silaha - KIPAJI APP

89
Silaha za Adui Samuel Imori i SILAHA ANAZOZITUMIA ADUI KUWAANGAMIZA WATU WA MUNGU ASKOFU SAMWEL IMORI.

Transcript of silaha - KIPAJI APP

Silaha za Adui Samuel Imori

i

SILAHA ANAZOZITUMIA

ADUI KUWAANGAMIZA

WATU WA MUNGU

ASKOFU SAMWEL IMORI.

Silaha za Adui Samuel Imori

ii

Haki Miliki@2018Samuel Imori

Mawasiliano;

+255765446611,+255715788219, +254707224495, +255 715 788 219

Email [email protected]

ISBN: - 978-9987-9995-6-9

Toleo la – Tano

Angalizo:-

Kitabu hiki ni mali halali ya Bishop Samwel Imori, ni makosa kunakili

au kutoa nakala za kitabu hiki bila idhini ya mwandishi. Nunua nakala

halisi ili kuinua huduma hii.

Kimechapishwa na

Truth Printing Company

0764 425 704/ 0652 383 590

[email protected]

Ubungo Dar es salaam Tanzania

Silaha za Adui Samuel Imori

1

YALIYOMO

UTANGULIZI: .............................................................................................. 2

SILAHA ANAZOTUMIA SHETANI KUWAANGAMIZIA

WANADAMU ............................................................................................... 5

Fedha ni nini? Biblia inaisemeaje fedha?. .............................................. 12

HITIMISHO ................................................................................................ 86

Silaha za Adui Samuel Imori

2

UTANGULIZI:-

Namshukuru Mungu aliyeniwezesha kukiandika kitabu hiki vipo

vitabu vingine vilivyo tangulia na ipo mistari mbalimbali katika

Biblia ilinifanya niandike hivyo vitabu vilivyotangulia,

Kipo kitabu cha

1. Vikwazo vya kuurithi uzima wa milele sehemu ya kwanza

2. Vikwazo vya kuurithi uzima wa milele sehemu ya pili

3. Kanisa ni nini?

4. Zijue huduma 5 katika kanisa

Baadhi ya mistari iliyonifanya niandike vitabu hivyo vilivyotangulia

ni hii hapa chini,

Luka13:24

Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba maana

nakwambia kwamba wengi watataka kuingia wasiweze.

Math7:22-23

Wengi watanambia sikuile Bwanabwana, hatukufanya unabii kwa

jina lako? Na kwajina lako kutoa pepo, nakwajina lako kufanya

miujiza mingi? Ndipo nitakapo waambia dhahiri sikuwajua ninyi

kamwe, ondokeni kwangu ninyi mtendao Maovu.

Silaha za Adui Samuel Imori

3

1kor9:26-27

Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, sikama asitaye, napigana

ngumi vivyo hivyo sikama Apigaye hewa, bali nautesa mwili wangu

na kuutumikisha, isiwe nikiisha kuwahubiri Wengine mwenyewe

mtu wa kukataliwa niwe.

Hiyo ndio mistari iliyonifanya nikae chini nakutafuta majibu:-

Kwamba wengi watataka kuingia katika uzima wa milele

lakini wasiweze, Nini kitawazuia na wanataka?

Kwamba wengi watajitetea kwamba walifanya miujiza mingi

kwa jina la Yesu lakini atawafukuza, maana yakewaende

wakaishi na mapepo waliokuwa wanayafukuza”fikiri hapo

kidogo”

Yakwamba mtumishi wa Mungu aliamua kuutesa mwili wake,

akaamua kuu tumikisha ili, Asije akaingiza wengine mbinguni

naye akakuta anakataliwa.

Mistari hiyo ndiyo ilionifanya nikae chini nitafute majibu, ndio vitabu

hivyo vine vikazaliwa.

Sikutaka kuishia hapo nilipo kutana na mstari ufuatao hapo chini-;

Hosea4:6a

“watu wangu wana anaangamizwa kwa kukosa maarifa

Mungu alimtumia mtumishi wake akatamka maneno hayo,ndugu

msomaji wangu wa Kitabu hiki usemi huo ni mgumu, sio wa

Silaha za Adui Samuel Imori

4

kawaida watuwangu wanaangamizwa ni watu wa Mungu maana

amewaita waziwazi kwamba “Watu wangu”

Nilishtuliwa na maneno hayo na ndipo nikakaa chini, nikatafuta

nikataka kujua kile kinachowaangamiza watu hawa wa Mungu, ndipo

kitabu hiki kikazaliwa.

Napendamno kumshukuru Mungu aliyenisaidia kukiandika, nakutakia

kila la kheri unapokisoma.

Kikafanyike msaada kwako wewe unayekisoma sasa na kwa

mwingine yeyote pia atakaye kisoma.

Katika Jina la Baba/Mwana na Roho mtakatifu,

Amen

Silaha za Adui Samuel Imori

5

SILAHA ANAZOTUMIA SHETANI KUWAANGAMIZIA

WANADAMU

Hosea4:6a

Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.

1kor 2:11

Shetani asije akapata kutushinda kwa maana hatukosi kuzijua hila

zake

Efeso 6:16

Zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani ambayo kwa hiyo mtaweza

kuizima mishale yote yenye moto ya Yule mwovu.

1thes 2:18

Kwahiyo tulitaka kuja kwenu naam mimi Paul, mara ya kwanza na

mara pili shetan akatuzuia.

Maandiko yote hapo juu yaliotangulia yanatosha kukutaarifu ya

kwamba tuko vitani na kwa kuwa tukovitani vema tujue tunapigana

na nani?

Na tukiisha jua tunayepigana naye tusiishie hapo tutafute kuzijua

silaha anazozitumia

Silaha za Adui Samuel Imori

6

Kwa upande wetu Mtume Paul alituandikia kwamba tuvae silaha zote

za Mungu ndipo tutaweza kupambana na huyo adui yetu tunaye

pambana naye.

Vita yetu tutashinda, lakini tusipojua silaha anazotumia, kwa

vyovyote atatushinda.

Neno la Mungu limetuambia hivi “watu wangu wanaangamizwa kwa

kukosa maarifa”

Kwa kukosa ujuzi, kukosa kuzijua silaha anazozitumia huyo adui yetu

Kama tunataka tushinde sharti tuzijue hila zake, tujue kwamba hana

mchezo, tujue anarusha mishale yenye moto ikimpata mtu

haimuumizi tuu bali humchoma pia ni mishale yenye moto.

Tumeendelea kuona waziwazi Mtume Paul akielezea vita hiyo kwa

kutamka kuwa walikuwa wamejipanga waende kwa wathesalonike

lakini, anasema waziwazi kwamba shetani akawazuia, akafanikiwa

kuwazuia

Mtume hatuambii kututishia wala hakuogopa kusema pengine

kwamba atadhalauliwa au pengine ataonekana hana nguvu hapana

alilielezea waziwazi jambo hili ili litusaidie kujipanga sawa sawa,

litusaidie kufikiri, na tuweze kutambua kwamba kama huyu adui yetu

hatutajua jinsi ya kumkabili,basi ni dhahiri kwamba atatuangamiza

kama yanenavyo maandiko yakwamba watu wa Mungu

tunaangamizwa kwa kukosa maarifa.

Maarifa haya yanayosemwa ni ujuzi wa jinsi ya kupigana na huyo

anayeitwa mwizi, au mwivi, Biblia inasema katika kitabu cha

Silaha za Adui Samuel Imori

7

Yohana 10:10

Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu, mimi nalikuja ili

wawe na uzima kisha wawe nao tele.

Tumelisikia jina la huyu adui yetu anaitwa mwivi, mwivi ni mtu Yule

anayechukua visivyo vyake, tena Akaitwa muuaji,mchinjaji, kwahiyo

kila anapotutembelea huwa anakuja atimize hayo ambayo ni majina

yake.

Huja ili aibe, achinje, aue, wakati mwingine kwa kutozielewa kazi

zake anatuumiza, kutokuelewa kwamba yeye ni, mwizi, mwuuaji.

Nilipokuwa na tafakari jambo hili la muuaji, nikalikuta andiko katika

Biblia linasema hivi, waulize wanyama nao watawafundisha.

Nilipousoma mstari huo ilinichukua muda kulitafakari hilo, tuusome

mstari huo kwanza ndipo tuendelee kujifunza

Ayubu 12:7

Lakini sasa waulize hao wanyama nao watakufundisha,na nyuni

wa aangani hao watakuambia.

Nilipoutafakari sana mstari huo, nilipata kuelewa kwamba wanyama

wanaoufahamu wa kuwajua maadui zao.

Nilimtazama sungura akifukuzwa na mbwa, hawezi kusimama, hata

akichoka namna gani, hawezi kusimama, tangu alipo zaliwa naamini

wazazi wake walimfundisha sungura kwamba mbwa ni adui yao, ni

muuaji wao,hana utani, akimkuta sungura anamla, kwamba mbwa

Silaha za Adui Samuel Imori

8

anapomkamata sungura niukweli usio pingika huwa analiwa, na kwa

mfano huo, wana wa Mungu wakifundishwa wakamjua vizuri huyo

wanayemwita shetani, wanayemwita ibilisi, huyowanayemwita

mpinzani wao, jina lake tumelisikia ni muuaji, yeye anapomwendea

mtu ni ili amuue wala hana utani, kama vile ambavyo mbwa

hanautani anapomkabili sungura nia yake huwa ni kumuua, nasi

tukielewa kuwa huyo anayeitwa mwizi, haji kwautani wala haji

kubahatisha yeye anakuja ili aue, nasi tukielewa vizuri tutajiponya, au

tutatafuta mbinu za kuweza kumkabili ndio maana imeandikwa

kwamba yeye atakayeshinda atapewa kuketi pamoja na Yesu, kama

yeye alivyoshinda.

Sikumoja nilikuwa nimealikwa Ibada mahali Fulani, vijana

walisimama kuimba, wimbo uliokua unaimbwa nilifuatilia yale

maneno waliyokuwa wakiyatamka, ya likuwa yanasema hivi, nita

nukuu machache

Wimbo ulikuwa unasema hivi;-

tutapita katikati yao, wakipita kwa chini tutapita kwa juu

Wakipita kwa juu tutapita kwa chini

Wakipita kushoto tutapita kulia

Wakipita kulia tutapita kushoto

Nliwaza sana nilipo yasikiliza hayo maneno, na waliokuwa wakiimba

ni wakristo, wanapambana na huyo adui yetu tulie mtaja hapo juu

yakwamba ni mwivi, huyo ambaye ni muuaji. Sasa nikajiuliza, hivi

Silaha za Adui Samuel Imori

9

hawa waimbaji wanasema, wapite kulia pindi wakigundua kuwa

muuaji huyu yupo kushoto, na wapite juu pindi wakigundua kuwa

muuaji yuko chini, mwisho wasiku wataitwa wameshinda au

wataitwa wamekwepa? hili swali lilinifanya nichukue muda wa

kutosha kujiuliza kama watu hawa wanaoitwa kanisa wanajifahamu

kuwa wao ni nani?

Ndio maana nikaandika kitabu kiitwacho“KANISA NI NINI”.

Jina mojawapo la kanisa ni askari, ukisoma utaelewa vizuri Askari

kazi yake sio kumkwepa adui kwa kupita kulia wakati yeye adui

akipita kushoto.

Nia yangu ya kukiandika kitabu hiki ni kuyafungua macho ya wale

wanaopigana vita na adui huyu anaeitwa ibilisi, shetani, mwizi, ndio

maana tumeona jambo muhimu ambalo lilifanya niandike kitabu hiki

kwamba “watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa”

Katika mstari huu tunasikia sauti ya Mungu ikisema watu wake

wanaangamizwa kwa kukosa maarifa

Wanaangamizwa na nani?

wamekosa maarifa ya kufanyaje?

Kwa vyovyote yupo anayewaangamiza na kwa vyovyote yapo

maarifa, au ujuzi ambao watu wake hawa wameyakosa, ambayo

wanatakiwa kufundishwa ili waepuke kuangamizwa.

Ni vizuri pia wafundishwe, vizuri kumhusu huyo mwizi, pamoja na

silaha anazozitumia, naomba Mungu atusaidie ili macho ya mioyo

Silaha za Adui Samuel Imori

10

yetu yatiwe nuru, tupate kuona yatupasayo kuyatenda katika sikuhizi

za kumalizia

Kama nilivyotangulia kusema kwamba jina mojawapo la kanisa ni

Askari

2 Tim 2:3

Ushiriki taabu pamoja nami kama askari mwema wa kristo Yesu.

Hakuna askari yeyote anayeweza kwenda vitani bila silaha, hawezi

kwenda mikono mitupu, lazima awe na silaha. Napenda uelewe kuwa

hata huyo anayeitwa mwizi au mwivi naye niaskari pia, nimesema

askari sharti awe na silaha, adui yetuyeye anazo silaha anazozitumia

katika vita.

Kabla hatujaendelea kujifunza napenda nikupe picha ya kile kinacho

fanyika ili huyo mwizi ampate mtu amwangamize, huwa anatumia

kitu kinachoitwa mtego, mfano mzuri wakujifunza ni kwa mvuvi

Wavuvi wengine hutumia ndoano, kwawale msioijua ndoano, ni

chuma kilichotengenezwa maalumu kwa kunasia samaki, lakini

mvuvi akirusha ndoano pekeyake kwenda kwenye maji, kamwe

samaki hawezi kukila chuma ,mpaka akifiche kile chuma na kitu

kinachitwa chambo, chambo ni ya mnyoo, anauvalisha kwenye

ndoano, samaki anapokuja haoni chuma ila anaona mnyoo, yeye

anaudaka na kuumeza ule mnyoo, akiisha meza ndio anasikia

kunaswa, mvuvi anachofanya anavuta ndoano inanasa Yule samaki,

mnyoo ule huwa umemaliza kazi yake, hapo samaki anajikuta tayari

Silaha za Adui Samuel Imori

11

yuko nje ya maji, ndoano memnasa Yule samaki tayari kwenda

kufanyika kitoweo

1Tim 2:24-26

Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi, balikuwa

mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu

akiwaonya kwa upole wao washindanao naye, ili kama ikiwezekana

Mungu awape kutubu na kuijua kweli, wapate tena fahamu zao

nakutoka katika mtego wa ibilisi, ambao hao wametegwa naye hata

kuyafanya mapenzi yake.

Mistari hiyo hapo juu inaelezea vizuri kwamba ibilisi anayo mitego,

nia yake ni kuwa nasa, kuwa kamata, wakristo kama vile mvuvi

anavyotumia mbinu za kumkamata samaki, kwa kutumia chambo

(mnyoo)

Vivyo hivyo huyu adui shetani naye anao ujuzi wa kuweza

kuwakamata wanadamu, anayo minyoo yake anayoivisha kwenye

ndoano yake ili awapate.

Shetani anayo minyoo yake anayoitumia kwasasa, au kwenye kitabu

hiki nitajikita kwenye mnyoo mmoja ambao umetumiwa na huyo adui

yetu kuwaangamiza watu wa Mungu.

Mnyoo huu unaitwa Fedha. (pesa)

Nimeeleza vizuri nilipotoa mfano wa mnyoo,mnyoo kama mnyoo

hauna tatizo lolote kwa wengine ni chakula kizuri sana, ukimwambia

Silaha za Adui Samuel Imori

12

mtu kuwa mnyoo, hata akikuuliza je waweza kutuambia ubaya wa

mnyoo ni nini?

Itakuwa vugumu kutamka ubaya wa mnyoo maana haupo, ila ukiuliza

idadi ya samaki waliokamatwa kwa kumeza ndoano iliyovalishwa

mnyoo, utakuta samakiwengi sana, mnyoo ulivalishwa juu ya ndoano,

samaki hakuona ndoano bali aliona mnyoo na akaumeza mnyoo ila

kumbe ndani ya ule mnyoo kulikuwa na ndoano.

Fuatana na mimi ninapokwenda kuuelezea mnyoo anaoutumia ibilisi

kuwaangamiza watu wa Mungu

“watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa”

Fedha ni nini? Biblia inaisemeaje fedha?.

Mhubiri 10:19

karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, na divai huyafurahisha

maisha, na fedha huleta jawabu la mambo yote.

Watu wengi wanapousoma mstari huo wanauchukua hivyo kwamba

ni jawabu la mambo yote.

Mtu akisema mambo yote ana maana gani?

Ukiuliza mambo yote maana yake nini?

Mtu anayeona karibu atasema mambo yote mazuri,nitakubaliana naye

kwa haraka haraka kwamba ni mambo yote mazuri, ukitaka kusafiri,

Silaha za Adui Samuel Imori

13

kula vizuri, kujenga nyumba nzuri, gari nzuri, chuo kizuri, yaani

chochote kizuri unacho kijua kuwa ni kizuri, unapopishana na

magari,unaweza ukalinganisha gari na gari kwa utofauti wa ubora

wake au gharama yake,unaingia hoteli ya bei juu,zingine unasikia

nyota tatu, nyota tano, n.k yote hayo inatajwa fedha,unaingia kwenye

ndege umakuta daraja la 1, la2, na la 3 yote hayo inatajwa fedha ndio

maana Biblia ikasema nijawabu.

Baada ya kukuonyesha uzuri kabisa wa fedha, nivizuri tuangalie

Biblia imesemeaje fedha, au imeizungumziaje-

1Tim 6:10

Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha,

ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani

nakujichoma kwa maumivu mengi.

