UFUGAJI BORA WA KUKU - Lantern e-Books

30
UFUGAJI BORA WA KUKU Uboreshaj wa Ufugaj wa Kuku wa Kenyej Ufugaj wa Kuku Chotara Magonjwa, Knga na Tba yake Vmelea, Knga na Tba Vsumbufu na Maovu ya Kuku, Knga na Tba Pus B. Ngeze TANZANIA EDUCATIONAL PUBLISHERS LTD

Transcript of UFUGAJI BORA WA KUKU - Lantern e-Books

UFUGAJI BORA WA KUKU • Uboreshaj� wa Ufugaj� wa Kuku wa K�enyej�• Ufugaj� wa Kuku Chotara• Magonjwa, K�nga na T�ba yake• V�melea, K�nga na T�ba • V�sumbufu na Maovu ya Kuku, K�nga na T�ba

P�us B. Ngeze

TANZANIA EDUCATIONAL PUBLISHERS LTD

��

Tanzan�a Educat�onal Publ�shers Ltd,TEPU House,Barabara ya Uganda,K�wanja Na. 45, K�talu MDA, S�mu: 0685 997583/0758 147871/0784 690277Baruapepe : [email protected]�: tepu.co.tzS.L.P. 1222, Bukoba, Tanzan�a.

© P�us B. Ngeze 2008 Toleo la kwanza 2008 Toleo la p�l� 2013 Toleo la tatu 2015

ISBN 978-9987-07-016-9

Hak� zote z�meh�fadh�wa. Ha�ruhus�w� ku�ga, kutafs�r�, kup�ga chapa, kunak�l� au kuk�toa k�tabu h�k� kwa j�ns� ny�ng�ne yoyote �le b�la �dh�n� ya maand�sh� ya Tanzan�a Educat�onal Publ�shers Ltd.

���

YALIYOMO Uk.Utangul�z� .................................................................... �x

1 ASILI, MAANA YA KUFUGA, MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUAMUA KUFUGA, FAIDA NA HASARA ZA KUKU ............................................. 11. As�l� ya kuku ............................................................................... 12. Sehemu kuu za kuku ................................................................... 13. Mfumo wa uzaz� wa kuku ........................................................... 24. Maana ya ufugaj� ......................................................................... 25. Mambo ya kuz�ngat�a kabla ya kuanza ufugaj� wa kuku ............ 26. Fa�da za kuku .............................................................................. 37. Hasara za kuku ............................................................................ 4

2 AINA KUU NA MAKABILA YA KUKU ................................ 6 1. Kuku wa k�enyej� .................................................................... 6 2. Kuku wa k�gen� ....................................................................... 6 A: Kuku wa k�zaz� menyu .......................................................... 7 · Kuku wepes� ......................................................................... 7 · Kuku waz�to .......................................................................... 8 B: Kuku chotara .......................................................................... 11

3 MAMBO YANAYOATHIRI UFUGAJI BORA WA KUKU NCHINI ..................................................................................... 14 1. Kutojua umuh�mu wa kufuga kuku na namna ya kuwafuga .. 14 2. Kutokuwa na ujuz� wa kufuga kuku ..................................... 15 3. Upungufu au ukosefu wa Mtaj� ............................................. 15 4. Magonjwa na v�melea ........................................................... 16 5. Uchache au kutokuwapo kwa v�tuo vya kuangul�a v�faranga 16 6. Kutopat�kana kwa urahs� chakula cha kuku .......................... 16 7. Utaf�t� mdogo ........................................................................ 17

4 MIFUMO YA UFUGAJI WA KUKU ....................................... 18 Mambo ya kuzingatia katika kuchagua aina ya mfumo .... 18

1. Madhumun� ya kufuga ....................................................... 18

�v

2. Mtaj� ul�onao ...................................................................... 183. Ukubwa wa eneo ul�lonalo ................................................. 184. Idad� ya kuku watakaofugwa ............................................. 18

Aina za mifumo ...................................................................... 191. Ufugaj� hur�a ..................................................................... 192. Ufugaj� wa ndan� na nje .................................................... 20 (a) Ufugaj� kwa kutum�a nyumba na ua ............................ 20 (b) Ufugaj� wa kutum�a nyumba ya kukunja �nayoham�sh�ka ............................................................ 223. Ufugaj� wa ndan� kwa ndan� .............................................. 23

(a) Ufugaj� wa kutum�a matand�ko .................................... 23(b) Ufugaj� kat�ka nyumba ya waya .................................. 26

5 BANDA BORA LA KUKU .................................................... 291. S�fa za banda bora la kuku ................................................ 292. V�faa v�navyoh�taj�wa kat�ka banda la kuku ..................... 33

6 MAHITAJI NA UMUHIMU WA MAJI NA CHAKULA KWA KUKU ........................................................................... 37

1. Utangul�z� ........................................................................... 372. Fa�da za chakula bora ........................................................ 373. Mfumo wa mmeng’enyo wa chakula ................................ 384. A�na za vyakula na kaz� zake ............................................ 39

7 UPATIKANAJI WA VYAKULA VYA KUKU WA UMRI NA AINA TOFAUTI .............................................................. 46

1. A�na na mah�taj� ya vyakula kwa kufuata umr� ................ 462. Kanun� ya kuj�tengenezea chakula ..................................... 473. Kukokotoa uw�ano wa kubad�l� chakula kuwa mazao ya kuku .............................................................................. 48

8 UBORESHAJI WA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI ....................................................................... 52

1. Utangul�z� ......................................................................... 52

v

2. S�fa za kuku wa k�enyej� ................................................... 533. Nj�a za kuboresha ufugaj� wa kuku wa k�enyej� ................ 53

9 UFUGAJI WA KUKU WA KUTAGA .................................... 601. S�fa z�nazotak�wa kwa Watagaj� ........................................ 602. Maandal�z� yanayotak�wa kabla ya kuleta watagaj� ......... 613. Maandal�z� ndan� ya nyumba ya kufug�a kuku wa maya� 624. Matunzo baada ya ku�ng�za kuku kat�ka nyumba ............ 645. Uokotaj� wa maya� ........................................................... 666. Usaf�shaj� wa maya� na kuyapanga kat�ka gred� .............. 667. H�fadh� ya maya� .............................................................. 678. Uwekaj� wa kumbukumbu ............................................... 679. Mambo yanayosabab�sha utagaj� ukosekane kab�sa, upungue au maya� yawe na kasoro .................................... 6810. J�ns� ya kutambua kuku wanaotaga ................................... 6811. Mpang�l�o wa ufugaj� kuku wa maya� utakao kuhak�k�sh�a mapato kwa k�p�nd� k�refu .......................... 6912. Sababu za maya� meng� kuvunj�ka kund�n� ..................... 6913. Mambo ya kufanya �l� kuku waendelee kutaga v�zur� ..... 6914. Mambo yanayoweza kusabab�sha upungufu wa �dad� ya maya� ................................................................................ 70

