Matambiko Katika Jamii yA Wasambaa
-
Upload
independent -
Category
Documents
-
view
6 -
download
0
Transcript of Matambiko Katika Jamii yA Wasambaa
SURA YA KWANZA
UTANGULIZI WA UTAFITI
1.1Utangulizi
Utafiti huu ulihusu nafasi ya matambiko katika jamii ya
wasambaa wanaoishi mkoani Tanga katika wilaya ya Lushoto
na ile ya Korogwe. Utafiti huu ulijikita zaidi katika
wilaya ya Lushoto hususani katika Tarafa ya Mtae na
katika kata ya Rangwi.
Utafiti huu umegawanyika katika sehemu tano; sura ya
kwanza ambayo imehusisha dhana na maana mbalimbali, usuli
wa utafiti, historia ya wasambaa, tatizo la utafiti,
malengo ya utafiti, maswali ya utafiti, umuhimu wa
utafiti, mipaka ya utafiti, nadharia ya utafiti na
hitimisho. Sura ya pili imehusisha mapitio ya machapisho
mbalimbali, sura ya tatu imehusisha mbinu za ukusanyaji
wa data, vyanzo vya data na taarifa, sampuli na
1
usampulishaji. Sura ya nne imehusisha uchambuzi wa data
na sura ya tano imehusisha muhtasari wa utafiti na
hitimisho.
1.1.2 Dhana ya Matambiko
Masebo, J. A. (2007), anasema, tambiko ni sadaka inayotolewa kwa
mwenyezi mungu, miungu au mahoka, mizimu na pepo kwao
binafsi au kupitia kwa mwenyezi mungu wakati wa kusalia
miungu.
Kitula, K. na Catherine, N. M. K (2010) wanasema, neno
matambiko linatokana na imani kuwa mababu waliofariki
wana uwezo wa kuona matendo ya watoto na wajukuu wao
walio hai. Inadhaniwa kuwa wanapokasirika watoto hupata
matatizo ya magonjwa, vifo na mabalaa mengine. Ili kupoza
hasira zao huko walikolala basi hupikwa pombe na vyakula
vinavyokwenda kumwagwa makaburini au kuliwa na waganga
ambapo vitendo hivyo ndio matambiko.
Wikipedia, kamusi elezo huru, wanasema, Kila kabila lina
aina ya matambiko linayofanya kulingana na mila zake na
aina ya matatizo.
2
Makabila ya maeneo ya Tanga, Pwani na Morogoro hufanya
matambiko yao makaburini, kwenye miti mikubwa, milimani,
mapangoni, ziwani, baharini, makaburini na porini na
kupeana majina maalum ya mababu na kuvaa kago (alama)
mikononi. Kwa wasambaa wale wanaohusika na shughuli ya
utekelezaji wa matambiko huwa wamevalia nguo maalumu
maarufu kama kaniki (hizi ni nguo kama kanga lakini
zinakuwa nyeusi). Wasambaa hushikamana na mila au
desturi, ngoma za mashetani, mizuka na vinyamkera vyao
kama alama ya kuwaheshimu na kuwaenzi mababu zao wa kale.
Kamusi ya karne ya 21 (2011) wanasema, tambiko ni sadaka
au ada inayotolewa kwa mwenyezi mungu, miungu, pepo au
mizimu moja kwa moja au kwa mungu kupitia kwa miungu.
Yapo matambiko yaliyotolewa na wazee maarufu waliopewa
jukumu hilo. Matatizo yaliyoshindikana kwa mababu zetu
yalipelekwa kwa miungu ili iwasaidie kuyatatua.
Assumpta, K.M. (2011) amebainisha baadhi ya sifa za
matambiko ambazo ni kama ifuatavyo;
3
I. Matambiko ni sanaa inayotendeka.
II. Matambiko hayatolewi na mtu yeyote bali na wazee
maarufu walioteuliwa na jamii husika.
III. Matambiko hufanywa mahali maalumu kama vile chini ya
mti mkubwa, makaburini, mapangoni, milimani, mtoni,
njia panda au hata porini kutegemeana na jamii
husika.
IV. Matambiko yaliandamana na sala na ni utanzu wa
maigizo ambao unaendelea kufa.
Masebo, J. A (2013) anasema matambiko yana umuhimu na
hasara katika jamii kama ifuatavyo;
Umuhimu wa tambiko
Matambiko hujenga imani kama chombo cha kutatulia matatizo ya
jamii husika.
Tambiko husaidia kuendeleza mila na desturi za jamii husika
Tambiko husaidia kujenga na kuimarisha mahusiaano miongoni
mwa wanajamii
Matambiko huiongoza jamii katika mapambano dhidi ya matatizo
mbalimbali yanayoikabili jamii.
4
Hasara ya matambiko
Matambiko hujenga dhana potofu katika jamii kwa kuamini
nguvu fulani bila kuwa na uhakika au uthibitisho wa
kisayansi
Matambiko huleta hasara kubwa kwa jamii husika kwani
kafara, sadaka, za matambiko inahitaji wanyama/vyakula
ambavyo watu hutumia pesa nyingi kuvipata vitu hivyo.
Matambiko huwafanya watu kuishi kwa wasiwasi mkubwa kwani
panapotokea tatizo na uwezo wa kufanya tambiko haupo
wanajamii hao hupatwa na hofu maishani kwa kushindwa
kutimiza yale wanayodhani wazee/mahoka wanahitaji
kufanyiwa.
Masebo, J. A (2013) anasema matambiko yana wahusika
maalumu na madhari/mahali maalumu kama ifuatavyo;
Wahusika
Hawa ni wale wazee maarufu walioteuliwa na jamii kuendeleza
shughuli za matambiko, si kila mtu katika jamii anaweza kufanya
tambiko.
5
Mandhari/Mahali
Tambiko linaweza kufanyika porini/msituni, njia panda, kwenye
miti mikubwa, kwenye mawe makubwa, makaburini, mapangoni,
mtoni, ziwani, baharini, kwenywe nyumba maalumu na mahali
popote kutegemeana na aina ya tambiko.
1.2 Usuli wa utafiti
1.2.1Historia ya wasambaa
Kirama, Kh. (1953) anasema, jamii ya wasambaa inapatikana
katika milima ya usambara kaskazini mashariki mwa
Tanzania.Wasambaa ni jina ambalo limetokana na neno
kusambaa. Inasemekana kwamba jamii hii asili yao ni Kenya
na walikuja katika milima ya usambara kukimbia vita baina
yao na wamasai wakiwa wanagombea malisho ya wanyama wao
na hatimaye wakajikuta wanavuka mbuga ya mkomazi na
kusambaa katika milima ya usambara na hatimaye ikawa
chimbuko la jina wasambaa kwa maaana ya kwamba wamesambaa
katika milima. Ambapo kwa sababu walisambaa karibu katika
kila safu nayo ikaitwa milima ya usambara. Kwa asili
wasambaa wapo katika aina zaidi ya kumi lakini wote
6
husikilizana kwa lugha moja-Kisambaa ambao ni; wasambaa
washee, wahea, wanango, ntandaa, wakijewa, wagamo,
wang’hwasho na wakilindi.
Wikipedia, kamusi elezo huru wanasema wasambaa ni kabila
kutoka eneo la Milima ya Usambara, kaskazini-mashariki ya
nchi ya Tanzania, mwaka 2001 idadi ya Wasambaa
ilikadiriwa kuwa 664,000. Wasambaa kama wanavyojulikana
sana wanaishi kwenye milima ya usambara na lugha yao
kubwa ni kisambaa. Wasambaa wamegawanyika katika koo
mbalimbali ndani ya jamii zao ambazo ndio utambulisho
wao. Koo au ukoo ni jambo la muhimu sana katika maeneo ya
usambaa kwani wanajamii wa kisambaa wanatambuana kwa
majina ya ukoo. Alama maarufu ya koo za kisambaa ni
majina yanayoanza na SHE kama, Shemboko, Shekiango,
Shekimwei, Sheiza, Shembilu, Shekinyashi, Sheshe,
Shedodo, Shekalage, Shekifu n.k koo nyingi za kisambaa
zinajulikana kwa kuanza na majina hayo na Lugha yao ni
Kisambaa.
7
Kirama, Kh. (1953) Chakula, kwa wasambaa chakula chao cha
asili ni ugali wa mhogo (bada) kwa maharage pamoja na
ugali wa mahindi kwa kweme au mbegu za maboga. Mavazi kwa
watu wa awali walikuwa wanavaa nguo ambazo zinatokana na
maganda ya miti ambayo yanasuguliwa na mafuta ya samli
mpaka yanakuwa laini na kuwa tayari kuvaliwa.Vazi hilo
linavaliwa na wanaume na wanawake lakini linakuwa na
majina tofauti kwa wanaume zinaitwa “UKOPA” na kwa
wanawake zinaitwa “VINGUNGU”Imani, wasambaa wanaamini juu
ya Mungu wa kweli ambaye ni Mungu wa juu/mbinguni na
duniani ndiye haswa wanayemuabudu. Lakini pia wanaamini
juu ya miungu, mashetani, mizimu na ndio haswa pia
wanaitambikia. Pia Wasambaa wanaamini mambo ya
kishirikina na uchawi. Shughuli za uzalishaji mali
wasambaa hujishughulisha zaidi na kilimo na ufugaji kama
shughuli zao kubwa. Katika kilimo hulima mazao ya aina
mbalimbali kama vile mihogo, mahindi, maharage, viazi
ambapo mazao hayo hutumika kama chakula chao kikuu, kwa
wasambaa kukosekana kwa mihogo na mahindi ni ishara ya
8
njaa. Kuoa na kuolewa mwanaume anayetaka kuoa humtuma
mshenga kwa wazazi wa msichana kueleza nia yake. Wazazi
wakikubali kwa kutambua umuhimu wa familia kama kuongeza
uzao wanakaa kifamilia, kisha watamtuma mjumbe, ambako
wanakula pamoja na kutajiwa mahari kulingana na utaratibu
wa kisambaa kuwataka upande wa kiume wapange siku ya
kwenda ‘kupiga hodi’ kwa mwanamke, siku hii ndipo
wataambiwa rasmi kwamba wamepata binti. Siku hiyo upande
wakike wataandaa chakula maalamu kwa wageni. Utawala
wasambaa wanauongozi ulio imara na wakuheshimiwa sana na
kiongozi wao anajulikana kama zumbe. Elimu wasambaa kama
makabila mengine wana elimu ya jando na unyago ambapo
vijana wakifikia umri stahili wanaingia jandoni na
sherehe kubwa hufanyika. Ngoma wasambaa wana ngoma yao
maarufu sana ambayo hujulikana kama mdumange ngoma hii
hupigwa katika shunghuli mbalimbali za kijamii. Kifo kwa
wasambaa wanaimani kuwa mtu mwema akifa kuna ishara
zinatokea kama mvua kubwa na mtu huyo anaenda mahali
pazuri ambapo wanaamini ni peponi lakini kwa mtu muovu
9
kuna ishara mbaya kama kaburi kuwa gumu katika uchimbaji,
kukutana na mwamba ndani ya kaburi, kutokea nyoka na
mambo kama hayo.
