiyo, Watanzania pamoja na kwamba wanatudaikwamba uchumi wetu unakua, sasa wanataka kuiona ile feelgood factor. (Makofi)

[NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA]

215

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Kama asilimia 70 ya Watanzania wako kwenye kilimo, lazimamipango yetu hii ijielekeze kwenye kutafuta ufumbuzi wanamna ya kuwapa Watanzania hawa feel good factor yakuona kwamba maendeleo haya na wao kule chiniyanawafikia. Kwa hiyo, hayo tunayapokea kutoka kwaWaheshimiwa Wabunge na tumekaa na wenzetu wa upandewa Tume ya Mipango na Wizara ya Fedha, Jumamosi na janaJumapili, tumekubaliana kwamba mipango hii pamoja nautekelezaji wake izingatie haya kwa sababu ndiyo Wabungewamedai kwa niaba ya Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalolazima tuliweke mbele katika kutathmini kilimo cha Tanzania,ni kwamba kilimo cha Tanzania ni small holder farmingambayo kwa kiasi kikubwa, mkulima wa Tanzania nimwanamke. Mwanamke ndiyo mhimili wa kilimo chaTanzania na kwa maana hiyo mwanamke ndiyo mhimili wauchumi wa Tanzania, it is the fact. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo ambalotumelizungumza na tumekubaliana kwamba ni lazimatwende tukatengeneze mikakati ya makusudi kwamba ilemikakati ya msingi, ambayo inabadilisha kilimo, kwa maanaya transforming agriculture, access to finance (uwezeshaji),lazima iwe na nafasi maalum ya kuzingatia mchango wamwanamke na vijana ili huko mbele tutakakokwenda tusiwekama tunakwenda kama vipofu tu tunaongozwa, hilo jambomoja. Kwa maana hiyo, tunakamilisha kwa mwaka huu sualala Benki ya Kilimo na pawe na window maalum kwa ajili yavikundi vya akina mama na vya vijana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni miundombinu,hatuwezi kutoka hapa tulipokuwa bila ya kuwa namiundombinu maalum ya kilimo na kwa Serikali hii, jamanitukubaliane wanaosema, wanaobeza kama hamtakikuona, ndiyo hivyo tutafanyaje, lakini kuna suala la RuralRoads, Rural Energy, Rural Water, miradi ya irrigationinatusumbua kwa sababu kwa kiasi kikubwa miradi yaumwagiliaji imekuwa haipati usimamizi mzuri. TumepitishaSheria Bunge lililopita na ninyi wenyewe Wabunge mmeridhia,

[NAIBUWAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA]

216

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

tunapitisha mradi wa umwagiliaji wa shilingi bilioni moja,halafu bado haufanyi kazi, lazima mtu awajibike kwa sababuzile ni fedha za umma. Sasa kwa utaratibu huu,tunakubaliana kwamba mpango huu unaweka mikakatiambayo inapewa nguvu ya kisheria ya kuhakikisha kwambamikakati yetu ya kilimo inapata utekelezaji mzuri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala lingine ambalolimezungumzwa, nalo ni suala la masoko ya mazao.Wakulima wamezungumza kwa uchungu kwamba saanyingine tunapitisha mikakati, wakulima wanahamasika,wanalima, wanazalisha zaidi lakini mazao yanakuwahayapati soko. Haya yanaendana na yale mawili, kwa maanaya uwezeshaji, ambao siyo suala la uwezeshaji tu kwawakulima wakubwa lakini pia, mpango huu unataka kujikitaili hii sekta ya fedha iwe na uwezo wa kuwafikia wakulimawa kati. Hata hivyo, suala la masoko, lina Wizara mbili sasa,lina Wizara ya Viwanda na Biashara na sisi Kilimo, Chakulana Ushirika, tumekubaliana kwamba tulitengenezee mkakatimaalum ili masoko ya mazao ya kilimo isiwe ni tatizo tenakwa wakulima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambaloWaheshimiwa Wabunge wamelizungumzia na tumelisikia, nisuala la kuhakikisha kwamba wakulima wanahamasikakweli. Kwa mfano, kama sasa hivi tunajua tuna tatizo kubwala ushirika, ambapo kwenye maeneo mengi ushirikaumechangia kudumaza hamasa ya kilimo kuzalisha zaidi kwamaana ya surplus. Mtu anazalisha kile kinachomwezesha yeyetu kula na familia yake, hazalishi zaidi, kwa sababu hanamotisha, anazalisha na ushirika unamuumiza. TumepitishaSheria ya Ushirika hapa na sasa tumekubaliana kabisakwamba katika misingi hii, ushirika hautatumika tena kamachaka la watu kuhujumu wakulima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, katika yale yajumla ambayo nilitaka kuyasema ni access to technology.Hakuna mabadiliko ya kilimo yasiyozingatia mchango wasayansi kwenye kilimo. Tumefika hatua, tuna watu kwamakusudi wanahamasisha watu kutumia mbegu mbovu,

[NAIBUWAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA]

217

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

dawa za ajabuajabu, kwa sababu wao wana misingi yabiashara mle ndani. Tuna watu ambao kwa sasa hivi kwamfano kwa zao la korosho, kama dunia nzima wanatumiasulphur ya maji, dawa ya maji ya kupulizia, sisi badotunatumia sulphur ya unga. Dunia nzima wanatumia pambahybrid, sisi bado mpaka leo tunataka tutumie mbegu zile zapamba za kienyeji na watu wanataka kuandamanaKahama, Shinyanga kwa sababu ya kutumia mbegu hizowakati mbegu hizo ziliachwa kutumiwa huko duniani miakazaidi ya 40 niliyopita. Haya ni mambo ambayo lazimatukubaliane ndugu zangu, kwamba sisi kama ni nchi ambayoni agricultural based na uchumi wetu unaegemea hapo,lazima tutengeneze utaratibu wa kuhakikisha kwambasayansi inakuwa ni msingi wa maendeleo ya kilimo na hakunamaendeleo ya kilimo bila utafiti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tulichosema, nikwamba kwa kiasi kikubwa kwenye mpango huu, utatengakiasi cha fedha maalum kabisa ambazo zitakwenda kwaajili ya utafiti na ugani, kwa maana ya kuwapatia wakulimawa Tanzania elimu ya kilimo cha kisasa. Hatuwezi kuendelea,hata kama mtu unalima na jembe la mkono, lakini badokuna vitu vya msingi ambavyo vinakuwezesha kutoka kwenyegunia nne kwa eka moja ya mahindi, kwenda kwenye gunia20, wakati wenzetu duniani wanalima mpaka gunia 40.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, haya ndiyomambo tunataka tupeleke na mpango huu kwa kiasikikubwa unaunga mkono haya na Waheshimiwa Wabungemmesisitiza kwamba pawe na mabadiliko makubwa katikakilimo cha Tanzania. Naomba niseme tu kwamba pia katikaSerikali ni mkakati wa kuondokana na huu ukuaji wa asilimia4.3 kila mwaka, twende kwenye wastani wa ukuaji waasilimia sita katika sekta ya kilimo. Tukifika hapo, tunamatarajio kwamba wakulima walio wengi, wale asilimia 70,watafikiwa na maendeleo haya kwa maana ya ile feel goodfactor ambayo tunaitarajia, kila mtu aone kwambatunavyokwenda uchumi unakua lakini na sisi wote kwapamoja tunakua.

[NAIBUWAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA]

218

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yako mambo ambayolazima tufanye na ninaomba niwasihi WaheshimiwaWabunge, kwenye mpango huu utakaokuja, kuna mambokwenye kilimo lazima yatabadilika, kwa mfano, suala lapembejeo, mwaka huu tumeweka shilingi bilioni 120 lakinitumefikia kaya laki laki nane, lakini fikra ni kufikia kaya milionimbili. Ili tufikie kaya milioni mbili, lazima tuweke zaidi ya shilingibilioni 200, lakini tukiweka shilingi bilioni 200 kwenyepembejeo, maana yake lazima tutoe shilingi bilioni 100kwenye kitu kingine, that is the art of budgeting. Kwa hiyo,naomba niwasihi tu Waheshimiwa Wabunge kwambatumesikia vipaumbele vyao lakini tutakapofika mwezi wapili na hiyo rasimu itakapokuja, tutambue kwamba kupangani kuchagua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Profesa Anna Tibaijuka,dakika ni 10.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YAMAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanzakabisa, naomba nimpongeze mtoa hoja kwa mpango mzuriambao tumeuona hapa mbele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa sekta yaardhi, nichangie tu kwa kusema kwamba na sisi tumejipanga,hasa kuziwezesha zile sekta ambazo zina kipaumbele katikakutekeleza mpango huu ambao uko mbele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika sekta ya ardhiambayo ni sekta mtambuka, ni wazi kwamba watekelezajiwengi, sekta mbalimbali inakuwa vigumu kwenda mbelebila sisi kuwa tumeshawawezesha kufanya hivyo. Kwa hiyo,tulivyojipanga sisi, tunaangalia ardhi kwa misingi mitatu.Kwanza, kuna ardhi za vijiji, ambazo pia hujumuisha ardhiza hifadhi. Tatizo kubwa ambalo tutalishughulikia katikamwaka huu, ni kujaribu kuondokana na migogoro ya ardhi.Wachangiaji wengi hapa wamegusia, kwa sababukunakuwepo na mgongano, pressure ya matumizi ya ardhi

[NAIBUWAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA]

219

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kati ya wakulima na wafugaji, kati ya hifadhi na wakulimana kati ya watumiaji mbalimbali wa ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu tumejaliwa ardhikubwa, lakini pia kama wote tunavyotambua, MwenyeziMungu pia ametujalia sisi wenyewe tunaendelea kuongezeka.Kwa hiyo, kila mwaka tutakuwa tunaona kwamba kunapressure ya ardhi, eneo linakuwa dogo, sisi tunaongezeka,lakini ardhi haiongezeki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika sekta ya kilimo kamaalivyomaliza kuchangia Mheshimiwa Malima hapa,tunahimiza sana utumiaji wa kisasa wa ardhi. Sisi kamawapangaji wa ardhi, tunatambua matumizi bora ya ardhi,lakini tunapopanga matumizi bora ya ardhi, hapohapotunahimiza uhifadhi wa ardhi, lakini pia teknolojia namapinduzi ya kilimo na ufugaji. Hasahasa, nikijikita kwenyesekta ya ufugaji, jambo ambalo tumelizungumza sana katikaBunge hili ni kwamba ufugaji wa sasa hivi, kwa sisi kamawapangaji wa matumizi ya ardhi, tunahimiza ufugaji wakisasa. Ufugaji wa kuhamahama, unaanza kupitwa nawakati. Ni jambo gumu sana lakini bila kulitambua hili,itakuwa vigumu kuondokana na migogoro ya ardhi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naposema umepitwa nawakati sina maana kwamba tuache kufuga, lakini ninamaana kwamba tuache kuhama na mifugo. Sasa hivi,asilimia 70 ya kitoweo tunakipata kwenye mifugo ambayohaihami. Asilimia 70 ya nyama inayouzwa Tanzania haitokanina wafugaji wanaohamahama au pastoralists, inatokamana mixed farmers yaani wale wakulima mseto, wanakuwana mifugo, wanakuwa na mazao, hao ndiyotunawategemea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunafanya kazikwa karibu sana kama sekta mtambuka na wenzetu katikaWizara ya Mifugo, kuboresha nyasi. Ili ufuge bila kuhama,lazima ufanye mambo matatu. Lazima uwe na maji yakutosha pale ulipo, ni lazima uzuie magonjwa ya mifugo napia lazima uwe malisho yaliyoboreshwa. Sasa ukishafanya

[WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI]

220

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

mambo hayo matatu, huna tena haja ya kufugafuga, utakutaheka moja ya malisho inaweza sasa kubeba ng’ombe wengizaidi, inaitwa carrying capacity. Katika jambo hili tunajikitahasa kwa kutoa elimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine ambachotumejikita nacho sasa ni tension au tuseme migogoro katiya Miji inayokua, matumizi ya makazi na ya wakulima.Sehemu nyingi za Miji inakua kwa kasi, Mji kama wa Dar esSalaam unakua kwa kasi na sasa hivi ndiyo tuna mpangowetu Kabambe wa Mji Mpya wa Kigamboni. Mji Mpya waKigamboni tumeupa kipaumbele kabisa na tunapiga hatuanzuri. Katika Mji Mpya wa Kigamboni tunatarajia kwambatutaweza kuongeza wakazi wa Kigamboni kutoka takribani100,000 tulio nao sasa hivi tunatarajia kufikisha watu kamalaki nane au milioni moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kusudi uweze kuwa naMji wa watu milioni moja, ni lazima upange Makazi vizuri,lakini upangaji Miji siyo Kigamboni tu, ni Tanzania nzima. Kwahiyo, Wizara inaweka kipaumbele kwa Dar es Salaam MasterPlan. Tunataka Miji yote mikubwa iwe na master plan. Sasahivi tumejitahidi, Halmashauri zimejitahidi kupima viwanjalakini maelekezo tuliyotoa ni kwamba ukipima viwanja bilakuwa na master plan, unakosea maana yake unawezaukafanya makosa ukajikuta kwamba bomoabomoahaitaisha. Kwa hiyo, suala la kupanga makazi linakuwajambo muhimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wachangiaji wengiwamezungumzia mambo specific, hapa yamesemwa katikaBunge kwa mfano, mchangiaji kutoka Tanga, kuna suala lamashamba ya Mkoa wa Tanga, ambayo kusema kweli katikaMikoa yote ya Tanzania yenye mashamba makubwa Tangainaongoza na wananchi wa Tanga wala siyo siri, wengi waowanahitaji ardhi hizi zirejeshwe kwao kusudi wawezekuzitumia. Mchakato wa kurejesha ardhi hizi unaendelea,tulipofikia tunahitaji habari zaidi kutoka kwa Halmshauri naWilaya mbalimbali za Tanga ili tuweze kwenda mbele. Kuna

[WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI]

221

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

mashamba mawili ambayo sasa hivi tumeshafikisha kwaMheshimiwa Rais, tunasubiri uhaulishaji. Kwa mfano, Shambala New Korogwe na Kibaranga Farm, hili liko Muheza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu nyingine nyingiambapo tumekuta pia migogoro kati ya wakulima na hifadhi,nadhani mnaona na sisi tunafanya kazi pamoja na wenzetuwa Maliasili kuhakikisha kwamba hifadhi itakuwa yabinadamu lakini pia hifadhi ya wanyama. Kwa hiyo, katikamatumizi ya ardhi sisi tunatafuta balance kwamba kila kituni cha lazima, lakini lazima zaidi wananchi wawe na ardhiya kutumia. Sasa wananchi hawawezi kuwa na ardhi yakutumia kama wenyewe pia hawaendi mbele, hawaendina teknolojia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika sekta yetu ingawajesisi siyo core sector katika Big Results Now, lakini sasa hivitumekaribishwa na Mheshimiwa Rais kuingia katika Barazala utekelezaji la Big Results Now. Hii ni kutokana na kutambuakwamba bila matumizi ya ardhi kupangwa, bila mipangoya ardhi kuwepo, itakuwa vigumu kwenda kwa kasi ambayotunaihitaji. Katika hili, niseme kwamba sasa hivi tunajaribukufanya kazi na sekta nyingine hasa za miundombinu nauchukuzi tuwe tunapanga kwa pamoja. Kwa sababutusipopanga kwa pamoja, wakati mwingine unawezakujikuta uko kwenye juhudi bila maarifa. Kwa mfano, katikasekta ya usafirishaji, kuhakikisha kwamba tunapopangabarabara, zitakidhi viwango? Nimefurahi sana kusikiawachangiaji wengi leo mkizungumzia sekta ya reli. Sisitunatambua kwamba pia sekta ya reli itatusaidia, kwasababu barabara zinachukua sehemu kubwa ya ardhi. Kunasehemu nyingine ambapo ukifika, unakuta ni milima nakadhalika inaweza kuwa vigumu kupitisha barabara kubwazinazotosha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kwambaWizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, suala lanyumba hatujalisahu. Shirika letu la Nyumba linaendelea lakinimimi hapa ni Waziri wa Nyumba, siyo Waziri wa NationalHousing. Kwa hiyo, tunahimiza sana Halmashauri sasa hivi

[WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI]

222

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kupanua mawazo na kwenda mbele ya National Housingkwamba Halmashauri zetu zihimizwe kuwa na CouncilHousing. Huwezi kutatua, huwezi kuwa na makazi bora kamaunategemea Shirika moja. Kwa hiyo, katika sekta ya ardhiutaona kwamba mwaka huu tutakuwa tunaboresha nyumbazetu za tembe, hizi za kienyeji, tuwe na nyumba bora na hizihazitaweza kujengwa na Shirika la Nyumba ambalolinaendelea kufanya kazi nzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa, suala la fidia.Wizara ya Ardhi imejikita katika kuleta fidia endelevu. Sisihatutaki fidia ambayo …

(Hapa kengele ililia kuashiria kwishakwa muda wa mzungumzaji)

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YAMAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkonohoja. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Sasa tumwite Mheshimiwa Dkt.Mwakyembe.

WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti,ahsante. Kwanza, naunga mkono hoja na vilevile nianze kwakumpa pole mdogo wangu mpendwa Mheshimiwa JosephMbilinyi, Mbunge wa Mbeya Mjini. Amedai ambulance kwamiaka mitatu bila mafanikio, hata mimi kaka yake Mbungewa Kyela nilidai ambulance kwa miaka kama mitatu bilamafanikio lakini nikagundua Serikali ina mambo mengi yakuhudumia, nikajinyima kidogo, nimenunua Noah ,nimeikabidhi Hospitali ya Wilaya ya Kyela. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huo ni ushauri wa bure tu.Ubunge si kufoka tu, kulalama na kulaumu, tenda. Hataukinunua Bajaji mbili, nina uhakika kabisa wana Mbeya Mjiniwatathamini mchango huo kuliko ngonjera za kulalama.(Makofi)

MBUNGE FULANI: Safii!

[WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI]

223

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Anna Abdallah,anataka kujua kwa nini ujenzi wa Kiwanja cha Ndege chaMtwara haujitokezi katika mpango huu. Naomba tuniwahakikishie Waheshimiwa Wabunge kwamba kutokanana shughuli ambazo zinafanyika Kusini mwa Tanzania,Kiwanja cha Ndege cha Mtwara, tutakijenga na kitakuwaKiwanja cha Kimataifa chenye ukubwa sawa na Kiwanja chaJulius Nyerere na ujenzi kama mambo yote yataenda vizuriutaanza mwaka ujao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari tuna Kampuni kubwaya Kichina inaitwa AVIC International ikishirikiana na Kampuniya Shapriya ya Tanzania, wameshafanya feasibility study kwafedha yao wenyewe na vilevile preliminary design. Vyanzovya fedha ya ujenzi vimeainishwa, kuna Mashirika makubwamawili ya Bima tayari yamejitokeza kudhamini mkopo huo,SINO SURE ya China na ATI ya Afrika. Kazi ya kitalaaminayoendelea sasa hivi ni kuhakikisha kuwa fedha ya mkopokwa mradi huo inaendana na mahitaji yetu na vipaumbelevyetu na vilevile ina masharti nafuu yanayobebeka.

Mheshimiwa Sylvester Mabumba, anaishauri Serikalikukipanua Kiwanja cha Ndege cha Kigoma ili kihudumie nanchi za jirani. Kiwanja cha Ndege cha Kigoma, pengine kwafaida ya Waheshimiwa Wabunge, ni miongoni mwa viwanjasaba, ambavyo tulishavifanyia upembuzi yakinifu na usanifuwa kina kutokana na fedha ambayo tulikopa kidogo Benkiya Dunia kama dola laki nane na dola laki nne tukatoa sisiwenyewe. Ni Kiwanja ambacho kipo pamoja na viwanjavingine vya Arusha, Bukoba, Shinyanga, Sumbawanga,Tabora, ambavyo viko katika ngazi mbalimbali yautekelezaji, lakini Kiwanja cha Mafia ambacho kipo kwenyekundi hilihili vilevile, chenyewe tumeshamaliza kimeanzakupokea ndege. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulishaanza ujenzi waKiwanja cha Ndege cha Kigoma, ambacho runway yakeingekuwa mita 1800, kwa kuweza kupokea ndege ndogo zakatikati, lakini kutokana na hoja hizo za WaheshimiwaWabunge na ukweli kwamba Kigoma imekaa mahali

224

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ambapo inaweza kuwa kiungo muhimu katika usafiri waanga ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Serikali ikaamuakurefusha runway ya Kigoma kwa mita zaidi ya 1300, ilikiwanja hicho sasa kiwe na barabara ya kurukia na kutuandege yenye urefu wa mita 3,100 kuwezesha ndege kubwaaina ya Boeing, Embraer, Airbus yenye kubeba abiria zaidi ya150 kutua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mapema mwaka huu Benkiya Dunia ilikubali kutupa pesa Dola Milioni tisa ili tuwezekurefusha hicho kiwanja kwa hiyo mita 1300 na wakatupamasharti ya kwamba ifikapo mwezi Machi, tuwetumeishawalipa wananchi wa Kigoma fidia ya shilingi bilionimoja 1.5. Tukajitahidi, tumelipa hiyo pesa na Benki ya Duniaikatuma ujumbe wake Kigoma kwenda kuhakikisha kamafidia ili l ipwa. Tuliwapokea kwa shangwe nyingi lakinipakatokea maandamano mafupi pale yakiongozwa nakijana mmoja anayeitwa kwa jina la Bukumbura, wakidaiwamepunjwa. Vijana wenyewe tulikuja kugundua hawanahata viwanja pale, kwa kutegemea tu kwamba Benki yaDunia ni Benki ya Dunia inaweza ikawa na pesa za ziada.Benki ya Dunia ime-withdraw pesa yake kwenye mradi huo,kwa hiyo, Kiwanja cha Ndege cha Kigoma, kitabakia mita1,800 kutokana na hayo maandamano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue fursa hiikumpongeza sana Mkuu wa Mkoa wa Kigoma – KanaliMstaafu Machibya. Yeye ilimuuma sana, nani ametushikashati huyo, akamtafuta huyo kijana lakini baadaye akaamuakumpekua, akagundua huyo kijana anatumia majinamatatu. Yeye ni Bukumbura a.k.a. Erick Fundi Rugeze, a.k.aEric Nyandwi na kwamba kiongozi huyo wa maandamanoya siku hiyo siyo raia wa Tanzania ila raia wa Burundi.Tumempeleka Mahakamani, siwezi kuendelea zaidi ya hapolakini runway ya Kigoma itabakia mita 1,800, tutakapopatapesa baadaye tutaongezea. (Makofi)

Mchungaji Peter Msingwa na Mheshimiwa Rita Kabati,wanataka ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Nduli,kilichopo Iringa, uonekane kwenye Mpango. Mbona suala

[WAZIRI WA UCHUKUZI]

225

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

hili tumeshalieleza mara nyingi sana hapa Bungeni kwambatumeshapata fedha kutoka Benki ya Dunia na sasa hivitumeshapata approval, tumeshaanza tayari upembuziyakinifu katika viwanja 10 vilivyopo nchini ambavyo tutaanzandani ya mwaka huu wa fedha na immediately there aftertuanze ujenzi wa viwanja hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanja hivyo mbali nakiwanja cha Nduli cha Iringa, tuna Kiwanja cha Musoma,sijui kama Mheshimiwa Dkt. Kebwe, yupo, unasikia hapo?Tuna Lake Manyara, tuna Moshi, tuna Tanga, MheshimiwaStephen Ngonyani unasikia hilo? Tuna Lindi, tuna KilwaMasoko, tuna Songea, tuna Njombe na Singida. Kwa sababuza kimsingi kabisa, tumeingiza vilevile kiwanja cha ndege yaSimiyu kwenye mchakato huu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa DeogratiusNtukamazina, anataka Shirika la Ndege la ATCL ianze sasakuruka na ameenda mbali kwa kusema nchi ndogo kamaRwanda inawezaje kuwa na ndege nyingi na sisi hatuna?Nataka kusema kwamba kupanga ni kuchagua, sisi na jiranizetu hao unaowataja wote tulipata pesa kutoka AfricanDevelopment Bank (ADB). Wenzetu waliamua kununuandege, sisi tukaamua kujenga barabara kutoka Iringa kujaDodoma na kutoka Minjingu kwenda Singida. Kwa hiyo,baadaye tutanunua tu hizo ndege. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ATCL,wameliongelea wengi, kwa upande wa Serikali, kazi kubwakwanza ni kusafisha mizania ya ATCL na tumeshafanya hivyo.Sasa hivi ATCL inapendeza kweli na inawatamanisha watuwengi ndani na nje ya nchi, wanataka sasa ubia na ATCL.Kwa sasa tuna mazungumzo na Kampuni moja ya Oman navilevile tuna mazungumzo na Kampuni kubwa ya China yaNdege ya AVIC International na tutawataarifu matokeo yamajadiliano haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa EugenMwaiposya, Mheshimiwa Dkt. Kebwe, Mheshimiwa Ngonyani,Mheshimiwa Dkt. Kikwembe, Mheshimiwa Peter Serukamba,

[WAZIRI WA UCHUKUZI]

226

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Ismail Aden Rage, Mheshimiwa Herbert Mntangi,Mheshimiwa Masele na Mheshimiwa Kakoso na wengine,wemeongelea sana suala la reli. Naomba niwajibu kwaujumla kwamba, ukiachia reli ya TAZARA, tunao mtandaowa reli wenye urefu wa kilometa 2,707 na madaraja 5,123.Vyote hivi vina umri wa miaka 108. Tumeanza kazi kubwakama short measures kuondoa hizo reli zilizochakaa nakuweka mpya. Mpaka sasa tumeweza kutandika reli mpyakilometa 634, tumejenga madaraja mapya yanayowezakuhimili mzigo mkubwa zaidi ya madaraja 183. Tunao piampango wa muda mrefu nao ni kujenga reli kuanzia Dar esSalaam mpaka mpakani mwa Rwanda na Burundi kwastandard gauge, upana zaidi ili iweze kubeba mzigo zaidina iweze kuwa na kasi zaidi. Tumedhamiria vilevile kubadilishamtandao mzima wa reli ya kati kwenda kwenye standardgauge. Gharama za mradi huu ni dola za Kimarekani bilionitano, tunaongea na wawekezaji mbalimbali kama vileChina, Japan na Marekani kuhusu ujenzi wa reli hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, reli ya Tanga mpakaMusoma yenye kilometa 1038 na reli ya Mtwara mpakaMbambay, imeshapata mwekezaji na mjenzi ambaye niChina Engineering II. Reli ya Tanga mpaka Musomaitatugharimu dola za Kimarekani bilioni 3.0 na reli ya Mtwarakwenda Mbambay itatugharimu dola za Kimarekani bilioni3.6. Tusubiri tu haya majadiliano kwa sababu pia hii ni mikopoambayo hatuwezi tu kuivamia bila kuangalia madhara yakekiuchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Gati Na.13 na 14 kunamalalamiko ya kuchelewa, Waheshimiwa Wabunge na ninyimsisahau. Katika Mkutano wa Tano, mwezi Aprili, 2013, Bungeliliagiza Wizara ya Uchukuzi kuajiri Independent Consultant,kuweza kupitia gharama za mradi huu, mliona kwamba nikubwa mno. Tumefanya kazi hiyo mwishoni mwa mwaka2012 tukaweza kupata jibu hilo. Vilevile Kampuni ya CCCiliyokuwa itakiwa ijenge hayo magati tukaiondoa tumewekaKampuni mpya ya CHECC.

