Methali za Kiswahili zilizoachwa: sababu na athari zake kwa ...
-
Upload
khangminh22 -
Category
Documents
-
view
0 -
download
0
Transcript of Methali za Kiswahili zilizoachwa: sababu na athari zake kwa ...
The University of Dodoma
University of Dodoma Institutional Repository http://repository.udom.ac.tz
Humanities Master Dissertations
2015
Methali za Kiswahili zilizoachwa: sababu
na athari zake kwa jamii
Juma, Aley Rashid
Chuo Kikuu cha Dodoma
Juma, A. R. (2015). Methali za Kiswahili zilizoachwa: sababu na athari zake kwa jamii.
Dodoma: Chuo Kikuu cha Dodoma
http://hdl.handle.net/20.500.12661/540
Downloaded from UDOM Institutional Repository at The University of Dodoma, an open access institutional repository.
METHALI ZA KISWAHILI ZILIZOACHWA: SABABU NA ATHARI ZAKE KWA
JAMII
Aley Rashid Juma
Tasnifu Iliyowasilishwa kwa Ajili ya kukamilisha Masharti ya Shahada ya
Uzamili ya Sayansi ya Jamii katika Fasihi ya Kiswahili
Chuo Kikuu cha Dodoma
Oktoba, 2015
i
ITHIBATI YA MSIMAMIZI
Aliyesaini hapo chini, anathibitisha kwamba, ameisoma tasnifu inayoitwa;
MethalizaKiswahili Zilizoachwa: Sababu na Athari zake kwa Jamii, na
amependekeza kwamba, inafaa ikubaliwe na Chuo Kikuu Cha Dodoma, kwa ajili
ya tunzo ya Shahada ya Uzamili katika Fasihi ya Kiswahili.
…………………………….
Profesa Frowin Paul Nyoni
(Msimamizi)
Tarehe ……………………..
ii
IKIRARI NA HAKIMILIKI
Mimi,Aley Rashid Juma, nathibitisha kuwa tasnifu hii ni kazi yangu halisi na kwamba
haijawahi kuwasilishwa na wala haitawasilishwa katika Chuo Kikuu kingine chochote,
kwa ajili ya utunuku wa Shahada yoyote ile.
Saini ……………………….
Tarehe …………………….
Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuzalisha, kunakili, wala kusambaza sehemu
yoyote ya tasnifu hii, kwa namna yoyote, bila ya kibali cha maandishi, kutoka kwa
mwandishi au Chuo Kikuu Cha Dodoma.
iii
TABARUKU
Natabaruku kuitolea hidaya tasnifu hii kwa hawa wafuatao:
Kwanza ni mpendwa mama yangu, Mwatima Vuai Mkanga. Yeye ndiye aliyenizaa
nakunilea kwa umakini mkubwa hadi kufikia ukubwani. Pia,ndiye mwalimu wangu wa
kwanza wa maadili, dini na mbinu za maisha yangu ya baadaye kwa jumla. Kila
nimuonapo huvuta hisia za mbali kwa kiasi gani alivyopata tabu kwa ulezi wa peke yake
bila ya kuwa naye karibu mfarijimume wake kwa kazi hiyo ngumu. Nakiri kuwa sina
cha kumlipa zaidi ya kuwa karibu naye, na kumuonesha mapenzi ya dhati kwa bawa la
huruma, ucheshi na msaada wa hali na mali, huku nikimuombea kwa Mwenyezimungu
ampe umri mrefu wenye afya na kheri nyingi, Amin.
Pili ni Baba yangu mzazi, Bwana Rashid Juma Ali. Kwa hakika alitamani sana
kuendelea na maisha katika hii dunia ili ashirikiane na mama katika kumlea mtoto wao
kwa huruma na mapenzi, lakini haikuwezekana, kwaniumri wake ulimalizika kwa
kutangulia mbele ya haki siku ishirini na tatu tu tokea kuzaliwa kwa mwanawe
mpendwa. Roho na nafsi yangu zinalitembelea kaburi lake kila siku ili kupata hisia za
mapenzi yake kwangu na yangu kwake kwa kumuomba Mwenyezimungu amsamehe
makosa yake, na amuweke mahali pema Peponi, Amin.
iv
SHUKURANI
Kwanza, namshukuru kwa dhati na kwa unyenyekevu wote Mwenyezimungu
aliyeniumba, kunikuza, kunipa afya, akili na fahamu na kisha akaniwezesha
kuikamilisha kazi hii muhimu na ya kihistoria katika maisha yangu.
Pili, napenda kumshukuru kwa dhati msimamizi wangu wa utafiti huu Profesa Frowin
Paul Nyoni ambaye amejaa busara, hekima na ucheshi katika kutoa maelekezo ya kazi
hii hadi pale ilipokamilika. Juhudi zake za kipekee sitazisahau maishani mwangu na
namuahidi kumuenzi kwa kufuata nyayo zake.
Tatu, nawashukuru wahadhiri wangu wote wa programya Shahada ya umahiri ambao ni
Dkt. Khatib, Prof. Madumulla,Dkt. Ponera, Dkt. SebondenaDkt. Songoyi. Maarifa yao
yalikuwa ndiyo msingi muhimu wa kazi hii ya utafiti katika Fasihi ya Kiswahili.
Nne, ninawashukuru kwa dhati wanafunzi wenzangu wote wa fani ya Fasihi ya
Kiswahili mwaka 2013/2015. Ushirikiano na msaada wao kwangu, ulisadifu vyema
katika kuyamudu masomo yangu na katika kuikamilisha kazi hii muhimu.
Tano, naishukuru pia familia yangu, mke wangu mpenzi Fatma Nassor Ali na watoto
wangu wapendwa Abdulhamid, Layla, Aisha, Abdulbasit na Latifah kwa heshima,
upendo na ustahamilivu wao mkubwa katika kipindi chote cha mimi kuwa mbali nao.
Shukrani zangu nyengine ni kwa muhisani wanguambaye alikuwa na kazi kubwa ya
kunipa moyo, ushauri na misaada ya hali na mali kila nilipokwama kwa muda wote wa
progam na kazi yangu hii ya utafiti.
Hao wote niliyowataja hapo juu, ndugu na wengineo ambao sikupata nafasi ya kuwataja
ama kuwaainisha hapa, nawashukuru kwa dhati, na kwa jumla, nawaombea kheri na
mafanikio katika maisha yao yote, Amin.
v
IKISIRI
Tasnifu hii inahusuMethali za Kiswahili Zilizoachwa: Sababu na Athari zakekwa
Jamii. Methali za Kiswahili zilizoachwa ni semi zenye muhutasari wa mawazo ya
busara kwa mkato zinazotokana na jamii ya Waswahiliambazo, kwa sasa
hazitumikitena. Methali hizo zilichunguzwa katika jamii ya Waswahili waishio Zanzibar
ambayo katika utafiti huu inajulikana kwa jina la jamii ya Wazanzibari.Utafiti ulilenga
kuzibainisha baadhi ya methali hizo, kuchunguza sababu na athari za kuachwa kwake
katika jamii hiyo.Sababu ya kuchunguza suala hilo ilitokana na mtafiti kubaini baadhi ya
methali hizo ambazo zilimvutia na kuona kuachwa kwake ni hasara kwani jamiiitapoteza
vitu muhimu. Hivyo, shabaha ya kufanya utafiti huu nikuibua upya matumizi ya methali
hizo ili jamii iweze kufaidika na hekima, falsafa, mafunzo na mvuto wake.
Mbinu zilizotumika kupata data ni udurusu wa maandiko, udodosaji, mahojiano na
mjadala wa kikundi. Jamii tafitiwa ni ya Wazanzibari kwa kuwa ndiko ulikofanywa
utafiti huu. Data zilizopatikana kutoka uwandani zilichanganywa na zile za
maktabani.Nadharia ya Uamilifu yenye msingi wa kuangalia kazi ya fasihi simulizi
ilitumika.
Matokeo ya utafiti yamebainikuwepokwa methali zilizoachwaambazo baadhi yake
zimeoneshwa katika tasnifu hii. Pia,zipozinazotumiwa sana,kwa wastani na kwa
nadra.Sababu za kuachwa methali hizo ni mvuvumko wa maendeleo ya sayansi na
teknolojia, ukosefu wa taasisi za kuzihifadhi na kuzirithisha, mabadiliko ya msamiati
uliotumika katika methali hizo, na kuibuka kwa methali nyingi mpya.Athari chanyakwa
jamii, ni kuondoka kwa msamiati mgumu usiotumika sasa,na kuiruhusu lugha kuwa na
mabadiliko chanya ya maendeleo ya sayansi na teknolojia. Kwa upande wa athari hasi ni
kufifia kwautamaduni wa Wazanzibari,jamii kuzikosa adili za methali hizo, na jamii
kukosa burudani itokanayo na methali hizo.Kwa matokeo hayo, utafiti huu ni muhimu
kwa walimu, wanafunzi, wataalamu, na jamii nzima ya Wazanzibari na Waswahili kwa
jumla.Tasnifu hiiina sura tano za ripoti ya utafiti,marejeleo pamoja na baadhi ya
viambatisho vya utafiti huu.
vi
YALIYOMO
ITHIBATI YA MSIMAMIZI ..............................................................................................
IKIRARI NA HAKIMILIKI ............................................................................................. ii
TABARUKU ................................................................................................................... iii
SHUKURANI ................................................................................................................... iv
YALIYOMO ..................................................................................................................... vi
SURA YA KWANZA ....................................................................................................... 1
UTANGULIZI ................................................................................................................... 1
1.1 Usuli wa Tatizo la Utafiti ............................................................................................. 1
1.2 Tamko la Tatizo la Utafiti ............................................................................................ 7
1.3 Malengo ya Utafiti ....................................................................................................... 8
1.4.1 Lengo la Jumla .......................................................................................................... 8
1.4.2 Malengo Mahususi .................................................................................................... 8
1.5Maswali ya Utafiti ......................................................................................................... 8
1.6Umuhimu wa Utafiti ..................................................................................................... 9
1.7Nadharia ya Uchanganuzi wa Data ............................................................................... 9
1.8Mipaka ya Utafiti ........................................................................................................ 12
1.9Muhutasari wa Sura ya Kwanza .................................................................................. 13
SURA YA PILI ................................................................................................................ 14
MAPITIO YA MAANDIKO ........................................................................................... 14
2.2 Mapitio ya Maandiko Kuhusu Fasihi Simulizi .......................................................... 14
2.3 Mapitio ya Maandiko Kuhusu Semi .......................................................................... 18
2.4Mapitio ya Maandiko Kuhusu Methali ....................................................................... 21
2.5Mapengo Yanayojitokeza Kutokana na Mapitio ya Maandiko................................... 32
2.6 Muhutasari wa Sura ya Pili ........................................................................................ 32
SURA YA TATU ............................................................................................................. 33
USANIFU NA MBINU ZA UTAFITI ............................................................................ 33
3.1 Utangulizi ................................................................................................................... 33
3.2 Mpango wa Utafiti ..................................................................................................... 33
vii
3.3 Eneo la Utafiti ............................................................................................................ 34
3.4 Walengwa wa Utafiti.................................................................................................. 34
3.4.1 Jamii Tafitiwa.......................................................................................................... 34
3.4.2 Aina na Dhana ya Usampulishaji ............................................................................ 35
3.5 Ukusanyaji wa Data ................................................................................................... 36
3.5.1 Njia na Zana za Ukusanyaji wa Data ...................................................................... 36
3.5.1.1Udurusu wa Kimaktaba ......................................................................................... 36
3.5.1.2 Mahojiano ............................................................................................................ 37
3.5.1.3 Mjadala wa Vikundi ............................................................................................. 37
3.5.1.4 Udodosaji ............................................................................................................. 37
3.5.1.5 Uchunguzi ............................................................................................................ 38
3.5.2 Zana za Kukusanyia Data........................................................................................ 38
3.5.3 Mchakato wa Ukusanyaji wa Data .......................................................................... 39
3.6 Uchanganuzi wa Data ................................................................................................ 40
3.7 Uhalali na Uthabiti wa Matokeo ya Utafiti ................................................................ 43
3.8 Itikeli za Utafiti .......................................................................................................... 43
3.9 Muhutasari wa Sura ya Tatu ...................................................................................... 44
SURA YA NNE ............................................................................................................... 45
UWASILISHAJI NA MJADALA WA MATOKEO YA UTAFITI ............................... 45
4.1 Utangulizi ................................................................................................................... 45
4.2 Methali za Kiswahili Zilizoachwa katika Jamii ya Wazanzibari ............................... 45
4.2.1 Miktadha ya Maisha ya Jamii ya Wazanzibari ....................................................... 45
4.2.1.1 Muktadha wa Kijografia na Kiuchumi ................................................................. 47
4.2.1.2 Muktadha wa Kiutamaduni .................................................................................. 48
4.2.1.3 Muktadha wa Kifasihi .......................................................................................... 50
4.2.2 Methali za Kiswahili Zilizoachwa .......................................................................... 52
Jeduwali la methali zilizoachwa katika jamii ya Waswahili Zanzibar ............................ 56
4.3 Sababu za Wazanzibari Kuacha Baadhi ya Methali za Kiswahili ............................. 70
4.3.1 Mvuvumko wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia ............................................ 71
4.3.2 Mabadiliko ya Msamiati Uliotumikakatika Methali hizo ....................................... 74
4.3.3 Kuwepo kwa Methali Nyingi Mpya ........................................................................ 76
viii
4.3.4 Ukosefu wa Taasisi za Kuzihifadhi na Kuzirithisha Methali.................................. 78
4.4 Athari za Kuachwa kwa Baadhi ya Methali za Kiswahili.......................................... 79
4.4.1 Tija Zilizopatikana .................................................................................................. 80
4.4.1.1 Kuondoka kwa Msamiati Mgumu (Usiotumika) ................................................. 80
4.4.1.2 Kuiruhusu Lugha Kulandana na Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia .............. 81
4.4.2 Madhara yanayopatikana ........................................................................................ 82
4.4.2.1Kufifia kwa Utamaduni wa Wazanzibari .............................................................. 82
4.4.2.2 Jamii Kuzikosa Adili za Methali .......................................................................... 83
4.4.2.3 Jamii Kukosa Burudani Inayotokana na Methali hizo ......................................... 84
4.5 Muhutasari wa Sura ya Nne ....................................................................................... 86
SURA YA TANO ............................................................................................................ 88
MUHTASARI, HITIMISHO NA MAPENDEKEZO ..................................................... 88
5.1 Utangulizi ................................................................................................................... 88
5.2 Muhutasari wa Tasnifu ............................................................................................... 88
5.3 Utoshelevu wa Nadharia Iliyotumika ........................................................................ 90
5.4 Mchango Mpya wa Utafiti ......................................................................................... 91
5.5 Maoni na Mapendekezo ya Mtafiti ............................................................................ 91
MAREJELEO .................................................................................................................. 93
VIAMBATISHO .............................................................................................................. 99
A: Barua za Ithibati ya Kufanyia Utafiti .......................................................................... 99
A1: Barua ya kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma............................................................... 99
A2: Kibali cha Ruhusa ya Kufanyia Utafiti Zanzibar. ................................................... 100
B: MIONGOZO YA USAILI, DODOSO NA UDURUSU WA MAKTABA .............. 101
B1: Mwongozo wa Hojaji kwa Wataalamu na Wazee wenye uzoefu ........................... 101
B2: Mwongozo wa Usaili kwa Wanafunzi wa Sekondari na Diploma ya Kiswahili .... 102
B3: Mwongozo wa Dodoso kwa Wakufunzi na Vyuo na Watu wa Mitaani ................. 103
B.4: Mwongozo wa Udurusu wa Maktaba ..................................................................... 105
C.2: Methali Zinazotumiwa kwa wastani katika Jamii ya Wazanzibari ........................ 110
C.3: Methali zinazotumiwa kwa nadra katika jamii ya Wazanzibari............................. 113
ix
VIFUPISHO VILIVYOTUMIKA
BAKIZA Baraza la Kiswahili la Zanzibar
UZ Zanzibar University
SUZA The State University of Zanzibar
TAKILUKI Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni
TATAKI Taasisi ya Taaluma za Kiswahili
Bi Bibi
Bw. Bwana
Prof. Profesa
Dkt. Daktari
Na. Namba
1
SURA YA KWANZA
UTANGULIZI
Utafiti huu ulichunguza sababu na athari za kuachwa kwa baadhi ya methali za
Kiswahili, katika jamii ya Wazanzibari.Sura hii imeelezea vipengele vya usuli na tamko
la tatizo la utafiti, malengo na masuali ya utafiti.Vipengele vingine vilivyoelezewa
katika sura hii ninadharia, umuhimu pamoja na mipaka ya utafiti.
1.1 Usuli wa Tatizo la Utafiti
Jamii ya Waswahili wa Zanzibar, kama jamii za Waswahili wengine, imekuwa na
umuhimu mkubwa na fasihi simulizi ya Kiswahili. Wenyeji wa Zanzibar mara
nyingi wameshuhudia vikao vya mabibi na mababu wakiwasimulia hadithi murua
wajukuu zao (Othman na Yahya, 2004). Pia, wameshuhudia mara nyingi maghani ya
mashairi, ngoma, maigizo na semi zikitumika katika sherehe zao za arusi, jando na
unyago. Aidha, wamekuwa wakiwasikia watu wakiwasilisha ujumbe kwa kutumia
moja ya semi za Kiswahili. Hadi hii leo amali hizo zimekuwa zikiendelea kufanyika,
ingawa kwa sasa hivi zimekuwa zinapungua kwa kiasi kikubwa kutokana na sababu
mbalimbali.
Fasihi simulizi imegawika katika matawi kulingana na muundo, tabia, uwasilishwaji
na muktadha wa matumizi yake. Hakuna idadi iliyokwishakubalika na wataalamu
wote juu ya matawi hayo, lakini wataalamu wengi wamekaribiana katika
2
kuzibainisha aina hizo zinazoitwa tanzu za fasihi simulizi.Kwa mujibu wa Mulokozi
(1989), tanzu za fasihi simulizi ni sitana amezigawa kwa kuzingatia umbile na tabia
ya kazi inayohusika, pia kwa kuzingatia muktadha na namna ya uwasilishaji wake
kwa hadhira. Tanzu hizo ni mazungumzo, masimulizi, maigizo, ushairi, ngomezi
pamoja na semi. Kwa kuwa kila moja ya tanzu hizi ni pana na ina mambo mengi
ndani yake, ndio maana utafiti huu, ulijiegemeza katika utanzu mmoja peke yake,
ambao ni utanzu wa semi.
Mulokozi (1996) anaeleza kuwasemi ni tungo au kauli fupifupi za kisanaa ambazo
hubeba maana au mafunzo muhimu ya kijamii. Semi ni moja ya utanzu wa fasihi
simulizi unaojumuisha tanzu ndogondogo za lakabu, mafumbo, methali, misemo na
vitendawili. Naye Wamitila (2004), anazieleza semi kuwa ni kundi la tungo za fasihi
simulizi ambazo ni fupifupi na zina matumizi ya taswira, tamathali na ishara kwa
mapana. Ujumbe wake huwasilishwa kwa njia ya mkato, yenye mkokotezo na
kukumbukika haraka.Kwa kawaida, utanzu wa semi tofauti na tanzu nyengine za
fasihi simulizi, hutumika mara nyingi zaidi, takriban kila siku na katika kila aina ya
muktadha ndani ya jamii yoyote ile. Kila jamii moja huwa na semi zake, ingawa kwa
baadhi yake huwa na uhusiano mkubwa wa kimaana baina ya semi za jamii moja na
nyengine. Semi hutofautiana kutokana na lugha, utamaduni, itikadi na idili za jamii.
Jamii ya Waswahili nayo, inazo semi zao na ni wajuzi wa matumizi yake. Huzitumia
katika mazungumzo yao ya kawaida, nakatika sherehe zao mbalimbali. Mara nyingi
watunzi wa fasihi andishi ya Kiswahili, nao wamekuwa ni weledi wa kuzitumia semi
mbalimbali katika kazi zao. Kwa jamii ya Kiswahili, semi hutumiwa na walimu
3
wanapofundisha, viongozi wanapohutubia, wazazi wanapowaasa au kuwashajihisha
watoto wao, vile vile semi hutumiwa na hata watu kwa wapenzi wao au wagomvi
wao (Salum, 2007). Wote hao huzitumia semi hizo, kwa madhumuni mbalimbali
kama vile kuelimisha, kuburudisha, kuonya, kuasa, kukosoa na kuadabisha.
Kutokana na upana wa matumizi ya semi kwa jamii za Wazanzibari, ndio maana
maandishi ya semi yakawa yameenea katika sehemu mbalimbali za jamii yao. Katika
zama hizi, semi Zanzibar huandikwa kwenye kanga, magari, makawa, mikoba, kuta
za nyumba, mapazia, milangoni kwenye fulana na kadhalika (Mbaruk, 2011:10).
Wataalamu wamevibainishavipera vya semikuwa ni lakabu, mafumbo, methali,
misemo, nahau na vitendawili. Kutokana na upana wa utanzu wa semi, haikuwa
rahisi kwa mtafiti, kuvishughulikia vipera vyote na hivyo, utafiti huu ulijikita katika
kipera kimoja ambacho ni methali.
King‟ei (1998), anasema kuwamethali ni usemi mfupi, wenye maana pana, na busara
au hekima ulio na mizizi katika jamii fulani na unaoelimisha, kuasa au kukejeli watu
au vitendo fulani katika jamii lakini kwa njia iliyofumbwa na kuwekewa tasfida. Nao
Mulokozi (1996), na Njogu na Chimerah (1999) wanazieleza methali kuwa ni semi
fupifupi zinazoeleza kwa muhutasari fikra au mafunzo mazito yaliyotokana na
uzoefu wa kijamii. Mara nyingi mawazo hayo huelezwa kwa kutumia tamathali hasa
sitiari na mafumbo. Methali ni utanzu tegemezi ambao kutokea kwake kunategemea
fani nyengine za kushikamana nazo.Mifano ya fani hizo ni mazungumzo, hotuba au
majadiliano mazito katika miktadha maalum ya kijamii. Baadhi ya methali huwa ni
vielelezo au vifupisho vya hadithi fulani inayofahamika vizuri kwa jamii. Methali
nyingi zina muundo wa sehemu mbili, sehemu ya kwanza inayoanzisha wazo na ya
4
pili inayokamilisha au kulikanusha wazo hilo. Kwa mfano; Tamaa mbele mauti
nyuma, na Haraka haraka hainaBaraka. Hata hivyo, methali hazina ulazima wa
kuwa na muundo kama huo, kwani zipo zenye miundo tofauti na huo.
Kama ilivyo kwa kipera chochote cha fasihi simulizi, methali nazo asili yake ni jamii
husika. Hivyo, methali za Kiswahili chimbuko lake ni jamii ya Waswahili, ambapo
nyingi zao zimebuniwa kutokana na lugha ya Kiswahili na lugha za Kibantu. Hata
hivyo, baadhi ya methali za Kiswahili zina asili ya lugha za kigeni, hasa Kiingereza
na Kiarabu. Sifa za methali za Kiswahili kwanza ni kupokewa kutoka kizazi hadi
kizazi, pili ni uchache wa maneno na tatu ni kuwa na maana iliyokamili. Sifa
nyingine ni kuwa na maana za kifalsafa, maana na matumizi yake kutegemea
muktadha, na mara nyingi huwa na muundo wa swali na jibu. Kwa upande wa
dhima, methali za Kiswahili zina dhima ya kuonya, kuhimiza, kuliwaza, kutilia
mkazo jambo, kukejeli na kudhihaki. Dhima nyengine ni kuhifadhi utamaduni,
kushauri, kudumisha matumizi ya msamiati, kuelimisha na kuburudisha.
Jamii ya Waswahili inazo methali za Kiswahili nyingi sana. Inakadiriwa kuwa ni
zaidi ya methali elfu mbili na mia tano. Methali zimeanza kuwepo miaka mingi
iliyopita, kiasi cha kukadiriwa tokea kuanza kwa jamii ya Waswahili, na zimekuwa
zikirithiwa kutoka kizazi hadi kizazi. Methali zimekuwa zikibuniwa katika kila zama
ya maisha ya mwanadamu. Kubuniwa huko hutokana na mahitaji ya jamii kwa
mujibu wa idili za jamii husika. Kwa hivyo, jamii ya Waswahili imeshuhudia
methali za aina kwa aina zikitumika katika jamii yao, bila kumjua nani mwanzilishi
5
wake. Methali hizo, ni nzuri katika matamshi, mafunzo, hekima na falsafa, na
miundo yake.
Yapo maelezo mengi yaliyoelezwa kuhusu uzuri na umuhimu wa methali kwa jamii
ya Waswahili na hata jamii nyengine duniani.Katika maelezo hayo wapo
waliozifananisha methali na roho katika mwili (Finnegan, 1979).Wapo
waliozifananisha na viungo katika chakula (Mhilu, 2011).Pia,wapo waliozifananisha
na mafuta bora ya kupikia chakula. Wote hao wameeleza hayo kwa lengo la
kuonesha umuhimu wa methali katika jamii na kwa hakika methali ni muhimu katika
lugha ya jamii yoyote ulimwenguni ikiwemo ya Kiswahili. Pamoja na uzuri na
umuhimu huo wa methali katika jamii ya Waswahili, kwa muda mrefu sasa, baadhi
ya utajiri na urithi huo mwema, umekuwa ukiachwa kutumiwa katika jamii ya
Wazanzibari. Tatizo hili lilikuwepo tangu zamani, lakini limejitokeza zaidi katika
miaka ya elfu mbili na kuendelea hadi sasa. Kunamethali nyingi zilizokuwa zikitoa
mafunzo mema na zenye utajiri wa misamiati mizuri ya lugha zimeachwa kutumiwa
(Farsi, 1979: Hassan, 2013). Kwa mfano: “Mkataa chinjo hupata mtanda”, “Endapo
juu kipungu hafikilii mbinguni”, “Boi manda malipo yake parapanda”, “Sumu ya
huyu ni dawa ya mwengine”, “Utamu wa wazimu aujuaye mwendawazimu
mwenyewe” na nyengine nyingi. Methali hizo sasa hazisikiwi zikisemwa katika
mazungumzo ya kawaida, hazionekani kutumika katika maandishi, wala hazijulikani
na kizazi kilichopo, isipokuwa kwa sasa zimebakia katika kumbukumbu za wazee
wachache waliobaki hai katika mitaa au katika vitabu vichache vilivyotungwa
zamani.
6
Hali hii si nzuri na haifai kufumbiwa macho, kwani kuachwa moja kwa moja
zisitumike ni hasara kwa jamii, kwa sababu kwa mujibu wa Msuya(1979),fasihi
simulizi, zikiwemo semi na hasa methali, ni hazina kubwa ya hekima na falsafa
ambazo kwa kawaida huwa hazipatikani hata vitabuni. Kwa hivyo, hali hiyo
inaonesha wazi kuwa, kuna haja ya kulishughulikia suala la kuachwa kwa baadhi ya
methali za Kiswahili, katika matumizi ya jamii ya Waswahili ikiwemo ya
Wazanzibari. Kumekuwepo fununu kuwa sababu ya kuachwa kutumiwa fasihi
simulizi zikiwemo methali ni mtindo wa maisha, kwa maana kuwa binadamu na
viumbe wengine huwepo duniani kwa kipindi na kisha wakatoweka na kuja
wengine; na hivyo, methali nazo hufuata mkumbo huo. Maendeleo ya sayansi na
teknolojia yaliyoshamiri ulimwenguni hivi sasa ni sababu nyengine
inayofikiriwa.Pia,ni kutokana na dhana potofu kuwa fasihi simulizi ni sanaa ya watu
wajinga wasiojua kusoma, ambapo kwa sasa hali hiyo inatoweka kwa nguvu
(Khamis, 1983). Hata hivyo, hizi ni baadhi ya sababu zinazofikiriwa kijuujuu tu,na
hazina uhakika wowotekwani hadi hivi sasa haujafanywa utafili juu ya suala hili.
Umuhimu wa fasihi simulizi unaonekana wazi duniani kote hivi sasa. Hali hii
imesababisha uonekane pia na umuhimu wa kuzitunza tanzu zake. Hii ndio sababu
jamii nyingi zinashughulika katika kuzifanyia tafiti mbalimbali tanzu zao za fasihi
simulizi, kwa lengo la kuziimarisha na kuziwekea mustakabali mwema wa siku
zijazo (Khamis, 1983). Fasihi simulizi ya Kiswahili nayo inahitaji kufanyiwa tafiti
kama hizo, katika tanzu zake zote. Hadi sasa hakujakuwa na tafiti nyingi na za
kutosha zinazohusiana nayo. Hii ni kwa sababu mbali mbali zikiwemo za uchache
wa wataalamu na za kiuchumi. Tafiti zilizofanyika bado ni chache sana kuiwezesha
7
fasihi simulizi ya Kiswahili kuimarika katika nyanja za kitaaluma na kimaendeleo.
Kwa ajili hiyo, utafiti wowote wa fasihi simulizi ya Kiswahili kipindi hiki, utakuwa
ni muhimu katika kuisogeza kwenye lengo la juu, ikitarajiwa kuwa ni pamoja na
tafiti zinahusiana na methali za Kiswahili kama huu.
1.2 Tamko la Tatizo la Utafiti
Zimekuwepo baadhi ya tafiti zilizofanywa kuhusu semi kwa jumla au baadhi ya vipera
vyake zikiwemo methali, lakini tafiti zote hizo hazijagusia sababu wala athari za
kuachwa kutumiwa kwa methali hizo katika jamii ya Waswahili. Kwa mfano,
Madumulla (2005) amefanyia kuhusu methali na misemo katika jamii ya Wahehe.