Tumeanzia mstari huo unaosema vizuri waziwazi kwamba lipo shina

la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha(kuzipenda fedha)hapa

ndipo penye matatizo ndugu zangunimekuelekeza uzuri wa fedha,

jinsi inavyoweza kukufanyia mambo mazuri, kukusafirisha vizuri,

kukulisha vizuri, kukufanya ukanyage mahali ambako usingeweza

kabisa kukanyaga, fedha hiyo inakufanya utembelee gari ambayo

usingeweza kabisa kuitembelea bila fedha.

Nakwakuwa kila mtu anapenda vitu vizuri, asafiri vizuri, ale vizuri na

ukumbuke kinachosababisha hivyo vitu vizuri ni fedha na Biblia

imetuambia shina la mabaya yote ya kila namna ni kupenda fedha

Silaha za Adui Samuel Imori

14

Haikusema tusipende maisha mazuri, haikusema tusipende nyumba

nzuri,ila imesema tusipende fedha kwanini?

Kinacholeta mambo hayo yote yanayoitwa mazuri ni fedha.Na ili mtu

avipate hivyo, lazima aitafute fedha maana ndiyo inayoleta, na kama

fedha ndiyo inayoleta mambo mazuri inamlazimu mtu aipende na

kama akiipenda fedha, itamlazimu atafute kwa njia yeyote, hapo

ndipo unasikia wizi, unyanganyi, ujambazi, kutokuwa waaminifu,

ndio maana neno la Mungu limetuambia tusiipende fedha hiyo.

Ebr 13:8

Msiwe na tabia ya kupenda fedha, mwe radhi na vitu mlivyonavyo,

kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, sitakupungukia kabisa wala

sitakuacha kabisa.

Biblia inatueleza vizuri kwamba tabia ya kupenda fedha ni mbaya

sana, kama nilivyotangulia kusema kwamba mtu akiipenda fedha

ataitafuta kwa njia yeyote ile, iwe njia ya halali au iwe njia ya haramu

ilimradi tu anaipenda.

Neno la Mungu limetuambia kwamba Mungu wetu ametuahidi

kwamba hatatuacha kabisa, hatatupungukia kabisa, hii kauli ya neno

la Mungu kutuambia kabisa.Utakumbuka Bwana wetu Yesu akiwa

msalabani, alisema Baba mbona umeniacha?

Hakusema mbona umeniacha kabisa.

Silaha za Adui Samuel Imori

15

Hii inamaanisha kwamba Mungu wetu katika kutupitisha katika

masomo mbalimbali anaweza akatuacha katika masomo, ila

nikwamuda sio kabisa.

Isaya 54:7-8

Kwa kitambo kidogo nimekuacha, lakini kwa rehema nyingi

nitakukusanya.

Kwa ghadhabu ifurikayo nalikuficha uso wangu dakika moja lakini

kwa fadhili za milele nitakurehemu, asema Bwana mkombozi wako.

Hapo tumeendelea kuona kwamba kwa dakika moja Mungu aweza

kukuacha, lakini sio kabisa, kwa hiyo tunatakiwa kuwa wavumilivu

wakati tunapo pitia mambo magumu, tunapopitia taabu, mateso ya

aina yeyote, pengine nikupungukiwa, wengine nitaabu ya aina yeyote.

Zaburi 91:15

Ataniita nami nitamwitikia, nitakuwa pamoja naye taabuni,

nitamwokoa na kumtukuza.

Ndugu msomaji wangu hakuna mtu yeyote duniani awezaye kusema

kwamba anaipenda taabu, maana yake shida, mateso, hakuna mtu

ataipenda hali hiyo, lakini wale wanao safari kuelekea mbinguni

taabu kwao haiwafanyi wamwache Mungu, ila wata mwita Mungu

naye ameahidi kuwa pamoja nao katika taabu, ndipo awaokoe na

awatukuze. Kipindi hicho akiwepo taabuni hapo ndipo neno la

Mungu linasema atakaye vumilia mpaka mwisho ndiye ataokoka.

Mathayo 24:13

Silaha za Adui Samuel Imori

16

Lakini mwenye kuvumilia mpaka mwisho ndiye atakaye okoka.

Habari ya wokovu huu ambao Yesu aliuleta kuupata nirahisi tu,

nikumkiri Yesu na kumwamini unapata haki na wokovu.

Rumi 10:9-10

Kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako na kuamini moyoni

mwako kuwa Mungu alimufufua katika wafu utaokoka.

Hiyo ndio hatua anayopitia mtu anapata haki, na anapata wokovu,

ndio tukasoma hapo juu katika

Math 24:13

Kwamba atakaye vumilia mpaka mwisho ndiye ataokoka, kumbe

mtu anapookoka anatakiwa awe ameamua kutoka moyoni, vizuri

ajue kwamba ametoka katika utawala ule wa giza, amejiunga na

ufalme wa Mungu, mtu huyo atafahamu kwamba upande ule wa

pili unamtafuta ili umrudishe tena kwenye utumwana wengi

wamewezwa, nawakajikuta wanarudi kule walikotoka.

Wakati mwingine utajikuta unapitia hali ya kupungukiwa, unaweza

kupungukiwa vitu mbali mbali fedha ikiwa ni miongoni, hapo ndipo

Yule adui anapoweza kuleta kwako mnyoo (fedha) ili akunasie kama

mvuvi anavyo nasa samaki kwa kutumia mnyoo kama nilivyo eleza

hapo mwanzo

Filp 4:11-13

Silaha za Adui Samuel Imori

17

Sikwamba na sema hayo kwakuwa nina mahjitaji, maana

nimejifunza kuwa radhi na hali yeyote nilionayo, najua kudhikiwa,

tena najua kufanikiwa, katika hali yeyote na katika mambo yote,

nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na

kupungukiwa.

Mstari 13

Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

Mtume Paul anatufundisha waziwazi katika neno la Mungu, kwamba

amejifunza kuwa na hali iwayoyote, alijifunza njaa,shibe akahitimu

ndipo alipomalizia mstari 13, watu wengi wanakariri mstari huo

unaosema kuwa anayaweza mamboyote katika yeye aliyekuwa

anamtia nguvu.

Utakumbuka kule mwanzo katika kitabu cha mhubiri, tumesoma

unaosema”fedha ni jawabu la mambo yote”. Ndipo nikakumbuka

Biblia inaposema mambo yote,wengi wanatazama mazuri tu wala

hawaelewi kuwa nipamoja na mabaya yote, Paul nalieleza vizuri

akiwafundisha wafilipi akasema alikuwa amefundishwa kushiba,

kuona njaa, alikuwa amefundishwa kupungukiwa na akawa

amefundishwa kuwa navyo au kufanikiwa, ndipo akafikia uamuzi

huo yakwamba anayaweza mamboyote katika Yesu kristo, hii ni

kusema nini? akiwa na njaa bado ataendelea kuwa na Yesu, akishiba

bado shibe haitambadilisha amwache Yesu.

Hayo yote ni mafundisho ambayo sharti tuyapitie tunapofundishwa na

Mungu wetu.

Silaha za Adui Samuel Imori

18

Zab 30:6-8

Nami nilipofanikiwa nalisema, sitaondoshwa milele.Bwana, kwa

radhi yako wewe uliuimarisha mlima wangu. Uliuficha usowako,

nami nika fadhaika. Ee Bwana nalikulilia wewe, Naam, kwa

Bwana naliomba dua .

Ninaendelea kukuonyesha jinsi mafanikio yanayoletwa na kile

tulichokiona kikiitwa fedha, tumeona mtumishi wa Mungu Daud

akisema alipofanikiwa alisema hataondoshwa milele, hapo unaweza

ukaiona silaha nyingine inayojitokeza inaitwa “kiburi”anatamka

mdomoni mwake kuwa hataondoshwa, kwa lugha nyingine

atatamalaki wazi, ataishi milele. Mtu akitamka ati hataondoshwa

milele unaona wazi wazi kiburi na kiburi kinamfanya mtu asiendelee

kujifunza.

1kor 8:2

Mtu akidhani ya kuwa anajua neno hajui neno lolotebado, kama

impasavyo kujua.

Hii inatukumbusha kwamba tusichoke kujifunza, tusichoke kuongeza

elimu. Nakumbuka kunamsemo usemao”Elimu haina mwisho”

Mungu atusaidie kuendelea kuwa wanafunzi wa Yesu.

2YOH 1:9

Kila apitaye cheo wala asidumu katika mafundisho ya kristo, yeye

hana Mungu, yeye adumuye katika mafundisho hayo huyo ana

Baba na Mwana pia.

Silaha za Adui Samuel Imori

19

Haya yote ni mafundisho mazito kwamba mwanadamu sikuzote,

analo la kujifunza hakuna anayeweza kusema sasa nimemaliza

kujifunza , mmoja asema elimu ni bahari haimaliziki

Ukiwa wazi kuendelea kujifunza hautafikia kusema kama alivyo

sema mmoja kwamba alipofanikiwa alisema hataondoshwa milele,

alitakiwa aendelee kujifunza kwamba anapita katika dunia hii, na

akijua hilo mafanikio yasinge mlemaza kama yanavyo lemaza

wengine. Na mtu akishindwa kuelewa hivyo hatajiandaa nani rahisi

kiburi kumpata akadhani hatakufa,ebu tuone

Zab 89:47-48

Ukumbuke jinsi mimi nisivyo wakudumu kwa ubatili gani

umeiumba jamii ya wanadamu. Ni mwanamme gani atakaye ishi

asione mauti , atakaye jiokoa nafsi yake na mkono wa kuzimu

Mwandishi wa zaburi hiyo hapo juu alijua kuwa siyo wa kudumu

alijua anapita katika ulimwengu huu na mtu akijua hivyo, basi atakaa

mkao wa kupita, atajiandaa, wengi hawajui hivyo , kumbuka hata

zamani salaam walizopewa wafalme ni uishi milele ee mfalme, na

kweli walikuwa wanaitikia, lakini kwa uhalisia nani ataishi milele?

Nani atakayeishi asiione mauti?

Tena swali aliloliuliza ni hili, mwanamme gani ataishi asiione mauti?.

Hakusema ni mwanadamu gani ataishi asiione mauti, alisema ni

mwanamme gani atakayeishi asione mauti? Yupo mmoja ambaye

ataishi milele na milele

Silaha za Adui Samuel Imori

20

Uf 1:17-18

Nami nilipo mwona nalianguka miguuni pake kama mtu aliye kufa.

Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, usiogope,

mimi ni wakwanza na wa mwisho, na aliye hai, nami nalikuwa

nimekufa na tazama ni hai hata milele na milele.Nami ninazo

funguo za mauti na za kuzimu.

Maandiko hayo yanamsema Yesu mwokozi, mwana wa Mungu

mwokozi wa ulimwengu , aliye tumwa kuja ulimwenguni kuwaokoa

wanadamu kutoka katika dhambi zao. Hayo maandiko yanasema

anaishi milele na milele na yeyote atakaye mwamini atampa uzima

wa milele. Na mara unapompokea unakuwa na uwezo wa kufanyika

mwana wa Mungu.

Yoh 1:12

Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa

Mungu ndio wale waliaminio jina lake.

Ukisha mwamini ukafanyika, kuwa mwana wa Mungu, hapondipo

tayari unakuwa umefanyika kuwa askari, kama nilivyo tangulia

kusema kuwa askari sharti awe na silaha, anatakiwa ajue vizuri

kuitumia silaha yake na pia nikasema kuwa upande wa pili wao pia

wanazo silaha wanazo zitumia kupigana vita, hapo itategemea ni

askari yupi aliye fundishwa vizuri, huyo ndiye atashinda, kumbuka

mstari wetu ulio kibeba kitabu hiki ni ule usemao

Hos 4:6a

Silaha za Adui Samuel Imori

21

“watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa”

Mwizi huyu anayeitwa shetani nimekueleza kuwa anaomnyoo wake

anaoutumia kuwavulia watu na kuwatoa katika eneo wanalotakiwa

kukaa.kama vile samaki alivyoweza kuishi nchi kavu anapotolewa

majini, ndivyo na adui yetu anavyo watoa watu wa Mungu, walio

fanyika watoto wa Mungu kwenye eneo lao na ndipo

anapowaangamiza kama yanenavyyo maandiko.

Napenda tuendelee kuona mnyoo anaoutumia ambao nimekwambia

ni pesa, tutaendelea kuangalia Biblia ilivyoisemea pesa

Luka 16:14

Basi mafarisayo ambao wenyewe ni wapenda fedha, waliyasikia

hayo yote wakamdhihaki

Napenda tuangalie vizuri mstari huo, kumbuka Biblia imetuonya

kwamba tusiipende fedha ,madhara yake ni makubwa kama mtu

ataipenda fedha,

Mafarisayo walikuwa wanaipenda fedha na Yesu alipowahubiria,

mahubiri yake hayakuwafaa mafarisayo , kinyume chake

walimdhihaki, nini klichofanya wamdhihaki? Jibu ni rahsi sana –

walikuwa wanapenda fedha, unaona dhihaka ikazaliwa.

Silaha za Adui Samuel Imori

22

Yesu alikuwa ametuhubiri nini?

Luka 16:13

hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili kwa maana,

ama atamchukia huyu na kumpenda huyu, ama atashikamana na

huyo na kumdharau huyu, hamwezi kumtumikia Mungu na mali.

Biblia imesemea fedha kuwa ni bwana ikasema jinsi ilivyo vigumu

mtu kuwatumikia mabwana wawili Ooh! Kumbe Mungu ni Bwana na

Pesa ni bwana, unaweza ukaona cheo kingine cha fedha ni bwana;

naamini unaelewa maana ya bwana, Mheshimiwa, Mkubwa, Mzito,

wa Thamani, wa maana. Tunaendelea kuona jinsi Biblia ilivyotaja

fedha

Marko 14:11

Nao waliposikia walifurahi, wakaahidi kumpa fedha akatafuta njia

ya kumsaliti wakati wa kufaa.

Biblia inasema waliposikia walifurahi kwani walikuwa wamesikia

nini,

Marko 14:10

Yuda Iskariote, Yule mmoja katika wale Thenashala akaenda zake

kwa wakuu wa makuhani, apate kumsaliti kwao,

nadhani jibu tumelipata Yuda alenda akawaeleza kwamba yuko

tayari kumsaliti kwao, yaani kuwaonesha Yesu ili wamuue. Nao

waliposikia kwamba wamepata mtu atakayewaonesha wakafurahi na

Silaha za Adui Samuel Imori

23

waahidi kumlipa fedha kwa kazi hiyo, hapo unalo la kujifunza,

tunajifunza nini?

Yuda alitamanai apate fedha kwa njia ambayo aliona itamletea fedha

ni kumsaliti Mwokozi na ndivyo alivyofanya, na kweli aliipata, lakini

Biblia inatuambia kwamba mwisho wa siku alijuta kwa tendo hilo

hata fedha zile alizirudisha kwao wale waliompa nao walizikataa pia

mwishowe zikatupwa, mwisho wake utakumbuka kwamba

alijinyonga hakuweza kutubu dhambi hiyo ya usaliti na alifanya

hivyo ilia pate fedha.

Napenda tuendelee kutembelea Biblia kwa kuona baadhi ya mistari

inavyoongelea fedha

Mathayo 21:12

Yesu akaingia ndani ya hekalu akawafukuza wote waliokuwa

wakiuza na kununua hekaluni, akazipindua meza za wabadilisha

fedha na viti vyao waliokuwa wakiuza njiwa.

Hekalu ni mahali inapofanyika ibada na walikuwemo watu humo

wakifanya biashara, hapa tunajifunza nini? Tunajifunza kuheshimu

nyumba ya ibada, nyumba hiyo inatakiwa iheshimiwe Mungu wetu ni

mtakatifu, wao wale wamwabuduo wanatakiwa wamwabudu katika

Roho na Kweli. Na kwakuwa Mungu wetu hana upendeleo ndivyo

tunatakiwa tusiwapendelee watu katika hali zao, Yesu wetu

alipokuwepo duniani hakuwapendelea watu wenye vyeo wala wenye

fedha

Silaha za Adui Samuel Imori

24

Mathayo 22:15-16

Ndipo mafarisayo wakaenda zao wakafanya shauri jinsi ya kumtega

kwa maneno wakatuma kwake wanafunzi wao pamoja na

maherodi, wakasema mwalimu twajua ya kwamba wewe ni mtu wa

kweli na njia ya Mungu waifundisha katika kweli wala hujali cheo

cha mtu awaye yeyote kwa maana hutazami sura za watu

Mistari hiyo hapo juu inatundisha nini? Yesu alitufundisha jinsi ya

kuwa watu wa kweli, utakumbuka hata msemo wa kawaida wa

Kiswahli; “msema kweli ni mpenzi wa Mungu”, lakini utakumbuka

neno la Mungu linasema siku za mwisho watu hawataipenda kweli,

wataikataa na hilo ndilo linaendelea leo, Mtume Paulo alimwasa

mototo wake wa kiroho kuhusu siku hizo za mwisho

2 Timotheo 4:1-5

Nakuagiza mbele za Mungu na mbele za Kristo Yesu,

atakayewahukumu walio hai na waliokufa, kwa kufunuliwa kwake

na kwa ufalme wake, lihubiri neno, uwe tayari wakati ukufaao na

wakati usiokufaa,karipa,kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na

mafundisho, maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho

yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia

waalimu makundi makundi kwa kuwa wana masikio ya utafiti, nao

watajiepusha wasisikie yaliyo kweli na kuzigeukia hadithi za uongo,

bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya fanya

kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako.

Silaha za Adui Samuel Imori

25

Mtume Paulo aliziona siku za mwisho ambazo ndizo tulizonazo leo,

watu hawataki kweli watu wanataka maneno sio Neno, unajua

maneno hayambadilishi mtu, neno la Mungu ndilo peeke linaloweza

kumbadilisha mtu, mpaka afanane na Yesu, yeye Bwana Yesu

tumesikia kuwa hakujali cheo cha mtu wala sura ya mtu yeyote.