[WAZIRI WA UCHUKUZI]

227

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kutoa taarifakwamba kazi imeendelea na sasa hivi Kampuni hiyo yaCHECC imeshamaliza kile tunachokiita Topographical Surveyna vilevile Hydrographical Survey ambayo imewezakutuwezesha sasa kufahamu chini ya bahari pale kuna nini.Tumeshaonyeshwa kwamba chini ya bahari kuna mabombaya mafuta ambayo ni lazima tuyaondoe immediately, ni kaziya kitaalam. Vilevile kwa sababu Gati Na.13 na 14 itatumikakwa meli kubwa za kisasa za container, kipenyo cha kugeuzimeli kubwa kwa kweli ni kidogo, inabidi tumege maeneoya jirani kule siwezi kuyataja hapa, upenyo wetu ni mita 440tunahitaji mita 600. Kwa hiyo, yote haya ni maandalizi natunaweza kuanza, ni kama mchakato wa ujenzitumeshauanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Komba sualala meli, kwa kweli tumeliongelea sana, sijui nitoe ratiba. Mradiwa DANIDA, ujenzi wa meli mpya unaanza Juni, 2015 katikaMaziwa yote matatu. Ukarabati wa MV Serengeti, MV Umojana MV Victoria, unaanza Januari 2016. Vilevile tunao mradiwa South Korea ambapo ujenzi wa meli katika Maziwa yotematatu tunaanza mwaka 2014 yaani mwaka kesho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie tu kwa kusema,miradi ya miundombinu hasa reli, kwa kweli ni ya gharamakubwa sana. Nawashukuru Waheshimiwa Wabunge kwakuelewa umuhimu wa reli katika nchi yetu na kuwa tayarikujifunga mkanda kuweza kuingia katika uwekezaji huo nasisi tunaomba kuwahakikishia tu kwamba tutasimamia vizurihii miradi na ninaelewa kabisa, Bunge hili liko tayari kutuungamkono katika hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, wachangiajiwamemalizika. Sasa nitamwita mtoa hoja lakini kabla ahapo inabidi tukae kama Bunge.

[WAZIRI WA UCHUKUZI]

228

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

(Bunge lilirudia)

HOJA ZA SERIKALI

Mapendekezo ya Mpango waMaendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2014/2015

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, siku ya Jumamosi,Waziri na wataalam wake walikutana na Kamati ya Bajetikujaribu kutathmini yale mliyoyazungumza na kuona kwanamna gani inaweza kusaidia katika marekebisho yaMpango wetu. Kwa hiyo, sasa namwita mtoa hoja,Mheshimiwa Waziri wa Nchi!

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NAURATIBU): Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hiikukushukuru kwa kunipa nafasi ya kutoa ufafanuzi kuhusuhoja ya Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleokwa Mwaka 2014/2015. Aidha, nakushukuru wewe, NaibuSpika na Wenyeviti wa Bunge kwa kuongoza vizurimajadiliano.

Mheshimiwa Spika, kufuatia agizo lako la Kamati yaBajeti kukutana na Tume ya Mipango, tulikutana tarehe 2Novemba, 2013 na kuunganisha mawazo kuhusu yaliyotiliwamkazo katika mjadala unaoendelea. Tume ilifaidika namjadala huo na majibu nitakayoyatoa hapa ni pamoja namaelewano yaliyopatikana baina ya Kamati ya Bajeti na Tumeya Mipango. Kwa mara nyingine, naishukuru sana Kamatiya Bajeti kwa ushirikiano.

Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii pia kuwashukuruWaheshimiwa Wabunge wote waliochangia hotuba hii.Jumla ya Waheshimiwa Wabunge 120 wamechangia na katiyao 72 walichangia kwa kuzungumza hapa Bungeni naWaheshimiwa Wabunge 48 wamechangia kwa maandishi.Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, imepokea ushauri uliotolewana itaufanyia kazi katika maandalizi ya Mpango wa Taifawa mwaka 2014/2015. (Makofi)

229

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Spika, vilevile naomba nitumie nafasi hiikuwashukuru sana Mawaziri na Manaibu Waziri kutoka katikasekta zinazounganisha Mpango huu kwa maelezo fasaha naufafanuzi ambao umetolewa. Wameifanya kazi yangu mimikama Mtoa Hoja kuwa rahisi na naomba WaheshimiwaWabunge wachukue maelezo yote yaliyotolewa na Mawazirihawa, kuwa ni sehemu ya hitimisho la hoja hii.

Mheshimiwa Spika, hoja niliyoiwasilisha hapa Bungenisiyo Mpango bali ni Mapendekezo ya Mpango wa Taifa kwamwaka 2014/2015. Hii ni kukidhi matakwa ya Kanuni ya 94cha Kanuni za Kudumu za Bunge lako Tukufu za mwezi Aprili,2013, l inalotaka Serikali kuwasil isha mapendekezoyanayokusudiwa kutumiwa na Serikali katika kuandaa Mradina Programu za Maendeleo, itakayojumuishwa katikaMpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2014/2015.Lengo la kuwasilisha mapendekezo hayo, ni kupata maoniya wananchi kupitia wawakilishi wao walioko hapa Bungeni.Kwa maneno mengine, mpango huo utakuwa shirikishi kwanjia ya kuwashirikisha Wabunge kwa maana ya kwambamawazo wanayoyatoa hapa yanawakilishi mawazo yawananchi. Hakuna namna ambavyo tungeweza kushirikishavizuri zaidi kuliko hivyo.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo yautangulizi, naomba sasa nitoe ufafanuzi wa baadhi ya hojazilizojitokeza katika mjadala. Maelezo yangu yatagawanyikakatika sehemu mbili au tatu kama hivi ifuatavyo. Kwanzanitashughulika na mambo ya jumla ambayo yamejadiliwana Wabunge wengi. Pili, nitatoa maoni mahsusi yaliyotolewana Kamati ya Bajeti au Kambi ya Upinzani. Muda ukiruhusu,nitatoa maoni na kutoa majibu kwa baadhi ya hoja mahsusizilizotolewa na Mbunge mmoja mmoja au Wabunge kadhaalakini sina uhakika, kama muda kweli utaniruhusu.

SPIKA: Unayo saa moja.

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU)]

230

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NAURATIBU: Mheshimiwa Spika, kitu kimoja ambacho natakakuwaahidi Waheshimiwa Wabunge, nimeiagiza Tume yaMipango, itoe majibu kwa maswali yote nitakayotoa hapana ambayo sitatoa ili Wabunge mgawiwe na myatumiekama rejea wakati tutakapojadili Mpango huu mwezi Juni,2014. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa ni maelezo ya jumla na hojazilizotolewa. Hoja ya kwanza ilikuwa inazungumzia juu yampangilio wa mapendekezo kwamba mapitio ya utekelezajiina kurasa nyingi kuliko Mapendekezo ya Mpango kwaMwaka 2014/2015 na kwamba Mapitio ya Utekelezajiyawasilishwe katika mfumo wa bangokitita. Katika hali yakawaida ili kupanga vipaumbele au maeneo ya kuzingatiakatika maandalizi ya Mpango, ni muhimu kuzingatiamwenendo wa uchumi wa dunia na wa kikanda, ili kujuafursa na hatua zilizopo mbele yetu na mapitio ya Hali yaUchumi wa Taifa na hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wamiradi kwa mwaka uliotangulia na changamoto zake.Maelezo hayo, yanasaidia kuonyesha uwezo na udhaifu wetukuelekea Mpango unaofuata. Kwa hiyo, ni maelezo muhimukwamba huwezi kupanga Mpango bila kujua huko ulikotokahali ilikuwaje. Kwa hiyo, inabidi lazima tuwe na kurasaambazo zinaeleza Mpango umetekelezwa namna gani,kumekuwa na changamoto zipi, ili zituwezeshe kujua hukotunakokwenda hali itakuwaje.

Mheshimiwa Spika, pamoja na umuhimu wa Surainayorejea utekelezaji wa mwaka 2012/2013, maandalizi yaMpango wa 2014/2015, tutazingatia ushauri wa WaheshimiwaWabunge, kuwa na maelezo mafupi yanayoambatana nabangokitita, lenye takwimu za utekelezaji wa miradiinayoingia katika Mpango wa Maendeleo. Kwa hiyo,Mpango wetu utakaokuja Juni, 2014, utakuwa unazingatiaushauri huu wa Waheshimiwa Wabunge. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja ya pil i, ambayoimezungumzwa na Wabunge wengi sana, inasemavipaumbele vya Mpango ni vingi mno, vipunguzwe ili kuleta

231

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

matokeo ya haraka. Kwanza, kipaumbele namba moja chaMpango huu, ni kukuza uchumi. Hicho ndicho kipaumbelehasa, vingine vyote ni sub-vipaumbele lakini kipaumbelekikubwa ni kukuza uchumi ili ukuwaji huo utusaidie katikakujibu changamoto mbalimbali kama vile kupunguzaumaskini wa wananchi. Pili, kuweka ajira kila mwakazinazowapa ajira vijana, hayo ndiyo mambo ya msingi. Kwasababu unapopanga Mpango, ni lazima usema ni wa nini?Unataka kupata nini, unataka ku-achieve nini. Mpango lazimauwe ni wa uchumi lakini uwe ni wa uchumi wa wananchi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, unazungumza habariya kupunguza umaskini. Kama umaskini haupungui ni lazimatukae chini tuzungumze kwa nini haupungui na tuchukuehatua gani. Kwa maneno mengine tukuze uchumi, ilituboreshe maisha ya wananchi wakiwemo wakulima,wafanyakazi, vijana, wanawake na makundi mengine nakuwapatia watoto wa wakulima wafanyakazi na wananchiwote elimu na afya bora zaidi. Mpango lazima ujibu hojainayohusu maisha ya watu wa nchi hii.

Mheshimiwa Spika, wakati Mpango unawekavipaumbele, ulitazama hali ya nchi ilivyo na kubaini kwambahatuwezi kukuza uchumi bila kuondoa vikwazo vinavyozuiaukuaji wa uchumi na hivyo kuchelewesha maendeleo yaustawi wa wananchi na vikwazo vilivyogundulika ni kwanzamiundombinu duni kama vile nishati na umeme, ambapowote tunajua, hali ya umeme wetu huko tunakotoka natulipo, siyo nzuri sana. Kwanza, umeme ni ghali sana nahaupatikani kwa urahisi na ni watu wachache sana ndiyowanaopata nishati ya umeme. Kwa hiyo, bado kuna tatizokatika eneo hilo.

Mheshimiwa Spika, miundombinu ya uchukuziambayo Mheshimiwa Dokta Mwakyembe ameieleza vizurihapa, reli, bandari, viwanja vya ndege. Vilevile miundombinuya umwagiliaji maji, pamoja na maji kwa ajili ya wananchi,ambayo kupatikana kwake kunapunguza adha na kuwapamuda zaidi wa kufanya maendeleo yao, badala ya kuishiwanayasaka maji kwa muda wa masafa marefu.

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU)]

232

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Spika, tija ndogo katika kilimo nakutegemea mvua kwa ajili ya kilimo, ni maeneo ambayoyalionekana dhahiri kuwa yana upungufu na yanahitajimpango wa kuyaondoa pale. Ukosefu wa viwanda katikanchi ndiyo unaosababisha kukosekana kwa ajira na kwambarasilimali watu vilevile ujuzi wake unahitaji kuimarishwa. Tatizolingine ni huduma hafifu za utalii, biashara na huduma zakifedha. Yote yalionekana ni matatizo ambayo yanahitajikushughulikiwa. Ili kuondokana na hali hiyo, Mpango wamiaka mitano ulielekeza vipaumbele vitengenezwe ili kujibumatatizo hayo.

Mheshimiwa Spika, miundombinu kama bandari, relina umeme, ikapewa kipaumbele namba moja nainaambatana na umwagiliaji na vilevile maji kwa matumiziya wananchi. Kilimo cha mazao, mifugo na uvuvi, kikapewakipaumbele namba mbili. Viwanda hasa vinavyoongezathamani kwa mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi, vikapewakipaumbele namba tatu. Rasilimali watu inayohusisha elimu,afya na kadhalika ikapewa kipaumbele namba nne nahuduma za utalii biashara na fedha, zikapewa kipaumbelenamba tano.

Mheshimiwa Spika, hoja kwamba vipaumbele hivi nivingi nadhani siyo sahihi. Vipaumbele ni vitano tenavinategemeana. Reli, barabara, bandari na umeme ni lazimakwa maendeleo ya kilimo na biashara ya ndani na nje. Huwezikuwa huna bandari, huna barabara na huna umeme lakiniukawa unategemea kilimo kitakuwa, hakiwezi kukua kwasababu barabara ndiyo zinafikisha pembejeo kwa wakulima,barabara ndiyo zinafikisha mazao sokoni. Kwa hiyo, kamahuna miundombinu hii huwezi kukuza kilimo na huwezikukuza biashara kama una bandari lakini huna reli na hunabarabara.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, unaweza ukaona jinsivipaumbele vyenyewe vinavyohusiana. Hakuna viwanda bilaumeme na bila viwanda hakuna ajira. Pia viwanda nimuhimu kwa kilimo na kilimo ni muhimu kwa upatikanajiwa malighafi kwa viwanda. Kwa hiyo, unaweza ukaona jinsi

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU)]

233

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

vipaumbele vyetu hivi vinavyoitwa vingi vil ivyo navinavyoshabihiana. Kukosekana kwa huduma nzuri za fedhakunawakosesha wazalishaji, wafanyabiashara mikopo nakudumaza uchumi kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, pendekezo la Serikali hapa, siyokupunguza vipaumbele vilivyopitishwa na Bunge lako Tukufukatika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano mwaka 2011badala yake tujaribu kujikita katika kupanga vizuri mtiririkowa miradi na utekelezaji katika kila kipaumbele, kuongezajitihada za kuongeza mapato na kusimamia nidhamu yamatumizi. Mimi naamini tukisimamia nidhamu ya matumizitutakuwa na fedha ambazo zinaweza zikasaidia kutekelezamiradi. Hili siyo mara yangu kwanza kulisema na siyo maraya kwanza Waheshimiwa Wabunge kulisema. Nadhanitujikite katika kuona, hivi kweli fedha zetu zote zingetumika,hali yetu ingekuwaje?

