Njoo, Unifuate— Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili

130
AGANO LA KALE 2022 Njoo, Unifuate— Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili Kuishi, Kujifunza na Kufundisha Injili ya Yesu Kristo

Transcript of Njoo, Unifuate— Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili

AGANO LA KALE 2022

Njoo, Unifuate— Kwa Ajili ya Shule ya JumapiliKuishi, Kujifunza na Kufundisha Injili ya Yesu Kristo

NJO

O, U

NIFU

ATE—KW

A A

JILI YA SH

ULE YA

JUM

APILI: A

GA

NO

LA KA

LE 2022

AGANO LA KALE 2022

Njoo, Unifuate— Kwa Ajili ya Shule ya JumapiliKuishi, Kujifunza na Kufundisha Injili ya Yesu Kristo

Kimechapishwa na Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho Jijini Salt Lake, Utah

© 2021 na Intellectual Reserve,Inc.All rights reserved.Toleo: 8/19Tafsiri ya Come, Follow Me—For Sunday School: Old Testament 2022Swahili17091 743Kimepigwa chapa MarekaniMaoni na masahihisho yanakubaliwa. Tafadhali yatume, ukijumuisha makosa hayo, kwenda [email protected].

Njoo, UNIfUate—K wa ajIlI Ya ShUle Ya jUmapIlI : agaNo l a K ale 2022

YaliyomoNyenzo za Utangulizi

Wewe ni Mwalimu katika Kanisa la Yesu Kristo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . viiKutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . viiiMawazo ya Kuhimiza Kujifunza Binafsi na kama Familia . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . xNyenzo za Ziada . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . xiMpangilio wa Kufundisha . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .xiiMuhtasari wa Agano la Kale . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . xiii

Desemba 27–Januari 2: Musa 1; Ibrahimu 3 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 1Januari 3–9: Mwanzo 1–2; Musa 2–3; Ibrahimu 4–5 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 3Januari 10–16: Mwanzo 3–4; Musa 4–5 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 5Januari 17–23: Mwanzo 5; Musa 6 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 7Januari 24–30: Musa 7 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 9Januari 31–Februari 6: Mwanzo 6–11; Musa 8 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11Februari 7–13: Mwanzo 12–17; Ibrahimu 1–2 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 13Februari 14–20: Mwanzo 18–23 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15Februari 21–27: Mwanzo 24–27 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 17Februari 28–Machi 6: Mwanzo 28–33 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 19Machi 7–13: Mwanzo 37–41 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 21Machi 14–20: Mwanzo 42–50 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 23Machi 21– 27: Kutoka 1– 6 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 25Machi 28–Aprili 3: Kutoka 7–13 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 27Aprili 4–10: Kutoka 14–17 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 29Aprili 11–17: Pasaka . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 31Aprili 18–24: Kutoka 18–20 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 33Aprili 25–Mei 1: Kutoka 24; 31–34 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 35Mei 2–8: Kutoka 35–40; Mambo ya Walawi1; 16; 19 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 37Mei 9–15: Hesabu 11–14; 20–24 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 39Mei 16–22: Kumbukumbu la Torati 6–8; 15; 18; 29–30; 34 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 41Mei 23–29: Yoshua 1–8; 23–24 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 43Mei 30–Juni 5: Waamuzi 2–4; 6–8; 13–16 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 45Juni 6–12: Ruthu; 1Samweli 1–3 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 47Juni 13–19: 1 Samweli 8–10; 13; 15–18 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 49Juni 20–26: 2 Samweli 5–7; 11–12; 1 Wafalme 3; 8; 11 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 51Juni 27–Julai 3: 1 Wafalme 17–19 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 53Julai 4–10: 2 Wafalme 2–7 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 55

Julai 11–17: 2 Wafalme 17–25 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 57Julai 18–24: Ezra1; 3–7; Nehemia 2; 4–6; 8 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 59Julai 25–31: Esta . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 61Agosti 1–7: Ayubu 1–3; 12–14; 19; 21–24; 38–40; 42 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 63Agosti 8–14: Zaburi 1–2; 8; 19–33; 40; 46 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 65Agosti 15–21: Zaburi 49–51; 61–66; 69–72; 77–78; 85–86 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 67Agosti 22–28: Zaburi 102–103; 110; 116–119; 127–128; 135–139; 146–150 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 69Agosti 29–Septemba 4: Mithali 1–4; 15–16; 22; 31; Mhubiri 1–3; 11–12 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 71Septemba 5–11: Isaya 1–12 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 73Septemba 12–18: Isaya 13–14; 24–30; 35 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 75Septemba 19–25: Isaya 40–49 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 77Septemba 26–Oktoba 2: Isaya 50–57 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 79Oktoba 3–9: Isaya 58–66 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 81Oktoba 10–16: Yeremia 1–3; 7; 16–18; 20 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 83Oktoba 17–23: Yeremia 30–33; 36; Maombolezo 1; 3 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 85Oktoba 24–30: Ezekieli 1–3; 33–34; 36–37; 47 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 87Oktoba 31–Novemba 6: Danieil 1–6 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 89Novemba 7–13: Hosea 1–6; 10–14; Yoeli . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 91Novemba 14–20: Amosi; Obadia . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 93Novemba 21–27: Yona; Mika . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 95Novemba 28–Desemba 4: Nahumu; Habakuki; Sefania . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 97Desemba 5–11: Hagai; Zekaria 1–3; 7–14 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 99Desemba 12–18: Malaki . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 101Desemba 19–25: Krismasi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 103

vii

Wewe ni Mwalimu katika Kanisa la Yesu Kristo

Umeitwa na Mungu kufundisha watoto Wake katika njia ya Mwokozi . Umesimikwa katika wito huu kwa mamlaka ya ukuhani Wake mtakatifu . Hata kama wewe sio mwalimu mwenye uzoefu, kadiri unavyoishi kwa kustahili, kusali kila siku, na kujifunza maandiko, Baba wa Mbinguni atakuzawadia ushawishi na nguvu za Roho Mtakatifu ili kukusaidia kufanikiwa (ona 2 Nefi 33:1) .

Wale waliowekwa chini ya uangalizi wako ni watoto wa Baba wa Mbinguni, na Yeye anajua kile wanachohitaji na jinsi ya kuwafikia vizuri zaidi . Kupitia Roho Mtakatifu, Mungu atakuongoza wakati wa maandalizi yako na wakati unapofundisha . Atakufunulia kile unachopaswa kusema na unachopaswa kufanya (ona 2 Nefi 32:5) .

Madhumuni muhimu ya kufundisha injili na kujifunza ni kuzidisha uongofu katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo . Lengo lako kama mwalimu ni kuwasaidia wale unaowafundisha kufanya kila wawezacho kuwa waongofu zaidi—juhudi ambazo huenda zaidi ya muda wa darasani . Waalike wale unaowafundisha kushiriki kikamilifu katika kujifunza kuhusu Yesu Kristo na injili Yake

na kutenda yale wanayojifunza . Wahimize kufanya kujifunza kwao binafsi na kwa familia nje ya darasa kuwa lengo la msingi la kujifunza injili kwao . Wanapotenda kwa imani kwa kujifunza kama watu binafsi na familia, watamwalika Roho katika maisha yao na ni Roho ambaye ataleta uongofu wa kweli . Kila kitu ufanyacho kama mwalimu hakina budi kuelekeza katika lengo hili takatifu .

Fundisha tu mafundisho ya injili ya urejesho ya Yesu Kristo kama yanavyopatikana katika maandiko na maneno ya manabii wa siku za mwisho . Mafundisho safi—ya milele, ukweli usiobadilika uliofundishwa na Mungu na watumishi Wake—humwalika Roho na yana nguvu ya kubadilisha maisha .

Wito wa kufundisha ni wajibu mtakatifu, na ni kawaida kuhisi kuzidiwa wakati mwingine . Lakini kumbuka kwamba Baba yako wa Mbinguni ndiye aliyekuita, na Yeye hatakuacha kamwe . Hii ni kazi ya Bwana na unapohudumu “kwa moyo, uwezo, akili na nguvu zako zote” (Mafundisho na Maagano 4:2), Yeye ataongeza uwezo wako, kipawa, na vipaji, na huduma yako itabariki maisha ya wale unaowafundisha .

viii

Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili

Kujiandaa Kufundisha katika Shule ya Jumapili

Kujifunza binafsi na kama familia nyumbani kunapaswa kuwa kitovu cha kujifunza injili . Hii ni kweli kwako na kwa wale unaowafundisha . Unapojiandaa kufundisha, anza kwa kuwa na uzoefu wako mwenyewe katika maandiko . Maandalizi yako muhimu zaidi yatatokea wakati unapopekua maandiko na kutafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu .

Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia ni sehemu muhimu kwa vyote kujifunza kwako binafsi na maandalizi yako ya kufundisha . Itakusaidia kupata uelewa wa kina wa kanuni za mafundisho zinazopatikana katika maandiko . Itakuwezesha pia kuwatia moyo na kuwaalika washiriki wa darasa kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia ili kuboresha kujifunza maandiko kwao binafsi na kama familia (kwa msaada katika hili, ona “Mawazo ya Kuhimiza Kujifunza Binafsi na Kifamilia” katika nyenzo hii) . Unapofanya hivi, kumbuka kuwa makini kwa washiriki wa

darasa ambao mazingira ya familia zao yanaweza yasiruhusu kujifunza maandiko kama familia na jioni ya familia nyumbani kila mara .

Wakati wa maandalizi yako, mawazo na fikra vitakujia kuhusu watu unaowafundisha, jinsi kanuni katika maandiko zitakavyobariki maisha yao, na jinsi unavyoweza kuwatia moyo kuzigundua kanuni hizo wanapojifunza maandiko kwa ajili yao wenyewe .

Mawazo ya Kufundisha

Unapojiandaa kufundisha, ungeweza kupata mwongozo wa ziada kwa kuchunguza mihutasari katika nyenzo hii . Fikiria mawazo haya kama sio maelekezo ya hatua kwa hatua lakini badala yake ni kama mapendekezo ya kuchochea kupata mwongozo wako mwenyewe . Unawajua washiriki wa darasa lako, na utapata kuwajua hata vizuri zaidi pale mnapojifunza pamoja darasani . Bwana anawajua pia, na atakupa mwongozo wa njia nzuri zaidi za kuwasaidia washiriki wa darasa kujenga juu ya kujifunza injili wanakofanya majumbani mwao .

KUtUmIa Njoo, UNIfUate—K wa ajIlI Ya ShUle Ya jUmapIlI

ix

Nyenzo nyingine nyingi zinapatikana kwa ajili yako ili kuweza kutumia wakati unapojiandaa, ikiwa ni pamoja na mawazo katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia na magazeti ya Kanisa . Kwa maelezo zaidi kuhusu nyenzo hizi na zingine, ona sehemu yenye kichwa cha habari “Nyenzo za Ziada” ndani ya nyenzo hii .

Baadhi ya vitu vya Kukumbuka• Kujifunza Injili kunafanikiwa zaidi wakati kitovu

chake kinapokuwa nyumbani . Kama mwalimu, una wajibu muhimu wa kuunga mkono, kutia moyo, na kujenga juu ya washiriki wa darasa kujifunza injili nyumbani .

• Uongofu wa washiriki wa darasa katika Yesu Kristo na injili Yake utaongezeka wanapoelewa na kutumia mafundisho ya kweli . Wahimize kuandika na kutendea kazi misukumo wanayopokea kutoka kwa Roho Mtakatifu .

• Kufundisha ni zaidi ya kutoa mhadhara, lakini pia ni zaidi ya kuongoza tu majadiliano . Sehemu ya wajibu wako ni kutia moyo ushiriki ambao unaadilisha na msingi wake ukiwa katika maandiko . Unapaswa pia kushiriki umaizi wenye kushawishi ambao ulipokea pale ulipojifunza maandiko .

• Kumbuka kwamba washiriki wengi wa darasa wanapata uzoefu wa maana wanapojifunza maandiko yale yale nyumbani ambayo mtajadili darasani . Unaweza kuunga mkono kujifunza maandiko kwa kuwapa nafasi za kila mara za kuelezea wanachojifunza nyumbani .

• Baba wa Mbinguni anataka wewe ufanikiwe kama mwalimu . Ametoa nyenzo nyingi ili kukusaidia, ikiwa ni pamoja na mikutano ya baraza la walimu . Katika mikutano hii unaweza kushauriana na walimu wengine kuhusu changamoto zinazokukabili . Unaweza pia kujadili na kufanyia mazoezi kanuni za kufundisha kama Kristo .

• Watu hujifunza vizuri zaidi wanapokuwa na nafasi ya kufundisha . Mara kwa mara, fikiria kuwaruhusu washiriki wa darasa, ikijumuisha vijana, kufundisha sehemu ya somo . Fanya uamuzi huu kulingana na mahitaji na uwezo wa washiriki wa darasa . Kama unamualika mshiriki wa darasa kufundisha, chukua muda kumsaidia kujiandaa mapema kwa kutumia mawazo yanayopatikana katika nyenzo hii na katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Kumbuka kwamba kama mwalimu aliyeitwa, unawajibika ipasavyo kwa kile kinachofundishwa katika darasa .

Nyenzo hii inajumuisha muhtasari wa kufundisha kwa kila wiki ya mwaka . Wakati wa Jumapili ambayo Shule ya Jumapili haifanyiki, washiriki wa darasa wanaweza kuendelea kusoma Agano la Kale nyumbani kufuatana na ratiba ya muhtasari katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Wakati Shule ya Jumapili inafanyika, unaweza kuchagua kuruka somo au kuunganisha masomo mawili .

x

Mawazo kwa Ajili ya Kuhimiza Kujifunza Binafsi na kama Familia

Haya ni baadhi ya mawazo kukusaidia wewe kuwahimiza washiriki wa darasa kujifunza neno la Mungu nyumbani, kama mtu binafsi na kama familia . Kuwa makini kwenye ukweli kwani si washiriki wote wanaweza kujifunza maandiko pamoja na familia zao (kwa mfano, baadhi ya waumini wanaishi peke yao au ni muumini katika familia ambayo baadhi tu ni waumini) .

• Waalike washiriki wa darasa kushiriki na wengine uzoefu waliokuwa nao walipojifunza maandiko nyumbani . Kwa mfano, ungeweza kuwaomba waelezee mstari ambao uliwavutia na waelezee kwa nini waliona ni wa maana .

• Waombe washiriki wa darasa watoe mifano ya nini wanachokifanya ili kufanya kujifunza binafsi au kama familia kuwa na maana zaidi . (Baadhi ya mawazo yanaweza kupatikana chini ya “Mawazo ya Kuboresha Kujifunza Kwako Maandiko Binafsi” na “Mawazo ya Kuboresha Kujifunza Maandiko kwa Familia Yako” katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia.)

• Waombe washiriki wa darasa washiriki jinsi walivyofanya katika misukumo waliyopokea wakati wa kujifunza kwao binafsi maandiko au kama familia .

• Chukua dakika chache kuonyesha washiriki wa darasa baadhi ya nyenzo zinazotolewa na Kanisa ili kuwasaidia waumini kujifunza injili nyumbani . Nyenzo hizi zinajumuisha misaada ya kujifunza maandiko inayopatikana kwenye scriptures .ChurchofJesusChrist .org; “Hadithi za Maandiko” zinazopatikana kwenye children .ChurchofJesusChrist .org; mihutasari ya kufundisha na nyenzo zingine Njoo, Unifuate Kwa Ajili Ya Msingi; maudhui yanayolenga vijana kwenye youth .ChurchofJesusChrist .org; vitabu vya Kiada vya Seminari na Chuo; na video, sauti zilizonaswa, na picha zinazopatikana kwenye MediaLibrary .ChurchofJesusChrist .org . Nyingi za hizi zipo pia kwenye Gospel Library app .

• Tumia dakika chache kuelezea jinsi ya kutumia Gospel Library app ili kujifunza maandiko, ikijumuisha jinsi ya kuwekea alama mistari na kuandika misukumo .

• Mwalike mshiriki mmoja wa darasa au zaidi kusimulia jinsi walivyofundisha kanuni mahususi za injili katika familia zao .

NYeNzo z a zIada

xi

Nyenzo za Ziada

Nyenzo hizi zinaweza kupatikana katika app ya Makataba ya Injili kwenye ChurchofJesusChrist .org .

Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za WatotoMuziki mtakatifu humwalika Roho na hufundisha injili katika njia ya kukumbukwa . Katika kuongezea kwenye matoleo yalilochapishwa ya Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto, unaweza kupata rekodi za sauti na video za nyimbo nyingi za kanisa na nyimbo za watoto kwenye music .ChurchofJesusChrist .org na katika app za Music na Gospel Media .

Vitabu vya Kiada vya Seminari na ChuoVitabu vya kiada vya seminari na chuo vinatoa chimbuko la kihistoria na fasili ya mafundisho kwa kanuni zinazopatikana katika maandiko . Vinaweza pia kuchochea mawazo ya kufundisha kwa ajili ya madarasa ya Shule ya Jumapili .

Magazeti ya KanisaMagazeti ya Liahona na Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana yanatoa makala na tarifa zingine ambazo zinaweza kuongezea kanuni unazofundisha kutoka katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili.

Mada za InjiliKwenye Mada za Injili (topics .ChurchofJesusChrist .org) unaweza kupata taarifa muhimu kuhusu mada mbali mbali za injili, pamoja na viunganisho kwenye nyenzo saidizi kama vile mahubiri ya mkutano mkuu yanayoshabihiana, makala, maandiko, na video . Unaweza pia kupata Insha za Mada za Injili, ambazo hutoa majibu ya kina ya maswali ya injili na ya kihistoria .

Hubiri Injili YanguMwongozo huu wa wamisionari hutoa muhtasari wa kanuni za msingi za injili .

Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana (kijitabu)Nyenzo hii inatoa muhtasari wa viwango vya Kanisa ambavyo vinaweza kutusaidia kuishi injili na kufurahia wenza wa Roho . Unaweza kuirejelea mara kwa mara, hasa ikiwa unawafundisha vijana .

Video na SanaaSanaa za mchoro, video, na vyombo vingine vya habari vinaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kupata taswira ya mafundisho na hadithi zinazohusiana na maandiko . Tembelea Gospel Media katika MediaLibrary .ChurchofJesusChrist .org ili kupitia pitia mkusanyiko wa nyenzo za habari za Kanisa . Gospel Media pia inapatikana kama app ya simu ya mkononi . Picha nyingi ambazo unaweza kutumia katika darasa zinapatikana katika Kitabu cha Sanaa ya Injili.

Kufundisha katika Njia ya MwokoziKufundisha katika Njia ya Mwokozi inaweza kukusaida kujifunza kuhusu, na kutumia kanuni za kufundisha kama Kristo . Kanuni hizi zinajadiliwa na kutumiwa katika mikutano ya baraza la walimu .

xii

Mpangilio wa Kufundisha

Kila muhtasari katika nyenzo hii hufuata mpangilio wa kualika kushiriki na kufundisha mafundisho .

Alika Kushiriki

Kama sehemu ya kila darasa, waalike washiriki wa darasa kushiriki na wengine umaizi na uzoefu waliokuwa nao wiki iliyopita walipojifunza maandiko wao binafsi na kama familia na kutendea kazi kile walichojifunza . Wasaidie washiriki wa darasa kuona kwamba kujifunza kwao binafsi nje ya darasa ni muhimu . Uongofu wao binafsi utakuja sio tu kupitia mafunzo ya Jumapili bali pia kupitia matukio yao ya kila siku . Wakati washiriki wa darasa wanaposikia uzoefu na ushuhuda wa kila mmoja wao kuhusu injili ya Yesu Kristo, wana uwezekano wa kutafuta uzoefu sawa na huo wa kwao wenyewe .

Si kila mmoja atakuwa ameshasoma sura za kila somo, na hata baadhi ya wale waliosoma wanaweza kuhisi hofu kushiriki na wengine . Hakikisha washiriki wote wa darasa wanajiona kuwa wao ni sehemu ya thamani ya darasa, bila kujali wana kitu cha kushiriki na wengine au la .

Fundisha Mafundisho

Wewe na washiriki wa darasa lako mnapaswa kufokasi katika Yesu Kristo na mafundisho Yake—ukweli wa milele wa injili—unaopatikana katika vipengele vya maandiko vilivyotolewa . Unapojadili mafundisho kutoka kwenye maandiko, ni mistari ipi, dondoo zipi, uzoefu upi, maswali yapi, na nyenzo zipi za ziada ungeweza kushiriki na wengine? Ungewezaje kutumia nyenzo hizi kuwasaidia washiriki wa darasa kugundua na kuelewa kanuni za injili? Je, unawezaje kuwasaidia kujenga imani yao kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?

KUTOROKA KWENDA AMERIKA

PATRIAKI

KUTOKA

WAAMUZI

UFALME ULIOUNGANA

FALME ZILIZOGAWANYIKA (Ufalme wa Kusini) (Ufalme wa Kaskazini)

Adamu na Hawa

Henoko

Musa na Sipora

Ruthu

Samweli

Debora

Sauli

Gideoni

Daudi

Samsoni

Sulemani

Nuhu

Yoshua

Hana

Ibrahimu na Sara

Melkizedeki

Isaka na Rebeka

Yakobo na Lea, Raheli, Bilha, Zilpa

Yusufu na Asenathi

Isaya Mika

Nahumu Yoeli? Yeremia Obadia

Hagai Zekaria

Malaki?

Ezra

Sefania Habakuki

Eliya Elisha

Amosi, Yona na Hosea

Rehoboamu Uzia

Hezekia

Yosia

Zedekia

Zerubabeli

Ona pia “Mpangilio wa Matukio kwenye Bibilia” katika kiambatisho cha Biblia.

Yeroboamu I

Yeroboamu II Hoshea

Ahabu

Lehi na Saria Muleki

KUCHUKULIWA UTUMWANI (597 KK)

KUCHUKULIWA UTUMWANI (586 KK)

KURUDI YERUSALEMU (Miaka 530 BC)

KURUDI YERUSALEMU (Katikati ya miaka ya 400 KK)

Ezekieli Danieli

Esta

MAKABILA KUMI YA ISRAELI Kushindwa na Asiria na kutawanywa (722 KK)

Muhtasari wa Agano la Kale

BABELI

YUDA ISRAELI

PERSIA

1

DESEMBA 27–JANUARI 2

Musa 1; Ibrahimu 3“HII NDIYO KAZI YANGU NA UTUKUFU WANGU”

Unaposoma Musa 1 na Ibrahimu 3, weka akili zako na moyo wazi kwa misukumo kutoka kwa Roho . Atakutia msukumo kwa mawazo na fikra ambazo zitakusaidia kujiandaa kufundisha .

Alika Kushiriki

Washiriki wa darasa lako wanaweza kuwa wamepata uzoefu wa kupendeza waliposoma Musa 1 na Ibrahimu 3 nyumbani . Utawapaje washiriki wa darasa fursa za kushiriki uzoefu huo? Inaweza kuwa rahisi kama kuuliza maswali sawa na haya: Nini kilikuvutia ulipokuwa unasoma maandiko wiki hii? Nini kilikushangaza? Nini kilikufanya usimame na kufikiri? Nini kilikusaidia uhisi karibu zaidi na Baba yako wa Mbinguni na Yesu Kristo?

Fundisha Mafundisho

MUSA 1:1–10, 37–39; IBRAHIMU 3:22–26

Kama watoto wa Mungu, tuna takdiri takatifu.• Kweli zilizofunuliwa katika maono ya Musa na

Ibrahimu zinaweza kuwa na ushawishi wenye nguvu kubwa kwenye chaguzi zetu na kwenye uwezo wetu wa kushinda changamoto za maisha . Jinsi gani unaweza kuwasaidia washiriki wa darasa lako kugundua kweli hizi katika Musa 1 na Ibrahimu 3? Wazo moja ni kuligawa darasa

katika makundi na pangia kila kundi moja ya vifungu vifuatavyo: Musa 1:1–10; Musa 1:37–39; Ibrahimu 3:22–26 . Kila kundi lingeweza kutafuta majibu kwa maswali kama vile “mimi ni nani?” “Kwa nini nipo hapa?” na “Mungu anataka mimi niwe nani?” Baada ya muda wa kutosha, makundi yanaweza kushiriki majibu yao . Jinsi gani majibu haya yanaweza kushawishi matendo yetu ya kila siku?

Kristo na uumbaji, na Robert T. Barrett

MUSA 1:12–23

Tunaweza kupinga ushawishi wa Shetani.• Makabiliano ya Musa na Shetani, yanayopatikana

katika Musa 1:12–23, yanashikilia masomo ambayo yangeweza kusaidia washiriki wa darasa lako wanapokabiliwa na majaribu au udanganyifu kutoka kwa adui . Tunaweza kujifunza nini kutokana na majibu ya Musa? Video “I am a Son of God” (ChurchofJesusChrist .org) inaweza kusaidia

DesemBa 27–JanuaRi 2

2

washiriki wa darasa kujadili moja ya mbinu za Shetani—kutujaribu kuwa na wasiwasi na uzoefu wetu wa Kiroho (ona pia “Nyenzo za Ziada”) . Inaweza kuwa na maana kama washiriki wa darasa walishiriki mawazo na msukumo kusaidiana kila mmoja kugundua na kupinga juhudi za Shetani .

• Somo moja kutoka uzoefu wa Musa ni kwamba Shetani anatujaribu kwa kuiga ukweli na uwezo wa Mungu . Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kupata taswira ya hili, ungeweza kuleta darasani baadhi ya vitu ambavyo ni tafsiri za uongo za vitu vingine, kama vile mmea wa bandia au mwanaserere . Tunawezaje kuelezea kwamba hivi ni bandia? Nini baadhi ya vitu vya kuiga Shetani anatumia leo kutujaribu? Jinsi gani tunaweza kuvitambua na kuvikataa? (Kujifunza jinsi Musa alivyofanya hili, ona Musa 1:13–18 .) Jinsi gani Bwana anatusaidia katika juhudi zetu? (ona Luka 1:24–26) .

IBRAHIMU 3:22–28

Maisha haya ni fursa yetu kuonesha kwamba tutafanya kile Mungu anachoamuru.• Jinsi gani unaweza kuwasaidia washiriki

wa darasa kuona maisha yao kama fursa ya kuthibitisha uaminifu wao kwa amri za Mungu? Unaweza kuanza kwa kuwaomba kueleza kuhusu uzoefu walipotakiwa kuonesha uhodari katika ustadi—kwa mfano, shuleni, kazini, au kwenye timu ya michezo . Wanaweza kuelezea kuhusu kile walichotakiwa kufanya kujithibitisha wenyewe . Jinsi gani uzoefu huu ni sawa na kile kilichoelezwa katika Ibrahimu 3:24–26? Jinsi gani ni tofauti? Jinsi gani tunamjumuisha Baba wa Mbinguni na Mwokozi katika juhudi zetu za “kujithibitisha” wenyewe? (Ibrahimu 3:25) . Jinsi gani kujua kwamba tupo hapa kujithibitisha wenyewe kuwa watiifu kunaathiri jinsi tunavyopokea changamoto za maisha?

• Nini kingine tunajifunza kutoka Ibrahimu 3:22–28 kuhusu maisha kabla ya kuja duniani, au “hali zetu za mwanzo”? (mstari wa 26) . Kwa nini kweli hizi ni muhimu kwetu?

Nyenzo za Ziada

Usiwe na wasiwasi na kile kilichofunuliwa kwako.Mzee Jeffrey R . Holland alifundisha hili kuhusu uzoefu wa Musa katika Musa 1: “ujumbe wa Musa kwako leo ni: Usiache kujilinda . Usisadiki kwamba ufunuo mkubwa, baadhi ya maajabu, wakati wa kuangaza, ufunguzi wa njia ya kuvutia, ni mwisho wake . .  .  . Kama awali kumekuwa na mwangaza, kuwa mwangalifu dhidi ya majaribu ya kurudi kutoka kitu kizuri . Kama ilikuwa sahihi ulipoomba na kuamini na kuishi kwa hilo, ni sahihi hata sasa . Usikate tamaa wakati shinikizo linapokuwa kubwa . Kwa hakika usikate tamaa kwa kiumbe yule ambaye ameazimia uharibifu wa furaha yako . Kabiliana na mashaka yako . Shinda woga wako . ‘Kwa hivyo, usitupe ujasiri wako .’ [Waebrania 10:35] . Baki katika njia na uone uzuri wa maisha ukifunuliwa kwa ajili yako” (“Kwa hivyo Usitupe Ujasiri Wako,” Ensign, Machi . 2000, 7, 9) .

Kuboresha Ufundishaji WetuWasaidie wanaojifunza kugundua kweli katika maandiko. Kabla ya kuwaomba washiriki wa darasa kusoma vifungu vya maandiko, unaweza kuwapa kitu fulani mahususi kutafuta na kufikiria. Kwa mfano, wangeweza kutafuta kitu fulani wanachojifunza kuhusu mwokozi au kitu fulani ambacho wangetaka kushiriki na mwanafamilia. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 21.)

3

JANUARI 3–9

Mwanzo 1–2; Musa 2–3; Ibrahimu 4–5“HAPO MWANZO MUNGU ALIZIUMBA MBINGU NA NCHI”

Ili kujiandaa kufundisha, kwanza soma na kutafakari Mwanzo1–2; Musa 2–3; na Ibrahimu 4–5, na andika misukumo yako ya kiroho . Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia na mawazo hapo chini yanaweza kukusaidia kuelewa na kufundisha maandiko katika sura hizi .

Alika Kushiriki

Mungu alirudia mara kwa mara kutangaza kwamba vitu alivyovifanya wakati wa Uumbaji vilikuwa “vizuri” (ona Musa 2:4, 10, 12, 18, 21, 25, 31) . Waombe washiriki wa darasa kushiriki vitu vizuri walivyovipata waliposoma maandiko nyumbani wiki hii . Nini kilikuwa kizuri kuhusu vitu walivyogundua?

Fundisha Mafundisho

MWANZO 1; MUSA 2; IBRAHIMU 4

“Mungu Aliziumba Mbingu na Nchi.”• Washiriki wa darasa wanaweza kuwa

wametambua mifanano na tofauti miongoni mwa maelezo ya Uumbaji katika vitabu vya Mwanzo, Musa, na Ibrahimu . Watie moyo washiriki wa darasa kushiriki kile tafsiri ya Joseph Smith katika Musa 2 inachoongeza kwenye uelewa wetu wa maelezo ya Uumbaji katika Mwanzo 1 . Je ni umaizi gani wa ziada tunaoupata kutoka Ibrahimu 4? Kuruhusu watu zaidi kushiriki,

ungeweza kutia moyo darasa kufanya ufananisho huu katika jozi au makundi madogo . (Baadhi ya mistari ambayo ina tofauti muhimu imeandikwa kwenye “Nyenzo za Ziada .”) Tunanufaika vipi kutokana na kuwa na maelezo mengi? Ni nini maelezo haya yanapendekeza kuhusu kile Mungu anachotaka sisi tujue kuhusu Uumbaji?

• Wakati Mungu alipowaumba Adamu na Hawa, Aliwapa mamlaka juu ya nchi na vyote alivyoumba juu yake (ona mwanzo 1:28; Musa 2:28; Ibrahimu 4:28) . Jinsi gani Mafundisho na Maagano 59:16–21 na 104:13–18 inatusaidia kuelewa vizuri inamaanisha nini kutumia mamlaka kwa haki juu ya nchi?

• Siku chache kabla ya darasa, unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kuleta picha walizozipiga au walizonazo majumbani mwao ambazo zinawakumbusha juu ya uzuri wa uumbaji wa Mungu . Jinsi gani kujifunza kuhusu kazi ya uumbaji wa Mungu kunaathiri hisia zetu kuhusu Yeye, sisi wenyewe, na nchi? Washiriki wa darasa wangeweza pia kushiriki ujumbe gani wanahisi Mungu anao kwa ajili yetu katika maelezo haya ya Uumbaji katika Mwanzo 1; Musa 2; na Ibrahimu 4 . Kuimba au kusikiliza wimbo kuhusu Uumbaji, kama vile “For the Beauty of the Earth” (Nyimbo za Kanisa, namba 92) kungeweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuhisi shukrani kwa ajili ya uumbaji wa Mungu .

JanuaRi 3–9

4

Uumbaji, na joan hibbert durtschi

MWANZO 1:26–28; MUSA 2:26–28; IBRAHIMU 4:26–28

Sisi tumeumbwa kwa mfano wa Mungu.• Kwa nini ni muhimu kwetu kuelewa kwamba

tumeumbwa kwa mfano wa Mungu? Unawezaje kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari ukweli huu? Wangeweza kusoma Mwanzo 1:26–28; Musa 2:26–28; Ibrahim 4:26–28; au aya ya pili ya “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu” (ChurchofJesusChrist .org) . Jinsi gani ukweli huu unaathiri jinsi tunayojiona wenyewe, wengine, na Mungu? Washiriki wa darasa wangeweza kupata umaizi zaidi katika nyimbo kama vile “O My Father” au “Mimi ni Mtoto wa Mungu” (Nyimbo za Kanisa, na . 292, 301) .

• Katika video “Uumbaji Mkuu wa Mungu” (ChurchofJesusChrist .org), Rais Russell M .Nelson anatoa ushuhuda wa mwili wa kimiujiza wa binadamu (ona pia “Thanks Be to God,” Liahona, Mei 2012, 77–80) . Fikiria kushiriki video hii kabla ya kusoma Mwanzo 1:26–28; Musa 2:26–28; au Ibrahimu 4:26–28 kama darasa . Jinsi gani ushuhuda wa Rais Nelson unazidisha shukrani zetu kwa ajili ya kweli katika mistari hii?

MWANZO 1:27–28; MUSA 3:18, 21–25; IBRAHIMU 5:14–19

Ndoa kati ya mwanamume na mwanamke imetakaswa na Mungu.• Mitazamo mingi juu ya ndoa katika ulimwengu

leo imechepuka mbali na ukweli wa milele . Kusaidia darasa lako lijifunze kuhusu mtazamo

wa Mungu kuhusu ndoa, unaweza kuwaomba wasome Mwanzo 1:27–28; Musa 3:18, 21–25; au Ibrahimu 5:14–19 na waorodheshe ubaoni kweli wanazopata . Wangeweza kuongeza kwenye orodha yao kweli wanazopata katika “Familia: Tangazo Kwa Ulimwengu” (ChurchofJesusChrist .org) . Kwa nini kweli hizi ni muhimu kwetu?

Nyenzo za Ziada

Kufananisha hadithi za Uumbaji.

Mwanzo Musa Ibrahimumwanzo 1:1 musa 2:1 ibrahimu 4:1

mwanzo 1:16 musa 2:16 ibrahimu 4:16

mwanzo 1:26–27 musa 2:26–27 ibrahimu 4:26–27

mwanzo 1:30 musa 2:30 Ibrahimu 4:30

mwanzo 2:5 musa 3:5 Ibrahimu 4:30

mwanzo 2:5 musa 3:5 Ibrahimu 5:5

mwanzo 2:7 musa 3:7 ibrahimu 5:7

mwanzo 2:9 musa 3:9 ibrahimu 5:9

mwanzo 2:17–19. musa 3:17–19 ibrahimu 5:13–14

Kuboresha Ufundishaji WetuWasaidie wanafunzi walinganishe maandiko na wao wenyewe. “Kweli zilezile za injili ambazo zilimtia moyo na kumuidhinisha Ibrahimu, esta, lehi, na joseph Smith zinaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kukabiliana na changamoto za kisasa” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 21). Watie moyo wanafunzi kutumia kanuni wanazozipata katika maandiko kwenye hali zao wenyewe.

5

JANUARI 10–16

Mwanzo 3–4; Musa 4–5ANGUKO LA ADAMU NA HAWA

Unapojiandaa kufundisha kuhusu Mwanzo 3–4 na Musa 4–5, fikiri kuhusu maswali gani au shughuli zinaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa vyema Anguko la Adamu na Hawa .

Alika Kushiriki

Washiriki wa darasa wangeweza kwa kifupi kuangalia upya Mwanzo 3–4 au Musa 4–5, kuchagua mstari ambao upo dhahiri kwao, na kuushiriki na yule aliyeketi karibu nao . Kisha watu wachache wangeweza kushiriki utambuzi na darasa .

Fundisha Mafundisho

MUSA 4:1–13; 5:1–12

Tunahitaji uhuru wa kuchagua na upinzani ili tuweze kukua.• Kwa sababu uhuru wa kuchagua—haki iliyotolewa

na Mungu kufanya chaguzi—ni sehemu muhimu ya maisha ya duniani, sisi wakati mwingine hatulipi umuhimu suala hilo . Kuongeza kwa kina shukrani ya washiriki wa darasa kwa ajili ya zawadi hii, wangeweza kusoma na kujadili Musa 4:1–4 . Mistari hii inafundisha nini kuhusu umuhimu wa uhuru wa kuchagua? Kwa nini mpango wa Mungu ungeharibiwa kama tusingekuwa na uhuru wa kuchagua? Dondoo katika “Nyenzo za Ziada” zinaweza kutoa baadhi ya utambuzi .

• Pengine washiriki wa darasa walijifunza ujumbe wa Rais Dallin H . Oaks “Upinzani katika Vitu Vyote” (Liahona, Mei 2016, 114–17) kama sehemu ya mafunzo yao binafsi au kifamilia wiki hii . Muda wote wa wiki, unaweza kufikiria kuwaalika watu wachache kuja wamejiandaa kushiriki kitu fulani kutoka katika ujumbe wake ambacho kiliwasaidia kuelewa Anguko la Adamu na Hawa (ona hususani sehemu ya I na II) . Kwa nini Baba wa Mbinguni anaturuhusu tupate uzoefu wa “upinzani katika vitu vyote”? (ona 2 Nefi 2:11–16) . Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kusoma Mafundisho na Maagano 29:39–40 na kujadili kwa nini majaribu ya Shetani ni muhimu katika mpango wa Mungu . Jinsi gani Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanatusaidia tunapokabiliana na majaribu?

Kuondoka Edeni, na annie henrie Nader

Adam

u na

Haw

a, n

a D

ougl

as m

. Fry

er

JanuaRi 10 –16

6

MUSA 4: 4–12; 5:13–33

Shetani anatafuta “kutudanganya na kutupofusha”.• Musa 4:4–12; 5:13–33 inaweza kuwasaidia

washiriki wa darasa lako kutambua baadhi ya njia ambazo kupitia hizo Shetani anatujaribu kufanya uovu . Unaweza kuwaomba nusu ya darasa kusoma Musa 4:4–12 na nusu nyingine kusoma Musa 5:13, 18–33 . Wanaposoma, wangeweza kuorodhesha njia Shetani alizomjaribu Adamu na Hawa na watoto wao . Jinsi gani anajaribu kwa kutumia vitu sawa na hivi leo? Jinsi gani Baba wa Mbinguni anaweza kutusaidia kupinga uongo wa Shetani?

MWANZO 3:1–7; MUSA 4:22–31; 5:4–15

Upatanisho wa Yesu Kristo unatoa matumaini na ukombozi kutokana na Anguko.• Tunavyoelewa zaidi athari za Anguko, ndivyo

zaidi tunavyokuwa na shukrani kwa upatanisho wa Yesu Kristo . Washiriki wa darasa wangeweza kutafuta athari za Anguko katika Mwanzo 3:1–7; Musa 4:22–31 na kuorodhesha kile wanachopata ubaoni . Kisha wangeweza kutafuta Musa 5:4–12, 14–15 kujifunza kuhusu mpango wa Mungu wa kutukomboa kutokana na athari hizo (ona pia 2 Nefi 2:19–25; Alma 12:22–34) na orodhesha kile wanachokipata ubaoni . Wangeweza pia kushiriki kile kinachowavutia kuhusu shuhuda za Adamu na Hawa za Yesu Kristo zinazopatikana katika mistari 10–12 . Jinsi gani tunahisi kuhusu mpango wa Mungu baada ya kusoma maandiko haya?

• Hadithi ya Adamu na Hawa ya matumaini na ukombozi inaweza kuwatia moyo washiriki wa darasa wakati maisha yanapokuwa magumu . Fikiria kuwaomba kutafuta maneno na virai katika Musa 5:7–12 ambavyo vinaeleza tumaini ambalo Adamu na Hawa walihisi wakati walipojua kwamba Mwokozi angeweza kuwakomboa . Lini tumehisi tumaini sawa

na lile Adamu na hawa walilohisi? Fikiria kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki nyimbo zao za kanisa wanazozipenda kuelezea tumaini ambalo linakuja kupitia upatanisho wa Mwokozi . Mngeweza kuimba baadhi ya hizi nyimbo pamoja .

Nyenzo za Ziada

Tunaweza kujichagulia wenyewe.Mzee Dale G . Renlund alifundisha:

“Lengo la Baba yetu wa Mbinguni katika malezi siyo kufanya watoto Wake kutenda kile kilicho sahihi; ni kufanya watoto Wake wachague kufanya kile kilicho sahihi na hatimaye kuwa kama Yeye . Kama Yeye angetaka tu sisi tuwe watiifu, Angetumia zawadi na adhabu za papo hapo kushawishi tabia zetu .

“Lakini Mungu hapendezwi na watoto Wake kuwa tu ‘wanyama’ waliofunzwa na watiifu ambao hawataweza kutafuna kwenye ndara Zake katika sebule ya selestia . Hapana, Mungu anataka watoto Wake wakue kiroho na kujiunga Naye katika kazi ya familia” (“Chagueni Hivi Leo,” Liahona, Nov . 2018, 104 .) .

Kuboresha Ufundishaji WetuZidisha ushiriki wa washiriki wa darasa. Shughuli nyingi zinaweza kufanywa kama darasa, katika vikundi vidogo, au katika jozi. Tumia mbinu mbalimbali ili kuruhusu watu kushiriki wale ambao wasingeweza kwa njia nyingine kupata nafasi. (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 33–34.)

7

JANUARI 17–23

Mwanzo 5; Musa 6“WAFUNDISHENI WATOTO WETU VITU HIVI KWA UWAZI”

Kabla hujasoma nyenzo yoyote ya ziada, soma na utafakari Mwanzo 5 na Musa 6, na uandike misukumo yako ya kiroho . Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia na muhtasari huu vinaweza kukupa mawazo kuhusu jinsi ya kuwasaidia wale unaowafundisha kugundua kweli zinazowahusu .

Alika Kushiriki

Jinsi gani unaweza kuwatia moyo washiriki wa darasa kushiriki utambuzi na uzoefu waliokuwa nao walipokuwa wakijifunza Mwanzo 5 na Musa 6? Ungeweza kuyaandika majina Adamu na Henoko ubaoni na waombe washiriki wa darasa waandike kitu fulani ambacho mmoja wa manabii hawa alifanya au kufundisha ambacho kilikuwa na maana kwao .

Fundisha Mafundisho

MUSA 6:26–39

Bwana anatuita kufanya kazi yake licha ya mapungufu yetu.• Kuna uwezekano mkubwa kwamba mtu fulani

katika darasa lako amehisi—au anahisi—upungufu kuhusu wajibu nyumbani au kanisani . Kujenga imani ya washiriki wa darasa kwamba Bwana anaweza kuwasidia, ungeweza kwaomba wasome uzoefu wa Henoko unaopatikana katika

Musa 6:26–39 . Jinsi gani Mungu alimsaidia Henoko kufanya kazi yake licha ya woga wa Henoko? Waombe washiriki wa darasa kufikiria kuhusu mifano mingine ya watu walioshinda unyonge wao na wakakamilisha kazi ya Bwana, iwe ni kutoka katika maandiko au maisha yao wenyewe . Ni mifano gani tunaweza kushiriki? (Ona pia Kutoka 4:10–16; Yeremia 1:4–10; 2 Nefi 33:1–4; Etheri 12:23–29) .

• Wengi wa mitume na manabii wa leo wameelezea wasiwasi wao unaofanana na wa Henoko wakati walipoelezea jinsi ilivyokuwa kupokea miito yao . Uzoefu wao ungeweza kuongeza uelewa wa washirika wa darasa wa Musa 6:26–39 . Fikiria kurejea upya video “On the Lord’s Errand: maisha ya Thomas S . Monson” (churchofJesusChrist .org; kati ya dakika 35:46 na 39:40) au hotuba ya mshiriki wa Akidi ya wale Kumi na wawili aliyeitwa hivi karibuni (kwa mfano, ona shuhuda za Mzee Ronald A . Rasband, Mzee Gary E . Stevenson, na Mzee Dale G . Renland [Liahona, Nov . 2015, 89–94]) . Waache washiriki wa darasa washiriki kile kinachowavutia kuhusu mifano hii . Tunaweza kujifunza nini kutoka kwa viongozi hawa kuhusu hisia zetu za upungufu? Kauli kutoka kwa Rais Thomas S . Monson katika “Nyenzo za Ziada” inaweza pia kusaidia kama sehemu ya mjadala huu .

Pazu

ri m

no k

uliko

par

adiso

, na

Kend

al

Ray

johs

on

JanuaRi 17–23

8

MUSA 6:48–65

Imani, toba, ubatizo, na kumpokea Roho Mtakatifu kunatuandaa kurudi kwa Mungu.• Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa

Ajili ya Watu Binafsi na Familia unapendekeza kusoma Musa 6:48–62 kutafuta kile kila mmoja wetu lazima ajue na atende ili kukombolewa . Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki utambuzi wowote ambao ulikuja kutokana na kujifunza kule majumbani mwao . Au mnaweza kujadili Musa 6:48–62 pamoja darasani . Jinsi gani tunaweza kumjibu mtu fulani anayeuliza kwa nini imani, toba, ubatizo, na kumpokea Roho Mtakatifu ni muhimu? Jinsi gani Bwana anajibu swali hili katika mistari 53–65, na tunajifunza nini kutokana na jibu lake?

Wazazi wanapaswa kuwafundisha watoto wao injili.