Anaposema cheo hapo anasema fedha, maana ukisikia mtu kapanda

cheo, hapo ujue inatamkwa fedha na ukisikia hakutazama sura ya

mtu, anamaanisha nini? Nilikuwa nimetembelea nchi moja na

nilipokuwa huko nilitamani kwenda ibadani, mwenyeji wangu

aliniuliza swali hili”ungependa kusali katika kanisa la mchungaji

kabila gani? nilishangaa kwa swali hilo, akaendelea kusema waumini

wao wahuko wanakwenda kushiriki ibada ya mchungaji kabila

yao,unaona hao walikuwa wanatazama sura, kabila n.k.siku moja

naikumbuka, nilikuwa safarini jumamosi usiku gari yetu

ilituharibikia,jumapili ikatukuta na ilionekana tutakaa pale jumapili

yote, jumatatu spare itakapokuwa imeletwa ,na tulitembea kwa mguu

kidogo tukaingia mjini, Mungu bariki tukakuta kanisa,nilifurahi sana.

Vyombo vilisikika vikiimba kwa uzuri kabisa, naukumbuka wimbo

niliousikia ni huu;-

“nyimbo na tuziimbe tena, za alivyotupenda mbele, kwa bei ya

dhamani sana mbinguni huonana milele.”

Nilifurahi sana, nilienda nikaingia, nikakuta watu wachache, viti

vingi,nikaelewa kuwa bado wataendelea kuja. Niliingia nikanyoosha

moja kwa moja nikaenda kwenye viti vile vya mbele,sio kwa

wachungaji,viti vya mbele kwa wakristo nilipofika nilikaa, kama

ilivyo kawaida nilimshukuru Mungu, nikamaliza nikakaa sawa, mara

Silaha za Adui Samuel Imori

26

alikuja shemasi kwangu, akanisalimia, akaniomba niinuke nimfuate,

nilitii, alinitangulia kuelekea nyuma ya kanisa, akanionyesha kiti cha

nyuma kidogo kutoka kile nilicho kuwa nimekaa, akaniambii kaa

hapa, sikupapenda nilitamani nikae pale mbele niwezekumsikiliza

mhubiri vizuri, nikamuuliza kwanini unaniweka huku akanambia viti

vile nivya watu maalumu, wale wanao toa sadaka kuanzia 20,000/=

niwatu wazito, nilishangaa, nilikaa nikatulia kweli walianza

kuingia,walikuwa wazito ukiwatazama hata mavazi yao tu, nilisema

kweli hawa niwa 20,000/=ndipo nilipo elewa kile Yakobo

alichokiandika. Ndugu zangu imani ya Bwana wetu yesu kristo,

bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa kupendelea watu, maana

nikiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu, na

mavazi mazuri kasha akiingia na maskini, mwenye mavazi mabovu

nanyi mkimstahi Yule aliye vaa mavazi, mazuri na kumwambia keti

wewe hapa mahali pazuri na kumwambia Yule masikini simama

wewe pale, au keti miguuni pangu, je hamkufanya hitilafu mioyoni

mwenu mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu? ndugu zangu

wapenzi sikilizeni je Mungu hakuwachagua masikini wa dunia wawe

matajiri wa imani na warithi wa ufalme alio waahidia wampendao,

bali ninyi mmemvunjia heshima maskini, je matajiri hawawaonei na

kuwavuta mbele ya viti vya hukumu? Neno la Mungu wetu linasema

kwamba Mungu hana upendeleo, inakuwaje watu wake wanakuwa na

upendeleo, wanapendelea watu kwa kuwatazama sura zao, jinsia

zao,vyeo vyao ,urefu wao, udogo wao, utu uzima wao. Haifai kuwa

hivyo, Mungu atusaidie.Tunaendelea kuitembelea Biblia

ikitufundisha kuhusu fedha ambayo nimesema kwamba ni munyoo

ambao shetani anautumia, kama vile mvuvi anavyotumia mnyoo

kumnasa samaki.Nimesema mnyoo kama mnyoo hauna tatizo,wala

Silaha za Adui Samuel Imori

27

sio mbaya, ila ukimuuliza samaki au ukitafuta idadi ya samaki

walio vuliwa kwasababu walikula au walimeza mnyoo ni wengi mno,

fedha nayo kama fedha haina tatizo, wala fedha sio mbaya, wala

haina ubaya wowote ninzuri, lakini ukiuliza idadi ya watu

walioangamizwa na adui kwakutumia fedha ni wengi mno, na

tutaendelea kuangalia ili tupate kujifunza neno linalosema, yale

yaliyofunuliwa ni yetu ili tuyafanye pamoja na watoto wetu.

Kumb 29:29

Mambo ya siri niya Bwana, Mungu wetu; lakini mambo

yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu mileleili tuyafanye

maneno yote ya sharia hii.

Ndugu msomaji wangu mahali pale ambapo Biblia imekaa kimya

nasi tunapaswa kukaa kimya, pale ambapo imeongea ikatuelekeza

twapaswa kufanya vivyo hivyo au vile inavyo tuelekeza, vingine tuta

ongeza au tutapunguza na tukifanya hivyo, yenyewe inajisemea au

inajilinda kwa vile inavyo kataza.

Mith 30:5-6

Kila neno la Mungu limehakikishwa yeye ni ngao yao

wamwaminio, usiongeze neno katika maneno yake; asije

akakulaumu, ukaonekana umwongo.

.watu wengi wamelaumiwa na Mungu na wameonekana waongo pale

walipo punguza neno la Mungu na wengine wameonekana waongo na

Mungu amewalaumu pale pale walipo liongeza neno la Mungu.

Silaha za Adui Samuel Imori

28

Kumb 4:2

Msiliongeze neno ni waamurulo, wala msilipunguze,mpate

kuzishika amri za Bwana Mungu wenu niwaamuruzo.

Yapo mambo ambayo Mungu amewaamuru wanadamu, ni juu yao

kuyafanya au kuto kuyafanya, yote hayo yapo kwenye uwezo wa

mwanadamu, Mungu wetu hamlazimishi mtu,amempa uhuru wa

kuchagua.

UF 22:18-19

Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu

hiki, mtu yeyote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo

yalioandikwa katika kitabu hiki,na mtu yeyote akiondoa lolote

katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea

sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji

mtakatifu,ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.

Nimetangulia kukwambia ya kwamba Biblia haikuachwa tu bila

ulinzi, maana kila mtu angeingia tuu apunguze jambo, angeingia tu

aongeze jambo, lakini Mungu akaweka ulinzi, na inatulazimu tutii,

tufanye vile inatuagiza. Tunaendelea kuangalia inazungumzia nini

kuhusu fedha, kumbuka mstari muhimu ulio tufikisha hapa ni

Hosea 4:6a

“watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa”

Silaha za Adui Samuel Imori

29

Yoh 2:14-16

Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng’ombe na

kondoo na njiwa na wenye kuvunja fedha wameketi,akafanya

kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na

ng’ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha,akazipindua

meza zao akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, yaondoeni

haya,msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara.

Mungu atusaidie tuone kile Bwana wetu Yesu alichofanya, na

watuwengi wameshidwa kuelewa alichokifanya, neno la Mungu

linasema sisi ni hekalu la Bwana, ni nyumba ya Mungu, Mungu wetu

anatamani akae katika hekalu lake, ambalo ndilo sisi, yaani kanisa,

nakama ndivyo tunatakiwa kulisafisha liwe safi, vinginevyo hatakaa,

meza zilizomo zinatakiwa kupinduliwa, njiwa waliomo, fedha zinazo

badilishwa humo zinatakiwa kumwagwa

Gal 5:19

Bali matendo ya mwili ni dhahiri ndio haya, uasherati, uchafu,

ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira,

fitina faraka, unafiki, uzushi, husuda, ulevi, ulafi na mambo ya

nayofanana na hayo, katika hayo na waambia mapema kama

nilivyokwisha kuwaambia ya kwamba watu watendao mambo ya

jinsi hiyo hawata urithi ufalme wa Mungu.

Msomaji wangu tume muona Yesu akipindua meza alizozikuta

hekaluni hakukubaliana biashara ziendelee kwenye nyumba ya Baba

yake, na nimekuelezea kwamba nyumba ya Mungu sio ile ya

Silaha za Adui Samuel Imori

30

matofali, ni mioyo yetu ndio hii inaitwa kanisa, linatakiwa liwe safi

lisiwe na hila, lisiwe na doa lolote ndio kazi Yesu aliokuja kuifanya

chini ya jua.

Efeso 5:25-27

Enyi waume wapendeni wake zenu kama kristo naye alivyo lipenda

kanisa,akajitoa kwaajili yake,ili makusudi alitakase na kulisafisha

kwa maji katika neno,apate kujiletea kanisa tukufu,lisilo na

ila,wala kunyanzi wala lolote kama hayo;bali liwe takatifu lisilo na

mawaa.

Katika kitabu changu cha” kanisa ni nini”,nimeeleza vizuri kanisa ni

nini, watu wengi kwakuto kujua,wanajitahidi sana kuwa watakatifu

wakati wanapokuwa kwenye nyumba ya ibada pale wanatembea kwa

upole sana ,ukiwauliza ni kwanini wanafanya hivyo,wanasema ni

kwasababu wapo kanisani, maana wamepotoka hapo,utashangaa

wakiwa mbali na nyumba ya ibada wanaweza wakaongea

vyovyote,wakatenda vyovyote,akiwa mbali na nyumba ya ibada

anaweza akanywa kilevi, lakini akiwa katika nyumba ya ibada kamwe

hawezi kunywa kilevi, ukimuuliza atakwambia nyumba ya ibada

sharti iheshimiwe, hawajui yakwamba wao ndio nyumba ya Mungu

ya ibada, kwamba wao ndio kanisa, ndio hekalu la Mungu,na hekalu

linatakiwa liwe safi kama tulivyo tangulia kuona hapo juu.

1Kor 6:19-20

Au hamjui ya kuwa miili yenu ni hekalu la Roho mtakatifu aliye

ndani yenu, mliye pewa na Mungu? wala ninyi sio mali yenu

Silaha za Adui Samuel Imori

31

wenyewe,maana mlinunuliwa kwa thamani, sasa basi mtukuzeni

Mungu katika miili yenu.

Msomaji wangu tunatakiwa tuwe tayari wakati wowote,tuwe safi siku

zote sio jumapili, au jumamosi peke yake, ni siku zote.sikumoja

wanafunzi wa Bwana Yesu walimuuliza awaambie atakuja

lini.Walitamani wajue mpaka siku, lakini Yesu alisema hata yeye

hajui siku hiyo,a liwaambia dalili za kuja kwake, soma hapa chini

Math 24:36

Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna ajuaye, hata malaika

walio mbinguni, ila Baba peke yake

Mstari huo unanifanya niwaze sana, Mungu wetu ni waajabu ukweli

unabaki pale pale,kamaYesu angewaambia siku ya kuja na saa ya

kuja kulinyakuwa kanisa, naamini watuwengi sana wangeweza

kwenda naye,wangejiandaa muda ambao wangejua siku zimebaki

chache na saa chache, ndio wange kusanyika tayari kwa safari ya

mbinguni tayari kwa unyakuo. Fikiri kidogo ingekuwaje, nyumba za

ibada zisingetosha sikuhiyo.Wengine wangekuja imebaki siku moja,

wengine mpaka ingebaki saa moja, wengine hata dakika 10au5.

Haingekuwa na maana, wala wala wasingekuwa wanampenda

Mungu, bali wange kuja tukwa kuwa muda huo umefika, mpaka

Bwana Yesu anasema hakuna aijuaye hata malaika, hata mwana pia

ila Baba pekeyake, japo alijitahidi kuzitaja dalili za kuonyesha

kwamba siku hiyo imekaribia, na sasa tunaziona zikitimia moja baada

ya nyingine. Na mtumishi wa Mungu Paul pia aliona vyema

amuelezee kijana wake siku hizo za kumalizia atazijuaje

Silaha za Adui Samuel Imori

32

2Tim 3:1-7

Lakini fahamu neno hili ya kuwa siku za mwisho kutakuwako

nyakati za hatari, maana watu watakuwa wenye kujipenda

wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi,

wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio

safi, wasio wapenda wakwao, wasio taka kufanya suluhu,

wasingiziaji, wasio jizuia, wakali, wasiopenda mema, wasaliti,

wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda

Mungu, wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake, hao

nao ujiepushe nao.Kwamaana katika hao wamo wale wajiingizao

katika nyumba za watu, na kuchukua mateka, wanawake wajinga

wenye mizigo ya dhambi, walio chukuliwa na tama za namna

nyingi, wakijifunza sikuzote,ila wasiweze kabisa kuufikia ujuzi wa

ile kweli.

Msomaji wangu mpendwa unayesoma kitabu hiki, yawezekana bado

ulikuwa hauja zijua dalili za kurudi kwa Yesu kulinyakuwa kanisa,

alisema atatokea kama mwizi, mwizi hatoi taarifa ya lini anakuja

kuiba, mwizi anakuja ghafla na ndivyo Bwana wetu atakuja ghafla

kulichukua kanisa, kulinyakua, siku ambayo itakuwa ya kutisha,

sikuhiyo vitatokea vifo vya kutisha, fikiri kidogo,mtu atakuwa ndani

ya bus na dereva ameokoka,kanisa likinyakuliwa,dereva nae ata

nyakuliwa, ataliacha bus liendelee pamoja na wasafiri litaishia wapi?

fikiri kidogo ndege itakuwa angani ,wakati huo pailot atakuwa

ameokoka, atanyakuliwa, ndege hiyo itakuwa na abiria fikiri kidogo

mwisho wake utakuwa ni wapi? pengine itakuwa ni treni, dereva

wake ameokoka, ananyakuliwa , treni inabaki inaendelea na

Silaha za Adui Samuel Imori

33

safari,ukweli ni kwamba itakuwa siku ya kutisha, ndio maana

unashauriwa uwe mtakatifu siku zote, masaa yote na dakika zote,

ndio maana Bwana Yesu akasema watu wake wakeshe ,wawe macho,

wawe tayari, wakae mkao wa kuondoka.Mtume Paul

alimtahadharisha mtoto wake kwa kumuelezea atakavyo utambua

wakati huo utakapokuwa umefika, ebu zipitie dalili hizo zote moja

baada ya nyingine uzitafakari kwa undani, sitazielezea kila moja ila

ile moja inayo husu fedha, akaisema”watu watapenda

fedha”.Msomaji wangu, nilielezea hapo mwanzoni kwamba neno la

Mungu linatukataza kuzipenda fedha, nikaelezea kwamba fedha kama

fedha haina tatizo ila tatizo ni kuipenda ,nikasema nikasema ikitokea

ukakubwa na roho hiyo ya kuipenda fedha, utaitafuta kwa hali yoyote

hata ya aibu utaipokea.

1Tim 3:8

Vyivyo hivyo mashemasi nao wawe wastahivi si wenye kauli mbili,

si watu wa kutumia mvinyo sana, si watu wanaotamani fedha ya

aibu.

1Pt 5:2

Lichungeni kundi la Mungu lililokwenu, na kulisimamia, si kwa

kulazimishwa bali kwa hiari kama Mungu atakavyo, sikwakutaka

fedha ya aibu bali kwa moyo

Mdo 24:26

Pamoja na hayo alitaraji kwamba atapewa fedha na Paul, kwa hiyo

alimwita mara nyingi akaongea naye.

Silaha za Adui Samuel Imori

34

Neno la Mungu halikubaliani na rushwa lakini utakubaliana na mimi

kwamba rushwa imeuwa wengi, hata watumishi wa Mungu,

wanapofikia mahali pakusimama kidete kuipinga, rushwa

wanaharibiwa na wanaotoa. Mtumishi wa Mungu Paul hakukubaliana

na rushwa, yeye alikuwa tayari kusimama katika kweli

Mdo 20:33

Sikutamani fedha wala dhahabu, wala mavazi ya mtu.

Hili limekuwa tatizo kubwa katika siku zetu tulizonazo, watumishi

wengi wa Mungu wametamani mali za washirika wao, wametamani

fedha za washirika wao, wametamani nyumba, mavazi ya washirika

wao bila aibu wengine wamewaomba mali, wazi wazi wamegeuka

omba omba.

Mdo 8:18-20

Hata Simon alipoona ya kuwa watu wanapewa roho mtakatifu kwa

kuwekewa mikono ya mitume akataka kuwapa fedha akisema,

nipeni na mimi uwezo huu, ili kila mtu nitakaye mweka mkono

wangu apokee roho mtakatifu, lakini Petro akamwambia fedha

yako naipotelee mbali pamoja nawe kwa kuwa umedhania ya kuwa

karama ya Mungu ya patikana kwa mali, huna fungu wala huna

sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za

Mungu.Basi tubia uovu wako huu ukamwombe Bwana ili kama

yamkini usamehewe fikira hii ya moyo wako, kwamaana nakuona

ukatika uchungu kama nyongo, na tena ukatika kifungo cha uovu,

Silaha za Adui Samuel Imori

35

Simion akajibu akasema.Niombeeni ninyi kwa Bwana, yasinifikilie

mambo hayo mliyosema hata moja.