Mulokozi (1985) ametafiti kuhusu fani na maudhui katika methali za Kiswahili. Hassan
(2013) utafiti wake ni kuhusu dhima ya methali katika kudumisha maadili, Uledi (2012)
amefanyia kuhusu muundo na lugha katika methali na vitendawili. Ndaro (2012)
ametafiti kuhusu fani katika methali za Kidigo. Mgulu (2011) utafiti wake ulihusu
usanaa katika Methali, na Simchimba (2012) alifanyia falsafa ya Ki-Afrika katika
Methali za Kiswahili. Hawa wote wamefanyia tafiti zao juu ya muundo, lugha, dhima,
au fani na maudhui ya methali; na hivyo, kutougusia upande wa athari au sababu za
kuachwa kutumika kwa methali katika jamii yoyote ile. Mbrouk (2011) amefanyia
utafiti juu ya athari za semi kwa jamii ya Wazanzibari, lakini amejikita katika semi
zinazotumika katika kanga peke yake; na hivyo, kuacha pengo katika sababu na athari za
methali zilizoachwa kutumika katika jamii hiyo. Kwa sababu hiyo, utafiti ulihitajika ili
zijulikane sababu za kuachwa kwa baadhi ya methali katika jamii ya Wazanzibari, ikiwa
ni pamoja na kubainisha athari inayoweza kuipata jamii hiyo kutokana na tatizo hilo. Hii
8
ndio maana utafiti huu ulijikita katika eneo hilo ili kupata ukweli juu ya methali za
Kiswahili zilizoachwa, sababu na athari zake kwa jamii ya Wazanzibari.
1.3 Malengo ya Utafiti
Utafiti huu uliongozwa na malengo yafuatayo;
1.3.1 Lengo la Jumla
Lengo kuu ni kuchunguza sababu na athari za kuachwa kwa baadhi ya methali za
Kiswahili katika Jamii ya Wazanzibari.
1.3.2 Malengo Mahususi
a) Kubainisha methali za Kiswahili zilizoachwa katika jamii ya Wazanzibari;
b) Kuchunguza sababu za kuachwa kwa baadhi ya Methali hizo katika jamii ya
Wazanzibari, na;
c) Kuchunguza athari za kuachwa kwa baadhi ya methali hizo kwa jamii ya
Wazanzibari.
1.4 Maswali ya Utafiti
a) Ni methali zipi za Kiswahili zilizoachwa kutumiwa katika jamii ya Wazanzibari?
b) Kuachwa kutumiwa kwa methali za Kiswahili katika jamii ya Wazanzibari
kunatokana na sababu zipi?
9
c) Kuna athari gani zinazotokana na kuachwa kwa baadhi ya methali za Kiswahili
katika jamii ya Wazanzibari?
1.5 Umuhimu wa Utafiti
Utafiti huu una umuhimu ufuatao; Kwanza, unatarajiwa kuwa chachu ya kufufua
upya matumizi ya methali nzuri zilizokuwa zimeshaachwa katika miaka hii. Hali hii
itaisaidia jamii ya Wazanzibari kuzikumbuka na kuzitumia methali za asili, na hivyo
kuhifadhi na kuendeleza utamaduni, falsafa na maadili mazuri ya jamii yao. Pili,
utafiti huu utasaidia kitaaluma katika matumizi ya marejeleo kwa wataalamu
mbalimbali wakiwemo walimu na wanafunzi wa ngazi zote. Tatu, utafiti umeweza
kuibua mianya mipya itakayowahamasisha watafiti wengine kuifanyia utafiti zaidi
fani hii ya fasihi simulizi ya Kiswahili zikiwemo methali.
1.6 Nadharia ya Uchanganuzi wa Data
Nadharia iliyotumika kuuongoza utafiti huu ni ya Uamilifu. Nadharia ya Uamilifu
(Utendajikazi) hushughulikia kazi ya fasihi simulizi inayofanywa katika mfumo wa
kijamii. Hii ni nadharia inayokiangalia kipande cha kazi ya fasihi simulizi kuwa ni
sehemu ya mfumo wa kijamii (na hivyo kuwa sehemu ya utamaduni wao). Fasihi
hiyo iwe inatupa jambo la msingi, kiasi kwamba kipande hicho cha kazi ya fasihi
simulizi hutekeleza jukumu maalum katika jamii husika. Katika nadharia ya
Uamilifu inaelezwa kuwa kila kitu hujengwa na vipengele kadhaa na kila kipengele
kinakuwa na utendakazi mahasusi kwa jamii. Hivyo, kwa mujibu wa nadharia hii,
10
fasihi simulizi huchukuliwa kama ni sehemu ya kazi inayofanywa na kipengele
hicho cha sanaa, katika mfumo wa utamaduni.
Nadharia hii imezungumziwa na wataalamu mbalimbali. Kwa mujibu wa Wallace na
Wolf (1980), nadharia ya uamilifu iliasisiwa na wanasosholojia. Miongoni mwa hao
ni Malinowski (1884 – 1942). Ambaye ameichukulia fasihi simulizi kulingana na
utendakazi wake katika jamii. Naye Emile Durkheim (1858 – 1917) aliutazama
uamilifu kuwa ni mfumo unaoeleza sababu mbalimbali na athari za matukio ya
kijamii kama vile migomo juu ya mambo mbalimbali. Wanasosholojia wengine
walioizungumzia nadharia hii na kuyaunga mkono maelezo ya wataalamu
waliowatangulia kama Wolf na wenziwe, ni Angusle Comte (1787 – 1857), Herbert
Spencer (1830 – 1917), na Vilfredo (1848 – 1923). Baada ya hapo nadharia hii
ikaendelezwa na wanaanthropolojia akiwemo Radcliffe Brown (1881 – 1955).
Okpewho, Leech na Firthwalikuja kuiendeleza fasili iliyotolewa na Malinowski
kuhusu nadharia ya uamilifu. Wataalamu hawa walisema kwamba, uamilifu ni kazi
ambayo kipande cha kazi cha fasihi simulizi, hufanya kazi katika mfumo wa jamii.
Fasili hiyo inatoa jambo la msingi kuwa tanzu za fasihi simulizi kama semi
zikiwemo methali, hutekeleza mahitaji au matakwa ya jamii husika. Kwa hivyo,
kutumika kwa nadharia ya uamilifu katika utafiti huu ni muhimu kwa sababu ya
kuubainisha utendakazi wa methali za Kiswahili ambazo ni sehemu ya semi.Kwa
upande mwengine, nadharia ya uamilifu imeelezewa kuwa ni utathmini wa uhusiano
uliopo kati ya sanaa simulizi na mahitaji ya kijamii, kwani kulingana na nadharia hii,
mwanafasihi anahitajika kuzingatia hatua zifuatazo:
11
a) Kuueleza utamaduni wa jamii inayotumia utanzu huo wa fasihi simulizi, hasa
katika miktadha inayotumika utanzu huo, ili kusaidia kufahamu umuhimu wa utanzu
huo katika miktadha ya utamaduni.
b) Kuuelezea utanzu huo wa fasihi simulizi anaoushughulikia ili kuonesha hali halisi
inayopatikana katika jamii hiyo.
c) Kuuelezea utanzu huo kama ni chombo kinachotumika mara kwa mara, na kama
ni sehemu ya utamaduni, kulingana na mahitaji ya jamii.
d) Kuuelezea utendakazi wa utanzu huo katika mfumo wa maisha na jamii hiyo kwa
jumla.
Ili kuweza kutekeleza jukumu hilo maalum katika jamii hiyo, nadharia hii huzingatia
mihimili mikuu ifuatayo:-
a) Uelezaji wa kipandekazi cha fasihi simulizi kama kazi ya sanaa iliyomo katika
jamii yenye jukumu linaloitikia matakwa ya jamii hiyo.
b) Uendelezwaji wa kipandekazi hicho cha fasihi simulizi katika jamii hiyo.
c) Utendajikazi wake wa jukumu au dhima ya kipandekazi hicho cha fasihi simulizi
katika jamii.
Kwa mujibu wa nadharia ya uamilifu, dhana ya utendakazi humaanisha lile jukumu
linalotekelezwa na utanzu wa fasihi simulizi katika utamaduni wa jamii fulani.
Kutokana na ufafanuzi huu, inaonekana wazi kuwa fasihi simulizi ina jukumu la
kukidhi matakwa ya jamii kwa mielekeo ya tabia na kawaida za wanajamii husika.
12
Nadharia ya uamilifu pia huzingatia kuwa, fasihi simulizi inao utendakazi maalum
katika mfumo wa jamii iliomo ndani yake. Utendakazi huu huwa ni sawa kwa tanzu
na vipera vyote vya fasihi simulizi ukiwemo utanzu wa semi ambamo ndani yake
kuna kipera cha methali kilichoshughulikiwa na utafiti huu.
Nadharia ya uamilifu imeweza kuuongoza vema utafiti huu kwani, katika utafiti huu
kilichunguzwa kipandekazi cha fasihi simulizi cha methali zilizoachwa katika
matumizi ambayo kwa sasa ni sehemu kamili ya utamaduni wa jamii za Waswahili.
Hivyo, katika utafiti huu kulielezwa kwa kina juu ya methali za Kiswahili ikiwa ni
sehemu ya semi katika fasihi simulizi sambamba na utamaduni wa Wazanzibari.
Aidha, kwa vile utafiti ulichunguza sababu na athari za kuachwa kwa methali hizo,
ile namna ya utendakazi wa jukumu au dhima ya methali katika jamii ya
Wazanzibari iliweza kuelezwa ipasavyo. Vilevile, uendelezwaji wa methali hizo
kama ni kipandekazi cha fasihi simulizi katika jamii ya Wazanzibari imeweza
kufafanuliwa ipasavyo.
1.7 Mipaka ya Utafiti
Utafiti huu ulijihusisha na methali za Kiswahili zilizoachwa. Aidha, utafiti ulijikita
katika kujua sababu na athari za kuachwa kwa methali hizo tu. Hivyo, methali
nyenginezo na maeneo mengine yanayohusiana na methali hizo kama vile muundo,
lugha na mengineyo hayakuhusishwa katika utafiti huu isipokuwa kwa kurejelea
pale ilipolazimika.
13
1.8 Muhutasari wa Sura ya Kwanza
Sura hii ilielezea juu ya usuli na tamko la tatizo la utafiti, lengo kuu la utafiti, malengo
mahususi, masuali ya utafiti, pamoja na nadharia ya utafiti, umuhimu na mipaka ya
utafiti huu. Kwa ujumla, sura ilianza na usuli wa tatizo la utafiti uliozungumzia fasihi
simulizi, umuhimu na matumizi yake semi pamoja na methali. Tamko la utafiti ambalo
ni kuchunguza sababu na athari za kuachwa kwa baadhi ya methali za Kiswahili
limebainishwa. Pia, vipengele vya nadharia, umuhimu na mipaka ya utafiti viliweza
kujadiliwa katika sura hii.
14
SURA YA PILI
MAPITIO YA MAANDIKO
Sura hii inaelezea juu ya maandiko yaliyopitiwa kuhusiana na utafiti huu. Maandiko
yalikuwa ni kuhusu fasihi simulizi na umuhimu wake, semi kwa ujumla, methali za
Kiswahili na kumalizia kwa kuonesha mapengo yaliyojitokeza kutokana na mapitio
ya maandiko hayo.
2.2 Mapitio ya Maandiko Kuhusu Fasihi Simulizi
Njogu na wenzake (2001) wameonesha umuhimu mkubwa wa fasihi simulizi katika
jamii ya Waswahili. Wakiainisha matumizi ya fasihi simulizi kuwa ni chombo cha
kuwasilishia maadili ya jamii husika, pamoja na kuiburudisha, wanasema:
Katika jamii zote fasihi simulizi imetumiwa kuwasilisha maadili na
mafungu kemkem kuhusu jamii husika. Pia, imetumika ili
kustarehesha na kuburudisha kwa namna inavyotumia lugha,
uigizaji, utendaji, taharuki na mbinu mbalimbali za simulizi. Fasihi
hujidhihirisha katika nyimbo na ngoma, mashairi, maigizo, ngano,
methali, na vitendawili. (uk.85).
Kutokana na maelezo hayo, ni wazi kuwa fasihi simulizi ina umuhimu mkubwa kwa
jamii yoyote ile ikiwemo ya Waswahili. Vilevile, nyenzo pekee yamawasiliano ya
kijamii ni lugha; lugha isiyotumia sanaa huwa haiwasilishi ujumbe mzuri na kwa
njia nzuri. Hivyo, fasihi simulizi ni njia nzuri ya kuwasilishia ujumbe kwa jamii na
kwa namna iliyobora zaidi. Aidha, wanatoa maelekezo juu ya njia bora za
ufundishaji wa lugha ya Kiswahili hasa upande wa fasihi simulizi na kuonesha
15
namna hadithi, methali na tanzu nyengine za fasihi simulizi zinavyoweza kuwa
chachu ya maendeleo ya jamii katika lugha. Pia, maelezo yao yametaja tanzu za
fasihi simulizi kuwa ni nyimbo, ngoma, mashairi, maigizo, ngano, methali na
vitendawili. Kazi hii ina mchango katika utafiti huu kwa kuonesha haja ya
kushughulikiwa kwa kutafitiwa fasihi simulizi ya Kiswahili katika tanzu zake zote
ikiwemo ya semi ambayo ndani yake methali za Kiswahili zinapatikana.
Haji (1992) anaieleza fasihi simulizi kuwa ni ile inayobuniwa bila ya kuandikwa.
Akifafanua zaidi, anasema kuwa msanii huyatoa mawazo yake kwa kutumia maneno
ya mdomo, yaani kwa kusimulia.Pia, amegusia juu ya chanzo cha fasihi simulizi
kuwa ni uwezo wa binadamu wa kuwasiliana kwa maneno (lugha); na kuwa, kwa
vile haifahamiki lugha ilianza lini,vilevile na fasihi nayo haifahamiki ilianza lini.
Ameonesha pia kuwa fasihi simlizi ni yenye kurithiwa kutoka kizazi hadi kizazi.
Akiainisha tanzu zake, amezitaja kuwa ni ngano, visasili, migani, tamthilia,
vitendawili, methali na ushairi. Dhima za fasihi simulizi amezitaja za kuburudisha,
kuidilisha, kuamsha na kudadisi. Kazi yake ina mchango katika utafiti huu kwa vile
maelezo yake yaliakisi zaidi kwa mifano ya fasihi simulizi inayotumiwa na jamii ya
Wazanzibarizikiwemo methali.
Msuya (1979) anaizingatia fasihi iwe simulizi au andishi kuwa ni sehemu ya
utamaduni wa jamii na hivyo kila jamii iwe kabila au taifa hainabudi kuwa na fasihi
yake. Anaiona fasihi kuwa ni chombo cha kuielezea na kuitazamia jamii
kiutamaduni, kiuchumi, kisiasa na kihistoria. Katika kuonesha umuhimu wake ndani
ya jamii mbalimbali, ameizungumzia fasihi simulizi kuwa ina hazina kubwa zaidi za
16
falsafa na misemo yenye nguvu kwa kuliwaza, kufunda, kusuta na kutia mori. Katika
kuonesha uhusiano wa fasihi simulizi na semi zikiwemo methali anasema kuwa
fasihi simulizi haitokamilika kama isipoonyesha methali na vitendawili.Vilevile,
ioneshe na misemo mingine ya kufumba kama nahau na tamathali za maneno yenye
mchomo na maliwazo.Katika kuonesha umuhimu wa misemo zikiwemo methali
amezielezea kuwa ni kioo cha kuwatazamia watu kwa jumla katika nyanja zote za
maisha yao iwe siasa, uchumi, utamaduni na historia. Pia, aligusia asili ya misemo
kuwa ni hadithi ndefu zilizofupishwa, na mambo mengine ya kweli yaliyotokea
katika historia ya maisha yao. Hata hivyo, ameonesha shaka yake kuwa, pamoja na
kuwa misemo (methali) ya kale iliyohifadhiwa hadi leo kuwa mingi, lakini ipo
misemo kadhaa ambayo hubadilika kwa kufuata wakati, mazingira na watu
wanaoitumia. Anaendelea kufafanua maana na matumizi ya methali kadhaa za jamii
ya Waparehukuakizihusisha na methali za Kiswahili zaidi ya mia moja na hamsini.
Kazi hii ina mchango mkubwa katika utafiti huu ingawa haikuhusiana na methali za
Kiswahili moja kwa moja.Maelezo ya Msuyayameusaidia utafitikugundua kuwapo
kwatatizo la kuachwa kwa baadhi ya methali katika jamii.Hata hivyo, Msuya
hakuonesha ni methali zipi zilizobadilishwa ama kuachwa nani sababu gani za
kuachwa kwake na hivyo kuacha pengo lililotoa mwanya wa utafiti huu kufanyika.
Haji (1983) ameilezea fasihi simulizi kuwa ni chombo muhimu cha kuhifadhi
utamaduni wa jamii. Ameelezea kuwa iwapo jamii inahitaji kuufufua utamaduni
wake, hainabudi kuvipa kipaumbele vipengele muhimu ikiwemo lugha. Kwa mujibu
wa maelezo yake anaona kuwa, lugha ikiwa ni chombo na kielelezo kimojawapo cha
jamii ni lazima iangaliwe kwa undani na mapana yake. Aidha, amesisitiza kuwa
17
kuiangalia lugha kwa upande wa maandishi pekee si busara kwani kudhani kuwa
kuimiliki sanaa ya uandishi ndio kigezo pekee cha ustaarabu, uhai na maendeleo ya
jamii ni dhana potofu, kwani maandishi hayana historia kubwa katika maisha ya
mwanadamu. Kazi yake ilitoa msukumo katika utafiti huu kwa kuithibitisha lugha
kuwa ni kpengele muhimu kinachostahiki kupewa kipaumbele katika suala zima la
kufufua utamaduni wa jamii. Hivyo, kuzishughulikia methali zilizoachwa katika
lugha ya Kiswahili ni moja ya hatua ya kuipa kipaumbele lugha.
Khamis (1983) anaanza kwa kuwakosoa wale wanaodhani kuwa fasihi simulizi
haina nafasi tena kwa jamii ya sasa hivi ilioingia katika maendeleo ya sayansi na
teknolojia. Ameeleza kuwa hoja zinazotolewa kuonesha kuwa fasihi simulizi inakufa
hazina mashiko; na kwamba, kamwe fasihi simulizi haiwezi kuvizwa kwa vile nayo
ni chombo cha maendeleo.Pia, ni kwa sababu ni chombo cha wanyonge ambao
hawawezi kukosekana katika jamii. Akizungumzia nafasi iliyopewa fasihi simulizi
ya Tanzania, ametaja kuwa ni uhuru uliopo wa kuibuni na kuitumia, kufundishwa
mashuleni na vyuoni, kutumika kwenye vyombo vya habari kama redio na
televisheni, na kuundwa kwa vikundi maalumu vya utamaduni vya binafsi na kitaifa.
Pia,ameyataja matatizo yanayoikabili fasihi simulizi ya Tanzania kuwa ni athari
zilizoachwa na wakoloni, uchunguzi na uhifadhi wake na muwamko mdogo wa
kisiasa,kuwepo kwa jamii yenye lugha nyingi na kutokuwepo inayofahamika na
kutumiwa na watu wote. Matatizo mengine ni ufundishaji wake mashuleni na
vyuoni, uchache wa vikundi vya utamaduni, kupewa nafasi ndogo na duni katika
vyombo vya habari, pamoja na uchache wa kazi zilizoandikwa kuhusiana na
nadharia ya fasihi simulizi. Kwa ujumla, kazi yake inatoa changamoto ya umuhimu
18
wa kushughulikiwa kwa karibu fasihi simulizi za jamii mbalimbali za Tanzania,
ikiwemo jamii ya Wazanzibari ambako utafiti huu umefanywa.
Mapitio haya yanayojadili fasihi simulizi kwa jumla yameonesha maana, aina,
umuhimu na matumizi yake katika jamii na kuwa ipo haja ya kuisimamia fasihi hiyo
hadi pale itakapoleta tija inayotarajiwa na jamii husika. Mapitio haya yameusaidia
utafiti huu kwa kiasi kikubwa kwa kuonesha mwanga kuhusu umuhimu na matumizi
ya fasihi simulizi katika jamii. Hali hii inaimarisha kuona kuwa utafiti wa
kushughulikia methali za Kiswahili kama ni sehemu ya kuishughulikia fasihi
simulizi ya Ki-Tanzania.
2.3 Mapitio ya Maandiko Kuhusu Semi
Mbarouk (2011) anaeleza kuwa mara zote semi hujitofautisha na lugha ya kawaida
kwa kutumia kwake sana lugha ya picha na ishara; na kwamba,hali hiyo huifanya
lugha iwe na ladha maalumu kwa msemaji na wasikilizaji. Anamnukuu Finnegan
(1970) ambaye anaonesha umuhimu mkubwa wa matumizi ya semi katika jamii hasa
za Waswahili. Katika kuonesha umuhimu huo, ameeleza kuwa ndio maana semi kwa
jamii ya Zanzibar hutumika katika sehemu rasmi na zisizorasmi.Na katika sehemu
zote hizo semi huwa zinatekeleza dhima yake kwa ukamilifu. Anataja baadhi ya
dhima za semi na kuzitolea mifano kuwa ni kutoa ushauri ama nasaha, kwa
mfano“Asiyesikia la mkuu, huvunjika guu”. Nyengine ni kutoa mafunzo ya
kiutendaji na ya kimaadili; kwa mfano“Muamini Mungu si Mtovu”. Kutumia kejeli
na vijembe; kwa mfano“Mchamaago hanyele huwenda akawiya papo”, dhima ya
19
kushawishi na kushambulia; kwa mfano“Akiba haiozi”. Kwa ujumla, kazi hii
imesaidia kiasi kikubwa katika utafiti huu, kwani katika mifano mingi ya semi
zilizotumiwa ni methali. Pia, methali hizo ni zile zinazotumiwa kila siku, na hivyo
kutoa mwanya katika kuzipambanua na zile zisizotumika kwa sasa.
Mulokozi (1996) anauelezea utanzu wa semi kuwa ni utungo wa kisanaa wenye
kubeba maana au mafumbo muhimu ya kijamii na kuuhusisha na fasihi
simulizi.Akiutofautishana tanzu nyengine, anasema kuwa semi huchukua kauli fupi
na kuziainisha kwa kuvitaja vipera vyake kuwa ni methali, vitendawili, mafumbo,
misimu, lakabu, na kauli-tauria. Pia, ameashiria baadhi ya sifa za semi kupitia fasili
yake kuwa ni za kisanaa na pia hubeba ujumbe, mafunzo au maana nzito kwa jamii.
Hivyo, semi ni muhimu kuwepo katika jamii.Hata hivyo, Mulokozi hakuainisha
mambo mengine yanayohusiana na semi kama vile maana ya semi za Kiswahili,
matumizi, historia, mitindo na miundo yake. Hivyo, ni maeneo muhimu kuyatafiti
kwa maendeleo na mustakabali wa semi za Kiswahili. Kazi hii imeusaidia utafiti huu
kwa kuziainisha methali kuwa ni miongoni mwa semi na hivyo zinabeba sifa
zilizotajwa hapo juu ikiwa ni pamoja methali za Kiswahili zilizoachwa ambazo
utafiti huu unazishughulikia.
Msuya (1979), anazungumzia semi na umuhimu wake pamoja na nafasi au dhima
yake katika jamii hasa zakale enzi za mababu. Akitolea mfano wa misemo ya
Kipare, anasema:
Misemo inayodumu inasikika Upareni mwote maana lugha ya
kipare ina utajiri mwingi sana na misemo ya methali, nahau,
20
tamathali za usemi na kadhalika. Utajiri huu unadhihirika kwa vile
mzee wa kipare akiwa ametulizana katika mazungumzo ya kijadi,
hawezi kuzungumza kwa dakika tatu tano hivi bila kubandika
methali au nahau au tamathali za maneno…Misemo yao huwa kioo
cha kuwatazamia kwa jumla, ikiwa kisiasa, kiutamaduni, kiuchumi,
kihistoria, na kadhalika. Misemo hiyo imejaa hekima na falsafa ya
juu kwa sababu ilitumika pindi walipotaka kuwaadhibu wadogo na
kuwatanabahisha wakubwa. (Bila shaka walipotenda
makosa)…Misemo ya kale ya kale iliyohifadhiwa hadi leo ni mingi,
ila mingine imebadilika kwa kufuata wakati, mazingira na watu
wanaoitumia. (uk. 9-11).
Msuya ametaja misemo mingi ya Kipare, na akaihusisha na misemo zaidi ya mia
moja na sitini ya Kiswahili katika kazi yake. Pia,amegusia falsafa ya misemo
mbalimbali na asili yake. Kazi hii iliusaidia utafiti huu kwa kuzihusisha semi na enzi
za kale; hivyo,inadhihirisha kuwa semi zikiwemo methali zimeanza zamani na jamii
hupokezana kutoka kizazi hadi kizazi kwa njia ya kurithishana. Utafiti huu unaona ni
muhimu jambo hilo kudumishwa na ndio maana ya kuamua kutafiti sababu za
kuachwa kwamethali hizo.
Kwa ujumla, mapitio hayo yanaonesha umuhimu wa utanzu huu wa fasihi simulizi
katika maisha ya kila siku ya mwanadamu na namna asivyoweza kuuepuka katika
matumizi. Hii inadhihirisha pia haja ya kuingia kwa undani zaidi kwa kuviangalia
vipera vya utanzu huu wa fasihi simulizi. Lakini kutokana na wingi wake, si rahisi
kwa utafiti mmoja kushughulikiwa vipera vyote vya semi na kwa msingi huo, ndio
maana utafiti ulikiangalia kipera kimoja tu cha semi ambacho ni cha methali.
21
2.4Mapitio ya Maandiko Kuhusu Methali
Hassan (2013) anaibainisha miktadha mbalimbali ambayo methali hutumika. Akiitaja
miktadha hiyo ni pamoja na muktadha wa pwani, wa shuleni, wa sokoni, muktadha wa
dini, wa shughuli za kazi na muktadha wa shughuli za kijamii. Mingine ni miktadha ya
kisiasa, mazungumzo ya vijana (vijiweni) na muktadha wa nyumbani. Pia, ameonesha
sababu kadhaa za methali kutofautiana baina ya jamii moja na nyingine. Anazitaja
baadhi yake kuwa ni tofauti ya kimatamshi inayosababishwa na tofauti ya lahaja,
kupanuka kwa eneo la watumiaji, na usanifishaji wa lugha. Akataja sababu ya kufanana
kwa methali baina ya jamii kuwa ni historia ya maisha ya watumiaji wa lugha
husika.Kwa mfano, watumiaji wa lugha ya Kiswahili wana asili moja ya lugha za Ki-
bantu. Akinukuu katika Jarida la Taasisi ya Elimu Tanzania(1988: 6), anasema:
Ingawa kumbukumbu za historia hazitoshi katika kufikia maamuzi
wa chimbuko halisi la lugha ya Kiswahili, ushahidi wa kiisimu
uliopo unaonesha dhahiri kuwa Kiswahili ni lugha ya Ki-bantu.
Amethibitisha pia kuwa methali hubeba maadili na falsafa ya jamii husika.Ameyataja
baadhi ya maadili, falsafa na mitazamo inayobebwa na methali kuwa ni heshima na utii
kwa wazee na wakubwa, upendo na ushirikiano, kufanyakazi kwa bidii, kumcha Mungu,
sitara, subira, utamaduni na jamii.
Hassan anamueleza Saidi (1976) kwa kusema kuwa ni mwandishi aliyekusanya methali
zaidi ya mia mbili zinazozungumzia maudhui mbalimbali na zinazotumika katika
miktadha tofauti ya kijamii. Hata hivyo, anasema mwandishi huyo hakutoa maelezo
yoyote yahusuyo methali hizo; lakini amemalizia kazi yake kwa kuweka mazoezi ya
kumtaka msomaji akamilishe methali alizopewa kama ni sehemu ya kupima ufahamu
22
wake juu ya mada ya methali iliyotolewa mifano. Yawezekana kuwa alikusudia
kuzikusanya tu na kumwacha msomaji au msikilizaji, aweze kuangalia ni ujumbe gani
unaopatikana katika methali hizo. Kwa upande mwengine, Saidi ameikumbusha jamii
baadhi ya methali ambazo zinaanza kutoweka ili jamii hiyo iweze kuzihifadhi kwa ajili
ya kizazi cha sasa na kinachokuja. Kwa kiasi kikubwa, licha ya Saidi kutozitolea
ufafanuzi wowote methali hizo, lakini kazi yake imetoa mchango wa kuionesha jamii
methali ambazo, kwa kiasi Fulani, zimeanza kusahaulika katika matumizi; na hivyo,
kuusaidia utafiti huu kuthibitisha hali ya kuachwa kwa baadhi ya methali za Kiswahili
katika jamii.
Mgulu (2011) ameonesha kuwa methali zina vyanzo vingi kwa sababu zinatumikia
vipengele vyote vya maisha ambayo yamekusanya mambo mengi yasiyo na
kikomo.Anaongeza kuwa vyanzo vya methali ni sawa na bahari isiyokuwa na kikomo.
Anavitaja baadhi ya vyanzo hivyo kuwa ni tanzu na vipera vya fasihi simulizi, ibada,
matambiko, tiba asilia, ujenzi wa maadili mema na shughuli za kiuchumi za jamii
husika. Vyanzo vingine alivyovieleza ni misiba na majanga kwa upande mmoja, na kwa
upande mwengine, ni furaha na sherehe za kijamii. Mgulu ameonesha pia hatua
zinazochukuliwa katika kuondosha uwelewa mbaya juu ya methali za Ki-Afrika ambazo
zimekuwa zikipotoshewa falsafa na ukweli wake na wataalamu kutoka nje kutokana na
kutozielewa vema lugha na tamaduni Ki-Afrika. Miongoni mwa hatua alizozitaja kuwa
zimeshaanzwa ni kuanzishwa kwa tovuti maalumu inayozitolea maelezo methali za
jamii za Ki-Afrika inayoitwa African Proverbs, sayings and stories website:
www.afriprov.org. Hatua nyengine ni kuanzishwa kwa mradi wa kukusanya wataalamu
na waandishi wazalendo waliochunguza na kukusanya methali za jamii zao kwa shabaha
23
ya kuzihifadhi. Kutokana na mradi huo, kutoka mwaka 1999 hadi mwaka 2004, vitabu
kumi na vitatu vinavyohusiana na methali viliweza kuandikwa. Kazi hii iliibua hamasa
ya mtafiti juu ya kuchunguza methali za Kiswahili zilizoachwa kwa matarajio kuwa ni
mchango mwengine mpya wa kuziendeleza, kuzitunza na kuzihifadhi za Kiswahili ikiwa
ni moja ya rasilimali ya Afrika.
