P a g e UFAFANUZI (COMMENTARY) KIFUNGU CHA 25 CHA SHERIA NAMBA 83 YA MABADILIKO YA KATIBA KWA...

14
1 | Page UFAFANUZI (COMMENTARY) KIFUNGU CHA 25 CHA SHERIA NAMBA 83 YA MABADILIKO YA KATIBA KWA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA MADARAKA NA MIPAKA YA BUNGE LA KATIBA LA TANZANIA “Madaraka yake Yamebinywa na Mchakato, Sheria Na Muundo Wake” Mchakato wa Katiba Mchakato wa kupata katiba ya Jamhuri ya Muungano ulianza kwa kutungwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na baadaye kupitia sheria hiyo Tume ya kukusanya maoni ya wananchi ikaundwa kwa ajili ya kukusanya maoni na kuandaa rasimu ya katiba. Kwa mujibu wa sheria hiyo ya mabadiliko ya katiba kwa sasa tumebakiza hatua mbili ili kukamilisha mchakato wa katiba. Hatua hizo ni Bunge la Katiba na kura za maoni (Referendum). Hatua zote za mchakato wa kupata katiba zinatofautiana na zina mamlaka tofouti na zinapaswa kuwa shirikishi. Katika taifa lolote lile msingi wa uendeshaji wa Taifa hutegemea sana sheria kuu (Grund Norm). Katiba huainisha tunu na misingi ya nchi yoyote, pia hutoa migawanyo na ukomo wa madaraka na majukumu mbalimbali ya mihimili mikuu ya dola. Kutokana na umuhimu huu mchakato wa katiba ni lazima uwe shirikishi katika ngazi zote likiwemo hili la Bunge la Katiba. Katiba inapaswa kuakisi mambo ya wananchi ili kuifanya waimiliki na kuiheshimu katiba hiyo. Ukiwa na Katiba ambayo wananchi hawakushiriki vizuri, lazima Katiba hiyo itakuwa vigumu kupata utekelezaji na umiliki wa wananchi. Historia inatushitaki kuwa michakato mingi ya kikatiba baada ya kupata uhuru haikuwashirikishi bali ilihusisha tu viongozi. Katiba ya kwanza ya Tanganyika ya 1961 ilipatikana kupitia Bunge la Kikoloni, katiba ya 1962 ilipatikana kupitia white paper na sheria ya Bunge la Katiba ikatumika kugeuza bunge la kawaida kuwa Bunge la Katiba, hali kadhalika katiba ya Muungano ya 1964 na ile ya Muda ya 1695 zote hazikupata Baraka za wananchi. Mwaka 1977 Katiba yetu inayotumika hadi leo iliundwa na kamati ya chama iliyogeuzwa kuwa tume ya

Transcript of P a g e UFAFANUZI (COMMENTARY) KIFUNGU CHA 25 CHA SHERIA NAMBA 83 YA MABADILIKO YA KATIBA KWA...

1 | P a g e

UFAFANUZI (COMMENTARY) KIFUNGU CHA 25 CHA SHERIA NAMBA 83 YA MABADILIKO YA KATIBA KWA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA

MADARAKA NA MIPAKA YA BUNGE LA KATIBA LA TANZANIA “Madaraka yake Yamebinywa na Mchakato, Sheria Na Muundo Wake”

Mchakato wa Katiba Mchakato wa kupata katiba ya Jamhuri ya Muungano ulianza kwa kutungwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na baadaye kupitia sheria hiyo Tume ya kukusanya maoni ya wananchi ikaundwa kwa ajili ya kukusanya maoni na kuandaa rasimu ya katiba. Kwa mujibu wa sheria hiyo ya mabadiliko ya katiba kwa sasa tumebakiza hatua mbili ili kukamilisha mchakato wa katiba. Hatua hizo ni Bunge la Katiba na kura za maoni (Referendum). Hatua zote za mchakato wa kupata katiba zinatofautiana na zina mamlaka tofouti na zinapaswa kuwa shirikishi. Katika taifa lolote lile msingi wa uendeshaji wa Taifa hutegemea sana sheria kuu (Grund Norm). Katiba huainisha tunu na misingi ya nchi yoyote, pia hutoa migawanyo na ukomo wa madaraka na majukumu mbalimbali ya mihimili mikuu ya dola. Kutokana na umuhimu huu mchakato wa katiba ni lazima uwe shirikishi katika ngazi zote likiwemo hili la Bunge la Katiba. Katiba inapaswa kuakisi mambo ya wananchi ili kuifanya waimiliki na kuiheshimu katiba hiyo. Ukiwa na Katiba ambayo wananchi hawakushiriki vizuri, lazima Katiba hiyo itakuwa vigumu kupata utekelezaji na umiliki wa wananchi. Historia inatushitaki kuwa michakato mingi ya kikatiba baada ya kupata uhuru haikuwashirikishi bali ilihusisha tu viongozi. Katiba ya kwanza ya Tanganyika ya 1961 ilipatikana kupitia Bunge la Kikoloni, katiba ya 1962 ilipatikana kupitia white paper na sheria ya Bunge la Katiba ikatumika kugeuza bunge la kawaida kuwa Bunge la Katiba, hali kadhalika katiba ya Muungano ya 1964 na ile ya Muda ya 1695 zote hazikupata Baraka za wananchi. Mwaka 1977 Katiba yetu inayotumika hadi leo iliundwa na kamati ya chama iliyogeuzwa kuwa tume ya