Msomaji wangu unawezaukaona fedha inavyo weza kumfikisha mtu

aliye nayo, Simioni alisukumwa kwa ndani ampe mtume fedha, lakini

kwakuwa mtume wa Mungu wakweli alikuwa na macho ya rohoni,

hakuikubali fedha ile, macho yake yalifunguka, akaona uovu katika

moyo wa Simioni, akaona vifungo vya uchungu kama nyongo, wala

fedha zake hazikumsaidia, ndivyo ilivyo hata leo, wako watu

wamewaweka wachungaji mifukoni hata wange tenda dhambi

hawasemwiwengine mpaka wana vilabu vya pombe, lakini bado

niwatu wenye vyeo makanisani.Hawaguswi, hawaonywi,

hawakemewi, Petro akamwambia Simioni apotelee mbali na fedha

yake, kwa kuwa alidhani kwamba ufalme wa Mungu unapatikana

kwa mali, kama wengi wanavyodhani kwamba wanapokuwa na fedha

ni wa muhimu sana kuliko wengine wale wasio na fedha, kwa njia

hiyo wakadhani kwamba waweza wakafanya lolote na wasifanywe

lolote, Mungu atusaidie, atuhurumie, atupe macho ya rohoni,

tuwafungue watu waone, kama alivyo funguliwa Simioni na akahitaji

maombi, naamini alipata rehema, akaelewa yakwamba fedha haiwezi

kununua uzima wa milele, fedha haiwezi kununua ufalme wa Mungu,

vitu hivyo havilinganishi na chochote chini ya jua. Msomaji wangu

wa kitabu hiki kumbuka yakwamba kila andiko lenye pumzi ya

Mungu lafaakwa mafundisho na kuwaonya wanadamu.

2Tim3:16

Kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho, na kwa

kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kuwa

Silaha za Adui Samuel Imori

36

adibisha katika haki ili mtu wa Mungu awe kamili,amekamilishwa

apate kutenda kila tendo jema.

Nimeelezea jinsi Biblia inavyoongelea fedha, inavyoelezea, nikasema

fedha kama fedha sio mbaya wala haina ubaya wowote, ila fedha

hiyo kama mtu akiipenda, matokeo yake hayawi mazuri.

1Tim6:17-19

walio matajiri wa ulimwengu wa sasauwaagize wasijivune, wala

wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wa mtumaini Mungu

atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha,

watendemema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari

kutoa malizao, washirikiane na wengine kwa moyo, huku

wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate

uzima ulio kweli kweli.

Biblia inayo mambo mengi yakumfundisha mwanadamu aliyeubwa

kwa mfano wa Mungu. Maandiko hayo yanapeleka ujumbe kwa

matajiri wa ulimwengu huu kwamba waagizwe wasijivune,

auwasiringe, wasiuumainie utajiri wao, wasiutegemee utajiri,

wasiishie hapo wakaridhika na hali hiyo, bali wamtafute Mungu,

ufahamu wao uende zaidi ya huo utajiri wao wasidhani wataishi

milele, kama mmoja aliyefanikiwa akatamka kuwa hataona mauti.

Zab 30:6

Nami nilipofanikiwa nalisema sitaondoshwa milele.

Silaha za Adui Samuel Imori

37

Nakumbuka wakati Mungu alipokuwa amekusudia kuwabariki watu

wake, alipotaka kuongeza mali, walizokuwa nazo alitangulia

kuwaonya, kuwatahadharisha akawapelekea ujumbe

Kumb 8:11-20

Jihadharini usije ukamsahau Bwana Mungu wako kwakuto

kuzishika amri zake, na hukumu zake, na sharia zake,

ninazokuamuru leo,angalia utakapokuwa umekula na kushiba,na

kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake, na makundi yako ya

ng’ombe na kondoo yatakapo ongezeka, na fedha yako,na dhahabu

yako itakapoongezeka, na kilakitu ulichonacho kitakapoongezeka,

basi hapo moyowako usiinuke ukamsahau Bwana Mungu wako

aliyekutoa katika nchi ya misri, katika nchi ya utumwa,

aliyekuongoza katika jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka

za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji, aliyekutolea maji

kwenye mwamba mgumu, aliye kulisha jangwani kwa mana, wasio

ijua baba zako apate kukutweza, apate kukujaribu, ili kukutendea

mema mwisho wako.Hapo usiseme moyoni mwako nguvu zangu na

uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo,bali

utamkumbuka Bwana Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu

za kupata utajiri, ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako

kama hivi leo, lakini itakuwa, kama ukimsahau Bwana Mungu

wako na kuiandama miungu mingine, na kuitumikia na kuiabudu,

nawashuhudia leo ya kuwa mtaangamia bila shaka. Kama vile

mataifa yale ambayo Bwana anawaangamiza mbele yenu ndivyo

mtakavyo angamia, kwa sababu hamkutaka kuisikiliza sauti ya

Bwana Mungu wenu.

Silaha za Adui Samuel Imori

38

Kama nilivyotangulia kukuarifu kwamba fedha mara nyingi adui yetu

huitimia kama vile mvuvi anavyotumia mnyoo kumvua samaki, na

hapo juu tumeona vizuri Mungu wetu akiwapatia watu wake

maelekezo, anawaambia ya kwamba anaompango mzuri kabisa

kwaajili yao katika siku zao za usoni, siku zao za mwisho, ni mpango

wa kuwabariki, nimpango wa kuwainua, na kwakuwa anawapenda,

inamlazimu awatahadharishe mapema, amewajulisha waziwazi

kwamba chochote walichonacho kitaongezeka, ng’ombe, fedha,

dhahabu, n.k. Mungu wetu anatupenda sana na kwakuwa anatupenda

anajua alivyo tuumba, akatutengenezea mioyo na hakuacha

kututaarifu moyo ulivyo, katika kuelezea hali ya miili yetu alisema

hivi:-Mguuwako ukikukosesha uukate, mkono wako ukukukosesha

uukate, lakini alipofika kwenye moyo hakusema uukate, akasema

uulinde sana moyo kuliko kitu kingine chochote unachokilinda

hakutaka kuishia hapo alitoa sababu. Sababu aliyoitoa ni kwa kuwa

ndiko zinitoka chemichemi za uzima, hakusema uukate moyo,

hauwezi kukatwa. Katika kitabu change cha vikwazo vya kuurithi

uzima wa milele sehemu ya kwanza, nime uelezea moyo kirefu.

Mith 4:23

linda moyo wako kuliko vyote ulindavyo,maana ndiko zitokako

chemichemi za uzima.

Ni kwanini tunatakiwa kuulinda kuliko kiungo chochote?

Silaha za Adui Samuel Imori

39

Yer 17:9

moyo huwa ni mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa

kufisha nani awezaye kuujua.

Utakumbuka tumesikia Mungu akiwaelezea watu wake kwamba

watakapokuwa wamevuka, watakapokuwa wamefanikiwa kwa kila

kitu, mali zitakapoongezeka mioyo yao isiinuke, wakamsahau

Bwana, unaweza kusikia vile mafanikio yanavyoweza kusababisha

moyo wa mtu ukainuka, na ukamsahau Mungu aliye kuwezesha, aliye

kufanikisha kwenye hayo mafanikio.

Math 19:16-26

Na tazama mtu mmoja akamwendea akamwambia, mwalimu

nitende jambo gani jema ili nipate uzima wa milele? Akamwambia

kwani kuniuliza habari ya wema?Aliye mwema ni mmoja.Lakini

ukitaka kuingia katika uzima ishike amri:-Akamwambia zipi? Yesu

akasema ni hizi, usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo,

waheshimu baba yako na mama yako, nampende jirani yako kama

nafsi yako, Yule kijana akamwambia, haya yote nimeyashika,

nimepungukiwa na nini tena? Yesu akamwambia, ukitaka kuwa

mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape masikini,nawe

utakuwa na hazina mbinguni, kasha njoo unifuate, Yule kijana

aliposikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni,kwa sababu alikuwa

na mali nyingi, Yesu akawaambia wanafunzi wake,amini

nawaambieni yakwamba itakuwa shida kwa tajiri kuingia katika

ufalme wa mbinguni. Nawaambia tena, nirahisi zaidi ngamia

kupenya kwenye tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika

Silaha za Adui Samuel Imori

40

ufalme wa Mungu. Wanafunzi waliposikia walishangaa

mno,wakisema ninani basi awezaye kuokoka. Yesu akawakazia

macho, akawaambia kwa wanadamu hilo haliwezekani, bali kwa

Mungu yote yanawezekana.

Maelezo tuliyoyasoma hapo juu, umeona waziwazi kijana tajiri,

naamini alipokuja kwa Bwana Yesu alikuwa tayari kufanya lolote

ambalo Bwana angemweleza afanye, pengine angefika Bwana

amwambie atoe sadaka, au mchango, naamini angekuwa tayari, lakini

kile alichoagizwa kilimshinda,unaweza okaona jinsi mali inavyo

weza kukaa kwenye moyo wa mtu, ikautawala, akaipenda, kumbuka

tulisoma kwamba tusiipende, maana ukiipenda hautakubali kuiachia,

utaishikilia, itafanyika kama ndio kimbilo lako, Mungu hatapata

nafasi katika moyo wako, nyaraka zingine, zinasema kuwa kijana

baada ya kusikia hivyo, alikasirika, akakunja uso wake akaondoka.

Hakutaka tena kuendelea kumsikiliza Yesu akifundisha, hilo lilitosha

kumfukuza, akakosa amani, akaona jibu ni kuondoka, akaona hawezi

kuikosa mali, akaona vema akose mbimgu lakini abaki na mali. Hiyo

ndio hali ya matajiri wengi mioyo yao imewekwa kwenye mali,

ndiomaana mahali pengine imeandikwa hazina yako ilipo ndipo na

moyo wako ulipo.

Luk 12:16-21

Akawaambia mithali akisema, shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa

limezaa sana, akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema nifanyeje?

Maana sina pakuyaweka akiba mavuno yangu. Akasema nitafanya

hivi, nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa kubwa zaidi,

na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu, kisha

Silaha za Adui Samuel Imori

41

nitajiambia , ee nafsi yangu una vitu vyema vingi ulivyojiwekea

akiba kwa miaka mingi, pumzika basi, ule, unywe,ufurahi, lakini

Mungu akamwambia,mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka

roho yako,na vitu ulivyo jiwekea tayari vitakuwa vya nani? Ndivyo

alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.

Kama nilivyotangulia kusema kwamba yaliyofunuliwa kwetu niyetu

na watoto wetu tuyafanye, ukweli unabaki palepale kwamba duniani

ni mahali pa kupita, tukielekea mahali petu pa kudumu, mahali pa

milele. Mahali pa milele pa mwanadamu pameandaliwa, ni mahali

pawili tu , motoni na mbinguni pote hapo ni pa milele, hapa duniani

tunazo mali za hapa hapa duniani, hatutakwenda nazo mbinguni, na

utakumbuka anayetuchagulia pa kwenda kati yapawili sio Mungu

wala sio shetani ni kila mtu amepewa achague, amepewa uhuru huo,

hili ni jambo ambalo watu wengi hawajui, na wakajikuta

wanadanganywa kwamba wanaweza wakaombewa na wakawekwa

mahali pema peponi, ngoja tujifunze kidogo kuhusu hilo la

uchaguzi.Kitabu hiki kimekufikia kwa makusudi maalumu uweze

kuelewa kwamba umepewa uhuru huo wa kujichagulia mahali

utakapoishi milele na milele

Kumb 30:15-18

Angalia nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na

mabaya kwa hivi nikuagizavyo leo kumpenda Bwana Mungu wako,

kuenenda katika njia zake, na kushika maagizo yake na amri zake

na hukumu zake, upate kuwa hai na kuongezeka, Bwana Mungu

wako apate kukubarikia katika nchi uingiayo kuimiliki. Lakini

Silaha za Adui Samuel Imori

42

moyo wako ukikengeuka, usipotaka kusikia, lakini ukavutwa kando

kwenda kuabudu miungu mingine, na kuitumikia, nawahubiri hivi

leo hakika mtaangamia, hamtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu

ya nchi, uivukiayo Yordani, uingie kuimiliki.

Mungu wetu hamlazimishi mtu kumtii ila kama tulivyosoma hapo

juu, amemuwekea uchaguzi mbele yake, achague aidha amtii au

asimtii, napenda nikufungue macho, katika dunia hii wapo miungu

wengi, mmoja wapo ni shetani, anajulikana kama mungu wa dunia hii

na kwa kuwa miungu wako wengi twapaswa kuwa makini na unajua

miungu inapenda kuabudiwa, watu wanaiabudu pengine bila kujua,

wakidhani ndiyo Mungu wa kweli lakini Mungu wa kweli, wa pekee

yupo yeye ambaye ndiye muumba mbingu na nchi, ndiye aliepanga

mahali ambapo watu wataishi milele na milele ndiye huyo ninaye

sema habari zake nawakati alipokuwa anampatia mwanadamu nafasi

ya kuchagua,aliweka nchi iwe shahidi,aliweka anga liwe shahidi, kwa

hiyo mwanadamu anapochagua vibaya au vizuri mashahidi wapo.

Kumb 30:19

Nazishuhudia mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa

nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, Baraka na laana, basi

chagua uzima, ili uwe hai wewe na uzao wako, kumpenda Bwana

Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushika maneno yake kwani hiyo

ndio uzima wako, na wingi wa siku zako,upate kukaa katika nchi

Bwana aliyowaapia baba zako, Ibrahim na Isaka na Yakobo kuwa

atawapa.

Silaha za Adui Samuel Imori

43

Nimesema kwamba Mungu wetu anatupenda kwa sababu alituumba

kwa mfano wake, anatupenda upeo, hapendi mtu yeyote apotee ndio

maana akatuwekea mbele yetu tuchague, bado akatushauri kuwa

chagueni uzima, yaani kumtii, yaani kumheshimu yeye.Hata

alipoandaa moto wa milele ambao waliomkataa wataishi milele,

aliweka utaratibu wa jinsi watakavyotupwa humo, mwanadamu

atakuwa wa mwisho kabisa kutupiwa humo kwenye moto wa milele

(Jehanam) hii inatuonyesha wazi wazi kwamba Mungu hakupenda

mwanadamu aishi motoni milele, ebu tuangalie mpango wa kutupwa

humo motoni utakuwaje, naandika hii kwasababu wapo watu

wasemao ya kwamba hakuna jehanam,kwamba hakuna moto wa

milele.

Uf 19:20

Yule mnyama akakamatwa, na Yule nabii wa uongo pamoja naye,

yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo

aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama,

nao walioisujudia sanamu yake, hao wawili wakatupwa wangali hai

katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti.

Kama nilivyosema wapo watu wanadanganya watu ya kwamba

hakuna ziwa la moto, Biblia imetamka wazi wazi kuwa hao watajwa

hapo juu ndio watakao tangulia. Nani tena atafuata? tuendelee

kujifunza.

Uf 20:10

Silaha za Adui Samuel Imori

44

Na Yule ibilisi mwenye kuwadanganya, atatupwa kwenye ziwa la

moto na kibiriti, alimo Yule mnyama na Yule nabii wa uongo, nao

watateswa mchana na usiku hata milele na milele.

Tunaendelea kumwona shetani akiwafuata katika huo moto wa

milele, na baada ya hayo, nani tena atafuata?

Uf 20:14

Mauti na kuzimu Zikatupwa katika lile ziwa la moto.Hii ndio mauti

ya pili, yaani hilo ziwa la moto.

Mauti ni nini? mauti ni kifo, ni roho inayombeba mwanadamu,

tunaposema mtu amekufa, huwa amechukuliwa na roho inayoitwa

mauti, hiyo roho ikiisha kumchukua mtu inampeleka mahali

panapoitwa kuzimu, kuzimu ni wapi? Ni mahali ambapo roho zisizo

na Mungu zinatunzwa zikingojea kutupwa katika ziwa lile la moto

tulilolisoma hapo juu kwa hiyo huyo mauti na huyo kuzimu,

watatupwa kwa pamoja katika hiloziwa la moto wa milele na milele,

inaitwa ziwa la moto

Nani tena atafuata? nimeendelea tena kukuelezea habari ya ziwa la

moto wa milele na milele,tumeendelea kumsikia Mungu katika neno

lake, akitushauri tuchague kumcha yeye, na tukichagua kumcha yeye,

tutakuwa tumeepuka hilo ziwa la moto wa milele na milele.Nani tena

atafuata?

Uf 20:15

Silaha za Adui Samuel Imori

45

Na iwapo mtu yeyote hakuoenekana ameandikwa katika kitabu cha

uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.

Hapo ndipo tumeona mwanadamu akiwa wa mwisho kutupwa humo

katika lile ziwa la moto wa milele na milele, tumeona ushahidi ya

kwamba Mungu alimpenda mwanadamu, hakutaka mtuyeyote apotee

bali wawe na uzima wa milele, hakuna kitu kingine chochote

ambacho Mungu alikipatia kichague pakukaa milele na milele,

isipokuwa mwanadamu peke yake kama tulivyoona katika maandiko,

ya kwamba iwapo mtu yeyote ataonekana hakuandikwa katika kitabu

cha uzima, atatupwa katika lile ziwa la moto, waweza kuwa na swali

hili kwamba mtu anaandikwaje katika kitabu cha uzima?

Yoh 3:16

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa

mwanawake wa pekee, ili kilamtu amwaminiye asipotee, bali awe

na uzima wa milele na milele.

Nimeendelea kukuonyesha jinsi Mungu alivyompenda mtu, hata

akamtoa mwana wake wa pekee (YESU) ili azichukue dhambi zao, ili

wasamehewe, waiepuke jehanam ya moto wa milele na milele.

Yoh 5:24

Amini amini nawaambia, yeye alisikiaye neno langu na kumwamini

yeye aliyenipeleka yunauzima wa milele, wala haingii hukumuni,

bali amepita kutoka mautini na kuingia uzimani.