Simiyu (2011) ameelezea maana, upatikanaji, ubunifu, umuhimu pamoja na matumizi ya
methali. Akizielezea methali anasema kuwa mara nyingi methali hutegemea na huwa na
uhusiano mkubwa na mazingira, muktadha na mila za jamii husika. Kupitia methali,
utamaduni wa jamii husika husawiriwa na kuakisiwa kwa namna ya pekee. Akielezea
upatikanaji wa methali anasema, aghalabu hupatikana kwa mapokeo kutoka kizazi hadi
kizazi, akiwa na maana ya kuwa vizazi hurithishana fasihi simulizi. Hata hivyo, anakiri
kuwa methali zinaendelea kubuniwa hata sasa kutokana na miktadha, wakati na mahitaji
ya jamii. Kimuundo, anaungana na wataalamu wengine walioona kuwa kwa kawaida,
methali, hasa za Kiswahili, huwa na sehemu mbili, sehemu inayoibua wazo na ile
inayolikamilisha wazo hilo.Kwa upande wa ubunifu wake, anagundua kuwa methali
hutumia lugha maalumu na teule kwa ustadi mkubwa. Lugha inayopambwa kwa sitiari,
nidaa, tashbiha, taswira, balagha, takriri, mchezo wa maneno, tamathali za semi, tanakali
sauti, pamoja na mbinu nyengine za kinudhumu. Pia, katika ufafanuzi huo anadokeza tu
muktadha wa methali na mazingira, ijapokuwa hakuhusisha na jamii maalumu.
Sambamba na hayo, anautaja wakati, pahala, na mwingiliano au kufananakwa matumizi
ya methali za jamii nyingi. Kazi yake imetoa wigo mkubwa wa umuhimu wa methali
katika jamii na kuusaidia utafiti huu katika kuona namna methali zinavyosheheni
24
matumizi ya tamathali za semi jambo linaloufanya uzikodolee macho zaidi methali
zilizoachwa iwapo zimekidhi hitaji hilo.
Madumulla (1995-2005) anaonesha kuwa methali hutokana na ujuzi, sheria na tabia za
jamii husika.Anasema: “A short sayings in common use expressing a well-known truth
or common fact ascertained by experience or observation”. Yaani; Methali semi fupifupi
zinazoelezea mambo ya kweli yanayotambulikana na wanajamii au ukweli uliozoeleka
ambao hutokana na uchunguzi wa tajriba za maisha (Tafsiri ya Mtafiti).Aidha,
amedokeza kuwepo kwa taaluma maalum inayoshughulikia kwa upana methali
mbalimbali za ulimwengu inayoitwa Perimiolojia1 na amedokeza historia ya
methali.Anamnukuu Roger Wescott ambaye anasema;
Proverbs were older than epic but more recent than riddles and
placed their dates at 5000 years ago for epic, 10,000 years for
proverbs and 15,000 years for riddles.’ (Madumulla, 2005:20).
Methali ni kongwe zaidi kuliko tenzi, lakini ni za karibuni koliko
vitendawili, kwani inakadiriwa kuwa tenzi zilianza miaka 5000
iliyopita, ambapo methali ni miaka 10,000 iliyopita na vitendawili
ni miaka 15,000 iliyopita.(Tafsiri ya Mtafiti)
Maelezo haya yanathibitisha kuwa methali zimeanza zamani na hivyo huwa ni zenye
kurithiwa kutoka kizazi hadi kizazi. Jambo hili liliusaidia utafiti huu kwa kuonesha haja
ya kushughulikiwa methali zilizoachwa kwa vile huenda urithi huo muhimu ukakatika
usiendelee iwapo hazitoshughulikiwa.
1 Kwa mujibu wa Madumulla (1995), Paremiolojia ni kitengo cha kitaaluma kinachoshughulikia kwa
upana zaidi methali mbalimbali za ulimwenguni.
25
Wamitila (2004) anaielezea maana ya methali na kuonesha umashuhuri wake katika
jamii zote duniani. Anasema utanzu wa methali ni mmojawapo wa tanzu za sanaa-
jadiiya ambazo hutambuliwa haraka kutokana na lugha yake, muundo, pamoja na
yaliyomo. Anauelezea ubunifu uliomo, anasema kuwa muundo wa methali hutumia
mbinu maalumu za lugha zilizojengwa kishairi zinazochangia kujenga kumbukumbu
katika akili za wanajamii. Kwa upande mwengine, Wamitila anaonesha vigezo
mbalimbali vinavyotumiwa na wataalamu katika uainishaji wa methali. Anavitaja
baadhi kuwa ni kigezo cha kiabjadi (Kialfabeti), kimuktadha (kidhamira), kiuamilifu
(utenda kazi), kimtindo au kimuundo, kigezo cha kimaana, pamoja na kigezo cha
kiisimu (kisarufi). Sambamba na vigezo vya uainishaji, ametaja pia baadhi ya sifa za
methali, kama vile umapokeo, matumizi, urudiaji, sifa za kisarufi na kisintakisia,
matumizi ya sitiari, sifa za kisemantiki mfano usambamba, takriri, pamoja na kweli
kinzani. Sifa nyingine ni vitambulishi vya kimaana, kwa mfano matumizi ya vikale
na visifa vya kisauti kama vile mizani, takriri konsonanti na takriri irabu. Mbali na
maelezo hayo, Wamitila katika kazi yake anaonesha dhana ya Umataifa2 wa methali
akitolea mfano methali za kiduruma na kigiriyama zinazotokana na lugha za
Kibantu, zenye uhusiano mkubwa na lugha ya Kiswahili. Pia, ameyataja majukumu
ya methali katika jamii kuwa ni ya kimaadili, kiumbuji, kielimu, ufupishaji, kuakisi
mtazamo wa jamii pamoja na majukumu ya kibalagha. Mwisho wa uchambuzi wake
anataja mifano ya methali katika Kiswahili, Kigiriyama, Kikamba, Kikuyu na
Kipokomo. Kwa ujumla, Wamitila ameonesha namna kipera hiki cha semi
kinavyoshughulikiwa kwa upana katika jamii mbalimbali duniani kupitia taaluma
2 Umataifa wa methali ni mwingiliano au mfanano unaojitokeza katika methali za jamii mbalimbali.
Mfanano huo hutokea kiumbo, kiasi cha kuonekana kama zimetafsiriwa kutoka lugha moja na kwenda
nyingine.
26
inayojulikana kama paremiolojia. Kazi yake iliusaidia utafiti huu kwa kuona upeo
wa umuhimu wa kuzishughulikia methali za Kiswahili ili nazo ziweze kutoa
mchango kwa jamii ya Waswahili na dunia kwa jumla.
Njogu na wenziwe (2001) wanaonesha namna methali na semi nyengine
zinavyoweza kufundishwa kwa wanafunzi katika skuli za sekondari na vyuo.
Wanasema ni muhimu kufundisha methali kwa kuanza kuieleza maana ya nje
inayotokana na maana za maneno yaliomo, kisha kuifafanua kwa kuielezea maana
yake ya ndani. Baadaye ni kutaja matumizi yake katika maisha ya kila siku na
wakaongezea kuwa inawezekana kuitungia kisa. Katika kazi yao, wamezitaja
methali zaidi ya mia moja na hamsini. Humo, wameonesha methali zinavyoweza
kugawika katika makundi mbalimbali ya hali zilizomo katika jamii. Miongoni mwa
makundi waliyoyataja ni pamoja na kundi la methali za zaraa, au kuhimiza na
kuonya. Kundi la methali zinazoonesha uhusiano baina ya watawala na watawaliwa.
Jengine ni la methali zinazoelemea upande wa sayansi. Methali zinazorejelea katika
ngoma, muziki, kucheza, kuimba, midundo na hata ala za miziki. Methali
zinazofungamana na ulimwengu na anga yake. Makundi mengine ni ya methali
zinazohusu elimu, magonjwa na matibabu, bahari, pwani na yalioko, jinsia na zile
zinazohusu ujenzi. Kazi hii imeusaidia utafiti katika kuonesha mawanda ya methali
na namna yalivyozivaa nyanja zote za maisha ya wanadamu katika jamii. Hali hiyo
inaonesha upeo wa matumizi ya methali katika jamii na kuuthibitisha umuhimu
wake.
27
King‟ei na Ndalu (1999) wanaonesha umuhimu na mfano mzuri wa kuzihifadhi
methali za Kiswahili. Mbali na kutoa maana pana, usuli, sifa pamoja na dhima za
methali za Kiswahili,pia wameorodhesha methali za Kiswahili zaidi ya elfu mbili na
mia tano.Hivyo,kuifanya kazi yao kuwa ni ya kwanza iliyodhihirisha utajiri mkubwa
wa jamii ya Waswahili kuhusu methali. Methali hizo wamezipanga kwa mpango wa
kialfabeti, na kila moja wameitolea maana yake ya juujuu (nje), makusudio (maana
ya ndani) na matumizi yake. Kazi hii iliufaidisha utafiti huu kwanza kwa kuonesha
wingi wa methali za Kiswahili.Jambo hili liliangaziwa kwa undani zaidi kwa
kuhusishwa na sababu za kuachwa kwa baadhi ya methali nyengine katika matumizi
ya kila siku katika jamii ya Wazanzibari.Ingawaje methali nyingi zimekuwa na
tofauti ndogo ya namna zinavyotamkwa na jamii ya Wazanzibari, kwa vile
zimeandikwa kwa matamshi ya lahaja ya kimtang‟ata nchini Kenya. Pili, ni kazi
iliyotumika katika kuzibainisha methali zilizoachwa katika jamii ya Wazanzibari.
Hata hivyo, kazi hii haijagusia sababu na athari za kuachwa huko kwa jamii.
Njogu na Chimerah (1999) wanazielezea methali kuwa ni muhutasari wa wazo la
busara kwa mkato na kuzihusisha na mashairi.Hii ni kwa sababu pamoja na ufupi
wake, ndani yake hubeba takriri, vina na hata mizani (katika baadhi ya methali). Pia,
wameonesha umuhimu wa methali kufundishwa mashuleni na kutoa miongozo
mizuri ya namna ya ufundishaji wake ili kuzidi kuzipa uhai wa kimatumizi ndani ya
jamii husika, hasa kwa vijana ambao wanahofiwa si waelewa wa matumizi ya
methali kwa vile nyingi zao hawazifahamu. Ufafanuzi wao ulitoa msukumo mpya
wa kuzishughulikia methali ikiwa ni pamoja na namna ya kuzifundisha. Jambo hilo
28
liliusaidia utafiti huu kwa kuzirudishia methali zilizoachwa uhai wake iwapo fikra ya
kuzifundisha itafanyiwakazi.
Mtesigwa (1989) anaonesha wingi wa methali zilizopo katika jamii za Ki-Afrika
kwa kusema kuwa Lugha za binadamu zina utajiri mkubwa wa methali.Utajiri huu
umeenea na kupindukia katika lugha za Kiafrika hususan katika eneo la lugha za
Kibantu Kusini mwa Ikweta, na pia lugha za Kinegro huko Afrika Magharibi.
Amezielezea maana na sifa za methali na kubainisha ukaribu wa methali na
vitendawili na kuwa tafauti zao hubainika kupitia mbinu, muundo, na malengo ya
umbo husika. Akitaja sifa za methali ameonesha kuwa ni lazima ziwe fupi, zitumie
lugha ya kisanaa, zitoe mafunzo kwa jamii, na zivutie wasikilizaji kwa kutumia
kikamilifu tamathali za semi. Kwa maelezo yake, anaona methali lazima zitumie
lugha ya tamathali ili ziweze kukidhi haja inayokusudiwa. Maelezo hayo yametoa
msukumo katika utafiti huu kwa kuona kuwa kuna haja kubwa ya kuzichunguza
methali zilizoachwa iwapo zimekidhi mahitaji hayo kikamilifu au ni moja ya sababu
iliyosababisha kuachwa kwa kukosa mvuto unaochochewa na matumizi ya tamathali
za semi.
Shariff (1988) anabainisha namna mabalimbali za matumizi ya lugha katika jamii ya
Waswahili.Anasema kuwa Kiswahili cha kawaida kina tungo za namna tatu za
matumizi ya lugha ambazo hujitokeza zaidi. Kwanza, kuna utumiaji wa lugha
uliyowazi; pili, kuna utumiaji wa misemo; na tatu, kuna lugha ya kimafumbo
itumiwayo mara nyingi zaidi kiasi cha kuwaona Waswahili kuwa ni watu
wanaopenda sana kutumia misemo na mafumbo katika mazungumzo yao. Aidha,
29
ameonesha maana ya misemo, asili na matumizi yake. Pia, ameonesha kuwa baadhi
ya misemo, hasa ya zamani husahauliwa na jamii. pia, mingine huendelea kubuniwa
kila leo.Anasema:
Misemo mingi ya lugha hii inatokana na hekima za wajuzi wenye
busara. Misemo mingi huwa imepokewa kutokana na wavyele kama
lugha yenyewe, kwa jumla ilivyo. Tunaweza kusema kuwa baadhi
ya misemo ya zamani imekwishasahauliwa, lakini ni kweli pia
kuwa misemo mipya hutungwa na wasemaji wa lugha waliohai,
kwani katika kila zama hakukosekani watu wenye busara na wenye
kutunga misemo yao wenyewe inayolingana na mawazo yao ya
hekima… Misemo aghalabu ni maelezo juu ya jambo au mambo
fulani kwa mukhtasari na kwa lugha ya kuvutia. (Uk. 80).
Msamiati wa misemo katika kazi hii umekusudiwa kujumuisha vipera vyote vya
utanzu wa semi ikiwemo misemo yenyewe, methali na vipera vyengine. Kazi yake
imeusaidia utafiti huu kugundua ukweli kuwa methali bado huendelea kubuniwa, na
hivyo, kuanza kufikiria kwamba huenda ikawa ni moja ya sababu za kuachwa baadhi
ya nyengine.
Haji (1983) anaonesha usanii wa hali ya juu unaopatikana katika methali na
vitendawili. Ameanza kwa kukanusha madai yasemayo kwamba fasihi simulizi si
fasihi kwa sababu ina kasoro ya sanaa. Anaona kuwa kuwafikiria wakulima na
wafanyakazi hawawezi kuwa wasanii wa kiwango cha juu ni kasoro za kifikra na
kwamba kutokujua kuandika si sababu ya kuifanya jamii hiyo isiweze kuwa na
fasihi. Hayo yote ni mawazo dhaifu yasiyo na mashiko yoyote. Akibainisha usanii
unaopatikana katika methali, ametolea mifano methali za“Asolijua chozi amtazame
aliaye”, “Kuzunguka mbuyu si dawa ya shetani”, na “Kuku wa masikini hatagi;
30
akitaga haangui; akiangua halei”. Katika mifano hii, kuna matumizi ya sitiari, lugha
ya picha, na urejeshi, ambavyo vimejikita vema katika methali hizo na nyingi
nyinginezo za Kiswahili. Mbali na mbinu hizo, Haji anabainisha mbinu nyengine za
kisanaa kuwa ni lugha ya kishairi, mapigo, na takriri. Anatolea mfano wa methali ya
“Mchezea chuma huchuma, kama hakuchuma, tumbo hunguruma”. Mbinu nyengine
za kisanii zilizomo katika methali za Kiswahili ni tash-hisi na utumiaji wa maneno
machache.Anatoa mifano ya matumizi ya mbinu hii katika methali zifuatazo: “Kizito
huonjwa”, “Kieleacho huzama” na “Ndugu mtambie, usimkalie”. Kazi hii
inaubainisha kwa undani zaidi usanii wa methali, na hivyo, kuufaidisha utafiti huu
kuona tafiti zinazohusiana na methali ni miongoni mwa tafiti za kifasihi. Kwa
upande mwengine ni kazi iliyoufaidisha utafiti kwa kuona kuwa ipo mitazamo
dhaifu ya baadhi ya watu juu ya fasihi simulizi na kuonesha kuwepo kwa haja ya
kulichunguza jambo hili kwani linaweza likawa ni sababu ya kuachwa kwa baadhi
ya methali au athari zake kwa jamii.
Finnegan (1979) anaziona methali kuwa ni hazina kubwa iliyomo katika lugha za
wanadamu. Anazichukulia methali kuwa ni utajiri uliomo ndani ya lugha hasa zile za
Ki-Afrika hususan lugha za Kibantu. Katika kuueleza umuhimu wa methali katika
lugha anasema methali ambazo hutumika kama lugha ni muhimu kwa uhai wa
binadamu ambapo bila ya kuwepo kwake lugha inaweza kubakia lakini itabakia
kama umbo lisilo nyama, damu na roho.Finnegan anaziona methali kuwa ni mfano
halisi wa sanaa ya maneno yalioteuliwa kwa umakini mkubwa ili kutunza kwanza,
picha halisi ya jambo fulani.Pili, ni kuipatanisha hali halisi hiyo na funzo au maadili
fulani yanayokusudiwa katika jamii husika. Mtaalamu huyu ametoa maana ya
31
methali, kuonesha baadhi ya miundo na matumizi yake katika jamii ambapo
imeusaidia utafiti huu kutambua mchango mkubwa wa methaliza Afrika zikiwemo
za Kiswahili ambazo sehemu yake utafiti huu unazishughulikia.
Farsy (1979) anawazindua watu juu ya suala la kuweka kumbukumbu za
kimaandishi katika tanzu za fasihi simulizi hasa hadithi, methali na vitendawili. Hii
ni kwa sababu bila ya kufanya hivyo, urithi huu mzuri husahauliwa, na hatimaye
kupotea kabisa; jambo ambalo halifai kuachwa litokee kutokana na umuhimu wake
katika jamii. Farsy anaeleza:
Sikuzote napenda kushughulika na Kiswahili na jambo hilo
limenitia bidii kuandika kila methali niliyosikia katika mazungumzo
yangu, na hasa katika mazungumzo yangu na wazee. Methali
zinafaa sana kwa mafundisho ya adili; kwa hiyo ni jambo la
muhimu kwa waalimu kujua methali nyingi kama inavyowezekana,
na kuzitumia sana katika mafundisho yao. (Uk.i)
Farsy pia amebainisha kuwa waswahili wana utajiri mkubwa wa hadithi, methali na
vitendawili vilivyokusanya mambo mengi ya imani na desturi, kiasi kwamba si
rahisi kwa mtu mmoja kukamilisha zoezi la kuzikusanya kwa ukamilifu. Pia,
ameeleza kusudio la kuwahamasisha watu kuandika ni kuepuka kupoteza hazina na
rasilimali hiyo kutokana na kusahauliwa na jamii kutokana na jamii hiyo kukabiliwa
na mambo mengine ya kisasa. Katika kazi yake amekusanya methali zaidi ya mia
tano za Kiswahili na kuzitolea maana zake kwa lugha ya Kiingereza. Aidha,
ameandika kwa kutumia utaratibu wa kiabjadi, hivyo kumpa wepesi msomaji
anayekusudia kutafuta methali maalumu. Kazi hii ni miongoni mwa hazina kubwa
zilizouwezesha utafiti huu kupata data halisi za methali zilizoachwa kutumiwa katika
jamii pamoja na baadhi ya sababu zake.
32
2.5Mapengo Yanayojitokeza Kutokana na Mapitio ya Maandiko
Kwa Wataalamu waliojadili methali za Kiswahiliwanakubalianakimawazo katika
vipengele vya maana, sifa, matumizi, na muundo, dhima katika jamii, matumizi
katika tamathali, pamoja na kubeba kwake ukweli na falsafa ya jamii husika. Hata
hivyo, kazi hizobado zinatuibulia mapengo yafuatayo: Mosi niubainifu wa methali
za Kiswahili zilizoachwa na jamii ya Wazanzibari.Pili, ni kutofahamika sababu za
kuachwa kwa methali hizo.Tatu ni kutofahamika athari za kuachwa baadhi ya
methali kwa jamii ya Wazanzibari. Hivyo, mtafiti aliamuakulifanyia utafiti suala hili
la kuachwa kwa baadhi ya methali za Kiswahili katika jamii ya Wazanzibari ili
kuuziba mwanya huo uliojitokeza.
2.6 Muhutasari wa Sura ya Pili
Sura hii ilielezea juu ya maandiko yaliyopitiwa kuhusiana na utafiti huu. Maandiko hayo
yalikuwa ni kuhusu fasihi simulizi na umuhimu wake, semi kwa ujumla na methali za
Kiswahili. Sura ikamalizia kwa kuonesha mapengo yaliyojitokeza kutokana na mapitio
ya maandiko hayo.Sura inayofuata imejadili juu ya usanifu na mbinu za utafiti.
33
SURA YA TATU
USANIFU NA MBINU ZA UTAFITI
3.1 Utangulizi
Sura hii imeelezea juu ya mbinu, vifaa na mambo mbalimbali yaliyohusishwa katika
utafiti huu. Sehemu imeeleza mbinu na vifaa vya utafiti, mpango wa utafiti na
walengwa wa utafiti. Aidha, sehemu hii imeonesha jamii ya watafitiwa, mbinu za
kupatia sampuli, eneo la utafiti, ukusanyaji na uchambuzi wa data, udhibiti na miiko
ya ukusanyaji wa data.
3.2 Mpango wa Utafiti
Utafiti ulifanyika maktabani na uwandani. Maktaba zilitumika kufanya mapitio ya
maandiko. Mambo yaliyohusishwa katika eneo hili, ni usomaji wa vitabu vya
taaluma ya utafiti, lugha, na fasihi. Pia, zilisomwa makala, magazeti, majarida, tafiti
zilizotangulia, pamoja na ripoti.Kwa upande wa uwandani, maeneo yaliyohusika na
ukusanyaji wa data kwa njia za uchunguzi, udodosaji, mijadala ya vikundi na
mahojiano ni katika vyuo vikuu vilivyopo Zanzibar ambavyo ni Chuo Kikuu cha
Taifa cha Zanzibar, Chuo Kikuu cha Zanzibar na Chuo Kikuu cha Elimu cha
Zanzibar.Mitaa minne kutoka Mkoa wa Mjini Magharibi ambayo ni Sogea na
Kikwajuni kwa Wilaya ya Mjini na Mwanakwerekwe na Fuoni kwa Wilaya ya
Magharibi. Eneo jengine ni katika taasisi za BAKIZA na TAKILUKI. Maeneo yote
haya yaliweza kufikiwa ipasavyo.
34
3.3 Eneo la Utafiti
Utafiti huu ulifanyika katika Mkoa wa Mjini Magharibi katika kisiwa cha Unguja.
Eneo hilo lilihusisha vyuo vikuu vitatu; Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, Chuo
Kikuucha Zanzibar na Chuo Kikuucha Elimu cha Zanzibarili kupata Wakufunzi na
Wanafunzi wa fasihi ya Kiswahili. Pia, utafiti ulihusisha taasisi za BAKIZA na
TAKILUKI zinazohusiana na lugha ya Kiswahili na fasihi yake ili kupata wataalamu
wa lugha na fasihi ya Kiswahili. Vile vile ulihusisha mitaa ya Kiwajuni, Sogea,
Mwanakwerekwe na Fuonikwa ajili ya kupata wazungumzaji wa kawaida wa lugha
ya Kiswahili. Sababu yakuteuliwa eneo hilini kuwa katika Zanzibar ndio Mkoa
pekee wenye mchanganyiko wa watu kutoka sehemu zote za Zanzibar.Hii
ilirahisisha upatikanaji wa taarifa zilizokusudiwa. Aidha, ni maeneo yenye wazee
mashuhuri, watu wa kawaida na maskani wanamozungumza watu shughuli zao za
kiuchumi, siasa na utamaduni.Kwa upande wa maktabani maktaba nne zilihusishwa
katika utafiti huu ambazo ni maktaba za SUZA, UCEZ, UDOM pamoja na maktaba
kuu ya Zanzibar. Lengo la kwenda maktaba hizo ni kupata maandiko mbalimbali
yaliyohusiana na utafiti huu.
3.4 Walengwa wa Utafiti
3.4.1 Jamii Tafitiwa
Jamii tafitiwa ilihusisha makundi yafuatayo:
a) Wakufunzi na Wanafunzi wa lugha ya Kiswahili na fasihi katika vyuo vikuu.
35
c) Wazee wenye ufahamu na uzoefu wa matumizi ya methali katika mitaa.
d) Watu wa kawaida wanaozungumza lugha ya Kiswahili mitaani.
e) Wataalamu kutoka taasisi zinazohusiana na lugha ya Kiswahili na fasihi yake.
f) Methali za Kiswahili zinazotumiwa na jamii ya Waswahili wa Zanzibar.
g) Maandiko mbalimbali yahusuyo fasihi simulizi na semi kwa umashuhuri wake.
3.4.2 Aina na Dhana ya Usampulishaji
Sampuli hiyo ya walengwa ilipatikana kutokana na maumbile ya utafiti husika pamoja
na mkabala uliyouongoza utafiti wenyewe. Sampuli ilipatikana kwa kutumia njia ya
sampuli lengwa kwa kuwa ni mwafaka kwa utafiti wa kitaamuli kama huu. Kwa hivyo,
watafitiwa walichaguliwa kulingana na matakwa ya utafiti huu. Hivyo, kutokana na
makundi ya walengwa wa utafiti huu, jamii ya watafitiwa ilikuwa na watu mia moja na
ishiriniiliyogawanywa kama ifuatavyo:
a) Wakufunzi sita na Wanafunzi thalathini wa somo la fasihi ya Kiswahili kutoka
katika vyuo vikuu vilivyoteuliwa. Uzoefu wakusoma maandiko yanayohusu methali
utasaidia kugundua tofauti ya sasa na zamani katika matumizi ya methali.
b) Wazee sita wenye ufahamu na uzoefu wa matumizi ya methali kutoka katika
mitaa ya iliyoteuliwa. Watu hawa wanaaminika kuwa na kumbukumbu za methali
zilizoachwa.
c) Wazungumzaji wa kawaida thathini na mbili kutoka katika mitaaminne
ilioteuliwa. Lengo ni kupata uwelewa wao kuhusu methali zilizoachwa.
36
d) Wataalam wane wa lugha ya Kiswahili na fasihikutoka taasisi zilizoteuliwa. Watu
hawa wana uzoefu wa tafiti mbalimbali zinazohusiana na fasihi ya Kiswahili.
e) Wanafunzi ishirini na nne wa kadato cha sita,kumi wa Diploma wanaosoma fasihi
ya Kiswahili pamoja na walimu sita wa skuli ya sekondari wa somo la fasihi. Lengo
ni kuhakiki methali wasizozifahamu miongoni mwa zilizokusanywa kwa utafiti huu.
3.5 Ukusanyaji wa Data
Njia na zana mbali mbali zilitumika ili kurahisisha zoezi zima la ukusanyaji wa data
zinazohitajika katika utafiti huu. Njia na zana zilizotumika ni hizi zifuatazo:
3.5.1 Njia na Zana za Ukusanyaji wa Data
Katika utafiti huu njia zifuatazo ziliweza kutumika:
3.5.1.1Udurusu wa Kimaktaba
Udurusu ulifanyika katika maktaba nne za Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar,
Chuo Kikuu cha Dodoma, Chuo Kikuu cha Elimu cha Zanzibar pamoja na maktaba
kuuya Zanzibar. Katika maktaba hizo, vitabu vya taaluma ya utafiti, lugha, na fasihi
viliweza kupitiwa. Aidha, makala, majarida, tafiti zilizotangulia, ripoti na maandiko
mbalimbali yaliyosaidia kupata data zilizohitajiwa yalisomwa kupitia maktaba hizo.
Zana zilizotumika kwa njia hii ni daftari na kalamu kwa ajili ya kuandikia
kumbukumbu za maandishi muhimu yaliopatikana katika maandiko kama ni data za
utafiti.
37
3.5.1.2 Mahojiano
Mahojiano yalifanyika kwa Wazee sita wenye uwezo mzuri wa kuzifahamu na
kuzitumia methali kutoka mitaa minne iliyoteuliwa kutoka Mkoa wa Mjini
Magharibi. Pia, ilitumika kwa Wataalamu wanne kutoka taasisi za BAKIZA na
TAKILUKI. Mbinu hii iliwezesha kupatikana taarifa zilizosahihi kwa kiasi kikubwa.
Zana zilizotumika kwa njia hii ni daftari, kalamu, kamera ya picha jongefu pamoja
na muongozo wa usaili uliotayarishwa.
3.5.1.3 Mjadala wa Vikundi
Njia hii ilitumiwa katika utafiti huu kwa wanafunzi ishirini na nne wa kidato cha sita
skuli tatu za sekondari; Chukwani, Lumumba na Bembela, wanane kila skuli,
wanafunzi kumi wa Diploma chuo cha Ualimu Mazizini na kwa walimu sita wa
Kiswahili kutoka Skuli ya Mwembeladu. Zana zilizotumika katika njia hii ni daftari,
kalamu, simu yenye picha na kinasa sauti, orodha za methali na muongozo wa usaili.
3.5.1.4 Udodosaji
Njia hii ilitumiwa kwa Wakufunzi sita wawili kutoka kila Chuo, baina ya SUZA, UZ
na UCEZ na kwa Wanafunzi thalathini wa shahada ya kwanza wa fasihi ya
Kiswahili kumi kutoka kila chuo. Njia hii ilitumia za ya dodoso zilizogawiwa kwa
watafitiwa.
38
3.5.1.5 Uchunguzi
Njia hii ilitumika kwa kuhudhuria katika baadhi ya misiba na sherehe za arusi. Pia,
katika baraza za mazungumzo za vijana na wazee katika mitaa iliyoteuliwa. Sehemu
hizi mtafiti alichunguza matumizi ya methali za Kiswahili kwa ujumla wake katika
mazungumzo yao ya harakati za maisha yao. Zana ziliotumika katika njia ni shajara,
kalamu pamoja na simu yenye picha jongefu na mgando na kinasa sauti.