2 | P a g e

katiba na baadae tume hiyo kupeleka maoni yake kwa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM). Kamati hii ya Chama ndiyo ilipeleka rasimu kwenye Bunge ili kujadiliwa na kupitishwa. Michakato yote hiyo haikushirikisha wananchi tofouti na huu wa sasa. Mamlaka na Mipaka ya Bunge la Katiba Hivi karibuni, siku chache kabla ya kuanza kwa Bunge la Katiba kumetokea mikinzano tofouti kuhusu madaraka na mipaka ya Bunge la Katiba. Utata huu umeanza pale Rais Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM aliposema katika maadhimisho ya miaka 37 ya CCM huko Mbeya tarehe 3, February 2014. Rais Kiwete alinukuliwa na gazeti la umma la Daily News akisema;

“The assembly will be free to discuss and shape the final draft of the Constitution in the way they deem fit, adding that the assembly may even produce a “totally different document” if it can reach a common understanding and manage to compose it” Bunge litakuwa huru kujadili rasimu ya katiba kwa wanavyoona ni sawa, na ikiwezekana Bunge linaweza kuja na rasimu tofouti kabisa kama watahafikiana na kuweza kuandaa rasimu hiyo” President Kikwete.

Maneno na mawazo kama haya yalirudiwa tena na Prof Issa Shivji alipokuwa akitoa mada katika kongamano la wajumbe wapya wa Bunge la Katiba hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Prof Shivji alidai kuwa;

“Rasimu ya Katiba sio Msahafu, Bunge la Katiba linaweza kubadili rasimu na kuja na rasimu mpya kabisa. Bunge ndio chombo cha maamuzi na wanauwezo wa kuibadili rasimu” Prof Shivji

Katika mafunzo hayo kwa wabunge wa Bunge la Katiba, Prof Shivji alitoa msimamo wake na mimi kutoa msimamo wangu na kuwafanya wajumbe hao waende Bungeni na maswali juu ya mamlaka halisi ya Bunge la Katiba. Maneno hayo ya Prof Issa Shivji na Rais Jakaya Kiwete yanapingana na msimamo wa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Sinde Warioba. Jaji Warioba katika mkutano wa serikali na wanasiasa uliondaliwa na Kituo cha Demokrasia

3 | P a g e

Tanzania alilisitiza kuwa Bunge la Katiba halina mamlaka ya kubadili masharti na mambo ya msingi wa katiba bali wanauwezo wa kujadili na kuboresha mambo ya kawaida. Kwa mujibu wa Jaji Warioba Bunge la Katiba la Tanzania halina mamlaka ya kubadili masharti ya katiba kwa kuwa mchakato huu wa Tanzania ni tofouti na nchi zingine kama Africa Kusini, Namibia na Cambodia ambapo Bunge maalumu ndio lililopewa jukumu la kuandika Rasimu. Katika mazingira haya Bunge Maalum linauwezo kabisa wa kuandika Rasimu mbadala. Mimi binafsi kama mwanasheria naungana moja kwa moja na Jaji Warioba na kusisitiza kuwa Bunge Maalum la Katiba la Tanzania halina madaraka ya kubadili Rasimu hii zaidi ya kuijadili, kuiboresha na kuileta kwa wanachi kwa ajili ya kupitishwa.Mzozo huu pia umeendelea hadi katika mikutano ya awali ya Bunge la Katiba. Mwanasheria Mkuu wakati anajibu hoja za wajumbe naye ameendelea kushikilia kuwa Bunge la Katiba linaweza kuja na katiba mpya kabisa. Nasema Bunge letu hili halina mamlaka yoyote kubadili rasimu hii kwa sababu kuu zifuatazo: Kwanza, Bunge hili halina mamlaka ya kubadili rasimu hii zaidi ya kujadili, kuboresha na kuongeza masharti ya mpito.Kifungu cha 25 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83. Bunge lina madaraka tu ya kujadili na kupitisha masharti ya katiba, kutunga sheria ya masharti ya mpito, Kanuni za kuendeshea Bunge hilo na masharti yatokanayo. Hivyo kwa mujibu wa sheria hii tayari madaraka ya Bunge hili yamewekewa mipaka na wakitaka kuja na rasimu mbadala watakuwa wamevunja sheria hii. Kutokana na tafsiri yangu kama mwanasheria, Bunge Maalum linapaswa kuzingatia masharti ya kifungu hiki cha 25 wanapotunga Kanuni za Bunge Maalumu na wanapokuwa wanaendesha mjadala. Wanapaswa kuhakikisha hawatungi kanuni zitakazopingana na kifungu hiki. Kuna uwezekano mkubwa

