Huzuni katika nyimbo za taarab za waimbaji Bi Fatma Issa na ...
-
Upload
khangminh22 -
Category
Documents
-
view
0 -
download
0
Transcript of Huzuni katika nyimbo za taarab za waimbaji Bi Fatma Issa na ...
The University of Dodoma
University of Dodoma Institutional Repository http://repository.udom.ac.tz
Humanities Master Dissertations
2016
Huzuni katika nyimbo za taarab za
waimbaji Bi Fatma Issa na Shakila Said
Rashid, Zeyana Omar
Chuo Kikuu cha Dodoma
Rashid, Z. O. (2016). Huzuni katika nyimbo za taarab za waimbaji Bi Fatma Issa na Shakila
Said (Tasnifu shahada ya uzamili). Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma.
http://hdl.handle.net/20.500.12661/850
Downloaded from UDOM Institutional Repository at The University of Dodoma, an open access institutional repository.
HUZUNI KATIKA NYIMBO ZA TAARAB ZA WAIMBAJI BI
FATMA ISSA NA SHAKILA SAID
Na
Zeyana Omar Rashid
Tasnifu Iliyowasilishwa kwa Ajili ya Kukamilisha Mahitaji ya Shahada ya Uzamili
ya Sayansi ya Jamii katika Fasihi ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Dodoma
Chuo Kikuu cha Dodoma
Oktoba, 2016
i
ITHIBATI
Aliyetia saini hapa chini anathibitisha kuwa ameisoma tasnifu hii iitwaayo “Huzuni
katika nyimbo za taarab za waimbaji Bi Fatma Issa na Shakila Said”, na
kupendekeza ikubaliwe na Chuo Kikuu cha Dodoma kwa ajili ya kukamilisha
masharti ya Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha
Dodoma.
…………………………………
Dkt. Muhammed Seif Khatib
(Msimamizi)
Tarehe…………………………
ii
IKIRARI
NA
HAKI MILIKI
Mimi Zeyana Omar ninathibitisha kuwa tasnifu hii ni kazi yangu halisi na haijawahi
kuwasilishwa na haitawasilishwa katika chuo kikuu kingine kwa ajili ya shahada
yoyote.
Saini……………………
Hairuhusiwi kunakili, kutafsiri, kupiga chapa au kuiga sehemu yoyote ya tasnifu hii
bila ya ruhusa ya mwandishi au Chuo Kikuu cha Dodoma
iii
SHUKURANI
Kwanza kabisa, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa
kunijaalia uzima na afya njema katika kipindi chote cha kukamilisha utafiti huu. Pili,
ninamshukuru msimamizi wa utafiti huu, Dkt Muhammed Seif Khatib ambaye
alikuwa mwongozaji wa kazi hii na alifanya juhudi kubwa kuhakikisha kuwa utafiti
huu unamalizika katika hali ya ubora zaidi. Mwenyezi Mungu amlipe ujira mwema,
Amina.
Aidha, nawashukuru walimu wangu wote walionifundisha kozi za Fasihi ya
Kiswahili ambao kwa kiasi kikubwa waliweza kupanua uelewa wangu ulionisaidia
kukamilisha utafiti. Tatu, nawashukuru wazazi wangu Bi Fatma Almasi na Bwana
Omar Rashid ambao mbali na kunileya na kunipatia elimu, walifanya kazi kubwa ya
kuhakikisha kuwa namaliza masomo yangu kwa mafanikio mkubwa. Mwenyezi
Mungu awape umri mrefu na wenye afya njema katika maisha yao. Vilevile
ninawashukuru ndugu zangu Rukaiyya Omar, Tauhida Omar na Ali Omar kwa
kuonesha upendo wao wa dhati kwangu na kumlea mtoto wangu katika misingi bora
wakati nikiwa masomoni. Nitakuwa mwizi wa fadhila iwapo sikumshukuru mume
wangu mpenzi Bwana Mbarouk Nassor kwa kunivumilia pale nilipomwacha na
upweke lakini bado kaendelea kunidhihirishia upendo wake kwangu katika kipindi
hicho kigumu.
Nne, ninawashukuru walimu na wanafunzi wenzangu, Mabwana Kassim Simai,
Makame Pandu, Khamis Saleh, pamoja na Mabibi Zuleikha Abdallah, Bushura
Khamis na Salama Omar kwa mashirikiano na kubadilishana mawazo juu ya tafiti
zetu.
iv
TABARUKU
Ninaitabaruku tasnifu hii kwa mume wangu mpenzi, Bw Mbarouk N Mbarouk na
watoto wangu Ak-thar Mbarouk na Afnaan Mbarouk kwa kunijali katika kipindi
chote cha masomo yangu. Ipokeeni kazi hii kama zawadi katika maisha yenu.
Nawapenda nyote.
v
IKISIRI
Utafiti huu uliongozwa na malengo matatu ambayo yaliweza kusaidia na kubainisha
huzuni katika nyimbo za taarab za waimbaji Fatma na Shakila. Tafiti, makala, vitabu
na maoni ya wadau mbalimbali kuhusiana na suala zima la taarab asilia yalisaidia
kuchunguza dhamira pamoja na sababu mbalimbali zilizowasukuma wasanii wateule
kutunga na kuimba nyimbo za huzuni.
Utafiti huu ulifanyika uwandani na maktabani na kutumia mbinu ya usaili, udodosaji
na ushuhudiaji katika kukusanya data. Maeneo yaliyotumika katika ukusanyaji wa
data za nyimbo za taarab ni studio za Zenji FM na Coconut FM katika mkoa wa
Mjini Magharibi Unguja. Data zilichambuliwa kwa kuongozwa na nadharia ya
uhalisia ambayo imeongozwa na misingi yake mikuu miwili ambayo ni ushabihi
ukweli na msingi wa kimhakati. Nadharia hii ya uhalisia iliyotumika ilisaidia
kufanunua sababu zinazowasukuma wasanii kutunga nyimbo hizo, athari na hata
dhamira za nyimbo hizo.
Matokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa huzuni humfika kila mtu katika jamii na ni
jambo lisiloweza kuepukika kwa mwanadamu yoyote yule. Nyimbo za huzuni
hutungwa kutokana na matukio mbalimbali ambayo yanawafika watu katika jamii.
Matukio hayo yaweza kuwa ya kijamii, kisiasa, na hata kiuchumi. Lakini katika
utafiti huu imedhihirika kuwa mara nyingi huzuni hutokea kutokana sababu za
kijamii kama vile kusalitiwa, kufiwa, ubinafsi, kukosa bahati na mengineyo. Ingawa
tafsiri ya awali na mawazo ya watu wengi ilionesha kuwa taarab ni muziki wa furaha
na ramsa, utafiti huu umebainisha kuwa sio kila nyimbo ya taarab ni ya furaha.
vi
YALIYOMO
ITHIBATI ...................................................................................................................... i
IKIRARI NA HAKI MILIKI ....................................................................................... ii
SHUKURANI ............................................................................................................. iii
TABARUKU ............................................................................................................... iv
IKISIRI ......................................................................................................................... v
YALIYOMO ............................................................................................................... vi
ORODHA YA VIELELEZO NA PICHA .................................................................. ix
SURA YA KWANZA ................................................................................................. 1
1.1 Utangulizi ............................................................................................................... 1
1.2 Usuli wa Tatizo ...................................................................................................... 1
1.3 Tamko la Utafiti ..................................................................................................... 3
1.4 Wasifu wa Fatma Issa Juma ................................................................................... 3
1.5 Malengo ya Utafiti ............................................................................................... 15
1.5.1 Lengo Kuu ......................................................................................................... 15
1.5.2 Malengo Mahsusi .............................................................................................. 15
1.6 Maswali ya Utafiti ................................................................................................ 15
1.7 Manufaa ya Utafiti ............................................................................................... 15
1.8 Nadharia ya Utafiti ............................................................................................... 15
1.9 Hitimisho .............................................................................................................. 16
SURA YA PILI: MAPITIO YA MAANDIKO ...................................................... 17
2.1 Utangulizi ............................................................................................................. 17
2.2 Chimbuko la Taarab Zanzibar .............................................................................. 17
2.3 Maandiko Yahusuyo Taarab ................................................................................ 19
2.4 Pengo la utafiti ..................................................................................................... 24
2.5 Hitimisho .............................................................................................................. 24
SURA YA TATU: USANIFU NA MBINU ZA KUKUSANYIA DATA ............. 25
3.1 Utangulizi ............................................................................................................. 25
3.2 Mpango wa utafiti ................................................................................................ 25
3.3 Eneo la utafiti ....................................................................................................... 25
vii
3.4 Walengwa wa Utafiti ............................................................................................ 25
3.4.1 Jamii ya Watafitiwa ........................................................................................... 26
3.4.2 Usampulishaji na Sampuli Iliyotumika ............................................................. 26
3.5 Ukusanyaji wa Data ............................................................................................. 27
3.5.1 Njia za ukusanyaji wa data ................................................................................ 27
3.5.2 Usaili ................................................................................................................. 27
3.5.3 Dodoso .............................................................................................................. 27
3.5.4 Ushuhudiaji ....................................................................................................... 27
3.6 Zana za kukusanyia data ...................................................................................... 28
3.6.1 Kamera .............................................................................................................. 28
3.6.2 Simu .................................................................................................................. 28
3.6.3 Daftari na kalamu .............................................................................................. 28
3.6.4 Ngamizi ............................................................................................................. 28
3.7 Mchakato wa Ukusanyaji Data na Uthabiti wake ................................................ 28
3.8 Mipaka ya Utafiti ................................................................................................. 29
3.9 Vikwazo vya Utafiti na Utatuzi wake .................................................................. 29
SURA YA NNE: UWASILISHAJI, UCHAMBUZI NA MATOKEO YA
MJADALA WA UTAFITI ...................................................................................... 30
4.1 Utangulizi ............................................................................................................. 30
4.2 Dhana ya Huzuni .................................................................................................. 30
4.3 Nyimbo za huzuni za waimbaji wateule .............................................................. 31
4.4 Sababu za Kutunga Nyimbo Za Huzuni ............................................................... 37
4.4.1 Usaliti ................................................................................................................ 37
4.4.1.1 Usaliti wa mume na mke ................................................................................ 37
4.4.2 Msiba ................................................................................................................. 39
4.4.3 Maliwazo na Ufariji .......................................................................................... 40
4.4.4 Choyo na Husuda .............................................................................................. 41
4.4.5 Ufitini na uchongezi .......................................................................................... 43
4.4.6 Huzuni na hali halisi ya maisha ......................................................................... 44
4.4.7 Huzuni na majuto .............................................................................................. 46
4.4.8 Huzuni na bahati ................................................................................................ 48
4.5 Dhamira ya Huzuni katika Nyimbo za taarab na tija zake ................................... 50
viii
4.5.1 Kupanua dhana ya Taarab ................................................................................. 50
4.5.2 Kuelimisha ........................................................................................................ 50
4.5.3 Kuliwaza ............................................................................................................ 51
4.5.4 Kuzindua ........................................................................................................... 52
4.5.5 Kurekebika tabia ............................................................................................... 53
4.5.6 Ujenzi wa hisia na huruma ................................................................................ 53
4.5.7 Kuonesha ujasiri ................................................................................................ 55
4.6 Athari zinazopatika katika Nyimbo za Huzuni .................................................... 56
4.6.1 Athari Chanya ................................................................................................... 56
4.6.1.1 Kuifanya jamii kujua matatizo yake ............................................................... 56
4.6.1.2 Kufariji na kuliwaza ....................................................................................... 56
4.6.1.3 Kugusa nafsi ya msikilizaji ............................................................................ 56
4.6.2 Athari hasi za Nyimbo za Huzuni ..................................................................... 57
4.6.3 Tofauti ya Fatma na Shakila .............................................................................. 57
4.6.4 Mfanano wa Fatma na Shakila .......................................................................... 58
4.7 Hitimisho .............................................................................................................. 59
SURA YA TANO: MUHTASARI, HITIMISHO NA MAPENDEKEZO .......... 60
5.1 Utangulizi ............................................................................................................. 60
5.2 Muhtasari wa Tasnifu ........................................................................................... 60
5.3 Utoshelevu wa Nadharia Iliyotumika ................................................................... 61
5.4 Mambo Mapya Yanayoibuliwa na Tasnifu Hii .................................................... 62
5.5 Mapendekezo wa Tafiti Zijazo ............................................................................. 62
5.6 Maoni ya Mtafiti juu ya Utafiti Huu .................................................................... 63
MAREJELEO ........................................................................................................... 64
VIAMBATISHO ....................................................................................................... 66
A: Mwongozo wa usaili kwa wataalamu wa Fasihi. .................................................. 66
B: Dodoso kwa wanfunzi waliotafiti taarab asilia...................................................... 67
C: Nyimbo za waimbaji wateule Zilizotumika katika kazi hii ................................... 69
D: Picha mbali mbali zinazohusiana na utafiti ........................................................... 76
ix
ORODHA YA VIELELEZO NA PICHA
Shakila akifanya biashara nyumbani kwake Charambe (Utafiti, 2016)
Mtafiti akimuhaji bi Shakila huko yumbani kwake Charambe Dar es Salaam.
(Utafiti, 2016)
Mtafiti akimuhoji bi Fatma huko nyumbani kwake Kwa Alamsha, Zanzibar.
(Utafiti, 2016)
1
SURA YA KWANZA
1.1 Utangulizi
Fasihi simulizi ina vipera vyake muhimu katika jamii. Taarab ikiwa kipera cha fasihi
simulizi imejidhihisha kuwa na jukumu la kuelimisha, kuburudisha na kuhuzunisha
kupitia mashairi na muziki wake. Sura hii imejadili kuhusu usuli wa tatizo, tamko la
utafiti, wasifu wa waimbaji teule, malengo ya utafiti, maswali ya utafiti, manufaa ya
utafiti, nadharia ya utafiti na hitimisho.
1.2 Usuli wa Tatizo
Neno taarab limefasiriwa na wataalamu mbalimbali na kuweza kutoa maana yenye
kukaribiana. Kwa mujibu wa Rais mstaafu wa Tanzania Mzee Mwinyi, akinukuu
kamusi ya „Al- Maurid‟ anasema, “Taarab ni furaha iliyokithiri, raha iliyoje, starehe,
staladhi, tafrija, muziki, kuimba au kughani” (Khatib, 2014:1)
Pia, kwa mujibu wa kamusi ya Kiarabu na Kiingereza Al- Faraidal- Durriyya neno la
taarab lililokaririwa na Khatib (2014: 1) linanyambulika na kuwa „tariba, Yatrib, au
Taraba, maneno yote hayo yanamaanisha furaha. Kamusi jengine la A Learner‟s
Arabic- English Dictionary inaeleza kuwa neno, “Taarab lina maana ya kutiwa
hamasa, kuwa na furaha, kusherehekea karamu, kuimba, au kupiga muziki”. (Khatib,
2014: 1)
Nae Andanega (2002) anasema kuwa; “neno taarab linahusiana na aina ya ngoma
inayoitwa tarabu na pia na neno la Kiurdu- Kihindi tarabu, maana yake ni furaha”
(Andanega, 2002: 109).
Kutokana na tafsiri ya maana zote hizo, taarab ina maana ni ile hali ya upigaji muziki
kwa „furaha‟. Taarab hupigwa katika shughuli mbalimbali za kijamii ambapo watu
2
huburudika kwa kupitia mashairi yake. Hata hivyo, tatizo lililojitokeza na
kushangaza ni kuwa tafsiri zote hizo zinaelekeza taarab kimaana katika furaha na
ramsa tu na kusahau kuwa taarab huweza kubeba dhamira za simanzi au hata tanzia.
Zipo nyimbo nyingi ambazo mashairi yake hubeba hali ya jitimai, maafa au majonzi
ambayo yanawakumba wanadamu katika maisha yao ya kila siku. Taarab haimo
katika ombwe, kwa hivyo mashairi yake lazima hugusa maisha ya watu katika jamii.
Kihistoria, wakati taarab inaatikwa Zanzibar katika kasri ya Sultan, nyimbo nyingi
zilizoimbwa wakati huo zilikuwa ni za kumsifu na kumtukuza Sultani aliyepo
madarakani. Nyimbo za kuombea dua juu ya mapenzi ya Sultani na Malkia wake;
kumsifu muumba na maumbile ya ulimwengu na nyimbo nyengine za mikasa za
kumfanya Sultani atabasamu na acheke nazo hazikukosa (Khatib: 2014- 4). Kadri
siku zilivyozidi kuyoyoma na kubadilika kwa mifumo ya kiutawala Zanzibar,
nyimbo za taarab nazo zikabadilika na zikawa nazo ni zenye kubeba hisia tofauti
kama vile kupashana, kupalilia mapenzi baina ya watu wawili, kejeli au za simanzi.
Ni dhahiri kuwa katika maendeleo ya muziki wa taarab hivi sasa, nyimbo za huzuni
nazo zimeibuka kila pembe mithili ya uyoga. Hali hii ya kwenda sambamba kwa
nyimbo za furaha na huzuni zimekuwa ni sehemu ya maisha ya mwanadamu.
Ongezeko hili la nyimbo za huzuni katika tasnia ya muziki wa taarab haliendani
kabisa na dhamira na lengo halisi la asilia la uanzishwaji wa muziki wa taarab.
Wakati ule wa zamani wa watawala wa kisultani ndani ya kasir, taarab ilikusudiwa
kuwapa furaha na starehe tabaka tawala ikiwa ni sehemu ya burudani wakati wa
mapumziko yao. Haikutarajiwa Sultan awe na huzuni, kwani yeye hupewa kila kitu
atakacho. Taarab baada ya kutoka nje ya majengo ya Sultani na kuwa muziki wa
makabwela, tanzia na huzuni, haziachi kuwepo katika maisha yao halisi.
3
1.3 Tamko la Utafiti
Muziki wa taarab unapendwa sana na kwa sasa umeweza kupaa sana katika anga za
mwambao wa Afrika Mashariki na baadhi ya nchi jirani. Taarab hii imezigusa nyoyo
za watu kwa mashairi yake yanavyoakisi hali halisi ya maisha na utamu wa muziki
wake. Hivyo, sasa zipo nyimbo nyingi ambazo zinazungumzia maudhui na dhamira
ambazo zimekuwa za kudumu katika tasnia ya ushairi wa taarab kwa miaka nenda
miaka rudi. Hata hivyo, nyimbo zenye kuakisi mapenzi ya kusifu zipo nyingi na
zimeziteka nyoyo za watu wengi. Maisha ya binadamu ya uhalisia hayaogelei raha na
furaha tu, yapo mambo kadha yanayomsibu mtu na humpa huzuni na jitimai. Hivyo
zipo nyimbo nyingi zinazobeba dhamira za huzuni ambapo wasanii wa taarab
hutumia usanii wao kwa lengo la kuakisi hisia zao juu ya maafa ambayo yanatokezea
katika maisha yao au jamii inayowazunguka. Licha ya kuwepo kwa tafiti nyingi
ambazo hueleza mambo mbalimbali yatokeayo katika jamii, lakini hakuna utafiti
uliofanywa kuchunguza dhamira na sababu zinazowasukuma wasanii katika miaka
ya karibu kutunga na kuimba nyimbo za huzuni katika taarab. Kwasababu hiyo,
mtafiti wa kazi hii imechunguza nyimbo za huzuni zilizoimbwa na wasanii wateule
Fatma Issa na Shakila Said kwa azma ya kuzibaini sababu za kuibuka nyimbo za
huzuni katika jamii kinyume na lengo la asili la kuasisi taarab.