Wikipedia, kamusi elezo huru, wanasema, wasambaa ni
miongoni mwa makabila ambayo watu wake wamesoma. Wasambaa
pia ni kabila la watu wanaopenda haki yaani hawapendi
kuonewa wala kumuonea mtu.Wasambaa ni watu wa ushirikiano
sana na waonapo au kusikia mtu yeyote ana tatizo wapo
tayari kumsaidia. Kisiasa ni watu makini sana katika
kutawala na wana ushawishi mkubwa sana kwani walio wengi
wana busara na wanajua kusikiliza mambo kwa umakini pia
ni waadilifu sana na wanasimamia sheria na taratibu.
Katika utafiti huu mtafiti aliangalia wasambaa kwa ujumla
wao hivyo historia ya wasambaa itaegemea wasambaa kwa
ujumla wao. Kipindi kirefu sasa tangia miaka ya nyuma,
wataalamu mbalimbali walijitokeza na kujaribu kuangalia
na kufanya tafiti juu ya matambiko kama kipengele
kimojawapo cha fasihi simulizi. Wataalamu hao waliweza
10
kuangalia matambiko katika baadhi ya makabila na
waliangalia mambo mbalimbali zaidi ya matambiko
yanayofanywa baada ya kutokea ajali au mtu kunusurika
kufa.
Japo tafiti hizo mbalimbali zimeweza kufanyika na
kufanikiwa kwa kiasi chake, lakini bado kiu ya hadhira
haikuweza kukatwa kwa kuwa hakuna tafiti ambazo
zimeengalia kwa kina mambo kadha wa kadha yanayopatikana
katika dhana ya matambiko kama vile; vifaa vitumikavyo
wakati wa matambiko, wahusika wa matambiko, mandhari na
mambo mengine mengi ambayo katika utafiti huu mtafiti
amejaribu kupitia kwa kina mambo hayo muhimu.
1.3 Tatizo la utafiti
Tafiti mbalimbali zilishafanywa juu ya matambiko lakini
tafiti hizo zilijikita zaidi katika matambiko ya jamii
nyingine za kaskazini mashariki mwa Tanzania kama jamii
ya wachaga, wapare na wameru, hata hivyo tafiti ambazo
zishafanywa katika kabila la wasambaa zimejikita zaidi
11
katika asili ya aina fulani tu ya wasambaa wakilindi
ambapo kulingana na Khalidi Kirama (1953) anasema asili
ya wasambaa wakilindi ni handeni na wanatokana na mtu
aliyefahamika kama Mbegha. Mtafiti katika utafiti huu
alijikita zaidi kuangalia/kutafiti juu ya nafasi ya
matambiko katika jamii ya wasambaa, mazingira ambayo
matambiko hufanywa katika jamii ya wasambaa, vifaa
ambavyo vinatumika au ni maalumu katika kufanya matambiko
na mambo mengine yanayoendana na zoezi zima la matambiko
ambapo kwa hakika watafiti waliotangulia hawajawahi au
kufikia kuchunguza mambo kama hayo au hata kufanya
utafiti wa kina.
1.4 Malengo ya utafiti
Utafiti huu ulikuwa na malengo ya aina mbili, lengo kuu
moja na malengo mahsusi matatu
12
1.4.1 Lengo kuu
Kuchunguza nafasi ya matambiko katika jamii ya wasambaa
1.4.2 malengo mahsusi
I. Kuchunguza dhima/umuhimu wa matambiko katika kukuza
fasihi ya jamii ya wasambaa.
II. Kuchunguza vipindi, mazingira ambayo matambiko
hutekelezwa katika jamii ya wasambaa.
III. Kuchunguza na kubaini vifaa vinavyotumika katika
kutekeleza zoezi zima la matambiko katika jamii ya
wasambaa.
1.5 Maswali ya Utafiti
I. Matambiko yana dhima/umuhimu gani katika jamii ya
wasambaa?
II. Matambiko hufanywa vipindi na mazingira gani katika
jamii ya wasambaa?
III. Vifaa gani hutumika katika kutekeleza zoezi la
matambiko katika jamii ya wasambaa?
13
1.6 Umuhimu wa Utafiti
Utafiti huu ni muhimu kitaaluma kwa jamii wasambaa kwa
ujumla kwa sababu matambiko ni kipengele muhimu cha
fasihi simulizi kwani hutunza na kukuza historia ya jamii
ya wasambaa, wakiwa wanajua walikotoka walipo na
wanakoenda. Kwa kuwa matambiko hushughulikia maswala
kadha wa kadha yanayoikumba jamii husika kiimani na hata
kiitikadi.
1.7 Mipaka ya Utafiti
Utafiti huu ulijikita zaidi katika kuangalia kwa kina juu
ya nafasi ya matambiko katika kukuza fasihi simulizi ya
jamii ya wasambaa, vipindi na mazingira ambayo matambiko
hutekelezwa, wahusika pamoja na vifaa ambavyo hutumiwa
katika kukamilisha jambo hilo.
1.8 Nadharia ya Utafiti
14
TUKI (2009:63) wanasema nadharia ni taratibu, kanuni na
misingi ambayo imejengwa katika muundo wa kimawazo kwa
madhumuni ya kutumiwa kama kielelezo cha kuelezea jambo.
Kulingana na Massamba na wenzake.
1.8.1 Uhalisia Mazingaombwe/Uhalisia Ajabu (Magical
Realist Theory)
TUKI (2009) wanasema hii ni dhana iliyobuniwa na msanii
wa ujerumani Franz Roh, katika kitabu chake Nach-
expressionnism, magischer realismus. Probleme der neusten
europaischer malalerei. Dhana hii huhusishwa na waandishi
wa marekani ya kusini au hata nchi zinazoitwa ulimwengu
wa tatu na hutambulishwa na sifa mbalimbali. Sifa hizi ni
za kuyaelezea matukio ya kifantasia au ya ajabu au
kichawi kwa namna ya moja kwa moja kwa namna inayofanana
na yaonekana kama ya kawaida tu. Mpaka uliopo kati ya
mambo yanayoweza kupatikana katika ulimwengu halisi na
yasiyowezakana huwa madogo sana. Sababu hasa ya matumizi
ya mtindo huu ni kuonesha kuwa matukio ya aina hii
15
hupatikana katika maisha ya kawaida katika jamii
zinazohusika. Nadharia hii inasisitiza kuwa fasihi
haiwezi kujitenga na hali halisi ya maisha ya watu katika
jamii ambamo fasihi imeundwa na kutumika. Waandishi
wanaoandika katika msingi huu hushikilia kuwa mtizamo wao
wakiuhalisia unawakilisha msimamo wa jamii zao. Yaani
mambo yanayotekelezwa kama ya ajabu na kichawi ni sehemu
ya mwonoulimwengu wa jamii hizo.
Msingi mkubwa wa nadharia hii ni usimulizi unaosimulia
mambo au matukio kama yanavyotokea katika ulimwengu
halisi au unaokaribia na uhalisia, mwandishi anapaswa
kuyamulika na kuyaakisi maisha katika nyanja zote
kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa. Uhalisia
unaongoza na kusisitiza uwasilishaji wa maisha ya jamii
kwa uaminifu na usanifu mkubwa, uhalisia unapinga na
kukataa aina yoyote ya majaribio. Nadharia hii itasaidia
kwa kiasi kikubwa katika utafiti huu kwa kuwa matambiko
yanazungumzia jamii na watu ambao kwa hakika waliishi na
ni halisi pia yanazungumzia maisha halisi ya mwanadamu
16
hususani muafrika. Nadharia hii kimsingi inahusika sana
na jamii ambazo zimechelewa hususani jamii nyingi za
Afrika na Tanzania kwa ujumla. Jamii ya wasambaa ni jamii
ambayo kimsingi bado inaegemea sana mambo haya ya
matambiko hivyo nadharia hii itakuwa kama mwanga katika
utafiti huu kwani mambo ya matambiko ni mambo ya ajabu
ajabu.
Zamora (1995) Nadharia ya uhalisia mazingaombwe ilianza
mnamo mwaka wa 1925 na muasisi wake alikuwa mhakiki wa
sanaa wa Kijerumani aliyeitwa Franz Roh.Dhana ya Roh ya
nach-expressionism, magischer realism ikitafsiriwa katika
lugha ya Kiswahili inaashiria hali ya ajabu au
mazingaombwe. Uhalisia ajabu unaeleza miujiza iliyomo
kwenye uyakinifu wa kila siku.
Mbatiah, M. (2002:60) anafafanua uhalisia ajabu hivi,
istilahi hii inatumiwa kuelezea mkondo wa uandishi ambapo
mazingira, matendo na matukio ya kifantasia husawiriwa
kwa kuiga mtindo wa uhalisia yaani kuyaeleza mambo kwa
17
njia ya moja kwa moja kana kwamba ni mambo ya kawaida.
Wasanii wanaotumia mkondo huu hudhamiria kuonesha kuwa
ingawa mambo yanayoshughulikiwa ni ya kiajabuajabu
hutokea katika maisha ya kawaida ya jamii husika. Katika
uhalisia wa ajabu ndoto na uhalisia vinachanganywa.
Nadharia hii itasaidia sana kwa shughuli za matambiko na
zenyewe ni za kimazingahobwe kwani watekelezaji
wanawasiliana na viumbe ambao hawaonekani na hakuna
ushahidi wa kisayansi ya kuthibitisha mawasiliano hayo
japo kuna uhalisia lakini kwa kiasi fulani.
Njogu na Wafula (2007) wanaeleza Uhalisia ulitokana na
matatizo yaliyokuwa yanawakabili watu, matatizo hayo
yaliwafanya watu kuanza kushutumu ulimbwende na matamanio
ya kilimbwende yalikuwa ya kiusingizini (kinjozi) zaidi
yakilinganishwa na shida na matatizo yaliyokuwa
yanawakabili watu. Walimbwende wao walitunga mambo ya
usingizini na waliishi ndotoni. Katika msingi huu
matatizo yanayokabili jamii ya wasambaa na
18
yanayosababisha kufanyika kwa matambiko ni mambo halisia
kabisa ila wanaopewa jukumu la kuyatatua au kuleta ahueni
dhidi ya matatizo hayo hapo ndio uhalisia wa ajabu
unapokuja.
Wamitila, K.W (2002) anasema dhana ya uhalisia huelezea
aina ya mitizamo au tapo la kifasihi ambako kazi ya
kifasihi zinachukuliwa kama zilivyohifadhiwa au kuakisi
sifa za kimsingi zinazohusishwa na uhalisia.