3.5.2 Zana za Kukusanyia Data
Zana zilizotumika katika utafiti huu ni za kuhifadhia sauti, picha na
maandishi.Miongoni mwa zana hizo ni shajara, daftari, kalamu, karatasi, kamera ya
picha jongefu, simu yenye picha jongefu na mgando na kinasa sauti. Zana hizo
zilitumiwa katika njia mbalimbali za kukusanyia data ambazo ni za mahojiano,
udodosaji, uchunguzi, mijadala ya vikundi na udurusu wa maktaba kama
zilivyoelezewa hapo juu.
Zana nyengine muhimu zilizotumika ni Kompyuta na flashi.Hizi ni
zanazilizotumiwa tokea mwanzo hadi mwisho wa utafiti huu. Zana hivi
zinategemeana katika kazi zake na zilihitajika sambamba. Katika utafiti huu
kompyuta na flashi zilitumika kuhifadhia mahunzi laini (soft copy) ya kazi zote
zilizohusiana na utafiti ikiwa ni pamoja na data za maktabani, uwandani pamoja na
ripoti nzima ya utafiti. Kwa upande wa kompyuta mbali na kuhifadhia data za utafiti
na ripoti, katika utafiti huu ilitumika kama ni sehemu ya maktaba ambapo mtafiti
alisoma vitabu na nyaraka zilizohusiana na utafiti zinazopatikana mtandaoni.
39
Pia,ilitumika kuchapishia mchanganuo wa data na ripoti ya utafiti. Kwa jumla,zana
hizizilitumika muda wote wa kazi ya utafiti na hata baada yake.
3.5.3 Mchakato wa Ukusanyaji wa Data
Mtafiti alitumia daftari na kalamu kukusanyia data za Maktabani. Kisha alitumia
shajara, daftari, kalamu, karatasi, kamera ya picha jongefu, simu yenye picha
jongefu na mgando na kinasa sauti kukusanyia data za Uwandani kupitia njia za
mahojiano, udodosaji, uchunguzi pamoja na mijadala ya vikundi.
Katika hatua ya kuzitafuta datahizo, njia na zana mbalimbali zilitumika. Moja ni njia
ya udurusu wa kimaktaba. Katika njia hii, kazi kama vile Swahili Sayings ya Farsi
(1958), Yatokanayo na Fasihi Simulizi ya Msuya (1979), Kamusi ya Methaliya
King‟ei na Ndalu (1989), na Tanzu za Lugha ya Njogu na wenzake, Nafasi yaFasihi
Simulizi katika Jamii ya Tanzania ya Khamis (1983), na Athari za Semi za
Kangakatika Jamii, ni miongoni mwa kazi zilizoupa utafiti huu utajiri mkubwa wa
kuzipata methali za Kiswahili, sababu pamoja athari zake kwa jumla.Njia nyengine
ziliyotumiwa kuzipata data za utafiti huu ni za mjadala wa vikundi,mahojiano na
dodosoambapo kwa njia hizo vilevile methali, sababu na athari nyingi zilipatikana.
Kwa mfano, katika mjadala na walimu wa somo la Kiswahili. Mtafiti aliweza
kukusanya zaidi ya methali mia moja na thalathini na sababu na athari kwa wastani.
Pia, methali zilikusanywa kupitia njia ya kisasa ya kutafuta katika mtandao nakupata
kurasa zilizo andikwa methali za Kiswahili. Kwa mfano, katika Blog ya Mwambao
ndani yake kuna methali za Kiswahili zilizoitwa za Mwambao mia tatu thamanini na
40
nne zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiingereza. Njia ya uchunguziilitumika katika
baadhi ya baraza za wazee, maskani za vijana, katika misiba na sherehe za harusina
kupata methali za Kiswahili. Kutokana na njia zote hizo, mtafiti alifanikiwa
kukusanya methali mia tano na ishirini na sita, sababu na athari zaidi ya ishirini kila
moja, kiwango ambacho kiliweza kutosheleza kuzibainisha methali zilizoachwa
miongoni mwazo, pia sababu na athari za msingi, kazi ambayo ndio iliyofanywa
baada ya hatua hiyo.
3.6 Uchanganuzi wa Data
Uchanganuzi pamoja na uwasilishaji wa matokeo ya data za utafiti huu ulifanywa
kwa umakini mkubwa kwa njia ya maelezo huku ikihusishwa kwa ukamilifu misingi
ya nadharia ya uamilifu iliyoteuliwa kuuongoza utafiti huu. Aidha, data zote
zilizopatikana maktabani na uwandani, zilichanganywa na kuchanganuliwa vyema
kwa mujibu wa malengo mahasusi ya utafiti. Uchanganuzi wa data ulikuwa kama
ifuatavyo:
Hatuazilizotumiwa katika kuzibainisha methali zilizoachwa ni hizi zifuatazo:
Kwanza ni mtafiti kuipitiya orodha ya methali zilizokusanywa. Kwa njia hii, methali
mojamoja ilifikiriwa iwapo inafahamika au la. Kila methali iliokumbukwa
iliwekewa alama na isiyokumbukwa iliachwa. Zoezi hilo lilibainisha methali
zinazojulikana na zile ambazo hazikumbukwi miongoni mwa zilizokusanywa. Hatua
ya pili ni kuzisikiliza methali ambazo hazikukumbukwa katika vikundi vya
majadiliano. Kila kikundi kilitakiwa kukumbuka methali wanazozifahamu huku
41
zikifuatiliwa kwa makini zile zisizokumbukwa katika hatua ya awali iwapo zitaweza
kutajwa katika vikundi. Hatua hii ilweza kuzibainisha zaidi methali zinazojulikana
na zisizokumbukwa miongoni mwa zile zilizotengwa hatua ya kwanza. Hata hivyo,
hatua hii haikuweza kuzipambanua wazi zile zilizoachwa kwani baadhi yake zimo
zilizoshuhudiwa kutumika katika sehemu tofauti za uchunguzi wa utafiti huu. Hivyo,
katika methali ambazo hazikutajwa zimo zilizoachwa kwa kutojulikana na zimo
zilizoachwa kwa kusahauliwa, jambo lililosababisha kuwepo kwa hatua nyengine ya
kuzipambanua aina mbili hizo.
Hatua ya tatu ni kwenda katika madarasa matatu ya wanafunzi wa kidato cha sita,
darasa la wanafunzi wa diploma na walimu wa Kiswahili. Katika hatua hii, methali
ilitajwa sehemu yake ya mwazo na kuwaachia wanafunzi waimalizie methali hiyo
sehemu ya mwisho. Kigezo cha mtafiti katika majaribio haya matano, ni kuwa kila
methali iliyoweza kukamilishwa ndio iliosahauliwa kutajwa katika jaribio la hatua
ya pili na iliowashinda kuijaza ndio isiyojulikana na hivyo kuwa ni miongoni mwa
zile zilizoachwa. Hatua hii ilizibainisha methali zilizosahauliwa na zilizoachwa.
Pamoja na ubainifu wa hatua hiyo, mtafiti alitaka kuhakikisha zaidi kuhusu methali
hizo kwa hatua ya mwisho ya kuzihakiki.Katika kuzihakiki methali zilizoachwa,
kwanza aliwapelekea watu maalum watano waliozipitia moja moja ili kubaini iwapo
zipo walizowahi kuzisikia zikisemwa mtaani, redioni au sehemu yoyote, au kuziona
katika maandishi au kuzikumbuka kwa namna yoyote ile. Pili, ni kwa ulinganisho
wa mtafiti katika mapitio ya maandiko ya baadhi ya kazi za miaka ya thamanini na
kurejea nyumba na zile miaka ya tisini hadi mwaka 2014. Na tatu ni katika
42
uchunguzi wa mazungumzo ya Wazanzibari katika baadhi ya baraza zao za
mazungumzo na katika baadhi ya shughuli zao za kijamii zilizohudhuriwa na mtafiti.
Katika hatua ya kuchanganua data zenye sababu za kuachwa kwa methali hizo,
kwanza ziliwekwa sababu zote zilizobainika kupitia udurusu wa maktaba katika
dodoso, mahojiano na mijadala ya vikundi ambapo mtafitiwa aliichunguza kila
sababu na kuikubali aliyoiona ndio na kuikataa aliyoiona sio hatua ambayo
ilizithibitisha baadhi na kuziondoa nyengine. Katika hatua nyengine watafitiwa hao
mbali na kutakiwa kukubali au kukataa sababu zilizopitia udurusu wa maktaba, pia
walipewa uhuru wa kutoa sababu wanazoziona ndizo na ambazo hazijatajwa. Kupitia
fursa hii sababu kadhaa zilitajwa ambazo zilichambuliwa na kuwekwa katika
mafungu stahiki.
Uchanganuzi wa data zilizolenga kupata athari, nazo zilikusanywa kupitia njia
zilizotajwa hapo juu ambapo mtafitiwa alitakiwa kutaja athari anazozijua yeye.
Watafitiwa walitoa athari nyingi ambazo katika uchambuzi wake athari
zinazolingana ziliwekwa kundi moja. Hatua hiyo ilikuzikusanya athari hizo katika
makundi na kuziondoa zile ambazo zilizoonnekana sio za msingi. Aidha, makundi ya
athari hizo yalichambuliwa kwa kina zaidi hatua iliyobainishakuwapomakundi
yaliyohusiana na mengine ambayo yaliunganishwa pamoja. Makundi hayo nayo
yalichanganuliwa ili kubaini ya athari zenye madhara na ya athari zenye tija kwa
jamii.
43
3.7 Uhalali na Uthabiti wa Matokeo ya Utafiti
Uhalali wa matokeo ya utafiti ni namna ya kuyafanya maotokeo ya utafiti yawe na
maelezo yenye vigezo vinavyopima mambo yaliyotakiwa kupimwa katika utafiti huo.
Ambapo, uthabiti wa utafiti ni namna utafitiunavyoweza kutoa matokeo yanayofanana
na tafiti nyingine za baadaye zinazolingana nao. Uhalali na uthabiti ni vipengele
vinavyohusiana na kutoshelezana katika utafiti.hivyo, ni vigumu kuwa na utafiti
wenye matokeo yaliyo thabiti lakini yasiwe na uhalali wa matokeo hayo (Kothari,
2009).
Kwa mujibu wa Ponera (2010), uhalali wa matokeo ya utafiti huthibitishwa kwa
mambo kama vile: Kwanza, ni kupitia kuyabainisha malengo ya utafiti pamoja na
mipaka yake. Pili, ni kupitia matumizi mazuri ya njia za kukusanyia data
yanayowezesha kupata data zinazotoa matokeo ya utafiti kwa kiwango cha uthabiti
kinachoridhisha. Tatu, ni kupitia matumizi ya lugha nyepesi na rahisi kufahamika
kwa watafitiwa juu ya kinachotafitiwa hali inayoyafanya majibu wanayoyatoa
yahusiane na yalingane na malengo ya utafiti husika. Hivyo basi, utafiti huu
uliofanywa pia ulijiegemeza katika misingi hii ili kuweza kujenga uhalali na uthabiti
wa matokeo yake. Hivyo, matokeo ya utafiti huu ni thabiti na halali.
3.8 Itikeli za Utafiti
Kwa mujibu wa Ponera (2010), itikeli za utafiti ni kanuni na mmiko yote ya kisheria,
kijamii na kiutamaduni inayopaswa kuzingatiwa na kufuaywa wakati wa ukusanyaji
44
wa data za uwandani. Katika ukusanyaji wa data za utafiti huu, kanuni ya kuchunga
miiko yote ya utafiti iliyohitajika zilifuatwa. Hivyo, masuala ya kupata vibali vya
ruhusa ya kufanya utafiti kutoka Chuo Kikii cha Dodoma, Serikali ya Mapinduzi
Zanzibarna sehemu nyengine zilizohusika yalifuatiliwa kabla kuanza kwa utafiti.
Aidha, masuala kama vile kutunza siri za taarifa, ridhaa ya watafitiwa pamoja na
kutoainisha majina yao yalizingatiwa kikamilifu. Hali hiyo, ilizingatiwa pia katika
uchukuaji wa picha na sauti kwa baadhi ya watafitiwa wa utafiti huu kwa kadri
ilivyowezekana, kwa ajili ya kuweka kumbukumbu nzuri za utafiti.
3.9 Muhutasari wa Sura ya Tatu
Sura ya tatu imeelezea juu ya mbinu, vifaa na mambo mbalimbali yaliyohusishwa na
kazi ya ukusanyaji na uchambuzi wa data. Aidha, imeeleza mbinu zilizotumika
katika utafiti huu ni udurusu wa maktaba, dodoso, mahojiano na mijadala ya vikundi.
Kwa upande wa vifaa vilivyotumika ni madaftari, kalamu, miongozo ya usaili,
kamera, na simu.Sura imeelezea mpango na walengwa wa utafiti. Pia, imeonesha
jamii ya watafitiwa, mbinu za kupatia sampuli, eneo la utafiti, ukusanyaji na
uchambuzi wa data, udhibiti na miiko ya ukusanyaji wa data. Sura ya nne inajadili
juu ya uwasilishaji na mjadala wa matokeo ya utafiti.
45
SURA YA NNE
UWASILISHAJI NA MJADALA WA MATOKEO YA UTAFITI
4.1 Utangulizi
Sura hii ina uchambuzi wa data za utafiti.Sura inaundwa na sehemu kubwa
nne.Sehemu ya kwanza inajadili juu ya methali zilizoachwa katika jamii ya
Wazanzibari. Sehemu ya pili inajadili sababu za jamii ya Wazanzibari kuacha baadhi
ya methali. Sehemu ya tatu inajadili athari za kuachwa kwa baadhi ya methali hizo.
Sura inamalizia kwa muhutasari wa matokeo ya mjadala huo.
4.2Methali za Kiswahili Zilizoachwa katika Jamii ya Wazanzibari
Nadharia iliyotumika katika utafiti huu inamtaka mtafitikuelezea utamaduni wa jamii
inayotumia utanzu wa fasihi simulizi unaotafitiwa ambao, katika utafiti huu ni methali
za Kiswahili zilizoachwa ili kusaidia kufahamu umuhimu wake kabla ya kuueleza na
kuuchunguza utendakazi wa utanzu husika. Hivyo, maelezo yanayofuta yanakusudiwa
kutekeleza hitaji hilo.
4.2.1 Miktadha ya Maisha ya Jamii ya Wazanzibari
Kwa mujibu wa Shariff na Mazrui (1994), Waswahili wameelezewa katika maana
mbalimbali kulingana na mielekeo ya watoaji wa maana hizo. Anasema baadhi
wamewaeleza Waswahili kwa kuwanasibisha na uafrika, baadhi wamewanasisha na
lugha na wengine wamewanasibisha na eneo la kijografia.Ananukuu baadhi ya maana
46
hizo anasema maana iliyotolewa katika Encyclopaedia Britanica kwa kiingeraza kuwa
Waswahili ni waliochanganya damu ambayo ni matokeo ya muda mrefu ya kuingiliana
kati ya Wanigro wa pwani na Waarabu pamoja na mchanganyiko wa damu ya watumwa
kutokana na takriban, makabila yote ya Afrika Mashariki.Pia, ananukuu maandishi ya
kale ya Mombasa yaliyoandikwa kiasi ya miaka mia mbili nyuma anasema kuwa
Waswahili ni jamii ya watu maalumu waliotafauti na Waarabu. Ni watu ambao
walikuwa washupavu katika kulinda usalama na uhuru wao, na mara kwa mara
wakiwagonganisha vichwa maadui zao ili kuutetea uhuru wao; na mas-ala ya
kuchanganya nasaba na Waarabu halikuwa ni jambo walilolitilia maanani. Kutokana na
maana mbalimbali kwa ujumla wake Waswahili ni mchanganyiko wa watu kutoka
makabila tofauti, ambao wametokea katika mwambao wa Afrika ya Mashariki na
wakawa wanatumia lugha ya Kiswahili katika kuwasiliana. Kwa ufahamu huo rangi,
kabila au wanakotokea ni vigezo vya ziada ambavyo kukubalika au kukatalika
kutatemea na muktadha wa maana inayotolewa.
Kwa vigezo vilivyotajwa hapo juu ni wazi kuwa watu wanaoishi katika visiwa vya
Zanzibar ni moja ya jamii ya Waswahili duniani. Hii ni kwa sababu Wazanzibari ni
mchanganyiko wa jamii nyingi zilizotoka sehemu mbalimbali zilizounganishwa pamoja
na utamaduni wenye kutumia lugha ya Kiswahili kama lugha yao kuu. Katika
kuthibitisha kuwa Wazanzibari ni jamii ya Waswahili, Shariff anasema “Katika wakati
huo Waswahili bado walikuwa wametawaliwa na Waarabu ambao hawakuifanya
Zanzibar kuwa ndio mji mkuu wa serikali mpaka ilipofikia mwaka 1832” (uk. 140).
Kwa hivyo, jamii ya Wazanzibari ni moja ya jamii za Waswahili duniani.
47
4.2.1.1 Muktadha wa Kijografia na Kiuchumi
Zanzibar ni visiwa viwili vikubwa vya Unguja na Pemba na vyengine vidogo kadhaa
vinavyovizunguka.Visiwa hivyo viko upande wa Mashariki wa Bara la Afrika.Kwa
upande wa Magharibi, vimepakana na mwambao wa Tanzania Bara, na sehemu
zilizobakia vimezungukwa na bahari ya Hindi. Visiwa vyengine vinavyoungana na
hivyo ni ambavyo ni Tumbatu, Uzi, Pungume, Vundwe, Bawe, Changuu na Misali kwa
upande wa Unguja. Kwa upande wa Pemba ni Kojani, Kisiwapanza, Maziwang‟ombe na
Fundo ambavyo baadhi yake sehemu ya jamii ya wazanzibariinaishi. Mji mkuu wa
visiwa hivyo ni Zanzibar uliopo eneo la Magharibi mwa kisiwa cha Unguja.
Kwa mujibu wa takwimu za Bodi ya Sensa ya watu na makaazi ya Zanzibar (2011),
wakaazi wa Zanzibar kwa sasa ni zaidi milioni moja na laki mbili. Wakaazi wengi wa
Unguja wanaishi sehemu za Kasikazini, Magharibi na Kati zenye ardhi nzuri ya kilimo.
Kwa upande wa Pemba, wakaazi wake wamesambaa takriban sehemu zote za kisiwa,
kwa vile eneo lote, isipokuwa sehemu chache ni lenye ardhi nzuri kwa kilimo. Shughuli
kuu za kiuchumi ni kilimo, biashara na uvuvi. Kwa upande wa kilimo, hulima karafuu,
mwani na viungo kama mazao ya biashara. Vile vile hulima mpunga, nafaka, muhogo,
migomba na vilimo vya maweni, kwa mazao ya chakula. Biashara za ndani na nje
zimeifanya Zanzibar kwa miaka kadhaa itambulikane kama ni kituo cha kibiashara tokea
zama za wakoloni.
48
4.2.1.2 Muktadha wa Kiutamaduni
Kwa mujibu wa Othman na Yahya (2004), Utamaduni ni jumla kuu inayokusanya
mambo yote ya asili yanayotendeka katika jamii hiyo. Mambo hayo ni kama vile lugha,
mila, itikadi, desturi, shughuli za kijamii kama harusi na misiba, ngoma, dini, malezi,
mavazi na hata tabia. Aidha, mazingira na historia nazo huchangia kwa kiasi kikubwa
mwelekeo wa utamaduni wa jamii husika uonekane kama hivyo ulivyo. Kwa kuwa kila
jamii duniani inao utamaduni wake, hivyo ndivyo ilivyo kwa jamii ya Wazanzibari yaani
wanao utamaduni wao. Wenyeji wa Zanzibar ni wahamiaji wa kale waliohama makwao
kwa sababu za kiuchumi na kuhamia Zanzibar. Baadhi ya wahamiaji hao walitoka nchi
za jirani na wengine nchi za mbali. Baadhi ya miji hiyo ni Somalia, Lamu, Mombasa,
Mzizima (Dar es salam), Yemen, Ngazija, Oman na Barahindi. Mchanganyiko wa jamii
zote hizi, dini na lugha inayowaunganisha wote ndizo zilizochangia kuujenga utamaduni
binafsi wa Mzanzibari na kuupa sura uliyonayo hivi sasa.
Kwa mujibu wa Al-Ismaily (1999), kiutamaduni, Zanzibar imeathiriwa zaidi na
utamaduni wa Kiislamu kwa vile wakaazi wake zaidi ya asilimia tisini na tano ni
wafuasi wa dini ya Uislamu. Hali hiyo, inaufanya utamaduni wao wa mavazi, shughuli
za kijamii kama arusi na mazishi, vyakula na mapisi, na maingiliano baina yao, ufanyike
kwa taratibu za kiislamu kwa kiasi kikubwa. Aidha, kitabia wanasifika sana na sifa za
upole, ukarimu, utulivu, upendo, ujamaa wa damu, na kushikamana na mafundisho ya
dini zao kwa kiasi kikubwa. Lugha kuu na rasmi ya wakaazi wa Zanzibar ni Kiswahili.
Kwa mujibu wa Khatib (1983), Zanzibar kuna lahaja kuu nne za Kiswahili ambazo ni
Kimakunduchi (Kikae) inayozungumzwa Kusini mwa kisiwa cha Unguja, Kitumbatu
49
inayozungumzwa kisiwani Tumbatu na maeneo ya Kaskazini ya Unguja, Kipemba
inayozungumzwa kisiwani Pemba, na Kiunguja inayozungumzwa Unguja Mjini na
maeneo ya Magharibi na ya Kati ya kisiwa cha Unguja. Kiunguja Mjini ndiyo lahaja
iliyosanifiwa na kurasimishwa kuwa ndio matamshi ya lugha kuu ya Kiswahili. Pamoja
na kuwa lugha kuu ya jamii ya Wazanzibari ni Kiswahili, jamii hiyo ina mchanganyiko
mkubwa wa watu wa makabila na mataifa mbalimbali duniani. Akiulezea utamaduni wa
Waswahili wa Zanzibar Sengo (1992) anasema:
Kazi kubwa ya kitaalamu juu ya utamaduni wa Kiswahili, ambayo
tunaijua hadi sasa ni tasnifu ya udaktari wa falsafa iliyoandikwa na
mwalimu Sengo kuhusu Sanaajadiiya ya Visiwani. Mwandishi
wake alivitalii visiwa vya Pemba na Zanzibar kwa utafiti wa kina na
kuibuka na hoja za kuueleza utamaduni wa Waswahili wa Visiwani
kwa kuheshimu utata uliosababishwa na Bahari ya Hindi.
Waswahili wenyewe wana michanganyiko, tangu ya maumbile,
damu, historia, asili, sababu, matukio, itikadi, imani n.k. Bahari ya
Hindi, historia ndefu ya Uislamu na lugha ya Kiswahili, ni baadhi
ya sababu kuu za kuwafanya Waswahili kujihisi wamoja kilugha,
kiutamaduni na kihisia. Uafrika asilia umepewa nafasi ya mwanzo
katika haki na hadhi ya Waswahili. Suala la ugozi lisitazamwe
kisiasa tu kwani kimaumbile watu tumepakwa rangi mbalimbali ili
tutambuane na tuelewane kirahisi katika kuendesha mambo yetu ya
kila siku maishani (uk. 12).
Kutokana na maelezo hayo ya Sengo, niwazi kuwa jamii ya Wazanzibari ni yenye
michanganyiko kadhaa ikiwemo ya itikadi, imani, damu na makabila. Aidha, kutokana
na lugha ya Kiswahili, watu hawa wameunganishwa na kujihisi ni wamoja katika
utamaduni wao uliochukuwa takriban kutoka katika kila kabila hasa Uafrika, Uarabu,
Uhindi na Ushirazi. Kwa hivyo, Wazanzibari ni jamii ya Waswahili yenye utamaduni
wake halisi unaozitofaisha na tamaduni za jamii nyengine za Waswahili.
50
4.2.1.3 Muktadha wa Kifasihi
Jamii ya Waswahili ya Zanzibar ina uhusiano mkubwa na fasihi ya Kiswahili iwe
andishi au simulizi. Kwa upande wa fasihi andishi kumetokea waandishi na wataalamu
wengi wa fasihi andishi ya Kiswahili ambao wameandika, kuhakiki, na kufanya tafiti
nyingi za Kiswahili. Mfano wa wanafasihi hao niSaid Ahmed Muhammed aliyeandika
Asali Chungu (1977), Kivuli Kinaishi (1990), na Sikate Tamaa (1980). Mwandishi
mwengine ni Shafi Adam Shafi aliyeandika Kasri ya Mwinyi Fuadi (1978), Kuli (1979)
na Vuta N’kuvute (1999). Muhammed Said Abdulla kwa upande wake ameandika
Mzimu wa Watu wa Kale (1960), Duniani kuna Watu (1976) naBwana Msa (1984).
Mohamed Suleiman Mohamed ameandika Kiu (1972), Nyota ya Rehema (19) na
Muhammed Seif Khatibu ameandika Fungate ya Uhuru (1988) naWasakatonge
(2003).Kazi zote hizo na nyengine nyingi, zinasifika sana kwa ufasaha wake wa lugha,
kiasi cha kuzifanya kuwa ni burudani na kigezo tosha cha maadili na utamaduni wa
jamii ya Waswahili wa Zanzibar pia kuziwezesha kutumika katika kufundishia fasihi
Mashuleni na Vyuoni.
Sambamba na fasihi andishi, fasihi simulizi nayo imetamalaki vyema katika fani zake
zote za hadithi, ushairi, maigizo, nyimbo pamoja na semi zikiwemo methali ndani yake.
Mara nyingi jamii imeshuhudiwa ikikaa katika mitaa na vijiji kwa nyakati tofauti na
hasa jioni, watoto na watu wazima wakisimuliana hadithi, vitendawili na kucheza
michezo mbali mbali. Nyimbo zinazoendana na aina ya ngoma zao kama taarabu asilia
na za kisasa, ngoma za kiutamaduni kama msewe na maumbwa nazo ni nyingi sana.
Kwa ujumla fani hii ya fasihi simulizi ndio mlezi wa wanajamii wote waswahili. Hii
imewafanya Waandishi nao waitumie kiasi kikubwa fasihi simulizi zikiwemo methali na
51
semi mbalimbali katika kazi zao. Hali hii, inathibitisha wingi wa kazi za fasihi simulizi
zinazotumiwa na jamii ya waswahili inayoishi Zanzibar. Akithibitisha wingi wa simulizi
hizo katika shairi lake la "Utamaduni Udumu," Maalim Haji Chum kama
alivyonukuliwa na Sengo (1992) anasema:
Kuna nyingi simulizi, ambazo zatia hamu
Za kale na siku hizi, kuzitunza ni muhimu
Tusiige upuuzi, ja kuabudu mizimu
Utamaduni udumu, vizazi hadi vizazi.
Methali na misemo mingine imo katika data ya mswada wa Maalim
Haji Chum. Misemo hii ni katika jumla ya mafumbo na vijembe
vya Kiswahili. Mifano: kuku mna wana halembewa bwe (kuku
mwenye watoto halengwi jiwe), kulya nguru si kazi, kazi kumosa
(kula nguru si kazi, kazi ni kumuosha) mdota asali hadoto umoja
(muonja asali haonji mara moja), si kiya mna kuche simba (si kila
mwenye makucha ni simba). Katika mafumbo yao, huwa wanasema
makubwa na mazito sana (uk.8).
Dondoo hili linathitisha kuwa simulizi hizo sio tu ni nyingi, bali pia ni zenye mafumbo
mazito na ambayo ndio hasa chem chem ya jamii za Waswahili ikiwemo ya Wazanzibari
kupenda kuzitumia simulizi zao hizo.
Kutokana na maelezo hayo kuhusu jamii ya Wazanzibari na utamaduni wake, utafiti
umebaini kuwa jamii ina uhusiano mkubwa na lugha ya Kiswahili. Hii ni kwa sababu
pamoja na kuwa Wazanzibari wana asili mbalimbali kama vile Makabila ya lugha za
Kibantu, Kiarabu, Kihindi na Kingazija, lakini wote hao hawatumii lugha hizo bali wote
hutumia lugha ya Kiswahili katika mawasiliano hata kama lafudhi zao zinawatofautisha.
Vilevile, utafiti umebaini kuwa jamii hii kama zilivyo jamii nyengine za Waswahili ina
matumizi makubwa ya methali za Kiswahili. Hili limethibitishwa katika uchunguzi
uliofanywa katika shughuli za kijamii katika sherehe na misiba pamoja baraza za
mazungumzo zilizohudhuriwa na mtafiti kwa vile, sehemu zote hizo methali zilikuwa
52
zikitumiwa. Kwa mfano, katika baraza moja ya mtaa3methali zifuatazo zilitumiwa:
“Mafahali wawili hawakai zizi moja”, “Hayawi hayawi, huwa”, na “La kuvunda halina
ubani”. Methali hizi zilikuwa zinasemwa na watazamaji wakati bao na karata
zinachezwa katika baraza hiyo. Hali hiyo ilibainika pia katika harusi na misiba. Kwa
hivyo, hali hiyo inabainisha kuwa Wazanzibari kutumia methali katika miktadha
mbalimbali ya maisha yao ni sehemu ya utamaduni wao.
C1: Methali hutumika hata katika mazungumzo ya kawaida katika Baraza za
mazunguzo. Mtafiti (aliyevaa shati ya njano anayeonekana uso) akiwa katika moja ya
Baraza hizo katika mtaa wa Sogea akifuatilia matumizi ya methali katika mazugumzo.
4.2.2 Methali za Kiswahili Zilizoachwa
Methali za Kiswahili zilizoachwa ni istilahi iliotumika katika utafiti huu, kuziwakilisha
methali maalumu. Methali hizo ni zile zilizokosa nafasi ya matumizi katika harakati za
kijamii kuanzia kipindi cha miaka ya tisiini hadi hivi sasa. Methali hizo, zilikuwa
mashuhuri sana na zikitumiwa katika jamii za Wazanzibari, lakini kwa sababu
zimeachwa kutumiwakwa sababu zisizofahamika, hivi sasa zimeshasahaulika na sehemu
3 Uchunguzi huo ulifanywa mtaa wa Sogea kwa Ayuba siku ya Jumatano tarehe 8/4/2015 saa 10:00 za
alasiri.