MUSA 6:51–63

“Wafundisheni Watoto Wenu Vitu Hivi kwa Uwazi.”• Katika Musa 6:51–63 Tunajifunza juu ya

kweli za injili ambazo Bwana alizifundisha kwa Adamu na kumtaka kuzifundisha kwa uzao utakaokuja . Pengine washiriki wa darasa wangeweza kutengeneza orodha ya kweli hizi kwa kujifunza vifungu vidogo vya mistari, kama vile mistari 51–52, 53–57, 58–60, 61–63 . Kwa nini kweli hizi ni za thamani kwa vizazi vinavyoinukia vya leo? Nini ungetaka vijana wajue kuhusu mwokozi kutokana na mistari hii? Washiriki wa darasa wanaweza kuwa radhi kushiriki mawazo au uzoefu ili kusaidiana wao kwa wao

kufundisha kweli hizi kwa matokeo yanayotakiwa kwa watoto na vijana . Nini kingine tunaweza kujifunza kutoka katika maelekezo ya Bwana kwa wazazi katika Mosia 4:14–15 na Mafundisho na Maagano 68:25–28; 93:40–50?

• Kuongezea kwenye kile Musa 6 inachofundisha kuhusu wajibu wa wazazi kwafundusha watoto wao, unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kuangalia moja au zaidi ya video zifuatazo: “Parenting: Touching the hearts of our Youth,” “Proclamation Series: Children,” or “Mother in Israel” (ChurchofJesusChrist .org) . Tunajifunza nini kutokana na video hizi kuhusu kufundisha injili kwa watoto wetu? Kama unawafundisha vijana, ungeweza kuwaomba kushiriki jinsi wanavyoweza kuwasaidia wazazi wao katika juhudi zao za kufundisha injili nyumbani .

Nyenzo za Ziada

“Aitwaye na Bwana, Bwana humstahilisha.”Rais Thomas S . Monson alifundisha: “Baadhi yenu wanaweza kuwa na aibu kiasili au kujifikiria mwenyewe una mapungufu katika kukubali wito . Kumbuka kwamba kazi hii siyo yako na yangu peke yangu . Hii ni kazi ya Bwana, na wakati tunapokuwa katika kazi ya Bwana, tuna haki ya usaidizi wa Bwana . Kumbuka kwamba aitwaye na Bwana, Bwana humstahilisha .” (“Duty Calls, Ensign, Mei 1996, 44) .

Kuboresha Ufundishaji WetuRoho Mtakatifu ni Mwalimu. jukumu lako kama mwalimu ni muhimu, lakini kumbuka kwamba Roho mtakatifu ni mwalimu wa kweli. wasaidie washiriki wa darasa kujifunza kutoka kwa Roho na kushiriki na kila mmoja kile wanachojifunza.

9

JANUARI 24–30

Musa 7“BWANA AKAWAITA WATU WAKE SAYUNI”

Unaposoma Musa 7, fikiria kuhusu watu unaowafundisha na jinsi unavyoweza kuwasaidia kuelewa kile sura hii inachofundisha kuhusu Sayuni na kanuni zingine za injili .

Alika Kushiriki

Wakati mwingine swali rahisi na dakika chache za kutafakari zinatosha kusaidia watu kushiriki kile wanachojifunza nyumbani . Pengine ungeweza kuwapa washiriki wa darasa muda mfupi wa kurejea tena Musa 7, kupata mstari ambao unawafanya kuhisi shukrani kwa ajili ya kweli zilizorejeshwa katika kitabu cha Musa, na kisha kuushiriki .

Fundisha Mafundisho

MUSA 7:16–21, 27, 53, 62–69

Tunaweza kuijenga Sayuni katika wakati wetu.• Ipi ingekuwa njia bora ya kuwasilisha wazo

la Sayuni katika darasa lako? Moja ya wazo lingekuwa kuwasiliana na washiriki wa darasa wiki moja kabla ya darasa na kuwaomba kuleta kitu kutoka nyumbani ambacho wanahisi kinawakilisha tabia za watu wa Sayuni, kama ilivyoelezwa katika Musa 7:18 . Mnapojadiliana mstari huu pamoja, washiriki wa darasa wangeweza kueleza umuhimu wa kitu walichokileta .

tunapaswa kujitahidi kuwa “wa moyo mmoja na wazo moja” (musa 7:18).

• Video “We Come Together and Unite as One” (ChurchofJesusChrist .org) ingeweza kukusaidia kuanza majadiliano kuhusu jinsi tunavyoweza kuwa “wa moyo mmoja na wazo moja” (Musa 7:18) katika kata zetu na familia . Fikiria kuwaomba washiriki wa darasa kufikiria kuhusu wakati walipohisi umoja miongoni mwa familia zao au wakati wakiwahudumia wengine katika Kanisa au jumuiya . Watu walifanya nini kujenga umoja katika hali hizi? Nini tunaweza kujifunza kuhusu Sayuni na umoja kutoka Musa 7? (Ona hususani mistari 16–21, 27, 53, 62–69) . Haya ni baadhi ya maandiko mengine ambayo yangeweza kusaidia: Wafilipi 2:1–4; 4 Nefi 1:15–18; Mafundisho na Maagano 97:21; 105:5 .

MUSA 7:28–44

Mungu analia kwa ajili ya watoto Wake.• Baadhi ya watu wanaweza kumwona mungu kama

yuko mbali, asiyefikiwa, na hata asiyejali . Jinsi gani unaweza kutumia ono la Henoko kusaidia darasa

Pend

anen

i, na

em

ma

don

alds

on t

aylo

r

JanuaRi 24–30

10

lako kuelewa kwamba Mungu anahusika katika maisha yetu na anatujali? Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kusoma Musa 7:28–44 na kutengeneza orodha ya baadhi ya sababu Mungu alikuwa analia . Mistari hii inakufundisha nini kuhusu jinsi Mungu anavyohisi kuhusu watoto Wake? Maelezo kwenye “Nyenzo za Ziada” yanaweza kuchangia kwenye mjadala huu .

• Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unapendekeza kutafakari kile Musa 7:28–31 inachofundisha kuhusu Mungu . Kwa wale waliofanya hili nyumbani wanaweza kuwa tayari kushiriki mawazo yao na darasa . Au ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kutafakari mistari hii na kuijadili katika darasa .

MUSA 7:59–67

Bwana atarudi tena katika siku za mwisho.• Jinsi gani unaweza kuwasaidia washiriki wa darasa

lako kugundua kile Musa 7:59–67 inachofundisha kuhusu Ujio wa Pili wa Mwokozi? Pengine ungeweza kuorodhesha kweli mbili au tatu au matukio kutoka katika mistari hii ubaoni na watake washiriki wa darasa kutafuta katika mistari na kuongeza kwenye orodha . Kwa nini ni baraka kuwa na kumbukumbu ya ono la Henoko—moja ya utabiri wa mwanzo kabisa wa Ujio Wa Pili?

Nyenzo za Ziada

Mungu analia kwa ajili ya watoto Wake.Mzee Jeffrey R . Holland alifundisha:

“Katikati ya ono kuu la binadamu ambalo mbingu ililifunua kwa yeye kuona, Henoko, akiangalia vyote baraka na changamoto za maisha ya kufa, anageuza

macho yake kuelekea kwa Baba na anafadhaishwa kumwona akilia . Anasema kwa mshangao na kustaajabu kwa huyu kiumbe mwenye uwezo mkubwa mno katika ulimwengu: ‘Yawezekanaje wewe kulia?’  .  .  .

“Kuangalia kuelekea matukio ya takribani siku yoyote, Mungu anajibu: ‘Tazama ndugu zako hawa; wao ni kazi ya ustadi wa mikono yangu mwenyewe . .  .  . Niliwapa amri, kwamba yawapasa kupendana, na kwamba yawapasa kunichagua Mimi, Baba yao; lakini tazama, wao hawana urafiki na jamaa zao, nao wanaichukia damu yao wenyewe . .  .  . Kwa sababu hiyo mbingu zote hazipaswi kulia, zikiwaona hawa watakaoteseka?’ [Musa 7:29–33, 37] .

“Onesho lile moja, lililoribitiwa linafanya zaidi kufundisha uasilia wa kweli wa Mungu kuliko maandiko yoyote ambayo theolojia ingeweza kutoa . .  .  . Ni picha gani isiyofutika ya ahadi za Mungu katika maisha yetu! Ni hasira gani kwa mzazi wakati watoto Wake hawamchagui Yeye wala ‘injili ya Mungu Aliyoituma! [Warumi 1:1] . Jinsi gani ilivyo rahisi kumpenda mtu fulani ambaye kwa kipekee anatupenda sisi!” (“Fahari ya Mungu,” Liahona, Nov . 2003, 72) .

Kuboresha Ufundishaji WetuWahimize washiriki wa darasa kujifunza maandiko nyumbani. Njia moja unayoweza kuwahimiza kujifunza maandiko nyumbani ni kutoa muda kwa washiriki wa darasa kushiriki uvumbuzi na umaizi kutoka kwenye kujifunza kwao binafsi na kama familia. (Ona Kufundisha Katika Njia ya Mwokozi, 29.)

11

JANUARI 31–FEBRUARI 6

Mwanzo 6–11; Musa 8“NUHU AKAPATA NEEMA MACHONI PA BWANA”

Muhtasari huu unasisitiza kanuni zinazopatikana katika Mwanzo 6–11 na Musa 8, lakini hizi sio kanuni pekee ambazo ungeweza kuzilenga unapofundisha . Amini misukumo ya Roho unayopata unapojifunza maandiko .

Alika Kushiriki

Fikiria kuwataka washiriki wa darasa kushiriki ujumbe wa kiroho kwa ajili ya wakati wetu kutokana na hadithi ya Nuhu au Mnara wa Babeli . Watie moyo kushiriki maandiko ambayo yanasaidia ujumbe huu .

Fundisha Mafundisho

MWANZO 6–8; MUSA 8

Kuna usalama wa kiroho kwa kumfuata nabii wa Bwana.• Uovu katika siku za Nuhu unaweza

kutukumbusha sisi juu ya uovu tunaouona unatuzunguka leo . Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kufaidika kutokana na masomo ya hadithi ya Nuhu, ungeweza kuandika kwenye ubao Maonyo na Uthibitisho. Washiriki wa darasa wangeweza kuhakiki Mwanzo 6–8 au Musa 8:13–30 na kupata kitu fulani wanachohisi ni onyo muhimu kwa wakati wetu na kitu fulani wanachofikiria kinathibitisha (ona pia “Nyezo za Ziada”) . Wangeweza

kuandika kile wanachokipata chini ya kichwa cha habari kinachofaa ubaoni . Kwa nini hadithi ya Nuhu ni yenye thamani kwetu leo?

MWANZO 9:8–17

Alama na ishara zinatusaidia kukumbuka maagano yetu na Bwana.• Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa

Ajili ya Watu Binafsi na Familia unapendekeza kusoma Mwanzo 9:8–17 na kutafakari jinsi ishara au alama zinavyoweza kutumika kama ukumbusho wa maagano yetu . Kuwasaidia washiriki wa darasa kushiriki mawazo yao, unaweza kuleta darasani kiasi kidogo cha vitu ambavyo vinatukumbusha kuhusu vitu muhimu—kama vile pete ya ndoa, bendera ya taifa, au kishikizo cha jina la mmisionari—na zifananishe na “ishara” ya upinde wa mvua . Nini Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 9:21–25 (katika kiambatanisho cha Biblia) inatufundisha kuhusu ishara? Jinsi gani Mungu anatumia ishara au alama kutusaidia kukumbuka maagano yetu?

MWANZO 11:1–9

Njia pekee ya kufika mbinguni ni kwa kumfuata Yesu Kristo. • Maelezo ya watu wa Babeli kujenga mnara

yanatoa utofauti wa kuvutia kwenye maelezo ya Henoko na watu wake kujenga Sayuni,

Kiel

elez

o ch

a n

uhu

akito

ka k

wen

ye s

afina

, na

Sam

law

lor

JanuaRi 31–FeBRuaRi 6

12

ambayo washiriki wa darasa walijifunza wiki iliyopita . Makundi yote mawili ya watu yalikuwa yakijaribu kufika mbinguni lakini katika njia tofauti . Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kuorodhesha ubaoni chochote wanachokumbuka kuhusu watu wa Sayuni (ona Musa 7:18–19, 53, 62–63, 69) na nini wanajifunza kutoka mwanzo 11:1–9 na Helamani 6:26–28 kuhusu watu wa Babeli . Ni Tofauti gani wanazozipata? Hii inakufundisha nini kuhusu juhudi zetu kurudi kwenye uwepo wa Mungu?

Kielelezo cha mnara wa Babeli, na David Green

• Jiji la kale la Babeli halipo tena, lakini kiburi na mambo ya kidunia lililoashiria yapo . Kuwasaidia washiriki wa darasa kutumia masomo kutoka Mnara wa Babeli kwenye maisha yao, anza kwa kuwataka kurejea Mwanzo 11:1–9 . Kisha ungeweza kugawa vipande vya karatasi na watake washiriki wa darasa kuandika vitu watu wanavyovifanya ambavyo vinawavuta mbali na Mungu; kisha, kwenye vipande vingine vya karatasi, wangeweza kuandika vitu watu wanavyofanya ambavyo vinawavuta karibu zaidi kwa Mungu . Unaweza kufurahia kupanga kundi la kwanza la karatasi kwenye ubao katika umbo la mnara na kundi la pili katika umbo la hekalu . Mungu ametoa nini kutusaidia “kufika mbinguni”? (Mwanzo 11:4; ona pia Yohana 3:16) . Mnaweza kuimba wimbo juu ya mada, kama vile “Nearer, My God, to Thee” (Nyimbo za Kanisa, na . 100) .

Nyenzo za Ziada

Masomo kutoka kwa Nuhu.Rais Henry B . Eyring alisema:

“Kushindwa kukubali ushauri wa kinabii hupunguza nguvu zetu za kukubali ushauri zaidi baadae . Muda muafaka wa kuweza kuamua kumsaidia Nuhu kujenga safina ulikuwa ni mara ya kwanza alipoomba . Kila muda alipoomba baada ya hapo, kila kushindwa kuitikia kungeweza kupunguza umakini kwa Roho . Na kwa hiyo kila muda ombi lake lingeonekana la kipumbavu zaidi, mpaka mvua ilipokuja . Na kisha ilikuwa wameshachelewa .

“Kila muda katika maisha yangu ambapo nimechagua kuchelewa kufuata ushauri wa kuvuvia au kuamua kwamba nilikuwa sihusiki, nilikuja kujua kuwamba nilijiweka katika njia ya kudhuru . Kila muda nilipousikiliza ushauri wa manabii, kuhisi ukithibitishwa katika sala, na halafu kuufuata, niligundua kuwa nilisogelea usalama” (“Finding Safety in Counsel,” Ensign Mei 1997, 25) .

Kwa nini Mungu alituma Gharika?Baadhi ya Watu wanastaajabu kuhusu haki ya Mungu katika kutuma gharika “kumfutilia mbali mwanadamu” (Mwanzo 6:7) . Mzee Neal A . Maxwell ilieleza kwamba wakati wa Gharika Kuu, “uharibifu ulikuwa umefikia kiwango cha kuharibu uhuru wa kuchagua kwamba roho hazikuweza, katika haki, kuletwa hapa” (We Will Prove Them Herewith [1982], 58) .

Kuboresha Ufundishaji WetuRuhusu Muda kwa ajili ya kutafakari. maswali mazuri yanahitaji kutafakari, kutafiti, na misukumo. Wape washiriki wa darasa dakika chache kutafakari swali kabla ya kuomba majibu. (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 31–34.)

13

FEBRUARI 7–13

Mwanzo 12–17; Ibrahimu 1–2“KUWA MFUASI MKUBWA WA HAKI”

Nini Roho Mtakatifu amekufundisha wiki hii ulipokuwa unajifunza Mwanzo 12–17 na Ibrahimu 1–2? Kuwa na uhakika kuwapa washiriki wa darasa fursa kushiriki kile ambacho Roho Mtakatifu amewafundisha .

Alika Kushiriki

Ili kuwapa washiriki wa darasa fursa za kushiriki kitu fulani walichojifunza kutoka Mwanzo 12–17 na Ibrahimu 1–2, wangeweza kila mmoja kuchagua mtu aliyetajwa katika sura hizi na kukamilisha sentensi kama zifuatazo: “Ibrahimu alinifundisha                   ” au “Sara alinifundisha                    .”

Fundisha Mafundisho

MWANZO 15:1–6; 17:15–22; IBRAHIMU 1: 1–19

Mungu atatubariki kwa ajili ya imani yetu na matamanio ya haki.• Uzoefu wa Ibrahimu na Sara uliorekodiwa katika

Mwanzo 15; 17; Ibrahimu 1 unaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kudumisha imani ili matamanio yao ya haki yakamilishwe katika muda wa Bwana . Jinsi gani Unaweza kuanzisha majadiliano kuhusu kanuni hii? Wazo moja ni kuliomba darasa kutafuta

mwanzo 15:1–6 na Ibrahimu 1:1–19 na kuelezea matamanio ya Ibrahimu na hali ngumu . Jinsi gani Ibrahimu na Sara walionesha imani yao katika nyakati za matatizo? (Ona Waebrania 11:8–13) . Jinsi gani matamanio yao ya haki hatimaye yalikamilishwa? (Ona Mwanzo 17:15–22; 21:1–3; Mafundisho na Maagano 132:29; Ibrahimu 1:31) . Jinsi gani tunaonesha imani yetu wakati matamanio yetu ya haki bado hayajakamilishwa kama tunavyotaka yawe? Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki jinsi ambavyo Mwokozi amewasaidia katika hali kama hizo .

• Baadhi ya washiriki wako wa darasa wanaweza kupokea msaada kidogo kutoka kwa familia zao pale wanapojitahidi kuishi injili—na wanaweza hata kukabiliana na upinzani . Tunajifunza nini kutokana na mfano wa Ibrahimu katika Ibrahimu 1:1–19 ambacho kinawezaa kuwasaidia wale wanaojitahidi kuishi kwa haki katika hali kama hizi?

• Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kusoma Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 14:36–40 (katika kiambatanisho cha Biblia) na kushiriki kile wanachojifunza kuhusu imani na matamanio ya Ibrahimu . Wanaweza pia kushiriki jinsi walivyobarikiwa wakati walipotumia imani yao kulipa zaka .

Kiel

elez

o ch

a Ib

rahi

mu

na S

ara

na

dill

een

mar

sh

FeBRuaRi 7–13

14

IBRAHIMU 2:6–11

Agano la Ibrahimu linatubariki sisi wote.• Kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa agano la

Ibrahimu ni nini, unaweza kushiriki maelezo ya Rais Russell M . Nelson katika “Nyenzo za Ziada” (ona pia Mada za Injili, “Agano la Ibrahimu,” topics .ChurchofJesusChrist .org) . Washiriki wa darasa wanaweza kuwa wamejifunza kuhusu agano la Ibrahimu kutoka Ibrahimu 2:6–11, kama ilivyopendekezwa katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki kile walichojifunza, au darasa lingeweza kujifunza mistari pamoja . Ni ahadi gani na majukumu tunayopokea kupitia agano la Ibrahimu? Video “Special Witness—President Nelson” inaweza kusaidia kujibu swali hili (ChurchofJesusChrist .org/media- library/video/2011- 04- 18- special- witness- president- nelson) . Tunahitaji kufanya nini kupokea msaada Bwana alioahidi kwa ajili yetu? Jinsi gani tunaweza, kama uzao wa Ibrahimu, kubariki “familia zote za dunia”? (Ibrahimu 2:11) .

MWANZO 14:18–19; TAFSIRI YA JOSEPH SMITH, MWANZO 14:25–40

“Melkizedeki alikuwa mtu wa imani.”• Kwa sababu ya Urejesho wa injili, waumini

wengi wa Kanisa wana ufahamu wa Ukuhani wa Melkizedeki, lakini baadhi hawajui kuhusu mtu Melkizedeki . Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza zaidi kuhusu yeye, pengine ungeweza kuwaomba kufikiria kwamba walikuwa wameombwa kumtambulisha kwa mtu fulani ambaye hakumjua na tengeneza orodha ubaoni ya vitu watakavyosema . Wangeweza kuweka msingi wa vitu hivi kwenye kile wanachosoma katika Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 14:26–27, 33–38 (katika kiambatanisho cha Biblia); Alma 13:13–19; na Mafundisho na Maagano 107:1–4 . Je, tunajifunza nini kuhusu Ukuhani wa Melkizedeki kutokana na mistari hii?

Melkizedeki akimbariki Ibrahimu, na walter Rane

Nyenzo za ZiadaBaraka za agano la Ibrahimu.Rais Russell M . Nelson alifundisha:

“Agano ambalo Mungu alilifanya na Ibrahimu na baadaye kuhakikishwa na Isaka na Yakobo ni la umuhimu kupita mpaka . .  .  . Bwana alitokea katika siku hizi za mwisho kufanya upya agano lile la Ibrahimu . .  .  . Pamoja na kufanywa upya huku, tumepokea, kama wale wa kale, ukuhani mtakatifu na injili ya milele . Tuna haki ya kupokea utimilifu wa injili, kufurahia baraka za ukuhani, na kustahili kwa baraka kubwa mno za Mungu—zile za uzima wa milele” (“Maagano;” Liahona, Nov . 2011, 87–88) .

“Hatima ya baraka za agano la Ibrahimu hutunukiwa katika mahekalu matakatifu . Baraka hizi zinaturuhusu kuja mbele katika Ufufuko wa Kwanza na kurithi viti vya enzi, falme, uwezo, himaya za kifalme, na mamlaka, kwenye ‘kuinuliwa kwetu na utukufu katika vitu vyote’ [Mafundisho na Maagano 132:19]” (“Special Witnesses of Christ,” Ensign, Apr . 2001, 7) .

Kuboresha Ufundishaji WetuToa ushuhuda kila mara. Ushuhuda wako rahisi, wa kweli kuhusu ukweli wa kiroho unaweza kuwa na ushawishi wenye nguvu kwa wale unaowafundisha. Kwa mfano, ungeweza kushiriki ushuhuda wa kawaida kuhusu jinsi maagano yalivyobariki maisha yako.

15

FEBRUARI 14–20

Mwanzo 18–23“JE, KUNA KITU CHOCHOTE KILICHO KIGUMU KWA BWANA?”

Unapojiandaa kufundisha, kumbuka kwamba washiriki wa darasa wanaweza kuwa walikuwa na uzoefu wao wenye maana wakati waliposoma Mwanzo 18–23 . Unaweza kufanya nini cha kuwatia moyo kushiriki uzoefu huu na umaizi? Fikiria kuruhusu umaizi huo kushawishi majadiliano ya darasa .

Alika Kushiriki

Majaribu yetu na mateso mara nyingi huwa nyakati za ufafanuzi katika maisha yetu . Mwanzo 18–23 inaelezea nyakati kadhaa kama hizo katika maisha ya Ibrahimu na Lutu . Pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki mstari walioupata wakati wa kujifunza kwao binafsi wiki hii ambao unaelezea wakati wa ufafanuzi unaowezekana kwa Ibrahimu . Kisha wangeweza kushiriki kile walichojifunza kutokana na hilo .

Fundisha Mafundisho

MWANZO 18:9–14; 21:1–7

Bwana anatimiza ahadi Zake kwa wakati wake Mwenyewe.• Maelezo kwenye mistari hii yanaweza kuwa ya

kutia moyo kwa washiriki wa darasa wanaojiuliza kama ahadi za Mungu kwao zitatimizwa . Kwa kuanza majadiliano, inaweza kusaidia kuwaomba washiriki wa darasa kurejea upya na mtu mwingine katika darasa maelezo ya

ahadi za Mungu kwa Ibrahimu na Sara kwenye mwanzo 17:4, 15–22; 18:9–14 na utimilifu wa ahadi hizo kwenye Mwanzo 21:1–7 . Ni nini katika mistari hii kinaonekana kwa washiriki wa darasa? Ni kweli gani tunazipata kutokana na uzoefu wa Ibrahimu na Sara wa kushiriki na rafiki ambaye anakata tamaa kwamba Mungu atatimiza ahadi Zake? Maandiko gani mengine au uzoefu binafsi tunaweza kuushiriki? (ona, kwa mfano, Warumi 8:28; Waebrania 11; Mormoni 9:19–21; Mafundisho na Maagano 88:64) . Ni uzoefu gani washiriki wa darasa wangeshiriki ambao kupitia huo ahadi za Mungu zilitimizwa katika maisha yao? Jinsi gani tunahimili imani yetu wakati baraka zilizoahidiwa zinaweza kutopokewa katika maisha haya? (ona Waebrania 11:8–13) .

MWANZO 7:15–26

Kama wafuasi wa Yesu Kristo, hatuna budi kuukimbia uovu na kutokuangalia nyuma. • Masomo gani unayohisi washiriki wa darasa

wangeweza kujifunza kutokana na maelezo ya familia ya Lutu wakikimbia kutoka Sodoma na Gomorra? Somo moja linalowezekana limependekezwa katika kauli ya Mzee Jeffrey R . Holland katika “Nyenzo za Ziada .” Pengine ungeweza kulishiriki na darasa baada ya kufanyia muhutasari matukio yaliyoelezwa kwenye Mwanzo 19:15–26 . Kwa njia zipi au katika hali

Sara

na

Isaka

, na

Scot

t Sno

w

FeBRuaRi 14–20

16

gani wakati mwingine sisi “[huangalia] nyuma” (mstari wa 26) wakati tunatakiwa kuangalia mbele kwa imani katika Mwokozi? Pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu ambao unaelezea kwa mfano umuhimu wa kutokuangalia nyuma . Ni nini Luka 9:62 inaongeza kwenye uelewa wetu wa wazo hili?

Kukimbia kutoka Sodoma na Gomorra, na julius Scknorr von Carolsfeld

MWANZO 22:1–14

Utayari wa Ibrahimu kumtoa dhabihu Isaka ni mfano wa Mungu na Mwanae.• Maelezo ya Ibrahimu kumtoa mwanawe

kama dhabihu yanaweza kutufundisha kuhusu dhabihu ya Baba wa Mbinguni ya Mwanae . Njia moja ya kuchunguza maelezo haya ni kupangia nusu ya darasa kutafakari Mwanzo 22:1–14 kutoka kwenye taswira za Ibrahimu na Mungu Baba, wakati nusu nyingine ikitafakari maelezo haya kutoka taswira ya Isaka na Yesu Kristo . Waombe washiriki wa darasa kushiriki umaizi wanaoupata . Kwa upekee, nini washiriki wa darasa wanajifunza ambacho kinaongeza shukrani zao kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo? Kama sehemu ya majadiliano haya, ungeweza kuonesha picha ya Ibrahimu akimchukuwa Isaka Kutolewa Dhabihu (Kitabu cha sanaa za Injili, na . 9) au onesha video “Akedah (The Binding)” (ChurchofJesusChrist .org) .

Nyenzo za Ziada

“Imani siku zote imeelekezwa kuelekea badaaye.”Mzee Jeffrey R . Holland alifundisha:

“Inawezekana kwamba mke wa Lutu aliangalia nyuma kwa uchungu kwa Bwana kwa kile alichokuwa Anamtaka kuacha nyuma . .  .  . Kwa hiyo si tu kwamba aliangalia nyuma; aliangalia nyuma kwa kutamani. Kwa kifupi, upendo wake kwa yaliyopita ulizidi kujiamini kwake kwa siku za baadaye .  .  .  .

“ .  .  . Ninawasihi nyinyi, msiwepo kwenye siku zilizopita tayari wala kutamani bure kwa ajili ya jana, hata kama jana hizo zilikuwa za kupendeza sana . Yaliyopita ni ya kujifunza lakini siyo ya kuyaishi . Tunatazama nyuma kudai makaa kutoka kwenye uzoefu unaowaka na si majivu . Na tunapookuwa tumejifunza kile tunachokihitaji na tumepata ubora ambao tumepata uzoefu wake, hivyo tunatazama mbele na kukumbuka kwamba imani siku zote imeelekezwa kuelekea badaaye. . . .

“ .  .  . [Mke wa Lutu] hakuwa na imani . Alitilia mashaka uwezo wa Bwana kumpa yeye kitu kizuri zaidi kuliko alichokuwa nacho tayari . Inavyoonekana, alifikiri kwamba hakuna ambacho kingeweza kuwa kizuri kama kile alichokuwa anakiacha nyuma .  .  .  .

“ .  .  . kuishi maisha ya zamani, ikiwa ni pamoja na makosa yaliyopita, kwa kweli sio sahihi! Siyo injili ya Yesu Kristo” (“The Best Is Yet to Be,” Ensign, Jan . 2010, 24, 26–27) .

Kuboresha Ufundishaji WetuAhidi baraka. wakati unapowaalika wale unaowafundisha kutenda yale wanayojifunza, toa pia ushuda juu ya baraka ambazo mungu amewaahidi wale wanaofanya hivyo. (ona pia Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 35.)

17

FEBRUARI 21–27

Mwanzo 24–27AGANO LIMEFANYWA UPYA

Unaposoma Mwanzo 24–27, sali kujua jinsi unavyoweza kuwatia moyo washiriki wa darasa kuwa na uzoefu wao wenyewe wa kujifunza kutoka kwenye maandiko .

Alika Kushiriki

Kuwatia moyo washiriki wa darasa kushiriki utambuzi wao kutoka Mwanzo 24–27, ungeweza kuwaomba wachague kifungu mahususi ambacho kinawatia moyo na wakiandike kwenye kipande cha karatasi . Kusanya karatasi, na chagua baadhi za kusoma na jadilini kama darasa .

Fundisha MafundishoMWANZO 24

Ndoa ya Agano ni muhimu kwa mpango wa milele wa Mungu.• Umuhimu ambao Ibrahimu aliuweka kwenye

kumtafuta mke kwa ajili ya Isaka unatoa fursa kujadili umuhimu wa ndoa ya agano katika mpango wa Mungu kwa ajili yetu . Kuanza majadiliano, washiriki wa darasa wangeweza kupitia kwa haraka mwanzo 24 na kushiriki vitu Bwana alivyofanya kusaidia kuwaleta Isaka na Rebeka pamoja katika ndoa . Kwa nini ndoa ni muhimu kwa Bwana? Kuwasaidia washiriki wa darasa kujadili swali hili, ungeweza kushiriki pamoja nao kauli ya Mzee D . Todd Christofferson

katika “Nyenzo za Ziada .” Jinsi gani tunaweza kusaidia kuhakikisha kwamba malengo ya Mungu kwa ajili ya ndoa yametimizwa?

• Waulize washiriki wa darasa ni sifa gani wameziona kwa mwenza, wazazi, au wenza wengine waliooana ambayo imechangia kwenye ndoa yenye uaminifu, ya furaha . Maelezo katika Mwanzo 24 yanaonesha sifa ambazo zinaweza kumsaidia mtu kutengeneza furaha katika ndoa—na katika vipengele vingine vya maisha . Kwa mfano, katika mstari wa 12 tunajifunza kuhusu kuongozwa na sala, na katika mstari wa 19 tunajifunza kuhusu kutoa juhudi za ziada katika huduma . Kanuni gani zingine zinaweza kupatikana katika sura hizi? Washiriki wa darasa wanaweza pia kuangalia kwenye “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu .” (ChurchofJesusChrist .org) .

MWANZO 25:29–34

Tunaweza kuchagua kati ya kukidhi haja haraka na vitu vya thamani kubwa.• Jinsi gani unaweza kuwasaidia washiriki wa darasa

kupata mafunzo binafsi kutokana na uzoefu wa Yakobo na Esau? Wazo moja ni kuwaomba kutengeneza orodha mbili ubaoni—moja ya baraka za milele Mungu anazotaka kutupatia na vitu vingine vya kiulimwengu ambavyo vinatuvuta kutoka kwenye baraka hizo . Kisha washiriki wa Darasa wangeweza kusoma Mwanzo 25:29–34, wakibadilisha “urithi” kwa kitu fulani kutoka kwenye orodha ya kwanza na “chakula cha dengu” na kitu fulani kutoka kwenye orodha ya pili . Jinsi

Kiel

elez

o ch

a Re

beka

, na

dill

een

mar

sh

FeBRuaRi 21–27

18

gani adui anajaribu kutushawishi kubadilisha baraka za Mungu kwa vitu ambavyo havina thamani? Fikiria kuwaomba washiriki wa darasa kupeana ushauri juu ya jinsi ya kulenga kwa Mwokozi na baraka za milele Anazotupatia .

MWANZO 26:18–25, 32–33

Yesu Kristo ni chemchemi ya maji ya uzima.• Mwanzo 26 inataja mara kadhaa kwamba Isaka

na watu wa nyumba yake walitakiwa kuchimba visima kupata maji, na hii mara nyingi ilihitaji juhudi kubwa . Ukweli huu ungeweza kukusaidia kuwafundisha washiriki wa darasa kuhusu juhudi zilizohitajika kuleta “maji ya uhai” ya Mwokozi ndani ya maisha yetu (ona Yohana 4:10) . Pengine ungeweza kueleza hili kwa mchoro ubaoni wa chanzo cha maji kilichofunikwa kwa uchafu mwingi . Washiriki wa darasa wangeweza kufanya zamu kupangusa kiasi cha uchafu wakati wanapoelezea jinsi wanavyoweza kupata maji ya uzima ya Mwokozi . Watie moyo kutumia Guide to the Scriptures kupata mistari ambayo ina uhusiano na vitu wanavyoshiriki .

Kisima katika Beer‑sheba ya kale, ambapo ibrahimu na isaka walichimba visima.

Nyenzo za ZiadaNdoa na familia ni uumbaji wa Mungu.Mzee D .Todd Christofferson alitoa baadhi ya sababu kwa nini ndoa na familia ni muhimu sana kwa mpango wa Mungu:

“Familia iliyojengwa juu ya ndoa ya mwanamume na mwanamke hutoa mazingira bora kwa mpango wa Mungu kushamiri—mazingira kwa ajili ya kuzaliwa kwa watoto, ambao huja katika usafi na wasio na hatia kutoka kwa Mungu, na mazingira kwa ajili ya kujifunza na kujitayarisha watakayohitaji kwa ajili ya ufanisi wa maisha ya duniani na uzima wa milele katika ulimwengu ujao . Kiasi fulani cha familia zilizojengwa katika ndoa kama hizo ni muhimu sana kwa jamii kustahimili na kustawi .  .  .  .

“ .  .  . Lakini madai yetu ya jukumu la ndoa na familia msingi wake si sayansi ya kijamii bali ni juu ya ukweli kuwa ni uumbaji wa Mungu . Ni Yeye hapo mwanzoni alimuumba Adamu na Hawa katika mfano wake, mwanamume na mwanamke, na akawaunganisha wao kama mume na mke kuwa ‘mwili mmoja’ na kuongezeka na kuijaza nchi . Kila mtu anabeba mfano wa kiungu, lakini ni katika muungano wa ndoa ya mwanamume na mwanamke kama kitu kimoja kwamba pengine tunaweza kupata maana kamili kabisa ya sisi kuumbwa katika mfano wa Mungu—mwanamume na mwanamke . .  .  . Ndoa kama hiyo .  .  . ni sawa na sehemu ya mpango wa furaha kama Anguko na Upatanisho” (“why Marriage, why Family,” Liahona, Mei 2015, 52) .

Kuboresha Ufundishaji WetuLenga ufundishaji wako kwenye mafundisho. Unapowaalika washiriki wa darasa kushiriki, hakikisha unaendelea kurejesha majadiliano kwenye mafundisho katika maandiko. unaweza kufanya hivi kwa kuwaomba wanafunzi wasome vifungu vya maandiko darasani, kuuliza maswali kuhusu nini maandiko yanasema, na kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki ushuhuda wao juu ya mafundisho yanayofundishwa.

19

FEBRUARI 28–MACHI 6

Mwanzo 28–33“KWELI BWANA YUPO MAHALI HAPA”

Unapojiandaa kufundisha, kwa sala fikiria kanuni zipi katika Mwanzo 28–33 zitasaidia sana kwa washiriki wa darasa lako . Mawazo yafuatayo yamekusudia kuongeza kwenye mafunzo yako binafsi na mwongozo wa kiungu .

Alika Kushiriki

Moja ya baraka ya kukusanyika katika darasa la Shule ya Jumapili ni kwamba waumini wanaweza kusaidiana kupata maana katika maandiko . Watie moyo washiriki wa darasa kushirikiana na yule waliyekaa karibu naye kile Roho Mtakatifu alichowafundisha walipojifunza maandiko wiki hii . Wachache wangeweza kualikwa kushiriki pamoja na darasa kile walichojadiliana . Hii inaweza kutengeneza mahala pazuri pa kuanzia kwa ajili ya majadiliano ya darasa .

Fundisha Mafundisho

MWANZO 28:10–22

Ndani ya Hekalu tunafanya maagano na Mungu.• Unawezaje kuwasaidia washiriki wa darasa

lako kupata maana ya uzoefu wa Yakobo huko Betheli, kama ilivyoelezwa katika Mwanzo 28:10–22? Wanaweza kuanza kwa kurejea Mwanzo 27:41–45; 28:1–5 na kufikiria maisha ya Yakobo wakati ule . Jinsi gani Yakobo

alikuwa akijisikia? Washiriki wa darasa kisha wangeweza kuchunguza Mwanzo 28:10–22 . Jinsi gani uzoefu huu ulimbariki Yakobo? Jinsi gani aliweza kufarijiwa? Jinsi gani uzoefu wa Yakobo unaweza kututia moyo tunapoabudu ndani ya hekalu? Darasa lingeweza pia kuimba, kusoma, au kusikiliza “Nearer My,God to Thee, “ambayo ina msingi kwenye mistari hii (Nyimbo za Kanisa, na . 100) . Wangeweza kushiriki virai kutoka kwenye wimbo au kutoka Mwanzo 28:10–22 ambavyo vingewakumbusha juu ya uzoefu waliokuwa nao kwa kujaribu kusogea karibu zaidi kwa mwokozi .

• Ngazi Yakobo aliyoiona katika ndoto yake mara nyingi imekuwa ikifananishwa na maagano ya hekaluni . Pengine ungeweza kuwaonesha au kuchora picha ya ngazi na hekalu . Washiriki wa darasa wangeweza kurejea Mwanzo 28:10–22 na kuzungumza kuhusu kile ambacho ngazi katika ndoto ya Yakobo inatufundisha kuhusu hekalu . Nini kingine tunachokipata katika mistari hii ambacho kinatukumbusha juu ya baraka tunazopokea kwa sababu ya maagano yetu ya hekaluni? (Ona “About the Temple Endowment” na “About a Temple Sealing” [temples .ChurchofJesusChrist .org] .)

• Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari ahadi za agano la Ibrahimu ambalo Bwana alilifanya upya na Yakobo, ungeweza kuwaomba wasome Mwanzo 28:10–15 na kuzungumza

FeBRuaRi 28–machi 6

20

kuhusu jinsi tunavyoweza kupokea baraka hizi leo (ona pia Mwanzo 12:2–3) . Wangeweza pia kusoma maelezo ya Rais Russell M . Nelson katika “Nyenzo za Ziada,” wakitafuta baraka ambazo zinakuja kutokana na kufanya na kushika maagano . Jinsi gani Yakobo alibarikiwa kwa kupokea ahadi zinazopatikana katika Mwanzo 28:10–15? Ni mahusiano gani tunayoyaona kati ya matukio katika mistari hii na matukio katika Mwanzo 29 na 30 (Yakobo akioa na kuzaliwa kwa watoto wake)? Ni kwa jinsi gani Bwana anatubariki tunapofanya na kushika maagano matakatifu?

Kielelezo cha Yakobo na esau wakikumbatiana, na Robert T. Barrett

MWANZO 32–33

Mwokozi anaweza kutusaidia kushinda kutokuelewana katika familia zetu.• Mwanzo 32–33 inaweza kuwatia moyo washiriki

wa darasa wanaotaka kupata uponyaji katika mahusiano ya familia zao . Inaweza kuwa ya kusaidia kumwomba mshiriki wa darasa kwa kifupi kufanya muhutasari wa matukio yaliyoandikwa katika Mwanzo 27 . Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unajumuisha maswali ya kutafakari wakati wa kujifunza Mwanzo 32–33 . Pengine washiriki wa darasa wangeweza kuchagua moja ya maswali haya na kutafuta majibu katika sura hizi . Wanaweza pia kuwa radhi kushiriki uzoefu waliowahi kuwa nao kwa kuimarisha mahusiano ya kulazimishwa katika familia zao . Watie moyo kuzungumza kuhusu jinsi Baba wa Mbinguni alivyowasaidia .

Nyenzo za Ziada

Sisi ni watoto wa agano. Rais Russell M . Nelson alifundisha:

Wakati wa ubatizo tunaweka agano kumtumikia Bwana na kutii amri Zake . Tunaposhiriki sakramenti, tunafanya upya agano hilo na kutangaza utayari wetu kujichukulia juu yetu jina la Yesu Kristo . Kwa hiyo tumeasiliwa kama wana na mabinti zake na tunajulikana kama kaka na dada . Yeye ni Baba wa maisha yetu mapya . Hatimaye, katika hekalu takatifu, tunaweza kuwa warithi wa pamoja kwa baraka za familia ya milele, kama mwanzo ilivyoahidiwa kwa Ibrahimu, Isaka, Yakobo na uzao wao . Kwa hiyo, ndoa za selestia ni agano la kuinuliwa .

“Tunapotambua kwamba sisi ni wana wa agano, tunajua sisi ni nani na kile Mungu anachotarajia kutoka kwetu . Sheria yake imeandikwa katika mioyo yetu . Yeye ni Mungu wetu na sisi ni watu Wake . Wana wa agano wenye msimamo wanabaki imara, hata katika mateso . Wakati fundisho hilo likipandwa ndani ya mioyo yetu, hata maumivu ya kifo yanafanywa kuwa nafuu na nguvu yetu ya kiroho inaimarishwa” (“maagano,” Liahona, Nov . 2011, 88) .

Kuboresha Ufundishaji WetuWasaidie wanaojifunza kufanyia kazi ushawishi. “Uongofu wa kweli unajumuisha zaidi ya kuhisi Roho tu akithibitisha ukweli katika nafsi zetu; ni lazima pia tuufanyie kazi ukweli huo. Zaidi ya kuwasaidia wanaojifunza kuhisi na kumtambua Roho, wasaidie kutenda juu ya ushawishi wanaoupokea” (Kufundisha katika njia ya mwokozi 10).

21

MACHI 7–13

Mwanzo 37–41“BWANA ALIKUWA PAMOJA NA YUSUFU”

Haikusudiwi kwamba ufundishe shughuli zote katika muhutasari huu . Unapojiandaa kufundisha, omba kwamba Roho akusaidie kujua ni shughuli gani (kama zipo) katika muhutasari huu zitakidhi vyema mahitaji ya darasa lako .

Alika Kushiriki

Kuwatia moyo washiriki wa darasa kushiriki kile walichojifunza katika kujifunza kwao binafsi na kifamilia, ungeweza kuwaomba kutafuta kirai katika Mwanzo 37–41 ambacho kinaelezea somo au kanuni wanayohisi ni muhimu .

Fundisha MafundishoKUTOKA 37:1–28; 39; 40:1–19; 41:9–45

“Bwana alikuwa pamoja na Yusufu” katika shida zake.• Kama Yusufu, washiriki wa darasa lako wanaweza

kuwa wanakabiliana na majaribu . Kulisaidia darasa kupata mwongozo wa kiungu katika mfano wa Yusufu, ungeweza kuwagawa katika makundi matatu na kuliomba kila kundi kurejea upya moja ya vifungu vya maandiko vifuatavyo: Mwanzo 39: 40:1–19; au 41:9–45 . Kila kundi kisha lingeweza kushiriki njia ambazo Bwana alikuwa na Yusufu katika changamoto zake . Kama inafaa, washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu wakati Bwana alipokuwa pamoja nao wakati wa majaribu magumu . Jinsi

gani tunaweza kujifunza kuona vyema uwepo wa Bwana katika maisha yetu?

• Somo hili linalofundishwa kwa vielelezo linaweza kueleza jinsi tunavyoweza kuinuka juu ya shida: weka kitu chepesi, kama vile mpira wa plastiki, chini ya chombo kilichojazwa nusu yake kwa mchele mkavu au maharage . Mwombe mtu fulani atikise chombo polepole mpaka mpira uinuke mpaka juu . Jinsi gani Yusufu alikuwa kama mpira? Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki mifano ya Bwana kumsaidia Yusufu kuinuka juu ya shida kutoka Mwanzo 37:5–11; 39; 40:1–19; 41:9–45 . Wangeweza pia kushiriki nyakati Bwana alipowasaidia katika njia sawa na hizo .

• Ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kuimba au kusoma maneno ya wimbo kuhusu kufanya chaguzi za haki, kama vile “Do What Is Right” (nyimbo za Kanisa, na . 237) . Kisha washiriki wa darasa wangeweza kupata utambuzi au virai katika Mwanzo 37:1–28; 39; 40:1–19; 41:9–45 ambavyo vinaelezea jumbe za wimbo . Jinsi gani Yusufu alibarikiwa, licha ya shida zake, wakati alipofanya kile kilicho chema? Lini Bwana ametubariki katika nyakati za shida kwa kufanya jambo jema?

MWANZO 37:5–11; 40; 41:1–38

Kama tuna imani, Bwana atatuongoza na kututia moyo.• Ingawa sio kila mtu anapokea ufunuo binafsi

kupitia ndoto, kuna vitu tunaweza kujifunza kuhusu ufunuo kutokana na uzoefu wa Yusufu,

Kiel

elez

o ch

a Yu

sufu

wa

mis

ri ge

reza

ni, n

a Je

ff W

ard

machi 7–13

22

watumishi wa Farao, na Farao . Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kurejea upya Mwanzo 37:5–11; 40:5–8; 41:14–25, 37–38 na kushiriki kila kitu walichojifunza kuhusu ufunuo . ungeweza pia kuwaomba kushiriki kile ambacho kimewasaidia kujiandaa kupokea, kuelewa, na kufanyia kazi ufunuo .