10 UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA .................................. 731. Maana na s�fa za kuku wa nyama .................................... 732. Upat�kanaj� wa v�faranga wa kuku wa nyama ................. 733. Mambo ya kuz�ngat�a �l� kufan�k�sha ufugaj� wa kuku wa nyama ......................................................................... 734. Utunzaj� wa kuku wa nyama ............................................ 74

11UBORESHAJI WA UTOTOAJI NA MALEZI YA VIFARANGA VYA KUKU WA KIENYEJI ........................ 76

1. Utotoaj� wa v�faranga kwa kutum�a makoo badala ya v�atam�o ............................................................................. 762. V�ota kwa aj�l� ya kuatam�a .............................................. 763. S�fa za koo anayefaa kuatam�a maya� .............................. 77

v�

4. S�fa za maya� ya kuatam�a ................................................ 785. Utunzaj� wa kuku anayeatam�a ......................................... 786. Malez� ya v�faranga .......................................................... 797. K�p�nd� cha kuku kulea v�faranga ..................................... 808. Ugonjwa mbaya wa v�faranga na udh�b�t� wake .............. 819. Usaf� wa v�ota, vyombo vya kul�a chakula na kunywea maj� ................................................................................... 81

12 UTOTOAJI WA VIFARANGA KWA KUTUMIA VIATAMIO .......................................................................... 82

1. Kuchagua maya� yanayofaa .............................................. 832. Kutayar�sha k�atam�o ........................................................ 843. Upevushaj� na utotoaj� wa v�faranga ............................... 844. Utotoaj� na hadhar� ndan� na nje ya chumba cha kutotolea ........................................................................... 86

13 MALEZI YA VIFARANGA WA KUKU WA KIENYEJI NA KUKU CHOTARA ............................................................. 88

1. Nj�a za kupata v�faranga .................................................. 882. Kanun� za kulea v�faranga ............................................... 893. Nj�a kuu za kulea v�faranga ............................................. 90

(a) Kwa kutum�a makoo ................................................ 90(b) B�la kutum�a makoo ................................................. 92

14 TARATIBU ZA KULEA NA KUKUZA VIFARANGA WA KUKU CHOTARA NA KUKU KIENYEJI .................. 100 A: Vifaranga wa kuku chotara ............................................. 100 1. Maandal�z� yanayotak�wa .............................................. 100 2. Mambo ya ms�ng� ya kuz�ngat�wa .................................. 101 3. Maandal�z� ya chumba au banda la kulelea v�faranga .... 101 4. Tarat�bu za kuz�ngat�a kabla na baada ya ku�ng�za v�faranga bandan� (chumban�) ........................................ 102 B: Vifaranga wa kuku wa kienyeji ....................................... 104

C: Mfano wa utaratibu wa kulea vifaranga wa kuku wa nyama ................................................................................. 105

v��

15 MAMBO YANAYOATHIRI AFYA ZA KUKU .................. 107 1. Athar� za mambo makuu .................................................... 107 1.1 Chakula ........................................................................ 107 1.2 V��n� vya magonjwa ..................................................... 109 1.3 V�melea ........................................................................ 109 1.4 Sumu ............................................................................ 110 2. Kaz� za V��n�l�she, Mad�n� na V�tam�n� kat�ka m��l� ya kuku ................................................................................... 111 2.1 Chakula ........................................................................ 111 2.2 Mad�n� .......................................................................... 111 2.3 V�tam�n� ....................................................................... 112

16 NJIA ZA KUZUIA KUKU WASIAMBUKIZWE NA MAGONJWA ................................................................ 114

17 MAGONJWA, KINGA NA TIBA ....................................... 1211. Mdondo ......................................................................... 1212. Gumboro ....................................................................... 1253. Koks�d�a ........................................................................ 1264. Homa ya Matumbo . ...................................................... 1295. Ndu� ya kuku ................................................................ 1336. Mahepe ......................................................................... 1357. Ugonjwa sugu wa upumuaj� ......................................... 1368. Ugonjwa wa kuhara wa v�faranga v�dogo .................... 1379. Ugonjwa Mkamba unaoambuk�za ................................ 13810. Saratan� ya kuku ........................................................... 13811. K�p�ndup�ndu cha ndege wa kufuga ............................. 13912. Homa ya kuku ............................................................... 140 13. Kukohoa kohoz� la damu .............................................. 14114. Mafua ya Ndege ............................................................. 14115. Ugonjwa wa v�faranga v�dogo ...................................... 14416. Kupooza ......................................................................... 14517. Kuv�mba kwa m�guu .................................................... 14518. Magonjwa yaletwayo na v�melea vya ngoz� . ................ 14619. Magonjwa yaletwayo na m�nyoo . ................................. 147

v���

20. Magonjwa yaletwayo na sumu ...................................... 14721. Magonjwa yaletwayo na ukosefu wa v�rutub�sho muh�mu vya vyakula .................................................... 148

18 VIMELEA NA VISUMBUFU VYA KUKU ....................... 151A: Vimelea ........................................................................... 151 1. V�melea v�navyoshambul�a kuku kwa nje .................. 151 2. V�melea v�navyoshambul�a kuku kwa ndan� .............. 157B: Visumbufu ...................................................................... 160

19 MAOVU YATENDWAYO NA KUKU KUNDINI NA KINGA YAKE .................................................................... 162

1. Kudonoana ..................................................................... 1622. Ulaj� wa maya� ............................................................... 163

20 UTAFUTAJI WA SOKO NA MAANDALIZI YA MAZAO YA KUKU KWA AJILI YA KUUZA .................. 165

1. Maana ya soko na utafutaj� wake .................................. 1652. Utayar�shaj� wa mazao makuu ya kuku ......................... 166

21UFUGAJI WA KUKU KIBIASHARA NA UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU ZA UFUGAJI .................................. 169

1. Soko na mtaj� wa kuanz�sh�a ufugaj� ............................. 1692. Utunzaj� kumbukumbu za ufugaj� .................................... 170 (a) Maana ya kumbukumbu ............................................ 170 (b) A�na za kumbukumbu ................................................ 170 (c) Fa�da za kumbukumbu. .............................................. 174