53
kubwa ya jamii ya wazee hawazikumbuki tena. Sio hivyo tu, bali utafiti umegundua
kuwa jamii ya vijana wao hawazifahamu kabisa. Methali hizo kwa sasa zimebakia katika
kumbukumbu za wazee wachache na katika baadhi ya vitabu vichache vilivyoandikwa
zamani. Methalihizo ambazo sasa jamii ya Wazanzibari haizitumii tena, ndio methali
zilizoachwa kwa mujibu wa utafiti huu.
Kuwepo kwa methali zilizoachwa kumethibitishwa kwa njia za udurusu wa maktaba,
mahojiano na dodoso. Kwa mfano, Farsi4 (1979) anaeleza wazi kuwa kutokana na
kuingizwa kwa elimu ya kisasa, na kizazi cha wazee kutoweka ambao ndio walionayo
fasihi simulizi, imani za nchini, vitendawili, methali na hadithi vinasahauliwa. Maelezo
yake yanathibitisha kuachwa methali pia yanaonesha kuwa tatizo hili limeanza zamani
kwa vile kipindi alicholizungumzia suala hili ni tokea miaka ya hamsini.Ingawa kwa
mujibu wa maelezo hayo suala la kuachwa kwa baadhi ya methalilimeanza zamani,
utafiti unaonesha kuwa bado linaendelea hadi sasa na katika miaka hii linaendelea kwa
kasi.Akiielezea kazi ya mwandishi Said iliyokusanya methali zaidi ya mia mbili za
Kiswahili, Hassan(2013) anasema kuwa mwandishi huyo kwa upande mwengine
anaikumbusha jamii baadhi ya methali ambazo zinaanza kutoweka ili (jamii hiyo) iweze
kuzikumbuka na hata kuzihifadhi kwa ajili ya kizazi cha sasa na cha baadaye.Aidha,
kupitia mahojianona wazee pamoja na watu wa makamo, nao wamekubaliana na ukweli
huo. Kwa mfano, wakati wa mahojiano na Bibi Asiya Miraji Khamis5 wa Kikwajuni
juualikirikuwa ni kweli siku hizi ziko methali zilizoachwa kutumiwa na kuongeza kuwa
4 Said Saleh Farsi ni mwandishi wa miaka ya khamsini aliyekusanya kazi mbali mbali za fasihi ya
Kiswahili Zanzibar. Miongoni mwa kazi zake ni Swahili Sayings 1 ya methali na Swahili Sayings2 ya
Vitendawili na kauli mbalimbali za kiitikadi walizonazo jamii ya waswahili Zanzibar. 5 Mahojiano hayo yalifanyika Ijumaa tarehe 03/02/2015 baina ya mtafiti na Bi Asiya. Bi Asiya ni
miongoni mwa wazee mashuhuri wenye ufahamu na ujuzi wa matemizi methali katika mazungumzo.
54
si methali tu, bali hadithi, vitenawili na hata maneno mengine ya zamani. Akitolea
mfano wa neno la kumkaribisha mgeni „starehe‟, ambalo kwa anahisi sasa halitumiki
kwani hajawahi kulisikia na lilikuwa ni neno la kawaida. Pia, maelezo yaSaid Ahmed6
kuwa baadhi ya kazi huwa zina muda maalumu, na unapopita zinaweza kuachwa, hivyo,
na kazi za fasihi simulizi zinaweza kuachwa na kutoweka kabisa kwa vile hazikuwa na
kumbukumbu ya kimaandishi. Kwa hivyo, kuachwa kwa baadhi ya methali za Kiswahili
katika jamii ya Wazanzibari nijambo lisiloshaka na hivyo kutoa mwanya kwa utafiti huu
kuzibainisha, ambapo matokeo halisi ya hatua zilizochukuliwa katika kuzibainisha
methali hizo ni haya yafuatayo:
Hatua ya kuipitiya orodha ya methali mia tano na ishirini na sita zilizokusanywa, utafiti
ulibaini methali mia tatu na hamsini ni zenye kujulikana kwa vile mtafiti alizikumbuka.
Kujulikana kwa methali hizo na mtafiti, kunathibitisha kuwa hizo ni methali
zinazoendelea kutumika hadi sasa katika jamii ya Wazanzibari. Methalimia moja na
sabini na sita zilizobakia ambazo mtafiti hakuzikumbuka,zilitengwa kwa hatua
inayofuata ambayo ni hatua ya kuzisikiliza kupitia vikundi vitano vya
majadilianovilivyotakiwa kutaja methali wanazozifahamu. Katika hatua hii,methali mia
tatu na kumi na saba zilikumbukwa na mia mbili na tisa hazikutajwa miongoni mwa
methali mia tano na ishirini na sita zilizokusanywa. Methali ambazo hazikutajwa
zilipambanuliwakati ya zilizosahauliwa na zilizoachwa.Kwa hatua hiyo, methali mia
moja na tano kati ya mia mbili na tisazilibainika kusahauliwa na mia moja na kumi tisa
zilizobakia ndizo zilizoachwa. Aidha, katika zoezi la kuzihakiki methalizilizoachwa,
6 Profesa Ahmed said Mohamed ni mtaalamu wa lugha ya Kiswahili na Mwandishi mashuhuri wa kazi za
fasihi andishi ya Kiswahili kutoka Zanzibar. Ameandika kazi nyingi za riwaya, tamthilia na ushairi.
Mahojiano kati yake na Mtafiti yalifanyika Jumatatu 9 /3/2015 katika ukumbi wa TAKILUKI.
55
matokeo yamebainisha kuwa methali thalathini na moja zinajulikana kwa vile
zilikumbukwa, na zilizobakia thamanini na nne, ndizo zilizothibiti kuwa ni miongoni
mwa methali nyingi za Kiswahili ambazo sasa jamii ya Wazanzibari haizitumii tena.
Kwa ujumla, utafiti umebaini kuwa,katika matumizi ya kawaidakwa jamii ya
Wazanzibari, methali hujigawa makundi manne. Kundi la kwanza ni la methali
maarufu sana. Hizi ni methali zinazotumiwa mara kwa mara. Utafiti ulibaini kuwa
watu wa rika zote wanazifahamu na kuzitumia takriban kila siku katika harakati za
maisha yao. Methali hizi zimebainika kuingia katika kundi hili kwa kule kupatikana
katika dodoso, vitabu na katika vikundi vyote vitano vya mijadala. Katika utafiti huu
methali mia mbili na kumi na nne ziliingia katika kundi hili. Kundi la pili, ni la
methali zinazofahamika kwa wastani. Hizi, ni zile ambazo zinatumiwa kwa wastani
katika jamii ya Wazanzibari. Katika mijadala ya vikundi, zilitajwa mara tatu au
mbilina hazikutajwa sana katika dodoso na pia hazikupatikana kwa wingi katika
vitabu vilivyotungwa miaka ya tisini hadi sasa. Methali mia moja na hamsini na tano
ziliingia kundi hili kati ya mia tano na ishirini na sita. Kundi la tatu ni la methali za
nadra. Methali hizi ni zile zinazotumiwa kwa uchache ambazo na zaidi hutumiwa na
wazee. Methali hizi hazikujulikana na vijana wengi pia zilipatikana kwa uchache
katika dodoso na zilitajwa katika kikundi kimoja tu kati ya vikundi
vitano.Methalisabini na tatu kati ya mia tano na ishirini na sita ziliingia kundi hili.
Na kundi la nne ni la methali zilizoachwa. Methali hizi,hazikupatikana katika dodoso
wala hazikutajwa katika vikundi vyote. Wanafunzi nao walipotajiwa sehemu ya
mwanzo hawakuweza kuzikamilisha. Hii nikuonesha kuwa methali hizi rika za
vijana na wanafunzi hawazifahamu kabisa. Methali hizi zilizopatikana katika vitabu
56
vya miaka ya hamsini na sitini, na kwa baadhi ya wazee katika mahojino. Methali
hizi hasa ndizo zilizokusudiwa kubainishwa katika utafiti huu ambapo ulibaini
methali thamanini na nne kati ya mia tano na ishirini na sita zilizochunguzwa
zimeachwa.
Methali za Kiswahili zilizothibiti kuwa zimeachwa katika jamii ya Waswahili ya
Zanzibar kwa mujibu wa utafiti huu ni hizi zifuatazo:
Jeduwali la methali zilizoachwa katika jamii ya Waswahili Zanzibar
Na. Methali
iliyoachwa
Etimolojia yake Maelezo ya jumla
kuhusu maana na
matumizi yake
1. Angakaanga,
tu chini ya
gae.
Asili ya methali hii ni
sehemu zenye
wafinyanzi.
Maana yake hata kama
atakaanga, sisi tupo
chini ya gae la
kukaangia (muhindi,
mtama).
Methali hii hutumika
wakati siri inapofichuka.
Maana yake ni kuwa
Hapana siri inayoweza
kufichika kwa watu hao
hata wasiijue.
2. Atangaye
sana na jua
hujua.
Asili yake katika taasisi
za elimu.
Anayehangaika na juwa
likampata katika
kujifunza jambo huweza
kilijua.
Hutumika katika
kushajihisha watu
wasivunjike moyo katika
kutafuta elimu.
Maana yake mtu
anayejishughulisha kwa
bidii kubwa hufanikiwa.
3. Atangazaye
mirimo si
mwana wa
ruwari.
Asili yake katika
shughuli za kiutawala.
Kuamrisha si lazima
kwa mwenye mamlaka
tu.
Ruwari(Liwali kiongozi)
Inatumika kuhimiza
utiifu kwa yoyote
anayetoa amri au
ushauri.
Maana yake ni kuwa
unapopewa amri
57
Mirimo (kazi,mashauri) usiidharau kwa
kuangalia aliyeitoa.
4. Avuliwaye
nguo
huchutama.
Asili yake kwa watu
wanaojiheshimu.
Mtu aliyevuliwa nguo
lazima achutame ili
ajisitiri.
Mtu anayefanya jambo
la aibu hana budi kuona
haya.
5. Boi manda
malipo yake
parapanda.
Asili yake enzi za
utumwa.
Boi manda (Mtumishi
wa hadhi ya chini)
Parapanda (zogo, kelele)
Hutimika wanapo
kuwepo watumishi
wanaonyanyaswa.
Watumishi wa hali za
chini hawathaminiwi.
6. Chombo cha
kuzama
hakina
usukani.
Asili yake sehemu
zenyepwani.
Maana yake chombo
kinachozama kwa
kuvuja maji hakiwezi
kuokolewa.
Hutumika wakati jambo
limeshaharibika sana.
Iwapo jambo limekiuka
mipaka na linazidi
kuzorota, si rahisi
kulirekebisha na hivyo
hapana haja ya
kuendelea kupoteza
muda kulishughulikia.
7. Dunia duara,
ukiichezea
utachera.
Asili yake sehemu za
malezi ya maadili.
Utachera (utasumbuka)
Mtu akijishughulisha
sana na mambo ya dunia
atahangaika na kupata
tabu bila ya mafaniko.
8. Endapo juu
kipungu
hafikii
mbinguni.
Asili yake ni sehemu
zenye viongozi
wanaojiona sana.
Kipungu (aina ya ndege
anyeruka juu sana)
Kadri anavyoruka juu
sana, hawezi kuzifikia
mbingu.
Hutumika anapotokea
mtu anayejiona kwa
cheo au mali.
Kujivuna si jambo jema
kawni mwisho wake ni
mtu kuharibikiwa.
9. Fungato
haliumizi
kuni.
Asili yake ni vijijini.
Mzigo uliofungwa
vyema haumuumizi
mbebaji.
Hutumiwa kwa
kuhimiza kusaidiana.
Jambo likiharibika kwa
mmoja tushirikiane
kulitengeneza.
10. Hakuna
nafsi tupu.
Asili yake sehemu za
malezi ya maadili.
Hutumika
kutahadharisha watu.
58
Hakuna mtu asiye na
mawazo katika akili
yaake.
Kila mtu ana mawazo
katika nafsi na hivyo
kumsikiliza ni muhimu,
huenda yakafaa.
11. Hasara
humfika
mwenye
mabezo.
Asili yake sehemu za
malezi ya maadili.
Mabezo (dharau, jeuri).
Anayepuuza ushauri
huishia kuhasirika.
Hutumika kuonyea tabia
mbaya ya dharau.
Inatuonya kutodharau
tunayoambiwa ili tuje
tukajuta.
12. Jina jema
hung‟ara
gizani.
Asili yake sehemu za
malezi ya maadili.
Jina la mtu mwema
husifiwa kila wakati.
Hutumiwa kuhimizia
kuwa wema katika jamii.
Inatuhimiza tuwe na
tabia njema ili tupate
utajo mwema.
13. Jogoo hulia
“uta wangu
ukule”.
Asili yake sehemu zenye
mifugo hasa ya kuku.
Uta wangu ukule (silaha
yangu iko mbali nami.
Hutumika kuwashutumu
wanaotoa visababu vya
uongo wanapokosa
kuwajibika.
Inatuasa tusiwe na tabia
ya kutowajibika kwa
kutegemea kutoa
dharura za uongo.
14. Joka la
mdimu
linalinda
watundao.
Asili yake sehemu za
kilimo cha matunda ya
viungo (ndimu, limao)
Nyoka aishiye mdimni
huwazuia wanaotaka
kuchuma ndimu.
Hutumika atokeapo mtu
anaewazuia wengine
jambo japo yeye hana
haja nalo.
Inatuasa tusiwe na tabia
ya uchoyo wa namna
hiyo.
15. Jungu bovu,
limekuwa
magae.
Asili yake sehemu zenye
wafinyanzi.
Jungu lililovunjika
huweza kuvunjika zaidi
hadi kubakia magae tu.
Hutumika atokeapo mtu
muovu akizidisha uovu
wake katika jamii.
Inatahadharisha kuwa
mtu akiwa muovu
huweza kuzidisha uovu
wake hasa asipokanywa.
16. Kanga hazai
ugenini.
Asili yake sehemu zenye
misitu yenye mawe.
Kanga (aina ya ndege
wa msituni kama kuku)
Hutumika kumtetea mtu
mgeni anaposhindwa
kufanya baadhi ya
mambo ugenini.
59
Kanga akihamishwa
kupelekwa ugenini
hushindwa kutaga
mayai.
Ugeni una shida zake,
hivyo ni vyema
kuwastahamilia wageni
wanaposhindwa kufanya
baadhi ya mambo.
17. Kikuu
pachika
kitakufaa
masika.
Asili yake sehemu zenye
vibanda vya mapaa ya
makuti, nyasi.
Kikuukuu usicho na haja
nacho kihifadhi,
kitakufaa kipindi cha
mvua za masika
Hutumika kushajihisha
uwekaji wa akiba.
Usidharau kilichotumika
usichokuwa na haja
nacho kwa muda huo. Ni
muhimu kukitunza
huenda kitakufaa
baadaye.
18. Kisokula
mlimwengu,
sera nale.
Asili yake sehemu za
malezi ya maadili.
Asichoweza kukila
binadamu hicho ni cha
shetani (ibilisi)
Hutumika kuwaasa watu
kuachana na mabaya.
Inatushauri kuachana na
mabaya kwani hayana
faida kwa wanadamu.
19. Kiwi cha
Yule, ni
chema cha
huyu; hata
ulimwengu
uwishe.
Asili yake sehemu za
malezi ya maadili.
Kibaya cha mtu hakiwi
chema kwa mwengine
daima.
Kitu kikiwa kibaya kwa
mmoja na muhali kuwa
chema kwa mwengine.
Inatuasa kutoshughulika
na vitu viso faida kwetu.
20. Koko haidari
mai.
Asili yake sehemu za
pwani.
Mbegu za mkoko
hazigusi maji ingawa
mkoko wenyewe umo
majini.
Hutumika kuonesha hali
ya kinyume na kawaida.
Mtu huweza kuishi
kwenye mazingira
mazuri au mabaya lakini
asiweze kuathiriwa
nayo.
Inatushajiisha kuwa
makini.
21. Kucha
Mungu si
kilemba
cheupe.
Asili yake katika
sehemu za ibada.
Kumwogopa Mungu ni
katika moyo na si kwa
kuvaa kilemba safi
kichwani.
Hutumika katika
kuwaaidhi watu kuwa
nan yoyo safi.
Inatufunza kuwa tabia
ya mtu kiimani na
vitendo vyake ndio
kipimo cha utu wake na
60
wala sio mavazi au
maneno yake matupu.
22. Kufa kwa
mdomo,
mate
hutawanyika
Asili yake sehemu za
malezi ya maadili.
Mtu anapokufa mate
hupotea kinywani
mwake.
Hutumika wakati
mambo Fulani
yanapoharibika kwa
kuondoka msimamizi.
Inatufunza kuwa makini
kukabili mambo ili
yasiharike kwa
kuondoka Yule
anayeyasimamia.
23. Kula
kutamu,
kulima
mavune.
Asili yake sehemu za
kilimo.
Mavune (Uchovu, tabu).
Kula chakula ni raha
lakini kukilima
shambani ni tabu sana.
Hutumika kushajihisha
watu kufanya juhudi au
kuwasuta wanaopenda
kula bure bila kufanya
kazi.
Si vema kutegea
kufanya kazi na kusubiri
kutumia bure.
24. Kutu kuu ni
la mgeni.
Asili yake sehemu za
malezi ya maadili.
Kutu kuu (makaribisho
mazuri).
Makaribisho mazuri na
ukarimu hufanyiwa
mgeni.
Hutumika kufunzia
ukarimu na ihsani kwa
wageni.
Inatuhimiza kuwafanyia
wema wageni ili
waweze kuwa na furaha
ijpokuwa wapo ugenini.
25. Kutwanga
nisile unga,
nazuia mchi
wangu
Asili yake ni katika
sehemu za vilimo vya
nafaka (mtama,
mpunga).
Ikiwa nitatwanga halafu
nikose japo sehemu ya
nnachotwanga, ntazuia
mchi wangu nisitwange.
Hutumika kuhimiza
malipo ya jasho la mtu
baada ya kufanya kazi.
Mtu anapokosa manufaa
ya mchango wake katika
jambo, huweza kuacha
kuchangia na huenda
likakosa kufanikiwa.
26. Lipitalo,
hupishwa.
Asili yake sehemu za
malezi ya maadili.
Jambo la mpito
huachiwa lipite.
Hutumika kuwaasa
wanaong‟ang‟ania
jambo la mpito
wasiloweza kulipata.
Inatuasa kutoshindana
na mambo ya kuzuka
tusiyoweza kuyapata.
61
27. Maafuu
hapatilizwi.
Asili yake sehemu za
malezi ya maadili.
Maafuu (mpungufu wa
akili).
Mtu mwenye akili
pungufu hapaswi
kuadhibiwa kwa
kukosea jambo.
Hutumika kuwaasa
wanaowatesa watu kwa
jambo wasiolielewa.
Inatuonya kutochukua
hatua kali kwa wale
wanaoshindwa kufanya
jambo kwa kutokuelewa.
28. Majumba
makubwa
husitiri
mambo
makubwa.
Asili yake katika
shughuli za kiutawala.
Mamlaka makubwa
huweza kufanya mambo
makubwa (mazuri au
mabaya) bila ya
kujulikana na wengi.
Hutumiwa
linapojitokeza jambo
kubwa lakushangaza
katika familia za
watukufu.
Inatutanabahisha kuwa
katika tawala au
majumba ya wakubwa
hufanyika mengi ila
huwa hayatangazwi.
29. Maneno
makali
hayavunji
mfupa.
Asili yake sehemu za
biashara ya nyama.
Maneno makali ya fitina
hayamuathiri mwenye
uwezo zaidi na makini.
Hutumika kuwashauri
watu wasishituliwe na
tetesi za watu fitina.
Maneno ya fitina na
uongo hayamuathiri mtu
makni asiyebabaika.
30. Mavi
usoyala,
wayawingia
ni kuku?
Asili yake sehemu zenye
mifugo hasa ya kuku.
Winga (fukuza)
Mtu hawezi kutumia
mavi yake kwa nini
awainge kuku
wanapoyala?
Hutumika kukanyia
tabia ya ubakhili.
Inatufunza tusiwe na
tabia ya ubakhili wa
kuwanyima wengine
hata vile tusivyovihitaji.
31. Mbinu
hufuata
mwendo.
Asili yake sehemu za
malezi ya maadili.
Mbinu za mikono
hufuata jinsi mtu
anavyokwenda.
Hutumika kuhimiza
kuwafuata wakubwa
wetu (wazazi, viongozi)
Inatufunza kuwa ni
vyema kwenda
sambamba na
wakumbwa wetu na si
vema kupingana nao.
32. Mchakacho
ujao,
haulengwi
na jiwe.
Asili yake sehemu za
ardhi za maweni,
mashamba.
Mchakacho (sauti za
majani
yanayokanyagwa)
Sauti za hatua ya kitu
Hutumika
kutahadharisha pupa ya
kufanya mambo.
Haifai kufanya jambo
kwa pupa kabla ya
kulijua lilivyo.
62
kinachokuja bila
kukijuahakirembewi
jiwe.
33. Mfa maji
hukamata
maji.
Asili yake sehemu zenye
maji (mito, maziwa,
bahari).
Anayekufa kwa maji
hachagui cha kukamata
kujiokolea.
Hutumika kuwanasihi
wenye shida kueleza
shida zao.
Mwenye tabu au shida
hutafuta kila aina ya
msaada ili kuitatua shida
yake.
34. Mgeni
hachomi
chaza mtaani
akanuka.
Asili yake sehemu zenye
bahari.
Mgeni achomapo chaza
ugenini hafikilii kunuka.
Hutumika mgeni
akiteleza kufanya jambo
baya.
Inatuhimiza kusamehe
wageni wanapokosea
kwani huwa hukosea
kwa bahati mbaya tu.
35. Mkata hana
kinyongo.
Asili yake sehemu za
kufunza maadili.
Mkata (Masikini)
Masikini siku zote huwa
haoneshi kuudhika
kwake.
Hutumika kumliwaza
mnyonge
anapokasirishwa.
Inatufunza kuwa
masikini ni mtu
anayebeba mengi ya
tabu na kuyastahamilia.
36. Mkata
hapendi
mwana
Asili yake sehemu
zenyejamii za masikini.
Masikini huwa hapendi
kuwa na mtoto kwa
kuchelea gharama.
Hutumika kuonesha
woga wa watu duni wa
kubeba gharama
wasizozimudu.
Inatuasa kutowatwisha
mizigo wasioimudu.
37. Mkataa
chinjo
hupata
mtanda
Asili yake sehemu za
mauzo ya vitoweo
(nyama).
Chinjo -nyama nzuri
Anayekataa nyama
iliyonona kwa kuchagua
kwake huishia na
ngumu.
Hutumika
kumtahadharisha mtu
anayechagua sana.
Mtu anayekataa cha
kupewa kwa kudhani
atakachochagua
mwenyewe ndio chema,
huambulia na kibaya
kwa kutoelewa vema.
38. Mkate
mkavu wa
nyumbani ni
bora kuliko
nyama
shuwa ya
Asili yake sehemu za
mifugo mauzo ya
nyama.
Nyama shuwa- nyama
laini, iliyonona.
Ni bora kula mkate usio
Hutumika kuhimiza
kuthamini maisha ya
nyumbani.
Mtu huridhika kuwa
kwao japo kuna dhiki
63
pengine. na kitoweo uliowenu
kula nyama iliyonona
lakini sio yenu.
kuliko kuwa ugenini
ijapo kuna mazuri zaidi.
39. Mkono
mmoja
hauchinji
ng‟ombe.
Asili yake sehemu za
machinjio ya wanyama.
Mkono mmoja peke
yake hauwezi kuchinja
ng‟ombe.
Hutumika kuhimiza
ushirikiano wa watu.
Ufanisi wa mambo
hauwi mzuri bila ya
kuwa na ushirikiano.
40. Mkosa
kitoweo
humangiria.
Asili yake sehemu zenye
jamii za masikini.
Humangiria – hukadiria
kwa umakini.
Aliyekosa kitoweo
hukitumia kwa uangalifu
sana kichache
kilichosalia.
Hutumika katika
kutahadharisha
matumizi ya fujo,
isirafu.
Inatufunza tusiwe na
matumizi mabaya ya
vitu tulivyojaaliwa
kuvipata kwa wasaa au
kwa tabu, tutahasirika.
41. Mla cha
uchungu na
tamu hakosi
Asili yake sehemu zenye
jamii za masikini.
Anayekula vyakula
vibaya, hatakosa
kubahatika kula na
vitamu.
Hutumika kuwaliwaza
waliofikwa na yale ya
kustahamiliwa.
Inatufunza kuwa
wastahamilivu wakati
wa dhiki ili kuipata
faraja ya baadaye.
42. Mla kwa
miwili hana
mwisho
mwema.
Asili yake sehemu za
kufunza maadili.
Anayekula kwa kutumia
mikono yote miwili
mwishowe hufikwa na
mabaya.
Hutumika kuwaasa watu
kuacha tama.
Mwenye tamaa ya
kutaka kufaidi kwa
kutumia hila na uongo
mwishowe hupata
hasara.
43. Mla mbuzi,
hulipa
ng‟ombe.
Asili yake sehemu za
mifugo mauzo ya
nyama.
Anayepewa mbuzi
humlipa kwa kutoa
ng‟ombe. Au
anayekamatwa kwa
kuiba mbuzi atalipishwa
kutoa fidia ya ng‟ombe.
Hutumika kuhamasisha
kushuru fadhila.
Mtu akitendewa wema
mdogo, hukumbuka na
kulipa kwa wema
mkubwa zaidi.Au
hutumika kuhadharisha
ubaya wa wizi.
Anayekamatwa kwa
wizi huishia kulipa fidia
ya kubwa zaidi ya
alichoiba.
64
44. Mlilala
handingwan
dingwa;
mwemacho
haambiwi
tule
Asili yake sehemu za
kufunza maadili.
Handingwandingwa –
hahisi njaa.
Aliyelala haumwi na
njaa, aliye macho
hasubiri kuitwa kula.
Hutumika atokeapo
mvivu anayelalamikia
njaa.
Inatufunza kutokuwa
wavivu kwa kudhani
hatutaumwa na njaa.
45. Mnyamaa
kadumbu
Asili yake ni lahaja ya
Kimakunduchi.
Aliyenyamaza ndiye
aliyeshinda.
Hutumika anpotokea
msemaji sana.
Inatufunza kuwa kusema
sana hakuna faida.
46. Mpemba
hakimbii
mvua ndogo
Asili yake na kisiwani
Pemba.
Mpemba hakmbii mvua
ndogo kwa kuzowea
kuona mvua kubwa.
Hutumika anapotishiwa
mwenye hali kubwa.
Mwenye kufikwa na
misukosuko mikubwa
hatishiki kwa midogo.
47. Msafiri
masikini
ajapokuwa
sultani
Asili yake sehemu zenye
utawala wa Kiarabu.
Msafiri ni sawa na
masikini hata kama ni
Mfalme.
Hutumika kuelezea
mwenye hali ya juu
anapokabili hali duni.
Mtu hubidi kuishi
maisha duni hata kama
alikuwa na hadhi kubwa
pale inapobidi.
48. Msasi
haogopi
mwiba
Asili yake ni sehemu
zenye misitu na usasi.
Anayewinda wanyama
msituni haogopi
kuchomwa na miiba.
Hutumika kuliwazia
panapotokea matatizo.
Inatufanza kuwa wajasiri
kukabiliana na matatizo
tukitarajia kupata
mafanikio.
49. Mshale
kwenda
msituni
haukupotea
Asili yake ni sehemu
zenye wawindaji
wanyama.
Mshale ulioelekezwa
msituni huwa
haukupotea bure.
Hutumika kuhimiza
uvumilivu.
Sio kila juhudi
zinazofanywa hutoa
matunda haraka,
huwenda ukachelewa.
50. Mtaka unda
haneni
Asili yake sehemu za
kufunza maadili.
Anayekusudia kutenda
jambo hana haja ya
kusema.
Hutumika kuhimiza
utendaji kuliko kusema.
Inatufunza tuwe
watendaji zaidi na
tusijisifu au kujitangaza.
51. Mteuzi
haishi tama
Asili yake sehemu za
kufunza maadili.
Anayependa kuchagua
huwa na tamaa siku
zote.
Hutumika kuasa kuwa
na tama.
Inatufunza tusipende
kuchagua huenda
tukapoteza fursa
muhimu.
65
52. Mtoto
msikivu hula
cha siri
Asili yake sehemu za
kufunza maadili.
Mtoto anayewasikiliza
wakubwa zake hupata
mpaka vya ndani.
Hutumika kushajihisha
utiifu kwa wakubwa.
Inatufunza kuwa
tunapofuata ushauri wa
wakubwa zetu, hupata
mafanikio tusioyatarajia.
53. Mtoto wa
mhunzi
akikosa
kufua,
huvukuta
Asili yake sehemu
zinazofuliwa vyuma.
Mhunzi – mfua vyuma.
Mtoto wa mfua vyuma
anapokosa kufua vyuma
mikono yake humuuma.
Hutumika kuonesha
athari ya kazi nzito.
Jambo lolote lenye
mazoweya kuliacha
linaleta matatizo.
54. Mtumi wa
kunga
haambiwi
maana.
Asili yake ni sehemu
baraza za wazee.
Kunga – jambo la siri.
Anayetumwa kupeleka
siri sehemu haambiwi
undani wa siri hiyo.
Hutumika kuhimiza
kufanya siri mambo
muhimu.
Inatufunza watu
tunapowatuma mambo
ya siri tusiwaeleze
makusudio ili siri
isifichuke.
55. Mvungu
mkeka.
Asili yake sehemu za
ndani katika nyumba.
Mvungu – chini ya
kitanda.
Sehemu ya chini ya
kitanda huwa kama
mkeka kwa kuhifadhia
vitu vingi vizuri.
Hutumika kuonesha
umuhimu wa kutunza
mambo.
Moyo wa mwanadamu
ni kama mvungu kwa
kuhifadhi siri nyingi.
56. Mvuvi
anajua
pweza alipo
Asili yake ni sehemu
zenye amali ya uvuvi.
Pweza – aina ya samaki.
Mvuvi wa pweza ndiye
anafahamu pweza
anamoishi.
Hutumika kuwaenzi
wenye ujuzi wa jambo.