Mheshimiwa Spika, wote tunajua na wote tunakubalikwamba kuna kitu kinaitwa manunuzi, kinachukua 70% natunajua tatizo hili la mfumo wetu wa manunuzi na jinsi beizinavyokuwa kubwa kiasi kwamba ukienda sokoni unakutabei zipo chini lakini bei za manunuzi zipo juu. Tukiweza ku-solve hii problem na nadhani Hazina wanaijua sasa natutasaidia nao katika ku-solve, inaweza ikatupa surplus natukaona kumbe utekeleza unaweza ukafanyika vizuri kamafedha hizi zitakuwa saved. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pendekezo la Serikalinimeshalieleza lakini pamoja na vipaumbele na miradiinayoambatana na vipaumbele, kunahitajika uwekezajikatika maeneo mengine ambayo yana uhusiano na maeneoya kipaumbele ya kitaifa. Kwa mfano, maeneo hayo nimadini, ardhi, nyumba, makazi na utawala bora, kwasababu haiwezekani ukawa na vipaumbele ambavyovinapuuza haya. Huwezi kukuza kil imo kama ardhihaikupimwa, huwezi kuondokana na mgogoro huu wawafugaji wanagombania ardhi na wakulima bila kupimana huwezi vilevile kuwa na nchi ambayo utawala wakehauzingatii mahitaji ya wananchi na kuweka amani halafu

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU)]

234

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ukategemea mpango utatekelezwa. Kwa hiyo, katikamiundombinu na katika vipaumbele hivi, huwezi kuyaonahaya lakini yana supplement utekelezaji wa miradi ile.Vilevileyapo mambo ambayo yalijitokeza ambayo yanachukuafedha kama ushirikiano wa kikanda, utambulisho wa taifa,Katiba Mpya na mazingira, yote ni mambo muhimu katikautekelezaji wa mpango huu. Kwa hiyo, ninachotaka ku-urgeni kwamba vipaumbele vipo, vinaingiliana lakini tutazamenidhamu katika matumizi, tuongeze mapato na hapotunaweza kupiga hatua zaidi ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, hoja nyingine ambayoimezungumzwa na Waheshimiwa Wabunge wengi naambayo kwa kweli hata mimi inanigusa na inanipa matatizokidogo, ni kwamba Mpango wa Maendeleo ulenge katikakujibu matatizo ya umaskini wa Tanzania na hili ni jambolinazungumzwa sana. Wanasema uchumi unakua kwa 7%na umekuwa unakua na ukizungumza na Wachumiwatakwambia uchumi wenu ni stable kwa sababu unakuakwa 6.5% mpaka 7% na kwa miaka kadhaa mfululizo. Kwahiyo, kwa upande huo wa macro, unaweza kuona mamboni mazuri sana. Tatizo letu lipo katika namna uchumiunavyojibu problem ya umaskini.

Mheshimiwa Spika, Mapendekezo ya Mpango kwamwaka 2014 yameandaliwa kwa kuzingatia haja yakuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi lakini vilevile kupunguzaumaskini. Eneo moja ambalo linaweza kutusaidia sana katikakupunguza umaskini ambalo Ndugu yangu Adam Malimaamelizungumzia, ni eneo la kilimo. Ni eneo muhimu katikakukuza uchumi lakini vilevile ni eneo muhimu katikakupunguza umaskini. Katika kuendeleza kilimo, tumekaa nandugu zetu wa kilimo, katika kutafuta jibu la swali hili nakwa kuwa Tume ndiyo inaweka rasilimali kulingana namahitaji ya vipaumbele kwa Mpango huu, yapo mamboambayo tumekubaliana na napenda Bunge hili lielewetumeyaona vipi na tunataka kufanya nini.

Mheshimiwa Spika, kwanza, lazima tukuze kilimo lakinikusema hivyo tu haitoshi, tunakikuza namna gani? Una vituo

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU)]

235

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

vya utafiti na ninapozungumza kilimo, naomba nitafsiriwenazungumzia mifugo na uvuvi maana yote kwa terminologyni kilimo. Unakuwa na utafiti, uko ndani ya Chuo cha Utafitilakini matokeo yake hayamfikii mkulima. Kwa hiyo, unawezaukalipa pesa, ukatengeneza utafiti, ukaandika vitabuvikubwa kabisa lakini kama matokeo hayo ya utafiti hayafikikwa mkulima basi mkulima atabaki hivyohivyo alivyo namatokeo ya utafiti yatabaki separate. Kwa hiyo, nachotakakusema ni kwamba tumekubaliana na wenzetu wa kilimotuunganishe suala la utafiti na huduma za ugani ili vituo vyautafiti viwe na uhusiano wa moja kwa moja na ugani ilimaarifa yanayotoka kwenye vituo vya utafiti yawezekuwafikia wakulima.

Mheshimiwa Spika, vilevile tumekubaliana kwambasuala la mbolea lisiwe ni suala la Fire Bridged kwamba wakatikilimo kinakuja lori linakimbizana na mvua kupeleka mboleakwa wakulima. Ushauri tulioutoa na tumekubaliana nikwamba mbolea ingekuwa kama bidhaa nyingine tukwamba wale wanaotaka kufanya biashara ya mboleawawe na mbolea kulekule vijijini wakati wote na kwa hiyomvua ikija itakuta mbolea iko vijijini, hiyo inaweza ikatusaidia.Sasa hivi hali ilivyo ni kwamba unakimbizana na lori, mboleana mvua. Mimi nadhani tukiwa-encourage hawa wanaotakakuuza mbolea wakae na mbolea, wakati wote wanawezawakanunua mbolea na kuuza. Kuna maeneo ambayombolea wakati wote ina soko, hilo nalo tumelifikiria. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la ushirikalimekwishazungumzwa na Mheshimiwa Malima na nadhanina Sheria mpya inaweza ikasaidia.

Mheshimiwa Spika, kuongeza fursa za mikopo kwawakulima ndiyo jambo ambalo ni jipya kwa Tanzania.Tunatoa ruzuku kwa sababu hakuna mkopo. Mkulima waLudewa akitaka kwenda kukopa hana mahali anawezakukopa. Mimi nimetembea kuangalia kilimo katika nchiambazo zimepiga hatua kama Vietnam, suala la mikopolipo mpaka kwenye ngazi ya Wilaya. Sasa tumeanzisha Benki

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU)]

236

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ya Kilimo na Benki hii itafungua milango yake Januari yaanimiezi michache ijayo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, matumaini yetu ni kwamba ilebenki itafanya kazi nzuri na itakuwa na uhusiano na SACCOSza wakulima wadogo ili mikopo hii iweze kufika na ili mkulimaakitaka mbolea na mbegu za kisasa, akitaka jembe la plauna akitaka power tiller aweze kuweka dhamana kwa njiaya SACCOS yake apate mkopo kutoka Benki ya Kilimo kwamasharti nafuu zaidi kuliko masharti ambayo yapo kwenyemabenki ya sasa. Hiyo itatusaidia sana katika kuboreshakilimo. Hakuna modernisation kama hakuna credit na hakunamodernisation kama hakuna matumizi ya sayansi katikakilimo.

Mheshimiwa Spika, suala la masoko limezungumziwavizuri nadhani inatakiwa kutazamwa vizuri ili kuhakikishakwamba tunapata manufaa.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni scheme zaumwagiliaji, Mheshimiwa Said Amour Arfi alipokuwa anajadilijambo hili alisema katika Mkoa wa Katavi kuna scheme sitana inayofanya kazi ni moja. Unaweza kwenda kila Mkoa,utakuta kuna scheme ambazo hazifanyi kazi. Tumekubalianana Tume kwamba mwaka huu tutatoa fedha kwa ajili yakuimarisha zile scheme na mwaka huo unaokuja tuhakikishekwamba scheme zote zinafanya kazi kwa manufaa yawahusika. Hiyo ndiyo itatusaidia katika kuonyesha njia yanamna ya kuweza kufika tunakotaka kwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuimarisha masoko na vilevileupimaji wa ardhi ya kilimo na mifugo uongezewe kasi naurasimishaji unaofanywa na MKURABITA upewe rasilimali zaidi.Kwa sababu matatizo yetu mengine haya ya wafugajiwanagombana na wakulima, yanatokana na kutopima, kuleambako tumepima kuna nafuu. Kwa sababu watuwakishajua eneo lao ni hili inakuwa ngumu sana kukaribishawengine kama halitoshi, lakini kama watu wanachunga tukama mbuga, watasema njoo na wewe eneo ni kubwahalafu watafika watakuta kwamba wala siyo kubwa kama

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU)]

237

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

walivyofikiria. Kwa hiyo, nafikiri tukiwekeza katika kupima nakurasimisha ardhi na vilevile upimaji na urasimishajiutawasaidia wakulima kuweka rasilimali yao ya ardhi kamadhamana ya kupata mikopo.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalotumelizungumza na ni muhimu sana tuliweke katika Mpangounaokuja wa mwaka 2014, ni juu ya usindikaji wa mazao.Hili limezungumzwa na Wabunge wengi na leo MheshimiwaMichael Laizer amekuwa anazungumza sana kuhusu Nyamalakini mazao mengi yanahitaji usindikaji. Hili kwa kwelitumezungumza na Tume na kwa kweli tunachosema nikwamba labda tuanze kutazama uwezekano wa namnaya kuwasaidia wawekezaji wa ndani. Tuwe na sera mahsusiambayo inawasaidia. Wapo wawekezaji wa ndanininawajua kwa mfano ukienda kwenye pamba wako watuwana ginneries wangependa sasa kutoka kwenye ginnerieswaende kwenye utengenezaji wa nyuzi na nguo lakiniwakijaribu mtaji inakuwa ngumu sana kupata. Wenginenawajua akina Gungu wana ginnery, kina Njaru wa Bariadiwaliwahi kujaribu, tunawajua akina Elihilary wa Shinyangawalitaka kujaribu kutengeneza kiwanda cha kutengenezapamba ya Hospitalini lakini wakifika mahali wanakwamakwenye eneo la mtaji.

Mheshimiwa Spika, mimi nadhani tukiwa nadeliberate policy na tujaribu na Tume tumeiambia ijaribukupeleka mapendekezo Serikalini ili tuweke mkakati ambaoutasaidia wawekezaji wa ndani waanze kutoa mchangounaoongeza thamani ya mazao kwa kuwekeza katikaviwanda. Hili ni jambo ambalo tunaliweza kwa sababu nchinyingi zimefanya. Nimekwenda China juzi, nikawauliza ninyiubinafsishaji mliufanye, wakasema hiyo haiko kwenyeterminology yetu, sisi tunakaribisha watu wa nje lakinitunashirikiana nao, tunafanya joint venture. Nilikwenda Korea,wao kabisa toka mwanzo pamoja na uhusiano wao naMarekani waliwekeza kwa kuwasaidia watu wao palepale,wakawekeza na nguvu yote ya uchumi iko mikononi mwaWakorea. Kwa hiyo, mimi nafikiri hili jambo tunawezatukalijaribu na tukaweza. Haya mambo yote tukifanya katika

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU)]

238

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

sekta ya kilimo na viwanda, vitatuongezea uzalishaji wachakula, itasaidia kupunguza mfumuko wa bei na vilevileumaskini wa kipato unaweza ukapata majibu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwenendo wa deni la taifaumekwishaongelewa na Naibu Waziri wa Fedha. Namshukurukwa maelezo yake mazuri sana ya ufasaha na ameonyeshavitu ambavyo tunafanya kwa kutumia deni hilo kamabarabara na hata UDOM hii ni deni, hatujalipa lakini ipo.Hata ukidaiwa unasema tunadaiwa lakini tumejenga UDOM.Kwa hiyo, hakuna namna unaweza ukakwepa mambo haya,dunia nzima inakopa hata Marekani wanakopa China. JuziChina pressure ya Wachina ilipanda wakati wanagombanaWashington kwa sababu benki ukiikopa na wewe hutakikulipa na huweki ukomo wa madeni benki inasikitika naWachina nao ndiyo benki ya Amerika. Kwa hiyo, mambohaya yapo duniani, tutaendelea kukopa lakini ili mraditusikope halafu tukafanya deni likashindwa kuhimilikatukarudi kwenye HIPIC.

Mheshimiwa Spika, hoja ya tano ni Mpangounaandaliwa bila kujua vyanzo vya mapato. Tulikubalianakwamba tutatumia shilingi trilioni 8.9 kwa kila mwaka. KatikaMpango tunaoupendekeza kuna shilingi trilioni tano lakiniukweli ni kwamba hatukukusudia trilioni zote zitoke katikabajeti ya Serikali, kiasi kinachobakia tulikubaliana kwambakitatoka kwenye sekta binafsi. Jambo ambalo tutalifanya nikujaribu kuifanya Tume i-truck ili ijue sekta binafsi inawekezawapi na kiasi gani. Katika Mipango yetu inayokuja na katikakueleza utekelezaji, sehemu hii itajitokeza katika tathmini.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, hoja ya sita ilisema Serikali iandaeutaratibu mzuri wa kuwezesha vijana kujiajiri. Hili lilikuwa nijambo kubwa ambalo limezungumzwa sana na miminakubali kwamba Serikali ni lazima iwe na mkakati wakusaidia vijana. Kulingana na sensa ya watu na makazi yamwaka 2012, asilimia 67.1 ya nguvukazi ya Tanzania ni vijanawa umri kati ya miaka 15-35. Kundi hili la vijana ndiyo lenyekiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira kwa 13.4% au zaidi

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU)]

239

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

ikilinganishwa na wastani wa 12.7% ya ukosefu wa ajira kwavijana dunia nzima.