1.9 Hitimisho
Kwa kuhitimisha, sura ya kwanza iliweza kuangalia,
utangulizi, historia ya kabila la wasambaa, dhana ya
matambiko kama ilivyotafsiriwa na wataalamu mbalimbali.
Vilevile ndani ya sura ya kwanza kuna usuli wa utafiti,
tatizo la utafiti, malengo ya utafiti, maswali ya
utafiti, umuhimu wa utafiti, mipaka ya utafiti na
nadharia ya utafiti ambayo ndiyo iliyomuongoza mtafiti
katika utafiti huu.
19
SURA YA PILI
MAPITIO YA MACHAPISHO MBALIMBALI
2.1 Utangulizi
Sura hii ilimuongoza mtafiti katika kukusanya data
zinazoendana na mada tafitiwa. Pia sura hii ilijumuisha
machapisho au mapitio mbalimbali ya kazi za waandishi
wengine zinazoendana na mada ya utafiti ili kujua
matambiko hususani katika jamii ya wasambaa kama
inavyooneshwa na wataalamu mbalimbali katika sura hii.
2.2 Mapitio ya Machapisho Mbalimbali
20
Masebo, J. A. (2007) anasema, tambiko ni sadaka inayotolewa kwa
mwenyezi mungu, miungu au mahoka, mizimu, pepo kwao binafsi
au kupitia kwa Mwenyezi Mungu wakati wa kusalia miungu.
Matambiko ni sanaa kwa kuwa shughuli zenyewe zinakuwa na
ufundi wa aina fulani. Zinatendeka mahali maalumu na
wanaohusika wanakuwa watu wa umri fulani na maalumu. dhana
ya matambiko inatumiwa kuhusiana na jamii nyingi za kiafrika
kuelezea shughuli za utoaji wa kafara na sadaka. Matambiko
yalikuwa na umuhimu na uzito mkubwa katika jamii za kijadi
kuliko jamii za siku hizi. Katika jamii ya wasambaa matambiko
bado yalichukuliwa kuwa na umuhimu mkubwa sana kama ilivyo
katika jamii nyingine. Kwa mfano Miaka ya 1993 katika jamii
ya wasambaa hususani jimboni Mlalo palitokea mafuriko,
mafuriko hayo yalileta maafa makubwa kwani watu
walipoteza maisha, mali, nyumba hata mashamba
yaliharibiwa vibaya! Jamii ile ilihusianisha tukio/janga
lile na kukasirika kwa miungu/mizimu/ mababu zao juu ya
kusahau masuala ya kutambika kwa zumbe mkuu kimweri au
kudharau mambo ya matambiko. Lakini jamii ile ya wasambaa
mpaka leo panapotokea njaa, ukame, vifo na hata ajali
lazima wakatambike kwa zumbe wakiwa wanapeleka kondoo,
21
vyakula vya aina mbalimbali kwa ajili ya kukamilisha
zoezi hilo la kuomba msamaha kwa mababu waliotangulia.
Ilipozama MV Bukoba viongozi wetu badala ya kutafiti
chanzo cha tatizo waliwakusanya wazee kufanya matambiko,
pengine ilikuwa mbinu ya kuwapumbaza watu wasihoji uzembe
uliosababisha ajali hiyo mbaya! Lakini tunaona kuwa sio
jamii hii ya wasambaa tu hata jamii nyingine na serikali
kwa ujumla.
Wamitila, K. W. (2002) anasema, dhana ya matambiko
inatumiwa kuhusiana na jamii nyingi za kiafrika kuelezea shughuli
za utoaji wa kafara na sadaka. Matambiko yalikuwa na umuhimu
na uzito mkubwa katika jamii za kijadi kuliko jamii za siku hizi.
Kimsingi tambiko ni sanaa kwa kuwa shughuli zenyewe zilikuwa
na ufundi wa aina fulani. Zilitendeka mahali maalumu na
waliohusika walikuwa watu wa umri fulani na maalumu. Jamii ya
wasambaa bado wanashiriki kwa ndani sana mambo haya ya
matambiko na kuna sehemu maalumu za kufanya shughuli hizo za
utoaji sadaka.
Kitula, K. na Catherine, N. M. K. (2010) wanasema, neno
Matambiko linatokana na imani kuwa mababu waliofariki
wana uwezo wa kuona matendo ya watoto na wajukuu wao
22
walio hai. Kadhalika inadhaniwa kuwa mababu hao
waliotangulia, wanapokasirika wakiwa katika dunia ya wafu
(kuzimu) watoto waliowaacha duniani hupatwa na matatizo
kama vile magonjwa, vifo au mabalaa mengine. Katika
kupoza hasira zao huko "walikolala" basi hupikwa pombe na
vyakula vinavyokwenda kumwagwa makaburini au kuliwa na
waganga. Kimsingi itikadi za ushirikina ndizo haswa
zinazozua shughuli za miviga, matumizi fulani ya lugha
kama vile methali, hadithi na nyimbo. Iwapo imani hizi
zisingekuwepo shughuli za miviga kama miviga na matambiko
hazingekuwepo. Watu hufanya matambiko sababu wanaamini
jambo fulani lilitendeka au kutokea hasa yale mabaya
sharti yapatiwe suluhisho. Matatizo hayo ni kama; vifo
hususani vile vya kutatanisha, vita, njaa, magonjwa,
ajali, kukosa/kupata watoto, ukame na hata mafuriko.
Katika baadhi ya makabila likiwepo kabila la wasambaa
hata viapo hufanywa kwa kuwataja mababu moja kwa moja au
kwa ishara, huko alikolala yaani huyo anayesema
anathibitisha akimshuhudia babu, baba (mahoka) yake
23
aliyekufa kuwa akisemacho ni sahihi! Utekelezaji wa
matambiko huandamana na mihanga ya pombe, vyakula, kafara
ya damu hususani ya wanyama ili kuilaza mizimu
iliyochachamalia familia, koo na hata jamii fulani.
Masebo, J. A (2013) anasema, matambiko yana umuhimu na
hasara katika jamii kama ifuatavyo;
2.2.1 Umuhimu wa tambiko
I. Matambiko hujenga imani kama chombo cha kutatulia
matatizo ya jamii husika.
II. Tambiko husaidia kuendeleza mila na desturi za jamii husika
III. Tambiko husaidia kujenga na kuimarisha mahusiano
miongoni mwa wanajami
IV. Matambiko huiongoza jamii katika mapambano dhidi ya
matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii.
2.2.2 Hasara ya matambiko
I. Matambiko hujenga dhana potofu katika jamii kwa
kuamini nguvu Fulani bila kuwa na uhakika au
uthibitisho wa kisayansi.
II. Matambiko huleta hasara kubwa kwa jamii husika,
kwani kafara, sadaka, za matambiko inahitaji
24
wanyama/vyakula ambavyo watu hutumia pesa nyingi
kuvipata vitu hivyo.
III. Matambiko huwafanya watu kuishi kwa wasiwasi mkubwa
kwani panapotokea tatizo na uwezo wa kufanya tambiko
haupo wanajamii hao hupatwa na hofu maishani kwa
kushindwa kutimiza yale wanayodhani wazee/mahoka
wanahitaji kufanyiwa.
Katika jamii ya wasambaa matambiko yana faida kadhalika
yana hasara kama ambavyo Masebo, J. A. (2013)
alivyofafanua.
Masebo, J. A (2013) anasema, matambiko yana wahusika
maalumu na mandhari/mahali maalumu kama ifuatavyo;
2.2.3 Wahusika
Hawa ni wale wazee maarufu walioteuliwa na jamii kuendeleza
shughuli za matambiko, si kila mtu katika jamii anaweza kufanya
tambiko.
2.2.4 Mandhari/Mahali
25
Tambiko linaweza kufanyika porini, njia panda, makaburini,
mapangoni, mtoni, ziwani na kwenye miti mikubwa na mahali
popote kutegemeana na aina ya tambiko. Katika jamii ya wasambaa
matambiko yanafanywa na watu maalumu pia katika mazingira
maalumu kama ambavyo wataalamu mbalimbali
walivyofafanua/kueleza.
Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) (2010) wanasema
tambiko ni kitendo cha mtu au jamii kutekeleza ada
maalumu kutuliza mashetani au mizimu. Pia matambiko yana
husiana sana na ushirikina ambapo ushirikina ni tabia ya
kuamini uwezo wa kiumbe kingine juu yako badala ya ule wa
Mwenyezi Mungu. Kimsingi matambiko yanaandamana na mambo
ya uganga hivyo ushirikina unahusiana sana na mambo ya
matambiko. Ni dhahiri kabisa ushirikina unahusiana sana
na mambo ya uganga na matambiko na katika jamii ya
wasambaa haya mambo na ibada hizi ziko na zinahusiana kwa
karibu sana kwa kuangalia vitendo vya mazoezi hayo.
M’nganuth, T. K. (2007/2008) anasema kila palipotokea
janga/tatizo lolote palikuwa na haja ya kufanya tambiko.
Muafrika katika asili yake aliamini Mungu/miungu, mizimu
26
na mahoka. Nyimbo mbalimbali za kumsihi mungu
ziliambatana na na tambiko. Nyimbo za matambiko
zinapatikana kwa wingi katika miviga kama vile shughuli
za kaya pia katika ngoma za pugwa kwa waswahili na jamii
nyingine. Katika jamii ya wameru suala la matambiko
linaenda pamoja na nyimbo maalumu ambazo huibwa wakati
tambiko fulani likitekelezwa.
Mfano;
Wimbo ufuatao ni wa Kimeru ambao uliimbwa wakati wa kutoa
tambiko/sadaka hasa baada ya kipindi kirefu cha kiangazi
kuomba neema fulani kwa Mungu/miungu, mahoka, pepo na
hata mizimu.
Ingwe muningu baba
Jukia iromba rietu
Tukikwerncaga
I ii murungu twingirue kiao
Turi baku
Twingirue kiao turi baku
Kiiru kiiru turi baku
27
Tafsiri-kiswahili
Ewe mungu baba
Pokea dua zetu
Tunakusihi
Sisi jumuiya ya watu wa meru
Ewe mungu baba tuhurumie
Sisi ni wako
Ewe mungu sisi ni wako.
Nyimbo za aina hii zilipatikana kwa wingi katika miviga
kama vile shughuli za kawaida za kaya kadhalika katika
ngoma za mashetani/pungwa katika jamii ya wasambaa na
jamii nyingine zinazifanana na hizo.
2.3 Hitimisho
Wataalamu mbalimbali na waandishi nguli wa mambo ya
fasihi wamefanya tafiti mbalimbali kuchunguza dhama ya
matambiko. Dhana hiyo ndiyo inayotoa mwanga kwa wasomaji
kuelewa maana ya matambiko. Lakini wataalamu hao
hawajawahi kuangalia matambiko katika jamii ya wasambaa
hususani katika mambo kama; sababu za kufanya matambiko,
mazingira ya matambiko, vifaa na hata umuhimu wa
28
matambiko. Utafiti huu ulijaribu kuambaa kwa kina katika
kila kipengele ili kutoa picha halisi ya matambiko katika
jamii husika.