Ukitaka kuelimika juu
ya jambo fulani
mwendee mwenye ujuzi
nalokwasababundiye
awezaye kutoa ushuri
sahihi juu ya jambo hilo.
57. Mwacha
asili ni
mjasiri.
Asili yake sehemu za
kufunza maadili.
Anayeacha utamaduni
wa kwao huwa ni mtu
mpuuzi.
Hutumika kuuenzi
utamaduni wa jamii.
Kuacha utamaduni wa
asili na kufuata wa
kigeni huwa nikama
utumwa asiye na kwao.
58. Mwamba na
wako
hukutuma
umwambie.
Asili yake ni sehemu za
kufunza maadili.
Anayemsema jamaa
yako mbele yako huwa
Hutumika kuhadharisha
tabia ya kusengenya.
Mwenye kufanya ubaya
bila kificho, huwa
66
anakutuma umwambie. hawachelei wale
wanaomuona.
59. Mwana maji
wa Kwale
kufa maji
mazowea.
Asili yake ni mwambao
wa pwani.
Kwale – mji ulioko
Pemba na Tanga.
Mkaazi wa Kwale kufa
kwa ajali ya maji si
jambo la kustaajabisha.
Hutumika kuasa tabia ya
kujigamba.
Si vema kufanya jambo
kwa kujiona hodari
kwani huweza
kuliharibu na hata
kujipata mwenyewe.
60. Mwana
mkuwa
nawe ni
mwenzio
kama wewe.
Asili yake ni sehemu za
kufunza maadili.
Mtoto anayelelewa nawe
naye ni mwenzio kama
ndugu yako wa
kuzaliwa.
Hutumika kuhimiza
uhusiano mwema.
Kuishi pamoja na mtu
wan je ya familia yako
kwa muda mrefu
kunajenga uhusiano
mwema wa kijamaa
kama ndugu wa
kuzaliwa pamoja.
61. Mwana wa
ndugu
kirugu,
mjukuu ni
mtu mbali
Asili yake ni sehemu za
kufunza maadili.
Kirugu – kipele
kinachouma.
Mtoto wa ndugu yako ni
mtu wako wa karibu
zaidi kwa kuwahudumia
kuliko mjukuu wako.
Hutumika kukumbusha
uhusiano wa jamaa wa
karibu.
Inatufunza kuwa jamaa
wa mtu wa karibu nao ni
muhimu kwa kuwajali
na kuwasaidia kama
mwanao na mjukuu
wako.
62. Mwekaji
kisasi
haambiwi
mwerevu.
Asili yake katika
mapambano.
Anayeweka kisasi cha
kutendewa uovu si
katika watu wenye
busara.
Hutumika kuhimiza
kusameheana na
kustahamiliana.
Inatufunza kuwa haifai
kulipizana kisasi
tunapokoseana na badala
yake tujenge tabia ya
kusameheana.
63. Mwenye
njaa hana
miiko.
Asili yake katika jamii
masikini.
Mtu mwenye njaa kali
huwa hachagui chakula.
Hutumika kuhimiza
kufanya kila aina ya
bidii ili kufanikiwa.
Ni muhimu kutumia
maarifa mbalimbali ili
kutosheleza mahitaji
yanayokabili.
64. Mwibaji na
watwana,
Asili yake ni sehemu
zenye utumwa na
Hutumika kuasa tabia
mbaya.
67
mlifi ni
mwungwana
ubwana.
Watwana – watu
wanaotumiliwa, Kilifi –
mji ulioko Kenya.
Mwizi wenziwe ni watu
wanaotumiliwa lakini
mtu wa Kilifi yeye ni
mtu mwenye heshima.
Muovu siku zote
hujulikana kwa tabia
yake ya kukaa na watu
wenye zinazolingana
naye. Na mwema na
hukaa na watu wema
wenziwe.
65. Mwili wa
mwenzio ni
kando ya
mwilio.
Asili yake ni sehemu za
kufunza maadili.
Mwenzako ni mtu wa
mbali na nafsi zenu ni
tofauti.
Hisia katika kupokea
mambo zinatofautiana.
Hutumika kuonesha
utofauti wa hisia za
watu.
Yanayompata mtu
mmoja (mema au
mabaya) athari yake ni
tofauti na kama
yangempata mtu
mwengine.
66. Mzika
pembe ndiye
mzua
pembe.
Asili yake sehemu zenye
imani za kishirikina
(kwenye waganga).
Anayeizika pembe ndiye
aijuaye ilipo na ndiye
awezaye kuizikua.
Hutumika kuonesha
umuhimu wa kumpata
muhusika katika kutatua
tatizo.
Mtatuzi bora tatizo ni
yule aliyesababisha
tatizo kwa vile
analifahamu vizuri.
67. Mzowea
kutwaa,
kutoa ni vita.
Asili yake ni sehemu za
kufunza maadili.
Aliyezowea kupewa kila
mara huona vigumu
kutoa yeye.
Hutumika aokeapo mtu
bahili na mwenye tamaa.
Inatufunza tusiwe na
tabia mbaya za uchoyo
na ubahili.
68. Mzungu wa
kula
hafundishwi
mwana.
Asili yake ni katika
kipindi cha ukoloni.
Mtoto hafundishwi
namna ya kula kwa vile
huweza kugundua
mwenyewe.
Hutumika kuonesha mtu
anavyoweza kujikimu.
Mtu hahitaji
kufundishwa jinsi ya
kujitosheleza haja zake
za msingi bali hubuni
njia mwenyewe hizo.
69. Ndege
mwigo hana
mazowea.
Asili yake sehemu za
ufugaji hasa ndege.
Ndege anayefanya
mambo kwa kuiga
wenziwe huwa hapati
kujifunza mwenyewe.
Hutumika atokeapo mtu
anayefanya mambo kwa
kufuata mkumbo.
Anayefanya jambo kwa
kuiga tu si kwa ujuzi
huwa hapati ujuzi huo na
huwa hafanikiwi.
70. Ndugu
chungu,
Asili yake ni sehemu za
ufinyanzi.
Hutumika kuonesha
umuhimu wa ndugu au
68
jirani
mkungu.
Mkungu – ufuniko wa
chungu.
Umuhimu wa ndugu
kwa mtu ni kama
chungu na jirani ni kama
mkungu.
jirani.
Inatufunza kuwathamini
ndugu na majirani lakini
si sawa kuwathamini
majirani zaidi kuliko
ndugu.
71. Ndugu mwui
afadhali
kuwa naye
Asili yake ni sehemu za
kufunza maadili.
Mui – mbaya.
Nduguyo mbaya ni bora
uwe naye kaliko
kumkosa.
Hutumika kuonesha
umuhimu wa kumuenzi
ndugu.
Hata kama ni mbaya,
ndugu ni vema kuwa
naye kwani anweza
kutatua matatizo yako
kuliko marafiki
wanaoweza kukukimbia.
72. Nimekupaka
wanja, wewe
wanipaka
pilipili?
Asili yake ni sehemu za
kilimo cha viungo.
Inakuwaje mimi
nikupake wanja wewe
unipake pilipili?
Hutumika kumsimanga
anayelipawema kwa
ubaya.
Inatuasa kuthamini
wema tuliotendewa kwa
kurejesha wema na sio
ubaya.
73. Njia ya siku
zote haina
alama.
Asili yake ni sehemu za
usafirishaji na biashara.
Njia ya kupitwa
kikawaida haihitaji
kuekewa alama kwani
haipotezi.
Hutumika kuonesha
umuhimu wa uzowefu.
Jambo linalofanywa
mara kwa mara husaidia
kufanywa vizuri na bila
ya taabu kubwa.
74. Nta si asali;
nalikuwa
nazo si
uchunga.
Asili yake ni sehemu za
kurina asali.
Nta – utomvu
unaoyashikilia mavuna
ya jumba la nyuki.
Nta si sawa na asali na
aliyekuwa nazo si sawa
na aliyenazo sasa.
Hutumika kumkashifu
anayejitapa kwa
alichokuwa nacho kabla.
Mtu hapaswi kuringia
vitu duni alivyovimiliki
zamani na sasa hanavyo,
huwa hakuna faida
yoyote.
75. Nyimbo ya
kufunzwa
haikeshi
ngoma.
Asiliyake ni sehemu
zenye utamaduni wa
ngoma.
Nyimbo ya kujifundishia
haitegemewi kukesheza
ngoma.
Hutumika kuonesha
ubaya wa kutegemea
vitu vya mpito.
Haifai kutegemea vitu
vya mpito ambavo
havidumu.
76. Paka
hakubali
kulala chali.
Asili yake ni sehemu
zenye mifugo ya
nyumbani.
Hutumika kuonesha
tabia ya werevu wa mtu.
Mtu mwerevu si rahisi
69
Paka hakubali kulala
chali kwa wepesi wake
wa kujigeuza haraka.
kuwezwa na matatizo
kwani anazo njia nyingi
za kutatua matatizo
yake.
77. Radhi ni
bora kuliko
mali.
Asili yake sehemu za
mafunzo ya maadili.
Radhi za (Mungu,
wazee, mke, mume) ni
bora kuliko kuwa na
mali nyingi bila ya
radhi.
Hutumika kuonesha
thamani ya kuridhiwa.
Inatufunza kushughulika
kutafuta radhi zaidi
kuliko mali kwani mali
bila ya radhi hainufaishi.
78. Radhi za
wazee ni
fimbo
maishani.
Asili yake sehemu za
mafunzo ya maadili.
Kukosa radhi za wazazi
ni adhabu kubwa ya
maisha.
Hutumika kuonesha
thamani ya wazee.
Mwenye radhi za wazee
husitirika na aliyezikosa
husumbukamaishani.
79. Shimo la
ulimi mkono
haufutiki.
Asili yake sehemu za
mafunzo ya maadili.
Ulimi unaweza kutoboa
shimo lisiweze kuzibwa
kwa mikono.
Hutumika kuhadharisha
madhara ya ulimi
unapotumiwa vibaya.
Inatufunza tuyafikirie
kwa makini
tunayoyanena kabla ili
yasije yakaleta madhara
makubwakwa jamii.
80. Simbiko
haisimbuki
ila kwa
msukosuko.
Asili yake ni sehemu za
bahari.
Simbiko – uzi wa
ndoana.
Fundo ya uzi wa ndoana
huwa haifunguki mpaka
kwa tabu au
kufunguliwa makusudi.
Hutumika kuonesha
umakini wa uhusiano.
Watu wenye uhusiano
wa dhati si rahisi
kuachana au kutengana
ila kwa uhasidi mkubwa
uliokusuduwa
kuwatenganisha
makusudi.
81. Tonga si
tuwi.
Asili yake sehemu zenye
minazi.
Ukubwa wa nazi sio
wingi wa tuwi.
Hutumika kulinganisha
maarifa ya vijana na
wazee.
Maarifa ya kijana
hayawezi kushinda yam
zee licha ya nguvu na
uzima alizonazo kijana.
82. Ukitaja
nyoka, shika
fimbo
mkononi.
Asili yake ni mazingira
ya mitaa yenye misitu.
Hutumika kuhadharisha
hatari.
Inatufunza tujiandae
kwa hatari inayotokea
ghafla wakati wowote.
83. Umekuwa Asili yake ni maeneo ya Hutumika kuhimiza
70
nguva,
huhimili
kishindo?
pwani.
Nguva – samaki
anyonyeshaye wanawe.
Huuwawa kwa wepesi
sana.
kuwa na ujasiri.
Inatufunza tusiwe dhaifu
bali tuwe wajasiri katika
kukabiliana na matatizo
yanayotukabili.
84. Waraka ni
nusu ya
kuonana.
Asili yake ni mazingira
ya kijamii.
Waraka – barua.
Kutumiana barua na
nusu ya watu kuonana.
Hutumika kuhimiza
kukumbukana.
Inatufunza kuwa ni
muhimu kwa waliombali
kukumbukana japo kwa
kuandikiana barua.
4.3Sababu za Wazanzibari Kuacha Baadhi ya Methali za Kiswahili
Sehemu hii inafafanua sababu mbalimbali ambazo utafiti huu umebaini kuwa ndizo
zinazosababisha kuachwa kwa baadhi ya methali za Kiswahili katika jamii ya
Wazanzibari. Katika hatua ya kwanza ya kuchanganua data zenye sababu za
kuachwa kwa methali hizo, utafiti umebaini sababu nane ambazo zilipendekezwa na
mtafiti kwa watafitiwa wake. Katika hatua ya kuyachambua majibu ya watafitiwa,
utafiti umebaini sababu tano ndizo zilizokubalika na jamii ya watafitiwa. Aidha,
katika hatua ya kuzichambua sababu walizozitoa watafitiwa binafsi, utafiti ulibaini
sababu nyingizinarejea katika zile sababu za awali zilizopendekezwa na
mtafiti.Sababu zilizobaki hazikuonekana kuwa ni sababu za msingi za tatizo hilo na
hivyo kuachwa.
Uchambuzi wa data za sababu za kuachwa methali ulitumia muhimili wa pili wa
nadharia ya uamilifu. Msingi huu unaangalia utendaji kazi wa jukumu la kipande
kazi hicho cha fasihi simulizi katika jamii ambapo utafiti ulibaini methali hizo
hazitekelezi dhima zake ipasavyo. Sababu ya msingi ya kushindwa kutekeleza dhima
zake ni kukosa nafasi ya matumizi katika jamii ya Wazanzibari, jambo
71
lililosababisha kuchunguza sababu za kutotumiwa na kugundulika mambo kadhaa
kuwa ndio yanayosababisha kuachwa kwa methali hizo.Kwa ujumla, utafiti
umegundua sababu kuu zifuatazo:
4.3.1 Mvuvumko wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia
Kwa mujibu wa Oxford Advanced Learners Dictionary of current English (2000),
Sayansi ni taaluma ya maumbile na mwenendo wa asili wa kiulimwengu unaotokana
na msingi wa ukweli unaoweza kuthibitishwa kwa kwa njia za majaribio. Teknolojia
ni utumiaji wa taaluma ya sayansi kimatendo katika kubuni na kutengenezazana na
mashine mpya (uk. 1051, 1230) (Tafsiri ya Mtafiti). Kutokana na fasili hizo,
inafahamika kwamba, Sayansi na teknolojia ni msamiati unaotumika kuwakilisha
taaluma ya kisasa inayotolewa kwa uchunguzi, majaribio, vipimo na kisha
kuthibitishwa kwa utafiti au uchunguzi na baadaye kutumika katika ubunifu na
utengenezaji wa zana, mitambo au mashine bora zinazorahisisha utendakazi na
kuleta mabadiliko ya haraka ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni yanayotokana na
matumizi ya uvumbuzi huo wa kitaalamu.
Jamii nyingi zimekumbwa na mabadiliko ya aina hii. Hii ni kutokana na ukweli
kwamba mabadiliko ya aina hii kwa kiasi kikubwa yamerahisisha maisha ya
wanadamu katika shughuli zao nyingi za kimaisha. Sekta mbalimbali duniani leo
zimefikia kiwango cha hali ya juu kabisa kwa ufanisi. Kwa mfano, sekta ya viwanda,
biashara mfano huduma za kibenki, kilimo mfano zana za kilimo, kuvunia na
madawa. Pia, sekta ya elimu mfano matumizi ya kompyuta na vyuo vikuu vya
72
kimitandao, sekta ya afya mfano madawa na upasuaji wa haraka pamoja na sekta ya
habari mfano ujenzi wa vituo vya redio na televisheni na zana za kurushia
matangazo. Yote haya yamekuwa kwa kasi katika jamii za wanadamu kutokana na
wepesi wake wa utengenezaji na matumizi ya zana za kisasa ambapo hali hiyo
imekuja kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia yaliyofikiwa.
Hata hivyo, maendeleo haya ya sayansi na teknolojia pamoja na kuonekana kuwa ni
hatua muhimu ya kimaendeleo kwa upande mmoja, kwa upande mwengine imeleta
athari hasi katika sekta kadhaa. Hivyo, kama ilivyo kwa mambo mengi kuwa na
athari hasi na chanya, na ndivyo ilivyo kwa maendeleo hayo yanayotokana na
sayansi na teknolojia. Akithibitisha hali hiyo, Kitabuge (2011) anasema kuwa
ugunduzi katika suala la sayansi na teknolojia kwa kawaida huwa na manufaa na
madhara kwa viumbe, na kuongeza kuwa uchanya na uhasi wa athari hizo unaweza
kuonekana kwa kuangalia hali ya utendaji au awasilishaji wa fasihi simulizi ilivyo
sasa katika jamii. kwa mujibu wa maelezo haya, ni wazi kuwa pamoja na kuwa
fasihi simulizi imenufaika, bali pia imeathiriwakutokana na maendeleo hayo.
Sababu hii inaonekana kuwa wazi zaidikiasi cha kukubalika na jamii kubwa ya
watafitiwa. Hii ni kutokana na ukweli kuwa suala la maendeleo ya sayansi na
teknolojia limeathiri mfumo mzima wa maisha ya wanadamu, ikiwa ni pamoja na
lugha zao hasa upande wa fasihi.Khamis (1983) anathibitisha athari hasi mbaya
itokanayo na sayansi na teknolojia kwa kusema kuwa fasihi simulizi imevizwa kwa
maendeleo ya kiufundi na uvumbuzi wa mashine kadhaa, hasa za uchapaji na za
mawasiliano kama vile redio, teprikoda na televisheni. Yesaya (2011) anaonesha pia
73
athari hasi ya sayansi na teknolojia kupitia sekta ya habari katika fasihi simulizi ya
watoto anasema maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano ambayo
nimatokeo ya kukua na kuenea kwa sayansi na teknolojia duniani katika karne hii ya
ishirini na moja, yameathiri sana muundo wa nyimbo za watoto waishio mijini.
Maendeleo haya ya sayansi na teknolojia yaliyosababisha kutokea na kuenea kwa
vyombo vya habari na mawasiliano. Nyimbo nyingi za watoto waishio mijini
zimeathiriwa na maendeleo haya.Kutokana naugumu wa kuyaepuka na athari zake
kwa fasihi simulizi yote kwa jumla ni kubwa.
Katika jamii ya Wazanzibari maendeleo haya nayo yameshajikita vyema. Hali hiyo
imefanya mwenendo wa utamaduni wao kubadilika. Kwa mfano, hivi sasa vikao vya
wazee na vijana na watoto wao vimetoweka kutokana na elimu hii Farsi (1958).
Utamaduni wa kusikiliza methali, hadithi na vitendawili umetoweka. Nafasi ya vikao
hivyo, imechukuliwa na mshughuliko wa vijana katika elimu ya kisasa (sayansi na
teknolojia) kwa upande mmoja, na vyombo vya habari kama vile redio, simu, video
na televisheni kwa upande mwengine. Vyombo hivyo vyote vina uchache wa
kuwasilisha kazi za fasihi simulizi au kukosa kabisa. Kwa hivyo, kutokana na
kukosekana kwa njia hiyo ya asili, na uchache uliopo wa mawasilisho ya kazi za
fasihi simulizi, kazi hizo husahauliwa na hatimae kuachwa kama ilivyotokea kwa
methali hizo.
Ukichukua mfano wa methali; “Angakaanga, tu chini ya gae”, “Avuaye nguo
huchutama” na “Kutwanga nisile unga, nazuia mchi wangu”. Hizi ni methali ambazo
kwa wakati wake zilitumika sana na ni nzuri lugha na ujumbe wake. Ila mambo
74
yanayoelezwahivi sasa jamii ya waswahili ni nadra sana kuyatumia. Mambo kama
chungu kwa sasa mbadala wake ni sufuria ambayo haitoi gae. Pia ukaangaji wa
nafaka kama mtama ama mahindi ni nadra sana kwani sasa kuna mashine za kusagia.
Utamaduni kuvua nguo kwa kuchutama pia umetoweka baada ya ujenzi wa vyoo
vinavyositiri kwa uhakika kwani lengo ni kuepusha kukashifika kwa vile makaazi
halisi ya wakati huo mara nyingi hayakusitiri ipasavyo. Pia masuala ya kutwanga
kupembua unga wa makapi, matumizi ya vinu na michi vinatoweka katika jamii ya
Wazanzibari baada ya kuibuka vifaa kama blenda na mashine za kusagia. Hayo ni
mabadiliko yanayotokana na maendeleo hayo.
4.3.2Mabadiliko ya Msamiati Uliotumikakatika Methali hizo
Katika hali halisi, mambo mengi duniani hayakuwepo hapo kabla, baadae yametokea na
tena yatatoweka. Vilevile, kuna mambo kadhaa ambayo yapo leo lakini hayakuwepo
zamani. Hali hiyo, pia ndiyo inayomkabili mwanadamu na maisha yake hapa duniani.
Lakini hapa hoja ni kuwa, kwa vile binadamu hutoweka, vilevile na mambo yake pia
hufuata mwendo huo. Kwa hivyo, lugha nayo huwepo na baadae hutoweka. Ndio maana
leo kuna oradha ya lugha kadhaa zilizokuwa zinatumika hapo zamani, na hivi sasa
hazipo tena pia, kuna lugha nyingi zilizopo leo zamani hazikuwepo. Kwa hivyo, iwapo
lugha nzima huweza kutoweka, na sehemu ya lugha ni wepesi zaidi kutoweka. Bila
shaka, kuna uwezekano mkubwa wa vitu vya lugha kama hadithi, nyimbo na methali
vikawepo kwa wakati fulani na baadaye kutoweka. Hali hii ipo zaidikwa fasihi simulizi
ya Ki-Afrika ikiwemo ya Kiswahili ambayo ilihifadhiwa kupitia vifua vya watu kwa
muda mrefu kabla ya kuwepo kwa maandishi.
75
Kazi za fasihi simulizi huwa na uteuzi wa maneno maalumu yanayotumika katika
jamii. Uteuzi huu hufanywa kwa ufundi mkubwa. Mbali na uteuzi wa maneno hayo,
pia, mpangilio wake huwa kwa ufundi. Kwa sababu hiyo, ndio maana kazi hizo hasa
za fasihi simulizi huvutia usikivu wake na hupendwa kutumiwa na kila rika la
kijamii.Methali hutumia lugha maalumu na teule kwa ustadi mkubwa. Lugha yake
hupambwa kwa sitiari, nidaa, tashbiha, taswira, balagha, takriri, mchezo wa maneno,
tamathali za semi, tanakali sauti, pamoja na mbinu nyengine za kinudhumu (Simiyu,
2011). Pamoja na yote hayo, vitu hivyo huweza kubadilika ladha yake kwa tatizo la
kukosa matumizi ya baadhi ya misamiati iliyotumiwa katika methali hizo kwenye
jamii ya leo ya Wazanzibari.
Baadhi ya methali hizi zina misamiati ambayo kwa sasa jamii ya Wazanzibari
haiitumii tena. Hali hii,huwafanyavijana wasizifahamu methali hizo. Jambo hilo
huwafanya wazee wenye methali hizo nao waziache na kutumia zile zenye maneno
yanayoeleweka zaidi. Kwa mfano maneno kama vile, „humangiria‟, „Mkata‟ na
„handingwandingwa‟ katika methali; “Mkosa kitoweo humangiria”,
“Mlilalahandingwandingwa,mwemacho haambiwi tule” na“Mkata hana kinyongo”.
Maneno haya kwa sasa jamii ya Wazanzibari haiyatumii tena. Hii ndio maana baadhi
ya watafitiwawalipotakiwa kueleza maana za maneno hayo yaliwashindakutokana na
ugeni uliopo katika maneno hayo nandio maana sababu hii watafitiwa wengi
wamekubaliana nayo.Kuachwa kwa misamiati hiyo hutokana na mabadiliko ya
kijamii yanayotokea. Msamiati unapobadilika ule wa awali husababisha kuachwa
kwa methali hiyo. Kwa maana hiyo, methali zote zenye misamiati ya zamani,
ambayo sasa haitumiki tena ipo hatarini kuachwa. Kuachwa huko hutokana na
76
kutokidhi mahitaji ya jamiiya Wazanzibari iliyopo sasa ambapo kwa mujibu wa
msingi wa kwanza wa nadharia ya uamilifu imebainika kuwa methali hizo hazikidhi
mahitaji ya jamii ya Wazanzibari kwa upande wa misamiati yake, ingawa kwa
upande wa dhima zake kwa jamii bado zinakidhi matakwa ya jamii hiyo.
4.3.3 Kuwapo kwa Methali Nyingi Mpya
Utafiti ulibaini pia kuwa hivi sasa kuna methali nyingi za Kiswahili. Hali hii ni
tofauti kidogo na hapo zamani, bila shaka wingi huu umetokana na kujumuika kwa
methali zilizorithiwa tokea zama za mababu, na zile zilizobuniwa baadae na
zinazoendelea kubuniwa hadi leo. Hali zinaonesha kuwa mpaka miaka ya sitini na
sabiini, methali zilikuwa kwa mamia. Vitabu vingi vilivyotungwa muda huo
vilivyokusanya methali, idadi ya methali ilikuwa ni kati ya mia moja hadi mia sita.
Kwa mfano, Farsy (1979) amekusanya methali mia tano na ishirini.Bali miaka ya
thamanini hadi sasa methali ni kwa maelfu. Mfano ni Kamusi la Methali
lililoandikwa na King‟ei na Ndalu, toleo la kwanza la (1989) lilikuwa na methali
zaidi ya elfu moja na mia tano, lakini katika toleo jipya la miaka ya elfu mbili, lina
methali zaidi ya elfu mbili na mia tano.Akithibitisha wingi huu wa methali,
Mtesigwa (1989) ameeleza kuwalugha za binadamu zina utajiri mkubwa wa methali,
lakini utajiri huu umezagaa na kupindukia katika lugha za kiafrika, hususan katika
eneo la lugha za Kibantu (Kikiwemo Kiswahili) Kusini mwa Ikweta, na pia za Ki-
Negro huko Afrika Magharibi.(Uk. 2-5).
77
Wingi huu wa methali uliopo hivi sasa, unatokana na kukusanyika baina ya zile za
kale zilizopatikana kwa njia za kurithishana na zile zinazoendelea kubuniwa hadi
sasa. Hivyo, methali nyingi hazikuwepo kale, lakini zile zilizoanzia huko kale bado
zipo zinaendelea kuwepo hadi hii leo. Katika hali ya kawaida ni vigumu jamii
kuweza kuzitumia methali zote hizo wakati mmoja. Hii ni kwa sababu methali
hutumika kwa mujibu wa miktadha maalumu. Na ukweli ni kwamba, kutokana na
wingi huo, muktadha mmoja utakuwa na methali nyingi za kuweza kutumika.Jambo
hili litasababisha baadhi yake zitumike zaidi, nyengine kwa wastani, nyengine kwa
nadra sana, lakini nyengine zisikumbukwe kabisa. Kwa mfano methali ya kale
kabisa ni “Waraka ni nusu ya kuonana”. Katika mazingira ya zamani njia pekee ya
kuwasiliana na mtu aliyembali ni njia ya maandishi. Kwa kuwa maandishi hayo
hayakuwa na mfumo maalum yaliweza kuitwa „waraka‟. Masomo ya skuli
yalipoanza kukawa na kitu kinaitwa „barua‟ na hivyo methali ya “Barua ni nusu ya
kuonana” ikaibuliwa. Lakini sasa kutokana mabadiliko ya kijamii, methali ya
“Salamu ni nusu ya kuonana” imeibuliwa. Ingawa methali hizi ni tatu, lengo lake ni
moja. Hata hivyo, methali hii ya mwisho ina mawanda makubwa zaidi. Salamu
inakusanya ile ya waraka, barua, barua pepe, ujumbe mfupi wa simu. Kwa mujibu
wa msingi wa tatu wa nadharia iliotumika unaoangalia utendajikazi wa jukumu au
dhima ya kipandekazi hicho cha fasihi simulizi katika jamii, methalihiyo ndio
inyokidhi mahitaji ya jamii ya Wazanzibari zaidi kwa wakati huu ambao mambo
hayoyote yanapatikana katika jamii yao.Hii inasababisha kutumiwa methali hii zaidi
na kuachwa zile za awali zenye mawanda mafupi.
78
4.3.4Ukosefu wa Taasisi za Kuzihifadhi na Kuzirithisha Methali
Jambo lolote muhimu halina budi kushughulikiwa ili lipate kuimarika, na si kawaida
ya jambo hilo kudumu kutokana na umuhimu wake peke yake. Umuhimu wa lugha
unafahamika katika jamii, bali namna inavyostahiki kushughulikiwa ni jambo
linalotia mashaka. Ingawa serikali imeunda taasisi za kuishughulikia lugha ya
Kiswahili kwa ujumla wake, lakini hatudhani kama taasisi hizo zinawezeshwa
kuishughulikia lugha hiyo katika nyanja zake zote. Mifano ya taasisi hizo ni Baraza
la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA) na Taasisi ya Kiswahili na lugha za kigeni
(TAKILUKI). Yumkini ikaonekana eneo kama methali halijachukuliwa hatua yoyote
na taasisi hizo. Hiyo inatokana na taasisi hizo kutowezeshwa kifedha na kitaaluma.
Mbali na hizo, kunataasisi iliyorithiwa, ya wazee kukaa na watoto na wajukuu zao,
ambayo nayo kwa sasa imedhoofishwa na harakati za masomo ya kiskuli pamoja na
maendeleo ya habari na mawasiliano. Hivyo watoto na wazee wanakosa muda wa
kukaa pamoja kama ilivyokuwa hapo zamani. Baada ya taasisi hizo, hakuna taasisi
nyengine inayoshughulikia wigo huu wa methali za Kiswahili katika jamii ya
Wazanzibari.
Watafitiwa wengi wamelaumu kuwa mfumo wa elimu haukutilia nguvu masuala ya
ufundishaji wa taaluma kama hizi za lugha kwa kiwango cha kutosha kuifanya jamii
kuona umuhimu wa kutunza na kutumia rasilimali lugha kama methali. Katika
kubainisha manung‟uniko yake Bwana Juma Saadati Haji7 anasema taasisi hizo
kama zingelishughulikia suala hilo, ingelionekana kazi ya methali angalau moja
7 Mahojiano baina ya mtafiti na Bwana Juma Saadati yalifanyika 24/3/2015 huko nyumbani kwake mtaa
wa Kikwajuni juu.