Yusufu akitafsiri Ndoto za Mnyweshaji na Mwoka mikate, na François Gérard

MWANZO 39:1–20

Kwa msaada wa Bwana, tunaweza kukimbia majaribu.• Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa

kushiriki kile walichojifunza kuhusu kuepuka majaribu wakati wanaposoma Mwanzo 39 wiki hii . Yusufu alifanya nini kushinda majaribu? (Ona mistari 7–12) . Video “Leave the Party” na “Dare to Stand Alone” (ChurchofJesusChrist .org) zinatoa mifano ya watu walioepuka majaribu . Fikiria kuwaomba washiriki wa darasa kutengeneza orodha ya vitu tunavyoweza kufanya ili kuvuta uwezo wa Bwana wakati tunapokabiliana na majaribu . (Washiriki wa darasa wangeweza kupata mawazo katika Mathayo 4:1–11 au katika maandiko yaliyoorodheshwa chini ya “Tempt, Temptation” katika Mwongozo kwenye Maandiko [scriptures .ChurchofJesusChrist .org] .)

• Jinsi gani unaweza kutumia mfano wa Yusufu kuwasaidia washiriki wa darasa kuepuka jaribu la kufanya dhambi ya uasherati? Kwa kuongezea kwenye kurejea upya Mwanzo 39:1–20, washiriki wa darasa wangeweza kuangalia video “Chastity: What are the Limits?” (ChurchofJesusChrist .org) au kurejea upya “Sexual Purity”

(katika Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana (2011), 35–37) . Wangeweza kushiriki kile wanachojifunza kuhusu kuepuka mawazo, maneno, na matendo ambayo yanaelekeza kwenye dhambi ya uasherati . Kurejea upya “Toba” (katika Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana, 28–29) kunaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa fursa ambayo Yesu Kristo anatoa kwetu ya kutubu .

MWANZO 41:15–57

Tunapaswa kujiandaa kwa ajili ya uwezekano wa taabu.• Ungeweza kumwomba mshiriki mmoja wa darasa

kuelezea ndoto za Farao (ona Mwanzo 41:15–24) na mwingine kushiriki tafsiri za Yusufu (ona mistari 25–32) . Yusufu alishauri kufanya nini? (Ona mistari 33–36, 47–49) . Ni mafunzo gani maelezo haya yanayo kwa ajili ya wakati wetu? (Ona ushauri wa Rais Gordon B . Hinckley katika “Nyenzo za Zaida”) .

Nyenzo za Ziada

Jiandae kwa ajili ya nyakati za matatizo.Rais Gordon B . Hinckley alisema: “Ninawasihi nyinyi muwe wenye staha katika matumizi yenu; mjiwekee nidhamu wenyewe katika manunuzi yenu ili kuepuka madeni kadiri iwezekanavyo . Lipa deni haraka kadiri uwezavyo . .  .  . Kuwa na akiba, hata kama itakuwa ndogo” (To the Boys and to the Men, Ensign, Nov . 1998, 54) .

Kuboresha Ufundishaji WetuKusikiliza ni kitendo cha upendo. muombe Baba wa mbinguni akusaidie kuelewa kile washiriki wa darasa lako wanachosema. Unapotoa usikivu wa makini kwa jumbe zao zinazozungumzwa na zisizozungumzwa, utakuja kuelewa vyema mahitaji yao” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 34).

23

MACHI 14- 20

Mwanzo 42–50“MUNGU ALIYAKUSUDIA KUWA MEMA”

Mzee David A . Bednar alisema, “Uelewa wa kiroho ambao nyinyi na mimi tumebarikiwa kuupata .  .  . kwa kawaida hauwezi kutolewa tu kwa mtu mwingine” (“Tafuta Kujifunza kwa Imani,” Ensign, Sept . 2007, 67) . Utawezaje kuwasaidia washiriki wa darasa kupata uelewa wa kiroho kwa ajili yao wenyewe?

Alika Kushiriki

Kuwapa washiriki wa darasa fursa ya kushiriki kitu fulani walichokipata chenye maana katika kujifunza binafsi maandiko au kifamilia, ungeweza kuuliza maswali kama haya mwanzoni mwa darasa: ni mstari gani katika sura hizi uliuelewa vizuri? Ni mstari gani ulijikuta ukiusoma zaidi ya mara moja? Ni mstari gani uliushiriki na mtu mwingine? Ni msitari gani ilikulielekeza kwenye majadiliano ya kiutambuzi na familia yako au marafiki?

Fundisha Mafundisho

MWANZO 45:1–15; 50:15–21

Msamaha Huleta amani.• Kabla hujaanza majadiliano kuhusu nini uzoefu

wa Yusufu unafundisha kuhusu msamaha, inaweza kusaidia kumpata mtu fulani kwa kifupi aelezee hadithi katika Mwanzo 37; 39–45 . Kwa nini iliweza kuwa vigumu kwa Yusufu kuwasamehe kaka zake? Uzoefu gani au fikra ziliweza kumpa Yusufu nguvu kuwasamehe?

(Ona, kwa mfano, mwanzo 45:1–15 au 50:15–21) Jinsi gani mfano wa Yusufu unatusaidia kuwa wenye kusamehe zaidi?

Video “Forgiveness: My Burden Was Made Light” (ChurchofJesusChrist .org) inatoa mfano mwingine unaotia moyo wa msamaha . Jinsi gani Mwokozi anatusaidia kusamehe wengine?

• Baraka gani zilikuja kutokana na msamaha wa Yusufu kwa kaka zake? Inaweza kuwa ya kupendeza kufananisha mahusiano katika familia ya Yakobo mwanzoni mwa hadithi (ona, kwa mfano, Mwanzo 37:3–11) pamoja na hali yao mwishoni (ona Mwanzo 45:9–15; 50:15–21) . Ni jukumu gani msamaha ulifanya katika mabadiliko ya familia ya Yusufu? Jinsi gani mambo yangeweza kuwa tofauti kama Yusufu asingekuwa radhi kusamehe? Unaweza kumwomba mshiriki wa darasa kupendekeza njia ambayo hadithi hii ingeweza kuzisaidia familia leo kushinda mabishano na wivu .

MWANZO 45:5–11; JOSEPH SMITH TRANSLATION (KATIKA KIAMBATANISHO CHA BIBLIA)

Kazi za Yusufu, Musa, na Joseph Smith zinashuhudia juu ya misheni ya Yesu Kristo. • Kwa nuru ya ziada ya injili ya urejesho, tunajua

kwamba Yusufu, ambae aliokoa familia yake kwenye njaa, pia alitabiri juu ya baraka kuu

Kiel

elez

o ch

a Yu

sufu

wa

mis

ri, n

a Ro

bert

 T. B

arre

tt

machi 14–20

24

ambazo siku moja zitakuja kupitia Musa na Joseph Smith . Na manabii wote hawa wanatuelekeza kwa Mkombozi Wetu Mkuu, Yesu Kristo . Kuwasaidia washiriki wa darasa kumwona Mwokozi katika huduma za manabii hawa watatu, ungeweza kuchora chati ubaoni sawa na ile inayopatikana katika “Nyenzo za Ziada .” Washiriki wa darasa wangeweza kufanya kazi pamoja kuijaza . Kisha wangeweza kuongeza safu zinazoelezea kazi ya Yusufu wa Misri, Musa, na Joseph Smith, wakitumia kile wanachosoma kutoka Mwanzo 45:5–11 na Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 50:24–38 (katika kiabatanisho cha Biblia) . Jinsi gani huduma za manabii hawa zunashuhudia juu ya, na kuelekeza kwenye misheni ya Mwokozi? (Kwa baadhi ya mifano ya mifanano kati ya maisha ya Yusufu wa Misri na maisha ya Mwokozi, ona Mwanzo 37:3 na Mathayo 3:17; Mwanzo 37;26–28 na Mathayo 26:14–16; Mwanzo 45:5–7 na Luka 4:18; na Mwanzo 47:12 na Yohana 6:35; ona pia Musa 6:63 .)

Kielelezo cha Yusufu wa misri, na paul mann

MWANZO 50:19–21

Mungu anaweza kutusaidia kupata maana katika majaribu yetu.• Ingawa yawezekana haikuwa wazi alipokuwa

akipitia majaribu yake makali, Yusufu hatimaye aliweza kuangalia nyuma kwenye shida zake Misri na kuona kwamba “Mungu aliyakusudia kuwa mema” (Mwanzo 50:20) . Kama tungeweza kumtembelea Yusufu alipokuwa shimoni au gerezani, jinsi gani tungeweza kumfariji? Jinsi gani wazo lililoelezwa katika Mwanzo 50:19–21 litatusaidia katika nyakati za majaribu? Pengine

washiriki wa darasa wataridhia kuzungumza kuhusu njia ambazo Mungu amewabariki hata kupitia uzoefu mgumu walioupata . Kwa mfano mmoja, ona video “Unto All the World: The Sam Family” (ChurchofJesusChrist .org) . Ni nini Mafundisho na Maagano 122 inaoongeza kwenye uelewa wetu wa kanuni hii?

Nyenzo za Ziada

Maisha ya manabii yanashuhudia juu ya Yesu Kristo na misheni yake.Maisha ya Yusufu wa Misri, Musa, na Joseph Smith yanaweza kutukumbusha juu ya Yesu Kristo . Washiriki wa darasa wangeweza kujaza chati hii na kisha kuongeza safu kwa ajili ya Yusufu wa Misri (ona Mwanzo 45:5–11), Musa (ona Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 50:24, 29, 34–36 [katika kiambatanisho cha Biblia]), na Joseph Smith (ona Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 50:26–28, 30–33 [katika kiambatanisho cha Biblia]) .

Yesu Kristo

Nani alikombolewa?

walikombolewa kutoka nini?

Nini kilifanyika kuwakomboa?

Kuboresha Ufundishaji WetuUliza maswali ambayo yanaalika kushuhudia. Kuuliza maswali ambayo yanawatia moyo wanafunzi kutoa shuhuda zao kunaweza kuwa njia ya kufaa ya kumwalika Roho. Kwa mfano, unapofundisha mwanzo 45:1–15, ungeweza kuuliza maswali kama “baraka gani umezipata kama matokeo ya kumsamehe mtu fulani?” (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 32).

25

MACHI 21–27

Kutoka 1–6“NIMEKUMBUKA AGANO LANGU”

Uliposoma Kutoka 1–6, fikiria kuhusu watu unaowafundisha . Kweli zipi katika sura hizi ni za kufaa kuwa za maana kwao? Ni kwa jinsi gani utaweza kuwasaidia kugundua kweli hizi?

Alika Kushiriki

Wazo moja la kuwatia moyo washiriki wa darasa kushiriki kile wanachojifunza ni kuandika swali kama hili ubaoni: Unaposoma Kutoka 1–6, ulitambua nini ambacho hukutambua kabla? Waombe washiriki wa darasa kushiriki majibu yao .

Fundisha Mafundisho

KUTOKA 1–2

Yesu Kristo ni Mkombozi wetu. • Hata kama Mwokozi hakutajwa kwa jina katika

Kutoka 1–2, maelezo haya yanaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kujenga imani katika misheni Yake kutukomboa kutoka utumwa . Washiriki wa darasa wangeweza kupata maneno au virai katika Kutoka 1–2 ambavyo vinaelezea taabu walizokumbana nazo wana wa Israeli . Jinsi gani maelezo haya yanafanana na utumwa wa kiroho au taabu zingine tunazokumbana nazo? Jinsi gani wana wa Israeli walitafuta kukombolewa, na jinsi gani Mungu aliwajibu? (Ona pia Kutoka 2:23–25; 3:7–8) . Jinsi gani tunatumia

nguvu za Mungu tunapohitaji kukombolewa? Jinsi gani Mungu anajibu maombi yetu kwa ajili ya msaada? Washiriki wa darasa wangeweza kutafuta utambuzi wa ziada katika ujumbe wa Rais Russell M . Nelson “Drawing the Power of Jesus into Our Lives” (Liahona, Mei 2017, 39–42) .

Musa katika Nyasi, © Providence collection/licensed from goodsalt.com

KUTOKA 3–4

Tunapofanya kazi ya Bwana, tunaweza kuwa na nguvu za Bwana.• Mhuhtasari wa wiki hii katika Njoo,Unifuate—Kwa

Ajili ya watu binafsi na Familia unapendekeza kuchunguza Kutoka 3–4 kutafuta jinsi Bwana alivyojibu wasiwasi wa Musa kuhusu kazi ya kuwakomboa Wana wa Israeli kutoka utumwani . Kama washiriki wa darasa lako walifanya shughuli hii nyumbani, waombe kushiriki kile walichojifunza . Au mngeweza kufanya shughuli hii kama darasa . Hususani, washiriki wa darasa wangeweza kuchunguza Kutoka 3:11–18; 4:1–17,

Mus

a na

Kich

aka

Kina

chou

ngua

, na

har

ry

ande

rson

machi 21–27

26

kutafuta wasiwasi wa Musa na majibu ya Bwana kwa kila moja wapo . Jinsi gani majibu ya bwana yangetusaidia wakati tuna wasiwasi kuhusu uwezo wetu wa kufanya kazi Yake?

KUTOKA 3:5

Tunapaswa kuonesha heshima kuu kwa vitu na sehemu takatifu.• Jinsi gani unaweza kutumia mfano wa Musa kutia

moyo majadiliano kuhusu jinsi tunavyopaswa kuvichukulia vitu vitakatifu? Kwa mfano, baada ya kusoma Kutoka 3:5 pamoja, ungeweza kuonesha vitu vitakatifu au picha za vitu vitakatifu (kama vile maandiko au mahekalu) na vitu vya kawaida au picha za vitu vya kawaida (kama vile vitabu vya kidunia au majengo ya kawaida) . Washiriki wa darasa wangeweza kuzungumza kuhusu vitu vingine wanavyofikiri ni vitakatifu na kushiriki jinsi wanavyoonesha heshima kuu kwa vitu hivyo (ona pia Mambo ya Walawi 19:30; Mafundisho na Maagano 6:10–12) . Kwa nini Mwokozi anatutaka kuvichukulia vitu vitakatifu kwa heshima kuu?

KUTOKA 5:4–9, 20–23; 6:1–13

Azma za Bwana zitatimizwa katika muda wake mwenyewe.• Inaweza kukatisha tamaa wakati juhudi zetu

za dhati kufanya mema hazionekani kufanya kazi—pengine rafiki hashawishiki kwenye juhudi zetu za kuhudumia au sala zetu za kwa ajili ya mtoto mtukutu zinaonekana hazijibiwi . Kujifunza kuhusu uzoefu kama huo aliokuwa nao Musa, washiriki wa darasa wangeweza kusoma Kutoka 5:4–9, 20–23 . Bwana alimsaidia vipi Musa kushinda hisia zake za kukata tamaa? (Ona Kutoka 6:1–13) . Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu wakati hawakuona matokeo ya mara moja kutokana na jitihada zao za kumtumikia Bwana . Uzoefu alioupata Musa katika sura hizi unatufundisha nini kuhusu jinsi tunavyoweza kuitikia katika hali kama hizo? (Ona pia “Nyenzo za Ziada .”)

Nyenzo za Ziada

Tunawatumikia wengine kwa ajili ya Bwana.Rais Joy D . Jones alieleza jinsi yeye na mume wake walivyotumikia kwa uaminifu katika kazi waliyopangiwa ya kuhudumu lakini hawakuona mafanikio kutokana na juhudi zao . Wawili hao walitafakari na kusali kwa ajili ya mwongozo . Akisimulia jibu kwa sala zao, Rais Jones alisema:

“Tuligundua kwamba tulikuwa tukijaribu kwa uaminifu kuhudumia familia hii na kumtumikia askofu wetu, lakini tulipaswa kujiuliza kama kweli tulihudumu kwa sababu ya upendo kwa Bwana . Mfalme Benyamini aliweka wazi tofauti hii wakati aliposema, ‘Tazama, nawaambia kwamba kwa sababu niliwaambia kuwa nimewatumikia maishani mwangu, sitamani kujivuna, kwani nimekuwa tu katika utumishi wa Mungu’ [Mosia 2:16; msisitizo umeongezwa] .

“Hivyo nani hasa Mfalme Benyamini alikuwa akimtumikia? Baba wa Mbinguni na Mwokozi . Kujua ni nani na kwa nini katika kutumikia wengine kunatusaidia kuelewa kwamba onyesho kuu la upendo ni kujitolea kwa Mungu” (“Kwa ajili Yake,” Liahona, Nov . 2018, 50) .

Kuboresha Ufundishaji WetuShiriki uzoefu wa kiroho. Njia moja ya kualika ushawishi wa Roho mtakatifu katika darasa lako ni kuwatia moyo washiriki wa darasa kushiriki kile Roho mtakatifu alichowafundisha walipokuwa wakijifunza maandiko wiki hii.

27

MACHI 28–APRILI 3

Kutoka 7–13“KUMBUKENI SIKU HII, MLIYOTOKA NCHI YA MISRI”

Uwezo wako wa kuongozwa na Roho katika kufundisha kwako utaongezwa zaidi pale unapokuwa na uzoefu wako wa kiroho wa kujifunza Kutoka 7–13 .

Alika Kushiriki

Fikiria swali moja au mawili ambayo yatawatia moyo washiriki wa darasa kushiriki utambuzi na uzoefu waliokuwa nao walipojifunza Kutoka 7–13 binafsi na pamoja na familia zao . Kwa mfano, unaweza kuuliza, “Ulisoma nini wiki hii ambacho kiliimarisha imani yako katika Yesu Kristo?” au “Ulisoma nini ambacho kilikuwa baraka kwa familia yako?”

Fundisha Mafundisho

KUTOKA 7–12

Tunaweza kuchagua kulainisha mioyo yetu.• Kuwasaidia washiriki wa darasa kufikiria

kuhusu utayari wa kutoa mioyo yao kwa Mungu, ungeweza kuwaomba kila mmoja wao kusoma vifungu vifuatavyo vya maandiko: Kutoka 7:14–25; 8:5–15; 8:16–19; 8:20–32; 9:1–7; 9:8–12; 9:22–26; 10:12–15; 10:21–29; 12:29–33 . Kisha wangeweza kuandika ubaoni maneno au virai ambavyo vinaelezea jinsi Farao alivyojibu mapigo kumi yaliyotumwa na Mungu juu ya

Wamisri . (Unaweza kutaka kutambua kwamba marejeo ya tafsiri ya Joseph Smith yanaonesha kwamba Farao ilishupaza moyo wake .) Kwa nini Farao aliweza kujibu jinsi alivyojibu? Kwa nini inakuwa mara kwa mara vigumu kuachia mioyo yetu na mapenzi yetu kwa Mungu? Jinsi gani Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanatusaidia kushinda magumu haya?

• Kwa kuleta darasani kitu kigumu na kitu laini, ungeweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa inamaanisha nini kuwa na moyo mgumu au laini . Ungeweza kupitisha vitu hivyo viwili kuzunguka darasa, wakati mtu fulani anasoma moja ya maelezo ya moyo wa Farao yanayopatikana kwenye Kutoka 7–10 (kama vile Kutoka 9:22–35) . Kwa nini “mgumu” ni maelezo mazuri ya moyo wa Farao? Aya hizi zinafundisha nini kuhusu kile inachomaanisha kuwa na moyo laini? (Kama inasaidia, washiriki wa darasa wangeweza kutafuta utambuzi katika moja au zaidi ya maandiko haya: 1 Nefi 2:16; Mosia 3:19; Alma 24:7–8; 62:41; Etheri 12:27 .) Ni jinsi gani Mwokozi anatusaidia kulainisha mioyo yetu? Video “A Change of heart” (ChurchofJesusChrist .org) inaweza kuongeza kwenye uelewa wao .

• Kusaidia washiriki wa darasa kufikiria kuhusu kwa nini Bwana alituma mapigo juu ya Misri, ungeweza kumwomba kila mshiriki wa darasa kuchagua rejeleo moja kutoka kwenye orodha ifuatayo na kutafuta sababu zinazowezekana:

Kiel

elez

o ch

a m

usa

na h

arun

i kat

ika

mah

akam

a ya

Far

ao, n

a Ro

bert

 T. B

arre

tt

machi 28–aPRili 3

28

Kutoka 3:20; 7:5, 17; 9:14–16; 10:1–2 . Ungeweza pia kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki jinsi ambavyo wamejifunza kwamba “hakuna yoyote kama [Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo] duniani kote” (Kutoka 9:14) .

KUTOKA 12

Pasaka na sakramenti zinafundisha kuhusu ukombozi kupitia Yesu Kristo.• Kuadhimisha sikukuu ya Pasaka kuliwasaidia

watoto wa Israeli kukumbuka kwamba Bwana alikuwa amewakomboa kutoka utumwani . Kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa ishara ya Pasaka, ungeweza kutengeneza safu mbili ubaoni zenye vitabulisho Ishara na Maana Inayowezekana, pamoja na picha ya Jesu Kristo juu ya safu . Washiriki wa darasa wangeweza kujifunza Kutoka 12:1–13 na kuandika ubaoni chochote kutoka katika mistari hii ambacho kingeweza kuashiria ukombozi wetu kupitia Yesu Kristo . Wangeweza kisha kujadili nini ishara hizi zinatufundisha kuhusu Upatanisho wa Mwokozi (ona jedwali katika “Nyezo za Ziada” kwa ajili ya mawazo machache) . Video “The Passover” (ChurchofJesusChrist .org) inaweza kuwasaidia kupata taswira ya kile wanachokisoma kwenye Kutoka 12 .

Kama mlo wa pasaka, sakramenti inatusaidia sisi kumkumbuka mkombozi wetu, Yesu Kristo.

• Kwa baadhi ya watu, sakramenti si mara zote ya kiroho kama ambavyo ingetakiwa kuwa . Fikiria jinsi ambavyo majadiliano ya Kutoka 12 yangeweza kuwasaidia washiriki wote wa darasa kupata maana ya kina zaidi katika Sakramenti .

Kwa mfano, baada ya washiriki wa darasa kurejea upya Kutoka 12, unaweza kuwaomba kushiriki kile ambacho Waisraeli kutoka kipindi hicho wangeweza kusema kama mwana au binti angewauliza Pasaka ilimaanisha nini kwao . Washiriki wa darasa kisha wangeweza kujadili nini wangeweza kusema kama mtu fulani angeuliza sakramenti inamaanisha nini kwao, ikiwa ni pamoja na utambuzi wowote wanaopata kutoka kwenye Pasaka . Ungeweza kuwapa washiriki wa darasa muda wa kutafakari nini wanaweza kufanya kumkumbuka Mwokozi kila siku . Video “Always Remember Him” (ChurchofJesusChrist .org) ingeweza kuwasaidia .

Nyenzo za Ziada

Pasaka inafundisha kuhusu Mwokozi.

Ishara Maana Inayowezekana

mwanakondoo (Kutoka 12:3–5)

Yesu Kristo

damu kwenye vizingiti vya mlango (Kutoka 12:7).

damu ya kupatanisha ya Yesu Kristo, anayetuokoa

Kumla mwanakondoo (Kutoka 12:8)

Kumfanya mwokozi sehemu ya maisha yetu

mboga chungu (Kutoka 12:8)

Uchungu wa utumwa (dhambi)

Kuboresha Ufundishaji WetuSikiliza. “Kusikiliza ni tendo la upendo. . . . muombe Baba wa mbinguni akusaidie kuelewa kile washiriki wa darasa lako wanachosema. Unapotoa usikivu wa umakini kwa jumbe zao zinazozungumzwa na zisizozungumzwa, utakuja kuelewa vyema mahitaji yao, mashaka yao, na matamanio yao” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 34).

29

APRILI 4–10

Kutoka 14–17“SIMAMENI KIMYA, NA MUONE WOKOVU WA BWANA”

Fikiria kuhusu jinsi uzoefu wa wana wa Israeli unavyotumika kwa washiriki wa darasa lako . Ni uzoefu gani utakuwa wa msaada mno kwao kujadili?

Alika KushirikiKutoka 14–17 imejazwa na maelezo ya kukumbukwa . Mshiriki wa darasa angeweza kuchora picha ya tukio kutoka sura hizi wakati washiriki wengine wa darasa wakikisia nini yeye anachokichora . Waombe kushiriki kile walichojifunza kutokana na maelezo hayo .

Fundisha MafundishoKUTOKA 14

Baba wa Mbinguni hutuokoa tunapomfuata Roho.• Bahari ya Shamu ilionekana kama mwisho wa

Waisraeli, lakini Mungu alijua vitu wasivyovijua . Kurejea upya maelezo ya uvukaji wa kimiujiza wa Bahari ya Shamu kungeweza kuwakumbusha washiriki wa darasa juu ya nyakati Mungu alipowakomboa kutokana na majaribu yao . Ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kurejea upya Kutoka 14 na kushiriki kile kinachowavutia zaidi kuhusu maelezo haya . Pia watie moyo kushiriki uzoefu wao wa kukombolewa kutoka kwenye majaribu, pamoja na mistari kutoka kwenye sura ambayo inajenga imani yao kwamba Mungu anaweza kutukomboa sisi .

• Inaweza pia kuvutia kusoma pamoja Mafundisho na Maagano 8:2–3 . Mistari hii inafundisha nini kuhusu Musa? Jinsi gani mistari hii inaathiri tunavofikiri kuhusu matukio katika Kutoka 14? Inapendekeza nini kuhusu jinsi tunavyotafuta ukombozi kutokana na majaribu yetu? Fikiria kile ambacho maelezo katika “Nyenzo za Ziada” yangeweza kuongezea kwenye mjadala wenu .

KUTOKA 15:23–27; 16:1–15; 17:1–7

Bwana atakidhi mahitaji yetu tunaposafiri kupitia maisha.• Kutoka 15–17 inatupa maelezo mengi ambayo

yanaweza kujenga imani ya washiriki wa darasa katika uwezo wa Bwana na utayari wake kukidhi mahitaji yetu ya kimwili na kiroho . Pengine kila mshiriki wa darasa angeweza kujifunza moja ya vifungu vifuatavyo, akitafuta jumbe za kiroho: Kutoka 15:23–27; 16:1–15; 17:1–7 . Wape baadhi ya washiriki wa darasa nafasi ya kushiriki kile walichopata . Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia maelezo haya kumtia moyo mtu fulani ambaye ana mahitaji yake ya kimwili au kiroho ambayo hayajatimizwa?

• Washiriki wa darasa wangeweza pia kusoma mistari hii na kutambua mifano ya kunu’gunika . Jinsi gani tunaweza kuelezea kwa mtu fulani ina maanisha nini kunu’gunika? Nini baadhi ya matokeo ya kunun’gunika ambayo yanaleta hatari kubwa? Pengine washiriki wa darasa wangeweza

Baha

ri ya

sha

mu

aPRili 4–10

30

kushiriki ushauri juu ya jinsi ya kuepuka jaribu la kunun’gunika dhidi ya Bwana tunapokabiliana na majaribu magumu .

• Inaweza kusaidia washiriki wa darasa kufananisha mana iliyoelezwa katika Kutoka 16 na chakula roho zetu zinachohitaji . Ni mifanano gani tunayoiona? Ni mafunzo gani ya kiroho Bwana angetaka kuwafundisha Waisraeli kwa kutuma mana katika njia Aliyofanya? (Ona Yohana 6:31–35, 48–58) . Ungeweza pia kuonesha moja au zaidi ya video inayopatikana katika “Nyezo za Ziada .”

KUTOKA 17:8–16

Tunabarikiwa tunapowaidhinisha viongozi wetu.• Maelezo ya Haruni na Hur wakishikilia juu

mikono ya Musa yanaelezea kwa mfano umuhimu wa kuwaidhinisha wale walioitwa kutuongoza . Ungeweza kuwaomba washiriki wachache wa darasa kuigiza uzoefu wakati mshiriki mwingine akiusoma kwa sauti kubwa . Jinsi gani juhudi za Haruni na Hur kushikilia mikono ya Musa zinafanana na juhudi zetu za kuwaidhinisha viongozi wetu? Jinsi gani tunaonesha kwamba tunawaidhinisha viongozi wetu?

Nyenzo za Ziada

Unaweza kupokea maelekezo yaliyo ya binafsi.Dada Michelle Craig alifundisha:

“Kama mfuasi mwaminifu wa [Mwokozi], unaweza kupokea msukumo binafsi na ufunuo, wenye kukubaliana na amri zake, ambao unastahili kwako . Mnazo misheni za kipekee na majukumu ya kipekee ya kutekeleza maishani na mtapewa mwongozo wa kipekee kuyatimiza .

Nefi, kaka wa Yaredi, na hata Musa wote walitakiwa kuvuka sehemu kubwa iliyokuwa na maji—na kila mmoja ilifanya hivyo kwa njia tofauti . Nefi alifanyia kazi ‘mbao kwa ufundi maalumu’ [1 Nefi 18:1] . Kaka wa Yaredi alijenga mashua ambazo zilikuwa “zimekazwa kama bakuli’ [ona Etheri 6:5–8] . Na Musa “alitembea juu ya nchi kavu katikati ya bahari .” [Kutoka 14:29] .

“Kila mmoja wao alipokea mwongozo binafsi, uliowafaa wao, na kila mmoja alionesha uaminifu na kutenda . Mungu anawakumbuka wale wanaotii na, kwa maneno ya Nefi, “atatayarisha njia kwa ajili yetu [sisi ili] kutimiza kitu ambacho ameamuru .’ [1 Nefi 3:7] Tambua kwamba Nefi anasema, ‘njia ‘—sio ‘ile njia .”

“Je, sisi tunakosa au kupuuza utumishi binafsi kutoka kwa Bwana kwa sababu ametayarisha ‘njia” tofauti na ile tunayoitarajia? (“Uwezo wa Kiroho,” Liahona, Nov . 2019, 21) .

VideoKatika video “Daily Bread: Pattern,” “Daily Bread: Experience,” na “Daily Bread: Change” (ChurchofJesusChrist .org), Mzee D . Todd Christofferson alishiriki utambuzi kuhusu muujiza wa mana .

Kuboresha Ufundishaji WetuWatie moyo Wengine Kutoa Ushuhuda. wengi wa wale unaowafundisha wana ushahidi binafsi wenye nguvu wa ukweli wa kushiriki. waalike kushiriki shuhuda zao kwa kuwauliza maswali ya kawaida, kama vile, “Umebarikiwa vipi kwa kumfuata nabii?” (ona pia Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 11.)

31

APRILI 11–17

Pasaka“ATAMEZA MAUTI HATA MILELE”

Unapojiandaa kufundisha siku ya Jumapili ya Pasaka, fikiria jinsi unavyoweza kuwasaidia washiriki wa darasa kupata shukrani za kina kwa ajili ya, na ushuhuda wa dhabihu ya upatanisho wa Yesu Kristo na Ufufuko .

Alika KushirikiPengine ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki kile wao au familia zao walichofanya kuimarisha imani yao katika Yesu Kristo na Upatanisho wake wakati wa majira ya Pasaka .

Fundisha MafundishoKwa sababu Mwokozi alishinda kifo, sisi vilevile tutaishi tena.• Kwa vile leo ni Jumapili ya Pasaka, fikiria

kurejea upya maelezo ya maandiko ya Pasaka ya kwanza—Kufufuka kwa Yesu Kristo (ona Yohana 20:1–17) . Ungeweza kumtaka mshiriki wa darasa kueleza hadithi katika maneno yake mwenyewe . Ungeweza pia kuonesha video “He has Risen” (ChurchofJesusChrist .org) . Washiriki wa darasa wanaweza pia kufurahia kuimba nyimbo kuhusu Mwokozi na kusoma maandiko yanayohusiana (marejeleo yameorodheshwa chini ya kila wimbo katika Nyimbo za Kanisa) . Washiriki wa darasa kisha wangeshiriki vifungu wanavyovipenda kutoka kwenye nyimbo na hisia zao kuhusu Mwokozi .

• Kusaidia darasa lako kuwa na shukrani juu ya jinsi Agano la Kale linavyoshuhudia juu ya Yesu Kristo, ungeweza kuwaomba kurejea upya maandiko kwenye jedwali kwenye muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia, vilevile vifungu katika Kitabu cha Mormoni ambavyo vinafuatana na jedwali . Tunajifunza nini kuhusu Mwokozi na misheni yake kutoka katika vifungu hivi? Kwa nini ni muhimu kujua kuhusu utabiri huu?

Tunaweza kupata amani na furaha kupitia Upatanisho wa Mwokozi.• Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa

Ajili ya Watu Binafsi na Familia unajumuisha orodha ya maandiko yanayoelezea amani na furaha inayokuja kupitia Yesu Kristo . Kama washiriki wa darasa walisoma maandiko haya nyumbani, watie moyo kushiriki mawazo yao na hisia kuyahusu . Au mngeweza kusoma maandiko machache kama darasa na kuzungumza kuhusu amani na furaha tunayohisi kwa sababu ya mwokozi na Upatanisho Wake . Jinsi gani tunaweza kushiriki baraka hizi na watu ambao wanaweza kuwa wanapambana kupata amani na furaha katika maisha yao? Ungeweza pia kumwomba mshiriki wa darasa kusoma ujumbe wa Rais Russell M . Nelson “Joy and Spiritual Survival” (Liahona, Nov . 2016, 81–84) wakati wa wiki iliyotangulia darasa na kuja darasani

Kiel

elez

o ch

a ka

buri

tupu

na

mar

yna

Kriu

chen

ko

aPRili 11–17

32

akiwa amejiandaa kushiriki nini ujumbe huu unafundisha kuhusu kupata furaha kwa Mwokozi .

• Unaweza kujisikia kutiwa moyo kuongoza majadiliano kuhusu jinsi ya kuwasaidia wengine kupata amani na furaha katika Kristo . Ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kufikiria kuhusu mtu fulani wanayemjua—pengine mtu fulani wanayemhudumia—ambae pengine anahitaji msaada wao, huduma, au hata kusikia tu ushuhuda wao wa Kristo na Upatanisho Wake . Watie moyo washiriki wa darasa warejelee kwenye maandiko (kama vile yale katika “Nyenzo za Ziada”) wanapofikiria huduma wanayoweza kutoa au shuhuda wanazoweza kushiriki ili kuwaimarisha wale wanaowazunguka . Waombe washiriki wachache wa darasa kushiriki mawazo yao kuhusu kuhudumu kama Yesu alivyofanya .

Kupitia Upatanisho Wake, Yesu Kristo ana nguvu ya kutusaidia kushinda dhambi, kifo, majaribu na udhaifu.• Njia mojawapo ya kuwasaidia washiriki wa

darasa kutafakari baraka zinazokuja kupitia Upatanisho wa Mwokozi ingeweza kuwa kuandika vichwa vya habari ubaoni Dhambi, Kifo, Majaribu, na Udhaifu. Kila mshiriki wa darasa angeweza kusoma mojawapo ya maandiko yaliyoorodheshwa katika “Nyenzo za Ziada” na kutakafari jinsi Mwokozi anavyotusaidia kushinda vitu vilivyoandikwa ubaoni . Washiriki wa darasa wanaweza kuandika marejeleo ya maandiko yao chini ya moja au zaidi ya vichwa vya habari ubaoni na kushiriki ushuhuda wao wa Mwokozi na Upatanisho Wake .

• Hadithi na anolojia zinaweza kutusaidia kuelewa Upatanisho wa Kristo . Kwa mfano, ungeweza kumwomba mshiriki wa darasa kushiriki moja ya hadithi au analojia katika ujumbe wa Mzee Walter F . González “The Savior’s Touch” (Liahona, Nov . 2019, 90–92) au ujumbe wa Dada Neill F . Marriott “Abiding in God and Repairing the Breach” (Liahona, Nov . 2017, 10–12) . Ni nini

hadithi hizi na analojia zinatufundisha kuhusu Upatanisho wa Kristo? Waombe washiri wa darasa kufanya kazi katika jozi kufikiria juu ya hadithi au analojia zao wenyewe .

• Tunajifunza nini kutoka mistari ifuatayo kuhusu gharama ambayo Yesu Kristo alilipa kwa ajili ya wokovu wetu: Isaya 53:3–5; Mosia 3:7; Mafundisho na Maagano 19:16–19? Ni gharama gani Baba yetu wa Mbinguni alilipa? (Ona Yohana 3:16) .

Nyenzo za Ziada

Maandiko kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo• Isaya 61:1–3

• Ezekieli 36:26- 28 .

• Mathayo 11:28–30

• Luka 1:46–55

• Warumi 8:35–39

• Alma 7:10–13

• Alma 11:42–45

• Moroni 10:32–33

• Mafundisho na Maagano 19:15–19

• Musa 5:9–12

Kuboresha Ufundishaji WetuWashukuru wanafunzi wako. “Usizame sana kwenye somo kiasi cha kusahau kuwashukuru wanafunzi kwa michango yao. Wanahitaji kujua ya kwamba unathamini utayari wao wa kushiriki umaizi na shuhuda zao” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 33).

33

APRILI 18–24

Kutoka 18–20“YOTE AMBAYO BWANA AMEYASEMA TUTAYAFANYA”

Soma Kutoka 18–20, na andika misukumo unayopata kuhusu jinsi ya kuwasaidia washiriki wa darasa lako kujifunza kutoka kwenye sura hizi . Hata misukumo midogo inaweza kukuongoza kwenye uzoefu wa kujifunza wenye maana .

Alika Kushiriki

Kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki kile ambacho walijifunza, ungeweza kuandika ubaoni 18, 19 na 20—sura walizosoma katika Kutoka wiki hii . Waombe washiriki wa darasa kuandika, karibu na kila nambari ya sura namba za mistari ambayo wangependa kuijadili kutoka katika sura ile . Wakati washiriki wa darasa wanashiriki umaizi wao, waulize washiriki wengine wa darasa kama walikuwa na umaizi kuhusu vifungu sawa na hivyo .

Fundisha Mafundisho

KUTOKA 18:13–26

Tunaweza kusaidia “kubeba mzigo” wa kufanya kazi ya Mungu.• Ungeweza kuwatia moyo darasa lako

kujadili ushauri Yethro aliompa Musa (ona Kutoka 18:13–26) kwa kuwataka kufikiria kwamba wana mazungumzo na mtu fulani anayehisi kwamba miito yake ya Kanisani, wajibu wa familia, au majukumu mengine ni “mazito mno” na kwamba yeye “atadhoofika”

(Kutoka 18:18) . Jinsi gani ushauri katika Kutoka 18:13–26 utasaidia? Ni ushauri gani wa ziada tungeweza kushiriki kutokana na uzoefu wetu binafsi?

• Kuzungumza kuhusu Kutoka 18:13–26 kunaweza kutoa fursa ya kujadili jinsi kuhudumia kunavyoweza kutusaidia “kubeba mzigo pamoja na” viongozi wetu katika kazi ya Bwana (Kutoka 18:22) . Ni sifa gani ambazo Yethro alipendekeza kwa Musa kuzitafuta kwa hao ambao wangehudumu kama “watawala” wa watu? (Ona Kutoka 18:21) . Kwa nini sifa hizo ni muhimu katika juhudi zetu za kuhudumiana? Jinsi gani kuhudumia wanafamilia, waumuni wa Kanisa, na wengine kunasaidia “kubeba mzigo” wa viongozi wetu wa Kanisa? Kama sehemu ya majadiliano yenu, ungeweza kuonesha moja ya video zinazohusiana zinazopatikana kwenye Ministering .Churchof JesusChrist .org .

Kuhudumia wengine ni moja ya njia tunayoweza kushiriki katika kazi ya Bwana.

mlim

a nd

ani y

a m

isri

kim

apok

eo u

liam

inik

a ku

wa

mlim

a si

nai.

aPRili 18–24

34

KUTOKA 20:2–11.

Tunapaswa kumweka Bwana kwanza katika maisha yetu.• Unaweza kufikiria juu ya kazi ambayo inaenda

vyema wakati tunapokamilisha hatua za muhimu kwanza? (Mifano inaweza kujumuisha kufumbua mlinganyo wa hesabu au kufuata maelezo ya upishi) . Shiriki na darasa baadhi ya mifano unayoifahamu, na watake kufikiria yao wenyewe . Jinsi gani kukamilisha hatua muhimu kwanza kuna uhusiano na amri katika Kutoka 20:2–11? Ni nini amri zinatufundisha kuhusu kumweka Mungu kwanza katika maisha yetu? Ni vitu gani ambavyo tunaweza kujaribiwa kuviweka mbele Yake? (Kwa baadhi ya mifano, ona maelezo katika “Nyenzo za Ziada .”) Kurejea upya Kutoka 20:2–11 kunaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kufikiria juu ya msimamo wao wa kumweka Mungu kwanza .

KUTOKA 20:2–17.

Mungu ni mwenye rehema.• Jinsi gani utaweza kuwasaidia washiriki wa

darasa kuelewa umuhimu wa Amri Kumi katika wakati wetu? Ungeweza kuligawa darasa katika jozi na waombe kusoma Kutoka 20:2–17 na kisha mjadiliane jinsi kutii kila amri kunavyowabariki, familia zao, na watu wanaowazunguka . Pia ungeweza kuonesha video “Obedience of the Ten Commendments” (ChurchofJesusChrist .org) . Ni baraka gani Baba wa Mbinguni anatuahidi kwa kutii amri Zake? (Ona kwa mfano, Mosia 2:41) . Jinsi gani amri hizi zinaonesha upendo wa Mungu kwetu?

Nyenzo za ZiadaHakuna miungu wengine.Rais Spencer W . Kimball alifundisha kwamba kuna mliganisho kati ya kuabudu kwa kale kwa sanamu zilizochongwa na tabia za watu wa leo . Alisema:

“Kuabudu sanamu ni miongoni mwa dhambi mbaya mno .  .  .  .

“Sanamu za kisasa au miungu ya uongo inaweza kuwa kwa mfano kama vile nguo, nyumba, biashara, mashine, magari, boti za starehe, na vifaa vingine vingi ambavyo hutupotosha kutoka kwenye njia ya uungu .  .  .  .

“Vitu visivyoshikika vinafanya kama miungu iliyo tayari . Shahada na barua na vyeo vinaweza kuwa sanamu .  .  .  .

“Watu wengi wanajenga na kuweka samani nyumbani na kununua magari kwanza—na kisha wanaona ‘hawawezi’ kulipa zaka . Wanamwabudu nani? Kwa hakika sio Bwana wa mbingu na dunia .  .  .  .

“Wengi huabudu uwindaji, safari ya uvuvi, likizo, pikiniki za mwisho wa wiki na matembezi . Wengine wanazo kama sanamu zao michezo, baseball, soka, vita ya mafahali, au gofu .  .  .  .

“Bado sanamu nyingine ambayo watu huabudu ni ile ya nguvu na ufahari . .  .  . Miungu hawa wa uwezo, utajiri, na wenye mahitaji mno na ni halisi hasa kama ndama wa dhahabu wa wana wa Israeli nyikani” (Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Spencer W. Kimball [2006], 146–47) .

Kuboresha Ufundishaji WetuLenga kwenye kanuni chache. “Kuna mengi ya kujadili katika kila somo, lakini siyo lazima kushughulikia kila kitu katika kipindi kimoja cha darasa ili kugusa moyo wa mtu—mara nyingi kipengele kimoja au viwili muhimu huwa vinatosha” (Kufundisha Katika Njia ya Mwokozi, 7).

35

APRILI 25–MEI 1

Kutoka 24; 31–34“USO WANGU UTAKWENDA PAMOJA NA WEWE”

Acha maneno haya kutoka kwa Mzee Jeffrey R . Holland yaongoze maandalizi yako ya kufundisha: “Watu wengi hawaji kanisani kutafuta tu ukweli mpya wa injili . .  .  . Wanakuja wakitafuta uzoefu wa kiroho . .  .  . Wanataka imani yao iimarishwe na tumaini lao lifanywe upya” (“A Teacher Come from God,” Ensign, Mei 1998, 26) .

Alika Kushiriki

Washiriki wa darasa wangeweza kufikiria kwamba rafiki anasema, “Sisomi Agano la Kale; sioni kama lina muhimu kwa maisha yangu .” Waulize ili wajibu kwa kushiriki kitu ambacho wameona kina maana katika utafiti wao wa hivi karibuni wa Agano la Kale .

Fundisha Mafundisho

KUTOKA 31:12–17

Tunaiheshimu Sabato kama ishara ya msimamo wetu kwa Bwana.• Unaweza kuanza kwa kuwauliza washiriki

wa darasa ikiwa wamewahi kuelezea kwa mwanafamilia au rafiki kwa nini wao wanazichukulia Jumapili tofauti na siku zingine . Waalike washiriki kile walichosema au kile wanachoweza kusema baadaye . Kusoma Kutoka 31:12–17 au maelezo kwenye “Nyenzo za Ziada” yanaweza kuwapa mawazo ya ziada . Ni jinsi gani chaguzi zetu za siku ya Sabato zinaelezea msimamo wetu kwa Yesu Kristo?

• Hata hivyo adhabu iliyoelezewa katika Kutoka 31:14–15 hazitumiki leo, zinaonyesha jinsi Bwana anavyohisi kuhusu Sabato . Kwa nini amri hii ni muhimu sana? Kujadili maandiko haya kunaweza kusaidia: Kutoka 31:12–17; Isaya 58:13–14; Mafundisho na Maagano 59:9–13 .

Kwa kuiheshimu sabato, tunaonyesha upendo wetu kwa Bwana.

KUTOKA 32; 34:1–17

Dhambi humaanisha kuachana na Mungu, lakini Yeye hutoa njia ya kurudi.• Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari

na kuifanya hadithi kuwa yao katika Kutoka 32, kwanza waombe kila mmoja kupitia upya sura kibinafsi au katika vikundi . Kisha waombe washiriki wa darasa wachukue nafasi ya Waisraeli ambao walikua hawana subira wakimngojea Musa arudi na wakaamua kutengeneza sanamu ya dhahabu . Je, ni hisia gani ambazo ziliweza kuwaongoza kwenye kuabudu sanamu?