1.4 Wasifu wa Fatma Issa Juma
Fatma Issa Juma ni mwimbaji, mtia sauti na mshairi wa taarab asilia. Amezaliwa
Kianga Wilaya ya Magharibi „A‟mwezi wa Oktoba mwaka 1957. Fatma ni mtoto wa
pili kati ya watoto wanne wa mzee Issa Juma. Mtoto wa kwanza ni mvulana ambaye
anaitwa Juma Isa Juma aliyezaliwa mwaka 1954, akifuatiwa na ndugu zake
Mwajuma 1966, Pili Issa Juma na kitinda mimba Mwatima Issa Juma. Akiwa mtoto
wa miaka mitatu, Fatma pamoja na wazazi wake walihama Kianga na kuhamia mjini
4
katika mtaa wa Rahaleo. Mama yake Fatma anaitwa Ajuza na yeye pia alikuwa ni
mwimbaji wa taarab katika mwaka 1963 akiwa na kikundi kilichojulikana kwa jina la
African Social Light. Katika shughuli zake za uimbaji, Ajuza alikuwa akimchukuwa
mtoto wake Fatma tarabuni. Huko ndiko alikoanza Fatma kuathiriwa na uimbaji
akiwa na umri mdogo sana.
Kama ilivyo kawaida ya watoto wa Kiislamu, Fatma alipelekwa madrasa katika
mwaka 1962. Alipokuwa katika madrasa, alishriki kuimba kasida akiwa na umri
mdogo sana. Aliporudi chuoni (madrasa) Fatma alikuwa akizikariri na kuziimba
nyimbo ambazo alizisikia katika kikundi cha mama yake. Hapo ndipo mama yake
alipokigundua kipaji cha mtoto wake.Kipaji cha Fatma kiliimarishwa zaidi pale
Fatma alipokwenda katika shughuli ya mama yake mdogo.Huko kulikuwepo Taarab
ya Kidumbaki. Midundo ya Kidumbaki ilimwingia Fatma ndani ya moyo na bila
kujijua. Alianza kutoa vipande vya nyimbo ambazo alikuwa akizisikia katika
kikundi cha mama yake. Mbali na kukariri nyimbo za mama yake lakini pia aliweza
kutunga beti za nyimbo katika shughuli hiyo. Anakumbuka mila na desturi za
Waswahili pale inapotokezea yeye kuimba ubeti mzuri katika taarab baadhi ya wazee
humrushia mchele kama ni ishara ya kumpongeza au kutema mate chini kuonesha
ishara ya kumwondelea husda.
Fatma alisoma katika skuli ya msingi Kidutani (Agakhan). Baadaye alihamishwa
katika skuli ya Kidutani kubwa ambayo sasa inajulikana kama Taasisi ya Kiswahili
na Lugha za Kigeni na kumalizia katika skuli ya Haileselasie. Skuli zote hizo zipo
katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
Fatma aliolewa mwaka 1971 na bwana Saaduni Makanjira, ni mwenyeji wa Pongwe
na Fuoni. Fatma aliolewa akiwa bado mwanafunzi wa darasa la kumi. Katika mwaka
5
1972 alijifungua mtoto wake wa mwanzo ambaye anaitwa Mrisho. Baadaye
aliachana na Saaduni na kukaa ujane. Katika kipindi cha ujane alibahatika kuzaa
watoto kumi, lakini waliobahatika kuwa hai ni watoto watatu tu ambao ni Hamdani
Abdallah aliyezaliwa mwaka 1976, Rahma mwaka 1980 na Afuwa mwaka 1982.
Kati ya watoto hawa ni Hamdani pekee ndiye aliyerithi kipaji cha mama yake lakini
yeye amejikita katika muziki wa rumba na anaishi huko Muscat, Oman.
Fatma kutokana na kupenda sana muziki wa taarab na kubanwa na harakati za ndoa,
aliacha kusoma na kujishughulisha na muziki wa taarab. Mnamo mwaka 1973 mama
yake Ajuza alimpeleka katika kikundi cha Culture Musical Club cha Zanzibar.
Mwaka 1976 aliacha rasmi shughuli za uimbaji na kushughulikia kulea watoto wake.
Katika mwaka 1977 Fatma alishindwa kujizuia kutoshiriki katika taarab, alirudi tena
katika uwanja wa taarab. Mwaka 1977 uliokuwa ndiyo mwaka iliyozaliwa
CCM.Yeye alipangiwa kuimba nyimbo ya chama kipya hiki. Hiyo ilikuwa ni nyimbo
yake ya mwanzo kumtoa ukumbini. Baadaye kikundi cha Culture kilisafiri nje ya
Zanzibar kwa muda wa miezi sita hivi yeye hakushirikishwa. Fatma ikambidi
kwenda kikundi cha taarab cha Kidongochekundu katika mwaka 1978. Katika
kikundi cha taarab Kidongochekundu huko alitunga nyimbo yeye mwenyewe na
kuimba nyimbo nyingine ambazo aliyojizolea umaarufu mkubwa. Nyimbo
iliyomkosha uso ilijulikana kwa jina la „Wali mtamu na Muhogo Vilevile‟ .
Katika mwaka 1985, Fatma alirudi tena Culture.Baada ya kurudi tena Culture
alipewa nyimbo kuimba jambo lilomfanya wasanii wenzake kumuonea gere. Baadhi
ya nyimbo alizopewa kuimba katika Cultureni kama; „Mbuzi‟, „Kiwe‟, „Maafa‟ na
kadhalika. Hasada na choyo cha wenzake kilikuwa kikubwa, kwasababu hiyo,
ilimfanya atunge wimbo mwenyewe kujitetea. Alitunga wimbo wake wa mwanzo
6
ndani ya Culture inaitwa „Bugudha sitaki‟. Baadaye akatunga „Haya Maumbile
Yangu‟ wimbo ambayo ilipata washabiki wengi sana hadi leo. Alikuwa na kawaida
Fatma ya kutunga wimbo kila baada ya mwaka. Mwaka uliofata akatunga wimbo
nyengine iitwayo „Kunionya Sikatai‟.Alipotunga wimbo huu munkari wa mahasimu
zake ukapungua. Baadaye akatunga nyimbo nyengine ziitwazo “Hivyo ndivyo ilivyo
Dunia”na“Fitina”. Kupitia nyimbo hizi, Fatma alizidi kung‟ara na kufahamika
katika kila pembe ya mji wa Zanzibar na Dar es Salaam.
Mnamo mwaka 1990, Fatma akajiunga na kikundi cha sanaa cha Jeshini akiwa
mkufunzi wa taarab, akiwafundisha waimbaji chipukizi kuimba. Mbali ya kuwa
mwalimu katika kikundi hicho pia aliweza kutunga nyimbo tatu ambazo ni Hasama,
Ewe Nuru Yangu na nyingine. Fatma hakudumu katika kikundi hiki kutokana na
mgogoro uliokuwepo wa wasanii kati ya Jeshi na wasanii raia. Kutokana na mgogoro
huo wasanii raia wote waliondolewa katika kikundi hicho.
Baadaye Fatma aliitwa na Maryam Hamdan na kumuomba ajiunge na kikundi cha
mumewe cha Twinkling Star. Katika kikundi hiki aliimba na kurikodi nyimbo ya
„Hachochoeki‟ na „Nimehifadhika‟. Fatma hakudumu katika kikundi hiki kwasababu
uongozi waCulture ulimtaka tena arudi katika kikundi na ndipo hapo aliporudi na
kuimba nyimbo nyingi ambazo nyingine hakutunga yeye.
Mnamo mwaka 1994, msanii John Komba alimtaka kujiunga na kikundi cha
TanzaniaOne Theatre (T.O.T) kwa lengo la kumsaidia katika shughuli za uimbaji na
utungaji. Baada ya muda mfupi zilianza tafrani na mashaka katika kikundi hicho.
Baada ya miezi mitano Fatma ikatokea bahati ya kwenda Ujerumani na wasanii
wenzake wa kikundi cha Culture. Akiwa safarini, Fatma alipokea barua ya kumtaka
awe mkufunzi wa kikundi kipya kilichoanzishwa na Wizara ya Habari Utamaduni na
7
Michezo ya Serikali ya Zanzibar. Alikubali na kukitumikia kikundi hicho cha Sanaa.
Kama anavyosema yeye mwenyewe Fatma, “sina bahati nimejawa na mikosi”. Baada
ya muda mfupi ndani ya kikundi hiki, zilianza fitina na majungu kupitia waimbaji
wenzake. Baada ya kutokea kwa sitofahamu hizo ndipo alipotunga nyimbo zifuatazo;
Tenda na wewe Usifiwe, Mtachoka Vyenu Visa, na Huniwezi. Nyimbo nyengine tatu
ni Kheri Adui Shetani Kama Adui Kiumbe, Nenda Utakako, Hukusingiziwa. Baadaye
alihamia katika kikundi cha JKU akiwa mkufunzi na huko nako aliimba wimbo wa
„Kwa Mola Hakuna Kubwa‟. Kama ilivyo imekuwa ada ya kuwa, akiwepo katika
kikundi chochote kile lazima fitina na majungu yatokee na ndipo hapo alipoachana
na kikundi hiki. Baadaye alijiunga na kikundi cha Chuo cha Mafunzo (Magereza) na
akaimba nyimbo ya „Sitojali Kuchukiwa‟. Wimbo mwingine ambayo anatarajia
kuizindua hivi karibuni inaitwa „Maskini wa Bahati Tajiri wa Mikosi.
Siku zote “Waridi huchanua waridi” ndiyo hivyo kilivyo kwa kipaji cha Fatma
kwani ni urithi kutoka kwa wazazi wake wote wawili. Mama yake alikuwa ni
mwimbaji katika kikundi cha (Afican Light). Katika maisha yake Fatma anavutiwa na
kuwashabikia sana waimbaji wawili ambao ni Sabah Salum na Rukia Ramadhan wa
Zanzibar.
8
Picha namba 1: Mwimbaji wa Taarab bibi Rukia Ramadhan akiimba katika moja ya
shughuli iliyofanyika katika ukumbi wa Ngome Kongwe, Zanzibar
(Chanzo: Utafiti, juni 8, 2016)
Chanzo: www.bing.com/images/search?q=images of rukia ramadhan
Nyimbo zote ambazo yeye Fatma alizitunga na kutia muziki mwenyewe ni miongoni
mwa masahibu yaliyomkuta mwenyewe katika maisha yake. Kwa sasa Fatma ana
matatizo ya miguu na anapoimba hukaa kitako kutokana na maradhi hayo. 1
1.4 Wasifu wa Shakila Said
Picha namba 2: Mwimbaji wa Taarab bibi Shakila Said akiwa jukwaani (Chanzo:
Utafiti, juni 13, 2016)
Chanzo: www.bing.com/images/search?q=images of shakila said
1 Mahojiano kati ya mtafiti na msanii nyumbani kuhusu maisha yake yamefanyika kwake Kwa
Alamsha, tarehe 22/ 11/ 2015
9
Kuzaliwa na Ukoo Wake
Mzee (2013) anadai kuwa Tatu ndilo jina lake alilopewa Shakila lakini kutokana na
mahojiano yetu na msanii huko nyumbani kwake Charambe Dar es Salaam tarehe
12/3/2016 anasema kuwa Shakila ndilo jina sahihi alilopewa na wazazi wake na siyo
Tatu kama ilivyobainishwa na Mzee. Shakila alizaliwa mwaka 1947 katika Kitongoji
cha Malindi, Kata ya Pangani Mashariki, Wilaya ya Pangani Mkoa wa Tanga. Baba
yake mzazi ni Said Hamisi Dobi, mkulima mwenye asili ya Kiomboi Singida katika
kabila la Wanyiramba. Mama mzazi wa Shakila aliitwa Khadija Mohammed
Chatungwi wa kabila la Mnguu kutoka Mkoa wa Morogoro. Shakila alikuwa ni
mtoto wa kwanza kwa mama yake na mtoto wa pili kwa baba yake. Alitanguliwa
kuzaliwa na dada yake, Fatma ambaye ni mtoto wa mke wa kwanza kwa Said huku
akifuatiwa na ndugu zake ambao ni Salimu, Bijuma, Kirimbati na Kitinda mimba
wao Zanana.
Kama ilivyo kawaida ya Waislamu wote, mtoto lazima asome madrasa. Wazazi wa
Shakila nao hawakuwa nyuma kufanikisha suala hili. Mnamo mwaka 1953 Shakila
alipelekwa madrasa ya mwalimu Awadhi, Pangani, Tanga kupata elimu ya Kur-ani.
Shakila alisoma kwa juhudi zake zote na kuhitimu juzuu zote thelathimi akiwa katika
umri mdogo. Madrasa ni kitovu cha elimu ya Uisilamu. Katika madrasa huadhimisha
kila mwaka uzawa wa Mtume (s.a.w). Katika hafla hizo Shakila alikuwa kinara wa
kughani kasida mbalimbali katika shughuli hizo na ndiyo sababu iliyomsaidia hadi
leo kughani mashairi yake katika maonesho tofauti. Alipofikia umri wa kuanza shule,
wazazi wake walimpeleka shule ili aweze kuelimika na kufuta ujinga. Mwaka 1956,
Shakila alianza kusoma elimu ya msingi katika shule ya msingi huko Kimba,
Pangani. Alipofika darasa la nne, Shakila aliacha kusoma na kuendelea madrasa na
mara alipohitimu, alifungua madrasa yake na kuwasomesha watu wazima.
10
Mwanadamu hupitia vipindi tofauti vya maisha hususan katika suala la ndoa. Hivyo,
ndivyo ilivyomtokea Shakila katika maisha yake ya ndoa kwani ameweza kuolewa
mara kadhaa na waume wanne tofauti katika nyakati tofauti. Kwa mujibu wa Mzee
(2013), Shakila aliolewa kwa mara ya kwanza akiwa katika umri mdogo ingawa
hakuweka bayana umri huo. Aliolewa mwaka 1960 na mume aitwaye Waziri Ayuob
ambaye alifanikiwa kupata naye mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Waziri
aliyezaliwa mwaka 1963. Kwa vile mume huyu alikuwa chaguo la wazee wake na
siyo lake hakukaa naye sana na hatimaye aliachika.
Katika utamaduni wa Kiislamu, si vizuri sana na wala haipendezi mwanamke kukaa
ujane, Shakila aliolewa kwa mara ya pili na mume ambaye alimpenda na kumridhia
yeye mwenyewe. Mwaka 1968 aliolewa na Khatib Akida ambaye alikuwa mutribu
mwenzake wa taarab na ndiye aliyempa msukumo Shakila katika uimbaji wake.
Bwana huyu alizaa naye watoto wanne.Wa kwanza ni mvulana aitwaye Hamad 1969,
na wasichana watatu ambao ni Lucky alikufa 1972, Mwanahawa mwaka 1973 na
Maembe mwaka 1975. Kifo cha mumewe Akida kilipotokea ndicho
kilichowatenganisha.
Baada ya kukaa eda ya miezi minne na siku kumi Shakila aliolewa na mume wa tatu
aliyeitwa Kibwana Salehe Mkali. Aliishi naye kwa muda wa miaka minane. Bwana
huyu alizaa naye watoto watano ambao ni Hadija 1978, Bijaa 1980, Mape 1986,
Bachu 1988 na Mgeni 1990.
Baada ya kuachana na Mkali, Shakila aliolewa ma mume wa nne aliyeitwa Saaduni
Amiri ambaye alizaa naye mtoto mmoja aitwaye Shani 1993. Kati ya watoto 12
aliozaa Shakila, Mape pekee ndiye aliyerithi kipaji cha kuimba. Aliimbia Dar
11
Modern Taarabna sasa amehama katika kikundi hicho na wanajitegemea yeye na
mama yake. Shakila hivi sasa hana mume baada ya kuachana na mumewe Saaduni.
Nyota njema huonekana asubuhi na ndivyo hivyo ilivyojidhihirisha kwa kipaji cha
Shakila. Alianza kupenda kuimba kupitia michezo mbalimbali ambayo wakiicheza
na watoto wenziwe utotoni. Lakini kipaji hiki kiligundulika rasmi kwake Shakila
alipokuwa darasa la tatu mwaka 1958 wakati alipochaguliwa na walimu wake
kumburudisha hayati Mwalimu J. K. Nyerere, aliyekuwa mwasisi wa TANU na Rais
wa kwanza wa Tanganyika na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipotembelea
Wilaya ya Pangani mwaka 1958. Katika tukio hilo, Shakila alionesha kipaji chake
mbele ya viongozi na watu waliohudhuria kwa kuimba bila ya haya katika ngoma
iitwayo Msanja.Umahiri wa Shakila uliwapagaisha watazamaji na kutojizuia katika
sehemu walizokaa huku nderemo na vifijo vikitawala katika ukumbi hii ilitokana na
mvuto wa sauti yake pamoja na ustadi wake wa kucheza (Mzee, 2013).
Kila mwimbaji huwa na mtu au mutribu ambaye humvutia na kumuathiri ndani ya
moyo wake. Shakila alivutiwa sana na uimbaji na sauti nzuri ya marehemu Ummu
Kulthum wa Misri (1904- 1975) na marehemu Siti binti Saad (1888-1950), mwimbaji
wa zamani wa taarab asilia Zanzibar.
Picha namba 3: Mwimbaji wa zamani wa Taarab asilia Marehemu bibi Siti binti
Saad akiwa katika shughuli ya kutoa burudani (Chanzo: Utafiti,
juni 8, 2016)
Chanzo: www.bing.com/images/search?q=images of siti bint saad
12
Picha namba 4: Mwimbaji wa zamani wa nyimbo za Kiarabu bibi
Ummukulthoum (Chanzo: Utafiti, juni 13, 2016)
Chanzo: www.bing.com/images/search?q=images of ummukulthoum
Mnamo mwaka 1961Shakila alijiunga na kikundi cha kwanza cha taarab kilichoitwa
Black Star. Katika kikundi hiki Shakila alikuwa mwimbaji na mtunzi, mumewe
Khatib Akida mume wa pili akiwa mpigaji wa tashkota. Katika kikundi hiki Shakila
aliimba nyimbo nyingi na kutokana na ustadi wake wa kuimba na alijikumbia sifa
kemkem kutokana na sauti yake nyororo anapoghani. Alivuma zaidi pale nyimbo
zake na zile alizoshirikishwa zilipoanza kurekodiwa katika Redio Tanzania Dar es
Salaam (RTD). Baadhi ya nyimbo hizo ni Mpenzi Amini (1962), Pilipili Usoila
Yakuwashiani? (1962), Majuto Yamenipata Kukosana na Mpenzi (1963), Kitumbili
Namba Moja na Kitumbili Namba Mbili (1965).