Silaha za Adui Samuel Imori

46

Yawezekana ulikuwa na maswali kwamba jina la mtu linaandikwaje

katika kitabu cha uzima? Neno la Mungu linatufundisha wazi wazi ya

kwamba ukiamua kumpokea Bwana Yesu katika moyo wako na

ukamkiri kwa kinywa chako ya kwamba Mungu alimfufua katika

wafu,unapokea wokovu, na tayari unafanyika kuwa mwana wa

Mungu, na tayari unakuwa umechagua uzima, tayari unakuwa

umechagua kuishi mbinguni milele, tayari unakuwa umeiepuka ile

jehanam tulioisoma, kwamba jina lake lingine ni ziwa la moto wa

milele na milele.Baada yakuona yakwamba mahali palipotengwa ili

wanadamu wakae milele ni sehemu mbili, mbinguni milele na milele,

sehemu ya pili ni motoni milele na milele nia hasa ya adui yetu

ambae ni shetani angependa aende na wanadamu wote kwenye ziwa

la moto, ndio maana anajitahidi kuwavuta, kuwarubuni na hawezi

akawarubuni tu watakatifu, kumbuka nimekuelezea mapema vile

ambavyo mvuvi anajitahidi kuwavuna samaki, vile asivyo wakamata

kwa ndoano tupu, yeye hutumia chambo, mnyoo, nikasema mnyoo

kama mnyoo hauna tatizo, wala hauna ugomvi na samaki, nichakula

kizuri kwa samaki, lakini mnyoo huo huo mvuvi anapouchukua,

anautumia kuivishia ndoano, na samaki anapoona anafikiri kwamba

ni chakula, kumbe kimegeuka si chakula tena bali ni chambo, hatajina

linabadilika, linatoka kuwa mnyoo linakuwa chambo.

Kwa mfano huo huo wa jina kubadilika hata fedha nayo inayo tabia

hiyohiyo ya majina kubadilika.Mtu anapoambiwa atoe mali ili aweze

kupewa mke, bado ni fedha ileile lakini inageuka na kuitwa

mahali.Mtu akiomba fedha ilia toe huduma Fulani, katika ofisi Fulani,

ni fedha tena anaitaja idadi, lakini hapo inajificha inajisema, rushwa,

chai, kitu kidogo ukipeleka mototo shule unaambiwa fedha kiasi gani

Silaha za Adui Samuel Imori

47

unatakiwa ulipe, ukiisha itoa inaitwa ada, karo.Ukitaka kusafiri,

unaenda stand, utaombwa fedha, lakini utasikia jina linabadilika

wanasema nauli, hiyo ni mifano michache tu jinsi fedha inavyoweza

kujigeuza geuza, kulingana na hali ya mahali hapo, tutaendelea

kuiangalia fedha jinsi Biblia inavyoiongelea

Yak 5:1-6

Haya basi ,enyi matajiri lieni,mkapige yowe kwa sababu ya

mashaka yenu yanayowajia, mali zenu zimeozi na mavazi yenu

yameliwa na nondo, dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu,

na kutu yake itawashuhudia, nayo itakula miili yenu kama moto,

mmejiwekea akiba katika siku za mwisho, angalieni ujira wa

wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila,

unapiga kelele na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa

BWANA wa majeshi, mmefanya anasa katika dunia na

kujifurahisha kwa tama, mmejilisha kwa tama, mmejilisha kwa

mioyo yenu kama siku ya machinjo, mmehukumu mwenye haki,

mkamwuua wala hashindani nanyi.

Utakumbuka kule mwanzoni neno la Mungu lilituambia kwamba

fedha ni jawabu la mambo yote, na nikakwambia nijawabu la mambo

yote kwenda kulia na kwenda kushoto.Mtu mzuri akiwa na fedha basi

fedha hiyo inamfanya apate majibu ya mambo yake yote anayotaka

ayatimize.Mtu mbaya naye pia anapokuwa na fedha zitamfanya apate

majibu ya mambo yake yote anayotaka ayatimize.Neno la Mungu

limewaelekeza katika kitabu cha Yakobo, kwamba matajiri walie

sikulia tu hakutoshi wapige yoe.Ameendelea kusema dhahabu zao na

fedha zao zimeingia kutu, hili ni neno gumu, ameeleza jinsi matajiri

Silaha za Adui Samuel Imori

48

wanavyoshindwa kuwalipa watu wanaowafanyia kazi,wanaishia tu

kulia kwa Mungu na akasema kilio chao kimefika kwa Mungu,

akaendelea kuonyesha jinsi mwenye haki anavyoonewa na tajiri,

anaumizwa, hajibu chochote, hana ubavu wa kumjibu tajiri,

tumeendelea kuwaona matajiri vile wanavyoweza kuutumia utajiri

wao vibaya, wakawa wamemkasirisha Mungu, wameua wenye haki

wengi, yatima wengi, wajane wengi ,wengine kwakuwa wanazo

fedha wanatoa rushwa, wanafanikiwa kuwafunga watu wasiona hatia

ili tu kwa kuwa hawana fedha, hapo ndipo fedha inaweza ikamfikisha

mtu, akawa apate jawabu la mambo yote.

Uf 3:17-19

Kwakuwa wasema mimi ni tajiri, nimejitajirisha wala sina haja ya

kitu, nawe hujui yakwamba wewe umnyonge, na mwenye mashaka,

na maskini, na kipofu na uchi, nakupa shauri ununue kwangu

dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi

meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako, isionekana na dawa ya

macho ya kujipaka macho yako, upatekuona, wote niwapendao

mimi nawakemea na kuwarudi, basi uwena bidii ukatubu.

Neno la Mungu linatufundisha nini katika mistari hiyo hapo juu?

kumbuka tumesoma kwamba matajiri walie tena wapige yowe, na

hapo tunaambiwa kunawatu wanaodai ni matajiri, na kweli ni matajiri

wa mali za dunia, Biblia ina wataka, inawapa ushauri, wanunue

dhahabu iliyosafishwa kwa moto, hii dhahabu iliyosafishwa ni

nini?anasema akisha inunua ndipo atakuwa tajiri, lakini hataki anadai

yeye tayari ni tajiri,

Silaha za Adui Samuel Imori

49

Akaendelea kumwelezea kwamba anunue mavazi meupe apate kuvaa

ili aibu ya uchi wake isionekane, kwa lugha nyingine yuko uchi,

akaendelea kumwambia anunue dawa ya kupaka macho yake yapate

kuona kwa lugha nyingine haoni. Mungu wetu anaendelea kutusaidia

ili tupate kuelewa kilicho mbele yetu, tuweze kukaa mkao

unaotakiwa, neno la Mungu linatukumbusha wazi kwamba mtu

ambaye ni tajiri katika ulimwengu huu, anayo magari, majumba na

mengine yote tunayoyafahamu, halafu hana Mungu, huyo mtu ni

maskini wa kutupwa,Yesu akamwambia Yule mtu aliyejitajirisha,

akavunja maghala madogo, akajenga makubwa, kisha akaiambia nafsi

yake ikae sasa ile, ifurahi,akifikiri ndio amefika, lakini neno la

Mungu likamjia likamwambia hivi:-“mpumbavu”likamwambia leo

hii wanaitaka roho yako, je mali hiyo ulijiwekea itakuwa ya nani?

Mistari hii ninayokupa hapa watu wengi hawapendi kusikia, lakini ni

ukweli usiopingika, mwanadamu aliandikiwa, ili kumkumbusha ya

kwamba anapita, anaelekea mahalipale alipopachagua, mstari

ulionifanya niwaze sana na kuendelea kutafuta kinacho waangamiza

watu wa Mungu ni ule ambao Mungu alimtumia mtumishi wake nabii

Hosea.

Hosea 4:65

“watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa”

Mungu wetu hapendi tuangamizwe ndio maana aliamua kutuma

watuishi wake ili wawasaidie watu wake wasiangamizwe, akawatoa

wengine mitume/manabii/wainjilisti/wachungaji/na waalimu.Baada

Silaha za Adui Samuel Imori

50

yakuwa amewatoa hao, kusudi wasaidiane, hao tena wanawapoteza

watu wake, na bado Mungu hajanyamaza anapiga kelele akisema

hivi.

Isaya9:16

Kwamaana wawaongozao watu hawa ndio wawakoseshao, na hao

walioongozwa na watuhao wameangamia.

Nimeendelea kurudia rudia kusema, jinsi Mungu wetu

anavyotupenda, jinsi asivyopenda tuangamie ndio maana akamleta

Yesu mwokozi.Naye akajitoa kwaajili yetu akatufia msalabani,

akaimwaga damu yake takatifu, akaifanya kazi ya ukombozi,

akatamka katika kinywa chake akiwa msalabani, maneno

kadhaa.Nivema tujifunze kutokana na hayo maneno aliyoyatamka

aliwaombea maadui zake akiwepo msalabani, alimkabidhi mama

yake kwa Yohana ili amtunze, alisikika akitamka waziwazi kwamba

”imekwisha” nimeyachukua hayo mambo matatu aliyoyasema akiwa

msalabani, ili yatufundishe, yatufungue tupate kujua tunavyotakiwa

kutumia vinywa vyetu na mida yetu tuliopewa na Mungu

kuishi.Sikumoja nilimuuliza kijana mmoja swali, naye alinijibu vizuri

kwa kulingana na uelewa wake.

Swali lilikuwa hivi: Yesu alikuja kufanya nini duniani?

Jibu: alikuja kutuokoa kwa kuimwaga damu yake msalabani.

Swali: je nihilotu pekeyake?au kuna jambo lingine?

Jibu: nadhani ni hilo tu,sidhani kamalipo jambo lingine.

Silaha za Adui Samuel Imori

51

Yawezekana hata wewe unalijua hilo jibu moja, zuri kabisa la kweli,

lakini kama ungeulizwa uitaje kazi nyingine au sababu nyingine

tofauti na hiyo ya kumwaga damu.Ungepata jibu la kujibu? au na

wewe ungejibu kama Yule kijana alivyonijibu kwamba hajui kazi

nyingine aliokuja kufanya duniani?

Yesu kristo alipokuja duniani alijisema wazi wazi kwamba ametoka

kwa Baba yaani Mungu, watu hawakumwamini, lakini alisema kweli,

akajielezea wazi wazi kwamba yeye ndiye njia kweli na uzima”

Yoh 14:6

Yesu akamwambia, mimi ndimi njia na kweli na uzima, mtu haji

kwa Baba ila kwa njia ya mimi.

Alikuwa anasemaje hapo? anasema wazi wazi kwamba mtu akitaka

afike kwa Baba yake, ambaye ndiye Mungu, muumba mbingu na

nchi, amtazame vile anavyotembea, vile anavyofanya naye afanye,

vile anavyosema naye aseme hivyo atafika, na kwa njia hiyo,

mtumishi wa Mungu Petro akatuandikia hivi:-

1Pt 2:21-23

Kwasababu ndiyo mliyoitiwa, maana kristo naye aliteswa kwaajili

yenu akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.Yeye hakutenda

dhambi wala hila haikuonekana kinywani mwake, yeye

alipotukanwa hakurudisha matukano alipoteswa hakuogofya, bali

alijikabidhi kwake ahukumuye kwa haki.

Silaha za Adui Samuel Imori

52

Nimechagua mambo matatu aliyo yatamka alipokuwa msalabani,

alikuwa ameyafundisha katika mafundisho yake, sasa akayaweka

kwenye vitendo.

Math 5:38-48

Mmesikia kwamba imenenwa jicho kwa jicho na jino kwa jino,

lakini mimi nawaambia, msishindane na mwovu, lakini mtu

akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili, na mtu atakaye

kushtaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia, na mtu

atakayekulazimisha mwendo wa maili moja nenda naye

mbili.Akuombaye mpe, naye atakaye kukopa kwako usimpe kisogo,

mmesikia kwamba imenenwa umpende jirani yako na umchukie

adui yako, lakini mimi nawaambia wapendeni adui zenu,

waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye

mbinguni, maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema,

huwanyeshea mvua wenye haki na wasiohaki, maana mkiwapenda

wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? hata watoza ushuru

je hawafanyi yayo hayo? Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu,

mwatenda tendo gani la ziada? hata watu wa mataifa je! Nao

hawafanyi kama hayo? Basi ninyi mtakuwa wakamilifu kama Baba

yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Nimetangulia kukuelezea kwamba Yesu alikuja duniani kutuonyesha

jinsi ya kutembea kuelekea kwa Baba yake, ndipo sa akasema “mimi

ndiye njia kweli na uzima”

Silaha za Adui Samuel Imori

53

Alifundisha jinsi ya kuwatendea maadui zetu, naye akawaombea

maadui walio mtukana msalabani ndipo alipofungua mdomo wake sio

kuwalaani, bali kuwaombea kwa Baba yake, ndipo akasema, “Baba

uwasamehe” Baada ya kuwa amewaombea maadui zake akatimiza

kile alichokuwa amekifundisha kumhusu adui.Alijua anaondoka, na

alikuwa anamheshimu mama yake, sio kumheshimu tu tunaona

alikuwa anamtunza, alitii neno la Mungu.

Waheshimu baba yako na mama yako.

Na sasa muda wake ulikuwa umefika tayari yuko msalabani,

hangeendelea tena kumhudumia mama yake, akamkabidhi kwa

Yohana, aliyekuwa mwanafunzi wake, aliyempenda.

Yoh 19:25-27

Na penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake

Yesu, na umbu la mama ye mariamu wa kiopa, na Mariamu

Magdalena, basi Yesu alipomuona mama yake, nayule mwanafunzi

aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake “Mama

tazama mwanao”, kisha akamwambia Yule mwanafunzi, tazama

mama yako, na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua

nyumbani kwake.

Waheshimu baba yako na mama yako ni amri ambayo Mungu

aliwapa wanadamu, akaendelea kusema kuwa ukiwaheshimu utapata

heri, na utaishi miaka mingi, Yesu alimuheshimu mzazi wake

hakutaka kumwacha hewani, siku tulizonazo wapo watu wengi

hawajali, hawaheshimu wazazi wao. Nikukumbushe tu kuwa wapo

Silaha za Adui Samuel Imori

54

wazazi wa aina mbili; wa kimwili na wa kiroho, wote ni wazazi

tunatakiwa kuwaheshimu kama tunataka tupate heri, kama tunataka

tuishi miaka mingi katika nchi tuliyopewa. Msomaji wangu bado

hujachelewa yawezekana wazazi wako wangali hai hawajatoka

ulimwenguni, nenda watafute kabla hawajaondoka, wakubariki,

mmoja akasema nenda wakutemee mate

Jambo la mwisho alilotamka ni “imekwisha” akiwa na maana

“nimemaliza” alikuwa anatangaza wazi kwamba amemaliza, aliijua

kazi iliyo mleta, ndio maana alisema imekwisha, alijua Baba yake

alimtuma kuja kufanya nini ,na huyo ndio ametutuma, kama tunataka

kuifurahisha mbingu sharti tujue tumetumwa kufanya nini, sharti

tujue ni nini kinaifurahisha mbingu, sikumoja wanafunzi wa Yesu

walirudi wanafurahi sana, wanashangilia, wakisema

“pepo wanatutii”

Yesu akawakataza kwamba hilo siyo la kufurahia, ila la kufurahia ni

hili”majina yenu yameandikwa mbinguni”yawezekana mimi na wewe

tunafurahia miujiza inayotendeka, mapepo yanavyotutii, magari

tunayoyaendesha, majumba makubwa tulio ya jenga, mavyeo

makubwa tulionayo, mapesa tuliojikusanyia, wakristo tulio

wakusanya, lakini isikie sauti ya Mungu inasema msifurahie hayo

Lk 10:20

Bali furahini yakwamba majina yenu yameandikwa mbinguni.

Silaha za Adui Samuel Imori

55

Ni hatari kubwa, na upumbavu mkubwa, kama tutafurahia hayo na

huku majina yetu hayapo huko mbinguni.Yawezekana tukafurahia

hayo yote kumbe majina ama hayajaandikwa ama yamefutwa.

Uf 3:5

Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta

kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake

mbele za Baba yangu, na mbele za malaika zake.

Yesu anatueleza jinsi tutakavyofanya majina yetu asiyafute ni pale

tutakaposhinda, tutakaposhinda nini? anasema yeye ashindaye, tuone

ashindaye nini?

Yoh 16:33

Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu,

ulimwenguni mnayodhiki, lakini jipeni moyo, mimi nimeushinda

ulimwengu.

Ndugu yangu mpendwa, ulimwengu unaendelea kuwavuta wanadamu

ili uende nao kubaya, kule katika lile ziwa la moto tulilolisoma hapo

mwanzoni.Yeye mwenyewe alitufundisha namna ya kutembea,

namna ya kutamka, mpaka akatamka “imekwisha”bado tutaendelea

kumsikiliza kutufundisha jinsi ya kutamka. Math 9:13

Lakini nendeni mkajifunze maana yake maneno haya, nataka

rehema, wala si sadaka, kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali

wenye dhambi.

Silaha za Adui Samuel Imori

56

Yesu kristo mwana wa Mungu aliyekuja akaishi kama mwanadamu

hapa duniani, alizijua sadaka, ndio maana anatamka wazi wazi ya

kwamba lengo lake, kusudi lake siyo sadaka, siyo fedha, kuhubiri

kwake siyo ni ili apate fedha, alilijua neno la Mungu, maana tulisoma

kwamba

“Msiwe na tabia yakupenda fedha”

Hapa anaonyesha wazi wazi kwamba lolote analolifanya sio kwa

sababu apate fedha, yaani fedha sio kipaumbele, ila kipaumbele ni

kuwatafuta wanadamu waliopotea awarudisha kwa muumba wao,

ndio maana akawaambia waende wajifunze, wasije wakamdhania

kwamba anatafuta fedha kutoka kwao.