Mheshimiwa Spika, pamoja na hatua mbalimbaliambazo Serikali imekuwa ikichukua kukabiliana na tatizo laajira nchini kupitia Mifuko ya Uwezeshaji na Mifuko ya Vijana,Serikali sasa imeandaa program ya ajira kwa vijanaitakayoelekezwa kwa kipindi cha miaka mitatu yaani 2013/2014 na mwaka 2015/2016. Baadhi ya malengo ya programhiyo ni kupatikana fursa za ajira 840,000 kwa kuwezesha jumlaya miradi 10,000 ya wahitimu wa elimu ya juu 30,000 kutokavyuo mbalimbali watatoa ajira za moja kwa moja kwawahitimu wengine 270,000 na ajira zisizo za moja kwa mojakama 540,000.

Mheshimiwa Spika, program hii itatekelezwa kwakuzingatia maeneo makuu matatu. Inalenga kujenga uwezowa vijana katika stadi ya kazi, ujasiriamali na kuwapatiamikopo vijana ili kupata mitaji, nyenzo na vifaa vya kufanyiakazi na kuwapatia vijana maeneo ya uzalishaji na biashara.Serikali inapanga kutenga fedha za kutosha katika kipindihusika ili kuwezesha utekelezaji wa program hii.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Edward alikuwaamelizungumza jambo hili na akazungumza juu ya CRDB.Mpango huu CRDB inashiriki kama mdau lakini ni mpangowa Serikali katika kujaribu ku-solve hii problem ya vijana.Vilevile kuna nafasi kama 65,000 katika sekta ya umma nasekta rasmi ambayo vilevile itatoa fursa kwa vijanawanaoajiriwa moja kwa moja na ambao ni wage earners.

Mheshimiwa Spika, hoja ya saba ilihusu sababu zakuanzisha kitengo kingine cha utekelezaji yaani hapawalikuwa wanazungumza juu ya Big Results Now naPresidential Delivery Unit. Nadhani jambo hili limeshaelezwamara nyingi na pengine ni vizuri niokoe muda wa Bunge lakoTukufu kwa sababu jambo hili tumelizungumza lakini kamabado kuna maelezo yanayohitaji mazungumzao zaiditutaendelea kulijadili.

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU)]

240

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Spika, tulikubaliana na Kamati ya Bajetikwamba tutapata fursa ya hawa jamaa waliopo kwenyePresidential Delivery Unit walete maelezo juu ya shughuliambazo wameanza nazo na kuonyesha speed ganiitakuwepo. Kwa hiyo, wanaandaa na tutapata muda wakukutana na ile Kamati. Hata hivyo, katika siku zijazotutaweza kutoa suala hili kwa Wabunge wote ili wawezekuelewa kitu gani hasa kinafanyika na Wabunge wakielewaWatanzania wataelewa kupitia kwa Wabunge.

Mheshimiwa Spika, hoja ya nane ilihusu ulinzi nausalama kwamba haukuwa katika kipaumbele. Suala hilil i l ipigiwa debe sana na Mama Abdallah ambaye niMwenyekiti wa Ulinzi na Usalama. Katika suala hili natakakusema kwa ufupi tu kwamba kwenye Mpango hatukuwekafedha kwa ajili ya ulinzi na usalama zinatolewa na hazipokatika bajeti hii. Hakuna namna unaweza ukalinyima fedhaJeshi la Polisi halafu ukasema utatekeleza Mpango,utatekeleza wapi? Ni lazima iwemo amani na utulivu katikanchi, ni lazima mipaka yetu ilindwe ndiyo Mpango huu uwezekutekelezwa kikamilifu. Kwa hiyo, nataka kuwaondolea hofukatika jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lipo jambo la Ofisi ya Rais, Tumeya Mipango na capacity yake ya kuweza kutekeleza mambohaya. Tume ya Mipango il iundwa kama think tank,haikukusudiwa kwa kweli kuwa chombo kikubwa sana. Maranyingi kinatumia watu wengine kama universities na wasomiwengine katika maeneo mengine kwa ajili ya kufanyashughuli zake kwa ku-contract. Ukitaka kila kazi ifanywe nahii Tume, kwa kweli hii Tume itakuwa kubwa kuliko ambavyoungeweza kufikiria kwa sababu kila fani kutakuwa nawataalam; wataalam wa gesi, wataalam wa mafuta,wawepo wa kilimo na nini, itakuwa kubwa sana lakiniinapotokea suala ambalo ni specialized, Tume hii ina-contractout.

Mheshimiwa Spika, hayo ndiyo maeneo ya jumlaambayo yameongelewa katika kikao hiki na mengineyamejibiwa vizuri na Waheshimiwa Mawaziri.

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU)]

241

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Spika, katika ufafanuzi mdogouliotolewa kwenye Kamati ya Bunge ya Bajeti, liko suala lamatumizi ya kawaida ukil inganisha na matumizi yamaendeleo na kwamba fedha za matumizi ya kawaidazinaonekana ni nyingi. Mimi nadhani hapa nirudie tena, sualala msingi hapa ni matumizi mazuri, nidhamu katika matumiziya fedha za Serikali. Hata hivyo, kimsingi ukifanya maendeleo,unaongeza matumizi ya kawaida, hakuna namna unawezaukakwepa. Ukijenga shule mpya, unahitaji vitabu zaidi,unataka Walimu zaidi na kwa hiyo mshahara zaidi. Ni vigumusana kuzuia kuongezeka kwa matumizi ya kawaida lakiniunaweza ukaya- control kama unatumia vizuri. Kamaukitumia vizuri basi unaweza ukasema kwa kweli hakuna hajaya kuwa nazo nyingi sana kwa sababu chache zilizopozinafanya kazi iliyokusudiwa.

Mheshimiwa Spika, fedha za maendeleo zilizotolewakatika robo ya kwanza ni asilimia ndogo zaidi ukilinganishana zile zilizokwenda kwenye mipango ya matumizi yakawaida. Hii ni kweli na nimezungumza na Wizara ya Fedhajuu ya jambo hili na wamenieleza ni kwa nini ilitokea hivyo.Kwa sababu kuna shughuli nyingi sana ambazozimegharamiwa katika quarter ya kwanza. Kumekuwepo navikao vya Bunge ambavyo vilihitaji fedha wakati uleule,kumekuwepo kwa ununuzi wa chakula kwa ajili ya Hifadhiya Chakula kuwahi Julai ili chakula kiweze kupata soko, kwahiyo fedha zilienda kwenye matumizi ya kawaida, mikopoya wanafunzi wa elimu ya juu ilibidi lazima fedha zipatikanewakati uleule, vilevile ruzuku ya pembejeo za kilimo ili kuwahimsimu wa kilimo nazo zinatolewa wakati mmoja, kuhuishaDaftari la Wapiga Kura na kugharamia mitihani ya Darasa laSaba, Kidato cha Pili na Kidato cha Nne, yote yalihitaji fedha.Kwa hiyo, ili kuweza kuyafanya hayo kwa quarter ya kwanza,fedha zil ienda nyingi zaidi kuliko zil izoenda kwenyemaendeleo. Tumekubaliana na Hazina kwamba quarter yapili, quarter ya tatu mpaka ya mwisho, hili pengo lililotokeakwenye quarter ya kwanza litafidiwa ili tusiathiri mipango yamaendeleo.

Mheshimiwa Spika, suala lingine, Serikali haina budi

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU)]

242

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kuhakikisha kwamba kila mdau anayehusika katika Mipangoya Maendeleo kwa nafasi yake ya kiutendaji anatimiza wajibuwake. Aidha, watendaji wanaokwamisha utekelezajiwawajibike. Hilo tunalikubali na kwa kweli tumeweka BigResults Now, tumeanza mfumo ambao unawajibishawatendaji ambao wanashindwa kutimiza wajibu wao nahiyo itakuwa extended kwenda kwenye Serikali yote baadaye.

Mheshimiwa Spika, mapendekezo ya Mpango waTaifa yanatakiwa yaanishe malengo mahsusi (defined specifictargets). Tunakubali maoni hayo na tutajaribu kuyafuatilia.

Mheshimiwa Spika, Serikali iendelee kutengenezamipango thabiti kuendesha rasilimali watu. Tunakubali narasilimali watu inaendelea kushughulikiwa na vyombombalimbali.

Mheshimiwa Spika, ushiriki katika sekta binafsi kwasuala la kukuza elimu na ujuzi uwe wazi. Serikali imekuwaikishirikiana kwa karibu sana na sekta binafsi katika jambohili na kama mnavyojua, universities za binafsi zote Serikaliinatoa mikopo kwa wanafunzi ili watoe nafasi ya elimu kwavijana wengi zaidi badala ya ku-confine mikopo kwauniversities za Serikali.

Mheshimiwa Spika, mapendekezo ya Mpango waMaendeleo yaoneshe kuwa yanazingatia utekelezaji nachangamoto zinazojitokeza. Ushauri huu utazingatiwa katikajambo hili.

Mheshimiwa Spika, Serikali itoe msukumo unaohitajikaili kuhakikisha mradi wa kitaifa wa kimkakati unatekelezwakwa malengo na kwa muda tuliojiwekea. Tutajitahidi kuonajambo hili linafanyika.

Mheshimiwa Spika, malengo ya utekelezaji wa mfumowa Big Results Now wanasema hayajaeleweka. Nimesematutaendelea kuyaeleza lakini tumeanza kufanya utaratibuambao unawapa wananchi uelewa. Kwa mfano, ushiriki walabs zile ulikuwa unashirikisha sekta binafsi na ya umma.

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU)]

243

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Uzinduzi wa wazi ‘open day’ wa Mfumo wa Tekeleza kwaMatokeo Makubwa ulifanyika waziwazi. Uzinduzi rasmi na wawazi wa mpango wa kila eneo kuu la matokeo. Taarifakuhusu BRN iko kwenye tovuti. Ushiriki wa wataalam wa PDBna MDU katika mikutano ya sasa, jambo hili linafanyika. HataMikoani ambapo hiki kitu hakikuwa kimekusudiwa lakiniMikoa yote imeambiwa na wameanza kuunda timu zakufuatilia. Kwa sababu kuna maeneo muhimu sana ambayoyanatekelezwa Mikoani, kwa mfano, maji ya kunywa yakokatika Big Results ambako tunataka watu milioni saba(7,000,000) waweze kupata maji safi na salama katika mudawa miaka mitatu. Suala hilo linafuatiliwa na PresidentialDelivery Unit lakini vilevile Mikoa yenyewe ambayo iko karibuna utekelezaji wa miradi ya maji vijijini itafuatilia.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ni umeme hasa ulewa vijijini ambao tunataka ifikapo mwaka 2015/2016 tuwezekuwapa umeme asilimia 30 ya wananchi wa Tanzania. Hilojambo linahitaji usimamizi huku center na vilevile katika Mikoakufuatilia mapendekezo hayo.

Mheshimiwa Spika, mapendekezo ya Mpango waMaendeleo wa Taifa kwa mwaka 2014 kutoanisha kwa kinamiradi iliyoibuliwa na mfumo wa Big Results Now. Miradi hiiitakuwa katika sehemu ya Mpango ujao na tutakuja kuijadiliitakapofika Juni kuonesha sekta gani Big Results Nowwatakuwa wanafanya nini, lakini iko katika maeneo yale sitatu na hayataongezeka sana.

Mheshimiwa Spika, eneo la kuondoa umasikini wakipato nimeshalizungumza. Bajeti ya maendeleo kutolindwa,tumesema sasa tutajaribu kufanya ringfencing ili kuhakikishakwamba fedha hizi haziyumbi wala hazitoki kwenyedevelopment.

Mheshimiwa Spika, idadi ya watu nchini imekuwakubwa na kwa hiyo ukuaji wa uchumi unakwenda chini zaidiukilinganisha na idadi ya watu. Hili ni jambo kubwa lakiniunalifanyaje hasa maana watu wanazaa na hakuna sheriainayowazuia kufanya hiyo shughuli ya kuzaa? Kwa hiyo, wapo.

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU)]

244

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Jambo kubwa hapa ni kutazama utaratibu wa kukuzauchumi.

Mheshimiwa Spika, wengine wamesema hapa tunalotatizo watu hawafanyi kazi, labda hil i l inawezalikatupunguzia tatizo kwamba badala ya watu kukaa tu aukukaa wanalalamika, tungejiwekea utaratibu ambaoutawawezesha watu hawa kufanya kazi. Wakifanya kazi nauchumi ukikua watu wataongezeka. Ziko nchi zina watuwengi kuliko sisi. Uchina wana watu 1.5 bilioni lakini wanakulawote watu wale ila wanakuna vitu vingi, lakini wapo nawanaendelea vizuri tu. (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nadhani suala la msingihapa siyo kuona ongezeko la watu kama ni problem, sualala msingi hapa ni kuweka taratibu za kiuchumi ambazozitafanya ongezeko la watu liende sambamba na ukuaji wauchumi ili ukuaji wa uchumi uweze ku-service ongezeko lawatu.

Mheshimiwa Spika, hatua nyingine ni majibu kwamasuala kutoka kwenye Kambi ya Upinzani. Rafiki zanguwa Kambi ya Upinzani wametoa maneno mengi kidogo, sinampango wa kuyajibu yote kwa sababu mengine kwa kweliwalikuwa wanauliza maswali tu. Kwa mfano, kuna mahaliwanasema wamesoma Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM)halafu wanauliza sasa itakuwaje? Jibu lake hilo ni rahisi, Ilaniya CCM itafanyiwa tathmini na CCM. CCM itaenda kwawananchi kueleza. Sasa wale ambao wana mashaka nautekelezaji wataonana na CCM kulekule vijijini. CCM itakuwainaeleza na wenzetu wanajibu halafu mambo yatajipa tuna waamuzi ni Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, sikuona kama kunatatizo na ndiyo maana tulikuwa na ndugu Hamad pale TBCnikasema kwa nini mnataka kupakua kabla ya kupika? Majiyakichemka ndiyo unaweka unga, lakini ukianza kuwekaunga na maji hayajachemka badala ya kupika ugaliunakuwa uji. Sasa nadhani tujipe time tu mambo hayayataeleweka. Bado tuna miaka miwili, tumetekeleza mitatu

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU)]

245

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

na maelezo mmeyasikia namna utekelezajiutakavyokwenda. Kwa hiyo, tusubiri.