SURA YA TATU
MBINU ZA UTAFITI
3.1 Utangulizi
29
Sura hii iliwasilisha mbinu mbalimbali zilizotumika
kumsaidia mtafiti katika kukamilisha utafiti wake, mbinu
alizotumia mtafiti katika kukusanya data ambazo kwa namna
moja ama nyingine zitajibu maswali ya utafiti huu, mbinu
za utafiti, eneo la utafiti, vyanzo vya data, njia za
ukusanyaji data, sampuli na usampulishaji, vifaa vya
ukusanyaji data na uchanganuzi wa data.
Utafiti huu ulihusu nafasi ya matambiko katika kabila la
Wasambaa linalopatikana mkoa wa Tanga hususani katika
safu za milima ya usambara.
3.2 Mbinu za Ukusanyaji Data
3.2.1 Hojaji
Mtafiti alitumia mbinu hii ili kuweza kupata data
mbalimbali zinazohusu matambiko katika kabila la
Wasambaa. Baadhi ya maswali mtafiti aliyouliza yalikuwa
kama ifuatavyo;
30
I. Matambiko yana umuhimu gani katika jamii ya
wasambaa?
II. Matambiko hufanywa vipindi na mazingira gani?
III. Vifaa gani hutumika katika kutekeleza zoezi la
matambiko?
3.2.2 DodosoMtafiti ametumia mbinu ya kuuliza maswali katika
maandishi na kuwapatia wanajamii wa Rangwi ili kupata
data anazozihitaji. Watu waliotakiwa kujibu maswali hayo
ni watu wote wazee kwa vijana wanaoishi katika kata ya
Rangwi.
3.3 Vyanzo vya Data na Taarifa
Kamusi ya Kiswahili Sanifu (2004:59) ilieleza kuwa data
ni taarifa au takwimu inayotumiwa kuelezea au
kuthibitisha hoja fulani. Taarifa ni habari inayotolewa
ili kujulisha jambo fulani (uk 388). Ili mtafiti kuweza
kukamilisha utafiti wake alitumia vyanzo mbalimbali vya
31
data kama vile vitabu, majarida, makala, magazeti na
hotuba mbalimbali.
3.3.1 Data za Msingi
Kothari (1992:95) anasema, data za msingi ni zile data
zilizokusanywa kwa mara ya kwanza na hivyo ni data
halisi. Kwa msingi huo data za msingi zilizokusanywa
kupitia mahojiano na wazee mashuhuri ambao ni wasambaa
wanaoishi maeneo ya katika tarafa ya Mtae katika kata ya
Rangwi.
3.3.2. Data Fuatizi
Kothari (1992:95) anasema data fuatizi ni zile data
ambazo tayari zilikwishakusanywa na watafiti wengine ama
kuandikwa kama ripoti, makala. Data za namna hii ni
muhimu kwa sababu ndizo zilikazothibitisha data za msingi
za utafiti na kuupa mashiko utafiti huu.
3.4. Sampuli na Usampulishaji
32
Sampuli yetu katika utafiti huu ni wasambaa wa jamii ya
Lushoto wa tarafa ya Mtae katika kata ya Rangwi. Mtafiti
alitumia usampulishaji nasibu katika kukusanya data
ambapo kila kipengele kilichofaa kwa kutoa taarifa kuhusu
nafasi ya matambiko katika jamii ya wasambaa ili
kurahisisha uchukuaji wa data.
Sampuli nasibu imependekezwa kutumika kwa sababu ndiyo
njia inayofaa na kumpa mtafiti uhuru wa kuchagua nukuu
ilikayofaa kutumika kama data katika utafiti huu.
3.5. Mbinu za Uchambuzi wa Data
Data zilichambuliwa katika mkabala wa kimaelezo yaani
mkabala usio wa kiidadi au kitakwimu. Hii ni kwa sababu
utafiti huu haukuhusisha takwimu, data zilipangwa
kulingana na malengo na maswali ya utafiti ili
uchanganuzi wa data hizo uendane na malengo ya utafiti.
Data zote zilipewa msimbo wa nukuu na zilichambuliwa kila
moja ili kuweka utafiti huu katika mtiririko na mpangilio
wenye upatanifu. Data zote zilizoambatanishwa kama msimbo
33
wa nukuu zilichambuliwa kila moja na nafasi yake ili
kurahisisha uchakataji wa data. Data fuatizi zilinukuliwa
pale ilipobidi ili kuthibitisha data za msingi.
3.6. Vifaa vya Ukusanyaji wa Data
Vifaa vilivyotumika katika ukusanyaji wa data maktabani
ni kalamu, penseli na karatasi kwa ajili ya kunukuu data
za msingi, data fuatizi na vipengele vinginevyo muhimu.
Kompyuta ilitumika kwa ajili ya kufanya mawasiliano ya
kimtandao (barua pepe, na hata mitandao mingine ya
kijamii) pia ilitumika katika kupitia vitabu na mapitio
yaliyokuwa hayapatikani maktabani. Mtafiti alitumia
kompyuta na kinyonyi data (flashi) kwa ajili ya uchapaji,
unyonyaji data na utunzaji wa kumbukumbu za utafiti huu.
3.7 Eneo la Utafiti
3.7.1 Uwandani
Utafiti huu ulifanyika katika mkoa wa Tanga wilayani
Lushoto katika tarafa ya Mtae katika kata ya Rangwi
34
kijijini Emao ambako wakilindi ndio asili yao. Eneo la
Rangwi lilichaguliwa kutokana na ukweli wa kuwepo wazee
wengi ambao kwa kina wanajua maana ya matambiko, jinsi
yanavyofanywa, sababu, umuhimu kila kitu ambacho
kinahusiana na matambiko wanakijua lakini pamoja na hayo
yote walio wengi ni wasambaa ambao haswa ndio utafiti huu
uliwagusia sana. Pia mtafiti ni mzaliwa wa mazingira ya
usambara hivyo ni rahisi kupata data katika mazingira
halisi ya jamii anamoishi mtafiti ili kujua jamii yake
ilikuwa wapi na inaelekea wapi.
3.7.2Maktabani
Lakini pia mtafiti amefanya utafiti wa maktabani. Utafiti
umefanyika katika maktaba ya Chuo Kikuu Kishiriki cha
Jordan tawi la Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino
kilichopo mkoani Morogoro, maktaba ya mkoa wa Morogoro na
katika mtandao (internet). Maktaba hizo zimetumiwa na
mtafiti kwa kuwa data zote muhimu zinapatikana katika
maktaba hizo, ikiwa ni pamoja na vitabu na matini
35
mbalimbali zinapatikana humo. Maktaba hizo zimeteuliwa na
mtafiti kwani ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha
Jordan na ni mkazi wa Morogoro na ni rahisi kwake kufika
katika maeneo aliyoyateua, hii imemrahisishia mtafiti
ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama za utafiti.
3.8 Hitimisho
Katika sura hii mtafiti aliangalia eneo la utafiti ambalo
mtafiti alitapitia kwa madhumuni ya kukamilisha utafiti
huu. Vilevile mtafiti aliangalia mbinu za ukusanyaji wa
data, vifaa vilivyotumika katika kukamilisha utafiti huu
pamoja na sampuli mbalimbali za utafiti huu wa nafasi ya
matambiko katika jamii ya wasambaa.
36
SURA YA NNE
UCHAMBUZI WA DATA
4.1 Utangulizi
Sura hii inahusu uchambuzi na uwasilishaji wa data
zilizokusanywa kwa kuzingatia nadharia ya uhalisia
mazingaombwe. Katika tasnifu hii mchakato umelenga
kuchambua malengo ya utafiti ili kuweza kuchakata data
vizuri. Malengo ya utafiti ndiyo zana iliyomsaidia
mtafiti kujibu maswali ya utafiti, katika kufanikisha
utafiti huu mtafiti alitumia njia kuu tatu ambazo ni;
njia ya kuwahoji wenyeji wa mkoa wa Tanga hususani katika
wilaya ya Lushoto tarafa ya Mtae katika kata ya Rangwi,
njia ya watafitiwa kujibu maswali ya dodoso na mwisho
njia ya kutembelea maktaba na maeneo ya asili ambayo yapo
37
katika kata ya Rangwi (data za msingi na data fuatizi)
lengo ni kufanikisha kazi hii pamoja na kuonesha nafasi
ya matambiko katika jamii ya wasambaa.
Katika utafiti huu mtafiti ameonesha mchango wa washiriki
wa utafiti huu kwa kuzingatia jinsia, elimu, umri.
JINSIA IDADI ASILIMIA
WANAWAKE 10 40%
WANAUME 15 60%
JUMLA 25 100%
Kielelezo Na. 1 Jinsia ya washiriki
Kielelezo hapo juu kinaonesha idadi ya washiriki katika
utafiti kuwa idadi ya wanaume wanaoshiriki katika
shughuli za matambiko ni kubwa sana ukilinganisha na
idadi ya wanawake katika jamii ya wasambaa ambapo ni
dhahiri kabisa kuwa wanaume ndio watendaji wakuu katika
utekelezaji wa matambiko.
Miaka Idadi Asilimia
38
18-24 3 12%
25-35 2 8%
36-45 5 20%
56-60 5 20%
60-zaidi 10 40%
Jumla 25 100%
Kielelezo Na. 2 Umri wa washiriki
Katika kielelezo hapo juu, tunaona kuwa washiriki wenye
umri zaidi ya 60 ndio walio wengi na hawa ndio washiriki
wakubwa katika kutekeleza matambiko katika koo nyingi za
wasambaa kundi hili husaidiwa kwa karibu mno kwa lengo la
kurithisha kazi hiyo na kundi la miaka 56-59 na kwa kiasi
kidogo kundi la miaka 36-45. Kundi la miaka 25-35 pamoja
na 18-24 wao walitoa mawazo yao tu juu ya matambiko
katika jamii ya wasambaa.
Kiwango Idadi Asilimia
39
Wasiosoma 1 4%
Msingi 15 60%
Sekondari 6 24%
Chuo 3 12%
Jumla 25 100%
Kielelezo Na. 3 Kiwango cha elimu ya wahusika
Kielelezo hapo juu kinaonesha viwango vya elimu ambapo
kundi kubwa inaonesha ni la wale waliopata elimu ya
msingi wakifuatiwa na wale waliobahatika kupata elimu ya
sekondari na chuo na mwisho kabisa ambao hawajasoma.
Je? Kuna mavazi maalumu katika kutekeleza shughuli za
matambiko katika jamii ya wasambaa
Majibu Idadi Asilimia
Ndiyo 25 100%
Hapana _ _
Hawajui _ _
Jumla 25 100%
Kielelezo Na 4 Uwepo wa mavazi maalumu katika matambiko;
40
Kielelezo hapo juu kinaonesha kuwa washiriki wote 25 sawa
na asilimia 100 wamekiri kuwa kuna mavazi maalumu ambayo
hutumika katika kutekeleza shughuli za matambiko katika
jamiii ya wasambaa ambayo ni kaniki (kanga yenye rangi
nyeusi), vitambaa vyeupe na nyeusi pamoja na shanga za
rangi mbalimbali.