Nyimbo nyengine ni Hujui Alacho Kuku (1968), Jongoo Wacha Makuu (1969), na
Akukataye Hakwambii Toka (1969), Mapenzi ni Kama Donda. Kikundi hiki
kilijizolea umaarufu siku hadi siku na hivyo kukodiwa katika harusi na sherehe
mbalimbali za kiserikali na binafsi. Baadaye kikundi hiki kiligawanyika kutokana na
matatizo ya uongozi katika matumizi ya fedha.
13
Mnamo mwaka 1970, kilianzishwa kikundi kingine cha Taarab kilichoitwa Lucky
Star maarufu kama Nyota Njema. Makao makuu ya kikundi hiki yalikuwa barabara
ya 13 mjini Tanga. Shakila na mumewe pamoja na watribu wengine kutoka Black
Star wakajiunga katika kikundi hiki. Kutokana na mialiko mbalimbali hasa ya nje
Shakila aliweza kupata umaarufu zaidi kutokana na kipaji chake cha kuimba.
Kwa mujibu wa Mzee (2013), Shakila alikuwa ni mwimbaji mkuu katika kikundi cha
Lucky Star. Nyimbo zake zilipendwa sana kutokana na maudhui yake na pia
zinaburudisha kutokana na uzuri wa sauti yake. Baadhi ya nyimbo alizotungwa na
kushirikishwa akiwa katika kikundi cha Lucky Star ni Sina Tabasamu (1971), Hali
ya Masikitiko (1971), Mapenzi Yamepungua (1972), La Mateso Penzi (1972),
Mapenzi Yako ni Chumo (1972) na Chumo Jema ni Ibada (1972). Nyimbo nyengine
ni Karibu Mwenge Karibu (1973), Ninauliza Wenzangu Nini Dawa ya Mapenzi
(1974), Wachuma Mali Huli Yakuhadaa Dunia (1974), Mapenzi Yanacheka (1975),
na Viva Frelimo (1975). Alidumu katika kikundi hiki mpaka alipofiwa na mumewe
Akida.
Kutokana na suala la kuimba kuwa limo ndani ya damu yake, Shakila hakutaka
kuacha muziki wa taarab. Katika mahojiano na mtafiti nyumbani kwake Shakila
amebainisha kuwa amejiunga na JKT mwaka 1980 na kutumikia Jeshi hilo kwa muda
wa miaka thelathini, kinyume na maelezo ya Mzee (2013) na kwamba Shakila
alijiunga na JKT mwaka 2001akiwa mwalimu katika kikundi hicho namwimbaji.
Makao makuu ya kikundi hiki yapo Mgulani Dar es Salaam. Katika kikundi hiki
Shakila alizidi kung‟ara ndani na nje ya Afrika Mashariki na aliendelea kutunga,
kuimba na kuwafundisha waimbaji chipukizi nyimbo mbalimbali. Baadhi ya nyimbo
hizo alizotunga ni kama Baba Musa Tulizana (1986), Kiyanga Yanga (2002),
14
Kitanda (2003), Mzigo (2005), Kobe Nakutuma (2008), Uliza Kwanza (2012),
Usishindane na Fupa (2012)na Naita Tanga.
Kwa mujibu wa Shakila katika mahojiano yetu ya (tarehe 12. 3. 2016) huko
nyumbani kwake Charambe amesema kuwa, ametunga na kuimba nyimbo nyingi
ambazo pia ametia muziki mwenyewe. Baadhi ya nyimbo hizo ni kama vile Naita
Tanga ambayo ameiimba kwa lugha ya Kizigua, Mzigo, Mapenzi Yamepungua,
Mapenzi ni Kama Donda, Kobe Kamwambie Mwewe na kadhalika. Sababu
iliyompelekea kutunga nyimbo hizo ni matatizo ya kimapenzi ambayo yamemkuta
yeye mwenyewe katika maisha yake.
Kutokana na juhudi za Shakila katika uimbaji na utunzi, kila kikundi alichojiunga
alikifanya kipate umaarufu mkubwa. Hivyo, aliweza kupata mialiko mbali mbali ya
binafsi na ya kiserikali. Katika mialiko hiyo alifanya maonesho katika nchi za Ufini,
Misri, Swiden, Ujerumani, Ufaransa na Denmark.
“Chanda chema huvikwa pete”, huu ni usemi maarufu uliozoeleka kutumika katika
jamii ya Waswahili. Mara nyingi mtu akifanya vizuri hupewa zawadi ambayo
aghlabu hataisahau katika maisha yake. Hivyo ndivyo ilivyo kwa Shakila kwani
kupitia tasnia ya muziki wa taarab amejizolea tuzo tofauti tofauti. Baadhi ya tuzo
hizo ni tuzo ya Zeze ya mwaka 2000, iliyotolewa na Mfuko wa Utamaduni Tanzania
(Tanzania Cultural Fund). Tuzo nyingine alizopata ni ile2 ya mwimbaji mkongwe wa
Taarab kupitia Tuzo za Muziki za Kilimanjaro (Kilimanjaro Tanzania Music Award).
Shakila amestaafu kuimba Taarab mwaka 2009, na hivi sasa ni Mwenyekiti wa
Chama cha Waimbaji wa Taarab Tanzania (Mzee: 2013).
2 Mahojiano kati ya mtafiti na msanii nyumbani kwake Charambe, Dar-es-Salaam, tarehe 12/ 3/ 2016
(Shakila Said alifariki tarehe 19/08/2016, saa tatu usiku Hospitali ya Temeke)
15
1.5 Malengo ya Utafiti
1.5.1 Lengo Kuu
Utafiti huu ulilenga kuchunguza dhamira za nyimbo za huzuni katika taarab.
1.5.2 Malengo Mahsusi
a) Kubainisha baadhi ya nyimbo za huzuni za waimbaji wateule.
b) Kubainisha sababu zilizopelekea kutungwa kwa nyimbo hizo, na;
c) Kutathmini jamii ilivyopokea dhamira na athari za nyimbo hizo.
1.6 Maswali ya Utafiti
Utafiti huu uliongozwa na maswali yafuatayo:
a) Ni zipi nyimbo za huzuni za Bi Fatma Issa na Shakila Said?
b) Ni sababu gani mahasusi zilizopelekea kutungwa kwa nyimbo hizo?
c) Jamii imezipokeaje dhamira na athari za nyimbo za huzuni za waimbaji hao?
1.7 Manufaa ya Utafiti
Tasnifu hii imekuwa chachu ya kuwawezesha wasomaji kujua dhamira na sababu ya
kutungwa kwa nyimbo zenye za taarab zenye maudhui ya huzuni katika jamii. Pia,
utafiti huu umeuwezesha jamii kugundua nafasi na mchango wa nyimbo za huzuni
katika jamii. Aidha, umesaidia kuondosha dhana kuwa nyimbo hizo za taarab ni za
furaha na ramsa tu na sivyo vyenginevyo.
1.8 Nadharia ya Utafiti
Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya uhalisia. Hivyo, ukusanyaji wa data,
uchambuzi na uwasilishaji wa data hizo uliongozwa na nadharia hiyo. Nadharia hii
ilizuka baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia baada ya watu wengi kuathirika na
madhara ya vita hivi. Athari hizo ni kama vile umasikini, njaa, vifo, mporomoko wa
16
uchumi na kadhalika. Nadharia hii iliasisiwa na mwanafalsafa Hegel katika miaka ya
1980 ya karne ya ishirini. Nadharia hii imeweza kuhusishwa na kazi ya kifasihi za
Kiswahili, na imebainisha misingi mikuu miwili ambayo inaweza kutumika katika
kuongoza uatafiti huu. Misingi hiyo ni;
a) Msingi wa kimhakati. Huu ni msingi ambao unaeleza matukio kama
yalivyo katika maisha ya kila siku bila ya kubadilisha kitu hata kimoja.
b) Msingi wa ushabihi ukweli. Huu ni msingi ambao unakaribia kueleza
matukio kama yalivyo bila ya kuongeza au kupunguza.
Kwa vile nadharia hii imeelezea matukio kama yalivyo katika jamii, nyimbo za
huzuni ni mojawapo ya kazi ambazo zinaakisi hali halisi inayoikumba jamii kila
siku. Huzuni ni sehemu ya matukio ambayo humtokea kila mtu katika maisha ya kila
siku. Hakuna mtu anayeweza kukwepa si masikini si tajiri. Nadharia hii imesaidia
kubainisha jinsi gani wasikilizaji na watazamaji kuweza kuguswa na nyimbo hizo
ambazo zinabeba maudhui ya huzuni. Aidha, imesaidia kutambua sababu
zinazowasukuma wasanii kutunga mashairi yenye huzuni na masikitiko katika jamii
zao. Kwa vile hali ya huzuni huwasonenesha wanajamii kwa kiasi kikubwa katika
jamii, nadharia hii ya uhalisia imeongoza na kuufanikisha utafiti huu kwa muda
muafaka.
1.9 Hitimisho
Katika sura hii ya kwanza utafiti umeangalia utangulizi, usuli wa tatizo, tamko la
utafiti, wasifu wa wasanii teule ambao ni Shakila na Fatma, malengo ya utafiti,
maswali ya utafiti na manufaa ya utafiti. Aidha, sura hii ilifafanua nadharia
iliyotumika katika utafiti huu ambayo niNadharia ya Uhalisia na misyake mikuuni
msingi wa kimhakati na ushabihi ukweli. Sura inayofuata itazungumzia mapitio ya
maandiko.
17
SURA YA PILI
MAPITIO YA MAANDIKO
2.1 Utangulizi
Sura hii imefafanua maandiko mbalimbali yanayohusiana na mada hii. Maandiko
hayo yamegawika katika sehemu kuu tatu. Kwanza ni maandiko yanayohusiana na
chimbuko la taarab. Pili, maandiko ya tafiti mbalimbali yanayohusina na taarab na
hatimaye makala mbalimbali zinazohusiana na taarab.
2.2 Chimbuko la Taarab Zanzibar
Kila jambo au kitu ambacho hutokea katika ulimwengu huu huwa na asili na chanzo
katika kuibuka kwake. Waandishi wengi wameandika vitabu, majarida na makala
kuelezea chimbuko, historia na maendeleo ya taarab Zanzibar. Kati ya hao ni Khatib
(2014), Mgana (1991) na kadhalika. Khatib (2014) katika Taarab Zanzibar, anaeleza
juu ya asili na vipindi mbalimbali vilivyopitia Taarab huko Zanzibar kama vile
kipindi cha ukoloni na ubepari na hadi baada ya Mapinduzi. Pia anaendelea kuelezea
kuwa lengo la Taarab la asili ni kuliwaza, kubembeleza, kukumbusha, kumithilisha,
kufurahisha na kupoza moyo. Lengo lingine ni, kusuuza nyoyo za watu waliojinamia
kwa huzuni na masaibu mbalimbali yanayowafika wanadamu.
Inaaminika kuwa taarab Zanzibar ilianza katika kipindi cha Sultan Seyyid Barghash
(1870-1888) (Khatib 2014, Mgana 1991). Mfalme huyu inasemekana alikuwa ni mtu
mwenye kupenda starehe na anasa, hivyo muziki wa taarab ukawa unapigwa katika
kasri yake ya Beit-el-Ajaib. Mapema Sultan Seyyid Barghash (1870- 1888) aliagiza
watu waliokuwa wajuzi kutoka Misri kuja kumpigia muziki huo. Baadaye alimpeleka
mtu maalum huko Misri aliyeitwa Muhammed Ibrahim, ili apate kufundishwa stadi
hii ya muziki wa taarab (Khatib: 2014-1-2). Aliporudi mutribu huyu Misri alikuwa
18
tayari ameshajua kuimba na kutambua kuzitumia ala za taarab. Inaaminika nyimbo
za taarab wakati huo zilikuwa za Kiarab kitupu.Kikundi maalum cha taarab ya Sultan
kikaanzishwa. Sanaa hii ilieendelea kumstarehesha Sultan na aila yake hata baada ya
kifo cha Seyyid Barghash. Alipoingia katika utawala naye sultan Khalifa bin Haroub
(1911-1960), aliidumisha na kuipalilia sanaa hii ya taarab kwa lengo la
kumstarehesha yeye mwenyewe kwa kumwondolea mawazo na machofu ambayo
yamkabili katika mwili, akili na moyo wake.
Picha namba 5: Mtawala wa Zanzibar Sultan Seyyid Barghash (1870-1888)
(Chanzo: Utafiti, juni 14, 2016)
Chanzo: www.bing.com/images/search?q=images of seyyid barghash
Hivyo, taarab ilikua na kuendelea hata baada ya kuondoka kwa mifumo ya kisultani
kiutawala.Vikundi vya watu binafsi vilianzishwa mapema sana. Vikundi vya
mwanzo ambavyo vilioanzishwa ni pamoja na; Naad Akhwan Safaa mwaka 1905,
Mwaka 1908 ilifatiwa na Naad Shuub1910 (Khatib: 2014). Vikundi vyengine
vilianzishwa mwaka 1945 Royal Air Force, 1945 Nuru- l-Uyunn, 1945 Sahib el Ari,
1945 Navy, 1945 Banati,1955 Michenzani 1957 Miembeni 1964 Kwa Alamsha 1964
Culture1964 1985 Wardah el Baidha 1986 Mila na Utamaduni 1986 Polisi 1986
19
Jeshi 1989 Ilyas& The Twinkling Star na mwaka 1989 Bwawani Musical Club.
(IssaMgana: 1991). Taarab ya vikundi vyote hivyo vilifata mtindo wa taarab asilia.
Baadaye vikundi vifuatavyo vikafata mtindo wa taarab ya kisasa vikiwemo East
Afican Melody; Tanzania One Theater (TOT); Zanzibar Stars, Dar-es-Salaam
Modern Taarab na vyenginevyo. Kadri siku zilivyoendelea kusonga mbele, muziki
wa taarab uliweza kupokea mabadiliko makubwa katika utumiaji wake wa vyombo
vyake vya asili na hata kucheza katika majukwaa. Hali hii ilichangiwa sana na suala
usasa wa matumizi ya vyombo vya elektroniki vitumiavyo umeme kuanza kutumika.
Vifaa ambavyo vikitumika katika muziki wa taarab wa asili kama vile Udi, Violin,
Dumbaki na Dafu vimeanza kuachwa. Wapo wanaoamini kuwa uasili wa taarab
asilia na utamu wake umeanza kupotea. Sababu kuu ni mabadiliko ya vyombo na
kuingiza uchezaji jukwaani. Sanaa ya Taarab kama zilivyo sanaa nyingine huenda na
wakati na pia huvuka mipaka na kuenea sehemu nyingi (Khatib, 2014).
2.3 Maandiko Yahusuyo Taarab
Muziki wa Taarab kwa kiasi kikubwa umeweza kuenea kwa kasi sana kutokana na
mahadhi na mashairi yake kuwakonga na kuwasuuza mioyo ya walio wengi. Wapo
wataalamu wengi sana ambao wametoa mchango wa kitaaluma ikiwemo katika suala
hili ikiwemo kuweza kupembua ni kwa jinsi gani muziki huo wa taarab unaweza
kuleta tija kwa wanajamii. Yapo maandiko mengi ya kiutafiti na makala yaliyojadili
taarab katika mielekeo tofauti. Wapo watafiti ambao wamezungumzia kuhusiana na
kipengele cha maudhui ya taarab lakini wametofautiana kwa kiasi katika tafiti hizo
zao.
20
Alawiy (2007) alifanya utafiti wake juu ya“Nyimbo za mafumbo za taarab
zinavyochangiakudumisha maadili ya jamii ya Wazanzibari”. Katika utafiti wake huo
alieleza kuwa nyimbo za taarab zimechangia sana katika kuendeleza na kukuza
maadili ya Wazanzibari. Pia alielezea kuwa asilimia kubwa ya nyimbo za taarab
zinalinda mila na desturi pamoja na heshima ya jamii, akihusisha utamaduni wa
Wazanzibar ambao hutumia lugha yenye staha na stara.
Saleh (1980) alifanya utafiti juu ya “Maudhui ya nyimbo za taarab za Unguja”. Yeye
alibaini kuwa lugha ndiyo kipengele muhimu kinachosaidia jamii kupata maudhui
hayo kwa urahisi zaidi. Saleh kwa upande wa fani anaeleza kuwa baadhi ya nyimbo
za taarab hutumia lugha nzito yenye mafumbo ndani yake ambayo si rahisi kwa
mtazamaji na msikilizaji kuupata ujumbe uliokusudiwa kwa haraka.
Mtafiti mwengine aliyeshughulikia nyimbo za Taarab ni Thabit (2007) ambaye
alitafiti juu ya “Nyimbo za taarab katika jamii ya Zanzibar”. Matokeo ya utafiti
wake yanaonesha kwamba maudhui ya nyimbo za taarab yana umuhimu katika
kusaidia kujenga malezi na maadili mema katika jamii ya Wazanzibar.
Alhabib (2012) katika utafiti wake wa matumizi ya “lugha katika nyimbo za taarab”
anabainisha kwamba lugha ya nyimbo za taarab imejaa mafumbo, sitiari, ishara,
taswira na picha na hivyo kuwa kivutio kwa wasikilizaji wake.
Broughton na wenzake (2000) kama alivyonukuliwa na Khamis (2012:20) wanadai
kwamba, kimaudhui, nyimbo za taarab zinalenga ziadi kwenye mapenzi. Nyimbo
hizi hutumia fani ya mafumbo na sitiari zaidi ambazo huwafanya watu waso na
uelewa na ujuzi wa sanaa hii kutoelewa maudhui ya nyimbo hizo. Hata hivyo,
21
wameona kuwa kuna baadhi ya nyimbo za siasa ambazo zinaeleweka kwa vile
hazitumii mafumbo.
Katika mwelekeo wa fani katika taarab, mengi yamefanyiwa utafiti.
Mzee (2013) amefanya utafiti kuhusu “Maudhui katika Nyimbo za Taarab za Bi.
Shakila” Kwake yeye alihusisha na fani ameona kwamba matumizi ya lugha yana
mchango mkubwa katika kuibua dhamira mbali mbali. Hivyo nyimbo hizo hutumia
vipengele mbali mbali vikiwemo vya tamathali za semi, methali na mafumbo ili
kuweza kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa hadhira. Mzee anaendelea kwa
kubainisha kuwa vipengele vya lugha vinaweza kuficha lugha ya karaha na matusi
katika kufikisha maudhui hayo. Hivyo, vinaweza kuadilisha, kuionya na kuikosoa
jamii bila ya kuleta mfarakano miongoni mwa jamii. Aidha kuhusu maudhui
(dhamira) yaliyomo katika nyimbo za Bi Shakila kwake yeye anaona kuwa
yanasawiri hali halisi ya maisha yaliyopo katika jamii.