VITABU VYA MAREJEO ........................................................... 175

TAFSIRI KWA KINGEREZA YA MAGONJWA NA VYAKULA VYA KUKU .............................................................. 176

�x

UTANGULIZI Ndege maarufu wanaofugwa na b�nadamu kwa aj�l� ya maya� na nyama yao n� wa a�na s�ta z�fuatazo: kuku, bata, batamz�nga, bata buk�n�, nj�wa na kanga. Kat� ya hao s�ta, ndege al�ye maarufu za�d� ya weng�ne n� kuku. Kutokana na umaarufu huo, k�tabu h�k� k�nahusu ndege huyu. Kuku wanaofugwa hapa nch�n� hutengwa kat�ka a�na kuu mb�l�: (a) Kuku wa K�enyej� na (b) Kuku wa K�gen�. Kuku wa K�gen� nao hutengwa kat�ka a�na kuu mb�l�, yaan� (a) Kuku K�zaz� Menyu na (b) Kuku chotara. Hapa nch�n� kuku wanaofugwa za�d� n� Kuku wa k�enyej� na Kuku chotara. Kuku chotara n� kwa aj�l� ya ufugaj� wa k�b�ashara. Kuku K�zaz� Menyu hawafugw�. Inak�s�wa kuwa as�l�m�a t�s�n� (90%) ya makaz� nch�n�, hasa ya V�j�j�n�, yanafuga kuku. Kuku wanaofugwa za�d� n� wale wa k�enyej�. Kwa makaz� meng�, �dad� ya kuku wanaofugwa ha�z�d� kum� (10). Mfumo wa ufugaj� unaotum�wa n� Ufugaji Huria. Yaan�, kuku huach�wa jukumu la kuj�tafut�a malaz�, chakula, maj� na kuj�l�nda dh�d� ya v�sumbufu vyake. Ak�ugua hat�b�shw�! Atakufa au atapona. Madhumun� ya ufugaj� huu s� ya k�b�ashara, n� ya kuj�pat�a k�toweo k�dogo, maya� kwa aj�l� ya watoto na fedha k�dogo ak�uza mazao yao, yaan�, kuku kwa aj�l� ya nyama na maya�. Ufugaj� wa k�b�ashara huendeshwa na wafugaj� wachache wa m�j�n�. Hutum�a kuku chotara kwa kufuata kanun� za ufugaj� bora wa kuku. Wafugaj� wa a�na h�yo s� weng� hata m�j�n�. H�� n� kwa sababu watu weng� huogopa kufuga kuku chotara b�la kuwa na ujuz� wa kanun� za ufugaj� bora wa kuku hao. K�tabu h�k� k�meandal�wa �l� kuwashaw�sh� watu weng� V�j�j�n� na M�j�n� kuanz�sha shughul� ya ufugaj� wa kuku k�b�ashara. Shughul� h�� �nal�pa sana. Mfugaj� anaweza kuachana na umask�n� baada ya m�aka m�w�l� (2) tu. K�tabu h�k� k�naeleza:• Namna ya kuboresha Ufugaj� wa Kuku wa K�enyej� �l� waweze

kuongezeka k��dad�, waongeze uwezo wa kutaga maya� na waongeze uz�to wa nyama.

• Namna ya kufuga k�b�ashara kuku chotara wa kutaga na wa nyama.• Kanun� za Ufugaj� Bora wa Kuku ambazo n� pamoja na h�z� z�fuatazo:

(�) Kuchagua na kufuga kuku wenye s�fa nzur�.

x

(��) Kuwapat�a kuku nyumba bora.(���) Kuwapat�a kuku chakula bora kwa kuz�ngat�a umr� (v�faranga na kuku wakubwa) na a�na ya kuku.(�v) Kuwapat�a kuku maj� saf�, salama na ya kutosha.(v) Kuzu�a na kudh�b�t� maambuk�z� ya magonjwa.(v�) Kudh�b�t� v�sumbufu vya kuku, kama v�le v�melea, wadudu,

ndege na wanyama.(v��) Kudh�b�t� v�tendo v�ovu vya kuku.(v���)Kutafuta soko la maya� na nyama ya kuku.(�x) Kuandaa maya� na kuku wa nyama kwa aj�l� ya soko.(x) Kuweka kumbukumbu muh�mu za ufugaj� wa kuku.

K�tabu h�k� k�natoa ufafanuz� wa kanun� h�zo.Mbal� na kuandal�wa mahsus� kwa aj�l� ya wafugaj� na wale wanaotaka kuanz�sha ufugaj� wa kuku, �mekusud�wa k�tabu h�k� k�wasa�d�e p�a Maof�sa Ugan� na Wataalamu wa M�fugo, hususan, wa kuku, �l� waweze kuwasa�d�a wafugaj� wapya na wa zaman� wa kuku kusud� waweze kufuga k�b�ashara. Soko la nyama ya kuku ambayo n� nyeupe na maya� n� kubwa sana. K�la s�ku walaj� wa mazao hayo maw�l� wanaongezeka na wataendelea kuongezeka. Watu wal�o na umr� wa m�aka hams�n� na kuendelea wanashaur�wa na madaktar� kula za�d� nyama ya kuku na samak� badala ya nyama nyekundu ya ng’ombe, mbuz�, kondoo n.k. A�dha, watoto wadogo, v�jana na watu waz�ma, was�okuwa na tat�zo la sh�n�k�zo la damu au magonjwa ya moyo, wanashaur�wa kula maya� kwa afya nzur�. Kwa h�yo, n� busara ufugaj� wa kuku nch�n� upewe msukumo mpya, kuanz�a ndan� ya fam�l�a, v�j�j�, kata, w�laya, mkoa na ta�fa. Natuma�n� k�tabu h�k� k�tatoa mchango wa kutosha kat�ka msukumo huo �l� kuondoa umask�n� kwa watakaoamua kufanya h�vyo k�b�ashara na kuwa na ta�fa lenye afya, kuanz�a kwenye ngaz� ya fam�l�a. Lengo n� k�la fam�l�a kufuga kuku k�sasa �l� kutosheleza mah�taj� ya fam�l�a na z�ada �uzwe �l� kuj�pat�a fedha. K�la fam�l�a nch�n� �naweza kufuga kuku wachache.N� matuma�n� yangu kuwa k�tabu h�k� k�tawaf�k�a walengwa na watak�soma, watak�elewa na watatum�a el�mu �l�yomo �l� waweze kuboresha Ufugaji wa kuku wa kienyeji na Ufugaji wa kuku chotara wa kutaga na wa nyama.