Majibu Idadi Asilimia
Ndiyo 20 80%
Hapana 2 8%
Hawajui 3 12%
Jumla 25 100%
Kielelezo Na. 5 Je, matambiko yana msaada wowote katika
matatizo ya wasambaa?
Katika kielelezo hapo juu, asilimia 80 ya washiriki
wamekiri kuwa matambiko yana msaada mkubwa mno katika
jamii ya wasambaa kwa sababu wanapotambikia mizimu yao
matatizo husika hupungua ama kutoweka kabisa mfano watu
hupona magonjwa, waliopotea wanaonekana, walioenda mbali
41
na nyumbani kwa muda mrefu bila mawasiliano hurudi mara
matambiko yanapofanywa.
Kimsingi kabla ya kuangalia suala lenyewe linalobeba kazi
hii ni vizuri kuangalia mambo muhimu yanayohusu kabila
hili la wasambaa kama; historia fupi ya kabila la
wasambaa, maelezo mafupi ya matambiko katika kabila la
wasambaa pamoja na chimbuko la matambiko katika kabila
hili.
4.2 Maelezo Mafupi Kuhusu Matambiko Katika Jamii ya
Wasambaa
Katika mahojiano na mtafitiwa mzee Matimua R. K anasema
katika jamii ya wasambaa matambiko ni njia ya
kumuunganisha mwanadamu na muumba wao kwa kumtolea mungu
sadaka na shukrani. Kulingana na maelezo ya wasambaa
walioshiriki katika utafiti huu wanadai kuwa matambiko ni
sehemu ya maisha yao katika kupambana na changamoto za
kimaisha. Na pale itokeapo jamii imeingia katika magumu
ya aina yeyote basi kimbilio linaloaminika kuleta utulivu
42
juu ya tatizo husika ni matambiko tu. Kwa wasambaa kuna
sala mbalimbali ambazo kwa hakika wanajamii huzitumia
katika nyakati tofauti tofauti ili kuomba Baraka kwa
mungu wanayemuamini ambapo amepewa majina kama Zumbe
Mnkhalamo (Mungu wa neema), Zumbe Tate (Mungu Baba)
ambapo katika sala zao huanza kumtaja yeye akifuatiwa na
majina ya watu waliotangulia kuanzia mkubwa mpaka mdogo
na ndipo hutaja nia zao zote na kuzikabidhi kwa miungu
yao.
Katika kipindi hiki ambapo jamii ya wasambaa ina
mchanganyiko wa dini yaani dini ya Kikristo na Kiislamu
matambiko bado yana nafasi kubwa kwa sababu ndani ya
jamii hii bado matambiko yanafanyika katika namna mpya.
Kwa wakristo walio wengi wanafanya misa za kuombea
marehemu wao (kumbukumbu) ambapo katika familia ama koo
hufanya ibada hizo lakini ndani yake kuna matambiko
yanafanyika kwa usiri mkubwa kwa sababu dini haziruhusu
matambiko. Kwa wakristo ibada za kuombea wafu zinaenda
sambamba na uikaji wa vyakula pamoja na uchinjaji wa
43
wanyama ambako vyakula hivyo huliwa na watu walioalikwa
katika shughuli hizo. Kwa upande wa waislamu hakuna
tofauti sana na wakristo kwani ibada za kuwaombea wafu
hufanywa sambamba na uchinjaji wa wanyama na upikaji wa
vyakula. Kimsingi matambiko yapo na yanaendelea ila
yanaenda kuvaa sura na jina lingine katika jamii ya
wasambaa.
Kulingana na Zamora, P. na Faris, W. B. (2005)
wakimrejelea Haen, D. wanasema kwamba uhalisia
mazingaombwe unabuni ulimwengu mbadala kwa hiyo
unarekebisha makosa ambayo uhalisia wetu unayategemea ili
kuwepo. Na ndio maana jamii ya wasambaa kwao matambiko ni
sehemu ya maisha yao kwa sababu wao wanaamini kuwa, kuna
ulimwengu mwingine baada ya maisha ya hapa duniani kufika
mwisho. Ambapo wao wanaamini kuna ulimwengu wa kuzimu
ambapo wanajamii waliotenda mema baada ya kufa roho zao
huenda huko kuzimu na wanajamii ambao matendo yao
hayakuwa mazuri roho zao hazifiki huko ila hutangatanga
duniani. Na ndio maana wasambaa hufanya matambiko ili
44
kurekebisha pale walipokosea ili mizimu iwawie radhi na
kuishi kwa amani kwa sababu wanaamini roho za mizimu zipo
katika ulimwengu mbadala na huu tuishio, na mizimu
wanafuatilia kazi/shughuli zetu za kila siku.
4.3 Chimbuko la Matambiko Katika Jamii ya Wasambaa.
Kwa mujibu wa mzee Imamu Abdi Kaniki katika mahojiano na
mtafiti wa tasnifu hii alidai kuwa matambiko katika jamii
ya wasambaa yameanza zamani sana enzi za mababu na mababu
Kirama, Kh. (1953) Katika kitabu chake cha Habari za
wakilindi amebainisha kuwa jamii ya wasambaa hususani
wakilindi ambao aliwazungumzia sana amesema walikuwa
wanatambika kwa miungu yao kuomba mambo mbalimbali hata
pale wanapoenda kinyume na maagizo ya mababu zao
(miungu). Pamoja na haya yote jamii ya wasambaa kama
ilivyo kwa jamii nyingine za kiafrika inaonesha kuwa
walianza matambiko zamani sana katika harakati za
mwanadamu kutafuta suluhu ya mambo ambayo kwa uwazi
yalikuwa nje ya uwezo wake kama vile ukame, vifo,
45
mafuriko, vimbunga na hata radi. Matambiko yalifanywa ili
kuomba msaada kwa mungu ili kupata ahueni juu ya shida
husika. Hivyo ni ukweli kuwa matambiko yalikuwepo tangia
zamani katika jamii ya wasambaa na sio suala ambalo
wameiga kutoka nje.
Chanady (1985) anasema kwamba uhalisia ajabu unahusu
matukio yasiyo ya kawaida, ya kiujiza au chochote kilicho
kinyume cha uhalisia wa kawaida. Katika hali hii kwa
sababu matukio yanayohitaji matambiko mengi yanatokea
katika hali ya ujabu kama vimbunga, radi, mafuriko na
vifo vya kutatanisha.
Wikipedia (2014) wanasema jamii ya Wasambaa, Wabondei,
Wasegeju, Wazigua na Wadigo za Mkoa wa Tanga zimeanza
kutambika kwa ajili ya mizimu yao katika mapango maarufu
sana ya Amboni tangia karne ya kumi na sita, hii
inadhihisha kwamba matambiko yalianza siku nyingi mno
katika jamii ya wasambaa.
4.4. Umuhimu wa Matambiko Katika Jamii ya Wasambaa
46
Matambiko yana nafasi na umuhimu mkubwa sana katika jamii
ya kabila la wasambaa, mtafiti aliweza kuhojiana na
wanajami 25 ambapo wanaume walikuwa 15 na wanawake 10
ambapo miongoni mwa watafitiwa 19 wamekiri matambiko yana
umuhimu wa kuwa sawa na asilimia 79 na washiriki 3 sawa
na asilimia 9.5 wamesema matambiko hayana umuhimu na
washiriki 3 wamesema hawajui chochote sawa na asilimia
9.5 kama inavyooneshwa katika kielelezo kifuatacho.
Majibu Idadi Asilimia
Ndio 19 76%
Hapana 3 12%
Hawajui 3 12%
Jumla 25 100%
Kielelezo Na. 6 Umuhimu wa matambiko
Matokeo yanabainisha baadhi ya umuhimu wa matambiko
katika jamii ya wasambaa wanaoishi kaskazini mwa Tanzania
kama ifuatavyo;
i.Matambiko hujenga imani
47
ii.Matambiko husaidia kuendeleza mila na desturi
iii.Matambiko hujenga mahusiaano mema
iv.Matambiko huiongoza jamii katika mapambano na matatizo
4.4.1 Matambiko Hujenga Imani
Matambiko hujenga imani kama chombo cha kutatulia matatizo ya
kijamii katika jamii husika katika misingi ya kwamba inapotokea
janga kwa mfano mafuriko, ukame, njaa, ajali, magojwa na
kufanywa matambiko katika namna mbalimbali kutegemeana na
tatizo wanajamii washakuwa na imani kwamba baada ya kufanya
hivyo lazima patakuwa na ahueni juu ya tatizo lao kama tu
wametekeleza kama wahenga wanavyotaka kwani wanahusianisha
matatizo na kuchukia kwa mababu waliotangulia.
Strecher (1999) anafafanua uhalisia ajabu kama kile kinachotendeka
wakati ambapo ukweli wa ndani wa mandhari ya juu unapoingiliwa
na kitu ambacho ni cha kiajabu sana kuaminika. Matambiko katika
jamii ya wasambaa huwajengea imani ya ajabu sana wanajamii
husika kutokana na mambo ya ajabu ambayo yanatokea na
yanayofanywa wakati wa matambiko na matokeo yake.
4.4.2 Matambiko Husaidia Kuendeleza Mila na Desturi
Matambiko husaidia kuendeleza mila na desturi za jamii ya
wasambaa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Matambiko yana
umuhimu mkubwa sana kwa sababu yenyewe ni kama njia ya
kuwafundisha wanajamii jinsi ya kutatua matatizo yao kijamii.
48
kwa jinsi hiyo mila na desturi za jamii husika huendelea kutoka
kizazi kimoja hadi kingine kwa sababu wakati wa matambiko
katika jamii ya wasambaa huhusisha wake kwa wanaume, wazee
na vijana ambapo vijana huona jinsi wazee maalumu
wanavyofanya, hivyo hata kesho hawapo nao wameshajua taratibu
za kufuata katika kutunza na kuendeleza mila na desturi za kabila
la wasambaa.
Louis, P. (2005) anasema uhalisia ajabu unapaswa kueleweka kwa
kadiri fulani kama mkabala wa kuuwakilisha uhalisia kwa kukiuka
mipaka kati ya dhana, vitu au hali. Katika jamii ya wasambaa ni
ukweli kabisa kuwa matambiko ni chombo kikubwa cha kuendeleza
mila na desturi za jamii hii. Matambiko huvuka mipaka ya dunia
hii na kusogea mbali na kufikia upeo wa juu wa dunia nyingine
ambayo kwao wanaamini ni kuzimu yaani sehemu maalumu
zinakoishi roho za watu waliokufa hususani za wale waliotenda
mambo mema. Na wasambaa wana imani kuwa matatizo ni
matokeo ya kuchukia kwa mizimu.