4 | P a g e

sana katika kuandaa kanuni hizi Bunge Maalum likajikuta linajipa madaraka ya kutunga “Rasimu ya Tatu” na kutupilia Rasimu hii ya wananchi. Inawezekana kabisa watu wakatumia wakati mwingine udhaifu wa sheria zetu kutafsiri vifungu kwa maslahi yao binafsi. Kuna baadhi ya watu wataweza kutafsiri kifungu hiki cha 25 kwa malengo ya kutaka kuonyesha kuwa Bunge la Katiba lina mamlaka ya kuja na rasimu mpya kabisa kitu ambacho si cha kweli. Kifungu cha 25(1) Kinasema;

“Bunge litakuwa na mamlaka ya kujadili na kupitisha maharti ya katiba inayopendekezwa, kutunga masharti ya mpito na kutunga masharti yatokanayo kama Bunge Maalum litakavyoona inafaa”

Kifungu hicho 25(1) kina sentensi tatu. Kwa mujubu wa sheria namba moja ya tafsiri ya vifungu vya sheria, neno kama “litakavyoona inafaa” liililotumika katika kifungu cha 25 linamaanisha sentensi ya pili na siyo sentensi inayozungumzia kujadili na kuboresha. Kwa maana hiyo Bunge linaweza ongeza masharti ya yatokanayo na ya mpito kadiri watakavyoona inafaa na si vinginevyo. Uhuru wa kama watakavyoona inafaa haitumiki katika mambo ya msingi ya katiba. Katika Rasimu ya Kanuni za Bunge Maalum la katiba, angalau kifungu cha 5 kimejaribu kutenganisha huo utata uliokuwa unatumika vibaya. Tofouti na sheria yenyewe rasimu ya kanuni imeweka kifungu hicho katika makundi mawili 3:

5. (1) Kwa mujibu wa kifungu cha 25 cha Sheria, Bunge Maalum litakuwa na mamlaka ya- (a) kujadili na kupitisha Rasimu ya Katiba; na (b) Kutunga masharti ya mpito na masharti yatokanayo na Rasimu ya Katiba kadri litakavyoona inafaa.

Kanuni hizi zimeweka bayana kuwa uhuru wa kadiri litakavyoona inafaa lipo kwenye masharti yatokanayo na na masharti ya mpito kama inavyojieleza kwenye kifungu (b).Tunaposema tunaposema masharti ya mpito na yatokanayo tunaaminisha yale masharti sawa nay ale ya mpito yaliwekwa katika sura ya 17 ya Rasimu ya Katiba.