1

1Sura ya

ASILI, MAANA YA KUFUGA, MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUAMUA KUFUGA, FAIDA NA HASARA ZA KUKU.

1. Asili ya KukuAs�l� ya kuku wanaofugwa popote dun�an� n� a�na fulan� ya ndege wa mw�tun� ambao wal�kamatwa na kufugwa kwa madhumun� mbal�mbal�. Kat� ya m�aka elfu nne (4,000) na elfu tano (5,000) �l�yop�ta watu wa wakat� huo wal�anza kutotoa v�faranga b�la kutum�a makoo. Mnamo karne ya kum� na t�sa (19), watu wal�anza ufugaj� wa kuku kama shughul� mojawapo ya k�l�mo. Mafunzo ya ufugaj� bora wa kuku yakaanz�shwa kwenye baadh� ya Vyuo vya K�l�mo. Baadaye, shughul� za ufugaj� wa kuku z�l�panul�wa kat�ka nch� mbal�mbal�.

2. Sehemu kuu za kukuKuku n� ndege anayefugwa. Ana sehemu kuu kama z�navyoonekana kat�ka mchoro hapa ch�n�:

Sehemu za kuku

J�cho

Paja

S�k�o

Undu

Mk�aMdomo

Bawa

MguuV�dole

Tumbo

K�fua

Tundu la pua

2

3. Mfumo wa uzazi wa kukuMfumo wa uzaz� wa kuku n� kama ul�vyoonyeshwa kat�ka mchoro ufuatao:0

Mfumo wa uzazi wa kuku

4. Maana ya UfugajiUfugaj� n� shughul� mojawapo ya k�l�mo ambayo �nahusu uzal�shaj�, utunzaj�, ul�shaj� na t�ba kwa mojawapo ya a�na kadhaa za m�fugo. A�na h�zo n� pamoja wanyama wakubwa (kama v�le ng’ombe, faras�, punda, mbuz� na kondoo) na wanyama wadogo (kama v�le sungura, mbwa, pamoja na paka). Weng�ne n� kuku na a�na ny�ng�ne za ndege, kama v�le bata, batamz�nga, batabuk�n�, kanga na nj�wa. A�na ny�ng�ne ya m�fugo n� samak� na wadudu kama v�le nyuk� na v�pepeo. K�la a�na ya m�fugo �na fa�da zake, ny�ng�ne z�k�wa n� maalumu. Mkul�ma huamua kufuga moja au za�d� ya a�na h�zo kwa sababu mbal�mbal�.

5. Mambo ya kuzingatia kabla ya kuanza Ufugaji wa KukuK�la mtu anaweza kufuga kuku. Lak�n�, s� k�la mtu anaweza kuwafuga k�uchum� na kupata fa�da ya kutosha. Kwa upande mw�ng�ne, kwa v�le kuna nj�a mbal�mbal� na madhumun� tofaut� ya kufuga kuku, wafugaj� wataweza kuchagua mfumo wa kuwafuga. Kabla ya kuanza kufuga na afuge k�as� gan� cha kuku, kuku wa

Chembek�ke UtumboKloaka

MkunduGole

Mferej� wa kusaf�r�sha maya� kutoka ovar� kwenda Mj� wa m�mba

3

a�na �p� na kwa kutum�a mfumo up�, n� laz�ma mfugaj� aj�ul�ze na kuz�ngat�a mambo yafuatayo:(a) madhumun� ya kufuga kuku.(b) A�na ya kuku wa kufuga.(c) Mtaj� al�onao au �wapo anazo s�fa za kuweza kupata mkopo.(d) Iwapo analo eneo l�nalofaa kwa ufugaj� na l�nalotosha.(e) Maz�ng�ra na tab�a ya nch� ya mahal� al�po.(f) Iwapo l�po soko zur� la kuuza mazao ya kuku.(g) Iwapo ana el�mu na ujuz� wa a�na ya kuku anaotaka kufuga.(h) Iwapo huduma za ugan� z�napat�kana kat�ka sehemu h�yo. Huduma

h�z� hutolewa na wataalamu wa m�fugo, hususan, wa kuku.(�) Je, ser�kal� �nayo m�pango na programu ya kuendeleza ufugaj� wa

kuku?(j) Je, upo uwezekano wa kupata v�faranga au kuku wa kufuga,

pamoja na mah�taj� yake kama v�le dawa, vyakula, maj� saf�, v�faa vya kujengea n.k. kwa be� nafuu na kwa wakat� unaofaa.

6. Faida za kukuKuku wana fa�da ny�ng�. Z�l�zo muh�mu za�d� n� h�z� z�fuatazo:(a) Mayai na nyama kwa matumizi ya familia Kuku hula nafaka na vyakula vya a�na ny�ng�. Huv�geuza vyakula

h�v� kuwa maya� na nyama. Nyama ya kuku �na prot�n� ny�ng�. Maya� yana prot�n� ny�ng�, v�tam�n� na mad�n�. Kwa h�yo, b�nadamu ak�la maya� na nyama ya kuku huj�pat�a prot�n� ny�ng�, v�tam�n� na mad�n� kwa urah�s�. A�dha, mfugaj� wa kuku huj�pat�a maya� na nyama kwa aj�l� ya fam�l�a yake.

(b) Urahisi wa kuchinja kuku kwa ghafla N� rah�s� kuch�nja kuku kul�ko mbuz� au ng’ombe. Uk�pata mgen�

wa ghafla n� rah�s� kumch�nj�a kuku kul�ko mnyama wa a�na ny�ng�ne.

(c) Uwezo wa kutumia chakula kidogo kutengeneza mayai na nyama Kuku wana uwezo mkubwa sana wa kutum�a k�as� k�dogo cha

chakula chao kutengeneza maya� na nyama. (d) Urahisi wa kuwafuga katika eneo dogo la ardhi A�dha kutokana na kuku kuwa na umbo dogo �nakuwa rah�s�

4

kuwafuga kat�ka sehemu ndogo ya ardh�.(e) Fedha kwa mfugaji Mfugaj� ak�uza maya� na nyama ya kuku huj�pat�a fedha, tena

ny�ng�.(f) Mbolea K�nyes� cha kuku k�mechangany�ka na mkojo wake. N� mbolea

nzur� sana kwa kurutub�sha udongo. Mbolea ya kuku �na n�trojen� ny�ng�. Upotevu wa mbolea n� k�dogo sana. A�dha, gharama za uchukuz� na za kutandaza mbolea h�� n� ndogo uk�l�ngan�sha na kutum�a samad�. Kuku aroba�n� (40) wak�fugwa ndan� ya nyumba yenye matand�ko, huweza kutoa tan� moja ya mbolea kwa mwaka. M�mea �nayostaw�shwa kwa mbolea h�� hustaw� v�zur�.