4.4.3 Matambiko Hujenga Mahusiano Mema
Matambiko katika jamii ya wasambaa husaidia kujenga na
kuimarisha mahusiano mema miongoni mwa wanajamii. Katika
jamii ya wasambaa ikitokea wanajamii wamepishana kuna mambo
ya kufanya ili kuwaleta katika hali ya uelewano, ambapo hufanya
viapo maalumu ili yule aliyemkosea mwenzake iwe kwa makusudi
au kwa bahati mbaya asirudie tena na kwa kiapo hicho wanajamii
waliokoseana wanaahidi mbele ya wazee kwamba
49
hawamesameheana na hakuna mwenye kinyongo na mwenzake
baada ya hapo anachinjwa kondoo kama kosa ni kubwa na kula
pamoja ikiwa ni ishara ya kupatana na baadhi ya nyama na uchafu
uliokuwa tumboni mwa mnyama huyo huzikwa ikiwa ni ishara ya
kuzika tofauti zao na kuanza maisha mapya. Na ikitokea miongoni
mwa mmoja akamkosea mwenzake anadhurika hata kufa. Kwa jinsi
hiyo jamii kupitia matambiko panakuwa na mshikamano chanya.
Kulingana na Hean, D. T. (2005) anaelezea uhalisia mazingaombwe
kwa kuchukua michoro iliyo na uhalisia kama picha ya kamera
lakini iliyoibua hisia kwa kuchanganya uhalisia na ukosefu wa
uhalisia. Ambapo katika jamii ya wasambaa, kwa kukoseana
miongoni mwa wanajamii katika hali ya kibinadamu, ambapo hali
hiyo ni ya kawaida au ina uhalisia kabisa ila njia ya kuelewana au
kuwaleta pamoja wanajamii haina uhalisia kuanzia matendo
yenyewe ya kuwapatanisha kwani wanahusishwa viumbe ambao
hawapo katika uhalisia na hata dunia wanayoishi hatuijui kabisa.
Hatimaye wanajamii waliokoseana katika hali ya uhalisia hupata
hofu ya ajabu na kuelewana na kuheshimiana katika hali ya
kiajabuajabu. Na ndio maana mmoja wapo anapomkosea mwenzake
kwa mara nyingine tena kwa makusudi anapata madhara makubwa
ikiwa hata kufa katika hali isiyo ya kawaida.
4.4.4 Matambiko Huiongoza Jamii Katika Kupambana na
Matatizo
50
Matambiko huiongoza jamii katika mapambano dhidi ya matatizo
mbalimbali yanayoikabili jamii husika. Katika jamii ya wasambaa
kuna matatizo mbalimbali ambayo yanaitatiza jamii hii kwa mfano
ukame, mafuriko, njaa, ajali na mambo mengine mengi kwa
kupitia matambiko jamii huongozwa katika kupambana nayo kwani
inapotokea ukame na pengine wanajamii wanatumia vibaya
rasilimali zilizopo kama misitu kwa kupitia matambiko wanapata
ujumbe juu ya kutunza misitu au hata kutumia mito kwa shughuli
maalumu na sio shughuli ambazo ni za kuharibu mazingiza kwani
kwa kufanya hivyo wahenga wanakasirika na kuwaletea matatizo
hayo kama adhabu.
Njogu na Wafula (2007) wanaeleza Uhalisia ulitokana na
matatizo yaliyokuwa yanawakabili watu, matatizo hayo
yaliwafanya watu kuanza kushutumu ulimbwende na matamanio
ya kilimbwende yalikuwa ya kiusingizini (kinjozi) zaidi
yakilinganishwa na shida na matatizo yaliyokuwa
yanawakabili watu. Hapa wasambaa nao walikuwa
wanakabiliana na matatizo yao ya kawaida kwa kutafuta
suluhu kutoka kwa mizimu, miungu yao ambayo kiuhalisia
nguvu hizo hazina nguvu ila kiajabuajabu mizimu na miungu
ina nguvu sana hususani katika kutatua matatizo.
51
4.5. Athari za Matambiko Katika Jamii ya Wasambaa
Mtafiti alipenda kujua kama kuna hasara ama athari zozote
zinazoweza kusababishwa na utekelezaji wa matambiko. Kutokana
na majibu ya watafitiwa zipo hasara nyingi ambazo hutokea pindi
matambiko yanapofanywa washiriki walio wengi wamekiri kuwepo
kwa hasara hususani pindi matambiko yanapofanywa kwani
huhitaji pesa na wanyama. Ambapo watafitiwa 20 sawa na asilimia
80 wamekiri kuwepo kwa hasara, watafitiwa 4 sawa na asilimia 16
wamesema hakuna hasara yeyote kwani sadaka kwa miungu yao
hawaoni uwepo wa hasara na mtafitiwa 1 sawa na asilimia 4
amesema hajui uwepo au kutokuwepo kwa hasara.
Majibu Idadi Asilimia
Ndiyo 20 80%
Hapana 4 16%
Hawajui 1 4%
Jumla 25 100%
Kielelezo Na. 6 Athari za matambiko
Hasara zilizoanishwa na watafitiwa ni kama ifuatavyo;
I. Matambiko hujenga dhana potofu
II. Matambiko huleta hasara kubwa kwa jamii
III. Matambiko huwafanya watu kuishi kwa wasiwasi mkubwa
52
4.5.1 Matambiko Hujenga Dhana Potofu
Matambiko hujenga dhana potofu katika jamii kwa kuamini
nguvu fulani bila ya kuwa na uthibitisho wa kisayansi.
Matambiko hufanywa kwa kuamini miungu, mahoka, na mababu
waliotangulia ambapo wanajamii hujenga imani imara kabisa
kuwa wao ndio kila kitu na hata pale litokeapo tatizo
huhusianisha na kuwakasirisha na hivyo wanalazimika
kuwafanyia tambiko ama ibada kubwa za kishetani ambapo
huenda sambamba na upikaji wa vyakula na uchinjaji wa
wanyama jambo ambalo sio sahihi.
Marquez, G. (1925) yeye anachukulia uhalisia ajabu
kwamba, mambo yanayoelezewa kuwa ya kiajabu na kichawi ni
sehemu ya mwonoulimwengu wa jamii hizo. Wasambaa wao
wanaamini juu ya matambiko hata kama wachache huyaona
kama dhana potofu, wao wanichukulia kama sehumu ya maisha
yao. Mambo mengi yanayofanyika wakati wa matambiko
huhusiana sana na shughuli za kichawi, kuanzia vitendo na
53
hata nyimbo za matambiko hazina tofauti na zile za
kichawi.
4.5.2 Matambiko Huleta Hasara Kubwa kwa Jamii.
Matambiko huleta hasara kubwa kwa jamii husika kwani
kafara, sadaka za matambiko zinahitaji wanyama na vyakula
ambavyo wanajamii hutumia pesa nyingi kuvipata kwa
kuamini kuwa kwa kufanya hivyo hasira zao zitatulia na
mambo yataenda vizuri katika jamii husika jambo ambalo ni
kuongeza majukumu yasiyo ya lazima. Ambapo baadhi ya
vyakula na nyama huwekwa makaburini, mapangoni, mtoni,
baharini wakiamini waliotangulia (miungu, mahoka, mizimu)
watakula jambo ambalo kimsingi halina ushahidi kisayansi.
Robert, R. P.J. (1949) katika kitabu chake cha “Beliefs
in spirits” anasema mizimu ni viumbe ama roho za watu
waliokufa. Iwapo mtu atakufa katika hali nzuri bari roho
yake itaenda katika kijiji cha wafu kiitwacho kuzimu. Na
ikiwa mtu atakuwa katika hali ambayo sio nzuri roho yake
haifiki katika kijiji hicho bali hutangantanga mapangoni,
54
msituni, ziwani, mtoni, mabondeni na hata mashambani na
roho hizi huweza hata kuwadhuru watu wazima. Kutokana na
maelezo hayo walio hai hufanya matambiko makubwa
kutokomeza roho hizo ambazo huwasumbua mara kwa mara na
kukwamisha shughuli za kawaida za kibinadamu.
4.5.3 Matambiko Huwafanya Watu Kuishi kwa Wasiwasi Mkubwa
Matambiko huwafanya watu kuishi kwa wasiwasi mkubwa
kwani panapotokea tatizo na uwezo wa kufanya tambiko
haupo wanajamii husika hupwatwa na hofu kubwa maishani
kwa kushindwa kutimiza yale wanayodhani wazee, mahoka
wanahitaji kufanyiwa.
4.6. Mazingira Ambapo Matambiko Hufanyika
Katika mahojiano na mtafitiwa Ndg. Mngazija K.A anasema
matambiko katika jamii ya wasambaa hufanywa katika
mazingira maalumu sana na tulivu. Maeneo hayo ni lazima
ufikapo hapo uwe na utulivu na nidhamu ya hali ya juu
kulingana na viashiria vyake kwani katika jamii ya
wasambaa huchukuliwa kama maeneo matakatifu kulingana na
55
imani ya jamii husika. Katika jamii ya wasambaa miungu
yao inasadikiwa kuwa huishi katika mazingira kama mtoni,
mapangoni, juu ya milima mikubwa, kwenye misitu mikubwa,
kwenye majabali makubwa, kwenye nyumba maluumu (nyumba za
duara zilizoezekwa kwa majani ya migomba) pamoja na
makaburini. Katika maeneo ya usambaani wasambaa mara
nyingi huenda kutambika kwa zumbe Kimweri ambapo pana
mazingira mbalimbali ambayo yanasadifu matambiko
kulingana na tatizo husika. Pia kuna milima mbali mbali
kama Mlima Mzoghoti ambao upo eneo la Rangwi, masitu wa
Kideghe ambao upo katika kata ya Rangwi katika kijiji cha
Goka pamoja na mito mbalimbali.
Wamitila (2008) anadai kuwa uhalisiaajabu ni kuwepo
matukio ambayo ni vigumu kuyaeleza katika misingi wa
uhalisia wa kawaida katika jamii. Katika jamii ya
wasambaa mazingira ambayo matambiko hufanywa ni ya ajabu
japo yapo katika uhalisia wa kawaida na vigumu kuyaelezea
katika msingi wa kawaida. Kwa mfano vinyumba vya mizuka
ambavyo hutumika sana katika kufanyia shughuli kadha wa
56
kadha za matambiko na kiganga. Ambapo katika vinyumba
hivyo huwekwa vyakula, pesa na hata damu wakiamini mizimu
na mizuka huchukua kama sadaka yao kwao.