5 | P a g e

Sheria yenyewe imeacha mianya mingi ambayo kimsingi inaweza tumika vibaya, ilipaswa kuweka mipaka ya Bunge moja kwa moja (express provisions) kama ilivyokuwa kuwa kwa tume na hatua zingine zilizoainishwa katika mchakato wa katiba. Kwa mfano Tume ilipewa mipaka na mambo ya kuzingatia katika kifungu cha 9 cha sheria ya mabadiliko ya katiba, hali kadhalika tasisi ya kupiga kura za maoni ambayo ni mchakato wa mwisho nayo inamipaka yake ambayo ni kupiga kura ya ndiyo au hapana na si vinginevyo. Mwanasheria Mkuu, Jaji Werema alifanya kosa la kisheria kuwaambia wabunge kuwa makatazo na misingi ya utendaji yanatoka katika kifungu cha 9. Kifungu hiki hakina uhusiano kabisa na mamlaka ya Bunge. Mbaya zaidi katika Rasimu ya Kanuni za Bunge pia kosa hili limejirudia. Kosa la kisheria lipo zaidi katika kifungu cha 79(2) (a) ambacho kimewataka wabunge kufanya maboresho ambayo hayatakuwa kinyume na kifungu cha 9 cha seria ya mabadiliko ya Katiba. Kifungu hicho hakina uhusiano wowote na Bunge Maalum, ila ni kifungu ambacho kinatoa mipaka ya Tume tu. Tulifanya kosa kubwa kutunga sheria bila kuweka mipaka ya Bunge la Katiba katika mfumo ambao mtu yeyote ambaye si mwanasheria angeweza kuelewa kama ilivyo katika kifungu cha 9 kwa Tume. Nashauri Kanuni ziweke mipaka ya Bunge hili vizuri kwa kuzingatia kifungu 25, kwani kifungu cha 9 hakina uhusiano na Bunge. Sheria ingepaswa kueleza wazi wazi kuwa misingi ya Kikatiba (Constitutionalism) katika rasimu hii haipaswi kubadilishwa na Bunge la Katiba. Misingi hiyo ni pamoja na mgawanyo wa madaraka, (Separation of Powers), Uhuru wa Mahakama, Tunu na misingi ya Taifa, haki za binadamu na mengineyo yanayoingia katika masharti ya kikatiba. Pamoja na hayo udhaifu huu wa kisheria bado Bunge la Katiba katika mchakato huu halina mamlaka ya kubadili mambo yote ya msingi katika rasimu

6 | P a g e

ya katiba. Hivyo kwa mujibu wa sheria hii Bunge lina mamlaka kamili ya kujadili na kuboresha rasimu tu na si kutunga rasimu nyingine. Kazi yao ni kupendekeza katiba itakayotiwa mhuri na wananchi kwa kura ya ndiyo. Sheria hii ilipaswa kuweka majukumu na mipaka ya Bunge la Katiba kama ilivyokuwa kwa sheria iliyoanzisha Bunge la Katiba la Uganda. Lengo la kufanya hivi ilikuwa ni kuwabana wanasiasa wasihamishie migongano yao kwenye Bunge la katiba. Jambo la msingi katika mchakato wa Katiba ni kuangalai chombo hiki kama kinazingatia misingi ya uundwaji wa katiba. Hutegemea pia chombo hiki kinaaminiwa kwa kiasi gani na wananchi, pia utashi wa kufanya kazi yake kwa kuzingatia matakwa ya wananchi na si vikundi vya kijamii ni jambo la kuzingatiwa. Kutokana na mkanganyiko huu wa kisheria ni muhimu Bunge la Katiba likapewa elimu kuhusu majukumu yake na mipaka yake. Sheria ilikosea sana kuacha kufafanua zaidi kipengele cha kuonyesha majukumu na mipaka ya Bunge. Pili, Mchakato uliotumika hapa Tanzania tayari umeshaiwekea mipaka Bunge Maalumu kubadili Rasimu hii ya pili. Mchakato wa Katiba mpya Tanzania umepitia hatua za msingi zifuatazo:

i. Kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Bunge la sasa, ii. Kuundwa kwa Tume ya Katiba, iii. Kukusanya maoni ya Wataalum, iv. Kukusanya maoni ya Watanzania, v. Kujifunza kutokana na uzoefu wa nchi nyingine, vi. Kuchambua na kutathimini maoni ya Wananchi, vii. Kuandika Toleo la Kwanza la Rasimu ya Katiba viii. Wananchi kujadili Toleo la Kwanza la Rasimu ya Katiba

7 | P a g e

ix. Bunge Maalumu kujadili na kuboresha Rasimu ya Pili ya Katiba na hatimaye badaye

x. Kura za Maoni za Wananchi katika kuridhia ama kukataa Katiba.

Mchakato huu wa kupata katiba mpya umepata mamlaka katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Sura 83. Kila hatua kwa mujibu wa sheria hiyo uliwekewa mipaka na madaraka, mfano Tume ilikuwa na mipaka na madaraka yake. Mchakato huu tofouti na Nchi nyingine kama za Misri ndio hasa umeinyima Bunge Maalumu meno na mamlaka ya kuitupilia mbali Rasimu ya Katiba badala yake mchakato huu hutoa mamlaka ya kujadili na kuboresha tu Rasimu. Mchakato huu ulikuwa shirikishi na wananchi walishrikishwa toka kwenye utungaji wa sheria yenyewe na hata kwenye uteuzi wa wajumbe wa tume. Upatikanani wa wajumbe wa Tume ulihusisha watanzania kupitia makundi yao kama ya vyama vya sisa, ya kidini, Taasisi zisizo za kiserikali na mengineyo. Pia tume ilizunguka nchi nzima na kukusanya maoni ya wananchi na makundi mengine. Kwa utaratibu na mchakato huu Bunge Maalum kama anavyosema Warioba ni wazi halina mamlaka ya kubadili Rasimu.