Kiel

elez

o ch

a Ye

hova

aki

mto

kea

mus

a na

w

azee

70

wa

isra

eli,

na Je

rry

har

ston

aPRili 25–mei 1

36

Washiriki wengine wa darasa wanaweza kujaribu kuwashawishi kubaki wakweli kwa Bwana na nabii Wake . Washiriki wa darasa wanaweza kuzungumza juu ya kile kinachowashawishi wao kushika maagano yao . Tunaweza kufanya nini ili kuwasaidia wale ambao wanaweza kusumbuka katika kushika maagano yao?

• Wakati watu wanaposoma Agano la Kale, wakati mwingine wanashangazwa na adhabu kali ambazo Bwana aliamuru kwa ajili ya dhambi . Kutoka 34:1–9 inaweza kuwasaidia kuona kwamba wakati Mungu hajali visingizio vyetu vya kutenda dhambi, Yeye pia ni mwenye huruma, akiwasamehe wale wanaotubu . Huenda washiriki wa darasa wangesoma kifungu hiki na kutafakari maswali kama haya: Je, tunajifunza nini kuhusu Bwana kutoka kwenye mistari hii? Kwa nini tunahitaji kujua vitu hivi kumhusu Yeye? Unaweza kusema kwamba Tafsiri ya Joseph Smith, Kutoka 34:7 (katika Kutoka 34:7, tanbihi e) inafafanua kwamba Mungu “hatawaondoa waasi .” Hii inaweza kumaanisha nini? Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki jinsi walivyoshuhudia rehema ya Mungu . Inawezekanaje kwa Mungu kuwa vyote mwenye rehema kamilifu na mwenye haki kamilifu? (ona Alama 42:13–15) .

• Kutoka 34: 6–17 inaweza kuonekana kama maelekezo ya kuwasaidia Waisraeli kutubu dhambi zao za kuabudu sanamu (iliyoelezewa katika Kutoka 32) . Tunapata nini katika mistari hii ambacho yawezekana kiliwasaidia Waisraeli kutubu? Je, tunajifunza nini kuhusu Bwana na toba kutokana na maelekezo haya?

KUTOKA 33:11–17

Tunahitaji uso wa Mungu katika maisha yetu.• Ni jinsi gani utawasaidia washiriki wa darasa

kuyafanyia kazi yale Bwana aliyoyasema kwa Musa katika Kutoka 33:11–17? Unaweza kuanza kwa kupitia upya kazi ambayo Mungu bado alihitaji Musa kuitekeleza (ona Kutoka 33:1–3) .

Ni nini tunakipata katika mstari wa 11–17 ambacho kingeweza kumuimarisha na kumfariji Musa? Washiriki wa darasa wanaweza kufikiria juu ya kitu ambacho Mungu anataka wafanye—kama vile kutimiza wito wa Kanisa, jukumu la familia, au fursa ya kutumikia . Kisha wangeweza kusoma tena mistari hiyo . Je, ni utambuzi gani tunaupata kuhusu jinsi Mungu atakavyotusaidia sisi?

Nyenzo za Ziada

Sabato ni ishara.Rais Russell M . Nelson anaelezea: “Katika miaka ya ujana wangu, nilijifunza kazi za wengine ambazo ziliorodhesha vitu vya kufanya na vya kutofanya katika Sabato . Haikuwa hadi baadaye ndipo nikajifunza kutoka katika maandiko kwamba mwenendo wangu na mtazamo wangu juu ya Sabato ilikuwa ishara kati yangu mimi na Baba yangu wa Mbinguni [ona Kutoka 31:13; Ezekieli 20:12, 20] . Kwa uelewa huo, sikuhitaji tena orodha ya vya kufanya na kutofanya . Nilipohitaji kufanya maamuzi ya kujua kama shughuli ilikuwa au haikuwa sahihi kwa ajili ya Sabato, nilijiuliza mwenyewe, ‘Ni ishara gani ninataka kumwonyesha Mungu?’ Swali hilo lilifanya uchaguzi wangu kuhusu siku ya Sabato kuwa dhahiri zaidi” (“The Sabbath Is a Delight,” Liahona, Mei 2015, 130) .

Kuboresha Ufundishaji WetuFundisha kupitia Roho. “lengo kuu la kila kitu anachofanya mwalimu wa injili—kila swali, kila kifungu cha maandiko, kila shughuli—ni kumualika Roho mtakatifu ajenge imani na kuwaalika wote kuja kwa Kristo” (Kufundisha katika Njia ya Bwana, 10).

37

MEI 2–8

Kutoka 35–40; Mambo ya Walawi 1; 16; 19“UTUKUFU KWA BWANA”

Unapokuwa na uzoefu wa maana kwa kusoma maandiko, utaweza kufundisha na kushuhudia unapokutana na washiriki wa darasa siku ya Jumapili . Unaweza kufanya nini ili kuwahamasisha washiriki wa darasa kufanya vivyo hivyo?

Alika Kushiriki

Sura za usomaji wa juma hili hutumia alama kufundisha juu ya Yesu Kristo na dhabihu Yake ya kulipia dhambi . Unaweza kuanza darasa kwa kuwaalika washiriki wa darasa kuandika au kuchora ubaoni kitu walichopata katika Kutoka 35–40 au Mambo ya Walawi 1; 16; 19 ambayo yaliwafundisha kuhusu Mwokozi . Waalike waelezee kuhusu kile walichojifunza .

Fundisha Mafundisho

KUTOKA 35–40

Bwana anatutaka sisi tuwe watakatifu kama Yeye alivyo.• Wakati washiriki wa darasa walipojifunza

Kutoka 35–40 wiki hii, wanaweza kuwa walitafakari jinsi vitu vya maskani ya kale vinavyogeuza mawazo yao kwa Yesu Kristo . Kama walifanya, wahimize washiriki mawazo yao . Jedwali katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia lingeweza kusaidia kwenye majadiliano haya .

Ungeweza pia kuzungumza juu ya kile alama hizi zinazohusiana na maskani zinafundisha juu ya kuwa watakatifu zaidi . Ni kwa jinsi gani Yesu Kristo hutusaidia sisi kuwa watakatifu zaidi?

• Kwa wengi, wazo la kuwa watakatifu zaidi linaweza kuonekana kuwa haliwezi kufikiwa . Je, utawasaidiaje washiriki wa darasa kuelewa kwamba kuwa watakatifu ni sehemu ya mpango wa Baba wa Mbinguni kwetu? Mnaweza kusoma pamoja maelezo ya Rais Henry B . Eyring katika “Nyenzo za Zaida .” Inamaanisha nini kuwa mtakatifu? Ni jinsi gani mahekalu ya siku za mwisho na kazi tunazozifanya humo zinatusaidia kuwa watakatifu zaidi? (ona pia Mafundisho na Maagano 84:19–24; 109:6–26; 128:15–18) . Kisha ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki jinsi vitu hivi vilivyowasaidia—au wengine wanaowajua—kuwa watakatifu zaidi .

• Nyumba ya Bwana ya Waisraeli jangwani ni sawa kwa njia nyingi na mahekalu yetu ya siku za mwisho . Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kuorodhesha vitu walivyojifunza kuhusu nyumba ya Bwana katika Kutoka 35–40 ambavyo vinawakumbusha yale tunayoyapitia katika hekalu . Kama wanahitaji msaada, ungeweza kuwaelekeza kwenye mistari katika Mwanzo 40 ikirejelea pazia, madhabahu, mavazi matakatifu, kuoshwa, na upako . Ni kwa jinsi gani hekalu linatusaidia kuja kwa Kristo? Tunaweza kufanya nini ili kufokasi muda wetu juu Yake tuwapo hekaluni?

mei 2–8

38

MAMBO YA WALAWI 1:1–9; 16

Kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, tunaweza kusamehewa.• Ingawa wazo la dhabihu ya wanyama linaweza

kuonekana geni kwetu leo, kuna mengi tunayoweza kujifunza kutokana na desturi hizi kuhusu dhabihu ya Yesu Kristo ya kulipia dhambi . Ili kuanza majadiliano, unaweza kuonyesha picha za Mwokozi akiwa Gethsemane na msalabani (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na .56, 57) . Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki maneno ambayo wanaona yanahusiana na dhabihu ya Yesu Kristo ya kulipia dhambi . Kisha alika washiriki wa darasa kupitia Mambo ya Walawi 1:1–9 au Mambo ya Walawi 16, ambayo inaelezea dhabihu za wanyama, na kupata maneno ambayo wanahisi pia yanahusiana na dhabihu ya Mwokozi . Ni kwa jinsi gani dhabihu hizi za zamani zinaweza kutusaidia kuelewa vyema Upatanisho wa Yesu Kristo? Washiriki wa darasa wanaweza kuimba wimbo kuhusu Mwokozi na kushiriki hisia zao kuhusu Yeye .

Wana wa israeli walitoa matoleo kwa ajili ya nyumba ya Bwana kwa “moyo wa kupenda” (Kutoka 35:5). Kielelezo na corbert Gauthier, © lifeway collection/licensed from goodsalt.com

• Inaweza kuwa yenye msaada kwa washiriki wa darasa kulinganisha dhabihu ya Bwana iliyotakiwa katika kipindi cha Agano la Kale na dhabihu Anayoitaka kwetu leo . Kwa mfano, wangeorodhesha njia tunazotoa dhabihu kwa Bwana na kazi Yake, kama vile kuhudumu katika wito, kulipa matoleo ya mfungo, kufanya kazi ya historia ya familia, au kutumikiana . Kisha mnaweza kusoma pamoja Mambo ya Walawi 1:1–9 na uwaalike washiriki wa darasa

kutafuta vitu vya matoleo viliyoelezewa katika mistari hii ambavyo vinaweza kuhusiana na matoleo ambayo Bwana anatuomba tutoe leo (ona 3 Nefi 9:19–20; Mafundisho na Maagano 64:34) . Tunaweza kujifunza nini kutoka Musa 5:7 kuhusu jinsi tunavyopaswa kuona dhabihu zetu kwa ajili ya kazi ya Bwana?

Nyenzo za Ziada

Mungu anaweza kutufanya kuwa watakatifu.Rais Henry B . Eyring alifundisha:

Furaha kuu huja kutokana na utakatifu mkuu wa mtu binafsi .  .  .  . Maandiko yanatufundisha kwamba miongoni mwa vitu vingine, tunaweza kutakaswa au kuwa watakatifu zaidi wakati tunapoonesha imani katika Kristo, kuonesha utiifu wetu, kutubu, kutoa dhabihu kwa ajili Yake, kupokea ibada takatifu, na kushika maagano yetu tuliyoweka Naye .  .  .  .

“Wimbo ‘More Holiness Give Me’ [Nyimbo za Kanisa, na . 131] unapendekeza njia ya kusali kwa ajili ya msaada wa kuwa watakatifu zaidi . Mwandishi kwa busara anapendekeza kuwa utakatifu tunaotafuta ni zawadi kutoka kwa Mungu mwenye upendo, itolewayo baada ya muda fulani, baada ya kufanya yote tunayoweza” (“Utakatifu na Mpango wa Furaha,” Liahona, Nov . 2019, 100–101, 103) .

Kuboresha Ufundishaji WetuTumia muziki mtakatifu. Ujumbe ulioko katika nyimbo unaweza kuimarisha mafundisho katika maandiko. Kwa mfano, kuimba wimbo kama “more holiness give me” au “I Stand all amazed” (Nyimbo za Kanisa, na. 131, 193) kunaweza kuimarisha ujumbe uliofundishwa katika mambo ya Walawi 16 na 19.

39

MEI 9–15

Hesabu 11–14; 20–24“MSIMWASI BWANA, WALA MSIOGOPE”

Moja ya njia bora ya kujua nini cha kuzingatia wakati wa darasa ni kuwauliza washiriki wa darasa kile walichoona cha maana walipojifunza maandiko . Hii itafunua kile ambacho ni muhimu kwao na nini wako tayari kujifunza .

Alika Kushiriki

Wakati mwingine kinachohitajika kuwahimiza washiriki wa darasa kushiriki utambuzi waliopata kutoka kwenye masomo yao ni kuuliza swali rahisi kama “Roho Mtakatifu alikufundisha nini uliposoma maandiko wiki hii?” Kisha wape muda kutafakari na kujibu .

Fundisha Mafundisho

HESABU 12

Kusema mabaya dhidi ya nabii wa Bwana humkosea Bwana.• Kusoma Hesabu 12 kunaweza kusaidia washiriki

wa darasa kuelewa uzito wa kusema mabaya dhidi ya nabii wa Bwana . Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kusoma sura hii na kuongea kuhusu ni jinsi gani Bwana anajisikia kuhusu watumishi Wake . Kulingana na mstari wa 1–2, unafikiri inamaanisha nini kusema dhidi ya nabii wa Bwana? Nini hatari ya kufanya hivyo? Je, tunaweza kujifunza nini kutokana na matendo ya Musa kwa Waisraeli katika mstari wa 13 na 15?

HESABU 12:3.

“Musa alikuwa mpole sana.”• Watu wengine wanaweza kushangaa kusoma

kwamba kiongozi aliye hodari kama Musa, ambaye alisimama mbele ya Farao na kufanya miujiza ya kushangaza kwa nguvu za Bwana, pia alikuwa “mpole sana .” Ungeweza kutumia Hesabu 12:3 kuanzisha mjadala kuhusu upole wa kweli ni nini . Ungeweza kurejelea ufafanuzi katika “Mpole, Upole” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures .ChurchofJesusChrist .org) . Kama darasa, ungeweza pia kutafuta viashiria vya upole wa Musa katika Hesabu 12 .

• Ni ushahidi gani mwingine wa upole wa Musa tunaweza kujifunza? (ona, kwa mfano, Kutoka 18:13–25; Hesabu 11:26–29; Waebrania 11:24–27; Musa 1:10–11) . Unaweza pia kusoma na kujadili jinsi Mwokozi alivyoonyesha upole (ona Mathayo 11:29; 27:11–14; Luka 22:41–42; Yohana 13:4–5) . Mifano ya Musa na Mwokozi—au watu tunaowajua—inatufundisha nini kuhusu upole? Kwa nini Mungu anataka tuwe wapole?

HESABU 13–14.

Kwa imani katika Bwana, tunaweza kuwa na matumaini kwa ajili ya siku zijazo.• Unapojadili hadithi kuhusu Waisraeli

12 walioipeleleza nchi ya ahadi na kutoa ripoti yao, fikiria kuwauliza washiriki wa darasa jinsi

mei 9–15

40

wanahisi hadithi hii inaweza kutumika kwa hali wanazokabiliana nazo . Kwa kusaidia, ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kuorodhesha vitu kutoka Hesabu 13:23–33 ambavyo vinaweza kufananishwa na kitu fulani katika maisha yetu . Kwa mfano, nchi ya ahadi inaweza kuwakilisha kitu ambacho Bwana anataka tufanikishe, nguzo za zabibu zinaweza kuwa baraka, majitu yanaweza kuwa changamoto tutakazokabiliana nazo, na kadhalika . Watie moyo washiriki wa darasa kushiriki kile wanachohisi Bwana anaweza kutaka wajifunze kutokana na hadithi hii .

wapelelezi kumi wa Israeli waliogopa; Yoshua na Kalebu walikuwa na imani. © lifeway collection/licensed from goodsalt.com

HESABU 21:4–9

Kama tunamtazama Yesu Kristo kwa imani, Yeye anaweza kutuponya kiroho.• Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujadili

hadithi katika Hesabu 21:4–9 na kujenga imani yao katika Mwokozi, unaweza kuandika maswali kama haya ubaoni: Je, nyoka wa shaba anawakilisha nini? Je, kuumwa na nyoka kunaweza kuwakilisha nini? Kwa nini watu wengine walikataa kumtazama yule nyoka wa shaba? Tunawezaje “kumuangalia” leo? Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki majibu wanayoyapata wanaposoma Hesabu 21:4–9; 1 Nefi 17:40–41; Alma 33:18–22; na Helamani 8:13–15 . Ni baadhi ya mambo gani rahisi Mwokozi anatualika kufanya ili kupokea uponyaji Wake? Kwa nini wakati mwingine ni vigumu kufanya vitu hivyo rahisi? (ona “Nyenzo za Ziada” kwa

maoni kadhaa juu ya hili) . Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki ni kwa jinsi gani kufanya mambo haya kumeleta nguvu ya Bwana katika maisha yao .

Nyenzo za Ziada

“Vitu vidogo na rahisi.”Mzee L . Whitney Clayton alielezea juu ya askofu ambaye aliwashauri washiriki wa kata wanaokabiliwa na changamoto mbali mbali ngumu katika maisha yao:

“Ushauri wake kwa washiriki wa kata mara nyingi ulijumuisha kurudi kwenye mazoea rahisi ya imani, kama vile kusoma Kitabu cha Mormon[,] .  .  . kulipa zaka, na kuhudumu katika Kanisa kwa moyo wa dhati . Mara kwa mara, hata hivyo, majibu yao kwake yalikuwa ya kutiliwa shaka: ‘ .  .  . Je, kufanya yoyote kati ya mambo hayo kuna uhusiano gani na maswala ambayo ninakabiliana nayo?

“ .  .  . Wale ambao hufikiria sana juu ya kufanya ‘vitu vidogo na rahisi’ [Alma 37:6]—wakitii katika njia zinazoonekana kuwa ndogo—wanabarikiwa kwa imani na nguvu ambazo zinaenda mbali na matendo halisi ya utii wao wenyewe na, kwa kweli, njia hizi zinaweza kuonekana kabisa hazihusiani na maswala tunyokabiliana nayo” (“Lolote Atakalosema Kwenu, Fanyeni,” Liahona, Mei 2017, 98) .

Kuboresha Ufundishaji WetuZingatia kile kilicho muhimu zaidi. haiwezekani kuelezea kila hadithi au kila kanuni. mfuate Roho, na uzingatie mahitaji ya washiriki wa darasa unapoamua jinsi ya kutumia muda wa darasa. Kumbuka kwamba nyumbani, siyo darasani, ni kitovu cha kujifunza injili.

41

MEI 16–22

Kumbukumbu la Torati 6–8; 15; 18; 29–30; 34“JIHADHARI USIJE UKAMSAHAU BWANA”

Musa aliongozwa kiungu ili kuwafundisha watoto wa Israeli kulingana na mahitaji yao (ona Kumbukumbu la Torati 6:1) . Unapojifunza Kumbukumbu la Torati, tafuta mwongozo wa kiungu wa kujua ni kanuni gani za kufundisha, kulingana na mahitaji ya washiriki wa darasa .

Alika Kushiriki

Kwa sababu Kumbukumbu la Torati lina maneno ya mwisho ya Musa kwa wana wa Israeli, unaweza kualika washiriki wa darasa kushiriki kitu walichopata katika Kumbukumbu la Torati ambacho wangependa kukiingiza katika maneno yao ya mwisho kwa watoto wao au wajukuu . Wakiwa wanashiriki, waombe kuelezea kwa nini walichagua maneno hayo .

Fundisha Mafundisho

KUMBUKUMBU LA TORATI 6:4–7, 20–25; 8:2–5, 11–17; 29:18–20; 30:6–10, 15–20

Bwana anatutaka tumpende Yeye kwa mioyo yetu yote.• Katika Kumbukumbu la Torati, kuna vifungu

ambavyo vinaweza kutusukuma kufikiria juu ya hali ya kiroho ya mioyo yetu . Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kushiriki mawazo yao kuhusu vifungu hivi, ungeweza kuchora moyo ubaoni . Kisha yagawanye maandiko yafuatayo miongoni mwa washiriki wa darasa: Kumbukumbu la Torati 6:4–7, 20–25; 8:2–5, 11–17; 29:18–20;

30:6–10, 15–20 . Waalike washiriki wa darasa kuandika rejeleo ndani ya moyo ikiwa inafundisha juu ya kitu ambacho tunapaswa kuwa nacho mioyoni mwetu au kuandika rejeleo nje ya moyo ikiwa inafundisha jambo ambalo tunapaswa kuepuka . Inamaanisha nini kujitoa kwa mioyo yetu yote kwa Baba wa Mbinguni?

• Je, tunaelezeaje familia yetu na wengine kwa nini tunatii amri za Mungu? Baada ya kutafakari swali hili, washiriki wa darasa wangesoma Kumbukumbu la Torati 6:4–7, 20–25 au maelezo katika “Nyenzo za Ziada” na kushiriki mawazo yao . Ni jinsi gani utambuzi huu unavyogusa jinsi sisi tunavyojisikia kuhusu amri au maagano?

KUMBUKUMBU LA TORATI 6:4–9, 20–25

“Fundisha [maneno ya Bwana] kwa bidii kwa watoto wako.”• Wakati mwingine inasaidia kusikia maoni

juu ya njia ambazo wengine wanafundisha na kujifunza injili katika nyumba zao . Kujadili jinsi washiriki wa darasa wanavyofuata ushauri katika Kumbukumbu la Torati 6:4–9, 20–25 inaweza kuwapa darasa lako nafasi ya kujifunza kutoka kwa kila mmoja . Tunafanya nini ili kufundisha na “kuzungumza juu ya” (mstari wa 7) neno la Mungu kama mistari hii inavyoelezea? Ni uzoefu gani tunaweza kushiriki ambao Bwana alituongoza katika juhudi zetu?

Kiel

elez

o ch

a m

usa

juu

ya m

lima

Neb

o,

© p

rovi

denc

e Co

llect

ion/

licen

sed

kuto

ka

good

salt.

com

mei 16–22

42

KUMBUKUMBU LA TORATI 15:1–15

Kusaidia wenye shida kunahusisha mikono ya ukarimu na mioyo iliyo tayari.• Bado hatujafika katika siku “ambayo

hakutakuwa na maskini kati yenu” (Kumbukumbu la Torati 15:4), kwa hivyo kanuni kuhusu kuwasaidia maskini katika Kumbukumbu la Torati 15 bado ni muhimu, hata kama mazoea fulani kuhusu madeni na watumishi yamebadilika . Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kurejea upya Mistari ya 1–15 na kutafuta kanuni kuhusu kuwasaidia maskini na wenye shida ambao wangependa kujadili . Maswali kama haya yanaweza kusaidia majadiliano: Inamaanisha nini “kufungua mkono wako wazi” kwa wale walio na shida? (mstari wa 8, 11) . Je, moyo wetu una nafasi gani katika kuwasaidia wengine? (ona mstari wa 7, 9–10) . Tunaweza kujifunza nini kuhusu kuwasaidia wenye shida kutokana na mfano wa Bwana? (ona mstari 15) .

KUMBUKUMBU LA TORATI 29:9; 30:15–20

Bwana anatualika kuchagua kati ya “maisha na mema, na kifo na uovu.”• Inaweza kufurahisha kulinganisha maneno

ya Musa katika Kumbukumbu la Torati na mafundisho ya mwisho ya Lehi na familia yake katika 2 Nefi 1–4 . Labda washiriki wa darasa wangeweza kutafuta mifanano na tofauti kati ya vifungu hivi: Kumbukumbu la Torati 29:9 na 2 Nefi 4:4; Kumbukumbu la Torati 30:15–20 na 2 Nefi 2:26–29 . Je, Lehi alipanua vipi yale yaliyofundishwa na Musa? Kwa nini maneno kama maisha na kifo ni njia nzuri ya kuelezea uchaguzi wetu wa “kushika” au “kugeuka” kutoka kwenye amri za Mungu? (Kumbukumbu la Torati 30:16–17) . Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki kile wanachokipata katika vifungu hivi ambacho kinawashawishi “kuchagua maisha” (Kumbukumbu la Torati 30:19) .

Nyenzo za Ziada

Tunashika maagano yetu kwa sababu tunampenda Mungu.Rais Linda K . Burton alifundisha:

“Juu ya sababu zote tunazopaswa kuwa na bidii zaidi katika kushika agano letu, sababu hii ni ya kuvutia sana kuliko zote—upendo .  .  .  .

“‘Ikiwa tunathamini kikamilifu baraka nyingi ambazo ni zetu kupitia ukombozi uliofanywa kwa ajili yetu, hakuna kitu ambacho Bwana angetaka kutoka kwetu ambacho hatungefanya kwa shauku na kwa hiari’ [ Joseph Fielding Smith, “Importance of the Sacrament Meeting,” Relief Society Magazine, Oct . 1943, 592] . Kulingana na maelezo haya ya Rais Joseph Fielding Smith, kushika agano ni njia mojawapo ya kuonyesha upendo wetu kwa Upatanisho usioweza eleweka, usio na mwisho wa Mwokozi na Mkombozi wetu na upendo mkamilifu wa Baba yetu wa Mbinguni” (“The Power, Joy, and Love of Covenant Keeping,” Liahona, Nov . 2013, 114) .

Kuboresha Ufundishaji WetuSikiliza. “Kusikiliza ni tendo la upendo. . . . muombe Baba wa mbinguni akusaidie kuelewa kile washiriki wa darasa lako wanachosema. Unapotoa usikivu wa umakini kwa ujumbe wao unaozungumzwa na usiozungumzwa, utakuja kuelewa vyema mahitaji yao, mashaka yao, na matamanio yao” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 34).

43

MEI 23–29

Yoshua 1–8; 23–24“UWE HODARI NA MOYO WA USHUJAA”

Unaposoma Yoshua 1–8 na 23–24, fikiria ushauri wa “tafakari humo mchana na usiku” (Yoshua 1:8) . Zingatia mawazo yanayokujia . Haya yanaweza kukuongoza kwenye mawazo ya kufundishia kwa ajili ya darasa lako .

Alika Kushiriki

Waalike washiriki wa darasa kushiriki kifungu kutoka kwenye kusoma kwao wiki hii ambacho kiliongeza imani yao katika Yesu Kristo . Kwa mfano, yawezekana walitafakari njia ambazo misheni ya Yoshua ilivyowakumbusha juu ya misheni ya Yesu Kristo . Kwa nini tunashukuru kwa ajili ya hadithi zilizoko katika kitabu cha Yoshua?

Fundisha Mafundisho

YOSHUA 1:1–9

“Uwe hodari na Moyo wa Ushujaa.”• Yoshua aliambiwa, “Uwe Hodari na Moyo wa

Ushujaa” mara kadhaa (ona Kumbukumbu la Torati 31:7, 23; Yoshua 1:6–7, 9) . Labda washiriki wa darasa wangenufaika kwa kujadili kile ambacho Bwana anamaanisha kwenye kifungu hiki . Wangeweza kuchunguza Yoshua 1:1–9 kwa ajili ya ushauri ambao Bwana alimpa Yoshua ili kumsaidia kuwa hodari na jasiri . Wanaweza pia kushiriki mifano ya watu wanaowajua ambao wana tabia hizi . Je, Yoshua alionyeshaje nguvu na ujasiri

katika masimulizi yanayopatikana katika kitabu cha Yoshua? (kwa mfano, ona sura ya 3, 6, na 8) . Washiriki wa darasa wangeweza kuelezea jinsi wao wanavyojaribu kuwa hodari na shujaa kwa ajili ya Kristo .

YOSHUA 1:8

Neno la Mungu linaweza kuifanya njia yetu iwe yenye mafanikio.• Ili kuwatia moyo washiriki wa darasa katika

masomo yao binafsi ya maandiko na ya familia, unaweza kusoma Yoshua 1:8 kama darasa . Tunaweza kujifunza nini kutoka kwenye mstari huu kuhusu jinsi ya kujifunza maandiko? Pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki kile wanachokifanya ili “kutafakari” katika maandiko “mchana na usiku .” Je, Bwana amefanyaje “njia yetu kuwa yenye mafanikio” na kutupatia “mafanikio mema” tunapojifunza neno Lake?

Neno la mungu linaweza “kuifanya njia [yetu] iwe yenye mafanikio” (Yoshua 1:8).

Kiel

elez

o ch

a m

usa

akim

taw

aza

Yosh

ua, n

a D

arre

ll Th

omas

mei 23–29

44

YOSHUA 3–4

Tunaweza kushuhudia “maajabu” ya Mungu.• Labda washiriki wa darasa wangenufaika

na hadithi fupi ya Waisraeli wakivuka Mto Yordani . Unaweza kugawanya darasa katika jozi na kualika kila jozi kusimuliana hadithi hii, wakipeana zamu ya kusema sentensi moja kwa wakati (wahimize waangalie katika Youshua 3 ikiwa wanahitaji msaada wa kukumbuka hadithi hiyo) . Kisha, kama darasa, wangeweza kujadili maelezo yoyote ambayo yana maana kwao . Je, tunajifunza nini kutoka kwenye hadithi hii ambacho kinaweza kutusaidia kupata uzoefu wa “maajabu” ya Bwana katika maisha yetu? (verse 5) . Ni “maajabu” gani aliyoyafanya kwa ajili yetu? Kwa nini ni muhimu kwamba kila kizazi kina tukio la kiroho ambalo linawafundisha wao kwamba “Bwana .  .  . ni mwenye nguvu”? (Yoshua 4:24) .

• Ingawa sisi sote tunahitaji kuwa na uzoefu wetu wenyewe wenye kujenga imani, kukumbuka kile ambacho Bwana amewafanyia mababu zetu pia ni muhimu . Kulingana na Yoshua 4, Waisraeli walifanya nini ili kuvisaidia vizazi vijavyo kukumbuka uvukaji wa Mto Yordani? (ona Yoshua 4:1–7) . Je, sisi tunafanya nini kuhakikisha kwamba uzoefu wetu hausahauliki na vizazi vijavyo?

YOSHUA 6–8

Utii huleta nguvu ya Mungu katika maisha yangu.• Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa

Ajili ya Watu Binafsi na Familia inapendekeza kulinganisha vita vya Waisraeli dhidi ya Wakanaani katika Yoshua 6–8 pamoja na vita vyetu binafsi dhidi ya majaribu . Ungeweza kuwauliza washiriki wa darasa ni mawazo au hisia gani walizokuwa nazo wakati walipokuwa wakisoma sura hizi na wazo hili la mlingano

katika akili . Au unaweza kuonyesha mistari maalum ambayo inaonekana kuendana na vita vyetu ili kuepuka dhambi, na wangeweza kuzungumza juu ya kile mistari hiyo inafundisha juu ya kupata kuufikia uwezo wa Mungu katika maisha yetu . Baadhi ya mistari hii inaweza kujumuisha Yoshua 6:1–5, 18, 20; 7:11–13 .

YOSHUA 23–24

“Chagueni hivi leo mtakayemtumikia.”• Labda ingewasaidia washiriki wa darasa

kutumia Yoshua 23–24 kwao wao wenyewe ikiwa watafikiria kuwa wao walikuwa Waisraeli wakimsikia Yoshua akitoa ushauri huu mwishoni mwa maisha yake . Unaweza kuwapa mistari michache kusoma kimya kimya na kisha uwaombe washiriki kitu kutoka kwenye mistari hiyo ambacho kingewahamasisha kubaki waaminifu kwa Bwana . Wanaweza pia kushiriki jinsi walivyofanya maamuzi binafsi kuhusu “nani watamtumikia” (Yoshua 24:15) . Kwa nini walifanya maamuzi haya?

• Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kuchagua kifungu kutoka Yoshua 23–24 ambacho kinawahamasisha kuchagua kumtumikia Mungu na kisha kuunda bango au kumbukumbu yenye kifungu hiki cha maneno ili kuonyesha nyumbani au kwenye mitandao ya kijamii .

Kuboresha Ufundishaji WetuUkuaji wa kiroho hutokea nyumbani. washiriki wa darasa lako wanahitaji kuwa na uzoefu wao wenyewe wa kiroho nje ya darasa ili kubaki kuwa wa kiroho zaidi. Tafuta njia za kutumia muda mfupi ulio nao kuwahamasisha kupata chakula cha kiroho katika maandiko nyumbani—binafsi na pamoja na familia zao. (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 18.)

45

MEI 30–JUNI 5

Waamuzi 2–4; 6–8; 13–16“BWANA AKAWAINULIA MWOKOZI”

Kumbuka kwamba mwalimu muhimu zaidi ni Roho Mtakatifu . Unawezaje kuwasaidia washiriki wa darasa kufundishwa na Roho Mtakatifu ukiwa unajadili kweli kutoka kwenye kitabu cha Waamuzi?

Alika Kushiriki

Andika ubaoni majina ya baadhi ya waamuzi wanaopatikana katika Waamuzi 2–4; 6–8; 13–16 (kama vile Debora, Baraka, Gideoni, na Samson) . Wape washiriki wa darasa dakika chache kurejelea sura hizi na kuandika chini ya jina moja ubaoni ukweli waliojifunza kutokana na uzoefu wa mtu huyo .

Fundisha Mafundisho

WAAMUZI 2:11–19; 3:5–12; 4:1–16

Bwana hutoa ukombozi tunapopotoka.• Kuchunguza mzunguko wa Israeli wa uasi,

huzuni, toba, na ukombozi kunaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kutambua nguvu ya Mungu ya ukombozi katika maisha yao wenyewe . Washiriki wa darasa wangeweza kufanya kazi katika vikundi vidogo ili kutafuta mzunguko ulioelezewa katika Waamuzi 2:11–19; 3:5–12 . Je, wana wa Israeli waliokolewaje kutoka kwenye mzunguko wao wa dhambi na mateso?

Tunajifunza nini kutokana na kitabu cha Waamuzi kuhusu jinsi tunavyoweza kuepuka dhambi na mateso? Ni zipi baadhi ya njia ambazo kwazo Mungu hutukomboa sisi? Pia unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kutafuta na kushiriki maandiko ambayo yanamshuhudia Bwana kama Mwokozi na Mkombozi wetu (kwa mfano, 2 Samueli 22:1–3; Zaburi 40:16–17; 1 Nefi 1:19–20; Mosia 23:21–23; Mafundisho na Maagano 138:23) .

• Waamuzi 2:19 inarekodi kwamba Waisraeli mara kwa mara walimwacha Mungu na kugeukia sanamu . Labda washiriki wa darasa wangeweza kufupisha mstari huu kwa njia ya onyo kwao . Ni katika njia zipi sisi wakati mwingine “tunasujudu” kwa “miungu wengine”? Ni kwa jinsi gani Mungu anaweza kutusaidia kubadili “njia yetu ya ukaidi”?

• Ili kuanza majadiliano juu ya jinsi Debora na Baraka walivyoikomboa Israeli kutoka kwa Wakanaani, unaweza kumuuliza mshiriki wa darasa kufupisha hadithi kwa darasa (inaweza kusaidia kuwasiliana na mshiriki huyo wa darasa siku chache kabla ili aweze kujiandaa) . Darasa linaweza kuongelea kuhusu sifa alizokuwa nazo Debora ambazo zinawavutia . Je, ni jinsi gani Debora aliwashawishi wana wa Israeli kumfuata Bwana? Labda unaweza kusoma pamoja Waamuzi 4:14 na kujadili

Kiel

elez

o ch

a d

ebor

a ak

iyao

ngoz

a m

ajes

hi

ya Is

rael

i, ©

pro

vide

nce

Colle

ctio

n/lic

ense

d ku

toka

goo

dsal

t.com

mei 30 –Juni 5

46

maana ya tamko la uaminifu la Debora: “Je, Bwana hakutoka atangulie mbele yako?” Je, ni namna gani Bwana huenda mbele yetu? (Ona pia Mafundisho na Maagano 84:87–88) .

WAAMUZI 6- 8

Bwana anaweza kufanya miujiza tunapoamini katika njia Zake.• Kujifunza wito wa Gideoni wa kuhudumu

kunaweza kuwahamasisha washiriki wa darasa katika huduma yao wenyewe . Unaweza kuwaomba kusoma na kujadili Waamuzi 6:11–16 . Tunajifunza nini kutoka kwenye uzoefu huu? Ili kuwasaidia kujifunza kutoka Waamuzi 7, unaweza kualika mshiriki mmoja au zaidi wa darasa kujifanya kuwa wanajeshi wa Gideoni na kusimulia hadithi kutokana na mtazamo wa wanajeshi hao . Washiriki wengine wa darasa wanaweza kuwauliza maswali kuhusu uzoefu wa wanajeshi hawa . Je, ni mifanano gani tunaiona kati ya hadithi hii na kile kinachotokea katika maisha yetu? Je, tunajifunza nini kuhusu Bwana kutoka kwenye hadithi hii?

WAAMUZI 13–16

Nguvu huja kutokana na uaminifu kwa maagano yetu na Mungu.• Utawasaidia vipi washiriki wa darasa kugundua

vyote ukweli wenye kutia moyo na maonyo muhimu kutoka katika hadithi ya Samsoni? Njia mojawapo inaweza kuwa kuwaalika nusu ya darasa kupitia Waamuzi 14–16 wakitafuta mistari inayoonyesha kuwa Bwana alikuwa na Samsoni . Nusu nyingine inaweza kutafuta mistari inayoonyesha kwamba Samsoni hakuwa na msimamo mkamilifu kwa Bwana . Waombe washiriki wa darasa kuelezea kile walichokipata . Maisha ya Samson yanatufundisha nini sisi kuhusu kutii maagano tunayofanya na Mungu? Maelezo na Dada Ann M . Dibb katika “Nyenzo za Ziada” yanaweza kusaidia .

Samson Anaangusha Nguzo Chini na james tissot na wengine

Nyenzo za ZiadaSomo kutokana na maisha ya Samson.Dada Ann M . Dibb alifundisha: “Samsoni alizaliwa na uwezekano mkubwa wa kuwa mtu muhimu . Mama yake aliahidiwa, ‘Yeye ataanza kuwakomboa Israeli kutoka katika mikono ya Wafilisti’ [Waamuzi 13:5] . Lakini Samsoni alipokua, aliangalia zaidi majaribu ya ulimwengu kuliko mwelekeo wa Mungu . Alifanya chaguzi kwa sababu ‘zilimpendeza [yeye] vizuri’ [Waamuzi 14:3] badala ya kwamba chaguzi hizo zilikuwa sahihi . Kwa kujirudia, maandiko hutumia kifungu cha maneno kisemacho ‘basi akateremka’ [Waamuzi 14:7] wanaposimulia safari, matendo, na chaguzi za Samsoni . Badala ya kuinuka na kung’aa ili kutimiza uwezekano wake wa kuwa mtu muhimu, Samsoni alishindwa na ulimwengu, akapoteza nguvu aliyopewa na Mungu, na akafa kifo cha kutisha, kifo cha mapema” (“Arise and Shine Forth,” Liahona, Mei 2012, 118) .

Kuboresha Ufundishaji WetuTenga muda kwa ajili ya wanafunzi kushiriki. “wakati wanafunzi wanapoelezea kile wanachojifunza, hawahisi tu Roho na kuimarisha shuhuda zao pekee, bali pia wanawahimiza washiriki wengine wa darasa kugundua ukweli wao wenyewe. . . . Tenga muda kwa ajili ya wanafunzi kushiriki katika kila somo.” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 30.)

47

JUNI 6–12

Ruthu; 1 Samweli 1–3“MOYO WANGU WAMSHANGILIA BWANA”

Ni muhimu kuwa tayari kufundisha, lakini hakikisha kwamba mipango yako ni pamoja na kuwapa washiriki wa darasa fursa ya kushiriki kile walichojifunza .

Alika Kushiriki

Ili kuwahimiza washiriki wa darasa kushiriki kile walichojifunza wiki hii, unaweza kuwaalika waandike ubaoni neno au kifungu kutoka Ruthu 1–4 au 1 Samweli 1–3 ambacho kiliwahamasisha wakati wa masomo yao ya binafsi au ya familia . Soma machache kwa sauti, ukiuliza washiriki wa darasa washiriki jinsi maneno na vifungu hivyo vimewahamasisha .

Fundisha Mafundisho

RUTHU; 1 SAMWELI 1–2

Kristo anaweza kugeuza msiba kuwa ushindi.• Ingawa washiriki wa darasa lako wanaweza kuwa

na majaribu yao binafsi ambayo ni tofauti na yale ya Ruthu na Hana, wanaweza kujifunza kutokana na njia ambazo wanawake hawa waaminifu walitumia kwenye upotevu na maumivu ya moyo . Ili kuwasaidia kufanya hivyo, unaweza kugawanya darasa katika vikundi vidogo na alika kila kikundi kusoma sura kutoka Ruthu 1–4 au 1 Samweli 1 . Kwenye ubao, unaweza kuandika

maswali kama haya: Ruthu au Hana walikuwa wanakabiliwa na majaribu gani? Walionyeshaje imani yao katika Bwana wakati wa majaribu yao? Vikundi vingeweza kutafuta majibu kwa moja au zaidi ya maswali na kuelezea kile wanachopata . Tunajifunza nini kutoka katika hadithi hizi kuhusu jinsi Bwana anavyoweza kutusaidia katika majaribu yetu?

Kwa Ajili ya Mtoto Huyu Niliomba, na elspeth Young

• Sio kila mtu anayeomba mtoto hupokea mmoja, na sio kila mtu ambaye mwenzi wake hufa anaolewa au anaoa tena . Lakini changamoto zetu binafsi, bila kujali ni nini, zinaweza kuwa fursa za kurejea kwa Mwokozi na kuimarisha imani yetu Kwake . Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kusoma Ruthu 2:11–12 na 1 Samweli 1:9–11 na kuongelea jinsi majaribu ya Ruthu na Hana yalivyoimarisha uhusiano wao na Bwana . Washiriki wa darasa pia wanaweza kushiriki jinsi imani yao wenyewe ilivyoimarishwa kwa sababu walimgeukia Yesu Kristo wakati wa jaribu .

Popo

te W

ewe

Uend

ako,

na

Sand

y fr

eckl

eton

gag

on

Juni 6–12

48

Ili kuunga mkono mjadala huu, unaweza kualika mshiriki mmoja au zaidi wa darasa kuja akiwa amejiandaa tayari kushiriki mawazo kutoka katika moja ya ujumbe ufuatao: Ujumbe wa Dada Reyna I . Aburto “Iwe Mawingu au Jua, Bwana, Kaa pamoja Nami!” (Liahona, Nov . 2019, 57–60); sehemu yenye kichwa cha habari “Furaha ya Kushinda kupitia Kristo” kutoka kwenye ujumbe wa Mzee D . Todd Christofferson “Furaha ya Watakatifu” (Liahona, Nov . 2019, 16–17); au maneno ya Rais Elaine S . Dalton katika “Nyenzo za Ziada .” Waombe washiriki wa darasa kushiriki kile walichojifunza kuhusu jinsi majaribu yetu yanavyoweza kuwa fursa kwa ajili ya imani kubwa katika Yesu Kristo .

1 SAMWELI 2:18–36; 3

Tunapaswa kusikiliza na kutii sauti ya Bwana.• Kunaweza kuwa na watu katika darasa lako

ambao, kama Samweli, wamesikia sauti ya Bwana lakini hawakugundua kama ni ya Kwake . Unwaeza kuwaalika washiriki wa darasa kupitia upya 1 Samweli 3, wakiangalia kile ambacho Samweli alifanya ambacho kinaweza kutusaidia katika juhudi zetu za kusikia na kutii sauti ya Bwana . Unaweza pia kuwaomba washiriki wawili wa darasa kuigiza tena maongezi kati ya Samweli na Eli .

• Wakati mwingine tunajikuta katika hali kama ya Eli—tunakuwa na fursa ya kumsaidia mtu kutambua sauti ya Bwana . Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki jinsi walivyofanya hivi kwa marafiki, washiriki wa familia zao, au wengine . Ni maandiko au uzoefu gani ambao tumeshiriki kuwasaidia wengine kuelewa ni jinsi gani Bwana anawasiliana na sisi? (ona, kwa mfano, Mafundisho na Maagano 6:22–23; 8:2–3; 9:7–9) .

Nyenzo za Ziada

Hatuko peke yetu kamwe.Rais Elaine S . Dalton alifundisha:

“Safari ya maisha wakati mwingine hutupeleka kwenye njia zisizotarajiwa . Kuna milima na kona katika barabara ambayo hakuna yeyote kati yetu anayeweza kutarajia . Lakini kwa kila moja ya milima na kona hizi pia kuna fursa—fursa ya kuchagua majibu yetu na mpango wetu wa utekelezaji . Ugumu katika maisha unaweza kuwa fursa za kutusaidia kuwa karibu zaidi na Mwokozi na kumtumaini Yeye kikamilifu . Katika mchakato wa kuishi karibu na Yeye kila siku, tunakuza sifa na tabia kama za Kristo .  .  .  .

“Kama Ruthu na Hana, sisi sote tutapata shida . Yawezekana tusiweze daima kuelewa usanifu wa Bwana wa maisha yetu, lakini ni ushuhuda wangu kwamba hatuko peke yetu kamwe . Yupo nasi daima, na anatuahidi, ‘Hamuwezi kuona kwa macho yenu ya asili, kwa wakati huu, mipango ya Mungu wenu juu ya mambo yale ambayo yatakuja hapo baadaye, na utukufu utakaofuata baada ya taabu kubwa’ [Mafundisho na Maagano 58:3]” (“Masomo kutoka kwa Ruthu na Hana,” Ensign, Apr . 2006, 35, 37) .

Ona pia Yohana 14:18; Alma 38:5 .

Kuboresha Ufundishaji WetuNi SAHIHI kusema “Sijui.” wakati unapaswa kujaribu kadiri uwezavyo kujibu maswali ambayo washiriki wa darasa wanayo, Bwana hategemei wewe ujue kila kitu. Wakati unapokuwa hujui jinsi ya kujibu kitu fulani, kiri hilo na utoe ushuhuda wa ukweli wa kile unachojua. (Ona 1 nefi 11:16–17; Kufundisha katika Njia ya Mwokozi. 24.)

49

JUNI 13–19

1 Samweli 8–10; 13; 15–18“VITA NI VYA BWANA”

Unapojiandaa kufundisha, kumbuka kwamba washiriki wa darasa wanaweza kuwa na uzoefu wenye tija kwa kusoma maandiko nyumbani . Je, unaweza kufanya nini ili kujenga juu ya uzoefu huo?

Alika Kushiriki

Kuhimiza washiriki wa darasa kushiriki kile walichojifunza wiki hii, wape muda wa kufikiria juu ya hisia zozote walizokuwa nazo kuhusu 1 Samweli 8–10; 13; 15–18 Kisha waombe washiriki mstari ambao ulichochea hisia .