(g) Manyoya Manyoya ya kuku n� meroro. Kwa sababu h��, yanafaa kujaza

magodoro, m�to n.k. Manyoya haya yanapendwa na n� ya gharama. Kwa h�yo, yak�uzwa humpat�a mkul�ma fedha. Anaweza p�a kuyatum�a kwa mah�taj� ya fam�l�a yake.

(h) Huangamiza wadudu waharibifu Kuku wanaweza kuangam�za wadudu. Baadh� yake huhar�bu

m�mea ya mazao shamban� na mavuno yal�yoh�fadh�wa maghalan�. Kuku hula mchwa, nz�ge, panz� na a�na fulan� za wanyama wadogo kama v�le nyoka.

5. Hasara za kukuPamoja na fa�da z�l�zoelezwa hapo juu, kuku huleta hasara p�a. Kuku wanaofugwa na kuachwa hur�a kuj�tafut�a chakula na kuj�l�nda:(�) Huhar�bu mazao shamban�. Huweza kula maua, m�mea m�changa

au majan� yake.(��) Huweza kuvuruga udongo ul�otengenezwa kwa aj�l� ya kupanda

mbegu.(���) Huvuruga na kutawanya matandazo yal�yo shamban�.(�v) Wadudu, kama v�le ut�t�r�, wanaoshambul�a kuku, huweza p�a

kuwasumbua b�nadamu.

5

MASWALI YA KUJIPIMA UELEWA

1. Taja a�na nne (4) za ndege wanaofugwa.

2. Taja a�na kuu mb�l� za kuku.

3. Kuku wa k�enyej� n� wa a�na gan�?

4. Eleza kwa k�fup� kuku wa k�gen�.

5. Taja kanun� s�ta za ufugaj� bora wa kuku.

6. As�l� ya kuku n� �p�?

7. Kufuga n� n�n�?

8. Taja mambo matano ya kuz�ngat�a kabla ya kuanza ufugaj� wa kuku.

9. Taja fa�da s�ta za ufugaj� wa kuku.

10. Taja hasara tatu za kuku.

6

AINA KUU NA MAKABILA YA KUKU Makundi makuu ya kukuKuku wanaofugwa nch�n� wamegawany�ka kat�ka makund� maw�l� yafuatayo:(a) Kuku wa k�enyej� (k�as�l�) na (b) Kuku wa k�gen�.

1. Kuku wa kienyejiWafugaj� weng� wa kuku nch�n� hufuga a�na kadhaa za kuku wa k�enyej�. J�na l�ng�ne la kuku wa k�enyej� n� kuku wa as�l�. Tab�a za kuku hawa s� maalumu na huweza kubad�l�kabad�l�ka na kutofaut�anatofaut�ana. Tab�a h�zo n� pamoja na ukubwa wa kuku, uz�to, rang� ya manyoya, uwezo wa kutaga maya� na k�wango cha kukua. Kuku wa k�enyej�:(a) hukua polepole.(b) N� wadogo kwa umbo.(c) Maya� yao huwa madogo. (d) Nyama yao n� ngumu, lak�n� �k�p�kwa na ku�va v�zur� �na harufu

nzur� na ladha yake n� nzur� p�a. Kutokana na a�na ya vyakula wanavyokula, nyama yake n� maarufu sana, hasa kwa walaj� wa m�j�n�.

2. Kuku wa kigeniKuku hawa as�l� yao n� nje ya nch�, yaan�, z�l��ng�zwa nch�n� kutoka nch� ny�ng�ne za nje. Kuku hawa hutengwa kat�ka a�na kuu mb�l�, yaan�: (a) K�zaz� menyu na (b) Chotara. S�fa za kuku wa k�gen� n� h�z� z�fuatazo:(a) Hukua haraka.(b) N� wakubwa kwa umbo, kwa h�yo, wana nyama ny�ng�.(c) Hutaga maya� meng� na makubwa.(d) Nyama yake n� la�n�.

2Sura ya

7

A: Kuku wa kizazi menyuKuku hawa n� menyu kwa a�na moja na hutengwa kat�ka makund� maw�l� yafuatayo: (a) Kuku wepes� na (b) kuku waz�to.

(a) Kuku WepesiKuku wa kund� h�l� huwa na mw�l� mdogo na hata wak�wa na mw�l� mkubwa, huwa wepes� za�d� wak�l�ngan�shwa na kuku wal�o kat�ka kund� la kuku waz�to. Kutokana na kuwa wadogo kul�ko kuku wakubwa, hawafa� kufugwa kwa aj�l� ya nyama. Wafugwe kwa aj�l� ya kupata maya�, au maya� na nyama.

Sifa:(�) Wana umbo dogo.(��) N� watagaj� wazur� wa maya�. Kuku mmoja hutaga maya� 140-300

kwa mwaka. Idad� hal�s� ya maya� hutegemea matunzo mazur� wanayoyapata.

(���) Hutaga maya� yenye ganda jeupe.(�v) N� wakal�.(v) Hutaga maya� kum� na maw�l� kwa uw�ano wa 1:82 kwa k�lo moja ya

chakula.(v�) Hukua haraka. Wanakomaa upes� za�d�. Mtetea anaweza kutaga

ak�wa na umr� wa m�ez� m�nne au m�tano, ak�wa na uz�to wa wastan� wa k�logramu moja na nusu.

(v��) Lobu zao za mas�k�o n� nyeupe.(v���) Undu au ushung� au upanga huwa n� mkubwa. Kwa tembe undu

huweza kuonekana kama wa jogoo.(�x) Kwa kawa�da hawaonyesh� dal�l� za kuatam�a maya�. S�fa h�� n� nzur�

kwa ufugaj� wa kuku wa maya�, lak�n� s�fa h�� n� mbaya kwa ufugaj� kwa aj�l� ya kuangua maya� kwa kutum�a temba.

Makabila ya Kuku WepesiKab�la l�nalofugwa za�d� hu�twa Leghorn. A�na ya kuku wal�o kat�ka kab�la h�l� hutambul�wa kwa rang� zake, nao n�:(�) White Leghorn: Hawa wana rang� nyeupe.(��) Black Leghorn: N� weus�.