Jinsi ushirikiswaji wa wananchi unavyokuwa wazi ndivyo madaraka ya Bunge Maalum yanavyopungua…mantiki ni kuzuia Bunge Maalum kunyang’anya madaraka ya wananchi “Pupular Soveregnity”. Jaji Warioba,

Kwa mujibu wa mchakato wa katiba wa hapa Tanzania Bunge Maalum ni sehemu ya mchakato na kamwe hawawezi kuwa juu ya mchakatato wa katiba. Nasema hivyo kwa kuwa tayari michakato mingine imekwisha kamilika kwa mujibu wa sheria ya mabadilko ya katiba. Kulipa Bunge madaraka ya kubadili rasimu nzima ni sawa na kutaka Bunge lifanye kazi ya mabaraza ya Katiba na kazi ya Tume ya Katiba.

8 | P a g e

Tume ya Katiba ilikuwa na majukumu ya kuandaa wananchi na kutoa elimu ya katiba, kukusanya maoni ya wananchi wa aina zote, kujifunza kutokana na uzoefu wa nchi nyingine, kuchambua na kutathimini maoni ya wananchi, kuandika toleo la kwanza, kuchambua na kutathmini maoni ya wananchi kuhusu toleo la kwanza na kuandaa tole la pili kwa ajili ya Bunge la Katiba. Hivyo basi kusema kuwa Bunge lina mamlaka ya kubadili rasimu nzima ya katiba ni sawa na kusema Bunge lifanye kazi zote zilizokwisha fanywa na hatua za awali za mchakato. Bunge ni hatua ya pili kutoka mwisho wa mchakato wa katiba na halina budi kuheshimu nafasi ya michakato mingine. Kudai kuwa Bunge lije na katiba mpya ni sawa na kusema waanze upya kukusanya maoni, wapitie mabaraza ya katiba, wachambue maoni na kuandika rasimu mpya. Je nauliza kama watakuja na rasimu mpya kabisa , watakuwa wametengeneza kwa kutumia maoni ya watu wa nchi ipi au maoni yao wenyewe?. Na kama tulikuwa tunajua Bunge la watu 600 linaweza tengeneza katiba ya watu milioni 44, kwanini tuliruhusu michakato mingine kama ya Tume na ukusanyaji wa maoni ya wananchi? Bunge linapewa nafasi kubwa katika hatua ya kujadili (Debating) hasa baada ya wananchi kutoa maoni na Tume kuandaa rasimu. Hivyo Bunge linafanya mjadala wa kitaifa juu ya rasimu ya katiba na kuifanya katiba pendekezwa. Katika kujadili Bunge wanaiboresha rasimu kwa kuangalia vifungu, kuweka masharti na kuboresha mambo mengine kama muundo na lugha. Hapa ndipo eneo ambalo kuna uwezo wa kufikia muafaka mambo ya msingi. Nchi nyingine zimekuwa zikialika wataalam kufafanua baadhi ya hoja kwenye hatua ya mjadala. Nchi hizo ni Timor [2002], Afghanistan [2004], Nepal [2014], and Zimbabwe [2000].) Ila katika hatua hii kuna hatari kubwa pia ya kuibuka makundi na kutoelewa kabisa kama ilivyokuwa nchini Kenya 2010.