Naye Hamisi (2012) alifanya utafiti juu ya “Matumizi ya Taswira na Mafumbo
katika Nyimbo za Mapenzi na Taarab Asilia.” Anaeleza kwamba taarab, hasa ile
asilia imedhamiriwa kuadilisha jamii. Katika kufanikisha suala hilo, wasanii
hutumia lugha yenye staha na ile aliyojengwa kwa namna inayobeba na
kuzungumzia masuala mazito badala ya kutumia lugha ya wazi isiyoficha hata yale
yasiyotakiwa kutamkwa na au kusikika hadharani. Yeye anaona kuwa yapo maneno
ambayo kwa mujibu wa mila na desturi za jamii ya Waswahili hayapaswi kutamkwa
wazi wazi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kufanya hivyo ni sawa na kubomoa
badala ya kujenga maadili ya jamii.
22
Watafiti wengine wamejadili taarab na maendeleo yake katika mwelekeo tofauti ya
kifani na maudhui. Mbali ya wataalamu hawa kuhusisha taarab na dhima yake ya
kimaudhui na kifani, wengine wameangalia katika njanja tofauti.
Mzee (2011) alifanyia utafiti juu ya “Nyimbo za taarab asilia za Zanzibar”, katika
uchunguzi wake amezungumzia jinsi taarab zinavyokuwa na zinavyoendeshwa
katika harakati mbalimbali za maisha zikiwemo sherehe za harusi, matamasha,
kwenye shughuli za kisiasa na hata za biashara. Pia alielezea jinsi ya taarab asilia
inavyolinda utamaduni wa Mswahili.
Farhan (1992:4) amefanya utafiti juu ya “Historia ya nyimbo za taarab”. Yeye
ameeleza kuwa wakati wa kipindi cha miaka ya arubaini mpaka sitini nyimbo za
taarab zaidi zilikuwa zinazungumzia maswali ya mapenzi. Lakini kadri miaka
ilivyosonga mbele maudhui ya mapenzi yanabadilika kulingana na mabadiliko ya
jamii.
Ndungo na Wafula (1993) katika makala yao wamezungumzia kuhusiana na chanzo
na maendeleo ya taarab katika jamii ya Waswahili. Kwa ufupi sana wameeleza
muundo wa taarab ulivyokuwa.
Igobwa (2007) katika makala yake ya “Taarab na Chakacha”anadai kwamba taarab
inachukuliwa kama shughuli ya kijamii. Igobwa akimnukuu Ntarangwi (2003:149)
anaelezakuwa muziki wa taarab huwa unapigwa kwenye harusi za Waswahili kwa
kuwafurahisha waliokusanyika huku ukitumia mashairi ya Kiswahili yenye mvuto.
Anaeleza kuwa nyimbo hizi huwa zinatungwa upya katika onesho kutokana na
mchango wa wasikilizaji.
23
Khatib (1982) katika makala yake ya, Tarabu ni fasihi simulizi?, ameona kuwa
tarabu ni muziki wenye kupigwa na kuchanganywa na nyimbo ambao utaweza
kukidhi vitabia vya sanaa ya fasihi simulizi. Anaendelea kufafanua kuwa vitabia
hivyo vya taarabu na vile vya kazi nyengine ya fasihi simulizi kadiri vinavyoachana
au kukaribiana. Pia amehitimisha kwa kueleza kuwa tarabu asilia ina utendaji wenye
mipaka na ufinyu ukilinganisha na utendaji wa tanzu zingine za fasihi simulizi.
Zeid (2016), amebainisha kuwa taarabu asilia ni tarabu ambayo ina heshima na
inajali utu wa mtu kwani mtu anaposimama juu ya jukwaa huwa anajiheshimu na
kutulia na kuimba kwa staha zaidi na vile vile hutumia lugha ya mafumbo ambayo
inataka ujuzi kufumbua fumbo lilokusudiwa. Kuhusu tarabu ya sasa ni tarabu
ambayo inajali maslahi mtu tu nasi vyenginevyo. Mawazo yake yanashabihiana na
yale ya Shakila ambapo amesema kuwa “Waimbaji wa sasa wanaimba kwa lengo la
kujipatia kipato fulani na wala haina lengo la kuwaburudisha jamii nzima”.3
Imebainika kuwa watafiti wengi wamefanya tafiti zao katika maeneo tofauti
kuhusiana na suala zima la taarab. Wamegusia chimbuko la taarab asilia na mipasho,
maudhui, fani na maeneo mengine. Hata hivyo kazi zote hizo hazijajikita kuongelea
taarab na kuwa kiasili, katika chimbuko lake, ni muziki wa raha na ramsa. Na
kwamba sasa dhana ya kuongelea huzuni na simanzi sio ngeni na ni sehemu ya
mabadiliko katika tasnia hii. Katika muktadha huu hakuna aliyejadili juu ya taarab
imegeuka kuwemo dhamira za huzuni. Utafiti huu umeliziba pengo hilo.
3 Mazungumzo ya mtafiti na Shakila Charambe, tarehe 12/ 3/ 2016
24
2.4 Pengo la utafiti
Kulikuwepo na pengo kubwa katika dhamira za nyimbo za taarab asilia na za mtindo
wa kisasa na kuamini kuwa taarab kidhamira ni za furaha, bashasha na vicheko. Hata
lengo la kuanzishwa muziki huu ulikuwa ni kutoa maudhui yanayobebwa na muziki
wa furaha tu. Hakuna kazi ya utafiti iliyatanabahisha hilo. Utafiti huu umetoa
muelekeo mpya.
2.5 Hitimisho
Katika sura hii mjadala ulijikita katika maandiko mbalimbali yanayolandana na
malengo ya utafiti huu. Utafiti huu uliangalia maandiko yenye maana taarab na
chimbuko lake. Aidha, maandiko yaliangaliwa na mabadiliko ya kidhamira kutoka
mtazamo wa kiasili kuiona taarab ni muziki wa furaha na kuwa sasa muziki wa
majonzi, simanzi na huzuni. Sura inayofuata itazungumzia usanifu na mbinu za
kukusanyia data.
25
SURA YA TATU
USANIFU NA MBINU ZA KUKUSANYIA DATA
3.1 Utangulizi
Sura ya tatu imefafanua mpango wa jumla wa utafiti huu, mbinu zilizotumika
kukusanyia data na zana na vifaa vya utafiti vilivyotumiwa. Utafiti umebainisha
jamii ya watafitiwa, eneo la utafiti, mchakato mzima wa ukusanyaji ulivyokwenda
uchambuzi wa data, ikiwemo uhalali wake na uthabiti wa matokeo ya utafiti.
3.2 Mpango wa utafiti
Utafiti huu mchakato wake ni wa kitaamuli kwa vile ulionekana kuwa ni bora zaidi
na ulitumia njia ya maelezo katika uchambuzi wa data. Utafiti ulifanyika uwandani
na maktabani. Mtafiti alitumia njia ya uwandani zaidi kuliko maktabani kutokana na
uhalisia wa utafiti wenyewe. Hii ni kwasababu wahojiwa walikuwa wametawanyika
sehemu mbalimbali kama vile mitaani, katika vituo vya redioni na mashuleni. Utafiti
huu pia uliongozwa na nadharia ya uhalisia ambayo ililingana na matakwa ya utafiti
huu.
3.3 Eneo la utafiti
Utafiti huu ulifanyika katika kisiwa cha Unguja katika Wilaya ya Mjini na viunga
vyake. Maeneo haya yaliteuliwa kwa kuangalia vigezo thabiti ambavyo upatikanaji
wa data ulikuwa ni rahisi. Eneo la mji wa Unguja ni sehemu yenye wadau na
wapenzi wa muziki wa taarab ambao kwa kiasi kikubwa wanafuatilia kwa karibu
sana nyimbo za Shakila na Fatma.
3.4 Walengwa wa Utafiti
Walengwa wa utafiti huu waligawanyika katika maeneo makuu mawili ambayo
ndiyo yenye jamii ya watafitiwa na sampuli ya utafiti.
26
3.4.1 Jamii ya Watafitiwa
Walengwa wa utafiti huu walikuwa ni wapenzi wa nyimbo za taarab za Shakila na
Fatma wengine ni waendeshaji wa vipindi vya taarab vya redio, waimbaji wa nyimbo
zenyewe ambao walishirikishwa. Hata watafiti wa kazi za taarab walihusishwa.
Mgawanyiko wa makundi ulikuwa kama ufuatao;
a) Wapenzi mbalimbali wa tasnia ya taarab asilia hasa wa nyimbo za Shakila na
Fatma;
b) Watangazaji wa redio wa nyimbo za taarab asilia,
c) Wasanii wateule wa muziki wa taarab ambao ni Shakila na Fatma.
d) Wanafunzi walioshughulikia na taarab asilia katika tafiti zao.
3.4.2 Usampulishaji na Sampuli Iliyotumika
Kwa mujibu wa Kothari (2003), sampuli nzuri ni ile iliyo ndogo, jumui na
itakayomuwezesha mtafiti kuidhibiti. Kombo (2006) anaona: “Kusampulisha ni
mchakato wa kuchagua idadi ya wawakilishi wenye tabia sawa na walengwa wa
utafiti”. Kutokana na mawazo ya wataalamu hao, kwa hivyo sampuli hii
imeyazingatia hayo na iliteua na kuchagua wawakilishi ambao walitumika katika
kazi husika. Hivyo, kwa utafiti huu, sampuli ilichaguliwa kwa kuzingatia mbinu ya
usampulishaji lengwa ili kupata uwakilishi halisi. Makundi ya sampuli halisi
yalikuwa kama hivi ifuatavyo;
a) Washabiki kumi wa tasnia ya muziki wa taarab asilia.
b) Watangazaji watano wa muziki wa taarab;
c) Wanataaluma kumi na tano waliofanya tafiti za taarab;
d) Wasanii wawili teule ambao ni Shakila na Fatma.
27
3.5 Ukusanyaji wa Data
Kipengele hiki kinaelezea njia na zana mbalimbali ambazo zimetumika katika
ukusanyaji wa data.
3.5.1 Njia za ukusanyaji wa data
Mtafiti alitumia data za awali kupitia njia ya usaili, ushuhudiaji na udodosaji. Mbinu
hizi zilifanya utafiti huu kuwa halisi zaidi kwani mtafiti alipata kushiriki kikamilifu
katika maonesho kadhaa ya taarab. Pia mtafiti alipata muda wa kuona CD na
kusikiliza nyimbo za waimbaji wateule.
3.5.2 Usaili
Mtafiti alitumia mbinu ya usaili kwa washabiki na wapenzi wa muziki wa taarab
hususan nyimbo za Shakila na Fatma na hata kwa watangazaji wa vipindi vya taarab
asilia katika redio. Mtafiti alitumia njia hii ili kupata taarifa hata kwa wale wote
ambao hawajui kusoma na kuandika. Kwa upande wa watangazaji wa redio mbinu
hii ilimsaidia mtafiti kubadilishana mawazo nao ana kwa ana ili kupata taarifa za
undani na maoni yao kuhusiana na taarab asilia.
3.5.3 Dodoso
Mtafiti alitumia dodoso wakati wa kukusanyia data. Dodoso zilitumika kwa wale
wenye uwezo wa kusoma na kuandika. Mbinu hii ilitumika kuwahoji wanafunzi
ambao wamefanya tafiti zao kuhusiana na taarab asilia ili kupata maoni na mawazo
yao kuhusu utafiti huu.
3.5.4 Ushuhudiaji
Mtafiti alitumia mbinu hii kwa kushiriki baadhi ya maonesho ambayo yalitendeka
katika majukwaa mbalimbali ili kuona jinsi gani nyimbo hizo zinavyoathiri au kuteka
nyoyo za watu.
28
3.6 Zana za kukusanyia data
Mtafiti atatumia zana tofauti ili kukamilisha utafiti. Zana hizo ni pamoja na;
3.6.1 Kamera
Kamera ilitumiwa na mtafiti kupiga picha sehemu ambazo zitaonesha waimbaji na
pale waimbaji wakiwa jukwaani. Pia ilitumika picha kupiga nao waimbaji hawa
wateule na makundi mengine ya watafitiwa.
3.6.2 Simu
Mtafiti alitumia simu kwa ajili ya mawasiliano na ukusanyaji wa data na pia kwa ajili
ya kurekodi na kupiga picha.
3.6.3 Daftari na kalamu
Mtafiti alitumia daftari na kalamu katika ukusanyaji wa data ili kuandika taarifa
muhimu zinazohusiana na utafiti na kutunza kumbukumbu muhimu kutoka kwa
wasailiwa.
3.6.4 Ngamizi
Mtafiti alitumia ngamizi katika kuchapa na kuangalia baadhi ya taarifa katika tovoti
mbali mbali.
3.7 Mchakato wa Ukusanyaji Data na Uthabiti wake
Utafiti huu ulifuata taratibu sahihi zipasazo kufuatwa na mtafiti. Mtafiti aliomba
ridhaa kwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma pamoja na kupata kibali katika
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Raisi wa Zanzibar ambaye ndiye mtoa kibali kisheria
kwa upande wa Tanzania Zanzibar ili kupata uhalali wa kuingia sehemu mbalimbali
kukusanya data. Aidha, tahadhari ilichukuliwa katika kuhakikisha kuwa taarifa zote
zinazotoka kwa wahojiwa zimekuwa siri. Data za uwandani zimekusanywa kwa njia
29
ya usaili, dodoso na ushuhudiaji. Mwongozo wa usaili utatumika kuwahoji wasanii
teule pamoja na wadau wa muziki wa taarab. Pia, walihojiwa wataalamu wa fasihi
hususan wa fasihi simulizi kwa njia ya ushuhudiaji. Mtafiti pia alitembelea maonesho
mbalimbali ya taarab na kuangalia na kusikiliza CD za nyimbo za waimbaji wateule.
3.8 Mipaka ya Utafiti
Utafiti huu ulijikita zaidi katika kuchunguza namna ya mashairi ya taarab ya huzuni
yanavyojitokeza katika nyimbo za taarab hasa za Shakila na Fatma. Nyimbo
nyengine zote za waimbaji hao ambazo hazihusiani na huzuni hazikushughulikiwa
katika utafiti huu. Pia utafiti haikujadili muziki au tuni za waimbaji wateule.
3.9 Vikwazo vya Utafiti na Utatuzi wake
Mtafiti alipata vikwazo pale baadhi ya wahojiwa kutokuwa tayari kutoa majibu ya
maswali ya mtafiti, na kukataa kuchukuliwa picha zao. Mtafiti alifanya jitihada ya
kuondoa dhana potofu za wahojiwa kwa kuwaelimisha juu ya malengo ya utafiti na
baadae walikubali. Hali ya kupungukiwa fedha za kuendesha mchakato wa utafiti
kwa vile waimbaji wanaishi Zanzibar na Dar es Salaam ulijitokeza. Katika hili
mtafiti ilimbidi atafute kwa wahisani mbalimbali. Jambo ambalo lilifanikiwa na
kufanikisha mchakato huu.
3.10 Hitimisho
Sura hii imejadili mambo mbalimbali ikiwemo mpango wa utafiti, eneo la utafiti,
walengwa wa utafiti, ukusanyaji wa data, mipaka ya utafiti na vikwazo vya utafiti na
utatuzi wake ambavyo vyote vimefafanuliwa kwa kina katika sura hii.
30
SURA YA NNE
UWASILISHAJI, UCHAMBUZI NA MATOKEO YA MJADALA WA
UTAFITI
4.1 Utangulizi
Sura hii imejadili kwa kina matokeo ya utafiti. Mjadala huo umegawanywa katika
sehemu kuu tatu kwa kuzingatia maswali na malengo ya utafiti huu. Sehemu ya
kwanza imefafanua sababu zilizowashawishi kutunga nyimbo zenye maudhui ya
huzuni. Sehemu ya pili imefafanua dhamira za nyimbo zenyewe na athari zake hasi
na chanya. Sehemu ya tatu na ya mwisho imelinganisha tofauti na mfanano kati ya
waimbaji wateule Fatma na Shakila. Hivyo, katika kila sehemu ya sura hii data
ziliwasilishwa kwa njia ya maelezo na kuongozwa na nadharia teule ya Uhalisia
ambayo husawiri hali halisi ya maisha ya mwanadamu katika maisha yake ya kila
siku.
4.2 Dhana ya Huzuni
Huzuni kama dhana ngeni katika muziki wa taarabkwa mwanadamu ni ile hali ya
masikitiko, majonzi, jitimai au simanzi ambayo mtu huipata ndani ya nafsi yake.
Huzuni huwa na visababishi kadhaa katika jamii. Hali hizo ni kama vile matokeo ya
misiba, maradhi, usaliti na kadhalika. Dhana ya huzuni katika maisha mwanadamu si
ngeni masikioni mwa walio wengi, kwani hali hii hujitotokeza mara kwa mara katika
maisha halisi ya watu kila siku. Mwanadamu hupatwa na huzuni kupitia mambo
mbalimbali anayotendewa au yalomsibu. Huzuni humfika mtu yeyote lakini kila mtu
huwa na namna yake ya kuipokea au kuikabili. Mwengine humfika akanyamaza
asitake mwengine ajue. Huweza mtu ikampata akasononeka nayo na mwishowe
kumuathiri. Wale wachache wenye vipaji wakiwemo washairi na waimbaji
31
hawaifutiki huzuni ikawatesa, bali huitoa hadharani kama dukuduku kwa njia ya
sanaa. Watu wa aina hii aghlabu huzuni haiwaumizi.