Mheshimiwa Spika, lakini kuna mambo wamesemaambayo yanahitaji majibu. Kwa mfano, Serikali itoe tathminiya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya kipaumbelesambamba na taarifa za matumizi ya fedha. Hili litafanyika,kwenye Mpango unaokuja kufika Juni tutakapokuwatunazungumza Mpango utakuwaje tutazungumza utekelezajiwa mwaka uliopita umekuwaje na fedha kiasi ganizimetumika. Kwa hiyo, ni jambo linakubalika.

Mheshimiwa Spika, hakuna umakini katikakuhakikisha Mpango wa Miaka Mitano kwa kuwa kifungu(c) katika kitabu cha mapendekezo ya Mpango kinasemamiradi imeibuliwa mwaka 2012/2013. Labda hiyo ni error, lakinimiradi yote inayotekelezwa iliibuliwa chini ya Mpango waMaendeleo wa Miaka Mitano mwaka 2011.

Mheshimiwa Spika, hoja nyingine ambayo imesemwani kwamba wananchi hawashirikishwi. Mimi nataka kusemakwa maana ya Mpango huu na kwa maana ya level hii yakitaifa, tunashirikisha. Tunazungumza na Kamati za Bunge,tunapata mawazo ya Wabunge wote na mawazo yale ndiyotunaenda kuyatafsiri katika kutengeneza Mpango. Matumainiyangu ni kwamba Halmashauri za Wilaya katika ngazi ya chinina yenyewe itakuwa vilevile inafanya kama tunavyofanyasisi kwa kuwashirikisha wananchi ili miradi yao iwe inakuwasehemu ya mpango wa Halmashauri. Tusipofanya hivyo kwakweli itakuwa mipango hii inapangwa na bureaucrats, lakinikwa kuwashirikisha viongozi na wawakilishi wa wananchitunawashirikisha wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali imeshindwa kutekelezamatakwa ya Mpango kwa kushindwa kufufua reli. NadhaniMheshimiwa Dkt. Mwakyembe, ameeleza vizuri. Kwanza,nataka niseme kwamba ile reli ya kati lazima tutaifufua,lazima tufufue reli na pengine siyo vizuri sana ku-complain,sijui nani wamekutana, wanataka kujenga ya kwao! Wachawajenge ya kwao na sisi tujenge ya kwetu. Kwani nani

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU)]

246

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

amemzuia mtu kujenga reli yake? Halafu wafanyabiasharahawa ni rational, ukijenga reli kutoka Dar es Salaam mpakaKabanga na mfanyabiashara yuko Burundi na pale ni kilomita125, hawezi kupeleka mzigo wake kilomita 2700.Watakaopeleka ni wale ambao wanafuata siasa, lakinibiashara ya faida atakwenda kwa reli fupi. Kwa hiyo, sisitutajenga reli na ukijenga mpaka pale Kabanga na ile Nikeliliyokuwa inazungumzwa na Mheshimiwa Mbunge kutokaKagera, Nikel yenyewe ile ikichimbwa inatosha kufanya ilereli kuwa viable.

SPIKA: Waziri tumia microphone maana naonaunaongelea pembeni. (Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NAURATIBU): Ilikuwa imenoga kidogo. (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nasema tujenge reli,tuache kulalamika. Reli imefanyiwa feasibility study ,Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe ametueleza na kinachobakiani kuamua kwa kutazama nani ambaye tunawezakushirikiana naye kujenga kwa gharama kiasi gani na kwamanufaa yapi. Nadhani hilo ndiyo jambo la msingi. Kwa hiyo,hilo nalo limekwishapata ufumbuzi wake.

Mheshimiwa Spika, maeneo ya kipaumbeleyaliyotajwa na Serikali katika Mpango wa Miaka Mitanoyanahitaji kufanyiwa mabadiliko na tuyaelekeze kwenyemaeneo mapya. Hil i kwa kweli nasikitika kwambahatutaweza kwenda hivyo. Mwakani tunaanza kufanyatathmini ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano natathmini ile itatusaidia kuona vipaumbele vya Mpangounaofuata viweje. Hapo ndipo tunaweza kuzungumza vipya,lakini kwa sasa tuendelee na hivihivi. Utaacha kipi maanahatujatekeleza mambo makubwa? Tunataka umeme,hauwezi kusimamisha umeme. Tunataka reli, hauwezikusimamisha reli. Tunataka barabara tena za Ilani ya CCM,lazima zijengwe na Waziri ametueleza pale kwamba zikocommitted na zimeandikwa. Hizo ndiyo hoja zilizotolewa nawenzetu wa Upinzani, tunawashukuru sana.

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU)]

247

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Spika, tumejitahidi sana, actually hataukitumia hotuba yako ukanung’unika bado utaachamanung’uniko halafu towa nawe point inayosaidia Mpango.Katika suala hili la kupanga na kutekeleza, nafikiri tuwenationalistic kwa sababu Mpango wenyewe ni wa nchi yetuwote.

Mheshimiwa Spika, l iko suala la ajiranimeishalizungumzia, la reli nimeishalizungumzia na lilikuwalimesemwa na wadau wengi vilevile. Liko suala la barabarana lenyewe limeelezwa vizuri sana, usafiri wa angaumezungumzwa vizuri tu na Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe.Nishati, Maji, Kilimo nacho nimekizungumza na mimi pamojana Mheshimiwa Malima amezungumzia. Mawasiliano, sualala mifugo, ardhi, yote haya yamezungumzwa.

Mheshimiwa Spika, suala la elimu halikupata mtu wakulizungumza lakini kwa kweli kwenye BRN tumekubalianasuala kubwa la msingi ni kuboresha mfumo wetu wa elimu.BRN ina maelezo mengi sana ambayo inatakiwa itekeleze ilikuifanya elimu iweze kuboreka. Sasa tunazungumza matumizini makubwa, juzi Waziri Mkuu alinituma kwenda kufunguamkutano wa Walimu kule Arusha, nikaenda kuwasikiliza walahawana hoja nyingine isipokuwa mshahara tu, tunatakamshahara zaidi. Nikawaambia nitaenda kumwambiaaliyenituma, lakini ukiongeza mshahara wa Walimu ndiyounaongeza matumizi ya kawaida vilevile. Kwa hiyo, yakomambo ambayo huwezi kuyakwepa.

Mheshimiwa Spika, nihitimishe maelezo haya kwakusema kwamba tumefaidika kwa kiwango kikubwa tu namaelezo ambayo yametolewa na wadau mbalimbali katikasuala hili na wengine ambao wamelieleza kutoka katikaWizara husika, wamenisaidia sana ili kupunguza maelezoyanayotakiwa.

Mheshimiwa Spika, kuhusu BRN kuna wenginewanakosea kwa kweli, wanafikiri BRN ni Mpango, wanasemampango huu mpya. Wengine wanasema mlisema KilimoKwanza, mmeacha tena mnasema Matokeo Makubwa Sasa,

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU)]

248

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

jamani! Matokeo Makubwa Sasa siyo Mpango wa Maendeleo,ule ni mfumo wa kufuatilia maendeleo ili yaweze kutekelezwakama yalivyopangwa. Mpango ni ule wa miaka mitano, hatazile labs haziongezi mipango, zinatafsiri utekelezaji wamipango iliyopo. Unasema nishati tufikie MW 2780 ifikapomwaka 2015/2016. Zile labs zinasema miradi gani tufanyekuweza kufikia lengo. Mpango unasema tujenge reli ya kati,lab inasema mambo ya kufanya ili reli ya kati iweze kuimarikani moja, mbili, tatu. Pale haufanyi Mpango, pale unatafsiriMpango halafu baada ya kutafsiri kwenye mpango BRNwanafuatilia sasa kuona ya kwamba ile kazi ambayowamefanya kwenye lab katika kutafsiri Mpango waMaendeleo wa Miaka Miatano inatekelezwa namna gani.Hiyo, ndiyo shughuli lakini siyo kwamba tukisema Tekelezakwa Matokeo Makubwa Sasa, basi hiyo ni sawasawa naKilimo Kwanza, aah bwana! Hilo nalo ni jina la mfumo, lakinimambo mengine yanakwenda kama yalivyopangwa.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo,nikushukuru tena kwa kunipa nafasi na nimalize kwa kusematumefaidika na maelezo yaliyotolewa na ufafanuzi ulenadhani unatuweka katika mazingira mazuri ya kupangaMpango wa Maendeleo.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, naombakutoa hoja. (Makofi)

MHE. WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI:Mheshimiwa Spika, naafiki!

SPIKA: Hoja imeungwa mkono, sasa nawahoji kuhusuhoja hii.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa waMwaka 2014/2015 yalipitishwa na Bunge)

[WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU)]

249

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kwa hiyo, Kamatiyetu ya Mipango tumetoa maoni yetu kwa Serikali ilikuboresha Mpango ule utakaohusika. Kwa hiyo, wataendeleana shughuli zao na sisi itakapofika mwezi Machi tunaendeleana mzunguko wetu wa bajeti. Kwa hiyo, kwa sababu yaKatiba tunakusudia kuwa na Bunge karibuni kusudi tumalizeshughuli zetu halafu tuachie ukumbi kwa ajili ya Bunge. Kwahiyo, Mpango huu kama alivyosema ni mapendekezoambayo mmetoa na wataendelea kuyafanyia kazi katikakuimarisha Mpango ambao utatengenezewa bajeti katikamwaka unaokuja.

Kwa hiyo, tuwashukuru sana Mheshimiwa Waziri waNchi na wataalam wako wote wa Tume ya Mipango, kwakazi nzuri na muendelee kufanya hivyo kusudi hatimayetuweze kuboresha namna ya kupanga mipango yetu nakuweza kusimamia bajeti yetu kama inavyostahili tuwe navitu ambavyo kila mtu anaweza kuelewa ni kitu ganitunafanya, tunakwenda wapi na tunamalizia wapi. Kwa hiyo,tunawapongeza kwa hatua hii ya kwanza, muendelee vizurihuko mnakoendelea. Huu ni mwanzo wa kazi na ndiyomwanzo wa budget cycle, kwa hiyo, tunawatakieni hheri.

Waheshimiwa Wabunge, ilipaswa siku ya kwanzatumeanza Bunge kutangaza haya lakini kidogo tulighafirika.Katika Mkutano wa Kumi na Mbili, Bunge lilipitisha Muswadawa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba(The Constitutional Review Amendment Bill 2013.

Kwa taarifa hii, napenda kuliarifu Bunge hili Tukufukwamba Muswada huo umekwishapata kibali chaMheshimiwa Rais na kuwa Sheria iitwayo Sheria ya Mabadilikoya Katiba Na.6 ya Mwaka 2013 (The Constitutional ReviewAmendment Act No. 6 of 2013). (Makofi)

Kwa hiyo, Mheshimiwa Rais alisaini na kwa maanahiyo haizuii kufanya mabadiliko, lakini Sheria kamailivyopitishwa na Bunge imeishasainiwa. Kama kuna haja ya

250

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

mabadiliko basi yanaweza kuja, lakini sheria ile ilisainiwa.Kwa hiyo, naomba niseme hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri wa Nchi, hoja ya kuhairisha Bunge.

KUAHIRISHA BUNGE

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, UWEKEZAJINA UWEZESHAJI: Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuniya 28(7), naomba kutoa hoja ya kuahirisha Kikao cha Bungehadi kesho tarehe 5 Novemba, 2013.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI:Mheshimiwa Spika, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

SPIKA: Hoja imeungwa mkono, Mheshimiwa EsterBulaya.

MAELEZO YA BINAFSI

Maelezo ya Mheshimiwa Ester A. Bulaya KuitakaSerikali Kufanya Mabadiliko ya Sheria ya Dawa

za Kulevya na Kuanzisha Mahakama Maalum yaKushughulikia Wahalifu wa Dawa za Kulevya

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Spika, kwa mujibuwa Kanuni za Kudumu za Bunge, Kanuni 28(8), napendakutoa Maelezo Binafsi.

Mheshimiwa Spika, lakini pia naomba maelezo yanguyote yarekodiwe kama ambavyo nimeyawasilisha, kutokanana muda nimetengeneza summary ambayo nitaisoma,inaendana na maelezo ambayo nimewasilisha katika ofisiyako.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 28(8)ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la mwaka 2013,

[SPIKA]

251

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

napenda kutoa Maelezo Binafsi ya juu ya tatizo sugu lauagizaji, uuzaji na usafirishaji wa dawa za kulevyalinaloongezeka kwa kasi kubwa nchini, lengo likiwa ni kuitakaSerikali ifanye mabadiliko/marekebisho ya Sheria ya Dawaza Kulevya na Kuanzisha Mahakama Maalum kushughulikiawahalifu wanaojihusisha na usafirishaji na biashara ya dawaza kulevya.