9 | P a g e

Katika mchakato wa kutengeneza katiba, siku zote bunge la katiba haliwezi kuwa Tume ya kuandaa rasimu. Kazi ya kuanda (Drafting) ni ya kitaalum zaidi na ndio maana imeachiwa Tume. Tume inapendelewa kufanya kazi kwa kuwa kwanza nia wachache, wanauwezo wa kitaaluma, pia wanakuwa na nafasi kubwa ya kuaminika na jamii kwa kuwa hawa upande wowote. Pia ni rahisi kukubalika na makundi yote ya kijamii tofouti na Bunge ambalo tayari linamakundi mbalimbali na mengine yanahisi yameachwa nyuma. Ingawa katika michakato mingine kama uandaaji wa katiba ya umoja wa nchi za Ulaya, Somalia 2004 mjadala wa Bunge la katiba haukuwepo.Maanake ni kwamba rasimu ilitoka kwa waandaji (Drafters) na kwenda moja kwa moja kupigiwa kura. Mfumo wa maamuzi kuhusu katiba mara nyingi kunapaswa kuwe na chombo kimoja cha kupitisha katiba na wakati wote kura ya maoni imetumika. Tofauti na Kenya 2005, ilianza na vyombo vingi vya vya kuridhia katiba, walitumia bunge la kawaida, Tume ya Katiba na mwishoni kwa maamuzi ya mahakama ikaamuliwa kura ya maoni. Nasema kwa amri ya Mahakama kwa kuwa kuna shauri (Njoya v Attorney General [2004] L.L.R. 4788 HCK) lilifunguliwa na kuhoji mwenendo wa mchakato wa katiba Kenya 2002-2005, na baadaye Mahakama kuona walikosea kutokuweka na kipengele cha kura ya maoni. Mchakato wa Kenya ulizua migogoro kwa kuwa walikuwa mara nyingi wanakiuka misingi ya uandaji wa katiba. Mfano wao Kenya walitumia bunge la kawaida kama chombo cha kuridhia katiba ya nchi.Mchakato wa Kenya ulianza 1997 lakini katika makundi makundi, ndipo badaye Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Prof Yash Pal Ghai akafanikiwa angalau kuunganisha kundi la wanasiasa na lile la makundi ya kijamii na kidini (Ufungamano). Baada ya Serikali ya Arab Moi kung’olewa madarakani na Muungano wa Upanga Mwekundu (NARC),Tume ya Katiba (KCRC) iliendelea na mchakato. Na baadaye Ghai draft ya katiba ikapatikana ali maarufu kama Bomas Draft.

10 | P a g e

Baadaye serikali kupitia mwanasheria mkuu wa Kenya wakaanda rasimu yao iitwayo Wako’s Draft nayo ikapingwa vibaya kwenye kura za maoni 2005. Na kuazia hapo Kenya ikaingia kwenye mgogoro wa kikatiba na kuwa chanzo kikuu cha machafuko ya mwaka 2007-2008. Taswira ya Kenya toka 2000-2008 inatuonyesha ni jinsi gani tusipokuwa makini katika mchakato wa katiba tunaweza itumbukiza nchi katika mgogoro mkubwa. Ndipo baadaye Tume ya Maridhiano kupita sheria ya mabadiliko ya Kenya ya 2008 (Constitution of Kenya Review Act, 2008) ikaanzisha mchakato mpya hadi kupata katiba mpya 2010. Mchakato ulipitia muundo wa hatua 4; Kamati ya Wataalam, Bunge la Katiba, Kamati za Bunge la Katiba na Kura za Maoni. Lakini wakati mwingine matumizi ya kura za maoni yanaweza kuwa na faida na hasara na inategemea sana michakato mingine imekwendaji kuanzia kwenye kukusanya maoni na Bunge la katiba. Nchi nyingi zimeingia katika mgogoro sana katika mchakato wa kura za maoni mfano huo ni nchi jirani ya Kenya (2005 na 2010) na Iraq 2004. Lakini kuna nchi zingine ili kunusuru migogoro hupeleka hoja ambayo ina mvutano mkubwa kwenye kura za maoni na zingine kuishia Bungeni, Mfano 2008 Maldives walifanikiwa kufanya hivyo. Tanzania kama Bunge litashindwa kuridhia suala la Muundo wa Muungano wanaweza wakaacha ili badaye ipigiwe kura ya maoni na wananchi kama suala linalojitegemea. Lakini ukweli unabakia kuwa kura za maoni ni njia nzuri ya kujua kama maoni ya wananchi yamezingatiwa kwenye katiba inapendekezwa. Tatu, Muundo wa Bunge hili Maalum linajinyima nguvu ya kuwa na mamlaka ya kubadili Rasimu ambayo inanguvu ya wananchi. Bunge la Katiba halipaswi kuwa na sura ya Bunge la uwakilishi la kawaida. Bunge la Katiba linapaswa kuwa na mkusanyiko wa makundi karibu yote ya kijamii na siyo vinginevyo. Bunge hili limeundwa kwa aslimia 75 na Bunge la sasa na Baraza la Wawakilishi, kitaalum tayari Bunge hili Maalum linakosa uhalali wa kuitwa