79
kama kitabu kikawa kinanunuliwa na watu wakawa wanazisoma. Dai hili
limethibitishwa na ndugu Amur8 ambaye amesema:
Ni kweli BAKIZA mpaka sasa haijatayarisha kazi rasmi kama hiyo.
Hii imesababishwa na changamoto nyingi. Moja ni kwamba
BAKIZA ina majukumu mengi. Kazi za uhariri wa ripoti
mbalimbali za serikali na mashirika, utunzi na uhariri wa vitabu
mbalimbali. Changamoto nyengine ni ya uchache wa wataalamu
ambao majukumu ni mengi. Kwa upande mwengine ni ukosefu wa
fedha za kutosha kukidhi mahitaji yote hayo. Hata hivyo, katika
Kamusi la Kiwahili fasaha BAKIZA imeweka baadhi ya methali
kadhaa za Kiswahili mwishoni. Hii ni kuonesha umuhimu wake na
nia ya kulishughulikia suala hilo kwa umuhimu wa kipekee hapo
baadaye.
Pia, kutokana na maoni ya watafitiwa, umuhimu wa mambo mengi huoneshwa kwa
kutiliwa mkazo katika mifumo ya utoaji wa elimu, na hivyo jambo ambalo mfumo
wa elimu haukulitilia mkazo hubakia kama ni jambo lisilo na umuhimu mkubwa
kwa jamii. Miongoni mwa mambo ambayo jamii inaona hayakutiliwa mkazo ni
methali. Baadhi ya maelezo ya watafitiwa wanaounga mkono hoja hii ni:
Methali hazitiliwi nguvu na mfumo wa elimu, Methali hazisisitizwi
matumizi yake katika taasisi za elimu, Kutokuwepo sera ya serikali
juu ya matumizi ya methali, Kuwepo kwa elimu rasmi ya
mashuleni, Kuibuka kwa wasomi wengi wa kisasa.9
4.4 Athari za Kuachwa kwa Baadhi ya Methali za Kiswahili
Katika kuchunguza athari zinazoikabili jamii kutokana na hali hiyo, utafiti
umegundua kuwa zipo athari chanya zenye kuleta tija naathari hasi zinazoleta
8 Ndugu Amur Salum ambaye ni Afisa wa BAKIZA aliyasema hayo katika mahojiano yake na mtafiti tarehe
14/4/2015. 9 Maelezo hayo wameyatowa Watafitiwa katika dodoso na mahojiano katika kujibu suali la sababu za
kuachwa methali hizo.
80
madharakwa jamii. Data zilizolenga kupata athari zilikusanywa kupitia njia
zilizotajwa hapo juu ambapo mtafitiwa alitakiwa kutaja athari anazozijua.
Watafitiwa walitoa athari nyingi ambazo, katika uchambuzi athari zinazolingana
ziliwekwa kundi moja. Hatua hiyo ilizikusanya athari hizo katika makundi manane,
baada ya kuondolewa zile zilizoonekana kuwa sio athari za msingi katika utafiti huu.
Katika makundi manane ya athari hizo, baada ya uchunguzi wa kina makundi mawili
yalibainika kuhusiana na mengine mawili, ambayo baada ya kuunganishwa yalibakia
makundi matano ambayo nayo baada ya kuchanganuliwa mawili yalibainika kuwa ni
ya athari zenye tija na matatu yaliobakia ni ya athari zenye madhara kwa jamii.
4.4.1 Tija Zilizopatikana
Katika kuchunguza athari za tatizo hilo, watafitiwa walitakiwa kutaja athari
chanyawanazozifahamu. Hata hivyo, utafiti unaonesha kuwa tatizo hili kwa kiasi
kikubwa linakabiliwa na athari hasi zaidi kuliko chanya. Utafiti umebaini athari
chanya zifuatazo:
4.4.1.1 Kuondoka kwa Msamiati Mgumu (Usiotumika)
Kutokana na msingi wa tatu wa nadharia ya uamilifu inayoonesha utendajikazi wake
wa jukumu au dhima ya kipandekazi cha fasihi simulizi katika jamii.Msingi huu ndio
uliotumika katika katika kuzichambua athari zilizotolewa na watafitiwa. Utafiti
umebaini kuwa methali zimeachwa kutokana na kukosa utendajikazi wake
uliosababishwa na kuwa na misamiati ambayo jamii ya Wazanzibari kwa sasa
haiyatumii.
81
Baadhi ya methali zilizoachwa zina msamiati mgumu, na pengine kutokana na
ugumu wake huenda ikawa ndio sababu ya kuachwa kwake kama ilivyooneshwa
katika sehemu iliotaja sababu za kuachwa kutumiwa methali hizo. Kwa mfano,
maneno kama vile „humangiria‟, „Mkata‟ na „handingwandingwa‟ katika methali;
“Mkosa kitoweo humangiria”, “Mlilala handingwandingwa”; mwemacho haambiwi
tule” na “Mkata hana kinyongo”. Maneno haya, kwa sasa, jamii ya Wazanzibari
haiyatumii tena ambayo yanaonekanakuwa na ukakasi wa kuyatamka maneno hayo.
Kwa hiyo, miongoni mwa athari nzuri za tatizo hilo ni kuondoa katika lugha
msamiati mzito, mgumu au wenye ukakasi katika matamshi ya lugha ya Kiswahili.
4.4.1.2 Kuiruhusu Lugha Kulandana na Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia
Dhana iliyopo hapa ni kuwa kuachwa kwa baadhi tu ya methali ni katika mabadiliko
ya lugha. Mabadiliko haya huenda yakawa yanatoa mwanya wa ufanisi wa kuifanya
lugha iweze kuoana na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Hii ni kutokana na
kuingia kwa msamiati mpyaambao baadaye methali zitautumia. Si kila mabadiliko ni
mabaya, bali inategemea mabadiliko yenyewe yanavyokuja. Bila shaka kutokea kwa
mabadiliko yanayoruhusu mambo yanayohusu maendeleo ya kisasa yanayotokana na
sayansi na teknolojia, jamii itayapokea kwa mikono miwili kwa vile hakuna jamii
isiyopenda kuendelea.
Watafitiwa walioiibua athari hii walitoa maelezo yafuatayo; Kukuza maendeleo ya
sayansi na teknolojia katika lugha, Kuwaruhusu watu kupata methali mpya
zinazoendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, Kwenda sambamba na
82
maendeleo ya sayansi na teknolojia. Hoja hii ingawa imeibuliwa na watafitiwa
wachache, lakini mtafiti anakubaliana nayo. Hata hivyo, mabadiliko hayo yakiwa ni
kinyume chake, hali haitakuwa ya ufanisi na hivyo kuwa ni athari mbaya kwa
jamii.Kwa ujumlautafiti umebaini athari hizi zifuatazo:
4.4.2 Madhara yanayopatikana
4.4.2.1Kufifia kwa Utamaduni wa Wazanzibari
Methali za Kiswahili zimebeba mambo mengi sana ya mila, desturi, maadili na ya
kitamaduni. Aidha, methali hubeba hekima na falsafa ya hali ya juu ambazo kwa
kawaida huwa hazipatikani katika lugha ya kawaida. Kila methali hutoa sehemu ya
hekima, falsafa, mila, desturi, maadili na jambo la kitamaduni.Kwa mfano methali
isemayo; “Kikuu kuu pachika, kitakufaa masika”, ina ujumbe na hekima kuhusu
kutodharau kilichotumika baada kupatikana kingine. Ndani yakemna utamaduni wa
Kiswahili wa kuwa na sehemu za kupachika vitu kama pakacha, vikapu au mikoba
katika mapaa ya nyumba. Hii ni falsafa ya kujiwekea akiba hata kwa vitu
vilivyotumiwa, kwani haijulikanini kipi kitakachomfaa mtu wakati wa dhiki kama
kipindi cha masika. Kwa hiyo, ni wazi kuwa methali zinapoachwa kutumiwa, huwa
sehemu hiyo ya utamaduni unaoelezewa katika methali hizo huwa hatarini kupotea.
Wakisisitiza hilo, baadhi ya watafitiwa:
Zitasahaulika na hivyo kupotea kwa utamaduni, Baadhi ya mila na
desturi za waswahili zitapotea, Kutoweka kwa hadhi ya utamaduni
wa waswahili, Kupotea kwa baadhi ya mila, desturi na silka za
waswahili, kupotea kwa miiko ya kimazungumzo iliyoachwa na
83
wazee wetu wa asili, Kuchangia kuporomoka kwa madili ya jamii,
na Jamii itakosa maadili na busara10
.
4.4.2.2Jamii Kuzikosa Adili za Methali
Mbali na falsafa, hekima, maadili, mila, na desturi zinazopatikana katika methali,
kwa upande mwengine, methali hutoa ujumbe na mafunzo maalum kwa jamii.
Mafunzo hayo huweza kuwa ya kukanya, kuasa, kushajihisha, kuadilisha. Kila
methali huwa na funzo au mafunzo yake muhimu ambayo jamii huyatumia katika
harakati zao za maisha, na hivyo jamii isipozitumia methali hizo, athari yake
kuyakosa mafunzo hayo vilevile.Kuhusu ukweli kuwa methali zina mafunzo mengi,
Farsy anelezea kwa kusema kuwa Methali zafaa sana kwa mafundisho ya adili (za
jamii), kwa hiyo ni jambo la muhimu kwa waalimu kujua methali nyingi kama
inavyowezekana, na kuzitumia sana katika mafundisho yao.” (Farsy, 1958)Naye
Mulokozi katika kulithibitisha hilo, amesema:“Kutokana na ufupi na usanii wake,
methali huweza kutoa mafunzo au maonyo kwa mafanikio zaidi kuliko maelezo ya
kawaida”.(2000:36). Hoja hii pia imetolewa na wafitiwa kadhaa akiwemo Bi.
Sabra.11
Baadhi ya watafitiwa hao wanasema:
Watu kutopata mafunzo yanayohusiana na methali hizo, Kukusa
maneno ya hekima kwa kizazi kipya, Kukosa baadhi ya mafunzo
yanayopatikana ndani yake, Athariya jamii ni kutopata kuelimika
kupitia methali hizo, Athari ya jamii kutopata kuonywa na
kushauriwa, Jamii itapotoka kwa kukosa mafunzo ya methali za
kizamani zinazoachwa, na Kuwa na jamii isiyojali mafunzo mema
ya wazee wa kale.
10
Maelezo hayo wameyatoa watafitiwa kupitia dodoso na kuthibitishwa Afisa wa BAKIZA Bw. Rashid
Abdu Rai katika mahojiano yake na Mtafiti yalifanyika tarehe 14/4/2015 hapo Ofisini kwake. 11
Maelezo hayo wameyatoa watafitiwa katika dodoso na kuthibitishwa na Bibi Sabra Mohamed,
mwalimu wa somo la Kiswahili skuli ya sekondari ya Mwanakwerekwe.
84
Adili za jamii yoyote ni pamoja na masuala mazima ya historia inayoihusu jamii hiyo.
Kwa muda wote methali pia hutumika kama chombo cha kuhifadhia mambo kemkem ya
jamii. Miongoni mwa hayo ni utamaduni na historia ya jamii husika. Mambo kadhaa ya
kitamaduni na kihistoria katika jamii yanapatikana kupitia methali pamoja na tanzu
nyengine za fasihi simulizi. Msuya anasema:
Kwa hiyo ni chombo cha kuelezea na kuitazamia jamii
kiutamaduni, kiuchumi, kisiasa na kadhalika… Misemo yao
huwa kioo cha kuwatazamia kwa jumla, ikiwa kisiasa,
kiutamaduni, kiuchumi, kihistoria na kadhalika. Misemo hiyo
imejaa hekima na falsafa ya juu kwa sababu ilitumika pindi
walipotaka kuwaadibu wadogo au kuwatanabahisha wakubwa.
(Msuya, 1979: 7-11).
Ni kweli methali nyingi zimebeba mambo ya kihistoria katika jamii.Baadhi ya
methali huwa ni ufupisho wa matukio hayo ya kihitoria yaliyotokea katika jamii
hapo zamani.Mulokozi(2000) anasema kuwa baadhi ya methali huwa ni
vielelezo au vifupisho vya hadithi fulani inayofahamika vizuri kwa jamii. hoja
iliotolewa na zaidi ya watafitiwa saba. Baadhi ya maelezo yao ni; Kutoweka kwa
sehemu ya historia ya jamii, Kupotea kwa uhalisia wa jamii ya waswahili,
Kupoteza uhalisia wa waswahili katika jamii, Kupotea historia ya waswahili,
Kusahau na Kudharau kabisa ugumu walioupata wahenga, na Kutokujua asili na
walipotokea kizazi cha sasa hivi.Kwa hivyo, methali hizo zisipotumika sehemu
ya historia ilizozibeba zitakuwa hatarini kupotea.
4.4.2.3 Jamii Kukosa Burudani Inayotokana na Methali hizo
Fasihi yoyote pamoja na kutoa mafunzo, ina dhima au jukumu kubwa la
kuiburudisha na kustarehesha jamii. Methali ikiwa ni sehemu muhimu ya
85
fasihisimulizi pia infanya kazi hiyo ya fasihi. Njogu na wenzake wanalieleza
jukumu hilo kwa kusema kuwa Katika jamii zote fasihi simulizi imetumiwa
kuwasilisha maadili na mafungu kemkem kuhusu jamii husika. Pia, imetumika ili
kustarehesha na kuburudisha kwa namna inavyotumia lugha, uigizaji, utendaji,
taharuki na mbinu mbalimbali za simulizi.Methali huleta burudani kwa kule
kutumia tamathali za semi kwa wingi. Mulokozi anasema kuwa mara nyingi
mawazo na falsafa ya methali huelezwa kwa kutumia tamathali, hasa sitiari, na
mafumbo. Uzuri ulioje ni kuwa tamathali zinazotumiwa na methali hutokana na
mazingira halisi ya kijamii na kimaumbile ya watumiaji wa lugha inayohusika.
Kwa hivyo, mambo hayo, yakiunganishwa na ufundi wa uteuzi wa maneno na
mpangilio wake, huzifanya methali hasa zinapotumika katika miktadha sahihi,
ziwe ni burudani tosha kwa jamii. Hili linathibitishwa zaidi na matukio halisi ya
wanajamii kujibizana wao kwa wao kwa kutumi methali tupu katika
mazungumzo yao ya kutaniana.
Baadhi ya maelezo waliyoyatoa watafitiwa walioiibua hoja hii ni; Jamii kukosa
kuburudika kutokana na methali hizo, Jamii kutopata kuburudika kwa methali
hizo, na kukosa raha ya mazungumzo wanayoipata jamii kutokana na methali
hizo. Ingawa watafitiwa walioiibua ni wachache, lakini kutokana na nguvu ya
hoja yake, mtafiti anakubaliana nayo kuwa ni miongoni mwa athari mbaya
zinazoikabili jamii kutokana na tatizo hilo. Kwa jumla, kwa mujibu wa
watafitiwa, jamii inonekana kuathirika vibaya kwa kutotumika baadhi ya methali
hizo kwa athari hizo zilizojadiliwa hapo ambazo moja ni kupotea kwa sehemu ya
Mila, Desturi, Maadili na Utamaduni wa Waswahili. Pili ni Kukosa Mafunzo
86
yanayopatikana kutokana na Methali hizo. Tatu nikupotea kwa sehemu ya
historia ya waswahili. Na nne ni;Jamii kukosa burudani inayotokana na methali
hizo. Athari nne hizi zimekubalika kikamilifu na mtafiti. Watafitiwa pia
wameibua hoja nyengine mbili zinazoipata jamii kwa tatizo hilo. Hoja hizo moja
niKuvunjika kwa Uhusiano na Mafahamiano ya Kijamii kama Ilivyokua Zamani,
na hoja pili ni Kuibuka kwa uoni mbaya kwa baadhi ya wanajamii kuwa methali
zimepitiwa na wakati. Ingawa hoja mbili hizi mtafiti anaziona haziakisi moja
kwa moja na tatizo linalojadiliwa katika utafiti huu.
4.5 Muhutasari wa Sura ya Nne
Sura hiiimejadili matokeo ya utafiti. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwakuna
methali kadhaa za Kiswahili ambazo jamii ya Wazanzibari imeshaziacha. Aidha,
utafiti umeonesha pia kuwa, matumizi ya methali katika jamii hiyo, yamegawanywa
katika makundi manne. Makundi hayo ni ya methalimashuhurizinazotumika mara
kwa mara, methali za wastani zinazotumika kwa wastani katika jamii, methaliza
nadra zinazotumika mara moja moja,na methali ambazo tayari zimeshaachwa
kutumiwa na jamii.
Matokeo yamebaini kuwa ziko sababu kadhaa zinazosababisha kuachwa kwa
methali hizo.Sababu hizo nikutokuwepo taasisi za kuzihifadhi na kuzirithisha
methali, mvuvumko wa Maendeleo ya sayansi na teknolojia, mabadiliko ya msamiati
usiotumikasasa katika methali hizo, na Kuibuka kwa methali nyingi mpya
zinazotumika sasa.
87
Kwa upande wa athariutafiti umebaini kuwepo kwa athari chanya na hasi kwa jamii.
atharichanya za kuachwa kwa methali hizo nikuondoka kwa msamiati usiotumika
kwa sasa, na nyengine nikuiruhusu lugha ya Kiswahili kwenda sambamba na
maendeleo ya sayansi na teknolojia.Athari hasi kwa jamii ni kufifia kwa utamaduni
wa Wazanzibari, jamii kuzikosa adili za methali hizo,na jamii kukosa burudani
inayotokana na methali hizo.
88
SURA YA TANO
MUHTASARI, HITIMISHO NA MAPENDEKEZO
5.1 Utangulizi
Sura hii inawasilisha muhutasari wa tasnifu. Sura ina sehemu nne. Sehemu ya
kwanza inazungumzia juu ya muhtasari wa tasnifu. Sehemu ya pili ni utoshelevu wa
nadharia. Sehemu ya tatu inahusu mchango mpya wa utafiti huu. Na sehemu ya nne
ni maoni na mapendekezo.
5.2 Muhutasari wa Tasnifu
Kwa ujumla, tasnifu hii iliangalia juu ya sababu na athari za kuachwa kwa baadhi ya
methali za Kiswahili katika matumizi ya jamii ya waswahili Zanzibar. Tasnifu hii,
imegawiwa katika sura tano.Sura ya Kwanza ilianzia kwa usuli wa mada, tamko la
utafiti, lililofuatiwa na malengo ya utafiti. Sura hiyo pia imebainisha maswali,
umuhimu na mipaka ya utafiti pamoja na nadharia iliyotumika katika ukusanyaji na
uchambuzi wa data.
Sura ya Pili imezungumzia juu ya mapitio ya maandiko. Mtafiti alipitia vitabu,
majarida, na hata baadhi ya tovuti, zilizomuwezesha kupata maelezo yanayohitajika
kuhusiana na mada ya utafiti. Maelezo yalioelezwa katika sura hii yanahusu fasihi
simulizi na umuhimu wake, semi za Kiswahili, na methali za Kiswahili. Ndani yake
mlioneshwa namna wataalamu walivyozama katika kuzitolea maana na asili ya kila
kimoja kati ya fasihi simulizi, semi na methali, pia katika kuonesha umuhimu wake
89
na matumizi ya kila kimoja. Mwisho wa sehemu hiyo imeoneshwa mapengo ya
kiutafiti yaliojitokeza kutokana na mapitio hayo.Sura ya tatu, imeeleza mbinu na njia
mbali mbali zilizotumiwa katika utafiti huu. Vile vile sura imeeleza eneo na
mawanda ya utafiti, na pia jamii ya watafitiwa. Sura imeonesha pia juu ya umakinifu
wa mbinu na vifaa vilivyotumika katika ukusanyaji wa data.
Sura ya Nne imeonesha namna data hizo zilivyochambuliwa na kutafsiriwa. Data
zilichambuliwa kwa kutumia mkabala wa kifafanuzi. Pia, utafiti ulilazimika
kuonesha hali halisi ya kijamii ambayo kwa kiasi kikubwa imekwenda sambamba na
ubunifu wa utafiti wenyewe. Uchambuzi uliongozwa na malengo ya utafiti pamoja
na maswali yake kama yalivyooneshwa katika sura ya kwanza. Kutokana na
malengo na maswali hayo, mtafiti alipata nafasi ya kutumia maswali yaliokuwemo
katika mbinu za dodoso, mahojiano na mjadala wa kikundi. Kwa ujumla uchambuzi
huo ulifanikiwa kwa vile uliweza kutoa matokeo yaliolingana na mabunio ya utafiti
huu.
Sura ya tano ni hii inayowasilisha muhutasari wa tasnifu ya utafiti, utoshelevu wa
nadharia iliotumika katika utafiti, mchango mpya wa utafiti pamoja na maoni na
mapendekezo yaliotokana na utafiti yanayopaswa kufanyiwa kazi kwa siku zijazo au
katika tafiti zijazo.
90
5.3 Utoshelevu wa Nadharia Iliyotumika
Kutokana na misingi ya nadharia hii, mtafiti aliweza kuzieleza methali za Kiswahili,
na kuonesha umuhimu wake na matumizi yake kama ni kipandekazi cha fasihi
simulizi ya Kiswahili katika utamaduni wa jamii ya Wazanzibari. Aidha, mtafiti
alionesha hali ya uendelezwaji wa kipandekazi hicho na kugundua kuwa si nzuri
kulingana na hadhi na umuhimu wa methali za Kiswahili katika jamii. Vilevile,
mtafiti alionyesha jukumu na dhima ya methali za Kiswahili katika jamii ya
Wazanzibari. Mbali na kuzingatia misingi hiyo, mtafiti pia alikwenda sambamba na
hatua zilizopendekezwa katika kuifanyia kazi nadharia hii ya umilifu. Hivyo, alianza
kuuchunguza utamaduni wa Waswahili wanaoishi Zanzibar na uhusiano wao na
matumizi ya methali.Baadaye alizitafiti methali za Kiswahili na namna
zinavyotumiwa katika jamii hiyo. Vilevile,zilelezewa methali hizo namna ya
kutumika kwake kama chombonakama sehemu ya utamaduniwaWaswahilina
kiwango kinachotumika, kulingana na mahitaji ya jamii yao. Na mwisho ni kuzieleza
methali hizo namna zinavyotendakazi katika jamii hiyo.
Kwa kutumia misingi na hatua hizo, utafiti huu umefanikiwa kwa kiwango kizuri.
Kwani kwa kuangalia kwa undani juu ya utamaduni wa waswahili wa Zanzibar, na
kwa kuziangalia kwa kina methali za Kiswahili na matumizi yake katika jamii,
hatimae imewezekana kugundua methali ambazo kwa sasa jamii haizitumii. Na pia
kugundua sababu na athari za kuachwa kutumiwa kwa methali hizo. Hivyo, nadharia
hii ya uamilifu, imeweza kukidhi haja ya utafiti huu.
91
5.4 Mchango Mpya wa Utafiti
Utafiti umeibua mambo mapya kuhusu methali, ambayo hapo kabla hayakuwa
yakifahamika. Moja ni kwamba methali ni utanzu maarufu wa fasihi simulizi na
zinashuhudiwa zikitumika kila siku na kila sehemu, lakini haikufahamika kuwa
matumizi ya methali huwa yanapita katika mikondo minne. Pili, sababu zinazo
sababisha methali kuachwa kutumiwa, na tatu ni athari za hali hiyo kwa jamii.Hayo
yote ni miongoni mwa mchango mpya wa utafiti huu katika fasihi ya Kiswahili na
hasa fasihi simulizi ya Kiswahili.
5.5 Maoni na Mapendekezo ya Mtafiti
Azma kuu ya utafiti huu ilikuwa ni kuchunguza sababu na athari ya kuachwa kwa
baadhi ya methali za Kiswahili katika jamii ya Waswahili. Matokeo yameonesha
kuwapo kwa tatizo hilo, sababu na athari zake kama zilivyoelezwa katika sura
iliyopita. Pamoja na hali hiyo, utafiti umegundua baadhi ya mianya inayohitaji
kuzibwa, ili kuziimarisha methali za Kiswahili. Miongoni mwa maeneo hayo
Kwanza, ni athari za utandawazi katika methali za Kiswahili. Pili, ni matumizi ya
methali kwa kuzingatia miktadha zinamotumiwa. Tatu, ni athari ya maendeleo ya
sayansi na teknolojia katika methali za Kiswahili. Hivyo, mtafiti anapendekeza
kufanyika tafiti nyengine katika maeneo hayo ili kuhakikisha kuwa methali za
Kiswahili zinaimarika katika matumizi ndani ya jamii ya Waswahili Zanzibar.
Kwa upande wa mapendekezo, mtafiti anapendekeza Kwanza, kwa Jamii yenyewe
kuona umuhimu wa kutumia methali zao katika mazungumzo yao mbalimbali kwani
92
watafaidika na ladha yake na kuepukana na karaha ya kutumia maneno makavu kwa
nyakati nyingi zaidi. Aidha, Wazee ni jukumu lao kuendeleza mwenendo wa kukaa
na vijana wao kwa lengo la kuwaidilisha na kuwaburudisha kwa mazungumzo
yaliyokolezwa kwa matumizi ya methali ili wajifunze lugha njema na pia urithi wa
methali uweze kuendelezwa. Pili, mtafiti anapendekeza kwa Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Amali Zanzibar, kuuruhusu muhutasari kulitanua somo la Kiswahili
katika mawanda ya semi, hasa methali, ili vijana waweze kufunzwa kwa kiwango
cha kuwawezesha kuzihifadhi na kuzitumia kwa usahihi kama walivyopendekeza
wahojiwa wengi miongoni mwa wanafunzi na wataalamu katika maoni yao.
Tatu, mtafiti anapendekeza kwa Serikali kuanzisha kitengo maalumu katika vyombo
vyake vinavyohusika na lugha ya Kiswahili kitakachozisimamia methali na semi za
Kiswahili kwa ujumla katika kuzikusanya, kuzihifadhi, kuzitafsiri kwa lugha mbali
mbali, na kuzisambaza kupitia vitabu nje na ndani ya nchi.Kwa kufanya hivyo,
kutaonesha umuhimu wa kutunzwa na kutumiwa na jamii na hivyo, jamii kuweza
kuzienzi na kuzitumia ipasavyo, jambo litakaloziimarisha na kuikuza fasihi simulizi
na lugha ya Kiswahili kwa ujumla. Mwisho, mtafiti anapendekeza kwa Waandishi na
Wasanii kuzitumia ipasavyo methali za Kiswahili katika kazi zao za fasihi andishi.
Kufanya hivyo, ni njia nyengine muhimu ya kuzihifadhi methali, kufupisha maneno
na kutanua ujumbe pamoja na kuzikoleza kazi zao, kama walivyokuwa wakifanya
waandishi wa zamani, mfano, Shaaban Robert, Saidi Mohamed, Said Ahmed na
wengineo, ambao kazi zao zinavutia hadi leo hii na haziishi hamu kuzisoma.
93
MAREJELEO
Abudu, M. (1978), Methali za Kiswahili, Shungwaya, Nairobi.
Abudu, M. na Baruwa, A. (1981), Methali za Kiswahili, Kitabu cha Pili na Tatu,
Shungwaya Publishers, Nairobi.
Balisidia, M.L. (1987), Tanzu na Fani za Fasihi Simulizi, Katika Mulika Na. 19, uk.
2-9.
Bukenye, A.S, nw (1997), Oral Literature: A Senior Course, Nairobi Longhorns
Publishers.
Chiraghdin, S. (1990), Kiswahili na Wenyewe. Kiswahili 44:01.
Chuachua, R. (2008), Uingizaji wa Methali Katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu,
TUKI, Dar es Salaam.
Farsy, S.S. (1979), Swahili Sayngs, Nairobi East African Literature Bureau.
Ferster, J. (2005),Arguing Through Literature, A Thematic Anthology And Guide to
Academic Writing, McGraw-Hill Companies, New York.
Finnegan, R. (1979), Oral Literature in Africa, Great Britain, Oxford University
Press.
Haji, A.I. (1992), Fasihi, Katika Misingi ya Uhakiki wa Fasihi, TAKILUKI,
Zanzibar.
Haji, M.O. (2006), Vipera vya Fasihi simulizi: Kidato cha 1-4, Zanzibar.
94
Hassan, A. U. (2013), Dhima ya Methali Katika Kudumisha Maadili Katika Jamii ya
Wapemba, Tasnifu kwa Ajili ya Shahada ya Pili, Chuo Kikuu cha Dodoma.
Ireri Mbaabu, (1985) Utamaduni wa Waswahili, Kenya publishing & Book
Marketing Co. Ltd. Nairobi.
Khamis, S.A. (1983), Nafasi ya Fasihi Simulizi katika Jamii ya Kitanzania, Mulika,
Na. 15, uk. 3-13.
King‟ei, K. na Ndalu, A. (1998), Kamusi ya Methali: Toleo Jipya, East African
Publishers, Nairobi. Dar es Salaam. Kampala.
Madumulla, J. S. (1995), Proverbs and Sayngs: Theory and Practice, TUKI, Dar es
Salaam.
Madumulla, J.S. (2009), Riwaya ya Kiswahili: Nadharia, Historia na Nadharia ya
Uchambuzi, Phoenix Publishers Ltd. Nairobi, Kenya.
Mauya, A. B. (2006), Semi: Maana na Matumizi, TUKI, Dar es Salaam.
Mbarouk, S.S. (2011), Athari za Semi za Kanga Katika Jamii, Tasnifu kwa Ajili ya
Shahada ya Pili, Chuo Kikuu cha Dodoma.
Mduda, F na John, J (2011), Kiswahili kidato cha tano na sita, Oxford University
Press, Dar es Salam.
Mgulu, H.A. (2011), Usanaa Katika Methali za Kisambaa (SHIMO), Tasnifu kwa
Ajili ya Shahada ya Pili, Chuo Kikuu cha Dodoma.
95
Mhilu, G.G. nw (2011), Kiswahili kwa Shuleza Sekondari Kidato cha tatunanne,
Nyambari Nyangwine Publisher, Dar es Salam.
Mieder, W. (1978), The Use of Proverbs in Psychological Testing, Journal of
theForklore Institute, Na. 15, uk. 45-55.