4.3 Nyimbo za huzuni za waimbaji wateule
1. KHERI ADUI SHETANI KAMA ADUI KIUMBE
Tutahadhari adui kiumbe, daima asikusibu Mungu akuepushie
Ujue si mzuri hata chembe, huwa hataki sababu mashakani akutiye
Hata kuchoka hachoki kwa kila pembe, na wala haoni tabu hasarani aingiye
Hata kama kitu huna masikini hambe, basi atakusulubu maisha uyajutiye
Adui umuonapo mkimbiye, kheri adui shetani kama adui kiumbe
Malipo ni duniyani, akhera hwenda hisabu viumbe
Kwa kweli wanalingana mfitini na hasidi, chanzo chake huwa choyo shoti
uwatambuliye
Tena wengi wapo hufanya juhudi, huzua yaliyo siyo ili wakuvurugiye
Huwa mkarimu kwao na hujitahidi, hakosi kisingizio mwema adui hanaye
Japo mwenyewe chako kakubariki wadudi, watakwendea mbio hadi lao
litimiye
Mja mwanadamu kufikiri na kuhisi, ndio hasa tarajio liburi simfnyiye
Maana wivu chuki hasada binafsi, huambatana na choyo husuda akuonee
Na kufanyiana hayo yake nafsi, roho mbovu alonayo yataka ajaliwaye
Mpewa hapokonyeki hapana dadisi, mtengenezaji hayo mola ndiye atoaye
Mjue hana kosa apewaye, kheri adui shetani kama adui kiumbe
Malipo ni duniani, akhera hwenda hesabu viumbe
Ni yeye mwenye uwezo mshirika hana, kwake hakuna lawama huwapa
wamuombaye
Wewe uonavyo mengineyo huna, nawe usikate tama muombe akujaliye
32
Kuchukuwa kwa kuwana si uungwana, ni tabia mbaya jama ziwacheni
mtubiye
Huu si wakati tena wakufatanafatana, yapo mengi yalazima ya thawabu
jichumiye
Mja mwishowe akusaidiye, kheri adui shetani kama adui kiumbe
Malipo ni duniani, akhera hwenda hesabu viumbe
KIITIKIO
Imani imewasakama wakiona yakwendea
Imani zimewahama rohoni wanaumiya
Lo! Po! Yasini mate chini ninatema
Kunusuru ya jaliya nahizi tabia mbaya
Mwimbaji: Fatma Isa
2. ASOKASORO HAKUNA
Hicho kilonichukiya maovu kunikataza, ikiwa nnakoseya wajibu kuniongoza
Ikiwa nnakosea wajibuweni kuniongoza, wala sioni vibaya mimi kunielekeza
Kinachonipa udhia, ni kule kuniapiza
Aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Asokasoro hakuna, aloumbwa na muweza
Mwenye lile hili hana, ndio shani yake azza
Tabia kutolingana, sijambo lakushangaza
Kinachonikera sana, nisonalo kupakaza
La msingi niiteeni, na wala sitopuuza
Sikatai nambieni, wallahi tawasikiza
Mengine msinidhani, yakuwa nitawabeza
Name tawashukuruni, kwa vile mmenifunza
33
Kama kosa nimefanya, na iwe nimeteleza
Dogo msilipe mwanya, likaja likatatiza
Mukawa mwayakusanya, nyinyi mnoendeleza
Hivyo sitokaa kimya, lazima tawaeleza
Kiitikio
Kunisema sichukui
Kusengenya haifai
Ni hekima njema rai
Kunionya sikati
Mwimbaji: Fatma Isa
3. HAYA MAUMBILE YANGU
Ubinafsi na choyo, nyoyoni vyawasumbuwa
Kutwa kazi yenu hiyo, zimewajaa shakawa
Kufanya niyapendayo, kwangu kosa limekuwa
Hilo haliwezekani, na wala halitokuwa
Leo nakuelezeni, muache kunichunguwa
Msijitie shidani, haya nimejaaliwa
Kwani hasa jambo gani, nyie lakulaumiwa
Kama baya kwenu nyie, kwangu nnaona sawa
Nawambia msikie, msio fahamikiwa
Fedhehani msingiye, kukaa kujizuzuwa
Lilobaki mnachie, sitaki kulaumiwa
Wengi wamenihasimu, na thamani kunitoa
Mwapita kumwaga sumu, kila ovu kutupiwa
34
Bure mnanituhumu, yafitina kuyagawa
Nami ni mwanadamu, si vyema kulaumiwa
Kiitikio
Nami ni mja mwezeni
Hata mkinichukiya
Aibu yangu ndo yenu
Kama mtafikiriya
Mwimbaji: Fatma Isa
4. AKUKATAAYE HAKWAMBII TOKA
Akukataaye, hakwambii toka
Huona mamboye, yamebadilika
Waweza ukae, huwezi ondoka
Nipende kwa dhati, au nikataye
Usinidhihaki, la kweli nambiye
Kama hunitaki, kheri nituliye
Watu hutendana, zaidi ya hayo
Wakatukanana, kupita mifano
Mwisho hupatana, yakesha maneno
Mwimbaji: Shakila Said
5. MAPENZI YAMEPUNGUA
Nilipokuwa na pendo, na ikawa twapendana
Hukuwa navyo vishindo, wala hatukupigana
Umebadilika mwendo, ni kheri tukaachana
35
Duniani wengi wapo, wapenzi kila aina
Usidhani peke yako, uzuri mnapitana
Sina haja pendo lako, dunia hii pana
Kiitikio
Mapenzi yamepunguwa mimi nimeshayaona
Kila nikiyachunguza hakwishi kuoneana
Mapenzi yamenguwa.
Mwimbaji: Shakila Said
6. MAPENZI NI KAMA DONDA
Nimechoka vumiliya, leo nawapasuliya
Nimekuwa siku hizi, kila siku ninaliya
Nanyi hamuniulizi, kipi ninacoliliya
Ni kama donda mapenzi, leo nawaelezeya
Waweza funga pumzi, kuzimu ukaingiya
Wala hayana mjunzi, yoyote humuelemeya
Nimempenda fulani, jina sitowatajiya
Alikuwa msikizi, kila ninalomwambiya
Alikuwa mtimizi, yote nilohitajiya
Kiitikio
Mapenzi ni kama donda
Yaingiapo moyoni
Nimechoka vumiliya
Leo nawapasuliya.
Mwimbaji: Shakila Said
36
7. KIFO CHA MAHABA
Kifo cha mahaba, ni cha idhilali
Hakina haiba, wala afadhali
Bali tajikaba, nifilie mbali
Kufa kwa mahaba, nia adhabu kali
Leo ni msiba, usio mithali
Kesho ni adhaba, mbele ya jalali
Ewe mahabuba, niepushe hili
Niwewe twabiba, hapana wa pili
Hapanda jaziba, tajiua kweli
Mwimbaji: Shakila Said
8 NENDA UTAKAKO
Nenda utakaponenda nenda hujazuiliwax2
Japokua nakupenda kwa hilo siyoumbuax2
Katu mm sitojali zako inda ulichoweka chuku
Kwapwani sitokuganda kwako nikajizuzua
Wapowengi mdhubuti mapenzi wanoyajuax2
Wanaopend kwa dhati wenyehdhi namurua
Kamwe sijiombei umauti kwa wewe sitojiuwa
Name nishajidhatiti lolote utoamuwa
Unavuma nje wavuma kipanga waallahi sikukutambua
Unataka sikuyapinga ari pia ilikuwa
Kama mboni yamachoni nnavokuenga mamlaka yote umepewa
Kumbe vile ni mjinga hujui kusaminia
Nalia na moyo wangu weweulonisumbua
Kwakukwachia pendo langu si ila yangukuchungua
37
Tena nenda niko radhi roho yangu wala sitolaumiwa
Katambe na ulimwengu mimi hutonikomoa
KIITIKIO
Nenda utakako mwanakwenda usojua kupenda
Baki hukohuko ewe nunda ucnitoeroho bure
Pendo halitaki pupa nakwambia ukijua
Mara moja hukutupa watu wasikutambue
Daima asosikia madhila kujitakia
Tena wala usirudi tena nenda nakusabiliya
Endelea nawako ujana mwisho utajijutia
Na Yule ng‟ombe nimchezeeeee
4.4 Sababu za Kutunga Nyimbo Za Huzuni
4.4.1 Usaliti
Huzuni yeyote kwa binadamu huwa na sababu. Ukiacha sababu ya kimaumbile kama
kifo, nyingi ya sababu ni matendo ya mtu kwa mwengine. Usaliti lina asili ya neno
„salata‟ yenye maana usaliti au ujeuri. Usaliti katika mapenzi ni tendo la
kumdanganya mpenzi wake mtu. Usaliti ni ile hali ya mtu kutojiaminisha kwa
mwenza au kumwendea kinyume juu ya mambo ambayo hayatakiwi kufanyiana
katika maisha. Usaliti hujitokeza katika maisha ya kila siku kutokana na matendo na
vituko tofauti. Tuone aina ya usaliti na aina ya watu wanaosalitiana. Mwenye
kusalitiwa hukumbwa na simanzi na huzuni.
4.4.1.1 Usaliti wa mume na mke
Usaliti wa mume na mke katika jamii zetu siyo jambo geni katika macho na masikio
ya watu wanaoishi katika jamii. Huyaona matukio haya kila mara katika maisha yao
38
ya kila siku. Usaliti sasa umezoeleka sana katika jamii zetu. Wakati mwengine usaliti
humtarajii mtu kwendea kinyume na mambo ambayo wahusika wamekubaliana
katika masuala ya biashara au siasa. Katika familia, mume au mke huweza kufanya
kitendo cha ndoa nje ya ndoa huu nao usaliti. Hali hii hupelekea kuzuka kwa
migogoro na mitafaruku katika ndoa. Yote haya hujiri kutokana na mmoja kati ya
wapenzi wawili au wote wawili kukosa uaminifu kwa mwenziwe katika maisha yao
ya kila siku. Mshairi na mwimbaji mmoja aliyefikwa na masaibu hayo ametunga
wimbo wa “Nenda Utakako”kuelezea yaliyomkuta.Moja ya beti ya shairi lake
anamruhusu mpenzi ende atakako kisa amesalitiwa. Hata hivyo, anakiri kuwa bado
anampenda sana mpenzi wake hivyo lakini anashindwa kuvumilia inda zake.Wimbo
huu ndani yake unaonesha jinsi ya usaliti ulivyojitokeza kwake. Naye Fatma anatoa
dukuduku lake;
Nenda nenda utakapo nenda nenda hujazuiliwa
Japo kuwa nakupendakwa hilo sitoumbuwa
Katu mimi sitojali zako inda ulichoweka chukuwa
Kwapani sitokuganda kwako nikajizuzuwa
Hali hii ya usaliti wa kimapenzi inajitokeza pia kwa msanii mwengine. Si mwengine
ila ni Shakila katika wimbo wake wa “Mapenzi Yamepungua”. Shairi linasema;
Ulipokuwa na pendo Naikawa twapendana
Hukuwa navyo vishindo Wala hatukupigana
Umebadilika mwendo Ni kheri tukaachana
Duniani wengi wapo Wapenzi kila namna
Ulidhani peke yakoUzuri unapitana
Sina haja pendo lako Dunia hii pana
39
Beti zote hizo mbili zinaonesha jinsi mmoja ya mpenzi anavyoweza kubadili
mwenendo wake wa kuwa na mwengine kwa kificho. Shairi la pili linaonesha kuwa
hapo awali Shakila alikuwa na mume ambaye alimkinai, alimuamini na alimpenda
sana. Awali ya pendo lao mume hakuwa na visa na hawakudiriki kupigana. Shakila
anaamini kuwa katika dunia hii wapo wengi awezaye kumpenda na hayupo yeye
pekee yake. Wazuri kupita mpenzi wake wa zamani pia wapo. Dunia ina nafasi
atapata mwengine ampendaye. Katika muktadha huu usaliti kati ya mume na mke ni
jambo ambalo limeenea duniani kote hasa katika wakati huu wa maendeleo ya
sayansi na teknolojia na utandawazi. Matokeo ya hayo yote ni muhusika kukumbwa
na huzuni na majonzi kama ile iliyooneshwa na washairi na waimbaji wa nyimbo
Nenda Utakako na Mapenzi Yamepungua.
4.4.2 Msiba
Msiba ni ile hali ya mtu kuondokewa na mwenza wake au mtu wake wa karibu sana.
Hali hii ikijitokeza, mwanadamu hawezi kuizuia.Mungu huwa tayari ameshalipanga
limtokezee mja wake. Kuondokewa na mpendwa wake kwa kuaga dunia moyo
hujawa na huzuni na simanzi ambazo ni vigumu kuizuia.Wimbo wa “Mapenzi ni
kama Donda”ulioimbwa na Shakila ni wimbo unaonesha ni kwa jinsi gani Shakila
alivyoumia baada ya mumewe kufikwa na mauti na kumuacha yeye akiwa mpweke
mwenye simanzi katika maisha yake. Shairi laomboleza;
Ni kamadonda mapenzi leo nawaelezea
Waweza funga pumzikuzimu ukaingia
Wala hayana mjuzi yoyote humuelemea
Hapa mshairi ametumia jazanda ya donda katika wimbo wake kufananisha ni kwa
jinsi gani anavyoumia ndani ya mtima wake baada ya kuondokewa na mumewe
ambaye amemzoea na aliyekuwa akimtumikia na kumtunza katika shida zake zote.
40
Jazanda ya dondani jeraha kubwa ambalo huleta maumivu makali katika mwili.
Jeraha huleta homa na wakati mwengine husababisha mauti lisipotibiwa. Pia msanii
ametumia jazanda ya kuzimu pahala kunakoaminiwa hukaa watu waliokufa. Yeye
kumfika msiba huo anajiona mwenye kuzibwa pumzi na huenda donda la mapenzi
humfikisha yeye huko. Kutokana na hali hiyo, msanii ametumia jazanda hiyo
kuonesha uchungu, simanzi na jitimai kutoka katika sakafu ya moyo wake pale
anapomkumbuka mume wake ambaye hayupo katika ulimwengu huu na hutamwona
tena. Muziki wa taarab umetumika hapa kama daraja ya kuiwasilisha huzuni za
muathirika kwa umma.
4.4.3 Maliwazo na Ufariji
Imebainika kuwa baadhi ya wasikilizaji wanapozisikiliza nyimbo za taarab za asilia
zenye maudhui ya huzuni na majonzi nao wao huguswa kwa hisia nzito kutokana na
kukumbuka hali ambayo hata wao imewakuta. Mmoja ya washabiki wa nyimbo hizi
zikiwemo nyimbo za mwimbaji Fatma anasema, anapozisikia nyimbo za huzuni
hukumbuka mambo ambayo yanayowasibu watu kadhaa katika jamii yake.
Anaposikiliza nyimbo hizo wakati mwengine hujikuta anatokwa na machozi kama
vile yeye ndiye yaliyomfika masahibu ndani ya moyo wake. Nyimbo
inayomuhuzunisha zaidi ni ile isemayo Haya Maumbile Yanguiliyoimbwa na
kutungwa naFatmaIssa. Kutokana na muziki wake, mashairi yake na hata uimbaji
wake wenye naghama basi hujikuta mshabiki huyu Fatma Ali ni mateka.
Hububujikwa na machozi bila ya kujijuwa. Beti zifuatazo za shairi lake limejaa hisia,
simanzi na sonono;
Ubinafsinachoyo nyoyoni vyawasumbua
Kutwa kazi yenu hiyo imewajaa shakawa
Kwangu yepi muonayo mageni msoyayajuwa
Kufanya niyapendayo kwangu koslimekuwa
41
Hili haliwezekani na wala halitokuwa
Leo nakuelezeni muachkunichunguwa
Msijitie shidani haya nimejaaliwa
Kwani hasa jambo gani mie lakulaumiwa
Wapo walonihasimu wengi nathamani kunitowa
Nawambia msikie msiofahamikiwa
Fedhehani msingie kukaa kujisumbuwa
Lilobaki mnachie sitaki kulaumiwa
Haya Maumbile Yanguni nyimbo iliyotungwa, kuweka sauti na kuimbwa na Fatma
Issa. Nyimbo hii huwahuzunisha na kuwasikitisha watu wengi kutokana na mlio wa
vinanda unavyoyayatika na tungo ya mashairi yake yanavyosisimuwa. Mwimbaji
anawatolea uvivu waivu na mahasimu wake kwa kuwapasha kinagaubaga.
Anawalaumu kwa ubinafsi wao na choyo na hufika kumchukia.Fatma anahoji
walimwengu kuwa hayo anayoyatenda kwa kupenda mwenyewe imekuwa kosa?
Halikuwahi kutendwa? Kwa kuwa hayo ni majaaliwa yake kwanini atolewe thamani
na kuhasimiwa na kulaumiwa na wenzake? Hataki kulaumiwa, aachwe! Fundo la
moyo lenye masikitiko linalobainishwa kupitia beti za nyimbo ya taarab.
4.4.4 Choyo na Husuda
Nyimbo nyingi za taarab kwa kawaida zikiwemo za huzuni hutungwa kutokana na
matakwa ya mtunzi mwenyewe binafsi. Hata hivyo hutokea washairi kuombwa
kuwatungia wengine lakini baada ya nyimbo kutungwa huwa ya wote. Msanii
huimba nyimbo kwa kuiweka tayari jamii, kuitia hamu na kwamba mtu yeyote
anaweza kuihusisha na jambo lililomsibu. Hivyo, msanii huichora taswira ya huzuni
ili kuitaka hadhira imuunge mkono. Hali ya choyo na husuda inamwathiri mwimbaji
na mshairi Fatma. Choyo ni ubahili na ni roho mbaya ambayo mja huijenga ndani ya
42
nafsi yake dhidi ya mwengine. Husda ni kijicho ambacho mtu huonesha kwa
kumwonea gere mwengine. Yote mawili haya, hatimaye huleta madhara kwa
mlengwa husika. Utafiti huu uliohusisha na nyimbo za taarab asilia zinazoimbwa
zimeenda sambamba na matukio ambayo yanakumba jamii katika suala hili la choyo
na husda. Mara nyingi choyo na husuda husababisha madhara kwa wanajamii
ikihusisha mitafaruku na migogoro. Fatma, mtunzi na mwimbaji, akiwa mtunzi
amebainisha kuwa baadhi ya wasanii wenzake wanamwonea choyo na kuwa na
husuda kutokana na kipaji chake cha kuimba ambacho yeye anaamini kuwa
amejaaliwa na Mola wake. Mara kadhaa wasanii wenzake hukaa vipembeni
kumsema na kumkebehi na hata kumfitinisha kwa mkuu wake wa kazi. Kadhia hiyo
ndiyo iliyomfanya atunge wimbo waAsokasoro Hakuna.Wimbo huo unasema;
Kile kilonichukiza maovu kunikataza
Ikiwa nnapotea wajibu kuniongoza
Wala sioni vibaya mimi kunielekeza
Kinachonipa udhia ni kule kuniapiza
Asokasoro hakuna aloumbwa na muweza
Mwaenye lile hili hana ndio shani yake azza
Tabia kutolingana sijambo la kushangaza
Kinachonikera sana nisonalo kupakaza
Kunisema sichukui
Kusengenya haifai
Ni hekima njema rai
Kunionya sikatai
43
Hizi ni baadhi ya beti ambazo zinaonesha jinsi gani msanii anavyochukizwa na suala
zima la husuda na choyo ambacho watribu wenzake humfanyia kwa lengo la
kutimiza ubaya wao. Mwimbaji analalamikia waovu wake na wale wanaomwonea
choyo na kumwekea husuda. Anaamini kuwa yeye kama binadamu si mkamilifu
hakosi ila wala kasoro. Hata hivyo, anawanyooshea kidole wenzake kuwa hata wao
hawakosi ila, hivyo anakataa kusengenywa lakini anakubali kuonywa. Anachukizwa
na kuapizwa, kusingiziwa yaso ya ukweli lakini yuradhi kukatazwa maovu na
kuelekezwa. Muziki wa taarab umemsaidia mtunzi na mwimbaji kwa huzuni kutoa
dukuduku lake.
4.4.5 Ufitini na uchongezi
Fitina na kuchongeana, ni ile hali ya kuchonganisha watu au kufanya wasielewane.