11 | P a g e

Bunge la Katiba kwa kuwa halina tofauti na Bunge la sasa na Baraza la Wawakilishi. Miaka ya nyuma kupitia sheria ya Bunge la Katiba miaka ya 1961, ilikuwa ni Bunge hilo hilo la kawaida linageuzwa kuwa Bunge la Katiba. Utaratibu huo ndio umefanya katiba ya sasa ikose uhalali wa kikatiba. Barani Africa nchi nyingi baada ya Ukombozi kuanzia miaka ya 1960-1980 zimekuwa zikutumia katiba ambazo hazikufuata utaratibu mzuri na shirikishi katika kuziandaa. Mchakato huu wa kugeuzwa mabunge ya kawaida kuwa Bunge la Katiba mara nyingi huondoa uhalisia wa kuwa na katiba ya wananchi. Kuanzia mwaka 1990 tumeshuhudia vuguvugu la kutaka kupata katiba za wananchi na si za watawala. Uganda mchakato ulianza 1988 -1995, Kenya ulianza 1997-2010 na Tanzania sasa ilianza 1998- 2014. Bunge letu hili pia nalo ni wazi kuwa ni lile lile bunge la kawaida limegeuzwa kuwa Bunge la Katiba na Rais kutumia nafasi yake ya viti maalum kuwateuwa wanasiasa 201 kujiunga na wanasiasa wenzao kujadili rasimu ya katiba ya Watanzania.Bunge Maalumu linapaswa kushirikiksha makundi yote ya wananchi. Kundi ambalo limechukua asilimia 75 ya Bunge la sasa ni wanasiasa na mmbaya zaidi wanasiasa wa upande mmoja. Tulipaswa kulitambua hili kabla ya kuamua idadi ya wajumbe wa Bunge la Katiba. Mbaya zaidi hata wale wajumbe 201 ambao wangepaswa kwa mujibu wa sheria kutoka katika makundi yasiyo ya kisiasa tumeona nao wanatoka kwa asilimia zile zile 75 toka kundi lile lile la wanasiasa. Kati ya wajumbe hao 201 kulikuwa na nafasi 40 tu za wanasiasa, lakini cha kushangaza tumeona wanasiasa na viongozi wa vyama vya siasa hasa CCM wakiteuliwa kupitia nafasi za makundi mengine. Mfano, Katika kundi la Asasi za Kiraia, katika nafasi ya watu 20 wajumbe takribani 10 ni makada na viongozi wa CCM, halikadhalika katika makundi mengine hali ni hiyo hiyo ya uwepo wa makada na viongozi wa vyama vya siasa.

12 | P a g e

Muundo huu wa Bunge la Katiba, tayari umeipokonya Bunge hili madaraka ya kubadili ama kutunga Rasimu mbadala kwa kuwa halina makundi yote ya kijamii. Na kama watabadilisha Rasimu hii, ni dhahiri kuwa Katiba hiyo itakuwa ni ya vyama vya siasa hasa chama chenye wajumbe wengi Bungeni (CCM). Na endapo watabadilisha mambo ya msingi ni wazi Katiba hiyo itapigiwa kura ya hapana na wananchi kwa kuwa wameondoa maoni ya wananchi na kuweka maoni ya vyama vyao (Hasa chama chenye makada wengi kwenye Bunge la Katiba). Bunge hili lingepaswa kuwa na moja ya tatu (1/3 ya wanasiasa tena wa vyama vyote) na mbili ya tatu (2/3) wa makundi ya kijamii ili angalau liweze kujiongozea uhalali wa kubadili mambo ya msingi. Muundo huu tayari wazi wazi umejionyesha unamakundi ya kisiasa yenye misimamo tofouti. Kwa kuwa hali hii ilishaonekana mapema, Rais Kikwete alipaswa kutumia busara ya hali ya juu kupunguza nguvu ya wanasiasa Bungeni kwa kuteuwa makundi yasiyo na uhusiano na vyama vya siasa, badala yake wote ni mashaidi wateule karibu wote ni wanasiasa. Mchakato wa katiba ya Uganda 1980-1995 ulikuwa na taswira nzuri kwa kuwa wajumbe 230 wa Bunge la Katiba walipigiwa kura na kuchaguliwa na si kuteuliwa. Wakati mwingine utaratibu huu unaweza rudisha imani ya wananchi. Na mchakato kama huu wakati mwingine hulipa bunge hilo sio mamlaka ya kujadili bali kuwa chombo cha mwisho kupitisha katiba. Tume ya Katiba chini ya Jaji Ben Odoki iliundwa kukusanya maoni na kuandaa rasimu na badaye kupelekwa katika bunge kuidhinishwa. Nne, Bunge la katiba ni taasisi ndani mchakato wa katiba. Tofouti na mabunge ya kawaida Bunge la Katiba sio chombo cha uwakilishi bali ni taasisi inayojitegemea katika mchakato wa katiba. Taasisi haihitaji uwakilishi na wala si chombo cha uwakilishi na ndio maana yoyote yule anaweza kuwa mjumbe wa chombo hiki bila kuzingatia kachaguliwa na wananchi ama lah.