8

(���) Brown Leghorn: N� hudhurung�.

White Leghorn

Kab�la l�ng�ne n� M�norcas. Lak�n�, hawa hufugwa kwa uchache uk�l�ngan�sha na Leghorn. Ancona n� kab�la j�ng�ne. Anafanana na Leghorn.

Ancona

(b) Kuku WazitoKwa kawa�da kuku hawa huwa na mw�l� mkubwa na huwa waz�to wak�l�ngan�shwa na kund� la kuku wepes�. Hawa n� kuku wa nyama.

9

Hufugwa kwa aj�l� ya kul�wa nyama. Kwa v�le kuku hawa n� wakubwa, hula chakula k�ng� na huh�taj� nafas� kubwa ya nyumba kul�ko kuku wepes�. Kwa kawa�da hufugwa kwa aj�l� ya nyama na maya�. A�dha, wanaweza kufugwa �l� kupata mbegu bora kutokana na kuku wetu wa k�enyej�.

Sifa:(�) Hukua haraka sana.(��) Wana nyama nyeupe na nzur�.(���) N� wapole, lak�n� wanaweza kubad�l�ka na kuwa wakal�. (�v) Wana uz�to mkubwa. Wak�shakua na kukomaa, temba huf�k�a uz�to

wa k�lo 2.8 na jogoo huf�k�a uz�to wa k�lo 3.6 kwa wastan�.(v) Muda ambao kuku huchukua kutoka k�faranga mpaka wakat� wa kukomaa n� mrefu za�d� kul�ko ule wa kuku wepes�, hata kama

makund� haya yanafugwa kwenye hal� z�l�zo sawa.(v�) Kwa kawa�da wanaweza kuonyesha dal�l� ya kuatam�a maya�.(v��) Umbo lao n� mraba.(v���) V�chwa vyao n� v�dogo uk�l�ngan�sha na umbo la m��l� yao.(�x) Wana sh�ngo nene na fup�.

Makabila ya Kuku WazitoMakab�la maarufu kat�ka kund� h�l� n� haya yafuatayo:(i) Rhode Island Red

Rhode Island Red

10

Kuku hawa wana rang� kar�bu nyekundu. Wanafugwa sehemu ny�ng� sana nch�n�. Wametum�ka kutoa mbegu bora kwa kuwachanganya na kuku wa k�enyej�.

(ii) Australorp Kuku hawa wana rang� nyeus� (labda kama wamechangany�ka

damu).(iii) New Hampshire

New Hampshire

Kuku hawa n� wakubwa, weupe na mchangany�ko wa manyoya meng�.(iv) Light Sussex

Light Sussex

Hawa hufugwa za�d� kwa aj�l� ya maya�. Kwa ujumla n� weupe na wana manyoya meng� sh�ngon�.

168

kusagwa �l� kul�sha kuku na wanyama weng�ne. Watakuwa wamej�pat�a kal�s�.

(g) Makaka ya mayaiHaya nayo yanaweza kusagwa na kutum�ka kul�sha kuku, kwa h�yo, kuj�pat�a kal�s�.

MASWALI YA KUJIPIMA UELEWA

1. Eleza kwa ufup� maana ya soko.

2. Soko la maya� na nyama ya kuku n� ........................

3. Eleza kwa ufup� nj�a bora ya kuch�nja kuku.

4. Eleza kwa ufup� namna ya kutayar�sha maya� kwa aj�l� ya soko.

5. Taja mazao meng�ne matano ya kuku.

169

UFUGAJI WA KUKU KIBIASHARA NA UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU ZA UFUGAJI

1. Soko na Mtaji wa kuanzishia ufugajiUfugaj� wa kuku k�b�ashara n� shughul� ya b�ashara kama v�le kuendesha b�ashara ya duka, k�wanda, nyumba ya kulala wagen�, baa, hotel� ya kuuza chakula n.k. Kama mwenye duka au k�wanda hana soko la kuuza b�dhaa al�zonazo au anaz�uza kwa hasara, atalaz�m�ka kufunga duka h�lo au k�wanda h�cho. Atafanya h�vyo baada ya kuj�kuta mtaj� unaz�d� kupungua na matum�z� kwa mwez� au mwaka n� makubwa kul�ko mapato. K�l�chotokea n� kuwa ama wateja wamepungua kutokana na sababu mbal�mbal� au hakufanya utaf�t� kabla ya kuanza a�na h�yo ya b�ashara �l� kujua ukubwa wa soko. Hal� n� h�yo hata kwa ufugaj� wa kuku.

K�tabu h�k� k�nazungumz�a ufugaj� wa kuku k�b�ashara. Lengo n� kumwondoa mfugaj� kat�ka kund� la mask�n�. Kwa h�yo, �l� kufan�k�wa, laz�ma mfugaj� kabla hajaamua kuanza kufuga kuku k�b�ashara afanye yafuatayo:(a) Afanye utafiti wa kina �l� kujua ukubwa wa soko la maya� au nyama

ya kuku. Kama hawez� kufanya kaz� h�yo, bas� aombe msaada wa wataalamu wa Halmashaur� ya W�laya, Man�spaa au J�j�. Matokeo ya utaf�t� huu nd�yo yatakayokusa�d�a kufanya uamuz� wa kufuga au kutofuga au ufuge kuku wa kutaga au kuku wa nyama na k�as� gan�.

(b) Apate uhakika wa kupata mtaji wa kuanzishia na kuendeshea biashara hii.

Ufugaj� wa k�sasa wa kuku unah�taj�:• Ujenge nyumba nzur� ya kuku.• Ununue maramba, nyas� kavu n.k. kwa aj�l� ya matand�ko ndan�

ya nyumba ya kuku.• Ununue vyombo vya kul�a (chakula) na kunywea (maj�).

21Sura ya

170

• Ununue v�faa (vyombo) v�takavyotum�ka kutoa joto kat�ka chumba cha v�faranga.

• Kununua chakula, chanjo na dawa za kutum�a had� utakapoanza kuuza maya� (baada ya w�k� 6 - 10) au kuuza nyama ya kuku.

• Kuwal�pa wafanyakaz� m�shahara.• Kufanya mal�po ya a�na ny�ng�ne.