Mara nyingi fitina hutokea pale neema ikimfika mtu mmoja na yule anayekosa
hufitini. Katika jamii za Waswahili fitina hujichomoza katika masuala tofauti ya
kijamii. Kwa mfano, mwanamke anapojaaliwa kupata mume, watu wa karibu wa
yule mume au mke hutia fitina kwa kumzulia maovu ambayo kwayo yana lengo la
kufitinisha kwa kutotaka afanikiwe katika ndoa yake. Hata katika sehemu za kazi
napo huzuka fitina ambazo mara nyingi huathiri shughuli za kazi. Ingawa jambo la
kutiliana fitina limezoeleka katika mitaa, vijiji na ndani ya jamii zetu, lakini jambo
hili pia hujitokeza katika vikundi vya sanaa. Mfano bayana na hai umemtokea msanii
Fatma. Nyimbo ya Fitina iliyoimbwa na Fatma inaonesha jinsi gani watu
wanavyotiliana chonza na fitina kati yake na mpenziwe. Mashairi anaeleza chimbuko
la fitina hiyo;
Chanzo chake hata tukazoeana
Kufika kunipa vyakekwa moyo bila khiyana
44
Wasiwasi sina kwake napokea kwa mapana
Dhamira na lengo lake kuja kutia fitina
Sema namshasema khabari tunapeana
Za ulimwengu mzima mengi tunaaambizana
Kumbe nia kunichuma anielewe bayana
Karudi kiguu nyuma kenda kuzusha fitina
Kitu kilichonipoza ni kule kumshiba sana
Bila ya kumchunguza tukawa tumevaana
Yale yanayotutaza kukaa kuelezana
Mwisho wake yake jazauhasidinafitina
Hizi ni baadhi ya beti ambazo zinaonesha jinsi gani utiliaji wa fitina ulivyoshamiri na
kuota mizizi dhidi ya mshairi. Msanii anaonesha alivyokuwa naye mpenzi wake wa
karibu na ambaye wamekinaiana na kushibana na kupeana yale ya moyoni. Pia,
amefadhiliwa kwa mengi hata amekuja kubaini kuwa alikuwa akimchuma na
akimwendea kinyume kwa kuyasema yao ya siri kwa wengine. Lililomponza ni kule
kumuamini bila ya kiasi na kuacha kumchunguza. Malipo yake ni kumuhasidi na
kumfitini. Fitina na choyo aliyofanyiwa na wenzake imeibua simanzi kubwa kwake.
Hali hiyo imeifanya nyimbo hii iwe ya huzuni.
4.4.6 Huzuni na hali halisi ya maisha
Utafiti huu umebaini kuwa, wapo baadhi ya watu ambao walisikiliza nyimbo hizi za
huzuni hapo zamani na bila ya kutambua nyimbo hizi zina mchango katika jamii.
Watu hawa walikuwa wamezoweya kusikiliza nyimbo za furaha pekee. Hii ni
kwasababu na kuwa jambo ambalo linazungumziwa la huzuni huwa halijamgusa bali
akisikiliza nyimbo kwa lengo la kujiburudisha tu. Bwana Ali wa skuli ya Nyuki
45
4anasema kuwa hapo zamani nyimbo za huzuni alikuwa hazitilii manani sana
kwasbabu alikuwa anamwona mwimbaji ni mtu mwenye kusikitika tu kwa hiyo hapo
kwake yeye hakuona faida yoyote ya hizi nyimbo. Lakini kwa kadri siku
zilivyoendelea kusonga mbele na yeye binafsi kukabiliwa na matatizo mbalimbali
katika jamii ndipo anapojenga taswira kuwa kumbe nyimbo hizi zilikuwa zikionesha
hali halisi ya maisha ya mwanadamu. Akitolea mfano nyimbo ya Asokasoro
Hakunani wimbo ambao umeimbwa zamani lakini kwasasa ndiyo wimbo anauelewa
lengo na dhamira yake katika jamii. Hivyo, kutokana na hali hiyo mtafiti amebaini
kuwa nyimbo za huzuni huweka kumbukumbu akilini mwa msikilizaji. Asokasoroni
wimbo uliotungwa na kuimbwa na Fatma ambao mashairi yake humkumbusha Ali
vitu vingi ambavyo hapo awali hakuvitambua. Baadhi ya beti za nyimbo zinasema
hivi;
Wala sioni vibaya mimi kunielekeza
Kinachonipa udhia ni kule kuniapiza
Asokasoro hakuna aloumbwa na muweza
Mwaenye lile hili hana ndio shani yake azza
Tabia kutolingana sijambo la kushangaza
Kinachonikera sana nisonalo kupakaza
Kunisema sichukui
Kusengenya haifai
Ni hekima njema rai
Kunionya sikatai
4 Ali Khatib ni mwalimu wa skuli ya nyuki niliyezungumza naye tarehe 22/4/2016
46
Wimbo huu anapousikiliza humkumbusha mbali sana na kwa kuwajuwa
walimwengu walivyokuwa na tabia ya kusengenyana na kupakaza uovu ambao hata
wakati mwingine haupo katika ulimwengu huu. Hivyo, mwimbaji anadhihirisha
huzuni zake kwa kusema kuwa si jambo jema kukaa na kuanza kumsengenya na
kumsema, jambo la msingi ni kukaa na kumwita na kumuonya kwa mambo yote
ambayo mja anahisi kuwa si mazuri na hiyo ndiyo itakuwa ni njema. Nadharia ya
uhalisia meakisi utafiti huu kwa msingi wake wa umhakati kwa kusadifiana na
maisha ya kila siku ya jamii, kwani masuala ya kuoneana choyo, kusengenyana
yametawala jamii zetu kiasi ambacho wasanii hutumia kalamu zao kuionya jamii juu
ya matendo hayo maovu.
4.4.7 Huzuni na majuto
Nyimbo za huzuni zinapotungwa na wasanii hutunga baada ya wao kutendewa
ghiliba ambazo nyingine huwa za kimapenzi. Wengine hukata tamaa ya kuwa na
mpenzi huyo tena. Shakila katika wimbo wake waAkukatae Hakwambii Toka, yeye
mwenyewe akiwa mwimbaji amebainisha jinsi gani anavyoonesha majuto juu ya
yule ambaye alikuwa akimpenda kwa dhati katika maisha yake. Hata hivyo, mpenzi
huyo hakuonesha mapenzi ya dhati kwake. Hali hiyo ilimpelekea Shakila kuwa na
majuto ndani ya moyo wake. Mwimbaji anaamini kuwa huyu mpenzi wake
anamfanyia vitimbi vinavyoonesha kuwa amemchoka na vinaashiria kumkataa. Hata
hivyo linalobainika ni kuwa hamwambii waziwazi kama hamtaki bali humfanyia
ishara, vitendo na vituko vya kumkataa. Shakila analalamika kwa kuimba;
Nipendekwa dhati au nikataye
Usinidhihaki la kweli nambiye
Kama hunitaki kheri nituliye
Kheri nituliye kama hunitaki kheri nitulie
47
Katika ubeti huu anaonesha jinsi gani mpenzi wake alivyokuwa hamjali na
hamthamini katika maisha yake. Hivyo, msanii Shakila anaamuwa kubadilisha nia
yake na kuaamua bora abaki peke yake kuliko kumng‟ang‟ania mtu ambaye hana
habari naye. Mwimbaji anampa masharti mpenzi wake kuwa ampende kikweli na
kwa dhati kama hawezi amwambiye waziwazi kama hamtaki na asimdhihaki.
Mwimbaji Fatma kwa upande wake na kwasababu ya mashaka kama hayo na yeye
ameamua katika nyimbo nyengine anaonesha majuto yake kwa mpenzi wake ambaye
alimthamini na kumsabilia hapo awali kila kitu katika maisha yake. Lakini
mwishowe huyu mpenzi alimfanyia vituko ambavyo hakuvitegemea. Mpenzi wake
huyo alikuwa akibadilisha wanawake wa kila aina. Ndipo hapo Fatma aliposhindwa
kuvumilia akaamua atunge na aimbe yeye mwenyewe nyimbo ya Nenda
Utakapo.Wimbo huu unaonesha jinsi ya mume asivyothamini mapenzi ya mke
ambaye anampenda. Kwa machungu na huzuni tele, Fatma anaghani;
Unavuma mja wavuma kipanga wallahi sikukutambuwa
Unayataka sikupinga maridhiya nilikuwa
Kama mboni ya macho nnavyokuenga mamlaka yote umepewa
Kumbe vile nimjinga hujui kuthaminiwa
Nalia na moyo wangu wewe ulonisumbuwa
Kukwachia pendo langu si ila yangu kuchunguwa
Tena nenda niko radhi roho yangu wala sitolaumiwa
Katambe na ulimwengu mimi hutonikomowa
Beti hizi mbili zinaonesha jinsi msanii anavyoujitia moyo wake kwa kumpenda mtu
ambaye hana utu wala uungwana. Mwimbaji ameonesha huzuni zake kwa
kumfananaisha mpenzi wake na ukwere wa kipanga ndege apendaye kunyaka
vifaranga vya kuku sawa na “wasichana”. Alimridhia kwa kila kitu na kumuenzi
48
kama mboni ya macho yake. Alimsabilia kila kitu chake, kwa kufanya hivyo
alimwona mjinga. Kwa vituko hivyo yupo tayari kuachana naye ili atambe na
wanawake wengine waliojaa ulimwenguni.
4.4.8 Huzuni na bahati
Licha ya kila mtu katika jamii kujaribu kufanya mengi sana yenye kupendeza na
kuleta tija lakini watatokea watu wachache tu watakaosifu na kukujali lakini kwa
wengine watakudhihaki na kukudharau. Na wakati mwengine mtu hata afanye kitu
kizuri cha namna gani, hakitathaminiwa, badala yake atachukiza na kubandikwa ila
katika jamii husika. Yote haya yanajiri kwasababu ya mtu kukosa bahati katika jamii.
Utafiti huu umebaini kuwa nyimbo ambazo Fatma amezitunga na kuziimba yeye
mwenyewe zimejikita katika kumkosesha bahati. Jambo hili amelidhihirisha katika
mahojiano kati ya msanii huyu na matafiti huko nyumbani kwake (tarehe
22/11/2015) mtaa wa Kwa Alamsha Zanzibar. Alieleza kuwa yeye binafsi ni mtu
ambaye hana bahati hata kidogo kwani kila kikundi anachojiunga nacho huzuka
migogoro katika kipindi kifupi tu anapokaa katika kikundi hicho. Kwa matokeo hayo
ndipo yeye alipojiaminisha kuwa yeye hana bahati ya kupendwa na wasanii
wenzake. Yeye anaamini kinachomponza ni kipaji chake cha kuimba. Hali hii ndiyo
inayompa hamu na shauku ya kutunga nyimbo nyingi yeye mwenyewe binafsi.
Yawezekana ukosefu wa bahati kama huo upo kwa watu wengine. Kwake yeye hili
limepalilia kipaji chake. Wimbo waSijali Kuchukiwa, uliotungwa na yeye Fatma
ambao unaonesha jinsi ambavyo Fatma anavyochukiwa na watribu wenzake. Ingawa
yeye anajitahidi kukaa nao kwa wema na hisani, haiwi nusura kwake ya kupata
bahati. Fatma kwa huzuni analalama;
Sitoyalipiza katu hayo unayonitendea
Kuvumiliya si kitu mitihani ya duniya
49
Ninange kwa kila mtu na ubaya kunitiya
Kitachokulipa ni utu uovu sitokufanyia
Kinyume siendi siendi kuntu hata ukinichukiya
Rohoni mwangu siweki kitu japo nishayazoeya
Kama nimekukosea mie yailahi ndiye hakimu
Na kama unanioneya ni yeye atohukumu
Hukumu hukumu hakimu hukumu
Ongeza kunifisidi kwa kisa na kila mambo
Tukana niite hasidi ukioniona vikumbo
Kustahmili nazidi subira ndo zangu nyimbo
Japo wanikera hadi sitokujibu kwa fumbo
Madhali Mungu shahidi kwako siongezi jambo
Hakimu wa haki wadudi yatakwisha majigambo
Bahati yangu miye kwa binaadamu mbaya
Hata niwafanyie nini kwa binaadamu mbaya
Ni wabebe mgongoni kwa binaadamu mbaya
Ni wape cha mvunguni kwa binaadamu mbaya
Hawana shukurani
Hizi ni beti ambazo Fatma anaonesha jinsi alivyokuwa hana bahati kwa wenzake.
Kila kukicha wenzake humsakama na kumsema vibaya katika jamii. Mwimbaji
analidhihirisha hili pale anaposema kuwa hatolipiza kisasi abadani kwa ubaya wote
ambao wenzake wanayomfanyia. Wala rohoni mwake yeye haweki fundo kwani
yote hayo ameshayazowea kumfika katika ulimwengu na kwake hakuna geni hata
moja. Anaamini kuwa yote hayo ni miongoni mwa mitihani tu ya duniya. Anaendela
kulalamika kuwa hata afanye hisani na awabebe mgongoni basi malipo yake ni
50
majungu tu na fitina. Yeye anamwachia Mungu amlipiye na yeye atazidi kuvuta
subira.
4.5 Dhamira ya Huzuni katika Nyimbo za taarab na tija zake
Katika kulijadili suala hili wahojiwa wengi wametoa maoni tofauti.Wahojiwa wapo
kutoka makundi tofauti. Wapo wale watangazaji wa vipindi vya redio za taarab asilia
na walimu wa somo la Fasihi.
4.5.1 Kupanua dhana ya Taarab
Sanaa ya fasihi kwa kiasi kikubwa imetajirika kutokana na muziki huu wa taarab
kukua na hasa katika kipengele cha dhana ya taarab ya asili kuwa taarab ni furaha.
Kiasili nyimbo zilizotungwa zilikuwa ni za furaha tu na zilikuwa zikitungwa kwa
madhumuni ya kustarehesha watawala. Miaka nenda miaka rudi, taarab imekua na
kubeba maudhui ya furaha, ramsa, huzuni na majonzi. Kutokana na hali hiyo,
wasanii wamepata uhuru wa kutunga nyimbo zenye maudhui wanayoyataka wao
wenyewe na kuanzia hapo ziliibuka nyimbo za huzuni katika jamii zetu. Nyimbo
hizo za huzuni zimeonesha matatizo mbalimbali ya kijamii yenye kuhusisha na
mambo mengine ya majonzi, jitimai na simanzi.
4.5.2 Kuelimisha
Wapo wahojiwa wanaoamini kuwa nyimbo zenye kubeba maudhui ya huzuni huwa
zinaelimisha jamii kwa kiasi kikubwa sana. Hawa huamini kuwa msanii
anapoiwasilisha nyimbo yake, jamii hupata ujumbe na sababu la tokeo lenyewe.
Kupitia dhamira za nyimbo hizi jamii hupata uelewa wa matukio na sababu zake.
Hivyo, kupitia nyimbo hizi jamii huweza kuepukana kwa namna moja ama nyengine
na mambo maovu ambayo yapo kinyume na silka na tamaduni za Waswahili. Jamii
hufunzwa kuepukana na husuda, choyo na fitina. Usaliti wa kimapenzi unaobebwa
51
na chuki zisizo na msingi, huweza kuepukwa. Haya hujiri kutoka na na nyimbo
ambazo zinaimbwa kwakuwa zinatoa elimu juu ya athari ya mambo hayo ambayo
hayapendezi katika jamii. Hivyo, ingawa nyimbo hizo hutungwa kuelezea masahibu
yaliyomfika mtu lakini pia huelimisha jamii kuachana na mambo hayo yasiyo na
msingi katika jamii. Tunaona nyimbo Mapenzi Yamepungua, msanii amefaulu
kuonesha mume ambaye haijali ndoa yake na aendaye kinyume na mkewe. Kupitia
nyimbo hii, jamii inaelimika kuwa makini katika ndoa na kuachana na mambo
ambayo hayaleti faida yoyote katika maisha yenu.
4.5.3 Kuliwaza
Kupitia nyimbo za huzuni wanajamii wanaliwazika kutokana na mashairi, vinanda
vinavyotumika na sauti ya mwimbaji ya masikitiko kupitia nyimbo hizo. Nyimbo
nyingine za taarab ni za mahadhi na mashairi ya majonzi, ziimbwapo huleta huzuni
kwa jamii na iimbwapo huleta faraja. Faraja huwapa nguvu kutekeleza majukumu
kwani mashairi ya nyimbo hizo huzungumzia matatizo yanayoikumba jamii yao. Bw.
Ali Nahoda wa Coconut FM na Bi.Fatma Mohamed wa Zenji FM wote hao ni
watangazaji wa vipindi vya taarab asilia wao wanapozisikiliza nyimbo za huzuni
hasa nyimbo ya Fatma Issa ya Asokasoro Hakuna nyoyo zao wenyewe huliwazika
kwani katika nyimbo hiyo mwimbaji na mtungaji huyu amegusia hali halisi ya
maisha. Moja ya beti ya kibwagizo cha nyimbo hiyo kinasema;
Kunisema sichukuwi
Kusengenya haifai
Ni hekima njema rai
Kunionya sikatai
52
Hapa Fatma anaiasa jamii yake kuwa mtu anapofanya kosa ni vizuri kumwita na
kumwambia kwa njia ya hekima kabisa bila ya kukaa vipembeni na kumsengenya
kwa maneno mabaya. Kupitia beti hii, wote Bw. Ali na Bi. Fatma, 5wameridhika
kwa maoni yake anavyoielekeza na kushauri namna bora ya kuishi bila ya kuoneana
choyo na kusengenyana.
4.5.4 Kuzindua
Miongoni mwa dhamira ya nyimbo za huzuni ni kuizindua jamii kwa yale mambo
ambayo yametendwa kwa siri na ambayo hayajulikani. Wahojiwa katika utafiti huu
wamesema kuwa kupitia nyimbo za huzuni jamii hupata kuyajuwa na kuelewa
mambo tofauti ambayo yapo kinyume na utamaduni, silka na desturi za maisha.
Mambo hayo yanayosababishwa na udhaifu wa binaadamu uliomo ndani ya moyo
wake. Ili jamii iondokane na tabia hizo ziendazo kinyume na desturi na mwenendo
mwema wa jamii, nyimbo hizi hubainika kuwa ni funzo. Hivyo basi, jamii inaposikia
jambo hilo mwimbaji ameliimbiya, watu hutanabahi na kuliona kosa na kupata
uelewa. Mfano mzuri ni wa nyimbo ya Kheri Adui Shetani Kama Adui Kiumbe
ambayo msanii anaonesha kuwa bora mwanadamu kuwa na uadui tena bila ya
kificho na shetani kuliko na mwanadamu mwenzake katika dunia. Kiumbe huyu
mwanadamu akikusudia lake hufanya kila mbinu ili amtiye ubayani mtu ili apate
achukize katika jamii. Likifanikiwa hili ataridhika na kufurahia kuona kiumbe
mwenziwe anateseka, kudhalilika na anaadhirika katika ulimwengu huu.