2Kor12-14

Tazama hii ni mara yatatu ya mimi kuwa tayari kuja kwenu,wala

sitawalemea, maana, sivitafuti vitu vyenu bali nawatafuta ninyi,

maana haiwapasi watoto kuweka akiba kwa wazazi, bali wazazi kwa

watoto.

Bwana wetu Yesu kristo alitumwa na Baba yake, alipomaliza kazi

yake naye akawatuma watumishi wake, nao wanatamka wazi wazi

kwamba hawatafuti vitu, ya kwamba vitu sio kipaumbele, magari,

majumba, vyeo n.k bali wanatafuta roho za watu, ni rehema, maana

yake huruma, na wengi wametumbukia wakaingia kutaka mapato ya

aibu kama tulivyoona huko nyuma.

Silaha za Adui Samuel Imori

57

Math 12:7

Lakini kama mngalijua maana yake nini maneno haya, nataka

rehema, wala si sadaka, msingali walaumu wasio na hatia.

Bwana wetu aliendelea kusisitiza kwamba wapo watu wanalaumiwa

bila sababu yoyote, na akasema kusudi lake la kuja, la kuhubiri,

kusudi lake la kuombea wagonjwa, siyo fedha, hapana, ni huruma, na

msaada, ni kuzipata roho zao sio vitu vyao na wanafunzi wake pia

tunapaswa kufuata nyayo zake alizozipitia na hiyo ndio njia ya

kwenda kwa Baba yake, ambaye ndiye Mungu wa kweli.

Filp 3:17-19

Ndugu zangu, mnifuate mimi mkawatazame wao waendao kwa

kufuata mfano tulio wapa ninyi, maana wengi huenenda, ambao

nimewaambieni mara nyingi habari zao, kuwa niadui za msalaba

wa kristo, mwisho wao ni uharibifu muungu wao ni tumbo, utukufu

wao ukatika fedheha yao, waniao mambo ya duniani.Kwa maana

sisi wenyeji wetu uko mbinguni, kutoka huko tena tunamtazamia

mwokozi, Bwana wetu Yesu kristo atakaye ubadili mwili wetu wa

unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza

ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini

yake.

Mtumishi wa Mungu Paul alikuwa anawaonya ndugu zetu wafilipi

kwa machozi, maana walikuwapo watu ambao walikuwa wanadai

kwamba wana mtumikia Mungu. Kumbe walikuwa ni maadui wa

msalaba hawakutaka shida yeyote, walikuwa wanaye mungu wao

Silaha za Adui Samuel Imori

58

akawaelezea wazi wazi kwamba mungu wao alikuwa ndugu aitwaye

“tumbo”, wengi hata siku zetu tulizonazo Mungu tumbo

amewaendesha watu sana,wanamtumikia, na hana malipo atakayo

walipa, neno la Mungu linasema hivi” vyakula ni kwa tumbo”lakini

vyote vitatoweshwa, ndugu yangu mpendwa, haujachelewa bado

yawezekana ulikuwa una mtumikia muungu tumbo, waweza badilika,

naukampata Mungu wa kweli, muumba mbingu na nchi.Yeye

aliewapa wanadamu wachague watakapoishi milele. Zaburi49:16-

17

Usiogope mtu atakapopata utajiri, na fahari ya nyumba yake

itakapozidi, maana atakapokufa hatachukua chochote.

Mpendwa msomaji wangu, neno la Mungu ni kweli, na sisi tu

mashahidi kwamba tumewaona majiri wengi walio wahi kuwepo

chini ya jua, na mwisho wao walikufa, lakini ukweli unabaki pale

pale ya kwamba hawakuchukua kitu chochote, hata kimoja, kinyume

chake walifunikwa nguo moja tu, shuka nyeupe, jina la shuka hiyo ni

sanda, mmoja akasema ni nguo pekee yenye bei rahisi kuliko nguo

zote, baada ya kufunikwa nguo hiyo, wengine ndio imetoka hivyo,

wengine wanawekwa kwenye sanduku, kisha kaburi huchibwa na

mwili wa mtu huyo hushushwa mle ndani ndani, analazwa humo,

watu wamemzunguka, wapo wanaolia kiliokweli maana alikuwa

msaada kwao, wapo ambao wanalia ila ni kwa sababu wengine nao

wanalia, lakini kiuhalisia wanashukuru kimoyo moyo kwa kuwa

jamaa alikuwa ni kero kwao, wengine wanajipanga ni nini

watachukua, ndio maana unaona hawaishii hapo kumweka kaburini,

wanaleta nondo, wanaleta smenti. Huo ndio una kuwa mwisho wa

Silaha za Adui Samuel Imori

59

mtu huyo ama amesha fika kwa Mungu atakakokaa milele na milele.

Ama ameshafika kuzimu atakakokaa milele na milele, kama

nilivyokwisha kukuelezea kwamba Mungu wetu alitupatia tuchague,

bado tukiwa hai, lakini viongozi wetu wengine wakatudanganya, na

kweli tukadanganyika kwamba ukifa utaombewa, sasa unamsikia mtu

anaomba hivi

“ee Baba mpokee mtu huyo na umuweke mahali pema peponi”Huo ni

uongo mkubwa, niutapeli ni kuwadanganya wajinga, hakuna sala ya

jinsi hiyo chini ya jua, hakuna sala ya jinsi hiyo kama nilivyokwisha

kukuelezea yakwamba Yesu wetu ndiye njia na alipo kuja

alitufundisha mambo mengi moja wapo ni hilo la kuwaombea wafu,

hakusema popote kwamba mfu anaombewa, napenda tuone jinsi

alivyo lifundisha hilo

Lk 16:19-31

Akasema, palikuwa na mtu mmoja tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya

zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa, na masikini

mmoja jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda

vingi naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo

yalioanguka katika meza ya Yule tajiri hata mbwa wakaja

wakamlamba vidonda vyake, ikawa Yule masikini alikufa,

akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahim, Yule tajiri

naye akafa, akazikwa, basi kulekuzimu aliyainua macho yake

alipokuwa katika mateso akamwona Ibrahimu kwa mbali, na

Lazaro kifuani mwake, akalia akasema ee Baba Ibrahim,

nihurumie umtume Lazaro achovye ncha ya ya kidole chake

majini auburudishe ulimi wangu, kwa sababu ninateswa katika

Silaha za Adui Samuel Imori

60

moto huu, Ibrahim akasema, mwanangu kumbuka ya kwamba

wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na

Lazaro vivyo alipata mabaya, na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa,

na wewe unaumizwa, na zaidi ya hayo kati yetu sisi na ninyi

kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda

kwenu wasiweze, wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu,

akasema basi, baba yangu kwakuwa ninao ndugu watano ili

awashuhudie, wasije wao pia wakafka mahali hapa pa mateso,

Ibrahim akasema, wanao Musa na manabii, na wawasikilize wao.

Akasema la baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye

kwa wafu watatubu. Akawaambia wasipowasikia Musa na manabii,

hawata shawishiwa hata mtu akifufuka katika wafu.

Nilichotaka kukuonyesha hapa ni kuifahamu njia ya kwenda juu kwa

Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu kristo, alituelezea kwamba

ukichelewa kuchagua pale utakapoishi milele baada ya kufa kwako,

basi utakuwa umechelewa na ujue usipo mchagua Yesu aliye njia ya

uzima, basi elewa umemchagua moto wa milele na milele, hakuna

mahali pengine tofauti ambapo watu wataishi milele na milele tofauti

na mbinguni au motoni. Ameeleza vizuri alikuwepo mtu tajiri,

akawepo na mwingine maskini Lazaro, wote walikufa, Lazaro

alichukuliwa mpaka mapumzikoni tajiri naye akafa, akaenda

matesoni alipokuwa huko alijaribu kutafuta msaada kwa Ibrahim,

tumeona haukupatikana tumeendelea kumuona akawahurumia ndugu

zake aliokuwa amewaacha duniani, bado haikusaidia chochote

akajulishwa kwamba mtu anapokufa mambo yake yameishia hapo,

yale unayoyasikia ati tumuombee marehemu, ule ni upumbavu,

kwanini nimeuita upumbavu? mpumbavu amesema hakuna Mungu,

Silaha za Adui Samuel Imori

61

hiyo ndio sifa ya mpumbavu, nimemwita mpumbavu kwasababu

kuombea wafu nisawa na kusema hakuna Mungu, maana ka kweli

unasema Mungu yupo basi ungemtafuta, ungemuuliza ili akuelekeze

namna ya kuwaombea watu wale ambao bado hawajafa, sasa

unasubiri mtu afe, hukumwonya aache dhambi zake alipokuwa hai,

ukaendelea hata kupokea sadaka zake za wizi, za rushwa, za dhuluma

na hukumwonya, hukumwambia vile Mungu wake anataka aishi,

akiisha kufa ndio unamwambia Mungu amweke mahali pema. Mahali

pema wapi? Mshahara wa dhambi ni mauti, naomba tulielewe hilo

kabla hatujafa tutengeneze maisha yetu na Yesu atuokoe tutakuwa

tumechagua uzima wa milele na milele.

Mith 14:20

Masikini huchukiwa hata na jirani yake bali tajiri ana marafiki

wengi.

Niukweli usiopingika ya kwamba masikini huchukiwa hata na jirani,

ila tajiri anamarafiki wengi, katika kitabu changu cha vikwazo vya

kuurithi uzima wa milele ni meelezea kirefu habari ya marafiki, Neno

linasema usimwamini rafiki, nikaandika aina saba za marafiki,

ukisoma utaelewa vizuri, sasa kama wewe ni tajiri, elewa hivyo unao

marafiki wengi, humo humo hata wasaliti wako wamopia, Yesu

alikuwa na wanafunzi kumina mbili msaliti alikuwemo mmoja basi

wakiwa ishirini na nne watakuwa wapo wasaliti wawili, sasa neno

limesema kwamba tajiri anao marafiki wengi, kwa vyovyote pia

wasaliti niwengi.

Silaha za Adui Samuel Imori

62

Mith 18:23

Masikini hutumia maombi bali tajiri hujibu kwa ukali.

Hawa wawili ni wanadamu wote pengine umri wao ni mmoja,

pengine elimu yao ni moja, pengine kabila laoni moja, pengine urefu

wao au ufupiwao ni mmoja, pengine wote wanao watoto na wake pia,

lakini sikia kwakuwa mmoja nitajiri anajibu kwa ukali, nini

kinamfanya ajibu kwa ukali? ”utajiri”, utajiri ni nini?ni fedha,Yule

mwingine ni masikini, ametumia maombi, nini kinamfanya atumie

maombi amekosa nini fedha. Napenda kurudia rudia baadhi ya

sentensi ili usisahau, nilikueleza kuwa nakuonyesha baadhi ya

misemo au mafundisho ambayo Biblia inasemea kuhusu fedha.

Mith 19:4

Utajiri huongeza rafiki wengi, bali masikini hutengwa na rafiki

yake.

Mungu wetu hakuacha kutu patia taarifa, leo wapo matajiri ambao

wana marafiki wengi, wanaweza wasijue ni kwanini wana marafiki

wengi, kumbe nikwaajili ya utajiri, hii inamaana kuwa utajiri ukiisha

tu, na marafiki hao wala hatawaona, hii inamaanisha kwamba, sio

marafiki wakweli, katika kitabu change cha vikwazo sehemu ya

kwanza nimeelezea vizuri sana kirefu kuhusu aina ya marafiki,

nikawaelezea kwamba wako aina saba, hao wote inabidi tujifunze, ili

tuweze kujihadhari na marafiki wabovu wasio wazuri wanaweza

kutuangamiza

Silaha za Adui Samuel Imori

63

Ay 34:19

Sembuse huyo asiyependelea nyuso za wakuu, wala hawajali

matajiri kuliko masikini kwani wote nikazi ya mikono yake.

Bwana wetu aliwataarifu wanadamu wazi wazi kwamba yeye

hapendelei mtu kwa kuwa ni tajiri, anasema wote ni mali yake yeye,

na hili linatuhakikishia kwamba kweli Yesu alitoka kwa Mungu,

twaweza kuwaona wakimtembelea na kumwambuia jinsi

walivyokuwa wamemchunguza na kumjua, hakujisema ila

walimsema hivi,

Math 22:15-16

Ndipo mafarisayo wakaenda zao, wakafanya shauri jinsi ya

kumtega kwa maneno, wakatuma watu kwake wanafunzi wao

pamoja na maherodi wakasema mwalimu twajua yakuwa wewe ni

mtu wa kweli, na njia ya Mungu waifundisha katika kweli wala

hujali cheo cha mtu awaye yeyote kwa maana hutazami sura za

watu.

Watu hawa tumewasikia waziwazi wakimsalimia Yesu wakisema

jinsi alivyo lisema neno la Mungu katika kweli, bila unafiki, bila

kuficha ili mtu mwenyewe abaki kuamua, njia

Atakayeitembea wakamwambia kuwa wamemfahamu kwamba hajali

cheo cha mtu wala haangalii sura ya mtu awayoyoyote, laiti

watumishi wa Mungu wange mfanana, nao wangetambulikana kwa

jinsi hiyo, lakini tofauti kubwa ipo leo kati ya matajiri na masikini,

niombi langu Mungu atusaidie kwa njia ya Roho mtakatifu.

Silaha za Adui Samuel Imori

64

Yer 9:23-24

Bwana asema hivi,mwenye hekima asijisifu kwasababu ya hekima

yake,wala mwenye nguvu asijisifu kwasababu ya nguvu zake,wala

tajiri asijisifu kwaajili ya utajiri wake, bali ajisifuye na ajisifu

kwasababu hii ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, yakuwa

mimi ni Bwana, nitendaye mema, na hukumu, na haki katika nchi,

maana mimi napendezwa na mambo hayo asema Bwana.

Yaangalie vizuri maagizo hayo, Mungu wetu alipowatazama

wanadamu aliwaangalia akakuta wanajisifu, kila mmoja alikutwa

analo la kujisifia, wengine urefu wao, wengine unene wao, wengine

elimu yao ,wengine vyeo vyao, wengine nyumba zao, wengine

magari yao, ndipo akawahurumia wote, akawasaidia wapate kujua,

nikipi ambacho mtu anapaswa ajisifie, alikuta wengine wanajisifia

dini zao,wengine wanasema dini yetu ni kubwa ,wengine wanasema

dini yetu niya kwanza wengine niya pili n.k. yeye akawahurumia

akawaambia mtu yeyote akitaka kujisifia, kujisifu kutakakokuwa kwa

maana ni Yule aishie kunifahamu, anijue mimi, ajue mimi nataka

nini, ajue maagizo yangu kwa wanadamu, hivyo atakuwa kheri huyo

atakuwa amechagua fungu jema.

Yak 1:9-11

Lakini ndugu asiye na cheo afurahi kwa kuwa ametukuzwa, bali

tajiri kwakuwa ameshushwa, kwa maana kama ua la majani

atatoweka, maana jua huchomoza kwa hari, huya kausha majani,

ua lake hunyauka uzuri wa umbo lake hupotea, vivyo hivyo naye

tajiri atanyauka katika njia zake.

Silaha za Adui Samuel Imori

65

Neno la Mungu limeendelea kumsaidia tajiri ajifahamu, utajiri usije

ukamziba masikio, usije ukamziba macho yake asione,

akalinganishwa na majani, maua jinsi yanavyo weza kupendeza,

kumeremeta kwa rangi mbalimbali, na jinsi yanavyoweza kunukia

vizuri lakini jua likichomoza, likilipiga lile ua jani lake linainama na

kuanguka uzuri wake wote, unaishia hapo, harufu nzuri yote inaishia

hapondipo likafananishwa na tajiri aliyechanua, alie utegemea utajiri

wake, alie jisifia utajiri, bila kumtegemea Mungu ,utajiri aliojisifia,

asijisifie kumjua Mungu kama tulivyosoma hapo juu.

Mdo 5:1-11

Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe,

aliuza mali.Akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake mkewe naye

akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume,

Petro akasema, Anania kwanini shetani akujaza moyo wako

kumwambia uongo Roho mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya

thamani ya kiwanja. Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? na

kilipokuwa kimeisha kuuzwa, thamani yake haikuwa uwezo wako?

Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia

uongo mwanadamu bali Mungu, Anania aliposikia maneno hayo

akaanguka akafa, hofu nyingi ikawapata watuwote walioyasikia

haya, vijana wakaondoka wakamtia katika sanda, wakamchukua

nje wakamzika, hata muda wa saa tatu baadae mkewe akaingia

naye hana habari ya hayo yaliotokea. Petro akamjibu, niambie

mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? akasema ndio kwa thamani

hiyo, Petro akamwambia imekuwaje hata mkapatana kumjaribu

Silaha za Adui Samuel Imori

66

Roho wa Bwana? angalia miguu ya walio mzika mumeo iko

malangoni,nao watakuchukua nje wewe nawe, mara akaanguka

miguuni pake akafa wale vijana wakaingia, wakamkuta amekufa

wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe, hofu nyingi

ikawapata kanisa lote nawatu wote walioyasikia hayo.