Mheshimiwa Spika, nimeona ni wakati muafaka kutoamaelezo haya, ili Bunge lako Tukufu na Serikali ipate fursa yakuona uzito wa tatizo hili kutokana na ukweli kwamba katikamiaka ya karibuni tatizo la dawa za kulevya katika nchi yetulimeongezeka kwa kasi ya ajabu hali inayopelekea atharikubwa za kiuchumi, kijamii na kiafya. Mbaya zaidi kundikubwa linaloathirika ni kundi la vijana ambao ndio nguvukazi ya Taifa letu. Mbaya zaidi, sasa hivi, wafanyabiasharahawa wa dawa hizi haramu wameanza kuwatumia watotowa shule za msingi chini ya falsafa yao mpya “wapatewakiwa wadogo… wafanye watumwa wa dawa za kulevya…na kupata uhakika wa soko la baadaye pale ambapowatakuwa wameajiriwa au wamejiajiri”. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tafiti za hivi karibuni za Umoja waMataifa (World Drug Report, United Nations Office on Drugsand Crime (UNODC), 2013) zinaonyesha kwamba kunaongezeko kubwa na la kutisha katika matumizi ya dawa zakulevya aina ya Heroin na kwa njia ya kujidunga katika nchiza Kenya, Libya, Mauritius, Shelisheli na Tanzania (Chris Beyrerand others. “Time to Act: a call for comprehensive responsesto HIV in people who use Drugs “, The Lancet, Vol .376. No.9740 (14th August 2010) pp 551-563). Halikadhalika, Ripoti yampya ya hivi karibuni ya ofisi ya Umoja wa Mataifa yakupambana na mihadarati na uhalifu (UNODC), imetamkabayana kwamba Tanzania ni kinara wa kupitisha dawa zakulevya katika nchi za Afrika Mashariki na Mkoa wa Tangaukitajwa kama Mkoa hatari zaidi!

Mheshimiwa Spika, ripoti hiyo inasema jumla ya Tani64 za dawa za kulevya aina ya Heroin ilisafirishwa bilakukamatwa kwenda au kupitia Afrika Mashariki ikiwamo

[MHE. E A. BULAYA]

252

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Tanzania kati ya 2010 na 2013. Kwa Mkoa wa Tanga, ambaoumetajwa wazi kama eneo hatari zaidi Afrika Masharikiwastani wa ukamataji wa shehena za dawa za kulevyaeneo hilo umefikia kilogram 1,011 mwaka 2013 toka kilogram145 mwaka 2010 na kwamba Dola za Kimarekani takribanmilioni 160 zinatumiwa na Watanzania na Wakenya kilamwaka kwa utumiaji na usafirishaji kwa mwaka! Hili siojambo la kufumbia macho, lazima tuchukue hatua sasa.

Mheshimiwa Spika, lazima tuchukue hatua sasa, kwasababu kama nilivyoainisha hapo juu kwamba kwa kipindicha miaka mitatu tu (2010-2013), wakati Tani 64 za dawa zakulevya zilipita bila kukamatwa…zikiwa mtaani zikiharibuvijana na watoto wetu katika kipindi hicho hicho, kiasikilichoweza kukamatwa ni tani 1.6 tu! Takwimu hizo za kutishazinatoa picha kwamba sehemu kubwa ya shehena za dawaza kulevya hupitishwa bila kugundulika au kukamatwa navyombo vya dola!

Mheshimiwa Spika, taswira ya nchi katika Jumuiya yaKimataifa. Maelfu ya Watanzania wanatumikia vifungombali mbali ikiwamo vifungo vya maisha nje ya nchi,wengine wengi wamepoteza maisha kwa kunyongwa.Nitatoa mifano michache; China peke yake inasemekanakuna wafungwa 176 (99% - dawa za kulevya). Taarifa kwamujibu wa Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Kimataifa, Ndugu Mkumbwa Ally. Brazil kunawafungwa zaidi ya 103 (Takwimu za Tume ya Kuratibu udhibitiwa Dawa za Kulevya nchini na Hong Kong kuna zaidi yaWatanzania 200 wenye kesi za dawa za kulevya, ambapo130 zimeshakwisha hukumiwa na kesi 70 zikiwa zinaendelea!

Mheshimiwa Spika, aibu ya hivi karibuni, ambayohatuwezi kuikwepa ni meli iliyosajiliwa Tanzania (upandewa Zanzibar- MV Gold Star) iliyoripotiwa kukamatwa nchiniItalia ikiwa imesheheni tani 30 za dawa za kulevya zenyethamani ya pauni milioni 50 (sawa na bilioni 123 zaKitanzania).

[MHE. E A. BULAYA]

253

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Spika, uhalifu huu unaofanywa namtandao huu wa watu wachache, lakini wenye nguvuumewafanya Watanzania wanaokwenda nje ya nchikudhalilika kutokana na upekuzi unaofanywa dhidi yao kwahofu kwamba yawezekana na wao wamebeba dawa hizoharamu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hali ya dawa za kulevya.Changamoto ya dawa za kulevya sio tatizo letu peke yetuni tatizo ambalo hata Jumuiya ya kimataifa imekuwaikipambana nalo kwa kipindi kirefu kwani tafiti zinaonyeshakwamba asilimia tano ya idadi ya watu wazima duniani(watu takribani milioni 230) wanakadiriwa kutumia dawa zakulevya.

Mheshimiwa Spika, tukiwa sehemu ya Jumuiya hii yaKimataifa, Waheshimiwa Wabunge mtakumbuka kuwatarehe 19 Desemba, 1988 Jumuiya ya Kimataifa ilipitishaMkataba wa kupambana na dawa za kulevya yaani UnitedNations Convention Against Illicit Traffic in Narcotic Drugs andPsychotropic Substances. Tanzania ni sehemu ya Mkatabahuo na hili limewekwa wazi hata kwenye kifungu cha 55 chaSheria ya Kuzuia Dawa za Kulevya [sura 95 ya sheria zetu kamazilivyorekebishwa mwaka 2002]. Mkataba wa mwaka 1988ulikuwa unakazia zaidi Mkataba wa mwaka 1961 (SingleConvention on Narcotic Drugs, 1961), Itifaki (Protocol) za 1972zil izofanyia marekebisho Mkataba wa mwaka 1971(Convention on Psychotropic Substances, 1971). Licha yajuhudi zote, tatizo la uuzaji na usafirishaji wa dawa za kulevya,limezidi kuwa kubwa.

Mheshimiwa Spika, hali ya dawa za kulevya nchini namadhara kwa afya ya biandamu. Mwaka 1995 tulitungaSheria ya Kuzuia Biashara ya Dawa za Kulevya ambayo ilianzakufanya kazi mwaka 1996 kupitia GN.No.10/1996. Sheria hiyoinatumika Bara na Zanzibar. Kabla ya Sheria hiyo tulikuwatuna Sheria iitwayo The Dangerous Drugs Ordinance (Cap.95).Pamoja na kutungwa kwa Sheria mpya, tatizo la dawa zakulevya limeendelea kuwa kubwa zaidi hapa nchini.Ukamataji wa dawa za kulevya kwa miaka ya nyuma ilikuwa

[MHE. E A. BULAYA]

254

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

kidogo na idadi ya walioathirika (wateja) ilikuwa ni ndogokulinganisha na sasa hivi.

Mheshimiwa Spika, ni kwa bahati mbaya sana, lichaya ukubwa wa tatizo, pamoja na athari zake kwa jamii yaWatanzania, hakuna tafiti zinazoonyesha ukubwa wa tatizokwa nchi nzima, tafiti nyingi zilizofanywa zimejikita katikamaeneo machache yaliyoathirika zaidi na dawa za kulevya.(Kwa mwaka 2012 kumekuwa na huduma za kijamii kwawatumiaji wa dawa za kulevya ambapo waaathirika 27,176walionwa katika asasi zilizo chini ya Tanzania Aids PreventionProgramme (TAPP). Kwa mwaka 2013 hadi mwezi Septemba,2013, mpaka sasa kuna clinic mbili zinazotoa huduma zadawa za kulevya ambapo Muhimbili ina waathirika 576 naMwananyamala 376. Idadi ya waathirika walioonwa nakupata huduma hadi mwezi Septemba, 2013 ni waathirika15,106 kwa Mkoa wa Dar es Salaam).

Mheshimiwa Spika, tafiti zinaonyesha kwamba dawazinazotumika kwa wingi ni bangi, mirungi, heroine,mihadarati, vidonge na cocaine. Tafiti iliyofanywa na Shirikala Umoja wa Mataifa linalohusika na mapambano dhidi yadawa za kulevya UNODC (United Nations Office on Drugsand Crime) zinaonyesha kwamba 0.2% ya Watanzania,ambao ni karibia watu milioni 1.2 wameshawahi kutumiadawa za kulevya aina ya heroine.

Mheshimiwa Spika, halikadhalika, Shirika la AfyaDuniani (World Health Organisation -WHO) linaripoti kuwatakribani 0.2% ya Watanzania wameathirika na Ugonjwa waTB na takwimu za kitaifa katika program ya Kifua Kikuu naUkoma Tanzania zinaonyesha maambukizi ya TB ni 0.4% wakatitafiti katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili inaonyeshakwamba maambukizi ya TB kwa wanaotumia dawa zakulevya ni 11% ambayo ni mara 44 zaidi ya kiwango chamaambukizi kwa watu ambao hawatumii dawa za kulevya.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa maambukizi yaUKIMWI, takwimu za mwaka 2011/2012 za TACAIDS,zinaonyesha kwamba 5.1% ya Watanzania wameathirika na

[MHE. E A. BULAYA]

255

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

virusi vya UKIMWI wakati tafiti ndogondogo zinaonyeshamaambukizi ya virusi ya UKIMWI kwa watu wanaotumia dawaza kulevya ni mara 10 zaidi ya maambukizi ya kawaida. Kwamfano 51.9% ya wanaotumia dawa za kulevya kwa njiakujidunga sindano, 37% wanaotumia dawa za kulevya kwanjia ya kuvuta na kufanya biashara ya ngono na 22.6% kwawanaotumia dawa za kulevya kwa njia ya kuvuta.

Mheshimiwa Spika, madhara ya kiafya kwa utumiajiwa dawa za kulevya sio tu katika magonjwa ya TB namaambukizi ya virusi vya UKIMWI, bali pia katika homa yaini. Japokuwa hakuna tafiti za kitaifa zilizofanyika kuhusianana mchango wa matumizi ya dawa katika homa ya ini, tafitindogondogo za mwaka 2012 zinaonyesha kati ya 65% mpaka75.6% ya watumiaji wa dawa za kulevya wameathirika kwahoma ya ini, hasa homa ya ini aina ya Hepatitis. Homa ya inini hatari sana katika kupata magonjwa sugu ya ini ikiwepokansa ya ini na ini kushindwa kufanya kazi.

Mheshimiwa Spika, ukubwa wa tatizo na utendaji wavyombo vya dola. Kesi kubwa ya kwanza inayohusu dawaza kulevya ni ile ya mfanyabiashara NURDIN AKASHA @HABABV.R [1995] TLR. 227 (CAT) ambaye tarehe 20/7/1993 alikamatwanyumbani kwake Msasani Village akiwa na paketi 105 zamenthaqualone (mandrax) alizoziingiza nchini kutokaMombasa akitumia malori yake. Sasa hivi tunaongeleauingizaji wa kilo kadhaa za dawa za kulevya na siyo paketitena.

Mheshimiwa Spika, mwezi Machi, 2010 kilo 92 za dawaza kulevya aina ya Heroine zilikamatwa maeneo ya Kabuku,Mkoani Tanga na tayari washitakiwa watano wanatumikiakifungo. Tarehe 19/12/2010, kilo 50 za dawa za kulevya ainaya Heroine zilikamatwa tena Wilayani Handeni, Mkoa waTanga. Mwezi Septemba, 2011, kilo 179 za dawa za kulevyaaina ya Heroine zilikamatwa Dar es Salaam. Tarehe 14/6/2011,kilo 35 za dawa za kulevya aina ya Heroine zilikamatwaMkoani Mbeya na tarehe Januari kilo 211 za dawa za kulevyazilikamatwa Mkoani Lindi.

[MHE. E A. BULAYA]

256

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Spika, utendaji wa Ofisi ya DPP.Natambua jitihada zinazofanywa na baadhi ya watendajiwa Serikali ya Awamu ya Nne katika vyombo vya dola kwakufanikisha jit ihada za kuwakamata watuhumiwawanaojihusisha na dawa za kulevya. Kutokana na jitihadahizo, kuanzia mwaka 2008 mpaka mwaka huu wa 2013,watuhumiwa wa dawa za kulevya ni kama ifutavyo:-

(i) Cocaine kilo 395 zilikamatwa na washitakiwawaliokamatwa ni 1074.

(ii) Heroine ki lo 768.8 na washitakiwawaliokamatwa ni 1130.

(iii) Mirungi kilo 56,562 na washitakiwawaliokamatwa ni 3,712.

(iv) Bangi kilo 487,472 sawa na tani 487 nawashitakiwa waliokamatwa ni 20,255.

(v) Mandrax kilo 5 na gramu 9 na washitakiwawaliokamatwa ni 20.

Mheshimiwa Spika, licha ya juhudi za baadhi yawatendaji waaminifu kuwakamata watu walioko katikamtandao huu hatari kumekuwa na hujuma za dhahiri dhidiya wanaopambana na dawa za kulevya. Moja kati ya ofisiinayoshutumiwa kuwa na maafisa wanaoshirikiana nawanamtandao, ni ofisi ya DPP.

Mheshimiwa Spika, mtandao katika Ofisi ya DPP naMahakama. Natambua kazi nzuri na jitihada zinazofanywana baadhi ya watumishi wazalendo kwa upande kwa Ofisiya Muendesha Mashtaka, Majaji na Mahakimu waaminifu.Hata hivyo, katika ofisi hizo za umma, kumekuwa na baadhiya watumishi ambao wamekuwa wakihujumu kesi za dawaza kulevya kwa kushirikiana na watuhumiwa katika kupangajinsi ya kuwasaidia washinde kesi kwa kuwapatia taarifa zasiri zinazohusiana na ushaidi na jinsi ya kuharibu ushahidinzima.