4.7. Vyakula Ambavyo Hutumika katika Kutekeleza Matambiko
Katika mahojiano na Mama Mahemedi anasema, Mtambiko
katika jamii ya wasambaa yanahitaji maandalizi makubwa
sana ya vyakula kwani huhusisha vyakula mbalimbali
kulingana na uhitaji wa waliotangulia na hata pengine
vyakula ambavyo wahenga walikuwa wanavipendelea. Mara
nyingi sana huwa wanapika makande yasio na maharage,
wali, nyama, maziwa, maji, asali, pombe nazi, pamoja na
matunda mbalimbali kama vile ndizi na mananasi. Vyakula
hivi kikishapikwa huwekwa kwenye vyombo maalumu na
kupelekwa maeneo husika kama makaburini, njia panda,
mapangoni, milimani na hata kumwagwa mtoni wakiamini kuwa
waliotangulia watakula na kupokea sadaka yao na
kuwasamehe pale walipokosea au kuwajalia neema kadha wa
kadha kulingana na mahitaji yao.
57
4.8. Wanyama Wanaotumia Katika Matambiko Katika Jamii ya
Wasambaa.
Mzee Abdi Shekalaghe anasema matambiko ni suala takatiku
sana katika jamii ya wasambaa na linatekeleza kwa
kuhusisha wanyama maalumu kulingana na maaono ya wazee
kutoka kwa wahenga. Wanyama hao ni kama ng’ombe, mbuzi,
kondoo na kuku kulingana na uzito wa tatizo. Katika jambo
hili wanyama hao wanaandaliwa vizuri na husemewa maneno
mbalimbali na maalumu ambapo hufikia hatua mnyama husika
hata awe dume la ng’ombe hulala peke yake na kuchinjwa
bila kuleta fujo ya aina yeyote na katika mchakato wa
kupasua wazee husika huwa wanachunguza baadhi ya mambo
kwenye tumbo la mnyama husika na kung’amua iwapo ombi lao
limepokelewa au la.
Rio (1999) anadai kwamba uhalisiaajabu unahusu matukio
yasiyo ya kawaida au jambo lililo kinyume na uhalisia wa
kawaida. Katika jamii ya wasambaa ni jambo la ajabu
machoni pa watu ambapo Ng’ombe dume anasemewa maneno ya
58
ajabu mpaka analala mwenyewe bila ya kushikwa na watu
tayari kwa kuchinjwa. Katika uhalisia wa kawaida hakuna
jambo kama hilo na haliwezekani. Jambo kama hilo ni la
ajabu mno, hapo inathibitishwa kuwa matambiko yana nguvu
na nafasi kubwa katika jamii ya wasambaa.
4.9. Mambo Yanayosababisha Utekelezaji wa Matambiko
katika Kabila la Wasambaa
Katika mahojiano na watafitiwa Bw na Bi Mashanga
(wataalamu wa matambiko katika ukoo wa Kaniki) wanasema
kama ilivyo kila jamii ina utaratibu wa kufanya mambo na
mahitaji, matatizo pia hutofautiana hivyo katika jamii ya
wasambaa kuna sababu mbalimbali ambazo huwasukuma
wasambaa kufanya matambiko. Wasambaa hawafanyi matambiko
kama sherehe za kidini au kama burudani bali kama sehemu
maalumu kabisa ya kujiweka karibu na miungu yao
wanayoiamini wakiwa na nia moja tu ya kuiabudu sambamba
na kutoa sadaka za makafara kwa miungu yao na mizimu
wanayoamini ina nguvu. Katika mahojiano kati ya mtafiti
59
na wahusika kadha wa kadha katika nyakati tofauti
waibainisha sababu mbalimbali ambazo kwazo lazima
wanajamii watambike. Nazo ni kama ifuatavyo;
I. Taratibu za kikoo pengine kila mwisho wa mwaka
lazima watoe sadaka kwa wazee wao waliotangulia.
II. Ukame unaosababisha watu kukosa chakula maji kwa
muda mrefu kwa wanajamii pamoja na mifugo yao.
III. Mafuriko mfano mwaka 1993 katika jimbo la mlalo
yalitokea mafuriko watu wengi walipoteza maisha na
mali nyingi.
IV. Upotevu wa mali kama ng’ombe wengi mara nyingi
wasambaa wanaamini kuwa mali inapotokea katika
mazingira yasiyoeleweka basi kuna jambo haliko sawa
hivyo matambiko hayakwepeki.
V. Kupotea kwa mtu katika jamii ya wasambaa inapotokea
mtu amepota katika mazingira ya kutatanisha hapo
wanapata ishara kuwa wamekosea mahali Fulani hivyo
lazima wakatoe sadaka.
60
VI. Kumbukumbu ya waliotangulia (wafu waishio kuzimu),
Koo nyingi kulingana na magumu wanayokutana nayo
wameamua kuweka siku maalumu ya kufanya ibada hizo
ili kuepukana na adhabu mabalimbali hususani pale
wanaposahau kufanya matambiko au ibada hizo.
VII. Mahitaji ya Baraka mbalimbali kulingana na baraka
ambazo wasambaa wanaamini ni kwa neema ya miiungu
mizimu wanayoitambikia basi itokeapo mwanafamilia
amepata kile anachoamini ni Baraka hana budi kwenda
kufanya tambiko.
VIII. Katika jamii ya wasambaa itokeapo ajali miongoni mwa
wanaukoo wao wanachukulia ni adhabu kutoka kwa
waliotangulia hivyo ili kuwatuliza ni lazima kufanya
tambikoili kuwanususu na mambo kama hayo.
IX. Mara nyingi vifo vya kutatanisha huwapa hofu watu
wengi kadhalika katika jamii ya wasambaa vifo
ambavyo chanzo chake hakipo wazi ni lazima watu
warudi nyuma na kutafakari pale walipokosea na
kufanya tambiko.
61
X. Magonjwa katika jamii ya wasambaa magonjwa ya
mlipuko pia huhusianishwa na kukosea wahenga hivyo
itokeapo magojwa ya aina hii kama tauni ambayo
iliathiri sana watu wa jamii ile matambiko
yalifanywa ili kuomba radhi.
XI. Shukrani za Baraka walizopata, Baraka mbalimbali
kama kunusurika kufa, kupata motto, kufaulu masoma,
kujenga nyumba,kununua gari na mambo kama hayo
matambiko hufanywa ili kufungua njia kwa wanajamii
hao.
4.10. Muda Ambao Matambiko Hufanywa
Mzee Kaniki, A.I anasema matambiko katika jamii ya
wasambaa hufanywa katika vipindi maalumu kwani jamii ina
mambo ambayo ni ya msimu na mengine ni ya dharula.
Ngwatu, H.M anasema kabla ya mvua za vuli wanajamii
hujipanga kwa ajili ya matambiko ili kupata Baraka au
kufunguliwa njia kwa ajili ya shughuli za kilimo ambapo
baada ya hapo wazee kwa kushirikiana na wataalamu wa
62
mambo ya matambiko huandaa maji maalumu ambayo ni
mchanganyiko wa udongo, maji, unga wa nafaka mbalimbali
baada ya kuomba mambo kadha wa kadha vijana hutumwa
kwenda kunyunyiza maji hayo maalumu shambani (hande)
ambapo hakuna mwanajamii anayeruhusiwa kuanza kufanya
shughuli zozote za kilimo mpaka vijana wapiti au kumaliza
shughuli hiyo muhimu na baada ya vijana hao kumaliza ni
lazima watu wakae siku tatu ama nne ili maombi yao
yafike. Lengo ni kuomba Baraka, msamaha kwa miungu na
mizimu pamoja na kuwaondolea nuksi mbalimbali kunzia
nyumbani mpaka mashambani na hata katika shughuli zao
zote katika msimu huo, hapo wanajamii wanakuwa wamepata
ruhusa ya kuanza kuandaa mashamba tayari kwa msimu wa
kilimo. Kadhalika baada ya mavuno matambiko pia hufanywa
kwa lengo la kutoa shukrani kwa miuungu hao.
Matambiko pia hufanywa muda wowote patokeapo dharula kama
magonjwa ya mlipuko, ajali na mambo kama hayo ambayo
hutokea bila taarifa.
63
4.11. Uhalisia Mazingaombwe/Uhalisia Ajabu wa Nafasi ya Matambiko Katika Jamii ya Wasambaa
TUKI (2009) wanasema hii ni dhana iliyobuniwa na msanii
wa ujerumani Franz Roh, katika kitabu chake Nach-
expressionnism, magischer realismus.Probleme der neusten
europaischer malalerei. Dhana hii huhusishwa na waandishi
wa marekani ya kusini au hata nchi zinazoitwa ulimwengu
wa tatu na hutambulishwa na sifa mbalimbali. Sifa hizi ni
za kuyaelezea matukio ya kifantasia au ya ajabu au
kichawi kwa namna ya moja kwa moja kwa namna inayofanana
yaonekana kama ya kawaida tu. Mpaka uliopo kati ya mambo
yanayoweza kupatikana katika ulimwengu halisi na
yasiyowezakana huwa madogo sana. Sababu hasa ya matumizi
ya mtindo huu ni kuonesha kuwa matukio ya aina hii
hupatikana katika maisha ya kawaida katika jamii
zinazohusika. Nadharia hii inasisitiza kuwa fasihi
haiwezi kujitenga na hali halisi ya maisha ya watu katika
jamii ambamo fasihi imeundwa na kutumika.Waandishi
wanaoandika katika msingi huu hushikilia kuwa mtizamo wao
64
wakiuhalisia unawakilisha msimamo wa jamii zao. Yaani
mambo yanayotekelezwa kama ya ajabu na kichawi ni sehemu
ya mwonoulimwengu wa jamii hizo. Mtazamo huu umemuongoza
mtafiti wa tasnia hii kung’amua kuwa matambiko katika
jamii ya wasambaa kwamba hufanywa kwa sababu matatizo au
changamoto mbalimbali yanakuwepo ndani ya jamii ya
wasambaa na matambiko katika hatua za utekelezaji wake
panakuwepo na uhalisia mkubwa kwa sababu vitu
vinavyotumika ni vya asili mno na uajabu au mazingaobwe
ni zile ishara kubwa zitokeazo mfano alama zionekanazo
katika tumbo la mnyama husika, mnyama kulala peke yake na
kuchinjwa, radi na mvua kubwa baada ya tambiko ikiwa ni
ishara ya kupokelewa kwa sadaka husika, kwa kututia
nadharia hii mtafiti ametazama nafasi ya matambiko katika
jamii ya wasambaa.
4.12. Hitimisho
Katika sura hii mtafiti amejikita katika kuchambua data
mbalimbali zilizopatikana na zinazohusu nafasi ya
65
matambiko katika jamii ya wasambaa. Mtafiti ameangalia
pia vipindi ambavyo matambiko hufanywa, vifaa vitumikavyo
katika zoezi la matambiko katika jamii ya wasambaa,
wahusika, vyakula vinavyotumika pamoja na mavazi
yanayotumika huku akiongozwa na nadharia ya uhalisia wa
mazingaobwe. Nadharia hii uhalisia mazingaobwe/uhalisia
ajabu (Magical Realist theory) imekuwa msaada mkubwa
katika kukamilisha utafiti huu kwani mtafiti ameweza
kubaini umuhimu, hasara, sababu pamoja na namna ambavyo
matambiko hufanywa katika jamii ya wasambaa. Vizazi vya
leo vinaenda kusahau na kuacha utanzu huu muhimu wa
fasihi simulizi hivyo mtafiti aliliona hilo na ndio
sababu kuu iliyomsukuma kufanya utafiti huu ili kutunza
na kuiendeleza fasihi ya wasambaa.