Fundisha Mafundisho

1 SAMWELI 9:15–17; 10:1–12; 16:1–13

Mungu huwaita watu kwa unabii kutumikia katika ufalme Wake.• Hadithi ya Mungu akiwachagua Sauli na

Daudi kwa njia ya unabii na ufunuo yaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa jinsi watu wanavyochaguliwa kuhudumu katika Kanisa leo . Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kusoma 1 Samweli 9:15–17; 10:1–12; na 16:1–13, wakiangalia vifungu ambavyo vinaweza kuwasaidia kuelewa ina maana gani “kuitwa na Mungu” (Makala ya Imani 1:5) . Je, inaleta tofauti gani, kwa watu walioitwa na kwa wale wanaowakubali, kujua kwamba Mungu huchagua watu kuhudumu katika Kanisa Lake?

Kielelezo cha Samweli akimpaka mafuta Sauli, © lifeway Collection/licensed kutoka goodsalt.com

1 SAMWELI 13:5–14; 15

“Kutii ni bora kuliko dhabihu.”• Ili kujadili kwa nini ni muhimu kumtii

Bwana, unaweza kualika darasa kupitia upya 1 Samweli 13:5–14 na kutafuta mitazamo na tabia ambazo zilisababisha anguko la Sauli . Je, tunaweza kujifunza nini kutokana na makosa ya Sauli?

• Wakati hatujui sababu zote za Sauli kuamriwa kuwaua Waamaleki wote na wanyama wao, kuna masomo ya kujifunza kutokana na majibu yake kwa amri hiyo . Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutambua masomo haya, unaweza kuandika kwenye ubao Kutii ni bora kuliko . . . na waalike washiriki wa darasa kutafakari kifungu hiki wakati mnapitia upya pamoja matukio kutoka 1 Samweli 15 . Je, ni baadhi ya mambo gani mazuri tunayofanya katika maisha yetu ambayo

Daud

i na

Golia

thi,

na S

teve

Net

herc

ott

Juni 13–19

50

wakati mwingine sisi huchagua badala ya kumtii Mungu? Kwa nini utii kwa Mungu ni bora kuliko vile vitu vingine vizuri?

1 SAMWELI 16:6–7

“Bwana huutazama moyo.”• Baada ya kusoma 1 Samweli 16:6–7, washiriki

wa darasa wangeweza kushiriki mawazo yao kuhusu nini maana ya kutazama “moyoni” (mstari wa 7) . Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kuona kwa njia anazoona Bwana? Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu ambao uliwafundisha umuhimu wa kuangalia moyoni badala ya muonekano wa nje .

1 SAMWELI 17

Bwana anaweza kutusaidia kushinda changamoto yoyote.• Katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo,

Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia washiriki wa darasa wametafakari maneno ya watu mbali mbali yanayopatikana katika 1 Samweli 17 . Fikiria kuliomba darasa kushiriki kile walichojifunza kutokana na shughuli hii . Hasa, walijifunza nini kuhusu Daudi?

• Washiriki wengine wa darasa lako labda wanakabiliwa na changamoto ambazo zinaweza kuonekana kuwa za kutisha kama vile Goliathi alivyofanya kwa Sauli na jeshi lake . Je, unawezaje kutumia hadithi ya Daudi na Goliathi ili kuwasaidia washiriki wa darasa kukabiliana na changamoto zao na imani katika Bwana? Labda unaweza kuonyesha picha ya Daudi na Goliathi (kama mojawapo katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia) . Washiriki wa darasa wanaweza kuorodhesha ubaoni baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kuwa “Goliathi” katika maisha yetu . Kisha wanaweza kutafuta mistari katika 1 Samweli 17 ambayo inaonyesha imani ya Daudi, ambayo ilimwezesha kumshinda Goliathi (ona pia taarifa katika “Nyenzo za Ziada”) .

Pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu ambao waliuhisi Bwana aliposaidia kupigana vita vyao .

Nyenzo za Ziada

Kuwashinda Akina Goliathi wetu.Rais Gordon B . Hinckley alifundisha:

“Kuna akina Goliathi wanaokuzunguka, wakubwa wanene wenye nia mbaya ya kukuangamiza . Hawa sio wanaume wenye urefu wa futi tisa, lakini ni wanaume na taasisi zinazodhibiti mambo ya kuvutia japo ni mabaya ambayo yanaweza kukupa changamoto na kukudhoofisha na kukuangamiza .  .  .  .

“ .  .  . Lakini hauhitaji kuogopa ikiwa una kombeo la ukweli mikononi mwako . .  .  . Una mawe ya wema na heshima na uadilifu wa kutumia dhidi ya maadui hawa ambao wangependa kukushinda . Kwa kadiri unavyohusika, unaweza kuwapiga ‘katikati ya macho,’ nikisema kwa mfano . Mnaweza kuwashinda kwa kuwa na nidhamu ninyi wenyewe ili kuwaepuka . Unaweza kusema kwa wengi wao kama vile Daudi alivyomwambia Goliathi, “Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana’ [1 Samweli 17:45]” (“Overpowering the Goliaths in Our Lives,” Ensign, Mei 1983, 46, 51) .

Kuboresha Ufundishaji WetuWito wako ni una mwongozo wa kiungu. Kama mwalimu, umeitwa na mungu ili kubariki watoto Wake. Kadiri unavyoishi ukiwa mwenye ustahiki wa msaada wake, Yeye atakupa ufunuo unaoutafuta. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 5.)

51

JUNI 20–26

2 Samweli 5–7; 11–12; 1 Wafalme 3; 8; 11“UFALME WAKO UTATHIBITISHWA MILELE”

Unapojifunza maandiko, kwa maombi tafuta kujua ni kanuni zipi zitakuwa za maana zaidi kwa washiriki wa darasa lako ili uweze kuzingatia kwenye mahitaji yao .

Alika Kushiriki

Ili kujua ni nini washiriki wa darasa waliona cha maana katika kusoma kwao maandiko, unaweza kuwauliza waandike kumbukumbu ya kifungu ambacho kiliwahamasisha kwenye karatasi na kisha kuweka karatasi hiyo kwenye chombo . Kisha washiriki wa darasa wangeweza kuchagua karatasi kutoka kwenye chombo hicho, na darasa linaweza kusoma na kujadili mafungu hayo ya maneno .

Fundisha Mafundisho

2 SAMWELI 6:1–8

Lazima tufanye kazi ya Mungu katika njia Yake.• Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa

kusoma 2 Samweli 6:1–8 na fikiria ni maonyo gani historia hii inayo kwetu sisi leo . Maelezo ya Brigham Young katika “Nyenzo za Ziada” yanaweza kusaidia . Je, ni njia zipi tunaweza kujaribu kufanya kazi ya Mungu kwa njia nyingine tofauti na vile alivyoelekeza? Kwa nini hii ni hatari? Labda washiriki wa darasa

wangeweza kushiriki uzoefu ambao kwa huo walijifunza kuamini maelekezo ambayo Bwana hutoa kwa ajili ya kukamilisha kazi Yake .

2 SAMWELI 11

Tunapaswa kila mara kujilinda dhidi ya dhambi.• Kujifunza kutokana na janga la chaguzi mbaya

za Daudi lililoandikwa katika 2 Samweli 11 inaweza kutusaidia kuepuka makosa kama hayo . Labda darasa lingeweza kusoma pamoja 2 Samweli 11:1–17 na kutambua uchaguzi ambao Daudi alifanya ambao ulimsababishia yeye kutenda dhambi . Je, Daudi angefanya nini tofauti? Unaweza pia kuwaomba washiriki wa darasa kuandika sentensi ambayo inaweza kusaidia kuhamasisha mtu kuepuka dhambi, kulingana na kile ambacho amejifunza kutoka 2 Samweli 11 . Waalike washiriki wachache wa darasa kutoa mawazo yao .

• Unaweza kutumia 2 Samweli 11 kujadili hatari za ponografia na dhambi nyingine za ngono . Kufanya hivi, darasa lingeweza kupitia kwa pamoja sehemu ya ujumbe wa Mzee L . Whitney Clayton “Blessed Are All the Pure in Hear” (Liahona, Mei 2007, 51–53) . Je, ni ushauri gani Mzee Clayton anatoa juu ya hatari za ponografia? Pia mnaweza kutazama video “To Look Upon” (ChurchofJesusChrist .org) . Mwokozi anawezaje kutusaidia kushinda majaribu au tabia hizi?

Mfa

lme

Daud

i Akit

awaz

wa, n

a je

rry

mile

s h

arst

on

Juni 20 –26

52

Pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki maoni ambayo wameona yanafaa katika juhudi zao za kulinda familia zao dhidi ya ponografia au kushinda athari za ponografia . Ujumbe wa Dada Linda S . Reeves “Protection from Pornography—a Christ- Focused Home” unaweza kusaidia (Liahona, Mei 2014, 15–17; ona pia “Nyenzo za Ziada”) .

hekalu ni nyumba ya Bwana.

1 WAFALME 8:22–61

Mahekalu huleta baraka.• 1 Wafalme 8 inaelezea baraka ambazo Sulemani

alitafuta kwa watu wake wakati hekalu lilipokamilishwa . Unaweza kugawanya mistari ya 22–61 miongoni mwa washiriki wa darasa na waombe waelezee kitu wanachokipata katika mistari yao ambacho kinawachochea katika ibada yao ya hekaluni . Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki jinsi kuabudu katika nyumba ya Bwana kulivyobariki maisha yao .

1 WAFALME 8:61; 11:1–11

“Moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana.”• Inamaanisha nini “ mioyo [yetu] na .  .  . iwe kamili

kwa Bwana”? (1 Wafalme 8:61) . Je, hiyo ni tofauti na matendo yetu kuwa kamili? Kwa jinsi gani? Washiriki wa darasa wanapotafakari maswali haya, wangeweza kusoma 1 Wafalme 11:1–11 na kuona kitu ambacho Bwana anasema juu ya moyo wa Sulemani . Tunawezaje kuepuka makosa aliyoyafanya?

Nyenzo za Ziada

Kusimamisha safina.Rais Brigham Young alifundisha: “Achilia mbali Ufalme, Bwana anasimamisha safina; na ikiwa inashindana, na inaonekana inahitaji kutulia, ikiwa njia ni kidogo wakati mwingine, na kwa muonekano wote unatishia kuangushwa kwake, kuwa mwangalifu jinsi unavyonyosha mkono wako kuituliza; wacha tusiwe wenye kuingilia kati yale ambayo hayatuhusu; achana nayo, ni kazi ya Bwana” (Discourses of Brigham Young, sel . John A . Widtsoe [1954], 66) .

Kuzilinda familia dhidi ya Ponografia.Dada Linda S . Reeves alifundisha: “Je, tunawezaje kuwalinda watoto na vijana wetu? Machujio ni zana muhimu, lakini chujio kubwa zaidi ulimwenguni, na la kipekee ambalo hatimaye litafanya kazi, ni chujio la ndani ya mtu binafsi ambalo linatokana na ushuhuda wa kina na wa kudumu wa upendo wa Baba yetu wa Mbinguni na dhabihu ya Mwokozi wetu ya kulipia dhambi kwa ajili ya kila mmoja wetu” (“Protection from Pornography—a Christ- Focused Home,” Liahona, Mei 2014, 16; ona pia Joy D . Jones, “Kushughulikia Pornografia: Linda, Jibu, na Ponya,” Ensign, Okt . 2019, 22–27) .

Kuboresha Ufundishaji WetuHakikisha kwamba unafundisha mafundisho ya kweli. “Kila mara jiulize, ‘Ni kwa jinsi gani kile ninachofundisha kitawasaidia washiriki wa darasa langu kujenga imani katika Kristo, kutubu, kufanya na kushika maagano na mungu, na kupokea Roho mtakatifu?’” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 20).

53

JUNI 27–JULAI 3

1 Wafalme 17–19“BWANA AKIWA NDIYE MUNGU, MFUATENI”

Makusudi ya maandiko—na darasa lako—ni kujenga imani katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo . Kusudi hili na liongoze maamuzi unayofanya juu ya nini cha kufundisha na maswali gani ya kuuliza .

Alika Kushiriki

Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelezea utambuzi wao kuhusu 1 Wafalme 17–19, unaweza kuwaalika wafikirie kichwa cha habari kwa kila sura hizi . Je, ni mistari gani iliyowafanya wafikirie juu ya vichwa hivi?

Fundisha Mafundisho

1 WAFALME 17:8–16; 19:19–21

Mwaliko wa kutoa dhabihu ni fursa ya kuifanyia mazoezi imani yetu.• Mfano wa mjane wa Sarepta unaweza

kuwashawishi washiriki wa darasa lako wakati ambapo imani yao inajaribiwa . Unaweza kuanza kwa kuwaomba waorodheshe chaguzi ambazo zinahitaji imani katika Yesu Kristo . Kisha wangeweza kusoma kifungu katika 1 Wafalme 17:8–16 na kuongea kuhusu kile ambacho hadithi hii inawafundisha kuhusu kuwa na imani . Wahimize washiriki wa darasa kushiriki hisia zao kuhusu mjane huyu na jinsi mfano wake unavyowapa mwongozo wa kiungu

wa kutumia imani yao . Je, imani yake inafanana vipi na imani ambayo Elisha alionyesha katika 1 Wafalme 19:19–21? Labda washiriki wa darasa wangekuwa tayari kushiriki dhabihu waliyofanya kwa Bwana na jinsi Bwana alivyowabariki .

• Hadithi ya mjane wa Sarepta pia inaweza kutufundisha juu ya baraka zinazotokana na dhabihu . Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kutafakari ni jinsi gani wangejibu kauli kama hizi: “Sina uwezo wa kulipa zaka” au “Nina shughuli nyingi sana kukubali wito wa kutumikia .” Je, 1 Wafalme 17:8–16 inatufundisha nini ambacho kinaweza kutumika kwenye maelezo haya? Ni jinsi gani maarifa yetu juu ya Mwokozi hutusaidia wakati tunapoombwa kutoa dhabihu? Maneno ya Mzee Lynn G . Robbins katika “Nyenzo za Ziada” pia yangeweza kusaidia .

1 WAFALME 6:17–39

“Bwana Akiwa Ndiye Mungu, Mfuateni.”• Majadiliano ya 1 Wafalme 18:17–39 yangeweza

kuwasaidia washiriki wa darasa kuwa na msimamo zaidi wa kumfuata Yesu Kristo na kumtumaini Yeye . Baada ya kupitia upya hadithi hii na darasa, unaweza kuandika ubaoni swali ambalo Eliya aliwauliza watu wa Israeli: “Mtasitasita katikati ya mawazo mawili hata lini?” (mstari wa 21) . Washiriki wa darasa na waelezee kile wanachohisi swali hili lina maanisha nini . Je,

Eliya

Ana

bish

ana

dhid

i ya

Mak

uhan

i wa

Baal

i, na

jerr

y h

arst

on

Juni 27–Jul ai 3

54

ni sababu gani watu wanaweza kuwa walikuwa “wakisimama” (ambapo inaweza kumaanisha kusita, kuyumba, au kulegea) kati ya kumfuata Bwana na kumfuata Baali? Kwa nini wakati mwingine tunakuwa na shaka kuhusu kumfuata Yesu Kristo? Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu ambao umewasaidia wao kuchagua kumfuata Mwokozi .

mfano wa maelezo ya 1 Wafalme 19:11–12. Nabii, © Robert Booth charles/Bridgeman images

1 WAFALME 19:1–12

Bwana mara nyingi huongea kwa njia tulivu, rahisi.• Watu wengi wana changamoto ya kutambua

wakati Bwana anapowasiliana na wao . Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutambua zaidi sauti ya Bwana, ungeweza kuwaalika kusoma 1 Wafalme 19:1–12 na kuelezea kile Eliya alichojifunza . Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki mambo ambayo umewafundisha kuhusu njia tofauti Bwana anazoongea nao . Ukitaka unaweza kuonyesha video ya “How Can I Feel the Holy Ghost More Often?” (kutoka “Face to Face with President Eyring and Elder Holland” [worldwide youth broadcast, Mar . 4, 2017], ChurchofJesusChrist .org) .

• Ili kusaidia majadiliano ya haraka juu ya kifungu “sauti ndogo tulivu,” unaweza kuonyesha vitu (au picha za vitu) ambavyo vinaweza kusaidia washiriki wa darasa kutafakari kifungu hicho . Washiriki wa darasa wangeweza kupendekeza

mifano mingine . Kwa nini maneno “tulivu” na “ndogo” ni njia nzuri za kuelezea sauti ya Roho? Kwa maelezo mengine, washiriki wa darasa wangeweza kusoma maandiko kama Helamani 5:30; 3 Nefi 11:3–7; Mafundisho na Maagano 6:22–23; 8:2–3; 9:8–9; 11:12–14; 36:2 . Wanaweza kushiriki maandiko mengine juu ya kumtambua Roho . Je, maandiko haya yanashauri nini juu ya kile tunachopaswa kufanya ili kusikia sauti ya Bwana? Video “Feeling the Holy Ghost” au “Voice of the Spirit” zinaweza kusaidia (ChurchofJesusChrist .org) .

Nyenzo za Ziada

Mjane wa Sarepta.Mzee Lynn G . Robbins alisema: Eliya alielewa fundisho kwamba baraka huja baada ya kujaribiwa kwa imani yetu [ona Etheri 12:6; Mafundisho na Maagano 132:5] . Hakuwa mbinafsi . Kama mtumishi wa Bwana, Eliya alikuwepo ili kutoa, sio kuchukua [ona 1 Wafalme 17:13–16] . .  .  . Sababu mojawapo Bwana anaelezea mafundisho kwa mifano ya mazingira halisi kabisa ni ili kuondoa visingizio . Kama Bwana anatarajia hata mjane masikini kulipa sarafu yake, hiyo inawaacha wapi wengine wote ambao wanaona kuwa haifai au sio rahisi kutoa dhabihu?” (“Zaka—ni Amri Hata kwa Fukara,” Liahona, Mei 2005, 35) .

Kuboresha Ufundishaji WetuKuwa chombo kinyenyekevu cha Roho. “lengo lako kama mwalimu sio kuwasilisha somo lenye kuvutia bali ni kuwasaidia wengine kupokea ushawishi wa Roho mtakatifu, ambaye ni mwalimu wa kweli” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 10).

55

JULAI 4–10

2 Wafalme 2–7“YUKO NABII KATIKA ISRAELI”

Unapojiandaa kufundisha, soma 2 Wafalme 2–7 ukitafuta mwongozo wa kiungu kwa ajili ya maisha yako mwenyewe . Kisha sikiliza ushawishi kuhusu ujumbe ambao utabariki washiriki wa darasa lako .

Alika Kushiriki

Wakati mwingine washiriki wa darasa wanahitaji muda wa kupitia upya kwa ufupi sura walizosoma kabla ya kuweza kuelezea utambuzi walioupata kutoka kwenye usomaji wao binafsi wa maandiko . Jaribu kutoa dakika chache kwa ajili ya hili mwanzoni mwa darasa; kisha waalike washiriki wa darasa kuelezea kitu walichojifunza .

Fundisha Mafundisho

2 WAFALME 26

Mungu anaweza kufanya miujiza katika maisha yetu.• Unapojadili miujiza katika 2 Wafalme 2–6,

inaweza kusaidia kuwauliza washiriki wa darasa kufafanua neno muujiza. Unaweza kuelezea utambuzi huu kutoka kwa Rais Howard W . Hunter: “[Miujiza] ni dhihirisho la nguvu za [Mungu] ambazo hatuna uwezo wa kuzielezea au kuzielewa kikamilifu . .  .  . Ishara hizi na maajabu yalikuwa dhahiri zaidi katika maisha na huduma

ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu mwenyewe . Lakini ya kushangaza na kujazwa maajabu kama vile ilivyokuwa, miujiza mingi ya Kristo ilikuwa ni akisi tu ya maajabu makubwa zaidi ambayo Baba yake alikuwa ameyafanya mbele yake na anaendelea kufanya kote kutuzunguka sisi . .  .  . Kutakuwa na miujiza mingi kila wakati ikiwa tuna macho ya kuona na masikio ya kusikia” (“The God That Doest Wonders,” Ensign, Mei 1989, 15–16) . Je, utambuzi huu unatusaidiaje sisi kuona mkono wa Mungu katika maisha yetu?

• Fikiria kuwauliza washiriki wa darasa kuorodhesha miujiza iliyoelezewa katika 2 Wafalme 2–6 . Je, tunajifunza nini kuhusu Bwana kutoka kwenye miujiza hii? Washiriki wa darasa pia wanaweza kuwa tayari kuzungumza juu ya miujiza—mikubwa au midogo—ambayo wao au familia zao wamepata . Je, tunawezaje kutambua vyema miujiza ya Mungu maishani mwetu—pamoja na ile ambayo ni tofauti na ile tuliyotarajia?

• Washiriki wa darasa wanaweza kupata msukumo kulinganisha baadhi ya miujiza ambayo Elisha alifanya na mingine ambayo Yesu Kristo alifanya (ona 2 Wafalme 4:8–37 na Luka 7:11–16; 2 Wafalme 4:42–44 na Yohana 6:1–13; 2 Wafalme 5:1–15 na Luka 17:11–19) . Miujiza hii inatufundisha nini sisi kuhusu Mwokozi na manabii Wake?

Kiel

elez

o ch

a el

isha

aki

mw

onye

sha

mtu

mis

hi w

ake

mag

ari y

a m

oto,

© R

evie

w

& h

eral

d pu

blis

hing

/lice

nsed

from

go

odsa

lt.co

m

Jul ai 4–10

56

2 WAFALME 5:1–19

Ikiwa sisi ni wanyenyekevu na watiifu, Yesu Kristo anaweza kutuponya.• Somo moja tunaloweza kujifunza kutokana na

kupona kwa ukoma wa Naamani ni umuhimu wa unyenyekevu . Ili kuanza majadiliano, unaweza kuandika kwenye ubao kiburi cha Naamani na unyenyekevu wa Naamani. Washiriki wa darasa wanaweza kutafuta 2 Wafalme 5:1–19 na kuandika ubaoni vifungu vya maneno vinavyoonyesha kiburi au unyenyekevu wa Naamani . Je, ni kwa jinsi gani sisi wakati mwingine tuko kama Naamani? Je, wakati mwingine tunakuwaje kama watumishi wake? Ni kwa jinsi gani tumekuja kujua kile alichokuja kukijua Naamani?

• Somo jingine tunaloweza kujifunza kutoka kwenye hadithi hii ni thamani ya kumtii Mungu katika mambo madogo . Unaweza kuanza kwa kusoma 2 Wafalme 5:9–12 na kuomba mawazo ya washiriki wa darasa kuhusu ni kwa nini Naamani “akaondoka kwa hasira” (mstari 12) . Kwa nini wakati mwingine tunapendelea kufanya “jambo kubwa” ambalo Mungu hutuomba sisi, kuliko mambo rahisi? (mstari 13) . Nini thamani ya kufanya mambo haya rahisi?

2 WAFALME 6:8–23

“Wale walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao.”• Sisi sote tunazo nyakati ambapo tunahisi tuko

pekee yetu au tunaogopa . Fikiria jinsi kujadili hadithi hiyo katika 2 Wafalme 6:8–23 inavyoweza kusaidia washiriki wa darasa ambao wanajisikia hivi . Unaweza kuanza kwa kuwauliza tu washiriki wa darasa ni nini kinachowavutia kuhusu mistari hii . Wanaweza pia kushiriki matukio wakati “Bwana alipofungua macho [yao]” (mstari 17) na kuwasaidia kuona kwamba hawako peke yao (ona pia “Nyenzo za Ziada”) . Je, tunawezaje kusaidiana ili “tusiogope”? (mstari 16) .

Nyenzo za Ziada

“Tufungue macho yetu ya kiroho.”Inarejelea hadithi katika 2 Wafalme 6:8–23, Mzee Ronald A . Rasband alisema:

“Yawezekana au haiwezekani kutumiwa magari ya moto ili kuondoa hofu zetu na kuwashinda mashetani wetu, lakini somo ni bayana . Bwana yu pamoja nasi, anatujali na anatubariki katika njia ambazo ni Yeye pekee ndiye anayeweza kufanya hivyo . Sala inaweza kushusha chini nguvu na ufunuo ambao tunauhitaji ili kulenga mawazo yetu juu ya Yesu Kristo na dhabihu Yake ya kulipia dhambi . Bwana alijua ya kwamba wakati mwingine tungejisikia woga . Nimelipitia hilo vivyo hivyo na wewe pia .  .  .  . Katika Kanisa hili tunaweza tukawa wachache kwa idadi kulingana na jinsi dunia inavyofafanua ushawishi, lakini tunapofungua macho yetu ya kiroho, ‘walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao’ [2 Wafalme 6:16]” (“Usifadhaike,” Liahona, Nov . 2018, 18–19) .

Kuboresha Ufundishaji WetuWarejeze wanafunzi kwenye maandiko. wakati wowote unapoweza, wahimize washiriki wa darasa kurejelea kwenye maandiko na maneno ya manabii walio hai kwa ajili ya kupata mwongozo, majibu ya maswali, na msaada. neno la mungu ni chanzo kikuu cha ukweli. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 21.)

57

JULAI 11–17

2 Wafalme 17–25“ALIMTUMAINI BWANA MUNGU WA ISRAELI”

Rejelea misukumo uliyoiandika wakati wa kujifunza kwako binafsi 2 Wafalme 17–25 wiki hii . Ni vifungu gani vya maneno kutoka kwenye sura hizi unahisi vitakuwa na maana kwa washiriki wa darasa lako?

Alika Kushiriki

Wakati washiriki wa darasa wanaposhiriki kile wanachojifunza nyumbani katika masomo yao ya maandiko, washiriki wengine wa darasa wanaweza kuhisi msukumo wa kusoma maandiko kwa wiki nzima . Unaweza kuanza darasa kwa kualika washiriki wa darasa kujibu swali kama “Roho Mtakatifu amekufundisha nini wakati uliposoma sura ulizopangiwa kusoma wiki hii?”

Fundisha Mafundisho

2 WAFALME 18:28–36; 19:1–7, 14–19

Tunaweza kubaki wakweli kwa Bwana wakati imani yetu inapingwa.• Ukweli katika 2 Wafalme 18–19 unaweza

kutusaidia kujua jinsi ya kujibu wakati imani yetu inapopingwa . Ni kwa jinsi gani utaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kugundua ukweli huu? Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki sababu kadhaa kwa nini wanamwamini Mungu na mpango Wake . Kisha wanaweza

kupekua 2 Wafalme 18:28–35, wakitafuta sababu ambazo Waashuru waliwapa watu huko Yerusalemu wasimtumaini Bwana . Ni jinsi gani Shetani hujaribu kutushawishi sisi tuwe na shaka na imani yetu leo? Washiriki wa darasa kisha wangeweza kupekua 2 Wafalme 19:1–7, 14–19 kwa ajili ya kile tunachoweza kujifunza kutoka kwa Hezekia juu ya jinsi ya kujibu wakati imani yetu inapopingwa . Ni kwa jinsi gani Bwana anatusaidia kushinda changamoto za imani yetu? Je, ni mapendekezo gani mengine ambayo washiriki wa darasa wanayo ya kufanya upya imani yao na kumwamini Bwana?

• Unaweza kumwalika mshiriki wa darasa aje darasani akiwa amejiandaa kufupisha mazungumzo ambayo Waashuru walikuwa nayo na maafisa wa Hezekia karibu na kuta za Yerusalemu (ona 2 Wafalme 18:17–36) . Kabla hajasimulia hadithi, waalike washiriki wa darasa kufikiria kwamba wao ni wakazi wa Yerusalemu wakisikiliza mazungumzo haya . Wangeweza kuwa na mawazo au hisia gani? Wangeweza kufanya nini? Unaweza kuwapa washiriki wa darasa sehemu za ujumbe wa Mzee David A . Bednar “Kwa hiyo Walinyamazisha Hofu Zao” (Liahona, Mei 2015, 46–49) na waalike kutafuta ushauri ambao ungeweza kuwasaidia wakati wa hofu au shaka . Je, imani yetu kwa Yesu Kristo imetusaidiaje wakati wa changamoto?

Kuto

roka

kwa

Waf

ungw

a na

jam

es t

isso

t na

wen

gine

Jul ai 11–17

58

2 WAFALME 22:8–20; 23

Maandiko yanaweza kugeuza mioyo yetu ielekee kwa Bwana.• Kujadili juu ya nguvu ambayo neno la Mungu

ilivyokuwa katika maisha ya Mfalme Yosia na watu wake inaweza kuwahamasisha washiriki wa darasa kutafuta nguvu hiyo katika maisha yao wenyewe . Unaweza kuanza majadiliano kwa kuwaalika washiriki wa darasa kufikiria jinsi maisha yao yanavyoweza kuwa tofauti kama hawangekuwa na maandiko . Kisha wanaweza kupekua 2 Wafalme 22:8–11; 23:1–6, 24 ili kujua jinsi Yosia na watu wake walivyobadilika waliposikia neno la Mungu kutoka kwenye maandiko ambayo yaligunduliwa tena hivi karibuni katika hekalu . Je, maandiko yametusaidiaje kuja karibu zaidi na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo?

• Mabadiliko makubwa ambayo neno la Mungu lilikuwa nayo juu ya Yosia na watu wengi katika ufalme wake linaweza kuwahamasisha washiriki wako wa darasa kutafuta mabadiliko kama hayo katika maisha yao . Baada ya kujadili mabadiliko haya (ona 2 Wafalme 23:1–6, 21, 24), washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu ambao kifungu cha maandiko au hadithi hii ilivyoleta mabadiliko katika maisha yao . Labda wangeweza kuzungumza juu ya kwa nini walikuwa wakipokea ujumbe wa andiko hilo wakati huo katika maisha yao . Maelezo katika “Nyenzo za Ziada” yanaweza kuongezea kwenye mjadala wako .

maandiko yanaweza kusaidia kugeuza mioyo yetu kumwelekea Bwana.

Nyenzo za Ziada

Gundua tena maandiko.Rais Spencer W . Kimball alisema:

“Nina hakika kwamba kila mmoja wetu, wakati fulani katika maisha yetu, lazima tuyagundue maandiko sisi mwenyewe—na sio kuyagundua mara moja tu, lakini tuyagundue tena na tena .  .  .  .

Kwa nguvu kabisa napata hisia kwamba ni lazima sisi sote turudi kwenye maandiko kama vile Mfalme Yosia alivyofanya na kuyaacha yafanye kazi kwa nguvu ndani yetu, yakituhamasisha kufanya uamuzi usiotetereka wa kumtumikia Bwana .  .  .  .

“Mimi ninajikuta hivyo wakati ninapochukulia mahusiano yangu na uungu kuwa kitu cha kawaida na wakati inapoonekana kwamba hakuna sikio la kiungu linasikiliza na hakuna sauti ya kiungu inayozungumza, kwamba niko mbali, mbali sana . Kama nikijizamisha mwenyewe katika maandiko umbali hupungua na hali ya kuwa wa kiroho hurudi . Hujikuta nikiwapenda zaidi wale ambao lazima niwapende kwa moyo wangu wote na akili na nguvu, na nikiwapenda zaidi, Huona kuwa ni rahisi kuishi kulingana na ushauri wao” (Teachings of Presidents of the Church: Spencer W. Kimball [2006], 62–63, 67) .

Kuboresha Ufundishaji WetuTumia visaidizi vya kujifunza maandiko. Njia mojawapo ya kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa maandiko ni kuwaelekeza kwenye nyenzo kama vile mwongozo wa maandiko na makala za mada za Injili (ChurchofJesusChrist.org). Wanaweza pia kupata habari yenye kusaidia katika sehemu za “mawazo ya Kuweka akilini” katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia.

59

JULY 18–24.

Ezra 1; 3–7; Nehemia 2; 4–6; 8“HII NI KAZI KUBWA NINAYOIFANYA MIMI”

Unapowaalika washiriki wa darasa lako kuelezea kitu kile kilichoonekana cha kipekee kwao katika vitabu vya Ezra na Nehemia, pia shiriki mawazo yoyote uliyopokea ulipokuwa ukijisomea .

Alika Kushiriki

Wakati mwingine kuandika maneno muhimu au vifungu vya maneno ubaoni kunaweza kuwakumbusha washiriki wa darasa mambo waliyojifunza kutoka katika maandiko na kufanya iwe rahisi kwao kuelezea . Kwa mfano, unaweza kuandika Jenga Upya, Karabati, na Anzisha Upya ubaoni na waalike washiriki wa darasa kushiriki mistari kutokana na usomaji wao ambayo inahusiana na mojawapo au zaidi ya maneno haya .

Fundisha Mafundisho

EZRA 3:8–13; 6:16–22

Mahekalu yanaweza kuleta shangwe.• Kusoma kuhusu shangwe ambayo Wayahudi

walijisikia wakati hekalu lao likijengwa upya inaweza kusaidia washiriki wa darasa kujisikia kuwa na shukrani kwa mahekalu katika siku zetu . Labda unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kurejelea Ezra 3:8–13 na 6:16–22 na kisha kujadili njia kadhaa ambazo Wayahudi walisherehekea ujenzi huo na kuwekwa wakfu kwa hekalu . Kwa nini ujenzi wa hekalu ni sababu ya kusherehekea?

Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki jinsi mahekalu, na kazi tunayofanya humo, zinavyowaletea furaha . Maelezo katika “Nyenzo za Ziada” yanaweza kuwatia moyo washiriki wa darasa kuona shangwe ya kazi ya hekaluni .

hekalu linaweza kuwa chanzo cha shangwe katika maisha yetu.

EZRA 4–5; NEHEMIA 2; 4; 6

Tunaweza kusaidia kazi ya Mungu kusonga mbele licha ya upinzani.• Vitabu vya Ezra na Nehemia vinaelezea watu

wanaotimiza kazi muhimu licha ya upinzani kutoka kwa maadui zao . Ili kuanza majadiliano, unaweza kuuliza washiriki wa darasa ile “kazi kubwa” ya Nehemia (Nehemia 6:3) inaweza kulinganishwa na nini katika maisha yetu . Ni kazi gani muhimu ambayo Mungu ametupa kufanya? Kisha unaweza kusoma Ezra 4:4 na kujadili jinsi Shetani anavyojaribu kudhoofisha mikono yetu na kutusumbua katika kufanya kazi ya Mungu . Je, tunajifunza nini kutoka kwa Nehemia na

Kiel

elez

o ch

a he

kalu

la z

erub

babe

li, na

Sa

m l

awlo

r

Jul ai 18–24

60

wafanyakazi wenzake katika Nehemia 2:18–20; 4:6–9na 6:1–3? Je, inamaanisha nini kuwa na “moyo wa kufanya kazi” katika huduma ya Mwokozi? (Nehemia 4:6) . Fikiria kushiriki sehemu ya ujumbe wa Rais Dieter F . Uchtdorf “We Are Doing a Great Work and Cannot Come Down” (Liahona, Mei 2009, 59–62), hususani sehemu mbili za mwisho .

• Unaweza kuhisi kuhamasika kuongoza mjadala ukilinganisha juhudi za Zerubabeli za kujenga tena hekalu na juhudi zetu za kuhudhuria hekaluni na kufanya kazi ya uokoaji huko . Kwa mfano, ungeweza kuandika ubaoni vichwa vya habari viwili: Zerubabeli na Sisi. Chini ya Zerubabeli, washiriki wa darasa wangeweza kuandika kile “maadui wa Yuda na Benyamini” (Ezra 4:1) walichofanya ili kujaribu kuwazuia Zerubabeli na Wayahudi kujenga upya hekalu (ona Ezra 4) . Chini ya Sisi, washiriki wa darasa wanaweza kuorodhesha njia ambazo adui hujaribu kutuzuia kuhudhuria hekaluni . Wangeweza kisha kupeana ushauri wao kwa wao kuhusu jinsi tunavyoweza kutafuta msaada wa Bwana katika kushinda huo upinzani .

NEHEMIA 8:1–2

Tunabarikiwa tunapojifunza maandiko.• Labda washiriki wa darasa wangeweza kusoma

Nehemia 8:1–12 pamoja na kujadili jinsi Ezra na watu wake walivyojisikia kuhusu Mungu na neno Lake . Wahamasishe washiriki wa darasa kurejelea kwenye mistari maalum ambayo inaonyesha jinsi walivyojisikia . Waalike washirki wa darasa kuelezea jinsi wanavyojisikia kuhusu neno la Mungu . Ni kwa jinsi gani tunaweza kuboresha juhudi zetu za kusoma neno la Mungu?

Nyenzo za Ziada

Pata shangwe ya hekalu.Rais Russell M . Nelson alifundisha:

“Tunaweza tukapewa mwongozo wa kiungu siku nzima kuhusu mambo ya hekaluni na historia ya familia ambayo wengine wamepata . Lakini ni lazima tufanye kitu fulani ili tuweze kuipata shangwe hiyo sisi wenyewe . Ningependa kutoa changamoto kwa kila mmoja wetu ili hisia nzuri ya kazi hii iweze kuendelea na hata kuongezeka . “Ninakualikeni ninyi kwa sala mfikirie ni dhabihu gani—hususani dhabihu ya muda—ambayo mnaweza kuitoa ili kufanya kazi zaidi ya hekaluni na historia ya familia kwa mwaka huu .

Sisi tumejiingiza katika kazi ya Mwenyezi Mungu . Yu hai . Yesu ndiye Kristo . Hili ni Kanisa Lake . Sisi ni watoto Wake wa agano . Anaweza kututegemea” (Russell M . Nelson na Wendy W . Nelson, “Fungua Mbingu kupitia Kazi za Hekaluni na Historia ya Familia,” Liahona, Okt . 2017, 39) .

Kuboresha Ufundishaji WetuWajumuishe wazazi wa vijana. Kama unawafundisha vijana, waelezee wazazi wao kile unachowafundisha. Wanaweza kukusaidia kuelewa mahitaji ya vijana wao na jinsi ya kuwasaidia. hii pia inaweza kuwa njia nzuri ya kuhimiza majadiliano ya kifamilia juu ya kile ambacho vijana wanajifunza darasani. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 27.)

61

JULAI 25–31

Esta“WEWE HUKUUJIA . . . KWA A JILI YA WAKATI KAMA HUO”

Je! Unawajua vizuri washiriki wa darasa lako? Jaribu kumjua vizuri mshiriki mmoja wa darasa kila wiki . Hii itakusaidia kuzingatia mahitaji yao unapojiandaa kufundisha (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 7) .

Alika Kushiriki

Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki na mtu aliyekaa karibu naye kitu ambacho Roho aliwafundisha, kitu ambacho wamekuja kukielewa vizuri zaidi, au kitu walichokifananisha na maisha yao wakati waliposoma kitabu cha Esta . Kisha wachache wao wanaweza kuelezea kwa darasa zima .

Fundisha Mafundisho

ESTA

Bwana hutuweka katika hali ambapo tunaweza kuwabariki watu wengine.• Washiriki wa darasa lako wanaweza kuwa

walitafuta njia ambazo Bwana alifanya iwezekane kwa Esta kuwaokoa Wayahudi, kama inavyopendekezwa katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia . Waalike kuelezea walichokipata . Au mngeweza kuangalia mifano michache kwa pamoja (ona Esta 2:21–23; 3:10–14; 4:14–16) . Tunaweza kufanya nini ili kutambua mkono wa

Mungu katika maisha yetu? Maelezo ya Mzee Neil L . Anderson katika “Nyenzo za Ziada” ina jibu la swali hili .

• Ili kuwasaidia washiriki wa darasa lako kufikiria juu ya jinsi Bwana alivyowaandaa wao “kwa ajili ya wakati kama huu” (Esta 4:14), waalike wasome Esta 4:10–17 . Je, maneno ya Mordekai kwa Esta yangemsaidiaje kufanya uamuzi wa kuwatetea watu wake? Kama vile Mungu alivyomweka Esta katika nafasi ambayo angeweza kuokoa Wayahudi, je, ni mazingira gani ambayo anatuweka sisi ili tuweze kuwabariki wengine? Je, tunawezaje kuwa vyombo bora zaidi mikononi mwake? Kusoma maelezo ya Dada Virginia U . Jenses katika “Nyenzo za Ziada” kunaweza kuwahamasisha washiriki wa darasa kufikiria nyakati ambazo walihisi kuwa wao ni vyombo kwa ajili ya Bwana . Waombe washiriki na wengine uzoefu wao, kama watakavyoongozwa na Roho .

ESTA 4

Kufunga kunaonyesha utegemezi wetu kwa Bwana.• Unaweza kutumia Esta 4 kujadili baraka

zinazotokana na kufunga . Unaweza kuwa na mshiriki wa darasa akapitia matukio ambayo yalisababisha Esta na Wayahudi wengine kufunga . Kwa nini wao walichagua kufunga? Kwa nini sisi tunachagua kufunga? Mnaweza

Esta

, na

jam

es jo

hnso

n

Jul ai 25–31

62

kupitia kwa pamoja maandiko ya ziada kuhusu kufunga, kama vile Isaya 58:6–12 na Mathayo 4:1–4; 17:14–21 (ona pia Mwongozo wa Maandiko, “Mfungo, Kufunga,” scriptures .ChurchofJesusChrist .org) . Labda wewe au washiriki wachache wa darasa mnaweza kuelezea matukio ambayo yanaonyesha jinsi kufunga kunavyoleta nguvu ya Bwana maishani mwetu .

ESTA 3:1–11; 4:10–17; 5:1–4

Kufanya jambo sahihi mara nyingi huhitaji ujasiri mkubwa.• Hadithi za Mordekai na Esta kwa ujasiri

wakisimama kwa ajili ya haki inaweza kuhamasisha washiriki wa darasa kuwa na ujasiri wa kufanya jambo sahihi . Unaweza kuwaomba nusu ya darasa kusoma kuhusu Mordekai (ona Esta 3:1- 11) na nusu nyingine kusoma kuhusu Esta (ona Esta 4:10–17; 5:1–4) . Kama wangekuwa hapa leo, Mordekai na Esta wangesema nini ili kututia moyo sisi wakati ambapo ni vigumu kufanya yaliyo sahihi? Washiriki wa darasa pia wanaweza kuelezea hali ambapo walilazimika kutenda kwa ujasiri . Ungeweza kuonyesha video “Courage”(ChurchofJesusChrist .org) au lialike darasa kuimba au kusoma maneno ya wimbo kuhusu kusimamia ukweli, kama vile “Do What Is Right” (Nyimbo za Kanisa, na . 237) . Kisha jadili video au wimbo unafundisha nini kuhusu kuwa na ujasiri .

Esta mbele ya Mfalme, na minerva K. Teichert

Nyenzo za Ziada

Mkono wa Mungu.Mzee Neil L . Andersen alifundisha:

“Wakati mwingine tunaweza kuona mkono wa Bwana katika maisha ya wengine lakini tukashangaa, “Ninawezaje kuuona kwa uwazi zaidi mkono Wake katika maisha yangu mwenyewe?’  .  .  .

Unaposhika amri na kuomba kwa imani ili uuone mkono wa Bwana katika maisha yako, nakuahidi kwamba Yeye atafumbua macho yako ya kiroho, na utaona kwa uwazi zaidi kwamba wewe hauko peke yako” (“Ufalme Wako Uje,” Liahona, Mei 2015, 121–22) .

“Kwa ajili ya wakati kama huo.”Dada Virginia U . Jensen alifundisha: “Siamini kwamba mimi na wewe tuko hapa wakati huu wa kipekee kwa bahati mbaya . Ninaamini kwamba, kama Esta wa zamani, sisi ‘tumeujia ufalme kwa wakati kama huo’ [Esta 4:14], wakati ushawishi wetu, mfano wetu, nguvu zetu, na imani yetu inaweza kusimama kama kinga dhidi ya wimbi la uovu linalotishia kumeza nyumba zetu, familia zetu, na wapendwa wetu” (“Creating Places of Security,” Ensign, Nov . 1997, 89) .

Kuboresha Ufundishaji WetuNenda kwenye Maandiko kwanza. maandiko lazima yawe chanzo chako cha msingi cha maandalizi na kujifunza kwako. usisahau kwamba maneno ya manabii wa sasa hukamilishana na maandiko nayo ni maandiko pia. (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 17–18.)

63

AGOSTI 1–7

Ayubu 1–3; 12–14; 19; 21–24; 38–40; 42“BADO NITAMTUMAINI YEYE”

Ni ukweli gani ambao Roho Mtakatifu alikusaidia kujifunza wakati uliposoma kitabu cha Ayubu? Unataka kushiriki nini pamoja na darasa lako?

Alika Kushiriki

Washiriki wa darasa ambao walisoma Ayubu wiki hii wanaweza kuwa wamegundua ukweli ambao ulikuwa na maana kwao . Ili kuwachochea washiriki, unaweza kuandika kwenye ubao Nimejifunza kutoka kwa Ayubu . . . na waulize washiriki wa darasa jinsi gani wangekamilisha sentensi hii .

Fundisha MafundishoAYUBU 1–2; 12–13; 19:23–27

Uaminifu wetu kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo unaweza kutusaidia kubaki waaminifu katika hali zote.• Sura mbili za kwanza za Ayubu, ambazo

zinaelezea Shetani akihoji sababu za uaminifu wa Ayubu, zinaweza kusaidia washiriki wa darasa kutathmini sababu zao za kuwa waaminifu kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo . Washiriki wa darasa wanaweza kuanza kwa kuorodhesha sababu kadhaa ambazo mtu anaweza kuchagua kutii amri za Mungu . Kisha wanaweza kupekua Ayubu 1:6–12; 2:1–6 ili kujua kile Shetani alichosema kuhusu uaminifu wa Ayubu . Kwa

nini itakuwa hatari kumtii Bwana kwa sababu tu alizopendekeza Shetani? Jibu la Ayubu katika Ayubu 1:20–22; 2:9–10 linafunua nini kuhusu Ayubu? Washiriki wa darasa wangeweza kuzungumza kuhusu kwa nini wao walichagua kubaki waaminifu kwa Mungu .