5 Fatma Ali Mohd ni mtangazaji wa Zenji FM na Ali Nahoda ni mtangazaji wa Coconut FM
nilozungumza nao tarehe 22/4/2016 huko Mombasa na Migombani Zanzibar
53
4.5.5 Kurekebika tabia
Kupitia nyimbo za huzuni za taarab, jamii inapata manufaa makubwa kutokana na
kuwa nyimbo hizi huirekebisha jamii kwa kuona chimbuko la tatizo, athari na
matokeo yake na suluhisho. Nyimbo huweza kuifanya jamii ibadilike na kuachana na
mambo ambayo hayapaswi kufanywa na mwanadamu baada ya kuonekana madhara
yake. Nyimbo hizi hukemea husuda na mambo mengine yakiwemo choyo na maovu
mengine. Mfano wa nyimbo za huzuni ambazo zinashajiisha watu kutooneana choyo
na gere bali mtu afanye bidii ili aweze kufanikiwa na mambo yake ni kama vile;
Haya maumbile YangunaAsokasoro Hakuna nyimboiliotungwa na kuimbwa na
Fatma. Nyimbo ya aina hizi zinakataza tabia ya husuda na kuoneana maya na
humtaka mtu atafute njia mbadala ambayo itamwezesha kufanikiwa katika maisha
yake. Pia, kupitia wimbo waMapenzi Yamepunguaulioimbwa na kutungwa na
Shakila, mwimbaji anawasihi wawili wapendanao wawe na mapenzi ya kweli ili
waweze kupiga hatua za kimaendeleo katika jamii. Wasia unaotolewa ni kuwa si
busara wala si hekima mpenzi mmoja kumdanganya mpenzi mwingine.
4.5.6 Ujenzi wa hisia na huruma
Tumeona kuwa nyimbo hizi za huzuni za taarab jinsi zinavyoweza kuteka hisia za
huruma kwa wasikilizaji. Waimbaji wanapowasilisha kazi zao hudhihirishiwa tatizo
wanalolizungumzia mbele ya hadhira ambayo wao huliona kama ni la kwao. Hapo
ndipo mtu baada ya kusikia nyimbo inamjia huruma, majonzi na simanzi kwa
kumuhurumiya yule aliyepatwa na hilo tatizo akiamini mwimbaji mbele yake ndiye
muhanga. Kwa mfano Bw. Ali 6anasema kuwa anapoisikiliza nyimbo ya Mapenzi ni
Kama Donda moyo wake hupatwa na mshituko na majonzi na kumuhurumia mtu
6 Bwana Ali Haji wa skuli ya Faraja niliyezungumza naye tarehe 6/4/2016 huko skuli ya Sekondari
Faraja Zanzibar
54
huyu ambaye amefanyiwa ukatili ambao haustahili kufanyiwa mwanadamu.
Mwimbaji Shakila, kwa madaha, jinsi anavyonung‟unika katika nyimbo yake hii,
huuvaa uhusika wa muhanga na kujihisi kama yeye ndiye mwenye jeraha limtesalo
kimapenzi. Hivyo, kupitia nyimbo hizi za huzuni mtu hukumbuka matukio tofauti
ambayo labda yalimkuta yeye au mtu mwingine ambaye huleta simanzi na majonzi.
Kwa mtu anaposalitiwa kwa kawaida huwa ana majonzi ya muda mrefu ambayo kwa
mara moja hayawezi kusahaulika tena kwa muda mfupi. Kwa hiyo, mara anaposikia
nyimbo ambayo msanii naye amesalitiwa huliona lile tatizo lilomfika kuwa siyo la
peke yake bali ni humfika kila mtu ambaye bado anavuta pumzi katika ulimwengu
huu. Matokeo yake mtu huyo huliwazika na kujiona kuwa bado ni mtu duni na dunia
haijamtenga bali ipo pamoja naye. Hata hivyo kwa mtu ambaye pia hajapatwa na
tatizo kubwa, humuhurumia yule mtu ambaye amefikwa na tatizo, yeye humgusa
ndani ya moyo wake.
Kwa mfano, Amina tunamwona asemavyo kuwa anapoisikiliza nyimbo ya Fatma Isa
ya Asokasoro Hakuna hupatwa na simanzi kubwa ndani ya moyo wake na huamini
kuwa kweli mwanadamu hapendelei kuona mtu anapata neema yoyote katika dunia
bali hujipendelea yeye binafsi tu. Amina7 anaungama kuwa hata akiisikiliza nyimbo
ya Shakila ya Macho Yanacheka Moyo Unalia ambaye akivuta taswira ya viungo
viwili hivi vya macho na moyo “macho kuwa yanacheka na moyo unalia” ambavyo
havina uhai lakini vimepewa ubinaadamu na vina mvuto mkubwa na hisia kali katika
moyo. Nyimbo hii humuathiri sana yeye. Pamoja na hayo atharia ya uhalisia
inaonekana kusibu katika utafiti huu kwa kutumia msingi wa pili wa ushabihi ukweli
pale msanii anapovipa uhai vitu visivyo uhai na msikilizaji kuvipokea kwa hisia
7 Amina Ali ni mwalimu wa skuli ya Faraja ambaye nimezungumza naye tarehe 23/ 4 /2016 hapo
skuli ya Faraja Zanzibar
55
zinazokaribia ukweli. Kwa mfano anaposema „macho yanacheka‟ kiuhalisia si kweli
lakini kwa dhamira ya ndani utaona kuwa macho yanacheka.
4.5.7 Kuonesha ujasiri
Wahojiwa wengine katika utafiti huu wamebainisha kuwa miongoni mwa nyimbo za
huzuni, zaonesha ujasiri kwa upande mmoja na ukatili wa watu katika jamii kwa
upande wa pili. Mtu aliyetendwa uovu huweza kustahmili matukio ya kikatili
ambayo yanamkumba katika mazingira magumu. Hata hivyo, muathirika huyo
huchukua maamuzi magumu na ya kijasiri ya kumkwamuwa kutoka katika janga.
Kwa hivyo, msanii anapoimba nyimbo yake kuhusu masaibu yaliyomkuta huwa
anaitaka jamii kutonyongeka na mambo ambayo yaathiri maisha yao. Msikilizaji na
mtazamaji anatakiwa awe jasiri na shujaa wa kutoa maamuzi yanayostahiki ili kukata
minyororo ya kifungo ambacho hakina manufaa yoyote. Yashauriwa mtu
anapotendewa na mpenzi wake ubaya anapaswa afikiri njia mbadala ambayo itaweza
kumkwamuwa katika hali aliyonayo. Fatma, 8mwimbaji na mtunzi alipofikwa na
matatizo hayo alipata ujasiri wa kumfukuza mume ambaye alikuwa akimwendea
kinyume kila siku na hatimaye akaamua kuachana naye na kukaa peke yake bila
mpenzi. Baada ya kuona kuwa yeye yamemkuta mambo kama hayo na akaamini
kuwa hata katika jamii matukio kama hayo hayakosekani hivyo, akaamuwa kutunga
nyimbo ya Nenda Utakapo ili kuwahamasisha jamii kujenga ujasiri na kupiga moyo
konde.
8 Mazungumzo yangu na Fatma Issa tarehe 22/11/2015 nyumbani kwake Kwa Alamsha Zanzibar
56
4.6 Athari zinazopatika katika Nyimbo za Huzuni
Ama kwa hakika hakuna kitu hata kimoja katika ulimwengu huu kikakosa athari
katika jamii. Athari hizo zitatofautiana kutokana na mitazamo ya mtu binafsi na jamii
husika. Utafiti huu umegundua athari zifuatazo;
4.6.1 Athari Chanya
4.6.1.1 Kuifanya jamii kujua matatizo yake
Mara nyingi wanajamii hukumbwa na matatizo mbalimbali ambayo huwatweza
walio wengi. Msanii anapotunga nyimbo yake hufikiri kuwa lile tatizo
analoliwasilisha ni lake peke yake, ukweli ni kuwa wenye matatizo kama hayo wapo
wengi. Lakini pale nyimbo hiyo inavyotoka na kupokelewa watu wengine
hutanabahi kuwa tatizo lile siyo lake peke yake. Hubainika kumbe nyimbo hiyo
huwagusa wengi na huzuni hiyo hufikwa na masaibu au matatizo kama hayo watu
kadha wa kadha. Kwa mantiki hii nyimbo hubaki kuwa ni mali ya kila aipendaye.
4.6.1.2 Kufariji na kuliwaza
Kutokana na uhalisi wa matukio tofauti ambayo yanaikuta jamii na maafa
mbalimbali yanayotokea, nyimbo hizi huwafariji na kuliwaza watu ambao
wamekutwa na matatizo hayo katika jamii. Bila ya kupata faraja na maliwazo hayo
kutoka nyimbo hizi, baadhi ya watu wangebaki kulia na kuyayatika kwa kukosa
maliwazo. Hali ingetokea mwanadamu asingefanya shughuli zake za kimaendeleo na
dunia ingedumaa.
4.6.1.3 Kugusa nafsi ya msikilizaji
Mara nyingine mtu ambaye anasikiliza nyimbo ambayo tukio lake limemgusa hufikia
hatua ya kulia kwa kutokwa na machozi kutokana na uhalisi wa tukio husika. Kwa
mfano mtangazaji waZenji Bi Fatma Ali anasema kuwa mara nyingi anaposikiliza
57
nyimbo za Fatma hujikuta analia bila sababu kutokana na mashairi yake
yanavyomuingia ndani ya moyo wake na kuhisi kuwa lile tatizo analolizungumzia na
yeye linamhusu.
4.6.2 Athari hasi za Nyimbo za Huzuni
Katika kipengele hiki wapo wahojiwa ambao hawapati athari yoyote wanaposikiliza
nyimbo hizo bali wamesema kuwa hakuna athari yoyote wanayoipata, kwao nyimbo
hizo ni sehemu ya kupata burudani tu katika moyo wao. Kwa mfano Nahoda
mtangazaji waCoconut FM anasema kuwa anapozisikiliza nyimbo hizo huwa hapati
athari yoyote licha ya kuburudika tu ndani ya moyo wake na kuamini kuwa matukio
mabaya kama hayo siyo vizuri kufanyiana walimwengu.
4.6.3 Tofauti ya Fatma na Shakila
Ni ukweli usiopingika kuwa panapotokea wasanii stadi wawili wa uimbaji taarab
lazima zitakuwepo tofauti ambazo zinaweza kutofautisha kati ya mwimbaji mmoja
na mwengine. Jambo hili hutokea kwasababu ya vionjo mbalimbali vinavyotumika
katika kujenga kazi zao. Kwa kiasi kikubwa Fatma anaposimama jukwaani huteka
nyoyo za wengi pale anapowasilisha kazi yake jukwaani na mashairi ya nyimbo yake
hugusa moja kwa moja matukio ambayo yapo katika jamii. Vile vile vyombo vya
taarab vitumikavyo na ucharazaji wake vina utofauti mkubwa pale aimbapo Fatma.
Nyimbo zake hutumia vyombo vya asilia kama vile fidla, udi, qanuni na nai jambo
ambalo huufanya muziki uonekane wa kipekee na kiasilia zaidi.
Uimbaji wa Shakila ni tofauti kwani yeye nyimbo zake hutumia vyombo vya kisasa
kama vile gita, organ, accordion na kadhalika. Hivyo, kupitia utofauti huu wa
vinanda na mtindo wa muziki, uimbaji wa Fatma unaonekana kuwa ni bora kuliko
ule wa Shakila. Pia kuna tofauti nyingine kati ya uimbaji wa Fatma na Shakila,
58
kupitia suala zima la mitindo ya mahadhi ya nyimbo zao. Kwa mwimbaji Fatma,
anapoimba nyimbo zake husisimua nafsi ya hadhira yake kutokana na kuimba kwake
kwa naghama, masikitiko na huzuni kubwa. Hali hii huifanya hadhira ishiriki moja
kwa moja katika tukio la huzuni analolizungumzia. Shakila kwa upande wake,
nyimbo zake nyingi zimebeba maudhui ya mapenzi yasiyo na huzuni nzito. Lakini
Fatma nyimbo zake za mapenzi zinazungumzia matukio ya majonzi yanayoisibu
jamii. Fatma ameimba nyimbo zake katika hali mbili, za kumpenda mwenza wake na
maafa yaliyomkuta dhidi ya watribu wenzake waliokuwa hawampendi yeye apate
neema.
Amekuwa Fatma kama anavyoamini, akikosa bahati katika maisha yake. Anaamini
kuwa popote endapo na kushiriki sanaa hii ya taarab huwa hawapakosi fitina na
ubinafsi ambao husababishwa na wasanii wenzake katika kikundi chao. Yeye
anaamini inatokana na kipaji chake cha kuimba na kutunga nyimbo mbalimbali
zenye mvuto, na kwa hivyo, mafanikio yake wenzake hupatwa na choyo ambacho
inayoambatana na husuda. Yeye anaamini kuwa ustadi wake umemsababishia
madhara makubwa na sasa anayo itikadi kuwa, kwa vile anapoimba hukaa juu ya kiti
kutokana na maradhi ya miguu jambo analoliamini kuwa wenzake wamemfanyia
ushirikina. Kiumri Shakila ana umri wa miaka 69 na Fatma miaka 59. Wamepitana
kwa miaka kumi.
4.6.4 Mfanano wa Fatma na Shakila
Shakila na Fatma wote waimbaji na wote ni wanawake. Wote ni washairi na waweka
muziki katika nyimbo ingawa wote hawapigi chombo chochote. Wote ni waimbaji
wa taarabu asilia ambao huimba nyimbo zenye maudhui ya huzuni na pia huimba
nyimbo za furaha. Yawezekana hili ni sadfa pale mfumo wa maisha wa jamii ya
59
Tanga na Zanzibar kufanana kwani wote ni watu wa mwambao na pia ni Waisilamu.
Wote katika maisha wamekatishwa masomo yao ya shule ili waolewe. Wameolewa
wote na waume tofauti na kuzaa nao watoto wengi. Wote hivi sasa ni wajane na
maisha yao kiuchumi si mazuri. Wote wanaendelea na kuimba lakini nyota zao za
umaarufu zinafifia. Maumbo yao yakimbilia uzee na makunyuzi ya nyuso zao
zimepunguza haiba zao.
Tukihusisha matokeo ya utafiti huu na nadharia, ya uhalisia tutaona kwamba
nadharia hii jukwaani imesawiri yale yaliyomo katika utafiti huu kwani masaibu
yaliyowapata wasanii hawa ni mambo ambayo wanawake wengi yanawakuta katika
jamii zetu.
4.7 Hitimisho
Katika sura hii, matokeo ya utafiti yamewasilishwa na kuchambuliwa kulingana na
maswali ya utafiti. Maswali hayo yameakisi malengo ya utafiti yaliyokusudiwa.
Mjadala umegawanyika katika sehemu kuu tatu. Kwanza imechambuliwa sababu za
kutungwa kwa nyimbo za huzuni. Katika mjadala huo mtafiti ameonesha kuwa zipo
sababu mbali mbali ambazo zinazowasukuma wasanii hao kutunga nyimbo hizo.
Miongoni mwa sababu hizo ni matukio ambayo yanawakuta wasanii hao binafsi
katika harakati zao za kila siku. Pia, yapo matukio yatokanayo katika jamii ambayo
husababishwa kutungwa nyimbo. Sehemu ya pili imejadiliwa kwa kina dhamira za
nyimbo za huzuni pamoja na athari zake. Dhamira hizo ni kuelimisha, kuliwaza,
kuzindua, kurekebika tabia, ujenzi wa hisia na huruma na kuonesha ujasiri.Dhamira
mbalimbali ambazo zinakwenda sambamba na maisha halisi ya mwanadamu.
Sehemu ya tatu ya sura imeeleza jinsi washairi na waimbaji hawa walivyofanana na
kutofautiana kimaisha, kiumbaji na kitabia na kiwasifu.
60
SURA YA TANO
MUHTASARI, HITIMISHO NA MAPENDEKEZO
5.1 Utangulizi
Sura hii inawasilisha muhtasari na hitimisho la tasnifu hii. Kadhalika, sehemu hii
imetoa maoni kadhaa yaliyopatikana kutokana na utafiti huu. Aidha, sura hii
imeelezea jinsi nadharia ilivyosibu na kutoa mapendekezo kwa tafiti zijazo.
5.2 Muhtasari wa Tasnifu
Utafiti huu uliangalia juu ya nyimbo za huzuni za waimbaji Shakila na Fatma
ambayo ililifafanua nyimbo teule za huzuni za waimbaji hawa sababu, zilizopelekea
kutungwa kwa nyimbo hizo na tathmini juu ya jamii inavyozipokea nyimbo hizo za
huzuni.Tasnifu hii imegawika katika sura tano, ambapo kila sura imeeleza mawazo
yake makuu kwa muhtasari.
Sura ya kwanza imetoa mwelekeo wa tasnifu hii kwa kuanza na utangulizi, usuli wa
tatizo, tamko la utafiti, historia ya wasanii teule ambao ni Shakila na Fatma, malengo
ya utafiti, maswali ya utafiti na manufaa ya utafiti. Aidha, sura hii ilifafanua nadharia
iliyotumika katika utafiti huu ambayo niNadharia ya Uhalisia na misingi yake mikuu
ni msingi wa kimhakati na ushabihi ukweli.
Sura ya pili imefafanua maandiko yaendayo sambamba na utafiti huu. Sura hii
imeeleza maandiko mbalimbali yanayolandana na utafiti huu.Utafiti huu uliangalia
maandiko yanayofafanua chimbuko la taarab. Aidha, maandiko yahusuyo taarab
yaliangaliwa, na hatimaye utafiti huu ulionesha pengo la utafiti ambalo lilitoa
mwanya kwa mtafiti kuliziba pengo hilo.
Sura ya tatu imeeleza mbinu na vifaa vilivyotumika katika utafiti huu. Sura hii
inabainisha muongozo kamili wa utafiti ulivyokuwa, aina ya kundi lililohitajika kwa
ajili ya kutoa majawabu juu ya maswali ya utafiti pamoja namna data
61
zilivyokusanywa na kuchambuliwa kwa kuongozwa na nadharia iliyochaguliwa
ambayo ni nadharia ya uhalisia.
Sura ya nne imeonesha namna data zilivyowasilishwa na kutafsiriwa. Aidha,
malengo na maswali ya utafiti ambayo yalijibika na kugawika katika sehemu tatu
kuu. Kwanza, kuorodhesha baadhi ya nyimbo za huzuni za waimbaji wateule, pili
kubainisha sababu zilizopelekea kutungwa kwa nyimbo hizo, na kutathmini jamii
ilivyopokea nyimbo hizo za taarab na athari zake.
Sura ya tano inahusu hitimisho la utafiti huu kwa ujumla wake ikijengwa na
muhtasari wa kazi, matokeo ya utafiti, utoshelevu wa nadharia, pamoja na
mapendekezo juu ya tafiti zijazo.
5.3 Utoshelevu wa Nadharia Iliyotumika
Nadharia ya Uhalisia ndiyo iliyotumika katika kukusanya data na uchambuzi wake.