Fedha z�nazotak�wa z�naweza kuwa malak� kadhaa au mam�l�on� ya sh�l�ng�. Je, fedha h�zo unazo? Kama huna utapaswa kuz�kopa kutoka benk� au asas� ny�ng�ne za fedha z�nazokopesha. Swal� n� je, uk�omba mkopo utapewa? Us�popewa au us�pokuwanazo huwez� kufuga hata kama soko l�po! Kama utapewa mkopo, utalaz�m�ka kuendesha shughul� h�yo k�b�ashara.

2. Utunzaji, Aina na faida za Kumbukumbu za Ufugaji(a) Maana ya kumbukumbu

Kumbukumbu n� maand�sh� yal�yo sah�h� ya matuk�o, jambo au habar� �l�yotokea au ya mambo yal�yofany�ka kwenye shamba au yanayohus�ana na shughul� unayofanya. Il� baada ya k�p�nd� fulan� (mwez� au mwaka) kuweza kujua �wapo mrad� huu wa ufugaj� ul�leta fa�da au hasara, n� laz�ma utunze kumbukumbu ya mambo na matuk�o mbal�mbal� yanayotokea au kufany�ka kwenye shamba lako kuhus�ana na ufugaj� huu wa kuku.

(b) Aina za kumbukumbuZ�fuatazo n� a�na muh�mu za kumbukumbu za ufugaj� wa kuku:(i) Kumbukumbu ya chakula Iand�kwe k�la s�ku. Kumbukumbu h�� huanz�a tarehe 1 had�

tarehe ya mw�sho wa mwez�. Humsa�da mfugaj� kujua kama kuku wanakula haraka au polepole.

Tarehe A�na ya kuku

Idad� ya kuku Chakula Maelezo

A�na k�lo sh�l�ng�

Jumla

171

(ii) Kumbukumbu ya Utagaji Iand�kwe k�la s�ku. Humsa�d�a mfugaj� kujua ufan�s� wa

kuku wake kwa kul�ngan�sha chakula k�nachol�wa na maya� yanayotagwa au k�lo za nyama ya kuku �l� kupata uw�ano au as�l�m�a. Kuku wanaotaga v�zur� huf�k�sha as�l�m�a 85 ya kuku al�onao.

Tarehe Idad� ya kuku Ukusanyaj� wa maya� Maelezo

Jumla (iii) Kumbukumbu ya chanjo

Tarehe A�na ya

kuku

Idad� ya

kuku (s�ku)

Umr� wa

kuku (s�ku)

J�na la mtu al�yechanja

A�na ya

chanjo

Nj�a �l�yo-

tum�ka

Wate- ngene-

zaj�

Maelezo

Jumla

(iv) Kumbukumb ya matibabu

Tarehe A�na ya

kuku

Umr� A�na ya

dawa

Wate- ngene-

zaj�

J�na la mtu

al�yetoa

K�as� k�l�-

chotu-m�ka

Thaman� ya dawa

Matokeo Maelezo

Jumla

172

(v) Kumbukumbu ya Uanguaji / Utotoaji

Na.ya banda

Tarehe Idad� ya

maya�

Idad� ya v�faranga

wal�oangul�wa

As�l�m�a ya v�faranga

V�faranga v�navyouz�ka

Maelezo

Jumla

(vi) Kumbukumbu ya vifo vya kuku na Waliopunguzwa

Tarehe Na. ya banda/nyumba

Idad� ya kuku

A�na ya kuku

V�fo Wal�opunguzwa Sababu ya v�fo

Idad� sal�o

maelezo

Jumla

Kad� h�� �jazwe k�la s�ku. Humsa�d�a mfugaj� pamoja na

mambo meng�ne, kujua k�as� cha chakula cha kuwapat�a kuku wal�osal�a na �dad� ya maya� yatakayotagwa.

(vii) Kumbukumbu ya Vifaranga

Tarehe wal�pof�ka Na. ya chumbaIdad� yao Tarehe ya kuzal�waTarehe ya s�ku A�na

Tarehe Chakula k�l�chotum�ka Idad� yawal�okufa Meng�neyo

173

Kumbukumbu nyingine ni:• Up�maj� wa damu na v�nyes� vya kuku �l� kujua usalama

wao dh�d� ya maambuk�z� ya magonjwa na v�melea.• Up�maj� wa hal�joto kat�ka nyumba ya v�faranga na kuku. Kwa kutum�a kumbukumbu h�zo za k�la s�ku,

unaweza kukokotoa kumbukumbu za w�k� moja, mwez� mz�ma, robo mwaka, nusu mwaka na mwaka mz�ma.

(viii) Utunzaji wa Leja Leja n� kumbukumbu ny�ng�ne muh�mu ambayo laz�ma

uwe nayo na u�jaze k�la s�ku. Tum�a kurasa mb�l�. Ukurasa wa kushoto n� wa Matumizi. K�la s�ku and�ka a�na ya matum�z� na k�as� cha fedha k�l�chotum�ka. Upande wa kul�a and�ka Mapato au Mauzo. Mw�shon� mwa mwez� fanya ul�ngan�sho. Toa matum�z� kat�ka mapato. Sal�o l�pelekwe mwez� ujao na l�taonekana kama salio - anzia.

Angalia mfano ufuatao wa Leja

MATUMIZI MAUZO NA MAPATO

Tarehe A�na ya Matum�z�

K�as� Tarehe Chanzo cha Mauzo na Mapato

K�as�sh. sent� sh. sent�

JUMLAIl� uweze kujaza leja kwa usah�l� n� laz�ma:- Ununue v�tabu vya:

• Stakabadh� kwa aj�l� ya kuand�ka mapato na vyanzo vyake.• Hat� ya Mada� kwa aj�l� ya kuwapelekea Mada� watu unaowada�.• Hat� ya Makab�dh�ano kwa aj�l� ya kuwakab�dh� wal�oag�za kwa

mkopo mazao ya kuku unayouza.

174

- Ufungue akaunt� benk� �l� uweze ku�ng�za humo mauzo ya k�la s�ku pamoja na fedha ul�zol�pwa na watu ul�okuwa unawada�. U�ng�zaj� na utoaj� fedha benk� utakusa�d�a kuwaonyesha wal�okupa mkopo j�ns� unavyotum�a fedha zao na matokeo ya matum�z� ya mkopo huu.