• Wakati Ayubu alipokuwa na muda wakati alipokuwa akihangaika na mashaka na kukata tamaa, mwishowe matumaini yake katika Bwana yalimsaidia katika mateso yake . Ili kujifunza kutokana na mfano wa Ayubu, washiriki wa darasa wangeweza kutafuta baadhi ya mistari ifuatayo ili kubaini majibu kadhaa mazuri ya Ayubu kwa majaribu yake: Ayubu 1:21; 2:10; 12:9–10, 16; 13:15–16; 19:23–27 . Je, tunaweza kujifunza nini kutokana na majibu haya ambayo yanaweza kutusaidia kuwa na nguvu kiroho wakati tunapokabiliwa na majaribu? Kwa nini ni hatari kudhani kuwa majaribu ni adhabu ya dhambi?

• Tamko la Ayubu katika Ayubu 19:23–27 linaweza kuhamasisha washiriki wa darasa kutafakari na kushiriki kusadiki kwao wenyewe kwamba Mkombozi, Yesu Kristo, anaishi . Unaweza kuanza kwa kuwaalika washiriki wa darasa kutafakari kimya kimya maneno ya Ayubu katika mistari hii . Wangeweza kujadili maswali kama haya: Kwa nini ushuhuda wa Mkombozi wetu ni muhimu sana wakati wa majaribu kama yale Ayubu aliyoteseka? Ushuhuda wetu umetuimarishaje katika majaribu yetu?

Huku

mu

za A

yubu

,, na

Jose

ph B

ricke

y

aGOsTi 1–7.

64

Kuimba au kusoma maneno ya wimbo kuhusu Yesu Kristo, kama vile “Najua Mkombozi Wangu Anaishi” (Nyimbo za Kanisa, na .136), inaweza kuongeza ufahamu na nguvu ya kiroho kwenye majadiliano yako .

AYUBU 38

Mtazamo wa Mungu ni mkubwa kuliko wetu sisi.• Sehemu kubwa ya kitabu cha Ayubu

(sura ya 3–37) inajumuisha Ayubu na marafiki zake wakipambana na swali “Kwa nini mambo mabaya huwatokea watu wema?” Wakati Bwana hajibu swali hili kabisa katika kitabu cha Ayubu, Yeye anatoa ujumbe muhimu . Unaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kugundua ujumbe huu kwa kuwaalika wasome maswali ambayo Bwana alimuuliza Ayubu katika Ayubu 38:1–7, 18–24 . Tunajifunza nini kutoka katika maswali haya?

• Injili iliyorejeshwa ya Yesu Kristo inatoa nuru zaidi ambayo inaweza kutusaidia kuelewa sababu zingine za kuteseka ulimwenguni . Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki kweli wanazojua kwa sababu ya Urejesho wa injili ambazo zimewapa mtazamo mkubwa na uelewa juu ya mateso . Wangeweza kupata baadhi ya kweli hizi katika maandiko na maelezo yanayopatikana katika “Nyenzo za Ziada .”

Nyenzo za Ziada

Utambuzi wa siku za mwisho juu ya malengo ya mateso.Maandiko yafuatayo yanatoa utambuzi kuhusu malengo ya mateso:

• 2 Nefi 2:11–14

• Etheri 12:27

• Mafundisho na Maagano 58:3–5

• Mafundisho na Maagano 122

• Musa 5:10–12

Spencer W . Kimball alifundisha:

“Tukiangalia maisha ya duniani kama ndiyo maisha yote, basi maumivu, huzuni, kushindwa, na maisha mafupi yatakuwa msiba . Lakini kama tukiangalia maisha kama kitu cha milele kilichoanzia maisha yaliyopita kabla ya kuzaliwa na kisha maisha ya duniani na kuendelea hadi maisha ya milele yajayo baada ya kifo, ndipo matukio yote yanaweza kuwekwa katika mtazamo ulio sahihi .

Je, hakuna hekima katika [Mungu] ya kutupatia sisi majaribu ili tuweze kuyashinda, majukumu ili tupate kuyafikia, kazi ili tufanye misuli yetu iwe migumu, huzuni ili kuzijaribu nafsi zetu? Je, hatujaachwa kukabilina na majaribu ili kupima uwezo wetu, magonjwa ili tujifunze uvumilivu, kifo ili tuweze kuwa na maisha ya milele na walio tukuka?  .  .  .

Kama shangwe na amani na thawabu zingepewa mtenda mema papo hapo, hakungekuwa na uovu—wote wangefanya mema lakini sivyo kwa sababu ya haki ya kutenda mema . Kusingekuwa na mtihani wa nguvu, hakuna ukuaji wa tabia, hakuna ukuaji wa nguvu, hakuna uhuru wa haki ya kuchagua” (Teachings of Presidents of the Church: Spencer W. Kimball [2006], 15) .

Kuboresha Ufundishaji WetuMfuate Roho. huwezi kutabiri jinsi kila somo litakavyokwenda, lakini ushawishi wa Roho utakuongoza. iwapo mmejiandaa kiroho, Bwana atawapatia “katika saa ile ile, kile mtakachosema” (mafundisho na maagano 100:6), na inaweza kuwa kile tu washiriki wa darasa wanahitaji kusikia. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 10.)

65

AGOSTI 8–14

Zaburi 1–2; 8; 19–33; 40; 46“BWANA NDIYE MCHUNGAJI WANGU”

Panga njia za washiriki wa darasa kuelezea uzoefu wa kiroho ambao wanapata wanaposoma Zaburi .

Alika Kushiriki

Kuwaalika washiriki wa darasa kuelezea kile walichogundua katika Zaburi inaweza kuwa rahisi kama kuuliza maswali kama haya: Je, Roho alikufundisha nini uliposoma Zaburi wiki hii? Ni zaburi zipi zilizo kusaidia kujisikia karibu sana na Bwana?

Fundisha Mafundisho

ZABURI 1; 23; 26–28; 46

Zaburi inatufundisha kumtumaini Bwana.• Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa

Ajili ya Watu Binafsi na Familia unapendekeza kusoma Zaburi 1; 23; 26–28; 46 na kuangalia yafuatayo:

◦ Mwaliko wa kumtumaini Bwana

◦ Maneno ambayo yanamwelezea Bwana

◦ Maneno ambayo yanaelezea amani, nguvu, na baraka zingine Anazotoa

◦ Maneno ambayo yanawaelezea wale wanaomtumaini Yeye

Unaweza kuandika vifungu hivi vya maneno ubaoni na uwaalike washiriki wa darasa waandike, karibu na kila kifungu, kitu walichopata katika Zaburi 1; 23; 26–28; au 46 . Kama wanahitaji msaada, unaweza kuwaonyesha mistari hii: Zaburi 1:1–4; 23:1–6; 26:1, 6–8, 12; 27:1, 3, 8, 14; 28:1, 7; 46:1–3, 10 . Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki hisia walizokuwa nazo juu ya Mwokozi wanaposoma zaburi hizi .

• Kwa sababu Zaburi zilikuwa kama nyimbo kwa Waisraeli, unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kupendekeza nyimbo ambazo zinawakumbusha zaburi walizosoma wiki hii . Wanaweza kurejelea faharasa ya “Maandiko” mwishoni mwa kitabu cha nyimbo kwa maoni (ona pia orodha katika “Nyenzo za Ziada”) . Washiriki wa darasa wangeweza kuimba chache ya hizi nyimbo na kutambua mada za kawaida katika nyimbo na zaburi . Je, tunapata ujumbe gani wa amani na imani katika Yesu Kristo?

ZABURI 2; 22; 31:5

Zaburi zinaelekeza akili zetu kwenye maisha na huduma ya Yesu Kristo.• Kusoma Zaburi—hususani zile zinazoelekeza

kwenye maisha ya Mwokozi—inaweza kuwa njia nzuri ya kuimarisha imani katika Yesu Kristo . Unaweza kugawanya darasa katika vikundi vya watu wawili wawili au zaidi na kipe kila kikundi moja ya jozi zifuatazo za marejeleo: Zaburi 2:1–3 na Matendo ya

Bwan

a Nd

iye M

chun

gaji

Wan

gu, n

a Yo

ngsu

ng

Kim

, hav

enlig

ht.co

m

aGOsTi 8–14.

66

Mitume 4:24–28; Zaburi 2:7 na Matendo ya Mitume 13:30–33; Zaburi 22:1 na Mathayo 27:45–46; Zaburi 22:7–8 na Mathayo 27:39–43; Zaburi 22:16 na Luka 23:32–33; Zaburi 22:18 na Mathayo 27:35; Zaburi 31:5 na Luka 23:46 . Omba kila kikundi kutafuta jinsi unabii katika Zaburi ulivyotimizwa katika maisha ya Mwokozi na ujadili jinsi maandiko haya yanavyoimarisha ushuhuda wao juu ya Mwokozi .

Au unaweza kuandika marejeo ya maandiko ubaoni na uwaalike washiriki wa darasa waoanishe kifungu kutoka Zaburi na tukio linalofanana katika Agano Jipya .

Unaweza pia kualika washiriki wa darasa kushiriki marejeo mengine kwa Mwokozi ambayo walipata katika masomo yao juu ya Zaburi (kama vile Zaburi 34:20; 41:9; ona pia Luka 24:44) .

Baada ya washiriki wa darasa kujadili maandiko haya, wangeweza kuzungumza juu ya kwa nini zaburi hizi zingekuwa na maana kwa Wayahudi ambao walimjua Mwokozi . Kwa nini zinamaana kwetu sisi?

ZABURI 23.

“Bwana ndiye mchungaji wangu”• Kuwasaidia washiriki wa darasa kujadili picha na

ishara katika Zaburi 23, fikiria kuonyesha picha zinazohusiana na maoni katika zaburi, kama vile zile zilizo katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Unaweza kisha kuwaomba washiriki wa darasa watambue maneno au vifungu vya maneno vyenye maana katika zaburi na kujadili kile yanachoweza kuwakilisha . Kwa mfano, ni vipi misemo kama “katika malisho ya majani mabichi hunilaza” au “maji ya utulivu” huleta akilini? Je, “gongo” na “fimbo” vyanifariji inaweza kumaanisha nini? Inaweza kumaanisha nini kwa “kikombe” chetu kinafurika? Je, alama hizi zinatufundisha nini kuhusu Yesu Kristo? Unaweza kupendekeza kwamba washiriki wa darasa warudie zaburi hiyo, wakibadilisha baadhi ya alama na maana zinazopatikana zilizojadiliwa na darasa .

Nyenzo za Ziada

Nyimbo zinazohusiana na Zaburi.• Zaburi 8:3–9; 9:1–2. “How Great Thou Art”

(Nyimbo za Kanisa, na . 86)

• Zaburi 23. “The Lord is My Shepherd”,” “The Lord My Pasture Will Prepare” (Nyimbo za Kanisa, na . 108, 109)

• Zaburi 23:6; 150. “Praise to the Lord, the Almighty” (Nyimbo za Kanisa, na . 72)

• Zaburi 26:8. “We Love Thy House, O God” (Nyimbo za Kanisa, na . 247)

• Zaburi 27:1. “The Lord Is My Light” (Nyimbo za Kanisa, na . 89)

• Zaburi 33:1- 6; 95:1- 6. “For the Beauty of the Earth” (Nyimbo za Kanisa, na . 92)

• Zaburi 37:3- 9 ”Be Still, My Soul” (Nyimbo za Kanisa, na . 124)

• Zaburi 148. “All Creatures of Our God and King” (Nyimbo za Kanisa, na . 62)

Kuboresha Ufundishaji WetuTumia muziki. Nyimbo zinamwalika Roho wa Bwana, kuleta hisia za uchaji, hutuunganisha sisi kama washiriki, na kutoa njia kwetu ya kutoa sifa kwa Bwana. nyimbo hutupeleka kwenye toba na matendo mema, hujenga ushuhuda na imani, huwafariji wachovu, kuwafariji wenye kuomboleza, na kutupa mwongozo wa kiungu wa kuvumilia hadi mwisho” (Nyimbo za Kanisa, ix).

67

AGOSTI 15–21.

Zaburi 49–51; 61–66; 69–72; 77–78; 85–86“NITATANGAZA YALE AMBAYO AMEFANYA KWA A JILI YA NAFSI YANGU”

Fikiria ushauri wa Mzee David A . Bednar ukiwa unajiandaa kufundisha: “Kuzungumzia na kusimulia peke yake siyo kufundisha . [Kufundisha] injili katika njia ya Bwana kunajumuisha kuchunguza na kusikiliza na kutambua kama vigezo vya awali kabla ya kuanza kuongea” (“Becoming a Preach My Gospel Missionary,” New Era, Okt . 2013, 6) .

Alika Kushiriki

Njia mojawapo ya kuwaalika washiriki wa darasa kuelezea kitu walichosoma wiki hii ni kuandika kwenye ubao “Midomo yangu itafurahi sana” au “Ulimi wangu nao utasimulia haki yako” (Zaburi 71:23- 24) . Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki kile walichokiona kwamba huwasaidia “kushangilia sana” au “kuzungumza juu ya haki [ya Bwana] .”

Fundisha Mafundisho

ZABURI 51; 85–86

“Wewe, Bwana, U mwema, na umekuwa tayari kusamehe.”• Zaburi 51 inaelezea hisia ambazo wengi wetu

tunakuwa nazo tunapotafuta kutubu na kusamehewa . Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa vizuri toba na kuhisi msukumo wa kutubu mara nyingi, unaweza kupendekeza kwamba wachunguze Zaburi 51 wakiwa na swali hili akilini: Kutubu kuna maana gani?

Kisha waache washiriki majibu yanayopatikana . (Nyenzo za Ziada” ina utambuzi wenye kusaidia .) Kwa nini toba wakati mwingine inaonekana kutotamanika? Je, tunapata kitu gani katika zaburi hii ambacho kinaweza kufanya toba kuwa yenye shangwe?

• Je, tunawezaje kuelezea jinsi kupokea msamaha wa dhambi kupitia nguvu ya Yesu Kristo ya kulipia dhambi kunavyokuwa? Waalike washiriki wa darasa kutoa mawazo yao, na wahimize kutafuta vifungu vya maneno katika Zaburi 51; 85–86 ambavyo vinaelezea matokeo ya msamaha Wake wenye utakaso katika maisha yetu (kwa mfano, ona Zaburi 51:1–2, 7–12; 85:2–9) . Fikiria kuonyesha picha au vitu ili kusaidia washiriki wa darasa kutambua misemo hii . Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki maoni yao kuhusu Mwokozi Yesu Kristo na utayari wake wa kulipa kwa ajili ya dhambi zetu ili sisi tuweze kusamehewa . Unaweza pia kuimba pamoja wimbo kuhusu dhabihu ya Mwokozi ya kulipia dhambi, kama vile “I Stand All Amazed” (Nyimbo za Kanisa, na . 193) .

• Ili kutubu, tunahitaji imani sio tu kwamba Yesu Kristo anaweza kutusafisha lakini pia kwamba Yeye atafanya hivyo. Washiriki wa darasa wanaweza kuwa wamepata vifungu vya maneno katika Zaburi 51; 85–86 wiki hii

Kuok

oa K

ile K

ilich

opot

ea, n

a m

icha

el T

. mal

m

aGOsTi 15–21.

68

ambavyo vimeimarisha imani yao katika utayari wa Bwana wa kusamehe . Wahimize kushiriki kitu walichokipata . Unaweza pia kuwaelekeza kwenye Zaburi 86:5, 13, 15 na waulize mistari hii inafundisha nini kuhusu Bwana . Inaweza kumaanisha nini kwamba Yeye ni “mwingi wa rehema na kweli”? (mstari wa 15) . Kwa nini ni muhimu kwetu kujua hili?

ZABURI 66:5–20.

Ushuhuda wetu juu ya Yesu Kristo unaweza kuwasaidia wengine kuja Kwake.• Moja ya baraka kubwa za kukusanyika pamoja

katika Shule ya Jumapili ni fursa ya kupata nguvu kutokana na imani na ushuhuda wa wafuasi wengine wa Yesu Kristo . Ili kutoa nafasi hii kwa darasa lako, unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kusoma Zaburi 66:16 na kutafakari swali hili: Kama ungetakiwa “utangaze kile ambacho [Bwana] amefanya kwa ajili ya nafsi [yako],” ungetangaza nini? Wakiwa wanatafakari, wanaweza kusoma mistari ya 5–20 kwa ajili ya kupata mawazo . Na waandike majibu yao . Kisha waalike “watamkiane” kwa kila mmoja—katika vikundi vidogo au kwa darasa zima—kile ambacho Yesu Kristo amekifanya kwa ajili ya nafsi zao .

tunaweza kushiriki na wengine shuhuda zetu kwa kile ambacho Bwana alitufanyia.

Nyenzo za Ziada

Toba inamaanisha badiliko.Rais Russell M . Nelson alielezea toba kwa njia hii:

“Wakati Yesu anapotuomba mimi na wewe ‘tutubu,’ Anatualika kubadili akili zetu, ufahamu wetu, roho zetu—hata jinsi tunavyopumua . Anatuomba tubadili jinsi tunavyopenda, tunavyofikiri, tunavyohudumu, tunavyotumia muda wetu, tunavyowatendea wake zetu, tunavyowafundisha watoto wetu, na hata jinsi tunavyoitunza miili yetu .

“Hakuna kinachotoa uhuru zaidi, cha kiungwana zaidi, au cha muhimu zaidi kwa maendeleo yetu binafsi kuliko ilivyo fokasi ya mazoea ya kila siku kwenye toba . Toba siyo tukio; ni mchakato . Ni ufunguo kwa furaha na amani ya akili . Inapoambatana na imani, toba hufungua kufikia kwetu kwenye nguvu za Upatanisho wa Yesu Kristo .  .  .  .

“Tunapochagua kutubu, tunachagua kubadilika! Tunamruhusu Mwokozi kutubadilisha kuwa toleo zuri zaidi la sisi wenyewe . Tunachagua kukua kiroho na kupokea shangwe—shangwe ya ukombozi katika Yeye . Tunapochagua kutubu, tunachagua kuwa zaidi kama Yesu Kristo!“ (“Tunaweza Kufanya Vizuri Zaidi na Kuwa Wazuri Zaidi,” Liahona, Mei 2019, 67) .

Kuboresha Ufundishaji WetuUliza Maswali Ambayo Yanagusa Moyo na Akili. “waombe wanafunzi kuelezea jinsi wanavyojisikia kuhusu kifungu cha maandiko, je, watu katika maandiko yawezekana walikuwa wakijisikiaje, au je, ukweli katika kifungu hiki cha maneno kinahusianaje na maisha yetu” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 31).

69

AGOSTI 22–28.

Zaburi 102–103; 110; 116–119; 127–128; 135–139; 146–150“KILA MWENYE PUMZI NA AMSIFU BWANA.”

Je, ni mafundisho gani katika Zaburi unahisi yatakuwa ya msaada zaidi kwa washiriki wa darasa lako? Unapojifunza wiki hii, tafakari jinsi unavyoweza kuwasaidia washiriki wa darasa kupata maana katika maneno ya zaburi hizi .

Alika Kushiriki

Wape washiriki wa darasa dakika chache kupitia upya zaburi walizosoma wiki hii, na waalike wachache kushiriki kifungu wanachopenda . Wahimize kushiriki kile walichofundishwa na Roho . Je, Zaburi zimeongezaje ufanyaji wetu binafsi wa ibada kwa Bwana?

Fundisha Mafundisho

ZABURI 102- 3; 116

Bwana anaweza kutufariji katika mateso yetu.• Je, washiriki wa darasa lako wamejisikia kama

mwandishi wa Zaburi 102 alivyojisikia? Je, tunawezaje kumgeukia Bwana tunapojisikia kuvunjika moyo au kufadhaika? Walipojifunza Zaburi 102, 103, na 116 nyumbani wiki hii, washiriki wa darasa yawezekana kuwa waliona vifungu vya maneno ambavyo vinawahamasisha kumgeukia Bwana katika majaribu yao .

Wahimize kuelezea kile walichokipata, au watafute vifungu vya maneno vyenye mwongozo wa kiungu kwa pamoja kama darasa . Washiriki wa darasa pia wanaweza kuzungumza kuhusu jinsi Bwana alivyowasaidia nyakati za shida .

• Washiriki wa darasa lako wanaweza kufurahia kuandika zaburi yao wenyewe kuhusu jinsi Bwana alivyowasaidia nyakati za majaribu . Hizi hazihitaji kuwa zaburi ndefu au ngumu—maneno rahisi tu yenye kuelezea imani, shukrani, na sifa . Washiriki wa darasa wanaweza kufanya kazi kila mtu peke yake au wawili wawili, na wanaweza kurejelea Zaburi 102, 103, na 116 kwa ajili ya kupata mawazo . Waalike watu wachache kushiriki zaburi zao, kama wanapenda . Mnaweza pia kuimba nyimbo pamoja kuhusu jinsi Bwana anavyotufariji, kama vile “Where Can I Turn for Peace?” (Nyimbo za Kanisa, na . 129) .

Uponyaji, na J. Kirk Richards

Kila

Got

i Lita

pigw

a, n

a J.

Kirk

Ric

hard

s

aGOsTi 22–28.

70

ZABURI 119

Neno la Mungu litatuweka katika njia Yake.• Ili kuanza majadiliano kuhusu Zaburi 119,

unaweza kualika washiriki wa darasa kuzungumza juu ya wakati ambapo walifuata njia ya kufikia waendako (inaweza kusaidia kuwasiliana na mtu mapema na kumwomba awe tayari kuzungumza juu ya hili) . Ni jambo gani lililofanya iwe vigumu kukaa kwenye njia hiyo? Ni nini kiliwasaidia kukaa juu yake? Kisha unaweza kuchora njia ubaoni na uwaalike washiriki wa darasa kuandika vifungu vya maneno kutoka Zaburi 119 ambavyo vinaelezea kile Bwana alichofanya ili kutusaidia kubaki kwenye njia Yake ya agano . Fikiria kushiriki nukuu za Rais Russell M . Nelson katika “Nyenzo za Ziada” kama sehemu ya mjadala wako .

• Washiriki wa darasa lako wanaweza kufaidika kwa kulinganisha kile Zaburi 119 inafundisha kuhusu kubaki kwenye njia ya Bwana na maandiko mengine ambayo yanafundisha ukweli kama huo . Fikiria kuligawa darasa katika makundi na kulitaka kila kundi kupitia vifungu vya maandiko kama haya: Zaburi 119:33–40, 105; Mithali 4:11–19; 1 Nefi 8:20–28; 11:25; 2 Nefi 31:17–21; Alma 7:9, 19–20 . Alika kila kikundi kuelezea kile walichojifunza . Wape washiriki muda wa kutafakari nini wameshawishika kufanya kulingana na kile walichojifunza .

ZABURI 139

Bwana anaijua mioyo yetu.• Kuelewa kuwa Bwana anatujua—mawazo na

matendo yetu, uimara na udhaifu—na kwamba Yeye anatupenda kunaweza kuwa na ushawishi mkubwa juu ya uchaguzi ambao tunafanya . Unaweza kualika darasa kutafuta vifungu vya maneno katika Zaburi 139 ambavyo vinafundisha ukweli huu muhimu . Je, maisha yetu yanaguswaje na kujua ukweli huu? Washiriki wa darasa pia wanaweza kujadili njia ambazo tunaweza kumwalika Bwana “uchunguze, Ee Mungu, na uujue moyo wangu” (mstari 23) .

Nyenzo za Ziada

Njia nyembamba iliyosonga.Rais Russell M . Nelson alisema:

“Ikiwa safari yetu maishani inatakiwa kuwa yenye mafanikio, tunahitaji kufuata maelekezo ya kiungu . Bwana alisema, ‘Nitegemeeni katika kila wazo; msitie shaka, msiogope’ [Mafundisho na Maagano 6:36] Na mtunga Zaburi aliandika, ‘Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga wa njia yangu’ [Zaburi 119:105] .  .  .  .

“Katika safari yako ya maisha, unakutana na vizuizi vingi na hufanya makosa . Mwongozo wa kimaandiko hukusaidia kutambua makosa na kufanya masahihisho muhimu . Unaacha kwenda katika mwelekeo mbaya . Unasoma kwa uangalifu ramani ya barabara ya kimaandiko . Halafu unaendelea na toba na kurejesha vinavyohitajika kurejeshwa ili kuingia kwenye ‘njia nyembamba iliyosonga inayoongoza kwenye uzima wa milele’ [2 Nefi 31:18]” (“Living by Scriptural Guidance,” Ensign, Nov . 2000, 17) .

Kuboresha Ufundishaji WetuWajumuishe wale wote wanaosumbuka. wakati mwingine washiriki wa darasa wanaosumbuka wanahitaji tu kujumuishwa ili wajisikie kupendwa. Fikiria kuwaomba wao kuchukua nafasi katika somo lijalo ukiwaalika kuja darasani, au kuhakikisha wanapata usafiri wa kuwaleta kanisani. usikate tamaa kama watashindwa kuitikia jitihada zako kwa mara ya kwanza. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 8‑ 9.)

71

AGOSTI 29– SEPTEMBA 4

Mithali 1–4; 15–16; 22; 31; Mhubiri 1–3; 11–12“KUMCHA BWANA NI CHANZO CHA HEKIMA”

Ni kwa jinsi jumbe katika Mithali na Mhubiri zingeweza kubariki maisha ya wale unaowafundisha? Fuata minong’ono na misukumo unayopokea unapojifunza na kujiandaa kufundisha .

Alika Kushiriki

Kuna ujumbe mwingi mzuri na ulio na nguvu katika Mithali na Mhubiri . Kabla ya kujadili vifungu mahususi, kama vile vilivyopendekezwa hapo chini, waalike washiriki wa darasa kushiriki baadhi ya vifungu wavipendavyo kutoka katika kujifunza maandiko kwao binafsi au na familia wiki hii .

Fundisha Mafundisho

MITHALI 1–4; 15– 31; MHUBIRI 1–3; 11–12

“Tega sikio lako kusikia hekima.”• Mwaliko wa kutafuta hekima na uelewa

umerudiwa kote katika Mithali . Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kushiriki na familia zao kile walichojifunza darasani? Njia moja inaweza kuwa ni kuandika hekima ubaoni na kuwaalika washiriki wa darasa waongeze nambari za mistari au virai kutoka katika Mithali au Mhubiri ambavyo wanahisi vinatoa umaizi kuhusu hekima . (Kama ingeweza kuwa msaada, unaweza kupendekeza kwamba washiriki wa darasa wapekue

Mithali 1–4; 15– 31; Mhubiri 1–3; 11–12 .) Tunajifunza nini kuhusu hekima kutoka kwenye maandiko haya? Ni kwa jinsi gani tunabarikiwa tunapotafuta hekima kutoka kwa Mungu?

MITHALI 1:7; 2:5; 3:7; 8:13; 15:33; 16:6; 31:30; MHUBIRI 12:13

“Usiwe mwenye hekima machoni pako; mche Bwana.” • Mada ingine inayopatikana kote katika Mithali

na Mhubiri ni “kumcha Bwana” (Mithali 1:7; ona pia Mithali 2:5; 3:7; 8:13; 15:33; 16:6; 31:30; Mhubiri 12:13) . Pengine washiriki wa darasa wangeweza kusoma baadhi ya mistari hii na kushiriki kile wanachohisi inamaanisha kumcha Bwana . Je, Ni kwa jinsi gani kumcha Bwana ni tofauti na aina nyingine za hofu? Unaweza kushiriki umaizi kutoka katika maelezo ya Mzee David A . Bednar yanayopatikana katika “Nyenzo za Ziada .”

Kujifunza Kumtumainia Bwana, na Kathleen peterson

aGOsTi 29– sePTemBa 4

72

MITHALI 3:5–7

“Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote.”• Washiriki wa darasa wanaweza kufurahia

somo la kielelezo ambalo linawasaidia kuelewa kile inachomaanisha “kumtumaini Bwana” na “wasizitegemee akili [zao] wenyewe” (Mithali 3:5) . Kwa mfano, unaweza kumwalika mshiriki wa darasa aegemee kitu fulani imara na thabiti, kama vile ukuta . Kisha yule mtu ajaribu kuegemea kitu fulani ambacho si imara, kama vile ufagio . Ni kwa jinsi gani onyesho hili linatusaidia kuelewa Mithali 3:5? Je, Mithali 3: 5–7 inafundisha nini kuhusu kumtumaini Bwana? Kwa nini si busara kutegemea uelewa wetu wenyewe? Ni kwa jinsi gani Bwana huongoza mapito yetu tunapomtumaini Yeye?

MITHALI 15:1–2, 4, 18,28; 16:24–32

“Jawabu la upole hugeuza hasira.”• Kuwasaidia washiriki wa darasa kujadili jinsi

wanavyoweza kuwa na amani zaidi na kutokuwa na ubishi katika maisha yao, unaweza kuwaalika wasome Mithali 15:1–2 .18; 16:32 . Kisha wangeweza kushiriki uzoefu ambao wamekuwa nao ambao unaonyesha ukweli katika mistari hii . Kwa mfano, ni lini kutumia “jawabu la upole” lilisaidia “kugeuza hasira”? (Mithali 15:1) . Au wanaweza kufikiria nyakati ambapo Mwokozi alitoa mfano wa kile kinachofundishwa katika mistari hii (ona Yohana 8:1–11; 18:1–11) . Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kufuata mfano Wake tunapotangamana na wengine?

• Hali waandishi wa Mithali hawakujua kuhusu mikondo mingi ya mawasiliano ambayo ipo katika siku yetu, ushauri katika Mithali 15 na16 unaweza kutumika katika aina zote za mawasiliano . Kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa hili, unaweza kumwalika kila mtu kuchagua mojawapo ya maandiko yafuatayo ili asome: Mithali 15:1–2, 4, 18,28; 16:24, 27–30 . Washiriki wa darasa kisha wanaweza kuzisema upya mithali zao katika aina ya ushauri kuhusu kutangamana na wengine kwenye mitandao

ya kijamii, kwa njia ya kutuma ujumbe, au kimtandao . Wanaweza kupata ushauri wa ziada wenye msaada katika “Lugha” katika Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, (2011), 21– 21 .

Nyenzo za Ziada

“Kumcha Mungu ni kumpenda na kumtumaini Yeye.”Mzee David A . Bednar alielezea:

“Hivyo, hofu ya Mungu inakua nje ya uelewa sahihi wa asili ya kiungu na misheni ya Bwana Yesu Kristo, utayari wa mapenzi yetu kumezwa na mapenzi Yake, na uelewa kwamba kila mwanaume na mwanamke atawajibika kwa dhambi zake mwenyewe Siku ya Hukumu . .  .  .

“Kumcha Mungu ni kumpenda na kumtumaini Yeye . Tunapomcha Mungu zaidi kabisa, tunampenda Yeye kwa ukamilifu zaidi . Na ‘upendo ulio kamili hutupa nje hofu’ (Moroni 8:16) . Ninaahidi mwanga angavu wa kumcha Mungu utafukuzia mbali vivuli vyeusi vya woga wa maisha ya mauti (ona Mafundisho na Maagano 50:25) tunapomtegemea Mwokozi, tunajenga juu Yake kama msingi wetu, na kusonga mbele juu ya njia yake ya agano pamoja na ahadi iliyotukuka” (“Kwa Hiyo Walizima Uoga Wao,” Liahona, Mei 2015, 48–49) .

Kuboresha Ufundishaji WetuFokasi juu ya Kristo. hakuna njia bora ya kuongeza imani ya wale unaowafundisha kuliko kukita somo lako juu ya mwokozi. Kupitia ufundishaji wako, waalike washiriki wa darasa kujenga “juu ya mwamba wa mkombozi wetu, ambaye ni Kristo, mwana wa mungu” (helamani 5:12).

73

SEPTEMBA 5–11

Isaya 1–12“MUNGU NDIYE WOKOVU WANGU”

Fikiria njia za kuwahimiza washiriki wa darasa kushiriki misukumo na uelewa waliopokea wakati wa kujifunza kwao binafsi na kama familia wiki hii?

Alika Kushiriki

Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unatoa mawazo kwa ajili ya kuelewa maandiko ya Isaya . Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki jinsi mojawapo ya mawazo haya, au kitu kingine, kilivyowasaidia kujifunza kutoka katika Isaya 1–12 .

Fundisha MafundishoISAYA 1–12

Maneno ya Isaya yote yatatimizwa.• Akiongea juu ya Isaya, Mwokozi alifundisha

kwamba “vitu vyote ambavyo alizungumza vimekuwa na vitakuwa, hata kulingana na maneno ambayo alisema (3 Nefi 23:3) . Unaweza kuanza kwa kujadili kuhusu Isaya kwa kushiriki andiko hili na kauli katika “Nyenzo za Ziada .” Unaweza kisha kuandika ubaoni siku ya Isaya, Huduma ya Mwokozi duniani na Siku za Mwisho. Washiriki wa darasa wanaweza kutafuta vifungu katika Isaya 1–12 ambavyo vinaweza kulingana na kirai kimoja au zaidi vilivyo ubaoni (kwa mfano, Isaya 2:1–5; 7:1–7; 7:10–14; 9:2–7; 10:20; 11:10; 12:1) . Kwa nini ni baraka kuwa unabii huu unapatikana kwetu leo?

ISAYA1; 3;5

“Acheni kutenda mabaya.”• Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa

kushiriki kitu walichojifunza kutoka katika kujifunza kwao binafsi na kama familia katika Isaya1, 3,5 kuhusu hali za kiroho za Ufalme wa Yuda katika siku za Isaya . Labda wangeweza kupitia tena sura hizi na kutengeneza orodha ya mistari na hali wanazoelezea . Ni ujumbe gani wa matumaini tunapata katika sura hizi? (Kama inahitajika, unaweza kuwarudisha washiriki wa darasa kwenye Isaya 1:16–20, 25–27; 3:10 .) Kama Yuda ya kale ilikuwa na ujumbe kwa ajili yetu, ungekuwa upi?

• Washiriki wa darasa wanaweza kujifanya kwamba walikuwa wanaishi katika Yerusalemu wakati Isaya alipotoa unabii . Unaweza kuwahoji wachache kati yao, ukiwauliza Isaya alisema nini na wao walijisikiaje . Kwa mfano, unaweza kuwauliza washiriki wa darasa kuongea kuhusu maneno ya Isaya yanayopatikana katika Isaya 1:16–20; 3:16–26; 5:20–23 . Je, Isaya alisema nini ambacho kinatuhamasisha sisi kutubu?

ISAYA 2; 4; 11–12

Mungu atafanya kazi kuu katika siku za mwisho.• Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari

jinsi unabii wa Isaya kuhusu siku za mwisho unavyotimizwa, unaweza kuchagua baadhi ya mistari kutoka katika Isaya 2; 4; 11–12 (kama vile Isaya 2:2–3; 4:5–6) . Waalike washiriki

Nabi

i Isa

ya A

tabi

ri Ku

zaliw

a kw

a Kr

isto,

na

har

ry

ande

rson

sePTemBa 5–11

74

wa darasa kutafuta vitenzi vya njeo ya wakati ujao katika hii mistari (kama vile “takuwa” au “taenda”) . Waalike wao wabadilishe baadhi na mahali pake waweke vitenzi vya wakati uliopo (kama vile “imekuwa” au nimeenda”) . Je, unabii huu unatimizwaje katika maisha yetu? Kwa nini ni muhimu kujua kuhusu unabii huu?

• Unaweza kusema kwamba wakati Moroni alipomtembelea Joseph Smith katika mwaka wa 1823, alinukuu Isaya 11 na kusema kwamba ulikuwa karibu kutimia (ona Joseph Smith—Historia 1:40; ona pia Mafundisho na Maagano 113:1–6) . Washiriki wa darasa wanaweza kusoma mistari michache kutoka katika Isaya 11 (kama vile mstari wa 6–12) na kufanya muhtasari kwa maneno yao wenyewe kwa kile ambacho Isaya alitabiri . Je, nafasi yetu sisi ni ipi katika kutimizwa kwa unabii huu?

“maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume” (isaya 9:6).

ISAYA 7–9

Isaya alitoa unabii juu ya Yesu Kristo.• Unaweza kuwauliza washiriki wa darasa kitu

walichojifunza kuhusu Yesu Kristo kutoka kwenye vifungu kama vile Isaya 7:14; 8:13–14; 9:2, 6–7 . Kwa mfano, kwa nini Imanueli ni jina zuri kwa Mwokozi? (ona Mathayo 1:23) . Ni kwa jinsi gani Yesu Kristo amekuwa “Mshauri” au “Mfalme wa Amani” kwetu sisi? Washiriki wa darasa pia wanaweza kushiriki vifungu vingine walivyovipata katika Isaya 1–12 ambavyo vinawakumbusha juu ya Yesu Kristo . Je, vifungu hivi vinatufundisha nini kumhusu Yeye?

• Kabla ya darasa, waalike washiriki wa darasa kuleta picha ya Kristo ambayo wanahisi inawakilisha mojawapo ya maelezo ya Mwokozi yanayopatikana katika Isaya 7–9 . Wakati wa darasa, wape muda kuonyesha picha waliyoleta na kuelezea jinsi inavyolingana na maneno ya Isaya .

Nyenzo za Ziada

Unabii wa Isaya unaweza kuwa na utimizwaji mwingi.Rais Dallin H . Oaks alifundisha: “Kitabu cha Isaya kina unabii mwingi ambao unaonekana kuwa na utimizwaji mwingi . Mmoja unaonekana kuhusisha watu wa siku ya Isaya au hali za kizazi kinachofuata . Maana nyingine, mara nyingi kiishara, unaonekana kurejelea matukio katika wakati wa meridiani, wakati Yerusalemu ilipoangamizwa na watu wake kutawanywa baada ya kusulubiwa kwa Mwana wa Mungu . Bado maana nyingine ya utimizwaji wa unabii huo huo unaonekana kuhusika na matukio yatanguliayo Ujio wa Pili wa Mwokozi . Ukweli kwamba wingi wa unabii huu unaweza kuwa na maana nyingi inadhihirisha umuhimu wa haja yetu ya ufunuo kutoka kwa Roho Mtakatifu hili kutusaidia kuutafsiri (“Scripture Reading and Revelation,” Ensign, Jan . 1995, 1995,8) .

Kuboresha Ufundishaji WetuMwalike Roho. “muziki mtakatifu, maandiko, maneno ya manabii wa siku za mwisho, madhihirisho ya upendo na ushuhuda, na nyakati za tafakuri ya kimya zinaweza kualika uwepo wa Roho mtakatifu” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,10).

75

SEPTEMBA 12–18

Isaya 13–14; 24–30;35“KAZI YA A JABU NA MWUJIZA”

Kabla ya kuweza kuwasaidia wengine kugundua ukweli katika kitabu cha Isaya, unahitaji kugundua ukweli huo wewe mwenyewe . Unaposoma wiki hii, fikiria ni ukweli upi unahisi kuvutiwa kuzingatia darasani .

Alika Kushiriki

Ili kuwahimiza washiriki wa darasa kushiriki kile wanachojifunza kutoka katika Isaya, unaweza kuwauliza jinsi ambavyo wangemjibu mtu ambaye anasema “Kitabu cha Isaya ni kigumu sana kukielewa .” Ni nini kinaweza kutusaidia kupata maana katika mafundisho ya Isaya? Ni vifungu vipi vimetusaidia kupata maana katika mafundisho ya Isaya?

Fundisha Mafundisho

ISAYA 24:21– 23; 25:6–8; 26:19; 28:16

Maandishi ya Isaya yanatuelekeza kwa Yesu Kristo.• Kama Nefi, washiriki wa darasa lako wanaweza

kuwa walifurahia katika ushuhuda wa Isaya juu ya Yesu Kristo (ona 2 Nefi 11:2) . Ungeweza kuwaomba wao kushiriki mistari yo yote waliyoipata katika usomaji wao wiki hii ambayo uliwafundisha kuhusu Mwokozi . Au unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki kile ambacho wao wamejifunza kuhusu Yesu Kristo

kutoka katika Isaya 24:21–23; 25:6–8; 26:19; 28:16 au mistari mingine ambayo wewe uliipata katika kujifunza kwako . Kwa nini ukweli huo ni wa thamani kwetu?

Yeye Anakuja Tena Kuongoza na Kutawala, na mary R. sauer

ISAYA 24:1–5; 28:1–8; 29:7–10; 30:8– 14

Ukengeufu maana yake ni kugeuka kutoka kwa Bwana na manabii Wake.• Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa

Ajili ya Watu Binafsi na Familia unapendekeza kutafakari baadhi ya sitiari ambazo Isaya alitumia kuelezea matokeo ya kugeuka kutoka kwa Bwana na kuwakataa manabii Wake . Waalike washiriki wa darasa kushiriki kile walichojifunza . Au unaweza kuwaalika wao kila mmoja kurejelea mojawapo ya vifungu hivi: Isaya 24:1–5; 28:7–8; 29:7–10; 30:8–14 . Kulingana na kile ambacho wamesoma, wanaweza kukamilisha sentensi hii: Kama tukigeuka kutoka kwa Bwana,

Kijis

itu K

itaka

tifu,

na

Bren

t Bor

up

sePTemBa 12–18

76

sisi ni kama .  .  .” Je, tunaweza kufanya nini ili kubakia waaminifu kwa Bwana na kuepuka ukengeufu? (Ona “Nyenzo za Ziada” kwa ajili ya mapendekezo .) Je, ni kwa jinsi gani Bwana anawabariki wale wanaobakia waaminifu Kwake?

• Ili kuanzisha mjadala kuhusu mitazamo na tabia ambazo zinaweza kutuelekeza kwenye ukengeufu, unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kupekua Isaya 24:1–5; 28:1–8; 29:7–10; 30:8–14 . Waombe kutafuta vitu ambavyo watu katika nyakati za Isaya walikuwa wanafikiria na kufanya . Tengeneza nembo ya onyo ubaoni ambayo inasema Onyo: Mitazamo na tabia zifuatazo zinaweza kuongoza kwenye ukengeufu. Washiriki wa darasa wanaweza kuorodhesha ubaoni kile wanachopata katika mistari . Wape fursa kushiriki jinsi wanavyojikinga wenyewe au familia zao kutokana na ukengeufu .

ISAYA 29:13–24; 30:18–26;35

Bwana anaweza kurejesha vitu ambavyo vimepotea au kuvunjika.• Hapa kuna swali unaloweza kuandika ubaoni

ambalo litaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari Isaya 29: Je, maandishi ya Isaya yanahusiana vipi na Urejesho wa injili katika siku yetu? Wahimize kufikiria juu ya swali hili wanaposoma kimya kimya Isaya 29: 13–24 . (Kama wanahitaji msaada, wanaweza kurejelea pia vifungu kama vile: 2 Nefi 27:6–26; Joseph Smith—Historia 1:17–19, 63–65 . Baada ya kuzungumza kuhusu swali lililo ubaoni, wanaweza kujadili kwa nini “ajabu” na “mwujiza” (Isaya 29:14) ni maneno mazuri ya kuelezea Urejesho wa injili . Tunajifunza nini kuhusu Urejesho kutoka katika “Urejesho wa Utimilifu wa Injili ya Yesu Kristo: Tangazo kwa Ulimwengu la Maadhimisho ya Miaka Mia Mbili”? (ChurchofJesusChrist .org) .

• Sura ya 30 na 35 ya Isaya ina vifungu kadhaa ambavyo vinaweza kukupa mwongozo wa imani kuu katika nguvu za Bwana za kuwabariki wale wanaomgeukia Yeye . Ili kuwasaidia washiriki

wa darasa kugundua vifungu hivi, unaweza kuwaalika wajifunze mojawapo ya Isaya 30:18–26 au Isaya 35 . Waombe waelezee maneno au virai walivyovipata vinavyoweza kumsaidia mtu kumgeukia Bwana kwa ajili ya ukombozi .

Nyenzo za Ziada

Kubaki mwaminifu kwa Bwana na Kanisa Lake.Rais M . Russell Ballard alitoa ushauri wa kutusaidia kubaki waaminifu kwa Bwana na kwa Kanisa Lake:

“Tunahitaji kupata uzoefu wa uongofu endelevu kwa kuongeza imani yetu katika Yesu Kristo na uaminifu wetu kwa injili Yake maishani mwetu mwote—siyo tu mara moja, bali kila mara [ona Alma 5:56] . .  .  .

“ .  .  . Maneno ya Bwana yanapatikana katika maandiko na mafundisho ya mitume na manabii . Yanatupatia ushauri na mwongozo ambao, unapofuatwa, utakuwa kama koti la kuokoa la kiroho na utatusaidia kujua jinsi ya kushikilia kwa mikono yote miwili . .  .  .

“Pamoja na kukuza desturi ya kujisomea maandiko kibinafsi, tunahitaji kuwa kama wana wa Mosia na tujitoe wenyewe ‘kwa kusali sana, na kufunga’ [Alma 17:3]” (“Kaa Chomboni na Ushikilie!” Liahona, Nov . 2014, 90–91) .

Kuboresha Ufundishaji WetuOnyesha imani katika uwezo wa wanafunzi. Baadhi ya watu katika darasa lako wanaweza wasijiamini katika uwezo wao wa kujifunza injili. Wahakikishie tena kwamba kadiri wanavyojitahidi kujifunza, Roho mtakatifu atawafundisha. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 29–30.)

77

SEPTEMBA 19–25

Isaya 40–49“WATULIZENI MIOYO, WATU WANGU”

Baadhi ya watu wanaweza kusitasita kushiriki fikra zao darasani kwa sababu wanahisi hawajui maandiko vizuri . Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuhisi kwamba umaizi wao wa kiroho unathaminiwa?

Alika Kushiriki

Fikiria kuandika swali kama lifuatalo ubaoni: Je, Roho alikufundisha nini ulipokuwa unajifunza Isaiah 40–49? Washiriki wa darasa wangeweza kutafakari swali hili na kuandika majibu, na wachache wanaweza kushiriki fikra zao .