[MHE. E A. BULAYA]

257

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

Mheshimiwa Spika, kutokana na kupanuka kwamtandao huu wa kuhujumu, licha ya kushirikiana nawashtakiwa, mtandao uliopo katika Ofisi hiyo ya DPPumekuwa ukituhumiwa kufanya njama za kushirikiana nabaadhi ya watumishi wa Mahakama hasa Majaji kuhamishakesi kupeleka kwa Majaji ambao wanadaiwa kuhusika namtandao huu (sihitaji kutaja majina ya Majaji hapa, baadhiyao wanafahamika na wengine wametajwa mara kadhaana vyombo vya habari).

Mheshimiwa Spika, kwa kutumia mtandao huo,baadhi ya Majaji wamekuwa wanatafsiri sheria kwa jinsiwanavyotaka na kuwapa dhamana watuhumiwa wa kesiza dawa za kulevya ambazo hazina dhamana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mfano mzuri ni kesi Na.6/2011,Jamhuri dhidi ya Fred William Chonde na wenzake ambaowalikutwa na kilo 179 za Heroine yenye thamani ya shilingibilioni 6.5. Washtakiwa hawa wanashitakiwa kwa kosa lakusafirisha dawa za kulevya ambalo kwa mujibu wa kifungucha 148(5)(a)(ii) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinaipamoja na kifungu cha 27(1)(a) cha Sheria ya KuzuiaUsafirishaji wa Dawa za Kulevya halina dhamana.

Kwa tafasiri yoyote ile aliyokuwa nayo MheshimiwaJaji, bado asingewapa dhamana kwani kifungu cha148(5)(a)(iii) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai nakifungu cha 27(1)(b) cha Sheria ya Kuzuia Usafirishaji wa Dawaza Kulevya kinazuia dhamana kwa kosa ambalo thamaniya dawa za kulevya inazidi shilingi milioni kumi. Kutokanana Mahakama kutoa dhamana, washtakiwa wawili raia yaPakistani wametoroka na hawapo tena nchini.

Mheshimiwa Spika, aidha, katika kesi ya R. v. MwinyiRashid Ismail @Mkoko, (KLR /IR 4143/2011), mshtakiwaaliomba dhamana Mahakama Kuu wakati kesi ilikuwa badoipo Mahakama ya Kisutu ndipo Wakil i wa Serikaliakamwambia Jaji kuwa anaomba kuifuta. Mheshimiwa Jaji,huku akifahamu kuwa kesi hiyo imefika mbele yake kwa ajiliya kusikiliza maombi ya dhamana tu na kuwa ilikuwa

[MHE. E A. BULAYA]

258

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

haijafikishwa Mahakama Kuu kwa taratibu wa sheria,aliamua kumfutia kesi mshtakiwa na kuamuru kuwa yukohuru.

Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo, katika kesi No.794/2011 katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, MheshimiwaHakimu aliwafunga kifungo cha nje kwa miezi kumi na tanowashtakiwa Abdurahman Shaban Sindanema, Said NassoroKhamis na Abdurahim Haroub Said waliokiri kosa la kuuzana kusambaza dawa za kulevya aina ya Heroine. Adhabuiliyotolewa na Hakimu huyu, haipo kwa mujibu wa sheria.Kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha Sheria ya Kuzuia Dawaza Kulevya, adhabu iliyowekwa kwa wauzaji au wasambazajiwa dawa za kulevya ni kifungo cha maisha na si chini yamiaka ishirini (20) jela kwa kipindi hicho.

Mheshimiwa Spika, kesi nyingine ni Na. 274/2005Jamhuri dhidi ya Yusuph Hashim Nyose aliyekamatwa na kilo1.3 za dawa za kulevya aina ya Heroine alizokuwa amemezana kisha kuzitoa kupitia njia ya haja kubwa baada yakukamatwa na zilikuwa na thamani ya shilingi milioni kumina mbili na laki sita (12,600,000/=). Pamoja na ushahidiuliotolewa Mahakamani na mashahidi sita (6) wa upandewa Jamhuri ikiwa ni pamoja na Mkemia aliyethibitisha kuwani dawa za kulevya na mashahidi walioshuhudia mshtakiwaakizitoa kwa njia ya haja kubwa, Hakimu alimuachilia huru.

Mheshimiwa Spika, katika hukumu yake Hakimualisema kuwa ameridhika kuwa hizo ni dawa za kulevya nazina madhara kwa binadamu na kuwa hana ubishi kuwamshtakiwa alikutwa nazo. Hata hivyo, alimuachilia huru kwakuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuelezea mbinuwalizotumia kumgundua mshtakiwa kuwa alikuwaamebeba dawa za kulevya kabla ya kumkamata.

Mheshimiwa Spika, mfano mwingine ni hukumuiliyotolewa tarehe 4/5/2007 inayoihusisha Jamhuri dhidi yaChriswell Simon Mobini (561/2007) ambapo mtuhumiwaalikamatwa tarehe 9/4/2007 katika uwanja wa JKNA akiwana pipi 93 aina ya Heroine yenye thamani ya zaidi ya shilingi

[MHE. E A. BULAYA]

259

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

milioni 30 za Kitanzania. Watuhumiwa hawa walifikishwaMahakama ya Kisutu na kufunguliwa mashtaka chini yakifungu 16 (1) (b) (i) cha dawa za kulevya.

Mheshimiwa Spika, katika shauri hil i, Hakimualimwachia huru baada ya mshtakiwa kulipa faini ya shilingimilioni moja za Kitanzania kwa maelezo kwamba kwakumtazama tu mtuhumiwa, anaonekana ni mgonjwa wavidonda vya tumbo na hivyo hawezi kupata huduma nzuriiwapo atapelekwa rumande! Hii ni mifano michache tu katiya mingi iliyopo! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kesi zilizopo Mahakamani. Kamanilivyoainisha hapo juu na ili kuonyesha msisitizo, naombanirejee takwimu husika kama ifuatavyo, kwamba kati yawatuhumiwa 26,191 waliokamatwa mpaka sasa, kuna jumlaya kesi 89 tu zinazosubiri kusikilizwa Mahakamani. Katika vikaovya Mahakama Kuu vilivyokaa kuanzia mwezi Agosti hadiOktoba, 2013 hakuna kesi hata moja ya dawa za kulevyailiyosikil izwa na kutolewa hukumu, japo zil ikuwazimepangwa.

Mheshimiwa Spika, dhana ya uhuru wa Mahakama.Natambua kuwa Mahakama ni mhimili unaojitegemea katikakutenda shughuli zake na iko huru. Natambua pia kuwaBunge haliwezi kuingilia shughuli za Serikali au Mahakamalakini pamoja na uhuru huo, Bunge hili limekuwa linakosoaSerikali pale linapoona imekosea. Kwa ujumla, lazima kuwena checks and balance. Pamoja na upungufu niliyoelezeahapo juu kuhusiana na mwenendo wa Mahakama katikakusikiliza kesi za dawa za kulevya, Mahakama imekuwainafanya kazi zake bila kukosolewa na chombo kingine nandiyo maana baadhi ya watumishi wamekuwa wakitumiadhana ya uhuru wa Mahakama vibaya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kutokana na matumizi mabayaya uhuru wa Mahakama kwa baadhi ya watumishi waMahakama, ni mapendekezo yangu kwamba Serikali iundeTume Maalumu ya Kiuchunguzi kuchunguza mwenendo wakesi hizi za dawa za kulevya ili watakaobainika kuwa

[MHE. E A. BULAYA]

260

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

wametumia nafasi/wadhifa/madaraka yao vibayawachukuliwe hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuvuliwamadaraka waliyonayo. Kwa kufanya hivyo, itaonyesha kuwahakuna aliye juu ya sheria na itakuwa ni fundisho kwawengine na taarifa ya Tume iletwe katika Bunge lako Tukufukwa hatua zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kesi kusikilizwa na Mahakimuwasio na mamlaka. Kwa ujumla watuhumiwa wotewanaokamatwa wakisafirisha dawa za kulevya hutakiwakufunguliwa mashtaka chini ya kifungu 16(1)(b)(i) cha Sheriaya Dawa ya Kulevya. Kosa hili halina dhamana na husikilizwana Mahakama Kuu peke yake. Hata hivyo baadhi yaMahakimu wamekuwa wakilisikiliza kesi hizo na wenginekushirikiana na Waendesha Mashtaka hubadilisha Hati yaMashtaka na kufanya wawe na mamlaka ya kusikiliza kesihizo. Mfano ni shauri la Jamhuri dhidi ya Shirima (CC 433/2009).

Mheshimiwa Spika, katika shauri hili, mtuhumiwaalikamatwa tarehe 2/05/2009 katika Bandari ya Dar esSalaam akiwa na kilo moja ya Heroine yenye thamani yaTshs.18,000,000/=…Tarehe 5/05/2009 alifikishwa Mahakamanina kufunguliwa mashtaka chini ya kifungu cha 16(1)(b)(i) chaSheria ya Dawa ya Kulevya. Tarehe 9/05/2009 Hati ya Mashtakailibadilishwa na mashtaka kuwa chini ya kifungu 12(d) yaSheria ya Dawa za Kulevya. Tarehe 14/7/2009 aliamriwa kulipafaini ya Tshs.4, 000,000. Ubadilishwaji wa vifungu vya sheriakatika hati ya mashtaka hulenga kuwasaidia watuhumiwawashtakiwe na makosa madogo badala ya yale makubwayenye adhabu kubwa kisheria.

Mheshimiwa Spika, kifungu cha 16(1)(b)(i) cha Sheriaya Dawa za Kulevya kinataja kosa la dawa za kulevya kuwakosa ambalo halina dhamana. Hivyo Waendesha Mashtakakwa kushirikiana na watuhumiwa, hupendelea kuwafunguliamashtaka madogo chini ya kifungu cha 12(d) cha Sheria yaDawa za Kulevya. Katika kesi ambazo watuhumiwawalifunguliwa mashtaka chini ya vifungu ambavyohaviendani na makosa yao halisi, Mahakama zimekuwa

[MHE. E A. BULAYA]

261

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

zikitoa adhabu ndogo ya faini na kuwaachia huru! Tenakatika mazingira mengine, kutoa hukumu ndogo kulikoambayo imeainishwa katika sheria.

Mheshimiwa Spika, upungufu wa Sheria. Sheria yaKuzuia Dawa za Kulevya haina adhabu kwa mtuanayesafirisha au anayekutwa na kemikali bashirifu (chemicalprecursors). Kemikali hizi ni muhimu sana katika kutengezadawa za kulevya aina ya Heroine na Cocaine, crystal-methamphetamine. Muathirika wa dawa crystal-methamphetamine hawezi kutibika maishani mwake(permanent brain damage). Kwa sasa hivi kuna wimbi kubwala uingizaji wa kemikali hizo zinazoenda kuangamiza nguvukazi ya Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, miongoni mwa matukio yauingizaji na usafirishaji wa kemikali hizo ni kesi ya Saada AllyKilongo aliyekamatwa uwanja wa ndege wa J.K. Nyerereakiwa na 10 kilo za Ephedrine. Nyingine ni kesi ya Agnes GeraldDelwaya (Masogange) na mwenzake waliokamatwa AfrikaKusini wakiwa na kilo 150 za Ephedrine. Aidha, RumishaeliMamkuu Shoo na mwenzake wamekamatwa kwenyeKiwanda cha kutengeneza Ephedrine nchini Kenya na tayarialikuwa na kilo hamsini (50) za kemikali hizo. Hawa watulicha ya madhara makubwa waliolitelea Taifa, wako mtaaniwanapeta na kujipongeza! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama hatutarekebisha sheriamapema iwezekanavyo, tutajikuta tunakuwa na kiwandaau viwanda vya kutengeneza dawa za kulevya hapa nchini.Hivyo, wauzaji badala ya kuagiza dawa hizo nje ya nchi,wataanza kutengeneza hapa na kuna taarifa kwamba pindidawa za kulevya zinapokosekana, wafanyabiashara huuzakemikali hizo na watumiaji wanatengeza wenyewe nakutumia.

Mheshimiwa Spika, kutokana na upungufu uliojitokezakama hoja yangu ilivyoeleza, naomba Serikali ifanye mamboyafuatayo:-

[MHE. E A. BULAYA]

262

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

1. Iunde Mahakama Maalum, harakaiwezekanavyo itakayokuwa na jukumu la kushughulikia kesiza dawa za kulevya tu kama ilivyo Mahakama ya Biasharana iliyokuwa Mahakama ya Ardhi. (Makofi)

2. Ifanye marekebisho ya Sheria ya Dawa zaKulevya kwa kuongeza makosa ya kusafirisha, kuuza aukukutwa na kemikali bashirifu. (Makofi)

3. Iundwe Tume ya kuchunguza baadhi ya watendajiwa Mahakama na Serikali ambao kwa makusudi wamekuwawakihujumu kesi za dawa za kulevya pamoja na jitihada zaSerikali katika kupambana na biashara hii haramu na kuletataarifa katika Bunge hili Tukufu. (Makofi)

4. Kiundwe haraka chombo huru chenye nguvuna mamlaka kamili kitakachokuwa na dhamana yakupambana na dawa za kulevya nchini.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. (Makofi)

(Hapa baadhi ya Wabunge walisimama kuunga mkonoMaelezo Binafsi ya Mheshimiwa Ester A. Bulaya)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, Maelezo Binafsihusimami wala hatujadili. Ndiyo ameshajieleza hivyo basi.Someni kifungu kinachohusika, ameshajieleza, ndivyoalivyoomba na amemaliza. (Makofi)

Kulikuwa na hoja ya Kuahirisha Bunge na ndiyoninayowahoji sasa. Hoja ilitolewa na Waziri wa Nchi kuhusuKuahirisha Bunge mpaka kesho saa tatu asubuhi.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

[MHE. E A. BULAYA]

263

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

SPIKA: Hamwezi kulala, hatuna hoja nyingine,naahirisha Bunge mpaka Kesho saa tatu asubuhi.

(Saa. 1.35 Usiku Bunge liliahirishwa Mpaka Siku yaJumanne, Tarehe 5 Novemba, 2013, Saa Tatu Asubuhi)