Nadharia hii imebeba mambo makuu mawili ambayo ni msingi wa kimhakati na
ushabihi ukweli. Msingi wa mwanzo, ni msingi wa kimhakati. Huu ni msingi ambao
husawiri matukio kama yalivyo katika jamii kwani tumeona ya kuwa nyimbo
ambazo zimetungwa huelezea matukio ambayo yanawafika wanajamii katika maisha
yao ya kila siku. Hivyo, nadharia hii imekwenda sambamba na matukio yote ambayo
yanamfika mwanadamu katika uhai wake. Msingi wa pili, ni ushabihi ukweli. Msingi
huu huelezea namna matukio yanavyokaribia kuelezea ukweli huo. Hivyo kutokana
na mnasaba huo tunaona kuwa nadharia hii ya Uhalisia imesawiri matukio yote
ambayo yanamtokezea mwanadamu katika maisha yake. Kwani mara nyingi msanii
anapotunga kazi yake huelezea ambayo yapo katika jamii, hivyo hata huzuni nayo
ipo katika jamii na huweza kumfika kila mtu iwe kwa siri au dhahiri.
62
5.4 Mambo Mapya Yanayoibuliwa na Tasnifu Hii
Mambo mapya yaliyomo katika tasnifu hii ni haya yafuatayo:
Dhana ya asili n maana ya taarab kuwa ni furaha na ramsa imepitwa na wakati.
Taarab sasa ni muziki wa furaha na huzuni.
Utafiti umebaini pia kuwa jamii inazichukulia nyimbo za huzuni katika mitazamo
tofauti. Wako wanaoangalia yaliyomo ndani ya nyimbo husika na kuyaakisi katika
mazingira halisi yalivyo katika maisha yetu ya kila siku kwa mfano usaliti, misiba,
choyo na ubinafsi. Na wapenzi wengi wa nyimbo za aina hii ni wale ambao
wameguswa na mikasa inayofanana na mashairi yaliyomo katika nyimbo hizi. Hata
hivyo katika nyimbo hizo wapo waliokuwa wanaoangalia sauti za waimbaji na
mtiririko wa vinanda kwa ajili ya kuburudika tu bila kuangalia maudhui ya ndani ya
nyimbo husika.
Pili, ni umahiri wa wasanii katika kuwasilisha hisia zao kwa kutumia vipaji viwili
kwa wakati mmoja, yaani kutunga na kuimba. Katika utafiti huu, msanii Bi Fatma
Issa anaoneka kutunga nyimbo kama vile ya Ubinafsi na Choyo na kuiimba
mwenyewe hii ni kutokana na kuguswa na majaribu ya waja moja kwa moja
yaliyokuwa yakimsibu kutoka kwa watu tofauti.
Mwisho, katika jambo la kusikitisha sana ni kuwa wasanii wote hawa wawili pamoja
na kutumia vipaji vyao kuelimisha na kuburudisha jamii bado kazi zao hii
hazikuwabadilisha maisha yao kuwa bora zaidi na kuziona thamani ya vipaji vyao.
5.5 Mapendekezo wa Tafiti Zijazo
Kukamilika kwa tasnifu hii haimaanishi ya kwamba ni mwiko kwa wengine kutafiti
katika kipengele hiki cha fasihi ikiwemo taarab. Hii ni kwa sababu utafiti huu
63
ulikuwa na malengo na mipaka yake. Hivyo, bado kuna maeneo kadhaa ambayo
yanatakiwa yafanyiwe kazi na watafiti wengine. Maeneo yanayopendekezwa ni:-
Mosi, katika muziki wa taarab kuna tofauti ya utungaji na uwasilishaji wa nyimbo za
taarab asilia na taarab ya kisasa, ni vyema kwa watafiti wajao kulinganisha na
kutofautisha uwasilishaji wa taarab hizi.
Pili, tukiangalia matokeo ya utafiti yalivyoonesha kubeba hadhi kubwaya wasanii
hawa lakini hatima yake maisha yao yalikuwa duni sana. Ipo haja ya kufanyiwa
utafiti wa kina juu ya sababu zinazopelekea wasanii hawa wakongwe wa muziki wa
taarab asilia kutonufaika na kazi yao.
Tatu, kiuhalisia imeonekana taarab asilia imepotea kwa kasi hivyo, ipo haja ya
kuchunguza sababu zilizopelekea wasanii wa taarab ya sasa kuhamia zaidi kwenye
taarab ya kisasa na kuiacha taarab asilia.
5.6 Maoni ya Mtafiti juu ya Utafiti Huu
Kutokana na matokeo ya utafiti huu napendekeza maoni yafuatayo kushughulikiwa
ili kuisaidia jamii:-
Mosi, kuwalazimisha wasanii wote wa taarab kujisajili katika haki miliki ili kuweza
kunufaika na kazi zao zinapotumika katika sehemu mbali mbali kama vile kwenye
kumbi za starehe, redio na televisheni ili wanufaike na kazi zao na ziwafaye sasa na
wanapostaafu shughuli hizo.
Pili, kuandaa makongamano yenye lengo la kujadili namna ya kuimarisha na
kurithisha kizazi kijacho sanaa ya taarab asilia kwenye utungaji na uwasilishaji na
wakati huo huo taarab ya kisasa iimarishwe zote, kwani zina umuhimu kwa jamii.
64
MAREJELEO
Alawiy, Z. (2007), “Nyimbo za Mafumbo za Taarab zinavyochangia kudumisha
maadili yajamii ya wazanzibar”, Ripoti ya utafiti kwa ajili ya Shahada
Chuo Kikuu Suza, (haijachapishwa).
Alhabib, E.A (2012) „Matumizi ya Lugha katika Nyimbo za Taarab‟.Tasnifu ya
Umahiri katika Kiswahili, Chuo Kikuu Huria Tanzania.
Andanega A.A.S (2002) “Bahari ya Elimu ya Ushairi”. Ndanda Mission Press,
Mtwara.
Fargion, J. T. (2014), Taarab Music in Zanzibar in Twentieth Century: A story of old
is gold, Ashgate Publishing Limited.
Far-han, I. (1992), Introduction of Taarab Music in Zanzibar.Makala iliyowasilishwa
katika International Conference on the history of Zanzibar (14-16,
Desemba).
Igobwa, E.S (2007), Taarab and Chakacha in East Africa: Transformation,
appreciation and Adaptation of two Popular Music Genres of Kenyan
coast, conference on music in the world of islam – Assah 8-13 August 1-
8
Juma, M. (2012) „Taarab Asilia‟. Tanzania Daima 13/7/2011
Khamis, A.M. (2012). Matumizi ya Taswira katika Nyimbo za Mapenzi za Taarab
asilia yaZanzibar. Tasnifu ya Umahiri katika kiswahili. Chuo kikuu cha
Dar es salaam.
Khatib, M. (2014), “Taarab Zanzibar”.Oxfrord university Press, Dar es Salaam.
Khatib, M.S (1982) „Taarab ni fasihi simulizi? Makala ya semina za Tuki Dar es
salaam. Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, uk 3
Kombo, D. Na tromp, d. (2006), Proposal and Thesis Writing, An Introduction,
paulines publications Africa.
Kothari, C. (2003), Research Methodology and Techniques, New international, (p)
ltd New Delhi.
65
Lange, S. (2000). Muungano and TOT: Rivals on the Urban Cultural Scene.
Mashindano / competitive music performance in east africa, mhariri ni
frank Gunderson and Gregory f.b. Dar es Salaam : Mkuki na Nyota
Publishers, uk. 67-85
Mgana, I. (1991), Jukwaa la Taarab Zanzibar.Hakapaino, Helsiniki Medi Africa.
Msokile, M. (1981), Nafasi ya Nyimbo za fasihi Simulizi katika jamii.Iliyoandikwa
katika makala za fasihi Simulizi.Chuo kikuu cha Dar-es-salaam.
Msokile, M. (1992), Kunga za fasihi na Lugha. Educationa publishers and
distributers.Dar-es-salaam.
Mulokozi, M. (1990), Tanzu za fasihi simulizi.Mulika toleo la 21.Chuo kikuu cha
Dar-es-Salaam.
Mzee F.A (2013), Maudhui katika Nyimbo za Taarab za bi Shakila. Tasnifu ya
Uzamili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (haijachapishwa).
Ntarangwi, M (2001) „a socio – historical and contextual analysis of popular musical
performance among the swahili of mombasa kenya. Cultural analysis
2001: 2:1-37 University of California, Los Angeles.
Ponera, A.S., (2014), Utangulizi wa Nadharia ya Fasihi Linganishi, Karljamer print
technology, Dar es salaam, Tanzania.
Saleh, S.S. (1980), „Nyimbo za taarab Unguja‟ Lugha Yetu namba 37. Jarida la
BAKIZA.
Senkoro, F.E.M.K (1987), Fasihi na jamii, Press and Publicity Center, Dar es salaam.
Thabit, W (2007), “Nafasi ya Maudhui ya Nyimbo za Taarab katika jamii ya
Zanzibar ya leo”.Ripoti ya utafiti ya shahada chuo kikuu cha Suza,
(haijachapishwa).
Wamitila, k.w. (2004), Kichocheo cha fasihi simulizi na andishi. Nairobi focus
publication ltd.
Zeid, O (2016) Mabadiliko ya Taarab Asilia. (Mahojiano na mtafiti).
66
VIAMBATISHO
A: Mwongozo wa usaili kwa wataalamu wa Fasihi.
1) Unafahamu nini kuhusu dhana ya huzuni?
2) Ni zipi nyimbo za huzuni ambazo unazifahamu?
3) Je ni kwa kiasi gani nyimbo hizo zinaweza kuathiri jamii?
4) Je wewe unafurahishwa na nyimbo hizo? Ikiwa ndio/ hapana kwanini
5) Ziko aina ngapi za huzuni?
6) Kwa maoni yako unahisi ni sababu zipi zinazowasukuma wasanii kutunga
nyimbo hizo?
7) Je upo umuhimu wowote wa kutunga nyimbo zenye maudhui ya huzuni?
67
B: Dodoso kwa wanfunzi waliotafiti taarab asilia
1) Unafahamu nini kuhusu dhana ya huzuni
…………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………
………………………
2) Taja sababu mbili zinazowasukuma wasanii kutunga nyimbo zenye maudhui
ya huzuni.
a) ……………………………………
b) …………………………………….
3) Ni kwa vipi nyimbo za huzuni zinaathiri jamii.
…………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………
………………………..
4) Ni mazingira yepi ambayo yanasababisha utokeaji wa huzuni katika
nyimbo hizo.
…………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………
……………………
4) Ni miktadha gani inayopelekea huzuni katika jamii?
…………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………..
68
5) Taja dhima za nyimbo za huzuni unazozijua ambazo zinajitokeza katika
nyimbo za taarab.
…………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………………….
…………………………………………………………………………………
6) Je ipo haja ya wasanii kutunga nyimbo ambazo zinabeba maudhui ya huzuni?
…………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………….
7) Toa maoni yako kuhusu nyimbo hizo.
…………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………….
69
C: Nyimbo za waimbaji wateule Zilizotumika katika kazi hii
2. KHERI ADUI SHETANI KAMA ADUI KIUMBE
Tutahadhari adui kiumbe, daima asikusibu Mungu akuepushie
Ujue si mzuri hata chembe, huwa hataki sababu mashakani akutiye
Hata kuchoka hachoki kwa kila pembe, na wala haoni tabu hasarani aingiye
Hata kama kitu huna masikini hambe, basi atakusulubu maisha uyajutiye
Adui umuonapo mkimbiye, kheri adui shetani kama adui kiumbe
Malipo ni duniyani, akhera hwenda hisabu viumbe
Kwa kweli wanalingana mfitini na hasidi, chanzo chake huwa choyo shoti
uwatambuliye
Tena wengi wapo hufanya juhudi, huzua yaliyo siyo ili wakuvurugiye
Huwa mkarimu kwao na hujitahidi, hakosi kisingizio mwema adui hanaye
Japo mwenyewe chako kakubariki wadudi, watakwendea mbio hadi lao
litimiye
Mja mwanadamu kufikiri na kuhisi, ndio hasa tarajio liburi simfnyiye
Maana wivu chuki hasada binafsi, huambatana na choyo husuda akuonee
Na kufanyiana hayo yake nafsi, roho mbovu alonayo yataka ajaliwaye
Mpewa hapokonyeki hapana dadisi, mtengenezaji hayo mola ndiye atoaye
Mjue hana kosa apewaye, kheri adui shetani kama adui kiumbe
Malipo ni duniani, akhera hwenda hesabu viumbe
Ni yeye mwenye uwezo mshirika hana, kwake hakuna lawama huwapa
wamuombaye
Wewe uonavyo mengineyo huna, nawe usikate tama muombe akujaliye
Kuchukuwa kwa kuwana si uungwana, ni tabia mbaya jama ziwacheni
mtubiye
Huu si wakati tena wakufatanafatana, yapo mengi yalazima ya thawabu
jichumiye
70
Mja mwishowe akusaidiye, kheri adui shetani kama adui kiumbe
Malipo ni duniani, akhera hwenda hesabu viumbe
KIITIKIO
Imani imewasakama wakiona yakwendea
Imani zimewahama rohoni wanaumiya
Lo! Po! Yasini mate chini ninatema
Kunusuru ya jaliya nahizi tabia mbaya
Mwimbaji: Fatma Isa
2. ASOKASORO HAKUNA
Hicho kilonichukiya maovu kunikataza, ikiwa nnakoseya wajibu kuniongoza
Ikiwa nnakosea wajibuweni kuniongoza, wala sioni vibaya mimi kunielekeza
Kinachonipa udhia, ni kule kuniapiza
Aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Asokasoro hakuna, aloumbwa na muweza
Mwenye lile hili hana, ndio shani yake azza
Tabia kutolingana, sijambo lakushangaza
Kinachonikera sana, nisonalo kupakaza
La msingi niiteeni, na wala sitopuuza
Sikatai nambieni, wallahi tawasikiza
Mengine msinidhani, yakuwa nitawabeza
Name tawashukuruni, kwa vile mmenifunza
Kama kosa nimefanya, na iwe nimeteleza
Dogo msilipe mwanya, likaja likatatiza
Mukawa mwayakusanya, nyinyi mnoendeleza
71
Hivyo sitokaa kimya, lazima tawaeleza
Kiitikio
Kunisema sichukui
Kusengenya haifai
Ni hekima njema rai
Kunionya sikati
Mwimbaji: Fatma Isa
3. HAYA MAUMBILE YANGU
Ubinafsi na choyo, nyoyoni vyawasumbuwa
Kutwa kazi yenu hiyo, zimewajaa shakawa
Kufanya niyapendayo, kwangu kosa limekuwa
Hilo haliwezekani, na wala halitokuwa
Leo nakuelezeni, muache kunichunguwa
Msijitie shidani, haya nimejaaliwa
Kwani hasa jambo gani, nyie lakulaumiwa
Kama baya kwenu nyie, kwangu nnaona sawa
Nawambia msikie, msio fahamikiwa
Fedhehani msingiye, kukaa kujizuzuwa
Lilobaki mnachie, sitaki kulaumiwa
Wengi wamenihasimu, na thamani kunitoa
Mwapita kumwaga sumu, kila ovu kutupiwa
Bure mnanituhumu, yafitina kuyagawa
Nami ni mwanadamu, si vyema kulaumiwa
72
Kiitikio
Nami ni mja mwezeni
Hata mkinichukiya
Aibu yangu ndo yenu
Kama mtafikiriya
Mwimbaji: Fatma Isa
4. AKUKATAAYE HAKWAMBII TOKA
Akukataaye, hakwambii toka
Huona mamboye, yamebadilika
Waweza ukae, huwezi ondoka
Nipende kwa dhati, au nikataye
Usinidhihaki, la kweli nambiye
Kama hunitaki, kheri nituliye
Watu hutendana, zaidi ya hayo
Wakatukanana, kupita mifano
Mwisho hupatana, yakesha maneno
Mwimbaji: Shakila Said
5. MAPENZI YAMEPUNGUA
Nilipokuwa na pendo, na ikawa twapendana
Hukuwa navyo vishindo, wala hatukupigana
Umebadilika mwendo, ni kheri tukaachana
Duniani wengi wapo, wapenzi kila aina
Usidhani peke yako, uzuri mnapitana
Sina haja pendo lako, dunia hii pana
73
Kiitikio
Mapenzi yamepunguwa mimi nimeshayaona
Kila nikiyachunguza hakwishi kuoneana
Mapenzi yamenguwa.
Mwimbaji: Shakila Said
6. MAPENZI NI KAMA DONDA
Nimechoka vumiliya, leo nawapasuliya
Nimekuwa siku hizi, kila siku ninaliya
Nanyi hamuniulizi, kipi ninacoliliya
Ni kama donda mapenzi, leo nawaelezeya
Waweza funga pumzi, kuzimu ukaingiya
Wala hayana mjunzi, yoyote humuelemeya
Nimempenda fulani, jina sitowatajiya
Alikuwa msikizi, kila ninalomwambiya
Alikuwa mtimizi, yote nilohitajiya
Kiitikio
Mapenzi ni kama donda
Yaingiapo moyoni
Nimechoka vumiliya
Leo nawapasuliya.
Mwimbaji: Shakila Said
7. KIFO CHA MAHABA
Kifo cha mahaba, ni cha idhilali
Hakina haiba, wala afadhali
74
Bali tajikaba, nifilie mbali
Kufa kwa mahaba, nia adhabu kali
Leo ni msiba, usio mithali
Kesho ni adhaba, mbele ya jalali
Ewe mahabuba, niepushe hili
Niwewe twabiba, hapana wa pili
Hapanda jaziba, tajiua kweli
Mwimbaji: Shakila Said
8 NENDA UTAKAKO
Nenda utakaponenda nenda hujazuiliwax2
Japokua nakupenda kwa hilo siyoumbuax2
Katu mm sitojali zako inda ulichoweka chuku
Kwapwani sitokuganda kwako nikajizuzua
Wapowengi mdhubuti mapenzi wanoyajuax2
Wanaopend kwa dhati wenyehdhi namurua
Kamwe sijiombei umauti kwa wewe sitojiuwa
Name nishajidhatiti lolote utoamuwa
Unavuma nje wavuma kipanga waallahi sikukutambua
Unataka sikuyapinga ari pia ilikuwa
Kama mboni yamachoni nnavokuenga mamlaka yote umepewa
Kumbe vile ni mjinga hujui kusaminia
Nalia na moyo wangu weweulonisumbua
Kwakukwachia pendo langu si ila yangukuchungua
Tena nenda niko radhi roho yangu wala sitolaumiwa
75
Katambe na ulimwengu mimi hutonikomoa
KIITIKIO
Nenda utakako mwanakwenda usojua kupenda
Baki hukohuko ewe nunda ucnitoeroho bure
Pendo halitaki pupa nakwambia ukijua
Mara moja hukutupa watu wasikutambue
Daima asosikia madhila kujitakia
Tena wala usirudi tena nenda nakusabiliya
Endelea nawako ujana mwisho utajijutia
Na Yule ng‟ombe nimchezeeeee
76
Picha namba 6: Mtafiti akimuhoji bibi Shakila Said huko nyumbani
kwake Charambe Dar es Salaam. (Utafiti, 2016)
D: Picha mbali mbali zinazohusiana na utafiti