13 | P a g e

Tunasema si chombo cha uwakilishi kwa kuwa wao wamepatikana kwa mujibu wa sheria, lakini wabunge wa mabunge ya kawaida huchaguliwa na wananchi. Chombo hiki kimewekwa Kama taasisi muhimu ndani ya mchakato wa katiba kwa lengo la kujadili na kuboresha rasimu ya katiba itokanayo na wananchi wenyewe. Ila nchi nyingine taasisi hii hutumika moja kwa moja bila kuwa na Tume ya kukusanya maoni. Tufauti kubwa ya chombo hiki na Bunge la Kawaida, ni kwamba hujadili rasimu ya katiba, kuiboresha na kutengeneza katiba itakayopigiwa kura na wananchi kwa lengo la kuhakiki kama mawazo yao kupitia Tume yamezingatiwa na chombo hiki cha kikatiba ama siyo. Lakini Bunge la kawaida hutunga sheria na kupeleka kwa Rais kama sheria iliyopendekezwa ili kupitishwa na Raisi kama sheria kwa niaba ya wananchi. Katika mchakato huu Rais amepewa mamlaka kwa kuwa sheria nyingi hutungwa bila kuwahusisha wananchi. Lakini kwa sheria mama ya nchi, wananchi walitoa maoni na ndio maana wao ndio wenye kauli ya mwisho na si Bunge la Katiba. Uwepo wa kura za maoni, hueleza wazi wazi kuwa Bunge la Katiba si chombo cha uwakilishi na pia hakina maamuzi ya mwisho. Umuhimu wa kura za maoni ni kwa ajili ya kuhakiki kama mawazo ya wananchi kupitia chombo yamezingatiwa na Bunge la Katiba. Kwa utaratibu inakuwa ni vigumu kusema Bunge la Katiba lina madaraka kuja na katiba ambayo ni tofouti na rasimu ya wananchi. Kama Bunge la katiba lingekuwa chombo cha uwakilishi tusingekuwa na haja ya kupiga kura za maoni kwani wale ni wawakilishi wetu. Na kama watafanya hivyo watachukuwa mawazo ya nani kwa kuwa wao sio chombo cha uwakilishi bali ni chombo tu ndani ya mchakato wa katiba wenye mamlaka ya kupendekeza katiba kwa wananchi baada ya kujadili rasimu ya katiba.Itambulike kuwa chombo hiki hakitengenezi rasimu tena bali kinaanda katiba itakayopendekezwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura.

14 | P a g e

Kama tungefuata utaratibu sahihi Bunge la katiba lisingekuwa na wabunge wala wawakilishi, bali lingekuwa na wajumbe si zaidi ya 300 wakiwemo baadhi ya wabunge na wawakilishi. Tena wangepigiwa kura kama ilivyokuwa Uganda. Namalizia kwa kuwashauri wabunge wa Bunge hili maalum wakizingatia mamlaka waliyopewa na wasiende zaidi ya mamlaka na madaraka yao kwani watakuwa wanaandaa katiba itakayokuja kupigiwa kura ya hapana.Na pia vigumu jopo la watu 600 tena wenye itikadi za kisiasa kukaa chini na kuanza kuandaa rasimu mpya. Kuandaa rasimu si jukumu la Bunge la Katiba bali wao wanajukumu la kuipa rasimu nguvu ya kuitwa katiba, pia kuandaa rasimu kuna hitaji utulivu na utaalamu na ndio lengo la kuwa na Tume ya watu wachache ambao pia pamoja na kupata maoni ya wananchi bado utaalamu wao utahitajika. Ni wazi kuwa michakato ya uandaaji wa katiba hutofoatiana toka nchi moja hadi nyingine. Nchi kama Misri waliunda Tume ambayo haikukusanya maoni ya wananchi bali waliandaa rasimu kama Tume ya Wataalum. Tunawasihi wasipeleke misimamo ya vyama kwenye Bunge la Katiba kwani kufanya hivyo ni sawa kuwadharau Watanzania na kuchezea rasimali za nchi. Bunge la Katiba lisipozingatia haya, watakuwa wanajiweka katika mazingira ya kufunguliwa kesi kwa kuvuruga mchakato wa katiba kama ilivyokuwa huko Kenya. Tunalitazama na endapo watakwenda kinyume tutaenda mahakamani. Na Onesmo Olengurumwa Mchambuzi na Mtafiti-Haki za Binadamu na Sheria [email protected]