Fundisha Mafundisho

ISAYA 40–49

Yesu Kristo anaweza kutufariji na kutupatia matumaini.• Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa

Ajili ya Watu Binafsi na Familia unapendekeza kutafuta ujumbe wa faraja na matumaini katika Isaya 40–49 na kuorodhesha baadhi ya vifungu vya kuanzia . Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki ujumbe wo wote waliopata . Wahimize kuongea kuhusu kwa nini ujumbe huu uliweza kuwasaidia Wayahudi wakiwa utumwani na jinsi unavyoweza kutusaidia sisi leo . Ungeweza kuwaelekeza kwenye vifungu ulivyovipata katika kujifunza kwako binafsi . Je, Bwana anatutaka sisi tujue nini kuhusu Yeye? Je, Yeye hutufajiri kwa

namna gani? Unaweza kuwakumbusha washiriki wa darasa kwamba “Bwana” katika Agano la Kale humrejelea Yehova, au Yesu Kristo .

• Wimbo “How Firm a Foundation” (Wimbo, na . 85) unachukua maneno ya Isaya Isaya 41:10; 43:2–5; 46:4 . Baada ya kusoma maandiko haya na kuimba aya husika za wimbo, washiriki wa darasa wanaweza kuongea kuhusu nyakati ambapo walihisi Bwana alikuwa pamoja nao na jinsi uzoefu wao ulivyowasaidia “kutoogopa .”

“atalilisha kundi lake kama mchungaji” (isaya 40:11).

ISAYA 40:1– 3, 9– 11; 43:8–13; 48: 20– 21; 49:1–9

“Ninyi ni mashahidi wangu.”• Inamaanisha nini kuwa “mashahidi” wa Bwana?

Washiriki wa darasa wanaweza kutafakari swali hili wanaposoma kifungu kimoja au zaidi kati ya vifuatavyo: Isaya 40:1–3, 9–11; 48:20–21; 49:1–9 . Maelezo katika “Nyenzo za Zaida” yanaweza pia kutoa baadhi ya majibu . Je, ni “habari njema” zipi ambazo tunashiriki kama

Yesu

Akim

pony

a Ki

pofu

, na

carl

hei

nric

h Bl

och

sePTemBa 19–25

78

mashahidi wa Bwana? Katika mistari hii ni nini hutusaidia “kutoogopa” kushiriki ushahidi wetu? (Isaya 40:9) . Washiriki wa darasa wangeweza kuongea kuhusu fursa walizonazo za kuwa mashahidi wa Bwana na ni kwa namna gani shuhuda zao zinaweza kuwabariki wengine .

• Ili kusaidia washiriki wa darasa kutumia mafundisho katika Isaya 43:8–13, ungeweza kuwaalika wao kufikiria kwamba waliitwa kuwa mashahidi na kusimama katika mashtaka mahakamani . Katika mashtaka haya, Yesu Kristo anashitakiwa kwa kudai kama ilivyoandikwa katika Isaya 43:11 . Kama tungeitwa kama mashahidi kuunga mkono madai ya Yesu (ona mstari wa10), tungetoa ushuhuda gani? Ni ushahidi gani kutoka katika maisha yetu ambao tungewasilisha?

ISAYA 48–10; 49:13–16

Bwana anaweza kututakasa kupitia mateso yetu.• Labda washiriki wa darasa wanaweza kujadiliana

jinsi maneno haya kutoka kwa Mzee Quentin L . Cook yanavyotusaidia kuelewa Isaya 48:10: “Sifa za tabia na haki ambazo hufuliwa katika tanuri la mateso hutukamilisha na kututakasa” (“Nyimbo Ambazo Hawakuweza Kuimba,” Liahona, Nov . 2011,106) . Wanaweza pia kuzungumza kuhusu jinsi “tanuri la mateso” linavyowasaidia kuwasafisha kiroho . Ni kwa jinsi gani Isaya 49:13–16 hutusaidia sisi wakati tunapoteseka? Ona pia video “The Refiner’s Fire” (ChurchofJesusChrist .org) .

Nyenzo za Ziada

Kusimama kama shahidi.Rais Margaret D . Nadauld alielezea kile inachomaanisha “kusimama kama mashahidi wa Mungu nyakati zote, na katika vitu vyote na katika mahali popote” (Mosia 18:9):

“Katika kusimama kama shahidi nyakati zote, tunaahidi kumpenda Bwana, kumheshimu Yeye nyakati zote—mchana na usiku, msimu wa jua na msimu wa baridi, wakati wa furaha na wakati wa huzuni—kumpenda Bwana na kuacha upendo uonyeshe namna tunavyoishi . .  .  .

“Kusimama kama shahidi katika nyakati zote humaanisha mambo yote —mambo makubwa, mambo madogo, katika mazungumzo yote, katika mizaha, katika michezo inayochezwa na katika vitabu tunavyosoma na muziki tunaosikiliza, katika mambo yote tunayounga mkono, katika huduma tunayotoa, katika mavazi tunayovaa, katika marafiki tulionao . .  .  .

“Hatimaye, sisi tunasema kwamba tulisimama kama shahidi katika mahali pote . Hiyo inamaanisha sio tu katika sehemu za umma bali katika sehemu za faraghani, sirini, sehemu za gizani, katika sehemu za nuru; kanisani, shuleni, nyumbani, au ndani ya magari; sehemu za milimani au sehemu za pwani; mtaani au bustanini . .  .  .

“Unapofikiria juu ya ukuu wa zawadi ya [Mwokozi] kwetu, ni kitu gani kidogo tunachoweza kumfanyia Yeye na Baba yetu wa Mbinguni ambaye alimtuma? Tunaweza kusimama kama mashahidi wa upendo Wake nyakati zote, katika vitu vyote, na katika mahali popote” (“Simama kama Shahidi,” Ensign, Mei 2000, 93, 95) .

Kuboresha Ufundishaji WetuAlika kujifunza kwa bidii. “wanafunzi hatimaye wanawajibika kwa kujifunza kwao wenyewe. Zingatia jinsi unavyoweza kuwasaidia wanafunzi kukubali na kutekeleza wajibu huu” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,29).

79

SEPTEMBA 26–OKTOBA 2

Isaya 50–57“AMEYACHUKUA MASIKITIKO YETU, AMEJITWIKA HUZUNI ZETU”

Njia muhimu zaidi ya kujiandaa kufundisha ni kusoma na kuyatafakari maandiko . Unahisi na kujifunza nini unaposoma Isaya 50–57?

Alika Kushiriki

Ili kuwachochea washiriki wa darasa kushiriki uzoefu walioupata walipokuwa wanasoma Isaya 50–57, unaweza kuandika ubaoni sentensi kama hii Imani yangu katika Yesu Kristo iliimarishwa nilipokuwa nikisoma. . . Waalike washiriki wa darasa kushiriki jinsi ambavyo wangekamilisha sentensi hii .

Fundisha Mafundisho

ISAYA 50–52

Siku za usoni ni angavu kwa watu wa Bwana.• Sisi sote tunazo nyakati ambapo tunahisi kuwa

dhahifu . Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutegemea nguvu za Bwana, ungeweza kumpatia kila mmoja kazi ya kusoma 1 Isaya 51–52 na kushiriki kile ambacho wamepata kinachoweza kumuimarisha mtu fulani ambaye anahisi kuwa dhahifu au amevunjika moyo . Unaweza pia kusema kwamba Mwokozi aliyefufuka alirudia baadhi ya maneno kwa watu katika Amerika (ona 3 Nefi 20:32–45) . Maneno ya Mwokozi katika 3 Nefi 20:30–34 yanaongeza nini kwenye uelewa wako wa lini unabii huu utatimizwa?

• Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unapendekeza kuorodhesha kila kitu ambacho Yeye aliwaalika watu Wake kufanya . Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki kile walichopata na kuongelea kuhusu kile mialiko hii inamaanisha kwao . Unaweza kutaka kufokasi kwenye mialiko katika Isaya 51:1–2, 6–8; 52:1–3, 9–11 . Je, tunaweza kutenda nini juu ya mialiko hii? Unaweza kuonyesha kwamba Mafundisho na Maagano 113:7–10 hutoa maelezo yenye kuvutia kwa Isaya 52:1–2 . Ni nini maneno haya yanaongeza kwenye uelewa wetu?

Kwa Sababu ya Upendo, na mchongaji angela johnson

ISAYA 52:13–15; 53

Yesu Kristo alijichukulia mwenyewe dhambi zetu na huzuni zetu.• Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kupiga taswira

kichwani maneno ya Isaya katika Isaya 53, unaweza kuonyesha picha kadhaa za matukio

Kuke

jeliw

a kw

a Kr

isto,

na

carl

hei

nric

h Bl

och

sePTemBa 26–OK TOBa 2

80

yanayozunguka Upatanisho wa Yesu Kristo (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na . 56–60) . Kisha ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kutafuta virai katika Isaya 53 ambavyo vinaelezea matukio kwenye picha . Maneno ya Isaya yanafundisha nini kuhusu kuteseka kwa Mwokozi kwa ajili yetu? Yanapendekeza nini kuhusu kwa nini Yeye aliteseka kwa ajili yetu? Je, mafundisho haya yanatushawishi kufanya nini?

• Ili kumwalika Roho Mtakatifu kushuhudia ukweli unaofundishwa katika Isaya 52:13–15; 53, unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kusoma mistari hii kimya kimya hali wewe unacheza wimbo kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo . Waalike washiriki wa darasa kutafuta maneno au virai katika maandiko ambavyo wanahisi ni muhimu hasa . Kisha waache washiriki kile ambacho wamepata na jinsi wanavyohisi kuhusu Mwokozi . Fikiria pia kuwaalika washiriki wa darasa kusoma Mosia 15:10–12, pale Abinadi alipoelezea ilimaanisha nini kwa kirai “mbegu yake .” Ni kwa jinsi gani hii inatusaidia kuelewa Isaya 53:10?

ISAYA 54

Yesu Kristo anatutaka sisi turejee Kwake.• Kujifunza Isaya 54 kunaweza kuwashawishi

washiriki wa darasa ambao wanajisikia kuvunjika moyo kwa sababu ya dhambi zao au udhaifu wao . Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kupekua sura ya 54 wakitafuta virai au mistari inayoonyesha jinsi gani Mwokozi anajisikia kuhusu sisi . Je, Yeye anataka sisi tujisikieje kuhusu dhambi zetu za zamani na udhaifu wetu? Je, Yeye hutaka sisi tuhisi vipi kuhusu Yeye? Wahimize washiriki wa darasa kushiriki chochote wanachojifunza kuhusu Yesu Kristo . Maelezo ya Rais Dieter F . Uchtdorf katika “Nyenzo za Ziada” yanaweza kuongezea kwenye mjadala wako .

Nyenzo za Ziada

Kwa Yesu Kristo tunaweza kuwa na matumaini.Rais Dieter F . Uchtdorf alifundisha:

“Bila kujali ni kiasi gani maisha yetu yameharibiwa . Bila kujali dhambi zetu ni nyekundu kiasi gani, uchungu mkubwa kiasi gani, wapweke kiasi gani, kutelekezwa, au kuvunjika kwa mioyo yetu . Hata wale wasio na matumaini, waliokata tamaa, ambao walisaliti uaminifu, walio salimisha heshima zao, au kumkufuru Mungu wanaweza kujengwa upya . .  .  .

“Habari za furaha za injili ni hizi: kwa sababu ya mpango wa furaha wa milele uliotolewa na Baba yetu wa Mbinguni mwenye upendo na kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, hatuwezi tu kukombolewa kutoka kwenye anguko na kurejeshwa kwenye usafi, bali tunaweza pia kuvuka mawazo ya maisha ya kidunia na kuwa warithi wa uzima wa milele na washiriki wa utukufu wa Mungu” (“Atakubeba Mabegani Mwake na Kukupeleka Nyumbani,” Liahona, Mei 2016,102) .

Kuboresha Ufundishaji WetuIshi kwa kustahili mwongozo wa Roho. Unapoishi injili kwa kustahili, unaishi ukiwa mwenye kustahili wenzi wa Roho ambaye ni mwalimu aliye bora. unapotafuta mwongozo wa Roho mtakatifu, atakupa mawazo na ushawishi kuhusu jinsi ya kutosheleza mahitaji ya wale unaowafundisha. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 5.)

81

OKTOBA 3–9

Isaya 58–66“MKOMBOZI ATAKUJA SAYUNI”

Unapojifunza mafundisho mazuri katika sura hizi, mwalike Roho akuongoze kwenye ujumbe ambao utakuwa na maana zaidi kwa washiriki wa darasa .

Alika Kushiriki

Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kuandika ubaoni marejeo ya mistari ambayo imewagusa wakati wa kujifunza kwao kwa maandiko wiki hii . Kama darasa, unaweza kisha kuangalia mistari hii na kuzungumza kuhusu ukweli unaopatikana humo . Umaizi huu unaweza kuongoza hata kwenye mazungumzo ya kina ya kanuni moja au zaidi zilizoorodheshwa hapa chini .

Fundisha Mafundisho

ISAYA 58:3–12

Mfungo huleta baraka.• Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujadili kwa

nini na jinsi Bwana ametuamuru sisi kufunga, unaweza kutengeneza safu mbili ubaoni zilizoandikwa “Hamfungi Kama Mfanyavyo Siku Hii ya Leo” na “Saumu Niliyoichagua Mimi.” Kisha washiriki wa darasa wanaweza kusoma Isaya 58:3–7, kujaza safu ya kwanza na maelezo ya jinsi Waisraeli walivyokuwa wakifunga na safu ya pili maelezo ya kufunga kama vile Bwana

anavyodhamiria . Ni kwa jinsi gani maelezo haya yanaathiri jinsi tunavyoona kufunga? Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki jinsi, katika uzoefu wao, kufunga kunavyotuongoza kwenye baraka alizoahidi Bwana katika mstari wa 8–12 .

• Baadhi ya washiriki wa darasa wanaweza kuwa walipata uzoefu katika kuelezea wengine kwa nini tunafunga . Waalike kuelezea kile wao walichosema . Ungeweza pia kumwalika mshiriki wa uaskofu kuzungumzia kuhusu jinsi matoleo ya mfungo yanavyotumika . Au unaweza kushiriki mojawapo ya mifano kutoka katika ujumbe wa Rais Henry B . Eyring “Je, Saumu Niliyoichagua, Siyo ya Namna Hii?” (Liahona, Mei 2015, 22–25) . Je, kufunga na kulipa matoleo ya mfungo husaidiaje “kuzilegeza kamba za nira” zetu wenyewe na wengine? (Isaya 58:6) .

ISAYA 61:1–3; 63:7–9

Yesu Kristo ni Mwokozi na Mkombozi wetu.• Wakati Yesu Kristo alipotangaza kwa watu

wa Nazareti kwamba Yeye alikuwa Masiya, Yeye alinukuu kutoka katika Isaya 61:1–3 (ona Luka 4:16–21; ona pia video “Jesus Declares He Is the Messiah,” ChurchofJesusChrist .org) . Labda washiriki wa darasa wangeweza kusoma Isaya 61:1–3 na kuzungumzia kuhusu kwa nini mistari hii ni maelezo mazuri ya huduma ya Mwokozi . Unaweza kuorodhesha ubaoni kila kitu ambacho Mwokozi alipakwa mafuta ili

Yesu

katik

a Si

nago

gi h

uko

Naza

reti,

by

gre

g K.

Ols

en

OK TOBa 3–9

82

kufanya na jadili kila kimoja kinamaanisha nini . Je, Mwokozi alitimizaje vipengele vya huduma Yake wakati wa maisha Yake duniani? Je, Yeye amevitimizaje katika maisha yetu?

• Washiriki wa darasa kisha wanaweza pia kusoma Isaya 63:7–9 na kushiriki jinsi Yesu Kristo alivyowabariki wao katika njia hizi .

• Isaya 61:1–3 hutumia lugha nzuri na ya kishairi kuelezea nguvu za Yesu Kristo za kukomboa kile kinachoonekana kuharibiwa . Ili kusaidia kutoa kielelezo cha mistari hii, fikiria kushiriki hadithi kuhusu kitu ambacho kilidhaniwa kupotea au kuharibika lakini kiligeuzwa kuwa kitu kizuri zaidi . Kwa mfano, tazama video “Provo City Center Temple” (ChurchofJesusChrist .org; ona pia “Nyenzo za Zaida”) au hadithi ya mwanzoni mwa ujumbe wa Rais Dieter F . Uchtdorf “Atakubeba Mabegani Mwake na Kukupeleka Nyumbani” (Liahona, Mei 2016, 101–4) . Washiriki wa darasa wanaweza kuzungumza kuhusu namna ambavyo wameona Bwana akiwapa watu kitu kizuri wakati walikuwa wanadhani maisha yao yameharibika .

ISAYA 65:17–25

Katika Ujio wa Pili, Bwana “atatengeneza mbingu mpya na dunia mpya.”• Isaya 65:17–25 huelezea hali duniani baada ya

Ujio wa Pili wa Mwokozi . Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kupitia tena mistari hii wakitafuta majibu ya maswali kama haya: Je, maisha katika “dunia mpya” yatakuwaje tofauti na maisha yalivyo katika dunia ya sasa? Unapata nini katika mistari hii ambacho kinakusababisha ufurahie?

Nyenzo za Ziada

Bwana “hatuachi katika majivu.”Baada ya kusimulia jinsi moto karibu uharibu Tabenakulo la Provo, kuwezesha kujengwa tena baadaye kama Hekalu la Provo City Center, Dada Linda S . Reeves alisema: “Mungu huruhusu tujaribiwe na kupimwa, wakati mwingine ili kufikia uwezo wetu wa juu . Tumeona maisha ya wapendwa wetu—na pengine yetu wenyewe—kistiari yakiteketezwa na tumejiuliza ni kwa nini Baba wa Mbinguni mwenye upendo na mwenye kujali angeruhusu mambo kama haya kufanyika . Lakini Yeye hatuachi katika majivu; Anasimama na mikono iliyo wazi, akitualika kwa shauku kuja Kwake .  .  .  . Yeye anajenga maisha yetu kuwa mahekalu mazuri kabisa mahali ambapo Roho Wake anaweza kukaa milele” (“Dai Baraka za Maagano Yako,” Liahona, Nov . 2013,119) .

Kuboresha Ufundishaji WetuPata kuwajua wale unaowafundisha. Kila mtu unayemfundisha ana chimbuko la kipekee, mtazamo, na jozi ya talanta. Fikiria tofauti hizi unapotafuta kuwasaidia wote katika njia ya maana na ya kukumbukwa. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 7.)

83

OKTOBA 10–16

Yeremia 1–3; 7; 16–18; 20“KABLA SIJAKUUMBA KATIKA TUMBO NALIKUJUA”

Mnapojifunza, fikiria kuhusu washiriki wa darasa lako, tafuta mwongozo wa Roho ili kujua ni ujumbe gani unaweza kuwa muhimu sana kwao .

Alika Kushiriki

Njia moja unayoweza kuhimiza kushiriki ni kuwaalika washiriki wa darasa kuandika kwenye kipande cha karatasi ukweli wa injili waliojifunza wakati wa kujifunza kwao Yeremia wiki hii . Unaweza kisha kuchukua vipande hivyo vya karatasi na chagua vichache vya kuvijadili kama darasa . Je, ni kwa jinsi gani maandishi ya Yeremia hutusaidia kuelewa ukweli huu .

Fundisha Mafundisho

YEREMIA 1:4–19

Manabii huitwa kunena neno la Bwana.• Unaweza kuanza mjadala kuhusu wito wa

Yeremia kama nabii kwa kuonyesha picha ya nabii aliye hai na kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki jinsi ambavyo wamekuja kujua kwamba yeye ameitwa na Mungu . Ungeweza pia kuwaomba kushiriki jinsi wamewasaidia wengine kujua ukweli huu muhimu . Je, ni kwa namna gani

maarifa haya yanabariki maisha yetu? Washiriki wa darasa wanaweza kuorodhesha ubaoni vitu ambavyo wamejifunza kuhusu nabii kutoka katika Yeremia 1:4–19 . Manabii katika siku yetu “wanang’oa” au “wanabomoa” nini? Ni nini wanajenga” na “kupanda”? (mstari wa 10) .

• Waalike washiriki wa darasa kushiriki kile Yeremia alichojifunza kuhusu yeye mwenyewe katika Yeremia 1:5 . Ni kwa jinsi gani maarifa haya yaliboresha huduma yake? Washiriki wa darasa wanaweza pia kusoma maelezo katika “Nyenzo za Ziada” na maandiko yafuatayo yanayounga mkono ukweli huu: Alma 13:1–4; Mafundisho na Maagano 138:53–56; Ibrahimu 3:22–23 . Ni kwa jinsi gani ukweli huu kuhusu maisha yetu kabla ya kuzaliwa unaathiri jinsi tunavyoishi maisha yetu ya duniani?

watu katika Israeli ya kale walitumia matangi kuhifadhi maji ya thamani.

Yere

mia

, na

wal

ter R

ane

OK TOBa 10 –16

84

YEREMIA 2; 7

Wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima.• Ili kuchochea mjadala kuhusu Yeremia 2:13,

unaweza kuchora ubaoni tangi la maji (bwawa kubwa chini ya ardhi) na chemichemi (kama chemichemi ya asili) . Washiriki wa darasa wanaweza kisha kusoma Yeremia 2:13 na kuzungumza kuhusu kwa nini ni bora kupata maji kutoka kwenye chemichemi kuliko kuchimba tangi la maji . Ni nini kinaweza kuwa kisawe cha kiroho cha kujenga matangi yaliyobomoka? Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kusoma mistari kutoka katika Yeremia 2 na7 na kushiriki baadhi ya njia Waisraeli walizoacha “chemichemi ya maji ya uzima” (ona kwa mfano Yeremia 2:26–28; 7:2–11) . Kwa nini “maji ya uzima” ni ishara nzuri ya kile ambacho Mwokozi hutupatia?

YEREMIA 3:14–18; 16:14–15

Bwana atawakusanya watu Wake.• Kwa sababu Yeremia alilinganisha kukusanyika

kwa Israeli kwa siku za mwisho na kukombolewa kwa Israeli kutoka Msiri kupitia Musa, unaweza kuonyesha picha ya Kutoka (ona muhtasari wa Aprili 4– 10 katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia) . Waalike washiriki wa darasa kujadili jinsi umuhimu wa Kutoka ulivyokuwa kwa Waisraeli kwa vizazi vingi . Washiriki wa darasa kisha wasome Yeremia 16:14–15 na kuzungumza kuhusu jinsi gani kukusanyika kwa Israeli katika siku za mwisho kutakavyo kuwa muhimu zaidi kwa watu wa Mungu (ona pia Yeremia 3:14–18) . Washiriki wa darasa ambao walirejelea “Tumaini la Israeli” kama sehemu ya kijifunza kwao binafsi wanaweza kushiriki kile walichojifunza kuhusu umuhimu wa kukusanyika kwa Israeli (ona Russell M . Nelson na Wendy W . Nelson, “Tumaini la Israeli” [worldwide youth devotional, Juni 3, 2018], nyongeza kwenye New Era na Ensign, Agosti 2018, 2–17, ChurchofJesusChrist .org) . Au mnaweza kupitia tena sehemu za ujumbe huo kama darasa . Je, Israeli inakusanywaje katika eneo letu?

Nyenzo za Ziada

Baba wa Mbinguni anawajua ninyi.Rais Russell M . Nelson alifundisha:

Roho yako ni chombo cha milele . Na Bwana akamwambia nabii Wake Ibrahimu: ‘Wewe ulichaguliwa kabla hujazaliwa’ (Ibrahimu 3:23] . Bwana alisema kitu kama hicho kuhusu Yeremia [ona Yeremia 1:5] na wengine wengi [ona Alma 13:2–3] . Yeye hata alisema hivyo kuhusu wewe [ona Mafundisho na Maagano 138:55–56] .

Baba yako wa Mbinguni amekujua wewe kwa muda mrefu sana . Wewe, kama mwana au binti Yake, ulichaguliwa na Yeye kuja duniani katika wakati mahususi, kuwa kiongozi katika kazi Yake kuu duniani . Wewe ulichaguliwa sio kwa sababu ya sifa zako za kimwili bali kwa sifa zako za kiroho, kama vile ushupavu, ujasiri, uaminifu wa moyo, kiu ya ukweli, njaa ya hekima, na shauku ya kuwahudumia wengine .

“Ulikuza baadhi ya sifa hizi kabla ya kuzaliwa . Nyingine unaweza kuzikuza hapa duniani kwa mwendelezo unapoendelea kuzitafuta” (“Maamuzi kwa Ajili ya Milele,” Liahona, Nov . 2013,107) .

Kuboresha Ufundishaji WetuIshi injili kwa moyo wako wote. wewe utakuja kuwa mwalimu kama Kristo unapoikumbatia injili na kuiishi kila siku ya maisha yako. Ufundishaji kama Kristo hauhitaji wewe kuwa mkamilifu—jaribu tu na endelea kujaribu. Unapofanya bidii kadiri uwezavyo na kutafuta msamaha unapokosea, unaweza kuwa mwanafunzi wa Kristo ambaye Yeye anakuhitaji wewe uwe. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 13–14.)

85

OKTOBA 17–23

Yeremia 30–33; 36; Maombolezo 1; 3“NITAGEUZA MASIKITIKO YAO KUWA FURAHA”

Tafakari misukumo uliyopokea wakati wa kujifunza kwako binafsi Yeremia na Maombolezo . Ni vifungu gani kutoka katika sura hizi unahisi vitakuwa vya muhimu zaidi kwa wale unaowafundisha?

Alika Kushiriki

Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kushiriki kile ambacho wamejifunza kutokana na kujifunza kwao maandiko, unaweza kuandika ubaoni virai kama Nimejifunza kwamba. . ., Nina ushuhuda wa. . ., au Nimepata uzoefu wa. . . Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki kitu fulani kutoka katika Yeremia au Maombolezo ili kukamilisha sentensi hizi .

Fundisha Mafundisho

YEREMIA 30–31; 33; MAOMBOLEZO 1:1–7; 3:1–5

Bwana atawatoa Israeli kutoka utumwani na kuwakusanya.• Uumbe wa matumaini katika unabii wa

Yeremia unaweza kuwapa washiriki wa darasa matumaini katika hali zao wenyewe . Labda darasa lako linaweza kujadili hali ambazo zinaweza kuwafanya watu katika siku yetu kuhisi kukosa matumaini kama vile katika nyakati za Yeremia walivyohisi (ona Yeremia 30:5; 31:15;

Maombolezo 1:1–7; 3:1–5; na nukuu katika “Nyenzo za Zaida”) . Unaweza kisha kugawa washiriki wa darasa katika vikundi vitatu na kualika kila kundi kupitia Yeremia 30; 31; na 33 kwa ajili ya ujumbe ambao unaweza kuleta matumaini kwa watu leo . Je, ni kwa jinsi gani Bwana ametusaidia kuvumilia majaribu?

YEREMIA 31:31–34; 32:37–42

“Nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.”• Kupitia tena Yeremia 31:31–34; 32:37–42

kunaweza kulisaidia darasa lako kutafakari maagano ambayo wamefanya . Njia moja ya kuhimiza mjadala kuhusu hii mistari ni kuwapa washiriki wa darasa dakika chache za kusoma mistari hiyo na kisha kuandika kwenye kipande cha karatasi swali ambalo wangependa kuuliza darasa kuhusu kile ambacho wamesoma . Kwa mfano, wanaweza kutaka kujadili kile inachomaanisha kuwa na sheria za Mungu zimeandikwa katika mioyo yetu (ona Yeremia 31:33) au jinsi maagano yanavyotusaidia kuja kumjua Bwana (ona Yeremia 31:34) . Unaweza kisha kukusanya maswali na kuchagua machache ya kujadili pamoja . Tunajifunza nini kutoka kwenye mistari hii ambacho kinatupa mwongozo wa kuwa hodari katika kushika maagano yetu?

Kilio

cha

Yere

mia

Nab

ii ku

toka

na n

a sa

nam

u ya

ku

chon

ga n

a N

azer

ene

Scho

ol

OK TOBa 17–23

86

maandiko yanaweza kutushawishi kutubu na kumgeukia Bwana.

YEREMIA 36

Maandiko yana nguvu za kutugeuza sisi kutoka kwenye uovu.• Washiriki wa darasa lako wanaweza kuwa

wamepata umaizi kuhusu maandiko walipokuwa wanajifunza Yeremia 36 nyumbani . Waalike kushiriki kile walichojifunza . Unaweza pia kuwapa washiriki wa darasa jina la mtu katika sura hii na uwaalike wasome kuhusu kile ambacho mtu huyu alifanya na neno la Mungu . Washiriki wa darasa wanaweza kujifunza maneno na matendo ya Bwana (ona mstari wa 1–3, 27–31); Yeremia (ona mstari wa 4–7,32); Baruki (ona mstari wa 4, 8–10, 14–18); Yehudi na Mfalme Yehoyakimu (ona mstari wa 20–26); na Elnathani, Delaya, na Gemaria (ona mstari wa 25) . Je, maneno na vitendo vinaonyeshaje jinsi tunavyohisi kuhusu maandiko?

Nyenzo za Ziada

Unaweza kuwa na matumaini daima.Rais M . Russell Ballard alitaja baadhi ya hali ambazo zinaweza kusababisha wengine wapoteze matumaini, na akatoa ushauri kuhusu mahali pa kupata matumaini .

Baadhi yetu tunaweza kuona maisha yetu yamejaa kukata tamaa, masikitiko, na huzuni . Wengi wanahisi kukosa matumaini kukabiliana na vurugu ambayo inaonekana kukithiri ulimwenguni . Wengine wanafadhaika juu ya wanafamilia ambao wamesombwa katika mkondo mkali, unaotanda wa maadili yaliyodorora na kushuka kwa viwango vya maadili . .  .  . Wengi hata wamejiuzulu wenyewe na kukubali uovu na ukatili wa ulimwengu usioweza kurekebishika . Wamekosa matumaini . .  .  .

“ .  .  . Wengine miongoni mwetu wamepoteza matumaini yote kwa sababu ya dhambi na uvunjaji wa sheria . Mtu anaweza kuwa amejiingiza sana katika njia za ulimwengu kiasi kwamba yeye haoni njia ya kuponyokea na kupoteza matumaini yote . Maombi yangu kwa wote ambao wametumbukia katika huu mtego wa adui ni kamwe wasikate tamaa! Bila kujali jinsi mambo yanavyokatisha tamaa au jinsi yanavyoelekea kuwa mabaya, tafadhali niamini, unaweza daima kuwa na matumaini . Daima” (“Shangwe ya Tumaini Inatimizwa,” Ensign, Nov . 1992, 31–32) .

“Kwa urahisi, tumaini letu moja kwa ajili ya usalama wa kiroho nyakati hizi za msukosuko ni kugeuza akili zetu na mioyo yetu kwa Yesu Kristo . .  .  . Imani katika Mungu na katika Mwanawe, Yesu Kristo, ni muhimu kabisa kwetu ili kudumisha msimamo sambamba kupitia nyakati za majaribu na dhiki” (“Shangwe ya Tumaini Inatimizwa,”32) .

Kuboresha Ufundishaji WetuMfuate Roho. huwezi kutabiri jinsi kila somo litakavyokwenda, lakini sikiliza ushawishi wa Roho, Yeye ataongoza somo. iwapo mmejiandaa kiroho, Bwana atawapatia “katika saa ile ile, kile mtakachosema” (mafundisho na maagano 100:6; ona pia Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 10).

87

OKTOBA 24–30

Ezekieli 1–3; 33–34; 36–37; 47“NAMI NITAWAPA NINYI MOYO MPYA”

Maneno ya Ezekieli yanahifadhiwa na Bwana kwa kusudi la hekima na yanaweza kuwabariki washiriki wa darasa lako . Tafakari hili unapojifunza maandishi ya Ezekieli wiki hii .

Alika Kushiriki

Watu ambao walimsikia Ezekieli waliona maneno yake yalikuwa ya ‘kupendeza” na “kufurahisha,” “lakini hawakuyatenda” (ona Ezekieli 33:30–33) . Washiriki wa darasa pia wanaweza kushiriki kifungu walichokipata katika maandishi ya Ezekieli kilichowapa mwongozo wafanye kitu fulani .

Fundisha Mafundisho

EZEKIELI 34

Bwana anatualika tuwalishe Kondoo Wake.Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kupata maana ya kibinafsi katika Ezekieli 34, unaweza kuandika ubaoni hali ambazo wanaweza kukabiliwa nazo, kama vile kujiandaa kuhudumu misheni, kulea watoto, au kupokea kazi ya kutumikia. Washiriki wa darasa wanaweza kuchagua moja na kutafakari wanaposoma kimya kimya Ezekieli 34: 1–10 . Waalike washiriki ni ushauri gani kulingana na mistari hii wanaoweza kutoa kwa mtu aliye katika hali waliochagua . Inamaanisha nini kujilisha wenyewe badala ya kondoo wa Bwana? Ni kwa jinsi gani wachungaji ni kama Mwokozi? (mstari wa 11–16) .

Unaweza kuhisi kupata mwongozo wa kuuliza maswali ambayo yanawasaidia washiriki wa darasa kutafakari sitiari katika Ezekieli 34:11–31 . Kwa mfano, ni nini kinaweza kuwakilisha “malisho mema” na “zizi jema” katika mstari wa 14? Ni nini tofauti kati ya kondoo “waliopotea” na “waliofukuzwa”? (mstari wa 16) . Ni jinsi gani Mwokozi anawaokoa aina zote za kondoo? Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki ishara zingine wanazoweza kupata katika hii mistari na kuzungumza kuhusu kitu ambacho hizi ishara zinawafundisha kuhusu Yesu Kristo .

EZEKIELI 37

Bwana anawakusanya watu Wake na kuwapa maisha mapya.• Kusoma Ezekieli 37 na kufikiria kuhusu ahadi

za Bwana kuhusu kukusanyika kwa Israeli kunaweza kutupa umaizi kuhusu kukusanya kunamaanisha nini na jinsi sisi tunavyoweza kushiriki katika hilo . Ili kuwasaidia kupata umaizi huu ungeweza kuandika kwenye ubao maswali kama Bwana anajaribu kutimiza nini kupitia ukusanyaji wa Israeli? Je, Yeye anatimizaje hilo? Unaweza kisha kuomba nusu ya darasa kusoma Ezekieli 37:1–14 na ile nusu nyingine kusoma Ezekieli 37:15–28 wanapotafuta umaizi hivi vifungu viwili vinaweza kutoa kwa maswali ubaoni . Inaweza kusaidia kueleza kwamba vijiti vya Yusufu na Yuda vilivyotajwa katika mstari wa 16–19 vinawakilisha Kitabu cha Mormoni na Biblia . Washiriki wa darasa wanaposhiriki

Njoo

, Uni

fuat

e, na

Sco

tt Su

mne

r

OK TOBa 24–30

88

majibu yao, wahimize kuzungumza kuhusu kazi yao katika kukusanywa kwa Israeli katika siku za mwisho .

ezekieli aliona ono la mto ukitiririka kutoka kwenye hekalu na kuponya Bahari ya chumvi.

EZEKIELI 47:1–12.

Hekalu huleta uponyaji wa kiroho.• Picha zinaweza kuwasaidia washiriki wa darasa

kuelewa ono lililoelezewa katika Ezekieli 47:1–12 . Kwa mfano, unaweza kuonesha picha ya hekalu, mto, jangwa, na Bahari ya Chumvi (ona picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia na picha za Biblia, na . 3, “Jangwa la Yudea”) . Inaweza kusaidia kuelezea kwamba Bahari ya Chumvi ina chumvi nyingi sana kiasi kwamba samaki na mimea haiwezi kuishi ndani yake . Washiriki wa darasa wanaweza kusoma mstari wa 1–12 na kushiriki ni nini kinachowavutia wao kuhusu maji yaliyoelezwa katika ono (ona pia Ufunuo 22:1 na kauli katika “Nyenzo za Ziada”) . Wanaweza pia kuchora picha za ono la Ezekieli . Je, maji ni ishara ya nini? Je, miti iliyoelezewa katika mstari wa 12 inawakilisha nini? Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki jinsi hekalu na baraka zake zimewaletea maisha ya kiroho na uponyaji .

Nyenzo za Ziada

Baraka za hekalu zinaweza kutuponya.Kurejelea maji yakitirirka kutoka hekaluni katika ono la Ezekieli (ona Ezekieli 47:1–12), Mzee Dale G . Renlund alisema:

Sifa mbili za maji zinazostahili kukumbukwa . Kwanza, ingawa mto mdogo haukuwa na kijito, ulikua na kuwa mto mkubwa, ukawa mpana na wenye kina kirefu kadiri ulivyotiririka . Kitu kama hicho hutokea kwa baraka ambazo hutiririka kutoka hekaluni wakati watu binafsi wanapounganishwa kama familia . Makuzi ya maana hutokea kwenda nyuma na mbele kupitia vizazi wakati ibada za kuunganisha zinapounganisha familia pamoja .

“Pili, mto ulihuisha kila kitu ambacho ulikigusa . Baraka za hekaluni vile vile zina nguvu za kushangaza za kuponya . Baraka za hekalu zinaweza kuponya mioyo na maisha na familia” (“Historia ya Familia na Kazi ya hekalu: Kuunganisha na Uponyaji,” Liahona, Mei 2018, 47–48; ona pia video “And the River Will Grow,” ChurchofJesusChrist .org) .

Kuboresha Ufundishaji WetuWasaidie wengine kumpokea Roho. mara nyingine walimu wanaweza kujaribiwa kufikiria ya kwamba ni elimu yao au mbinu zao au tabia zao zinazowashawishi wale wanaowafundisha. . . . Kusudi lako kama mwalimu sio kuwasilisha somo linalovutia bali ni kuwasaidia wengine kupokea ushawishi wa Roho mtakatifu” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 10).

89

OKTOBA 31–NOVEMBA 6

Danieli 1–6“HAKUNA MUNGU MWINGINE AWEZAYE KUOKOA”

Washiriki wengi wa darasa watakuwa wanafahamu baadhi ya hadithi zilizoko katika kitabu cha Danieli . Unapojifunza na kujiandaa kufundisha, tafuta mwongozo kutoka kwa Roho kuhusu jinsi unavyoweza kuwasaidia washiriki wa darasa kupata maana binafsi kutoka katika sura hizi .

Alika Kushiriki

Inaweza kuwa msaada kwa washiriki wa darasa kuelezea jinsi kujifunza kwao injili kibinafsi na kifamilia kunavyoendelea . Wakati washiriki wa darasa wanaposhiriki umaizi kuhusu kitu ambacho Roho amewafundisha wiki hii, unaweza kuwauliza kile walichokuwa wakifanya wakati wakijifunza ambacho kiliwaongoza kwenye umaizi huo .

Fundisha MafundishoDANIELI 1; 3; 6

Tunaweza kumtumaini Bwana wakati imani yetu inapojaribiwa.• Kuanza mjadala kuhusu jinsi Danieli, Shadraka,

Meshaki, na Abednego walivyoonyesha imani katika Bwana, unaweza kuwaomba washiriki wa darasa wachache kufanya muhtasari wa changamoto ambazo wanaume hawa wanne walikabiliana nazo, zilizoelezewa katika Danieli 1, 3, na6 . Kwa nini ingeweza kuwa vigumu kuwa waaminifu katika hizi hali? Ni hali gani mnazokabiliana nazo ambazo huijaribu imani yetu? Washiriki wa darasa wangeweza

kupekua Danieli 1:10–13; 3:15–18; 6:10, kutafuta jinsi hawa wanaume wanne walivyojibu changamoto zao . Je, ni kwa jinsi gani mifano yao inaweza kutusaidia katika jitihada zetu za kuwa wanafunzi waaminifu wa Yesu Kristo?

• Wengi wetu, kama vile Danieli na rafiki zake, tunahisi shinikizo la kushusha viwango vyetu . Nini baadhi ya vyanzo vya shinikizo hili maishani mwetu? Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza kutokana na mfano wa Danieli na rafiki zake, unaweza kugawa darasa katika makundi matatu na kupangia kila kundi kupitia mojawapo ya sura zifuatazo: Danieli 1, 3, au6 . Ni kwa jinsi gani Bwana aliwabariki Danieli, Shadraka, Meshaki, na Abednego wakati walipochagua kuwa waaminifu licha ya shinikizo walilokabiliana nalo? Kila kundi lingeweza kushiriki pamoja na darasa kile walichogundua . Washiriki wa darasa wanaweza kisha kushauriana pamoja kuhusu jinsi ya kubaki waaminifu licha ya shinikizo la kijamii au aina nyingine ya shinikizo . Wanaweza pia kujadili umuhimu wa kutafuta marafiki wema ambao watatusaidia katika viwango vyetu .

DANIELI 2

Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni ufalme wa Mungu duniani.• Kujadili Danieli 2 kunaweza kuwasaidia washiriki

wa darasa lako kuelewa jinsi Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho linavyotimiza hatima yake kama jiwe lililotolewa unabii

Dani

eli A

nata

fsiri

Ndo

to y

a Ne

buka

drez

a, n

a g

rant

Rom

ney

Claw

son

OK TOBa 31–nOvemBa 6

90

“lililochongwa mlimani” (mstari wa 45) . Kuanza, mnaweza kupitia kama darasa maelezo ya Danieli na tafsiri ya ndoto ya Nebukadreza, inayopatikana katika Danieli 2:31–45 . Kisha unaweza kuonyesha picha ya jiwe (au uchore moja ubaoni) . Waalike washiriki wa darasa kushiriki kile walichojifunza kuhusu ufalme wa Mungu kwa kuyalinganisha na maelezo ya jiwe katika Danieli 2:34–35, 44–45 . Pengine washiriki wa darasa wanajua baadhi ya historia ya Kanisa katika eneo lenu ambayo wanaweza kuelezea . Ni kwa jinsi gani tumeuona unabii wa Danieli ukitimia katika maisha yetu binafsi?

DANIELI 2:1–30

Kupokea ufunuo kunahitaji maandalizi ya kiroho.• Labda washiriki wa darasa wangeweza kufaidika

kutokana na kujifunza jinsi Danieli alivyojiandaa mwenyewe kupokea ufunuo uliohitajika kuelezea na kutafsiri ndoto ya Nebukadreza . Unaweza kuanza kwa kuwaomba washiriki wa darasa kurejelea Danieli 2:1–15 na kisha kueleza jinsi ambavyo wangejisikia kama wangejikuta wenyewe katika hali ya Danieli . Waalike wapekue Danieli 2:16–18 ili kujifunza kile ambacho Danieli alifanya . Je, tunajifunza nini kutoka katika Danieli 1:17 kuhusu jinsi Mungu alivyomwandaa Danieli? Je, tunaweza kujifunza nini kutoka kwa Danieli ambacho kinaweza kutusaidia tunapotafuta ufunuo wa binafsi? Je, tunaweza kujifunza nini kutokana na maneno na vitendo vya Danieli baada ya kupokea msaada wa Bwana? (ona Danieli 2:20–30) .

Kielelezo cha Danieli na rafiki zake wakikataa chakula cha mfalme, na Brian call

DANIELI 3

Wakati matokeo hayana uhakika, tunaweza bado kuchagua imani.• Tukio hili la Shadraka, Meshaki, na Abednego

linalopitikana katika Danieli 3 linaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa zaidi kile ilichomaanisha kuwa na imani katika Yesu Kristo . Unaweza kuwaalika washirki wa darasa kufanya muhtasari wa changamoto Shadraka, Meshaki, na Abednego waliyokabiliana nayo (ona Danieli 3:1–12) na kujadili jinsi wanavyoweza kujibu (ona Danieli 3:13–18) . Je, tunajifunza nini kuhusu imani kutokana na majibu ya wanaume hawa? Unaweza kuandika ubaoni virai Mungu wetu aweza. . . na Bali kama si hivyo. . . kutoka mstari wa 17–18 . Washiriki wa darasa wanaweza kupendekeza jinsi wanavyoweza kujaza nafasi zilizo wazi kwa hali ambazo wangeweza kukabiliana nazo . Kwa mfano, wanaweza kupendekeza “Mungu aweza kujibu maswali yetu yote” na “Lakini kama si hivyo, kwa subira nitamtumaini Yeye .” Washiriki wa darasa wanaposhiriki mifano, wahimize kuzungumza kuhusu jinsi gani Mwokozi hutusaidia na kutuimarisha hata wakati sisi hatujui jinsi matokeo ya mambo yatavyokuwa .

Kuboresha Ufundishaji WetuTumia ishara za kuonekana kwa macho. “Sanaa, ikiwa ni pamoja na picha, video, na maigizo, vinaweza kusaidia ushirikishwaji wa wanafunzi—hasa wale wanaojifunza kwa kuona—na tengeneza matukio ya kimaandiko kuwa ya kukumbukwa (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 22).

91

NOVEMBA 7–13

Hosea 1–6; 10–14; Yoeli“NITAWAPENDA KWA UKUNJUFU WA MOYO”

Unapojifunza na kujiandaa wiki hii, fikiria ni upi kati ya ujumbe mzuri na wenye kuinua kutoka katika kitabu cha Hosea na Yoeli ungeweza kukidhi mahitaji ya wale unaowafundisha .

Alika Kushiriki

Ili kuwahimiza washiriki wa darasa kushiriki kile walichojifunza wiki hii, unaweza kuwaalika waandike ubaoni neno au kirai ambacho kimewavutia wakati wa kujifunza kwao . Kisha wanaweza kuelezea kwa nini neno au kirai hicho kina maana kwao . Maneno hayo na virai hivyo vinaweza kusaidia kuongoza mjadala wako wote .

Fundisha Mafundisho

HOSEA 1– 3; 14

Bwana daima hutualika sisi turudi Kwake.• Ungeweza kuanza mjadala wa Hosea 1–3 kwa

kuandika ndoa ubaoni na kuwaomba washiriki wa darasa kuorodhesha maneno ambayo wanayahusisha na ndoa . Ni kwa jinsi gani kufanya agano na Bwana ni kama kuingia katika ndoa? Ni kwa jinsi gani kuvunja agano hilo ni kama kutokuwa mwaminifu kwa mwenzi? (Ona Hosea 2:5–7, 13) . Kisha darasa linaweza

kuzungumza kuhusu jinsi uhusiano katika Hosea na Gomeri huashiria uhusiano kati ya Bwana na watu Wake . Ni nini Hosea 2:14–23 na Hosea 14 zinatufundisha sisi kuhusu upendo na rehema ya Bwana? Je, ni kwa jinsi gani sisi tunaonyesha upendo na uaminifu wetu Kwake?