Msomaji mpendwa, tumeendelea kuiona hiistoria ya mtu mmoja

aliyekuwa kanisani wakati wake

mtume Petro, mtu huyu walikaachini, wakashauriana na mke wake,

wakaamua kuuza mali yao ambayo ni kiwanja, baada ya kukiuza,

wakashauriana kwamba wapeleke sehemu tu ya fedha kanisani,

zingine wafiche na ndiyo walifanya lakini Roho wa Mungu ndani ya

mtume Petro aliuona ule udanganyifu, akamuuliza wazi aeleze fedha

waliouza kile kiwanja, Anania hakuwa na roho ya toba, aliendelea

kudanganya hata mbele ya mtumishi wa Mungu Petro, tunaona

matokeo yake alikufa, hakuweza kutubu, na mkewake pia aliendelea

kuficha wizi waliokuwa wameufanya, naye pia tunaona kile kilicho

mtokea,wote wakawa wameangamizwa, kwa kuwa walikosa maarifa,

waliipenda fedha, wakaificha, laiti wangekuwa wameitii sauti hiyo

iliyo waambia wasiipende fedha mwisho wao hawa watu wawili

haukuwa mzuri kama tulivyoona.Jambo hili litufundishe, na Roho

mtakatifu atusaidie, mioyo yetu iwe mioyo ya nyama, mioyo yenye

toba, mioyo iliyo tayari kumrudia Mungu pale tunapogundua

tumekosea, moyo wa Anania uliendelea kuwa mgumu na moyo wa

Safira mke wake pia wote wakakutwa namauti. Mioyo yetu

inatakiwa iwe mioyo ya nyama.

Mark 4:13- 20

Silaha za Adui Samuel Imori

67

Akawaambia hamjui mfano huu? basi mifano yote mtaitambuaje?

mpanzi huyo hulipanda neno, nao wakiisha kusiia mara huja

shetani akaliondoa lile neno lililopandwa mioyoni mwao, kadhalika

na hawa ndio wapandao penye miamba, ambao kwamba wakiisha

kulisikia lile neno, mara hulipokea kwa furaha , ila hawana mizizi

ndani yao, hali hudumu muda mchache, kasha ikitokea dhiki au

udhia kwa ajili ya lile neno mara hujikwaa, na hawa ndio wale

wapandwao penye miiba, ni watu walisikiao lile neno, na shughuli

za dunia na udanganyifu wa mali , na tama za mambo mengine

zikiingia hulisonga lile neno likawa halizai na hawa ndio

waliopandwa penye udongo ulio mzuri, ni watu wasikiao lile neno

na kulipokea, na kuzaa matunda, mmoja thelathini, mmoja sitini na

mmoja mia.

Katika habari za maandalio ya moyo, ili neno lipandwe

yanamtegemea muandaaji, kama tulivyoona ya kwamba ipo aina nne

ya mioyo, upo moyo ambao unaruhusu udanganyifu wa mali,

zinausonga unakuwa hauzai, hii yote inatufundisha tujikague,

tuiandae mioyo yetu vizuri, ili neno linapopandwa lipate kuzaa

matunda.

Mith 16:1

Maandalio ya moyo niya mwanadamu, bali jawabu la ulimi latoka

kwa Bwana.

Mungu atusaidie tuiandae mioyo yetu iwe mioyo inayo lipokea neno

la Mungu kwa unyenyekevu, na tuweze kulitii, tuweze kutenda vile

linavyo tuagiza. Hapo tutaitwa kheri, kama nilivyosema kwamba

Silaha za Adui Samuel Imori

68

yapo maandiko mengine ni magumu, hata watu hawayapendi

kuyasikia, lakini maadamu yameandikwa, ni kwa ajili ya

mwanadamu, ili ayafanye au yamuonye, yamwadhibishe awe mtu

mkamilifu.

Lk 6:24

Lakini olewenu ninyi mlio na mali kwa kuwa faraja yenu

mmekwishakuipata ole wenu ninyi ambao mmeshiba sasa, ole wenu

ninyi mnao cheka sasa, kwa kuwa mtaomboleza na kulia, ole wenu

ninyi watu wote watakapowasifu kwa kuwa baba zao walitenda

manabii wa uongo mambo kama hayo.

Neno linasemaje?Walio na mali tayari wamepata faraja, kumbe mali

inaleta faraja, hapo tunatakiwa tusiridhike na faraja ile ambayo mali

inaileta wale walioshiba wanaambiwa ole, maana yake tusije

tukashiba tukajisahau, mmoja alipo shiba alitamka kwamba

hataondoshwa pia wanaocheka sasa wanaambiwa ole wao, uwe

makini, unapocheka, jiulize nini kinakuchekesha? neno linasema kila

jambo lina majira, unapocheka ujue ipo siku utalia, kama utakumbuka

vizuri, nilikuelezea hivi Mungu alipokusudia kuwabariki watu wake

wakati alipo watoa misri, aliwapa anyo, akasema

”JIHADHARINI”alianza na jambo hilo, kasha akawaambia huko

mnakokwenda, ninao mpango mzuri kabisa, kuwabariki katika

sikuzenu za mwisho, malizenu zitaongezeka na chochote mlicho

nacho kitaongezeka, akawaambia muwe makini, mthibiti mioyo yenu

isije ikainuka, mkashikwa na kiburi, mkanisahau.Mwanadamu ni

mwepesi sana wa kusahau anapopata raha kidogo, ni mwepesi

kusahau alikotoka, anapotajirika tu nirahisi kujisahau na kwa sababu

Silaha za Adui Samuel Imori

69

hiyo basi Mungu alimtumia mhubiri, kuwakumbusha wanadamu

kama ambavyo nakumbusha leo hivi hakuna jambo la kudumu chini

ya jua, kila jambo wanalopitia wanadamu ni la muda, vile ambavyo

mwanadamu sio wakudumu,basi hata hali aina yoyote anayoipitia sio

ya kudumu, uwe umasikini,utajiri,kiwe kilio au kicheko n.k

Mh 3:1-9

Kwa kila jambo kuna majira yake, na wakati katika kila kusudi

chini ya mbingu:-

-wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa

-wakati wa kupanda na wakati wa kung’oa yalio pandwa

-wakati wa kuua na wakati wa kupoza

-wakati wa kubomoa na wakati wa kujenga

-wakati wakulia na wakati wakucheka

-wakati wakuomboleza na wakati wa kucheza

-wakati wakutupa mawe na wakati wa kukusanya mawe

-wakati wakukumbatia na wakati wakuto kukumbatia

-wakati wakutafuta na wakati wa kupoteza.

-wakati wakueweka na wakati wa kupoteza

-wakati wa kurarua na wakati wa kushona

Silaha za Adui Samuel Imori

70

-wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia

-wakati wa kunyamaza na wakati wa kunena

-wakati wa vita na wakati wa amani

Je mtendaji anayo faida gani katika yale anayo jishughulisha nayo?

mistari hii yote kama utaisoma kwa utulivu, naamini utapata amani,

hutahangaika sana, maana imepangwa na mwenye kuumba

ulimwengu huu, ninachoomba ufananishe hivi, mchana una saa kumi

na mbili, maana yake nini? Mchana ukiisha pita umepita, lazima uje

usiku, na usiku ukiisha pita umepita,lazima uje mchana, napenda

tuendelee kujifunza kwamba lile alilolipanga Mungu ndilo

litakalotendeka, ndio maana Yesu alipokuwa anaomba ili kikombe

kimuepuke, alimpa Mungu nafasi ya kuingilia kati pale aliposema

hivi ”sikama nitakavyo, bali mapenzi yako yatimizwe” napenda

tujifunze kwamba hata kuku wote wangekusanyika,watangaze ngoma

waamuwe kwamba hawatawika, napenda nikwambie kutakucha

tuu.Wanaweza wakadhani hivi, kwa kuwa wanadamu wana wataja

taja wakati mwingine wanasema kabla ya majogoo tuondoke, hata

Bwana Yesu alitaja hivi:- Petro kabla ya kuwika jogoo utanikana

mara tatu, kwa hiyo jogoo anaweza dhani kwamba asipowika

hakutakucha, ndivyo ilivyo kwetu wanadamu kila jambo linamajira

yake, kwa maana hiyo basi, wakati wa kucheka unapofika, cheka

ukijua hautacheka milele, wakati wa kulia ukifika, lia ukijua hautalia

milele, wakati wa umaskini hauwezi kuwa masikini milele. Msomaji

wangu mpendwa usipoyaelewa haya, hali iwayoyote inaweza

ikakufanya ukakata tama, wapo waliowahi kuwa matajiri sana na leo

hawana kitu tena, wamebaki watu wa kawaida, wapo watu waliwahi

Silaha za Adui Samuel Imori

71

kuwa masikini mpaka wakafikia msemo usemao ati masikini wa

kutupwa, lakini leo watu hao nimatajiri wa kupindukia, na endelea

kukuonyesha vile fedha au mali zinavyoweza kutumiwa na adui yetu

zikafanyika mnyoo wa kumwangamiza mwanadamu kama

tulivyosoma kwenye maandiko kwamba,” Hos 4:6a watu wangu

wanaangamizwa kwa kukosa maarifa”

2Falme 5:20

Lakini Gehazi, mtumishi wa Elisha mtu wa Mungu

akasema.Tazama Bwana wangu amemwachilia huyo Naamani

Mshami, asivipokee mikononimwake vile vitu alivyovileta, kama

Bwana aishivyo, mimi nitamfuata mbio nipokee kitu kwake.Basi

Gehazi akamfuata Naaman, naye Naaman alipomwona mtu

apigaye mbio anakuja mbio nyuma yake, alishuka garini amlaki,

akasema je niamani? akasema, amani, Bwana wangu amenituma

kusema tanzama, sasa hivi wamenijia, kutoka milimani mwa

Efraimu vijana wawili wawana wa manabii, uwape nakuomba

talanta mbili, akamshurutisha, akafunga talanta mbili za fedha

ndani ya mifuko miwili, na mavazi mawili, akawatwika watumishi

wake wawili, nao wakayachukua mbele yake, naye alipofika

kilimani, alivitwaa mikononi mwao, akaviweka nyumbani

akawaacha wale watu kuondoka nao wakaenda zao, lakini yeye

akaingia, akasimama mbele za bwana wake, Elisha

akamwambia,watoka wapi Gehazi? Akanena mtumwa wako

hakwenda mahali, akamwambia je moyo wangu haukwenda na

wewe, hapo alipogeuka Yule mtu katika gari ili akulaki? je huu

ndio wakati wa kupokea fedha na kupokea mavazi,na mashamba ya

Silaha za Adui Samuel Imori

72

mizeituni na mzabibu na kondoo na ng’ombe na watumwa na

wajakazi? Basi ukoma wa naaman utakushika wewe na wazao

wako hata milele naye akatoka usoni pake mwenye ukoma kama

theluji.

Msomaji wangu mpendwa, hapojuu tunayo mambo mengi mno

yakujifunza, huyo mtumishi wa Elisha, ambaye jina lake ni Gehazi,

yeye kama tulivyo msoma alikuwa ana mtumikia Elisha, na Elisha

alikuwa anamtumikia Mungu, sikumoja alikuja mgonjwa wa ukoma

kumtembelea ili amponye, kutoka nchi ya Sham, alipofika alimkuta

Gehazi akiwa mlinzi na mtumishi wa Mungu

Elisha alikuwa ndani, Naaman aliomba aonane na Elisha, kwa hiyo

Gehazi aliingia ndani kwa Elisha akampa taarifa kwamba yupo mtu

nje, mtu mkubwa mwenye cheo amefuatana na msafara wake ana

ukoma, anataka kukuona, mtumishi wa Mungu Elisha hakubabaishwa

na cheo hicho, wala hakubabaishwa na zawadi, (sadaka) alizokuwa

nazo, akampatia Gehazi maelezo alimwambia aende katika mto

Yordani akajichovye mara saba, halafu aende kwao Ushamini, Gehazi

akayapokea hayo maelekezo, akayapeleka kwa Naaman, Naaman

aliposikia hivyo hakupendezwa alionekana kulalamika,akisema

maneno yafuatayo:-mimi nilizanikwamba angenijali angenitetemekea

mm ebu tone vile alivyojibu katika maandiko.

2Falm 5:11

Lakini Naamani akakasirika akaondoka akasema.Tazama

nalidhani bila shaka atatoka kwangu na kusimama, na kuomba

kwa jina la Bwana Mungu wake, na kupitisha mkono wake mahali

Silaha za Adui Samuel Imori

73

penye ugonjwa, na kuniponya mimi mwenye ukoma, je abana na

farpari, mito ya dameski, si bora kuliko maji yote ya Israel, je

siwezi kujiosha ndani yake, na kuwa safi? akageuka akaondoka

kwa hasira.

Naaman alikuwa mgonjwa wa ukoma ameenda kwa mtumishi wa

Mungu Elisha ilia pate msaada, na Mtumishi wa Mungu

amemwelekeza mtumishi wake Gehazi ampatie maelekezo naye

amempatia maelekezo, lakini yamemkasirisha, ameamua kuondoka

na ukoma wake, alichodai ni kwamba Elisha hakutoka amshike

amwombee, utakumbuka nilikueleza jinsi watu walivyo msalimia

Bwana wetu Yesu, wewe umtu wa kweli, njia ya Mungu waifundisha

katika kweli, hujali cheo cha mtu awaeyeyote, hutazami sura za watu.

Math 22:15-16

Mtumishi wa Mungu Elisha, hakutishwa na cheo cha Naaman, kama

vile maandiko yanenavyo kwamba Bwana wetu Yesu hakujali cheo

cha mtu wala sura za watu msomaji wangu, mwisho tunaona Naaman

anakubali akaenda akajichovya katika mto Yordan, nyama ya mwili

wake ikawa laini, ukoma ukamwacha, alifurahi sana, alikuwa tayari

kukutana na Elisha ampatie sadaka, alipofika alimkuta Gehazi,

akamuelezea kwamba tayari ni mzima, na alikuwa anataka aingie

amuone Elisha, si kumuona tu na kumpatia fedha, napenda tuendelee

kujifunza kwake, utakumbuka imeandikwa kwamba tumejengwa

katika misingi ya mitume na manabii, Bwana Yesu akiwa jiwe kuu la

pembeni.

Silaha za Adui Samuel Imori

74

2Falm 5:15

Akamrudia Yule mtu wa Mungu, yeye na mafuatano yake yote,

akaja akasimama mbele yake akasema, sasa tazama, najua ya

kwamba hakuna Mungu duniani mwote ila katika Israel, basi

nakuomba upokee mbaraka kwa mtumwa wako, lakini akasema,

kama Bwana aishivyo ambae nimesimama mbele zake sipokei kitu,

akamshurutisha apokee lakini akakataa Naamani akasema kama

sivyo lakini mtumwa wako na apewe mzigo wa udongo wa baghala

wawili, kwa maana mtumwa wako hatatoa tena sadaka ya

kuteketezwa wala dhabihu kwa miungu mingine ila kwa Bwana,

jambo hili Bwana amwachilie mtumwa wako, bwana wangu

akiingia nyumbani mwa Rimoni ili aabudu humo naye akitegemea

mkononi mwangu, nami nikijiinama nyumbani mwa Rimoni hapo

ninapojiinama nyumbani mwa Rimoni, Bwana amwachilie

mtumwa wako jambo hili, akamwambia, enenda kwa amani basi

akamwondokea mbali kidogo.

Naamini umeyasikia majibizano ya Naaman na mtumishi wa Mungu

aliyejuu Elisha,alilazimishwa na Naaman achukue zawadi lakini

Elisha alikataa katakata, nikwanini alikataa mali, fedha, dhahabu?

nilikwambia kilajambo lina majira yake hata kupokea nako yako

majira yake, upo wakati wa kupokea na wakati wa kuto kupokea,

hivyo ndivyo tunatakiwa kufahamu, wakati mwingine utayapokea

mapato ya aibu, wakati mwingine utamuuza Yesu kama Yuda

alivyomuuza kwa vipande thelathini,wakati mwingine utamwombea

mtu atapona, naye atamanio alipie huo uponyaji, nawe kwakuwa

unaitamani pesa na utamwambia anatakiwa alipie kiasigani, naye

Silaha za Adui Samuel Imori

75

akitoka hapo atajua, atawaza, kwamba huyu Mungu thamani yake ni

vipande thelathini, mwishowake utakuwaje? Fuatilia mwisho wa yuda

ulivyokuwa,wala haukuwa mzuri, alimaliza vibaya.Haponapo

tumemuona Gehazi, akiwaza moyoni mwake jinsi ya kupokea ile mali

alioikataa Elisha, naona Gehazi hakujua alichokuwa anafanya pale

kwa Elisha, labda hakuwa ameambiwa kwamba yukopale kujifunza

namna ya kumtumikia Mungu, alitakiwa kuwa makini sana,

kumwangalia Elisha anavyotumika. Alikataa sadaka zile za Naaman,

naye alipaswa kuziepuka, lakini kwakuwa hakuelewa somo hilo,

akajaribiwa, akazikimbilia, akazipokea kwa kudanganya kwamba

ametumwa na Elisha, akasema uongo na kilichotokea ni kibaya sana,

utakumbuka kwamba Elisha alikuwa ametumika chini ya Elia kwa

muda mrefu bila kuchoka, mpaka akafaulu kuupata upako ulio

kuwepo ndani ya Elia, na Gehazi naye alikuwa ametumika kwa muda

chini ya Elisha akitegemea kuupata upako uliokuwepo ndani ya

Elisha, matokeo yake tumeyaona alipodanganya, akakimbilia fedha,

dhahabu, Elisha alijisikia vibaya sana, akakumbuka muda alioupoteza

kumfundisha, moyo wake ukataabika ikamlazimu auite ule ukoma wa

Naaman, nao ukatii wito ukaja akauweka kwa Gehazi aliyekuwa

mtumishi wake, msomaji wangu huo ndio ulikuwa mwisho wa

Gehazi, alianza vizuri ,aliona miujiza mingi aliyoitenda mtumishi wa

Mungu Elisha, akitumiwa na Mungu,lakini haikumsaidia, haikugeuza

moyo wake usitamani fedha kama tulivyosoma huko nyuma kwamba

tusiipende fedha, tumeiona fedha ikifanyika mnyoo wa kumvua

Gehazi. Kutoka kwenye eneo lake la kuishi, maana alikuwa

anamtumikia Elisha mtumishi wa Mungu aliye hai, yeye Gehazi

aliishia kuchuma ukoma. Mafundisho ya Mungu wetu ni mazuri

kuliko fedha, lakini watu wengi wanapenda fedha kuliko mafundisho

Silaha za Adui Samuel Imori

76

ya neno la Mungu, jipime wewe unapenda nini kati ya mafundisho ya

Mungu na fedha na dhahabu? kuwa muwazi unapojibu.