(c) Faida za kumbukumbu Fa�da kuu za kumbukumbu n�:

(�) Kumwezesha mfugaj� kujua kama baada ya k�p�nd� fulan� (kwa mfano mwez�, robo mwaka, nusu mwaka, mwaka mz�ma n.k.) al�pata fa�da au hasara. Ak�shajua h�vyo, huchukua hatua za kuboresha ufugaj� au kufanya maamuz� meng�ne. Maamuz� hayo n� pamoja na kuacha ufugaj� wa a�na h�yo ya kuku. Kama al�kuwa anafuga kuku wa kutaga anaweza kuwauza wote na kuanza kufuga kuku wa nyama au akaacha kab�sa ufugaj� wa kuku wa a�na yoyote.

(��) Kumbukumbu h�zo z�tatum�ka kutengeneza hesabu za b�ashara kama v�le M�zan�a, Akaunt� ya Fa�da na Hasara n.k. Hesabu h�zo huweza kutum�wa na benk� au asas� ny�ng�ne z�natoa m�kopo kukupa au kukuny�ma mkopo mpya.

Mbal� na fa�da h�zo mb�l� kubwa, fa�da ny�ng�ne ndogondogo, lak�n� muh�mu, n� h�z� z�fuatazo: • Kukuwezesha kufanya maamuz� mbal�mbal� kama v�le k�as�

cha chakula cha kununua na kuwapa kuku.• Kujua n� k�as� gan� cha chakula kuku ul�onao wanakula k�la

s�ku.• Kujua ufan�s� wa kuku ul�onao kat�ka kubad�l� chakula

wanachokula kuwa nyama au maya�.• Kujua k�as� gan� cha maya� au nyama wanazal�sha.• Kujua �dad� ya maya� yanayotagwa k�la s�ku, ubora wake

n.k.• Kujua �dad� ya v�fo na chanzo chake.• Kujua a�na za magonjwa yanayoshambul�a kund� lake na

kwa n�n�?• Kujua gharama mbal�mbal� kwenye kund� lako, kama v�le

za chanjo, za kut�b�sha n.k.

175

Fomu za kumbukumbu z�l�zoelezwa kat�ka (�) had� (v�) z�band�kwe kwenye chumba cha kuku, hasa mlangon� kwa ndan�. K�la fomu (karatas�) �tosheleze s�ku za mwez� mz�ma. Z�jazwe k�la s�ku na kuondolewa asubuh� ya tarehe 1 ya mwez� ujao na kuband�kwa fomu mpya.

MASWALI YA KUJIPIMA UELEWA

1. Mtaj� n� ............................................................................2. Taja mambo maw�l� ambayo mfugaj� anatak�wa kuyafanya kabla ya

kuanza ufugaj� wa kuku wa k�b�ashara.3. Kumbukumbu n� n�n�?4. Taja a�na nne za kumbukumbu.5. Leja �na sehemu ngap�? Z�taje?6. Taja fa�da kuu mb�l� za kumbukumbu.

VITABU VYA MAREJEO1. Cheah Kok Kheong, Modern Agriculture for Tropical Schools, (Oxford

Un�vers�ty Press, London, 1973). 2. D.Joy & E.J. W�bberley, A Tropical Agriculture Handbook (Cassell Ltd,

1979).3. D.N.Ngug� & others, East African Agriculture: A Textbook for Secondary

Schools (Macm�llan Educat�on Ltd, London, 1978)4. W�ll�amson and W.J.A. Payne, An Introduction to Animal Husbandry

(Engl�sh Language Book Soc�ety and Longmans, Green & Co. Ltd). 5. Helen Cockburn (1968), Poultry Keeping in East African, East African

L�terature Bureau, Dar es Salaam, Na�rob� na Kampala. 6. Ngeze, P.B. Mwongozo wa Uhasibu wa Shamba (Tanzan�a Educat�onal

Publ�shers Ltd, 2007). 7. Ngeze, P.B. Misingi ya Kilimo Bora (Tanzan�a Publ�sh�ng House, 1976).8. N�ls Erneholm, Agriculture for Schools (He�neman Educat�onal Books,

Na�rob�, 1976) 9. Oluyem� Ak�nsanm�, Certificate Agricultural Science, (Longman, Group

Ltd, London, 1976). 10. P. Otmar Morger na P.B.Ngeze, Mkulima Stadi (Bened�ct�ne Publ�cat�ons

Ndanda/Peram�ho, 1985.)11. W�zara ya El�mu, Tanzan�a, Mkulima wa Kisasa, 1975.12. V.O. Ak�nyosoye, Senior Tropical Agriculture for West Africa (Macm�llan

Educat�on Ltd, London, 1976).13. Ukul�ma wa K�sasa, 2006, Ufugaji Bora wa Kuku.

176

TAFSIRI KWA KINGEREZA YA MAGONJWA NA VYAKULA VYA KUKU

Kiswahili Kingereza1. Mdondo Newcastle d�sease2. Gumboro Gumboro d�sease3. Koks�d�a Cocc�d�os�s d�sease4. Kupooza Fowl paralys�s 5. Homa ya matumbo Fowl typho�d 6. Ndu� ya kuku Fowl pox7. Mahepe Mareks d�sease8. K�p�ndup�ndu Fowl cholera9. Homa ya kuku Infect�ons coryza 10. Kulemaa kwa v�dole na m�guu Gout d�sease11. Ugonjwa sugu wa Upumuaj� Mycoplasmos�s chron�c

resp�rat�on 12. Ugonjwa wa Kuhara wa V�faranga v�dogo Coll�bac�llos�s 13. Mafua ya Ndege Av�an �nfuluenza (Fowl

plaque/B�rd flu)14. Ugonjwa wa Makamba unaoambuk�za Infect�ous Bronch�t�s 15. Saratan� ya kuku Av�an Leukos�s 16. Kukohoa kohoz� la damu Infect�ous laryngotrache�t�s 17. Ugonjwa wa v�faranga v�dogo Av�am encephalomyel�t�s 18. Kuv�mba mguu Bumble/ Swollen foot19. Magonjwa yaletwayo na m�nyoo D�seases caused by worms.20. Magonjwa yaletwayo na v�melea D�seases caused by sk�n vya ngoz� paras�tes21. Magonjwa yaletwayo na ukosefu wa D�seases caused by m�neral

v�rutub�sho kat�ka vyakula and v�tam�n def�c�ency22. Magonjwa yaletwayo na sumu D�seases caused by po�son 23. Chakula cha v�faranga Ch�ck mash24. Chakula cha kukuza kuku Growers’ mash25. Chakula cha kutag�sha Layers’ mash26. Chakula cha kuzal�sha Breeders’ mash27. Chakula cha kuku wa nyama Bro�lers’ mash.

THANK YOU FOR READING THE PREVIEW To read the entire book

please login and rent the book at www.lantern.co.tz