• Hosea 14 huelezea ahadi nyingi nzuri Bwana alizofanya kwa nyumba ya Israeli kama wangerudi Kwake . Labda washiriki wa darasa wanaweza kupekua sura hii wakitafuta ahadi hizi . Bwana alisema Yeye angefanya nini? Yawezekana kirai hiki “nawapenda kwa ukunjufu wa moyo” kina maana gani (mstari wa 4) . Je, isitiari ya mmea katika mstari wa 5–8 inatufundisha nini kuhusu baraka za Bwana kwetu sisi, ikijumuisha baraka za toba?

gomeri mwenye dhambi, ambaye huwakilisha Israeli, alipewa ukombozi na Bwana. Kielelezo na Deb minnard, leseni kutoka kwa goodsalt.com

nOvemBa 7–13

92

HOSEA 6:6; YOELI 2:12–13

Uchaji Mungu lazima usikike kwa ndani, hauonyeshwi nje pekee yake.• Hosea 6:6 na Yoeli 2:12–13 hurejelea dhabihu ya

mnyama na kuchana nguo kama ishara ya majuto . Hali desturi kama hizo inawezekana kuwa si za kawaida leo, mistari hii inaweza kutuongoza kwenye mjadala kuhusu kitu kilicho muhimu zaidi kwa Bwana . Mnaweza kusoma pamoja Hosea 6:6 na kujadili yawezekana mstari huu unamaanisha nini . Alika baadhi ya washiriki wa darasa kusoma Mathayo 9:10–13 na wengine kusoma Mathayo 12:1–8 . Kisha washiriki wa darasa wanaweza kufundishana jinsi matukio haya katika huduma ya Mwokozi yanatusaidia kuelewa kanuni inayofundishwa katika Hosea 6: 6 . Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kuishi kanuni hii katika siku yetu?

Mnaweza pia kusoma kwa pamoja Yoeli 2:12–13 na mjadili inamaana gani kurarua mioyo yetu na si mavazi yetu tu . Tunajifunza nini kutoka kwenye mistari hii kuhusu kile inachomaanisha kuwa wanafunzi wa kweli Yesu Kristo?

YOELI 2

“Nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili”• Ili kuanza mjadala wa Yoeli 2, unaweza kushiriki

pamoja na darasa kile ambacho Moroni alisema kuhusu unabii huu wakati alipomtembelea Joseph Smith katika mwaka wa 1823 (ona Joseph Smith—Historia 1:41) . Washiriki wa darasa wanaweza kuelezea jinsi wanavyohisi unabii katika Yoeli 2:28–32 unavyotimizwa katika siku yetu . Unaweza pia kujadili jinsi maneno ya Mzee David A . Bednar katika “Nyenzo za Ziada” yanavyohusiana na unabii wa Yoeli . Washiriki wa darasa wangeweza kujadili kile inachomaanisha kwao kuhisi mmiminiko wa Roho Mtakatifu katika maisha yao ya kila siku, Ni nini tunaweza kufanya kama tunahisi hatupokei mmiminiko kama huo? Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia “wana [wetu] na mabinti [zetu] kuupokea? (mstari wa 28) .

Nyenzo za Ziada

“Tunaweza kumtegemea Roho Mtakatifu kutuongoza.”Mzee David A . Bednar alifundisha:

“Mara nyingi tunafanya iwe vigumu kupokea ufunuo binafsi . Kwa kusema hilo, ninamaanisha, ahadi ya agano ni kwamba tunapoheshimu maagano yetu, tunaweza daima kuwa na Roho Mtakatifu kama mwenzi wetu wa kudumu . Tunaongea juu yake na tunachukulia kama kusikia sauti ya Bwana kupitia Roho Wake ni tukio la nadra . .  .  . [Roho] anapaswa kuwa pamoja nasi nyakati zote . Sio kila sekunde, lakini kama mtu anajitahidi vizuri awezavyo—hauhitaji kuwa mkamilifu—lakini kama wewe na mimi tunajitahidi tuwezavyo na hatutendi dhambi nzito, basi tunaweza kutegemea Roho Mtakatifu kutuongoza .

“ .  .  . Tunaonekana kuamini kwamba Roho Mtakatifu ni jambo la kidrama na kubwa na la ghafla, ilhali ni tulivu na dogo na huongezeka kidogo kidogo kwa muda . Hauhitajiki kutambua kwamba unapokea ufunuo ule muda ambapo unapokea ufunuo” (“Mzee David A . Bednar –Majadiliano” [ jioni pamoja na Kiongozi Mkuu mwenye Mamlaka, Feb .7, 2020], broadcasts .ChurchofJesusChrist .org) .

Kuboresha Ufundishaji WetuKuwa mwenye kukaribisha. wanafunzi wanaweza kujua kwamba unawajali na unajali ukuaji wao wa kiroho. njia moja ya kuwaonyesha hili ni kuwasalimu kwa moyo mkunjufu wanapowasili darasani. (Ona Kufundisha katika njia ya Mwokozi, 15.)

93

NOVEMBA 14–20

Amosi; Obadia“MTAFUTENI BWANA, NANYI MTAISHI”

Unapojifunza Amosi na Obadia, karibisha misukumo kuhusu kile unachopaswa kuwafundisha washiriki wa darasa lako . Andika mawazo haya, na utafute fursa za kuyashiriki katika darasa lako la Jumapili .

Alika Kushiriki

Kama vile tu Amosi na Obadia walivyowaonya watu wa siku zao, maneno yao pia yanatoa onyo kwetu leo . Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki mafundisho kutoka kwa Amosi na Obadia ambayo yanafaa kwetu .

Fundisha Mafundisho

AMOSI 3:7–8; 7:10–15

Bwana hufunua ukweli kupitia kwa manabii Wake.• Waalike washiriki wa darasa kushiriki ukweli

kuhusu manabii ambao wao waliupata katika kujifunza kwao binafsi au kama familia kwa Amosi 3 and Amosi 7 . Unaweza kuorodhesha majibu yao ubaoni . Ni ukweli gani mwingine kuhusu manabii tunaoujua? (Kwa mawazo zaidi, ona makala ya Mada za Injili, “Manabii,” [topics .ChurchofJesusChrist .org] .) Wahimize washiriki wa darasa kadhaa kushiriki jinsi walivyopokea ushuhuda wao wa kazi muhimu ya manabii katika mpango wa Mungu .

• Je, tunawezaje kumwelezea rafiki kwa nini ni muhimu kuwa na nabii katika siku yetu? Unaweza kuorodhesha ubaoni maswali ambayo mtu fulani ambaye si muumini wa Kanisa angeweza kuuliza kuhusu manabii . Je, tunawezaje kujibu baadhi ya maswali haya tukitumia Amosi 3:7–8 na 7:10–15?

• Kama sehemu ya mjadala wenu kuhusu manabii, ungeweza kushiriki mojawapo ya video zifuatazo: “We Need Living Prophets” or “Words of the Prophets” (ChurchofJesusChrist .org) . Je, ni kwa jinsi gani manabii wa siku za mwisho hutusaidia kusogea karibu na Yesu Kristo?

AMOSI 5; 8:11–12

Ukengeufu ni kama njaa ya kusikia maneno ya Bwana.• Ili kuanza mazungumzo kuhusu njaa Amosi

aliyoelezea katika Amosi 8:11–12, ungeweza kupata msaada kwa kifupi kupitia tena hali ya kiroho ya watu aliokuwa akiwahubiria . Je, ni kwa namna gani Waisraeli waligeuka kutoka kwa Bwana? (ona, kwa mfano, Amosi 2:6–8; 5:11–12) . Kwa nini itakuwa msaada kujua kuhusu kuanguka kwao? Washiriki wa darasa wanaweza kisha kusoma Amosi 8:11–12 na kuzungumza kuhusu kwa nini “njaa” na “kiu” ni maneno mazuri ya kuelezea hali ya wale wanaogeuka kutoka kwa Bwana . Washiriki wa darasa wanaweza pia kupekua Amosi 5

Mka

te w

a Uz

ima,

na

Chris

You

ng

nOvemBa 14–20

94

kutafuta mistari ambayo inaweza kutusaidia kuepuka ukengeufu katika maisha yetu (ona, kwa mfano, mstari wa 4, 11–12, 14–15, 25–26) .

• Kuelewa njaa ya kiroho ambayo huandamana na ukengeufu hutusaidia kuelewa karamu ya kiroho tunayofurahia kwa sababu ya Urejesho . Ungeweza kuandika maswali machache kuhusu Ukengeufu na Urejesho ubaoni, kama vile Kwa nini kulikuwa na Ukengeufu? Ni athari gani Ukengeufu ulileta kwa watoto wa Mungu’? Ni athari gani Urejesho ulileta? Wahimize washiriki wa darasa kupata majibu ya maswali haya na mengine wakitumia nyenzo zifuatazo: “Ujumbe wa Urejesho wa Injili ya Yesu Kristo” katika sura ya 3 ya Hubiri Injili Yangu ([2019], 36–39); makala ya Mada za Injili “Ukengeufu” (topics .ChurchofJesusChrist .org); video “The Great Apostasy” (ChurchofJesusChrist .org); na dondoo katika “Nyenzo za Ziada .” Waalike washiriki wa darasa kuzungumza kuhusu kweli zilizorejeshwa katika siku yetu ambazo hasa ni muhimu kwao .

tunaweza kuwa waokozi juu ya mlima Sayuni kwa kufanya kazi ya hekaluni na historia ya familia.

OBADIA 1:21.

“Waokozi watakwea juu ya Mlima Sayuni.”• Kwa nini kirai “waokozi .  .  . mlima Sayuni”

(Obadia 1:21) ni maelezo mazuri kwetu wakati tunapofanya kazi ya hekaluni na historia ya familia . Ni kwa jinsi gani kazi tunayofanya kwa niaba ya mababu zetu katika hekalu inatusaidia kuhisi kuwa karibu na Mwokozi Yesu Kristo?

Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki matukio ya hivi karibuni waliyopata wakati wakifanya kazi ya hekaluni na historia ya familia .

Nyenzo za Ziada

Masomo kutoka zamani.Rais M . Russell Ballard alifundisha:

“Katika kipindi kifupi cha miaka kinachoshughulikia Agano Jipya, .  .  . watu waligeuka dhidi ya Kristo na Mitume Wake . Anguko lilikuwa kubwa sana hata tumekuja kulijua kama Ukengeufu Mkuu, ambao ulisababisha karne za kudorora kiroho na ujinga inayoitwa Miaka ya Giza .

.  .  . Baba wa Mbinguni anawapenda watoto Wake wote, na Yeye anataka wao wote kuwa na baraka za injili katika maisha yao . Nuru ya kiroho haijapotea kwa sababu Mungu hugeuza mgongo Wake kwa watoto Wake . Badala yake, giza la kiroho hutokea wakati watoto Wake wanapogeuzia Yeye migongo yao kwa ujumla wao . Ni matokeo ya asili ya chaguzi mbaya zilizofanywa na watu binafsi, jumuiya, nchi na ustaraabu wote . Hii imethibitishwa tena na tena kote katika nyakati zote . Mojawapo ya masomo makuu ya mpangilio huu wa kihistoria ni kwamba chaguzi zetu, zote kama watu binafsi na kwa ujumla wote, huleta matokeo ya kiroho kwetu wenyewe na vizazi vyetu” (“Kujifunza Masomo ya Zamani,” Liahona, Mei 2009, 32) .

Kuboresha Ufundishaji WetuKuwasaidia wanafunzi kumtambua Roho Mtakatifu. “Kama unavyoshawishiwa na Roho mtakatifu, waulize wanafunzi wanajisikiaje na wanajisikia kushawishika kufanya nini. Wasaidie kuhusisha hisia zao za kiroho na ushawishi wa Roho mtakatifu” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 11).

95

NOVEMBA 21–27

Yona; Mika“YEYE HUFURAHIA REHEMA”

Uongofu wa kudumu unahitaji zaidi ya somo la kuvutia la Shule ya Jumapili wiki baada wiki . Wahimize washiriki wa darasa kutafuta uzoefu binafsi wa kiroho kote katika maisha yao .

Alika Kushiriki

Fikiria kuandika virai kama vifuatavyo ubaoni: Ukweli niliokumbushwa, Kitu kipya nilichojifunza, na Kitu ambacho ningependa kujifunza zaidi. Wape washiriki wa darasa muda kupitia kile walichojifunza katika Yona na Mika ambacho kinahusiana na mojawapo ya vifungu vya ubaoni .

Fundisha Mafundisho

YONA 1–4; MIKA 7:18–19

Bwana ni mwenye rehema kwa wote wanaomgeukia Yeye.Kukumbusha darasa lako rehema za Bwana kunaweza kuwasaidia wao kuhisi upendo Wake kwa ajili yao na kuwaongoza kutubu . Unaweza kualika darasa kusoma Mika 7:18–19 na kuorodhesha ubaoni baadhi ya matukio kutoka katika Yona 1–4 ambayo yanaonyesha Bwana anavyofurahia katika

rehema . Ni uzoefu gani mwingine wa rehema za Bwana tunaweza kushiriki—kutoka katika maandiko au maisha yetu wenyewe?

Kupata uzoefu wa rehema za Bwana kunaweza kutuongoza kuwa wenye rehema zaidi . Hapa kuna wazo moja ambalo linaweza kuwasaidia washiriki wa darasa lako kujifunza kuhusu rehema kutoka katika kitabu cha Yona . Unaweza kuandika swali kama hili ubaoni: Ni nini rehema za Mungu, kama ilivyoonyeshwa katika Yona 1–4, kinaweza kunifundisha kuhusu kuwa na mwenye rehema zaidi? Kila mshiriki wa darasa anaweza kuchagua sura moja ya kurejelea na kutafuta majibu ya swali hili . Wape washiriki wa darasa muda wa kutafakari juu ya nafasi walizonazo za kubadilisha mitazamo ya kuhukumu na badala yake kuwa wenye rehema kwa wao wenyewe au wengine .

Tunaweza kushiriki injili pamoja na watoto wa mungu.

Yona

kwe

nye

Ufuk

oni w

a Ni

nawi

, na

dan

iel

a. l

ewis

nOvemBa 21–27

96

YONA1; 3–4

Watoto wote wa Mungu wanahitaji kusikia injili.• Njia moja ya kupata masomo kutoka katika

hadithi ya Yona ni kuilinganisha na matukio ya wamisionari katika Kitabu cha Mormoni . Fikiria kutengeneza safu mbili ubaoni zenye vichwa Yona na Alma na wana wa Mosia. Alika darasa kutofautisha mtazamo wa Yona kuhusu kuwafundisha watu wa Ninawi (ona Yona1; 3–4) na mtazamo wa wana wa Mosia kuhusu kuwafundisha Walamani (ona Mosia 28:1–5; Alma 17:23–25) . Tunajifunza nini kutokana na zoezi hili kuhusu kushiriki injili na watoto wote wa Mungu?

• Kama Yona, wengi wetu tunaweza kujisikia kusita kuwaalika wengine kumgeukia Bwana . Ni nini baadhi ya sababu zilizomfanya Yona atoroke wito wake wa kuwaonya watu wa Ninawi? Kwa nini wakati mwingine tunasita kushiriki injili? Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki njia ambazo Bwana amewasaidia kushinda kusita kwao . Ushauri wa Henry B . Eyring katika “Nyenzo za Ziada” ungewasaidia washiriki wa darasa kutambua kanuni ambazo zinaweza kutia nguvu juhudi zetu za kushiriki injili .

MIKA 6:6–8

“Bwana anataka nini kwako?• Mika 6:6–7 inataja vipengele kadhaa vya kanuni

za ibada za Uyahudi ya kale . Lakini vitu fulani ni muhimu zaidi kwa Mungu kuliko kanuni za kuonyesha nje . Waalike washiriki wa darasa kutafuta vitu hivyo muhimu katika mstari wa 8 . Labda washiriki wa darasa wangeweza kutambua virai muhimu na kujadili kitu ambacho kila kirai kinamaanisha . Kisha wanaweza kuchagua virai wavipendavyo, watafute maandiko yanayohusiana katika Mwongozo wa Maandiko au wimbo unaohusiana katika kitabu cha nyimbo, na kuelezea kile walichojifunza . Kwa nini kanuni hizi ni muhimu kwa Bwana?

Nyenzo za Ziada

Upendo, mfano, na ushuhuda.Baada ya kujadili onyo la Yona kwa watu wa Ninawi, Rais Henry B . Eyring alisimulia tukio ambalo kwalo mama yake alimpatia onyo .

“Mimi bado nakumbuka mama yangu akiongea kwa sauti laini Jumamosi moja wakati wa alasiri ambapo, kama mvulana mdogo, nilimwomba ruhusa ya kufanya kitu nilichofikiri kilikuwa sahihi na cha kufaa na ambacho yeye alijua kilikuwa hatari . Mimi bado ninashangazwa na nguvu alizopewa, ninaamini kutoka kwa Bwana, kunigeuza kwa maneno machache tu . Ninavyoyakumbuka, yalikuwa: Eeh, nadhania wewe ungeweza fanya hivyo . Lakini chaguo ni lako .’ Onyo la pekee lilikuwa katika msisitizo alioweka kwa maneno ungeweza fanya na chaguo. Bado hiyo ilikuwa ya kutosha kwangu .

“Nguvu zake za kuonya kwa maneno machache tu zilichipua kutoka kwenye vitu vitatu mimi nilivyojua kumhusu yeye . Kwanza, nilijua ananipenda . Pili, nilijua yeye alikuwa tayari ameshafanya kile alichokuwa anataka mimi nifanye na kubarikiwa nacho . Na tatu, yeye alikuwa amewasilisha kwangu ushuhuda halisi kwamba chaguo ambalo mimi ningefanya lilikuwa muhimu kwamba Bwana angeniambia cha kufanya kama ningemwomba Yeye . Upendo, mfano, na ushuhuda: hivyo vilikuwa ndio funguo siku hiyo” (“Sauti ya Onyo,” Ensign, Nov . 1998,32) .

Kuboresha Ufundishaji WetuJiandae mwenyewe. mafundisho ya injili yenye nguvu huanza kwa kujiandaa wenyewe. Kabla ya kuandaa somo lako, fokasi juu ya kuujaza moyo wako na Roho mtakatifu kwa njia ya kujifunza na maombi yenye maana. (Ona Kufundisha Katika Njia ya Mwokozi, 12.)

97

NOVEMBA 28–DESEMBA 4

Nahumu; Habakuki; Sefania“MIENDO YAKE ILIKUWA KAMA SIKU ZA KALE”

Mfano wako kama mwanafunzi wa injili unaweza kuwa baraka kwa darasa lako . Waelezee jinsi gani Roho Mtakatifu anavyokusaidia kuelewa maandiko na kuonyesha kujiamini kwako kwamba Yeye anaweza kuwasaidia wao pia .

Alika Kushiriki

Ili kuwapa washiriki wa darasa fursa ya kuelezea umaizi kutoka katika kujifunza kwao maandiko, ungeweza kuandika Nahumu, Habakuki, na Sefania kama vichwa ubaoni . Kisha washiriki wa darasa wanaweza kuandika chini ya vichwa neno au kirai ambacho ni wazi kwao na sura na mstari ambapo wanaweza kukipata . Wape wao muda wa kuelezea kwa nini maneno haya au virai hivyo ni vya maana sana na kile ambacho Roho Mtakatifu amewafundisha .

Fundisha Mafundisho

NAHUMU 1

Bwana ni mwenye nguvu na ni mwenye rehema• Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—

Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia upendekeza kupekua Nahumu 1 kwa ajili ya mistari ambayo inaelezea sifa za Bwana . Unaweza kuwauliza washiriki wa darasa kitu walichojifunza kuhusu Bwana katika kujifunza kwao binafsi . Kwa mfano, tunajifunza nini kumhusu Yeye

kutoka katika mstari wa 1–9? Unaweza kutaja kwamba Nahumu alitoa unabii wa hukumu ya Bwana dhidi ya Ninawi, mji mkuu wa Ashuri, na kwamba Ashuri ilikuwa imewakandamiza Waisraeli kwa miaka mingi . Kwa nini ilikuwa muhimu kwa Waisraeli kusikia ujumbe wa Nahumu kutoka kwa Mungu? Kwa nini ni muhimu kwetu sisi leo?

“Bwana ni mwema, ni ngome siku ya taabu” (nahumu 1:7).

HABAKUKI 1:1–4; 2:1–4;3

Tunaweza kutumaini mapenzi ya Bwana na wakati Wake.• Ingekuwa msaada kwa washiriki wa darasa

kujua kwamba, kama wengi wetu, Habakuki alikuwa anasumbuliwa na kile alichokiona katika ulimwengu uliomzunguka . Labda washiriki wa darasa wangeweza kusoma Habakuki 1:1–4 na kufanya muhtasari wa wasi wasi wa Habakuki .

“mie

ndo

yake

ilik

uwa

kam

a si

ku z

a ka

le”

(hab

akuk

i 3:6

). Ha

po m

wanz

o ku

likuw

ako

Neno

, na

eva

tim

othy

nOvemBa 28–DesemBa 4

98

Wanaweza pia kulinganisha maswali yao na mengine katika maandiko, kama yanavyopatikana katika Marko 4:37–38 na Mafundisho na Maagano 121:1–6 . Je! maswali gani yanayofanana watu wanauliza kuhusu Mungu leo? Ni ushauri gani Bwana alitoa katika Habakuki 2:1–4 ambayo hukusaidia kutumaini mapenzi Yake na wakati Wake? (Ona pia Marko 4:39–40; Mafundisho na Maagano 121:7–8) . Washiriki wa darasa wanaweza kupata umaizi katika “Nyenzo za Ziada .” Wao wangeshiriki jinsi ambavyo Mwokozi amewasaidia wao “kuishi kwa imani [yao]” hata wakati wanapokuwa na maswali ambayo hayana majibu .

• Ili kuanza majadiliano ya Habakuki 3, ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kupitia sura hii na kushiriki madhihirisho ya sifa na imani waliyopata . Ili kuwasaida wao kutumia maneno haya kwa wao wenyewe, ungemwalika kila mshiriki wa darasa kuandika orodha ya baraka ambazo Mungu amempatia . Waalike kutafakari kitu ambacho kingefanyika kama angepoteza baadhi ya hizi baraka za kimwili . Someni pamoja Habakuki 3:17–19, na kujadili kwa nini ingekuwa vigumu “kufurahia katika Bwana” (mstari wa 18) wakati wa magumu kama yale yaliyoelezwa mstari wa 17 . Tunawezaje kukuza imani kama Habakuki?

SEFANIA 3:14–20

Bwana atafurahia pamoja na watu Wake katika Sayuni.• Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kupata

tumaini kwa ajili ya siku za usoni katika Sefania 3:14–20, ungeweza kuandika ubaoni “Furahi na kushangilia kwa moyo wako wote” kwa sababu.. . . Kisha washiriki wa darasa wanaweza kupekua mistari hii ili kuona baraka zilizoahidiwa kwa ajili ya siku za usoni ambazo zinaweza kuwasaidia kufuruahia leo . Ni jinsi gani ahadi hizi zinatusaidia wakati wa kipindi kigumu?

Nyenzo za Ziada

Imani maana yake ni kutumaini hekima, huruma, na wakati wa Bwana.Mzee Jeffrey R . Holland alisema:

“Je, ni kwa muda gani tutasubiri kupata msaada kutokana na ugumu ambao huja juu yetu? Je, kuhusu kustahimili majaribu binafsi wakati tunaposubiri na kusubiri, na msaada kuonekana kuja pole pole sana? Kwa nini kucheleweshwa wakati mizigo inaonekana kuwa mizito kuliko tunavyoweza kuibeba?

“ .  .  . Kutakuwa na nyakati katika maisha yetu ambapo hata jitihada zetu bora kabisa na za dhati, sala zetu za kusihi hazitazaa ushindi ambao tumeutamani, iwe hiyo ni kuhusu mambo mapana ya kidunia au yale madogo ya kibinafsi . Hivyo wakati tukifanya kazi na kusubiri kwa pamoja majibu kwa baadhi ya maombi yetu, ninawapeni ninyi ahadi yangu ya kitume kwamba zimesikika na zinajibiwa, ingawa pengine sio kwa wakati ule, au katika njia tunayotaka sisi . Lakini daima zinajibiwa katika wakati na katika njia ya mzazi wa milele mjua yote na mwenye huruma anavyopaswa kuyajibu . .  .  .

“ .  .  . Imani maana yake ni kumtumainia Mungu katika nyakati nzuri na mbaya, hata kama hiyo inajumuisha mateso fulani hadi tunapouona mkono Wake ukifunuliwa kwa niaba yetu” (“Kumsubiria Bwana,” Liahona, Nov . 2020, 115–16) .

Kuboresha Ufundishaji WetuUliza maswali yaliyo wazi. Unapowauliza washiriki wa darasa kuhusu uzoefu wao wa maandiko, “wajulishe kwamba hautafuti jibu mahususi bali kwamba una hamu ya kweli kujua kile wanachojifunza” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 29). Kwa baadhi ya mifano ya maswali yaliyo wazi, ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 31–32.

99

DESEMBA 5–11

Hagai; Zekaria 1–3; 7–14“UTAKATIFU KWA BWANA”

Unapojifunza Hagai na Zekaria, tafakari jinsi unavyoweza kuwasaidia washiriki wa darasa kupata maana katika unabii huu .

Alika Kushiriki

Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki mistari kutoka Hagai na Zekaria ambayo walitafakari au kujadili na wengine wiki hii na kujadili jinsi gani msitari hii imewasaidia wao kusogea karibu na Bwana .

Fundisha Mafundisho

HAGAI 1; 2:1–9

“Zitafakarini njia zenu.”• Ushauri katika Hagai 1 unaweza kuwasaidia

washiriki wa darasa kufikiria kuhusu vipaumbele vyao . Unaweza kuwaalika wasome Hagai 1:1–7 na kutafuta jinsi watu katika Yerusalemu walikuwa wakishindwa kuweka kipaumbele kitu kile ambacho Bwana aliwataka wafanye . Ni mambo gani Bwana ametutaka sisi tuyape vipaumbele vya juu katika maisha yetu? Ni vitu gani vinaweza kutuvuruga tusifokasi kwa Baba wa Mbinguni na Mwokozi na vipaumbele vyao . Pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu ambao umewasaidia wao “kutafakari njia [zao]” na vipaumbele vyao .

• Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kufikiria jinsi wanavyoweza kufokasi zaidi kabisa katika vipaumbele vya Bwana, unaweza kuwaomba wapitie Hagai 2:1–9 . Je, ni ushauri gani Bwana aliutoa ambao unaweza kutusaidia sisi kufanya kazi Yake? Washiriki wa darasa wangeweza kuelezea ni kwa namna gani wao wameweza kuweka vipaumbele vya Bwana kwanza katika maisha yao wanapokabiliana na majukumu yao mengine mengi muhimu . Je, Hagai 2:1–9 inafundisha nini kuhusu jinsi Bwana anavyotubariki sisi wakati tunapomweka kwanza katika maisha yetu? (ona pia “Nyenzo za Zaida”) Wape washiriki muda wa kuandika kile wamehisi kuongozwa kufanya kwa sababu ya majadiliano haya .

ZEKARIA 1–3; 7–8;14

Bwana anaweza kutufanya kuwa watakatifu.• Ili kuanza mjadala kuhusu utakatifu, mnaweza

kusoma pamoja Zekaria 14:20–21 . Washiriki wa darasa wangeweza kukielezea kirai hiki “Utakatifu kwa Bwana” kina maana gani kwao . Ni ushawishi gani unaweza kuwa juu ya watu kama wanaweza kuona kirai hiki “Utakatifu kwa Bwana” kimeandikwa kwenye kila chombo cha kila siku . Ni kwa jinsi gani kirai hiki kinatugusa kila tunapokiona kwenye mahekalu leo? Washiriki wa darasa wangeweza kusoma Zekaria 1:1–6; 3:1–7; 7:8–10; 8:16–17 na kujadili kitu ambacho wanajifunza kuhusu kuwa

hek

alu

la l

aie

haw

aii

DesemBa 5–11

100

mtakatifu ina maana gani . Kwa nini utakatifu wetu binafsi ni muhimu kwa Bwana? Je, Yeye anatusaidiaje kuwa watakatifu?

• Washiriki wa darasa wanaweza kupitia Zekaria 2:10–11; 8:1–8; 14:9–11, 20–21 na kushiriki misukumo yao kuhusu jinsi ambavyo ingekuwa kuishi pamoja na Mwokozi katika hali ya utakatifu . Je, kwa jinsi gani Bwana anataka kutuaandaa kuishi katika hali ambazo Zekaria alizoelezea? Ni kwa jinsi gani tunaweza kupata nguvu Zake ili kutusaidia kuwa watakatifu zaidi?

“tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; ni mnyenyekevu, amepanda punda, naam, mwana‑ punda, mtoto wa punda. (Zekaria 9:9). Kuingia kwa Shangwe, na harry anderson

ZEKARIA 9:9–11; 11:12–13; 12:10; 13:6–7

Yesu Kristo ndiye Masiya aliyeahidiwa.• Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuona

muingiliano kati ya maneno ya Zekaria na maisha ya Mwokozi, kama vile watu katika nyakati za Yesu walivyofanya, unaweza kugawa darasa katika makundi mawili . Wape washiriki wa darasa katika kundi la kwanza mojawapo ya vifungu hivi: Zekaria 9:9–11; 11:12–13; 12:10; 13:6–7 . Wape washiriki wa darasa katika lile kundi lingiine mojawapo ya vifungu hivi: Mathayo 21:1–11; 26:14–16; 26:31; Yohana19:37 . Kila mshiriki wa darasa anaweza kujaribu kupata mtu kutoka katika kundi lingine ambaye ana kifungu cha maandiko kinachooana na chao . Je, tunajifunza nini kuhusu Mwokozi kutoka kwenye mistari hii?

• Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari Zekaria 9:9–11, ungeweza kuonyesha picha ya Mwokozi akiingia kwa shangwe Yerusalemu (ona muhtasari wa wiki hii katika

Njoo, Nifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia) . Onyesha video “The Lord’s Triumphal Entry into Jerusalem” (LDS .org) . Washiriki wa darasa wanaweza kujadili jinsi ambavyo wangejisikia kuwa miongoni mwa watu wakimkaribisha Yesu mjini . Je, tunamkaribishaje Yeye katika maisha yetu, nyumbani mwetu, na katika jumuiya zetu .

Nyenzo za Ziada

“Zitafakarini njia zenu.”Baada ya kunukuu Hagai 1:4–7, Mzee Terence M . Vinson alifundisha:

“Tunaweza kuhisi shangwe ya kudumu pale Mwokozi na injili Yake vinapokuwa mfumo ambao tunajenga maisha yetu . Hata hivyo, ni rahisi sana kwa mfumo huo kuwa, badala ya, mambo ya ulimwengu, ambapo injili hukaa kama pendeleo la ziada au kama kuhudhuria tu kanisani kwa masaa mawili Jumapili . Wakati hii inapokuwa hivi, inakuwa sawa na kuweka mishahara yetu katika “mfuko uliotoboka toboka .”

“Hagai anatuambia sisi tuwekee sharti . .  .  .

“Hakuna hazina, wala jambo lolote la kuburudisha, wala cheo chochote, wala mtandao wo wote wa kijamii, wala mchezo wo wote wa video, wala mchezo wo wote, wala muunganiko wo wote na mtu maarufu, wala cho chote duniani ambacho kina thamani zaidi kuliko uzima wa milele . Kwa hiyo ushauri wa Bwana kwa kila mtu ni “zitafakarini njia zenu’” (“Wanafunzi wa Kweli wa Mwokozi,” Liahona, Nov . 2019, 9,11) .

Kuboresha Ufundishaji WetuSikiliza. Kusikiliza ni kitendo cha upendo. njia moja ya kusikiliza kwa makini ni kumtazama mtu ambaye anaongea. hii inatuwezesha kutambua mawasiliano yasiyo ya maneno. (Ona Kufundisha Katika Njia ya Mwokozi, 34.)

101

DESEMBA 12–18

Malaki“NIMEWAPENDA NINYI, ASEMA BWANA”

Baadhi ya vifungu katika Malaki vinaweza kuwa na umuhimu wa kipekee kwa darasa lako kujifunza . Unapojifunza, sali ili kutambua ni vifungu hivyo vinaweza ni gani . Kufanya hivi pia kutakusaidia kuhisi upendo ambao Bwana anao kwa ajili ya wale unaowafundisha .

Alika Kushiriki

Unaweza kuanza mjadala kuhusu kitabu cha Malaki kwa kuandika neno Ujumbe ubaoni . Wahimize washiriki wa darasa kushiriki ujumbe muhimu ambao wameupata katika kila sura ya Malaki . Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kukumbuka na kutafakari kile kilichoshirikishwa unaweza kuandika vifungu hivyo vya maneno ubaoni .

Fundisha Mafundisho

MALAKI 1:6–14.

Bwana anataka “dhabihu iliyo safi.”• Ili kuwahimiza washiriki wa darasa kuelezea kile

walichojifunza kuhusu dhabihu kutoka katika Malaki 1:6–14, ungeweza kuwaalika kupitia mistari kimya kimya na kujadili na mshiriki mwingine wa darasa kitu ambacho makuhani Waisraeli hawakuelewa kuhusu dhabihu . Je, ni kwa nini Bwana hutaka kilicho bora kutoka kwetu? Washiriki wa darasa wangeweza kutengeneza orodha ya dhabihu au sadaka, tunazofanya kwa Bwana leo . Kwa kila kitu

kilicho kwenye orodha, wanaweza kujadili ni kitu gani ambacho kinaweza kuifanya dhabihu kuwa “najisi” au “safi” (Malaki 1:7,11) .

MALAKI 3– 4

Unabii wa Malaki unatimizwa katika siku hizi za mwisho.• Ungeweza kuanza mjadala kuhusu Malaki 3–4

kwa kutaja kwamba Moroni alishiriki mistari katika sura hizi alipomtokea Joseph Smith (ona Joseph Smith—Historia 1:36–39) . Ni ukweli gani katika sura hizi washiriki wa darasa wanaona huenda ulikuwa na umuhimu wa kipekee kwa Joseph—na kwetu sisi —kujua? Washiriki wa darasa wangejipanga katika vikundi vidogo vidogo na kuorodhesha ukweli mwingi kadiri wanavyoweza . Himiza makundi kushiriki orodha zao na kujadili kwa nini kweli hizi ni muhimu katika siku za mwisho .

MALAKI 3:8–12.

Bwana hufungua madirisha ya mbinguni wakati sisi tunapolipa zaka zetu.• Ili kuwahimiza washiriki wa darasa kushiriki

shuhuda zao za sheria ya zaka, ungeweza kuwaalika kutafuta kanuni katika Malaki 3:8–12 na kushiriki jinsi walivyokuja kujua kanuni hizi ni za kweli . Wanaweza kuzungumza kuhusu jinsi ambavyo Bwana amewabariki—kiroho na

DesemBa 12–18

102

kimwili—kwa kulipa zaka . Au wanaweza kujadili masomo kuhusu zaka ambayo Mzee David A . Bednar alishiriki katika ujumbe wake “Madirisha ya Mbinguni” (Liahona, Nov . 2013, 17–20) na kushiriki kile ambacho wamejifunza wanapojitahidi kuishi sheria hii .

• Waombe washiriki wa darasa wasome Malaki 3:8–12 kimya kimya huku wakitafakari jinsi wanavyoweza kumfundisha mtu kwa nini Bwana anatutaka tulipe zaka . Wanaweza pia kusoma maelezo ya Rais Gordon B . Hinckley katika “Nyenzo za Ziada .” Je, tungependa wengine waelewe nini kuhusu zaka? Kwa mfano, Je, kulipa zaka maana yake ni nini? Je, ni kwa nini Bwana anataka sisi tuilipe? Je, ni kwa jinsi gani “madirisha ya mbinguni” (mstari wa 10) hufunguka tunapolipa zaka? Je ni shaka gani mtu angekuwa nayo kuhusu kulipa zaka, na tungemjibu namna gani? Waombe washiriki wa darasa kushiriki jinsi kutii amri hii kumeimarisha imani yao katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo .

Kielelezo cha eliya akiwatokea joseph Smith na oliver Cowdery katika hekalu la Kirtland, na Robert T Barrett

MALAKI 4:5–6.

“Nitawapelekea Eliya nabii.” • Washiriki wa darasa wangeweza kupata umaizi

wenye msaada kuhusu Malaki 4:5–6 kwa kulinganisha mistari hii na ile namna Moroni alivyoinukuu kwa Joseph Smith katika Joseph Smith—Historia 1:38–39 . (Inaweza kusaidia kuwa na mtu akiandika mistari ya kila toleo sambamba ubaoni .) Maneno ya Moroni yanaongeza nini katika uelewa wetu wa mistari

hii katika Malaki? Wangeweza pia kujadili maswali kama haya: Kina nani ndiyo “akina baba”? (ona Kumbukumbu la Torati 29:13) . Ni kwa jinsi gani mioyo yetu inageuzwa kuwaelekea baba zetu, na mioyo yao hugeuzwaje kutuelekea sisi? Ili kusaidia darasa lako kuelewa jinsi unabii wa Malaki ulivyotimizwa, wanaweza kusoma kuhusu wakati ambapo Eliya alikabidhi funguo za kufunga kwa Joseph Smith (ona Mafundisho na Maagano 110:13–16) . Kwa nini washiriki wa darasa wanashukuru funguo hizi zilirejeshwa?

• Malaki 4:5–6 inatoa fursa kubwa ya kuzungumza kuhusu kazi ya hekalu na historia ya familia . Labda washiriki wa darasa wanaweza kushiriki uzoefu walio nao wakati walipokuwa wanafanya kazi hii na jinsi uzoefu huu ulivyowasaidia kuigeuza mioyo yao kwa baba zao . Je, tunaweza kufanya nini ili kusaidia kizazi kijacho kuigeuza mioyo yao kutuelekea sisi?

Nyenzo za Ziada

Zaka suala la kiimani.Rais Gordon B . Hinckley alisema, “Sisi tunaweza kulipa zaka zetu . Hii sio suala la fedha sana bali kwani ni suala la kiimani zaidi . Mimi sijapata mlipa zaka mwaminifu ambaye hawezi kushuhudia kwamba katika njia halisi na ya ajabu madirisha ya mbinguni yamefunguliwa na baraka kumiminwa juu yake” (“Acha Tusogeze Kazi Hii Mbele,” Ensign, Nov . 1985,85) .

Kuboresha Ufundishaji WetuElezeni mahangaiko yenu na imani yenu. wakati mwingine watu ambao wanapitia majaribu hujihisi ni wapweke. inaweza kuwa sahihi mara moja moja kushiriki uzoefu binafsi kuhusu wakati ambapo ulikuwa unahangaika na jinsi mwokozi alivyokusaidia.

103

DESEMBA 19–25

Krismasi“NDIYE TULIYEMNGOJA, NAYE ATATUOKOA”

Wakati wa kujifunza kwako binafsi na maandalizi ya kufundisha, fikiria jinsi unavyoweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuona shangwe kuu ya kuzaliwa kwa Mwokozi . Mwalike Roho ashuhudie kwao juu ya upendo wa kukomboa wa Yesu Kristo .

Alika Kushiriki

Wakati wa Krismasi unaweza kuwa fursa nzuri ya kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki jinsi kujifunza kwao Agano la Kale kulivyoimarisha imani yao katika Yesu Kristo .

Fundisha Mafundisho Rasmi

Tunashangilia katika Mkombozi wetu.• Hata ingawa Krismasi inajulikana kama majira ya

shangwe, kuna wengi ambao hali zao zinafanya kuwa vigumu kupata shangwe, hata katika wakati huu wa mwaka . Ujumbe muhimu wa Krismasi ni kwamba Mwokozi anaweza kuifanya myepesi mizigo yetu na kutusaidia kupata imani na hata shangwe . Ili kushiriki ujumbe huu, unaweza kuandika ubaoni marejeo ya maandiko yafuatayo: Zaburi 35:9; Isaya 25:8–9; 44:21–24; 51:11; Sefania 3:14–20; Musa 5:5–11 . Kisha unaweza kuandika ubaoni swali kwa ajili ya washiriki wa darasa kutafakari wanaposoma vifungu hivi, kama vile Ni kwa sababu gani vifungu hivi vya maandiko hutoa za kuwa wenye shangwe? Waombe washiriki kile walichopata . Pengine unaweza

pia kuwapa muda washiriki wa darasa kuandika kuhusu shangwe yao wenyewe katika Mwokozi . Wangeweza kupata umaizi wa ziada kutoka katika ujumbe wa Rais Russell M . Nelson katika ”Nyenzo za Ziada .”

• Krismasi hutoa fursa za kueneza shangwe ya Kristo kwa wengine . Kabla ya darasa, unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kupitia ujumbe wa Mzee Ulisses Soares “Jeshi la Malaika wa Kisasa” (Ibada ndogo ya Urais wa Kwanza, Desemba 8, 2019, broadcasts .ChurchofJesusChrist .org) na waje wakiwa wamejiandaa kushiriki jinsi kitendo cha huduma kilimsaidia Mzee Soares na familia yake kuona shangwe ya Krismasi . Unaweza pia kushiriki sehemu za ujumbe wake katika darasa . Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki uzoefu wao wa vitendo vya kutoa au kupokea huduma wakati wa Krismasi . Ni kwa jinsi gani tunaweza kutenda juu ya mwaliko wa Mzee Soares wa kufuata mfano kamili wa Mwokozi wa upendo na ukarimu kwa binadamu”?

Ishara zinaweza kutusaidia kumkumbuka Yesu Kristo.• Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa

Ajili ya Watu Binafsi na Familia unaorodhesha baadhi ya ishara katika Agano la Kale ambazo zinafundisha kuhusu Yesu Kristo . Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki kile walichojifunza kuhusu Mwokozi kutoka katika ishara hizi na zingine walizozipata katika kujifunza kwao .

Kwa

Ajili

Yetu

Mto

to A

mez

aliw

a, n

a Si

mon

dew

ey

DesemBa 19–25

104

Je, tunajifunza nini kuhusu kumpata Mwokozi katika maandiko? Ni uzoefu gani umetufundisha kwamba “vitu vyote vimeumbwa na vimefanywa ili kumshuhudia [Yeye]” (Musa 6:63) .

Mungu alitupatia zawadi ya Mwana Wake.• Kutoa zawadi ni desturi ya Krismasi katika

tamaduni nyingi . Unaweza kuongoza mjadala na washiriki wa darasa kuhusu zawadi Mungu ametupatia, hasa zawadi ya Mwanawe, Yesu Kristo . Kufanya hili, unaweza kushiriki video “He is the Gift”(ChurchofJesusChrist .org) na kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki kile zawadi ya Mwokozi inamaanisha kwao . Tunawezaje kumwonyesha Baba wa Mbinguni shukrani zetu kwa ajili ya zawadi hii?

ISAYA 7:14; 9:6

“Na jina Lake litaitwa wa Ajabu.”• Nabii Isaya alitumia majina mengi na vyeo ili

kumwelezea Masiya, ambaye angezaliwa katika Bethlehemu (ona kwa mfano, Isaya 7:14; 9:6) . Labda washiriki wa darasa wanaweza kufurahia kujifunza zaidi kuhusu Mwokozi na misheni yake kuhusu vyeo hivi? Wanaweza kuchagua cheo kimoja na kutafuta vifungu vya maandiko ambavyo vitawasaidia kuelewa kile kinachomaanisha . Kwa mfano, wanaweza kujifunza zaidi kuhusu cheo “Mfalme wa Amani” (Isaya 9:6) kwa kusoma Zaburi 85:8; Isaya 52:7; Luka 2:14; au Yohana 16:33 . Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kupata maandiko mengine, pendekeza kwamba waangalie katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures .ChurchofJesusChrist .org) . Vyeo hivi vinapendekeza nini kuhusu Mwokozi na kile anachotufanyia sisi?

Nyenzo za Ziada

Yesu Kristo hutoa amani na shangwe.Rais Russell M . Nelson alifundisha:

“Wakati fokasi ya maisha yetu kwenye mpango wa Mungu wa wokovu .  .  . na Yesu Kristo na injili Yake, tunaweza kuhisi shangwe bila kujali nini kinatokea—au hakitokei—katika maisha yetu . Shangwe inakuja kutoka Kwake na kwa sababu Yake . Yeye Ndiye kiini cha shangwe yote . Tunaisikia wakati wa Krismasi pale tunapoimba, ‘Joy to the world, the Lord is come’ [Wimbo, na . 201] . Na tunaweza kuhisi hivyo mwaka mzima . Kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho, Yesu Kristo ndiye shangwe! .  .  .

“Kama vile Mwokozi anavyotoa amani ambayo ‘inapita akili yote’[Wafilipi 4:7], Yeye pia anatoa kiwango, kina, upana wa furaha ambayo inapita uelewa wa mwanadamu au uelewa wa kimwili” (“Furaha na Kupna Kiroho,” Liahona, Nov . 2016, 82) .

Kuboresha Ufundishaji WetuJitayarishe ukiwa na watu akilini. “acha uelewa wako juu ya wale unaowafundisha uongoze mipango yako. . . . Walimu walio kama Kristo hawatumii mtindo au mbinu moja tu; wao hufanya kila juhudi kuwasaidia watu kujenga imani yao katika Yesu Kristo” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 7).

NJO

O, U

NIFU

ATE—KW

A A

JILI YA SH

ULE YA

JUM

APILI: A

GA

NO

LA KA

LE 2022