Mith 8:10

Pokea mafundisho yangu wala sio fedha, na maarifa kuliko

dhahabu safi.

Neno la Mungu wetu linatushauri tupokee mafundisho ya Mungu,

tupokee maarifa ili tusiangamie, kumbuka mstari ule mzito

Hosea 4:6a

Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa.

Watu wengi kwa kupenda fedha na kuchukia mafundisho,

kilichofuata ni kukosa maarifa, na walipokosa maarifa, bila shaka

umesikia kilichofuata niwazi waliangamia.Wanadamu wanapenda

utajiri, lakini upo utajiri usio na mwisho ni utajiri gani huo?

Mith 8:18

Utajiri na heshima ziko kwangu, naam, utajiri udumuo na haki pia

Nimeendelea kukuonyesha, nabado tunaendelea kuuona, tukaona kila

jambo lina majira yake, tukauona hatautajiri na majira yake, aweza

mtu aliekuwa tajiri akawa masikini kama tulivyoona huko nyuma na

sasa tumekutana na utajiri ule udumuo, utajiri usio na mwisho, mimi

ningependa kuupata huo utajiri usio na mwisho utajiri udumuo milele

na milele ni upi huo?

Silaha za Adui Samuel Imori

77

Math 13:45-46

Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara,

mwenye kutafuta lulu nzuri, naye alipoona lulu moja ya thamani

kubwa, alikwenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua.

Napenda kuyarudia rudia mambo mengine ili yaweze kukaa, ili

yaweze kueleweka zaidi.Lulu ni aina ya madini yenye thamani sana,

Bwana akaitolea mfano yakwamba mfanya biashara mmoja

ilimlazimu afanye jambo aliloliona kwamba ni la muhimu sana

kwake, Yawezekana watu wengine hata wafanyabiashara wengine

waliokuwa wenzake hawakumwelewa kabisa, pengine walimbatiza

hata majina kadri walivyoona kwamba inafaa, tumesoma vizuri kuwa

alikuwa katika shughuli zake za kilasiku, akitafuta biashara zake,

alikuwa anatafuta lulu, siku moja akakutana na lulu ya thaman kubwa

tena moja tu, ilimlazimu afanye jambo alienda akauza vitu vyake

vyote alivyokuwa navyo vyoote, fedha alioipata, ilitosha anunulie ile

lulu moja tu kwa sababu ilikuwa ya thamani kubwa,

haikulimganishwa na kitu chochote alichokuwa nacho, ikabidi auze

vyooote. Nimemkumbuka kijana mmoja aliyeambiwa na Bwana Yesu

kwamba akitaka kuurithi uzima wa milele, aende akauze mali zake,

akiisha kuuza awagawie masikini halafu arudi aje kwa Bwana Yesu

apate kuurithi uzima wa milele, Biblia inasema kijana akakasirika

akaukunja uso wake akaondoka.Lakini mfanya biashara wa lulu

alifaulu. Alijinyenyekeza, akashuka, na huo ndio moyo wa Mungu,

ndivyo Yesu alivyotufundisha kwa mujibu wa maandiko yafuatayo

Silaha za Adui Samuel Imori

78

Filp 2:8

Tena alipoonekana ana umbo kama mwanadmu, alijinyenyekeza

akawa mtii hata mauti, naam mauti ya msalaba, kwahiyo tena

Mungu alimwadhimisha mno akamkirimia jina lile lipitalo kila

jina, ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni na

vya duniani, na vya chini ya nchi, na kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu

Kristo ni Bwana kwa utukufu wa Mungu Baba.

Mwana wa Mungu alie toka mbinguni, yeye alijinyenyekeza akawa

mtii, mahali pengine tunasoma wazi wazi kwamba alionewa na

akanyenyekea wala hakufunua kinywa chake, hata nimeukumbuka

wimbo tuliokuwa tunaimba zamani, tuliimba hivi, nanukuu

“Yesu kristo alikuwa na uwezo wa kupiga,

Lakini yeye alipopigwa alinyamaza kimya,

Alikuwa na uwezo wa kusema,

Lakini yeye aliposemwa alinyamaza kimya”

Linganisha mistari hiyo, hii hapa chini

Mith 18-23

Masikini hutumia maombi, bali tajiri hujibu kwa ukali.

Maneno ya mungu ni magumu ndio maana Yesu akawataka wasitoke

yerusalemu, bali wamungoje Roho mtakatifu aje awasaidie.nikwanini

tajiri anajibu kwa ukali?kwanini asitumie maombi, kwanini

Silaha za Adui Samuel Imori

79

asinyamaze? nini kinamsukuma ajibu kwa ukali? nimali aliyonayo,

imo kwenye moyo imemfundisha kwamba yeye ni bora kuliko mtu

mwingine, hana muda wa kujibu kwa upole, bali hujibu kwa ukali,h

awezi kujinyenyekeza, mtu akishiindwa kujinyenyekeza huyo moja

kwa moja anaendeshwa na kiburi, kikubwa ndicho kilimfanya licifer

atupwe chini, kiburi kikiwa ndani ya mtu kinamfundisha kwamba

yeye nibora kuliko mtu mwingine yeyote kiburi kikimpata mtu, huyo

ataishia kuangamia tu, hapo ndipo Lucifer alipo ishia.Mnyoo

mwingine ambao shetani anautumia kummaliza mwanadamu, mtu wa

kiburi utamjua katika kauli zake, mwenendo wake. Muasisi wa kiburi

ni Lucifer, amewaambukiza wengi, wenzetu waliotutangulia

walikisemea sana sana, nitakupatia maandiko machache

yanayoongelea kiburi, yako mengi ila nitakupatia machache.

Mith 8:13

kumcha Bwana ni kuchukia uovu kiburi na majivuno, na njia

mbovu na kinywa cha ukaidi pia nakuchukia.

Zab 10:2

Kwa kiburi chake asiye haki, mnyonge anafuatiwa kwa ukali, na

wanaswe kwa hila zizohizo walizoziwaza

Zab 12:3

Bwana ataikata midomo yote ya kujipendekeza, nao ulimi unenao

maneno ya kiburi

Silaha za Adui Samuel Imori

80

Zab 18:27

Maana wewe utawaokoa watu wanaoonewa, na macho ya kiburi

utayathiri.

Zab 19:13

Umzuie mtumishiwako asitende mambo ya kiburi, yasinitawale

mimi, ndipo nitakapokuwa kamili name nitakuwa safi, sina kosa

lililokubwa.

Zab 31:18

Midomo ya uongo iwe na ububu imneneayo mwenye haki maneno

ya kiburi kwa majivuno na dharau.

Zab 31:23

Mpendeni Bwana, ninyi nyote mliowatauwa wake, Bwana

huwahifadhi waaminifu humlipa atendaye kiburi malipo tele.

Zab 56:2

Adui zangu wanataka kunimeza mchana kutwa, maana waletao vita

juu yangu kwa kiburi ni wengi.

ZAB 73:6

Hivyo kiburi kimekuwa mkufu shingoni mwake, jeuri huwavika

kama nguo

Zab 101:5

Silaha za Adui Samuel Imori

81

Amsingiziaye jirani yake kwa siri huyo nitamharibu, mwenye

macho ya kiburi na moyo wa majivuno, huyo sitavumilia naye.

Zab 119:85

Wenye kiburi wamenichimbia mashimo ambao hawaifuati sharia

yako

Zab 119:122

Uwe mdhamini wa mtumishi wako apate mema, wenye kiburi

wasinionee.

Mpendwa msomaji wangu, tumeendelea kuona jinsi watu wa Mungu

wanavyoangamizwa kwa kukosa maarifa, Mungu wetu hapendi mtu

yeyote apotee, anatupenda mno, haya nimeyaeleza jinsi aduii yetu

anavyo waangamiza watu wa Mungu, ziko njia mbalimbali

anazotumia, sitaweza kuzielezea zote, ila zile chache ambazo

nimejaliwa kuzielezea, naamini macho yako yamefunguliwa,

umeziona na kama umeziona naamini utachukua hatua ya kujiweka

vizuri ili Yule adui yetu asikunase, na wewe uliye naswa tayari kwa

kuwa hukujua, naamini haujachelewa maadam unapumua, waweza

kabisa ukaamua kumtii Mungu na ukampinga huyo adui yetu, naye

atakimbia na utakuwa umebaki salama.

Rum 16:17-20

Ndugu zangu nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na

mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliojifunza,

mkajiepushe nao, kwa sababu waliohivyo hawamtumikii Bwana

Silaha za Adui Samuel Imori

82

wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe, na kwa maneno laini na

ya kujipendekeza waidanganya

mioyo ya watu wanyoofu, maana utii wenu umewafikilia watu wote,

basi nafurahi kwaajili yenu, lakni nataka ninyi kuwa wenye hekima

katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya naye

Mungu wa amani atamseta shetani chini ya miguu yenu

upesi.Neema ya Bwana wetu Yesu kristo na iwe pamoja nanyi

amen.

Luk 4:1-13

Na Yesu, hali amejaa Roho mtakatifu, alirudi kutoka Yordan,

akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani akijaribiwa

na ibilisi, na siku hizo alikuwa hali kitu, hata zilipotimia aliona

njaa, ibilisi akamwambia, ukiwa ndiwe mwana wa Mungu, liambie

jiwe hili liwe mkate Yesu akamjibu imeandikwa ya kwamba mtu

hataishi kwa mkate tu.Akampandisha juu, akamwonyesha milki

zote za ulimwengu kwa dakika moja,ibilisi akamwambia, nitakupa

wewe enzi hii yote na fahari yake kwa kuwa imo mikononi mwangu,

nami humpa yeyote kama nipendavyo, basi wewe ukisujudu mbele

yangu yopte yatakuwa yako. Yesu akajibu akamwambia,

imeandikwa msujudie Bwana Mungu, umwabudu yeye peke yake,

akamwongoza mpaka Yerusalemu akamuweka juu ya kilele cha

hekalu akamwambia, ukiwa ndiwe mwana wa Mungu jitupe chini,

kwamaana imeandikwa, atakuagizia malaika zake wakulinde, na ya

kwamba mikononi mwao watakuchukua usije ukajikwaa mguu

Silaha za Adui Samuel Imori

83

wako katika jiwe, Yesu akajibu akamwambia imenenwa usimjaribu

Bwana Mungu wako, basi alipomaliza kila jambo, ibilisi

akamwacha akaenda zake kwa muda.

Msomaji wangu mpendwa, Mungu wetu atusaidie tupate kuelewa,

tupate kufundishika, mwalimu wetu aliyekuja duniani kututolea damu

yake, yeye alitufundisha namna ya kuishi katika dunia hii, na kuufikia

ushindi, alikutana na adui yetu ibilisi na akahojiana nanaye, mwisho

akashinda alimjaribu kwa mambo yafuatayo” ibilisi akamwambia

ikiwa ndiwe mwana wa Mungu liambie jiwe hili liwe mkate, Yesu

akajibu imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu” “Ibilisi

akamwambia, nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwakuwa

imo mikononi mwangu, nami humpa yeyote kama nipendavyo, basi

wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako. Yesu akajibu

imeandikwa msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke

yake ukiwa ndiwe mwana wa Mungu jitupe chini, kwa maana

imeandikwa atakuagizia malaika zake wakulinde, mikononi mwao

watakuchukua usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.Yesu akajibu

akamwambia imeandikwa, usimjaribu Bwana Mungu wako.

Napenda tuyaangalie majaribu aliyomjaribu

1. Alikaa siku arobaini akaona njaa

Filp 4:11-13

Sikwamba nasema hayo kwakuwa nina mahitaji, maana

nimejifunza kuwa na radhi na hali yeyote nilionayo, najua

kudhiliwa, tena najua najua kufanikiwa, katika hali yoyote na

Silaha za Adui Samuel Imori

84

katika mamboYoyote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa

na vingi na kupungukiwa, nayaweza mambo Yote katika yeye

anitiaye nguvu.

2. Ibilisi akamwonyesha fahari, mali ya duniahii, yewye

hakuzitamani.

Filp 3:8

Naam zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa

ajili ya uzuri usio na kiasi.Wakumjua Kristo Bwana wangu, ambaye

kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote, Nikiyahesabu kuwa

kama mavi ili nipate kristo.

3. Ibilisi akamwambia ikiwa ndiwe mwana wa Mungu jitupe,

kwa mana imeandikwa atakuagizia malaika zake wakulinde

naya kwamba mikononi mwao watakuchukua, usije

ukajikwaa mguu wako katika jiwe

Ebr 10:26-29

Maana kama tukifanya dhambi kusudi, baada ya kuupokea ujuzi

ile kweli, haibaki tena Dhabihu kwa ajili ya dhambi, bali kuna

kutazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa Moto uliotayari

kuwa wao wapingao, mtu aliyedharau sharia ya musa hufa posipo

Huruma kwa neno la mashahidi wawili au watatu, mwaonaje?

haikumpasa adhabu Iliyo kubwa zaidi mtu Yule alie mkanyaga

mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya Agano aliyotakaswa

kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?

Silaha za Adui Samuel Imori

85

Msomaji wangu mpendwa tumemuona yule adui yetu ibilisi

akimwabia Bwana wetu Yesu kwamba ajitupe ”jitupe” maana yake

jirushe, hata kama ngazi zipo hakuna haja ya kutelemka polepole

kuzitumia, jitupe tu na Mungu atatuma malaika wakushike na,

wakusaidie usijikwae usiumie. Hii ni kusemaje, yapo mambo

ambayo neno la Mungu linatuelekeza jinsi ya kuyafanya, lakini

wakati mwingine tunakaidi, wakati mwingine tunaamua kutekeleza

mambo mbayo tunayajua wazi kabisa kwamba si sahihi, tunafanya

makusudi kabisa, ninaomba Mungu wetu mwenye huruma

atuhurumie, aturehemu, pale ilipotokea tukaanguka kwenye mtego

huo wa makusudi, mtego huo wakujitupa, tukajikuta yumejitupa ili

malaika watushike, wakati mwingine hawakutushika tukaangukia

pua maana tulifanya makusudi. Naomba uyatafakari majaribu hayo

yote ambayo Bwana wetu aliya pitia, na akashinda tumeona wazi

wazi njaa haikumsumbua, shibe haikumsumbua, fahari ya

ulimwengu huu haikumsumbua, kujirusha, kujiamulia kutenda

lolote lililo kinyume na Mungu hakufanya hivyo. Jikague

ujihakikishe ulivyo, wapi umeshindwa, wapi unatakiwa

uparekebishe, parekebishe maana bado ungali na muda wa kufanya

hivyo katika jina la Baba/Mwana na Roho mtakatifu Amen.

Silaha za Adui Samuel Imori

86

HITIMISHO

Nakushukuru sana wewe msomaji wangu mpendwa, kwa kutumia

muda wako kukisoma kitabu hiki , maana ningekiandika kasha

usikisome isingekuwa na maana. Naamini hauko vile ulivyokuwa

kabla hujakisoma, nakushauri umshirikishe mwingine Yule

umpendaye, ili naye akisome. Nakut akia ushindi katika safari

yako kwenda mbinguni, mahali utakapoishi milele na milele, mahali

ambapo hakuna kilio, wala mateso ya aina yeyote ile, kule ambapo

tutaishi na Baba yetu, muumba mbingu na nchi, niamaombi yangu

kwamba hautachoka katika safari hii, ambayo alituambia wazi

wazi, kwamba wale watakao shinda watavikwa mavazi meupe na

watapewa jina jipya.

Uf 2:17

Yeye aliye na sikio na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia

makanisa, yeye ashindaye nitampa baadhi ya le mana iliyofichwa,

nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya hilo limeandikwa JINA JIPYA

asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.

Uf 2:12

Yeye ashindaye nitamfanya nguzo katka hekalu la Mungu wangu

wala hatatoka humo tena kabisa, name nitaandika juu yake jina la

Mungu wangu na jina la mji wa Mungu wangu. Huo Yerusalem

mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu

mwenyewe lile JIPYA.

Silaha za Adui Samuel Imori

87

Msomaji wangu nakutakia safari njema iliyojaa ushindi, Mungu

akuwezeshe maneno haya usiyasikie tu, na ukaishia njiani, jitie

nguvu, uwena moyo mkuu, ufike ulipokee jiwe leupe lenye jina lako

“jipya”, nafurahia sana sana ninaposoma ya kwamba

.jina langu litakuwa jipya

.jina la Yesu litakuwa jipya

.jerusalemu itakuwa mpya

.nchi nayo itakuwa mpya

Ee Mungu tusaidie tuyaone mambo mapya, katika jina la YESU

Amen.