Mlacha, S.A.K. (1981), Methali Kama Chombo Muhimu katika Jamii, Mada ya
Semina, TUKI, Dar es Salaam.
Mlacha, S.A.K. na Hurskeinein, A. (1996), Lugha, Utamaduni na Fasihi Simulizi
yaKiswahili, TUKI, Dar es Salaam.
Mlacha, S.A.K.(1995), Fasihi Simulizi na Usuli wa Historia ya Pemba, TUKI, Chuo
Kikuu cha Dar es salaam.
Mohamed, S.A naVuzo, A. C (1991),Stadi za Kiswahili, Kidato cha tatu,Oxford
University Press, Nairobi.
Mohamed, S.A. & Ali, A. M. (1981), Hapa na Pale: Tungo za Sanaa, TAKILUKI,
Zanzibar.
Msuya, P.K. (1997), Fasihi na Methali, Mulika, Na. 9, TUKI, Dar es Salaam.
Msuya, Sh. K. (1979), Yatokanayo na Fasihi Simulizi, Tanzania Publishing House,
Dar es Salaam.
Mtesigwa, P.C.K. (1989), Methali ni nini? Jarida la Uchunguzi la Taasisi
yaKiswahili, Na. 56, uk.1-9.
Mulokozi, M.M. (1989), Tanzu za Faihi Simulizi, Katika Mulika, Na. 21, uk. 1-19.
96
Mulokozi (1996), Fasihi ya Kiswahili: Utanguli wa Fasihi ya Kiswahili, Chuo
Kikuu Huria cha Tanzania, TUKI Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Mutembei, A.K. (2006), “Nadharia ya Fasihi Simulizi na Maendeleo katika Sayansi
na Teknolojia”, Mulika, Na. 27, uk. 1-17.
Mzee, H. A. (1977), "Utamaduni, matumizi na misingi ya lugha ya Kiswahili",
MULIKA 11, Uk. 10.
Naaman, R.M. (1983), Methali na vitendawili, TAKILUKI, Tanzania Publishing
House, Dar es Salam.
Ndaro, J. N. (2012), Fani katika Methali za Kidigo,Tasnifu kwa Ajili ya Shahada ya
Pili, Chuo Kikuu cha Dodoma.
Ndugo, C.M. & Wafula, B.M. (1993), Tanzu za Fasihi Simulizi, University of
Nairobi, Nairobi.
Ngole, S.Y.A. & Lukas, N.H. (2002), Fasihi Simulizi ya Mtanzania, Kitabu cha pili,
TUKI, Dar es Salaam.
Njogu, K. & Chimerah, R. (1999), Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na Mbinu, Jomo
Kenyata Foundation, Kenya.
Njogu, K. nw (2001), Tanzu za lugha: Kitabu cha Wanafunzi, Jomo Kenyata
Foundation, Nairobi Kenya.
Nkwera, F.V. (ht), Tamrini za Fasihi, Commercial Printing, Co, Ltd, Dar es Salaam.
Ohly, R. (1981), Formula- Tungo ya Methali katika Kiswahili, TPH, Dar es Salaam.
97
Omar, C.K. & Mvungi, T. (1981), Urithi wa Utamaduni Wetu, Dar es salaam,
Tanzania.
Omar, C.K. (1976), Misemo na Methali Kutoka Tanzania, East Africa Literature
Bureau, Nairobi.
Othman, S. Y. na Abdulkarim, Y. (2015) Howani Mwana Howani: Tenzi za Zainab
Himid Mohammed, TUKI Dar-es-salaam.
Rashid, A.M. (1992), Semi, Katika Misingi ya Uhakiki wa Fasihi, TAKILUKI,
Zanzibar.
Reddy, G.S. and Anuradha, R. V. (2008), “PrimeKiswahili Proverbs, Origins,
Explanations, Examples”. Neelkamal Publications Pvt.Ltd, NewDelhi, India.
Salum, Z. A. (2007), “Changamoto juu ya Ufundishaji Fasihi Simulizi Katika Skuli
za Sekondari”: Kidato cha Nne Katika Enzi ya Utandawazi Zanzibar, Tasnifu
Shahada ya Kwanza, SUZA.
Senkoro, F. E.M.K. (2011),Fasihi, KAUTTO, Limited.
Shariff, I.N. (1988), Tungo Zetu. Trenton: The Red Sea Press, Inc.
Simchimba, E.A. (2012), Falsafa ya Ki-Afrika Katika Methali za Kiswahili,
Tasnifukwa Ajili ya Shahada ya Pili, Chuo Kikuu cha Dodoma.
Suleiman, M.S. (2009), A drop of Honey (Tone la Asali) Swahili- Eng. Language,
Express Printing Services.
98
Sengo, T.S.Y. (1985), “The Indian Ocean Complex and the Kiswahili folklore: The
case of Zanzibarian Tale-Performance”, Unpublished Ph.D Thesis. Khartoum
University.
TAKILUKI, (1981), Misingi ya Nadhariya ya Fasihi, Zanzibar.
TAKILUKI, (1992), Msingi ya uhakiki wa Fasihi kidato cha nne, EWW, Zanzibar.
Uledi, (2012), Muundo na Lugha katika Methali na Vitendawili kwa jamii ya
Wamakunduchi- Zanzibar, Tasnifu kwa Ajili ya Shahada ya Pili, Chuo Kikuu cha
Dodoma.
Wamitila, K.W. (2002), Uhakiki wa Fasihi: Misingi na Vipengele vyake, Phoenix
Publishers Ltd. Nairobi.
Wamitila, K.W. (2004), Kichocheo cha Fasihi Simulizi na Andishi. Focus,
Publications, Ltd.
101
B: MIONGOZO YA USAILI, DODOSO NA UDURUSU WA MAKTABA
B1: Mwongozo wa Hojaji kwa Wataalamu na Wazee wenye uzoefu
Sehemu A: Maelezo Binafsi ya Mhojiwa
a) Jina la Mhojiwa …………………b) Umri …………. c) Jinsia ………….
(d ) Anapoishi …………………… e) Dhamana/Cheo/Hadhi ya Mhojiwa …………
f) Kiwango cha Elimu ……………………… Uzoefu alionao ……………………
g) Mahali, Tarehe na Muda yalipofanyika Mahojiano ……………………………
Sehemu B: Maelezo Yahusianayo na Utafiti
1. Tunafahamu nini kuhusu methali. Maana, umuhimu, na matumizi yake.
2. Tunafahamu nini kuhusu methali za Kiswahili zilizoachwa kutumiwa?
3. Methali za Kiswahili zinatumikaje hivi sasa katika Jamii ya Waswahili wa
Zanzibar?
4. Je kwa unavyoona, kuna tofauti yoyote ya matumizi baina ya sasa na zamani?
5. Kwa maoni yako, methani zina umuhimu gani kwa Jamii ya Waswahili wa Zanzibar
hivi sasa?
6. Kuna methali kadhaa zilizokuwa zikitumiwa zamani, lakini sasa zimeachwa
kutumiwa kabisa katika jamii ya Waswahili wa Zanzibar. Tunaweza kuzitaja baadhi ya
methali hizo tunazozikumbuka? (Kuonesha orodha ya methali zinazofikiriwa kuachwa).
7. Tunaweza kufikiria ni sababu zipi zinazosababisha kuachwa kutumika kwa
methali hizo?
8. Kuachwa kutumiwa kwa methali hizo kunaleta athari zipi zaidi kwa jamii ya
Waswahili?
9. Kwa maoni yako, unaona methali zilizoachwa ziendelee kuachwa au zirejeshwe
katika matumizi kama zamani?
AHSANTE SANA KWA MSAADA WAKO
102
B2: Mwongozo wa Usaili kwa Wanafunzi wa Sekondari na Diploma ya Kiswahili
A: MAELEZO KUHUSU DARASA LA WASHIRIKI
Darasa: ………………………………………………………………
Skuli/ Chuo: …………………………………………………………
Siku na Tarehe iliofanyika usaili: …………………………………….
Idadi ya washiriki: …………………………………………………….
B: MAELEZO KUHUSU UTAFITI
1. Tunazifahamu methali za Kiswahili?
2. Methali zinatumika vipi katika jamii yetu?
3. Methali zina umuhimu wa kutumiwa katika jamii?
4. Naomba tuzitaje methali tunazifahamu kwa mpango wa kialfabeti. (Mtafiti
atawagawia baadhi ya wanafunzi karatasi zenye methali alizozikusanya na
kuwaamuru wazitie alama zile zitakazotajwa na wanafunzi wenzao)
5. Naomba methali hizi nitakazozitaja sehemu yake ya mwnzo mzikamilishe
sehemu yake ya mwisho (Mtafiti ataziwekea alama ya vyema kila methali
iliyokamilishwa kwa usahihi na alama ya x kwa methali iliyokosewa au ambayo
haikuweza kutajwa).
6. Methali hizi zilizokushindeni kuzijua ni kwa kuwa hivi sasa hazitumiki.
Mnadhani kwa nini methali hili hivi sasa hazitumiki?
7. Ni zipi athari za kuachwa kwa methali hizi katika jamii yetu?
8. Nini kifanyike kuiepusha hali hiyo isiathiri athari mbaya kwa jamii?
AHSANTENI SANA KWA USHIRIKI WENU MZURI
103
B3: Mwongozo wa Dodoso kwa Wakufunzi na Vyuo na Watu wa Mitaani
Hojaji kwa ajili ya Wakufunzi na Wanafunzi wa Fasihi ya Kiswahili Vyuo vikuu
Utafiti huu ni kwa ajili ya kukamilisha masomo ya Shahada ya Uzamili, katika fani ya
Fasihi ya Kiswahili, inayochukuliwa katika Chuo Kikuu cha Dodoma, (UDOM). Mtafiti
anafanya utafiti kuhusu Methali za Kiswahili Zilizoachwa: Sababu na Athari zake kwa
Jamii. Kwa hivyo, unaombwa kutoa mchongo wako kwa kujaza dodoso hili kwa
ukamilifu na usahihi kadri unavyoelewa. Maelezo yote utakayoyatoa yatakuwa ni kwa
matumizi ya utafiti huu.
Sehemu A: Maelezo Binafsi ya Mtafitiwa
a) Jinsia; ….………….. (b) Umri …………. (c) Anapoishi …………………
a) Kiwango cha Elimu ………………… (e) Kazi anayofanya …………………
f) Dhamana/Cheo/Hadhi ya Mjazaji wa hojaji; ………………………………
Sehemu B: Maelezo Yahusianayo na Utafiti
1. Unafahamu nini kuhusu methali za Kiswahili?
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
2. Kwa sasa hivi methali zinatumika vipi zaidi katika jamii ya Waswahili?
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
3. Methali za Kiswahili zina umuhimu gani katika jamii ya Waswahili?
……………………………………………………………………………………………
……………………………………………………………………………………………
4. Kuna methali kadhaa za Kiswahili zilizowahi kutumika hadi miaka ya tisiini, lakini
kwa sasa jamii haizitumii kabisa. Tafadhali zitaje methali unazozikumbuka wewe.
i) …………………………………………………………………………………
ii) …………………………………………………………………………………
iii) …………………………………………………………………………………
5. Miongoni mwa sababu za kuachwa kutumika kwa baadhi ya methali katika jamii ya
Waswahili wa Zanzibar ni hizi zifuatazo. Je unazikubali au unazikataa? (Weka alama ya
vyema kwa unazozikubali na alama ya x kwa unazozikataa)
104
NA. SABABU N/S
i Kwa sasa methali zimepitiwa na wakati katika matumizi.
ii Mvuvumko wa Maendeleo ya sayansi na teknolojia.
iii Kuibuka kwa methali nyingi mpya zinzotumika sasa.
iv Kwa kutumia misamiati mingi ambayo haitumiki kwa sasa.
v Mtindo wa maisha wa kuwepo na kutoweka kwa mambo.
vi Zinatumika lakini zimebadilishiwa misamiati yake ya asili.
vii Kutokana na Kuwepo methali nyingi sana hivi sasa.
viii Kutokuwepo taasisi za kuzihifadhi na kuzirithisha methali.
6. Unafikiria kuna sababu nyengine zaidi ya hizo? Tafadhali zitaje hapa chini
i) ……………………………………………………………………………….
ii) ………………………………………………………………………………..
iii) ……………………………………………………………………………….
7. Unadhani kuachwa kutumiwa kwa methali hizo katika jamii ya Waswahili kuna athari
njema, mbaya au zote? Jaza unapodhani ni sawa zaidi (Njema …. Mbaya … Zote….)
8. Tafadhali zitaje athari unazozifikiria wewe;
ATHARI NZURI:
i) ……………………………………………………………………………………
ii) ……………………………………………………………………………………
iii) ……………………………………………………………………………………
ATHARI MBAYA:
i) ……………………………………………………………………………………
ii) ……………………………………………………………………………………
iii) ……………………………………………………………………………………
9. Kwa maoni yako, unadhani kuna umuhimu wowote wa kuzihuisha na kuzihifadhi
methali za Kiswahili zilizoachwa katika jamii ya Waswahili? ..........................................
TUNAKUSHURU KWA MSAADA WAKO
105
B.4: Mwongozo wa Udurusu wa Maktaba
Vyanzo vya
kudurusiwa
Dondoo muhimu Lengo
Vitabu
Tahakiki
Makala
Ripoti mbalimbali
Tasnifu
Majarida
Tovuti
Dhana ya Fasihi
simulizi
Dhana ya semi
Dhana ya methali
Methali za
Kiswahili
Jamii ya waswahili
Kupata taarifa mbalimbali
zinazohusiana na fasihi simulizi.
Kupata taarifa mbalimbali juu ya
maana, chanzo, matumizi, na
umuhimu wa semi katika jamii.
Kupata taarifa mbalimbali juu ya
maana, chanzo, matumizi, na
umuhimu wa methali katika jamii.
Kupata taarifa mbalimbali
zinazohusiana na hastoria,
utamaduni, na uhusiano wa jamii ya
waswahili na fasihi simulizi.
106
C: Mgawanyo wa Matumizi ya Methali Kwa Jamii ya Wazanzibari
C.1: Methali Zinazotumiwa mara kwa mara katika Jamii ya Wazanzibari
1. Ada ya mja hunena, mwungwana ni kitendo.
2. Adhabu ya kaburi aijua maiti.
3. Aibu ya maiti aijua muosha.
4. Akiba haiozi.
5. Akili ni nywele kila mtu ana zake.
6. Akili nyingi huondoa maarifa.
7. Alalaye usimuamshe; ukimuamsha, utalala wewe.
8. Aliyekando, haangukiwi na mti.
9. Asiye kuwapo na lake halipo.
10. Asiyefunzwa na mamae, hufunzwa na ulimwengu.
11. Asiyejua maana haambiwi maana.
12. Asiyekuwepo na lake halipo.
13. Asiyesikia la mkuu huona makuu.
14. Avumaye baharini ni papa kumbe wengi wapo.
15. Baada ya dhiki faraja.
16. Baada ya kisa mkasa; baada ya chanzo, kitendo.
17. Baba wa kambo si baba.
18. Bandubandu! Huisha gogo.
19. Baniani mbaya kiatu chake dawa.
20. Bendera hufuata upepo.
21. Biashara haigombi.
22. Chanda chema huvikwa pete.
23. Chema chajiuza, kizuri chajitembeza.
24. Chovya - chovya yamaliza buyu la asali.
25. Chururu - si ndo! ndo! ndo!
26. Dalili ya mvua mawingu.
27. Damu nzito kuliko maji.
28. Dau la mnyonge haliendi joshi.
29. Dawa ya moto ni moto.
30. Dua la kuku halimpati mwewe.
31. Dua mbaya haombolezewi mtoto.
32. Fadhila ya punda ni mateke
33. Fimbo ya mbali hayiuwi nyoka.
34. Fuata nyuki ule asali.
35. Fumbo mfumbe mjinga, mwerevu huling‟amua.
36. Ganda la mua la jana chungu kaona kivuno.
37. Haba na haba hujaza kibaba.
38. Halla! Halla! Mti na macho.
39. Hamadi, kibindoni, silaha, iliyo mkononi.
40. Haraka haraka haina baraka.
41. Hasira, hasara.
107
42. Hayawi! Hayawi! Huwa.
43. Heri nusu shari, kuliko shari kamili.
44. Heri ya mchawi kuliko fitina.
45. Hewalla! Haigombi.
46. Hiari yashinda utumwa.
47. Ihsani (Wema, Hisani) haiozi.
48. Iliyopita si ndwele, ganga ijayo.
49. Jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza.
50. Jitihadi haiondoi kudura.
51. Jogoo la shamba haliwiki mjini.
52. Jungu kuu halikosi ukoko.
53. Kawia ufike kuliko kulala njiani.
54. Kidole kimoja hakivunji chawa.
55. Kikulacho ki nguoni mwako.
56. Kila ndege huruka na bawa lake.
57. Kimya kingi kina mshindo mkubwa/mkuu.
58. Kingiacho mjini si haramu.
59. Kipendacho moyo ni dawa.
60. Kipya kinyemi ingawa kidonda.
61. Kitanda usicho kilala hujui kunguni wake.
62. Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.
63. Kosa moja haliachi mke.
64. Kuishi kwingi, ni kuona mengi.
65. Kujikwaa si kuanguka, bali ni kwenda mbele.
66. Kukopa harusi, kulipa matanga.
67. Kwenye miti hakuna wajenzi.
68. La kuvunda (kuvunja) halina ubani.
69. Macho hayana pazia.
70. Mafahali wawili hawakai zizi moja.
71. Maji yakimwagika hayazoleki.
72. Majuto ni mjukuu, mwishowe huja kinyume.
73. Masikini haokoti, akiokota huambiwa kaiba.
74. Masikini na mwanawe, tajiri na mali yake.
75. Mbiu ya mgambo ikilia ina jambo.
76. Mchimba kisima hungia mwenyewe.
77. Mchonga mwiko hukimbiza mikono yake.
78. Mficha uchi hazai.
79. Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.
80. Mgema akisifiwa tembo hulitia maji.
81. Mgeni njoo mwenyeji apone.
82. Mkamia maji hayanywi, akiyanywa humkwama.
83. Mke ni nguo, mgomba kupalilia.
84. Mkono mtupu haulambwi.
85. Mkuki kwa nguruwe mtamu, kwa mwanadamu uchungu.
86. Mla kuku wa mwenziwe, miguu humwelekea.
87. Mla, mla leo; mla jana kala nini?
88. Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.
108
89. Moto hauzai moto.
90. Mpanda ngazi hushuka.
91. Msema pweke hakosi.
92. Msitukane wakunga na uzazi ungalipo.
93. Mstahimilivu hula mbivu.
94. Mtaka cha mvunguni huinama.
95. Mtaka nyingi nasaba, hupata mwingi msiba.
96. Mtoto akililia wembe, mpe.
97. Mtoto umleyavyo ndivyo akuavyo.
98. Mtu hakatai mwito, hukata aitiwalo.
99. Mtu hujikuna ajipatiapo.
100. Mtumai cha ndugu hufa masikini.
101. Mungu hamfichi mnafiki.
102. Mwana mkaidi hafaidi mpaka siku ya Idi.
103. Mwangaza mbili moja humponyoka.
104. Mwenda tezi na omo hurejea ngamani.
105. Mwenye kuumwa na nyoka akiona jani hustuka.
106. Mwenye macho haambiwi tazama.
107. Mwenye nguvu mpishe.
108. Mwenye shibe hamjui mwenye njaa.
109. Mwenzako akinyolewa wewe tia maji.
110. Mzazi haachi ujusi.
111. Mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi.
112. Mzowea kunyonga, kuchinja hawezi.
113. Ngoja! ngoja? huumiza matumbo.
114. Ngoma ivumayo haidumu.
115. Njia ya mwongo fupi.
116. Pabaya pako si pema pa mwenzako.
117. Paka akiondoka, panya hutawala.
118. Papo kwa papo kamba hukata jiwe.
119. Penye kuku wengi hapamwagwi mtama.
120. Penye miti hakuna wajenzi.
121. Penye nia ipo njia.
122. Penye wengi pana mengi.
123. Samaki mmoja akioza, huoza wote.
124. Sikio halipwani kichwa. Sikio halipiti kichwa.
125. Sikio la kufa halisikii dawa.
126. Siku njema huonekana asubuhi.
127. Siku utakayokwenda uchi, ndiyo siku utakayokutana na mk weo
128. Simba mwenda kimya ndiye mla nyama.
129. Tamaa mbele, mauti nyuma.
130. Taratibu ndiyo mwendo.
131. Uchungu wa mwana, aujuae mzazi.
132. Udongo uwahi ungali maji.
133. Ukenda kwa wenye chongo, vunja lako jicho.
134. Ukiona kwako kunaungua kwa mwenzako kunateketea.
135. Ukiona vinaelea, vimeundwa.
109
136. Ukuukuu wa kamba si upya wa ukambaa.
137. Ulimi hauna mfupa.
138. Usiache mbachao kwa msala upitao.
139. Usimwamshe aliyelala utalala wewe.
140. Usipoziba ufa utajenga ukuta.
141. Usisafiriye nyota ya mwenzio.
142. Usitukane wakunga na uzazi „ungalipo
143. Vita havina macho.
144. Vita vya panzi ni furaha ya kunguru.
145. Wastara hazumbuki, wambili havai moja.
146. Watende wao wakitenda wenziwo iwe mwao.
147. Wema hauozi.
148. Wengi wape, usipowapa watachukua kwa mikono yao.
149. Werevu mwingi mbele kiza.
150. Yaliopita si ndwele, tugange yaliomo na yajayo.
151. Zimwi likujualo, halikuli likakwisha.
110
C.2: Methali Zinazotumiwa kwa wastani katika Jamii ya Wazanzibari
1. Adui mpende.
2. Akili ni mali.
3. Akipenda, chongo huita kengeza.
4. Akumulikaye mchana usiku hukuchoma.
5. Alalaye usimuamshe; ukimuamsha, utalala wewe.
6. Aliyekando, haangukiwi na mti.
7. Aliyekupa wewe kiti, ndiye aliyenipa mimi kumbi.
8. Ana hasira za mkizi.
9. Anayekataa wengi ni mchawi.
10. Anayeonja asali huchonga mzinga.
11. Anayetaka hachoki hata akichoka keshapata.
13. Aninyimaye mbaazi, kanipunguzia mashuzi.
14. Apewaye ndiye aongezwaye.
15. Asiye na mengi, ana machache.
16. Asiyebahati habahatiki/ habahatishi.
17. Asiyekujua hakuthamini.
18. Bilisi wa mtu ni mtu.
19. Cha mlevi huliwa na mgema.
20. Funika kombe mwanaharamu apite.
21. Hakuna siri ya watu wawili.
22. Hamna! Hamna! Ndimo mliwamo.
23. Hapana marefu yasio na mwisho/ncha.
24. Hapana masika yasiyo na mbu.
25. Hauchi-hauchi, unakucha.
26. Heri kujikwaa dole, kuliko kujikwaa ulimi.
27. Jifya moja haliinjiki chungu.
28. Kamba hukatikia pabovu/pembamba.
29. Kata pua uunge wajihi.
30. Kila mwamba ngoma, ngozi huivutia kwake.
31. Kivuli cha fimbo hakimfichi mtu jua.
32. Kuagiza, kufyekeza.
33. Kuambizana kuko, kusikilizana hapana.
34. Kuchamba kwingi, kuondoka na mavi.
35. Kufa, kufaana.
36. Kulea mimba si kazi, kazi kulea mwana.
37. Kunguru mwoga hukimbiza bawa lake.
38. Kupanda mchongoma, kushuka ndio ngoma.
39. Kupoteya njia ndiko kujua njia.
111
40. Kwa mwoga huenda kicheko na kwa shujaa huenda kilio.
41. Kwenda mbio si kufika.
42. La kuvunda halina rubani.
43. Leo ni leo asemayo kesho ni mwongo.
44. Liandikwalo ndiyo liwalo.
45. Lila na fila hazitangamani.
46. Lisemwalo lipo; ikiwa halipo, lipo nyuma linakuja.
47. Maji ukiyavuliya nguo, huna budi kuyaoga.
48. Maji usiyoyafika hujui wingi wake.
49. Majuto ni mjukuu, mwishowe huja kinyume.
50. Mapenzi ni kikohozi, hayawezi kufichika.
51. Masikini akipata, matako hulia mbwata.
52. Mbio za sakafuni huishia ukingoni.
53. Mchagua jembe, si mkulima.
54. Mchagua nazi, hupata koroma.
55. Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo.
56. Mcheka kilema, hafi bila kumpata.
57. Mchelea mwana kulia, hulia yeye.
58. Mchovya asali hachovyi mara moja.
59. Mchumia juani, hula kivulini.
60. Mfinyazi hulia gaeni.
61. Mganga hajigangi.
62. Mjinga akierevuka mwerevu yupo mashakani.
63. Mjumbe hauawi.
64. Mkamatwa na ngozi ndiye mwizi.
65. Mkono mmoja haulei mwana.
66. Mkuki kwa nguruwe mtamu, kwa mwanadamu uchungu.
67. Moja shika, si kumi nenda uje.
68. Msafiri kafiri.
69. Mtaka yote hukosa yote.
70. Mtoto wa nyoka ni nyoka.
71. Mtumikie kafiri upate mradi wako.
72. Mtupa jongoo hutupa na mti wake.
73. Mume wa mama ni baba.
74. Mwana kidonda, mjukuu kovu.
75. Mwanga mpe mtoto kulea.
76. Mwanzo kokochi mwisho nazi.
77. Mwenye kovu usidhani kapowa.
78. Mwenye shoka hakosi kuni.
79. Mwizi hushikwa na mwizi mwenziwe.
80. Mwomba chumvi huombea chunguche.
112
81. Nahodha wengi, chombo huenda mrama.
82. Nazi mbovu harabu ya nzima.
83. Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu.
84. Ndugu wakigombana, chukua jembe ukalime, wakipatana, chukua kikapu
ukavune.
85. Ngoma ivumayo haikawii kupasuka.
86. Ng'ombe avunjikapo guu, hurejea zizini.
87. Ng'ombe haelemewi na nunduye.
88. Ngozi ivute ili maji.
89. Nimekula asali udogoni, utamu ungali gegoni.
90. Njia ya mwongo fupi.
91. Nzi kufa juu ya kidonda si haramu.
92. Painamapo ndipo painukapo.
93. Paka wa nyumba haingwa.
94. Panapo wengi hapaharibiki neno.
95. Penye mbaya wako, na mwema wako hakosi.
96. Penye wazee haliharibiki neno.
97. Penye wengi pana Mungu.
98. Sahani iliyofunikwa, kilichomo kimesitirika.
99. Sikio halilali na njaa.
100. Subira yavuta heri, huleta kilicho mbali.
101. Sumu ya neno ni neno.
102. Udugu wa nazi hukutania chunguni.
103. Ukiona zinduna, ambari iko nyuma.
104. Ukipewa shibiri usichukue pima.
105. Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni.
106. Ukitaka uzuri sharti udhurike.
107. Ukupigao ndio ukufunzao.
108. Uongo wa mganga ni nafuu ya mwele/ nimwele kupona.
109. Usikaange mbuyu ukawaachia wenye meno watafune.
110. Usile na kipofu ukamgusa rnkono.
111. Usisahau ubaharia kwa sababu ya unahodha.
112. Vikombe vikikaa pamoja havina budi kugongana.
113. Vita vya panzi ni furaha ya kunguru.
114. Wagombanao ndio wapatanao.
115. Ya kale hayako.
116. Yote yang‟aayo usidhani dhahabu.
113
C.3: Methali zinazotumiwa kwa nadra katika jamii ya Wazanzibari
1. Aisifuye mvuwa imemnyea.
2. Ajidhaniye amesimama aangalie asianguke.
3. Akutendae mtende, mche asiekutenda.
4. Angurumapo simba, mcheza nani?
5. Bura yangu sibadili na rehani.
6. Dua mbaya haombolezewi mtoto.
7. Gonga gogo uskilize mlio wake.
8. Hapana msiba usiokuwa na mwenziwe.
9. Hapana ziada mbovu.
10. Heri kufa macho kuliko kufa moyo.
11. Hukunyima tonge hakunyimi neno.
12. Ikiwa hujui kufa, tazama kaburi.
13. Ivumayo haidumu.
14. Jino la pembe si dawa ya pengo.
15. Kawaida ni kama sharia.
16. Kelele za mlango haziniwasi usingizi.
17. Kenda karibu na kumi.
18. Kila mlango na ufunguwo wake.
19. Kinga na kinga ndipo moto uwakapo.
20. Kisebusebu na roho kipapo.
21. Kuku mgeni hakosi kamba mguuni.
22. Kuzima koleo si mwisho wa uhunzi.
23. Lake mtu halimtapishi, bali humchefusha.
24. Lisilokuwapo moyoni, halipo machoni.
25. Maiti haulizwi sanda.
26. Mambo kikowa.
27. Manahodha wengi chombo huenda mrama.
28. Mcheza hawi kiwete, ngoma yataka matao.
29. Mchuma janga hula na wakwao.
30. Mgonjwa haulizwi uji.
31. Mla cha mwenziwe na chake huliwa.
32. Mpanda farasi wawili hupasuka msamba.
33. Mshoni hachagui nguo.
34. Mtoto akibebwa hutazama kisogo cha mamaye.
35. Mwacha asili ni mtumwa.
36. Mwamini Mungu si mtovu.
37. Mwanzo wa ngoma ni „Lele‟.
38. Mwenye kelele hana neno.
114
39. Mzaha, mzaha, hutumbuka usaha.
40. Ndugu chungu, jirani mkungu.
41. Nyani haoni kundule, huliona la mwenziwe.
42. Pele hupewa msi kucha.
43. Shoka lisilo mpini halichanji kuni.
44. Ukitaka kula nguruwe, chagua aliyenona.
45. Ulipendalo hupati, hupata ujaliwalo.
46. Ulivyoligema utalinywa.
47. Unamlaumu mwewe, kipanga yuwesha kuku.
48. Ushikwapo shikamana.
49. Usinivishe kilemba cha ukoka.
50. Uso umeumbwa na haya.
51. Uso wa kufadhiliwa uchini.