SURA YA TANO
HITIMISHO MUHTASARI NA MAPENDEKEZO
66
5.1Utangulizi
Tunapoongelea juu ya nafasi ya matambiko katika jamii ya
wasambaa, hapa tunaangalia na kubainisha umuhimu wa
matambiko, hasara za matambiko, wahusika wa matambiko
pamoja na mandhari au eneo matambiko yanapofanyika.
Mtafiti katika sura ya nne alichambua na
kubainishaumuhimu wa matambiko, hasara za matambiko,
wahusika wa matambiko pamoja na mandhari.
Vilevile mtafiti amechambua na kubainisha kwa kina
vipindi, mambo yanayosababisha kufanyika matambiko, vifaa
vinavyotumika katika matambiko, vyakula vinavyotumika
katika matambiko, miungu/mizimu inayotambikiwa, wanyama
watumikao, mavazi pamoja na msaada unaopatikana kwa
kufanya matambiko.
5.2 Muhtasari
Tasnifu hii imechunguza nafasi ya matambiko katika jamii
ya wasambaa inayopatikana kaskazini mashariki mwa
67
Tanzania, mkoani Tanga wilaya ya Lushoto katika tarafa ya
Mtae, kata ya Rangwi na kijiji cha Emao.
Sura ya kwanza inahusu utangulizi wa jumla ambao ulianza
kuelezea dhana ya Matambiko kwa kurejelea wataalam
mbalimbali, usuli wa utafiti, tatizo la utafiti. Malengo
ya utafiti, maswali ya utafiti, mipaka ya utafiti,
umuhimu wa utafiti pamoja na Nadharia ya utafiti
iliyomwongoza mtafiti katika kukamilisha utafiti wake.
Sura ya Pili inahusu mapitio ya machapisho mbalimbali
ambapo uchambuzi, tahakiki na tafiti mbalimbali
zimezofanywa na wataalam tofauti tofauti zilipitiwa
kutoka maktabani na mtandaoni, Mtafiti amewasoma wataalam
hao na kuweza kupata mwanga halisi na kuweza kufanya
utafiti huu, aidha kwa kurejelea nukuu mbalimbali katika
sehemu zinazohitajika bila kuongeza maneno ili
kukamilisha utafiti huu.
Sura ya Tatu inahusu mbinu za utafiti ambazo mtafiti
amezitumia katika utafiti huu, katika sura hii mbinu za
68
utafiti kama vile maktabani, uwandani na mtandaoni
zilitumika, sampuli na usampulishaji ziliweza kutumika
katika kukusanya data kwa kutumia vifaa maalumu kama vile
shajara, kalamu, kompyuta, kinyonyi na penseli katika
kunukuu data za msingi na data fuatizi katika kukamilisha
utafiti huu.
Sura ya nne inahusu uwakilishi na uchambuzi wa data. Hapa
data zilizokusanywa zimechakatwa kwa kuzingatia Nadharia
husika iliyomwongoza Mtafiti katika utafiti huu kwa lengo
la kuonyesha nafasi ya matambiko katika jamii ya wasambaa
umuhimu wake na hasara zake.
Sura ya tano ndiyo sura ya mwisho katika tasnifu hii,
sura hii inahusu utangulizi ambao ulieleza kwa kifupi
sura ya nne ilihusu nini pamoja na sura yenyewe
inazungumzia nini. Pia Mtafiti ameangalia muhtasari wa
tasnifu hii, Mchango mpya wa utafiti huu pamoja na
Mapendekezo mengine ya utafiti. Mtafiti katika sura hii
69
amebainisha maeneo mbalimbali ya kufanyiwa utafiti na
wanazuoni wengine katika hatua mbalimbali za kataaluma.
5.3 Mchango Mpya wa Utafiti Huu.
Utafiti huu umefanikiwa katika kubainisha nafasi ya
matambiko katika jamii ya wasambaa, umuhimu, hasara,
vipindi, mazingira, vyakula vitumi kavvyo na ujumbe
unaopatikana katika matambiko kwa jamii ya wasambaa na
wale ambao sio wasambaa. Hivyo basi Utafiti huu utakuwa
na umuhimu mkubwa katika tansinia hii ya nafasi ya
matambiko katika jamii ya wasambaa kwa kuwa umeweza
kubainisha umuhimu, hasara, wanyama watumikao, mavazi
yatumikayo mazingira yanayotumika pamoja na ujumbe ambapo
umeweza kuwapa mwanga wasambaa na hata wale ambao sio
wasambaa. Pia Utafiti huu utaamsha hisia za wasomaji na
kuchochea wanafasihi kuchunguza namna matambiko
yanavyoweza kutumika katika kufikisha ujumbe kwa jamii.
Aidha Utafiti huu utatoa mwanga kwa watafiti wengine
70
ambao watajikita katika suala zima la nafasi ya matambiko
katika jamii ya wasambaa mkoani Tanga.
5.4 Mapendekezo
Matambiko yana nafasi kubwa katika jamii ya kitanzania
kwani hutumika kuakisi masuala mbalimbali kwenye jamii
katika nyanja za kijamii, kiitikadi, kisiasa na kiuchumi
kama zilivyo tanzu nyingine za kifasihi. Hivyo mtafiti
anapendekeza tafiti zijazo zichunguze matambiko kwa
ujumla, ikiwa ni pamoja na kubaini aina nyingine za
matambiko. Pendekezo lingine kwa tafiti zijazo ziangalie
pia matambiko nje na ndani ya nchi yetu kwa lengo la
kukuza na kutunza fasihi ya jamii za kitanzania.
5.5 Matokeo ya Utafiti
Mtafiti alitimiza lengo la utafiti wake kwani kupitia
nafasi ya matambiko katika kabila la wasambaa, mtafiti
aliweza kuonesha umuhimu wa utafiti huu kwa wasomaji wa
tasnifu hii na jami ya wasambaa kwa ujumla. Kupitia
nadharia ya Uhalisia wa mazingaombwe, mtafiti ameweza
71
kuchambua matambiko katika kabila la wasambaa jinsi
yanavyofanywa, mazingira, wahusika, umuhimu na hata
athari zake.
Mambo hayo ndiyo yaliyomsukuma mtafiti kuweza kufanyia
utafiti wake na kuonesha jinsi umuhimu wa matambiko,
athari za matambiko, vyakula ambavyo hutumika katika
matambiko, wanyama wanaotumika katika matambiko ya
wasambaa.
5.6 Hitimisho
Katika sura hii ya Tano Mtafiti ameweza kuangalia
muhtasari wa mada kupitia sura zote tano, Mchango mpya wa
Utafiti huu pamoja na Mapendekezo kuhusu tafiti zijazo.
Ni matumaini ya mtafiti kuwa kazii hii ni mwanzo na
muendelezo wa kazi nyingine nyingi.
Marejeo
72
Assumpta, K.M. (2011) Fani ya Fasihi Simulizi kwa Shule za Upili,
Oxford university press.
Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) (2010) Kamusi ya Kiswahili
( toleo jipya) Oxford University Nairobi
Kamusi ya Karne ya 21 (2011) Longhorn Publishers (T) Ltd,
Nairobi. Kenya.
Kamusi ya Kiswahili Sanifu (2004) Oxford University Press.
Kenya.
Kirama, Kh. (1953) Habari za Wakilindi, Vuga Press
Kitula, K.- Catherine, N.M.K (2010) Misingi ya Fasihi Simulizi,
Kenya litearure Bereau.
Kothari, C. R. (1991) Research Methodology. Methods and Techning,
(2rd Edition). Wiley Eastern Limited. New Delh.
Masebo, J. A. (2007) Nadharia ya Fasihi Kidato cha Tano na Sita,Nyambari Nyangwine publishers.
Materu, B. L. (1982) Tanzu za Fasihi Simulizi Mulika namba 19,
Taasisi ya uchunguzi wa Kiswahili chuo kikuu cha Dar es
Saalam.
Mulokozi M. M. (1996) Fasihi ya Kiswahili OSW. Chuo kikuu cha
Dar es Salaam
Salimu, K. B.(1992) Kamusi ya Maana na Matumizi. Oxford univeritypress Nairobi, Dar es Salaam na Kampala.
73
Taasisi ya uchunguzi wa kiswahili (2008) Kamusi ya Kiswahili Sanifu,Nairobi, Kenya, University press, East Afrika L.t.d
Mng’anuth, K. T. (2007/2008) Fasihi Simulizi na Utamaduni,
Autolitho Ltd Nairobi Kenya.
TUKI (2004) Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Oxford University Press
TUKI (2009:63) Nadharia za Uhakiki wa Kazi za Fasihi, Oxford University
Press
TUMI (1988) Kiswahili kwa Shule za Sekondari; Chuo kikuu cha Dar
es Salaam
Wafula, R. M - Kimani, N. (2007) Nadharia ya Uhakiki wa Fasihi.
Jomo Kenyata Foundation. Nairobi.
Wamitila, K.W. (2008) Kanzi ya Fasihi, Misingi ya Uchanganuzi wa
Fasihi, Nairobi, Public Vide Muwa Publisher Limited.
Wamitila, K.W. (2006) Fasihi Istilahi na Nadharia, Nairobi
Phoenix publisher Ltd.
Wamitila, K.W. (2006) Uhakiki wa Fasihi Msingi na Vipengele Vyake,
Nairobi Phoenix publisher Ltd.
Wamitila, K.W.(2003) Kamusi ya Fasihi, Istilahi na Nadharia. EnglishPress Nairobi.
Wikipedia, Kamusi elezo huru, (2013) “Historia ya
Wasambaa”, http://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=washambaa&oldid=
889928 jamii (21/12/2013 saa 07:58)
74
Wikipedia, Kamusi elezo huru, (2013 “Milima ya Usambara,
http://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=milima ya usambara&oldid=
889928 jamii (09/02/2013 saa 10:56)
Wikipedia, Kamusi elezo huru, (2013) “Tarafa ya Mtae”,
http://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=mtae&oldid=451923jamii
(10/03/2014) (saa 15:53)
Wikipedia, Kamusi elezo huru, (2014) “Fasihi Simulizi ya
Kiafrika”, http://chomboz.blog.com/p/maisha.html (07/03/2014 saa
10:56)
Wikipedia, Kamusi elezo huru, (2014) “Matambiko na
Ushirikina”, [email protected] (10/02/2014) (saa
15:53)
75